SOMO: BISHANO KATI YA
UUMBAJI NA MABADILIKO YA VIUMBE
(Creation theory
against Evolution Theory)
Kwa miaka
Mingi sana sasa karibu 133 Dunia imekuwa taabuni sana na usumbufu mwingi
umetokea kutokana na kuvumiliwa vya kutosha kwa mafundisho potofu ya Charles
Darwin, kuhusu uumbaji, Dunia nzima imekubali mafundisho haya yaweze
kufundishwa mashuleni na kuharibu imani ya vijana wetu au kuwaingizia wazo la
kukataa uumbaji wa Mungu na kutokuyaamini maandiko, Imani ya Kikristo, Kislamu
na Kiyahudi, kwa Pamoja hazikubaliani kabisa na mafundisho hayo yenye nia ya
kumkataa Mungu, Biblia inaonya vikali juu ya wazo la kumkataa Mungu kuwa
linaleta upumbavu miongoni mwa wanadamu
Warumi 1:18-23 na 28-32 Biblia inasema hivi
[“18. Kwa
maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu
wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. 19. Kwa kuwa mambo ya Mungu
yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
20. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na
kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata
wasiwe na udhuru; 21. kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye
Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye
ujinga ikatiwa giza.
22.
Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; 23. wakaubadili utukufu wa Mungu
asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya
ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
28. Na kama
walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao
zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 29.
Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda,
na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, 30. wenye
kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye
majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, 31. wasio na ufahamu,
wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; 32. ambao wakijua
sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti,
wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. ]
Biblia
inaonya vikali kuwa hatupaswi kuyafuata mawazo hayo ya kipumbavu, na kuwa sio
kuyafuata tu hata kuyaunga mkono yaani kukubaliana na wayatendao!
Tutajifunza
somo hili kwa kuzingatia maswala kadhaa yafuatayo
·
Maana ya neno
wazo (Theory)
·
Wazo la
Mabadiliko ya Viumbe (Evolution Theory)
·
Wazo la
Uumbaji (Creation Theory)
1.
Maana ya neno wazo
(Theory)
Neno theory kwa tafasiri ya Oxford Advanced Learners Dictionary
Linasomeka hivi “Theory is a formal sets of Idea that intended to Explain why
something happens or Exist” kwa tafasiri isiyo rasmi tunaweza kusema hivi “wazo ni kikundi cha Fikra zinazokusudia
kuelezea kwanini jambo au kitu kimetokea au kuwepo” Hivyo ni muhimu kugahamu
kuwa tunapozungumzia Mabadiliko ya viumbe Evolution theory tunazungumzia wazo,
na tunapozungumzia wazo la Uumbaji
Creation Theory Tunazungumzia Kweli ya Mungu, Kwa vile wazo la uumbaji asili
yake si mwanadamu ni neno la Mungu na wazo la Maendeleo ya viumbe asili yake ni
mwanadamu.
2.
Wazo la mabadiliko ya
viumbe (Evolution Theory)
Evolution maana yake kupitia Oxford Advanced Learners Dictionary it is
the gradual development of plant or animal for over many years of adapt to
changes in their environment kwa tafasiri isiyo rasmi ni Maendeleo ya
kimabadiliko ya mmea au mnyama yanayotokana na kukabiliana na mazingira yake.
Mawazo haya yanasisitiza kuwa mwanadamu pia ni kiumbe aliyebadilika kwa
miaka kadhaa kwa kadiri alivyokuwa akikabiliana na mazingira yake, na kuwa
kuweko kwake hakutokani na kuumbwa lakini asili ya viumbe vyote ni maji na
kujiendeleza kwa viumbe hivyo
Mwanzilishi wa wazo hili anajulikana kama Charles Darwin ambaye aliishi
kati ya 1809 – 1882 Yeye alikuwa ni mtoto wa Mchungaji na Mkristo na
alijiingiza katika maswala ya sayansi ya wanyama, alikuwa Muingereza,alizaliwa
huko Shrewsbury February 12 1809 katika familia iliyokuwa na uwezo kama mtoto
wa tano, alisomea maswala ya Madawa huko Edinburgh na baadaye kuachana na
shughuli hizo na kujiunga na chuo kikuu cha Cambridge akijiandaa kuwa mtumishi
wa Kanisa, ingawa Darwin alikuwa akijinadi kama mkristo baadaye aliukana
ukristo na alikana kuwepo kwa Mungu, na lengo lake kubwa katika wazo lake hili
lilikuwa ni kukanusha kuwepo kwa Mungu, Hata ingawa Darwin alikanusha madai
hayo lakini wazo lake limatia moyo na
matokeo yake ni kuukanusha uumbaji wa Mungu na hili ndio kusudi kuu la kuwepo
kwa wazo hili
Biblia inasema mpumbavu amesema Moyoni hakuna Mungu, wameharibu matendo
yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema, Toka mbinguni Bwana
aliwachungulia wanadamu Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu,Wote
wamepotoka wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema La hata mmoja, Zaburi
14:1-3, 53:1
Ni muhimu kufahamu kuwa kwa namna
yoyote ile tusikubali mawazo haya ya kipumbavu yakafundishwa kwa vijana wetu
mashuleni, na ama kama serikali imeyapitisha yafundishwe ni muhimu dhana hii
ikashughulikiwa vilivyo na wazazi, wachungaji na watu wote wenye mapenzi mema,
hatukubali waka kama mkuu wa wajenzi mweye Hekima sikubali kujiunga na kundi
hili la kipumbavu lenye mlengo wa kumkataa Mungu na uumbaji wake
Biblia inaonyesha ya kuwa kuelimika kwenye faida na maarifa kunaanza na
kumcha Mungu Mithali 1;7 “kumcha Bwana ni chanzo cha Maarifa, Bali
wapumbavu hudharau hekima na adabu” Hakuna udhuru kwa vile uumbaji
unadhihirisha wazi kuwa Mungu yuko, na wazo la aina hii ni la kipumbavu na
lenye kumvunjia Mungu heshima Warumi 1:21 kwa Sababu walipomjua Mungu
hawakumtukuza kama ndiye Mungu, wala kumshukuru, bali walipotea katika uzushi
wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza”
Watanzania kama tunataka Baraka katika taifa letu ni lazima tukiri na
kukubali kuwa Mungu yupo, Serikali yetu inaweza isiwe na Dini kama inavyoelezwa
lakini Lazima iwe na Mungu, Lazima tutambue kuwa Mungu Muumba wa Mbingu na nchi
na vyote viujazavyo yuko, na nilazima tumuogope na kuwafundisha watoto wetu
kumuogopa na kumtambua!
Tukirihusu ujinga huu kuendelea kufundishwa Mashuleni inaweza kuja
kutushangaza kuwaona watoto wakirudi shuleni wakina na mashaka na Tourati,
Zaburi, na Injili kwa ujumla wataanza kuwa na mashaka na maandiko matakatifu,
ni lazima tuwakumbushe kuwa dhana hizo ni mawazo tu na sio ukweli “this teaching is only a theory (an
opinion based on observation) But its not reality” by Master Mason Rev. Innocent Kamote.
3.
Wazo la uumbaji (Creation
Theory)
Watu wanaoamini katika wazo la uumbaji kwamba Mungu aliziumba mbingu na
nchi, wako sahii na wanamuamini Mungu na maandiko Matakatifu, Biblia katika
kitabu cha Mwanzo inatuonyesha kuwa Mungu aliumba na kuanzisha kila kitu, Mwanzo
1:1 Hapo Mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi, Mwanzo 2:1 Basi
Mbingu na nchi zikamalizika na jeshi lake lote” ni wazi kuwa Mungu aliumba kila
kitu katika hali kamili kabisa, hakuna kiumbe ambacho kilibadilika kutokana na
mazingira, Biblia katika kitabu cha Mwanzo inaonyesha
·
Mwanzo wa
Anga, Mwanga, Ulimwengu sayari dunia, jua mwezi na nyota 1-1-18
·
Mwanzo wa
Maisha na uhai Mwanzo 1:19-25
·
Mwanzo wa
Binadamu Mwanzo 1:26-31 na 2
·
Mwanzo wa
dhambi ulimwenguni Mwanzo 3:1-7
·
Mwanzo wa
mpango wa ukombozi Mwanzo 3:8-24 na hasa 15
·
Mwanzo wa
maisha na familia Mwanzo 4:1-15
·
Mwanzo wa
ufugaji, na kilimo Mwanzo 4:2
·
Mwanzo wa
kuabudu Mwanzo 4:1-7
·
Mwanzo wa
mauaji Mwanzo 4;8
·
Mwanzo wa
maendeleo makubwa, ufalme na miji Mwanzo 4:16-9:29 hasa 4:17
·
Mwanzo wa
Ibada ya kweli hadharani Mwanzo 4:26
·
Mwanzo wa
Mataifa Mwanzo 10:1-11:32
·
Mwazno wa
Lugha mbalimbali Mwanzo 11:1,6-9
·
Mwanzo wa
Taifa Teule Israel Mwanzo 12-50
Biblia
inathibitisha kuwa Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba akiwa na akili kamili
kabisa na alimpa wajibu wa kuilima na kuitunza Bustani ya Aden Mwanzo 2:19-20, 15 Biblia inaonyesha
kuwa Adamu alitoa majina kwa wanyama wote na aliwekwa katika Bustani ya Aden
ili ailime na kuitunza Mwanadamu aliumbwa akiwa na akili timamu na uwezo mkubwa
wa kuleta maendeleo, wanadamu walipewa Lugha na Mungu hivyo si kweli kuwa lugha
ni sauti za Nasibu. Mwanadamu sio Nyani wala Sokwe
Mungu
alipokwisha kuumba alijisifia na kuufurahia uumbaji wake kwa kusema Mwanzo
1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya na tazama ni chema sana.
Biblia inaonyesha kuwa uumbaji wa Mungu ni kamili na hahukuhitaji “process from
primitive to Perfect”
Wazo la
Darwin linaanzia na kile ambacho Mungu amekifanya, watu waoamini katika dhana
hii hawawezi kujibu swala
1.
Ulimwengu na
vyote viujazavyo vimewezaje kuweko?
2.
Maisha na
uhai ulijianzishaje?
3.
Makusudi ya
Mwanadamu Duniani ni nini?
4.
Hatima ya
mwanadamu ni nini?
Ni wazi
Kabisa kuwa hata kisayansi wazo hili haliwezi kuthibitika kwa vile
sayansi inataka Uchunguzi (Utafiti) observation Majaribio (tested) na Uhalisia
(Naturalistic Evidence) Mpaka sasa hakuna mwanadamu anaweza kufanya njia hizo
kuu za kisayansi na kuthibitisha wazo la Darwin, kwa hiyo mtazamo wa Darwin ni
mtazamo tu na wala sio Sayansi
ü Mawazo ya Darwin hayatambui kuwa Sayansi ina mipaka
na haiwezi kujitosheleza kuelezea uumbaji
ü Inafundisha dhana na mawazo tu na inatafasiri vibaya
maandiko matakatifu na taarifa zake
ü Inakazia mawazo ya kisayansi kamma kwamba ndio
ukweli halisi
Biblia
ü Inaelezea vema na kutambua sababu na kusudi la
uumbaji
ü Inaelezea na kuchambua kwa undani kuwa Mungu ndiye
muumba na kuwa waliumba viumbe kamili na kila kimoja kwa aina zake na hakuna
mchakato endelevu wa kubadili viumbe hao, Nyani wataendelea kuwa nyani na
binadamu wataendelea kuwa binadamu
Wagalatia 1:9 Kama tulivyotangulia kusema , na sasa nasema tena mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea na alaaniwe
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.