Jumapili, 31 Januari 2016

DADA MREMBO AKAADHIRIWA NA TUMBO LA KUHARA!



Maswahibu haya niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ingawa hayakuwa yamenipata mimi lakini aliyekumbwa nayo basi niite alikumbwa na fedhea la mwaka  na nimeona nikusilimie ili uweze kujifunza na wengine wajue kwa faida yao.

Ilikuwa mwaka jana nasafairi kutoka Dar kwenda Arusha kwa ajili ya kwenda kula sikukuu ya Krismasi, wale wanaosafiri na  magari hayao  nafikiri wanafahamu kuwa wakifika katikati kwenye safari  wenye mabasi hayo huyaingiza hoteli  iliyoko karibu na njiani  ambayo sipendo kuitaja  jina  na kondakta  akaamuru  abiria washuke wakapate chochote lakini kwa dakika kumi , kama kawaida kwa sababu mimi nilikuwa karibu na mlango  nilikuwa wa kwanza kushuka  nikawahi hotelini  na kuangiza bisikuti pakiti mbili na soda  nikawa nimekaa kwenye kiti naendelea kula taratibu huku nikiangalia saa yangu  ya kwenye simu ya mkononi ili niende na muda wa kondakta wa basi.

 Tumbo la kuhara huwa halina Adabu!

Wakati naendelea ghafla  nikasikia sauti ya dada mmoja  akiita anko samahani naomba hiyo chumvi hapo mezani kwako, nilipogeuka nyuma ghafla  nikamwona aliyekuwa akinisemesha  ni dada mmoja aliyekuwa akila wali kwa mchguzi wa nyama pamoja na kachumbari, alikuwa ni msichana mrembo  kwa kweli jambo lililonifanya wakati nanyanyua ile chumvi kuimpa nikodoe macho kidogo kwa maana nyingine ni kama nilihamaki, muda wa kuondoka gari  ukawa umewadia  kwani gari lilishaanza kupiga  honi nami nikaelekea kwenye  basin a likaanza safari kuelekea Arusha  Baada ya safari kwa masafa ya kutosha nilimuona Yule dada akizungumza na kondakta wa basi jambo Fulani, Kondakta aliondoka na kumfuata dereva ambaye aliongea naye kwa sekunde kadhaa, basi lilisimama na ikatangazwa kwamba abiria wakajisaidie Nilijua Yule dada anataka kujisaidia, Abiria walirudi basini  na basi likataka kuondoka , lakini abiria mmoja alitahadharisha kuwa Yule dada aliyeomba basi lisimame alikuwa hajarudi na , ilibidi akina mama watumwe kwenda kuangalia kulikoni.

Baada ya muda tukaona wale akina mama waliokuwa wakienda kumfuatilia wakirudi na Yule dada aliyeniomba chumvi taratibu wanarudi kutoka nje  na kuingia kwenye basi, Na alipoingia alikwenda moja kwa moja kukaa kwenye siti yake huku abiria wengine wakimpa pole na wengine wakimwangalia tu bila kusema chochote na basi likaanza safari yake, lakini basi lilipotembea kama dakika hamsini hivi nikamwona Yule dada akinyanyuka tena kumwendea kondakta, na kwa sababu nilikuwa karibu na mlango  niliposikia maongezi ya safari hii kwani kondakata alikuwa akiongea na Yule dada kwa sauti kubwa baada ya kumuomba kuwa gari lisimame tena aende kujisaidia kondakta akaijbanza naye  kwa kumwambia haiwezekani  bwana tukimbize gari tukuwahishe hospitali, sisi tunakwenda kwa ratiba na kwa muda njiani trafiki watatukamata, Ghafla nikaona Yule dada akirukia mlango wa basi na kutaka kuufungua  huku basi linakwenda, ndipo abiria wengine wa basi wakataharuki  kulikoni huku wengine wakisimama kwenye viti vyao baada ya kuona tukio lile wakati Yule dada akiurukia mlango na kujaribu kuufungua  na kondakta kujaribu kumzuia,  nikamwona amechuhumaa chini  na huku amejiinamia na baada ya muda mfupi hariufu ya kinyesi ikatanda ndani ya basi zima na hususani  kwa siti za mbele , Na baadaye ikaonekana kuwa amejiharishia  tena vibaya mno, Ndipo tena wasamaria wema walipojitokeza na kwenda kumsaidia  na kubadilisha zile nguo kwa kumtaka atoke nje ya basi  lakini safari hii basi lilikuwa kwenye maeneo ya watu na sio zile sehemu maarufu za uchimbaji dawa, ndipo wakati huo ukazuka mjadala , wengine wakisema ashushwe akabadilishwe hivyohivyo mbele za watu nje ya basi, wengine wakisema asaidiwe ndani ya basi, wengine wakisema basi liwahishwe mpaka porini, wengine wakafungua mabegi yao kutoa mashati kumfunika wengine wakarudi viti vya nyuma kukimbia harufu ilimradi ilikuwa vurugu tupu tu.
Wakati hayo yakiendelea kukasikika kilio kingine cha sauti Para! t Para! Prataaaaapaa! Kumbe alikuwa amefanya tena vitu vingine palepale mlangoni, hayo yote yakiendelea akatokea mzee mmoja wa makamo  ndani ya basi akapaza sauti kwa nguvu nyie akina mama watu wa ajabu sana Yaani mwenzenu anaadhirika , badala ya kutoa khanga zenu mkaweka uzio wa dharula  hapo nje na kumsaidia mnaangalia tu,  Kweli wazo lile likafanya kazi kwa wengine hasa akina baba kufungua mabegi yao na kujitolea shuka na wengine waliotoa dawa ambazo walisafiri nazo wakati huo wakazi wa eneo lile walipoona uzio wa akina mama wamezunguka wakajazana kuona au kutaka kujua kulikoni, zoezi lile likakamilika  na safari ikaendelea  ambapo  dada Yule dada alishuka Moshi name nikaendelea  hadi Arusha huku nikijiuliza fedheha yote ile ya kujiharishia kwa Yule Dada huenda  shauri ya mikachumbari ile jamboa ambalo linanifanya hadi leo kuwa mwangalifu na kula hovyo hovyo njiani niwapo safarini.

AKAOMBA AACHIWE MKEWE KWA MAGOTI!



Kisanga hiki hakikunikuta mimi  lakini niliguswa sana na jamaa mmoja ambeye alifehdeheka kupita kawaida, sikuwa namjua jamaa huyu lakini nilimfahamu  kwenye ofisi moja, huyu jamaa alikuwa amefika hapo ofisini  kwa shughuli zake na mwenye ofisi, nilipochungulia na kumwona mgeni huyo nilitaka kurudi  nyuma  yaani kuacha  kuingia ofisini. Lakini mwenye ofisi aliniita na kuniambia niingie tu kama vile hawakuwa na jambo la siri na Yule mgeni wake.

Niliingia na kuwasalimia wote, mwenye ofisi na Yule mgeni. Kabla sijaanza kuzungumza chochote Yule mgeni alianza kuzungumza kuhusu jambo ambalo nadhani walishaanza kuzungumza na Yule jamaa yangu yaani mwenye ofisi
 
Mapeniz ni Darasa kubwa sana Duniani!


“Kama hivyo nilivyokuambia naomba sana unilindie ndoa yangu tafadhali naomba sana , Najua una hela na mke wangu anakupenda lakini ona huruma basi nionee huruma “ alisema Yule mgeni kwa sauti ambayo haikuwa ya mzaha  hata kidogo, Yule mwenyeji wangu yaani mwenye ofisi aliingilia kati na kusema “ sikiliza wee mtu, mimi natembea na mkeo lakini siyo kosa langu Nataka nikuambie ukweli kwamba sikuwahi kumtongoza bali mwenyewe ndiye alinianza na hata jana nimemwambia aachane na mimi lakini haelewi, sijui nimempa kitu gani kimemnogea Yule mtoto’ alisema na kucheka kidogo, 

Awali nilidhani ni mzaha wanafanya au labda kuna watu wanawaiga, lakini baadaye nikajua kuwa haukuwa mzaha nilipomuona Yule mgeni akiwa anatokwa na machozi. Niliogoipa sana baada ya kubaini kwamba ule haukuwa mzaha ni ukweli halisi, najua hata wewe itakuwa ni vigumu kwako kuamini jambo hili lakini nakuomba uamini.

Ati ndugu yangu mke wa mtu anakufuata anakung’ang’ania ufanye naye mapenzi wewe kama rijali utafanya nini? Yule mwenyeji wangu aliniuliza swali ambalo jibu lake lilikuwa rahisi kwangu. Lakini nisingeweza kulitoa. Nilitaka kumjibu kwamba ni kweli hata mama yako akikuambia ufanye naye mapenzi na kukung’ang’aniza inabidi ufanye kwa sababu anataka? Badala yake nilimwambia kama hujui kuwa ameolewa na yuko salama  unaweza kukubali Yule jamaa yangu alicheka  na kusema umemwona mke wa huyu jamaa bwana au unasema tu huyu jamaa ana mke sio wa kawaida  aisee ni mzuri sana . Nilijitahidi kukataa mwanzoni lakini nikashindwa, alisema akiwa hana wasiwasi, Yule mgeni aliporomoka kutoka kitini na kupiga magoti mbele ya meza ya yule mwenyeji wetu “Tafadhali bwana mkubwa niachie ndoa yangu mke wangu akiondoka si nimekuambia nitaona maisha hayana maana, kama mnafanya fanyeni lakini usiwe unamchukua usiku anawaacha watoto…’

Yule mwenyeji alimkatisha yuile jamaa ambaye kitendo chake cha kupiga magotio kwa mtu anayetembea na mkewe aliniingiza kwenye fedheha kubwa ajabu, nataka nikuambie kuwa nilijisikia kama nimevuliwa nguo na nina tembezwa mitaani, Nilikuwa natetemeka kidogo nilimuuliza Yule jamaa yangu hivi ni siriasi kweli au mnafanya mzaha? Yule jamaa yangu alisema nashangaa sana yaani mambo ya mapenzi yanakuja ofisini je mke wangu akitokea hapa sasa hivi akauliza sababu ya wewe kupiga magoti utasemaje? Yule mwenyeji alimuuliza mpiga magoti

Mpiga magoti aliinuka na kusema basi naomba uniachie mke wangu, halafu alinigeukia mimi na kuniambia braza mwambie ndugu yako namwomba sana aniachie ndoa yangu…’Ilibidi kwa kweli nisimame na kumuaga jamaa yangu kwa kumwambia nitapita baada ya dakika kumi malizaneni kwanza…’ jamaa yangu alitaka kunizuia nisiondoke Lakini kabla hajasema neno nilikuwa nimeshafika nje na kuondoka nani anataka kuona upuuzi kama huo duniani? Ambaye ni mstaarabu? Kwa ujumla niliumia sana sio siri najua utataka kujua walimalizana vipi na Yule jamaa mimi sio mbeya je angekuwa ndio mkeo? We ungefanyaje? Yesu alisema llolote usiotaka kufanyiwa na watu usiwafanyie na wewe.

NIKA BWABWANYA MWANAUME!



Nilikuwa nina miezi kama mitatu tangu kuoa kwangu, Ilikuwa ni juni mwaka 2003, mke wangu alikuwa akiniamini sana na hata wazazi wake hasa mama yake kwani alinifundisha shule ya msingi wakati akiwa mwalimu mwaka huo 2003 alistaafu.

 
Mdomo ulikipoza Kichwa !

Siku moja nilikuwa nyumbani na mke wangu alikuwa ameenda kwao, ilikuwa ni mapema bado kama saa nane  kwa hiyo sikuwa nategemea kumuona  kwa wakati ule  tulikubaliana kuwa angerudi jioni, nilikuwa nimekaa sebuleni nikiangalia televisheni, mara simu yangu ikaita, nilipunguza sauti tv yangu hadi mwisho na kupokea simu, ilikuwa inatoka kwa msichana ambaye nilikuwa nimeanza uhusiano naye kama mwezi mmoja nyuma , ukweli hadi leo najiuliza niliweza kufanya vipi jambo kama lile kwani sikuwa kabisa mpenda wanawake  na nilikuwa pia naheshimu ndoa yangu.

Nilipokea simu na kuanza kuzungumza naye usijali mpenzi kesho nitakuona …Nani first Lady? Hana neno huyu wala hawezi kunishtukia, kwani ananizimia sana, nimemshika kwelikweli, unajua nini ulichelewa kidogo tu kujitokeza kwangu lakini pale madhabahuni kabla ya miezi mitatu tu ulitakiwa uwe wewe na sio yeye niliendelea kubwata na kubwabwanya lakini hata hivyo hakujaharibika neno huku nimefungwa pingu za kanisani lakini moyo wangu uko kwako mpenzi, nakuhakikishia kwamba  nikiwa nawe kila kitu kinabadilika  kinakuwa super, Naanza kumchoka jamaa kwani hata nikiwa naye naiona sura yako kwake …”  ilinibidi ninyamaze kwani nilistuka kwa namna ambayo hata ingeweza kuniua kwa shinikizo unajua nini ? Nilimuona mke wangu akiwa na mama yake  wakiwa wamesimama, kwa kweli nilijifaragua sana kutaka kuwakaribisha  lakini walivyokuwa wakinitazama  nilinywea na sauti ikakauka  ‘Ulikuwa unaongea nini  na nani mke wangu aliuliza nilibabaika na kabla sijasema  ni..ni.. Jamaa mmoja …’ niliwashwa kibao cha maana sana  shavuni na mke wangu . Halafu alinivaa na kunitupa chini nilikuwa sina nguvu kabisa bwege hasa , kweli kufumaniwa ni kubaya sana, mama mkwe aliingilia kati na kuamua kumuondoa mwanae wapangaji upande wa pili wa nyumba nao walifika na kutuamulia. 

Mama mkwe alimshika mkono binti yake na kumwambia twende acha kila kitu humu ndani usichukue chochote inatosha kwa haya tuliyoyaona waliondoka na binti yake, nilibaki nikiwa nimefedheheka vibaya sana, wapangaji wa upande wa pili wa nyumba walionekana kufurtahia sana dhahama ile, kwani tulikuwa tukiwasema sana kuwa ndoa yao ni ya kuunga na gundi, Najua unataka kujua ilikuwaje baada ya pele huo ndio unaitwa umbeya!

Lakini kwa kukukata kiu yako ya umbea ni kwamba baada ya pale tulikuja kurudiana, Alikuja kunisamehe na baada ya kumueleza ukweli wote kwa kweli siku hizi nikiona mwanamke nisiyemjua ananichekea nafunga viatu vizuri ili kuanza mbio za marathoni zisizo na malipo maana nilikwisha kuyapata.
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Yesu Kristo NI Alfa na Omega!



ALFA NA OMEGA.
     “Alfa” ni herufi ya kwanza katika alfabeti za lugha ya kiyunani  kama ilivyo “A” katika alfabeti za Kiswahili na Vivyo hivyo “Omega” ni herufi ya mwisho katika alfabeti za kiyunani kama ilivyo “Z” katika alfabeti za Kiswahili.  Yesu Kristo anaposema hivyo anamaanisha kwa undani sana kwamba hata herufi zote za Alfabeti  zinamzungumza yeye katika lugha yoyote duniani na siyo kiyunani pekee Yesu ni Mwanzo na mwisho wa alfabeti zote zote humtaja yeye na kumtukuza hii pia humaanisha ya kuwa yeye ni yote katika yote.



YESU NI A.
Yesu kristo anaitwa A yaani ni Afya yetu Zaburi 42;5.11, 43;5 Yeye ni Afya yetu na Mungu wetu tunapokuwa na upungufu wowote katika Afya zetu yeye3 alikuja ili sisis tuwe na uzima tena tuwe nao tele Yohana 10;10 Yeye pia ni Ahadi ya uzima 2Timotheo 1;1 mganga yeyote akikuhaidi uzima  ahadi hiyo inaweza isiwe na uhakika lakini ahadi za Yesu ni ndiyo yaani ni hakika 2Wakoritho 1;19-20 Hesabu 23;19. Anaitwa pia Aliye juu Zaburi 46;4 wengine wako chini Yeye yu juu ya yote Yeye pia ni Aliyeko,Aliyekuwako na Atakayekuja Ufunuo 1;8,Yeye pia ni Amani ya Bwana. Zaburi 129;8 Yeye ni Amina Ufunuo 3;14. Anaitwa Arabuni ya roho zetu Efeso 1;14 yaani ni muhuri au uhakika.

YESU NI B.
Yesu huitwa Bwana wa mabwana Ufunuo 19;16 na pia huitwa Bwana mkubwa Luka 8;24 Huitwa pia Baraka ya Bwana  Kumbukumbu 33;23 ni Bwana wa vita Yoshua 10;14 kutoka 15;3 ni Bwana harusi wa kanisa Mathayo 9;15

YESU NI C.
Ni chakula cha uzima  Yohana 6;35 vyakula vingine hutupa uzima wa muda tu chakula hiki hutupa uzima wa milele yeye ni Chanda cha Mungu Kutoka 8;19 huitwa chapa ya nafsi ya Mungu Waebrania 1;13 na ni chemichemi ya maji ya uzima Yeremia 2;13 pia huitwa Chipukizi la haki Zekaria 6;12

YESU NI D.
Yesu Kristo ni dhabihu yetu Waefeso 5;2 alitolewa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu na kwa kupigwa kwake sisi tunmepona Isaya 53;5 hatuna haja tena ya kutoa kafara nyingine kama mbuzi kuku, na kuwapelekea waganga wa kienyeji

YESU NI E.
Yesu pia huitwa Elimu ya utukufu wa Mungu angalia katika 2Koritho 4;6 hakuna aliye na Elimu yenye utukufu kama Kristo wanadamu wenye madigrii kibao wana sehemu ndogo sana ya maarifa ukilinganisha na Kristo mwenye maarifa yote, ikumbukwe kuwa maarifa yote yanatoka kwake.

YESU NI F.
Yesu anapotajwa kama F katika Maandiko yeye ni Fadhili za Mungu Zaburi 57;3 tukikosa fadhili kwa wanadamu tumwendee Yesu yeye ni mfadhili wa ajabu atatupa mahitaji yetu yote Bure bila ya masharti.Huitwa pia Fahari ya Yakobo Zaburi 47;4 Yeye ni fahari yetu hatupaswi kumuonea aibu yeye pia ni Faraja Yetu au faraja ya Israel Luka 2;25,Ni fimbo ya Mungu Kutoka 4;20 na ni furaha ya bwana Nehemia 8;10

YESU NI G.
Yesu Kristo huitwa Gumegume Isaya 50;7 Gumegume ni aina Fulani ya jiwe ambalo ni gumu sana kwa kiingereza huitwa Flint mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika na yeyote ambaye litamwangukia jiwe hili litamsagasaga tikitiki Mathayo 21;44 Chochote kilichokigumu magonjwa mikosi balaa tuvilete kwa Yesu vitapondwapondwa kabisa

YESU NI H.
Yesu Kristo anatajwa pia kuwa ni Haki ya Mungu 2Koritho 5;21 hakuna mtu yeyote atakayehesabiwa haki mbele za Mungu isipokuwa katika Yesu Kristo aliye haki ya Mungu Warumi 3;26,5;1 Yeye pia ni Hakimu  Zaburi 50;6 ndiye  atakaye uhukumu ulimwengu Kristo pia ni Hekima yetu kwani huitwa Hekima ya Mungu 1Koritho 1;30iwapo tunalo hitaji la Hekima leo

YESU NI I.
Yesu huitwa pia Immanuel Mathayo 1;23 yaani ni Mungu pamoja nasi anatajwa pia kuwa ni Ishara Yesu ni udhihirisho wa uwezo wa Mungu mahali alipo kuna ishara Isaya 11;10

YESU NI J.
Jina la Yesu ni Jina lipitalo majina yote Wafilipi 2;9 si hilo tu Yesu ni Jiwe kuu la pembeni Matendo 4;11 Jiwe lililo hai 1Petro 2;24. Uimara wetu unatokana na jiwe kuu la msingi la pembeni na lililo hai yaani Yesu Kristo bila yeye hakuna uimara wowote

YESU NI K.
Yesu anaitwza kichwa cha kanisa Waefeso 5;23 yaani ndiye kiongozi mkuu wa kanisa lote,huitwa pia kiongozi mkuu wa wokovu wetu Waebrania2;10. Katika Waebrania 7;17;10;21 Ni Kuhani mkuu maana yake ndiye mpatanishi wetu mkuu 1Timotheo 2;5 yeye pia huitwa kweli Yohana 14;6 pia ni Kimbilio letu

YESU NI L.
Yesu Kristo ni Lulu moja ya thamani kubwa Mathayo 13;46 tukimpata katika maisha yetu tumepata lulu moja ya thamani kubwa yeye ndiye wa kumshika na sio dini Ufunuo 3;11 Dini au dhehebu Fulani sio lulu moja ya thamani

YESU NI M.
Ni Mfalme wa Wafalme Ufunuo 19;16 yapasa tumuogope na kumtii na kumuheshimu Ni Mfinyanzi wetu Isaya 64;8,Yeremia 18;1-6. Huitwa Mchungaji mkuu wa kondoo Waebrania 13;20 ni Mchungaji mwema Yohana 10;14. Ni Mlango wa kondoo Yohana 10;7 ni Moto ulao Waebrania 12;29, ni Mungu mkuu Tito 2;13 ni Mwana wa Mungu Yohana 9;35-37 ni Mwana wa Adamu Mathayo 26;64 Ni Mwokozi Tito 1;4,Mwalimu Yohana 3;2,na Muhukumu wetu siku ya mwisho Yohana 5;22

YESU NI N.
Yeye ndiye Nabii yule Yohana 6;14 huitwa pia Njia pekee ya kuingia mbinguni Yohana 14;6 ndiye Nyota ya kung’aa asubuhi Ufunuo 22;16 au Nuru ya ulimwengu Yohana 8;14 akiwa ndani yetu hatuta kwenda gizani kamwe yeye ni Neno Yohana 1;1

YESO NI O.
Yeye hutajwa kama Ondoleo la dhambi zetu Matendo 10;43 tukimuamini hutupa ondoleo la dhambi 

YESU NI P.
Pendo la Mungu Warumi 5;5 ni chimbuko la upendo la kweli

YESU NI R.
Ni Rafiki Luka 12;4.pia ni mwalimu mkuu sana anayeheshimika Rabi au Rabon Yohana 20;16

YESU NI S.
Yeshu huitwa Shahidi aliye mwaminifu Ufunuo 1;5 ni Simba wa kabila la Yuda Ufunuo 5;5

YESU NI T.
Tabibu mkuu Mathayo 9;11-12,Yeye ni Tumaini letu kuu Zaburi 71;5 ni Taraja letu Zaburi 71;5 ni Tegemeo letu Yeremia 17;5-8.

YESU NI U.
Yesu Kristo ni uzima wa milele Yohana 14;6 na ukombozi wetu 1Timotheo 2;6 na ndiye upanga wa utukufu Kumbukumbu 33;29 upanga huu unaweza kushughulikia na yeyote anaye kutesa

YESU NI V.
Yesu ni Vazi jipya Luka 5;36 Torati ni vazi kuu kuu lakini Kristo ni vazi jipya

YESU NI W.
Ni Wokovu wetu Zaburi 27;1 tukiwa na Yesu hatupaswi kumuogopa mtu awaye yote Hesabu 23;23 hata wachawi hatupaswi kuwaogopa kwani Yesu ni wokovu wetu

YESU NI Y.
Huitwa Yesu Mathayo 1;21 yeye ndiye aokoanye watu wake na dhambi zao bila Yesu hakuna wokovu.Yeye  ni Yeye yule jana leo na hata milele,ni Yeye ajaye wala hatakawia Ebrania 10;37.

YESU NI Z.
Yesu ndiye Zeri ya Gileadi Yeremia 46;11 nyakati za Biblia kulikuwa na dawa iliyoitwa zeri ambayo ilikuwa ikipatikana huko Gileadi dawa zote zikishindwa ndipo ilibidi itumike zeri ya Gileadi ilikuwa ni dawa isiyoshindwa ni zaidi ya muarobaini Zeri ni Yesu Kristo dawa isiyoshindwa kila kitu kinaposhindikana ndipo  tumuitie Yesu yeye hashindwi kitu.

Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima