Alhamisi, 25 Februari 2016

Jinsi ya Kujifunza Udereva !


VIPENGELE VYA UDEREVA VYA KUJIHAMI.
Ili kutekeleza kanuni ya kuzuia ajali, Dereva yeyote anatakiwa kuelewa vizuri mambo ya msingi yafuatayo;-

1.       Kujua
2.       Kuwa macho
3.       Kuangalia mbele
4.       Kuamua
5.       Ujuzi wa kugundua , hatari kwa haraka


KUJUA

Dereva anapaswa kuelewa michoro na alama za barabarani.
i.                     Alama za barabarani na michoro inawakilisha lugha, ambayo kila mtumiaji wa barabara anatakiwa kuijua vizuri, kuiheshimu na kuitafasiri kama inavyotakiwa.
ii.                   Kwa bahati nzuri inawakilishwa na vbitambulisho vya vikundi vikuu vitatu
a.       Rangi Nyekundu, Nyeusi, Njano, Nyeupe, bluu, kijani.
b.      Umbile Mviringo, Pembe tatu, Pembe nne na pembe tano.
c.       Alama – Maandishi, Picha na Michoro.
iii.                  Alama na michoro ya barabarani ni lazima ziwe na sifa zifuatazo.
a.       Zilenge kuongeza ufanisi wa mtandao wa barabara.
b.      Zitoe ujumbe ambao ni wazi unaoeleweka kirahisi kwa kila mtumiaji wa Barabara.
c.       Zizingatie sheria za  usalama barabarani za kitaifa na kimataifa
d.      Ziwe na muundo wa alama moja kitaifa unaolingana na makubaliano ya umoja wa kimataifa kwa alama za msingi.
e.      Ziwekwe sehemu ambazo ni lazima kuwepo, ili zitoe ujumbe sahii kwa watumia Barabara,
f.        Ziwekwe umbali unaotakiwa kutoka sehemu husika
g.       Zifanyiwe matengenezo ya marakwa mara.

Mambo ya msingi ya kujiuliza kwanza
a.       Alama ni kiashirio kinachomuongoza mtu kwenye mambo na kumfanya afanye mambo vizuri.
b.      Alama za barabara ni uongozi uliowekwa kisheria  kutoa muongozo wa kisheria  ili kumuwezesha dereva  aweze kufanya kazi zake kirahisi na  kwa ufanisi  ili kwamba atumiapo barabara  aweze kwenda kwa uysalama zaidi bila kupata au kusababisha ajali.
c.       Alama za barabarani ni kitu ambacho hakitarajiwi kutokuweko
d.      Wataalamu waliamua kukaa na kutunga alama za usalama barabarani  alama hizo zimegawanyika katika makundi makuu matano
·         Alama za Amri
·         Alama za Onyo
·         Alama za taarifa
·         Alama za maelekezo
·         Alama za michoro chini ya barabara , taa za kuongoza watumiaji wa barabara.

Alama za Amri
Alama hizi zimegawanyika katika makundi makuu matatu yafuatayo;-
-          Amri za kukataza.
-          Amri za kulazimisha au kuruhusu.
-          Amriza kutoa kipaumbele

Amri za kukataza ;-
Alama hizi zina waonyesha watumiaji wa barabara sehenu ya barabara iliyokatazwa au mwisho wa sehemu iliyokatazwa  kufanya jambo Fulani  kama itakavyoonyeshwa  kwenye alama yenyewe alama hizi ni halali

·         Katika mwelekeo wa kawaida wa wanaotumia barabara
·         Kutoka sehemu iliyopo hadi njia panda iliyo karibu na alama husika .
Alama za amri ya kukataza zina umbo la mviringo, mpaka mwekundu na picha au mchoro wenye rangi nyeusi, nyekundu au bluu katika madhari
Alama au amri ya kukataza zinawekwa karibu sana na sehemu husika 

Alama za kulazimisha  au kuruhusu
Ø  Hizi ni alma zinazzotumika kwa watumia barabara  kuelekea mwelekeo au njia Fulani kati ya nyingi zilizopo kwenye  njia panda , pia alama hizi zinatumika kuwaongoza wanaotembea kwa miguu na wapanda baiskeli kwenye njia moja kati ya njia zilizopo kwenye eneo husika
Ø  Amriza kulazimisha zina umbo la mviringo mpaka mdogo mweupe na picha ai mchoro mweupe katika madhari nyuma bluu alama hizi zinawekwa karibu sana na njia panda
Ø  Alama za kipaumbele na kupisha njia panda ni sehemu yenye migogoro mingi kati ya watumia barabara kuliko sehemu nyingine yoyote ile barabarani. Ili kurekebisha migogoro hiyo kati ya watumia barabara. Sheria ya Usalama barabarani  inatumika (toa kipaumbele  kwa madereva wa magari wanaokaribia njia panda kutoka kulia ) lakini sehemu yenye magari mengi  ambapo madereva hawawezi kutathimini vizuri hatari iliyopo basi sehemu hiyo njia panda  sheria ya usalama barabarani haitatumika  tena badala yake zitatumika alama za kipaumbele
Ø  Alama hizi zina maumbo mbali mbali kulingana na ujumbe au amri inayokusudiwa katika alama husika.

Alama za tahadhari au Onyo
Ø  Alama hizi zinawaonya madereva na watumia barabara wengine juu yaq hatari iliyopo au inayoweza kuwepo mbele yao
Ø  Alama hizi zinawqekwa upande wa kushoto wa barabara  kati ya mita mia hadi  mia mbili (100-200m) toka sehemu yenye hatari
Ø  Sehemu zenye njia panda nyingi hasa mjini umbali huo hupungua hadi mita hamisini  (50m)
Ø  Sehemu ya barabara yenye alama hizi dereva anatakiwa kupunguza kasi ya gari lake.
Ø  Alama za tahadhariu au onyo zina umbo la pembe tatu lenye kitako pembe mbili chini, mpaka mwekundu na picha au mchoro wa hatari iliyopo au inayoweza kutokea mbele katika mandhari ya nyuma nyeupe.

Alama za Taarifa
Ø  Alama za taarifa huwataarifu madereva na watrumia barabra wengine juu ya barabara , sehemu muhimu na sehemu senye huduma mbalimbali ambazo ni muhimu kwao , kati ya alama hiziz zipo pia  zenye uhusiano na sheria ya usalama barabarani ambazo zinatoa masharti Fulani ambayo  mtumiaji wa barabara akiamua kutumia sharti afuate sheria  na si vinginevyo Kwa Tanzania ni hiari ya dereva kutumia barabara hiyo ,lakini akiamua ni lazima aendeshe gari lake uelekeo ulioonyeshwa kwenye alama hiyo.
Ø  Alama za maeneo ya huduma, hizi ni taa ni alama zinazowafahamisha madereva na watumia barabara wengine juu ya huduma mbalimbali wanazoeweza kupata katika maeneo husika
Ø  Alama hizi zina umbo la pembe mraba nne, ulingo wa Bluu picha nyausi au nyekundu katika madhari nyeupe nyuma 

Alama za maelekezo
Ø  Hizi ni alama za kuwafahamisha madereva wa magari sehemu maalumu nba muhimu
Ø  Alama hizi zina umbo la pembe nne Mstatili au mraba ulingo wa bluu picha nyeupe au nyeusi madharri ya bluu au kijani nyuma.
Ø  Alama hizi zinawekwa kabla ya njia panda  au kwenye njia panda  ili kuwasaidia madereva na watumiaji wengine wa barabara  kuchagua barabara  zinazofaa kuwafikisha waendako na kuwaongoza kwenye mtanadao wa barabara kupita na hata kuzunguka  kwenye maeneo ya makazi ya watu

Alama za michoro ya chini ya barabara na taa za barabarani
Ø  Michoro ya barabarani ni ni mmichoro iliyochorwa kwa  lengo la kurekebisha msongamano wa magari pamoja na kuwaonya au kuwaongoza watumiaji wa barabara
Ø  Michoro hiyo ya barabarani imegawanyika katika makundi makuu yafuatayo;-
*      Mistari ya Onyo
*      Mistari ya kukataza
*      Mistari inayogawa njia katikati ya barabara  ya magari
*      Mistari inayogawa barabara
*      Mistari inayogawa njia ya  magari ya abiria  katika barabara
*      Mistari ya kutokea  pembeni mwa barabara  ya magari
*      Mistari ya kipaumbele
*      Mistari ya kusimama
*      Mistari hii pia huchoirwa karibiu na njia panda  sehemu ya barabara hii dereva hatakiwi kuvuka njia kwa sababu ya hatari iliyopo ikiwa atavuka basi avuke kwa tahadhari kubwa
Taa za kuongoza watumia barabara
Ø  Taa hizi zinalenga  kuondoa migogoro kati ya watumia barabara  kwenye njia panda au barabara zenye matumizi makubwa
Ø  Taa nyekundu humaanisha usiingie njia panda simama
Ø  Nyekundu na njano usiiingie nja panda simama
Ø  Njano usiingie kwenye njia poanda simama
Ø  Kijani ingia kwenye njia panda endapo ni salama.
LIJUE GARI LAKO.
Mfumo wagea Gea za Gari za aina mbali mbalizenye kutumia mfumo wa Manyo ( Manual)







Mfumo wa gea za kukanyaga katika magari manyo



CLUTCH ;            Kazi yake ni kuondoa gari  na kutenganisha Engine na Gearbox.
BRAKE  ;              Kazi yake ni kupunguza mwendo na kusimamisha gari
ACCELERATOR; Kazi yake ni kuongeza mwendo kasi wa gari na muungurumo na inapoachiwa kidogo mwendo hupungua, inaongeza kasi ya uhcomwaji wa mafuta.
Ni Muhimu Kukumbuka kuwa Unapotaka kusimama unatakiwaq kukanyaga Clutch na Brake kwa pamoja ili gari lisizime linaposimama.
Kazi ya gea namba moja Ni kuondoa gari na kupanda mlima mkali  na wakati wa kuteremka mlima mkali
Kazi ya gea namba mbili Ni kuifanya gari kuwa nyepesi zaidi na kuongeza mwendo
Kazi ya gea namba tatu na nne Ni kufanya gari kuendelea kuwa jepesi zaidi na kuongeza mwendo

Namna ya kupanga gea kutoka gea nzito kwenda gea nyepesi;
Kutoka          0-10    MPH Gea .  No 1
Kutoka        10-20    MPH. Gea . No 2
Kutoka        20-30    MPH. Gea.  No 3
Kutoka        30-40    MPH. Gea.  No 4
Kutoka        40-50    MPH Gea.   No 5
Kutoka        50-120  MPH.    Mwendo utaendelea kuzaliswa na gia No 1  &  2

Jinsi ya kupangua gea kubwa kwenda gia ndogo
Kama gari lilikuwa linatembea kiasi cha  mwendo upatao 60MPh itakubidi upunguze mwendo hadi 50MPH au 40MPh ndipo uingize gia nambari nne
Endapo inatembea mwendo kiasi 40 MPH itakubidi upunguze mwendo hadi kufikia 30MPH ndipo uingize gia nambari tatu
Kama gari ilikuwa inatembea kiasi cha mwendo upatao 30MPH itakubidi upunguze mwendo hadi kufikia 20MPH ndipo uingize gea nambari mbili
DASH BOARD
Dash board ni chombo ambacho kinamjulisha na kumwezesha dereva kugundua hitilafu zinazoweza kujitokeza anapoendesha gari barabarani kwa mfano
·         Kusoma speedmeter – hiki ni chombo ambacho  hupima kasi au mwendo wa gari
·         Mail gauge – hiki ni chomboambacho hupima au kuhesabu au kurekodi ni mwendo au umbali gani gari limetembea
·         Fuel gauge – ni kipimo cha kuonyesha ni kiasi gani cha mafuta aidha Petrol au diesel iliyoko kwenye tank la gari
·         Oil gauge – ni kipimo chenye kufanya kazi ya kuonyesha  ni kiasi gani cha oil kimebakia kwenye injini
·         Water temperature gauge  ni kipimo ambacho kinaonyesha joto la injini limepanda kiasi gani  na pia kuonyesha maji yamepata moto kiasi ghani kwenye radiator
·         Alternator gauge au alternator charge hiki ni chombo cha kuonyesha kuwa kifua umeme katika gari hakifanyi kazi kwa msingi huo maana yake ni kuwa haichaji na hivyo maana yake ni kuwa umeme haufuliwi
·         Right indicator – ni taa maalumu yenye mlio Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda upande wa kulia
·         Left indicator – ni taa maalumu yenye mlio Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda kushoto
Dash Board kama inavyoonekana katika mchoro chini.

Katika Dash Board kunakuwa na maswala kadhaa yanayoweza kusoma mambo kadhaa yafuatayo
0        2          6         8          6     4    2
Water temp
Brake Light
Alternator
Fuel gauge
Right
Left indicator

Fuel

UTUNZAJI WA GARI
Katika utunzaji wa gari kwa ujumla tunazungumzia ukaguzi wa gari.Ukitaka gari lako liwe katika hali nzuri kila ulitumiapo/kuwa na uhakika wa usalama wako na wa gari lako liwapo barabarani, ni muhimu sana kulikagua hari kila siku asubuhi kabala ya kuliendesha na pia kuwa na utaratibu wa kulifanyia service kila linapotembea kilomita kadhaa.
Ukaguzi wa gari
1.       Kitu cha kwanza kabisa ni kulikagua gari lako kwa nje, utafanya ukagfuzi wa matairi kwa kuangalia
·         Upepo na nati kama zimelegea au la
·         Kashata za Matairi kama hazijaisha yaani ziko kipara
Kisha utafungua Bonet na hapa utaangalia
·         Maji kwenye rejeta (radiator) kama yapo
·         Oil kwenye injini kwa kutumia deep stick
-          Hakikisha unapopima oil gari liko katika tambarare ili uweze kupata level halali ya oil
-          Oil inayotumika kwenye injini kwa kawaida ni nambari 40
-          Deef oil nambari 140
-          Gear box ni oil nambari 90
·         Mafuta ya Brake (Brake fluid) na clutch
·         Maji ya betrii, yaani unafungua betrii na kuangalia kama
-          Maji yamepungua unaongeza maji baridi Distrilled water
-          Kama ni jipya umemwaga maji yote na kuweka Acid maarufu kama maji makali HCI
-          Maji yakiisha ndani ya betrii , batrii itakufa baada ya hapo
-          Unafunga tena bonet.
2.       Sasa unaingia ndani ya gari na unaaangalia
·         Kaa kwenye kiti chako  na hakikisha kimekaa sawasawa
·         Kagua pedle zote  kama zinafanya kazi sawasawa yaani hapa tunazungumzia
-          Brake kama iko sawa na inafanya kazi
-          Clutch kama iko sawa na inafanya kazi
-          Acceletator kama iko sawa na inafanya kazi.
·         Kagua dashboard kama taa zote za vitu vyote zinafanya kazi vema yaani
-          Water temperature gauge
-          Alitanatory charge
-          Oil gauge
-          Fuel gauge
-          Mail gauge .n.k.
·         Waipa kama zinafanya kazi vema
·         Hand brake kama inafanya kazi vema
·         Usukani kama umekaa vema
·         Mkanda
·         Taa zite kama zinafanya kazi Hususani indicator
·         Wema side mirror vema  kukuwezesha kuona chochote kwa nyuma au pembeni
·         Kioo cha kuangalia magari nyuma pia kiwekwe kukuwezesha kuona
Ukimaliza yote hayo sasa uko huru au salama kuendesha gari lako.
KUONDOA AU KUENDESHA GARI.
Unapokuwa umekagua gari lako na kulikuta liko katika hali nzuri sasa unataka kuliendesha na kuanza safari na gari lako, unapoingia kwenye gari na kuikuta iko katika gea namba moja basi sasa unapaswa kufanya maswala yafuatayo.
i.                     Weka switch/ yaani ufunguo wa gari katika sehemu yake
ii.                   Kanyaga clutch mpaka mwisho
iii.                  Ondoa gea namba moja na kuliweka gari huru yaani free
iv.                 Ondoa mguu kwenye clutch
v.                   Anza kuwasha ufunguo wa gari Satrt/Switch gari
vi.                 Sikiliza muungurumo kidogo
vii.                Kanyaga clutch mpaka mwisho/pamoja na brake kulisaidia gari lisiweze kurudi nyuma
viii.              Ondoa gari kutoka kwenye free mpaka kwenye nambari moja  gea hii mara nyingi hujulikana kama gea ya kuondokea
ix.                 Legeza mguu wa kwenye clutch mpaka unasikia gari kama inaondoka hivi mlio unakuwa umebadilika na unakuwa constant
x.                   Kumbuka kutoa handbrake
xi.                 Ongeza mafuta kidogo na na kulegeza clutch na gari litaanza kuondoka na linapoondoka  achia clutch, lakini usiachie ghafla, taratibu baada ya kuona baada ya kuona gari liko kwenye mwendo wa kawaida
xii.                Lipe gari nguvu kwa kuongeza mafuta na badilisha gea nambari  moja kwenda nambari mbili, unapobadilisha gea hakikisha kuwa unaachioa accelerator na kukanyaga clutch  na baada ya gea kuingia unaachoia clutch na unakanyaga acceleretaor
xiii.              Utaendelea na safari kwa kubadilisha gea nambari mbili mpaka tatu na kuendelea
Kumbuka gea nambari moja sio ya kutembelea hivyo usiiache kwa muda mrefu bila ya kuibadilisha
Unapoendesha gari hakikisha kuwa una vyeti vyako ili isiwe kero kwa traffic vyeti hivyo ni
a.       Leseni ya kuendeshea driving Licence – hakikisha haijaisha na pia iwe ni daraja linalohusika
b.      Kadi ya njia (T.L.B)
c.       Kadi ya gari ambayo kwa kawaida huwa na
o   Jina la gari
o   Namba ya gari
o   Jina lako
o   Gari lilitengenezwa wapi
o   Limesajiliwa lini hapa nchini
o   Engine namber
o   Chases Nuimber n.k.
Vitu muhimu kuwa navyo unapoendesha gari ni pamoja na
·         Spare tyre-tairi la akiba
·         Jeki
·         Na spana ya kuondoa tairi Wheel spanner
Safari ya mbali
·         Kisanduku cha huduma ya kwanza chenya panadol, aspirin, spirit, iodine, bendeji, pamba, plaster, wembe mkasi, pini n,k.
·         Spana za dharula
·         Plaizi na Plier
·         Adjustable screw driver, plug spanner na sanduku nzima ya spanner
·         Kamba
·         Fan belt
·         Petrol au diesel na kitu kingine chochote utakachokiona muhimu katika gari lako kwa safari
Kuvumbua kasoro
1.       Kifaa au chombo kitakachokujulisha kuwa gari lako lina kasoro ni Dash  board.
2.       Pia kwenye mwili wako viungo vitakavyokufanya uvumbue kasoro ni
o   Macho yako kwa kuona
o   Sikio lako kwa kusikia
o   Pua yako kwa kunusa
Unapogundua chochote cha tofauti kwa kutumia vitu hivyo juu simamisha gari lako kagua na kugundua hitilafu.
Kuna aina tano “5” za Taa;-
·         Full Light Taa kubwa – Taa hizi zina mwanga mkali na hutumika wakati wa usiku  ili kuona masafa marefu, endapo mbele hakuna kitu chochote chenye mwanga mfano gari linguine ua pikipiki au baiskeli  n.k
·         Deem Light taa ndogo – Taa hizi hutumika  kama mbele yako kuna gari lililo kutangulia , pia kama mbele yako kuna gari lingine linakuja unapaswa kutumia deem light au kama mbele yako kuna kitu chenye mwanga  mfano pikipiki au baiskeli au hata gari linguine
Hakikisha kuwa mwendo wa gari hauzidi mwendo wa mwanga wa gari kwa msingi huo nenda mwendo sawa na wa taa zako
·         Indicator ziko mbili kwa kawaida
Indicator ya kulia ni kwaajili ya kuonyesha kuwa gari linapinda kulia au kwaajili ya kuomba nafasi ya Njia wakati unapotaka kulipita gari linguine Overtake au kumzuia dereva wa nyuma asi Overtake
Indicator ya kushoto ni kwaajili ya kuonyesha kuwa gari linapinda kushoto, kuruhusu gari la nyuma liweze kupita Overtake na kuonyesha kuwa gari linataka kusimama au kupaki kushoto
·         Parking light – Hutumika wakati gari linapokuwa limepaki hususani wakati wa usiku, au wakati wa ukungu ukungu mvua ua vumbi, pia mara giza linapoingia unashauriwa kuwasha Parking light  ni hatari kama unapark gari usiku bila kuwasha parking light kwani dereva wa gari nyingine anaweza asikuone  na akakugonga
·         Brake Light – Hutumika kumjulisha dereva  wa gari la nyuma kwamba  unapunguza mwendo au unasimama

UBADILISHAJI WA TAIRI
Utangulizi
Katika utaratibu wa kawaida ubadilishaji wa tairi unaweza kufanyika katika njia kama mbili zifuatazo;-
·         Kuisha kwa tairi – yaani baada ya tairi kulika limeisha linahitaji kubadilishwa
·         Pancha – wakati tairi linapopata pancha (Punctuare)
Kulika au kwisha kwa tairi
Kwisha au kulika kwa tairi ni jambo la kawaida  kutokana na msuguano  wa tairi na ardhi, hivyo ni vyema tairi linapokuwa limekwisha au liko kipara  zibadilishwe na kuvalishwa ganda  ama mpira mwingine mpya ili kwamba ;-
a.       Kuepuka usumbufu wa askari wa barabarani
b.      Kulinda maisha yako  nay a watu wengine
c.       Kuweka usalama wa gari
d.      Kuwa na uhakika uwapo safarini na wakati wote unaposhughulika na gari
e.      Kupita sehemu yoyote  bila ya kuwa na wasiwasi
Kwa msingi huo basi ni muhimu kwa tairi za gari kuwa nzima wakati wote ili kupunguza matatizo yaliyotajwa hapo juu.
Pancha (puncture)
Pancha hutokea wakati wowote na kwa tairi yoyote hususani zile zilizolika kashata zake. Unapokuwa na pancha ni vyema kuzingatia yafuatayo, iwapo utakuwa umekumbwa na pancha ni vyema kuzingatia yafuatayo iwapo pancha imekupata kwenywe njia inayopitisha magari wakato wote zingatia maswala muhimu yafuatayo;-
·         Egesha gari pembeni mwa barabara
·         Weka kibao au alama ya onyo kama unacho mbele na nyuma ya gari kiasi cha mita 100 ili kuashiria tahadhari ya matengenezo au uharibifuau marekebisho/Matatizo ya gari
·         Weka vigingi au mawe kwenye tairi la mbele  na nyuma isipokuwa tairi lililopatwa na pancha
·         Chukua wheel sperner na legeza nut za tairi iliyopata pancha
·         Chukua jeki tafuta sehemu itakayostahimili uzito wa gari kama vile kwenye chassis Frame nyuma ya aksel au kwenye kiti cha spring piga jeki juu ili tairi iachane  na ardhi
·         Chukua tena wheel spanner na malizia kufungua nut za tairi ya pancha kisha ondoa tairi hiyo.
·         Chukua tairi ya tahadhari (Spare tyre) funga sehemu ya tairi iliyopata pancha, Funga nut kwanza kwa mkono kisha nut mbili zinazoelekeana zikaze kwa kutumia wheel spanner, rudia tena nut zote kwa wheel spanner, rudia tena nut zote kwa kwa wheel spanner kwaajili ya kuzikaza usitumie bomba kwani unaweza kulegeza au kukata stud.
·         Weka tairi lililopata pancha kwenye gari ondoa mawe au vizuizi kwenye tairi, Ondoa vigingi ulivyoweka kwa kuashiria  magari mengine kuwa kuna matengenezo au matatizo barabarani
·         Washa gari kasha endelea na safari yako.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba unapopata matatizo ya pancha pitia kwa waziba pancha na kuziba tairi lako, iwapo tairi uliyoifunga ina kipara rudishia tairi lenye kashata uliyoiziba pancha na tairi zako zinapokuwa zimeisha kumbuka kufunga mipira mingine mipya
Vilevile kumbuka kutumia viegemezi supports kusaidiana na jeki wakati wa kubadilishja tairi, ili kwamba iwapo jeki itashindwa viegemezi vikusaidie kushika gari kuegemea chini upande wa tairi iliyopata pancha au upande unaobadilishwa tairi
VITU MUHIMU KUELEWA NDANI YA GARI KWA DEREVA MWANAFUNZI.
1.       Rejeta (radiator) – Kazi ya chombo hiki ni kuhifadhi maji ya kupooza Injini
2.       Oil – Kazi ya oil ni kulainisha vyuma vinavyokutana kwenye gari, Oili ni muhimu sana kwenye injini. Kwani ukosefu wa oil unaweza kusababisha injini kufa au kusimama (Knock)
3.       Mafuta ya brake (Brake Fluid).- Kazi yamafuta ya brake ni kusaidia gari liwe na brake  pamoja na clutch. Kwa hivyo unatakiwa kuangalia mafuta ya brake wakati wote pamoja na Clutch, unatakiwa kuangalia mafuta ya brake wakati wote yawepo kwenye kihifadhio chake.
4.       Betrii (Batery)- Kazi ya betrii ni kuhifadhi moto na kutoa moto kwa kusaidia shughuli kama kuwasha taa, kuanza mwendo wa gari (Starting) kuwa kwenye Moto/mwendo na kadhalika
5.       Ignition coil;- Kazi ya ignition coil ni kukuza moto utokao kwenye betrii na kuingia  kwenye distributor nayo inatoa huo umeme kwenye plugs ukiwa umepoa, plugs ndizo zinatoa moto kwenye injini.
6.       Distributor – Kazi ya distributor ni kugawanya moto kwenye injini na kufanya gari liwe na mlio mzuri na nguvu, chombo hiki kina waya tano na ukichomoa waya mmoja tu gari linbakuwa lina miss.
7.       Plugs;- Kazi ya plug ni kuchoma Petrol kwenye injini, Pulug inaposhindwa kuchoma inabidi uibadilishe ili kuepuka gari kuwa na miss.  
8.       Fuel Pump – Kazi ya fuel Pump ni kuvuta mafuta kutoka kwenye tank na kyapeleka kwenye Carburator
9.       Carburator – Kazi yake ni kupokea mafuta  kutoka kwenye fuel Pump na kuyachanganya  na hewa kwa kipimo maalumu kilichowekwa na kwenda kwenye injini
10.   Alternator – Kazi ya chombo hiki ni kuchaji betrii na kusaidiana na betrii ili kutoa moto wa betrii na kusababisha betrii isipungue moto wakati wote gari linapokuwa linatembea.
11.   Self start. – Kazi ya self start ni kuwasha gari wakati gari likiwa bovu na haliwezi kuwaka lenyewe, chombo hiki hifanya kazi wakati gari linasukumwa na kushituliwa.
12.   Gear box – kazi ya chombo hiki ni kubadilisha gea na kufanya gari liwe na mwendo  wa kasi zaidi au kupunguza kasi
13.   Differential – kazi ya chombo hiki ni kugawa mwendo unaotoka kwenye injini na kuupeleka kwenye matairi
14.   Cut Out – Kazi ya cut Out ni kufanya Marekebisho ya umeme kutoka kwenye Altarnator na kwa kipimo cha volt 12 kiingiacho kwenye betri.
SIFA ZA DEREVA.
·         Ni lazima ajue Sheria za barabarani na kanuni zake na kuzifuata
·         Anatakiwa asiwe mlevi wa Pombe au vilevi vya aina nyingine
·         Anatakiwa kuwa mtu wa kulikagua gari lake mara kwa mara
·         Awe mtu wa kuwajali watumiaji  wengine wa barabara
·         Asiendeshe kwa mwendo kasi wa kupita kawaida
·         Ni lazima uwe mtu wa kujihami
·         Ni muhimu unaposikia usingizi au kuchoka usiendeshe gari
·         Asiwe mtu wa mazungumzo yaliyokithiri kwenye gari au wakati wa kuendesha
·         Awe mpole na mwenye huruma
·         Asitumie viburudisho wakati anaendesha
·         Unapopigiwa simu ya mkononi ni muhimu kupark pembeni ndipo uipokee.
Ufahamu kuhusu injini.
Injini ni chombo au mashine ambayo hubadilisha nguvu ya joto (Heat energy) na kuwa nguvu ya mwendo (Mechanical Energy) kwa ujumla injini ina sehemu kuu tatu zifuatazo;-
·         Cylinder Head; Ni sehemu ambayo huwa upande wa juu wa injini
·         Engine block; Ni sehemu ya katikati ya injini ambayo sehemu kubwa ni chuma
·         Coil Samp; Ni sehemu ambayo huwa inakaa chini ya injini, hii ni sehemu ambayoOil ya  injini  inakaa.
Spring;
Kwa kawaida spring katika magari huwa ni za aina kuu mbili
·         Spring Bar – Hizi ni spiring za kawaida ambazo huwa ni vipande bapa vya chuma
·         Coil spring – Hizi huwa zimepindana kwa kwenda juu zimejikunjwa mfano wa dawa ya mbu ya kuchoma.
Grease;
Ni mafuta mazito ambayo kwa kawaida hutumika kupunguza kulika kwa vyuma yaani kupunguza msuguano “Friction” kwa kawaida Grease hupakwa sehemu yoyote ambapo chuma hukutana na chuma kingine

Unapotaka kuzima gari kumbuka;
·         Unapokuwa kwenye gia tahadhari usiachie clutch kwani kuna uwezekano likazima ghafla,kwa hiyo zima ukiwa umakanyaga clutch na brake halafu badilisha gia nambari moja, vuta hand brake kisha achia Clutch, halafu achia Brake na mwisho ondoa ufunguo.
·         Au ukitaka kuachia clutch kwaajili ya kuzima unachofanya ni kuweka gia huru free ndio uachie clutch, kanyaga tena clutch na badili gia kuwa Nombari moja, vuta hand brake na endelea kama hapo juu.



Pichani baadhi ya vifaa vya gari kama vinavyoonekana Picha kwa hisani ya Rev. Kamote home Bible Library. October 24, 2010.

UFAHAMU KUHUSU BIMA ZA MAGARI NA TARATIBU ZAKE.
Kwa kawaida sheria inaagiza kuwa magari yote ni lazima yawe yamekatiwa Bima na kinyume cha hayo utakuwa umevunja sheria ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Lakini ni muhimu kufahamu kuhusu bima
Zipo aina kuu mbili za Bima
1.       Third Party
Bima hii ni bima ambayo haitoi malipo gari linapokuwa limepata ajali , Bima hii hueleweka kama bima ndogo, iwapo utapata ajali kati ya gari mbili atakayelipwa ni mwenzako kama iwapo yeye anayo bima inayofanana na yako, iwapo atakuwa na bima ambayo ni kubwa utalipwa kutokana na bima yake.
2.       Comprihensive
Bima hii ni bima kubwa ambayo inakuwezesha kulipwa iwapo gari yako itapata ajali iwayoyote na kwa kawaida utaratibu ufuatao huwa unafuatwa.
a.       Dereva awe na umri unaostahili kuwa dereva au kufanya kazi hiyo ya udereva
b.      Leseni aliyokuwa nayo dereva kabla ya kupata ajali ni daraja linalostahili kuendesha gari hilo
c.       Leseni ya  Derevahuyo lazima iwe halali na ameipata kwa kufuata utaratibu wa kisheria, kinyume cha hayo Bima haiatalipwa wala haita husika  na hasara itokanayo na ajali hiyo kabla ya kupata ajali ni daraja
Iwapo katika gari yako kuna redio ni muhimu kuikatia Bima yap eke yake ili uweze kulipwa iwapo ajali itaharibu Redio hiyo.
UTARATIBU WA KUWASHA NA KUENDESHA GARI.
Unapomaliza kucheki gari yako unaingia ndani ya gari na kuiweka free gari au gea , halafu unaweka switch on na kuangalia taa ya heater, ikilazimika unawasha gari na baada ya hapo unaweka gea nambari moja  kasha unaachia clutch kidogo kidogo na utaona gari linaondoka utaangalia gari mpaka lizungushe  tairi raundi moja au zaidi halafu utaachia clutch kabisa.
Gari linapokuwa barabarani unatakiwa uwe macho na kusoma alama za barabarani na uwe mwangalifu usitoe macho tu unatakiwa kuwa makini kwa kila alama za barabarani.
Unapofika njia panda au keepleft
Hakikisha kwanza unasimama  unaagalia kulia kwako kama kuna mwenye gari anakuja na ameshafika unampisha  apite  na ambaye alikwisha kuingia kwenye mzunguko, halafu unawasha indicator na kuonyesha mwelekeo wa kule unakokwenda, utawasha ya kushoto kama unaingia njia ya kwanza.



Njia panda au keep left.
Kanuni za njia panda ua keep left.
·         Unapaswa kusimama na kuangalia kulia kwako kama gari imeshafika unaipisha ipite hususani ile ambayo imeshaingia kwenye mzunguko
·         Hakikisha kuwa unapiga indicator ya kulia  endapo hutaingia njia ya kwanza utabadilisha indicator ya kuonyesha mwelekeo wa kuelekea unakokwenda
·        
   50
   50
   50
   50
Unawasha indicator ya kushoto kama utaingia kwa njia ya kwanza


- Kibao cha namba moja kimekataza usiende spidi zaidi ya spidi hamsini
- Kibao cha namba mbili kimeruhusu kwamba unaweza kwenda zaidi ya spidi hamsini
- Kibao cha namba tatu kimekataza kwenda zaidi ya spidi hamsini
- Kibao cha namba nne kimeruhusu kwenda zaidi ya spidi hamsini.









Kanuni ya njia mbili Double Road kama hakuna keepleft  unapaswa kubana upande wako  kama umeshafika sehemu ya upande wako wa kuchepukia wa kule unakokwenda

Kama kuna keep left utapaswa kwenda kama keep lefti za kawaida .






Kama kuna barabara kuu na njia panda unabana upande wako wa kushoto ambao ndio sauti yako halafu unaelekea utakako.


                         



1.       Barabara hii uendeshaji wake ni sawasawa na uendeshaji wa barabara za kawaida za double road , kwenye uendeshaji unapofika kwenye kuchepuka unabana upande wako ambao utaingia
2.       Barabara nyngine  hazina barabara kuu wala ndogo ,ukubwa wa barabara  unategemea  taa ya kuongoza magari inapowaka
3.       Kisha barabara hii ina ukubwa sana kuliko ile ya double road ya kawaida.
4.       Iwapo barabara hii inauwezo wa ku-ovaertake pande zote ukiona hakuna hatari.
5.       Halafu bara bara hii inayoongozwa na taa inasema hivi;-
a.       Taa nyekundu inazuia magari yasipite
b.      Taa ya njano inasema ujiandae na kuondoka
c.       Taa ya kijani inaruhusu kuondoka
d.      Taa yam shale wa kijani inanukuu kuondoka kwenda mshale unakoelekeza hata kama taa nyingine zinawak
Rangi nyekundu maana yake simama subiri nyuma ya mstari buliochorwa hapa chini ya bara bara
Nyekundu na njano pamoja maana yake ni kusimama usipite mpaka rangi ya kijani imetokea
Rangi ya kijani maana yake unaweza kupita lakini njia ikiwa ni salama na pia ni muhimu kufanya tahadhari kwa watembea kwa miguu hususani unapokuwa unageukia kulia au kushoto
 
Mshale wa kijani maana yake unaweza kwenda upande ulioelekezwa na mshale huo na unaweza kufanya hivyo  haizuru hizo taa nyingine zinaonyesha nini
Rangi ya manjano maana yake simama nyuma ya mstari ulioko hapo chini, unaweza kwenda  ikiwa labda imekutokea iwapo ulikwisha kupita huo  mstari uliopo hapo chini hivyo au labda ulikuwa karibu sana.
MASWALI YA KUJIULIZA KWA DEREVA (MASWALI YA MDOKO).
1.       Wakati unaendesha gari ikatokea imewaka moto utafanyaje?
2.       Unapopata ajali utafanyaje?
3.       Ni vitu gani vya kuangalia kabla ya kuendesha gari?
4.       Eleza namna ya kugeuza gari katika barabara kuu
5.       Ni wakati gani unaporuhusiwa kuipita gari iliyoko mbele zako?
6.       Elezea umuhimu wa kukagua gari yako kabla ya kuondoka
7.       Kuna hajka gani wakati wa kupinda kona kubadilisha gea?
8.       Ni vitu gani vinavyotumia barabara
9.       Ishara za barabara zina faida gani?
10.   Taja sehemu nne ambazo ni makosa kuegesha gari
11.   Taja sehemu tatu ambazo ni marufuku kupiga honi
12.   Unatakiwa kusimama umbali gani nyuma ya gari lililosimama?
13.   Unatakiwa kuwa umbali kiasi gani toka gari linalokwenda mbele yako?
14.   Utamjulisha vipi Dereva wa gari lilioko mbele yako kuwa unataka kulipita wakati wa usiku?
15.   Taja mambo manne unayotakiwa kujihadharisha unapoendesha gari
16.   Utajuaje kama unaingia mjini au unatoka mjini kwenda nje ya mji?
17.   Ni mwendo kiasi gani unatakiwa kuendeesha unapokuwa nje ya mji?
18.   Taja sifa anazotakiwa kuwa nazo Dereva?
19.   Unatakiwa ufdanye nini kabla ya kupinda kulia?
20.   Ni gari la upande gani lenye haki ya kupita kwenye kona au mzunguko?
21.   Utafanaya nini kama unataka kupinda kulia iwapo kuna gari linalokuja mbele yako ?
22.   Taja vyeti unavyotakiwa kuwa navyo unapoendesha gari
23.   Ni mambo gani yanaweza kusababisha ajali taja matatu
24.   Utafanya nini Kama gari litazima ukiwa mlimani?
25.   Utaangalia nini kabla ya kuondoa gari lako?
26.   Alama ya mstari mweupe ulionyooka barabarani inakuonyesha nini?
27.   Alama ya mstari mweupe ulioachana achana unakuonyesha nini?
28.   Utafanya nini kablaya kufika mahali unapotaka kupinda?
29.   Utafanya nini unapopita mahali penye shule pasipo na alama ya kivuko cha watoto wa shule?
30.   Ni wakati gani unapotumia kioo cha kuangaliua nyuma unapoendesha gari?.
31.   Unapaswa kufanya nini unapoendesha gari wakati wa usiku?
32.   Elezea jinsi taa za magari zinavyofanya kazi?
33.   Utafanya nini iwapo gari lako limeharibika barabarani?
34.   Ni ishara gani utaiona kama mtu mashuhuri anapita na utafanya nini?
35.   Mahali gani unapaswa kuwapisha waendao kwa miguu?
36.   Utafanya nini kama unasikia usingizi unapoendesha gari?
37.   Ni sehemu gari za viungo zinatakiwa kuwa katika hali nzuri kabla ya kupata lesseni?
MASWALI KWA MADEREVA WA MAGARI YA ABIRIA:
1.       Ukiwa dereva unatakiwa uwe na tabia gani kwa abiria?
2.       Je dereva wa abiria anatakiwa kuvuta sigara katika gari anapoendesha kwa nini?
3.       Unapaswa ufanye nini ukiwa dereva wa gari la abiria wasafiri wanapopanda ndani ya gari?
4.       Utampa taarifa gani askari iwapo atakusimamamisha na kukuhoji?
5.       Kama gari yako inashukiwa kuwa ni mbovu na kukamatwa na askari utafanya nini?
6.       Je ukiwa ni dereva wa gari la abiria  unaruhusiwa kuzungungumza na mtu yoyote kwa nini?
7.       Utaegesha vipi gari kama abiria wanataka kuteremka?
8.       Kabla hujaendesha gari la abiria unatakiwa ufanye nini?
9.       Utahakikishaje kuwa abiria wote wamekaa sehemu zao kabla ya kuondoka ?
10.   Ni vitu gani visivyoruhusiwa kupakiwa katika gari la abiria?
11.   Vitu gani vinatakiwa kuwemo katika gari kwa tahadhari ya ajali au moto?
12.   Unatakiwa kwenda mwendo gani mjini na mwendo gani nje ya mji/
13.   Kila abiria anaruhusiwa kuchukua mzigo au uzito gani
14.   Kuna hatari gani iwapo gari litazidisha mzigo?
15.   Ipo haja ya kukimbizana ili uwahi abiria? Hatari zake ni zipi?
16.   Je abiria ana haki ya kutoa ushauri anapoona mambo yananyofanywa si sawa?
MASWALI KWA MADEREVA WA MAGARI YA MIZIGO.
1.       Gari linalobeba mizigo au mafuta lazima liwe na vifaa gani?
2.       Gari linalobeba vifaa vya hatari kama baruti, sumu na gas linatakiwa kuwasha taa ndogo?
3.       Je ni wakati gani unapotakiwa/Kuruhusiwa kuendesha gari lenye vifaa vya hatari?
4.       Kabla ya kuendesha gari lenye vitu vya hatari unapaswa kuangalia nini?
5.       Iwapo gari lako limeharibika katikati ya barabara unapaswa ufanye nini?
6.       Sheria inasema nini juu ya utumiaji wa taa ndogo au ni wakati gani unatakiwa kuwasha taa ndogo
7.       Abiria wanagapi wanaoruhusiwa kupakia katika gari la mizigo?
8.       Ni barabara gani utakalopitisha gari la mizigo mjini
9.       Ni sehemu gani za muhimu za gari zinazotakiwa kuwa madhubuti kwa kubeba mizigo?
10.   Eleza jinsi unavyotumia taa za gari lako usiku kama kuna gari nyingine inakuja mbele yako?
11.   Ishara gani utaitumia unapolipita au kupishana na gari lingine?
12.   Utafanya nini iwapo utakutana na gari lingine karibu ya daraja?
13.   Utatoaje ishara ya kusimama?
TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA;
1.       Endesha kistaarabu.
Ada ya mja kunena , Muungwana ni kitendo, Basi kama ni hivyo onyesha uungwana wako kwa kuendesha kistaarabu barabaraniUwe mpole na uwafikirie watumia barabara wenzako, uwe mvumilivu, mtulivu, usiwe na papara lazima uwajali watu na madereva wengine  unapoendesha barabarani.
2.       Fikiri kabla ya kuteenda.
Fikiri sana kabla ya kuamua, uwe na uhakika na kila hatua ya utekelezaji , usije ukadhani kuwa ni kosa lako tu linaloweza kuleta hatari barabarani, Hapana uwe tayari pia kuayamaliza na kuyaepuka makosa ya watumiaji wengine wa barabara
3.       Mkono  dirishani.
Unapoendesha au kuendeshwa usitoe mkono dirishani na kuuacha hapo hapo katika hali ya kupumzika  huku kisukusuku au kiwiko cha mkono kikiwa kimejitokeza nje ya dirisha
4.       Watoto ,Vilema na wasiojiweza.
Ni muhimu kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya watoto wadogo , vilema na ndugu wasiojiweza, hususani unapokuwa barabarani, hao wanahitaji huruma zako, moyo , msaada na uelewa wako wa dhati.
5.       Ishara alama na michoro ya barabarani.
Zijue ishara zinazotumika barabarani, jifunza zielewe ,uzimudu na kuziheshimu alama na michoro yote ya barabarani.
6.       Michezo Barabarani.
Wafundishe watoto namna ya kuziheshimu barabara na hasa namna ya kuzivuka  kwa usalama , uiswaruhusu watoto kucheza barabarani au karibu na barabara, Aidha usiwaruhusu watoto wadogo kuvuka barabara wakiwa peke yao bila kuongozwa.
7.       Dereva akiwa kazini;
Lazima abiria ajizuie kumyumbisha dereva mawazo yake  akiwa kazini,usibishane  naye wala kupiga gumzo naye wala kuimba kupiga kelele au kumshitusha na au kufanya kitendo chochote kile kitakachoathiri mawazo yake anapoedesha.
8.       Takataka.
Usitupe vipande vya sigara au takataka zozote barabarani
WAENDAJI BARABARANI.
a).  Kutembea.
1. Kutembea barabarani;
Kila mara tembea kwenye kijinjia cha waendaji  kwa miguu kama kipo, kama hakipo tembea nje ya barabara ili au ukingoni mwake  upande wa kulia mwa barabara ili uyaone kwa urahisi  magari yanayokuja mbele yako, ukifanya hivyo utapata nafasi kubwa ya kuyakwepa magari yanayojongea  uliko.
2. Kutembea na mtoto;
Usimwachie mtoto aende kwa imani yake mwenyewe, mshike kwa mkono wako wa kulia na utembee kati yake na barabara  upande wa magari.
3. Maandamano ya watu;
Kundi la watu linapofanya maandamano barabarani lipite upande wa kushoto  wa barabara , wawepo watu wa kutahadharisha usalama  na kuwatahadharisha watumia bvarabara wengine .
4.Kuzuia njia ;
Usiwazuie wenzako kwa kusimama katikati ya njia ya waendao kwa miguu kwa sababu yoyote ile.
5. Kuzurula barabarani;
Usisimame, kuzubaa kuzurula au kutangatanga  barabarani hasa kwenye kona  na sehemu yoyote  pofu au sehemu nyingine yeyote ya barabara ambapo dereva hawezi kukuona kwa urahisi.
6.       Kuelekea barabarani;
Uwe mwangalifu sana utapoelekea kwenye Barabara, angalia kwa makini kuhakikisha kuwa hakuna gari linalojongea upande uliko kaa chonjo.
Kuvuka Barabara;
1.       Kuvuka barabara ;
Kabla ya kuvuka barabara simama kwenye  ukingo  wa barabara kwanza halafu angalia kulia , kushoto , halafu kulia tena  kama hakuna gari vuka moja kwa moja mpaka ukingo wa pili usivuke kimshazari.
2.       Barabara kwenya gema au kisiwa;
Kama barabara ina gema katikati simama hapo kwanza baada ya kuvuka nusu ya kwanza ya barabara, hakikisha kuwa madereva wa upande wa pili wa barabara wamekuona hasa kama kuna giza.
3.       Kuvuka kwa kukurupuka ;
Usivuke barabara kama mwizi au mwenda wazimu na hasa usivuke mahali pengine popote kama kivuko cha waendao kwa miguu kipo karibu.
4.       Kuvuka kwenye kiyuo cha magari;
Usivuke barabara kwenye kituo cha kupandia au kuteremshia abiaria na hasa mbele au nyuma ya gari, abiria anapoingia au kutoka kwenye gari.
Kivuko cha pundamilia
1.       Kivuko cha punda milia
Hiki ni kivuko cha waendao kwa miguu. Usivuke kituo hicho mpaka umehakikisha kuwa abiria wamekuona na wapo tayari kukupisha , unapovuka  pepesa macho kulia kushoto na kulia tena , kama tahadhari kwa madereva ambao inawezekana  wameshindwa kusimama, chukua tahadhari wakati wote.
2.       Kivuko chenyae kisiwa
Kuna vivuko vingine vya watembeaji kwa miguu vyenye visiwa katikati ya barabara , endapo kisiwa kipo katikati ya kivuko cha punda milia , vuka kila nusu ya kivuko hicho kama kivuko kamili kinachojitegemea.
Vivuko Vinavyoongozwa.
1.       Vuvuko vinavyoongozwa na taa.
Unapovuka mahali panapoongozwa na taa fanya hivyo tu taa ya kuvuka ikiwaka
2.       Kivuko kinachoongozwa na askari.
Endapo Askari wa kuongoza magari haya yupo ni muhimu kuvuka barabara  tu askari akikutolea  ishara .
Kupanda na kuteremka.
1.       Kupanda na kuteremka kwenye gari;
Usidandie gari wala kuning’inia. Aidha usipande wala kushuka kwenye gari likiwa bado kwenye Msururu wa magari ngojea hadi litakaposimama na kuegeshwa pazuri au kwenye kituo kilichoidhinishwa.
2.       Kuingia na kutoka kwenye gari.
Hakikisha kuwa unaingia  na kutokea upande wa kushoto wa gari,ikiwa mlango wa kutokea uko kulia , basi hakikisha usalama wako  kwa kuangalia kulia na kushoto na ukitoka usivuke barabara mara moja.
Usiku, vizuizi na Mkokoteni.
1.       Matembezi ya usiku.
Unapotembea usiku;
Unapotembea usiku au kwenye giza , haklikisha kuwa umevaa nguo nyeupe  au zinazoonekana kwa urahisi gizani au shika kitu kinachong’aa, hali hii ni muhimu zaidi kwa  barabara za vijijini.
2.       Kuvuka vihunzi.
Usivuke vihunzi au vizuizi vyovyote vilivyojengeka , Pembeni mwa barabara ,unapotaka kuvuka.
3.       Mikokoteni.
Wenye mikokoteni pia hawana budi kuziheshimu sheria na kanuni zote za barabarani, sukuma mkokoteni pembeni kabisa mwa upande wa kushoto wa Barabara , toa ishara shii au kuvuka kwenye njia panda,
KWA MADEREVA WOTE;
Afya , usalama wako na wa gari;
1.       Afya ya dereva.
Usiendeshe gari isipokuwa kama una uhakika  wa afya  yako ya mwili na akili yako , Ni lazima mwili wako na fikira zako ziwe katika mtiririko mmoja ili kusababisha hali ya usalama barabarani, ulevi wa pombe , madawa ya kulevya  na uchovu huathiri uwezo wa kufikiri kwa makini , kupanga , kuangalia na kuamua sawia.
2.       Hali ya gari.
Hakikisha kuwa  gari lako lipo katika hali nzuri kabla ya kuliweka Barabarani, ukaguzi wa marakwa mara wa Breki, usukani, magurudumu na indiketa  ni wa lazima , Aidha  hakikisha kuwa kioo cha mbele ni kisafi na vipanguso  na Wepa  navyo vinafanya kazi kila wakati.
3.       Ubebaji Mizigo.
Usipakie au kubeba gari lako mizigo mingi na mizito kupita kiasi kinachokubalika kwa wastani.
4.       Shehena kubwa.
Ukipakia mzigo au shehena na ulio zagaa au kujipenyeza pembeni au nyuma  unatakiwa kuwa mwanagalifu sana  kwa mwendo. Na ni lazima  pia kuweka alama za kuwaonya  watumiaji wengine wa barabara kwa kufunga kitambaa chekundu, kama ni mchana au taa nyekundu kama ni usiku.
5.       Kofia ya usalama.
Ni vizuri kuvaa kofia ya Usalama kwaajili ya  kujikinga kichwa dhidi ya ajali ya kugongwa kichwa , kila unapoendesha chombo cha moto kama pikipiki n.k.
MADEREVA WAPYA NA MANJU;
Usikimbilie kuendesha gari subiri na kuhakikisha kuwa unafundishwa na mkufunzi aliye taalamika  na aliyelimbikiza ujuzi na uzoefu wa kutosha. Usianze kwa papara utaishia pabaya. kumbuka daima kuwa kuliendesha gari ni kitu rahisi sana  na karibu kila mytu anaweza kama akitaka  na akaweza katika siku chache tu . Kinachofanya mafunzo yawe ni kitu muhimu  na cha lazima  ni haja ya kujifunza mbinu mbalimbali za kuthibiti barabara , mazingira  na gari lenyewe, ni vizuri kujifunza  kuanzia hatuia za awali, Tabia njema  katika udereva  ili hatimaye  ujuzi na uzoefu wako ujengwe juu ya msingi imara itakayokusaidia  kuziepuka ajali za barabarani kwa urahisi zaidi. Ili uweze kuwa dereva  bora  mwenye msimamo wa usalama  barabarani, huna budi kuanza tangu mapema  kujifunza na kuyazingatia kati ya  mambo mengi  muhimu yafuatayo;
1.       Kuzijua kanuni
Ni lazima  uujue Udereva katika mapana na marefu yake uzijue uzikariri na kuzizingatia sheria na kanuni zote za usalama barabarani kujua huko kuambatane na makusudi ya kuzitekeleza kanuni hizo ipasavyo.
2.       Uwe dereva wa kujihami;
Ni vema ikumbukwe kuwa hata Dereva bora, anayejulikana kwa ustadi wake anaweza akasababishwa na watumiaji barabara wengine na akapata ajali.Falsafa ya dereva wa kujihami inaelekeza kuwa dereva asiridhike na kujua kwake sheria na kuzitekeleza kanuni tu, wala asifikiri kuwa madereva na watumiaji barabara wengine wote wanazijua na wataziheshimu sheria ipasavyo.Ni lazima aendeshe huku akiwa tayari kufidia na kurekebisha makosa yaw engine kwa sahihi za kuepusha shari na kuleta hali ya maelewano na usalama barabarani.
3.        usalama barabarani;
Dereva wa kujihami, kamwe haendeshi kwa kuwakomoa wanaofanya makosa barabarani.Udereva wa kujihami ni udereva wa kutumia akili.
4.        heshima kwa wengine;
Ni wajibu kwa dereva kuonyesha uungwana na kumheshimu kila mtumiaji barabara.Mwenye gari ndogo au kubwa,pikipiki, baisk eli , mkokoteni,n.k mpishe mwenye haraka au shida kila inapobidi, hata kama wewe ndiye mwenye haki  ya njia.
5.       ajali za barabarani;
Jitahidi kufahamu kuwa, ajali za barabarani hazitokei tu, bali husababishwa.Mara nyingi hutokea ikiwa ajizi imefanywa dhidi ya misingi hiyo, jizoeze na jizatiti kuibaini ukiwa barabarani.
6.       lijue gari lako;
Jitahidi na uwe na dhamira ya kuliijua gari lako lilivyoundwa.Ijue mitambo iliyopo ndani ya gari, viungo vyake na sehemu nyingine nyeti,zikiwa ni pamoja na maguridumu. Hali hii itakuweaesha kuwa na staha ya aina Fulani kabla hujaamua kwenda kasi Fulani na kuzuia uwezekano wa ajali hasa zile zenye asili ya kifundi.
UDEREVA WA KUJIHAMI;
Kila siku madereva wote hupambana na hatari ambazo haziwezi zikamhakikishia dereva usalama wake na wa gari wakati wote.Hatari hizo zinahusiana na hali ya gari, tabia na hulka ya waenda kwa miguu na hali ya barabara yenyewe.Lakini tofauti ya elimu,tabia hulka na ujuzi wa madereva wanapokuwa barabarani humpa mtihani mgumu sana Dereva bora na stadi.Azma ya usalama barabarani,imejengwa juu ya mategemeo ya kuwa na dereva wa kujihami, ambaye atahakikisha usalama barabarani,imefengwa juu ya mategemeo yakuwa na dereva wa kujihami, ambaye atahakikisha usalama barabarani wakati wote.
Dereva wa kujihami (tazama maana yake hapo juu Ibara Na.2)
Ni mtaalam wa medani za barabarani na anazo mbinu kadhaa anazozitumia katika kukwepa hatari na kujiokoa yeye gari lake na watumiaji barabara. Kwa jumla dereva wa kujihami huzingatia mambo matatu kabla hali haijamshinda, nayo ni;
a.             Hutambua hatari-uwezo wake wa kuhisi na kutambuahatari kubwa.Haendeshi kwa kudhani au k Udhani au kubahatisha, bali kwa kuwa na uhakika. Zing’amue hatari mapema na amua kuziepa hatari na  na vikwazo vya barabarani.
b.      Huelewa mbinu za uzuiaji-atajitahidi kuepuka hatari ama kuzuia janga kutokea.Jifunze mbinu mbali mbali na uzitumie kwa wakati ufaao au zinapohitajika.
c.       Huchukuahatua –huendesha kwa kujikiri mbele zaidi na akinusa tatizo huamua kutekeleza mara moja. Usingoje yatokee, epusha shari, wala usidhani kuwa atasimama yeye.Simama wewe.
TAHADHARI KWA JUMLA;
Watoto wadogo na hata wale wanaokwenda shule wamo hatarini zaidi kuliko watu wazima.
Walindeni na wafundisheni juu ya usalama barabarani.Wazee na wakongwe  nao ni wagumu kuwaza na kumaliza kasi ya mwendo wa vyombo vya moto vinavyowajengea wafikirieni hao pia.
Kumbukeni hali ya afya zao, udhaifu wa macho yao, uzito wa kutembea kwao.
Waendeshaji wa vyombo nao wajione kuwa wazima wa afya kabla ya kuendesha.Aidha magari yanayoendeshwa barabarani yawe mazima, katika hali nzuri na yakaguliwe mara kwa mara ili yasisababishe ajali za barabarani.Taa,breki ,usukani, magurudumu na viungo, vingine vithibitishwe kuwa vipo katika hali nzuri.
LESENI;
Leseni ni hali ya kisheria inaokuruhusu mhusika kuthibiti au kuendesha vyombo vya moto katika darafa lililoonyeshwa  katika leseni.Kwa hiyo pamoja na kuwa na leseni bado dereva anawajibika kujua mbinu mbalimbali za uzuiaji na kujifunza, kuzikariri na kuzizingatia kanuni na sheria mbalimbali za usalama barabarani.
Aidha ni vema ikumbukwe nia yautahini wa udereva ni kuhakikisha kuwa, mtahiniwa anazifahamu sheria za udereva bora na kwemba amefundishwa vya kutosha, amefanya mazoea ya sheria kiasi cha kuinukia kuwa dereva bora ambaye siyo hatari kwakebinafsi na kwa watumiaje barabara wengine.
STAHILI YA LESENI.
Chini ya miaka 16-Hapati leseni kabisa.
Miaka 18 hadi 20-Leseni za pikipiki na magari madogo na gari za biashara.Lakini siyo magari ya abiria wala yale makubwa ya mizigo.Miaka 21 na zaidi –Leseni za pikipiki gari ndogo magari makubwa ya mizigo nay a abiria.
KUMBUKUMBU
Mwombaji wa leseni za kuendesha  magari ya abiria au magari makubwa ya abiria analazimika kwanza kupata cheti cha kuthibitisha uzima wa macho yake kutoka kwa Daktari.
USALAMA WA GARI;
Usalama wa gari unahusu yafuatayo;
i.                Kuibiwa au kuharibiwa kwa gari.
ii.                   Kuibiwa kwa baadhi ya vifaa vilivyo sehemu ya gari hilo
iii.                  Na wizi unaokuwa ndani ya gari hilo.
 MAMBO YA KUZINGATIA;
1.       Usiache swichi ndani ya gari lako na ufunge usukani unapotoka nje au kuegesha.
2.       Funga gari lako unapokuwa hulitumii k.m ukiliegesha.
3.       Funga vioo na milango kila unapoegesha au kutoka. Usiache nafasi yoyote.
4.       Ondoa vitu vyote vyenye thamani au vifungie kwenye buti japo utakuwa umefunga milango na madirisha.
5.       Vioo vyote viandikwe namba ya gari.
6.       Hakikisha namba ya gari lako limewekewa bima.
7.       Tunza vizuri hati ya gari yako.kama hati ya kusajiliwa.Bima pamoja na anwani (jina)la udereva.Hivi vinaweza kumwezesha mwizi kuuza gari lako kwa urahisi zaidi.
8.       Watu wanaotiliwa mashaka kutokana na tabia zao wasipewe leseni.
9.       Tegeshea mtambo wa kuzuia wezi kama gari linao kama huna unaweza kuuweka.
10.   Weka kumbukumbu namba za vitu vya gari lako , kama radio na kadhalika
11.   Jihadhari na watu wanaoonekana kuwa na nia mbaya na gari lako , ikiwezekana jihami kwa kutoa taarifa polisi
12.   Funga tenki la mafuta kwa kifuniko imara ili wezi wasiyaibe au kuyaongeza  mafuta katika gari lako linapokuwa limeibiwa au kuporwa.
13.   Usiwaache watoto au watu wasiojiweza kwenye gari lililofungwa au lisiloingiza hewa
14.   Usiku egesha gari lako gereji au sehemu yenye mwanga wa kutosha utakaokuwezesha  kuwaona wezi kwa urahisi zaidi, lifunge vizuri.
15.   Tafakari juu ya usalama wa gari lako na usalama wako mwenyewe kabla hujatoka kwenye gari lako.
DARAJA ZA LESSEN.

Daraja la A; Pikipiki za aina zote
Daraja la B; Magari ya aina zote isipokuwa ya Biashara ya Mizigo naya abiria
Daraja la C; Aina zote za magari Tazama kumbuka hapo juu na mizigo
Daraja la D: Aina zote za magari sipokuwa magari ya mizigo na Abiria
Daraja la E: Aina zote za magari isipokuwa ya abiria
Daraja la F: Magari ya shughuli za ujenzi
Daraja la G: Magari ya katika shughuli za migodi na mashamba

MATAYARISHO YA UTAHINI:
Baada ya kujifunza vema Udereva, kuzijua na kuzitafakari sheria, ukiambatana na mazoezi mazito chini ya mkufunzi wa udereva, hatua ifuatayo ni ile ya kwenda polisi kutahiniwa.
Uko kwenye kituo cha utahini  mtahiniwa atawajibika kumthibitishia mtahini  kuwa anao uwezo wa kukiendesha chombo kwa uhakika na bila kubabaisha , Aidha amthibitishie  mtahini kuwa anazijua  sheria na kanuni zote za usalama barabarani.
Katika kuelekea huko kwenye kituo cha utahini mtahiniwa ajiandae na maswala yafuatayo.
a.       Lessen ya Muda (Provisional)
b.      Gari sahii kwa adaraja la lessen unayoiombea na gari liwe zima  lenye bima  na lessen  hai ya njia
c.       Stakabadhi ya ada ya utahini kutoka katika ofisi ya serikali ya mapato (Revenue). Na ada yoyote nyingine kama ipo
d.      Chunga muda na kituo ulichopangiwa kwa utahini kwani ukichelewa utahini utaahirishwa.  

UTAHINI;
Kumbuka daima kuwa baadhi ya mambo ambayo mtahiniwa anatakiwa kuyathibitisha katika majaribio au utahini ni kama yafuatayo;-
i.                      Umahiri wa kuliongoza gari katika barabara ya kawaida  na katika misururu ya magari mengine
ii.                   Umahiri wa kuyapita magari mengine, utumiaji wa aina mbalimbali za barabara na namna ya kutawala kasi ya mwendo.
iii.                  Umahiri wa kona na uendeshaji wa kurudi kinyumenyume.
iv.                 Uendeshaji wa  magari ya aina mbalimbali
v.                   Alama ya michoro ya barabarani pamoja na sheria  na kanuni za usalama Barabarani
Onyo kwa wanaotaka kujifunza udereva.
1.       Hakikisha kuwa unafundishwa na mkufunzi aliyetaalamika vya kutosha katika fani ya udereva.
2.       Usikubali kufundishwa na dereva anayeendesha kwa kubahatisha na mwenye kuleta mbwembwe njiani au asiyestaarabika.
3.       Usikubali kufundishwa kwenye mkweche wa gari yaani gari lisilokuwa katika hali nzuri.
Kumbuka kuendesha gari si kitendo rahisi sana ,Lakini suala siyo mradi kuendesha bali muhimu ni kujifunza mbinu mbalimbali  zitakazokuepusha na uwezekanao wa majanga uwapo barabarani.
UDEREVA BORA;
Dereva bora yeyote Yule lazima awe amepitia mafunzo ya udereva kikamilifu kutoka kwa mkufunzi aliyetaalamika vilivyo na mwenye ujuzi wa kutosha.
a.       Dereva bora ni lazima kwanza ajihusishe na  gari lake ipasavyo, katika azima hiyo ni lazima azingatie yafuatayo;-
1.       Kagua gari lako na hasa chunguza magurudumu, honi, milango, maji,mafuta ,taa zote pamoja na  za ishara  hii iwe tabia yako.
2.       Rekebisha chochote kibovu kabla ya kuendesha kwa mfano kiti cha kukalia, vioo, milango n.k.
3.       Jaribu breki zako kama zinafaa na uwe na tabia ya kufanya hivyo kabla ya kuendesha wakati wote.
4.       Uondokapo uhakikishe kuwa hakuna vizuizi mbele , nyuma na hata chini ya mvungu wa gari.
5.       Uendeshe tu ukiwa na uhakika na iwapo mgonjwa jizuie sana kuendesha gari.
b.      Kadhalika dereva  bora hana budi  kuzingatia kanuni zifuatazo kwa usalama wake  na watumiaji wengine wa barabara , baadhi yake ni;-
1.       Tuliza akili na fikira zako.
2.       Jifunze zikariri na uziheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani.
3.       Mwili na fikira zako barabarani ziwe kitu kimoja
4.       Fikiria kwanza kabla ya kutenda
5.       Jizoeze kujizuia  na uwe mwanagalifu sana barabarani
6.       Uwe mwanagalifu na mwepesi kabla ya kufanya uamuzi
7.       Uwe na ujuzi na uzoefu wa kutosha wa gari lako
8.       Uangalifu zaidi unahitajika unapoendesha gari mpya au ambayo sio yako.
9.       Endesha kwa akili, nenda kwa kasi mahali panapohitajika  na panapo faa kwa wakati unaofaa tu kumbuka  kuwa mjinga yeyote anaweza akaenda kasi  na akapata ajali.
10.   Tumia honi kwa akili na toa ishara zinazoeleweka tu.
11.   Uwe mwenye heshima na adabu kwa watumiaji wa barabara wote.
12.   Usiendeshe gari bovu aslani.
c.        Endesha kwa staha ;
1.       Kumbuka daima kuwa mjinga yeyote anaweza kuiwasha gari , akaiendesha akaigeuza  lakini kwa dereva bora huwajibika kwa hayo tu.
2.       Endesha kwa juhudi, maarifa na uangalifu ili kuepusha ajali, unapoelekea  kwenye njia panda , kipingamizi chochote au mzunguko keep left au kupita kwenye maeneo ya shule, hospitali na mahali popote  hatari na ni muhimu kukumbuka yafuatayo;-
I.                    Nenda kwa kasi ya kawaida itakayokuwezesha kusimama ikitokea hatari.
II.                  Toa ishara (Indicator) mapoema ili wenzako wajue makusudio yako.
III.                Jua namna ya kuzitumia barabara za aina mbalimbali kwa usalama na bila kujihatarisha mwenyewe au kuhatarisha wengine.
Kadhalika unaweza kuepukana na ajali za barabarani ukizingatia vipengele vifuatavyo;-
a.       Zijue hatari zinazokukabili barabarani, unapoelekea au ukifika kwenye hatari angalia kioo chako kwanza.
b.      Utoe ishara sahii kuwajulisha wengine unachotegemea kufanya.
c.       Punguza mwendo kabla hujapiga breki , na tazama kioo tena.
d.      Panga gia sahii, pita kwa uangalifu.
e.      Rekebisha kasi ya mwendo wako kwa kuchunguza kasi ya mwendo wa magarai mengine
f.        Kama kuna watumiaji wengine wa barabara wengine barabarani basi waonye kwa ustadi.
g.       Ukiisha kuipita hatari yoyote ile ondoka upesi hapo kwenye sehemu hatari.
Kwa maelezo zaidi ya upitaji salama kwenye sehemu za hatari  kama kwenye  njia panda  soma amelekezo   kwenye kitabu cha medani za barabarani cha H.B. Bantu ukurasa wa 37 hadi 42.
Dereva anbapaswa kuliweka gari kwenye msimamo au mkao mzuri  wa barabarani  anapoendesha gari lake kwa kasi  ya mwendo wa staha na akione kipingamizi chochote barabarani  kama watu , mawe, n.k, apunguze mwendo na kuwa tayari kusimama
Ukiwa unaendesha swala la uangalifu ni muhimu sana siku zote .Tumia macho yako wakati wote, Usilipite gari linguine (Overtake) sehemu
a.       Yenye kona
b.      Yenye mlima
c.       Yenye kivuko cha punda milia au kwenye kivuko cha Reli
d.      Kwenye njia panda
e.      Kwenye daraja
f.        Kwenye barabara nyembamba.
Ukifanya ajizi utapata ajali na kuhatarisha maisha yako nay a wengine aidha ni vema ukumbuke tena kuwa;-
a.       Uwe makini barabarani usiondoe macho yako barabarani
b.       Kila mara pepesa macho kwenye kioo
c.       Kila mara waone watumiaji wengine wa barabara kama chanzo cha ajali hivyo chgunga mienendo yao.
d.      Penye gari lililo simama mbele yako chunguza  kwa makini kama kuna anayevuka barabara
e.      Chunga sana watoto na wazee, wanaweza kuvuka barabara bila ya kuchukua tahadhari
f.        Unapoyapita  magari yaliyo pembeni  mwa barabara  yapite kwa uangalifu sana
g.        Usihisi tu kuwa dereva mwengine atakupa hali ya njia au kukuruhusu upite Subiri mpaka afanye hivyo.
h.      Usiendelee na mwendo kama  huoni mbele
i.         Pita kushoto Keep left unapoendesha gari bana upande wa kushoto wa barabara ispipokuwa unapolipita gari linguine.
j.        Kulipita gari linguine Overtake kunaweza kufanyika unapokuwa umahakikisha kuwa ni salama kufanya hivyo na kuwa upeo wako wa mchoni mkubwa na hakuna msururu wa magari au magari yanayongojea.
k.       Nenda polepole kama huoni mbele  sawasawa au huna uhakika  na hali ya barabara  na unapopitwa na magari mengine  punguza mwendo  na jitayarishe kusimama kila inapobidi.
l.         Jihadhari na kutaka kuwahi kwani kunaweza kusababisha kuyavuka magari mengine na utajilazimisha kukatisha barabara kwa nia ya kuyawahi magari mengine jambo ambalo linaweza kukusababishia usiyawahi.
m.    Kubadili njia kwenye barabara ya njia nyingine, usibadili kutoka njia moja kwenda njia nyingine  bila uangalifu , angalia kioo , toa ishara chunguza kwa macho.
UNAPOENDESHA INAKUPASA.
Inakupasa uwe katika nafasi ambayo inakuwezesha kutumia na kuongoza  gari lako ambavyo unaweza kuona sawasawa , barabara mbele na magari mengine n.k. Umpe heshima yule ambeye yuko katika kivuko  cha kuvukia barabra kwa miguu.
Angalia sheria za barabara na ishara (Traffic Signs) Simama ukitakiwa  na Ofisa wa Polisi kufanya hivyo, angalia ngalia kama taa zako ndogo na za pembeni zinawaka wakati wa usiku, haikupasi kuendesha bila tahadhari kwa mwendo ambao unaweza kuhatarisha  watu, ukisimama inakulazimu kuzima injini  na breki kabla ya kuacha gari, zima taa kunwa  za mbele wakati wa usiku lakini hakikisha kuwa taa ndogo zote  za nyuma na mbele zinawaka , Ikitakiwa na Polisi onyesha lessen yako ya kuendesha na cheti cha bima Insurance kwa ukaguzi.
Inawezekana kuvitoa popote kwenye kituo chochote cha pilisi unachopendaHaikulazimishi kuendesha gari lako unapokaribia kivuko cha watembea kwa miguu , kusimamisha moto wa gari  linalokokotwa na gari linguine penye “on waiting” yaani hakuna kungoja  palipokatazwa kusimama au kusimamisha magari, kupiga honi gari likisimama . aidha sheria inataka upatikanapo na hatari yoyote ambayo ni hasara au jeraha kwa mtu yeyote au gari  nyingine  au mnyama ni lazima kusimama na saidia kama kuna mtu aliyeumia na eleza ripoti polisi bila subira, Kwa madereva wa pikipiki skuta na waendeshaji wa  baiskeli baada ya mengi yanayotakiwa katika sheria zinazohusu madereva wa magari pamoja na zile zinazohusu  vivuko vya waenda kwa miguu pia zuinakuhusu , haikulazimu kuchukua watu zaidi ya mmoja kwa mshine ya miguu miwili  na abiria kuketi  kwa kutambaza miguu juu  anatakiwa ake sawa ashikwe sawa sawa.

Maoni 93 :

Unknown alisema ...

nimefurahia maelezo yako yanaeleweka

Unknown alisema ...

maelezo mazuri sana

Unknown alisema ...

nimejifunza kitu kizuri sana ila picha za dash board na za sehemu mbali zagari na ingini haionekani vizuri

Unknown alisema ...

nice

Unknown alisema ...

naam kiasi chake inafaa

Unknown alisema ...

naam kiasi chake inafaa

Emmanuel Lusula alisema ...

Nimependa sana kujifunza na kuelewa baadhi ya vitu ndani ya Maandalizi ya kuwpo mwanafunzi wa awali wa Udereva

Unknown alisema ...

Nimehamasika na hii kurasa. Nimejifunza mengi sana. Nawapa hongera kwa wale wote waliochangia kuunda huu ukurasa

Unknown alisema ...

alie fanya hii kazi mungu ambariki nimejifunza mengi nashukur sana

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima alisema ...

Asante Sana Maiko Ngalesoni mi ni Mchungaji niliweka tu taaluma hii ili kuwasaidia watu wemgi

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima alisema ...

Asante sana Macha Baraka Jina la Bwana libarikiwe

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima alisema ...

Thanks Charles Killenga

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima alisema ...

asante sana Mr. Emmanuel Edward

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima alisema ...

Amen nakushukuru jina la bwana libarikiwe

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima alisema ...

Asante sana

Unknown alisema ...

naomba kujua ni ishara gani natakiwa kuionyesha ninapotaka kuingia njia kuU (MAIN LOAD)

Gold alisema ...

Nimeipenda sana hiyo elimu ya kukijua chombo cha moto.

Gold alisema ...

Nimeipenda sana hiyo elimu ya kukijua chombo cha moto.

Gold alisema ...

Gold silver

Gold alisema ...

Nimeipenda sana hiyo elimu ya kukijua chombo cha moto.

Unknown alisema ...

Duuuu mungu azidi kukupa nguvu utuwezeshe wengi kuyafahamu haya mweeee

Unknown alisema ...

Sijawa kuendesha gari ila kwa muongozo huu umenifungua baadhi ya mambo.

Unknown alisema ...

nashukuru sana kwa aliye fanya kazi njema uliyofanya mungu akubark

Unknown alisema ...

Mungu akubariki sana Kaka yetu, nimefarijika sana kwa kupata ufahamu huu kuhusu maswala ya udereva. Mungu akubariki sana, na kama nikipata namba yako nitafurahi zaidi Brooh.

Unknown alisema ...

nameupenda ukurasa huu

Unknown alisema ...

Mungu akubariki sana

Unknown alisema ...

Kweli ukurasa huu nimejifunza mengi mno mungu akupe miaka mingi uendelee kutujuza zaidi

Unknown alisema ...

Saidi juma

Unknown alisema ...

Saidi juma

Unknown alisema ...

Naomba ungejibu na mwswali uliobyaacha

Unknown alisema ...

Umenifunza mengii japo kuna maswari nimeshindwa kuyajibuu ungetujibia namaswarii ingependezaa zaidii kujua jibu sahihi.

Unknown alisema ...

Safi sana, ubarikiwe na Mungu

Paulo group alisema ...

Nimejifunz kitu hapo

Unknown alisema ...

Ramadhani msamzi

Unknown alisema ...

Naitaj kujiunga

Unknown alisema ...

Good

Unknown alisema ...

Good

Namwa alisema ...

Yaani hapa ni shule tosha endelea kutoa elimu watu wengi wataelimika

Unknown alisema ...

Nmejifunza vitu vingi sana kupitia ukurasa huu

Unknown alisema ...

Vicent

OnaZote.com alisema ...

Mliki wa OnaZote.com nimependezwa na somo hili

Dainamo classic _-_mazoea mp3 alisema ...

Asante kwamaerezo mazuri

Unknown alisema ...

Kuna makundi mangapi ya askali barabrani

Unknown alisema ...

Kuna makundi mangapi ya askali barabrani

Unknown alisema ...

Kuna makundi mangapi ya askali barabrani

Unknown alisema ...

Nzuri sana imenisaidia baba mchungaji

Unknown alisema ...

Nimeupenda sana huu ukurasa muandaaji mungu ampe nguvu

Unknown alisema ...

Ni nzui kwakila dereva

Unknown alisema ...

Hili somo ni zuri sana kwa dereva yyt yule

Unknown alisema ...

Nimejifunza kitu hapa

Unknown alisema ...

Kwakusoma haya nimejua gari

Unknown alisema ...

Ahsa te

Unknown alisema ...

Asante

Unknown alisema ...

Ahsante kwa somo lako.

Unknown alisema ...

Nice lecture thanks

Unknown alisema ...

Iko poa sana umetusaidia wemgi

Unknown alisema ...

Namna ya kutumia H na L mkuu

Unknown alisema ...

Vincent sprian

Unknown alisema ...

Naomba kujiunga na mafunzo

Unknown alisema ...

Naomba kujiunga na mafunzo ya uendeshaji

Unknown alisema ...

Asante sana kwa maekekezo

Unknown alisema ...

Nimependa sana hii elimu, natarajia kuwa dereva na nimegain mambo mengi muhimu kutoka kwako. Ahsante Sana.

Unknown alisema ...

Asante sana nimepata uelewa mkubwa sana mungu akubariki

Unknown alisema ...

Somo zuri sana

Unknown alisema ...

Asante na mungu akutie nguvu mwandishi kiukwel imenisaidia sana

Unknown alisema ...

Ahsante

JOSEPH Shao alisema ...

Ahsante sana, nitapataje pdf

Revocatus alisema ...

Hiyo ni nzur

Unknown alisema ...

Mafundisho mazuri, tunashukuru Sana.

Changamoto tu ni kuwa michoro na baadhi ya alama hazionekani ila umegusa vitu vingi vya Msingi.

Kirui Kiprono alisema ...

hii shule iko wpi

Unknown alisema ...

Uko vzr mkuu

Unknown alisema ...

Nimekuelewa vizuli lakini ada shingapi ya udeleva wa magali ya mizigo

Unknown alisema ...

Nimeelewa vizuri Sana
Mungu akubariki kwa kutupa somo hili

Unknown alisema ...

Nashukuru nimeelewa zaid

Unknown alisema ...

Ubarikiwe sana kwa somo zuri ndugu

Unknown alisema ...

Nimependa Sana

Unknown alisema ...

Nimeelewa Sana mubarikiwe.

Kirui Kiprono alisema ...

Leonard

Unknown alisema ...

Nimefulahi Sana Kuna kitu nimejifunza ahsante Sana

Unknown alisema ...

Nimeipenda xana

Unknown alisema ...

Dah! nimejifunza niliyokuw siyajui so nimefurahi sana

Bila jina alisema ...

Vizur san

Bila jina alisema ...

Vizur san

Bila jina alisema ...

Thanks aki tumejifunza 2cioyajua endelea ku2pa elimu ndugu

Bila jina alisema ...

Chuo cha udereva wa maroli makubwa kwa dar es salama kinapatikana wapi

Bila jina alisema ...

Naitaji kujifunza, kuendesha gar ndogo au yoyot mawasiliano 0621091274

Bila jina alisema ...

Taa za barabara

Bila jina alisema ...

Safi sana

Bila jina alisema ...

Uko vzuri sana teacher

Bila jina alisema ...

Nashukuru teacher uko vizur sana na nimekuerewa vizur2

Bila jina alisema ...

Vizuri sana kwa posti nzuri hakika nimejifunza kitu

Bila jina alisema ...

Mungu akubariki sana Mtumishi,, nimejifunza mengi sana kuhusu gari kupitia huu ukurasa.

Bila jina alisema ...

Ubarikiwe....ilipotoa Mungu akuzidishie zaidi