Zaburi 46:1-3 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada
utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”
Utangulizi:
Moja ya matukio muhimu sana
ambayo Dunia inaweza kuwa imejifunza katika wakati huu wa Corona ni pamoja na
kukubaliana na Neno la Mungu kuwa Mungu ndio asili kuu ya usalama wa mwanadamu;
kukitokea vita, au serikali zetu zote zenye nguvu duniani zikashindwa, au
kukitokea matukio mabaya ya kutisha ambayo hata wenye nguvu duniani wanaogopa,
sisi tunapaswa kuelewa kuwa kiko chanzo kimoja kikubwa cha usalama ambacho ni
Mungu!
Watu wenye uwezo wa kufikiri Duniani
kama alivyo rais wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli walikaa na
kutafakari kwa kina na kugundua kuwa, hakuna kinachoweza kutuponya iwe ni
maendeleo makubwa duniani, iwe ni elimu, iwe ni sayansi na technolojia, vyote
haviwezi kuwa na majibu ya usalama wa kweli leo isipokuwa Mungu, Tumejifunza
leo kuwa lolote linaweza kutokea hata kwa sekunde moja tu na likaondoa usalama
na vyote vikashindwa kutusaidia isipokuwa maombi na kumtegemea Mungu vina uwezo mkubwa sana!
Rais wetu alifunga siku kadhaa
kule Dodoma, maombi yake binafsi, lakini vilevile alitangaza maombi ya kitaifa
kwa siku tatu, na akayaona majibu ya maombi na kisha akatoa muongozo na kisha
akatangaza shukurani na Tanzania ikawa na utulivu wa hali ya juu! Kwa nini kwa
sababu yeye kama rais ana serikali ana nguvu na ni mwana sayansi, lakini
alitambua kuwa msaada wa kweli unatoka kwa Mungu! Hakuna ulinzi mwingine wowote
isipokuwa kumgeukia Mungu tu na
kumtegemea ona
Zaburi 46:8-10 “Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari. Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.”
Mungu tu ndiye wa kutumainiwa Na
ni Mungu tu ndiye Mlinzi wa kweli, Niliposikia habari wakati wa tatizo la
Corona mwanzoni zilikuwa na utishio mkubwa sana hasa niliposikia Prince Charles yaani mtoto wa malikia
naye ameugua corona unajua nini? Hawa ndio watu wanaolindwa zaidi Duniani
kuliko mru yeyote Kikosi cha kumlinda malikia
kinaitwa SCOTLAND YARD SQUARD
Kikosi hiki kinamlinda malikia na familia yake kwa masaa 24 na kina makomandoo
waliofuzu mafunzo mbalimbali wapatao 185, wao pia wana jina lingine maarufu kama RPS yaani ROYAL PROTECTION SQUAD ukiacha kuwa wanalindwa, watoto na wajukuu
wa malikia wenywe ni askari waliofuzu na kushiriki vita za aina mbalimbali,
Gharama za ulinzi wa wajukuu wa malkia Prince
William na Prince Harry pekee unagharimu paundi laki tano 500.000. Paundi moja kwa sasa ni sawa na shilingi za
kitanzania 2900 hivi 500,000 X 2900 = 1,450,000,000 kwa mwaka wanalindwa na vifaa vya kisasa zaidi, Hapo
hatujaeleza gharama za ulinzi wa malikia na mwanae mkubwa Prince Charles, Ikiwa
mtu mkubwa kama huyu anaweza kupata virusi vya Corona sembuse wewe mbwa mfu tu! Je unadhani unakula vizuri kuliko yeye? Je
unadhani unachekiwa afya vizuri kuliko yeye? Je unadhani una madaktari bingwa
na hodari kuliko yeye?
Huwezi kuponyoka bila Mungu,
Daudi alielewa kuwa kuna siri ya ziada katika Mungu, ni Mungu pekee ndiye
anayeweza kutulinda na sio kinginecho
Zaburi 20:6-8 “Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.”

Mungu anatusubiri tu tuuitie msaada
wake tutambue kuwa yeye atatujibu na hatutategemea mbinu za kibinadamu pekee
bali Mungu atatokeza msaada katika kila hatari inayotukabili katika siku zetu
duniani, Tunapomkimbilia yeye hatupaswi kuogopa chochote tunapaswa kusimama kwa
imani na kutambua ya kuwa Bwana atakaa imara katika kiti chake cha enzi na
kudhibiti kila kinachoinuka mbele yetu!
Zaburi 46:1-3 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada
utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”
Ulinzi wetu na usalama wetu
unapatikana kwa imani kutoka kwa Mungu na sio mazingira yanayotuzunguka, yeye
Bwana ni mwenye nguvu yeye ndio Ngome, imani yetu inapaswa kumsadiki yeye kuwa
yuko mahali kote na ndiye anayetupa tumaini ni Mungu aliyejitambulisha kwetu
kwa Israel yaani Mungu wa Yakobo
Zaburi 46:7, “Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.” Tana mstari wa 11 “Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.”
Mungu anataka tumtegemee yeye tumtumaini yeye na hapendi tutegemee vitu na mambo mengine, yeye hutupa amani hata wakati wa hofu kubwa inayoikumba dunia yeye humwaga Baraka kwa watu wote wanaomtegemea
Yeremia 17:5-7 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake”.
Mungu atupe imani thabiti sana wakati huu, tumtegemee yeye na hata wakati wa hatari na majanga tumkumbuke yeye, tuendelee kuutegemea uwepo wake na ulinzi wake kwa sababu uwepo wake ni amani kubwa sana bila kujali nini kinatokea, Ayubu alipoteza kila kitu lakini alisimama imara kwa sababu alimtegemea Mungu, Wamtumainio Bwana ni kama Mlima sayuni hautatikisika wakaa milele, Zaburi 125:1 wengi wamepoteza uhai na kufa katika wakati huu wa Corona kwa sababu ya hofu na kutokuwa na imani kwa Mungu, hapa Tanzania watu wengi pia waliogopa lakini ashukuriwe Mungu kwamba tuna Rais anayemcha Mungu, na amekuwa sio rais tu bali ni mlezi wa kiroho wa taifa. Alisimama katika imani kuliko hata viongozi wa kiroho wengine, na aliwakosoa vikali hata wale waliofunga nyumba za ibada ! na kuwakumbusha kuwa imara kama Daniel Shadrack meshak na Abednego.

Mungu wetu habadiliki na kanuni
zake ni zilezile, Mungu yuleyule aliyetenda kazi nyakati za agano la kale ndiye
anayetenda kazi hata sasa, Biblia inasema hivi
Zaburi 105:5 “Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi inasema”
Zaburi 105:5 “Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi inasema”
Tukimtegemea Mungu tutakuwa
salama katika ulimwengu usio salama, tuendelee kutegemea yeye na kusimama
katika nafasi yetu, tunapoiangalia hali halisi leo tutaweza kukubaliana kabisa
kuwa ulimwenguni sio mahali salama lakini imani yetu ikisimama katika neno la
Mungu na ahadi zake na wote tukasimama imara katika imani na kuondoa hofu na
kuwa na ujasriri hakuna kitu kitakuja
kututikisa duniani.
1Wakoritho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume,
mkawe hodari.” Biblia inasema
Isaya 26:3 “Utamlinda yeye ambaye moyo wake
umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.”
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi
mwenye Hekima!
0718990796
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni