Jumatatu, 20 Desemba 2021

Nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwaajili ya Kristo!


Wafilipi 3:4-11 “Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu



Utangulizi:

Kwa watu au kampuni zinazofanya biashara neno hasara na faida ni maneno ya karibu sana katika misamiati ya kila siku ya maisha ya biashara, Kila wakati wanajua mwenendo wa biashara zao endapo wanapata faida au wanapata hasara, kusimama au kuendelea kwa Biashara yoyote ile kunategemeana na faida inayopatikana au hasara inayopatikana, kuendelea kwa biashara Fulani kunategemeana sana na jinsi biashara hiyo inavyoingiza faida, Marabi wa kiyahudi wengi walikuwa wanafahamu swala hili  la kibiashara nao wakalitumia katika kuainisha jambo lililo na umuhimu na lisilo na umuhimu  mfano utaweza kuona Mathayo 16:26 “Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”

Katika somo letu la msingi Paulo mtume anatumia mtindo huo huo kuonyesha maswala ya msingi kwake na maswala yasiyo ya msingi, Wafilipi 3:7-8 “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;Unapofanya uchunguzi wa kimaandiko utaweza kuona kuwa hasara na faida inayozungumziwa hapa ni mambo ambayo ni ya msingi na mambo ambayo sio ya msingi, na hii inatusaidia sisi nasi leo kujihoji na kutafakari kuwa ni mambo gani tunayapa kipaumbele kama mambo ya msingi na mambo yapi hatuyapi kipaumbele yaani mambo yasiyo ya msingi katika maisha!. Kwaajili ya hayo hapo tutaweza kugundua mambo yaliyo na faida kwetu na mambo yasiyo na faida kwetu, Paulo mtume aliyahesabu mambo yote yasiyo na faida kama hasara na kuyahesabu kuwa kama mavi kutokana na faida ya kumpata Yesu. Ni mambo gani hayo ya msingi ambayo aliyazingatia kisha baadaye akayaacha na kuona ni afadhali kupata hasara iwa mambo ambayo mwanzoni alifikikuwa yana faida kwake:-

1.       Dini za wazazi wetu.

 

Kama kuna jambo litawapa hasara kubwa sana watu wengi ni pamoja na kung’ang’ania dini za wazazi wao, hizi ni zile imani ambazo tumezirithi kutoka kwa wazazi wetu, imani hizi zitatuleta katika hasara kubwa badala ya faida, Paulo Mtume alikuwa akipambana vikali na watu waliokuwa wakihubiri dini ya kiyahudi na kufikiri kuwa ni dini bora zaidi kuliko kumpata Yesu, ni ukweli ulio wazi na dhahiri kuwa hakuna urithi wa kiroho, hali ya kiroho ya kila mtu inategemeana na yeye anavyokutana na Mungu kwa binafsi na sio kwa sababu ya wazazi, wake nyakati za namna hiyo kwa sasa haziko tena, watu wengi leo hii wako katika madhehebu au dini Fulani kwa sababu tu eti babu yake baba yake na ndugu zake wote walizaliwaga humo, kwa hiyo mtu yuko tayari kwenda Motoni na kutokumkubali Kristo kwa sababu tu anaiona dini ya baba zake kuwa ina faida, Wayahudi wengi sana walidhani kuwa Mungu atawahesabia haki kwa sababu wao ni watoto wa Ibrahimu, Yesu aliwajibu wazi kuwa huwezi kuwa mtoto wa Ibrahimu kisha ukawa muuaji, kwa vyovyote vile wayahudi hawakujua kuwa tayari wamekuwa na baba mwingine

 

Yohana 8:39-44 “Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu. Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo. Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu. Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu. Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.”   

 

Wayahudi wengi walijifikiri wako sahihi kwa sababu baba yao ni Ibrahimu, walidhani hali ya kiroho inaweza kurithiwa kwa jinsi ya mwili na kwa kushika mapokeo ya baba zao, Lakini Yesu alikuwa akiwajulisha kuwa huwezi kurithi hali ya kiroho bila kuamua kufuata mambo ya rohoni wewe mwenyewe, Paulo mtume anaonyesha hali kama hiyo kuwa kabla hajamjua Yesu alifikiri kuwa ana haki zote vilevile kama wayahudi wengine naye alikuwa mwenye bidii sana katika maswala ya imani akijua kuwa yatampa faida kubwa sana kwa kumpendeza Mungu kupitia taratibu za baba zake na mila za kwao na madhehebu ya kwao na kupitia vyuo vyao, lakini alipomfahamu Yesu alifahamu kuwa yale mambo ya kwanza aliyokuwa akiyashikilia na kufikiri kuwa na faida sasa anaachana nayo na kuyaiona kuwa ni hasara ukilinganisha na uzuri wa kumpokea Kristo:-

 

Wafilipi 3:3-7 “Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi.Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.”

 

Paulo anaonyesha kuwa yeye kama ni kuitumainia Dini aliitumainia sana, alitahiriwa siku ya nane kama dini yao ilivyoagiza,  alikuwa ni muisraeli yaani ni myahudi kama walivyo wayahudi wengine, alizaliwa katika kabila la Benjamin, alikuwa mwebrania halisi, na alikuwa wa madhehebu ya mafarisayo na aliishika torati, na aliliudhi kanisa na kuwatesa wakristo akifikiri kuwa ni sawa kwa mujibu wa dini yao, na aliishika torati hasa na kuwa kwa habari ya kuishika torati hakuwa na dhambi yoyote, Paulo anaonyesha jinsi alivyokuwa jemadari wa kuishi maisha ya haki kwa niaba ya dini yake  na aliipigania.

 

·         Aliishika torati tangu utoto, yeye alipitia mafunzo ya sharia chini ya mkufunzi aliyeheshimika sana na wayahudi aliyeitwa Gamaliel ona

 

Matendo 22:3 “Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;”

 

Matendo 5:34 “Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo,”

 

Gamaliel alikuwa ni Rabbi aliyeheshimika sana, kusoma kwake ni kama kusoma chuo kikuu kilichoheshimika sana kwa wakati huo kwa kuwa alikuwa ni Mwalimu wa sharia aliyebobea sana katika madhehebu ya mafarisayo, na Paulo mtume alikuwa mwanafunzi wa mkufunzi huyu wa kiyahudi. Lakini hata hivyo alipompata Yesu degree zake za dini ya kiyahudi alizihesabu kuwa si kitu au ni hasara ukilinganisha na kumpata Yesu Kristo!

 

·         Alikuwa Farisayo yaani moja ya madhehebu yaliyokuwa yakiheshimika sana kwa mitazamo mikali sana na iliyohesabika kama dini sahihi zaidi  Matendo 26:5 “wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa.”

 

·         Kwa habari ya wivu zeal yaani imani kali Paulo alikuwa na imani kali kiasi cha kutumika kuliudhi kanisa ona

 

Wafilipi 3:6 “kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia”. 

 

Matendo 8:3 “Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.”

 

Matendo 9:1-2 “Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu

                               

·         Kwa asili alikuwa myahudi ni wa uzao wa Ibrahimu

·         Kwa asili alikuwa mbenjamin kabila mojawapo halisi la kiyahudi

·         Kwa asili alikuwa mwebrania wa waebrania, yaani alizaliwa akiwa mwebrania kweli kweli na kiutamaduni yeye ni mwebrania kwelikweli ambapo napo hakuwa na sababu ya kubagulika  Palulo mtume anaonyesha kuwa alikuwa amekamilika idara zote kwa habari ya dini, yeye sio tu alimcha Mungu bali pia alikuwa tayari kuuwa  na kuwatesa na kuwafunga wale wote aliodhani kuwa  hawamchi Mungu kwa mujibu wa dini yake, Paulo mtume alikuwa mtu aliyejitoa katika dini yake kuliko kawaida huu ulikuwa ni wakati ambapo hakuwa amemjua Yesu,  maisha yake ya awali katika dini yake yalikuwa ya muhimu na ya faida kwa wakati huo akijua ya kuwa anaingiza kwake na kwa Mungu wake, Lakini sasa alipobaini ya kuwa kwa Yesu kunalipa zaidi akabadili kibao na kuhesabu yale ya zamani kuwa hayana faida kama kumpata Yesu

 

Wafilipi 3:7 “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;”     

 

Unaweza kuona wako watu ambao wanadhani imani walizozirithi zina faida kubwa sana kwao na hawataki kuachana nazo kwa sababu ni mila, kwa sababu ndugu zao wote ni wa aina hiyo, hawataki kuziachia wakidhani kuwa yana faida kwao, wako wenye kuabudu mizimu, wako wenye kushika dini Fulani na desturi za aina Fulani, au imani zao zimewafikisha mahali Fulani, labda wamesomea maswala kadhaa katika imani zao, wana degree, wana phd, wana diploma za aina mbalimbali, wana heshima, wana wivu kwaajili ya miungu yao, wanaheshimika katika dini zao, wamepewa vyeo ni wazee wa kanisa, wamehiji maeneo matakatifu wako karibu na viongozi wakubwa wa kidini  wanaamini kuwa wamewekeza kwa faida na kiwango kikubwa sana katika dini zao, vyovyote vile iwavyo Paulo mtume alipobaini kuwa Yesu, analipa aliachana na kila kitu na kuyahesabu yote kuwa ni hasara  na kuwa faida kubwa ni kumpata Yesu!

Paulo mtume alikuwa amejifunza ya kuwa hakuna mtu anaweza kuokolewa kwa matendo yake mema au sifa zake za zamani, Mungu hatuhesabii haki kwa sababu ya wema na matendo mazuri tuliyoyafanya katika dini zetu

Warumi 3:20-24 “kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria. Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;”

Tunaishi katika ulimwengu wa pongezi, na wengi wanadhani kwa kufanya vizuri wanaweza kukubalika kwa Mungu na wanadamu pia lakini ukweli unabaki palepale kwamba mafanikio ya kiroho yanapatikana kwa kumuamini Yesu tu, tunapofanya mema tukumbuke maelekezo ya Yesu ya kuwa tumefanya tu yatupasayo kufanywa, Luka 17:10 “Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.” Kutumainia lolote nje ya Yesu Kristo ni kutumainia hasara.

2.       Mila na desturi za baba zetu.

Jambo linguine kubwa litakalowatesa wengi na kuwapeleka Motoni ni kushika mila na desturi za baba zao au babu zao, Jambo hili vilevile liliwaathiri wayahudi, walidhani ya kuwa wanaweza kuokolewa kupitia mila zao na hivyo walishika sana mila zao na desturi kiasi cha kusahahu kujua Mungu anataka nini kwao kuna watu wengi sana leo wanayashika mapokeo ya madhehebu yao, mila na desturi za wazee wao na kuacha kuliangalia neno la Mungu kwa undani hii ilikuwa shida kubwa kwa wayahudi wa kawaida na kwa Paulo Mtume pia Mathayo 15:1-3 “Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema, Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?Yesu alikemea vikali sana na kuiita tabia hii kuwa ni ya kinafiki alionya vikali kutokuhubiri neno la Mungu na kuhubiri mila na desturi ambayo kwa lugha nyingine aliyaita maagizo ya wanadamu au mapokeo ya wanadamu ona Mathayo 15:7-9 “Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamuNabii Yohana aliwaonya vikali na mapema wayahudi kuwa kujifikiri ya kuwa wanaye baba ndiye Ibrahimu bila kufungua mioyo yao na kumpokea masihi kwa imani ona Mathayo 3:7-10 “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba; wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.” Swala la mila na desturi lilisumbua mno nyakati za kanisa la kwanza na linasumbua hata leo, watu wengi wameacha kweli ya neno la Mungu na wanasumbuliwa na mafundisho na mapokeo ya wanadamu na hivyo wanaweza kujikuta kuwa wanapata hasara kwa kufuata desturi za kidhehebu, kimila na taratibu zilizowekwa na wanadamu, Paulo aliyashika sana mapokeo ya baba zake ona Wagalatia 1:14 “Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.” Hata hivyo baada ya kumjua Kristo aliliasa kanisa kuachana na aina hii ya Elimu yenye kupotosha ambayo kismingi sio neno la Kristo Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.” Ukristo utakuwa na nguvu kubwa sana kama watu wataacha mapokeo ya kujifunza kulishika neno la Mungu ambalo kimsingi ni kumjua Yesu Kristo jambo hili ndio lenye faida kubwa sana kuliko tunavyoweza kufikiri.          

Faida kubwa iko katika kumjua Yesu Kristo

Tangu nyakati za nabii Yeremia maandiko yalionyesha kuwa jambo lanye faida kubwa na la kujivunia ni kumjua Yesu, Mungu anataka tujivunie kumjua yeye zaidi ya kitu kingine chochote!

Yeremia 9:23-24 “Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana,”       

Paulo anaiona faida kwa kumjua Yesu Kristo Wafilipi 3:8 “Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;”

Hili ndio jambo lenye faida kubwa mno, kumjua Yesu, kuwa na uhusiano naye na zaidi sana hata kutamani kwenda kukaa naye milele na milele Wafilipi 3:9-10 “tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;Kumjua Yesu kristo kuna faida kubwa sana, kumjua yeye kunaaanza na kusoma habari zake, ili tuziamini na kwa kumuamini yeye tunakuwa na uzima tena uzima wa milele ona Yohana 20:30-31 “Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake

Muhimu

Wafilipi 3:10-11 “ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.”

Kuna mambo mengi ambayo tungependa kuyajua duniani kwa sababu tunataka kuitawala dunia,na kuyajua mazingira yetu ya sasa na kukabiliana na changamoto za ulimwengi huu kila mmoja ana mengi ambayo kwayo anaweza kuyaona kuwa yana faida nyingisana, hata katika maisha tunatoa kipaumbele kwa mambo tunayodhani na kufikiri kuwa ni ya Muhimu na yana faida kubwa sana kama ilivyiokuwa kwa Paulo mtume hata hivyo tunapaswa kumuelewa kuwa kwa nini alitamani sana kumuona Kristo Paulo alikuwa na uelelewa kuwa kumjua Yesu Kristo lilikuwa jambo lenye faida pan asana na hivyo aliyahesabu mabo mengine yote kuwa ni hasara na kuyafafnanisha na mavi, ili kumpata Kristo

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!      

Alhamisi, 18 Novemba 2021

Alipita katikati yao Akaenda zake!


Luka 4:16-30Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe. Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe. Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; lakini yeye ALIPITA KATIKATI yao, akaenda zake.”



Utangulizi:

Moja ya maswala ya kushangaza sana ambayo huwa tunayasoma katika maandiko na kisha yakatuacha aidha hatujaelewa, au yakatushangaza sana ni pamoja na muujiza huu, wa Yesu kupita kati kati ya  waliokuwa wamejaa ghadhabu na wamepania kummaliza, lakini wakashangaa kuwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha!

Hii sio mara ya kwanza  tunasoma katika maandiko ya kwamba Yesu amewahi kuwepo au kupita kati kati ya watu  tena watu waliojaa ghadhabu na hasira ili wamdhibiti na kumwangamiza  na bado yeye akapita kati kati yao  bila wao kutambua  na kwenda zake waandishi wengi wa injili wanapata taabu namna ya kuelezea tukio hili na hivyo kuwafanya wasomaji wao kushindwa kuelewa au kupata kile kilichofanyika ona

 Yohana 8:48-59Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?  Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu. Wala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu AKAJIFICHA, akatoka hekaluni.”

Ni muhimu kufahamu kuwa Biblia ya kiingereza ya King James katika maandiko au maneno AKAPITA KATI KATI YAO AKAENDA ZAKE yanasomeka katika Luka 4:30But HE PASSING THROUGH THE MIDST OF THEM and went his way” na Katika hali kama hiyo tena Yohana 8:59 andiko lile LAKINI YESU AKAJIFICHA, linasomeka kwa kiingereza “then took they up stones to cast him, BUT JESUS HID HIMSELF and went out of the temple, GOING THROUGH OF THEM and so passed byYohana 10:39 “Wakatafuta tena kumkamata; lakini akatoka mikononi mwao.” Kumkamata Yesu halikuwa jambo rahisi kama watu wengi wanavyoweza kudhani, Hapa huu ulikuwa ni muujiza wa wazi, aidha kwa mujibu wa wanatheolojia wengi, walipigwa upofu, au walipigwa gazi, au Yesu alitoweka kwa jinsi ya muujiza biblia ya kiyunani inatumia maneno haya “DIELTHON DIA MESOU EPOREUETO”  kwa kiingereza  “But Passing through their midst he went his way”  kwa hiyo neno EPOREUETO  ambalo kiingereza klinasomeka “WENT HIS WAY”  pia linasomeka kama  “TRAVERSE” ambalo tafasiri yake inaweza kusomeka kama KUTOKOMEA, kama vile kitu kinapopotelea mwisho wa mto, au ndege inapopaa na ikapotelea angani, au meli inavyosafiri na kutokomea nje ya upeo wa macho ya kibinadamu kwa hiyo ukiangalia kwa undani sana swala hili utaweza kuona “HE BECAME INVISIBLE” yaani alitoweka na kuendelea na shughuli zake sehemu nyingine, kwa kukosa neno zuri la kuelezea ndio Yiohana anatumia neno kujificha au kutoweka mikononi mwao na Luka anaelezea vema kupita katikati yao na kwenda zake!

Katika maandiko hayo ya msingi utaweza kujiuliza maswali mengi kwamba ilikuwaje kuwaje Yesu, akapita kati ya watu waliokuwa wamekusudia kumdhuru, na kumuumiza, au inawezekanaje mtu ambaye watu wote wanamuangalia anajificha kama biblia ya Kiswahili ilivyotumia neno hilo kwenye injili ya Yohana na watu walikuwa wamekusudia kumkamata na kumtupa nje ya kilima wakiwa wamejaa ghadhabu?, watu wenye nguvu na ambao tayari walikuwa wamekwisha muweka mikononi mwao, ukweli ni kuwa kulikuwa na nguvu ya ziada na ya kiungu ya kupita kawaida ambayo wakati mwingine iliwafanya maadui wasimuone, yaani walipigwa upofu na kufanywa wasimtambue na hili lilikuwa ni jambo la kawaida kuweza kufanyika  mfano, angalia watu hawa:-

Luka 24:13-16 “Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue.”

Mungu katika mpango wake anazo njia zake za kuwaficha wapendwa wake ili wasidhurike na hatari ya aina yoyote ile, Ndio maana tunapokuwa na Mungu hatupaswi kuogopa jambo lolote lile, hatupaswi kuogopa wingi wa majeshi ya maadui,  wala mipango mikakati ya adui zetu kutuangamiza na kututupilia mbali, tunapaswa, tu kufahamu kuwa kuna wakati Mungu yu aweza kuwapiga upofu maadui zetu na wasituone na kuwa tunaweza kupita katikati yao na kuendelea na shughuli zetu bila madhara, Mungu ameahidi kutuokoa na mitego yote ya adui ona Zaburi 124:6-7 “Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokokaMungu ameahidi kutuokoa kama nudge anavyonusurika katika mitego ya adui, Jambo alilolifanya Yesu Kristo ni jambo la kawaida sana lililoweza kufanywa na manabii hata katika agano la kale, Wakati wa nabii Elisha yeye alitafutwa na jeshi kubwa sana la nchi ya shamu, na walikwenda maalumu kwaajili ya kumtafuta Elisha, na Elisha alizungumza nao vizuri tu  na kuwalisha kisha akwaacha waende zao ona

2Wafalme 6:8-23 “Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu kitakuwapo mahali fulani. Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami. Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili. Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli? Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala. Akasema, Enendeni, mkamwangalie aliko, nipate kupeleka watu kwenda kumchukua. Akaambiwa ya kwamba, Tazama, yuko Dothani. Kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote. Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote. Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha. Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria. Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, Bwana wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. Bwana akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria. Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige? Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao. Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli” 

Haijalishi kuwa leo mpendwa unapitia katika hali ya namna gani, inawezekana umebanwa kila upande, umezingirwa, na hali tata ambazo hujui utapenya vipi, kila kilicho kibaya kinakuandama na kukutafuta, adui wamejipanga kwamba wanakuharibia lakini leo nataka nikutie Moyo, ya kuwa upo muujiza wa kupita kati kati yao na kuenda zako, kwa amani, Muujiza huu unatuthibitishia ya kuwa adui hatatuona; Lakini sisi tutamuona na kuamua wapi pa kumpeleka na au wapi pa kupita, adui atadhani kuwa hatutaiona njia lakini Muuijza huu unatufundisha ya kuwa iko njia hata katikati ya kibano, ambacho kwa akili zako unaweza kudhani ya kuwa hutapenya lakini kwa neema ya Mungu utapenya, wiki hii kidato cha nne watakuwa na mitihani ya kitaifa na wengi wanaweza kuwa wanaogopa kwamba itakuwaje au wanafikiri itakuwaje hata wazazi wanaogopa na walimu vilevile tunawaza itakuwaje hofu inatufunika kana kwamba ule mtihani tunakwenda kufanya sisi, tunawaza tunavukaje? na pengine ibilisi amekusudia kukukwamisha na kukutupilia mbali ili kwamba historia yako isiwepo tena lakini nataka kukuthibitishia ya kuwa bwana anakusudia kukupitisha katikati ya mtihani huu wa kitaifa na uende zako Hekaluni ukamtukuze Mungu, hatupaswi kuogopa kwa sababu Mungu ana njia nyingi” atakusaidia. Na nafsi yako itaokoka katika mikono ya adui zako kwa namna ya kushangaza! 

Isaya 43:1-2 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.”  
   

Na Rev. Innocent Kamote.

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!



Jumamosi, 6 Novemba 2021

Kujengwa kwa Hekalu bila kelele!


1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.”               

Utangulizi:

1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba”                

Moja ya mambo makubwa sana na ya kushangaza ya zamani ni pamoja na teknolojia waliyoitumia katika ujenzi. Uwezo wao na ustadi wao wa ujenzi ulikuwa ni wa hali ya juu sana, Hekalu la Suleimani limeingia katika orodha ya moja ya maajabu makubwa ya kale ya Dunia kutokana na ubora na uzuri wake, Ujenzi wake ulitawaliwa na utulivu mkubwa sana, tunasoma kwamba wakati Hekalu la ibada lililokuwa linajengwa na Sulemani, wajenzi walihakikisha kila pande la tofali linalohusika katika ujenzi, linachongwa mbali na eneo la ujenzi huko kware (Mgodini walikochonga mawe) walikuwa makini kuchonga kila jiwe kwa ufanisi mkubwa na jiwe lilipokuwa tayari, lilipelekwa eneo la ujenzi wa Hekalu na likajengwa bila kelele yoyote kusikika.

Mawe yaliyotumika hayakuwa madogo na wala hayakuwa na maruturutu yaani yalikuwa yamenyooka, waliyaleta mawe hayo yalikuwa makubwa, yalikuwa ya thamani sana ambayo yalikwishachongwa mgodini ona:-

1Wafalme 5:17-18 “Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa. Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.”

Mawe hayo ya thamani kubwa yalichongwa na kuandaliwa mgodini, mbali na eneo la ujenzi, kisha yakaletwa mjini wakayaweka tayari, Wajenzi wa Suleimani na Hiramu na Wagebali hawa walikuwa wataalamu maalumu wa shughuli ya ujenzi huo wa Hekalu.  

Katika namna zote mbili yaani kimwili na kiroho, uzuri na ufahari na taratibu za ujenzi wa Hekalu ulikuwa ni mradi unaosimamiwa na Roho Mtakatifu maandiko yako wazi kuwa sisi ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Waefeso 2:19-22 “Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.”

Kila mtu aliyeokolewa ni hekalu la Roho Mtakatifu, kila mmoja ana thamani kubwa sana wote tumechongwa kwa jinsi ya kipekee mgodini na wote tumeletwa ili tuwe nyumba ya Mungu, na kuwa tumuabudu yeye na kuishi kwa amani bila malumbano wala mafarakano, kwa sababu kama mawe ya thamani kila mmoja lina thamani yake na linafaa kukaa pale lilipokusudiwa ona

1Petro 2:4-5“Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.       

1Wakorintho 3:16-17 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.”     

1Wakorintho 6: 19-20Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

Kwa hiyo tunakubaliana na maandiko kuwa kila aliyeokolewa ni Hekalu la Roho Mtakatifu na kwa umoja wetu ni jengo la Mungu na kila mmoja ni jiwe la thamani lililochongwa kwa ustadi, kutoka katika mgodi au kware ya giza iliyoko duniani na kuletwa na kuungamanishwa na Yesu Kristo ambaye ni jiwe kuu la pembeni, jiwe la msingi, hatujajichagua wenyewe bali ni Mungu ndiye aliyetuchagua  na kutuleta katika jengo lake, ili tumtukuze yeye na tena tumuabudu yeye na kumtumikia bila ya hofu yoyote.

Kwa nini hekalu halihitaji kelele?

Mungu amekusudia kutufanya sisi kuwa watu wake, na amekusudia kutupa utulivu, kelele asili yake ni huko mgodini, wakati wote unapotembelea mgodi au kware utasikia milipuko mikubwa ya kuvunjwa kwa mawe na mafundi wakitumia makrasha au mashine maalumu za kuvunja mawe, huko mafundi watayachonga mawe lakini yanapoletwa katika Hekalu yanakuwa tayari yanafaa kwa ujenzi, kelele zinawakilisha maisha ya duniani, kelele zinawakilisha taabu na uusumbufu wa kuwa nje ya uwepo wa Mungu, Kelele zinawakilisha hofu, kelele zinawakilisha kuwa uwepo wa Mungu umetoweka, kelele zinawakilisha hakuna ujenzi, bali kuna kuvunja vunja na kubomoa, na kuharibu.

Mahali kwenye hofu ya kifo, hofu ya utumwa hofu ya uvamizi, hofu ya uharibifu, hofu za maisha, hofu ya njaa, hofu ya kesho itakuwaje  ni mahali penye kelele  ni nje ya uwepo wa Mungu sio hekaluni, unapokuja kwenye uwepo wa Mungu Roho Mtakatifu tunapata utulivu wa ajabu na amani na tunatengwa mbali na kelele. Mungu amekusudia kumtenga kila mmoja wetu na kelele na kumpa kila mmoja wetu utulivu na amani.

Hutaogopa majeshi hodari yatatapopanga vita kwaajili yako Bwana anajua kuwa wewe ni hekalu lake kwa hiyo majeshi ya upinzani yatanyamazishwa, wakati wote Mungu Kama Mchungaji wetu hutuongoza katika maji ya utulivu

Zaburi 23:1-2, “Bwana ndiye Mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabishi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza

Israel walipomlilia Musa kwa sababu ya Majeshi ya farao yaliyokuwa yakiwafuatia kwa nyuma ili kuwarejesha tena utumwani, Musa alitoa unabii ya kuwa Bwana atawapigania nao watanyamaza kimyaa! Mungu anafahamu ya kuwa wanadamu wanahitaji utuilivu wanahitaji ukimya! Wanahitaji amani, wanahitaji kuwa mbali na hofu, wanahitaji maisha ya ushindi, wanahitaji kuthibitishiwa kuwa watakuwa mbali na kelele za kila aina:-

Kutoka 14:13-14 “Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya

Mungu atakustarehesha katika maskani yake utaburudishwa hata kutokee matetemeko, mafuriko sunami na mabadiliko yoyote yale sisi tunaokimbilia kwa Mungu kamwe hakuna atakayeogopa hakuna atakayetetemeshwa ukiwa katika uwepo wa Bwana ushindi unapatikana mapema asubuhi tu

Zaburi 46:1-5Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu. Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.”

Wewe unapokuwa Hekalu la Mungu huna sababu ya kupiga kelele, wala huna sababu ya kutikisika Mungu anafahamu wazi kuwa tunahitaji utulivu, tunahitaji kuwa kimya kisha yeye ataleta ukombozi, Daudi kila alipokuwa anakabiliwa na changamoto za aina mbalimbali alikumbuka anapaswa kutulia kimyaaaa na Mungu huyu yeye mwenyewe atazimaliza kelele

 Zaburi 62:1-2 “Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.”

Wanadamu hawapaswi kusumbuka, kama umechoshwa na kelele za dunia umechoshwa na wavunja mawe, kelele za kware, kelele za migodini wewe mfanye Bwana kuwa ndio mchungaji wako, utapata kila aina ya utulivu, utaandaliwa meza mbele za adui zako machoni pa watesi wako, hutakufa, hutaogopa mauti, utafarijiwa, utapata upako, nafsi yako itahuishwa, Baraka zitafurika nawe utakaa nyumbani mwa Bwana milele yaani kwenye utulivu!

Zaburi:23:1-6 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.”

Unapoona kelele maana yake nini?

Tunaweza kujibu kwa ufupi kuna uharibifu, mtu mmoja alisema kwa kiingereza hivi nanukuu “Destructive work is noisy, constructive work is silent” Kazi ya uharibufu ni ya kelele, na kazi ya ujenzi ni ya kimyakimya” Madhabahu ya Mungu ilikusudiwa pawe mahali pa ibada na hivyo katika torati Mungu aliagiza madhabahu isijengwe kwa kutumia chombo cha chuma yaani isichongwe! Kule kuchongwa kungeleata kelele ambazo Mungu hakutaka kuzisikia kupitia madhabahu yake au hekalu lake, kutumia chombo cha chuma kuichonga madhabahu au hekalu kungeweza kulitia unajisi hekalu!

Kumbukumbu 27:5-6“Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake. Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;”

Kutoka 20:25 “Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi.”

Kwa hiyo unapoona kelele Katika ujenzi wa hekalu maana yake ni kuwa;-

# Watu wameacha kufanya kazi waliyoitiwa wanafanya biashara nyingine Marko 11:15-17 “Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa; wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu. Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.”               

# Watu wakiwa mwilini, yaani udunia ukiingia, hekalu linakuwa na kelele 1Wakoritho 3:1-7  Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”

#Watu wameingiwa na tamaa ona Yakobo 4:1-5 “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?”

# Kila mtu anapokuwa na nia yake 1Petro 3:8-13 “Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya. Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?”

# Watu wema wanaposhikamana na waovu 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”

# Mbinguni hakutaingia chochote kilicho kinyonge

Ujenzi huu wa ajabu ambapo mawe yalikuwa yakichongwa mbali, huko kware au mgodini, yaliletwa katika kiwanja cha hekalu yakiwa yamekamilika unatukumbusha wazi kuwa shemu ya kuchongwa watu ni hapa duniani, Roho Mtakatifu hufanya maandalizi ya kutuandaa na kutuchonga tukiwa hapa Duniani, anatukarabati ndani na nje ili tufae kuwa chombo cha sifa na ibada lakini zaidi  kwamba baadaye tuweze kufika Mbinguni ambako huko ni eneo la utulivu na hakuna kuchongwa tena tutaingia tukiwa tumekamilishwa baada ya kupitia mchakato wa utakatifu duniani kule mbinguni hakuna chochote kilicho kinyonge kitakachoingia,

Wafilipi 1:6 “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;”

kila mmoja anapaswa kujiweka wakfu kwa maneno kama yale ambayo Suleimani aliyasema siku alipokuwa akiliweka wakfu Hekalu, alisema

1Wafalme 8:13 Hakika nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. Meno ya kiingereza ya mstari huu ni matamu zaidi kwani yanasema hivi “I have indeed built you exalted house, a place for you to dwell in forever” Mungu anataka tuwe makazi yake milele.

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Jumatatu, 1 Novemba 2021

Maisha ya viwango!


Warumi 12:1-2 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”

 


 Utangulizi:

 

Wote tunafahamu wazi ya kuwa tunaishi katika ulimwengu, unaoendeshwa kwa viwango, na kwa namna Fulani hatuwezi kamwe kukwepa kuishi kwa viwango, Dunia ina viwango vyake, na vingine tunavitumia katika maisha yetu ya kila siku, Lakini neno la Mungu vilevile linatuelekeza kuishi kwa  kiwango kinachokusudiwa, katika maandiko yaani neno la Mungu,  tunasoma hivi katika Warumi 12:1-2 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”Kuna neno muhimu ambalo hatuna budi kuliangalia kwa undani ili tuweze kupata maana iliyokusudiwa hususani neno MSIIFUATISHE NAMNA, na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo matatui yafuatayo:-

 

·         Maana ya Viwango

·         Umuhimu wa Viwango

·         Jinsi ya kuishi kwa Viwango

 

Maana ya viwango:-

 

Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Hebu tuliangalie andiko hilo vilevile katika tafasiri za kiingereza  ya New International Version (NIV) andiko hilo linasiomeka hiviDo not conform to the pattern of this world, but be transformed by the renewing of your mind, then you will be able to test and approve what God’s will is –his good, pleasing and perfect will.” Unapoangalia sasa tafasiri ya Biblia yetu ya Kiswahili na kiingereza utaweza kuona neno “MSIIFUATISHE NAMNA” Na Katika kiingereza cha NIV “DO NOT CONFORM TO THE PATTERN” maneno hayo sasa katika biblia ya kiyunani yanasomeka kama “PROTYPO” ambalo sasa maana yake halisi kwa kiingereza ni Standard, au Pattern, au Norm, au Exemplar, au Archetype, au Measure, au meter, au Gauge, au measurement, au values. Kwa hiyo utaweza kuona kwa mfano Biblia ya tafasiri ya kiingereza ya Good News inatumia maneno hayaDo not Conform yourselves to the STANDARDS of this world, but let God transform you inwardly by a comlete change of your mind. Then you will be able to know the will of God- what is good and is pleasing to him and is perfect. Kwa msingi huo ni kama neno la Mungu linawataka watu waliookolewa au wanaomcha Mungu kutokuishi sawa na viwango vya ulimwengu huu, Maana yake ni kuwa kuna aina ya kiwango cha maisha ambacho Mungu anakikusudia kwetu! Na maandiko yanataka tuishi zawa na viwango hivyo. Kwa hiyo neno Standard sasa tafasiri yake ni a level of quality or attainment, au Something used as a measure, norm or model in comparative evaluations, something used or accepted as normal or average, ni kipimo kinachohusika kupimia ubora wa mambo, wastani wa mambo, kwa kulinganisha na mengine

 

Umuhimu wa viwango:-

 

Katika ulimwengu tulio nao, viwango vina umuhimu mkubwa sana, na dunia ina vipimo vingi sana vya kupima ubora wa mambo kwa kina, mapana, na marefu, tunaishi katika ulimwengu ambao unajua kupima, na thamani ya kitu hupimwa kutokana na kiwango kinachokusudiwa, wakati mwingine fahari ya kitu Fulani duniani hata kama hakina maana inaangaliwa sana na ubora wa kiwango chake, sio hivyo tu watu wanaotumia kitu chenye ubora wa hali ya juu, huweza kujisikia kuwa wao ni maalumu sana na wakati mwingine hata kujivunia kitu hicho na kuwa na furaha kwa sababu kina ubora! Kwa hiyo dunia ni dunia ya viwango! Kila kitu duniani kinapimwa kutokana na kiwango chake!, Mataifa mengi yana mashirika yanayohusika na kupima au kuangalia viwango vya bidhaa, hapa Tanzania bidhaa huthibitishwa ubora wake kupitia shirika la (TBS) yaani Tanzania Bureau Standard , wao wakisha thibitisha kuwa kitu hiki kina ubora huweka neno yao, yako mashirika mengine pia ya kidini kama ya kislamu, huweka neno Halal au Haram kwa manufaa ya bidhaa hiyo kutumiwa na imani ya watu hao, Mashirika haya pia hufanya kazi ya kudhibiti bidhaa fake au zisizo na ubora, kwa hiyo dunia ina utaratibu wake wa kuweka kitu katika viwango mfano;-

 

·         Mataifa kwa mfano yako mataifa yanayoitwa yaliyoendelea na yanayoendelea, Developed and underdevelopment country (nchi zenye uchumi wa juu, wa wastani wa kati na wa chini)

·         Taaluma kwa mfano kuna Elimu ya juu na Elimu ya chini, Graduates and undergraduates

·         Matokeo ya mitihani secondary yanapimwa kwa migawanyo ijulikanayo kama Division I,II,III,IV na 0

·         Matokeo ya vyuoni zile degree ziko za aina saba kwa waingereza zinapimwa kutokana na viwango vya GPA yaani Grade Point Average, Marekani wao degree ni degree tu Lakini Waingereza Degree zao wanazigawanya kwenye maeneo saba mfano:-

 

*      Ukipata 70-100 utatunukiwa  degree First Class with honours ambayo ina GPA 4.0

*      Ukipata 65-69   utatunukiwa degree Upper second Class honours ambayo ina GPA  3.7

*      Ukipata 60-64   utatunukiwa degree Upper second class honours ambayo ina GPA 3.3

*      Ukipata 55-59   utatunukiwa degree lower Second class honours ambayo ina GPA 3.0

*      Ukipata 50-54   unatunukiwa degree lower second class honours ambayo ina GPA 2.7

*      Ukipata 45-49   unatunukiwa degree Third Class honours ambayo ina GPA 2.3

*      Ukipata 40-44   unatunukiwa degree Third Class honours ambayo ina GPA 2.0

 

·         Sio hivyo wote tunafahamu kuwa kuwa aina za simu tunazomiliki pia zina namna watu wanaziweka katika ubora, i-phone, sumsung, Nokia, Siemens, Motorola infinix, techno na kadhalika lakini sio hivyo tu zinatengenezwa wapi

 

·         Kumbuka hata aina za magari ambazo wazazi wetu wanamiliki yana ubora, wake, mabati, cement, unga na kila kitu duniani kinapimwa kutokana na ubora wake

 

·         Ni katika hali kama hiyo vilevile Mungu atazipima kazi ya kila mmoja na maisha ya kila mmoja duniani kwa msingi huo basi namna tunavyomtumikia Mungu duniani katika Nyanja yoyote ile mwisho wa siku Mungu atazipima kazi zetu kuwa zina thamani ya kiwango gani ona

 

1Wakoritho 3:12-15 “Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.”

 

Viwango ni Muhimu kwa sababu ndivyo vinavyotofautisha katia ya ubora wa jambo Fulani na lingine katika maisha yetu Mungu namekusudia sisi tuwe na viwango vya juu sana vya maisha tukiishi kwa viwango vya juu kabisa vya ubora Mungu atajivunia maisha yetu, Mungu hujivunia watu wake wanaoishi kwa ubora alioukusudia hapa Duniani lakini Mungu pia huuzunishwa tunapoishi chini ya kiwango ona 

 

Ayubu 1:1-8 “Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki. Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote. Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.  Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.”

 

Tunapoishi kwa kiwango Mungu hujivunia sana lakini tukiishi chini ya kiwango tutadharaulika, Paulo Mtume alimtaka Askofu kijana Timotheo kuzingatia kutunza ubora wake  katika Nyanja zote za usemi, mwenendo, imani, upendo na usafi, ili asije akadharaulika  ona

 

 1Timotheo 4:12-14 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha. Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.”

 

Jinsi ya kuishi kwa viwango:      

 

Warumi 12:1-2 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”

 

Mungu anamtarajia kila mmoja wetu kuishi kwa viwango vya juu ambavyo sio vya ulimwengu huu jambo hili linawezekana na ndio maana maandiko yanamtia moyo kila mmoja kuishi katika viwango vya juu, ushindi wetu dhidi ya adui yetu shetani na mafanikio kadhaa ya ahadi za Mungu kwetu yamewekwa katika kiwango, kila siku kuna kiwango ambacho Mungu amekusudia ukiishi  na ukifikie, kiwango cha juu cha kuishi maishanyanayompendeza Mungu ni kuishi maisha ya utakatifu, na kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo, hilo ndio lengo letu kuu.

 

1Petro 1:14-16 “Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”

 

Tukiishi maisha matakatifu tutaweza kufurahia kwa kiwango cha juu yale ambayo Mungu ameyakusudia kwetu katika ahadi zake na katika neno lake ili tuweze kufikia kiwango ambacho Mungu anakitaka hatuna budi kufanya yafuatayo.

 

1.       Amua kuishi kwaajili ya Mungu, Mungu ametupa kuchagua uzima au mauti laana au Baraka  Kumbukumbu 30:19-20 “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.”

               

2.       Vunja uhusiano na watu wasiomcha Mungu 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike

 

3.       Acha tabia mabaya zisizofaa na ufanye mwili wako kuwa Hekalu la Mungu Roho Mtakatifu  1Wakoritho 6:19-20 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

 

4.       Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha na Mungu atakupa rehema na neema ya kuishi maisha ya viwango Mithali 28:13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”

 

5.       Soma neno la Mungu kila siku na kuliishi Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”

 

6.       Chukia anachochukia Mungu na penda anachokipenda, usifanye maovu na Mungu atakutumia sana  Mungu Daniel 11:32 “Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.”

 

Kumbuka kuwa bidhaa nyingi zisizokidhi viwango huchomwa moto na kuteketezwa, kabisa, Mungu hataruhusu chochote kilicho kinyonge yaani kilicho chini ya ubora wake kingie mbinguni ona Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Hatuna budi kumuomba Mungu atuongezee viwango, atpeleke katika kiwango cha juu, na atupe neema ili kwamba tusiishi sawa na viwango vya watu wa dunia hii, bali sisi tukapate kuishi kwa kiwango cha juu, tukamtumikie Mungu kwa kiwango cha juu, kila tunachokifanya tuhakikishe tunakifanya kwa kiwango cha juu, Mungu ni Mungu wa viwango pia.

 

Na. Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!