Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 25 Desemba 2020

Upendo mwingi!

Yoahan 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.”



Utangulizi:

Moja ya maagizo ya mwisho kabisa ya Yesu Kristo kwa wanafunzi wake kabla ya kuteswa, kufa na kufufuka ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wake wanakuwa na upendo, wote tunafahamu kuhusu kupenda, lakini Yesu hakutaka tu tuwe tunapenda lakini alitaka wawe na upendo mwingi sana, unaweza kujiuliza upendo mwingi ni upendo wa namna gani? Biblia nyingine za Kiswahili zinatumia neno upendo mkuu, biblia ya kiingereza inatumia neno “The Great love” ambalo ka Kiswahili ni Upendo mwingi au upendo mkuu! Kwanini Yesu anazungumzia upendo mwingi kwani kuna upendo kidogo au mchache ndio kuna upendo kamili “Perfect Love au “sacrificial love” na upendo mwingine wenye upungufu!

Katika Lugha ya kiyunani neno upendo linaelezewa vizuri, sana kwa kuzingatia maeneo manne

1.       Phileo – Huu ni upendo au uhusiano wa kirafiki, unampenda mtu kwa sababu ni rafiki yako mahusiano yenu ni ya kirafiki, upendo huu una mipaka, kwa sababu unaweza kufa unaweza kuharibika ndio maana unaweza kuona watu wanafarakana na wanaweza hata kusalitiana na urafiki ukageuka kuwa uadui mkubwa

2.       Storge – Huu ni Upendo au uhusiano wa kindugu, unampenda mtu kwa sababu ni ndugu yako, mna uhusiano wa damu, uhusiano wa kubaiolojia ni babam ni mama, ni mama mdogo ni baba mdogo, ni binamu, ni shangazi, ni babu, ni bibi na kadhalika upendo huu pia una mipaka na unaweza kuharibika na ndugu wakageuka kuwa maadui wakubwa sana

3.       Eros – Huu ni upendo au uhusiano wa kimapenzi, ni upendo wa asili ya kibinadamu ambao mvutio wake unatokana na mapenzi, so unaweza kumpenda mtu kwa sababu ana usio mzuri, hana malolo, Yakobo alimpenda Raheli kuliko Leah kwa sababu Lea alikuwa na macho dhaifu alikuwa na malolo, unaweza kumpenda mtu kwa sababu ana makalio makubwa, mazito, hips za kutikisa dunia, ana chuchu zilizosimama, saa sita ni mkwaju wa nguvu umbo namba nane, potable au ana mzigo mzito wa kitikisa dunia na kadhalika huu ni upedno wenye hisia za kimapenzi

4.       Agape – Upendo huu sasa ndio unaoitwa upendo mwingi, ni upendo wenye kujitoa sacrificial love , upendo huu ni mgumu kuwa nao, ni watu wachahce sana wanaweza kuwa na upendo kama huu, Yesu aliuita upendo huu kuwa ni upendo mkuu, ni upendo mwingi, unahusisha kupenda mpaka kuyatia maisha yako kwaajili yaw engine Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele upendo huu mtu akiwa nao ndio tunasema amekomaa kiroho, ni upendo ambao una sifa za kipekee 1Wakoritho 15:1-13Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana. Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.”

 

Ukomavu wetu wa juu sana Kiroho utajulikana pale tunapokuwa tayari kuyatoa maisha yetu kwaajili ya wengine 

 

Yuda - Mwanzo 44:1-34,·  Alikuwa mwenye upendo mwingi sana alikuwa tayari kufa kwaajili ya kuitunza familia yake na baba yake na kwaajili ya ndugu zake

Daudi - 2Samuel 18:31-33·   alikuwa na upendo mwingi kiasi ambacho alilia kwaajili ya Absalom mwanaye japokuwa yeye alikuwa amekusudia kumuua baba yake

 

Yesu Kristo Yohana 15:13:- “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake· kwa ajili ya rafiki zake”.

 

1. Daktari mmoja wa Uingereza aitwaye Will Pooley alikuwa ni moja ya madaktari waliokuwa mstari wa mbele Nchini “Sierra Leone” huko walikuwa na wenzake wengi wakipambana na wagonjwa wa EBOLA na virusi vyake katika harakati hizo Madaktari wengi sana na Manesi wengi sana wakiwemo wa Afrika Magharibi waliambukizwa virusi vya ebola wakati walipokuwa wakiwauguza wagonjwa na wengi wao walikufa Ugonjwa utokanao na kirusi cha Ebola ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90. Shirika la afya duniani, WHO katikatovuti yake inasema kwa mara ya kwanza ulibainika mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan. Chanzo cha kirusi hiki hadi sasa hakijulikani lakini popo aina ya (Pteropodidae) wanaonekana kuwa wabebaji wa kirusi hicho, kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa. Maambukizi hupatikana kwa kila aina ya majimaji yanayotoka katika mwili wa binadamu ni ugonjwa hatari na unaoua kwa haraka na hauna tiba Will Pooley alipoupata ugonjwa huu alirejeshwa katika ndege maalumu na kuanza kutibiwa chini ya uangalizi maalumu huko uingereza Jambo la kushangaza ni kuwa baada ya kupona kwa bahati tu Will Pooley alitangaza nia yake ya kurudi tena Sierra Leone kusaidiana na wenzake kupambana na ugonjwa huo. Mtu huyu aliwashangaza wengi sana na kuwaogopedha wengi sana akiwa amepona kwa asilimia 100%alisema atarudi Africa kusaidia zaidi maana alizaliwa kwaajili ya hayo, jambo hili lilimfanya aandikwe kama shujaa na mwanadamu mwenye uwezo wa kujitoa kwa kiwango cha juu.

 

2. Maximilian Kolbe alikuwa ni Padre aliyetokea Poland aliuawa kama mfungwa tarehe 14 August 14,1941, Jeshi la wa NAZI waligundua kuwa baadhi ya wafungwa wamejaribu kutoroka na hivyo waliamua kuwaua wafungwa kadhaa, walijaribu kuwaua kwa njia mbalimbali, na hivyo walichagua wafungwa 10 ili wauawe na kifo chao kiliamuriwa kuwa kifo cha njaa, wafungwa waliamuriwa kujitoa mmoja mmoja yeye mwenyewe na mfungwa wa kwanza kuchaguliwa alijulikana kama Franciszek Gajowinczek mfungwa huyu alipochaguliwa alilia kwa huzuni kubwa akimtaja mkewe, watoto wake na familia yake na kusikitika kuwa hatowaona tena kutokana na swala hili Maximillian alisimama na kusogea mbele na kuomba afe yeye kwa niaba ya Franciszek ombi lake lilikubaliwa, wafungwa waliwekwa kizuizini kwa muda wa siku kadhaa bila kula wengine walikunywa mikojo yao ili waweze kuishi, Maximillian alikaa kwa wiki mbili bila kufa huku wengine wote wakiwa wamekufa, walimchoma sindano ya kufa hakufa na hivyo waliamua kukata kichwa Pope John Paul II alimtangaza kuwa Mtakatifu kutokana na moyo wake

 

3. Mifano hii inatusaidia kujua kile ambacho Bwana wetu Yesu amekifanya Pale alipojibu kuwa kwaajili ya haya Nalizaliwa alikuwa akimkumbusha Pilato kuwa yeye amekuja kuwafia wanadamu, amekuja kuwaonyesha upendo wa Mungu jinsi ulivyo Isaya 53:1-5 “Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Huu ni upendo mkubwa sana Yesu alikufa kwaajili yetu, Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunasimama upande wake siku zote za maisha yetu, tusihesabu damu yake ya thamani kuwa kitu cha hovyo tudumu katika wokovu na kuwa wavumilivu kwaajili ya Mungu wetu.”

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumanne, 26 Januari 2016

Ufahamu Kuhusu Ufunuo Wa Yohana


Maana ya Neno Ufunuo
Neno Ufunuo kwa kiingereza ni Reveletion au Disclosure au Apokalupsis kwa kiyunani Apokalupsis  Maana yake ni Mungu kujiweka wazi, au kujifunua kupitia uumbaji wake, Historia, Dhamiri ya mwanadamu na Maandiko kwa msingi huo linapotumiwa katika maandiko hutumiwa kwa maana mbalimbali tofauti na hakuna maana maalumu, Maneno makuu mawili ya kiyunani hutumika katika Biblia yaani Apokalupsis na Faneroun fanerou'n  ambalo maana yake ni yaliyo juu ya uweza wa kibinadamu, au yaliyo zaidi ya kufunuliwa, ni kupitia maneno haya makuu mawili ndio tunapata maana ya neno Ufunuo ambao kwa maneno ya kufupisha tunaweza kusema ni kuwekwa wazi kwa Maswala ambayo mwanzoni yalikuwa hayajawekwa wazi.
Kitheolojia ufunuo unaweza kuzungumziwa katika maana kuu mbili ufunuo wa Mungu wa Ujumla General or Naturral Reveletion na Special Reveletion. Ufunuo wa ujumla wa Mungu ni ushahidi wa kuweko kwa Mungu kwa wanadamu wote waliojuu ya uso wa Inchi kupitia uumbaji, Historia na dhamiri ya mwanadamu. Jambo hili linaweza kuthibitishwa na Maandiko kama Zaburi ya 19;1 Mbingu zahubiri utukufu wa Mungu na anga latangaza kazi ya mikono yake, Matendo 14;8-18,17:16-34, Warumi 1;18-32,2;12-16 na mistari mingine mingi. Dhana hii inakubalika na baadhi ya wakatoliki na waprotestant kwamba ni ya ufunuo wa ujumla ambao unamthibitishia mwanadamu kuwa Mungu yuko bila kuhusisha maswala ya imani bali kwa kujihoji Reasoning, wakati ufunuo maalum ni ule unaotokana na msaada wa Mungu ambao hupatikana kwa imani na uzoefu tu kupitia maneno ya Mungu. Ufunuo huo wa ujumla hauna msaada katika kumuwezesha mwanadamu kuokoka lakini kumfanya asiwe na udhuru kuwa hakuna Mungu.
Kwa ujumla ufunuo wa asili au ufunuo wa ujumla umejengwa katika misingi ya jumla ya kuthibitisha tu kuwa Mungu yupo lakini ni ufunuo usiotosheleza kwa habari ya kuleta wokovu lakini angalau unaweza kumsaidia mwanadamu kuwa na ufahamu huo kwa kuanzia, inasemekana kuwa hata wale wanaofikia hatua hii kwa namna Fulani wanajua hayo kupitia imani ingawaje eneo kubwa ni kwa kutumia akili, wakati dhana ya Ufunuo unaotokana na Mungu inajifunua kupitia Historia ya matukio ya kweli ya wokovu na ufunuo utokanao na ujuzi halali wa maandiko.

Baadhi ya wasomi huamii kuwa ufunuo Haufanani wala hauko sawa wakati wote na wanaamini kuwa hata Biblia yenyewe ni Matokeo ya ufunuo na ni nukuu za mafuno kwa watu waliokuwa wakijaribu kumtafuta Mungu na wakajaribu kumuelezea kwa ufahamu wao kupitia kazi za namna alivyojifunua kwa hiyo wao huamini kuwa ufunuo  hutokea wakati Mungu anapojifunua yeye mwenyewe kwa mtu na mtu huyo anapoitikia mwitikio wa Imani katika Kristo kwa hiyo Biblia kwao ni kiongozi tu wa uzoefu huo wa kimafunuo lakini yenyewe sio ufunuo kamili.
Maana ya ufunuo kwa Mtazamo wa Kibiblia.
Hatima ya ufunuo wa aina yoyote ile Bado ni makusudi ya Mungu kutuleta kwake ili tupate kumfahamu yeye, Mungu kujifunua kwa mwanadamu hakutegemeani na mfumo au kanuni maalumu au mfumo Fulani wa kimafundisho msingi wa kwanza ni mtu Binafsi kukutana na Mungu na hivyo kibiblia hata kukutana na kumfahamu Mungu wa kweli ni ufunuo hii ni kwa sababu .
§  Mwanadamu kuwa na ujinga wa kutokumfahamu Mungu ni sawa na Ujinga wa kutokujifahamu yeye mwenyewe hivyo kama mtu hamjui Mungu hawezi kujijua yeye mwenyewe.
§  Mwanadamu ana hatia anayotembea nayo inayomuhukumu kuwa amemkosea Mungu na hivyo ufunuo wa kweli katika kristo sio tu unampa maarifa bali unamkamilisha katika utakatifu na rehema na msamaha wa Mungu
Ufunuo wa Kibiblia ni ufunuo wa Mungu na matendo yake ya kweli kihistoria, Mungu alikamilisha mpango wake wa kumuokoa mwanadamu na mpango huo ulikamilishwa katika Yesu Kristo. Kwa msingi huo Hakuna Yesu Kristo wa Imani tu Lakini Pia tunaye Yesu Kristo wa Historia kwa hiyo “hakuna imani katika Kristo kama hakuna Kristo katika Historia”, Kwa hiyo Historia ya Kibiblia ni historia ya kile ambacho Mungu amesema na kutenda Mika 6;5 na Kristo ndiye ukamilifu wa Historia.
Agano la kale ni ufunuo uliokuwa unategemea kuja kwa Yesu Kristo na Agano jipya ni ufunuo unaoakisi na kuthibitisha ukweli wa ujio wa kristo. Kwa msingi huo kufanyika mwili kwa Bwana Yesu ndio ufunuo kamili wa Mungu na ndio kiini cha Injili Warumi 1;3,16, 1Wakoritho 15;1-4, Wagalatia 4;4, Waebrania 1;1,2, Ni wazi kuwa Mungu alijifunua kwa wanadamu kuhusu mpango huo wa wokovu kwa njia nyingi na kwa namna mbalimbali Waebrania 1;1-2 kwa hiyo ingawa ufunuo wa Mungu umekuja katika mwana wake kwa ukamilifu lakini Mungu alijifunua kwa njia mbalimbali kwa hiyo uko ukweli kuwa Mungu amejifunua pia kwa wanadamu kwa njia ya uumbaji, Historia na dhamiri ya mwanadamu yaani ufunuo wa jumla.
Ufunuo wa Kibiblia maana yeke ni ufunuo katika neno lake ni mkusanyiko wa matendo ya Mungu aliyoyatenda na kusema akiwasiliana na wanadamu katika njia maalumu na ujumbe wa agano jipya ni tafasiri ya matendo yake ufunuo huo wote wa agano la kale na agano jipya umefungwa katika tukio kuu la Ukombozi wa mwanadamu, Paulo anaonyesha kuwa Hata agano la kale lilikuwa likizungumzia tukio hilo la ukombozi wa mwanadamu 1Koritho 15;3-4 ni wazi kuwa wakati huu alipokuwa akinukuu maneno kama yanenavyo maandiko alikuwa akimaanisha Agano la kale kwamba nalo lilikuwa linaona kwa mbali ukombozi ukikamilisha katika kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu kwa hiyo Historia ya wokovu Kerygma katika agano jipya ni muendelezo wa kazi ya ufunuo ulioanza katika agano la kale hivyo neno la Mungu ni ufunuo wa wokovu kwa maana ya agano la kale na agano jipya.
Kwa msingi huo Ufunuo wote wa matukio yaliyopita, yaliyopo na yajayo yanakamilishwa katika tukio moja la Kufufuka kwa Bwana Yesu na hivyo Mungu amajifunua kwa msingi wa maswala yajayo kwa kiwango cha juu katika kristo na kwa mujibu wa Waebrania 1;2 kufanyika Mwili kwa Kristo kunakamilisha maswala ya ufunuo wa tulikotoka tuliko na tuendako ufunuo huo sasa unakuja kwa wanadamu kupitia neno lake yaani Biblia kwa hiyo Biblia sio tu muelekeo wa Ufunuo lakini yenyewe ni Ufunuo kamili
Ili ufunuo uweze kueleweka unapaswa kueleweka kwa kupitia kweli kuu Tatu
§  Mfunuaji ambaye kwa uwazi ni Mungu
§  Njia ya ufunuo ambayo ni maandiko na katika maandiko haya tunaambiwa kuwa Mungu alijifunua kwa Njia mbalimbali ambazo ni maono, Ndoto, usingizi mzito, Urim na thumim, kura, Muonekano wake mwenyewe akijidhihirisha theophanies, kupitia malaika, mazungumzo ya kiungu, historia na matukio na neno la Mungu au Kristo Yesu mwenyewe.
§  Mwisho Mpokeaji yaani mwanadamu ambaye amejiweka katika utayari wa kupokea na kushuhudia
Biblia hata hivyo ni matokeo matukio ya ufunuo wa Mungu ambapo anadhihirisha mpango wake wa ukombozi wa mwanadamu kupitia Yesu Kristo Katika neno Mungu anawasiliana na mwanadamu aliyeanguka ingawa uwazi kabisa wa ufunuo huo huja kwa muitikio wa imani wa kazi zilizofanyika lakini mwitikio huo hauwi wa aina binaamu mwenyewe kwa matakwa yake bali ni kazi kamili ya zawadi na msaada wa Roho Mtakatifu kazi hiyo ya ndani ya moyo wa mwanadamu inayompa uwezo wa kupokea ufunuo huo huitwa illumination au Estimoium kwamba mtu anaweza kukulia katika maandiko na kufunzwa katika maandiko lakini neno la Mungu likawa halijafunuliwa kwake 1Samuel 3;7 kwa hiyo ingawa Mungu alizungumza na Samuel zaidi ya mara tatu lakini halikuwa neno la Mungu kwake ni mpaka mara ya nne ndipo Samuel alipoweza kuelewa na neno la Mungu likawa neno la Mungu kwake, Ni mpaka mtu awe na uwezo wa kusikia na kupokea  kwa moyo ndipo kweli ya Mungu inapokuwa yake 1Thesalonike 2;13.
Mamlaka kubwa ya maandiko inatokana na kuvuviwa kwake na hivyo lafaa kwa mafundisho, kwa konya na kusahihisha na kutoa mafunzo ili kuwakamilisha watu wa Mungu 2Timotheo 3;16-17 kwa hiyo Biblia ni ya kimungu au ni ya Mungu kwaasili ingawa Mungu aliwatumia wanadamu kuiandika na waliandika ujumbe kamili kutoka kwa Mungu lakini uelewa kamili wa uvuvio huo lazima upokelewe katika mtazamo sahii wa Ufunuo kwa msingi huo awaye yote anayeisoma Biblia anapaswa kujua kwanza msomaji alikuwa anakusudia nini kwa wasomaji wake wakati huo, kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa mtu anapoisoma Biblia kwanza anapaswa kusikiliza baada ya kuelewa ujumbe uliokuwa ukizungumzwa na ujumbe kwa asili ulihusu nini ndipo unapaswa kujiuliza jinsi ujumbe huo unavyomuhusu kwa wakati alionao lakini hii ni hatua ya pili.
Ufunuo ni lazima utofautishe na maswala mawili Uvuvio (Inspiration) na kuangaziwa (illumination). Ufunuo ni mawasiliano ya taarifa kutoka kwa Mungu kumjia mwanadamu aliye katika hali ya anguko ili ajue kile ambacho Mungu anakisema au anakifanya kwaajili yake, Uvuvio unahusika na swala la Roho wa Mungu kuwatumia wanadamu kuandika kwa mamlaka yale aliyokusudia wanadamu wawe nayo katika neno lake, lakini ingawa maandiko yote yamevuviwa sio maandiko yote ni ufunuo ila tunaweza kuzungumza kwa ujumla wake tu kuwa maandiko ni ufunuo kamili wa Mungu kwaajili ya kuwasaidia wanadamu kumjua na kwaajili ya utukufu wa Mungu.
Kuangaziwa yani illumination ni kazi ya Roho Mtakatifu kumuwezesha msomaji wa neno la Mungu kuwa na uwezo wa kuelewa maandiko akisaidiwa na Roho Mtakatifu 1Koritho 2; 13-14 kwa hiyo katika ufunuo Mungu anafunua kweli zilizokuwa zimejificha lakini katika kuangaziwa iilumination aliyeamini anawezeshwa kuelewa. Kwa hiyo Ufunuo ni Namna alivyowasilisha, Uvuvio ni jinsi alivyowasilisha na kuangaziwa ni kwanini aliwasilisha hii inakuja kwa msaada wa Roho wa Mungu.


KITABU CHA UFUNUO WA YOHANA 
Neno ufunuo kama tulivyogusia awali ni neno linalotokana na lugha ya asili ya Kiyunani Apokavluyi  yaani Apocalypse ambalo maana yake ni Kuweka wazi au kufunua kwa msingi huo kitabu hiki kiliitwa The Apocalypse of John na sawa na neno hilo la Kiswahili Ufuno wa Yohana, hiki ni kitabu cha Mwisho katika mfululizo wa Vitabu vya Agano jipya, ni kitabu cha kipekee sana ukilinganisha na Vitabu vingine kwa ujumla, pekee katika Agano jipya ndio kitabu ambacho kinafanana kwa nguvu na Vitabu vya unabii kama Ezekiel, Daniel na Zekaria na kama ilivyo kwa Vitabu hivyo mwandishi alikuwa na kundi la watu waliokuwa wakizungukwa na mateso na dhiki, Ufunuo ulikuwa ni waraka kwa wakristo wa nyakati za karne ya kwanza, wakati wakristo wakiwa wametengana na dini ya kiyahudi na wakiwa wanatambuliwa kama kundi linalojitegemea kwa Serikali ya Kirumi.kwa hivyo kitabu cha ufunuo ni kitabu cha maswala yaliyokuweko na zaidi sana maswala yajayo it is an escatological book.

UFAHAMU KUHUSU KITABU CHA UFUNUO.

1.       Ufahamu kuhusu Historia ya kitabu cha ufunuo
§  Historia
§  Jamii
§  Dini
2.       Umoja
§  Mwandishi
§  Tarehe ya uandishi
§  Mahali
§  Makusudi
§  Muda
§  Malengo
3.       Kupitishwa kwenye kanuni
§  Kutambuliwa kwa kitabu cha Ufunuo.
§  Msimamo wa kanisa la Magharibi.
§  Msimamo wa kanisa la Mashariki.
§  Kukubalika kwa ujumla.
§  Jinsi ya kutafasiri litabu cha Ufunuo.
§  Theolojia katika kitabu cha Ufunuo.
§  Mgawanyo kamili.

Ufahamu kuhusu Historia ya kitabu cha ufunuo
Historia.
Mazingira ya Kitabu cha ufunuo yanachukua eneo la utawala wa Rumi ya zamani katika jimbo la Asia  ndogo  Asia minor, kulikuwa na uzushi wa kila aina ambao ulikuwa umefunika mazingira hayo pamoja na imani Potofu na Kanisa lilikuwa linapitia changamoto za Udunia na theolojia za kidunia kuingia katika imani, Ibada za sanamu, lakini pia kulikuwa na mafanikio makubwa sana ya kiuchumi, kulikuwa na majengo makubwa ya Miungu, waabudu, na watengenezaji wakubwa wa sanamu, utoaji wa sadaka kwa miungu, pamoja na hayo watawala wakubwa kama Nero (AD 54-68) na Domitian (AD 81-96) walikuwa waefikia kiwango kikubwa cha madai ya kutaka kuabudiwa na hivyo kuharibu aina nyingine za imani, Wakristo walikuwa wakikataa kuabudu wanadamu jambo lilolosukuma kuingia katika mateso na kudhalilishwa kwa hali ya juu kutokana na imani yao.
Jamii.
Msukumo wa dini hizi jamii na aina ya siasa na matukio tofauti tofauti yalisukuma na kuzalisha kanisa la kikristo kuwa na maamuzi magumu, na ili kanisa liendelee kuweko na kujitambua au kutambulika kama kanisa liliamua kuwa na msimamo, Mwandishi wa kitabu cha ufunuo alikuwa ametengwa na jamii kwaajili ya Imani na haishangazi kuona maandiko yake yakifunua uharibifu mkubwa wa utawala wa kirumi, tabia zao mavazi yao na hulka ya ukahaba mavazi yao mekundu na ya rangi ya dhambarau tabia ya mauaji mfano nikamwona mwanamke amelewa kwa damu ya mashahidi wa Yesu Ufunuo 17;6 ingawa maneno ya unabii yanaweza yakahusu nyakati nyingine lakini unapata picha ya mazingira ya wakati ule na kanisa na hali zake.
Dini.
Utengano mkubwa wa Ukristo na Dini ya kiyahudi ulikuwa mpana mara baada ya anguko la Yerusalemu mwaka wa 70 AD. Wakati ule Kanisa na sinagogi la kiyahudi walianza kuwa na muelekeo tofauti Fundisho la kuhesabiwa haki kwa imani nje ya matendo ya sheria lilikuwa ni kama upanga kwa wanasheria wa kiyahudi (Orthodox Judaism) na waamini wa Kikristo na kuharibiwa kwa hekalu mwaka wa 70 kuliharibu kabisa hata uhusiano mwembamba uliokuweko kati ya wayahudi na wakristo na kuharibika kwa uhusiano na kulaumiana na kushitakiana ndiko kulikopelekea kuweko kwa lugha kama Sinagogi la shetani Ufunuo 3;9 na matokeo yalikuwa ni kuachana kabisa kwa dini hizi mbili. Ndani ya kanisa kwenyewe kulikuweko matatizo ambayo yanaakisi katika barua zile kwa makanisa yale saba ya asia ndogo. Upendo ulikuwa umepoa, mmomonyoko wa kimaadili, Mafundisho potofu ambayo yalichochewa na waalimu wa uongo, kuongezeka kwa anasa na starehe na kadhalika Ufunuo ni kitabu ambacho pia kilikuwa kinajaribu kuamsha hisia za kumpenda Bwana na kuwapa maonyo wasomaji na kuwaandaa kwa ajili ya ujio wa Yesu Kristo na Hukumu ya mwisho pia kutia moyo kuwa hatimaye Mungu atakomesha siku moja uovu na huzuni na kiburi cha ulimwengu na amani ya kweli itatawala dunia.

Umoja.
 Mwanatheolojia R.H.Charles ambaye ameandika Commentary kubwa inayohisika na maswala ya Ufunuo kwa undani sana anachangia kuwa Mwandishi alikufa alipokuwa amekamilisha kuandika ufunuo 1 - 20;-3 katika kazi yake na shughuli ya umaliziaji iliwekwa katika mfululizo wa kazi zake na mwanafunzi wake mmoja mwenye akili kwa kufuata utaratibu alioubuni kuwa utahitimisha sawia mawazo yeke. Charles anaeleza kuwa Kitabu cha ufunuo kimepangiliwa katika mfumo wa mawazo yanayobebana kwa ufasaha jambo linaloleta umoja mpangilio na mtindo unaoonyesha umoja. Maono yote kwa ujumla yamelenga katika kiti cha enzi cha Mungu kama chanzo cha maono hayo na kwa vyovyote vile inaonekana kabisa kuwa mpangilio wake unatoka katika chanzo kimoja namna mawazo yanavyojegwa na tabia ya usafi wa maono yenyewe unadhihirisha wazi kuwa muandishi alikuwa Patmo utumwani na kuwa ujenzi wa mawazo ya ndani utangulizi wa kila waraka ulioandikwa kwa makanisa yale saba unalenga katika maono yele aliyoyaona mwandishi kuhusu Kristo na namna anavyohitimisha kwa ahadi ni wazi kuwa ahadi izo zilikuwa zinalenga ule mji mtakatifu wa Mungu ambao anahitimisha nao aidha mpangilio wa matukio na hatua za hukumu kutoka moja hata nyingine utaratibu wa kufunguliwa kwa muhuri  na ufafanuzi wae toka sura ya 5-mpaka – ya 20 hata kama kuna muingiliano Fulani haviaharibu umoja wa uandishi huo wa msingi wa uhalisia kuwa kitabu hiki kina umoja na kuwa kimeandikwa na mtu mmoja.
Mwandishi.
Mwandishi najaitambulisha kamaYohana amejiita Mtumwa wa Yesu Kristo ndugu wa wote wenye kuushiriki mateso na ufalme na subira ya Kristo Ufunuo 1; 1, 9 maono anayoyawakilisha kwenye kitabu hiki alionekana kuyapokea akiwa huko Patmo ambako alipelekwa utumwani kwaajili ya Jina la Yesu au imani ya Kikristo alifahamika kwa makanisa mengi ya Asia ndogo na aliwekwa katika daraja la Manabii Ufunuo 22:6, 9, 19, huyu ndiye mwandishi aliyeandika kitabu cha Ufunuo
Simulizi za kijadi zinaeleza kuwa mwandishi ni Yohana mwana wa Zebedayo ambaye pia ni mwandishi wa injili ya Yohana na nyaraka tatu zilizoitwa kwa jina lake Mwanatheolojia
§  Justin Martyr aliyeishi AD 150 alisema hivi Ufunuo umeandikwa na mtu mmoja miongoni mwetu ambaye jina lake aliitwa Yohana mmoja wa mitume wa Yesu Kristo.
§  Irenaeus Askofu wa Lyons alithibitisha kwa nakala nyingi zilizokuwa tayari kama ushuhuda kutoka kwa watu waliomuona Yohana Uso kwa uso
§  Tertulian aliyeishi AD 200 alielezea Ufunuo kama kitabu kilichoandikwa na Yohana na alimtambua Yohana ambaye alikuwa moja wa mitume wa Bwana
§  Origen AD 225 alichangia kuwa mwandishi ni Yohana mpaka karne ya pili na ya tatu Ufunuo wa Yohana kilianza kukubaliwa na makanisa na wasomi kama huko Alexandria
§  Ufafanuzi wenye kuonyesha mlengo mkubwa kabisa wa kuwa Yohana ndiye mwandishi ulitolewa na Dionysius wa Alexandria ambaye alikubaliana na mawazo mengi ya kijadi au masimulizi ya kijadi kwamba Yohana ndiye mwandishi alisema kuwa Ufunuo unajikiri wazi kuwa Yohana ndiye mwandishi wakati injili na nyaraka zake hazifanyi hivyo alisema misamiati na muundo wa Lugha na maarifa una nguvu za kuthibitisha kuwa Yohana ndiye mwandishi ingawa wengine wanahoji kuwa kitabu hiki kiliandikwa kwa mpangilo wa grama nzuri na fasaha za kiyunani jambo linalotia shaka kama Yohana Mwebrania ndiye aliyeandika.
§  Eusebius akifuata nyayo za Dionysius alihoji mamlaka ya kitabu cha ufunuo alichangia kuwa ni kweli kuwa Injili na nyaraka za Yohana hazikuwa na majina lakini zilithibitishwa kuwa zake na wale waliomjua na kuzipokea nyaraka zile  alisema zenyewe zinabeba ushahidi kuwa ni neno la Mungu na zinashuhudia wazi kuwa ziliandikwa na mtu ambaye alimuona Yesu kwa jicho lake Yohana 1;14, 21;24, ni wazi kuwa hata kama ufunuo kinataja jina la Yohana anayedhaniwa siye mwana wa Zebedayo lakini kuna maelezo yaliyo wazi katika Ufunuo 1;2 kuwa aliyeandika alimshuhudia Yesu wazi wazi kwa kumuona. Kwa msingi huo hata kama mtindo wa uandishi unaweza usikubaliane haimaanishi kuwa basi mwandishi wa injili na zile nyaraka siye mwandishi wa Ufunuo.

§  Mabadiliko ya misamiati wa uandishi katika nyaraka na injili tofautia na ufunuo unaweza ukachangiwa na maswala kadhaa kwa nini kuna tofauti kubwa Injili imenukuu habari za Yesu na ni wazi kuwa habari za Bwana Yesu mwana wa Zebedayo aliandika akikumbuka matukio ya siku nyingi wakati Yesu alipoishi duniani tena katika mtazamo wa Kikristo wakati ufunuo kiliandikwa mwandishi akiwa katika hali ya migandamizo Stress tena mwandishi akiwa utumwani au gerezani na kumbuka alichokuwa anakiandika ni maono. Injili iliuwa ikishughulikia mazingira yaliyokuwa sahii ya amani na mwandishi alikuwa akishuhudia wazi yaani iliandikwa katika mazingira ya maisha ya kawaida, Lakini ufunuo umejaa maono, ishara vitu vigeni watu wageni, viumbe vigeni na mazingira ambayo yalizingirwa na uwepo wa kimungu, lakini pamoja na hayo bado kuna kufanana kukubwa kwa matukio ya ufuno na uandishi wa Yohana
§  Alimuita Yesu kwa namna ileile aliyozoea kumuita Neno la Mungu Yohana 1;1 Ufunuo 19;13.
§  Alimuita mwanakondoo Yohana 1;29 Ufunuo 5;6
§  Mchungaji Yohana 10;11 Ufunuo 7;17
§  Anavyomzungumzia shetani ni kwa namna ileile Yohana 8; 44, 27, 14; 30, Ufunuo 2; 10, 12; 9, 20; 2, 7, 10.
§  Kisha msisitizo wa Kifo cha Yesu Kristo Yohana 12;32 na Ufunuo 1; 5, 5; 6
Kufanana huko sio lazima kuwe sawasawa lakini kunathibitisha wazi kuwa tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa maandiko haya ya Ufunuo ni wazi kuwa ni wa Yohana mwana wa Zebedayo. ni wazi uwa kitabu hiki kiliheshimika sana na makanisa ya Asia ndogo ambayo kihistoria walimjua Yohana vema kwa hivyo hakuna shaka kuwa Mwandishi ni Yohana mwana wa Zebedayo aliyekuwa Mtume wa Bwana Yesu. na kuna uwezekano kuwa labda injili ya Yohana iliwekwa sawa kiasi Fulani na msaidizi wake aliyehitimisha mchango wa mwisho katika Yohana 21; 24-25.
Yohana mwana wa Ngurumo Mtume wa upendo
Ni wazi kuwa kulingana na mapokeo na vyanzo vyote vinavyopatikana vinathibitisha wazi kuwa Yohana alikuwa ndiye mtume pekee aliyekufa kifo cha kawaida na bila shaka kuwa huyu ndiye mwandishi wa kitabu cha ufunuo
§  Yohana huyu alikuwa ni ndugu yake na Yakobo wana wa Zebedayo, ingawa wao mara kwa mara wanatajwa pamoja  Yohana anafahamika zaidi kutokana na maandiko yake na yakobo inaeleweka wazi kuwa alikufa mapema sana mongoni mwa mitumeYeye aliitwa na Yesu toka kuwa mvuvi wa kawaida kuwa mvuvi wa watu na pamoja na nduguye waliitwa na Bwana wana wa ngurumo hii inawezekana kutokana na tabia zao za ukali Luka 9;54
§  Yeye  na ndyguye wakati Fulani walikuja na ombi la ajabu kutaka kuketi upande wa kuume na kushoto Marko 10;35-37
§  Mapema katika utumishi wa Yesu Yohana aliwakilisha shitaka la kukemewa kwa mtu aliyekuwa anatoa pepo lakini hafuatani na wao Marko 9;38 ni wazi kuwa Kristo aliwakemea mara kwa mara katika makosa yao hayo yote
§  Kwaajili ya unyenyekevu uliojengeka baadaye ni wazi kuwa ilikuwa mara chache sana kujitaja jina lake katika ijnili yake badala yake alijiita mwanafunzi aliyependwa sana na Yesu Yohana 13; 23, 19, 26, 20; 2, 21; 17, 20. Mwana huyu wa ngurumo alikuwa amekwisha kujifunza kuachana na mambo ya ukuu na kuwa mwana wa upendo aligundua kuwa Upendo sio maneno bali ni matyendo, la muhimu sio cheo bali ni uwepo wa Mungu
§  Aliwaasa watu aliowaita watoto wake kupenda kwa matendo na sio kwa maneno 1Yohana 3;18 alikuwa ameacha kabisa tabia ya kuwa kimbelembele na kutaka kuwa wa kwanza na sasa anakemea hata watu wenye tabia kama ile 3Yohana 9
§  Hata ingawa alikuwa sasa amezeeka sana moto wa injili ulikuwa ukiwaka ndani yake alihesabu mateso ya uzeeni kuwa ushuhuda wa Yesu Ufunuo 1;9 mateso na shida alizozipata huko patmo halikuwa jambo la muhimu kulieleza zaidi ya kile alichoagizwa na Kristo
§  Ni wazi kabisa kuwa kila mmoja ana maswala ya kujifunza kutoka kwa Yohana mabadiliko yake kutoka tabia ya ngurumo mpaka kuwa mtume wa upendo, kutokujihusisha na kusimulia mapito na badala yake kile ambacho Yesu alikuwa amemuagiza, mzigo wa kulitia moyo kanisa kuliko kutaka kutiwa moyo yeye mwenyewe, kuwa katika roho siku ya bwana hata pamoja na kuwa katika mazingira magumu kunaonyesha jinsi alivyotoa kipaumbele kwa maswala ya ibada

Tarehe ya uandishi
Kuna hisia kubwa tatu kuhusu tarahe ya uandishi wa kitabu cha ufunuo wa Yohana kulingana na mitazamo tofauti tofauti
§  Epiphanius aliandika mnamo katika karne ya Tatu kuwa Yohana aliandika kitabu chake cha ufunuo mara baada ya kurudi kutoka Patmo wakati wa utawala wa Claudius mwaka 41-54 lakini tarahe hii haikubaliki kwani ni mapema sana makanisa mengi ya asia ndogo yalikuwa hayajaanzishwa wakati huu nah alia ya uhasama kati ya ukristo na serikali ya Rumi pia ilikuwa haijachachamaa, inchi ilikuwa haijaendelea katika ngazi ambayo kibabu kinaonyesha  kwa misingi huo kuna uwezekano kabisa kuwa Epiphanius alikuwa akizungumzia Nerp ambaye pia aliitwa Claudius.
§  Mjadala kuhusu kuandikwa kwa kitabu hiki wakati wa utawala wa Nero umejengeka saa AD 54-68 kutokana na kuweko kwa alama maarufu katika kitabu cha ufunuo yaani 666 kwa kuzijumuisha pamoja namba hizi unapata thamani ya namba za herufi NERON KESAR kwa kiebrania jumla ya namba hizo zilitambuka kumaanisha hilo.Maswala mawili yanaweza kuhusishwa kinyuma na dhana hii, kwamba kuna Herufi nyingi sana ambazo zikijumuishwa zinaweza kuleta idadi kama hiyo na pili kwa jamaii ya Asia ndogo ingekuwa vigumu kwao kuwahusisha na  matumizi ya herufi za Kiibrania
§  Tangazo la kuweko kwa Milima inayomsaidia Mwanamke katika ufunuo 17 imekuwa ikitumiwa pia kumaanisha wakati wa Nero, vile vichwa saba ni milima saba anayoikalia hupo  na mwingine hajaja bado naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache na Yule mnyama aliyekuwako naye hayuko yeye ndiye wa nane naye ni mmoja wa wale saba naye anaenda kwa uharibifu Ufunuo 17;9-11
§     Kama tukio hili linahusishwa na kupeana madaraka kwa watawala wa kirumi wafalemwa kwanza wa Kirumi ni pamoja na Julius Caesar, Caesar Augustus,Tiberius, Caligula na Claudius na kama hao watano wamekwisha kuanguka wasita ni Nero na hapo ndipo kitabu cha Ufuno kilipoandikwa yaani wakati wa utawala wa kaisari Nero.                Tafasiri hii sio uhakikisho  wa ukweli kuwa wafalme hao hawatupi uhakika kuwa kwa sabau hatujui ni yupi anahesabika kama wa kwanza Augustus au la kama ni Augusto basi Nero anahesabika kama mfalme wa tano na kwa kweli Nero hakutawala muda mrefu sana kiasi cha kuwa wa muhimu katika utawala huo na hivyo Vespecian anakuwa wa sita na Tito anakuwa wa saba na Domitian anakuwa wa nane lakini kitabu kinaashiria kuwa ulikuwa wakati wa ukatili mkubwa wa Nero lakini makanisa ya asa yalikuwa hayajafikia kiwango cha mafanikio makubwa wakati wa Nero.
§     Kwa mujibu wa maelezo ya jadi ufunuo ni kitabu kilichoandikwa wakati wa Utawala wa Domitian kwa mujibu wa ushuhuda wa Irenaeus, Clement wa Alexandria pia alikubali swala hilo na ni kweli kuwa katika wakati huo makanisa ya Asia yalifikia kilele kikubwa cha mafanikio na huu ulikuwa wakati wa utawala wa Domitian na huyu alikuwa na madai ya kuabudiwa  kama Dominus et dues akiwa anatajwa kama mnyama aliyekuwa na nguvu kubwa ya kisiasa Ufunuo 13;15 na inakubaliwa kuwa jumla ya namba ya mnyama huyo inamuhusu Domitian yaani 666 ambaye kwa idadi ya herufi za jina lake Domitian yaani A[utokrator] KAI[sar] DOMET [ianos] SEB[astos] GER[manikos].kwa kujumlisha idadi ya hesabu ya herufi zake kwa kiyunani unapata jumla ya namba hiyo 666 na kwa kuwa idadi hii inakubalika sambamba na jina la Domitian haliwezi kuthibitishwa inakenda sambamba na kukubalka pia kwa jina la Nero .

Mahali
§  Kisiwa cha Patmos mahali ambapo maono yalipokelewa na kuna uwezekano kuwa yalinukuliwa pale au baadaye huko Efeso, Patmos ni kisiwa kilichoko juu ya mwamba katika Bahai ya Aegean (Aegean Sea) katika ukanda wa bahari ya Asia ndogo, lilikuwa ni eneo la koloni la warumi, mahali hapo wafungwa wa kisiasa walipelekwa  wakilazimishwa kufanya kazi ngumu na kuchimba madini, Yohana alisisitiza kuwa alikuwa huko Patmo kwaajil ya neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo Ufunuo 1;9, aidha mafunuo hayo yaliandikwa hukohuko Patmo au vinginevyo ni wazi kuwa kulikuwa na muda mfupi sana tangu kupokelewa na kuandikwa kwa maono hayo na kwa namna yoyote ile yanaakisi lugha na mazingira ya Kirumi, na jimbo la Asia  ambako kwa wakati huo mwandishi ndiko alikotokea na alikoishi.
§  Patmo kwa kiyunani Pavtmo ni kisiwa klichoko pwani ya Asia ndogo kama maili 35 kusini magharibi mwa kisiwa cha Mileto ni kisiwa chenye miamba na milima na kima ukubwa unaokisiwa kama Mita kumi kwa sita na kina ukavu na baridi kali kwa sifa zake na ni mahali palipotumiwa na Warumi kama eneo la Mateso inaaminika kuwa miaka ya zamani wa Italy walikiitakisiwa hiki Palmosa wakimaanisha isiwa chenye Mitende kwa hiyo inaaminika kuwa zaman klikuwa na Miti ambayo ilkatwa na hatimaye kukiacha kisiwa hiki kkiwa kikavu nakuna uwezekano kuwa hakuna maji.
§  Ni katika kisiwa hiki ndio Yohana alipelekwa kuadhibiwa na Mtawala wa wakati huo Domitian na hapo ndipo alipopokea yale maono na kuyaandika Ufunuo 1;9-11
§  Historia ya kisiwa hiki libadilika mnamo miaka ya 1088 wakati mtawa Christodulos alipojenga Ngome ya kitawa ya Mtakatifu Yohana katika eneo ambalo zamani kulikuwa na Hekalu la Artemi na miaka ilivyokwenda watawa waliishi hapo na kujifunza maswala kadhaa na kulima pia kuliwekwa( Library) Maktaba Patmos ilikuwa mahali pa kazi za Wayunani wa Ki Othodox lakini 1453 walitafuta msaada kwa Papa wa rumi kwaajili ya usaidiwa dhidi ya waturuki kwenye Karne ya 16 kikawa chini ya waturuki lakini waliachiwa wajiongoze na kuendesha mambo yao chni ya sultani.Mwaka 1832 kisiwa kiliangukia katika utawala wa waturuki na baada ya 1912 kilirejeshwa kwa Warumi na ilipofika 1947 kilikabidhiwa kwa Wayunani au Ugiriki hata leo.
         
Makusudi
§  Makanisa ambayo viongozi wake wametajwa katika kitabu cha ufunuo yalikuwa yameunganishwa na barabara inayoelekea upande wa Kaskazini kupitia pwani ya Efeso mpaka Pargamo kupitia Smyrna. Kutoka Pargamo kuna njia nyingine inayoelekea kusini zaidi bara na kugusa miji ya Thyatira, Sardis, Philadelphia na Laodikia na kisha njia inarudi nyuma kuelekea Efeso, Kama mjumbe angelipewa Barua au ujumbe angeweza kukamilisha mzunguko huo kwa urahisi, Efeso ndio ulikuwa mji mkubwa mtukufu wa Hekalu kubwa la artemis na Huko Pergamo ndiko kulikokuwa na madhabahu kubwa ya Zeus, Thyatira ulikuwa mji wa kilimo na utengenezaji wa nguo
Muda
§  Utawala wa Domitian ulianza kwa usumbufu mkubwa, Uharibifu wa Pompeii na Herculaneum na mauaji ya kikatili ya uchunaji ngozi ya Vesuvius mwaka 79AD. Ikifuatiwa na matukio mabaya yaliyoipiga Rumi kwa magonjwa na uasi katyika mji mpaka 81AD wakati Domiian akiingia madarakani, Alipoingia madarakani aliamuru kuabudiwa na alijiita kwa Kilatin Dominus et Deus yaani Domitian ni Bwana na Mungu yeye alikuwa mtawala wa kwanza kujilinganisha na Munu, ingawa wengine walitaka kuabudiwa na walikuwa wakipokea Ibada hata kwa kulazimishwa,  Domitian alijitangaza kuwa Mungu na mama yake Domitia kuwa mungumke fedha yake ilikuwa na alama ya mwezi na mtotoaliyeketi katika njia ya kuzunguka dunia pamoja na sayari kwaajili ya kumkumbuka mwanae aliyefariki akiwa mdogo mwaka 83AD.
§  Heshima yote ambayo alikuwa anastahili kupewa mwokozi Yesu Kristo ilidaiwa kupewa Domitian, Domitian alikuwa muuaji, almuua mwana wa dada yake Titus Flavius Clemens na alimuua mke wake, Domitilla inasemekana kuwa Clemens alikuwa Mkristo na Domitilla alikuwa akifuata tamaduni za kiyahudi kwa siri, huku yeye aliamini kuwa hakuna Mungu “Atheism” Eusebius anaeleza kuwa Domitian alijistawiosha mwenyewe kama mrithi wa Nero kwa ukatili na mwenye kustahili kama Mungu, ni mfalme wa pili kuinua kiwango cha mauaji na mateso kinyume nasi.... Eusebius alikuwa akimnukuu Hegesippus aliyekuwa akishuhudia ushuhuda wa Yohana alipokuwa amerudi Efeso baada ya kuachiliwa wakati wa utawala wa Nerv mwaka 96.

Malengo
§  Kitabu cha ufunuo kiliandikwa kwa makanisa yaliyokuwa yamefunikwa na tishio la mateso kwa lazima, kulikuwa na tishio la maafisa waliokuwa wakipita huko na huko kutoa vitisho na kwa sababu ya aina ya mapito waliyokuwa wakiyapitia walihitaji kutiwa moyo ili waendelee na kusimama imara katika imani na kuwaonya dhidi ya uadui kutoka ne na ndani, na mafundisho potofu yenye ukengeufu, kwa hiyo pamoja na hali halisi iliyokuweko ndipo sa maswala haya yanajitokeza katika kitabu cha ufunuo.
§  Kanisa linatiwa moyo nakuelekezwa katika kutazamia ujio wa Yesu na kuwa atakuja kuwahukumu maadui na kuliokoa kanisa maswala ambayo yanajitokeza Ufuno 2;5, 16, 25, 3;3,11, 20 na msisitizo wa maneno tazama naja upesi 3;11, 22;7, 12, 20 kwa hiyo maandalizi ya ujio wa Kristo mara ya pili ni msingi wa kitabu cha ufunuo.

KUPITISHWA KWENYE KANUNI
§  Utambuzi wa mapema. Kulingana na ushahidi uliokuweko mwanzoni kitabu cha ufunuo hakikukubaliwa na makanisa yote mwanzonikilikuwa kinafikiriwa kuwa ni swala la mauzauza tu allusions kutoka kwa wachungaji wa Hermas 140AD, lakini haikuendelea kusadikiwa hivyo kwani Kutokana na Mwanahistoria Jerome Melito ya Sardis AD 160-190 aliandika katika michango ake akisimulia kuhusu Justin Martyr AD 135 alihibitisha kuwa kimeandkwa na Yohana mmojawa wanafunzi wa Bwana Yesu, Irenaeus aliyekuwa Askofu wa Lyons alikubali kuwa kitabu hiki kina asili ya utume na kinakubalika
§  Kanisa la magharibi Kanisa la Alexandria walkuwa wataalamu wa maswala ya kinabii na Clement alikikubali kuwa ni maandiko na wanafunzi wake ama Origen alikikubali ingawa Dionysius wa Alexandria alikataa kuwa sio cha Yohana ingawa alikuwa anajua kuwa kimekubaliwa na makanisa, katika kanuni ya kanisa la Roman iliyopitishwa na Muratorian Fragment AD.170 walikijmuisha kama moja ya Vitabu na mwanatheolojia Hippolytus (190-235) alikinikuu mara nyingi kanisa la Cathage ambalo lna asili ya Rumi pia walikkubali, Tertullian(190-220) alinukuu sura 18 kati ya 22 zilizokuweko, kanisa la maghari  la karne ya 2 kwa ujumla walikubali kitabu cha  ufunuo, ni sauti mbili tu kama ya marcion aliyekuwa na mipaka yake aliyojiwekea  kwani alikuwa myahudi na Alogi ambaye alipinga kazi za Epiphanius na Irenaeus na hakuunga mkono kazi yoyote au wazo lolote linalohusiana na unabii lakini mpaka karne ya tatu kilikuwa kimekubalika kabisa katika kanuni.
§  Kanisa la mashariki walikuwa kwa namna Fulani kama maadui wakubwa wa Ufunuo hii huenda ilichangiwa na kutiwa shaka na Dionysus Askofu wa Alexandria ambaye alikitilia mashaka, pia Eusebius 260-340 alifuata muongozo huo, yeye hakukiorodhesha kabisa kitabu hiki inawezekana hili pia lilichangiwa na kuweko kwa Ofisi ya Papana tafasiri yake kuhusu millennium,Ushawishi wa Eusebius uliuwa na nguvu, neye Cyril wa Yerusalem AD 315- 386 alikataza watu wa kanisa kukisoma kitabu cha ufunuo hadharani au madhabahuni na alikikataza kutumika hata kwa kujitoa binafsi, Baadaye makanisa ya Asia ndogo hayakujumuisha kitabu hiki kwa vile hakikuorodheshwa na mkutano wa Kanuni wa Synod wa Laodekia AD 360 wala katika katiba ya mitume wala katika orodha ya Gregory Nazianzus, Naye thoodore wa Mopsuestia AD 340-428 alikikikataa kitabu cha ufuno akiambatanisha na waraka wa kikatoliki aliongoza kanisa la ki Nestorian pamoja na shule ya Antiokia, Mpaka katika karne ya 4 na 6 ndipo hatimaye kitabu cha ufunuo kilikubalika na kanisa la mashariki, Andrew wa Kaisaria huko Kapadokia aliandika mafafanuzi ya kitabu hicho na Leontius ambaye alikuwa Msomi huko Yerusalem alisema ni kitabu cha mwisho kukubalika na kupita katika kanuni ya Vitabu vya agano jipya.
§  Kukubalika kwa ujumla.
Kukubalika kwa ujumla kwa kitabu cha ufunuo kulitambuliwa rasmi baada ya barua ya Festal wa Athanasuis kunadikwa kutoka Alexandria mwaka 367, na mkutano wa Damasine Council wa 382 na mkutanowa Carthage wa 397 na cheti maalumu cha kuvitambua Vitabu na maandiko ya agano jipya kwa wa magharibi, na huko mashaiki msimamo wa kanisa ulitolewa kwa uthabiti mnamo karne ya pili na mamlaka yake kutambuliwa baadaye.


Jinsi ya Kutafasiri Kitabu cha Ufunuo.

Ni muhimu kufahamu kuwa kutafasiri kitabu cha ufunuo ni swala Gumu kwa namna Fulani na hakuna tafasiri mbili zinazoweza kukubaliana sawasawa hii ni kwa sababu zinazungumzwa ishara na lugha za mafumbo na kuna wingi wa Maruweruwe Illusions maswala ambayo wakati mwingne ni vigumu kujua hatima yake, Kwa ujumla kuna shule kuu nne za kutafasiri kitabu hiki

1. Preterest:       Unabii huu ulitimizwa wakati wa Kanisa la kwanza lilipopitia katika
mateso yaliyoendeshwa na Warumi.  Wengine wanaamini kuwa unabii ulitimizwa mwaka 70 BK wakati Yerusalemu ulipoangamizwa.
2. Historicit:       Nabii hizi zinahusiana na watu na matukio mbalimbali yaliyotokea huko nyuma – km. Napoleon na kuinuka kwa Uislam.
3. Idealist:           Matukio yanaelezea mifano ya kiroho kuhusiana na mapambano kati ya Mungu na shetani uovu na haki.
4. Futurist:          Nabii hizi zinahusiana na matukio halisi yatakayotokea siku zijazo ili kukamilisha mpango wa Mungu. Ni wazi kuwa sisi tunaofuatilia makala haya tunaamini katika mfumo huu wa tafasiri za kitabu cha ufunuo kwani ndivyo tunavyoamini.
MAMBO MUHIMU:
               
Kitabu cha Ufunuo ni cha aina ya Apokrifa, hivyo:-
§  Kinatumia ishara na mifano kutoa ukweli
§  Malaika wanaoelezea matukio
§  Kinaonyesha ushindi wa Mungu juu ya shetani.

KANUNI ZA KUTAFSIRI NA MAANA ZAKE:
Kanuni Na. 1 - Acha Maandiko yatafsiri yenyewe – Eze. 12:1-16
Kanuni Na. 2 – Tumia mwonekano wa unabii – mf. Lk. 4:16-21; Isa. 61:1,2
Kanuni Na .3 – Tambua kutumia mara mbili kwa andiko la unabii
Kanuni Na. 4 – Elewa matumizi ya ishara na mifano.

Aina za mifano  Mfano                                                 Maana:
                Namba                                 moja                                      Mungu
                                                                Mbili                                      Kuhakikishwa
                                                                Tatu                                       Utatu
                                                                Nne                                       Dunia
                                                                Sita                                         Mwanadamu, uovu
                                                                Saba                                      Utimilifu wa Mungu
                                                                Kumi                                      Kukamilika kwa siasa
                                                                Kumi na mbili                     Mwisho wa kukamilisha

Wanyama                           Mwanakondoo                 Yesu
                                                Farasi                                    Uwezo wa Kijeshi
                                                Wanyama                            Mpinga Kristo na nabii wa uongo
                                                Vyura                                    Mapepo wachafu
                                                Silaha                                    Yesu

Rangi                                     Nyeupe                                               Utakatifu
                                                Nyekundu                           Damu vitani
                                                Nyeusi                                  Baa la Tauni
                                                Zambarau                            Anasa za Kifalme
                                                Kijani                                     Burudisho
                                                Kijivujivu                              Mauti.

Theolojia katika kitabu cha Ufunuo.
Ingawa maswala ya ufunuo hayatiliwi mkazo katika Theolojia ni muhimu kufahamu kuwa kitabu cha Ufunuo kina magfundisho yaliyowazi yenye kukazia kuhusu maswala yajayo au matukio ya mwisho wa dunia Escatology ni wazi kuwa tunaona katika maono haya hatima ya baadaye ya kanisa katika mpango wa Mungu na juu ya maswala yajayo
Kitabu hiki kwanza kinatuonyesha jinsi Mungu alivyo mwenyezi na kuwa ni Bwana juu ya yote ni wazi kuwa kiini cha kitabu hiki ni kiti cha enzi cha Mungu kitabu hiki kinatukumbusha kuwa Mungu ni Mwenyezi ni mkuu kuliko ufalme uwao wote ukiwamo ule wa Rumi, nguvu zake ziko juu kuliko hata taifa lenye kutisha na ndie mwamuzi wa jinsi gani, lina na wakati gani atahukumu na kuwa anajua namna ya kushughulika na wanadamu walio waovu na kila uasi wa aina binadamu yeye ni mwenyezi 4:8; 11:17; 15:3; 16:7, 14; 19:6, 15; 21:22 na ni muumba wa kila kitu 4:11; 14:7 na muhukumu wa wanadamu 20:11-15).
Utatu wa Mungu umegusiwa katika ufunuo 1; 4-5 ambako kuna mazungumzo juu ya yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Roh saba zitokazo katika kiti cha enzi cha Mungu na Yesu kristo ni wazi kabisa kuwa kitheolojia kuna utatu hapa na swala hili linajitokeza katika kitabukizima ingawa si katika namna ambayo inaorodheshwa pamoja kila wakat kwa hiyo kitabu kizima kinamfunuo yeye Kristo Ufunuo 1;1.
Katika kitabu cha Ufunuo kuna somo kuu la Ufahamu kuhusu kristo Christology, kuna Historia ya sifa za Kristo za kipekee Ni samba wa kabila la Yuda Ufunuo 5;5, alikuwa na mitume kumi na wawili 21;14 alisulubiwa huko Yerusalemu 11;8 na alifufuka kutoka kwa wafu 1;5,18, ametukuzwa 3;21 na ana sifa zote zilizoorodheshwa katika sura ya kwanza.
Ana mamlaka dhidi ya Historia 5;6-12 ndio ufunguo muhimu wa kitabu hiki, ni Kondoo aliyechinjwa kwa sadaka 5;6 kama samba wa Yuda ni Mrithi wa kiti cha Enzi cha Daudi 5;5 ni mwana wa Adamu aliyeshinda, atokeaye juu ya mawingu kukamilisha mavuno ya ulimwengu 14;15 Anaitwa Neno la Mungu 19;13 ni mlinzi wa kanisa 1;12-20 na muhukumu wa mwisho wa ulimwengu 11;15 na ndiye Nuru ya mji ule uja 21;23.
Kazi za Roho Mtakatifu zinaorodheshwa ingawa mkazo katika kushughulika na mtu mmoja mmoja haukaziwi sana, anawakilishwa kama Roho saba za Mungu Ufunuo 1;4 ndiye aliyetengeneza mazingira mpokeaji kupokea maono 1:10; 4:2; 17:3; 21:10. Inagwa matumizi ya neno roho yanaonekana kutumia neno Pnuvmati kumaanisha hali ya hisia alizokuwa akizipata muona maonao kuliko kuhusu nafsi lakini Roho yuko pamoja na Bibi harusi wa Yesu kristo na anahusika katika amri ya kuja na kunywa maji ya uzima ufunuo 22;17.
Hali ya mwanadamu mbele za mungu inawekwa wazi, wanadamu wamejitenga na ungu wanamuhofu 6;16, 17 na mawindo wazi ya pepo wachafu 9:4; 13:3, 14; 17:8 na hatimaye watahukumiwa kwa matendo yao Ufunuo 20;12-13, Wokovu unahakikishwa kwa waamini 7;3 mwisho wa walioamini na wasioamini unawekwa wazi kuwa waasi ni katika ziwa la moto 21;8 na waliokombolewa kwenye miwa Mungu 22;14.
Pia kuna theolojia ya hali za kiroho ambazo waamini wanapaswa kuwa nazo na zisizopaswa kuwa ambazo zinaelezwa kwa wingi katika kitabu hiki sura ya 1-3 mwanzoni, mfano uvumilivu wakati wa mateso, upendo kwa Yesu, uaminifu n.k vinakaziwa katika kitabu hiki.
Ulimwengu wa kiroho wa kishetani unawekwa wazi huku shetani na mapepo yakitajwa sawa na sifa zao 9;4-11 ni wazi pia kitabu cha ufunuo knaweka wazi kuwa mgogoro tulionao kati yetu na shetani ni wa kiroho na ni vita  na uwa ulianzia mbinguni na kuja duniani 12;7, hatinma yeke inawekwa wazi kuwa hatimaye atahukumiwa 12;9 na Mungu atashinda na shetani atatupwa katika ziwa la Moto 20;1-3,10. Na kongozi wa kisiasa aliye kiyume na maswala ya Mungu anayetajwa kama mnyama hatimaye ataharibiwa Ufunuo 13.
Swala la malaika nalo limazungumzwa kwa uapana sana katika kitabu cha ufunuo kuliko kitabu kingine chochote katika agano jipya kwa mafano kwa kila kanisa moja kna malaika  na pia wametajwa Karibu katika kila sehemu ya kitabu hikikuwa ni watumishi wa Mungu 5:2; 7:2, 3; 8:2; 10:1; 12:7; 14:6, 8, 9, 17; 15:1; 17:1; 18:1, 21; 19:17; 20:1; 21:9; 22:8 viumbe vyeye uhai Ufunuo 4;6-8 vinafanana na maserafi wa Isaya 6 na ni wazi kuwa vi viumbe maalumu sana  na pia tunawekewa wazi kuwa malaika na mapepo ni viumbe walio katika namna moja ya maumbile ya kiroho wakigawanywa kuwa wema na waovu Ufunuo 12;7
Ni wazi kuwa msingi na makazo wa Kitabu hiki ni mambo yajayo na mafundisho yote yanakubaliana na mpango wa Munu katika historia 2:7, 10, 17, 28; 3:5, 12, 20 eneo jingine linahusika na maswala ambayo hayaa budi kuja upesi na kutimia sifa za Mungu zinawekwa wazi,mpango wake wa uumbaji unawekwa wazi,umbaji mpya unawekwa wazi,kazi za Yesu za wokovu zinawekwa wazi, kazi za uovu zinawekwa wazi hali ya baadaye ya watu waliokombolewa zinawekwa wazi sura ya 19-22 hili ni lengo la  ki- eschatological
Mgawanyo kamili
Ingawa kitabu cha ufunuo kinaonekana kuwa ni maono lakini kimekaa katika mgawanyo mzuri na mapangilo mzuri unaofaa ambao unaweza kugawanywa katika maeneo makuu sita. Kupitia kukazia neno nalikuwa katika roho kila moja ya matukio haya katika kitabu hiki yanashughulika na tukio maalumu la kiufunuo. Kristo ndio ufunguo mkubwa wa kitabu cha ufunuo na ni wa muhimu kuliko mpangilio ingawa kuna muendelezo wa matukio kutoka mwanzo ambao unaweza kuorodheshwa kwa namna ifuatayo.
Utangulizi Ufunuo 1;1-18.
§  Jina : Ni Ufunuo wa Yesu Kristo 1,a
§  Waliotumiwa: Yesu,Yohana na malaika 1b-2
§  Baraka; Kwa kila asomaye ,na wao wayasikiao, kuyashika3
§  Salaam; kwa makanisa saba,kutoka kwa Yohana na Yesu Kristo 4-7
§  Utambulisho mkuu Yesu ni Alfa na Omega 8
§  Mamlaka ya kuandika kitabu;  9-11.
Mambo yale uliyoyaona Yesu kristo aliyetukuzwa 1;12-18
§  Agizo la kuandiki kitabu cha ufunuo 19-20
Mambo yale yaliyoko Maagizo kwa makanisa saba 2;1-3;1-22.
§  Kwa kanisa lilioko Efeso 2;1-7
§  Kwa kanisa lilioko Smyrna 2;8-11
§  Kwa kanisa lilioko Pergamo ;2;12-17
§  Kwa kanisa lilioko Thyatira2;18-29
§  Kwa kanisa lilioko Sardis3;1-6
§  Kwa kanisa lilioko Philadelphia3;7-13
§  Kwa kanisa lilioko Laodicea 3;14-22
Mambo yatakayokuwa baada ya hayo 4;1-16;21.
§  Hali halisi ya Kiti cha enzi cha hukumu naheshima na ibada huko mbinguni 4;1-11
§  Kitabu cha hukumu cha mwana kondoo 5;1-14
Kufunguliwa kwa Muhuri saba 6;1-8;5
§  Muhuri wa kwanza Farasi mweupe Ushindi wa mpinga Kristo na utawala 6;1-2.
§  Muhuri wa pili Farasi mwekundu vita  6;3-4
§  Muhuri wa tatu Farasi mweusi njaa 6;5-6
§  Muhuri wa nne Farasi wa kijivu kifo  6;7-8
§  Muhuri wa tano Nafsi chini ya madhabahu waliofia dini 6;9-11
§  Muhuri wa sita Hasira za mwana kondoo mapigo mazito kwa dunia 6;12-17
§  Muhuri wa saba ukimya matayarishio  ya tarumbeta saba 8;1-5
Kupigwa kwa tarumbeta saba 8;6-11;19
§  Hukumu dhidi  ya nchi 8;6-7
§  Hukumu dhidi  ya bahari 8;8-9
§  Hukumu dhidi  ya mito 8;10-11
§  Hukumu dhidi  ya mbingu 8;12
§  Hukumu dhidi ya wanadamu ole kuu tatu  8;13
§  Hukumu dhidi ya wanadamu wakaao ju ya inchi 9;1-11
§  Kutangazwa kwa Ole kuu 9;12
§  Kufunguliwa kwa malaika wanne waovu zaidi 9;13-21
§  Malaika na Muona maono 10;1-11;14
§  Kitabu kidogo 10;1-11
§  Kupimwa kwa hekalu 11;1-13
§  Kutangazwa kwa ole ya tatu 11;14
§  Kupigwa kwa tarumbeta ya saba 11;17-19
Ishara kuu 12;1-16;21
§  Mwanamke, mtoto wa kiume na Yule joka 12;1-17
§  Mnyama kutoka baharini 13;1-10
§  Mnyaka kutoka katika inchi 13;11-18
§  Mwana kondoo katika mlima sayuni 14;1-5
§  Malaika wa Habari njema 14;6-13
Kutangazwa kwa injili
Kuanguka kwa Babel
Kutangazwa kwa heri ya wafu waliobarikiwa
§  Mvunaji katika mawingu 14;14-16
§  Kushughulikiwa kwa mzabibu wa dunia 14;17-20.
Kumwagwa kwa vitasa saba vya mapigo 15;1-16-16;21
§  Wimbo wa Musa na mwanakondoo 15;1-4
§  Kufunguliwa kwa Hekalu na hema ya mbinguni 15;5-16;1.
§  Kumiminwa kwa kiatsa cha kwanza majipu mabaya 16;2
§  Kumiminwa kwa kitasa cha pili bahari kuwa damu 16;3
§  Kumiminwa kwa kitasa cha tatu mito na maziwa kuwa damu 16;4-7
§  Kumiminwa kwa kitasa cha nne jua kuunguza wanadamu 16;8-9
§  Kumiminwa kwa kitasa cha giza kwa ufalme wa mpinga kristo 16;10-11
§  Kumiminwa kwa kitasa cha kukauka kwa mto frati na vita vya Armageddon 16;12-16
§  Kumiminwa kwa kitasa cha saba Tetemoko la inchi 16;17-21

Ushindi wa Yesu Kristo 17;1-21;8
§  Hukumu dhidi ya Babel 17;1-18;24
§  Hukumu dhidi ya tamaduni 17;1-18
§  Hukumu dhidi ya mji 18 ;1-24
§  Muitikio huko mbinguni 19;1-10
§  Kushindwa vibaya kwa wakuu wa uovu 19;11-20;24
§  Ushindi wa Yesu Kristo 19;11-16
§  Kuharibiwa kwa mpinga kristo 19;17-21
§  Kufungwa kwa shetani 20;1-3
§  Utawala wa miaka 1000 Millennal reign 20;4-6
§  Kuharibiwa kwa shetan 20;7-10
§  Hukumu ya mwisho 20;11-14
§  Yerusalemu mpya 21;1-8
Yesu katika mji wa Mungu 21;9-22;5
§  Kutokea kwa mji 21;9-21
§  Mwangaza wa mji ule 21;22-23
§  Wakazi wa mji ule 21;24-27
§  Mandhari ya mji ule 22 ;1-5
§  Mausia ya Kristo 22;6-21
Mstari wa Msingi ni
§  Ufunuo 1;19 Basi Uyaandike mambo hayo uliyoyaona nayo yaliyopo na yale yatakayokuwa baada ya hayo

UCHAMBUZI WA KITABU CHA UFUNUO           

KITABU CHA UFUNUO:
Lengo la 1:  Taja mambo matano yanayoelezea chanzo cha Ufunuo katika sura ya 1:-
Mambo matano yaliyodhihirishwa katika sura ya 1 ni:-
  • Ufunuo wa Yesu Kristo 1:1
  • Ujumbe huu uliwasilishwa kwa Yohana kupitia Yesu Kristo, malaika na maono – 1:1,10-18
  • Ujumbe huo uliletwa kwa Yohana – 1:1,4,9,2
  • Alipewa ujumbe huu akiwa mfungwa katika kisiwa cha Patmo
  • Walengwa wa ujumbe yalikuwa makanisa saba katika Jimbo la Asia ndogo.
Kitabu hiki kiliandikwa wakati wa utawala wa Domitian aliyetaka watu wamwabudu kama Mungu.  Amri hii ilileta matatizo na mateso kwa wakristo.  Hivyo kitabu hiki kiliandika katika mazingira haya.

M A K U S U D I:
Lengo la 2:  Eleza kusudi la kuandikwa kwa kitabu hiki Kusudi la kuandikwa kitabu hiki liko katika sehemu tatu:-
  • Nyaraka zilizoandikwa zilikuwa za kukemea makanisa yaliyoridhia dhambi bila kuikemea.
  • Kutokana na mateso ya Domitian aliyetaka kuabudiwa – kitabu hiki kiliandika kuwatia moyo kuvumilia mateso na kuwa waaminifu hadi kufa.
  • Kiliandikwa kwa ajili ya Kanisa la Kizazi chake ili kuwaonyesha waamini juu ya mapambano waliyo nayo dhidi ya majeshi ya shetani.  Jinsi kuja kwa pili kwa Yesu Kristo kutakavyokomesha utawala mwovu wa mpinga Kristo.
M H U S I K A:
Lengo la 3 :  Eleza mhusika mkuu linazungumzwaje:
§  Mtiririko wa kitabu cha Ufunuo ni kuelezea kuja mara ya pili kwa Yesu Kristo (Ufu.1:7).  Mhusika Mkuu katika kitabu cha Ufunuo ni Yesu Kristo mwenyewe.  Yale aliyokwishafanya, anayofanya sasa na yale atakayofanya baadaye.
MWANDISHI NA TAREHE:
Lengo la 4: Orodhesha ushahidi wa Uandishi na Tarehe ya Kitabu cha Ufunuo:
§  Kitabu hiki kiliandikwa na Yohana Mtume wakati wa utawala wa Kaisari Domitian mnamo mwaka kati ya 91-96 BK.  Ushahidi tunaopata ni matumizi ya maneno “Logos” “Nikao” na “Ekkenteo” (kushinda na kuchoma).  Pia ushuhuda wa Viongozi wa mwanzo wa kanisa kama Justin Martyr unathibitisha kuwa mtume Yohana aliandika, ushahidi wa ndani ya kitabu unahusiana na kuwa kifungoni kisiwani Patmo huko Asia ya Kati.
SEHEMU KUU ZA KITABU:
Lengo la 5:  Eleza sehemu kuu za Kitabu.Katika Ufu. 1:19 Yesu mwenyewe anaelezea:-
  • Utangulizi – 1:1-8
  • Yale uliyaona 1:9-20
  • Nayo yaliyopo 2-3
  • Yatakayokuwepo baadaye – 4:1-22:6
*      Kanisa katika Utukufu – 4:1-5:14
*      Dhiki Kuu – 6:1- 19:21
*      Miaka elfu  -20:1-6
*      Gogu  na Magogu – 20:7-10
*      Kiti cheupe 2:11-15
*      Mambo yote mapya – 21:1-22:6
§  Hitimisho - 22:7-21
§  Maelezo ya Zaidi:
§  Ni maelezo ya kina kuhusiana na jambo lililokwisha elezwa tayari.
§  Sura ya 7- Wayahudi 144000 na waliovikwa mavazi meupe.
§  Sura ya10 - Malaika mwenye nguvu mwenye Gombo au kitabu
§  Sura 11:1-14 – Mashahidi wawili
§  Sura ya 12  - Mwanamke, mtoto na Joka
§  Sura ya 13   - Wanyama wawili
§  Sura ya 14 - 144,000 (Israeli), mwisho wa Injili kuhubiriwa, Tangazo la Kuangushwa kwa Babeli, mavuno ya mwisho na shinikizo.
§  Sura ya 17  - Wanyama wawili na kahaba mkuu
§  Sura ya 18  -    Babeli
MASWALI:
  1. Chanzo cha Ufunuo ni kipi?
  2. Taja makusudi matatu ya kitabu cha Ufunuo
  3. Nani mhusika Mkuu wa kitabu hiki?
  4. Taja sehemu kuu za kitabu hiki.




YALE YOHANA ALIYAONA: KRISTO ALIYETUKUZWA;

CHANZO NA KUSUDI LA UFUNUO:
Lengo la 1:  Eleza chanzo cha Kitabu cha Ufunuo na ujumbe wake. Chanzo cha ujumbe wa kitabu ni Mungu akiwa na lengo la kuifunua kweli kwa watumishi wa Mungu.  Hivyo kitaeleweka kwa watu wake kwa sababu wanayo hekima kutoka kwa Mungu.
EN TACHEI:
Lengo la 2:  Eleza maana ya neno “upesi” - Ufu. 1:1Yesu  alimtuma malaika wake kumwonyesha Yohana mambo ambayo hayana budi kuja upesi – neno upesi linatokana na neno la Kigriki “En Tachei” “En tachei"   likiwa na maana “mara moja “   upesi, ghafla, wakati wowote.

MAANA YA “MALAIKA”:

Neno au jina malaika lina asili ya kiyunani  ambayo ina maana pana kadhaa jina hilo kwa kiingereza ni Angel ambalo limetokana na jina la kiyunani Angelos (Angelos)ambalo lina maana ya mjumbe na kwa kiebrania ni Malakh (Malakh) ambalo pia maana yake ni mjumbe wa Mungu lakini pia jina hili lilitumiwa wanadamu au kwa kumaanisha maswala kadhaa yafuatayo;-
§  Neno hili angelos lilitumika pia kumaanisha “roho ya mtu aliyekufa” na matumizi kama hayo yanaonekana katika sehemu chache za agano jipya Mathayo 18;10 na katika Matendo 12;15 ambapo wanafunzi walifikiri Malaika wa Petro alikuwa anagonga mlango hii ni kwa sababu kimsingi wengi walifikiri Petro angekuwa ameshauawa na isingeliwezekana kutoka gerezani na kurudi nyumbani katika hali ya muujiza kama vile hii ni kwa sababu walishaomba kwaajili ya Yakobo na labda kuuawa kwa Yakobo pamoja na kuwa waliomba kuliwafanya waamini kuwa si rahisi kwa Petro kuweza kuwa hai. Jambo lingine ni lile fundisho kuwa wenye haki wanapokufa huwa kama malaika kwa msingi huo ni wazi kuwa roho ya mtu aliyekwisha kufa pia ilimaanisha wazi kutumiwa kama neno malaika.
§  Neno malaika pia linaweza kumaanisha “mjumbe wa Mungu aliye mwanadamu” mfano katika ufunuo 2;1-7, ingawaje pia kunauwezekano kuwa katika eneo hilo kitaalamu inakisiwa kuwa linaweza kumaanisha mambo manne hivi yaani  wajumbe ambao wanabeba gombo la chuo kwaajili ya kila kanisa, katika makanisa ambayo Yohana alikuwa akiyaandikia, 1Makabayo 1;44 hili linaweza kuthibitishwa na  ufunuo 1;11, ambapo agizo linaonyesha kuwa haya uyaonayo uyaandike katika chuo ukayapeleke kwa hayo makanisa saba  Efeso, na Simirna,  na Pergamo na Thiatira, na Sard na Filadelfia na Laodikia kutokana na mfumo wa lugha hii kunauwezekano wale waliopeleka magombo hayo wakaitwa wajumbe yaani Malaika, Pili inaweza kuwa inamaanisha  viongozi wa kila kanisa ambao husimamia makanisa  na huwasomea watu maandiko kama ilivyokuwa wakati wa matumizi ya masinagogi kwani nyakati za kanisa la kwanza kazi ya kiongozi ilikuwa ni kuwasomea watu maandiko kwa jamii ya wakristo walikuwa ni watu wanaowajibika kwa Mungu kama watu watakaotoa hesabu hivyo viongozi hao pia waliitwa malaika yaani wajumbe wa Mungu, Au malaika pia humaanisha viumbe wa kiroho wa Mungu ambao wanawakilisha maeneo halisi yaliko makanisa yale na imani hii ina mzizi katika fundisho la kitabu cha Daniel kuweko kwa malaika wa kila eneo, na pia kanisa lenyewe ni uwakilishi halisi wa maswala ya mbinguni hapa duniani.
Lengo la 3:  Eleza njia mbali mbali za Kibiblia kuhusiana na neno “Malaika” na Ujumbe alioonyeshwa Yohana (Ufu.1:2)
Ufu. 1:1 unaonyesha kuwa neno“malaika” lina maana ya mpeleka habari (tarishi). Hii inaonyesha kuwa Yesu Kristo alifunuliwa kwa Yohana na malaika.  Katika Biblia kuna malaika wa aina mbili: Wajumbe wa kimwili na wa Ki-Mungu.  Huyu malaika alitoa ujumbe kwa kutumia ishara na mifano.  Mambo mawili yaliyofunuliwa ni Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.
HERI SABA ZILIZOMO KATIKA  UFUNUO  (1:3-5)
Hizi ni baraka za Mungu kwa watu watakaotenda mambo Fulani.
Lengo la 4 : Orodhesha Heri hizo.
§  Ufu. 1:3 - “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyashika yaliyoandikwa..”
§  Ufu. 14:13 -Heri wafu wafao katika Bwana, tangu sasa wapate kupumzika.
§  Ufu. 16:15 - Heri akeshaye na kuyatunza mavazi yake asiende uchi..”
§  Ufu. 19:9 -   Heri walioalikwa karamu ya Arusi ya Mwanakondoo
§  Ufu.20: 6 -  Heri na Mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa Kwanza
§  Ufu. 22:7 - Heri yeye ashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
§  Ufu. 22:14 – Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa Uzima.
ROHO SABA ZA MUNGU – Ufu. 1:4
Lengo la 5: Onyesha Roho saba ni nini?
§  Roho Saba za Mungu maana yake ni ukamilifu wa huduma ya Roho Mtakatifu kwa Kanisa la Mungu.Ufunuo 4.5, Ufunuo 5;6 ni wazi kuwa utendaji Huu na Ufafanuzi huu kuhusu Roho Mtakatifu haumaanishi kuwa Roho wa Mungu amegawanyika lakini unawaklisha Utendaji mkamilifu wa Roho wa Mungu Isaya aliweka wazi Ukamilifu huu mapema ona katika Isaya 11;1-3Roho anatajwa kama, Roho ya Bwana, Roho ya Hekima, Roho ya Ufahamu, Roho ya Usahauri, Roho ya uweza, Roho ya Maarifa, Roho ya kumcha Bwana.
AINA TATU ZA KUJITAMBULISHA KWA YESU – 1:5,6
Lengo la 6: Eleza jinsi Yesu anavyojitambulisha.
(a)    Yesu ni Shahidi mwaminifu
(b)   Mzaliwa kwa Kwanza wa walio hai
(c)    Mkuu wa Wafalme wa dunia.
ALFA NA OMEGA –1:8
Lengo la 7:  Eleza sababu inayomfanya Yesu aitwe Alfa na Omega. Yesu anaitwa Alfa na Omega kwa sababu herufi za Kiyunani zinaelezea kuwa katika yeye Mungu Baba aliumba vitu vyote na katika yeye Baba ataleta mwisho wa kila kitu.Yeye ni mwanzo wa kila kitu yeye ni wa kwanza na wa mwisho yeye ni kila kitu A & Z.
NENO TAZAMA – 1:7
Lengo la 8: Eleza maana tofauti za neno Tazama, katika kifungu hiki lina maana ya:
Kuona kwa macho ya kimwili
Kuelewa au kufahamu
Kushangaa na kujiuliza.
SIKU YA BWANA - 1:10
Lengo la 9 : Eleza maana ya siku ya Bwana.          
§  Katika mstari huu una maana siku ya kwanza ya juma, Jumapili. Yohana alikuwa katika roho siku hiyo.
§  Nalikuwa katika Roho siku ya Bwana Yohana 20;1,19;26.Mdo 20;7 1Koritho 16;2
§  Yohana anatufundisha kitu cha ajabu sana kwani ingawa alikuwa ametengwa mbali na watu Imani na mazingira aliweza kuwa katika roho siku ya bwana, ni wazi kuwa liko bishano la kuhusu siku ya kuabudu ukweli siku hii ilikuwa ni siku ya jumapili siku ambayo Bwana Yesu alifufuka
§  Katika kitabu hiki utendaji wa Yesu unaashiria wazi kuwa  alikuwa amekusudia kabisa siku hii iwe maalumu kwaajili ya kuabudu, kuna matukio kadhaa yaliyojitokeza katika siku hii ya kwanza ya juma ambayo ni matukio ya kushangaza yanayoashiria kuwa Bwana aliikusudia itumike kwa makusudi ya kuabudu pia
*      Bwana alifufuka kutoka kwa wafu siku ya kwanza ya juma Mathayo 28;1,Marko 16;2,Luka 24;1 neno mia la kiyunani lilitumika katika mistari hii kumaanisha siku aliyofufuka Bwana
*      Aliwatokea wanafunzi wake  mara mbili  katika siku hiyo ya kwanza ya juma Yohana 20;19,26
*      Ujio wa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste ulitokea siku ya kwanza ya juma hili tunalijua kutokana na Walawi 23;15-16.Hata ilipotimia siku ya Pentekoste...Roho Mtakatifu akaja Matendo 2;1.
*      Kuna dalili nyingi kuwa wanafunzi wa nyakati za kanisa la kwanza waliiadhimisha siku hii hata ingawa uko ushahidi kuwa walikuwa wakikutana kila siku kwaajili ya kuabudu Matendo 2;46 lakini ni wazi katika maandiko kuwa siku hii baadaye ilikuwa maalumu
*      Paulo alifundisha wazi kabisa  umuhimu wa siku ya Bwana akiwataka wakoritho kujiandaa kumtolea Mungu katika siku hiyo 1Wakoritho 16;2
*      Mtakatifu Ignatio aliandika hivi, Tukiwa hatushiki  tena sabato bali tukiishi kulimgana na siku ya bwana  ambayo ndiyo nuru yetu alipofufuka
*      Justin Martyr alipokuwa akiandika utetezi wake wa imani kwa mtawala wa Rumi aliandika hivi  ”Jumapili ndiyo siku ambayo sisi tunakusanyika wote pamoja kwa sababu ndiyo siku ya kwanza ya juma
*      Katika mkusanyiko wa mafundisho yaitwayo mafundisho ya mitume  yaliyokusanywa mwaka 105 B.K. twaona taarifa kuwa mitume waliiamuru siku hii kuwa na ibada ya pamoja , na ushirika na kusomwa maandiko kwa sababu ni siku aliyofufuka Bwana
*      Eusobio mwandishi aliyeheshimika wa Historia ya Kanisa tangu Kristo hadi Kostantino aliandika   Tangu mwanzo wakristo walikusanyika kwehye siku ya kwanza ya juma
Historia ya sabato
*      Mungu alukuwa na sabato yake katika Mwanzo 2;2-3 hii ni sabato ya Mungu  na hakuna mahali pengine yeye amewahi kushika nyingine tangu wakati huo
*      Sabato nyingine ni ya kiyahudi Mungu aliwapa wao tu na sio wenine  Mwanzo 7;4-10,8;10-12, Sabato ya kiyahudi ilitajwa kwa mara ya kwanza katika Kutoka 16;21-30 hii iliwahusu waisrael tu na sio mataifa mengine wala sio kwa Wakristo Kutoka 31;13-17 hii ni Ishara ya Mungu kwa wana wa Israel tu milele Wagal;atia 3;19 torati na mabnabii vilifanya kazi hata wakati wa Yohana batizaji lakini Tangu wakati huo Habari za ufalme hutangazwa Luka 16;16.
*      Sabato ilikuwa ni kivuli tu cha maswala ya ujio wa Kristo wakolosai 2;7 kwa hiyo siku ya bwana haina uhusiano wowote na uvumi kuwa ni alama ya mnyama ufunuo 13
*      Jambo la mwisho la kuzingatia ni kuwa siku sio jambo la msingi sana katika swala la kuabudu ingawa wote tunajua kuwa jumapili ni siku ya bwana na kuwa imekubalika itumike na wakristo wote kwa kusudi la kuabudu lakini kama wengine wanaweza kuabudu siku nyingine yoyote kuabudu kulingana na mazingira husika hii isitufanye kufungwa na fundisho la kuabudu katika siku fulani Warumi 14;5-9.



SAUTI, AMRI NA MAONO – 1:10-16
Lengo la 10:   Elezea Yesu aliyeonwa na Yohana.Yohana alimwona Yesu katika Utukufu wake mkubwa mmno.
§  Vazi lililofika miguuni - Ukuu wa Yesu kama nabii, kuhani na mfalme.      
§  Kichwa na nywele zake - Utakatifu,, hekima na Umilele wa Yesu
§  Macho kama mwali wa moto- Anajua yote
§  Miguu kama  shaba iliyosuguliwa - Hukumu ya Yesu kwa watu
§  Sauti ya majimaji - Mamlaka na nguvu za Yesu
§  Mkono wake wa kuume               - Kujali, msaada na kudhibiti kwa Yesu
§  Upanga utokao kinywani - Neno lenye mamlaka ya Yesu
§  Uso kama jua katika nguvu zake – Utukufu, Ukuu na Utakatifu wake.

MAUTI NA KUZIMU - 1:17,18
Lengo la 11  : Eleza neno “Paradiso”, jadili mahali ilipo.
§  Kufuatana na Maandiko, Paradiso ni mahali pa kuwafariji watakatifu waliokufa.  Wakati wa Agano la Kale paliitwa kifuani pa Ibrahimu huko kuzimu.  Yesu alipokufa na kufufuka Paradiso ilihamishwa mbinguni.  Hivyo kuzimu Sheol HB au Hades GK ni mahali wanapokwenda waovu wanaokufa.  

NYOTA  NA  VINARA VYA TAA  - Ufu. 1:19,20

Lengo la 12:  Elezea maana ya nyota na Vinara.
§  Nyota Saba na malaika saba ikiwa na maana ya wachungaji wa Makanisa. Vinara Saba ni makanisa saba (Mst.20) ambayo yamewekwa kuwa nuru ya kumfunua Yesu Kristo kwa watu.  Yesu yupo katikati ya vinara kuonyesha uwepo wa Mungu upo ndani ya kanisa na wachungaji wapo mikononi mwake.

MASWALI:
1.       Neno “ Malaika” lina maana gani katika Ufunuo.
2.       Orodhesha heri zilizomo katika Ufunuo
3.       Siku ya Bwana inayotajwa Ufu.1:10 ni ipi?
4.       Nini maana ya Alfa na Omega – Ufu.1:8.

MAMBO YALE YALIYOPO, YESU NA MAKANISA SABA;
kabla Kristo hajaanza kuhusika na hukumu kwa ulimwengu anaanza kuhukumu watu wake yaani kanisa 1Petro 4;17, Ezekiel 9;6 Kila aunaposoma habari za makanisa haya saba utaweza kuona kuwa makanisa haya saba yanapita katika hukumu ya bwana ni wazi kuwa makanisa haya uiyaangalia kwa undani ni makanisa ya mahali pamoja lakini pia ni mtu mmojammoja binafsi ni wazi kabisa kuwa watakatifu watahukumiwa kwa hukumu yao maalumu na kuwa hawatahukumiwa pamoja na dunia katika eneo hili sasa tutakuwa tukiyaangalia makanisa yale saba na nyaraka zake na uchambuzi wake kutoka Ufunuo 2;1-3;22.




Makusudi makuu ya Nyaraka zile.
§  Makanisa yale saba yalikuwa ni makanisa halisi na yalikuwa na matatizo halisia yaliyoatakiwa kushughulikiwa kichungaji na kuonywa na kuongozwa na Mkuu wa kanisa ambaye ni Bwana Yesu mwenyewe
§  Makanisa yale saba pia huwakilisha nyakati saba za kihistoria katika kanisa tangu wakati wa kanisal  la kwanza  siku ya pentekoste hata wakati wa kuja kwa bwana , haya pia yanaweza kuwa makanisa au madhehebu ambayo yana mapungufu mbalimbali na baraka mbalimbali sambamba na hali ya yale makanisa saba, makanisa hayo pia yanawakilisha Roho za kinabii 19;10.
o   Apostolic Church 33-100 Kanisa la wakati wa Mitume kanisa lenye shughuli.
o   Persecuted Church 100-113 kanisa la Karne ya kwanza lililoteseka
o   Imperial Church 313- 476 Kanisa la kpindi cha lililopata ushindi na kanisa lililokosea
o   Medieval Church 476-1453 kanisa lililopoa kipindi cha giza kanisa lenye tatizo
o   Reformed Church 1453-1648 kanisa la kimapinduzi kanisa lililotazama nyuma
o   Morden church 1648-1970 kanisa la leo kanisa la kiinjilisti
o   Morden charismatic church 1970 mpaka leo. Kanisa lenye mafanikio
§  Makanisa haya saba yanawakilisha pia kujihusisha na mtu mmoja mmoja utaweza kuona lugha kama Yeye aliye na sikio na asikiye Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa Ufunuo 2; 7, 11, 17, 29, 3;6, 13, 22. Kwa msingi huo wakristo waweza kupokea halia za kutiwa moyo, kuonywa na kujengwa kupitia ujumbe huu wa makanisa yale saba 2Timotheo 3; 16.

Yaliyomo kwa Mukhtasari katika makanisa yale Saba.
Lengo la 1: Orodhesha mambo yaliyomo katika barua zilizoandikwa kwa. Makanisa Saba:
  • Salamu kwa Kiongozi wa kila Kanisa.
  • Tabia na hali za Yesu Kristo.
  • Yale Yesu anayajua kwa kila Kanisa
  • Yale anayoyafurahia katika kila Kanisa isipokuwa Laodekia
  • Yale Yesu aliyakosoa na kukemea katika kila Kanisa isipokuwa Smirna na Filedefia.
  • Ahadi kwa kila Kanisa
  • Ushauri kwa kila Kanisa kusikia ujumbe
  • Ahadi kwa washindi
N.B:  Jumbe kwa Makanisa saba inaelezea hali ya Kiroho iliyokuwemo ndani ya Makanisa hayo.  Hali hiyo inalingana na Makanisa ya vizazi vyote.

BARUA KWA KANISA LA EFESO: Kanisa lenye shughuli bila Upendo Ufunuo 2;1-7.
Lengo la 2:  Eleza Historia na hali ya Kanisa la Efeso.
§  Efeso ulikuwa mji na bandari wenye ibada za sanamu uliozungukwa na mashamba mazuri.
§  Ulikuwa ni mi wenye maswala ya dini za kipagani Animism hekalu la Mungu Artemis lilisimamishwa katika mji huu na lilikuwa kubwa na zuri kiasi cha kuingizwa katika moja ya maajabu saba ya kale ya Dunuia.
§  Artemis alikuwa ni mungu aliyehusika na maswala ya Uzazi alikuwa ni mungu mke aliyeaminika kuwa alishuka kutoka mbinuni Matendo 19; 35 na wayeyusha vyuma walitengeneza sanamu za mungu huyo na kuziuza.
  • Kanisa lilianzishwa na Paulo katika safari ya tatu ya Utume. Watu wengi waliokolewa na kuchoma uchawi wao na Vitabu vya uchawi na uganga Mdo.19:1-41.  Paulo alifanya kazi Efeso kwa muda wa miaka 3 , Mdo. 20:31
  • Baadaye Kanisa hili alilisimamia Timotheo ili kukemea mafundisho potofu yaliyoletwa na baadhi ya waamini 1Tim. 1:3.
  • Kanisa lilisifiwa na Yesu kwa mambo matano mazuri:-
§  Bidii, uvumilivu, kutovumilia uovu, kuwajaribu wajiitao mitume, kuchukia mafundisho ya wanikolao.Wanikolao yalikuwa ni mafundisho ya watu waliosemekana kuwa waliamini kuwa “Woman is For social not a Personal” Hivyo walibadilishana wanawake na walikubaliana na maswala ya Uasherati na Uzinzi, na walikula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu Kristo alichukizwa na aina iyo ya mafundisho a aliikataa tena na tena katika Mstari wa 6 na wa 15.
§  Hawakuchoka katika subira ya Kristo na walifundisha mafundisho sahii Mstari wa 3,6.
  • Lilikemea kwa kupoteza upendo wa kwanza; hivyo lilikuwa katika hatari ya kutengwa. Kanisa ni lazima lifanye uinjilisti likiongozwa na upendo wa Kristo.
Fundisho:    Uhusiano wetu na Yesu uwe wa kwanza kuliko vitu vyote, mfano Mke, watoto, kazi, nk.

BARUA KWA KANISA LA SMIRNA Kanisa lililoteswa –2:8-11
Lengo la 3:  Eleza hali na mistari ya Kanisa la Smirna.
§  Mji huu wa Smirna ulichukua jina kutokana na manukato yaitwayo Myrrh.ambayo yalikuwa ni manukato maalumu kwaajili ya kuandaa mazishi ya mtu aliyekufa manukato ya aina hii ndiyo yaliletwa na mamajusi kwa zawadi kwa Bwana Yesu kama unabii wa maziko yake, Smirna Ulikuwa mji  mzuri na ajiri katika Asia ya Kati
§  Ulikuwa na Wayahudi wenye nguvu na wapinzani wa Injili. Kanisa hili katika Historia ya kanisa wakati wa mateso hayo liliongozwa na Mchungaji aliyeitwa Polokapo ambaye alichaguliwa na Yohana kuwa Askofu wa Kanisa la Smirna Mchungaji huyo huenda alitiwa nguvu na waraka huu  kwani wakati aliposhkwa na kufikishwa mbele ya liwali na kuonywa kuwa alitakiwa tu kumkana na kumlaani Kristo ili kupata nafasi ya kuachiwa Huru asiliwe na simba, Yeye aliitunza Imani na alisema “Miaka themanini na sita nimemtumikia Kristo naye hajanitendea lolote Isipokuwa mema Nitawezaje basi kumlaani Bwana wangu na Mwokozi?” kwaajili ya maneno hayao alichomwa mto akiwa hai. Kumbuka maneno yale Uwe mwaminifu hata kufa name nitakupa taji ya Uzima Mstari wa 10.
§  Kanisa lilikuwa na watu maskini na wenye kupitia mateso.  Wayahudi walikuwa wanawatukana Wakristo. Tunajifunza kuwa Yesu anajua watu wake wako wapi na wanapitia halia gani na uwezo wao wa kuvumilia Mstari wa 8-9
§  Yeye anayetia moyo naye aliteseka na hatimaye alishinda anawatia moyo kuwa waaminifu na kutokuogopa.Yesu anaonya kuwa baadhi yao watatupwa gerezani wawe waaminifu mpaka kufa.
Fundisho:  Yesu Kristo anajua majaribu tunayopitia, anataka tuwe waaminifu na atatupa taji ya uzima.

BARUA KWA KANISA LA PERGAMO  Kanisa lillokosea – 2:12-17
Lengo la 4: Eleza hali na Historia ya Kanisa.
§  Mji wa Pergamo ulikuwa makao makuu ya kisiasa na dini katika Asia ya Kati.  Ndipo palikuwa pa kwanza kuanzisha kumwabudu Kaisari (kiti cha enzi cha shetani).
§  Ulikuwa mji wenye kuabudu miungu miungu kama Zeus na Athena iliabudiwa pia na likuwa mji wenye madawa au tiba za aina mbalimbali mungu Nyoka Asclepius aliyehudumiwa na makuhani alihusika na tiba, mji huu ulikuwa na maktaba kubwa yenye Vitabu 200,000 ulikuwa ni mi wenye kujaa maswala ya dini za kienyeji,zinaa, Falsafa na maswala ya elimu.
§  Yesu anajitambulisha kwa kuwa na upanga mkali maana yake anakosoa mafundisho potofu kulikuwa na makosa mawili ya kimafundisho,
a.       Fundisho la Balaam Mst 14 Hesabu 24;25-25;13 2Petro 2;15,16 Yuda1; 11-12 balaamu alishawishi watu kuabudu miungu na kujihusisha na uasherati wakati wa agano la kale na kuwakosesha watu wa Mungu
b.      Fundisho la Wanikolai Nicolaitans Mst 6,15 ni kundi lilofundisha kuwa hawapaswi kufungwa na sheria ya aina yoyote wako huru mbali na utumwa wa aina yoyote ilikuwa ni fundisho lisilojali maadili na mafundisho  hawakujali ni aina gani ya watu wanajiunga na kanisa walisema “Washinde watu ili uwatawale” wakatoliki walipoanza kanisa walichukua baadhi ya mafundisho ya wanikolai inasemekana hata kubadilishana wanawake ilikuwa Riksa ili kudumisha upendo wa ndugu.
§  Yesu analikosoa kwa kuwavumilia watu wenye Imani potofu.(Mafundisho ya Ballam – ibada ya sanamu na uzinzi- mafundisho ya Wanikolao uhuru usio na mipaka na zinaa).
§  Kanisa linasifiwa kwa uaminifu na kushikilia Imani. Na anamtaja mmoja ya watu waliokuwa waaminifu na kuuawa kwaajili ya ushuhuda wa Yesu Antipas Mst 13
§  Endapo watashinda wanaahidiwa
i.                     Mana iliyofichwa na jiwe jeupe
ii.                   Mana iliyofichwa ni Chakula cha kiroho na jiwe jeupe ni  kinyume cha jiwe jeusi ambalo humaanisha hukumu ambayo mtu huukumiwa na kutaabika waklati jiwe jeupe ni kwa maisha ya raha na maisha marefu
Fundisho:  Lazima waamini wasipinge imani potofu na mafundisho potofu.

BARUA KWA KANISA LA THIATIRA Kanisa lenye Tatizo –2:18-29
Lengo la 5:  Eleza hali na Historia ya Kanisa:
§     Kanisa lilikuwa katika mji wa viwanda vya nguo vya zambarau. Lydia alitokea hapa,Mji huu ulikuwa ni mji wa kibiashara , kilimo na eneo maarufu au zuri kwa ulinzi na Usalama  na kulikuwa na sifa za kiusalama na nguvu ya kijeshi nuo za rangi ya zambarau zilitengenezwa hapa Kumbuka matendo 16;14
§     Yesu anajitambulisha kama mwana wa Mungu akitokea katika utukufu wa Kiungu macho kama mwali wa moto na miguu kama shaba iliyosuguliwa sana juu ya maadui wake
§     Yesu alilisifu Kanisa kwa mambo manne – (upendo, imani, huduma, subira)
§     Yesu analikosoa Kanisa kwa kumridhia Mwanamke nabii wa uongo mwenye tabia za Yezebeli. Mstari wa 20,Yezebeli alikuwa mwanamke aliyeongoza taifa la Israel katika ukengeufu mkubwa 1Wafalme 16;29-34, alistawisha uasherati, uabudu sanamu, upagani, kumbua kuwa chachu kidogo huchachusha Donge zima 1Koritho 5;9.
§     Wakristo waaminifu watatawala mataifa na wanahaidiwa nyota ya alsubuhi.
Fundisho:  Yesu anachukia Kanisa likifumbia macho walimu wa uongoYesu anaahidi kuwashughulikia wote wafundishao uongo.

BARUA KWA KANISA LA SARDI Kanisa lililotazama nyuma - 3:1-6
Lengo la 6:  Elezea Historia na hali ya Kanisa:
§  Mji wa Sardi ulikuwa juu ya mlima kama kiasi cha futi 1000 juu katika njia kuu ya biashara.  Ulikuwa na ngome imara ya kijeshi  na tajiri, uliojengwa na Kaisari Tiberia.Raia walikuwa na usalama wa uhakika wakiamin kuwa mji wao ni wenye nguvuna ni vigumu kwa maadui kuuweza ni mi uliokuwa tajiri wenye kujulikana kwa vito vya thamani nguo n.k. mji huu ulikuwa umewekwa wakfu kwa mungu Artemis hivyo kulikuwa na ibada za kipagani
§  Yesu anajitambulisha kuwa anazo hizo Roho saba, kuonyesha kuwa anafahamu matendo ndani ya Kanisa. Watumishi wanawajibika kwake.
§  Kanisa linakemewa kwa kuonekana kwa jina liko hai, lakini ukweli limekufa.
§  Baadhi ya waamini yaani mabaki walikuwa safi, Mungu siku zote ana mabaki watu waaminifu.
Fundisho:  Kanisa linatakiwa kuwa hai Kiroho.
BARUA KWA KANISA LA FILEDEFIA Kanisa lililohubiri injili – 3:7-13
Lengo la 7: Eleza Historia na hali ya Kanisa
  • Kanisa lilikuwa katika mji uliojengwa na mfalme Pergamo. Ulichukua jina la mjenzi Akalus Phidadefia. Lilikuwa ni eneo lenye matetemeko makubwa ya nchi. Ulikuwa mji uliojawa na wanafalsafa,watu wa dini na zinaa, pia uliitwa mji wa ndugu wapendanao,Mfalme anawapenda ndugu zake hii ndio maana ya Philadelphus Filadelfia
  • Mji ulikuwa unakabiliwa na matetemeko na makao ya ibada ya kipagani. Uliitwa Athens ndogo.
  • Kanisa la mahali hapa lilikuwa na nguvu katika maswala ya kuhubiri injili na watu waliipokea injili na watu walikuwa waaminifu
  • Yesu analihaidi mlango uliofunguliwa.
  • Yesu analisifia Kanisa kwa mambo matatu.
    • Linazo nguvu kidogo
    • Limetunza Neno lake
    • Hawakulikana jina la Yesu.
  • Yesu analiahidi mambo manne:
    • Atawafanya kuwa nguzo katika Hekalu la Mungu
    • Ataandika jina jipya la Mungu juu yao
    • Ataandika juu yao jina la mji wa Mungu
    • Ataandika juu yao jina lako jipya.
Fundisho.  Kanisa linapaswa kuendelea kuhubiri injili.

BARUA KWA KANISA LA LAODEKIA  kanisa lenye mafanikio ya kimwili– 3:14-22
Lengo la 8: Eleza historia na hali ya Kanisa.
  • Kanisa lilikuwa katika mji tajiri kwa viwanda, nguo na maziwa, madawa na mabenki.
  • Mji huu uliopewa jina la malkia Laodekia mke wa mfalme Antioch ii aliyeitwa Laoduce ulikuwa na bomba la maji lililokuwa likisambaza maji kutoka katika chemichemi za maji ya moto kama miles 6 kutoka kusini mwa mji, maji hayo ambayo wanawake walipoyachota walifika nayo nyumbani yakiwa yamepoa au kuwa na uvuguvugu.
  • Jina Laodekia maana yake Popular Judgement au Popular Approval ikimaanisha kukubalika na watu, au kugfahamika sana, Kanisa la mahali hapa lilikuwa limetajirika katika maswala ya fedha na uchumi lakini kiroho walikuwa masikini,vipofu na uchi
  • Kanisa halina sifa njema Yesu analikemea kwa tabia ya uvuguvugu iliyo nayo na kulishauri kutubu.
  • Walifikiri kuwa wanaweza kujitosheleza, na  Yesu alikuwa amefungiwa nje, ni wazi kuwa kanisa la Laodikia linawakilisha kanisa la siku za mwisho kihistoria ambalo litakumbwa na ukengeufu mkubwa , pamoja na kuwa na mafaniko ya kiuchumi na utajiri wa vitu
§  Fundisho:  Yesu hapendi mtu vuguvugu anataka mtu aamue kumfuata yeye au hapana.kuwa moto au kuwa vuguvugu.
               
                HALI TATU ZA KIROHO:
1.       Hali ya moto - Mwamini mwaminifu aliyejitoa kikamilifu kwa Bwana. Ameokolewa na anamfuata Yesu Kristo kwa kila neno.
2.       Hali ya uvuguvugu –Ni mtu aliyeokolewa lakini hajafikia kiwango cha Kristo na Injili yake, Anashika baadhi ya mambo ya Mungu.
                3.    Hali ya Ubaridi - Mtu anaishi kama ulimwengu hana hamu ya mambo ya   kiroho na Mungu.
MASWALI:
  1. Orodhesha sifa zilizotolewa na Yesu kwa kila Kanisa.
  2. Orodhesha udhaifu unaotolewa kwa kila Kanisa.

MAMBO AMBAYO HAYANA BUDI KUWAKO BAADA YA HAYO:

·         KUNYAKULIWA KWA KANISA
·         KITI CHA ENZI CHA MUNGU
·         WAZEE ISHIRINI NA NNE
·         WENYE UHAI WANNE
·         KITABU CHENYE MUHURI SABA.

SEHEMU YA 3: MAENDELEO YA MATUKIO KATIKA SIKU YA MWISHO: KANISA NA DHIKI KUU:

MAANA YA USEMI “BAADA YA HAYO” – 4:1.
Lengo la 1: Eleza maana ya usemi huu:
§  Usemi huu unatokana na neno la Kigriki “Meta tauta” Metatauta likiwa na maana ya yale yatakayotokea baada ya kipindi cha Kanisa.
§  Ni wazi kuwa sura ya nne mstari wa kwanza unazungumzia maswala yatakayo kuwa sio tu baada ya Yohana kupelekwa katika maono mengine zaidi bali kunyakuliwa kwa kanisa na maandalizi kwaajili ya dhiki kuu.
§  Ni wazi pia kuwa tendo la kunyakuliwa kwa Yohana mwenyewe katikia ulimwengu wa kiroho na kuwa mbinguni kunawakilisha wazi kunyakuliwa kwa kanisa ili aonyeshwe maswala ambayo kanisa litayashuhudia wakiwa pamoja na Mungu mbinguni.Neno kanisa limetajwa mara 19 katika sura za nyuma  na halitajwi tena baada ya hapo hii ikiwa na maana wazi kabisa kuwa kanisa litatengwa na dhiki kuu kwani Yesu atalinyakua mapema
§  Ujio huu wa Kristo kulinyakua kanisa utakuwa wa aina yeke na utawashangaza wengi kwa sababu kuu mbili
i.                     Jinsi atakavokuja na kulinyakua kanisa
ii.                   Namna anavyoishi hata sasa kuwa alikufa na sasa yu hai.
§  Wayahudi wengi walikuwa wamechanganya unabii huu wa kuja kwa Yesu mara ya pili na ule ujio wa kwanza wao hawakona sana ule ujio wake wa kwanza bali huu wa pili
§  Na hata leo wengi wanapuuzia swala la kunyakuliwa kwa kanisa wakiupuuzia unabii huu ambao utajitokeza mapema kidogo kabla ya ujio huo wa mara ya pili.

Tofauti ya Kunyakuliwa kwa Kanisa na ujio wa Yesu mara ya pili.
Kunyakuliwa kwa kanisa
Ujio wa yesi Kristo mara ya pili duniani
§  Itakuwa ni mawinguni kama mwivi
§  Ni duniani kila jicho litamuona
§  Ni maalumu kwaajili ya kanisa
§  Yesu na kanisa lake Kwa ajili ya ulimwengu
§  Kwaajili ya kufarji na hukumu ya watakatifu
§  Kwaajili ya kuhukumu ulimwengu na kutawala
§  Atanyakua watu wake 1Koritho 15;51-58,1Thes 4;13-18
§  Kila jicho litamuona Ufunuo 3;3,16;15
§  mawinguni
§  Duniani mlima wa mizeituni.

§  Kristo atakuja mawinguni kwaajili ya watakatifu atakuja kama mwivi
§  Mara ya pili anarudi duniani na watakatifu kuitawala dunia
§  Uthibitisho wa kibiblia kuhusu unyakuo
Luka 21;34, 1Koritho 15;51,52
Makusudi ya kunyakuliwa kwa kanisa
Moja ya kusudi kubwa la kunyakuliwa kwa kanisa ni pamoja na hukumu ya watakatifu na baadaye kutolewa kwa taji za thawabu za aina mbalimbali kulingana na kazi aifanyayo kila mtu, Yesu atakaa juu ya kiti cha hukumu kiitwacho Bema kwa kiyunani yaani mahali palipoinuka Kama jukwaa wakaapo au akaapo Mgeni rasmi kwaajili ya kumtunuku washindi wa medal mbalimbali baada ya ushindi katika michezo,Bema inafanana na kiti cha hukumu na ni hukumu lakini hukumu isiyo na madhara, Wakati wa “Bema” kazi ya kila mtu aliyeokoka aliyoifanya katika kumtumikia Mungu itajaribiwa kwa moto ili ipate kufahamika thawabu ipi atakayopata (I Wakoritho 3: 13- 15). Ikiwa kazi aliyoifanya mtu ni ya thamani kama dhahabu, fedha au mawe ya thamani, itakapopitishwa katika moto, itazidi kung’aa na wengine wote watashangilia pamoja na malaika. Ikiwa kazi aliyoifanya mtu ilikuwa duni itakapopitishwa katika moto itateketea kama miti, majani au manyasi, na itakuwa nia aibu ingawa mtu ataendelea kuweko mbinguni, atakuwa kama mhalifu msalabani, bila kuwa na taji yoyote.
Hukumu ni nini?
Mjadala kuhusu Hukumu ni mjadala mpana sana Neno hukumu au Judgement katika kiingereza na Kiswahili lina maana kubwa kama ilivyo katika kiyunani pia wayunani wana maneno makuu mawili yanayotumika kuzungumzia hukumu liko neno KrimaKrima" Na pia neno lingine ni KrinoKrino" neno lile Krima la kiyunani lina maana ya kufanyiwa sawa na ulivyofanyaau kuadhibu, na neno la pili Krino lina maana ya Kufikiri nini kinafaa, kutoa uamuzi baada ya kufikiri kwa kina, kuamua au kutoa uamuzi wa mwisho. Neno Krima linaweza kutumika katika maeneo yote yanayohusu mwanadamu aliyeokoka kwa wanadamu wenzake mfano usilipe ubaya kwa ubaya, au usiadhibu au hukumu ya adhabu Warumi 8; 1. na neno Krino linaweza kutumika katika mtazamo wa uamuzi wa Mungu kwa ujumla tunaweza kufafanua neno hukumu katika mitazamo zaidi ya kumi.
1.       Hukumu ni uamuzi unaokuja mwishoni na kutangazwa mahakamani baada ya kusikilizwa kwa kesi Legal verdict
2.       Hukumu ni Tangazo la deni, wajibu, cheti, au barua inayomwajibisha mtu kwaajili ya jambo Fulani Obligation resulting from verdict.
3.       Hukumu ni uamuzi wa Hakimu au jaji  ni uamuzi wa haki unaotolewa kama hitimisho la kukata mjadala na uamuzi huo hufikiriwa kuwa ndio wa mwisho Decision of Judge
4.       Ni mawazo yanayotengeneza uamuzi ili kuondoa swala lenye utata au linaloleta mijadala Decision on disputed matter
5.       Ni uwezo wa kutengeneza wazo linalokubalika na kuingia akilini na kutenda sawa na kilichotegemewa au kisichotegemewa kwa jambo lililoleta utata.Discernment of good sense.
6.       Wazo litolewao baada ya kufikiri kwa kina snap judgement/Opinion
7.       Makadirio yanayofanyika baada ya uchunguzi au yanayofanyika kutegemeana na uchunguzi estimate based on Observation.
8.       Kutoa mapendekezo juu ya jambo Fulani Judging of Something
9.       Malipo ya uamuzi wa kimungu unaotokana na wajibu au matendo au tabia Divine Punishment.
10.   Ni tendo la kutoa taarifa au uamuzi unaokubalika kiakili, ulio sawa unaoeleweka au usioeleweka sawasawa na jambo Fulani Act of making statement.
Kwa msingi huo tunapozungumzia hukumu ni muhimu kufahamu kuwa tunazungumzia jambo pan asana na tunapozunghumzia hukumu ya watakatifu neno linaloweza kutumika ni Krino na sio Krima Kristo atakaposimama katika Kiti cha hukumu kiitwacho Bema atakua anafanya hukumu iitwayo Krino ni hukumu isiyo na madhara lakini itashangaza sana watu kwa kuwa inafanywa na Mungu mwenyewe katika mtazamo wake na usio wa kibinadamu.

1.       TAJI ISIYOHARIBIKA (INCORRUPTIBLE CROWN) 1 KORITHO 9: 23- 25, 2 TIMOTHEO 2: 4- 6.
Taji hii   watapewa watakatifu ambao walifanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine. Walijizua yote katika utoaji wao kwa ajili ya Injili, walijizuia yote katika maombi yao kwa ajili ya Injili na pia walitumia vyote walivyo navyo, muda, ujuzi vipawa cheo chao, uwezo wao wote n.k kukishiriki Injili pamoja na wengine.
2.       TAJI YA KUJIONEA FAHARI ( CROWN OF REJOICING) 1 WATHESALONIKE  2: 19, DANIEL 12: 3
Taji hii inaitwa taji ya kujionea fahari kwa sababu watakaoipata taji hii watang’ara kama nyota tofauti na wengine watakavyong’ara. Fahari yao itakuwa kubwa kuliko yaw engine. Mng’ao wao wa utukufu utakuwa mkubwa kuliko wengine. Taji hii watapewa wale waliowaleta watu wengi kwa Kristo kutokana na kushudia kwao au kuhubiri Injili. Washuhudiaji wale waliozaa watoto wengi katika injili yao ya mtu kwa mtu au vinginevyo na wakawaongoza mahali ambapo watakuzwa kwa mafundisho na kuwa watenda haki.
3.       TAJI YA UZIMA (CROWN OF LIFE) UFUNUO 2: 10.
Taji hii ni kwa wale waliopita katika mateso au mitihani mikubwa ya maudhi na kuchikiwa kwa ajili ya Kristo na wakashinda. Hawakupenda maisha yao kufa (Yakobo 1: 2, Ufunuo 12: 11. Mathayo 5: 11- 12, Waebrania 11: 24- 26, Zaburi 129: 2)
4.       TAJI YA HAKI (CROWN OF RIGHTEOUSNESS) 2 TIMOTHEO 4: 6- 8.
(a)    Taji hii ni kwa wale waliopenda kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Wakati wote moyoni walisema “Amina na uje Bwana Yesu” Walikuwa katika utakatifu wakati wote. Kila neno walilojifunza walilitendea wokovu kidogo, hivyo hivyo mpaka alipokua Yesu akawakuta katika hali ya kutubu.
(b)   Taji hii watapewa wale ambao wanachukua muda wao kuwafundisha watoto wachanga wengi wa kiroho mpaka wanakua. Namna yoyote ya kumsaidia mtu kujifunza, itakupa thawabu hii – kumuazima au kumpa vitabu au kaseti za mafunzisho mwenzio, kumpa nauli ili aende kwenye mafundisho , kazi  ya kudumu kanisani- kubeba watoto au kufanya lolote ili watu wawe na raha ya kujifunza n.k
(c)    Taji hii watapewa wale ambao wanawahudumia mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji, na Waalimu ili wapate urahisi wa kuzifanya kazi zao.
MLANGO UKAFUNGUKA MBINGUNI – 4:2
Lengo la 2: Eleza juu ya maoni ya kuwa tendo la Yohana kuchukuliwa toka duniani kupitia mlango uliofunguliwa kwenda mbinguni kunahusiana na unyakuo wa Kanisa.
§  Yohana alisikia sauti ya Yesu Kristo, Yohana anaambiwa “panda hata huku” mara moja.  Mambo yanabadilika mbinguni.
§  Kunyakuliwa kwa Yohana 4:1-2 kunaonekana kuwakilisha kunyakuliwa Kanisa kabla ya dhiki Kuu.  Hii inadhihirisha ya kuwa Kanisa litaondolewa kabla ya dhiki kuu.
§  Pia neno Kanisa halitumiki baada ya sura ya 3 hadi 22.

UPEKEE WA DHIKI KUU:
Lengo la 3: Eleza kwa nini dhiki kuu ni jambo la pekee katika historia ya Binadamu duniani.
§  Dhiki kuu ni tukio la pekee katika historia katika dunia, kwa sababu ni dhiki pekee ambayo inaitwa siku kubwa ya hasira ya Mungu.
§  Hakujawahi kuweko wala haitajuja iweko dhiki iliyo kuu kama hiyo katika Historia ya dunia
UNYAKUO WA KANISA –(1Thess. 4:11-13)
Lengo la 4: Eleza mambo yatakayotokea wakati wa kunyakuliwa Kanisa.
§  Tunaamini Kanisa litanyakuliwa kabla ya dhiki kuu, kwa sababu hatusomi neno lolote “Kanisa” kutoka Ufu. 4:1-22. Hivyo Kanisa halitapitia katika dhiki kuu (1Thes. 5:9).  Mambo mawili yatatokea wakati Yesu anakuja kwa mwaliko mkuu kutoka mbinguni- Baragumu Italia:
(a)    Kwanza, wafu waliolala katika Kristo watafufuliwa.
(b)   Pili, walio hai watabadilishwa na kunyakuliwa pamoja na wafu waliofufuliwa kumlaki Bwana hewani.
N.B: Yesu ataleta roho za waliokuwa katika Bwana pamoja naye ili kuungana na Miili iliyofufuliwa.

MANENO YANAYOTUMIWA KATIKA KUJA KWA YESU:
Lengo la 5: Eleza maana ya maneno ya Kigriki yanayotumiwa, maneno ni:
§  HARPADZO - Kunyakua kwa nguvu 
§  EPIPHANELA - Mng’ao
§  PAROUSIA  - Kuja mwenyewe.
MAJADILIANO YA MWASWALI MATATU KUHUSIANA NA SIKU ZA MWISHO (Mt. 24:3)
§  Mathayo haelezi jinsi Yesu alivyojibu maswali, Bali Luka anaelezea majibu.  Siku za mwisho zitaambatana na usaliti, wakristo wa uongo, chuki na mateso kwa waamini.  Pamoja na kurudi nyuma kwa watu, Injili itahubiriwa duniani pote.
§  Yesu alielezea matukio ambayo yangetokea mara moja na yale yangetokea baada ya muda mrefu katika taifa la Wayahudi hasa kuangamizwa kwa hekalu na mji wa Yerusalemu.  Alieleza.
§  Anaelezea na dalili zitakazoonyesha kuja kwake.
        Mt. 24:2-14 – Yesu anaelezea mambo yatakayotokea kabla ya Kanisa kunyakuliwa:-
*      Manabii na wakristo wa uongo watakaowadanganya watu wengi.
*      Kuongezeka kwa vita, njaa na matetemeko yatakuwa mwanzo wa utungu.
*      Mateso yataongezeka zaidi kwa waamini na wengi wao wataacha imani.
*      Vurugu, uhalifu na kuasi sheria za Mungu kutaongezeka.
*      Injili ya Kristo itahubiriwa duniani pote.
§  Mt. 24:42-44 - Hakuna ajuaye saa ya Yesu kuja kunyakua Kanisa. Siku itakuja ghafla kwa waamini na wasioamini.
§  Mt. 24:15-28 - Yesu anaelezea matukio yatakayotokea wakati wa kipindi cha dhiki ambayo waliookoka wakati huo watayaona kabla ya Yesu kurudi mara ya pili.
*      Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Danieli
*      Kutokea kwa manabii na wakristo wa uongo watakaowadanganya hata wateule.
*      Taabu na dhiki kubwa
*      Jua na Mwezi kutiwa giza na nyota kuanguka.
*      Yesu atarudi mara ya pili.
§  Mt. 25:1-13 – Mfano wa Wanawali Kumi:
*      Huu mfano unaonyesha unyakuo utawajia ghafla waamini waaminifu na wasio waaminifu. Yesu anatuasa kuwa hatangojea kanisa lote lijiandae.Hivyo kila mwamini anatakiwa kujiandaa kwa kuishi maisha matakatifu na kuwa na Uwepo wa Roho Mtakatifu.
§  Mt. 25:14-30  - Mfano  wa  Talanta:
*      Hapa Yesu anatueleza kanuni muhimu zitakazoamua nafasi ya mwamini katika ufalme wa mbinguni.  Nafasi na thawabu zitategemea jinsi ulivyojitoa kwa Bwana na Ufalme wake.
§  Mt. 25:31-46 – Hukumu ya Kondoo na Mbuzi:
*      Kondoo -ni watu waliookoka na wako hai wakati wa dhiki kuu.
*      Mbuzi – ni watu waovu waliosalia wakati wa dhiki kuu.
§  Hukumu inahusiana na :-
*      Kutenganishwa kwa watu waliookolewa na watu waovu.
*      Na matendo ya upendo na huruma kwa wale walioteseka kwa ajili ya Yesu.
*      Waovu watatupwa katika ziwa la moto na wenye haki watakuwa raia katika ufalme wa Mungu.
ANAYEZUIA NA MPINGA KRISTO:
Lengo la 6: Mtambue anayezuia uovu na mpinga Kristo:
§  Walimu wa uongo wamekuwa wanawaambia Wathesalonike kuwa siku ya Bwana imekwisha pita.  Hivyo waliamini kuwa wameachwa.
§  Mambo mawili ambayo lazima yatokee kabla ya dhiki kuu:
o   Uasi mkuu utatokea
o   Mpinga Kristo atatokea.
§  Roho Mtakatifu akitenda kazi kupitia Kanisa ndiye anazuia uasi na Mpinga Kristo.
§  Mwovu atakuja katika mamlaka kwa njia ya udanganyifu na kufanya miujiza.  Hivyo watu wengi watampokea kwa sababu ya kukataa kweli.
§  Jinsi tunavyoendelea mwisho wa nyakati uasi na uovu unaongezeka.  Utafikia kilele wakati wa mpinga Kristo.

MASWALI:-

1. Kunyakuliwa kwa Yohana kwenda mbinguni kunawakilisha nini?
2. Taja mambo mawili yatakayotokea wakati wa kunyakuliwa kwa Kanisa.
3. Katika waraka wa Wathesalonike Paulo anasema yupo azuiaye kutokea kwa mpinga
    Kristo. Huyo ni nani?
4. Ni mambo gani Yesu anaelezea katika sura zifuatazo:-
(a)    Mt. 24:4-14
(b)   Mt. 24:42-44
(c)    Mt. 24:15-28

MWENYE KITI CHA ENZI MBINGUNI – 4:3
Lengo la 1 : Mtambue mwenye kiti cha Enzi mbinguni.
Mwenye Kiti cha Enzi mbinguni ni Mungu mwenyezi. Anayeishi katika utukufu akiwa amezungukwa na viumbe vinavyomwabuudu.  Upinde wa mvua ulikizunguka Kiti unaonyesha Ahadi za Mungu.
MAELEZO KUHUSIANA NA WAZEE ISHIRINI NA NNE  - Ufu. 4:4
Lengo la 2: Elezea na kuwatambua wazee Ishirini na Nne (Ufu. 4:4)
Wazee wamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani mwao wanaonyesha ni watu waliokombolewa kwa sababu wao wametajwa kwa mara ya kwanza katika Ufunuo 4;4, 10 na kisha tena katika 5;8,14 na niwazi kuwa popote wanapotajwa wanawakilisha watakatifu wa agano jipya walionyakuliwa na sio malaika jina linalotumiwa kuwaita wazee hao kwa kiyunani ni Presbuteros ambalo kwa akawaida halitumiwi kuzungumzia malaika :-
§  Mavazi meupe ni kwa ajili ya watu waliokombolewa Ufunuo 5;11-14.
§  Taji za dhahabu wanapewa waliokombolewa baada ya kumshinda shetani-3:3
§  Kufuatana na Ufu.21:12-14 – ukuta wa Yerusalemu una milango 12 yenye majina ya makabila 12 ya Israeli na misingi 12 yenye majina ya mitume 12.
§  Hakuna katika Biblia ambapo malaika hutajwa kama wazee.
§  Kutokana na Ebr. 11:39,40 na Ufu. 21:12-14 inaonekana wazee hao huwakilisha watakatifu wa Agano la Kale na A/Jipya.
VITAMBUE VIUMBE HAI WANNE – 4:6-11
Lengo la 3: Eleza viumbe.
§  Viumbe hai wanne vipo kwa ajili ya kusifu Mungu mwenyezi.  Inawezekana viumbe hivi vinawakilisha viumbe wote. Viumbe vyote vitaleta utukufu na heshima mbinguni wakati vitakapokombolewa kutoka katika laana.Neno la kiyunani linalotumika kuwataja viumbe hao ni “Zoa” ambalo linaweza kutafasiriwa kama Mnyama, au walio hai, au viumbe na ni tofauti na neno lle mnyama linalotrumika katika maeneo mengine kama Ufunuo 13;18, 14;9-11, 15;2, 16;10 viumbe hawa ni wa kipekee na ni tofauti sana na wengine kama Makerubi, Maserafi na ni tofauti na wale wazee na wanaonekana kufanya huduma maalumu sana licha ya viumbe hao kuhisiwa kuwa wanawakilisha falme za wanyama wote yaani wa kufugwa wa porini wa anagani n.k pia huisiwa kuwakilisha mfumo wa injili zile nne katika kumuelezea Yesu Kristo.

UFUNGUO
MATHAYO

MARKO
LUKA
YOHANA
WASOMAJI
WAYAHUDU

WARUMI
WAYUNANI
KANISA
INJLI YA
UFALME

MATENDO
HEKIMA
UFUNUO
KIINI
YESU NI MFALME WA WAYAHUDI

YESU NI MTUMISHI MWAMINIFU WA MUNGU
YESU NI MWANA WA ADAMU
YESU NI MWANA WA MUNGU
ISHARA YA
SIMBA ishara ya nguvu na ufalme na UBWANA UFALME WA YESU

NG’OMBE alama ya utumishi uvumilivu na unyenyekevu
UTUMISHI WA YESU
 MWANADAMU Ishara ya Hekima ufahamu na utii
UANADAMU WA YESU
TAI Ishara ya ujasiri uungu asili ya mbinguni
UUNGU WA YESU

KITABU KILICHOTIWA MHURI - Ufu. 5:1.
Lengo la 4: Eleza maana ya kitabu hiki.
§  Kitabu hiki kina umuhimu sana kwa sbabu kina ufunuo wa Mungu kuhusiana na mambo yatakayokabili dunia na mwanadamu katika siku zijazo. Kinaelezea jinsi watu watakavyohukumiwa, ushindi wa Mungu na watu wake juu ya uovu.  Kila muhuri unapovunjwa jambo hutokea.
YESU KRISTO MWANAKONDOO ANAYESIFIWA – 5:6-14
Lengo la 5: Eleza maana ya Mwanakondoo aliyechinjwa.
§  Kristo anaonekana kuwa ni Mwanakodnoo aliyechinjwa.  Hii inaonyesha kujitoa kwake pale msalabani (Kalvari) kwa ajili ya dhambi za watu.  Ni kitambulisho cha kustahili, nguvu, mamlaka na ushindi wa Yesu juu ya msalaba.
§  Pembe Saba zinaonyesha nguvu na uwezo wa mtawala.
KUFUNGULIWA KWA MIHURI SITA – 6:1-17.
Lengo la 6: Taja vitu vinavyotokea baada ya kufungua mihuri sita.
§  Watu wengi wasioamini kuwa Kanisa litapitia katika dhiki kuu wanaamini kuwa kufunguliwa kwa mihuri ni mwanzo wa dhiki kuu.
§  Mhuri wa Kwanza- Mpanda farasi mweupe mwenye uta kinywani ni Mpinga Kristo.
Ufunuo 6;1-2 Daniel 7;8,23, 26, 8;8-10,20-25, 11;35-45,Wathesalonike 2;1-12 Ufunuo 13;1-18, 17;10-16. Mpinga Kristo ni kiongozi atakayekuwa na usahawishi mkubwa kwa dunia kama mtu mwenye majibu ya matatizo ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii Yeye atakapotokea atakuwa na nguvu ya kuzishawishi serikali kwa pamoja  na kueleta jibu la amani kwa Dunia anaonekana kuja katika farasi mweupe ili kumuigiza Kristo lakini Yeye siye mfalme wa mani hata kidogo lakini mpango wake ni kuiondoa amani yote iliokuwa imesalia  Yesu atakuja akiwa amepanda farasi mweupe lakini Hatakuwa na uta alma ya kivita kama aliyokuja nayo mtu huyu  Ufunuo 19;11-21 mpinga Kristo kuwa na uta ni Ishara ya uovu ona Zaburi 46;9 na Yeremia 49;35

§  Mhuri wa Pili- Farasi mwekundu anawakilisha vita na vifo vya kutisha.
Ufunuo 6;3-4 Mathayo 24;6-7 ni wazi kuwa hii ni hatua ya kujidhihirisha kwa moyo wa mpinga Kristo kwani kuja na Farasi mweupe kulikuwa na maana ya amani lakini amani hiyo sio ya kudumu  roho ya ukatili ya kushindana na kushinda inajifunua  ni wazi kuwa dunia itashuhudia umwagikaji mkubwa wa Damu ambao ni wa kutisha sana Farasi huyu atakuwa na nuvu ya kuiondoa amani duniani watu watauana hii itakuwa hali ambayo haijawahi kutokea au kuonekana duniani vinginevyo isingelipewa nafasi ya kuwamo katika dhiki hii kuu

§  Mhuri wa Tatu- Farasi mweusi unaonyesha njaa na ukame wa kutisha.
Ufunuo 6;5,6, Mathayo 24;7. Maandiko anapozungumza juu ya tukio la kupimwa kwa mkate au shayiri au nafaka ni wazi kuwa inazungumzia njaa ona 2Wafalme 7;1 na Ezekiel 4;10-17 ni wazi kabisa kuwa wakati wa dhiki ile kutatukia njaa halisi ambayo haijawahi kutukia katika Historia ya njaa duniani  njaa ya aina yoyote ambayo umewahi kuisikia au kuishuhudia ni mfano tu wa njaa kuu itakayoikumba dunia ya wakati wa dhiki kuu
       
§  Mhuri wa Nne - Farasi wa kijivu  akiwakilisha vita, njaa, tauni na hayawani Mauti na Kuzimu
Ufunuo 6; 7-8. Mathayo 24;7 ni wazi kuwa Tatizo linaendelea kuwa kubwa farasi huyu anawakilisha mauti na kuzimu huku vita , njaa na mengineyo yakiwakilisha aina za vifi vitakavyotokea wakati wa dhiki ile kuu ni wazi kuwa Robo ya watu watakufa vitani kwa upanga , njaa  ama kukosekana kwa chakula  na kuuawa na wanyama au hayawani wa inchi kwani njaa hii itawasumbua na wanyama wa mwituni ambao kwaajili ya kujikimu hawataogopa kuingia katika makazi ya watu  na kujiratia kitoweo hili halipendezi lakiini limeruhusiwa kwaajili ya kutimiza hukumu kubwa ya Mungu dhidi ya wanadamu wanaoikataa neema . Kumbuka kuwa muhuri hzi nne zitakuwa zikimwagwa kwa robo ya dunia ya wakati huo na sio ulimwengu mzima tunaoufahamu
§  Mhuri wa Tano - Watakatifu waliouawa wakiwa mbele ya Kiti cha Enzi. (chini ya madhabahu)
Ufunu 6;9-11,Mathayo 24;8-28 Ni wazi kuwa maonao haya yanaonyesha kuwa kuna watakatifu kadhaa ambao wataokolewa au roho zao kupokelewa mbinguni hata hivyo hili sio jambo la kutia moyo hata kidogo,Hawa ni watu ambao wataokolewa kwaajili ya kuuawa kwaajili ya Neno la Mungu na Ushuhuda wao watakuwa wamegharimika kwa kiwango cha kutisha sana , ni wazi kuwa roho zao zitalia kwaajili ya kisasi cha adui na watesi wao ni wazi kuwa ni gharama kwa mkristo kutarajia wokovu wakati wa dhiki kuu
§  Mhuri wa Sita - Tetemeko kubwa linalotikisa ulimwengu mzima Hasira ya mwanakondoo.
Ufunuo 6;12-17 Mathayo 24;29,30. Muhuri huu unaonyesha jinsi Kristo alivyo na nguvu kuu na kuwa Yeye ni mtawala juu ya yote na kuwa watu wote wanatambua nguvu na mamlaka kubwa aliyonayo na wanatambua ghadhabu aliyonayo mwana kondoo na kutafuta kujisitiri ingawa wanamtambua kama mwana kondoo wakati huu ni kwa sababu tu ya hofu kubwa waliyonayo lakini ni wazi kuwa wao walimpinga kwa muda mrefu na sasa wanalazimika tu kumuogopa mwanadamu hata akiwa na nguvu kubwa sana ni dhaifu sana mbele za Mungu.
MASWALI:                        
1. Je, Wazee Ishirina na nne ni akina nani?
2. Taja matukio yanayotokea kila muhuri unapofunguliwa. (Ufu. 6:1-17)

MATUKIO KATIKATI YA DHIKI KUU NA KUENDELEA: Ufunuo 7;1-17
Lengo la 1: Eleza matukio – dhiki kuu hadi mbingu mpya.
§  Kufungua mihuri saba na Baragumu saba miaka 3 na nusu ya kwanza.
§  Vitasa saba katika miaka 3 na nusu ya mwisho
§  Ufufuo wa Watakatifu
§  Utawala wa miaka 1,000
§  Hukumu ya mbele ya Kiti Cheupe.
§  Mbingu mpya na nchi mpya.
MALAIKA WANNE NA MALAIKA ANAYETIA MUHURI – 7:1-3
Lengo la 2: Eleza sababu za kutiwa muhuri wa 144,000.
Malaika wanne wanazuia upepo, na kuidhuru nchi.  Malaika mwingine anatokea kwa ajili ya kuwatia muhuri watumishi wa Mungu.  Lengo la kutiwa muhuri 144,000 ni kuwapa ulinzi wakati wa hukumu inapotolewa ili kwamba majeshi ya pepo waovu yasiwadhuru.Swala hili linafanyika kati ya muhuri le wa sita na kabla kidogo ya muhuri ule wa saba  kusudi ikiwa ni kuwalinda wateule  au mabaki  katika Israel.
WATU 144,000 - 7:4.
Lengo la 3: Eleza ni akina nani 144,000 kutoka makabila kumi na mbili.
§  Hawa ni Wayahudi watakaomwamini Kristo wakati dhiki kuu kutoka kabila 12 za Israeli.  Muhuri vipajini pao ni kuonyesha kuwa ni mali ya Mungu na watalindwa na Mungu kutokana na hukumu yake.
144,000 –WATAMBULIWA – 7:5-8.
Lengo la 4: Eleza sababu zinazofanya makabila mengine yameondolewa:
§  Majina ya Dani na Efraimu hayamo katika orodha ya makabila ya Israeli.  Hii inawezekana kwa sababu makabila haya yaliongoza taifa katika ibada za sanamu na uasi.
MKUTANO MKUBWA WA WALIOVAA MAVAZI MEUPE - 7:9-17.
Lengo la 5:  Eleza umuhimu wa watu hawa waliovaa nguo nyeupe (Ufu.7)
§  Hawa ni watu walioamini wakati wa dhiki kuu. Wametoka katika kabila duniani.  Watanyakuliwa mwishoni mwa dhiki kuu na kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo.  Ukweli huu unaonyesha watu wataokolewa wakati wa dhiki kuu.

Wazee 24
Mkutano Mkubwa
Wameketi Vitini
Wamesimama mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu
Wana Taji
Hawana Taji
Wana vinubi na vyelezo
Wameshika matawi ya mitende.

MALAIKA ALIYE NA CHETEZO CHA DHAHABU – 8:3,4
Lengo la 6 : Eleza ni nani malaika mwenye chetezo.
§  Muhuri wa Saba unafunguliwa kunakuwa na ukimya.  Hapa haijulikani maana yake.  Malaika aliye na chetezo ni Yesu Kristo kwa sababu katika A/Kale, makuhani peke yao walifukiza uvumba kuwaombea watu.  Katika A/Jipya Yesu Kristo ndiye kuhani mkuu, mpatanishi kati ya Mungu na watu.
TARUMBETA  au BARAGUMU  SITA  - 8:6-9:21
Lengo la 7: Eleza ni matukio gani yatakayotokea wakati wa kupigwa tarumbeta  Sita.
§  Tarumbeta ya 1 – Mvua ya mawe, moto, Damu Ufunuo 8;7.
Theluthi 1 ya miti na mimea ya nchi itateketea, bila shaka swala hili litaongeza njaa ambayo ilikuweko tangu kufunguliwa kwa Muhuri zile
§  Tarumbeta ya 2  Mlima unaowaka Ugfunuo8;8-9
Theluthi1 ya bahari kuwa damu na viumbe na meli Kuangamizwa, Bla shaka mlima huo wa moto ni kitu kama kimondo kiytakachoupwa juu ya bahari na theluthi ya viumbe vya baharini vitauawa na hivyo asili nyingine ya vitoweo au chakula kupungua, Biashara zitaathiriwa kwa kiwango kikubwa hasa kutokana na theluthi ya merikebu hukumu hii inatukumbusha hukumu ile iliyokuwa juu ya Inchi ya Misri wakati wa Nabii Musa.
§  Tarumbeta ya 3 – Pakanga , maji machungu Ufunuo 8;10-11
Theluthi 1 ya mito na chemchemi zitaathirika na watu wengi kufa hi ni kutoaka na kuanguka kwa nyota hii iitwayo pakanga mpinga Kristo pamoja na nguvu zake zote alizonazo atashindwa kutoa msaada  wakati watu watakapokuwa wanaangamia  kwa kunywa maji machungu.
§  Tarumbeta ya 4 – Giza kuu Ufunuo 8;12
Theluthi 1 ya jua ikapigwa, na 1 ya Mwezi na 1 ya nyota ili Theluthi itiwe giza ni wazi kuwa taa za ulimwenguni hazitakuwa na uwezo wa kudhibiti aina ile ya giza ambayo Mungu ataipiga kwa Dunia pigo hili pia latukumbusha uweza wa Mungu uliokuwa juu ya Nchi ya Misri ambayo nayo ilipigwa kwa Giza zito wakati wa siku za Nabii Musa.
§  Tarumbea ya 5 – Nzige wanaotesa Ufunuo 9; 1-12.
Majeshi ya pepo waovu kutesa watu wasio na muhuri wa Mungu kwa miezi mitano.inaonekana wazi kuwa Nyota  inayotajwa katika msatai wa Kwanza ni malaika ambaye alipewa funguo za kuzimu Hatuwezi kusema kuwa alikuwa ni malaika wa upande wa shetani kwani angewafungulia viumbe hao ili kuwatumia kwa maanufaa ya Ibilisi, lakini ni wakati wa kuruhusiwa kwa viumbe hao ambao watatesa na kuumiza watu hususani wale ambao hawana muhuri ya Mungu katika vipaji vyao, nzige hao wenye kutisha hata hivyo hawana mamlaka ya kuua isipokuwa kuumiza
§  Tarumbeta ya 6 – theluthi ya watu kuuawa Ufunuo 9; 13-15.
 Malaika wanne  walifunguliwa na kuuwa theluthi 1 ya watu bila shaka ni miongoni mwa malaika wale walioanguka  nguvu zao zinazidi zile za wale nzige kwani wao licha ya kudhuru pia wanaua kwa moto moshi na kiberiti  na kuuma kama nyoka wao wanaonekana kuwa viongozi wa jeshi la wapanda farasi wanaotajwa Mstari wa 16-19 wapanda farasi wapatao 200,000,000. Hata hivyo jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na mapigo hayo wanadamu waliosalia hawakuwa tayari kutubu dhambi zao Mastari wa 20-21 hii haina tofauti na wakati wa mapigo kule Misri ambapomoyo wa farao na watu wake ulikuwa mgumu.
§  Malaika mwenye nguvu Ufunuo 10;1-11;14
Lengo la 1  : Eleza ushahidi unaoweza kukusaidia kujua huyu malaika ni nani.
§  Ushahidi unatuonyesha kuwa huyu malaika mwenye nguvu ni Yesu ni huu ufuatao:-
§  Mwonekano wake ni  sawa na Yesu wa Ufunuo -  1:13-15
§  Kiapo chake anachoapa.Hakuna katika Biblia malaika aliyeapa.
§  Sauti yake kama simba aungurumapo.Biblia (Yoel. 3:16) inasema Bwana anaunguruma kama simba (Hosea 11:10, 11; Amosi 3:8) Usemi wa malaika “hapatakuwa na wakati baada ya haya” (Ufu.10:6-7).  Una maana kuwa yale yaliyokusudiwa hukumu juu ya uovu lazima utekelezwe.

*      Ni wazi kuwa malaika huyu mwenye nguvu ni Yesu Kristo mwenyewe kule kuvikwa winu kunatukumbusha lile tukio katika mlima wa ugeuko Marko 9;7 na pia wakati alipokuwa anapaa juu Matendo 1;9 pia ziko semi za Bwana mwenyewe akihusisha kurudi kwake na mawingu Mathayo 24;30 na nguvu na utukufu Yeye alisema Tangu sasa mtamwona mwana wa adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni Mathayo 26;64 pia usemi ule Tazama yu aja na mawingu Ufunuo 1;7
*      Ushahidi mwinne ya kuwa malaika huyu mwenye nguvu ni Bwana ni kuonekana upinde wa mvua ukiwa umemzungukakama alivyoona mapema Yohana katika Ufunuo 4;3 na ndivyo ilivyo kwa malaika huyu mwenye nguvu, pia inatukumbusha kuwa huyu ni Mungu mwenye kutunza maagano
*      Uso wake ulikuwa kama jua na miguu yake kaa nguzo ya moto hii ni sawa na kile alichokiona Yohana katika ufunuo 1;14-16 Yohana alipona mng’ao huo alianguka kama ilivyokuwa kwa Sauli wa Tarso malaika huyu alikuwa na kitabu kidogo ambacho yohana alikiona katika Ufunuo 5;1-4 ambacho kilimtia wasiwasi  na baada ya ufafanuzi tumaini Ufunuo 5;5-7,6;1. Ni wazi kuwa alikuwa Kristo mwenyewe mwana kondoo
*      Hakuna uthibitisho wa malaika ambaye alitumwa na Mungu na akaambatanisha kiapo, kuunguruma kwake kama simba ni wazi katika maandiko kulimaanisha Bwana mwenyewe Yoel 3;16,Hesea 11;10-11,Amosi 3;8. Ngurumo saba zilitokea wakati malaika huo alipotoa kilio cha Kwanza

§  YOHANA ATUMWA KUTOA UNABII - Ufu.10:8-11
Lengo la 2: Eleza maana ya Yohana kula kitabu kidogo.
Kitabu hicho alichokula Yohana kilikuwa na ujumbe uliokuwa unaeleza kukamilisha kusudi la Mungu kwa watu duniani.  Kilielezea mambo yatakayotokea.Kujua ujumbe kulikuwa kutamu kama asali, bali baadaye kulisababisha uchungu ndani ya moyo wa Yohana.  Hivyo Mungu anamwagiza akahubiri ujumbe huo ili watakaomwamini wapate uzima wa milele na wasioamini wapate kuhukumiwa.
MAELEZO ZAIDI KABLA YA BARAGUMU YA SABA – Ufu.11:1-14
Lengo la 3:  Eleza maana ya kupimwa kwa hekalu na mahusiano yake ni miezi 42.
1.       Kulipima Hekalu – 11:1,2:
Kupimwa kwa hekalu na madhabahu na kuhesabiwa kwa wanaoabudu kunamaanisha kuwa Wayahudi watajenga hekalu lao.  Kutokana na Agano lao na mpinga Kristo watakuwa na uhuru wa kuabudu.  Katikati ya dhiki kuu mpinga Kristo atavunja agano na kulinajisi hekalu.  Kipindi cha miezi 42 ambacho ni miaka 3 na nusu mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa, mpinga Kristo atawatesa na kuwaua Wayahudi waaminifu.  Mwisho wa miaka 3 na nusu utakamilisha mwisho wa kipindi cha mataifa.
2.       Mashahidi wawili  - 11:3-14
Lengo la 4:  Eleza kusudi la Mashahidi wawili, uwezo wao, matokeo ya ushuhuda wao na ni akina nani.
        Mashahidi wawili watatokea ambao watahubiri Injili kwa uwezo mkubwa huku wakileta hukumu na mapigo kwa wale wanaowapinga.  Watahubiri Injili kwa muda wa siku 1260.  Baada ya kumaliza ushuhuda watauawa na mpinga Kristo ambaye atakuwa amepona jeraha lake.  Miili yao italazwa mitaani na kushuhudiwa na watu kwa njia ya Televisheni.  Baada ya siku tatu,na nusu watafufuliwa na kupaa, matokeo yake kutakuwa na tetemeko kubwa la ardhi litakaloua watu 7000.
Mashahidi wanadhaniwa na wanatheolojia kuwa ni Henoko na Eliya kwa sababu hawakuonja mauti walitwaliwa mbinguni.
Sifa za mashahidi wa nyakati za dhiki kuu.
Mwanzo 5;24, Zekaria 4;10-14 Malaki 4;5-6 Waebrania 11;5 Kuna hisia za watu watatu wanaokisiwa kuwa mashahidi wa siku za nyakati za dhiki kuu watu hao ni pamoja na Eliya,Henoko na Musa hata hivyo kulingana na sifa za kimaandiko wanaokisiwa wanapaswa kuzifikia ni pamoja na
*      Mashahidi hao watatokea mbinguni Mstari wanne 4
*      Watapewa nguvu za kupita kawaida ambazo wasingeweza kuwa nazo na sio lazima wawe wamekuwa nazo katika wakati uliopita Mstari 3-10
*      Watahubiri na kufanya unabii kwa miaka mitatu na nusu wakiwa wamevikwa magunia  Mstari wa 3
*      Wao ndiyo ile mizeituni miwili na vile vinara mbele za Mungu wa mbinguni mstari wa nne
*      Wao ni lazima wawe ambao hawajawahi kufa na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa ni hukumu Waebrania 9;27
*      Wao watauawa katika barabara na kukaa hapo kwa siku tatu na nusu ndipo watanyakuliwa Mstari wa 7-12.
§  Kazi kubwa n ya mashahidi hawa ni kuionyesha dunia hii iliyoharibika uweza na nguvu za Mungu, hakua mtu atakayeweza kuwazuia wala kuwaua mpaka watimize huduma yao
§  Baada ya kukamilisha kazi mnyama  atokaye kuzimu atafanya vita nao na kuwashinda na kuwaua
§  Maadui wa Mungu watafurahi na miili yao itaachwa bila kuzikwa juu kwa siku tatu ili kuwaaminisha watu kuwa wamekufa kwelikweli na watasheherekea na kupeana zawadi
§  Hata hivyo furaha yao itakuwa ya muda mfupi kwani watafufuliwa na kisha kunyakuliwa juu ni wazi kuwa kupitia huduma yao watu wengi mmno wataokolewa wakati wa dhiki kuu.
Fundisho:  Mtumishi wa Mungu ataondolewa ikiwa amemaliza kazi.
§  Tarumbeta ya 7 – shetani anafukuzwa Ufunuo 11;15.
Sauti kutoka mbinguni kuwa ufalme ni wa Mungu bara gumu hii inalia katikati yaq kipindi cha dhiki kuu au katikati ya juma la sabini la nabii Daniel chini ya baragumu hii kuna matukio kadhaa yanajitokeza
KUPIGWA KWA BARAGUMU YA SABA - 11:15-19
Lengo la 5: Eleza mkazo wa baragumu lasaba.
Mkazo wa baragumu ya saba ni tangazo la kuwa falme za ulimwengu zimekuwa ufalme wa Yesu Kristo.  Pia inaonyesha kuwa hukumu inakaribia kumalizika, “kufunguliwa kwa Hekalu la Mungu mbinguni na sanduku la agano kuonekana hekaluni mwake”, ina maa lengo la agano ambalo ni ahadi ya ufalme linakaribia kutimizwa.  Mungu anatunza ahadi ya neno lake. Matetemeko ni dalili ya kuja kwa mwisho.
MWANAMKE NA JOKA.
MWANAMKE ALIYEVIKWA JUA – 12:1-6,13-16.
Lengo la 6: Eleza na kumtambua huyu mwanamke aliyevikwa jua na elezea na Kukimbia kwake:
Ishara 1:               Mwanamke huyu ni taifa la Israeli lenye makabila kumi na mbili ambamo Masihi anatokea kwake.Mwanzo 27;9-11,Isaya 54;5-10,Yeremia 3;1-14,Hosea 2;14-23,3;4-5,Mika 5;3 Zekaria 12;10,Warumi 11;25-27 Mathayo 24;15-22. Ni wazi kuwa mwanamke huyu sio kanisa hata kidogo, Mtoto mwanamume ni wale wayahudi 144,000hawa wanaitwa wazaliwa wa kwanza kwa Mungu na mwana kondoo
Ishara 2:               Joka lenye vichwa saba na taji maana yake ni shetani katika nguvu zake. Nyoka mbinguni ni malaika waasi aliofukuzwa nao kutoka mbinguni.  Mtoto aliyenyakuliwa ni Yesu Kristo aliyezaliwa na kufufuliwa na kupaa kwenda mbinguni.  Naye atatawala mataifa. Mwanamke alikimbia maana yake katikati ya dhiki kuu Israeli wanakimbia kutoka Utawala wa mateso ya mpinga Kristo.  Israeli atakimbilia Perta huko katika nchi Ya Yordan, na kuhifadhiwa kwa muda wa miaka 3 na nusu.  Hawa Waisraeli ni Uzao utakaosumbuliwa (Ufu. 12:13-17)
Mabaki ya mji wa wa Petra Kiyunani au Sela Kiibrania ambao ulikuwa chini ya serikali ya Edomu kama ngome zake zinavyoonekana leo huko ng’ambo yam to Yordani inaaminika kuwa ni katika mji huu Israel  wengi watakimbilia huko na kujificha Picha na maelezo kwa hisani ya Maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.
MASWALI:
1.       Ni ushahidi gani unaotuonyesha kuwa huyu malaika ni Yesu Kristo?
(a)    ________________________
(b)   ________________________
(c)    ________________________
2.       Nini matokeo ya ujumbe wa mashahidi wawili (11:3-14)
3.       Baragumu ya saba inaashiria nini?
4.       Taja ishara zilizomo katika Ufu. 12:12.
JOKA NA VIBARAKA VYAKE. 12:3-4.,7,9,13;2-4 16;12,20;2.
Lengo la 1: Mtambue joka na shughuli zake.
Huyu anajulikana kama shetani, joka la zamani la Ibilisi.  Majina yana maana gani?:-
§  Joka la zamani – mdanganyifu – Mwa. 3:1-13
§  Ibilisi - Mjaribu, mwenye hila, mpingaji – Mt. 4:1; Efe. 6:11;
§  Shetani - mshitaki – 1Pet 5:8; Zek 3:1
VITA MBINGUNI - Ufu. 12:7-12;  17:7-18
Lengo la 2: Eleza vita hivyo mbinguni.
§  Wakati wa dhiki kuu hakutakuwa na mapambano ya kiroho duniani tu, bali hata mbinguni kutakuwa na vita mbinguni.  Shetani na malaika zake watapigana na Mungu na malaika.  Shetani atatupwa chini na kutoruhusiwa mbinguni. Akiwa na hasira na akijua ana muda mchache anafanya vita na Waisraeli waaminifu walioko Israeli wanashindwa na kutetewa na Mungu.Hivyo anawaudhi mabaki wa uzao ambao Wayahudi waliotawanyika duniani waliomwamini Yesu Kristo.
MNYAMA ALIYETOKA BAHARINI MPINGA KRISTO – 13:1-10
Lengo la 3:  Elezea asili yake, chanzo cha nguvu za mnyama.
§  Huyu mnyama ni mtumishi wa shetani, ni mwanadamu aliyetoka katika watu wa dunia.  Baadhi ya wanatheolojia wanasema ni falme saba ambazo zimesumbua taifa la Israeli yaani-Misri, Syria, Babeli, Umedi na Uajemi, Ugriki na Rumi.  Pembe kumi ni viongozi kumi watakaotawala pamoja na mpinga Kristo kwa muda mfupi.
§  Atatawala kwa nguvu na mamlaka kwa muda wa miezi 42. Atakapofufuka au kupona jeraha lake atataka watu wote wamwabudu.  Atawatesa na kuwaua watakatifu wengi. Kutokana na uwezo aliopewa shetani atawaunganisha watu kupigana na Mungu.
§  Ni wazi kabisa kuwa  mnayama huyu ndiye mpinga Kristodamiel 7;8,11,20-25,8;23-27,11;36-45,2Thesalonike2;7-8,Isaya 14;4-17,Mathayo 24;15,Ufunuo 13;1-10,17;8,11. Huyu atakuwa ni mwanadamu kabisa ambaye ata kuwa ameasi na kujitoa kabisa kwa shetani ni mwana wa upotevu 2Wathesalonike 2;3 hata pamoja na nguvu atakazo kuwa nazo ufalme wake hauta kuwa ni wa dunia yote yeye atahusika na eneo la Rumi ya kale  atazitiisha nchi za Uyunani,uturuki na Misri kati ya zile dola kumi za Rumi iliyofufuka  na nyingine zinzjitolea tu kwake Daniel 7;8 Makao makuu ya kwanza ya Mpinga Kristo yatakuwa Babel na kisha atahamia Yerusalem kulingana na Isaya 14;4-11
MNYAMA KUTOKA KATIKA NCHI NABII WA UONGO - 13:11 -18
Lengo la 4 :  Elezea kuhusiana na mnyama wa pili.
§  Huyu mnyama anaonekana kama mwana-kondoo, lakini anasema kama joka.  Hii ina maana atajidai mpole, mwenye upendo na kujali, lakini tabia yake ni ya kishetani.  Huyu ataanzisha kanisa la uongo ambalo litamwabudu mpinga Kristo.  Atafanya miujiza minngi na kuwafanya watu wamwabudu mpinga Kristo. Watauwawa wale watakaopinga amri hiyo na kuwa waaminifu kwa Yesu Kristo.
NAMBA, JINA NA ALAMA YAKE – 13:16-18
Lengo la 5:  Jadili alama ya mnyama na umuhimu wake.
§  Ili kuwadhibiti wamwabudu mpinga Kristo atatumia silaha ya kiuchumi.  Wote wanaotaka kununua na kuuza wawe na namba au jina la mpinga Kristo pajini pa uso au mkononi.  Hivyo namba hiyo itawafanya watu wamkubali au wampinge mpinga Kristo – wasomi wengi wanahangaika kutafuta jina la mpinga Kristo lakini wanapingana.
§  Alama – Ufunuo 13;16 alama hii itakuwa halisi inayoweza kuonekamna kwa urahisi katika mkono wa kuume au kwenye paji la uso
§  Jina – Ufunuo 13;17 kuwa na jina la mnyama inawezekana kabisa kuwa ni kuwa na kitambulisho maalumu chenye saini yake ambacho kitahitajika kwa ajili ya huduma mbalimbali gharama ya kitambulisho hicho itakuwa nibei ya nafsi na roho na kuwa kila atakayepokea atalazimika kuapa na kuwa mwaminifu kumuabudu mpina kristo
§  Hesabu yake – Ufunuo 13;18 alama yake ni sita ,sita ,sita 666 hii ikimaanisha kuwa ni uthibitisho kuwa yeye ni mwanadamu mwanadamu mwanadamu kupokea chapa hii ni sawa na kukubali kumuabudu  Ufunuo 14;9-10. Jipu baya litamwagwa kwa wale watakaoipokea lama hiyo na mfululizo wa kumwagwa kwa vitasa utaanza
KAHABA MKUU - 17:1-6
Lengo la 6: Elezea kweli mbili kuhusu kahaba na mambo yake katika siku ya mwisho.
§  Huyu kahaba anawakilisha dini zote za uongo.  Katika Biblia kahaba ni mtu anayemwasi Mungu na kuabudu miungu mingine.  Hivyo kahaba huyu ataikana Imani na Injili ya Yesu Kristo. Hili ni kanisa la uongo litakalomsaidia Kristo kupata madaraka.  Litashiriki katika kuwatesa watakatifu.  Dini na siasa itatumika kutawala mataifa.  Baadaye mwishoni mpinga kristo atalichukia hili kanisa la uongo.  Hivyo ataiangamiza  tasisi hii.
UNABII WA SIKU ZA MWISHO  - Dan. 9:24
Mambo sita yatakayokamilishwa katika majuma sabini ni:-
§  Kumaliza makosa
§  Kukomesha dhambi
§  Kusamehe uovu
§  Kuleta haki ya milele
§  Kutia muhuri maono na unabii
§  Kupaka mafuta mahali patakatifu kabisa.
1. MWANAKONDOO NA 144,000 juu ya mlima sayuni  – 14:1-5
Lengo la 7:  Zitambue kweli kuhusiana na utambulisho na tabia za 144,000:           
§  Hali ya 144,000 ni wasafi kiroho, wamekombolewa kutoka duniani wameandikwa vipajini mwao jina la Baba na wanamfuata Bwana.Hawa ni watakatifu ambao hawakujinajisi na uchafu wa dhambi na ibada ya mpinga Kristo wala hawajawahi kusema uongo.Hawa ndio watakao uimba wimbo wa Mwanakondoo.Watakuwa wamechaguliwa miongoni mwa watakatifu walionyakuliwa kwenda mbinguni kabla ya dhiki kuu. 
2. TANGAZO LA MALAIKA WATATU – 14:6-13
Lengo la 8:  Jadili kwa kifupi yaliyomo katika matangazo ya malaika watatu.
§  Malaika wa kwanza anawataka watu wote duniani wamche Mungu kwa sababu saa ya hukumu imefika.
§  Malaika wa pili, anatangaza kuanguka kwa Babeli – yaani mifumo ya siasa, dini na uchumi ya dunia imefika kikomo.
§  Malaika wa tatu, anawaonya watu wanaokubali kupokea chapa watateswa katika ziwa la moto milele.
§  Wale watakaokufa katika Bwana watakuwa heri, kwani watapumzika taabu zao (mateso na kwenda kwa Bwana).
3. MAVUNO YA DUNIA - 14:14-20
Lengo la 9: Eleza mahusiano ya mavuno na shinikizo la divai.       
§  Mavuno haya yanahusiana na hukumu.  Mavuno ya zabibu ni dunia na shinikizo la divai linahusiana na ghadhabu ya hukumu ya Mungu, itakayowafikia wakazi wa dunia.  Ni umwagikaji wa damu wa kutisha.
MASWALI:
1.       Nini maana ya majina haya:
(a)    Joka la zamani ________________________
(b)   Ibilisi ________________________________
(c)    Shetani ______________________________
2.       Mpina Kristo atakapotoka atafanya nini?
3.       Nabii wa uongo atamsaidiaje mpinga Kristo?
4.       Kahaba mkuu ni nani?
5.       Namba ya mnyama 666 itatumikaje?
6.       Nini tabia za 144,000 walio pamoja na mwanakondoo? (Uf. 14:1-5)


MATUKIO YA MWISHO WA DHIKI KUU:
MAANDALIZI YA VITASA SABA.
1.       ISHARA KUU YA TATU –Ufu. 15:1-8
Lengo la 1:  Itambue ishara kuu ya tatu. Eleza umuhimu wake.
§  Ishara kuu inayotolewa hapa ni ya malaika wenye vitasa saba ambayo ni mapigo ya mwisho.  Ishara mbili zingine ni: Mwanamke aliyevikwa jua (Ufu.12:1) na Joka kubwa jekundu lenye pembe kumi na vichwa saba (Ufu. 12:3).  Ishara kuu ya tatu ni ya muhimu kwa sababu inahitimisha hasira na hukumu ya Mungu.
2.       KUMWAGWA KWA VITASA VYA GHADHABU YA MUNGU – 16:1-21
Lengo la 2: Eleza vitasa saba vinawakilisha nini na athari juu ya wanadhamu:

§  Kitasa 1:       Madonda mabaya na majipu ya kuumiza yawapata wanadamu walio na Alama ya mpinga Kristo. 16;2 ni pigo linalowahusu wale tu waliopokea alama ya Yule myama na sio kwa dunia nzima
§  Kitasa 2:       Viumbe hai vyote baharini vinakufa.16;3
§  Kitasa 3:       Mito na chimchemi za maji zageuka damu 16;4
§  Kitasa 4:       Jua likawaunguza wanadamu 16;8-9
§  Kitasa 5:       Giza kubwa juu ya utawala wa mpinga Kristo 16;10-11
§  Kitasa 6:       Vita vya Harmagedonia.16;12
§  Kitasa 7:       Ngurumo na tetemeko Babeli na miji ya mataifa yaangushwa. Visiwa na milima ikatoweka, mvua ya mawe kubwa ilinyesha. 16;17-21
Matokeo ya mapigo haya watu waliendelea na mioyo migumu na kumtukana Mungu.

KAHABA MKUU (Babel ya siri) – 17:1-18

§  Kahaba mkuu ni mji ule mkuu ulio na mamlaka juu ya wafalme wote.  Hii itakuwa ni Kanisa la uongo ambalo litakuwa na nguvu ya ushawishi kwa viongozi mbalimbali duniani, katika miaka 3 na nusu ya mwanzo ya dhiki kuu itamsaidia mpinga Kristo ili kupata madaraka.  Lakini mpinga Kristo atakapopata nguvu na kufufuka au kupona jeraha lake atafanya hila ya kumwangamiza.  Wakati wa kipindi cha miaka 3 na nusu ya mwisho mpinga Kristo atataka kuabudiwa na wote.  Hili kanisa la uongo litashiriki katika kuwaua watakatifu watakaopingana naye.
PEMBE KUMI - 17:10-15
Lengo la 3:  Elezea juu ya pembe kumi:
§  Mstari wa 10 unazungumzia wafalme saba, watano wameanguka na mmoja bado.  Watu wanaamini kuwa ni falme za Misri, Ashuru, Babeli, Uajemi na Umedi, Ugriki iliyokuwa bado kuanguka ni Rumi.  Wa saba unakuja ni jumuiya ya mataifa kumi.  Mpinga Kristo atakuwa ni mfalme wa nane.  Pembe kumi ni mataifa kumi yenye nguvu za kisiasa na watamsaidia mpinga Kristo na kupingana na Yesu Kristo.
KUANGUKA KWA BABELI NA MIFUMO YA KISIASA NA KIUCHUMI:
                HUKUMU YA BABELI - 18:1-24
§  Mji wa kisiasa na kiuchumu wa Babeli unatafsiriwa na wasomo kuwa unawezekana ni mji halisi ambao ni makao makuu ya mpinga Kristo.  Pia unafikiriwa kuwa ni mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa mwanadamu.
§  Maangamizi ya Babeli yanaonyesha kuanguka mifumo ya kisiasa na kiuchumi iliyotokea katika historia yote ya mwanadamu kama tulivyosoma katika Dan. 2 na 7, lazima mifumo ya falme za dunia hii kubatilishwa na kuondolewa ili ufalme wa Kristo uje.
§  Mungu ndiye suluhisho la matatizo yote ya kijamii na kiuchumi ambayo yamesababishwa na dhambi ya mwanadamu.
§  Mifumo ya kidunia na mpinga Kristo wataangamizwa.
KUJA MARA YA PILI KWA YESU:
SHUKRANI KWA AJILI YA HUKUMU JUU YA BABELI.-Ufu. 19:1-5
Lengo la 4:  Wataje wale wanaotoa sifa kwa Mungu mbinguni na kiini cha sifa zao.
§  Wale wanaotoa sifa na shukrani ni umati wa watu wengi, wazee ishirini na nne na viumbe hai wane – Mungu anawatia moyo.
§  Kiini cha sifa kwa wale wanaomsifu Mungu mbinguni ni
*      Kuangusha uasi wa shetani na hukumu ya haki ya Mungu
*      Tabia na asili ya Mungu chanzo cha ukombozi.
*      Kuanzishwa kwa ufalme wa Mungu katika historia ya mwanadamu.
HARUSI YA MWANA-KONDOO – 19:6-10
Lengoo la 5: Elezea karamu ya harusi ya Mwanakondoo na vazi la Bibi Harusi
§  Karamu ya Harusi ya Mwanakondoo inatangazwa katika Maandiko, ila haielezwi kwa undani.
*      Ni wakati wa kuunganika kwa Yesu Kristo na watu wake
*      Itafanyika katika wakati ambao Mungu amefanya
*      Wale tu walioalikwa watahudhuria Harusi hiyo, wale waliookolewa.
*      Mavazi ya Bibi Harusi ni matendo mema ya watakatifu.  Kukaa na kumtii Yesu Kristo.
KUFUNULIWA KWA MASIHI  - 19:11-21
Lengo la 6: Elezea wajibu wa Masihi aliyepanda farasi mweupe.
§  Yesu Kristo ni wakala wa ghadhabu ya Mungu na tumaini la waamini.  Yesu anamwaga hukumu juu ya waovu, lakini wakati huo ni chanzo cha faraja na utukufu kwa watu wake wanaoshuhudia utawala wa haki.  Yesu anakuja mara ya pili pamoja na watakatifu wake.  Anakuja akiwa mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana, Anakuja akiwa jemadari kuanzisha kweli na haki, kuhukumu mataifa na kufanya vita dhidi ya uovu.
*      Kuwatawala kwa fimbo ya chuma – maana yake kuwaangamiza mataifa.
*      Anakanyaga shinikizo la mvinyo – maana yake hukumu ya kutisha.

KARAMU YA MUNGU - 19:17-18

Lengo la 7:  Elezea karamu ya Mungu.
§  Hii ina mahusiano na vita ya Har-Magedonia, Mungu atawaangamiza watu waovu wengi wakati wa vita hivyo kiasi kwamba watahitajiwa ndege wala nyama wengi ili kusafisha uwanja wa vita.  Hii ni kwa sababu itakuwa vigumu kuzika watu.

HUKUMU YA MPINGA KRISTO NA NABII WA UONGO – 19:19-21

Lengo la 8: Elezea hukumu ya wanyama wawili waovu.
§  Mpinga Kristo atakusanya majeshi yake ili apigane na Bwana Yesu na majeshi yake.
§  Majeshi ya mpinga Kristo yatashindwa vibaya, mpinga Kristo na Nabii wa uongo watatekwa na kutupwa ziwa la moto.
§  Majeshi au watu waliopigana wakiongozwa na mpinga Kristo waliuawa.
MASWALI:
1.       Taja matukio yanayotokea wakati wa vitasa saba
2.       Kuanguka kwa Babeli kuna maanisha nini?
3.       Nani watakuwepo katika karamu ya Harusi ya Mwana kondoo?
4.       Nini hatma ya mwisho ya mpinga Kristo na nabii wa uongo?

UFALME WA KRISTO WA MIAKA ELFU NA ULIMWENGU UJAO:

MIAKA ELFU:
KUFUNGWA KWA SHETANI – 20:1-3
Lengo la 1:  Orodhesha mojawapo ya hali ya kiroho itakayokuwepo wakati Wa miaka elfu. Kwa nini kutakuwa na mafanikio?
§  Mojawapo ya hali ya kiroho ambayo itakuwepo wakati wa utawala wa miaka elfu ni ya kutokuwepo kwa udanganyifu hapa duniani.  Hii ni kutokana na kufungwa kwa shetani huko kuzimu kwa kipindi chote cha miaka elfu.
UFUFUO WA KWANZA – 20:4-6
Lengo la 2:  Taja watakaohusika katika ufufuo wa kwanza.
§  Kwanza kuna watakatifu watakaofufuliwa kabla ya dhiki kuu. Pili ni kundi la waamini watakaofufuliwa baada ya dhiki kuu ili kutawala pamoja na Kristo.  Hawa ndio walioteswa na kuuawa wakati wa dhiki kuu.  Watashiriki katika kutawala pamoja na Kristo.

MAONI MBALI MBALI KUHUSIANA NA MILLENIA:
Lengo la 3: Eleza maana ya Millenia na kueleza maoni mbali mbali.
Neno Millenia linatokana na lugha ya Kilatini likiwa na maana ya miaka 1,000. Sasa kuna maoni mbali mbali kuhusiana na millennia, nayo ni:-
  • Post Millenialism - Yesu atakuja wakati ulimwengu umejiandaa Kumpokea
§  Amillenialism - Hakutakuwa ufalme wa miaka elfu wakati wa kurudi kwa Yesu mara ya pili.
§  Premillenialism - Ulimwengu utakabiliwa na utawala wa Masihi- Yesu wa kipindi cha miaka elfu wakati Yesu atakaporudi  mara ya pili (Ufu.20) unasema kurudi kwa Yesu  mara ya pili kutafuatiwa na kufungwa kwa shetani  kuzimu na ufufuo wa wenye haki ambao watatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu.

HALI KATIKA UTAWALA WA MIAKA ELFU:
Lengo la 4: Eleza hali na maisha yatakayokuwepo wakati wa millennia.Mambo haya yatakuwepo katika kipindi hiki:-
Mwana simba atakaa pamoja na mwana kondoo kwa amani wakati wa utawala wa Yesu Kristo Duniani.
§  Amani duniani pote hapatakuwepo na vita wala jujifunza vita (Zab. 46:9; Isa. 2:4; 9:6-7; Mika 4:3-4)
§  Maendeleo makubwa ya kiuchumi – (Isa. 65:21-24; Amo.9:13-15; Mika 4:4-5)
§  Haki itatawala (Isa. 11:13-15; Yer. 23:5)
§  Watu wote watamjua Bwana (Isa.11:9; Habak.2:14; Zek.8:21-23)
§  Wanyama waondolewa ukali, watakula majani (Isa. 11:6-9; 65:25)
§  Nchi itarudishwa hali yake ya kwanza na kuzaa sana (Isa. 35:1,2; Amo. 9:13-15; Eze.36:8-12)
§  Maisha marefu (Isa.65:20-22)
§  Mabadiliko ya dunia ya kupokea mwanga wa jua na Mwezi (Isa.30:26)
Lengo la 5:  Taja wakazi wa ufalme wa miaka elfu.
§  Kutakuwa na aina mbili ya watu: Kwanza watakatifu waliokuja na Yesu ambao watatawala pamoja na Kristo.  Pili, ni watu wenye miili hii ya kawaida ambao walikuwa waaminifu wakati wa dhiki kuu na wale watakaozaliwa wakati wa miaka elfu . (Mt. 25).
BAADA YA MIAKA ELFU.
UASI WA MWISHO WA SHETANI - Ufu. 20:7-10
Lengo la 6:  Eleza sababu za shetani kufunguliwa na matokeo yake.
§  Shetani atafunguliwa kutoka gerezani baada ya miaka elfu ili awajaribu watu waliozaliwa wakati wa millennia.  Hii itawkuwa nafasi yao ya kuchagua kumtii mungu au shetani.  Watu wengi watamfuata shetani na kuizingira kambi ya watakatifu.  Kabla ya kuishambulia kambi, moto utashuka kutoka mbinguni na kuwangamiza. Shetani atatupwa katika ziwa la moto.

HUKUMU YA MWISHO MBELE YA KITI CHEUPE- 20:11-15
Lengo la 7:  Eleza kweli kuhusiana na hukumu ya mwisho.
Katika wakati huu watu wote waovu watafufuliwa na kusimama mbele ya kiti cheupe ili kuhukumiwa.
  • Mtu asiyeandikwa jina katika kitabu cha Uzima atahukumiwa.
  • Wote waliomkataa Yesu na wokovu wake watatupa katika ziwa la moto wa milele
  • Mauti na kuzimu zilitupwa katika ziwa la moto.
Jehanam ni moto mkali usiozimika kamwe, tanuru la moto ambako watu watasaga meno na kuomboleza.  Pia hii ndio mauti ya pili (Mt. 22:13; 25:30; 13:42,50; Mk. 9:43)
MPANGO MPYA - Ufu. 21-22
1.       MBINGU MPYA NA NCHI MPYA – Ufu. 21.
Lengo la 8: Eleza maana hasa ya mbingu mpya na nchi mpya.
§  Kulingana na somo hili ina maana ya kuwa mbingu na nchi ya sasa zitaondolewa.  Baada ya kuja mbingu mpya na nchi mpya (Isa. 51:6; 2Pet.3:7,10-12).  Nchi ya sasa inaondolewa kwa sababu imechakazwa na kunajisiwa na dhambi.  Nchi mpya haina bahari.
2.       YERUSALEMU MPYA – 21:2-22:5
Lengo la 9: Eleza jinsi mji ulivyo:
  • Mji huu unaitwa ni Bibi Harusi kwa sababu Mungu atakaa pamoja na watu wake.
  • Mji una milango 12 ambayo inawakilisha taifa la Israeli.  Pia una misingi 12 ambayo inawakilisha kanisa.  Hii ni kuonyesha umoja wa watakatifu wa A/Kale na A/Jipya.
  • Mji ni mraba wenye mapana, marefu na wimo sawa wa maili 1,500.  Ukionyesha kuwa utakuwa na makao ya kutosha ya watakatifu wote wa vizazi vyote.  Pia mji unajawa na utukufu na utakatifu wa Mungu.
  • Mji hauna hekalu kwa sababu Mungu na Mwanakondoo ndio hekalu lake.
  • Hakuna usiku katika mji huo
  • Barabara zake ni za dhahabu.
  • Kulingana na Wanatheolojia, mji huu utakaliwa na watakatifu wote kabla ya dhiki kuu.- yaani walionyakuliwa kabla ya dhiki kuu na wale watakaofufuliwa baada ya dhiki kuu.
  • Nchi mpya itakaliwa na watu wote ambao waliishi katika ufalme wa miaka elfu na walimkataa ibilisi na ushawishi wote. Inasemekana watakuwa mataifa wanaongozwa na wafalme.  Wafalme hao wataenda Yerusalemu kumtukuza Mungu kwa yale anayofanya katika nchi mpya (Ufu. 21:24-26)
  • Wakazi wa mji wa Yerusalemu ni washindi waliovumilia taabu na adha mbali mbali
  • Hawa hawataingia katika nchi hiyo:
  • Waoga ambao wanaogopa kumkiri na kumfuata Yesu Kristo Aliye hai (Mk. 8:35; 1Thess. 2:4)
  • Wasioamini – hawa ni pamoja na wakristo ambao wameanguka dhambini.
  • Waamini wote wanaosema wanamfuata Yesu, lakini wanaishi katika dhambi (1Kor. 6:9,10; Efe. 5:5-7; Gal. 5:19-21)
  • Hawa wote watatupwa katika ziwa la moto
  • Watakatifu watamwona uso wake – hili ndilo lengo la historia ya ukombozi.  Watamwona Yesu Mwanakondoo kwani wataishi naye. (Mt. 5:8; 1Yh. 3:2)
  • Mti wa Uzima ambao ni halisi unaonyesha mfano wa Roho Mtakatifu na Uzima, baraka na nguvu za kiroho zitokazo kwa Mungu. (Isa. 44:3; Yn. 7:37-39).

HITIMISHO - 22:6-21
Lengo la 10:  Eleza mambo muhimu yaliyomo katika Hitimisho;
1.       Anathibitisha kuwa unabii  huu ni wa kweli kwa sababu umetolewa na Bwana wa roho za Manabii ambaye aliwaongoza Manabii kunena
2.       Yesu anasema anakuja upesi na amebarikiwa yule atakayezingatia Unabii huu.
3.       Kila mtu atapokea kulingana alivyotenda hapa duniani.
4.       Baraka ni kwa wale wanaoshika amri zake ambao watapewa haki ya kuuendea mti wa uzima na kuingia mji wa Yerusalemu mpya.
5.       Watu waovu wanaosema uongo na wauaji watatupwa katika ziwa la moto wa milele
6.       Roho Mtakatifu na Bibi Harusi (Kanisa) wanafanya kazi ya kuwaalika watu kupokea Neno la wokovu.
7.       Kuna hukumu juu ya watu ambao wanachagua sehemu Fulani na kuziacha zingine katika unabii huu.  Hivyo hivyo kwa wale wanaongezea mawazo yao juu ya Neno.
8.       Yohana anaitikia kuwa uje Bwana hii inamaanisha:
(a)    Wakristo wa kweli wanaomba na wanahamu ya kurudi kwa Bwana kwani ndipo ukombozi wetu utakamilika.
(b)   Siku ya kurudi Yesu imekaribia ambapo atarudi katika utukufu wake.Je, mpendwa uko tayari kunyakuliwa?
MASWALI:
1.       Taja matukio mbali mbali yatakayotokea kabla ya Yesu Kristo kutawala?
2.     Eleza maana ya millennia kuhusiana na maoni ya:
(a)    Post millennialism _______________________
(b)   Amillennialism __________________________
(c)    Premillennialism ________________________
3.       Mambo gani yatakuwepo wakati wa utawala wa Kristo wa miaka elfu moja?
4.       Jehanam ni nini?
5.       Eleza kwa kifupi kuhusiana na mbingu mpya na nchi mpya.