Alhamisi, 29 Julai 2021

Mapepo yasalimu amri ya Mpiga Kinubi !

1Samuel 16:23 “Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.”



Utangulizi:

Moja ya maswala ya msingi sana katika mafundisho ya Biblia ni pamoja na swala la kusifu na kuabudu, wote tunafahamu jinsi ibada ya kusifu ilivyo na nguvu kubwa sana, na mara kwa mara maandiko yameonyesha Muitikio wa Mungu kufanya mambo makubwa sana pale anaposifiwa kwa njia ya nyimbo na vyombo mbalimbali kama kinanda, gitaa, ngoma na kwa lugha ya zamani kinubi. Na ndio maana utaweza kuona kuwa kusifu kwa njia ya vyombio na uimbaji stadi ni moja ya amri za kimaandiko na ushauri unaotolewa na mfale Daudi ona

Zaburi 33:1-4 “Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni Bwana kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe. Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.

Ziko sababu kadhaa kwanini Maandiko yanashauri hivyo  na daudi ni mojawapo ya watu waliokuwa waanzilishi na watu wenye moyo mkubwa wa ujuzi wa nguvu iliyioko katika sifa, katika maandiko kwa ujumla tunaona wazi nguvu iliyoko katika kusifu na kuabudu, lakini sio hivyo tu kuna faida kubwa na nyingi mno katika kumuimbia Mungu kunakoambatana na vifaa vya muziki

1.       Kusifu kunatupa njia ya kumfikia Mungu  Zaburi 100:1-5 “Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba; Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.” Kusifu katika ibada ndio ufunguo wa kuingia katika uwepo wa Mungu, jambo moja la kusikitisha sana ni kuwa katika makanisa mengi watu hufikiri kuwa ibada ya sifa ni ufunguzi tu wa ibada na kuwa sio sehemu muhimu ya ibada kwa hivyo utaweza kuona kuwa Watumishi wengi wa Mungu na wakati mwingine hata wageni wao hawajitokezi wakati wa sifa katika ibada na hujitiokeza baadaye sana wanapokaribia kupanda madhabahuni kwaajili ya kuhubiri  hili ni tatizo kubwa mno, Kusifu na kuabudu si sehemu ya kumfungulia mchungaji ibada au kulainisha mioyo ya watu ili neno la Mungu liingie vizuri ni sehemu kamili nay a muhimu sana ya ibada.

 

2.       Kusifu kunasambaratisha Kazi za adui Biblia  inataja neno kusifu kwa mara ya kwanza mara baada ya kuzaliwa kwa Yuda katika Mwanzo 29:35 “Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.” Jina Yuda maana yake Sifa au Kusifu haiajalishi utalikuta wapi jina hilo vyovyote iwavyo linamaanisha sifa, Maandiko yanamtaja Yesu kama Simba wa kabiola la Yuda ambaye ameshinda ona

 

Ufunuo 5:5 “Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.” Mara nyingi tunatembea tukiwa na hofu, dhidi ya shetani, mawazo yako, jirani zako na tunahofu ya kuwa nini kitatokea kwetu, Adui yetu mkuu ni Shetani yeye anatajwa katika maandiko kama simba aungurumaye ona katika

 

1Petro 5: 8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.”          

 

Hata pamoja na kutajwa hivyo katika maandiko ni muhimu kwetu kufahamu kuwa shetani pamoja na majeshi yake yote hayawezi kustahimili kwa simba wa Kabila la Yuda, wakati wana wa Israel wanataka kuichukua nchi ya kanaani na kupambana na adui zao walimuuliza Bwana ni nani atatutangulia Mungu aliwajibu Yuda atawatangulia mbele yenu, kinabii Mungu aklikuwa anaonyesha Sifa zikitangulia hakuna adui atakayeweza kusimama

 

Waamuzi 1:1-2 “ Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao? Bwana akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake.”   

 

Hii inatufundisha wazi tunapokuwa na vita ya kimwili au kiroho sifa itatangulia na itatuletea ushindi ona

 

2Nyakati 20:14-24 “Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya Bwana, katikati ya kusanyiko; akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu.  Kesho shukeni juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli.  Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi. Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana. Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana. Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka.”

 

Kumbe kuna vita nyingi sana ambazo wala hatukutakiwa kuzipigana kutanguliza sifa mbele ya jeshi kunatosha, sifa ni silaha kubwa sana katika ulimwengu wa roho inafanya kazi ni zaidi ya upanga wa adui tunapaswa tu kumuamini simba wa kabila la yuda na kujua ya kuwa atatupa ushindi, kwa hivyo iko siri kubwa sana katika kumsifu Mungu, adui atakimbia na kurudi nyuma na kusambaratika endapo tu tutatambua umuhimu wa kumsifu Mungu kwa nguvu zetu zote, akili zetu zote na ujuzi ufundi na ustadi wetu wote.

 

3.       Kusifu kunafungua milango ya vifungo – Matendo 16:24-26 “Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.Tunaona nguvu kubwa ya sifa kwamba sifa zinauwezo hata wa kufungua makomeo ya gereza kama ilivyokuwa hapa kwa Paulo na Sila hii maana yake hata magereza nyingi na vifungo vingi ambavyo tumefungwa na ibilisi, wachawi, wagananga na watu wenye jicho baya vinaachia ikiwa tu tutamsifu Mungu, ni wazi kuwa Paulo aliijua siri hii na Daudi aliijua siri hii na ndio maana maisha yao yote waliyaelekeza katika kumsifu Mungu siku zote

 

Mapepo yasalimu amri ya mpiga kinubi

Tumetambua kuwa kuna siri kubwa sana katika kumsifu Mungu, maandiko katika agano jipya yameamuru tuimbe zaburi pamoja na tenzi za rohoni kwa kadiri ya neema ya Mungu mioyoni mwetu ona Waefeso 5:19 “mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;” na Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” Maandiko yanataka tuimbe kwa moyo, kuna siri ya ajabu katika kumsifu Mungu kwa kuimba kunakoambatana na vyombo, Daudi ni mtu wa Muhimu na wa msingi aliyekuwa na ujuzi huo, mapema sana katika ujana wake na utoto wake alikwishakugundua siri inayokaa katika kusifu, Alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga kinubi mpaka mtu aliyekuwa na mapepo, pepo waliondoka na kumuacha hivyo mapepo yalisalimu amri ya mpiga kinubi 1Samuel 16:23 “Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.”

Hii inatufundisha kuwa ingawa Mungu alimpeleka Daudi katika kumtumikia Sauli lakini kijana huyu alikaa ikulu na kujifunza maswala kadhaa ya uongozi, huku akiendelea kupiga kinubi ambacho kiliondoa msongo wa mawazo kwa Sauli na kusababisha uponyaji hii ni dhahiri pia kwetu kwamba kumbe tukimsifu Mungu na kuwa na ufahamu kuwa kuna kitu cha ziada katika kumsifu Mungu, uweza wa Mungu tatatngulia, utafungua milango kwaajili yetu, utamfukuza mbali adui, uatasababisha adui asambaratike lakini mapepo yatakimbia roho mbaya zitaondoka, Daudi alikuwa mpiga kinubi hodari mno na anakumbukwa kwa uandiahi na utunzi wa zaburi nyingi sana na hata leo ukienda Israel utaweza kuona kuwa amejengeea sanamu yake ambayo inaoneysha wazi akiwa nameshikilia kinubi, mapepo yasalimu amri ya mpiga kinubi, sisi nasi ni muhimu kwetu kuwa na ujuzi na ufahamu huu na khakikisha kuwa tunamsifu Mungu na kumpoigia vigelegele na kumuinua na kusababisha ushindi mkubwa na nguvu za giza kutoweka hii itatokea na inaendelea kutokea kwa kila mtu anayetambua umuhimu wa kusifu katika jina la Yesu amen.

 

Na. Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumatatu, 26 Julai 2021

Ilikuwa vile ili iwe hivi!

Mwanzo 50:19-20 “Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.”


Utangulizi:

Je umewahi kutokewa na jambo gani baya duniani ambalo hutaweza kulisahau katika maisha yako? Ukiulizwa swali hili unaweza kutokwa na machozi na kujibu ni habari ndefu sana ndugu yangu, na unaweza kuvuta Pumzi na kuwa tayari sasa kusimulia yaliyokusibu!

Leo nataka kukuambia wazi kuwa hakuna jambo linoalotutokea Duniani liwe jema au baya ambalo linaweza kuzuia kusudi la Mungu ndani yako, Kusudi la Mungu ndani yako haliwezi kuzuilika.  Ayubu 42:2 “Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.” Mungu huweza kuitumia njia yoyote ile hata nia mbaya za watu kwa kusudi la kutuleta katika jambo jema, Hilo tunalijua! Tunajua kuwa njia za Mungu ziko juu sana kuliko mawazo ya kibinadamu, tunafahamu kuwa upumbavu wa Mungu una hekima kuliko uweza, ujuzi, ufahamu na maarifa ya kibinadamu

Warumi 8:28-30 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.”

Kila linalokutokea duniani hata kama linaonekana kuwa baya kwa wakati huo, ila ukakumbuka kuwa uko katika kusudi la Kiungu, basi ni vema ukafahamu kuwa Mungu yuko pamoja nawe hata katika hayo magumu unayoyapitia ili hatimaye aweze kuleta jambo jema, aweze kutokeza jambo zuri kwa utukufu wake  hata kama hujui kwa sasa, baadaye utakubaliana nami kuwa ilikuwa vile ili iwe hivi!

Ilikuwa vile ili iwe hivi!               

Mfalme mmoja alikuwa na punda wake amba0 aliwapenda sana, ikawa siku moja punda hao walidumbukia kwenye shimo kubwa sana ambalo ilikuwa ni vugumu kuwatoa, basi alijaribu kila njia lakini njia zote zilishindikana, hatimaye kwa masikitiko makubwa na kwa hasira aliamua kwamba atawazika punda wale katika shimo lile, hivyo aliagiza watumwa wake walete udongo na kuwafukia punda wale katika shimo lile wakiwa hai!

Kazi ya kuwazika Punda wakiwa hai ilianza watumwa walichimba udongo na kuusombelea kwa kusudi la kuwafukia punda wale, na kazi hiyo ikaaanza na kuendelea, hata hivyo bila watumwa wale kuelewa Punda wale kila walivyokuwa wakimwagiwa udongo wao walikuwa wakijikung’uta madongo yale  na hali hiyo iliendela mpaka shimo lile likajaaa na kumbe katika hali ya kushangaza punda wale walijikuta wanakuwa juu ya udogo uliokuwa umekusudiwa wazikwe na waliokuwa wakijikung’uta hivyo walijikuta juu ya shimo lililokuwa limejaa udongo na wao wakiwa wanajikung’uta na hivyo waliweza kutoka kwa urahisi sana !  na maisha yakaendelea! Unajua nini ilikuwa vile ili iwe hivi!

Wote tunajua habari za Yusufu, kwamba Ndugu zake walikuwa wamekusudia kumuua, lakini vilevile walimuuza Misri,  wakati huu haukuwa wakati mzuri kwa Yusufu kwa vyovyote vile, Ndugu zake ambao pia kwa wivu waligeuka kuwa adui zake walikusudia kumuangamiza na kuua kabisa ndoto zake ambazo zilikuwa zinawakera japo ndoto zile zilikuwa zimebeba kusudi la Mungu kwa manufaa ya wote! Wao walikuwa kweli wamemkusudia mabaya lakini ni ukweli ulio wazi kuwa  Mungu aliyakusudia mapito yake kuwa  mambo mema.  Mwishoni walitahayari, walimuinamia wote walimuomba radhi walifikiri atalipiza kisasi Lakini Yusufu Alikuwa amewasamehe kabisa, Mambo mema yalikuwa hitimisho la chuki zao

Mwanzo 50:19-20 “Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.” Yusufu ni ka ma alikuwa anawaambia ilikuwa vile ili iwe hivi, Ndugu msomaji wangu mimi binafsi siyajutii mapito yangu, niliumia wakati napita lakini najua ilikuwa vile ili iwe hivi, vyovyote vile, waltu walifanya hila, watu walitaka kua huduma, watu walitaka tusihubiri tena, watu walipigwa upofu, watu walijawa na wivu au chuki au uchungu au walikuwa wanaogopa nafasi zao vyovyote vile najua ilikuwa vile ili iwe hivi, hata kama sasa kuna unayoyapitia na inawezekana hujui kwanini unayapitia kumbuka tu iko hivyo ili iwe vile ahaaaa Mungu ana kusudi jema na maisha yako

Wako watu wanatamani utoweke, wanatamani wasikuone tena, wanateseka kwa wivu, wamejaa wivu wenye uchungu,  hwafurahii chochote chema kinachoendelea katika maisha yako, wanataka uteseke, wanataka ukione cha mtemakuni, wanataka upate taabu, na wakati mwingine kwa ujinga na upofu wanafikiri mawazo yao ya kijinga yanatoka kwa Bwana! No Mungu ni mwema wakati wote, Mungu anawachungulia na kuwacheka, waoa wamejaa chuki sana basi tu kwaajili ya uchungu mioyoni mwao, wanataka kukuzika ilihali uko hai, utasikiwa wanesema jamaa kwishinei, Jamaa ndio basi, waene vile waangalie kwanza nisikilize nataka nikutie Moyo kuwa hata kama hila zao zinaonekana kuwa zinafanikiwa kinyme na maisha yako  nataka nikuambie ni kwa kitambo tu, madamu jambo lako, maisha yako tumaini lako liko kwa Mungu, Mungu hajaishiwa mbinu za wokovu  wakati wao wanatufukia kumbe bila kujijua wanatuleta juu, wanatupeleka mahali ambapo tutalitimiza kusudi la Bwana Mungu wetu Haleluya! Usihuzunike wala kufadhaike katika hali yoyote unayoipitia kwa sasa unapopita unaweza usielewe ni kwa nini unapitia unachokipitia lakini baadaye utaelewa kuwa ILIKUWA VILE ILI IWE HIVI!

Isaya 55:8-9Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 

Tumanini Letu ni kwa Bwana Mungu wetu kwa maana ana uwezo wa Milele!

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Jumanne, 20 Julai 2021

Moyo wa ushujaa!

Kumbukumbu la Torati 31: 6 “Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.”


Utangulizi:

Neno la Mungu linamtaka kila mmoja wetu kuwa na moyo wa ushujaa, na kwamba tuwe hodari na kamwe tusiogope, na zaidi ya yote linatuhakikishia kuwa Mungu wetu atakuwa pamoja nasi katika yote tunayokabiliana nayo iwe jua iwe mvua neema ya Mungu inatosha kabisa katika kutufikisha katika mafanikio yote ya kimwili na kiroho tunayoyahitaji. Mungu huyu huyu aliyekuwa na wana wa Israel Jangwani kumbuka yuko pamoja nasi hata ukamIlifu wa dahari, Yuko pamoja nasi na zaidi ya yote amemuachilia Roho wake Mtakatifu mno eti akae ndani yetu, na kutuongoza na kutufariji na kutupa nguvu wakati wa mahitaji, kwa msingi huo hatupaswi kusitasita wala kuhofia au kuogopa jambo lolote zaidi ya kuwa na Moyo wa ushujaa! Biblia ya Septuajint version maneno moyo wa ushujaa yanasomeka hivi “Play the men and be strong”    au “Prove yourself a man” ambalo kwa tafasiri nzuri lingeweza kusomeka hivi “fanyeni kiume iweni na moyo wa ushujaa” unaweza kuona mfano katika 


1Wakoritho 16:13Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.”  Ni sawa na maneno ambayo Daudi alimuusia mwanaye Suleimani katika 1Wafalme 2:2-3 “Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume; uyashike mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;” 


Hatuwezi kuwa na mafanikio yoyote yale katika mwili na katika roho kama hatutakuwa na Moyo wa ushujaa. Maneno ya Mungu kupitia Musa mtumishi wake kwa wana wa Israel yalikuwa iweni na moyo wa ushujaa, simameni kiume, sina shaka kama jinsi ambavyo watu wote hawana shaka kuwa Mungu akisema yuko pamoja nasi basi yuko pamoja nasi kweli kweli, yeye sio kama rafiki zetu ambao wanaweza kukuambia tuko pamoja mzee lakini zinapotokea changamoto katika maisha yetu wanayeyuka, Mungu yuko Pamoja nasi kweli kweli, Lakini kama Mungu yuko pamoja nasi na anaendelea kuwa pamoja nasi, kwanini niwe au tuwe na moyo wa ushujaa?, kwanini maandiko yanatutaka tuwe na moyo wa ushujaa? Bila shaka hapa ndio kuliko na siri ya ushindi.


Israel walikuwa wanakaribia kabisa nchi ya kanaani, ilikuwa nchi njema kama Mungu alivyowaaminisha, Hata kama Israel ni jangwa kwa sehemu kubwa lakini ni nchi ambayo Mungu aliichagua ili aliweke jina lake na kutukuzwa kutoka hapo kwa dunia nzima kwa hiyo popote ambapo Mungu anasema ni pazuri ni pazuri, nchi hii ilikuwa njema, ilikuwa imejaa maziwa na asali, mizabibu na tini tende, na kadhalika na eneo zuri kwa malisho ya wanyama, lakini ilikuwa inakaliwa na wakanaani, na wakaani walikuwa hodari, walionekana kuwa majitu, na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maendeleo makubwa sana ikiwa imezungukwa na ngome zenye kutisha, walikuwa na utaratibu maalumu wa kiserikali walikuwa na wafalme na majeshi, walikuwa wameendelea kitaaluma kwa hiyo ni wazi kuwa Israeli walikuwa wakijilinganisha kwa namna yoyote ile na wakanaani, walijiona sio kitu, Lakini Mungu Yehova alikuwa amewaahidi kuwa atakuwa pamoja nao na kuwa wasiogope na kuwa hatawapungukia wala hatawaacha lakini jambo kubwa ilikuwa wawe na moyo wa ushujaa! Hilo tu ili kumiliki yale tunayopaswa kuyamiliki katika ulimwengu huu tunahitaji tu kuwa na moyo wa ushujaa ona 


Yoshua 1:6- 7 na 9 “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. 9Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”


Maana ya moyo wa ushujaa!

Kuwa na moyo wa ushujaa katika lugha ya kiibrania kulikuwa na maana ya kusimama kiume, au kuonyesha uanaume kweli kweli kwa kiingereza “Courage” ability to do something that which is frightens; bravery ambalo maana yake ni uwezo wa kufanya jambo lenye kutisha kwa werevu. Au kwa weledi, au nguvu ya kukabiliana na jambo lenye kutisha au kuogopesha au hatarishi kwa ushujaa mkubwa, ni uwezo wa kuamua kupambana na maumivu, tishio, mateso, hatari, au jambo lenye kutisha bila woga wowote, wala hofu yoyote, Ni uwezo wa kuthubutu kufanya au kukabiliana na jambo ambalo kwa akili za kibinadamu linaonekana kuwa gumu kwa imani kuwa utalifanikisha iwe mvua ama jua, kibiblia ushujaa huu unaambatana na kumuamini Mungu, ndio maana Mungu ameambatanisha na kuwa pamoja nasi, na ili kuiifikia ile ndoto, au lile tumaini au ile ahadi Waebrania 10:35-36 “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.” Kwa hiyo tunapokuwa na moyo wa ushujaa ndipo tunapoweza kupokea thawabu kuu na kutimiza mapenzi ya Mungu na kuifikia ile ahadi au ile ndoto au lile lengo tulilolonalo ambalo ni mapenzi ya Mungu, Katika ulimwengu huu vilevile ili tuweze kufikia malengo yetu ya kawaida hatuna budi kuhakikisha kuwa tunavaa moyo huu wa kijasiri, nina mshirika wangu mmoja anaishi maisha duni na yakawaida kabisa lakini ananiambia mchungaji mimi sitaki kuomba kwangu kuomba ni aibu kubwa hivyo napambana katika maisha, yeye anapambana kwa kuzunguka mitaani na kuuza mahindi ya kuchemsha na anapozunguka hazunguki kimya kimya anapiga kelele aiiiiimahindi ya kuchemshaaa kwa hivyo mimi nilimuhurumia lakini sikuwa na namna ya kumsaidia nilimnunuza mahindi matano ya kuchemsha na niliyagawa kwa watu waliokuwa mtaani ili wale nami nilikula moja tu, lakini nilitaka kumtia moyo kwa kununua mahindi yake kwa sababu nilifuarahia ujasiri alio nao, anapata ridhiki yake kwa sababu haoni aibu, ni mwanamke mzuri wa makamo hivi, ni mzuri, uzuri wake na biashara anayoifanya ni kama haviendani hivi, Lakini ndio njia ambayo Mungu amempa kupata ridhiki yake, yako mambo duniani ambayo ili tuweze kutoka katika hayo hatuna budi kuwa na moyo huu na kutokuogopa lolote hata kama ni kuangamia lakini tukiwa na kusudi la kukaa na kutimiza mapenzi ya Mungu, tunahitaji Moyo huu, ni moyo huu ndio unaoweza kutufanya tukasimama sokoni, viwanjani na kumuhubiri Yesu, ni moyo wa aina hii unaoweza kumfanya mtu akakubali kuwa Kondakta wa basi na kupata ridhiki yake, kuhutubia watu na kila jambo, kusoma, kujifunza na kufundisha kote kunahitaji moyo wa ushujaa, bila moyo huo ni vigumu kuyafikia malengo yetu na mapenzi ya Mungu, sasa tunawezaje kujifunza kuwa na moyo wa ushujaa? Hilo sasa linatuleta sasa katika kutafakari kipengele muhimu jinsi ya kuwa na moyo wa ushujaa:-


Jinsi ya kuwa na Moyo wa ushujaa!

Kuwa na moyo wa ushujaa ni swala la kujizoeza, na ndio maana maandiko yanatuamuru tuwe na moyo wa ushujaa,ushujaa hautoki kwa Mungu unatoka mioyoni mwetu pale tunapomuamini na kumtegemea Mungu, hivyo ni lazima kuamua kutoka moyoni ili kukabiliana na kile ambacho tunataka kukabiliana nacho, lakini tunawezaje kujua au kujipima au kujizoeza kuwa na moyo wa ushujaa yafuatayo ni maswala ya msingi sana yanayoweza kutusaidia kuwa na moyo wa ushujaa na kwa ufupi ukiwa na mambo haya na kuyafanyia kazi katika maisha yako utakuwa na moyo wa ushujaa;-


1.       Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kujihurumia -  Moyo wa ushujaa na mafanikio yake hauwezi kuwepo kwa mtu anayejihurumia, wengi tumeweza kuangamiza nafsi zetu kwa sababu ya kujihurumia, tumeshindwa wakati mwingine kufikia ndoto kadhaa kwa sababu tuna tabia ya kujihurumia, mtu anapojiandikisha kuwa askari ni kama mtu anayejiandikisha kuangamiza nafsi yake kwaajili ya nchi yake,kujiandikisha kuwa askari ni kujiandikisha kufa! huwezi kuwa mpiganani mzuri kama unajionea huruma, wala huwezi kuwa mwanafunzi mwema wa Yesu Kristo kama unajihurumia, wala huwezi kutoboa katika maswala kadhaa wa kadhaa ya maisha kama utajihurumia Mathayo 16:24-25 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.” Kwa hiyo kuwa mwanafunzi wa Yesu lazima uwe kama mtu unayepoteza maisha, unayekubali kuangamia, unayekataa nafsi yako kujifurahisha, watu wanaojihurumia hawawezi kamwe kuwa wanafunzi wa Yesu, lakini sio hivyo tu watu wanaojihurumia hawawezi kutoboa katika maisha haya!  Nyakati za torati katika agano la kale wanajeshi wote waliokuwa wameoa hivi karibuni au mtu aliyenunua shamba jipya na kadhalika Mungu aliagiza wasiende vitani, kwa sababu mawazo yao hayatakuwa tayari kuangamia na kuacha mke mpya nyumbani hivyo watu wote waliokuwa na mioyo ya hofu na sababu zinazoweza kuwafanya wasijikane nafsi walipaswa kuchujwa ili wasiende vitani ona Kumbukumbu la Torati 24 :5 “Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.” Au wale waliokuwa na hofu au woga walipaswa kurudi nyumbani Waamuzi 7:3 “Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu ishirini na mbili elfu wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi.” Unaona Mungu hakuhitaji watu wenye hofu au wanaotetemeka wanaoogopa vita wanaojihurumia wenye ndoa mpya hawa walitakiwa kurudi nyumbani, awaye yote ambaye anataka kufanikiwa lazima avae moyo wa ushujaa asijihurumie kamwe apambane kiume awe na moyo wa ushujaa #

 

2.       Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuchoka – ili tufanikiwe katika maisha yetu lazima tuwe na mioyo migumu, hatupaswi kuchoka, Biblia inamtaja punda milia au punda mwitu kama mnyama asiyechoka, aliyeizoelea nyika na ukijaribu kumtafuta utachoka wewe na hutaweza kumkamata au kumgeuza ona Yeremia 2:24 “punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao hawatajichokesha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.” Mtu mwenye moyo wa ushujaa moyo wake hauchoki haukati tamaa, unaendelea mbele hata kutokee vihunzi vya namna gani moyo unaendelea tena na tena katika kuyafikia malengo yake, watu wote mashujaa katika maandiko waliofanikiwa katika Nyanja mbalimbali walikuwa watu wasiochoka, watu wengi ambao wanachoka wanakata tamaa na kuishia njiani, kwa msingi huo hatupaswi kuchoka katika kutia bidii kwenye kila kitu tunachokifanya kwaajili ya utukufu wa Mungu, tusichoke katika kutenda mema na pia tusichoke katiika kumgojea bwana naye atatutokea na kututia nguvu Wagalatia 6:9 “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”. Isaya 40:31 “bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”  Watu wengi wenye mafanikio katika Nyanja mbalimbali ni wale wasiokuwa na moyo wenye kuchoka, maisha ya kwenda mbinguni na maisha ya kumngojea bwana yanawezwa na wale wasiochoka, Lakini vilevile tukitaka mafanikio ya aina mbalimbali basi hatupaswi kuchoka. #

 

3.        Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa kubaki peke yake -   Moja ya mambo ambayo yanaweza kumvunja mtu moyo ni pamoja na kuachwa peke yako, watu wengi sana hukata tamaa wanapobaki wenyewe, mtu mwenye moyo wa ushujaa wakati wote anakuwa tayari kupambana hata anapobaki peke yake, hayuko tayari kwenda kwa mkumbo au kufuata mkumbo, Hesabu 14:6-10 “Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope. Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote”. Yoshua 24:15Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.” Yoshua ni moja ya viongozi walioambiwa na Mungu moja kwa moja wawe na moyo wa ushujaa, wawe hodari na wasiogope, katika maisha yake anadhihirisha kuwa yuko tayari kusimama na jambo lililo jema na katika mapenzi ya Mungu hata kama atabaki yeye mwenyewe na nyumba yake, ukiisha kuyajua mapenzi ya Mungu na kujua lile kusudi lililoko kwako kamwe usikubali kufuata mkumbo katika kufanya ujinga wewe lenga katika kuyafanya mapenzi ya Mungu, hata kama inatokea migomo mashuleni vyuoni na kadhalika, wewe kama unajua kuwa mgomo huo hauna maslahi kwako na kwa Mungu simama mwenyewe ni wewe peke yako unayeweza kumdhihirisha Mungu wa kweli, Mungu sio mwanademokrasia kwamba anaangalia wengi wape yeye ni mwanatheocracia anaangalia wanaosimama upande wake, Nuhu alisimama na Mungu wakati mkumbo wa ulimwengu wa nyakati zake watu waliishi kwa anasa na kutokujali, Lutu aliishi kwa kumtii Mungu wakati watu wa miji ya Sodoma na Gomora  walipokuwa wakiendekeza dhuluma uovu uozo na mapenzi ya jinsia moja, Eliya alisimama mwenyewe wakati Israel walipokuwa wakimtumikia baali na yeye pekee nabii wa Bwana alisimama ona 1Wafalme 18:22-39 “ Ndipo Eliya akawaambia watu, Mimi nimesalia, mimi peke yangu, nabii wa Bwana; lakini manabii wa Baali ni watu mia nne na hamsini. Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie ng'ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini. Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu wakasema, Maneno haya ni mazuri. Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya. Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe. Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika.  Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita, walitabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala aliyeangalia.Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya Bwana iliyovunjika. Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la Bwana na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli. Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni. Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu. Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji. Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu.” Mungu hupendezwa na mtu anayejitambua na kutambua mapenzi ya Mungu, ili uweze kufabnikiwa huna budi kusimama mwenyewe, katika kutimiza kusudi lile ambalo Mungu amekuitia Biblia inasema usiandamane na mkutano kutenda uovu, maana yake usikubali kufuata wingi wa watu hususani kama watu hao wamepotea na kupotoka, kanuni hii inafanya kazi sio katika mazingira ya uovu tu na kumcha Mungu lakini inafanya kazi katika kuyafikia mafanikio ambayo lengo lake Mungu ameweka moyoni mwako kwa kuwa wewe ndiwe unayelitambua kusudi hilo simama mwenyewe, usikubali kufuata mkumbo, hata kama dunia itakuacha peke yako Kutoka 23:2 “Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;

 

4.       Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kupoteza nguvu zake – Kumbuka kuwa tunazungumzia Moyo wa ushujaa na hivyo hapa hatuzungumzii kamwe nguvu za kimwili, shetani anajua kuwa ili aweze kutukwamisha anajua wazi kuwa anapaswa kuujeruhi moyo, moyo wako ukiisha kukubali kujeruhika basi umepoteza nguvu zako, hata kama mtu ana miguvu kiasi gani ushindi wa mtu hatokanani na muonekano wake wa kimwili bali mtazamo wake wa moyoni, yako mambo ambayo ibilisi anaweza kuyatumia kujeruhi mioyo yetu ili tupoteze nguvu zetu watu wenye moyo wa ushujaa hawapaswi kupoteza nguvu zao!huwezi kuwa na nguvu kama utakubali shetani na watu waudhibiti moyo wako, na hisia zake mtu akifanikiwa kuudhibiti moyo wako na hisia zako amekupunguzia nguvu ya moyo wenye ushujaa, unajua ni kwanini maandiko yanatuasa kusamehe au kuwa na subira kwa sababu mtu asiyesamehe anapoteza nguvu unapoteza muda kumfikiri mtu anayekukwaza kuliko kufikiri unachopaswa kukifanya Mathayo 18:21-35 “Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.  Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata, akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho.Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.” Kumbe kutokuachia ni kutokujiachilia, hatupaswi kukaa chini na kuwafikiri wale waliotuumiza kwa vile watachelewesha kusonga kwetu mbele, sisi hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaachilia kutokuachilia kutatufanya tupoteze nguvu, kuachilia ni nguvu kubwa katika maisha yetu.

 

·         Mfano umeumizwa na unakaa chini kusikilizia maumivu yale badala ya kusamehe na kusonga mbele

·         Watu wanakusema vibaya au wanakosoa vikali kile unachokifanya unakaa kusikiliza maneno yao

·         Umedhulumiwa usipoteze muda kutafuta kurudishiwa tafuta njia mpya ya kupata kilichopotea mara dufu zaidi,

·         Mtu anafanya mambo ya kuumiza moyo wako nawe unasikilizia badala ya kupuuza, unabadili mtazamo wako na malengo yako kwa sababu ya maneno ya watu au vitisho, hakikisha unasahau unaachilia na kusonga mbele ukijihakikishia furaha katika maisha yako

·         Unapoteza muda kukaa chini na kulalamikia watu au mazingira kuwa ndio sababu ya kushindwa kwako,

·         Unasikitikia mambo yote uliyoshindwa kuyatimiza katika mipango yako, au unaketi chini kukumbuka mambio ya kushindwa kwako yaliyopita

Mtu wa Mungu unapokaa chini na kuanza kufikiria kile watu wanasema au wanakufanyia hutaweza kutoboa kumbuka kuwa hao wanakupotezea nguvu zako, unachotakiwa kukifanya ni kusonga mbele na kutokupoteza nguvu zako, wakati mwingine huhitaji hata kuwajibu wanaokushambulia Nehemia 4:1-3 “Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.”Wakati wote usikubali kukaa katika mambo ambayo yatakupotezea nguvu hakikisha kuwa unasonga mbele, usikubali kitu au jambo likukalishe chini, unapokuwa unakubali watu au mtu Fulani aushike moyo wako maana yake utahitaji watu wa kukutia moyo, wa kukusiafia ili ujisikie vizuri, utashindwa kukabiliana na wajibu muhimu ulioko mbele yako na mazingira yatakutawala na kukukalisha chini na kukuchelewesha, inuka songe mbele, usipoteze nguvu zako, acha kazi zako zijibu hoja za wapinzani wako!

5.       Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuangalia nyuma – Marrianne Williamsone aliwahi kusema hivi nanukuu  “we do not heal the past by dwelling there, we heal the past by living fully in the present” kwa tafasiri isiyo rasmi ni kama anasema hivi hatuwezi kujiponya na mambo ya nyuma kwa kukaa na kuyakumbuka tunaweza kujiponya na mambo ya nyuma kwa kuishi sasa, kwa lugha nyepesi wakati wote tunapaswa kuyasahau yaliyo nyuma na kuyaangalia yaliyo mbele Wafilipi 3:12-14 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.” Mtu mwenye moyo wa ushujaa wakati wote ataangalia mbele, hatupaswi kuangalia nyuma aidha kulikuwa na mafanikio au tulishindwa, wakati wote tuwaze kufikia malengo makubwa na kuyatimiza kwa ubora zaidi,  wachungaji wengi wakifikisha kanisa lina watu 200 tayari wanadhani wamefikia mahali pa kupumzika, mwanafunzi ana maksi tisini au themanini amepitisha kiwango cha matokeo yaliyowekwa na shule anaridhika, Mwalimu amefaulisha au shule na imashika nafasi Fulani njema mtu anadhani amefika, hatuna budi wakati wote kuhakikisha kuwa haturidhishwi na mafanikio madogo tunayoyapata ilihali tunaweza kwenda zaidi ya vile  kwaajili ya hayo ndugu zangu ni muhimu sana kuhakikisha kuwa tunaangaluia mbele, Mtume Paulo alikuwa ni mtume aliyefanya kazi kubwa kuliko wote, alikuwa muombaji na mwenye uwezo mkubwa sana wa kunena kwa lugha kuliko watu wote, alihubiri injili na kuupindua ulimwengu wa wakati wake. Aliishi maisha matakatifu na kuwa kielelezo, hata cha kuwataka watu wanfuate yeye kama anavyomfuata Kristo, alipewa mafunuo makubwa sana lakini anasema anasahau yaliyo nyuma na anayachuchumilia yaliyo mbele, kila wakati tuhakikishe kuwa tunaongeza viwango na kuachana na mafanikio madogo ya nyuma.

 

6.       Mwenye moyo wa uhujaa hapaswi kuwaogopa wanadamu inasemekana kuwa mwanadamu ndiye mnyama anayetisha zaidi kuliko wanyama wote, ili uwe na moyo wa ushujaa ni lazima ujifunze kutokuwaogopa wanadamu, wao ndio viumbe tunaoshindana nao katika mambo yote ndio wanaoweza kutumiwa na Mungu kwa mafanikio yako lakini vilevile ndio wanaoweza kutumiwa na ibilisi wakasimama kama vikwazo ili uweze kutoboa katika maisha yako usiwaogope wanadamu Kumbukumbu la torati 3:21-22 “Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda Bwana, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda Bwana kila ufalme huko uvukiako. Msiwache, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye awapiganiaye.” Ili uwe shujaa Mungu anataka kuona ukimuogopa yeye tu peke yake wale tunaoshindana nao ni wanadamu tu kama sisi, kwa msingi huo hatupaswi kwa namna yoyote kuwaogopa kwa kuwa wewe unapiganiwa na Mungu wako, Mungu akiisha kusema nawe na akiisha kukupa wazo la kufanya katika Nyanja yoyote lifanye maana Mungu yuko pamoja nawe na amekupa watu kwa msingi huo usiwaogope watu Yoshua 8:1 “Kisha Bwana akamwambia Yoshua, Usiche, wala usifadhaike; wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake;” kwa kawaida Mungu anakupa ushindi wa vita hata kabla hujaingia katika vita vyenyewe, na kwa sababu hiyo haitakuwa vema kabisa kuogopa, unapoogopa watu  na kufadhaika unaondoa uwepo wa Mungu maana yake unashindwa kumfanya Mungu atende kazi na wewe na kwa sababu hiyo utaleta kushindwa,  Zaburi 56:11 “Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?” Mwandishi wa zaburi hii ana ushahidi wa kushangaza yeye nguvu zake ziko katika kumtegemea Mungu kiasi ambacho  anajua kabisa kuwa akama ukiweka tumaini lako kwa Mungu ni dhahiri hofu taondoaka na hautaogopa chochote, kujifanya tu uko vizuri huku humtegemei Mungu ni kiburi,  Lakini kuweka tumaini kwa Mungu kunakupa ujasiri sio kusema tu humuogopi mwanadamu lakini hata majeshi yakijipanga kwa mtu anayemtegemea Mungu bado hawezi kuogopa ona Zaburi 27:1-3 “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.Kama utajifunza kutokuwaogopa wanadamu na kuangalia imani yako na kuweka tegemeo lako na tumaini lako kwa Mungu lazima ukumbuke kuwa ni Mungu ndiye atakayekupigania na kukusaidia na kukushuindia hivyo hupoaswi kuoopa changamoto ya aina yoyote ile na hupaswi kuwa na moyo wa unyonge, wewe utamwangalia Mungu tu.

 

7.       Mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa mabadiliko -  Tunaishi katika ulimwengu ambao mambo yanabadilika kwa haraka sana kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknoliojia, lakini moja ya maswala ambayo yanawatishia watu ni pamoja na mabadiliko watu wengi wanaogopa mabadiliko, kwa sababu hiyo wanapingana nayo, kwa mfano moja ya jambo ambalo watu wengi wanaliogopa katika taifa letu ni pamoja na mabadiliko ya katiba, watu wanaogopa sana lakini mabadiliko ya katiba hayaogopeshi kama yalivyo mabadiliko ya viongozi, kama tunaweza kubadili viongozi wetu kwa amani basi vilevile tunaweza kuibadilisha katiba yetu kwa amani, jambo la msingi tu ni kwa wale wanaoona hitaji la katiba mpya watoe Elimu ya kutosha kuinyesha kwanini sasa tunahitaji mabadiliko ya katiba, ili waoogopa wajue kwanini tunahitaji katiba mpya, dhambi ni kushinikiza tu kuwa ni lazima tuwe na katiba mpya huku hata wapiga kura wakiwa hawajui kwanini tuwe na kaiba mpya, tukiipata itatunufaisha nini ina manufaa gani, hakuna sababu ya kuogopa, kwa msingi huohuo watu wanaoweza kuleta mabadiliko na kutoboa ni wale ambao kwa namna Fulani hawaogopi kubadilika kwa mambo, ukiogopa mabadiliko utapoteza nafasi nyingi za muhimu ambazo zingekujilia kuliko kuogopa Zaburi 46:1-3 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”  Unaona mwandishi wa zaburi hii aonyesha kuwa haogopi mabadiliko, lazima akili ya mtu shujaa ijiandae kwa mabadiliko, na kukubaliana nayo, kama tumemtegemea Mungu tujue tu katika maisha yetu pia kwamba kuna kupanda na kushuka, kuna wakati kwa kila jambo, kuna kudhiliwa, kuna wakati wa magumu na kwa vyovyote vile hali yoyote ya mabadiliko haipaswi kuwa sababu ya kuondoa ujasiri katika maisha yetu Warumi 8:35-39 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”Mwandishi anaonyesha kuwa hakuna kitu maana yake hakuna aina ya mabadiliko ya maisha itakayomtenganisha na Yesu Kristo, iwe dhiki, au shida, au njaa, au uchi au hatari au upanga hata kama tunauawa iwe jua iwe mvua atabaki katika imani bila kujali hali ikoje? Wako watu wengine haki yao ya wokovu inategemeana na hali ya hewa, hali yao ya kumuamini Mungu, inategemeana na hali ya hewa na mazingira kukiwa na shida anamuacha Yesu, hawa ni watu wanaoogopa mabadiliko, unasikia watu wanasema wokovu wa siku hizi, kumbe kuna wokovu wa zamani, wa siku hizi je wa siku zijazo utakuwaje maandiko yanatuambia kuwa Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele, Neno la Mungu linatuonyesha kuwa watru wenye moyo wa ushujaa wanaendelea kubaki vilevile bila kujali kuwa mazingira yakoje hawaogopeshwi na mabadiliko, wakati wote huyatumia mabadiliko kama wimbi la kuelekea katika Nyanja nyingine, nimeona kuna wanafunzi wanaogopa mabadiliko, Mwalimu fulani hayuko sijui itakuwaje, fomart ya mitihani imebadilika sijui itakuwaje, syllabus imebadilika sijui itakuwaje, bei ya hiki na kile imepanda sijui itakuwaje kwani ilipokuwa nafuu ulifanya nini? Ndugu zangu mwenye moyo wa ujasiri haogopi mabadiliko!.

 

8.       Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa Kushindwa! – Kushindwa ni sehemu ya maisha tunajifunza mengi mazuri kwa watu waluioshindwa kuliko hata washindi, Biblia imejaa mifano ya watu wengi wanaoitwa mashujaa wa imani ambao maisha yao yamejaa ushindi kwa msaada wa Mungu hata hivyo Roho Mtakatifu hajaacha kuonyesha kushindwa kwa watu hao, tunawaonaga wachezaji wakikatwa mtama na kutibiwa na hatuimaye kuinuka tena na kuendelea na kucheza hawakati tamaa kwa sababu wameshindwa, shule za Private zamani zilikuwa ni shule za watu walioshindwa ndio wanachukuliwa na kuandaliwa na kufanywa washindi tena!, kushindwa ni moja ya changamoto kubwa sana katika maisha ya wanadamu na inaogopewa na watu wengi sana wengine hawataki hata kujaribu kwa sababu wanafikiri watashindwa! Kama ingekuwa unaweza kuchagua aina za washirika wa kuchunga kama mchungaji mimi ningetamani sana kuchunga watu walioshindikana, walioanguka, wenye madeni, wanyonge hao ndio ningetamani wanijie alafu nionyeshe uwezo wangu wa kichungaji na niwawezeshe wao kuonyesha uwezo wao na uzoefu wao wa kushindwa ulivyo wa muhimu sana na unavyoweza kuwaletea ushindi dhidi ya wale wanaofikiri wanaweza!  1Wakoritho 1:26-31 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.” Mungu huwa haogopi kushindwa kwa hiyo ana chagua vitu au watu dhaifu kisha anawatumia kwa utukufu wake, kushindwa kwetu katika maeneo mbalimbali hakukufanyi wewe uwe dhaifu bali kunakufanya wewe ujue ni changamoto gani unaweza kuziepuka na ukaleta ushindi, kwa hiyo lazima tujaribu tena na tena, Daudi jeshi lake lilikuwa na watu hodari sana lakini wengi waliomwendea na kujiunga naye walikuwa watu duni ona  1Samuel 22:1-2 “Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne.” Inashangaza sana kuona kwamba Daudi alikuwa jemedari yaani ni mkuu wa majeshi lakini tunaambiwa jeshi lake liliundwa na watu duni, watu waliokuwa na dhiki, waliokuwa na madeni tena wameshindwa kuyalipa huko watu waliojaribu maisha wakashindwa hao ndio wanaunda jeshi la Daudi unaweza kuona, lakini katika namna ya kushangaza sana hawa ndio waliotumiwa na Mungu na kuleta ushindi mkubwa, hawaogopi kushindwa kwa sababu inaonekana walishashindwa mara nyingi, Waamuzi 11:1-3 “Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha.Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine. Ndipo Yeftha akawakimbia hao nduguze, akakaa katika nchi ya Tobu; na watu mabaradhuli walikwenda na kutangamana na Yeftha, wakatoka kwenda pamoja naye.” Ni katika hali kama hiyo Yeftha pia tunaelezwa kuwa alikuwa mtu shujaa yaani jemadari na jeshi lake liliundwa na watu mabaradhuli, hii ni jamii ya watu walioshindwa maisha lakini baadaye walileta ushindi mkubwa, mtu anayeogopa kushindwa hawezi hajta kujaribu, tunaweza kukwepa mambo kadhaa wa kadhaa na hatimaye tukakosa mambo ya msingi na ya muhimu kwa sababu tu tunaogopa kujaribu kwa sababu ya kuogopa kushindwa! Kumbe kushindwa kunaweza kutupa uzoefu utakaotuletea ushindi wa kweli, tunajifunza vitu vingi kwa namna ya kushindwa, watoto kusimamam na kutembea na kujua mambo mengi kwa kujaribu na kushindwa, baiskeli kwa namna ya kuanguka na kuumia, lugha kwa namna ya kuanguka na kuumia, na hali ya kiroho wakati mwingine kwa kuanguka na kuinuka tena hatimeye kusimama

 

9.       Mtu mwenye moyo wa ushujaa haogopi kukataliwa -  watu wengi sana wanajiepusha na mambo Fulani kwa sababu wanaogopa kukataliwa, mtu anaweza kuona binti mzuri na akampenda lakini akashindwa kusema chochote kwa sababu anaogopa kukataliwa, hata wanandoa mtu anaweza kuogopa kuomba jambo Fulani kwa mwenzi wake kwa kudhani kuwa atakataliwa, kwa sababu ya kuogopa kukataliwa wakati mwingine katika maisha yetu tunabakia palepale na hatusiongi mbele Biblia imejaa ushahidi wa watu wengi ambao walikuja kufanya vizuri katika nafasi zao lakini mwanzoni walikataliwa Mwanzo 37:18-20 “Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.” Yusufu alikuwa na ndoto ambayo ingekuja kuwafaa ndugu zake lakini alipowasimulia hawakufurahi, walikusudia kumuangamiza ili waone ndoto zake zitakuwaje mkono wa mungu ulikuwa pamoja naye na akatoboa Matendo 7:9-10 “Wale wazee wetu wakimwonea wivu Yusufu, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja naye, akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.” Unapokataliwa huo sio mwisho wa maisha Oprah Winfrey alikuwa ni mtangazaji wa taarifa za habari jioni katika televisheni Fulani na alifukuzwa kazi kwa sababu hakuweza kuzuia hisia zake wakati akitoa habari, kwa hiyo alitimuliwa kama mtanzagaji asiyefaa, alianzisha kipindi chake kiitwacho Oprah Winfrey show na kuwa mtu maarufu sana na baadaye kuwa tajiri mkubwa na mtu mwenye kibali ambaye unaweza kusimama naye wakati wa kampeni za kisiasa, sasa ni moja ya watu wenye ushawishi mkubwa nchini Marekani, Msanii Harmonize ambaye alitokea WCB au wasafi hapa Tanzania unapomuona anaonekana kama kituko flani hivi na ndio hali halisi, lakini wakati anaanza sanaa alikataliwa na watu wanaohusika na kuinua vipaji katika mashindano maarufu yajulikanayo kama Bongo Star search, kwamba hafai na ajaribi fani nyingine, leo hii Harmonize ni moto wa kuotea mbali, hakujali kukataliwa, hakukata tamaa, alipambana kupigania ndoto zake kwa nguvu zake zote leo hii Harmonize ni next level  kwa hiyo neno la Mungu, kwa msingi huo mtu kukuambia haufai au kukukataa haimaniishi kuwa huwezi kuachieve au kufikia kile unachotaka kukifikia, hakikisha wakati wote unapambana kuifikia ndoto yako Yefta alikataliwa na ndugu zake lakini walipoozidiwa walienda kumuomba yeye awe mwamuzi juu yao Waamuzi 11:1-2Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha. Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.” Unaona hapa Yefta anakataliwa laiki mtu huyu alikuwa ni shujaa mno na baadaye wale walimkataa yalipowakuta walienda kumuomba aje awasaidie na akakubali kurudi na kuwasaidia watu wake ona Waamuzi 11:4-11 “Ikawa baadaye, wana wa Amoni wakapigana na Israeli. Ikatukia, hapo wana wa Amoni walipopigana na Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu; wakamwambia Yeftha, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa Amoni. Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu?  Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Kwa ajili ya hayo sasa tumegeuka kukuelekea wewe tena, ili uende pamoja nasi na kupigana na wana wa Amoni, nawe utakuwa kichwa chetu juu ya wenyeji wote wa Gileadi. Basi Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi Kwamba mwanirejeza kwetu tena ili kupigana na wana wa Amoni, naye Bwana akiwatoa mbele yangu, je! Mimi nitakuwa kichwa chenu? Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Yeye Bwana atakuwa shahidi kati yetu; hakika yetu tutafanya sawasawa na neno lako. Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya Bwana huko Mispa.”

 

10.    Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuwa na mashaka – ni ukweli ulio wazi kuwa watu wengi huogopa kujaribu mambo kwa sababu wanaona shaka, watu wana mashaka ya kujaribu kitu kingine, wanaogopa kuwa labda kujaribu kitu kingine kunaweza kusiwaletee maisha mazuri, lakini kukaa tu bila kujaribu kwa sababu ya mashaka kutakufanya udumae na Yesu aliwakemea wanafunzi wake mara kadhaa kutikana na kuwa na mashaka Mathayo 14:25-31 “Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.  Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? ” Yesu anatuonyesha wazi kuwa hakuna lisuilowezekana kwa mtu anayeondoa shaka ukiweka mashaka utashindwa lakini ukiondoa shaka utashinda angalia Marko 11:23-24 “Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Mashaka yatakuondoa kwenye malengo, mashaka yatakuondoa kwenye imani, amshaka yatakutupa nje ya mpango wa Mungu, mashaka yatakufungia mafanikio yako Yakobo 1:5-7 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.”

 

11.   Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa kukosolewa “Critics” -  kwa kawaida kukosolewa na au kuhukumiwa na wanadamu katika mambo tunayoyafanya, kukosolewa au kuhukumiwa na wanadamu katima maswala tuyafanyayo ni jambo la Muhimu sana, nani kawaiada  hivyo hatupaswi kuogopa kukosolewa wala kuhukumiwa wala, ukweli ni kuwa watu watakuhukumu na wakati mwingine kwa maneno makali, lakini ukiwa na moyo wa ushujaa utaishi sawa na thamani ya vile ulivyo, na hiyio ndio njia ya mafanikio ya kufanikiwa kwako, unaposoama sana ni rahisi wenzako kukuambia umetumwa na kijiji, unapojituma sana ni rahisi kuambiwa na wenzako unajipendekeza, Yesu alikosolewa katika kila anachokifanya na hata alipotoa Pepo walisema anatumia nguvu za giza za mkuu wa pepo Belizebul Mathayo 12: 22-24 “Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.” Paulo mtume alihakikisha kuwa wakati wote anakubali kila aina ya udhaifu, dharau, taabu udhalimu na mateso kwaajili ya Kristo Yeye alikuwa mtu mkubwa sana katia ulimwengu war oho alipata mafunuo makubwa sana kuliko mtu awaye yote lakini hakuwahi kujisifu, na alikubali kukosolewa wala hakukumtisha kwa sababu alimuweka Kristo mbele 2Wakoritho 12:1-10 “Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene. Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu. Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu. Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” Lengo lake yeye ilikuwa Yesu atukuzwe katika mazingira yote, kwa msingio huo basi hatuna budi kuhakikisha kuwa tunakabiliana na kutikuogopa aina yoyote ya kukosolewa tukijua ya kuwa kuna lengo tunakusudia kulifikia     .

12.   Watu wenye moyo wa ushujaa hawaogopi kupoteza maslahi yao – Kupoteza maslahi ni moja ya hofu inayowakumba watu wengi sana, kwa mfano kutokana na kujiunga na chama Fulani cha kisiasa na kupoinzana na kingine unaweza kujikuta unapoteza maslahi, kumfuata Yesu na kuacha dini nyingine inaweza kukufanya upoteze maslahi, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipoteza nafasi ya kuwa Mwalimu wakati wa ukoloni alipoanzisha TANU ili kuwaunganisha watanganyika wapiganie uhuru, kwa hiyo ni wazi kuwa wakati mwingine ili uelekee katika manufaa Fulani huna budi kukubali kupoteza maslahi yako, Wafilipi 3:7-11 “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;  ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.” Watu wanaowekeza katika biashara, na maswala mengine mara nyingi ni risk takers wako tayari kujilipua, lakini wakati mwingine tunaweza kuchukua hasara kwaajili ya kuwatetea wengine.

Hili ndilo jambo la msingi zaidi ambalo mwanadamu anaweza kulifanya ili Mungu awe pamoja na kumfanikisha katika kila jambo ni kuwa na moyo wa ushujaa, bila moyo wa haina hii huwezi kuitomboa katika Nyanja ya aina yoyote ile

 

Ujumbe: Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima