Alhamisi, 17 Mei 2018

Pembe ya Wokovu wangu!



Mstari wa Msingi: Zaburi 18:2-8Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na PEMBE YA WOKOVU wangu, na ngome yangu. Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu. Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.  Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala, Makaa yakawashwa nao.”


Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-

1.       Maana ya neno Pembe
2.       Maana ya pembe ya wokovu


Maana ya  neno Pembe. 

Neno Pembe ya wokovu limetajwa mara nytingi sana katika sehemu mbalimbali za Maandiko Matakatifu yaani Biblia, Lakini itakuwa muhimu zaidi kama tutafahamu kwa pamoja kwa kina na mapana na marefu maana ya Pembe ya wokovu, neno Pembe na uhusiano wake katika wokovu.

Neno Pembe katika Biblia waebrania wanaiita “SHOFAR” imetumika katika maandiko kuelezea mambo mengi sana, katika namna nyepesi wote tunafahamu kuwa Pepmbe ni aina mfupa mgumu unaojitokeza na kukua katika kichwa cha mnyama, Mwanzo 22:13, Pembe ya mnyama hususani kondoo mume inatumika kama silaha ya Kushambulia, Kulinda, kuonyesha mamlaka na utawala na kuleta Hofu, ni ishara ya nguvu, uweza na ushindi, kwa Msingi huo maandiko yanapotaja Pembe mara nyingi hutumika kuelezea uweza na nguvu.

Kwa lugha nyingine ya kinabii neno Pembe pia linatumika kuelezea kuhusu Serikali, au ufalme au nguvu ya dola yaani nguvu za ufalme huo unaweza kuona katika  Daniel 7:7, 24Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.; 24  Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Unaweza kuona hivyo Pembe huzungumzia NGUVU au uweza wa KIJESHI Dolla, kwa msingi huo taifa au kabila fulani linapoondolewa ngvu zake lugha ya kibiblia maana yake pembe zake zimekatiliwa mbali Yeremia 48:25Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema Bwana. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya Bwana                                            

Pembe pia hutumika kuelegea nguvu ya Upako yaani uwezo wa Roho Mtakatifu,Pembe katika agano la kale zilitumika pia kuweka mafuta maalumu ya upako ambao wangepakwa watu kama makuhani, manabii na wafalme kwa kusudi la kutimiza mapenzi ya Mungu mfano 1. Samuel 16:1-3 “Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako, 13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.” Aidha Pembe zilitumika kama tarumbeta za kumsifu Mungu na zilipopulizwa pembe kwaajili ya utukufu wa Mungu ngome za adui zilianguka na kusambatratika kabisa Yoshua 6:1-5Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili.


Tafasiri nyingine ya kibiblia ilihusu pembe za madhabau  kwa maana ya kuwa kila kona ya madhabau kulikuwa na pembe nne, pembe hizi zilivyunyiziwa damu wakati wa kutoa dhabihu ili kwamba watu waweze kufanyiwa upatanisho kwa mungu na kupata rehema, sehemu hii ya pembe pia ilitumika kwa ibada ya upatanisho kati ya Mungu na wanadamu Walawi 8:15Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.”  Eneo hili la pembe za madhabahu lilitumika pia kumaanisha MAKIMBILIO au kujisalimisha endapo mtu angekuwa na tatizo linalohitaji kujihami, au kujitakia rehema hususani alipataka kuuawa 1Wafalme 1:50Adonia naye akaogopa mbele ya Sulemani; akaondoka, akaenda, akazishika pembe za madhabahu.” Kwa hivyo kimsingi hizo ndizo maana ya Pembe kibiblia.

Maana ya Pembe ya wokovu!

Kama tulivyoweza kuona kwa uapana na kina na urefu kuhusu maana ya neno Pembe sasa ni muhimu kwetu tukarejea katika andiko letu la Msingi Zaburi 18: 2 “Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na PEMBE YA WOKOVU WANGU, na ngome yangu.” Hapo sasa utaweza kumuelewa vema mwandishi wa zaburi anapozungumzia kuhusu Pembe ya wokovu wake, kwamba ana maanisha nini, Pembe kwa msingi huo ilitumika kuelezea WOKOVU neno wokovu katika kiyunani ni SOTERIA  ambalo maana yake ni Nguvu ya kuweka Huru, Nguvu ya kukuondoa Hatarini, Nguvu ya kukulinda na Hatari, Nguvu ya ukombozi, Nguvu ya kuharibu mipango ya adui, Nguvu ya kusambaratisha nguvu za adui yako Zaburi 75:10 “Pembe zote za wasio haki nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka” Kazi hii ya ukombozi Israel walikuwa na ufahamu na Roho Mtakatifu aliwafunulia wazi kuwa Dola hii au nguvu au serikali hii inayoweza kuleta ukombozi, inayoweza kuvunja vunja nguvu za adui zako, inayoweza kuharibu kila aina ya nguvu za upinzani, inayoweza kukulinda, inayoweza kukuokoa, inayoweza kukupa rehema na neema, inayoweza kukutetea dhidi ya adui zako dhidi ya waliokudhulumu, dhidi ya waonevu, dhidi ya magonjwa, dhidi ya masononeko, dhidi ya ufisadi, dhidi ya fitina, faraka , masengenyo mateto kunenwa vibaya, kusingiziwa, kuvunja nuksi mikosi na balaa, kukuweka huru nguvu hii inaitwa PEMBE YA WOKOVU LUKA 1:67-75 “. Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema,  Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.  Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;  Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu; Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu, Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,  Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote.”(my god mya god ribasakarabashanda! Rebosokoroboshi ribabababaskataritoli yenderebekisha sanda) Zekaria akajazwa Roho Mtakatifu kwa msingi huo maneno hayo ni ya Roho Mtakatifu, Na hapo yanamtaja “YESU KRISTO” ndni yake kuna ukombozi, ndani yake kuna kuokolewa na adui zetu ndani yake kuna kutolewa mikononi mwa wanaotuchukia Mungu wangu, kumbe kwaajili ya amani yetu na ulinzi wetu hatuhitaji pembe za waganga wa kienyeji, kwa sababu tunayo pembe tumesimamishiwa Pembe ya wokovu, Jina Yesu maana yake ni wokovu, Yesu ni mwenye nguvum kama zilivyo nguvu za Pembe za wanyama wakali, wenye nguvu Yuko mwenye nguvu kuliko vyote yeye ni pembe ya wokovu wangu, yeye ndio kimbilio letu yeye ndio mahali sahihi pa kujisalimisha mmmmmhmmmm my God najisikia kuhubiri hapa kuna mtu nasema naye hapa viti haviwezi kukalila maana nimempata Yesu, nimepata nguvu nina upako nina ulinzi wa ajabu sio kitu kingine ni Yesu mwana wa Mungu aliye hai pambe ya wokovu wangu! 

Mungu akubariki tafadhali si mbaya ukinijuza jinsi ulivyobarikiwa na somo hili  sms or whatsapp 0718990796

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumanne, 1 Mei 2018

Neno la Mungu na utawala wa Kidemokrasia!



Ni muhimu kufahamu kuwa nyakati hizi tulizonazo ni nyakati za mwisho, Yeye ajaye anakuja wala hatakawia. Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.Katika nyakati hizi ambazo maandiko yanaziita za hatari; ni muhimu kuwa na ufahamu wa rohoni na kuwa na macho ya rohoni ili kwamba tuweze kujua majira na nyakati na kujiandaa vema na kurudi kwa Bwana Yesu, na ili kwamba pia tusiwe miongoni mwa hao wanaopotea.


Katika nyakati za kizazi cha leo tumekuwa tukisikia sana neno “Demokrasia” au utawala wa kidemokrasia na tumeona jinsi ambavyo kupitia utawala huu wa kidemokrasia kumekuwepo na mwamko mkubwa sana wa watu kutaka kuwa na uhuru, uhuru wa kuzungumza, uhuru wa kutoa au kupokea habari, uhuru wa kuchagua lolote mtu atakalo, uhuru wa kuamua, kumuoa au kuolewa na yeyote umtakaye uhuru wa kuabudu,Usawa wa kijinsia, vurugu na ugaidi pamoja na Haki za watoto, Hakiza Binadamu na aina nyingine za usawa na maswala yanayofanana na hayo, Yote yakiwa yamekuja na kifurushi hiki kiitwacho demokrasia kwa nini neno demokrasia linapata nguvu sana katika nyakati zetu, na linaonekana kuwa na washabiki wengi sana duniani? Leo tutachukua Muda kulitafakari neno hilo chini ya somo hili Muhimu Neno la Mungu na utawala wa kidemokrasia, na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele muhimu vifuatavyo:-

·         Maana ya neno Demokrasia
·         Mifumo ya utawala wa dunia na serikali za wanadamu duniani
·         Neno la Mungu na utawala wa kidemokrasia
·         Hatari ya uhuru uliokithiri chini ya mfumo wa Kidemokrasia

Maana ya neno Demokrasia.

Neno Demokrasi limetokana na neno la kiyunani “DemosKratein” ambalo ni muunganiko wa maneno mawili ya kiyunani Demos – ambalo maana yake ni watu na Kratein- ambalo maana yake kutawala au utawala, Kwa msingi huo neno Demokrasia maana yke ni Utawala unaotokana na nguvu ya watu au nguvu ya umma, Demokrasia ni mfumo wa siasa za dunia ambao unatoa mamlaka makubwa kwa watu kuamua, nani awaongoze, waongozwe vipi, wawajibike vipi, na kadhalika, Katika tawala za kidemokrasia viongozi nyeti kabisa huchaguliwa na watu, hivyo watu ndio wenye nguvu kuu ya maamuzi katika mifumo ya tawala za kidemokrasia, sio hivyo tu watu ndio wenye maamuzi ya kumkataa kiongozi na hata kumuwajibisha,  Mfumo huu wa utawala umepata nguvu kubwa sana katika nyakati hizi za mwisho wa dunia kuliko nyakati za tawala nyingine za kihistoria ambazo zimewahi kuitawala dunia, Katika maswala ya kiimani mfumo huu ni hatari zaidi kwa maisha ya kiroho na kanisa kuliko tunavyofikiri ingawa unaonekana kuwa unakubalika zaidi katika maisha ya wanadamu na unaungwa mkono zaidi duniani, na wakati mwingine tunaweza kusema kuwa una nguvu na umeangusha aina nyingine za tawala kwa vile zinaonekana kuwa za kizamani. Kabla hatujaona kwa undani hatari zake ni vema tukaangalia namna maandiko yalivyoweka wazi aina za tawala za serikali za wanadamu zilizotawala Dunia, kabla haujaa utawala wa Ufalme wa Mungu.


Mifumo ya utawala wa dunia na serikali za wanadamu duniani
 
Ni muhimu kufahamu kuwa mfumo wa utawala wa kidemokrasia na tawala nyingine duniani, sio kitu kigeni kwa wataalamu wa maandiko, Mungu ndiye ayatetawala Daniel 4:17 “Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.” Kwa kuwa Mungu ndiye anayetawala ulimwengu na ndiye anayeruhusu nani atawale na aina za utawala, Mungu anajua yote na hivyo aliwafunulia watumishi wake Tangu nyakati za Nebukadneza na Daniel ili kutujulisha majira na nyakati tangu wakati huo hata ufalme wa Mungu utakapotawala duniani, Unabii kuhusu mifumo ya serikali za dunia uko katika maono na ndoto aliyoota Nebukadreza na ikatafasiriwa na nabii Daniel kwa ajili ya vizazi vyote ili tuweze kuwa na akili ya kile kinachoendelea katika nyakati zetu, Unabii huu ulionyeshwa kwa njia ya Sanamu ya ajabu ambayo tutaiangalia na kupata uchanganuzi wake kama ifuatavyo:-



Daniel 2:1- 49. “Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake. Ndipo hao Wakaldayo wakamwambia mfalme, kwa lugha ya Kiaramu, Ee Mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu, akawaambia Wakaldayo, Neno lenyewe limeniondoka; msiponijulisha ile ndoto na tafsiri yake, mtakatwa vipande vipande, na nyumba zenu zitafanywa jaa. Bali kama mkinionyesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionyesheni ile ndoto na tafsiri yake. Wakajibu mara ya pili, wakasema, Mfalme na atuambie sisi watumishi wake ile ndoto, nasi tutamwonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu, akasema, Najua hakika ya kuwa mnataka kupata nafasi, kwa sababu mmeona ya kuwa lile neno lenyewe limeniondoka. Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake. Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kama hili kwa mganga, wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo. Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme, wala hapana mwingine awezaye kumwonyesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili. Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli. Basi ile amri ikatangazwa, na hao wenye hekima walikuwa karibu na kuuawa; watu wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauawe. Ndipo Danieli kwa busara na hadhari akamjibu Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, aliyekuwa ametoka ili kuwaua wenye hekima wa Babeli; alijibu, akamwambia Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, Mbona amri hii ya mfalme ina ukali namna hii? Ndipo Arioko akamwarifu Danieli habari ile. Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake;  ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni. Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake. Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme. Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi, Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonyesha mfalme ile tafsiri. Ndipo Arioko akamwingiza Danieli mbele ya mfalme kwa haraka, akamwambia hivi, Nimemwona mtu wa hao wana wa Yuda waliohamishwa, atakayemjulisha mfalme ile tafsiri. Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake. Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu; lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi; Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa. Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako. Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.  Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote. Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu; na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.  Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope. Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika. Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo. Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti. Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba. Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii. Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli. Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akiketi katika lango la mfalme.”

Ukiangalia kwa undani kuhusu tafasiri ya Daniel kutokana na ndoto aliyoiiota Nebukadreza ambayo ilikuwa ikionyesha dalili za kuja kwa ufalme wa Mungu tangu wakati wa utawala wa nebukadreza unabii huu unatuonyesha mifumo ya serikali za dunia kabla haijaja ile serikali ua utawala wa Masihi, Mungu ametaka kutujua sisi kuhusu wakati ujao, kwa kuchambua sasa tawala hizi ndoto hii ilikuwa na ujumbe ufuatao



1.       Kichwa cha Dhahabu – kiliwakilisha utawala wa Babeli uliokuwa chini ya Nebukadneza
Nebuchadnezzar alitawala kati ya mwaka wa 605-562 hivi kabla ya Kristo alikuwa ni mtawala mkubwa sana wa ufalme katika ufalme wa kabila za Wakaldayo, aliyeshinda falme kuu za Asia na asia ya kusini mashariki na utawala wa Dunia ya wakati huo, alijulikana kwa uhodari mkubwa wa ujenzi kwani alijenga miji mikubwa sana ukiwemo mji wa Babeli ambao ulikuwa wa kifahari sana, alikuwa ni mtawala mwenye nguvu aliyeruhusiwa na Mungu kuharibu Yerusalem na kuchukua mateka Wayahudi na hata kuwapeleka utumwani na kuwafanya watumwa wake, Utawala wake ulikuwa unawakilisha mfumo wa kidikteta kuitawala dunia ya wakati huo, Yaani wafalme au mfalme alikuwa na nguvu kuliko kitu chochote, mtu yoyote na sheria yoyote alichokiamuru yeye ndio kilikuwa jambo la mwisho na hakuna wa kumpinga Dunia ya wakati wake iliongozwa na Mfumo wa utawala wa Kidikteta

Utawala wa kidikteta ni mfumo wa utawala ambao mtawala anatumia nguvu ya dola kutawala, mamlaka nguvu na utawala anakuwa navyo yeye na huwezi kumpinga, Mtawala anajifikiri kuwa ana mamlaka yote juu ya kila kitu hata maisha ya watu, kumpinga kwako kungeweza kuhatarisha maisha, watu walipaswa kumuogopa na kumtii mtawala katika mazingira yoyote yale, utawala huu uliwakilisha aina za serikali za zamani za kifalme na watemi, utawala wakeulidumu kwa miaka kama 70 hivi na baadaye mifumo ya serikali za aina hii ilikuwepo duniani na kuondoka kidogokidogo.

2.       Kifua cha Fedha –  kiliwakilisha utawala wa uamedi na uajemi utawala wa sheria

Baada ya anguko la utawala wa kidikteta uliowakilisha na Nebukadneza mfumo wa utawala na serikali uliofuata uliigawanya babeli vipande viwili na kukaweko utawala wa waamedi na waajemi ambazo ni sawa na Iran na Iraq ya leo, utawala huu ulidumu kwa miaka 206 (536KK-330 KK) Utawala huu unawakilisha na madini ya Fedha maana yake hakukuwa bora sana ukilinganishwa na Madini ya dhahabu, utawala huu ulikuwa wa kisheria na hakuna aliyekuwa juu ya sheria utawala huu, Sheria iliheshimika zaidi na hata wafalme walitakiwa kuzitii, sheria iliheshimika sana ikiwekwa imewekwa na kila mtu alipaswa kuitii ni mara chache sana mfalme aliweza kutangua lakini hata hivyo wakati huu Hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria, hii inawakilisha mfumo wa serikali zilizofuata duniani baada ya ule wa kidikteta.

3.       Tumbo la Shaba – linawakilisha utawala ugiriki au uyunani chini ya Aleksandria

Utawala wa kiyunani au kigiriki unawakilishwa na madini ya shaba na ni sehemu ya tumbo, ulikuwa ni utawala wa kijeshi chini ya mfalme Alexander mkuu, utawala hu wa kiyunani ulidumu kwa miaka 300 (330KK-30KK), kinabii tawala za kijeshi zilifanana kiasi na tawala za kidikteta, shaba inafanana na dhahabu kwa kiwango fulani lakini si bora wala ya thamani kama Dhahabu na fredha huu ni mfumo wa nyakati za serikali za kijeshi zilizotawala sehemu mbalimbali duniani, Nguvu yako yamkijeshi ndiyo ingekuwezesha kuitawala Dunia.

4.       Miguu ya Chuma –Inawakilisha utawala wa warumi chini ya mataifa ya ulaya. Utawala wa kikoloni.

Aina hii ya utawala ilianzia huko ulaya ambapo wao hawakuwa wanachukua watu na kuwapeleka utumwani lakini badala yake waliwatawala watu hukohuko katika inchi zao. Kulikuwa na mabadiliko mengi sana nyakati za utawala huu, Utawala wa kikoloni ni utawala ambapo taifa kubwa na lenye nguvu Super power Nations, linaondoka na kwenda kuwatawala wengine kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kitamaduni. 

Utawala wa chuma unawakilisha utawala wa Kirumi ambao ulikuwa na unaowakilishwa na miguu ya chuma katika sanamu kabla haujagawanyika miguu miwili inawakilisha kugawanyika katika maeneo makuu mawili, mguu mmoja unawakilisha ubepari Magharibi chini ya ushawishi wa papa na kanisa lake  na mguu mwingine unawakilisha Ujamaa mashariki, chini ya utawala au ushawishi wa kiyunani  Kanisa la Othodox, Ukoloni ilikuwa ni sehemu ya utawala wa mataifa yote yanayowakilishwa na mguu wa kulia na wa kushoto, yaani magharibi na mashariki mpaka wakati wa mataifa yote kuwa huru na kujitegemea,

Kuchanua kwa mtini na miti mingine kunawakilishwa kinabii na swala zima la kupata uhuru kwa mataifa yaliyokuwa chini ya ukoloni Kama alivyoeleza Yesu katika unabii wake Luka 21:29-33Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie..
Tawala kubwa ni tawala ambazo zilipanua utawala wake mpaka katika mataifa mengine, tawala hizi kubwa zilidumu kwa karne nyingi na zilikuwa na hatua za maendeleo zilizowafuatiwa nazo, Ukoloni  na ubepari uliletwa na tawala hizi kubwa, Twala kuu zilidumu mpaka mwaka wa 30 KK – 1453 BK, Mtawala mkuu wa kwanza aliku kaisari Augusto. Yesu Kristo alizaliwa wakati wa mtawala huyu, watawala wengi waliofanikiwa walitawala wakati wa utawala wa rumi na waliwatesa sana wakristo, Mshauri wa Mtawala aliyeitwa Pliny na barua yake aliyoiandika kumshawishi Mtawala Trajan katika mwaka 112 jinsi ya kuwashughulikia wakristo ilikuwa na mchango mkubwa sana katika swala hili, ilipofika mwaka 117 wakati utawala wa Rumi ukiwa bado uko chini ya Trajan Ukristo ulikuwa na kuwa dini kubwa sana ulimwenguni yenye ushawishi mkubwa katika uatwala wa Rumi, Mtawala wa rumi alianzisha ibada za miungu ya Rumi na sanamu zake

Utawala huu uliweka sheria zenye lengo la kukandamiza na kutiisha, ili kuendeleza ulimwengu na jamii za ulimwengu na pia walianzisha maswala ya kuhamisha watu na maswala ya kutokuwatendea watu haki kama sehemu ya swala hilo, Baadaye swala hili linasemekana ndilo lililochochea kuweko kwa ukoloni na utumwa, Wanadamu waliaza kufanywa watumwa na kuwa kama bidhaa, wanadamu wengine wakiwanunua na wengine wakiwamiliki bila wao kuwa na uchaguzi wa nini cha kufanya na kuwatumikia mabwana zao, Mswada wa kukomesha  biashara ya utumwa ulipitishwa mwaka 1807 na Bunge la Waingereza, Lakini huko Zanzibar  Afrika Mashariki ambako ilikuwa bandari na soko kuu la utumwa na  chini ya utawala wa Waarabu wa Oman biashara iliendelea mpaka karne ya 19, na hii inafunua jinsi ambavyo wanadamu ni waovu na wabaya pasipo na Mungu. 

Ubepari ambao ulitawala magharibi unaweza kuelezewa kuwa ni mfumo wa kisiasa wenye misingi ya haki za binadamu za mtu au shirika kuwa na uwezo wa kimiliki mali.

Ukomonisti ambao ulitawala Mashariki ni wazo kutoka ugiriki ya kale, lililoelezewa na Plato kama wazo lenye daraja za ushirikiano na umiliki wa pamoja wa mali, hiki ndicho kilichikuja kuzaa ukomonisti, na usoshalisti, lengo likiwa ni kuwa na serikali ambazo watu wake wanashirikiana mali na ikawa kinyume na ubepari, Katika nyakati hizi baada ya kuchanua kwa Mtini yaani Israel na mataifa mengine yaani kupata uhuru athari za tawala hizi zilisalia katika mataifa mbalimbali hata leo na umeishababisha dunia kutokuwa na mshikamano hata sasa
5.       Chuma na Udongo.Inawakilisha mfumo wa serikali za Kidemokrasia ukoloni mambo leo na sharia Mchanganyiko wa mambo.

Inawakilisha tawala za kidemokrasia zinazoendelea lakini dhaifu, kwa mujibu wa unabii hii ni aina ya mwisho wa tawala za kibinadamu duniani na ni wa muda mfupi, utakuwa na uhuru mkubwa wa kupita kawaida kwa dhambi na uovu ambao utaenea dunaini, Uislamu udongo ukiwa na mgogoro mkubwa na mifumo ya serikali hizo kwa kuwa watafanya kazi ya kutafuta kuwa na mfumo waserikali zinazotaka kuwa na nguvu dhidi ya Kanisa. Uislamu umekuwa ukiendeleza chuki za wazi dhidi ya wayahudi na kanisa  na kuandaa njia ya ujio wa Mpinga Kristo, Chuma kinawakilisha tawala ambazo zina ushawishi wa Kikristo na udongo unawakilisha tawala zenye ushawishi wa kiislamu chini ya utawala wa Sharia, mtu anaweza asikubaliane na tafasiri hii lakini angalia kile kinachoendelea sasa duniani katika jamii yatu ya sasa utaelewa. Kuwa unabii  wa maandiko unatimizwa. Tawala za Chuma na Udongo haziwezi kushikamana na udongo ni dhaifu, inawakilisha tawala za Demokrasia na Sharia, kutokana na mkazo wa kukua kwa demokrasia na uhuru wa watu kuwa na sauti duniani na uhuru wa kuabudu, kutatokea kutokuelewana kukubwa sana katika jamii na mchanganyiko usioshikamana , huu utakuwa ni wakati wa kilele cha uovu wa aina binadamu na serikali chafu sana kutokana na kivuli cha Demokrasia kama tukakavyojadili kwa undani zaidi.

6.       Jiwe lisilochongwa kwa mikono ya kibinadamu linawakilisha Ufalme wa Mungu chini ya Yesu Kristo 

THEOCRACIA  huu ni utawala wa Mungu, Utawala ambao  Yesu Kristo baada ya kurudi kwake mara ya pili Duniani ataitawala dunia nzima, utakuwa utawala wa amani juu ya mataifa kwa miaka 1000, Hili jiwe ni Yesu Kristo atakapokuja mara ya pili duniani, ambaye atakomesha vita vya harmagedon,  na migogoro yote mikubwa duniani na  kufikisha mwisho aina zote za serikali za kibinadamu ambazo zinamalizikia na tawala za kidemokrasia, Atasitawisha amani na ufalme wake kwa kuyashinda mataifa yatakayokusanyika kwaajili ya vita vya Harmagedoni, Wayahudi na waisrael wote wakati huu watamkubali Yesu Kristo yeye waliyemchoma kuwa Ndiye Masihi Mfalme wa wafalme. Utakuwa ni ufalme wa utulivu na amani SHALOM au Irene itatawala Duniani. Huu ndio ufalme ambao Israel wanautazamaia makao makuu ya utawala huu yatakuwa Israel na mji mkuu utakuwa Yerusalem.

Neno la Mungu na utawala wa Kidemokrasi.

Historia inaonyesha kuwa kila aina ya utawala na mifumo ya kiserikali ilikuwa na faida zake na hasara zake, Mungu aliwaacha wanadamu wajitawale, baada ya kuwa wanadamu waliukataa utawala wake na kutaka kuwa huru kufanya kila wanaliloiona kuwa jema machoni pao, Mara kadhaa Mungu aliadhubu na kukemea wanadamu lakini walikuwa ni wenye shingo Ngumu Mwanzo 6:3 “BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Mungu aliona kuwa wanadamu wamekuwa na desturi ya kukataa ufalme wake na utawala wake na kwa sababu hiyo amewacha wafuate kila wanachikitaka, katika nyakati hizi za tawala za Kidemokrasia maovu yataongezeka mno kwa sababu madai makuu ya wanadamu yatakuwa kwenye uhuru wa kujifanyia kila wanaloliona jema machoni pao, wanadamu watakuwa wamechoka kuingiliwa  na kila mtu ataona anahitaji kuliamulia anachoweza kujiamulia na kwa sababu ya kukataa kuwa na Mungu, Mungu atawaacha wanadamu wafuate njia zao za uharibifu na kujiletea hukumu  

Warumi 1:18-25Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina

Huu ndio wakati ambapo watu watalikataa neno la Mungu na kufuata na kujitafutia waalimu kutokana na kuwawatafiti watafuata khadhithi na kulikataa neno la Mungu, katika nyakati hizi ndio watu wa Mungu tunatiwa moyo kwa maandiko kukemea kukaripia kuonya na kufundisha kwa bidii 

2Timotheo 4:1-5 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.”

 Mfumo wa utawala wa Kidemokrasia umeharibu sana jamii, muhubiri wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika “Creflo Dollar” aliwahi kuitwa polisi kutoa maelezo ya kumchapa kibao binti yake, kumekuwapo na sheria za kijinga kiasi ambacho huwezi kumuonya mtu, kumpiga mtoto ni kosa kubwa, wanawake wnahisi kuwa walikandamizwa kwa miaka mingi na sasa wanataka kuwa na sauti na maamuzi yao, kuwatii waume zao sawa na maandiko limeonekana kuwa swala la utumwa,  kudaiwa kwa haki na usawa wa kijinsia, ndoa za jinsia moja  ambazo zinatiwa moyo na mataifa yote ya kidemokrasia ambayo yanafikiri kuwa yameendelea sana, uhuru wa kuabudu uliokithiri kiasi ambacho watu wanaweza kufanya lolote kwa jina la Mungu, vikundi vya kigaidi vya watu wenye kuua wenzao kwa misingi ya chuki na visingizio vya dini zenye siasa kali, machafuko ya kila aina uhuru wa kutoa au kupokea habari, uhalifu wa kimtandao, wizi, udanganyifu na utapeli ufisadi na kadhalika ni matukio ambayo yametawala katika nyakati hizi za utawala wa chuma na udongo kabla haujaja utawala wenye nguvu wa Yesu Kristo, hizi ni dalili za ujio wa mpinga Kristo na kunyakuliwa kwa kanisa ambako wengi wataacha kutokana na kuvutiwa na uovu na anasa na tamaa za dunia hii
Yesu anaonya kwamba katika wakati huu watu wajihadhari 

Luka 21:34-36. “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.” 

Yesu ataikuta dunia iko katika hali mbaya sana kutokana na kuwepo kwa serikali ovu na legevu, ni lazima kanisa liwe macho na kutokukubali kuifuatisha namna ya ulimwengu huu 
  
Hatari ya uhuru uliokithiri chini ya mfumo wa kidemokrasia.

Uhuru wa kupita kawaida sio mpango wa Mungu kabisa tangu pale alipomuumba mwanadamu, Mungu alipomuumba mwanadamu aliweka mipaka ili kutokuruhusu uhuru uliokithiri, uhuru ambao ungemuongoza mwanadamu katika kumtenda Mungu dhambi, uhuru  bila mipaka sio mpango wa Mungu, kizazi tulicho nacho kwa bahati mbaya kinataka uhuru huo chini ya kifurushi cha maendeleo na demokrasi.

Kwa Adamu na Hawa Mungu hakuwapa uhuru bila mipaka Mwanzo 2:16-17 inasema “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” 

Kwa wana wa Israel Mungu hakuruhusu wawe na uhuru wa kujifanyia kila wanachokitaka kwani wangefanya dhambi aliwapa amri kumi na sheria nyingine ndogondogo ili waweze kuzizingatia, Kutoka 20-40, amri hizi zilipelekea wana wa Israel waweze kudumisha uhusiano wao na MUngu na watu wengine wanaowazunguka  

Kutoka 20:1-17Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako. Usiue.  Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.”

Kwa kanisa zaidi ya kuangalia amri kumi  Yesu Kristo katika hutuba yake ya mlimani aliweza kutoa muongozo wa kiroho ili kila mmoja aweze kuzingatia na ili aweze kuwasehemu ya  ufalme wa Mungu, katika injili ya Mathayo 5-7, Yesu alitoa na kuorodhesha sifa za kiroho ambazo mtu anapaswa kuwa nazo ili aweze kuwa na uhusiano na Mungu na kuurithi uzima wa milele. Aidha sheria maarufu ya Yesu Kristo iitwayo sheria ya dhahabu ni smingi muhimu katika kuishi kwa utaratibu Mathayo 7:12Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.”

Jambo la muhimu ninalotaka kulizungumzia hapa ni kwamba mfumo wa serikali za kidemokrasia unaoonekana kuwa ni mzuri zaidi na kupendwa ndio mfumo mbaya  na muovu na unaoharibu hali ya kiroho na kudhoofisha  uadilifu wa watu na Kanisa na ndio mfumo wenye kuvumilia dhambi kwa kiwango kikubwa na cha uhuru uliopitiliza, msisitizo wa kisheria unaendelea kuwa dhaifu kila siku, watu wanataka uhuru zaidi na wako tayari hata kuasi, viongozi wakubwa wa mataifa ya dunia wamekuwa wakichukuliana na kila kinachoonekana kuwa ni sawa na kwa ujumla wamelemazwa na mfumo huu. Mfumo huu wa kisiasa una nguvu ya shetani na wanadamu na hivyo kila kiongozi duniani atakayeonekana ana viashiria vya kidikteta anapigwa anadhoofishwa na Demokrasia inatawala kisha uovu mkuu unafuata hii ni sihara kuwa muda wa ile sanamu ya Nebukadreza umekamilika na sasa tunasubiri utawala wa Jiwe lisilochongwa kwa mikono Utawala wa Yesu Kristo duniani.

Asomaye na afahamu

Na mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote.