Jumapili, 25 Oktoba 2026

Apolo: Naye alikuwa hodari katika maandiko!


Matendo 18:24-26 “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.”




Utangulizi:

Mojawapo ya wahubiri wakubwa sana waliokuwa na mvuto wa kipekee katika nyakati za Kanisa la Kwanza sambamba na Petro (Kefa) na Paulo Mtume alikuwa ni Apolo, Muhubiri huyu wa injili na Mwalimu mbobevu aliyekuwa na mchango mkubwa sana katika kanisa alikuwa na uweza wa kipekee kiasi cha kuwekwa katika kiwango kimoja na Mtume Petro na Paulo katika kanisa la Korintho huku akisifiwa kama mtu aliyemwagilia maji mbegu iliypandwa na Paulo katika kanisa la Korintho, sio hivyo tu watu walijivunia na kujisifia muhubiri huyu katika makundi

1Wakorintho 3:21-23 “Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.”

Biblia inamuelezea Apolo kama moja ya wahubiri aliyekuwa na neema ya juu katika ufundishaji na kwamba alikuwa ni Myahudi kutoka Alexandria nchini Misri, aliyekuwa na uwezo mkubwa sana katika kunena, Hodari wa maandiko, mwenye ujuzi wa kina katika Agano jipya anatajwa kuwa muhubiri maarufu na mwalimu aliyebobea ambaye ana mchango mkubwa katika kanisa la karne ya kwanza, akitajwa kama mtu wa Elimu yaani msomi mtu huyu leo ana kitu ambacho tunaweza kujiufunza kutoka kwake na tutajifunza kwa kuzingatia vipengele vikuu muhimu vitatu vifuatavyo:-


·         Apolo Aliyekuwa Hodari katika maandiko.

·         Mchango wa Apolo katika Kanisa la kwanza.

·         Mambo ya kujifunza kutoka kwa Apolo.      

         

Apolo Aliyekuwa Hodari katika maandiko.

Apolo ni mojawapo ya wahubiri mashuhuri wa nyakati za kanisa la Kwanza ambaye mwandishi wa Injili na Historia wa nyakati za Kanisa la Kwanza Luka anashindwa kuacha kuzungumza habari zake, Muhubiri huyu na Mwalimu mashuhuri anatajwa katika kiwango cha juu pamoja na Paulo, Petro na yeye mwenyewe, hii inaonyesha wazi kabisa kuwa hakuwa mtu wa kuchukuliwa poa, kumbuka kuwa yeye hakuwa wala hakuwahi kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu waitwao mitume, na wala hakuwahi kuwa na Petro wala kuambatana na Paulo, na huenda hakuwahi kuwa miongoni mwa wanafunzi waliopata kumjua Yesu Kristo wakati wa huduma yake duniani, lakini anaelezewa katika maandiko kuwa hakuwa mtu wa kawaida, pamoja na kuwa hatupaswi kuwa washabiki wa wahubiri lakini uwezo wake na umahiri wake katika injili uliwafanya Wakorintho kutokumuacha pembeni katika makundi ya kishabiki yaliyojitokeza mwanzoni mwa huduma kwa kanisa hilo mpaka pale Paulo alipokemea makundi hayo kwa waraka wake  na kuwaelimisha wakorintho kwamba kila mmoja ana karama yake huyu hivi na huyu hivi:-

1Wakorintho 1:10-13 “Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?”

Kugawanyika kwa kanisa katika makundi ya kuwashabikia walimu wa neno la Mungu katika kanisa la Korintho halikuwa jambo jema na la busara lakini hata hivyo limetokea kutufunulia kitu kuwa kama Apolo aliwekwa katika kiwango kimoja au kuwa na kundi kati ya Paulo na Petro ni Dhahiri kuwa mtu huyu hakuwa wa kawaida na hapa tunataka kujifunza nini siri ya uwezo wake na ushawishi wake mkubwa katika jumuiya ya wanafunzi wa Yesu Pale Korintho? Apolo ni nani hasa?

-          Biblia inamuelezea Apolo kuwa alikuwa Myahudi, sawa na tu na alivyokuwa Petro na Apolo, lakini huyu alikulia katika jiji la Alexandria ambao ulikuwa moja ya miji ya kale na iliyokuwa maarufu sana kwa Elimu kule Misri ya kale, Mji huu ulianzishwa na mfalme wa Kigiriki aliyekuwa na umaarufu mkubwa Alexander the Great mwaka 331 Kabla ya Yesu Kristo, Mji huu ulikuwa ni moja ya mji uliokuwa kituo kikubwa sana cha Elimu na utamaduni katika ulimwengu wa Mediteranian kwa hiyo Apolo alikulia huko na alitokea huko

 

Matendo 18:24 “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko.”

 

Kwa msingi huo ni wazi kuwa Apolo alilelewa  na kusomea katika jiji hilo lililokuwa na ujuzi katika maswala ya Elimu, Falsafa, uwezo mkubwa wa mijadala, kujenga hoja na kujibu, utaalamu wa lugha, sheria, utamaduni na uwezo wa kujitambua na kutafasiri maandiko, Jiji la Alexandria pia lilikuwa jiji lenye vyuo vikuu vingi vya taaluma

 

-          Jina lake Apolo kimsingi ni jina la Kiyunani (Greek) “Apollōs” ambalo pia linahusishwa na jina la mungu wa kigiriki aliyeitwa “Apollo” au “Apaella”  ambalo maana yake kwa kiingereza ni “Sheepfold”  ambaye wajibu wake ulikuwa ni ulinzi wa kondoo na mifugo Protector of flocks and herds kwa hiyo jina Apollo maana yake ni Mlinzi wa Kondoo na wanyama wa kufugwa, hata hivyo Biblia haijasema kitu kuhusu uhusiano wa jina lake na miungu ya Kigiriki lakini tunaweza kupata picha ya kile ambacho jina lake linaakisi,  huyu alikuwa mtumishi wa Mungu na alikuwa muhubiri na Mwalimu mbobevu aliyekuwa akifundisha habari za Yesu. Kweli aliwalinda kondoo!

 

-          Mwenye uwezo mkubwa wa kuwasilisha kwa usahihi – Neno la Mungu linamuelezea Apolo kama mtu aliyekuwa na uhodari na mtu anayeweza kuwasilisha kwa usahihi habari za Kristo

 

Matendo 18:25 “Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.”

 

Kunena na kufundisha kwa usahihi kunamaanisha kuwa alikuwa anawasilisha kwa ufasaha  ujuzi aliokuwa nao kuhusu Kristo kupitia maandiko ya Torati, mtu huyu alikuwa na ujuzi wa maneno, elimu na uwezo mkubwa wa kujieleza kwa Kiyunani ni “Logios” kwa hiyo hakuwa mtu tu mwenye maarifa kichwani lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwasilisha kile alichokuwa anakijua, mtu anaweza kuwa ni Profesa au daktari wa falsafa wa jambo fulani au hata theolojia  lakini akawa hana uwezo wa kufundisha, Mtu anaweza kuwa na maarifa mengi sana kichwani lakini uwasilishaji wake ukawa unamfanya asieleweke kwa Apolo mambo yalikuwa tofauti alikuwa ni mtu aliyebobea katika kujifunza, mwenye maarifa, mwenye uelewa na anayeweza kuelezea kwa kina na sio hivyo tu alikuwa na nguvu ya ushawishi na uwezo wa kupata kibali, jambo hili lilimfanya kuwa Mwalimu mzuri, akikubalika, Uwezo wake mkubwa katika kufundisha unaonyesha umahiri wake mkubwa katika kijifunza pia

 

-          Mwenye kufundishika, Apolo pamoja na ujuzi mkubwa na sifa kubwa alizokuwa nazo pia alikuwa sio mtu mwenye kiburi na majivuno, alikuwa ni mtu anayeweza kuwekeka chini na kufundishika, wasomi wengi tulionao leo duniani ni “unteachable” wasiofundishika, Sivyo ilivyokuwa kwa Apolo yeye kama msomi alikuwa na ufahamu kuwa huwezi kujua mambo yote na kwa sababu hiyo elimu aliyokuwa nayo haikumpa kujivuna na unyenyekevu aliokuwa nao ulimfanya awe tayari kupokea darasa zaidi kutoka kwa Priscilla na Akila ambao walikuwa ni watenda kazi pamoja na Paulo mtume hawa walimualika na kumfundisha njia ya Bwana kwa usahihi zaidi na hivyo kumfanya asaidike maradufu, ujuzi haukumfanya ajivune! Na aliendelea kuwa Mwalimu bora zaidi

 

Matendo 18:25-26 “Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.”

 

1Wakorintho 8:1-2 “Na kwa habari ya vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.”

 

Pamoja na kuwa muhubiri mzuri na mtu mwenye elimu, mnenaji hodari, na mwenye uhodari katika maandiko Lakini alipoalikwa na Pricilla na Akila na kufundishwa njia ya Bwana kwa usahihi zaidi alisikiliza na kufundishika  hii ni dalili inayoonyesha kuwa Apolo alikuwa mnyenyekevu na ujuzi haukumletea majivuno alikuwa ni mwenye kufundishika hakusema mimi ni Muhubiri mkubwa, mimi nasimama mbele ya watu wengi na ninasikilizwa, mimi ni msomi lakini alikubali ushauri na kuwasikiliza wengine hii ilikuwa ni hekima kubwa kwa mtumishi huyu wa Mungu. Jambo lililofungua mlango wa kupokea neema kubwa zaidi na kumfanya kuwa Mwalimu aliyekubalika!

 

-          Apolo alikuwa ni mtu mwenye bidii – Kadiri tunavyojifunza kuhusu Apolo unaweza kupata picha kubwa ya aina ya mtu huyu wa kipekee inaonekana wazi kuwa alikuwa na elimu, alikuwa na ujuzi wa maandiko, alikuwa mnenaji hodari, alikuwa na uwezo wa kuwakilisha, alikuwa na ujuzi wa mawasiliano, alikuwa na moyo wa huduma alikuwa anafundishika, alikuwa mnyenyekevu, alikuwa na kipawa lakini juu ya yote hayo alikuwa na bidii, jambo lililomfanya awe muhubiri na mwalimu mwenye matokeo, tunajifunza kuwa pamoja na kumuamini Mungu na kujifunza na kumtumikia Mungu bado tunapaswa kuwa na bidii katika maswala yote ya kiroho Apolo alikuwa mwenye bidii, kila mtu wa Mungu anapaswa kuwa na bidii katika Nyanja mbalimbali za kiroho, na kimwili ili kujiongeza na ili tuweze kuwa msaada kwa wengi, lakini zaidi sana tuweze kuwa na ufanisi katika wito

 

Matendo 18:24-28 “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi. Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”  

 

-          Apolo alikuwa Mwalimu mwenye uwezo wa kuwajenga wengine – Neno la Mungu linaonyesha kuwa neema iliyokuwa juu yake ilimsaidia kuwajenga na wengine, maarifa na ujuzi mkubwa aliokuwa nao haukuwa kwa manufaa yake mwenyewe lakini alitumia kila alichokuwa nacho kuwajenga wengine jambo hili linaonyesha kuwa kweli mtu huyu alikuwa mtu wa Mungu na alikuwa na ujuzi wa kuyatumia maarifa aliyo nayo kwaajili ya mwili wa Kristo, kila mara sisi kama watu wa Mungu kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa wengine wanafaidika na kile Mungu ametupa badala ya kujawa na hila na wivu na umimi na kuyatumia maarifa yetu na akili zetu na nafasi zetu kuwakwamisha wengine kwa hila na husuda, Kila mtumishi wa Mungu mwenye afya nzuri ya kiroho anapokutana na wengine anapaswa kuwaachia athari ya imani zaidi, maarifa zaidi, ujasiri zaidi, utakatifu zaidi, wepesi zaidi, ujuzi zaidi, na uwezo mkuu wa kumtumikia Mungu zaidi, Apolo alikuwa ni mjenzi  alipokwenda makanisani aliwasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema, wewe umesaidia wangapi? Umeumiza wangapi? Umekwaza wangapi?, umebomoa wangapi? Apolo aliwasaidia sana wale waliokwisha kuamini.  

 

Matendo 18:27. “Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu.”

 

-          Apolo alikuwa ni mtetezi mkubwa wa imani – Moja ya wajibu wetu mkubwa tulio nao ni pamoja na kuilinda imani na kuitetea Apolo licha ya kuwa msomi, alikuwa na mnenaji hodari na mtaalamu wa maandiko aliutumia ujuzi wake alionao kuitetea imani na kumuhubiri Kristo, hii ilikuwa ni kama kilele cha mukhtasari wa imani yake alitumia mandiko kuwaelekeza watu kwa Yesu Kristo, huduma ya kweli ya kila mtumishi wa Mungu ni kuwapeleka kwatu kwa Yesu, ni kumfunua Yesu Kristo kwa jamii ya watu wote na kuilinda imani, ujuzi wa maandiko bila kumfunua Yesu Kristo inakuwa ni ujuzi wa maarifa tu, lakini neno la Mungu linapomfunua Yesu Kristo watu wanapata ujumbe kamili uliokusudiwa na Yesu na huu ndio wokovu wenyewe, Apolo alitumia ujuzi wake wa neno la Mungu kuwaelekeza watu kwa Yesu Kristo, na ndio ukweli kuwa maandiko yanamfunua Yesu tu

 

Matendo 18:28 “Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”

 

Yohana 5:38-40 “Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye. Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.”

 

-          Alikuwa hodari katika maandiko – Moja ya sifa yenye nguvu na mvuto Mkubwa ambayo Luka mwandishi wa injili na kitabu cha matendo ya mitume anaielezea kuhusu uwezo na nguvu za Apolo ni kuwa mtu huyu alikuwa hodari katika maandiko! Ona

 

Matendo 18:24 “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko.”

 

Kama kuna sifa ambayo natamani kila mtumishi wa Mungu awe nayo na tuachane na ubishi ni kuwa na ujuzi au uhodari katika maandiko kama alivyokuwa Apolo, Luka haandiki habari za Apolo kama jambo la kushitukiza na au la bahati mbaya Luka na timu yote ya umisheni ya Paulo walikuwa wamebaini uwezo mkubwa sana wa Apolo na ambao una faida kubwa sana katika mwili wa Kristo. “Naye alikuwa Hodari katika maandiko” neno Hodari linalotumika hapo katika kiyunani linatajwa kama neno “Dynatos”  ambalo kwa kiingereza ni sawa na neno Powerful, Mighty, Strong, au Possible likimaanisha kuwa mtu huyu alikuwa ni mwenye  Nguvu, Uwezo, Mamlaka  na ujuzi mkubwa katika maandiko, Apolo sio tu alikuwa msomaji wa kawaida wa maandiko yaani Biblia, lakini alikuwa na uweza mkubwa katika maandiko, alifahamu sana Agano la kale na alikuwa na ujuzi wa kulifafanua kuwa linasema nini kuhusu Kristo wote tunafahamu kuwa maandiko yote yanamtaja Yesu Kristo na kueleza habari zake kuanzia torati na manabii vitabu vyote vinaeleza kuhusu Yesu  ona

 

Luka 24:13-27 “Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.  Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.”

 

Ujuzi huu na uweza huo na mamlaka na ufahamu katika neno la Mungu aliokuwa nao Apolo ulimfanya awe muhubiri mwenye matokeo kokote alikokwenda na alikohudumu na kufundisha kimsingi alikuwa ni kama Mwalimu ambaye wakati Paulo amepanda yeye alikuja kutia maji, na kusababisha ustawi, uweza wake katika Bwana na neno lake kulileta ustawi mkubwa sana katika mwili wa Kristo kama watu watayajua maandiko,  na malengo yake watakuwa na msaada mkubwa kama aliokuwa nao Apolo, ujuzi katika maandiko unasaidia katika ukuaji wa Kiroho, unasaidia kuweka muongozo wa maisha ya kila siku, unawasaidia watu kufanya maamuzi sahihi, unawasaidia watu kujua kwa kina na mapana na marefu ufahamu wa kina na wa ndani kuhusu Mungu, unawatia moyo watu wakati wa mambo magumu, unawajenga watu kwa hekima, unawafundisha watu uadilifu na maarifa unawaunganisha watu karibu na Mungu unawajengea watu mahusiano mema, unawapa watu na kuwajengea imani, unawazamisha watu katika kujua ahadi za Mungu, unawatia watu nguvu na kuwajenga kiroho katika maisha ya kila siku, unawapa watu hekima na jinsi ya kufanya maamuzi sahihi, unawafundisha watu njia za Mungu na utajiri mkuu wa upendo wake na heshima kwa wengine, unawajengea watu matumaini wanapokuwa na hofu, huzuni na woga, inawapunguzia watu hofu na kuwakumbusha uweza wa kiungu wa kuwalinda, unatoa msaada wa ndani na kuleta utulivu wakati wa Magumu, kwa hiyo hii ina maana ya kuwa mtu anayejua maandiko na namna ya kuyatumia katika maeneo hayo yote huyo sio wa kawaida na anaweza kumsaidia mtu wa aina yoyote ile  na kuwaongoza watu katika kweli huu ndio uwezo mkubwa na wa juu zaidi wa Apolo aliokuwa nao na kwa sababu hiyo alikuwa Mwalimu kweli kweli anayefaa kwa nyakati zote! Mungu atupe kina Apolo wengi leo

Mchango wa Apolo katika Kanisa la kwanza.

Kama tulivyotangulia kuona habari za Apolo na uhodari wake katika maandiko jinsi ulivyo na maana, utaweza kwa jicho la haraka kugundua pia mchango wake mkubwa ulivyokuwa nyakati za Kanisa la kwanza ujuzi wake katika maandiko ulimfanya Apolo awe mtu mwenye mchango mkubwa sana katika nyakati za Kanisa la kwanza

1.       Aliimarisha sana wale walioamini – Matendo 18:27-28 “Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”

 

Apolo alitumiwa na Mungu kwa neema  kama mtu aliyewaimarisha sana waamini alivuka bahari na kwenda mpaka Akaya bila shaka Macedonia kule ulaya Ugiriki na alikaribishwa huko kwa barua na kuwa Msaada mkubwa kwa waamini, Mungu anamtumia Apolo sio kama Mwanzilishi wa makanisa bali anamtumia kama mtu anayeimarisha kile kilichoanzishwa Paulo mtu anaifananisha huduma ya Apolo kama mtu anayemwagilia huku yeye akiwa kama mtu aliyepanda kwa hiyo alikuwa ni Mwalimu mwenye kujenga umahiri wa waamini “Strengthener of the belivers” mwenye kuwatia nguvu waamini, mwenye kuimarisha waamini!

 

1Wakorintho 3:5-7 “Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”

 

2.         Alimuhubiri Kristo - Matendo 18:27-28 “Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”

 

Kutokana na ujuzi wake katiika maandiko aliweza kuonyesha kupitia maandiko na kuthibitisha kuwa Yesu ndiye Kristo kwa hiyo kitaalamu Apolo pia alikuwa au anajulikana kama Apologetic Preacher, Mwalimu aliyekuwa na uwezo wa kuitetea imani na kuithibitisha imani kwa kutumia maandiko na kuwasaidia watu katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu, hili ni la Muhimu kwetu tuwaelekee watu kwa Yesu na sio kwetu watu wamjue Yesu zaidi

 

3.       Alitambuliwa na Paulo kama mtumishi mwenzake – Utambuzi wa Paulo mtume kuhusu Apolo unatufundisha kuwa Muhubiri mzuri sio wewe peke yako, inatukumbusha kuwa Mungu anaweza kuinua wengine katika kiwango kama chako na kuzidi, na hatupaswi kuoneleana wivu, badala yake ni lazima tukubali kuwa kila mmoja ana majukumu yake ya kutekeleza katika mwili wa Kristo, Paulo anatambua hilo kuhusu Apolo na anasema kuwa sisi sote ni wahudumu ambao ninyi mliamini mmoja alipanda na mwingine akatia maji na mwenye kukuza ni Mungu, hivyo Kanisa halijengwi na mtu mmoja, Mungu huweza kumtumia huyu hivi na mwingine akatumiwa vile kwa utukufu wa Mungu, huyu anaweza kuwa mtume mwingine Mwalimu mwingine muhubiri na kadhalika

 

1Wakorintho 3:5-7 “Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”

 

Paulo anasema kuwa wao ni wafanyakazi katika shamba au jengo la Mungu  na hakuna mtu mwenye kanisa lake, au watu wake wala hakuna anayeweza kusema mimi ndiye mwanzilishi, au watu hawa ni wangu kila mmoja ana kazi yake katika mwili wa Kristo mmoja alipanda na mwingine akatia maji, leo hii watu wanamiliki makanisa makanisa ni mali yao na sio mali ya Kristo wanabaguana kuwa huyu alikuwa nje ya mfumo, huyu hajaitwa sawasawa huyu hapa ana dosari hii au ile, Paulo alimtambua Apolo na uwezo wake na hakumpiga vita kwa sababu alikuwa na mchango mkubwa katika kanisa la Mungu,  

 

4.       Aliimarisha makanisa – Apolo alikuwa na huduma ya Ualimu, Huduma hii ina umuhimu mkubwa sana katika kanisa la Mungu, kwa sababu inajenga watu na kuwaimarisha na kuwafanya waamini kuwa imara, inawalinda watu na mafundisho potofu, inawasaidia watu kumjua na kumtii Yesu Kristo, na zaidi sana inawabadilisha waamini wachanga  na kuwapa ukomavu huku ikiwaelekeza kumtumikia Mungu na kuielewa Biblia zaidi ya yote inaandaa viongozi wa kanisa wa baadae na kulifanya neno la Mungu liwe halisi katika maisha kutokana na umuhimu wake alitembelea makanisa mbalimbali na kote huko aliyaimarisha na kuwatia moyo waamini ona:-

 

Matendo 18:27-28 “Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”

 

1Wakorintho 3:5-7 “Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”

 

Tito 3:12-14. “Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi. Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii, wasipungukiwe na cho chote. Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.”

Mambo ya kujifunza kutoka kwa Apolo                

Kuna maswala kadhaa ya kujifunza kutoka kwa Apolo ambayo yanaweza kutuimarisha na kutujenga wahubiri wa kizazi hiki, Apolo alikuwa msomi asiye na majivuo na mtu aliyejua kuitumia elimu yake kwa maslahi ya ufalme wa Mungu, aidha alikuwa mtu anayefundishika na anayekubali kuongezewa kitu na unyenyekevu wake mkubwa uliweza kumbeba niseme katika kiwango sawa na Petro na Paulo kutajwa kwake na Luka japo kwa muktasari lakini maelezo yake yameweza kubeba kitu kikubwa sana ambacho kinatuhakikishia kuwa tuna kitu cha kujifunza kutoka kwake

1.       Kuwa hodari katika maandiko – Apolo alikuwa ni mwenye  Nguvu, Uwezo, Mamlaka  na ujuzi mkubwa katika maandiko na inaelezwa kuwa hii ilitokana na bidii aliyokuwa nayo, kwa hiyo pamoja na mambo mengine kila Mtumishi wa Mungu anapaswa kujifunza kutoka kwa Apolo kwamba tunapaswa kuweka Bidii katika kujifunza Neno la Mungu ili tuweze kuwafaa na wengine, watu wa Mungu hatupaswi kuwa wavivu katika kujifunza maneno ya Mungu badala ya kuzurula na kusoma magazeti ya udaku tunapaswa kutulia na kuwa na bidii katika kulihudumia neno na maombi, mtumishi wa Mungu usiwe mvivu katika kujifunza Neno.

 

Matendo 6:3-4 “Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno”

 

2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”

 

2.       Kufundisha neno la Mungu kwa Usahihi – Apolo alikuwa na juhudi na alitumia ujuzi wake na elimu yake kufundisha kwa usahihi neno la Mungu, na tumeona pia alikubali kujifunza kutoka kwa wengine, ni jambo la kusikitisha sana kuwa katika karne hii kuna watu wanaona kusoma chuo cha Biblia ni ujinga, kimsingi wanamuaibisha Roho Mtakatifu kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa elimu, kuna watu hata leo wanaona kwenda vyo vya Biblia ni kupoteza Muda, ni kupoteza upako na dhana nyingine nyingi za kipuuzi, kufundisha kweli ya Mungu kwa usahihi kunahitaji uwe na ujuzi wa kutosha namna ya kulifasiri neno la Mungu na sio kujitafasiria kama upendavyo tu ziko kanuni za kuzingatia ili uweze kufasiri kwa usahihi na zinahitaji ukae chini

 

2Petro 1:20-21 “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

 

3.       Alitumia kipawa chake kujenga  wengine -  Apolo hakuitumia Elimu yake na ujuzi wake kwaajili ya majivuno au ili aonekane alikuwa msomi hapana aliitumia kuwajenga wengine alikaa katika  kusudi lile lile kubwa la huduma ambazo Mungu ameziweka katika Kanisa kwa kusudi la kujenga mwili wa Kristo hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe na watu wakue na kufika katika cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

 

Waefeso 4:11-14 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

 

Matendo 18:27-28 “Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”

 

1Wakorintho 3:5-7 “Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”

 

Kila mtumishi wa Mungu ana nafsi yake katika mwili wa Kristo, lakini pia kuna nafasi ya mwingine Mwenye kazi ni Mungu, Apolo anatufundisha kuwa Madhabahu inahitaji maandalizi, Kipawa kinahitaji kunolewa kwa kusoma zaidi, Upako unahitaji nidhamu, Ufunuo wa kweli ni maandiko yaani neno la Mungu, Ushawishi una mvuto mkubwa tukiwa na tabia njema kwa sababu hiyo ni lazima tujifunze neno la Mungu, tujijengee uwezo wa kulifundisha, tukubali kukosolewa na kuwarekebisha wengine kwa upendo, lazima tuhakikishe tunamuhubiri Kristo, lazima tuujenge mwili wa Kristo na mwisho tumpe Mungu utukufu, Apolo alikuwa na thamani katika Kanisa kwa sababu alitumia kile alichokijua kumwinua Yesu Kristo na kuwajenga watu wa Mungu

Rev. Innocent Samuel Kamote.

Mkuu wawajenzi mwenye Hekima. 

Jumapili, 18 Oktoba 2026

Kujengwa kwa Hekalu bila kelele!


1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.”      

         


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa Ujenzi wa hekalu la Mungu lililojengwa na mfalme Sulemani unatufundisha mojawapo ya kanuni muhimu sana inayohusiana na kazi ya Mungu hususani katika Kanisa lake, Kwamba Mungu anataka kazi yake ifanyike kwa utulivu bila kelele lakini ikifanyika katika viwango vikubwa sana na vyenye ubora wa hali ya juu, huku kila kitu kikifanyika kwa utaratibu na hekima ya hali ya juu, Hatupaswi kamwe kuchanganya kelele na maendeleo, kazi kubwa na njema zaidi hufanyika mahali ambapo hakuna kelele! Hivi ndivyo Hekalu lile lilivyojengwa!

1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba”

Teknolojia ya ujenzi iliyotumiwa na mafundi wa Suleimani ilikuwa ni ya ajabu na yenye uwezo mkubwa sana, Mafundi walionyesha weledi, uhodari na ustadi kwani walilijenga Hekalu kwa ubora wa hali ya juu sana kiasi ambacho Hekalu hili liliiingia katika idadi ya mojawapo ya maajabu ya kale sana ya dunia, lilikuwa bora na zuri lakini mojawapo ya jambo la kushangaza na la kuvutia sana ni kuwa ujenzi wake ulitawaliwa na utulivu mkubwa na wa hali ya juu, ma tunataarifiwa kuwa chombo chochote cha chuma, kama nyundo, shoka na vinginevyo havikuhusika katika ujenzi, Kwa hiyo Suleimani alihakikisha ya kuwa zinakuwako sehemu kuu mbili moja ni Mgodini au machimboni huko ambako mawe yalikuwa yanachongwa  na eneo la ujenzi ambako mawe yalikuja kupachikwa bila kelele, tukuo hili la kushangaza linatufundisha nini, leo tutachukua muda kujifunza somo hili muhimu kujengwa kwa hekalu bila kelele kwa kuzingatia vipengele vikuu vitatu vifuatavyo:-

·         Kwa nini Hekalu halikuhitaji kelele

·         Maana ya kelele wakati wa ujenzi wa Hekalu

·         Kujengwa kwa Hekalu bila ya kelele

Kwa nini Hekalu halikuhitaji kelele!

Ni muhimu kwanza kufahamu kuwa Mungu katika mpango wake hakuwa ameruhusu chombo chochote cha chuma kihusika katika kutengeneza madhabahu yake, hii ni kwa sababu chombo chochote cha chuma kilikuwa ni najisi kwa sababu vyombo hivyo vilitumika kama silaha za mauaji na visingeliweza kutumika katika madhabau ya kutafuta Amani na Mungu, kwa vile chuma kilitumika maranyingi kutengenezea silaha za vita na umwagikaji wa damu, kuhusisha dhana hizo katika ujenzi wa madhabahu kungeitia unajisi madhabahu, sio hivyo tu chuma ni matokeo ya kazi ya Mwanadamu lakini Jiwe lisilochongwa kwa mikono ni kazi ya Mungu wa mbinguni

Kutoka 20:24-25 “Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng'ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia. Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi.”

Kumbukumbu 27:5-6 “Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake. Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;”

Mungu alikataza kutumia chombo chochote cha chuma kujengea madhabahu kwa sababu vyombo hivyo ni najisi, na sio hivyo tu Mungu alitaka kutufundisha kuwa wokovu ni kazi ya Mungu na sio ya Mwanadamu, kuchonga mawe kunawakilisha nguvu na akili na jituhada za kibinadamu, lakini Mungu alitaa kuonyesha kuwa wokobu na upatanisho ni matokeo ya kazi yake mwenyewe na sio sisi

Sasa wakati wa Suleimani katika ujenzi wa Hekalu Mawe yaliyotumika hayakuwa madogo na wala hayakuwa na maruturutu yaani yalikuwa yamenyooka, waliyaleta mawe hayo yaliyokuwa makubwa, na ya thamani sana ambayo yalikwishachongwa mgodini ona Mafundi wa Suleimani waliamua kuyachongea mawe hayo mbali na eneo la ujenzi lakini wakati wa ujenzi mawe yalikuwa yakipachikwa tu kulingaana agizo la mafundi:-

1Wafalme 5:17-18 “Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa. Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.”

Mawe hayo ya thamani kubwa yalichongwa na kuandaliwa mgodini, mbali na eneo la ujenzi, kisha yakaletwa mjini wakayaweka tayari, Wajenzi wa Suleimani na Hiramu na Wagebali hawa walikuwa wataalamu maalumu wa shughuli ya ujenzi huo wa Hekalu. Inasemekana kuwa jiwe moja lilikuwa na urefu wa mita 27 upana mita 9 kwenda juu mita 13, sawa na madarasa matatu ya kusomea. Kwa kuwa ujenzi huu wa hekalu ulihitaji mawe makubwa sana Suleimani aliamuru wayachonge lakini sio eneo la ujenzi wa nyumba ya Mungu bali yachongwe chimboni, au Kware katika eneo lingine mbali na eneo la ujenzi.

Katika namna zote mbili yaani kimwili na kiroho, uzuri na ufahari na taratibu za ujenzi wa Hekalu ulikuwa ni mradi unaosimamiwa na Roho Mtakatifu maandiko yako wazi kuwa sisi ni kazi ya Roho Mtakatifu. Mradi huu kinabii ulikuwa unazungumzia Kanisa, kila mtu aliyeokoka anafananishwa na jiwe la thamani na katika maandiko sisi tunaitwa mawe yaliyo hai, tunachongwa huko duniani machimbo au kware na tunatolewa huko na kuletwa katika jengo la Mungu na kuenea katika eneo lililokusudiwa, mawe haya yalichongwa kwa agizo la mafundi waashi, na kila jiwe lilitosheleza pale lilipotakiwa!

1Petro 2:4-5 “Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.”

Waefeso 2:19-22 “Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.”

Kila mtu aliyeokolewa ni hekalu la Roho Mtakatifu, kila mmoja ana thamani kubwa sana wote tumechongwa kwa jinsi ya kipekee mgodini na wote tumeletwa ili tuwe nyumba ya Mungu, na kuwa tumuabudu yeye na kuishi kwa amani bila malumbano wala mafarakano, kwa sababu kama mawe ya thamani kila mmoja lina thamani yake na linafaa kukaa pale lilipokusudiwa, endapo jiwe lile limekaa mahali pasipo pake au halijachongwa vizuri huko kware kama ilivyokusudiwa litasababisha kelele na kama nyundo na shoka na vyombo vya chuma vitatumika kulichongea hekaluni litatia unajisi unaona

1Petro 2:4-5“Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.”        

1Wakorintho 3:16-17 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.”     

1Wakorintho 6: 19-20 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

Kwa hiyo tunakubaliana na maandiko kuwa kila aliyeokolewa ni Hekalu la Roho Mtakatifu na kwa umoja wetu ni jengo la Mungu na kila mmoja ni jiwe la thamani lililochongwa kwa ustadi, kutoka katika mgodi au kware ya giza iliyoko duniani na kuletwa na kuungamanishwa na Yesu Kristo ambaye ni jiwe kuu la pembeni, jiwe la msingi, hatujajichagua wenyewe bali ni Mungu ndiye aliyetuchagua na kutuleta katika jengo lake, ili tumtukuze yeye na tena tumuabudu yeye na kumtumikia bila ya hofu yoyote. Kwa hiyo ukisikia kelele wakati waujenzi ujue kuna jiwe limaingia mahali pasipolihusu!

Kwa nini hekalu halihitaji kelele?

Mungu amekusudia kutufanya sisi kuwa watu wake, na amekusudia kutupa utulivu, kelele asili yake ni huko mgodini, wakati wote unapotembelea mgodi au kware utasikia milipuko mikubwa ya kuvunjwa kwa mawe na mafundi wakitumia makrasha au mashine maalumu za kuvunja mawe, huko mafundi watayachonga mawe lakini yanapoletwa katika Hekalu yanakuwa tayari yanafaa kwa ujenzi, kelele zinawakilisha maisha ya duniani, kelele zinawakilisha taabu na uusumbufu wa kuwa nje ya uwepo wa Mungu, Kelele zinawakilisha hofu, kelele zinawakilisha kuwa uwepo wa Mungu umetoweka, kelele zinawakilisha hakuna ujenzi, bali kuna kuvunja vunja na kubomoa, na kuharibu.

Mahali kwenye hofu ya kifo, hofu ya utumwa hofu ya uvamizi, hofu ya uharibifu, hofu za maisha, hofu ya njaa, hofu ya kesho itakuwaje  ni mahali penye kelele  ni nje ya uwepo wa Mungu sio hekaluni, unapokuja kwenye uwepo wa Mungu Roho Mtakatifu tunapata utulivu wa ajabu na amani na tunatengwa mbali na kelele. Mungu amekusudia kumtenga kila mmoja wetu na kelele na kumpa kila mmoja wetu utulivu na amani.

Hutaogopa majeshi hodari yatatapopanga vita kwaajili yako Bwana anajua kuwa wewe ni hekalu lake kwa hiyo majeshi ya upinzani yatanyamazishwa, wakati wote Mungu Kama Mchungaji wetu hutuongoza katika maji ya utulivu

Zaburi 23:1-2, “Bwana ndiye Mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabishi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza”

Israel walipomlilia Musa kwa sababu ya Majeshi ya farao yaliyokuwa yakiwafuatia kwa nyuma ili kuwarejesha tena utumwani, Musa alitoa unabii ya kuwa Bwana atawapigania nao watanyamaza kimyaa! Mungu anafahamu ya kuwa wanadamu wanahitaji utuilivu wanahitaji ukimya! Wanahitaji amani, wanahitaji kuwa mbali na hofu, wanahitaji maisha ya ushindi, wanahitaji kuthibitishiwa kuwa watakuwa mbali na kelele za kila aina:-

Kutoka 14:13-14 “Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya”

Mungu atakustarehesha katika maskani yake utaburudishwa hata kutokee matetemeko, mafuriko sunami na mabadiliko yoyote yale sisi tunaokimbilia kwa Mungu kamwe hakuna atakayeogopa hakuna atakayetetemeshwa ukiwa katika uwepo wa Bwana ushindi unapatikana mapema asubuhi tu

Zaburi 46:1-5 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu. Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.”

Wewe unapokuwa Hekalu la Mungu huna sababu ya kupiga kelele, wala huna sababu ya kutikisika Mungu anafahamu wazi kuwa tunahitaji utulivu, tunahitaji kuwa kimya kisha yeye ataleta ukombozi, Daudi kila alipokuwa anakabiliwa na changamoto za aina mbalimbali alikumbuka anapaswa kutulia kimyaaaa na Mungu huyu yeye mwenyewe atazimaliza kelele

 Zaburi 62:1-2 “Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.”

Wanadamu hawapaswi kusumbuka, kama umechoshwa na kelele za dunia umechoshwa na wavunja mawe, kelele za kware, kelele za migodini wewe mfanye Bwana kuwa ndio mchungaji wako, utapata kila aina ya utulivu, utaandaliwa meza mbele za adui zako machoni pa watesi wako, hutakufa, hutaogopa mauti, utafarijiwa, utapata upako, nafsi yako itahuishwa, Baraka zitafurika nawe utakaa nyumbani mwa Bwana milele yaani kwenye utulivu!

Zaburi:23:1-6 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.”

Maana ya kelele wakati wa ujenzi wa Hekalu

Unaposikia kelele wakati wa ujenzi wa hekalu maana yeke ni nini? Kelel zinaashiria kuna uharibifu umeingia mtu mmoja alizungumza maneno haya yenye hekima kwa lugha ya kingereza “Destructive work is noisy, constructive work is silent” Kwa tafasiri isiyo rasmi ya Kiswahili “Kazi ya uharibifu ina kelele, na kazi ya ujenzi ni ya utulivu” mahali ambapo panafanyika kazi ya Mungu au panapotakiwa kuwa na uwepo wa Mungu ni mahali panapozingatia utulivu, Mahali panapofanyika kazi ya Mungu panatakiwa kuheshimiwa sana  mahali pa ibada hapatakiwi kusikika mlio wa nyundo, wala shoka wala kelele za (crashers) mashine maalumu za kuvunja mawe, mawe yakijakuchongewa Hekaluni yatasababisha kelele na kulitia unajisi hekalu, Nyumba ya Mungu sio mahali pa mazoea ni mahali panapoogopesha na panatisha, mahali maisha ya watu yanakoshughulikiwa kimwili na kiroho hapahitaji kelele wala chokochko za aina yoyote kelele na milio ya nyundo na mashoka ni ishara ya kuingia kwa unajisi

Mwanzo 28:10-17 “Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.”

Kutoka 20:25 “Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi.”

Kumbukumbu 27:5-6“Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake. Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;”

Kwa hiyo unapoona kelele Katika ujenzi wa hekalu maana yake ni kuwa;-

*      Watu wameacha kufanya kazi waliyoitiwa wanafanya biashara nyingine Marko 11:15-17 “Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa; wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu. Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.”

       

*      Watu wakiwa mwilini, yaani udunia ukiingia, hekalu linakuwa na kelele 1Wakoritho 3:1-7  “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”

 

*      Watu wameingiwa na tamaa ona Yakobo 4:1-5 “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?”

 

*      Kila mtu anapokuwa na nia yake 1Petro 3:8-13 “Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya. Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?”

 

*      Watu wema wanaposhikamana na waovu 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”

 

*      Watu wanapoanza kuzaa matunda ya mwili Wagalatia 5:19-21 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.”

 

*      Watu wanapoanza kutafuta utukufu binafsi 3Yohana 1:9-10 “Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.”

 

Diotrefe alikuwa ni mtu mwenye tabia ya kutaka sifa na kutaka kuwa juu kwenye kila kitu cha kanisa neno apendaye kuwa wakwanza katika lugha ya kiyunani linatumika neno “Philoprōteuō” ambalo ni muunganiko wa maneno mawili “Philo” ambalo ni love au kupenda na Proteuo ambalo kwa kiingereza ni Distinction au Preeminece yaani mtu anayependa kutambulika au mtu mwenye kimbelembele, mtu anayependa kuingilia maswala yasiyomuhusu, mtu anayetafuta umaarufu hawa husababisha kelele makanisani

 

*      Watu wasiokubali matengenezo au maandalizi – Mawe yalipokuwa machimboni yalihitaji kukatwa na kutengenezwa ili likakae mahali panapolohuzu, lakini jiwe hiko halikutakiwa likatengenezewe katika eneo la ujenzi wa Hekalu, Mtu asiyekubali kubadilika na anasimamia msimamo yake tu ya zamani hata kama ni ya kipoumbavu anaweza kuwa tatizo katika kanisa na kuleta matatizo yaleyale kila sehemu anakokwenda

 

Mithali 24:3-9 “Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu. Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni. Mtu afikiriye kutenda maovu, Watu watamwita mtundu; Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu.”

Kujengwa kwa Hekalu bila ya kelele:

Ili hekalu liweze kujengwa bila kelele ni lazima kila mmoja wetu akubali kutengenezwa kwanza kabla ya kutaka kuonekana, Mungu alipowachagua wat kuwa watumishi wake aliwapitisha katika shule zake kwanza yaani kila mtu alikuwa na kipindi cha maandalizi kabla ya kuffikia hatua ya kuonekana au kuwa na nafasi ya utawala kwa hiyo huwei kuruka hatua ya machimbo, ukiruka hatua hiyo utatuletea kelele, tujifunze kufundishika, tujifunze kuomba, tujifunze kusikiliza, tusitake ushindi tu wakati wote, tukubali kurekebishwa, tusijijengee tabia ya kutafuta cheo, na tukiwa nacho tusijivune , tujifunze kunyamaza pale ambapo majibu sio lazima, tujifunze kusema kweli, tujifunze kuinua wengine, tusipende kutatfuta mashindan, tujijenge katika neno la Mungu tukubali kuchongwa kama mawe yalivyokuwa yanachongwa, fanya wajibu wako kwa bidi, usishindane na mtu, usitumie muda wako kufuatilia mambo yaw engine, hatujaitwa kuwa mawakala wa wengine, Mungu atatumia watu waliojengwa, Kanisa linahitaji watu wenye vipawa, lakini pia wenye tabia nzuri, linahitaji wahubiri wenye ujasiri, linahotaji viongozi walezi na wenye maono, linahitaji watu wanyenyekevu, hekaluni hakukuhityajika makelele, kwa sababu watu waliandaliwa kabla wewe ni jiwe  la namna gani?  Je utaingia mbinguni na kuwa nguzo katika hekalu la Mungu?

# Mbinguni hakutaingia chochote kilicho kinyonge

Ujenzi huu wa ajabu ambapo mawe yalikuwa yakichongwa mbali, huko kware au mgodini, yaliletwa katika kiwanja cha hekalu yakiwa yamekamilika unatukumbusha wazi kuwa shemu ya kuchongwa watu ni hapa duniani, Roho Mtakatifu hufanya maandalizi ya kutuandaa na kutuchonga tukiwa hapa Duniani, anatukarabati ndani na nje ili tufae kuwa chombo cha sifa na ibada lakini zaidi kwamba baadaye tuweze kufika Mbinguni ambako huko ni eneo la utulivu na hakuna kuchongwa tena tutaingia tukiwa tumekamilishwa baada ya kupitia mchakato wa utakatifu duniani kule mbinguni hakuna chochote kilicho kinyonge kitakachoingia,

Wafilipi 1:6 “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;”

Kila mmoja anapaswa kujiweka wakfu kwa maneno kama yale ambayo Suleimani aliyasema siku alipokuwa akiliweka wakfu Hekalu, alisema

1Wafalme 8:13 “Hakika nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. Maneno ya kiingereza ya mstari huu ni matamu zaidi kwani yanasema hivi “I have indeed built you exalted house, a place for you to dwell in forever” Mungu anataka tuwe makazi yake milele. Lakini atakaa na watu ambao wameandaliwa vizuri kwaajili ya utukufu wake

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!


Jumapili, 11 Oktoba 2026

Watu hawa wana nini, hata wakalia?


1Samuel 11:1-5 “Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni, akakwea na kupanga marago juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi, na sisi tutakutumikia. Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia. Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende mipakani mwote mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutakutokea. Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia. Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.”



 

Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa hapa duniani kuna aina nyingi sana za uonevu na aina nyingine za uonevu kimsingi haziwezi kuvumilika!, Katika maandiko yetu ya msingi, tunapata picha ya aina hiyo ya uonevu iliyowahi kuwakuta watu wa Yabeshi-Gileadi, Mfalme wa wana wa Amoni aliyeitwa Nahashi, aliwatokea na kuwazingira watu wa Yabeshi-Gileadi akitaka kuwapiga vita, watu hao walipojipima waliona uwezo wao ulikuwa mdogo walikuwa wanyonge na wakataka amani na mfalme huyu, na kwa kuona kuwa watu hawa ni wanyonge na wanataka amani naye Nahashi mwamoni, alipata kiburi zaidi na kuwapa sharti la kikatili sana aliwataka ili wawe na amani na yeye basi Israel wote wang’olewe jicho la kulia, jambo hili liliwatia hofu sana wana wa Israel na wakaomba siku saba za kutafakari na kutafuta mtu wa kuwasaidia, walipofika mjini na hasa mji wa Sauli ulioitwa Gibea ya Sauli na kueleza taarifa hizo watu wote wakainua sauti zao wakalia, Sauli alikuwa akitokea mashambani kwa bahati alikokuwa amefuata ng’ombe na kukutana na kilio kikubwa sana na ndipo alipouliza “Watu hawa wana nini hata wakalia?“

Inawezekana unausikia ujumbe huu nawe ukiwa katika hali ya kulia  na unainua sauti yako kulia kwa sababu mbalimbali, umefanyiwa mambo ya kikatili, umedhulumiwa, umetapeliwa na mtu uliyemuamini, uko katika mateso yasiyoweza kuelezeka, unazingirwa na hali zinazokuzidi nguvu, umekata tamaa kuna maeneo unahitaji mwokozi, umefunga siku saba kutafuta msaada, uko kwenye maswali makubwa yasiyokuwa na majibu, unajiuliza msaada wako utatokea wapi, najua leo Sauli hayuko Lakini Roho Mtakatifu yupo na kwa jina la Yesu Kristo atakutokezea msaada leo Mwokozi wetu Yesu Kristo anauliza watu hawa wana nini hata wakalia? Tegemeo letu kuu na la uhakika sio wanadamu, tegemeo letu kuu linatoka kwa Mungu mwenyewe na Roho wa Mungu anaguswa na kilio chako!

Zaburi 121:1-4 “Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.”

Zaburi 124:6-8 “Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.”

Tutajifunza somo hili, “Watu hawa wana nini hata wakalia?” kwa kuzingatia vipengele muhimu vitatu vifuatavyo:-

 

·         Kilio chako sio ishara ya udhaifu!

·         Watu hawa wana nini hata wakalia?

·         Kilio chako ni mwanzo wa wokovu wako!

 

Kilio chako sio ishara ya udhaifu!

1Samuel 11:1-5 “Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni, akakwea na kupanga marago juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi,na sisi tutakutumikia. Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia. Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende mipakani mwote mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutakutokea. Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia. Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.”

Nimuhimu kufahamu kuwa wana wa Israel wakati huu walikuwa ni wanyonge, walikuwa hawana uhakika wa kupata utetezi kutoka kwa wana wa Amoni, na Nahashi alikuwa anajiamini sana na kwa sababu ya uonevu aliokuwa nao aliweka sharti la kikatili kwaajili ya uonevu tu, akijua kuwa sio rahisi kutokea mtu akawasaidia wana wa Israeli, na wana wa Israel walifahamu unyonge wao hivyo walilia, kilio chao kilichojawa na huzuni hakikuwa udhaifu kwani walimpa Nahashi siku saba, wao walilia kwa sababu walimuhitaji mwokozi, waliona kuwa Nahashi,  alionyesha ukatili uliopitiliza na kuwa kama hakuna wa kumshughulikia basi ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa taifa, kwamba watu wa mji wa Gileadi na Israel nzima kila mwanajeshi ang’olewe jicho moja la upande wa kulia,  hii ilikuwa sio tu uonevu lakini adui alikuwa anataka kuweka alama ya milele na ya miaka mingi ya kuwashinda Israel,  wangwezaje kurusha mishale wakiwa na jicho moja, tena la kushoto, wangewezaje kujikinga na ngao, wangewezaje kutumia Kombeo, walilia na kupaza sauti kwa sababu walihitaji mkombozi katika janga hili, Mungu wa Israeli kamwe hangeweza kudharau machozi yao, kilio chao kilimfikia Mfalme mpya Sauli ambaye aliposikia watu wanalia Roho Mtakatifu alimshukia kwa nguvu na kuamsha nia na hari yake ya kutaka kuwasaidia, Maandiko yanatufundisha wazi kuwa Mungu huyajali machozi ya watu wake hasa wanapokuwa katika shida zao:-

Zaburi 34:17-19 “Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”

Zaburi 105:13-15 “Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.”

Kutoka 3:7-9 “BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.”

Inawezekana unausikia ujumbe huu au kuusoma ukiwa katika kuelemewa na huzuni, najua ya kuwa bila shaka unahitaji msaada wa Mungu na neno lake limeahidi kuwa anayajali machozi yako anajua maumivu yako, inawezekana machozi yako ni matokeo ya unyanyaswaji mahali, ni matokeo ya mateso mahali, ni matokeo ya dhuluma, ni matokeo ya uonevu wa pepo, uonevu wa wachawi, mateso yako ni matokeo ya majungu kazini, ni matokeo ya watu wasiopenda maendeleo yako, ni matokeo yauonevu wa unyonge wako, ni matokeo ya umasikini wako, ni maumivu ya moyo uliojeruhiwa, ni kukosa ada, ni kudhulumiwa shamba, kiwanja, nyumba, mirathi, ujane, yatima, uonevu nataka nikuhakikishie ya kuwa Mungu anasikia kilio chako anayajua maumivu yako na anayaona mateso yako, Mungu ameyahifadhi machozi yako na ameyaweka katika kichupa na bila shaka kimejaa

Zaburi 56:8-9 “Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?) Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;”

Watu hawa wana nini hata wakalia?

Sauli alikuwa anarudi kutoka shambani na ng’ombe zake, hakuwa tayari kwa vita alikuwa anatokea kwenye shughuli zake za kawaida lakini alisikia watu wanalia kilio cha kukata tamaa, watu wanaombolezea macho yao, hata kabla hayajang’olewa, Roho Mtakatifu alimjia kwa nguvu mara tu aliposikia habari za mateso ya watu wake na kukatatamaa kwao, hasira yake ikamuwaka akawaambia watu wa Yabeshi-Gileadi wasilie kwani kesho watapata wokovu wakati wa jua kali yaani mchana kweupeee, leo nasema usilie, utapa wokovu wako wakati wa jua kali.

1Samuel 11:5-11. “Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi. Na roho ya Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana. Naye akatwaa jozi ya ng'ombe, akawakata-kata vipande, kisha akavipeleka vile vipande mipakani mwote mwa Israeli kwa mikono ya wajumbe, kusema, Ye yote asiyetoka nyuma ya Sauli na Samweli, ng'ombe zake watatendwa vivi hivi. Basi utisho wa Bwana ukawaangukia wale watu, wakatoka kama mtu mmoja. Naye akawahesabu huko Bezeki; Waisraeli walikuwa mia tatu elfu, na Wayuda thelathini elfu. Nao wakawaambia hao wajumbe waliokuja, Waambieni watu wa Yabesh-gileadi, Kesho, wakati wa jua kali, mtapata wokovu. Basi wale wajumbe wakaenda, wakawaarifu watu wa Yabeshi; nao walifurahiwa. Kwa hiyo watu wa Yabeshi walisema, Kesho tutawatokea, nanyi mtatufanyia yote myaonayo kuwa ni mema. Ikawa, kesho yake, Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu; nao wakaingia katikati ya marago kwenye zamu ya asubuhi, wakawapiga Waamoni hata wakati wa jua kali; kisha ikawa wale waliosalia wakatawanyika, hata wasiachwe wawili wao pamoja.”

Mungu anafanya hivyo hata leo, Mungu anaweza kuamsha watu kwaajili yako, Mungu anaweza kukufungulia mlango, Mungu anaweza kubadilisha hali yako ya kushindwa kuwa ushindi, Mungu anaweza kubadilisha hali yako ya unyonge kuwa ujasiri, Mungu anaweza kuwatumiwa wale wanaoonekana kuwa wa kawaida kuleta wokovu, Mungu anakuahidi leo kuwa adui zako watapigwa mchana kweupee, haitakuwa kwa kificho, haitakuwa wakati wa asubuhi, wala haitakuwa wakati wa jioni ni mchana wakati wa jua kali wokovu wako utaonekana na kila mtu

Zaburi 34:15-17 “Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao. Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote.”

Zaburi 46:1-3 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”

Zaburi 136:10-12 “Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.  Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.”

Kumbukumbu 26:6-8 “Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito.  Tukamlilia Bwana, Mungu wa baba zetu; Bwana akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu.Bwana akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu;”

Wakati unapokuwa unalia na unahisi kama hujaona mabadiliko yoyote usufikiri ya kuwa Mungu amekusahau, kwa sababu bado hujaona dalili zozote Roho Mtakatifu hutulia lakini huamka na hasira zake hufurika yeye ndiye anayeitwa mkono ulionyooshwa yeye atafanyia kazi hitaji lako na atatumia njia mbalimbali kukuokoa na kukusaidia lakini kumbuka mkono wake ulionyooshwa utashughulika na kila aina ya uonevu Mungu hawezi kamwe kufumbia macho aina yoyote ya uonevu kilio chako kinamgusa kuliko unavyoweza kufikiri, yeye anauliza wakati wote watu hawa wana nini hata wakalia? Na hasira zake zinawaka akisha kujua ni kwanini unalia ananyoosha mkono wake na nikuhakikishie wokovu wako utapatikana mchana wakati wa jua kali!  Wazi wazi bila kificho adui wengine hawapaswi kushughulikiwa usiku wanapaswa kuoigwa mchana kweupee ili habari zienee mapema kuwa wametandikwa huku 

Kilio chako ni mwanzo wa wokovu wako!

Watu wa Yabeshi-Gilead walipoanza kulia ndipo Mungu alipowaletea msaada na kuwapa ushindi mkubwa, watu hawa waliokolewa kabisa na aibu iliyokuwa ikiwakabili, aibu yao ikageuzwa kuwa shangwe, ni muhimu kuwa na ufahamu kuwa unapoanza kulia leo sio ishara ya kushindwa, adui zako wanaweza kudhani kuwa wamekuweza kwa sababu ya sharti gumu walilokuwekea, lakini kumbe wanakuandalia safari ya kuelekea kwenye ushindi wako,  kilio chako ni sehemu ya mwanzo ya wokovu wako itakayokuletea ukombozi mkubwa, maandiko yanaonyesha kuwa unaweza kulia usiku na asubuhi ikawa ni furaha

Zaburi 30:2-5 “Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya. Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni. Mwimbieni Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake. Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.”    

Mungu aliyewaokoa watu wa Yabeshi ni yule yule anayeweza kukuokoa na wewe kutoka katika ukatili, dhuluma, uonevu na maumivu unayoyapitia, kilio ulicho nacho sasa au leo kitageuzwa kuwa furaha! Kaka yangu na dada yangu unayelia usikate tamaa, swali la Sauli lilikuwa ni swali kutoka kwa Mungu watu hawa wana nini hata wakalia? Swali hili linajibiwa na Mungu mwenyewe yeye ndiye anajua ni kwa nini unalia, anayajua maumivu yako anaujua uchungu wako na yuko tayari kuingilia kati machana wa jua kali Bwana analeta wokovu! Mungu wangu aliyenilinda mimi na watu wabaya akamtuma malaika wake na kunitetea siku zote za maisha yangu atakutetea nawe pia katika jina la Yesu Kristo mwana wake aliye hai amen! Watu hawa wana nini hata wakalia?

Zaburi 56:8-11 “Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?) Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu; Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?”

 

Rev. Innocent Samuel Kamote.

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima.