Jumapili, 18 Oktoba 2026

Kujengwa kwa Hekalu bila kelele!


1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.”      

         


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa Ujenzi wa hekalu la Mungu lililojengwa na mfalme Sulemani unatufundisha mojawapo ya kanuni muhimu sana inayohusiana na kazi ya Mungu hususani katika Kanisa lake, Kwamba Mungu anataka kazi yake ifanyike kwa utulivu bila kelele lakini ikifanyika katika viwango vikubwa sana na vyenye ubora wa hali ya juu, huku kila kitu kikifanyika kwa utaratibu na hekima ya hali ya juu, Hatupaswi kamwe kuchanganya kelele na maendeleo, kazi kubwa na njema zaidi hufanyika mahali ambapo hakuna kelele! Hivi ndivyo Hekalu lile lilivyojengwa!

1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba”

Teknolojia ya ujenzi iliyotumiwa na mafundi wa Suleimani ilikuwa ni ya ajabu na yenye uwezo mkubwa sana, Mafundi walionyesha weledi, uhodari na ustadi kwani walilijenga Hekalu kwa ubora wa hali ya juu sana kiasi ambacho Hekalu hili liliiingia katika idadi ya mojawapo ya maajabu ya kale sana ya dunia, lilikuwa bora na zuri lakini mojawapo ya jambo la kushangaza na la kuvutia sana ni kuwa ujenzi wake ulitawaliwa na utulivu mkubwa na wa hali ya juu, ma tunataarifiwa kuwa chombo chochote cha chuma, kama nyundo, shoka na vinginevyo havikuhusika katika ujenzi, Kwa hiyo Suleimani alihakikisha ya kuwa zinakuwako sehemu kuu mbili moja ni Mgodini au machimboni huko ambako mawe yalikuwa yanachongwa  na eneo la ujenzi ambako mawe yalikuja kupachikwa bila kelele, tukuo hili la kushangaza linatufundisha nini, leo tutachukua muda kujifunza somo hili muhimu kujengwa kwa hekalu bila kelele kwa kuzingatia vipengele vikuu vitatu vifuatavyo:-

·         Kwa nini Hekalu halikuhitaji kelele

·         Maana ya kelele wakati wa ujenzi wa Hekalu

·         Kujengwa kwa Hekalu bila ya kelele

Kwa nini Hekalu halikuhitaji kelele!

Ni muhimu kwanza kufahamu kuwa Mungu katika mpango wake hakuwa ameruhusu chombo chochote cha chuma kihusika katika kutengeneza madhabahu yake, hii ni kwa sababu chombo chochote cha chuma kilikuwa ni najisi kwa sababu vyombo hivyo vilitumika kama silaha za mauaji na visingeliweza kutumika katika madhabau ya kutafuta Amani na Mungu, kwa vile chuma kilitumika maranyingi kutengenezea silaha za vita na umwagikaji wa damu, kuhusisha dhana hizo katika ujenzi wa madhabahu kungeitia unajisi madhabahu, sio hivyo tu chuma ni matokeo ya kazi ya Mwanadamu lakini Jiwe lisilochongwa kwa mikono ni kazi ya Mungu wa mbinguni

Kutoka 20:24-25 “Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng'ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia. Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi.”

Kumbukumbu 27:5-6 “Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake. Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;”

Mungu alikataza kutumia chombo chochote cha chuma kujengea madhabahu kwa sababu vyombo hivyo ni najisi, na sio hivyo tu Mungu alitaka kutufundisha kuwa wokovu ni kazi ya Mungu na sio ya Mwanadamu, kuchonga mawe kunawakilisha nguvu na akili na jituhada za kibinadamu, lakini Mungu alitaa kuonyesha kuwa wokobu na upatanisho ni matokeo ya kazi yake mwenyewe na sio sisi

Sasa wakati wa Suleimani katika ujenzi wa Hekalu Mawe yaliyotumika hayakuwa madogo na wala hayakuwa na maruturutu yaani yalikuwa yamenyooka, waliyaleta mawe hayo yaliyokuwa makubwa, na ya thamani sana ambayo yalikwishachongwa mgodini ona Mafundi wa Suleimani waliamua kuyachongea mawe hayo mbali na eneo la ujenzi lakini wakati wa ujenzi mawe yalikuwa yakipachikwa tu kulingaana agizo la mafundi:-

1Wafalme 5:17-18 “Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa. Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.”

Mawe hayo ya thamani kubwa yalichongwa na kuandaliwa mgodini, mbali na eneo la ujenzi, kisha yakaletwa mjini wakayaweka tayari, Wajenzi wa Suleimani na Hiramu na Wagebali hawa walikuwa wataalamu maalumu wa shughuli ya ujenzi huo wa Hekalu. Inasemekana kuwa jiwe moja lilikuwa na urefu wa mita 27 upana mita 9 kwenda juu mita 13, sawa na madarasa matatu ya kusomea. Kwa kuwa ujenzi huu wa hekalu ulihitaji mawe makubwa sana Suleimani aliamuru wayachonge lakini sio eneo la ujenzi wa nyumba ya Mungu bali yachongwe chimboni, au Kware katika eneo lingine mbali na eneo la ujenzi.

Katika namna zote mbili yaani kimwili na kiroho, uzuri na ufahari na taratibu za ujenzi wa Hekalu ulikuwa ni mradi unaosimamiwa na Roho Mtakatifu maandiko yako wazi kuwa sisi ni kazi ya Roho Mtakatifu. Mradi huu kinabii ulikuwa unazungumzia Kanisa, kila mtu aliyeokoka anafananishwa na jiwe la thamani na katika maandiko sisi tunaitwa mawe yaliyo hai, tunachongwa huko duniani machimbo au kware na tunatolewa huko na kuletwa katika jengo la Mungu na kuenea katika eneo lililokusudiwa, mawe haya yalichongwa kwa agizo la mafundi waashi, na kila jiwe lilitosheleza pale lilipotakiwa!

1Petro 2:4-5 “Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.”

Waefeso 2:19-22 “Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.”

Kila mtu aliyeokolewa ni hekalu la Roho Mtakatifu, kila mmoja ana thamani kubwa sana wote tumechongwa kwa jinsi ya kipekee mgodini na wote tumeletwa ili tuwe nyumba ya Mungu, na kuwa tumuabudu yeye na kuishi kwa amani bila malumbano wala mafarakano, kwa sababu kama mawe ya thamani kila mmoja lina thamani yake na linafaa kukaa pale lilipokusudiwa, endapo jiwe lile limekaa mahali pasipo pake au halijachongwa vizuri huko kware kama ilivyokusudiwa litasababisha kelele na kama nyundo na shoka na vyombo vya chuma vitatumika kulichongea hekaluni litatia unajisi unaona

1Petro 2:4-5“Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.”        

1Wakorintho 3:16-17 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.”     

1Wakorintho 6: 19-20 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

Kwa hiyo tunakubaliana na maandiko kuwa kila aliyeokolewa ni Hekalu la Roho Mtakatifu na kwa umoja wetu ni jengo la Mungu na kila mmoja ni jiwe la thamani lililochongwa kwa ustadi, kutoka katika mgodi au kware ya giza iliyoko duniani na kuletwa na kuungamanishwa na Yesu Kristo ambaye ni jiwe kuu la pembeni, jiwe la msingi, hatujajichagua wenyewe bali ni Mungu ndiye aliyetuchagua na kutuleta katika jengo lake, ili tumtukuze yeye na tena tumuabudu yeye na kumtumikia bila ya hofu yoyote. Kwa hiyo ukisikia kelele wakati waujenzi ujue kuna jiwe limaingia mahali pasipolihusu!

Kwa nini hekalu halihitaji kelele?

Mungu amekusudia kutufanya sisi kuwa watu wake, na amekusudia kutupa utulivu, kelele asili yake ni huko mgodini, wakati wote unapotembelea mgodi au kware utasikia milipuko mikubwa ya kuvunjwa kwa mawe na mafundi wakitumia makrasha au mashine maalumu za kuvunja mawe, huko mafundi watayachonga mawe lakini yanapoletwa katika Hekalu yanakuwa tayari yanafaa kwa ujenzi, kelele zinawakilisha maisha ya duniani, kelele zinawakilisha taabu na uusumbufu wa kuwa nje ya uwepo wa Mungu, Kelele zinawakilisha hofu, kelele zinawakilisha kuwa uwepo wa Mungu umetoweka, kelele zinawakilisha hakuna ujenzi, bali kuna kuvunja vunja na kubomoa, na kuharibu.

Mahali kwenye hofu ya kifo, hofu ya utumwa hofu ya uvamizi, hofu ya uharibifu, hofu za maisha, hofu ya njaa, hofu ya kesho itakuwaje  ni mahali penye kelele  ni nje ya uwepo wa Mungu sio hekaluni, unapokuja kwenye uwepo wa Mungu Roho Mtakatifu tunapata utulivu wa ajabu na amani na tunatengwa mbali na kelele. Mungu amekusudia kumtenga kila mmoja wetu na kelele na kumpa kila mmoja wetu utulivu na amani.

Hutaogopa majeshi hodari yatatapopanga vita kwaajili yako Bwana anajua kuwa wewe ni hekalu lake kwa hiyo majeshi ya upinzani yatanyamazishwa, wakati wote Mungu Kama Mchungaji wetu hutuongoza katika maji ya utulivu

Zaburi 23:1-2, “Bwana ndiye Mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabishi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza”

Israel walipomlilia Musa kwa sababu ya Majeshi ya farao yaliyokuwa yakiwafuatia kwa nyuma ili kuwarejesha tena utumwani, Musa alitoa unabii ya kuwa Bwana atawapigania nao watanyamaza kimyaa! Mungu anafahamu ya kuwa wanadamu wanahitaji utuilivu wanahitaji ukimya! Wanahitaji amani, wanahitaji kuwa mbali na hofu, wanahitaji maisha ya ushindi, wanahitaji kuthibitishiwa kuwa watakuwa mbali na kelele za kila aina:-

Kutoka 14:13-14 “Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya”

Mungu atakustarehesha katika maskani yake utaburudishwa hata kutokee matetemeko, mafuriko sunami na mabadiliko yoyote yale sisi tunaokimbilia kwa Mungu kamwe hakuna atakayeogopa hakuna atakayetetemeshwa ukiwa katika uwepo wa Bwana ushindi unapatikana mapema asubuhi tu

Zaburi 46:1-5 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu. Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.”

Wewe unapokuwa Hekalu la Mungu huna sababu ya kupiga kelele, wala huna sababu ya kutikisika Mungu anafahamu wazi kuwa tunahitaji utulivu, tunahitaji kuwa kimya kisha yeye ataleta ukombozi, Daudi kila alipokuwa anakabiliwa na changamoto za aina mbalimbali alikumbuka anapaswa kutulia kimyaaaa na Mungu huyu yeye mwenyewe atazimaliza kelele

 Zaburi 62:1-2 “Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.”

Wanadamu hawapaswi kusumbuka, kama umechoshwa na kelele za dunia umechoshwa na wavunja mawe, kelele za kware, kelele za migodini wewe mfanye Bwana kuwa ndio mchungaji wako, utapata kila aina ya utulivu, utaandaliwa meza mbele za adui zako machoni pa watesi wako, hutakufa, hutaogopa mauti, utafarijiwa, utapata upako, nafsi yako itahuishwa, Baraka zitafurika nawe utakaa nyumbani mwa Bwana milele yaani kwenye utulivu!

Zaburi:23:1-6 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.”

Maana ya kelele wakati wa ujenzi wa Hekalu

Unaposikia kelele wakati wa ujenzi wa hekalu maana yeke ni nini? Kelel zinaashiria kuna uharibifu umeingia mtu mmoja alizungumza maneno haya yenye hekima kwa lugha ya kingereza “Destructive work is noisy, constructive work is silent” Kwa tafasiri isiyo rasmi ya Kiswahili “Kazi ya uharibifu ina kelele, na kazi ya ujenzi ni ya utulivu” mahali ambapo panafanyika kazi ya Mungu au panapotakiwa kuwa na uwepo wa Mungu ni mahali panapozingatia utulivu, Mahali panapofanyika kazi ya Mungu panatakiwa kuheshimiwa sana  mahali pa ibada hapatakiwi kusikika mlio wa nyundo, wala shoka wala kelele za (crashers) mashine maalumu za kuvunja mawe, mawe yakijakuchongewa Hekaluni yatasababisha kelele na kulitia unajisi hekalu, Nyumba ya Mungu sio mahali pa mazoea ni mahali panapoogopesha na panatisha, mahali maisha ya watu yanakoshughulikiwa kimwili na kiroho hapahitaji kelele wala chokochko za aina yoyote kelele na milio ya nyundo na mashoka ni ishara ya kuingia kwa unajisi

Mwanzo 28:10-17 “Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.”

Kutoka 20:25 “Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi.”

Kumbukumbu 27:5-6“Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake. Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;”

Kwa hiyo unapoona kelele Katika ujenzi wa hekalu maana yake ni kuwa;-

*      Watu wameacha kufanya kazi waliyoitiwa wanafanya biashara nyingine Marko 11:15-17 “Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa; wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu. Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.”

       

*      Watu wakiwa mwilini, yaani udunia ukiingia, hekalu linakuwa na kelele 1Wakoritho 3:1-7  “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”

 

*      Watu wameingiwa na tamaa ona Yakobo 4:1-5 “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?”

 

*      Kila mtu anapokuwa na nia yake 1Petro 3:8-13 “Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya. Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?”

 

*      Watu wema wanaposhikamana na waovu 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”

 

*      Watu wanapoanza kuzaa matunda ya mwili Wagalatia 5:19-21 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.”

 

*      Watu wanapoanza kutafuta utukufu binafsi 3Yohana 1:9-10 “Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.”

 

Diotrefe alikuwa ni mtu mwenye tabia ya kutaka sifa na kutaka kuwa juu kwenye kila kitu cha kanisa neno apendaye kuwa wakwanza katika lugha ya kiyunani linatumika neno “Philoprōteuō” ambalo ni muunganiko wa maneno mawili “Philo” ambalo ni love au kupenda na Proteuo ambalo kwa kiingereza ni Distinction au Preeminece yaani mtu anayependa kutambulika au mtu mwenye kimbelembele, mtu anayependa kuingilia maswala yasiyomuhusu, mtu anayetafuta umaarufu hawa husababisha kelele makanisani

 

*      Watu wasiokubali matengenezo au maandalizi – Mawe yalipokuwa machimboni yalihitaji kukatwa na kutengenezwa ili likakae mahali panapolohuzu, lakini jiwe hiko halikutakiwa likatengenezewe katika eneo la ujenzi wa Hekalu, Mtu asiyekubali kubadilika na anasimamia msimamo yake tu ya zamani hata kama ni ya kipoumbavu anaweza kuwa tatizo katika kanisa na kuleta matatizo yaleyale kila sehemu anakokwenda

 

Mithali 24:3-9 “Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu. Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni. Mtu afikiriye kutenda maovu, Watu watamwita mtundu; Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu.”

Kujengwa kwa Hekalu bila ya kelele:

Ili hekalu liweze kujengwa bila kelele ni lazima kila mmoja wetu akubali kutengenezwa kwanza kabla ya kutaka kuonekana, Mungu alipowachagua wat kuwa watumishi wake aliwapitisha katika shule zake kwanza yaani kila mtu alikuwa na kipindi cha maandalizi kabla ya kuffikia hatua ya kuonekana au kuwa na nafasi ya utawala kwa hiyo huwei kuruka hatua ya machimbo, ukiruka hatua hiyo utatuletea kelele, tujifunze kufundishika, tujifunze kuomba, tujifunze kusikiliza, tusitake ushindi tu wakati wote, tukubali kurekebishwa, tusijijengee tabia ya kutafuta cheo, na tukiwa nacho tusijivune , tujifunze kunyamaza pale ambapo majibu sio lazima, tujifunze kusema kweli, tujifunze kuinua wengine, tusipende kutatfuta mashindan, tujijenge katika neno la Mungu tukubali kuchongwa kama mawe yalivyokuwa yanachongwa, fanya wajibu wako kwa bidi, usishindane na mtu, usitumie muda wako kufuatilia mambo yaw engine, hatujaitwa kuwa mawakala wa wengine, Mungu atatumia watu waliojengwa, Kanisa linahitaji watu wenye vipawa, lakini pia wenye tabia nzuri, linahitaji wahubiri wenye ujasiri, linahotaji viongozi walezi na wenye maono, linahitaji watu wanyenyekevu, hekaluni hakukuhityajika makelele, kwa sababu watu waliandaliwa kabla wewe ni jiwe  la namna gani?  Je utaingia mbinguni na kuwa nguzo katika hekalu la Mungu?

# Mbinguni hakutaingia chochote kilicho kinyonge

Ujenzi huu wa ajabu ambapo mawe yalikuwa yakichongwa mbali, huko kware au mgodini, yaliletwa katika kiwanja cha hekalu yakiwa yamekamilika unatukumbusha wazi kuwa shemu ya kuchongwa watu ni hapa duniani, Roho Mtakatifu hufanya maandalizi ya kutuandaa na kutuchonga tukiwa hapa Duniani, anatukarabati ndani na nje ili tufae kuwa chombo cha sifa na ibada lakini zaidi kwamba baadaye tuweze kufika Mbinguni ambako huko ni eneo la utulivu na hakuna kuchongwa tena tutaingia tukiwa tumekamilishwa baada ya kupitia mchakato wa utakatifu duniani kule mbinguni hakuna chochote kilicho kinyonge kitakachoingia,

Wafilipi 1:6 “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;”

Kila mmoja anapaswa kujiweka wakfu kwa maneno kama yale ambayo Suleimani aliyasema siku alipokuwa akiliweka wakfu Hekalu, alisema

1Wafalme 8:13 “Hakika nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. Maneno ya kiingereza ya mstari huu ni matamu zaidi kwani yanasema hivi “I have indeed built you exalted house, a place for you to dwell in forever” Mungu anataka tuwe makazi yake milele. Lakini atakaa na watu ambao wameandaliwa vizuri kwaajili ya utukufu wake

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!


Jumapili, 11 Oktoba 2026

Watu hawa wana nini, hata wakalia?


1Samuel 11:1-5 “Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni, akakwea na kupanga marago juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi, na sisi tutakutumikia. Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia. Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende mipakani mwote mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutakutokea. Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia. Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.”



 

Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa hapa duniani kuna aina nyingi sana za uonevu na aina nyingine za uonevu kimsingi haziwezi kuvumilika!, Katika maandiko yetu ya msingi, tunapata picha ya aina hiyo ya uonevu iliyowahi kuwakuta watu wa Yabeshi-Gileadi, Mfalme wa wana wa Amoni aliyeitwa Nahashi, aliwatokea na kuwazingira watu wa Yabeshi-Gileadi akitaka kuwapiga vita, watu hao walipojipima waliona uwezo wao ulikuwa mdogo walikuwa wanyonge na wakataka amani na mfalme huyu, na kwa kuona kuwa watu hawa ni wanyonge na wanataka amani naye Nahashi mwamoni, alipata kiburi zaidi na kuwapa sharti la kikatili sana aliwataka ili wawe na amani na yeye basi Israel wote wang’olewe jicho la kulia, jambo hili liliwatia hofu sana wana wa Israel na wakaomba siku saba za kutafakari na kutafuta mtu wa kuwasaidia, walipofika mjini na hasa mji wa Sauli ulioitwa Gibea ya Sauli na kueleza taarifa hizo watu wote wakainua sauti zao wakalia, Sauli alikuwa akitokea mashambani kwa bahati alikokuwa amefuata ng’ombe na kukutana na kilio kikubwa sana na ndipo alipouliza “Watu hawa wana nini hata wakalia?“

Inawezekana unausikia ujumbe huu nawe ukiwa katika hali ya kulia  na unainua sauti yako kulia kwa sababu mbalimbali, umefanyiwa mambo ya kikatili, umedhulumiwa, umetapeliwa na mtu uliyemuamini, uko katika mateso yasiyoweza kuelezeka, unazingirwa na hali zinazokuzidi nguvu, umekata tamaa kuna maeneo unahitaji mwokozi, umefunga siku saba kutafuta msaada, uko kwenye maswali makubwa yasiyokuwa na majibu, unajiuliza msaada wako utatokea wapi, najua leo Sauli hayuko Lakini Roho Mtakatifu yupo na kwa jina la Yesu Kristo atakutokezea msaada leo Mwokozi wetu Yesu Kristo anauliza watu hawa wana nini hata wakalia? Tegemeo letu kuu na la uhakika sio wanadamu, tegemeo letu kuu linatoka kwa Mungu mwenyewe na Roho wa Mungu anaguswa na kilio chako!

Zaburi 121:1-4 “Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.”

Zaburi 124:6-8 “Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.”

Tutajifunza somo hili, “Watu hawa wana nini hata wakalia?” kwa kuzingatia vipengele muhimu vitatu vifuatavyo:-

 

·         Kilio chako sio ishara ya udhaifu!

·         Watu hawa wana nini hata wakalia?

·         Kilio chako ni mwanzo wa wokovu wako!

 

Kilio chako sio ishara ya udhaifu!

1Samuel 11:1-5 “Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni, akakwea na kupanga marago juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi,na sisi tutakutumikia. Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia. Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende mipakani mwote mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutakutokea. Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia. Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.”

Nimuhimu kufahamu kuwa wana wa Israel wakati huu walikuwa ni wanyonge, walikuwa hawana uhakika wa kupata utetezi kutoka kwa wana wa Amoni, na Nahashi alikuwa anajiamini sana na kwa sababu ya uonevu aliokuwa nao aliweka sharti la kikatili kwaajili ya uonevu tu, akijua kuwa sio rahisi kutokea mtu akawasaidia wana wa Israeli, na wana wa Israel walifahamu unyonge wao hivyo walilia, kilio chao kilichojawa na huzuni hakikuwa udhaifu kwani walimpa Nahashi siku saba, wao walilia kwa sababu walimuhitaji mwokozi, waliona kuwa Nahashi,  alionyesha ukatili uliopitiliza na kuwa kama hakuna wa kumshughulikia basi ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa taifa, kwamba watu wa mji wa Gileadi na Israel nzima kila mwanajeshi ang’olewe jicho moja la upande wa kulia,  hii ilikuwa sio tu uonevu lakini adui alikuwa anataka kuweka alama ya milele na ya miaka mingi ya kuwashinda Israel,  wangwezaje kurusha mishale wakiwa na jicho moja, tena la kushoto, wangewezaje kujikinga na ngao, wangewezaje kutumia Kombeo, walilia na kupaza sauti kwa sababu walihitaji mkombozi katika janga hili, Mungu wa Israeli kamwe hangeweza kudharau machozi yao, kilio chao kilimfikia Mfalme mpya Sauli ambaye aliposikia watu wanalia Roho Mtakatifu alimshukia kwa nguvu na kuamsha nia na hari yake ya kutaka kuwasaidia, Maandiko yanatufundisha wazi kuwa Mungu huyajali machozi ya watu wake hasa wanapokuwa katika shida zao:-

Zaburi 34:17-19 “Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”

Zaburi 105:13-15 “Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.”

Kutoka 3:7-9 “BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.”

Inawezekana unausikia ujumbe huu au kuusoma ukiwa katika kuelemewa na huzuni, najua ya kuwa bila shaka unahitaji msaada wa Mungu na neno lake limeahidi kuwa anayajali machozi yako anajua maumivu yako, inawezekana machozi yako ni matokeo ya unyanyaswaji mahali, ni matokeo ya mateso mahali, ni matokeo ya dhuluma, ni matokeo ya uonevu wa pepo, uonevu wa wachawi, mateso yako ni matokeo ya majungu kazini, ni matokeo ya watu wasiopenda maendeleo yako, ni matokeo yauonevu wa unyonge wako, ni matokeo ya umasikini wako, ni maumivu ya moyo uliojeruhiwa, ni kukosa ada, ni kudhulumiwa shamba, kiwanja, nyumba, mirathi, ujane, yatima, uonevu nataka nikuhakikishie ya kuwa Mungu anasikia kilio chako anayajua maumivu yako na anayaona mateso yako, Mungu ameyahifadhi machozi yako na ameyaweka katika kichupa na bila shaka kimejaa

Zaburi 56:8-9 “Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?) Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;”

Watu hawa wana nini hata wakalia?

Sauli alikuwa anarudi kutoka shambani na ng’ombe zake, hakuwa tayari kwa vita alikuwa anatokea kwenye shughuli zake za kawaida lakini alisikia watu wanalia kilio cha kukata tamaa, watu wanaombolezea macho yao, hata kabla hayajang’olewa, Roho Mtakatifu alimjia kwa nguvu mara tu aliposikia habari za mateso ya watu wake na kukatatamaa kwao, hasira yake ikamuwaka akawaambia watu wa Yabeshi-Gileadi wasilie kwani kesho watapata wokovu wakati wa jua kali yaani mchana kweupeee, leo nasema usilie, utapa wokovu wako wakati wa jua kali.

1Samuel 11:5-11. “Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi. Na roho ya Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana. Naye akatwaa jozi ya ng'ombe, akawakata-kata vipande, kisha akavipeleka vile vipande mipakani mwote mwa Israeli kwa mikono ya wajumbe, kusema, Ye yote asiyetoka nyuma ya Sauli na Samweli, ng'ombe zake watatendwa vivi hivi. Basi utisho wa Bwana ukawaangukia wale watu, wakatoka kama mtu mmoja. Naye akawahesabu huko Bezeki; Waisraeli walikuwa mia tatu elfu, na Wayuda thelathini elfu. Nao wakawaambia hao wajumbe waliokuja, Waambieni watu wa Yabesh-gileadi, Kesho, wakati wa jua kali, mtapata wokovu. Basi wale wajumbe wakaenda, wakawaarifu watu wa Yabeshi; nao walifurahiwa. Kwa hiyo watu wa Yabeshi walisema, Kesho tutawatokea, nanyi mtatufanyia yote myaonayo kuwa ni mema. Ikawa, kesho yake, Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu; nao wakaingia katikati ya marago kwenye zamu ya asubuhi, wakawapiga Waamoni hata wakati wa jua kali; kisha ikawa wale waliosalia wakatawanyika, hata wasiachwe wawili wao pamoja.”

Mungu anafanya hivyo hata leo, Mungu anaweza kuamsha watu kwaajili yako, Mungu anaweza kukufungulia mlango, Mungu anaweza kubadilisha hali yako ya kushindwa kuwa ushindi, Mungu anaweza kubadilisha hali yako ya unyonge kuwa ujasiri, Mungu anaweza kuwatumiwa wale wanaoonekana kuwa wa kawaida kuleta wokovu, Mungu anakuahidi leo kuwa adui zako watapigwa mchana kweupee, haitakuwa kwa kificho, haitakuwa wakati wa asubuhi, wala haitakuwa wakati wa jioni ni mchana wakati wa jua kali wokovu wako utaonekana na kila mtu

Zaburi 34:15-17 “Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao. Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote.”

Zaburi 46:1-3 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”

Zaburi 136:10-12 “Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.  Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.”

Kumbukumbu 26:6-8 “Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito.  Tukamlilia Bwana, Mungu wa baba zetu; Bwana akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu.Bwana akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu;”

Wakati unapokuwa unalia na unahisi kama hujaona mabadiliko yoyote usufikiri ya kuwa Mungu amekusahau, kwa sababu bado hujaona dalili zozote Roho Mtakatifu hutulia lakini huamka na hasira zake hufurika yeye ndiye anayeitwa mkono ulionyooshwa yeye atafanyia kazi hitaji lako na atatumia njia mbalimbali kukuokoa na kukusaidia lakini kumbuka mkono wake ulionyooshwa utashughulika na kila aina ya uonevu Mungu hawezi kamwe kufumbia macho aina yoyote ya uonevu kilio chako kinamgusa kuliko unavyoweza kufikiri, yeye anauliza wakati wote watu hawa wana nini hata wakalia? Na hasira zake zinawaka akisha kujua ni kwanini unalia ananyoosha mkono wake na nikuhakikishie wokovu wako utapatikana mchana wakati wa jua kali!  Wazi wazi bila kificho adui wengine hawapaswi kushughulikiwa usiku wanapaswa kuoigwa mchana kweupee ili habari zienee mapema kuwa wametandikwa huku 

Kilio chako ni mwanzo wa wokovu wako!

Watu wa Yabeshi-Gilead walipoanza kulia ndipo Mungu alipowaletea msaada na kuwapa ushindi mkubwa, watu hawa waliokolewa kabisa na aibu iliyokuwa ikiwakabili, aibu yao ikageuzwa kuwa shangwe, ni muhimu kuwa na ufahamu kuwa unapoanza kulia leo sio ishara ya kushindwa, adui zako wanaweza kudhani kuwa wamekuweza kwa sababu ya sharti gumu walilokuwekea, lakini kumbe wanakuandalia safari ya kuelekea kwenye ushindi wako,  kilio chako ni sehemu ya mwanzo ya wokovu wako itakayokuletea ukombozi mkubwa, maandiko yanaonyesha kuwa unaweza kulia usiku na asubuhi ikawa ni furaha

Zaburi 30:2-5 “Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya. Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni. Mwimbieni Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake. Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.”    

Mungu aliyewaokoa watu wa Yabeshi ni yule yule anayeweza kukuokoa na wewe kutoka katika ukatili, dhuluma, uonevu na maumivu unayoyapitia, kilio ulicho nacho sasa au leo kitageuzwa kuwa furaha! Kaka yangu na dada yangu unayelia usikate tamaa, swali la Sauli lilikuwa ni swali kutoka kwa Mungu watu hawa wana nini hata wakalia? Swali hili linajibiwa na Mungu mwenyewe yeye ndiye anajua ni kwa nini unalia, anayajua maumivu yako anaujua uchungu wako na yuko tayari kuingilia kati machana wa jua kali Bwana analeta wokovu! Mungu wangu aliyenilinda mimi na watu wabaya akamtuma malaika wake na kunitetea siku zote za maisha yangu atakutetea nawe pia katika jina la Yesu Kristo mwana wake aliye hai amen! Watu hawa wana nini hata wakalia?

Zaburi 56:8-11 “Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?) Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu; Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?”

 

Rev. Innocent Samuel Kamote.

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima.

Jumapili, 4 Oktoba 2026

Umuhimu wa Pango la Adulamu


1Samuel 22:1-2. “Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne.”




Utangulizi:

Wengi wetu tutakua tunafahamu kuhusu habari za Daudi kukimbilia katika pango la Adulamu, Pango hili liko maili 22.5 sawa na kilomita 36 kusini magharibi mwa jiji la Yerusalem na kilomita 13 magharibi mwa Bathelehemu, mipakani na nchi ya Wafilisti eneo hili ni maarufu na linajulikana kama Mahali pa kujificha, hasa kutokana na tukio la Daudi kukimbilia huko na kujificha alipokuwa anamkimbia mfalme Sauli aliyekuwa anataka kumuua, Adulamu pakawa mahali salama kwa Daudi na watu wote wenye huzuni, shida na madeni waliomuendea, Kimsingi Pango la Adulamu pamoja na tukio hili halisimami kama sehemu ya historia na usalama tu lakini linasimama kama eneo muhimu la maandalizi ya kiroho na uongozi na mabadiliko makubwa ya Daudi na watu wake, Kwa hiyo Adulamu pamejulikana kama eneo muhimu la kimchakato ambapo Mungu anawaandaa watu wake kabla hawajashika majukumu yao ya kimaongozi.

1Samuel 21:8-10 “Tena Daudi akamwambia Ahimeleki, Na hapa chini ya mkono wako, je! Hapana mkuki, au upanga? Kwa maana sikuleta upanga, wala silaha zangu, kwa sababu ile shughuli ya mfalme ilitaka haraka. Yule kuhani akasema, upanga wa Goliathi, yule Mfilisti, uliyemwua katika bonde la Ela, tazama, upo hapa, umefungwa ndani ya nguo nyuma ya naivera; ukipenda kuuchukua, haya! Uchukue, maana hapa hapana mwingine ila huo tu. Daudi akasema, Hapana mwingine kama ule; haya! Nipe. Basi Daudi akaondoka, akakimbia siku ile, kwa hofu ya Sauli, akamwendea Akishi, mfalme wa Gathi.”

1 Samweli 22:1-2 “Basi Daudi akaondoka huko, AKAKIMBILIA PANGO LA ADULAMU; na ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne.”              

Kwa msingi huo leo tutachukua muda kujifunza somo hili muhimu, lenye kichwa “Umuhimu wa Pango la Adulamu” kwa kuzingatia vipengele vikuu vitatu muhimu vifuatavyo:-

·         Maana ya Adulamu

·         Umuhimu wa Pango la Adulamu

·         Matokeo ya kupita katika Pango la Adulamu

Maana ya Adulamu

Neno au jina Adulam linatokana na neno la asili la Kiebrania  “Adullām” ambalo lina uhusiano na eneo lililokuwa lililokaliwa na rafiki mkubwa wa Yuda  mwana wa Yakobo aliyeitwa Hira, Hira alikuwa rafiki mkubwa sana wa Yuda ambao walishirikiana katika kufuga wanyama na mambo yao mengine ya kimaisha, Rafiki huyu mkubwa wa Yuda aliishi eneo hilo.

Mwanzo 38:1-3, 12 “Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira. Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake. Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri. 12 Siku nyingi zikapita, akafa binti Shua, mkewe Yuda. Yuda akafarijika, akaenda kwa watu wake wawakatao manyoya kondoo huko Timna, yeye na mwenzake Hira, Mwadulami.”

Neno au pango la “Adullām” limepata umaarufu sana baada ya Daudi kukimbilia huko kwaajili ya kuokoa uhai wake akimkimbia mfalme Sauli aliyekuwa anataka kumuua, huko aliungana na watu wengine wapatao  400 na baadae walifika 600 watu waliokuwa na madeni, waliokata tamaa na wale ambao hawakuridhishwa na hali ya mambo wakati wa utawala wa Sauli, kutokana na umaarufu wa tukio hili hata jina “Adullām” au Pango la Adulamu limebeba maana ya  Mahali pa siri,  au mahali pa makimbilio, au mahali pa kujificha, au mahali pa kujitenga na kujipanga kwa upya, au kimbilio la waliovunjika moyo, The secret place, The place of Refuge, the Hiding Place, Place of withdrawal, the place of retreat, or a place of brokenness.

Adulamu kumejipatia umaarufu kiroho kama mahali ambapo Mungu anamtenga mtu wake na kumuandaa kwaajili ya mpango wake mkuu wa baadae, ni eneo la utulivu, usalama na la kujipanga kwa upya ni kama shule ya Roho Mtakatifu, mahali ambapo ni kama Mungu anakuacha upoteze kila kitu, kisha uishi maisha ya ukimbizi, na kujiepusha na watu, kisha anakuweka na watu wanaoonekana kutokufaa ili uwabadilishe waweze kufaa, hivyo kwa jicho la kinabii Adulamu ni mahali muhimu ambapo sio tu kuwa mtu anakimbilia bali Mungu anampeleka mtu huko ili kumjenga na kumuandaa kwa huduma.

Umuhimu wa Pango la Adulamu

Mungu hakumruhusu Daudi kwenda Adulamu kama adhabu, lakini badala yake lilikuwa ni eneo muhimu kwaajili ya maandalizi ya kimkakati ya kumfanya kuwa mfalme mwenye nguvu sana, mwanadamu hajifunzi kuwa imara anapokuwa kwenye eno lenye starehe “Comfort zone” lakini mwanadamu anakuwa imara sana anapokuwa katika mazingira magumu na tatanishi yasiyo na faraja yoyote, kusudi kubwa Mungu anataka ukomae na usidumae, anataka ukue na hatimaye uje kuwa kiungo kizuri katika kutimiza mpango wake, wakati ambapo kimsingi Adulamu hakuonekani kuwa kwenye kufaa huko lakini ni shule ya Mungu ya kutengeneza sifa nzuri, na kuleta mabadiliko, kuondoa njia za zamani na mitazamo ya zamani na kupewa mipya itakayofaa kwaajili ya watu wa Mungu lakini zaidi ya mambo yote Adulamu ni mahali ambapo watu wa Daudi walijifunza kufunga na kuomba na kuabudu wakimtegemea Mungu, kuna mafunzo mengi ambayo Mungu aliwafunza watu wake waliokimbilia Adulamu

1.       Ni eneo la kukomazwa - Yakobo 1:2-3 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.”

 

Waebrania 12:11 “Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.”

 

Kwa nini kukomazwa au kuwa na uzoefu ni kwa muhimu?  Kukomazwa na kuzoezwa ni jambo la Muhimu na ni mchakato ambao kimsingi hautokei kama muujiza inachukua muda au inahitaji muda fulani, lakini muda huo utakujengea ukuaji katika Hekima, imani na kuwa na tabia za uungu, jambo hili ni la Muhimu kwa sababu pia litakusaidia kukupa uwezo wa kukabiliana na changamoto za aina mbalimbali na kukujengea uwezo na ubora katika maswala ya mahusiano, upendo wa kujitoa, kumjua Mungu kwa undani kuwa na Amani katika mazingira yote  na kuwa na uhusiano wa ndani sana na Mungu na watu wengine, hakuna jambo baya duniani kama kuja kuongozwa na kiongozi aliyekosa mafunzo na ukomavu, viongozi wengi wasiopitia Adulamu wamejawa na ubinafsi, choyo, kujihami, kukosa kujiamini na kushindwa kuchukuliana lakini kwa Daudi Adulamu lilikuwa eneo zuri la kuishi na watu na kuwavumilia.         

 

2.       Ni eneo la kujifunza kumtegemea Mungu - Kumbukumbu 8:2-3 “Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.”

 

2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.”

 

Kujifunza kumtegemea Mungu kuna umuhimu wake kwa sababu kutakujengea msingi usiotikisika hata pale Amani yako inapotikiswa, matumaini yako yanapogeuka, kusudi linapoonekana kuchelewa na uwezo wako wa kufanya mambo kwa nafsi yako unapoachwa katika mikono ya Yeye mwenye uwezo wa kuamua majira na nyakati, hutaogopa, utakuwa na nguvu ya ndani, utapata muelekeo sahihi na utakuwa na moyo wa unyenyekevu, Adulamu inatufunza kumtegemea Mungu.

       

3.       Ni eneo la mabadiliko makubwa - Kabla Mungu hajaanza kumtumia mtu anaandaa mazingira ya kutubadilisha, Mungu anaondoa kabisa kiburi na ubinafsi, anakufundisha kumtegemea yeye na sio swala la kukubalika na dunia au walimwengu, kwa hiyo ataruhusu majaribu ya aina mbalimbali ili akunoe na kukutengeneza, wakati mwingine ataruhusu upoteze kila kitu, akupime katika hali zote akuone unapofanikiwa na unapokosa tabia yako inakuwaje na baada ya vipimo vingi sana Mungu anakuamini na kukupa majukumu anayoyakusudia kukupa kubwa ni mabadiliko!

 

Wafilipi 4:11-13 “Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”

 

Daudi alikuwa ni kama mtu aliyepoteza kila kitu alipokimbiilia Adulamu, Lakini Mungu alimfundisha kumtegemea yeye aliishi alikula na aliendelea kuwa shujaa mwenye uwezo wa kuingia na kutoka na kuwasaidia watu wote duni waliokuwa wamemkimbilia, Daudi aliwatunza, aliwajenga kiroho na kuwafundisha vita, Mungu atatujaribu ili atunoe na kutupima kama dhahabu inavyopimwa ili tutoke tukiwa tunang’aa zaidi, Daudi na watu wake walijifunza vita, walijifunza ushujaa, walijifunza ukakamavu, walijifunza kufunga na kuomba, walijifunza kuabudu walijifunza kumtegemea Mungu na kuishi kijamaa na wakatoka huko wakiwa na mabadiliko makubwa tayari kwa kushika hatamu na kuwahudumia watu wa Mungu Ayubu 23:10 “Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.”

 

4.       Ni eneo la maandalizi ya kishujaa - Mungu hutumia changamoto kutujengea maandalizi na ushujaa, ili tuwe na nidhamu, subira uvumilivu na ujasiri, anaruhusu mazingira ambayo wewe ndie utakuwa tegemeo lake na hutajitumainia kwa lolote, anakubadilisha mtazamo na fikra na kukuandaa kivita, wayahudi ni taifa vumilivu na imara zaidi duniani kwa sababu ya kukutana na changamoto kali na kadiri wanavyoshambuliwa ndivyo wanavyokuwa imara na kujijengea uwezo mkubwa siku hadi siku, kupigana kwao sio kwaajili ya kushambulia bali kwaajili ya kujihami.  

 

2Wakorintho 10:5 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome ;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.”

 

Yeremia 29:10-13. “Maana Bwana asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa. Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.”

 

5.       Ni eneo la kuondoa udumavu - Mungu hafurahii udumavu wetu kiroho, iwapo anaona ukuaji wetu unaweza kuathiriwa anaondoa watu na mahali  na hali zote zinazoonekana kuwa na umuhimu wa kukulazimisha wewe ukue na kukomaa, kama mtu au watu na mazingira yanayoonekana kuathiri ukuaji wako anakuondoa wewe, anaondoa ulinzi, anaondoa faraja, anaondoa kuthibitishwa na watu anaweza hata kukuhamisha mazingira kama anaona ni madogo kwake kukusaidia kwenda kwenye kiwango kingine  anaingilia mielekeo yako, anafunga mlango, anakuweka kwenye chumba cha kusubiria, anaruhusu upate maumivu, atakufanya uishi kwa imani, anaondoa udumavu na kukuoa ukuaji wa kiroho.

 

Hosea 2:13 -17 “Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema Bwana. Kwa hiyo angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo. Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri. Tena siku hiyo itakuwa, asema Bwana, utaniita Ishi, Kwa maana nitayaondoa majina ya Mabaali kinywani mwake, wala hawatatajwa tena kwa majina yao.”

 

6.       Ni eneo la kutengwa -  Daudi alishakuwa mtu maarufu sana tangu siku alipomuua Goliath, watu wa mijini na vijijini walikuwa wanamtambua, wanawake waliimba na kumsifia kuwa amefanya kazi kubwa kuliko hata mfalme mwenyewe kwa hiyo alitajwa kama mtu shujaa aliyeiletea Israel ushindi mkubwa sana, aliozwa binti wa kifalme na alikuwa anakaa ikulu, na kwa kuwa alikuwa mtu wa kutegemewa alitakiwa kukaa katika uwanja wa vita akipigana vita mbalimbali mtu huyu mwenye sifa zote za kifalme badala ya kuwako ikulu sasa anaishi kama mkimbizi na kuishi katika pango huko Adulamu, Mungu alimtenga na umaarufu, Mungu alitaka kumtenga mtumishi wake kwa kazi maalumu

 

1Samuel 18:6-7 “Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.”

 

Wimbo huu uliashiria kuwa Daudi ni Mpiganaji hodari zaidi kuliko Sauli kwani wanawake walijaribu kumlinganisha na mtawala aliyekuweko na kwa sababu ya wimbo huu Sauli alipatwa na wivu na kuanza njama na mikakati ya kummaliza na kumuua Daudi, Mungu anaamua kumtenga Daudi na hatari hizo, kwaajili ya kumuandaa kuwa kiongozi hodari zaidi, mnyenyekevu, mvumilivu mwenye kujua wakati na majira ya Mungu, Mungu anaweza kukutenga na kukupeleka mahali ambapo utapata muda na utaendeleza uwezo wa kumuomba na kujitambua na kukomaa zaidi kwa ajili ya kazi yake  

 

7.       Ni eneo la mafunzo ya kiroho - Huko Adulamu Daudi hakuwa Mchungaji wa kondoo tu na Shujaa wa vita bali sasa alikuwa kiongozi, alifanyika kiongozi wa watu waliovunjika moyo, watu wenye uchungu moyoni, wenye madeni na wenye mizigo. Mungu alimtumia Daudi kuwafanya watu hao wanyonge kuwa mashujaa, walijigundua wao ni kina nani bila ufalme na walijigundua wao ni akina nani bila sifa na umati wa watu, Adulamu inaondoa sifa na kufunua kuwa wewe ni nani, Adulamu inakupa nafasi ya kujitazama kwa jicho lingine na sio vile wanavyosema watu!

 

1Samuel 22:1-2. “Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne.”

 

2Samuel 23:8-39. ”Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni,mkuu wa maakida ;huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu.Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti; ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu. Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai. Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu. Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana.  Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu. Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu.  Je! Huyo hakuwa na heshima maalumu miongoni mwa wale watatu? Kwa hiyo akawekwa kuwa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theruji. huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake. Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu; na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi; na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi; na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi; na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini; na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi;na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi; na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani, mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari;  na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni; na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi; na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi; na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya; na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri; na Uria, Mhiti; jumla yao ilikuwa watu thelathini na saba.”

Matokeo ya kupita katika Pango la Adulamu

Adulamu kulizalisha Serikali yenye nguvu sana, Daudi na watu wake waliokuwa wamekataliwa katika jamii tena wanatafutwa kuuawa waligeuka kuwa watu wema, waadilifu, wenye uchungu na taifa lao, na viongozi wa ufalme na majeshi ya kifalme na mashujaa wenye nguvu, walitoka wakiwa watu wanaomcha Mungu na wanaomtegemea Mungu kwa asilimia miamoja, Daudi aliwafunza watu wake kuwa kama yeye alivyo na kuwa na moyo kama wake.

Zaburi 34:17-19 “Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”

Zaburi 57:1-3 “Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita. Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu. Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa, Atukanapo yule atakaye kunimeza. Mungu atazipeleka Fadhili zake na kweli yake”

-       Adulamu Daudi na wenzake walitoka wakiwa mwenye nguvu zaidi – Daudi alikimbilia Adulamu akiwa Mkimbizi lakini alitoka akiwa kiongozi wa wakati mkamilifu uliokusudiwa na Mungu kwa Israel kuwa na kiongozi mcha Mungu, Adulamu iliwajenga, iliwapa uvumilivu, iliwafanya kuwa wa kiroho zaidi, iliwaimarisha kihisia, na kuwajengea ujasiri.

 

-     Adulamu iliimarisha uhusiano wao karibu na Mungu – Walikimbilia Adulamu wakiwa wenye mashaka, wenye wasi wasi, wenye woga na hofu, wakiwa na uchungu, wenye madeni na walikata tamaa lakini walitoka wakiwa mashujaa, Kule Adulamu Mungu atakuunganisha na watu utakaokuwa nao kiroho, watakaokupigania na watakaosimama na wewe na wito wako

 

-     Adulamu lilikuwa ni eneo la kuendeleza kipawa cha uongozi, - Daudi alijifunza jinsi ya kuongoza, jinsi ya kupangilia mfumo wa uongozi, jinsi ya kupanga wapiganaji, jinsi ya kuwatia moyo watu waliokata tamaa na jinsi ya kumtegemea Mungu, ukiweza kuongoza watu Adulamu hutasindwa kuongoza watu  Hebroni wala Yerusalem

 

-    Adulamu lilikuwa ni eneo la kuimarisha uhusiano na Mungu – Adulamu lilikuwa ni eneo la kujipanga upya kiroho, kulikuwa na ukimya, lilikuwa eneo la siri, sehemu ambayo unaweza kufurahia uwepo wa Mungu, walitoka wakiwa wamejifunza kuomba, kuimba zaburi, kumtegemea Mungu zaburi nyingi za Daudi zilitungwa na kuimbwa kutoka katika pango la Adulamu

Adulamu sio kuzuri lakini ni kwa Muhimu, ni kama sehemu ya upweke, ni kama sehemu ya kucheleweshwa, ni kama sehemu ya ukimya lakini kiroho ni eneo la kukujenga na sio la kukubomoa, Mungu akupeleke Adulamu lakini sio kwa kukutesa wala sio kwa adhabu wala sio kukuchosha lakini kwaajili ya kukuendeleza, unafichwa ili uandaliwe, unavunjwa ili utengenezwe, unasubiri ili utiwe nguvu, huwezi kuhitimu Adulamu kwa kuikimbia unahitimu Adulamu kwa kukubali kuwa kile Mungu alichokikusudia ndani yetu, kije kuwa dhahiri katika maisha yetu ya baadaye na kuwafaa watu wa Mungu.

Na. Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima