Jumatatu, 25 Desemba 2023

Hata ulipowadia utimilifu wa wakati !


Wagalatia 4:4-5 “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.”

 


 

Utangulizi:

Leo ni sikukuu ya Christmas, wakristo wote Nchini wanaungana na wakristo wengine duniani kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikotokeza zaidi ya miaka 2000 iliyopita huko Bathelehemu, Israel. Katika wakati huu ni muhimu kujikumbusha kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo hakukutokea kwa bahati mbaya kwani Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulitokea kwa wakati mkamilifu, katika mpango wa Mungu, watu wengi wanaweza wasielewe umuhimu wa Yesu kuzaliwa kwa wakati,  na ikawa kwao kama watu ambao walikuwa na shughuli nyingine wakati Yesu anazaliwa wasijue kuwa mwokozi amekuja kwaajili yao, Kuzaliwa kwa  Yesu Kristo huu ulikuwa ni mpango kamili wa Mungu, na ulitekelezwa ulipowadia utimilifu wa wakati, tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

·         Hata ulipowadia utimilifu wa wakati!

·         Kukombolewa kwa waliokuwa chini ya sheria

·         Kupokea hali ya kuwa wana

 

 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati.

Wagalatia 4:4-5 “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.”

Neno Utimilifu wa wakati katika Biblia ya kiyunani linasomeka kama “Pleroma - Chronos”. Pleroma ikiwa na maana ya Kujaa kabisa, au kukamilika completion or Filled, na Chronos ni Time  kwa hiyo utimilifu wa wakati kwa kiingereza Fullness of the time  yaani ni kama mtu aliyekuwa anakijaza chombo kwa muda maalumu, kisha kikajaa, au muda uliokusudiwa kwa kitu Fulani kutimia, kwa hiyo Kiswahili kilichotumika hapo ni sahihi na chepesi zaidi ya mafafanuzi sawa tu utimilifu wa wakati, Kwa hiyo Kuzaliwa kwa Yesu Kristo hakukutokea tu kwa bahati mbaya, bali kulitoka kwa wakati mtimilifu ambao Mungu alikuwa ameukusudia katika mpango wake!.

Huu ulikuwa ni wakati utawala wa kiyunani ulikuwa umeisha na umeacha athari ya Lugha ya Kiyunani (Greek) na tamaduni kadhaa za kiyunani (Hellenistic culture), Lugha hii kwa wakati huo ilikuwa ni lugha ya kisomi na iliyotumiwa na wasomi wengi wa nyakati zile jambo lilolopelekea Maandiko kutafasiriwa na hata kuandikwa katika kiyunani kwani ulimwengu wa wakati huo ulikuwa ni ulimwengu wa kisomi sana na athari zake zilikuwa zimeachwa na Wayunani.

Warumi walikuwa sasa ndio wanaotawala ulimwengu wa wakati huo na walikuwa ni watu waliohakikisha Amani inakuwepo kila mahali duniani, na pia waliunganisha ulimwengu wa wakati ule kwa mifumo ya bara bara zilizorahishisha mawasiliano na ulinzi mkali uliohakikisha Amani inatawala kila mahali duniani, utaratibu na ustawi mkubwa sana wa kijamii (Pax Romana)

Wayahudi walikuwa na matazamio Makali ya kutimizwa kwa unabii hususani wa Daniel kuhusu majuma sabini,  na walikuwa tayari wamejiandaa kumpokea Masihi, wakielewa wazi kuwa wakati wowote masihi atazaliwa, ili awakomboe na kuleta faraja na kuondoa uchovu wa kukandamizwa na utumwa wa kigeni na utumwa wa sheria

Pia ulikuwa wakati ambapo watu wamechoshwa na kufilisika sana kiroho, wamefilisika kidini na kiimani, na walikuwa wameshindwa kabisa kuishi sawa na sharia ya Musa ambayo kwa wakati huu ilikuwa inaonekana kuwa ina viwango ambavyo wanadamu wa kawaida hawaviwezi, dhambi ilikuwa imewaelemea na wanyama wa kutekeketzwa kwaajili ya dhambi lilianza kuonekana kama jambo lisilowezekana tena

Ni katika wakati huu Ndipo Yesu anazaliwa, anazaliwa katika wakati ambapo watu walikuwa wamefilisika kiimani, kidini na kiuadilifu, uadui kati ya mwanadamu na Mungu ulikuwa umeongezeka sana, kwa hiyo kuja kwa Yesu na kuzaliwa kwake kwa wakati hasa wakati ambapo wanadamu wamechoka, ilikuwa ni kuleta auheni na unafuu mkubwa, kuleta neema na kutangaza rehema ulikuwa ni wakati sahihi kwa wanadamu kutangaziwa wokovu ambao wameusubiri kwa muda wakati wa kukombolewa kutoka katika laana zinazotokana na wanadamu kushindwa kuzitii sheria za Mungu, kuelekea wazi katika adhabu ambazo kwa ukweli hakuna mtu angeweza kulipa  na ndio katika wakati huu sasa Mungu anamleta Yesu Kristo kwaajili ya ukombozi.

Sio hivyo tu Paulo mtume anazungumzia wakati ambapo mtoto wa kifalme ambaye alikuwa chini ya usimamizi anapoanza kuhesabika kama mtoto wa kifalme ambaye ameiva na yuko tayari kwa utawala na kuanza kujitegemea kutoka chini ya mwangalizi, kama ukiangalia vizuri kwa kina katika kitabu cha Wagalatia Paulo anazungumza yafuatayo:-

Wagalatia 4:1-5 “Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba. Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia. Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.”

Paulo anachokizungumza hapo, ni utaratibu uliokuwa unafuatwa katika nyumba za kifalme, ambapo mtoto wa kifalme anapokuwa mdogo anakuwa chini ya uangalizi wa mtu maalumu anayeitwa kwa kiyunani “EPITROPOS”  yaani kwa kiingereza  Domestic Manager or guardian yaani Mwangalizi maalumu wa watoto wa kifalme nyumbani, ambaye kazi yake ni kutoa maelekezo na kufundisha mtoto wa kifalme namna anavyotakiwa kuishi kama mfalme maelekezo anayoyatoa yanaitwa “PEDAGOGY”  yaani mafundisho na melekezo maalumu, kwa hiyo watoto wote wa kifalme huwa chini ya watu hao wakipokea maelekezo na mafundisho, wakielekezwa na kuamuliwa nini cha kufanya, wapi waende wapi wasiende, wakati mwingine hufudishwa hata vita au kupelekwa jeshini na kushiriki vita na wakati huu wanakuwa kama watumwa tu, mpaka  unapofikia wakati uliokusudiwa na mfalme  wawe wamefuzu Mfalme huwapangia majukumu ya kiutawala au kuwapa majimbo ya kurithi kiutawala ili watawale pamoja naye

Kwa msingi huo basi tunapozungumza kuhusu utimilifu wa wakati, ambao Paulo mtume anauzungumza ni wakati ambapo Mungu alikusudia sasa wa kuwaweka watu huru kutoka katika vifungo mbalimbali pamoja na kifungo cha sharia ya Musa (Torati), na kuwakomboa wanadamu ambao walikuwa wanateswa na mateso ya aina mbalimbali na laana zinazotokana na kuivunja torati sasa anazaliwa Kristo kwa wakati kwa kusuda la kutukomboa kutoka katika hali ya utumwa.

Wagalatia 3:11-14 “Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani. Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo.Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.”

Kwa hiyo utimilifu wa wakati unaozungumzwa hapo, kimsingi ni wakati wa kuwapa wote waliomuamini Yesu mamlaka kamili, ya kuondoka kuwa chini ya sheria na kuwa wafanya sheria hii ni Baraka kubwa sana kuliko zote, wakati Israel alipokuwa akiwabariki watoto wake na kutoa unabii ya kuwa masihi yaani mtawala atatokea katika kabila la Yuda, kabila hii ilibarikiwa pia kuwa haitakosa mfanya sheria katika miguu yake

Mwanzo 49:8-10 “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.”

Ni aina hii ya mamlaka, kutumikiwa, kuwa na uweza dhidi ya adui zetu, kutumainiwa, kutokukosa mawindo, kuogopwa, kuwa na mamlaka, kuwa wafanya sheria, hii inakuja kwa kila mtu anayemuamini Bwana Yesu na huu ni wakati wa furaha sana kwani kristo amekuja kutuondoa katika hali ya unyonge na kutuleta katika wakati wa kutawala na kumiliki na kuwashinda maadui zetu, hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu anamtangazia kila mmoja wetu kuwa umewadia utimilifu wa wakati sasa, ni wakati wa ushindi, ni wakati wa kutawala, ni wakati wa kumiliki, ni wakati wa kuweka huru, ni wakati wa kufurahia uhuru kutoka utumwani ni wakati wa kuondoka katika uonevu ni wakati wa Amani na utulivu ni wakati wa ustawi, ni wakati wamkunena kwa lugha mpya, ni wakati wa kutembea na uungu ndani yetu, wakati wa kupakwa mafuta, wakati wa kuzungumza kwa mamlaka ya kifalme, wakati wa ushindi, wakati wa upenyo, wakati wa kutoboa, wakati wa kuyataja yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako, Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuufurahia wakati mtimilifu uliokusudiwa kwa Baraka zake katika jina la Yesu Kristo Amen!  

Kukombolewa kwa waliokuwa chini ya sharia.

Katika utimilifu huo wa wakati Paulo mtume anaeleza kuwa moja ya sababu ya ujio wa Yesu Kristo ni kuwakomboa wanadamu katika laana ya torati, yaani wale waliokuwa chini ya sheria, hapa inamaanisha sharia ya Musa ambayo ki msingi inapatikana katika vitabu vitano vya Musa, ambayo ina maelekezo yote ya namna ya kumuabudu Mungu na kumtumikia jambo ambalo kwa ujumla halikuwa rahisi, kuivunja torati kuliambatana na tangazo la laana kubwa na nyingi sana  nzito na za kusikitisha mno angalia :-

Kumbukumbu la torati 28:15-56 “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo. Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie. Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie. Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani. Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza. Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa. Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa. Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako. Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima; hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona. Bwana atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa. Bwana atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe. Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza Bwana. Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu. Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika. Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani. Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo.Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza; nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele; kwa kuwa hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote; kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza. Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake; taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana; naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng'ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza. Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa Bwana, Mungu wako. Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako. Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu ya masalio ya wanawe waliosalia naye; hata asitake wao mmojawapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilichomsalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote. Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatirisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake,”

Kutii maagizo yote na amri zote za Mungu kwa wanadamu halikuwa jambo rahisi, ilikuwa ni dhambi na ilileta laana hii isingeliwezekana kwa wayahudi na hata wasio wayahudi, lilikuwa ni agizo gumu sana ambalo kila wakati lingekufanya ujione mwenye dhambi, unayestahili hukumu na hasira ya Mungu na kifo tu Petro mwenyewe alisema wazi kuwa sharia ya Musa lilikuwa ni kongwa ambalo sisi wala baba zetu tusingeliweza kulimudu angalia

Matendo 15:7-11 “Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.”

Unaona ni jambo la kushangaza ya kuwa walimu kutoka uyahudi walisambaa ameneo mbalimbali na kuwafundisha wakristo kuishika sharia ya Musa jambo ambalo lingewarudisha nyuma utumwani mahali ambako Kristo alikuwa amekwisha kuwatoa na hivyo kuishika sharia ya Musa tena kungeleta laana, kwa msingi huo Yesu alizaliwa kwa wakati ili pia aweze kumkomboa mwanadamu kutoka katika laana ya Torati ujio wa Yesu Kristo duniani ulikuwa ni kwa utimilifu wa wakati wakati wa kuwakomboa wanadamu kutoka katika kongwa zito la Sheria hii ina maana gani? Neno ukombozi linalotumiwa na Paulo katika Wagalatia  kwa kiyunani ni EXAGORAZO ambalo lina maana ya kununua, kwamba kama mtu ni mtumwa wa mtu na yuko chini ya sharia na unataka kumkomboa kutoka katika sharia za mtu huyo unamnunulia uhuru wake  na anakuwa huru mbali na sharia na adhabu za mtu huyo kwa hiyo yeye aliyenunuliwa na kuwekwa huru katika utumwa wa sharia maana yake hapaswi tena kuwa chini ya sharia na kanuni  za Musa ambazo wana wa Israel walilazimika kuzishika, sio hivyo tu hata laana za sharia hazituhusu, kwa namna yoyote ile tusingeweza sisi kuishika sharia yote ya Musa kwa uwezo wetu wenyewe na ndio maana Kristo alikuja kuitii kwa niaba yetu na kutulipia deni huko ndio kuikamilisha torati na manabii.

Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.”

Warumi 8:33-39 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Yesu amekwishakufanya kila kitu kwa niaba yetu, hatuwezi tena kuwa chini ya sharia ya kitumwa wala hatuwezi kuadhibiwa na Mungu kwa kushindwa kuishi sawa na sharia, wala hatuhitaji tena kuua au kuchinja wanyama kwaajili ya dhambi zetu na laana zetu kwani Kristo amemaliza kila kitu hii sasa ina maana gani tunaweza kufanya lolote tulipendalo hapana iko sharia ya kifalme tumeondolewa katika utumwa sharia ambayo ilikuwa Mwalimu, wa watoto wa mfalme, sasa tumekuwa wafalme wafanya sharia na iko sharia ya kifalme ambayo kwayo inatuongoza ni ipi hiyo hii hapa

Yakobo 2:8 “Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.”

Kwa hiyo kukombolewa katika laana ya torati maana yake ni kuwekwa huru katika kushika na kufuata sharia na kanuni ambazo zingeleta hasira ya Mungu juu yetu, kwa hiyo Yesu aliyahukumu hayo pale Msalabani na sasa sisi tunaweza kuishi kwa njia iliyo rahisi kumpenda Mungu na kuwapenda wanadamu wenzetu jambo ambalo litatupelekea kufikiri pale tunapotaka kuwafanyia dhambi wengine

Mathayo 7:12 “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.”

Kupokea hali ya kuwa wana.

Paulo anaeleza manufaa mengine ya Yesu kuja katika utimilifu wa wakati, kwamba tunapokea hali ya kuwa wana au watoto wa Mungu, hapa anamanisha kwa wale wanaompokea

Yohana 1:12 -13 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”

Ni mtoto yule yule aliyekuwa chini ya Mwangalizi sasa anapatiwa nafasi ya kutawala pamoja na baba yake, neno linalotumika katika maandiko kupokea kuwa mwana ni Adoption ambalo maana yake ni KUMRITHI au KUMUASILI, ni kitendo cha mtu hususani mtoto kupewa haki kwa baba mwingine  na kuhesabiwa kuwa amestahili kuwa mwanae wa kudumu aitwe kwa jina lake na kuwa na haki zote sawa na watoto wa baba husika jambo hili linathibitishwa kwa kuvunjiliwa mbali kwa hofu ya kuona Mungu kama Mtawala na kumuhisi Mungu kuwa ni baba na ndani yetu tunapewa uhakika wa kumuita Mungu baba yetu kupitia muunganiko wa kazi za Roho Mtakatifu, Baada ya kutununua na kutuweka huru mbali na sharia anatufanya kuwa watoto wake na sio watumwa tena

Wagalatia 4:6-7 “Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.”

Warumi 8:15 -16 “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;”

Ujio wa Yesu Kristo duniani kwa wakati mtimilifu ulikusudiwa na Mungu kutukomboa kutoka katika hali ya utumwa na kutupandisha kwa heshima katika ulimwengu wa roho ili awe baba yetu na tuweze kutawala pamoja naye, hatupaswi kuogopa tena, tunapaswa kuwa na ujasiri, dhambi sio tatizo tena, adhabu ya Mungu na hukumu zake hazina nguvu tena sharia ya kifalme ndiyo dira yetu hakuna kitu cha kututenga na upendo wa kristo, tunapoadhimisha siku kuu hii ya Christmas hatuna budi kufahamu kuwa Bwana wetu Yesu amekuja kuyapandisha juu maisha yetu amekuja kutupa thamani, amekuja kutubadilisha kutoka chombo cha hasira za Mungu na kuwa chombo cha upendo wa Mungu, sisi sasa tuna mamlaka kamili  sisi ni kama yeye ni wafanya sharia tunayoyatamka yanakuwa, kwanini kwa sababu sasa tunakuwa kama yeye alivyo  maana tu watoto wake na tamko la mfalme ni sharia ona  

1Yoahan 4:16-18 “Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; KWA KUWA, KAMA YEYE ALIVYO, NDIVYO TULIVYO NA SISI ULIMWENGUNI humu. Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.”              

Hapa hapa ulimwenguni sisi sio wa kawaida tena, maisha yetu yamebadilishwa kupitia kuja kwa Yesu Kristo kwa utimilifu wa wakati, kila mmoja anaweza kuutumia wakati huu kumkubali Yesu na kumkaribisha ili awe Bwana na mwokozi wa maisha yake, sisi tuliompokea tuliutumia wakati vizuri wewe nawe hujachelewa leo unaposikia ujumbe huu na unaposoma ujumbe huu anza kuchangamka ukijua kuwa Mungu anatupenda na ulipowadia utimilifu wa wakati alimtuma Kristo atukomboe, Kuna watu hapa leo ni wakati wao wa kuponywa, kuna watu ni wakati wao wa kutoka kwenye madeni, kuna watu ni wakati wao wa kupokea heshima, kuna watu ni wakati wao wa kuolewa, kuna watu ni wakati wao wa kutolewa katika vifungo vya utumwa, kuna watu ni wakati wao wa kuponywa, kuna watu ni wakati wao wa ukombozi, Kuna watu ni wakati wao wa kutoka katika adhabu, kuna watu ni wakati wao wa kufunguliwa, kuna watu ni wakati wao wa kupandishwa cheo, kuna watu ni wakati wao wa kuinuliwa, kuna watu ni wakati wao wa ushindi, kuna watu ni wakati wao wa kuongezeka, kuna watu ni wakati wao wakuzaa sana, kuna watu ni wakati wao wa kutoka katika magereza za aina mbalimbali, kuna watu ni wakati wao wa kuacha kudharaulika, kuna watu ni wakati wao wa kufurahia maisha, kuna watu ni wakati wao wa kukomesha udhalilishaji, kuna watu ni wakati wao wa kupata mpenyo, kuna watu ni wakati wao wa kuvikwa vazi jipya, kuna watu wakati wao mtimilifu umewadia wa kufurahia Baraka za Mungu wewe sio mtumwa tena, hofu imetupwa mbali, wewe ni mwana wa Mungu haleluyaaaaaaa!, leo nafanya sharia mpya kwa kukutangazia kuwa wakati wako mtimilifu umewadia Yesu Kristo yuko hapa leo kukuhudumia haleluyaaaaa!, wewe sio wa chini tena wewe ni wajuu, wewe sio wa kuonewa tena, wewe sio wa kupokea maagizo, wewe ni wa kutoa maagizo, Kuzaliwa kwa Yesu ulipowadia utimilifu wa wakati kumemuinua mwanadamu na kumleta katika heshima ile kubwa ambayo malaika wanaichungulia leo ni siku ya kusimikwa kwako kuwa mfalme na kutoka kifungoni, kutoka gerezani, kutoka kwenye migandamizo na kuwa mtawala na lolote utakalolitamka kwa jina la Yesu Kristo litageuka kuwa Baraka na kutimia na lolote watakalokutamkia la kukutakia laana litawarudia juu yao Hakuna mtu alimtukana mfalme akaishi, Happy Christimas !

 

Na Rev. Innocent Samuel Kamote.

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima. !







Jumapili, 24 Desemba 2023

Tuliiona Nyota yake!


Mathayo 2:1-12Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.”




Utangulizi:

Moja ya stori zenye mvuto mkubwa sana katika Biblia ni pamoja na stori ya ujio wa watu wenye hekima kutoka mashariki ya mbali waliokuja kutoka Mashariki ya mbali wakiongozwa na nyota mpaka Bethelehemu alikozaliwa Masihi, kwaajili ya kumuabudu, Stori hii Mathayo ameipa uzito mkubwa sana na maneno yao yenye mvuto mkubwa zaidi ni haya:- Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. Utamu wa maneno yao na matendo yao unanifanya leo nitulie na kutafakari pamoja nawe jambo kubwa ambalo Mungu amelifanya kupitia wenye hekima hao maarufu kama mamajusi kwa Kiswahili cha zamani, (kwa sasa wenye hekima- Wise man); Leo tutachukua muda kujifunza kwa kina na mapana na marefu kuhusiana na swala hili:-

Ufahamu kuhusu Mamajusi.

Mojawapo ya tukio maarufu na la kusisimua sana wakati inapokaribia sikukuu ya Krismasi ni pamoja na safari ya ujio wa Mamajusi kutoka mashariki, Kimsingi neno mamajusi kwa kiingereza “Magi” linatokana na neno la kiyunani MAGOS ambalo ni sawa na neno Magician ambao zamani walijumuishwa katika kundi la watu wenye hekima, wachawi na wanajimu waliokuwa na sayansi ya kutoa suluhu kunapotokea changamoto katika falme za Babeli  angalia kwa mfano katika kitabu cha Daniel

Daniel 2:1-3 “Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme. Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake.”

Daniel 5:4-9. “Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe. Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika. Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana. Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme. Basi wakaingia wenye hekima wote wa mfalme; lakini hawakuweza kuyasoma yale maandiko, wala kumjulisha mfalme tafsiri yake. Ndipo mfalme Belshaza akahangaika sana, uso wake ukambadilika, na wakuu wake wakaona fadhaa.”

Kwa hiyo ilikuwa kawaida ya wafalme wa zamani walipopata changamoto za aina mbalimbali katika falme zao kuwaita wenye hekima (Wiseman) ili waweze kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wanakutana nazo hawa ndio waliitwa MAGI au Mamajusi au wenye hekima, kwa kusudi la kutatua changamoto zao

Tukio linalofanana na hayo hapo juu lilitokea mapema zaidi ya miaka 1000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wana wa Israel walipokuwa wakitokea Misri na kuwapiga wafalme wa waamori, mfalme wa Moabu aliogopa sana na hivyo alimuita mchawi aliyeitwa Balaam ili aje kuwaroga au kuwalaani Israel wasiweze kumdhuru

Hesabu 22:1-6 “Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko. Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli. Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile. Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.”

Hata hivyo katika namna ya kushangaza Nabii huyu badala ya kuwalaani Israel yeye aliwabariki sawa na jinsi Mungu alivyomuamuru, Ujumbe wa Mungu kwa Balaki kupitia Balaamu ulikuwa na maonyo makubwa sana badala ya kulaani aliamuriwa kuibariki Israel na kutoa unabii kuwa atakuja mfalme mwenye nguvu sana na Mfalme huyo atawahukumu maadui wa Israel mfalme huyo mkuu ilionekana nyota yake alisema namwona lakini si sasa Namtazama lakini si karibu Nyota itatokea Katika Israel:-  

Hesabu 24:15-19 “Akatunga mithali yake akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema, Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho, Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia. Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa. Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini.”

Unabii huo kimsingi ulikuwa unamuhusu Daudi katika mawazo finyu na unamuhusu Yesu Kristo katika mawazo mapana, (in a narrow sense, Daivid, in a broad Sense Jesus)  Huenda unabii huu ulihifadhiwa na wanajimu wa ukaldayo, ama ulisomwa nao katika vitabu vya kale, ama walisoma kitabu cha Daniel na kuwa na ufahamu wa Muda kamili wa kuja kwa mfalme huyu mkuu sana wa wayahudi

Daniel 9:24-25 “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake MASIHI ALIYE MKUU; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.”                

Na au mara katika sayansi yao ya unajimu walipoiona nyota  ambao kwa kusema kweli walikuwa na uelewa wa moja kwa moja kuwa kiongozi huyo ni Mfalme mkuu wa ulimwengu mzima na anayepaswa kuabudiwa,

Katika kundi la wenye Hekima kulikuwa na wanajimu ambao nao walikuwa wakifanya kazi katika jumba la kifalme kazi yao kubwa ni kuwa waliamini katika mwendo wa nyota na walikuwa na uwezo wa kutambua kila jambo muhimu linalotokea duniani kupitia nyota, kwa hiyo ilikuwa ni kazi yao kutoa taarifa kwa mfalme endapo kuna jambo lolote Muhimu limetokea Duniani, waliamini kuwa mwenendo wa nyota unaashiria tukio Fulani duniani kwa hiyo ilikuwa ni kazi yao kuzisoma na kuzichunguza angani wakati wa usiku ili kutambua jambo muhimu linalotokea duniani na wakisha kugundua walimpa taarifa mfalme kuhusu taarifa walizozibaini.

Katika tukio hili wenye hekima hawa waliongozwa na nyota hii ambayo ilikuwa ikimwakilisha masihi ni kwaajili ya hayo sasa unaweza kuona Mathayo analichukua tukio la ujio wa mamajusi kama mojawapo ya tukio la kimuujiza linalomuonyesha Yesu kuwa ni Mfalme wa wayahudi na ni mfalme wa ulimwengu na kuwa amekuja kwaajili ya watu wote,

Mathayo 2:1-2 “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.”

Mamajusi walikuwa na utambuzi kupitia nyota waliyoiona kuwa ilikuwa inaashiria kwamba amezaliwa Mfalme na kiongozi mkuu sana swa na unabii wa Kiyahudi, baadaye Nyota hiyo iliwaongoza mpaka Bethelehemu mahali ambapo kweli walimkuta Mtoto huyo ambaye ni Bwana wetu Yesu Kristo, walijawa na furaha kubwa sana na walimuabudu na kutoa sadaka yao

Mathayo 2:8-12. “Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie. Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.”

Kinyume na furaha waliyokuwanayo mamajusi Mfalme Herode yeye hakuwa na furaha, badala yake aliwaita mamajusi na kutaka kujua muda sahihi tangu walipoiona ile nyota akidai kwamba ili na yeye aweze kwenda kumshujudia, hata hivyo akiwa na nia ovu na mpango wa siri wa kumuua mtoto Yesu

Mathayo 2:3-8 “Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli. Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie

Ashukuriwe Mungu kwa sababu alifahamu nia ya Herode na hivyo Mungu alisema na mamajusi na kuwaonya kutokurudi Yerusalem na kumpa taarifa mfalme kwani alikuwa na nia ovu,

Mathayo 2:1-13 “Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.”

Tukio hili linatufundisha ya kuwa Mungu ni mwenye nguvu kubwa sana na ndiye anayeutawala ulimwengu na vyote vilivyomo, yeye hufanya kazi katika mazingitra yoyote kutokezesha kile ambacho yeye anakitaka, anaweza kufanya chochote kwa kawaida au kwa njia ya muujiza, anaweza kuingilia kati lolote kwa yoyote kwa jinsi yoyote, Mungu yuko nyuma ya kila tukio linalotokea Duniani, Hakuna sababu ya kulaumu chochote wala kujisumbua kwa lolote linalotutokea Duniani wala hatupaswi kumuhoji Mungu kwanini hili linatokea, Mungu anajua kila kitu ana nguvu ya kutumia mazingira na ana nguvu ya kuwatumia watu wote, anauwezo wa kuzungumza hata na wanajimu, na wachawi na waganga na wenye hekima na hakuna mtu wa kukutikisa wala kubadilisha makusudi na mpango wa Mungu katika maisha yako na yangu!

Herode ambaye ni adui mkubwa wa Yesu Kristo aliweza kutambua kuwa Yesu ni nani na alimuogopa, alifahamu kuwa Yesu ndiye mtawala wa ulimwengu na ni mfalme mwenye nguvu na kuwa kila kitu katika maisha yake kinatakiwa kubadilika na hivyo alikusudia kumuua.

Dunia haiwezi kuvumilia kujua na kuona nyota yako iking’ara, hawawezi kufurahia mafanikio yako, unapoona unapigwa vita kubwa maana yake umebeba kusudi kubwa, vita kubwa kazi kubwa, mtu mkubwa majaribu makubwa, mtu mgumu majaribu magumu lakini yote katika yote Mungu anachukua utawala anamiliki kila jambo, Mungu ndiye mratibu wa kila jambo kwenye maisha yetu na hivyo hatupaswi kuogopa, kama alivyo mtetea mwanaye atatutetea na sisi, kama alivyomficha mwanae kule Misri atakuficha na wewe hata watakapoangamia wote wanaoitafuta roho yako, unapokaribia kuiadhimisha siku njema ya Christmas na kuadhimisha kuzaliwa kwake kumbuka yeye ni mtetezi wetu aliye hai na atakwenda kukutetea ni wakati wa nyota yako kung’aa na hakuna wa kukuzuia uwe na wakati mzuri na mkesha mzuri wa kuadhimisha kuzaliwa kwa Kirsto katika jina la Yesu Kristo ameen!

Zaburi 46:1-3 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!

Jumatatu, 11 Desemba 2023

Nyakati zangu katika mikono ya Bwana!


Zaburi 31:14-18 “Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni. Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.”




Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa hapa Duniani hasa Afrika sio kila mtu anaweza kufurahia mafanikio yako, mazungumzo ya watu wengi kukuhusu wewe au mimi hufanyika zaidi pale tunapokuwa tumeharibu au kuharibikiwa hayo ndio watu huyazungumza na kuyapa kipaumbele na kuyafurahia zaidi, kuliko tunapokuwa na mafanikio, na kama wako watu katika nafasi ambayo wanaweza kuhakikisha kuwa wanaharibu mafanikio yako wako tayari kuhakikisha ya kuwa wanakuharibia hawa wanaitwa kwa kiingereza DESTINY KILLERS, yaani waua ndoto, au watu ambao hawafurahii kuona unafanikiwa hawa ni wengi sana duniani kuliko wale wanaotaka ufanikiwe, hii ni kawaida tu kwa sababu wanadamu wana tabia ya wivu na hawawezi kufurahia mafanikio yako!, wengi wanafurahia tuwe sawa au uwe chini lakini usiwazidi wala usifanikiwe kuliko wao, wako pia watu ambao hujipanga kwa namna mbalimbali ili kuhakikisha ya kuwa hutoboi hawa wanaweza kuwa ni watu wanaotumiwa na shetani aidha wakijijua au wakiwa hawajijui, lakini wanakuwepo tu katika jamii kuhakikisha kuwa wanaharibu, wanaua, wanasambaratisha au wanahakikisha  kuwa hufiki mbali au hufikii na katika nyakati ambazo Mungu ameziandaa kwaajili yako!, wao wanaandaliwa kuhakikisha ya kuwa wanakukwamisha, wanachelewesha, wanaharibu juhudi zako au wanadhoofisha Nyakati ambazo Mungu anakusudia kwako, na hawaoni lolote jema kwako, wanazungumza mabaya kukuhusu, wanakutakia kuharibikiwa, wanatamani wakukwamishe na hata kuidhoofisha Imani yako, wakati huo wakidhani kuwa nyakati zako ziko katika mikono yao na wanasahau kabisa kuwa ni Mungu ndiye anayeshika majira na nyakati  na mipango ya mtu ni Mungu peke yake mwenye nyakati zetu!

Wafilipi 1:6 “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;”

Kumbuka ni Mungu ndiye aliyeanza kazi njema na wewe, na ni yeye ndiye atakayeimaliza, hakuna mwanadamu anayeweza kudai, au kujidai au kujisifu kuwa anashikilia hatima yako, wote wanaosema ngoja tuone, hatoboi, ameisha, tumemaliza hakuna anayeweza kumaliza kile ambacho Mungu amekisimamisha, mambo ya Mungu hukamilishwa na Mungu mwenyewe na wanaoshindana nawe wanajiweka katika madhara kwani wanaweza kujikuta kuwa wanapingana na Mungu heri wajiepushe

Matendo 5: 38-39 “Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.”

Akiyajua haya Daudi anasema Nyakati zangu ziko mikononi mwako Ee bwana na anamuomba Mungu amlinde na maadui zake, wala asimuache kuaibishwa, na wote wanaomfuatia wawe bubu, wanyamazishishwe kuzimu, leo tutachukua muda kujifunza somo hili NYAKATI ZANGU KATIKA MIKONO YA BWANA kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

1.       Maana ya zangu katika mikono ya Bwana

2.       Mifano ya uweza wa Mungu katika nyakati za watu mbalimbali

3.       Nyakati zangu katika mikono ya Bwana

Maana ya Nyakati zangu katika Mikono ya Bwana

Zaburi 31:14-18 “Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni. Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.”

Neno nyakati linalotumika hapo katika maandiko ya kiingereza linasomeka katika namna hii

Psalm 31:14-18 “But I trust in you, O Lord: I say You are my God” MY TIMES ARE IN YOUR HANDS Deliver me from my enemies and from those who pursue me. Let your face shiner on your servant; save me in your unfailing love. Let me noy be put to shame O Lord, for I have cried out to you, but let the wicked be put to shame and lie silent in the grave. Let their lying lips be silenced, for with pride and contempt they speak arrogantly against the righteous

Kifungu hiki cha maandiko ni mojawapo ya kifungu cha Muhimu sana katika zaburi hii, Mwandishi alikuwa akifanya maombi yanayoonyesha ya kuwa anamuamini Mungu na kuwa anamtegemea kwa Ulinzi wake na mafanikio ya maisha yake dhidi ya watu wote wale wanaiomtakia mabaya, Mwandishi sio tu kuwa alikuwa anatakiwa mabaya na adui zake lakini adui zake walikuwa wamekwishakuchukua hatua kadhaa kuhakikisha kuwa hafanikiwi, hatoboi hatoki na anamalizwa kwa namna yoyote ile, ni kama walikuwa wanafikiri kuwa wameshamuweza,  Lakini mwandishi anamwambia Mungu kwamba yeye anamwamini na kwamba alikuwa anafahamu wazi kuwa NYAKATI ZAKE ZIKO KATIKA MKONO WA MUNGU hivyo alipokuwa akikutana na vita na upinzani kutoka kwa maadui alikuwa anafahamu kuwa yeye anatakiwa tu Kumuomba Mungu, kwa sababu yeye alifahamu kuwa alizaliwa kwa kusudi la Mungu na kuwa yuko duniani kutimiza mpango wake katika wakati uliokusudiwa na Mungu!

Neno Nyakati zangu Katika mikono ya Bwana au kwa kiingereza My times in the hands of Lord  kwa kiebrania linasomeka kama ETH kimatamshi AYTH  ambalo maana yake ni Majira na Makusudi, katika biblia ya kiingereza ya KJV limetumika mara 257 kumaanisha muda, mara 16 kumaanisha majira, mara 7 kumaanisha kusudi na mara 10 kumaanisha Kazi maalumu, hii maana yake ni nini ? Mungu anapotupa muda wa kuishi ndani yake anatoa majira, muda kazi na majukumu ambayo kila mwanadamu anatakiwa ayatimize awapo duniani unaona!  Na ili uyatimize kuna HATIMA yaani kilele cha kutimizwa kwa majukumu hayo maalumu ambayo Mungu anayatoa kwa kila mtu kwa majira na nyakati zake!

Kwa hiyo Mwandishi anapojieleza kuwa Nyakati zangu zimo Mikononi mwake anamaanisha Hatima  yaani Destiny, kusudi, wajibu, muda na kazi maalumu aliyopewa na iliyokusudiwa kwake iko mikononi mwa Mungu, na kama ni hivyo basi ni wazi kuwa juhudi na jitihada za maadui na wapinzani, na wanena mabaya, na wanga, na wachawi, na majeshi,   na wazandiki na wafitini, na wapika majungu, na walozi, na wenye chuki, na wenye wivu na wenye husuda kamwe haziwezi kuharibu wala kukatisha kusudi la Mungu lililokusudiwa na Mungu kwa wakati wake na kuwa ni lazima litatimia, hafi mtu wala haaribikiwi mtu, kwa sababu hao woote hawana hatimiliki ya Nyakati zilizokuduiwa kwako

-          Habakuki 2:3 “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.”

 

-          Isaya 46:9-10 “kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.”

 

-          Hesabu 23:19 “Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?

Kwa hiyo ni Mungu ndiye aliyekusudia uzaliwe hapo ulipozaliwa, ni Mungu aliyekusudia uzaliwe mwanamke au mwanaume, ni Mungu aliyekusudia uzaliwe katika familia uliyozaliwa, ni Mungu aliyekusudia ufanye kazi unayoifanya ni Mungu aliyekusudia ufanye huduma unayoifanya, ni Mungu aliyekusudia uwe na mume uliye naye na mke uliye naye ni Mungu aliyekusudia uwe na cheo ulicho nacho na mambo haya yote Mungu aliyakusudia tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia, maana yake ni nini Hakuna mtu au pepo au malaika au jambo lolote lile linaloweza kuharibu mpango wa Mungu katika maisha yako kwa sababu hakuna adui anayeshikilia hatima yako, wala muda wako, wala kazi maalumu ambayo Mungu ameikusudia katika maisha yako kwa nini kwa sababu NYAKATI ZAKO ZIKO KATIKA MIKONO YA BWANA !

Waefeso 2:10 “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”

 

Mifano ya uweza wa Mungu katika nyakati za watu mbalimbali

Maandiko yamejaa mifano mingi sana ambayo Muda hauwezi kuruhusu kuipitia yote, lakini mifano michache nitakayoitumia hapa inatosha kabisa kuonyesha kuwa adui zako hawakuwezi, na hawana mamlaka ya kuharibu chochote na kama wakiharibu ujue tu Mungu alikusudia waharibu, kwa sababu maandiko yanaonyesha kuwa hatua zetu zote yaani njia za maisha yetu zote zinaratibiwa na Mungu ona

Mithali 20:24 “Mwenendo wa mtu watoka kwa Bwana; Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?

Mungu anapokuwa amekusudia jambo kwa Mtu na kwa wakati wake kisha akatokea mtu kuingilia kati kwa makusudi ya kuharibu, awe anajua au awe hajui, awe amatumiwa na shetani au awe hajatumiwa, awe ni ajenti wa ibilisi au vyovyote vile ni aidha mipango yao ifeli, au kupitia hila zao Mungu akupeleke katika mpango wake mwingine anaoukusudia kwa wakati huo kwanini kwa sababu Nykati zetu zimo katika mikono yake, hapa iko mifano ya watu waliozaliwa kwa wakati maalumu kwa kusudi la kufanya kazi maalumu katika majukumu maalimu kwa nyakati alizokuwa amekusudia Mungu kisha watu wakajitokeza na mikakakati ya kuharibu au kuzuia na haya ndio waliyokutana nayo:- ona

1.       Herode dhidi ya Mwana wa Mungu Yesu Kristo

 

Moja ya watu waliojaribu kuharibu maisha ya mtu mwingie ni pamoja na Herode Mfalme yeye alikuwa amekusudia kuyaharibu kabisa maisha ya Mwana wa Mungu Yesu Kristo, baada ya kusikia habari za kuzaliwa kwake na unabii aliosomewa na matamko ya wanajibu yaani mamajusi kuhusu hatima ya Yesu Kristo kuwa ni Mfalme mkuu wa wayahudi anayestahili kusujudiwa yeye alifadhaika na aliadhimia kuwa na mkakati wa kuharibu maisha ya Mwana wa Mungu

 

Mathayo 2:1-3 “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.”

 

Wako watu wanaotuzunguka wako kama Herode badala ya kufurahia mafanikio yako wao wanafadhaika wanaumwa na mafanikio yako, wanaumwa wanapoona ya kuwa unaenda kutoboa,  wanaumwa wanaposikia kuwa unaenda kuoa au kuolewa, au kupata kazi, au kupewa cheo au wanapogundua kuwa wewe ni tishio la mafanikio kwao wanatumia kila hila na ujanja ili yamkini ikiwezekana waharibu Mpango wa Mungu ndani yako lakini ashukuriwe Mungu kuwa hekima yake haichunguziki yeye anajua kuifanya kuwa upuuzi hekima ya dunia hii nay a shetani nay a wanadamu, wewe kama ni mwana wa Mungu kama ilibyokuwa kwa Yesu Kristo Mungu ataandaa mpango wa kukuokoa na kuchepusha njia za adui kile wanachokifikiri, sio kile ambacho Mungu atakifanya

 

Mathayo 2:8-14 “Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;”

 

Mungu alifanya njia kuhakikisha kusudia aliloliweka ndani ya Mwana wake linatimia na kuwa hakuna mpumbavu anaweza kuliharibu, kiburi cha Herode kilifanywa kuwa ujinga pale Mungu alipotokeza njia na kusema na mamajusi lakini vile vile alisema na Yusufu, nataka nikuhakikishie kile ambacho Adui zako wanadhani kuwa watafanikiwa hakitafanikiwa na Mungu ana njia na mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa anajitokeza kwako, kwa njia nyingine kuhakikisha ya kuwa kazi ile njema aliyoianza anaikamilisha hakuna anayeweza kushindana na kusudi la Mungu na kubadili mpango na nyakati alizozikusudia Bwana !

 

2.       Farao dhidi ya wana wa Israel

 

Farao alikwishakuambiwa mara kadhaa kusudi la Mungu kuhusu Israel, alielezwa wazi kuwa israel ni mzaliwa wa kwanza wa Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, na kuwa kusudi la Mungu wa waebrania ni kuwapeleka Israel katika inchi ya mkanaani aliyowaapia baba zao Ibrahim na Isaka na Yakobo, lakini kwa makusudi kabisa farao alikuwa akipingana na kusudi hili na akapigwa kwa mapigo kumi, hata baada ya pigo la mwisho yeye bado alitaka kuwaendea Israel na kuwarejesha tena katika inchi ya utumwa

 

Kutoka 14:5-8 “Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena? Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye; tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maakida juu ya magari hayo yote.Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri.”         

 

Unaweza kuuona moyo wa farao,? Bado walifikiri yeye na watumishi wake kuwa wanaweza kuamua hatima ya watu wa Mungu, wanaweza kuwarejesha nyuma wanaweza kuzuia mpango wa Mungu na neno lake  na kiapo chake kuwa anawapeleka katika inchi ya mkanaani na hivyo hata Mungu alipoigawa bahari ya shamu kwa ujinga walitaka kupita mle mle kinyume na kusudi la Mungu na hiki ndicho kilichowakuta

 

Kutoka 14:22-28 “Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto. Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa BWANA anawapigania, kinyume cha Wamisri. BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.”

 

Unaona hatima ya farao na majesi yake yote yalizikwa katika bahari ya shamu kwa nini kwa sababu alikuwa akishindana na kusudi lililokuwa ndani ya watu wa Mungu, nimefurahi Musa anavyomalizia mstari huu HAKUSALIA HATA MTU MMOJA  Bwana akufanyie hivyo na kuzidi mtu wa Mungu wote ambao wanakufuatilia ili kuhakikisha kuwa unaharibikiwa Bwana asimwache hata mmoja asisalie hata wa kutoa taarifa ya kilichotokea, awaye yote ambaye anazani kuwa ana mamlaka ya kushika Nyakati zako ajue wazi kuwa nyakati zako ziko katika mikono ya Bwana !

 

3.       Mawaziri dhidi ya Daniel

 

Wakati mwingine watu wanaodhani wanaweza kuharibu Nyakati zako kwaajili ya  sifa zako hupatwa na wivu tu, na kutafuta kuwa maarufu, au kutafuta kukuchafua ili wao waonekane au wawe na cheo kama ulichonacho hawajui kuwa wewe una upako wa huduma tofauti au niseme una kitu cha ziada ndivyo aklivyokuwa Daniel alipendwa aliwazidi watu katika sifa na cheo na uaminifu na watu wakawa wanatafuta namna ya kumpaka matope ili achafuke ili tu wamuharibie

 

Daniel 6:1-5 “Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote. Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.”

 

Ukiona watu wanatafuta kuchafua jina lako au kuwafanya wengine waamini kuwa haufai ujue kuna kitu cha ziada umewazidi, katika maisha yangu nimekutana na watu wengi sana wenye wivu wenye uchungu ambao sio tu wanatamani uharibikiwe lakini wanatamani usambaratike, wanatamani hata ndoa yako ife, wanatamani kazi zako ziharibike, ufukuzwe, uumwe, ufe upatwe na majanga na sio hivyo tu watakuandama wakiwa na wivu wenye uchungu, watatumia hata uchawi na majungu wakifikiri ya kuwa wamekuweza hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Daniel lakini mwisho wa siku Daniel aliyetupwa katika tundu la simba alipona na wao wakaliwa na simba na kutoweka duniani kwa nini kwa sababu nyakati za mtu wa Mungu ziko mikononi mwa Mungu

 

Daniel 6:20-24 “Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele. Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake. Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.”

 

Wwatu wote waliokuwa wakiwafuatia watu wenye kusudi la Mungu hatima ya maisha yao ilikuwa mbaya sana, Ndugu usiogope wote waliokuonea Mungu atawalipia maovu yao yatakuwa juu ya vichwa vyao, hawawezi kukuharibu, hawawezi kukufitini, hawawezi kukuzika na badala yake utawazika wewe, muda usingeweza kutosha kusema habari za Hamani na Esta na wayhaudi walokuwako shushani Ngomeni, wala muda wa balaamu dhidi ya waisraeli, wala musa wa Yusufu na kaka zake, wala Sanbalati na tobia dhidi ya Nehemia, na kadhalika wewe kama mwanafunzi wa biblia unajua yaliyowakuta Mungu hataacha uonelewe atawakemea wote na kuwachafulia usemi wao wote wanaoinuka kinyume nao na wote wanaojenga mnara wa babeli dhidi yako watachafuliwa usemi

               

Nyakati zangu katika Mikono ya Bwana

Zaburi 31:14-18 “Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni. Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.”

Kwa misingi hiyo utaweza kuona kuwa kadiri unavyokaribia au unapofikia kilele cha kusudi lile ambalo Mungu amelikusudia au hatima ile ya Muhimu ndio utaweza kuona vita kali sana inainuka, Mungu anapotaka kukuinua au anapokuwa amekuinua unakuta watu hawapendezwi, hawafurahii wanazungumza vibaya, wanakuchafua wanakuchukia, njia yako inatiwa tope inawekwa giza, upinzani unakuwa mkubwa dharau, masengenyo, majungu, mateso, au vita kali sana jua sasa kuwa unakaribia Baraka kubwa ambazo Mungu amezikusudia kwako, na nataka nikuhakikishie kuwa Mungu yule yule anayetupa neema kupenya atakupa neema izidiyo na kukusaidia wakati wa mahitaji yako  watu hawashindani na mtu mwenye nyota ndogo, watu wenye nyota ndogo siku zote hupiga vita watu wenye nyota kubwa kumbuka nyota ya Yesu na Herode!

Waebrania 4:16 “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”

Wakati huo mtegemee Mungu ukiwa na ufahamu kama aliokuwa nao Daudi mtumaini yeye, mfanye kuwa ndie Mungu wako jua kuwa nyakati zako ziko mikononi mwake kwa hiyo atakuponya na adui zako, atakupa kibali, atashughulika na wanaokufuatilia, atakuokoa kwa upendo wake, hatakuacha uaibike, wataaibishwa wao na kunyamazishwa katika kuzimu, na wanaosema mabaya watapigwa ububu!

Hatupaswi kuogopa lolote wala mtu yeyote wala manenmo yoyote ya wapuuzi na wajinga walio kinyume na mapenzi ya Mungu katika maisha yetu, hakuna mtu anayeshika hatima ya maisha yako isipokuwa Mungu mwenyewe

Kila mtu anaweza kupanga lolote analoweza kulipanga lakini shauri la bwana ndio litakalosimama Mithali 19:21 “Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.”

Haijalishi wanadamu wanajenga nini la msingi ni lile Mungu analolijenga  Zaburi 127:1 “Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.”    

Fahamu ya kuwa unaweza kuwa na vita kubwa na nyingi lakini ukimwambia Bwana yeye ndiye atakayepigana kwa niaba yako, Mungu ndiye aliyekusudia hakuna anayeweza kutangua kusudi, kupigana nawe adui zako ni kama wameamua kupigana na Mungu mwenyewe,  kwa kila jaribu uko mlango wa kutokea, Mwana wa Mungu alikuwa na maadui wengi walioinuka pasipo sababu lakini Yesu hakupoteza muda kujibizana nao alikuwa busy na majukumu ambayo Mungu amempa, ninaposema nyakati zangu katika mikono ya Mungu nina maana pana  sana hakuna mtu anaweza kudhibiti, kuongeza au kupunguza lolote lile katika makusudi ambayo kwayo Mungu ameyakusudia katika maisha yangu na yako kwa hiyo usiogope, Hakuna aibu itatutawala, hakuna vita hatutashinda, hakuna kikwazo hatutavuka, hakuna aibu haitazimishwa, hakuna kivywa hakitazibwa, hakuna kifo, hakuna kurudi nyuma, sio kwa sababu mimi na wewe ni wakamlilifu bali kwa sababu yeye ni mkamilifu, mpango wa Mungu ndani yetu hauwezi kuzimishwa na wazushi, ni fimbo yake na gongo lake ndilo linalotuongoza, tumeumbwa na Mungu na sio na watu, mimi na wewe tu  wana wa Mungu wagomvi wetu wanagombana na baba yetu haupaswi kuogopa kwa sababu NYAKATI ZAKO ZIKO KATIKA MIKONO YA MUNGU.


Na. Rev Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima



Jumatano, 6 Desemba 2023

Kutumia kwa Halali neno la kweli


2Timotheo 2:15-18 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu, na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.”



Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho sana, katika nyakati hizi, kumekuwepo na madhehebu mengi sana na kila dhehebu lina misimamo yake na mafundisho yake, hata hivyo kila Mkristo ana wajibu wa kuhakikisha kuwa yeye mwenyewe anakuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu Neno la Mungu na namna linavyotumiwa ili aweze kupambanua nani analitumia neno la Mungu kwa halali na nani analitia maji, yaani kulighoshi, kughoshi ni Kiswahili cha zamani chenye maana ya kuongeza maji, mfano unapokuwa na maziwa halisi, sasa ili yawe mengi unaongeza na maji yaani kuchakachua, kwa hiyo katika nyakati zetu hizi vilevile tunao watu wanaolichakachua neno la Mungu hivyo kila mmoja anapaswa kuwa na akili ya kujua nani anachakachua neno na ni nani analitendea haki, huu ni wajibu wa kila Mkristo na kila mwanafunzi wa Yesu!

2Wakorintho 2:17 “Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.”

Tatizo liliopo ni kuwa kila mtu duniani anaweza kuwa na tafasiri yake kuhusu neno la Mungu na akafikiri kuwa yuko sahihi, kwa sababu kila mtu anasema anaifuata Biblia anaiamini Biblia lakini wakati huo huo tunashuhudia kuwepo kwa tafasiri na misimamo tofauti tofauti kuhusu neno la Mungu, sasa basi, ikiwepo miongozo muhimu itatusaidia katika kulitumia neno la Mungu kwa halali na kuepuka changamoto nyingi zinazoweza kujitokeza, Mungu ni Mungu wa Utaratibu na sio Mungu wa Machafuko! Kwa hiyo ni wajibu wa Kila Mkristo kuyachunguza maandiko ili kujithibitishia kama kilichohubiriwa ni cha kweli bila kujali anayehubiri ni mtu wa namna gani au ana heshima kiasi gani hivyo ndivyo walivyokuwa watu waungwana katika kanisa la Baroya alipohubiri Paulo Mtume ona

Matendo 17:10-11 “Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.”

Watu wa Beroya walikuwa waungwana, kwa mujibu wa Luka kwanini kwa sababu bila kujali nani anahubiri walifanya kazi ya kuyachunguza maandiko kila siku ili wajithibitishie kuwa yanayohubiriwa ni kweli? Mungu hapendezwi na makundi makubwa ya watu ambao wanabaki kuwa maamuma kila siku, wajinga wasio na mafunzo, wasiothibitishwa, wasio na ujuzi kwa kiingereza wanaitwa LAY waliolala au LAY PERSON  a person who is not trained, not qualified or not having an experience in a particular subject or activity  unaona kwa wakatoliki wanaitwa WALEI, Mungu hajatuita ili tuendelee kutengeneza kundi kubwa la watu wajinga Agizo kuu linatutaka kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi, wawe wenye kufaa Qualified  wajue neno, wachambue neno, watafasiri neno wahoji maswali, wajibu maswali watengeneze mijadala yenye faida wawe wakomavu ! Waelimike

2Timotheo 4:1-4 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo

Waefeso 4:11-14 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

Kwa msingi huo leo tutachukua muda kutafakari na kujifunza kwa makini somo hili la thamani Kutumia kwa halali neno la kweli kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

·         Maana ya kutumia neno la Kweli kwa halali

·         Jinsi ya kutumia neno la kweli kwa halali

·         Kanuni za kutumia neno la kweli kwa halali

Maana ya kutumia neno la kweli kwa halali.

2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”

Paulo mtume alikuwa anamuagiza Timotheo aliyekuwa Askofu wa Makanisa ya Efeso kuhakikisha kuwa analitumie neno la Mungu yaani neno la Kweli kwa halali, Neno la kweli linalotajwa hapo ni Neno la Mungu yaani Biblia, kwa hiyo Mwalimu wa neno la Mungu anaagizwa hapo kuhakikisha kuwa analitumia kwa halali, nini maana ya kutumia neno la kweli kwa halali?

Ili tuweze kuelewa Mstari huu vizuri na kuweza kuweka msingi wa somo letu vizuri kwanza nitauweka mstari huu katika kiingereza

Study to shew thyself approved unto God, a workman that needeth not to be ashamed, rightly dividing the word of truth  

Kwa hiyo katika Biblia ya kingereza KJV ambayo ndiyo iliyotumika kuleta Biblia ya Kiswahili kwetu Mstari huo unasomeka namna hiyo, sasa nikianza na neno kutumia kwa halali neno la kweli, RIGHT DIVIDING tafasiri ya kiyunani ya neno hilo ni “ORTHOTOMOUNTA  ambalo ni neno la Kiyunani linaloundwa na misamiati miwili yaani “ORTHOS” na “TOMO” Orthos maana yake ni Perfectly right au Staright na neno Tomo ni CUT  kwa hiyo neno ORTHOTOMOUNTA maana yake mega sawa sawa, au kata sawasawa, au kata kwa ukamilifu,  maana yake hasa inatokana na asili ya kiroho ya neno kugawa mkate, au kuumega mkate

Matendo 2:46-47 “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, WAKIMEGA MKATE nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”

Neno la Mungu ndio Mkate wetu wenyewe kwa hiyo wakati wa kuuvunja mkate mvunjaji anatakiwa aukate sawasawa, kama vile watu wanavyokata keki na kutoa vipande vyenye uwiano ili kile kitakachomfikia mtu kiwe sawasawa bila upendeleo, kwa hiyo Lugha hii ndiyo inayotumiwa katika kuelezea namna tunavyopaswa kulitumia neno la Mungu kwa halali na sio kama kila mtu atakavyo au kila kanisa litakavyo au kila dhehebu litakavyo bali kama Mungu atakavyo ona

2Patro 1:19-20 “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, Kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.”

Unaona? Kwa msingi huo sio sawa kwa mujibu wa maandiko kwamba kila mmoja ajitafasirie maandiko kama apendavyo hapana, haiko hivyo, huwezi tu kwenda kwenye maandiko na ukachukua tu chpchote unachoweza kuchukua na kuunga mkono mawao yako au njia yako, Mungu katika hekima yake ameweka namna ya kuyatafasiri maandiko na ndio maana kuna umuhimu wa kujifunza neno la Mungu kama tunavyoweza kuona katika kipengele kifuatacho, hilo sasa linatuleta katika kutafakari kipengele cha pili

Jinsi ya kutumia neno la kweli kwa halali

Mungu ni Mungu wa utaratibu na wala sio Mungu wa machafuko!, Mungu ndiye mwanzilishi wa Muda, aliuumba ulimwengu kwa siku sita, na kila siku ilikuwa ni masaa 24, Mungu aliumba ulimwengu na akaweka anga, leo hii kutokana na maendeleo makubwa ya kisayansi, tumegundua kuwa ziko sayari kadhaa ambazo hulizunguka jua, nazo zimewekewa utaratibu na ndio maana hazigongani! 1Wakorintho 14:40 “Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.”

Taratibu zote zilizoko Duniani zimewekwa na Mungu, na wakati mwingine Mungu pia huweka watu wazazilishe au wasimamie utaratibu, ili mambo yote yatendeke kwa utaratibu, fikiria kwa mfano waliochinga baba bara kwa nchi zilizotawaliwa na uingereza magari barabarani hupita upande wa kushoto kwa njia ya kule linakoelekea gari, na zile zinazorudi hupita kushoto kwao ambako huwa ni kulia kwa anayekwenda, utaratibu wa namna hii pamoja na sharia zake barabarani ndio unaopelekea kuwepo kwa usalama na kupungua kwa matukio ya ajali,  jaribu kuwaza kama kusingelikuwa na utaratibu? Fikiria Hospitalini kwenye matibabu, Kama madaktari wangekuwa wanaandikia watu dawa hovyo hovyo, bila kuzingatia miaka, uzito, aina ya ugonjwa na dozi, je usalama wa wagonjwa ungekuwaje?  Mashuleni Kama kusingelikuwa na maswala ya hatua, wala silabasi wala walimu wa somo husika wala utaratibu wa vipindi kungekuwaje? Kungekuwa na machafuko na ukiangalia kwa makini utaweza kuona ilimutaratibu uweze kwenda vizuri watu wote hata madereva huwa wanaambiwa wasome, wasomee fani zao ili waweze kuufuata utaratibu uliokusudiwa katika Nyanja zao unaona?  Sasa ili neno la Mungu liweze kutumiwa kwa halali Paulo anamwambie Timotheo

2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”

Naomba tena niweke mstari huu katika kiingereza cha Biblia ya KJV King James Version mstari huo unasomeka hivi?

Study to shew thyself approved unto God, a workman that needeth not to be ashamed, rightly dividing the word of truth

Paulo mtume anapomwagiza Timotheo kutumia neno la Mungu kwa halali anaanza nan neno la Msingi kwenye Kiswahili JITAHIDI neno hilo KJV imetumia neno STUDY katika kiyunani ni SPOUDAZO ambalo maana yake ni BE DILIGENCE  yaani makinika, au chukua tahadhari zote au jielimishe study  kwa hiyo Mtafasiri wa maandiko au Mwalimu wa neno la Mungu anapaswa kutia bidi, kuwa makini, kusomea, kutafuta kwa bidi kutafasiri neno la Mungu kwa halali ili ampendeze Mungu, kama hatutakuwa makini na kila mtu akatafasiri maandiko anavyojisikia na atakavyo uelewa kuhusu Mungu na maagizo yake utakuwa haufanani duniani na neno hilo hilo litakuwa halijatumiwa kwa halali jambo litakalotuletea hukumu kubwa zaidi

Yakobo 3:1-2 “Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi. Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.”             

Msiwe waalimu wengi kwa kiyunani DIDASKALOS  yaani  Doctors, Master teacher,  neno hilo limetumika kumtaja Yesu mara 40 kama Mwalimu Master na limejitokeza katika biblia mara 58 katima mistari tofauti 57 yote ikionyesha mtu aliyebobea katika kufundisha, Mtaalamu wa kutafasiri maandiko au Mwalimu wa neno anatakiwa awe mtu aliyebobea na ili mtu awe mbobevu anapaswa kuwa na bidi katika kujifunza na kujisomea, kwa hiyo kimsingi maandiko yanatutaka tuwe wabobezi yaani tusomee, na ndio maana katika vyoa vya Biblia liko somo maalumu kwaajili ya kusomea jinsi na namna nzuri ya kutafasiri neno la Mungu somo hilo linaitwa HERMENEUTICS, somo hilo haliwezi kufundishwa katika somo moja kama hivi, lakini hapa nakupa tu tahadhari ya kawaida ili ujue kuwa sio kila mtu anaweza kuwa Mwalimu wa neno la Mungu na kazi hii ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine, Upako jni wa Muhimu, lakini na upako unaweza kumilikiwa na mtu yeyote, karama ni za Muhimu nazo zinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, hata hivyo, kutafasiri maandiko kunahitaji maarifa na ndio maana kuna walimu, kumbuka Naye alitoa wengine kuwa Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na WALIMU kwa hiyo ni kazi ya wabobezi kutuingiza katika huo utaalamu wa kutafasiri maandiko HERMENEUTICS sio mtu anaamka tu na ndoto zake na anakuwa muhubiri, kama jinsi ambavyo Dakrati haamki tu na kuwa daktari ili ashughulikie miili ya watu hali kadhalika hainuki tu Mtu na kusema ni muhubiri na mtafasiri wa neno la Mungu kama kujifunza na kukaa chini ya walimu utakupuuzia tutakuwa na wazushi wengi sana katika karne hii, waalimu wote wazuri akiwepo Yesu mwenyewe walikaa chini nya walimu kwanza kabla ya kuwanza kuwa walimu wa neno la Mungu, wako watu ambao hujidhani kuwa ni wa kiroho sana na wanapuuzia sana swala la kusoma wakifikiri kuwa ni kupoteza Muda wako wanaodhani kuwa kwa kuwa wamejaa Roho Mtakatifu basi hawahitaji kujifunza hapana Roho wa Mungu huwa anaongoza watu wakajifunze kwanza kabla ya kuwatumia

-          Musa alipata Elimu ya kawaida kule Misri kwa umri wake wote miaka 40, na kisha alijifunza maswala ya kiroho kwa Kuhani wa Midian Yethro kwa miaka 40 jambo hili lilipelekea Musa kuwa Mwalimu mzuri sana na kiongozi aliyeandaliwa kuweka misingi ya kiroho, kisiasa, kisheria na maongozi na taratibu zote duniani Matendo 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.”

 

-          Yesu Kristo Bwana wetu alikaa chini ya waalimu kabla ya kuwa Mwalimu ona Luka 2: 46-47 “Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.” Unaona na zaidi ya yote alijifunza kwa Mungu Roho Mtakatifu nay eye alikaa na wanafunzi wake miaka mitatu na nusu ndipo akawaamuru wakahubiri injili

 

-          Paulo Mtume alikaa chini ya Mwalimu maarufu aitwaye Gamaliel Matendo 22:3 “Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;” Paulo mtume licha ya kukaa chini ya Mwalimumaarufu Gamaliel na kujifunza maswala ya torati pia alikaa chini ya Roho Mtakatifu miaka 14 akijifunza injili aliyotukabidhi, ambayo alifundishwa na Yesu mwenyewe ona

 

Wagalatia 1:11-20 “Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski. Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo.”      

 

Aidha licha ya kuwa alifundishwa na Yesu mwenyewe mtume huyu ambaye alikuwa mwana sharia pia alikuwa na bidi ya kujisomea na alisisitiza kuwa wahubiri wajisomee ona 2Timothy 4:13 “Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi.”

 

Kwa hiyo Paulo anapomtaka Timotheo awe na bidii katika kujisomea alimaanisha kuwa huwezi kumtenga Muhubiri na tabia ya kujisomea, kutafakari na kuandaa neno la Mungu sawa na kanuni alizozikusudia Mungu, kila Muhubiri ni Mwalimu na hivyo kila Muhubiri anapaswa kusoma na kujisomea, kwenda shule na kuendelea kuwa na tabia ya kujisomea siku zote za maisha Yetu, kufundisha na kuwaelezea watu neno la Mungu hakupaswi kuwa kwa kukurupuka tu, Kanisani hakuna wajinga kuna watu wengine ni wasomi, wengine ni viongozi wengine wana akili wengine wana ujuzi, kwa hiyo sio mahali ambako utaokota biblia na kuondoa vumbi na kwenda kusema tu ili mradi unajua kusagia watu hapana kuna kanuni zake kuna hatua zake kuna utaratibu wake

 

Isaya 28:9-13 “Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa; ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia. Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.”

 

Kwa hiyo watu wanaohudumia roho za watu hawapaswi kuwa watu wa kuokota okota tu hapana wanapaswa kuwa watu wenye akili timamu, sio waliochoka, wala vichaa bali watu wenye akili na wanaojua kujifunza walio hodari katika maandiko ili waweze kuijenga jamii kwa hiyo tusifikiri kuwa Mungu anafurahia neno lake lipotoshwe tu hata wewe unaweza kuwa mkali pale watu wanapokunukuu vibaya,Kama tunamuheshimu Mungu hatuna budi basi kuyaheshimu na mambo yake badala ya kuibuka tu kama uyoga na ukachezea roho za watu, tukifanya hivyo kutakuwa na uwiano sawia  wa ujuzi wa neno la Mungu kwani ndio maana Yesu aliagiza kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi. Hilo sasa linatuleta katika mkutafakari kipengele cha tatu na cha mwisho

Kanuni za kutumia neno la kweli kwa halali

Kutafasiri neno la Mungu ni taaluma, ni sayansi, ni elimu na iko miiko ya jinsi na namna ya kulitafasiri neno la Mungu, kanuni hizo zikizzingatiwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa tafasiri za neno la Mungu na watu hawatatafasiri maandiko kama wapendavyo tu bali sawa na kanuni zilizoainishwa na kupendekezwa kitaalamu, Sayansi hii ya kutafasriri neno la Mungu inaitwa Hermeneutics hermeneutics ni nini kwa kiingereza

1.       Hermeneutics is a branch of Science that deals with the interpretation of scriputres especially the Bible

2.       Hermeneutics ni tawi la Maarifa linalohusika na utaalamu (kanuni) wa kutafasiri maandiko hususani Biblia

Sina mpango wa kufundisha somo hilo hapa, kwani haya ni maubiri tu, lakini nataka kutoa maswala ya kuzingatia wakati mtu anataka kufundisha neno la Mungu au kuhubiri, hii ni kwaajili ya watu wa kawaida watu wote, sio kwaajili ya wahubiri na wachungaji waliokwenda au waliopo vyuoni japo nimezingatia sana kuwafaa watu wote kama Neno la Mungu lilivyo:-

Ni muhimu kufahamu kuwa kwa nini Biblia inahitaji tafasiri? Au kutumiwa kwa halali, tunaweza kusema kuwa je Mungu si amewakusudia watu wote wafikiwe na neno lake jibu ni ndio lakini watu hao wana Historia tofauti, tamaduni tofauti, lugha tofauti, na muda au nyakati tofauti kwa hiyo kuna vitu vya kuzingatia wakati mtu anataka kutafasiri neno la Mungu, ndio maana umeweza kuona kwa mfano Paulo anamwambia Timotheo JITAHIDI katika Kiswahili lakini katika kiingereza STUDY bila kucheza na lugha iliyokusudiwa unaweza kujikuta hupati maana iliyokusudiwa! Kwa hiyo Lugha, Tamaduni, Historia, na muda unaweza kuwa kwazo kwa Muhubiri na mtafasiri wa maandiko na ndio maana tunahitaji miongozo! Miongozo hiyo inatusaidia

1-      Kulijua wazo kamili la Mungu alilolikusudia katika neno lake

2-      Kuzuia tafasiri zisizo za kweli ya neno la Mungu

3-      Kuzuia kupotoshwa kwa lengo la injili

4-      Kuzuia hukumu ya Mungu

5-      Kuleta uwiano wa ufahamu na mwenendo na tabia kwa wanafunzi wa Yesu duniani

6-      Maandiko yanahitaji Mtafasiri au mfafanuzi juhudi ya kusoma pekee haitoshi mpaka mtu akufafanulie ona Matendo 8:30-31 Biblia inasema hivi “Ndipo Filipo akakimbilia na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamwuliza, Je, yanakuelea hayo usemayo? Yule towashi akasema, Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia? Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye”.

Kwa hiyo kumbe kanuni zitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza au kuondoa kabisa changamoto na kutokuruhusu uzushi kulivamia kanisa la Mungu na kuondoa utata wa kiufahamu, kwa sababu Mungu anataka tuwe na nia moja

1.       Mtafasiri wa maandiko wakati wote anapaswa kuwa na NIA NJEMA Hakikisha kuwa una moyo safi, unakwenda katika maandiko kwa kusudi la kutafuta jambo jema la kuijenga jamii Matendo 24:16 “Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.” Unaweza kuwa msomi na unaweza usiwe msomi, lakini Mungu huchunguza nia ya moyo, huiangalia dhamira, unapodhamiria kuifundisha kweli unajiweka salama mbele za Mungu na unapodhamiria kupotosha kama balaam Mungu anaiona nia yako, kwa hiyo ili mtu awe na nia njema na dhamiri safi ni lazima awe na hofu ya Mungu nah ii ikiwepo utalichukulia neno la Mungu kwa tahadhari kubwa.

 

2.       Neno la Mungu limevuviwa kwa sababu hiyo kila mtu mwenye nia njema na dhamiri safi anapotaka kulitumia kwa kusudi la kuwasaidia watu wa Mungu, kuwaonya, kuwakemea, na kuwakamilisha anaweza bado kuwa kwenye upande sahihi ona 2Timotheo 3:16-17 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”

 

3.       Kumbuka kwamba maandiko yana tabia ya kujitafasiri yenyewe kwa msingi huo uko umuhimu wa kuzingatia andiko lingine na lingine linalolingana au kuunga mkono wazo la kile unachotaka kukisimamia, maana yake huwezi kuwa na fundisho linalotokana na Mstari mmoja kwa hiyo kila neno lithibitike kwa kina cha ushahidi wa maandiko mengine zaidi 2Wakorintho 13:1 “Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.” Kwa hiyo mtafasiri wa maandiko anapaswa kuzingatia uwiano wa fundisho lake na maandiko mengine au na biblia nzima uwiano huo wa kimaandiko unaitwa  “cross references” yaani nukuu ya andiko moja ama linguine linalofanana na lile unalotaka kuelezea fundisho lako

 

4.       Wakati mwingine ni salama Kurahisisha maandiko kwa kuyachukua kama yalivyo badala ya kufikiri kuwa kila andiko ni fumbo, watu wengi wanaodhani kuwa maandiko ni mafumbo wanaweza kushawishika kutafasiri kila kitu hata vile ambavyo havihitaji tafasiri, na matokeo yake wanapotosha, Hata hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kwani pia sio kila andiko unaweza kulichukua kama lilivyo kwa mfano

 

2Wafalme 6:25 “Biblia ya Kiswahili inasema hivi Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.”

 

Unapoona neno Kibaba cha mavi ya njiwa na ukachukua neno hilo kama lilivyo ni rahisi kufikiri kuwa Samaria kulikuwa na njaa mpaka mavi ya njiwa yaliuzwa! Jambo hilo sio sahihi na hapo ndipo unapoweza kuona umuhimu wa sayansi ya kutafasiri maandiko, andiko hilo hilo ukilisoma katika biblia ya kiingereza linasomeka hivi

 

2Kings 6:25 “There was agreat famine in the city; the siege lasted so long that a donkey’s head sold for eighty shekels of silver and quarter of a cab of seed pods for five shekels

 

Unapoanza tu kuangalia andiko hilo kitaalamu kwa kuanza kuangalia Lugha iliyotumika katika matoleo tofauti tofauti ya buiblia utagundua kuwa neno KIBABA CHA MAVI YA NJIWA, kwa kiingereza CUB OF SEED maana yake ni KIBAKULI CHA MBEGU kwa hiyo kwa maamuma kuchukua njia rahisi au kurahisisha tu kunaweza kuwa salama na kunaweza kuwa hatari ndio maana maandiko yanahitaji wataalamu.

 

5.       Andiko au mstari unaotaka kuubiri au kuutumia lazima uzingatie wazo zima MUKTADHA wa kile kilichokuwa kinazungumziwa hapo karibu na wazo zima la kibiblia, huwezi kuchukua nyuzi moja na kuiita nguo, nguo ni mkusanyiko wa nyuzi nyingi. Hakuna andiko lolote katika Biblia ambalo likitafasiriwa vizuri kwa kuzingatia Mazingira yake MUKTADHA litaleta utata wa kimaandiko. Na kama utata utatokea basi mtafasiri atapaswa kuelezea utata huo, bila kutafuta kupuuzia ukweli unaofunuliwa na andiko hilo

6.       Panua ufahamu wako kuhusu Lugha na matumizi ya lugha katika Biblia kuna lugha za mafumbo Kuna aina mbalimbali za Lugha za mafumbo zinzotumika katika Biblia inasemekana ziko lugha za mafumbo zilizotumika katika Biblia zaidi ya 200 pamoja na mifano yake ipatayo 800 lugha hizo za mafumbo ni kama vile:-

·         Misamiati – (Vocabulary)

·         Mifano na fumbo la maneno  (Parable and allegories)

·         Ulinganisho unaotumia maneno  kama,  na na ulinganishi usiotumia neno kama na (Similes and Metaphors)

·         Maneno ya kuongoza chumvi (Hyperboles)

·         Maneno ya kuhuisha au kukipa kitu au mnyama uhai au ubinadamu ( Personification)

·         Kumliganisha Mungu na mwanadamu (Antropomorphism)

·         Jina moja kwa niaba ya linguine (Metonymy)

·         Sehemu moja kwa jambo lote au Sehemu nzima kwa sehemu (synecdoche)

·         Kuzungumza kinyume cha uhalisia ( Irony)

·         Lugha za mficho  inayotumika badala ya neno chafu Figurative language au (Euphemism )

·         Mithali (Proverbs)

 

7.       Uwe na ufahamu wa kutosha kuhusu uhusiano ulioko kati ya agano la kale na agano jipya na ni matumizi yapi ya kiagano yanatumika mpaka sasa na yasiyotumika mpaka sasa na yaliyosalia vile vile

8.       Uwe na ufahamu wa kihistoria wa andiko na maana iliyokusudiwa na mwandishi na namna inavyoweza kutumika katika nyakati za leo

9.       Uwe na ufahamu wa jinsi na namna ya kutafasiri mifano ya kibiblia

10.   Uwe na ufahamu wa jinsi na namna ya kutafasiri unabii, kujua yaliyokwisha kutimizwa na ambayo badio hayajatimizwa

Hitimisho.

Hiyo ni miongozo tu ambayo inamsaidia mtu anayetaka kutafasiri maandiko kuweza kuizingatia ili aweze kulileta neno la Mungu kwa usahihi, Mtafasiri wa maandiko pia anapaswa kuwa na Nyenzo mbalimbali zinazoweza kusaidia katika kazi hii ya kutafasiri maandiko Nyenzo hizo ni pamoja na

NYENZO MUHIMU ZINAZOSAIDIA KATIKA KUYATAFASIRI MAANDIKO KWA USAHIHI

ROHO MTAKATIFU:

Ni nyenzo ya kwanza na ya Muhimu sana mtu awaye yote anayetaka kuwa mtafasiri mzuri wa Maandiko ni lazima akubali kujazwa Roho Mtakatifu kumbuka kuwa yeye ndiye aliyevuvia watu kuliandika neno na ni mwalimu anaweza kutukumbusha na kutufundisha kile ambacho Mungu amekikusudia kwetu hivyo lazima mtafasiri wa maandiko awe amejazwa Roho ikiwa wale waliokuwa mashemasi nyakati za kanisa la kwanza walizingatiwa kuwa wenye Roho je si zaidi sana wanaojitia katia kazi ya kuyatangaza Maandiko ona mfano wa Stefano Matendo 6;8-55 kwanini ni muhimu kuwa na Roho mtakatifu?

·         Ni Mtafasiri mzuri

·         Ndiye Mwandishi wa Biblia

·         Anajua kile Ambacho Mungu anakijua

HAKIKISHA KUWA UNA BIBLIA ZA MATOLEO TOFAUTI

·         Biblia ya Kiswahili na za aina mbalimbali za matoleo ya kiswahili cha kisasa             

·         English Bible matoleo tofauti

·         Zile zilizoandikwa katika Lugha Tofauti Tofauti (Greek, Hebrew, Latin, Aramaic, na kadhalika)

UWE NA UJUZI KUHUSU AINA ZA MATOLEO YA BIBLIA

Kwa kawaida kuna matoleo makuu ya aina tatu za kibiblia zile zilizotafasiri neno kwa neno Literal translations, Zile zilizotafasiri kutokana na maana iliyokusudiwa, Dynamic Equivalent na zile tafasiri huru za lugha za kisasa Free translation mfano

                     Literal translations.           Dynamic Equivalence translations.      Free translations

                       Neno kwa neno                             Maana kwa maana                          Tafasiri huru

UWE NA BIBLIA ZENYE MAFUNZO NDANI YAKE; STUDY BIBLES,  REFERENCE OR ANNOTATED

Uwe na Biblia zenye mafunzo Studies Bible Zinatoa maana ya baadhi ya aya:

1.                   Mfano mzuri ni Full life study Bible (NIV) Biblia ya mafunzo ya uzima tele

2.                   Life Application Bible (LB)

3.                   Dake Bible

4.                   Scafield Bible, na kadhalika  

Uwe na  uchambuzi wa kibiblia wa watu wa aina mbalimbali COMMENTARIES: (Zenye uchambuzi wa mstari kwa mstari au kifungu kwa kifungu na kadhalika ).

Baadhi ya Commentaries nzuri kwa mfano ni Pamoja na

1.       Adam Clarke’s Commentary

2.       The New International Commentary

3.       The Evangelical Bible Commentary

4.       Mathew Henry Commentary.

Uwe na kitabu chenye ulinganifu wa kila neno katika biblia kuanzia a mpaka z CONCORDANCES   ITIFAKI

    • Itifaki yenye maneno yafananayo
    • Itifaki za maana ya meneno mfano  Malazi yawe safi -Ndoa
    • Mlinganio wa maneno yanayopatikana katika sehemu nyingine za Biblia.
    • Mfano Upendo upi? – Agape? Phileo? Storge? Eros?
    • Mahali lilipo neno Fulani

Mfano wa itifaki nzuri ni pamoja na ;-

o   Young’s Analytical Concordance

o   Strong’s Exhaustive Concordance etc.

o   Niv Exhaustive Concodance.

o   Kumbuka nyingine zina Kamusi za  kiibrania na Kiyunani  Lexicons (=Dictionaries )

Uwe na VITABU VINAVYOHUSU TAMADUNI ZA KIBIBLIA & MASWALA YA UCHIMBAJI WA   MAMBO YA KALE

Hii itakusaidia kuufahamu na kuwa na ujuzi kuhusu mambo ya kale kama na maneno yaliyotumiwa kama Busu takatifu, Tundu la sindano na mambo mengineyo.

KAMUSI ZA BIBLIA NA ZA LUGHA ZA KAWAIDA & ENCYCLOPAEDIAS:

Zinafafanua maana ya maneno Mbalimbali kwa ajili ya maswala ya kibiblia na maswala ya kawaida

1.            Kamusi za kawaida ni pamoja na zile za Kiingereza na kiswahili

·         English Language Dictionary

·         Swahili Language Dictionary etc. (Kamusi)

2.            Kamusi za Biblia ni pamoja na zilizo maarufu kama zifuatazo nyingi ni za kiingereza

·         Unger’s Bible Dictionary                                       

·         Pictorial Bible Dictionary                                       

·         Westminster Bible Dictionary                                  

·         Greek Lexicon & Hebrew Lexicon                        

·         Kamusi za kitheolojia (Theological Dictionary).

·         Kwa ajili ya kujifunza Mambo mbalimbali ya kitheolojia Mfano ni

·          Baker’s Dictionary of Theology

4.            Encyclopedias,

                Mfano; - International Standard Bible Encyclopedia

Uwe na MAFAFANUZI YA KIBIBLIA (BIBLE HANDBOOKS :)

Kwa ajili ya ufafanuzi wa Maswala mbalimbali, Vifungu, Maandiko, Tamaduni, Matukio ya kihistoria,  Ugunduzi wa maswala ya kale (archaeology), na kadhalika

Mfano

·         Halley’s Bible Hand Book

·         Unger’s Bible Hand Book

Uwe na MASOMO MBALIMBALI AU JUMBE MBALIMBALI (TOPICAL BIBLE).

Vitabu vinavyo weka mpangilio wa ufafanuzi wa masomo mbalimbali vikiwa na maandiko yoote husika sawa book arranged according to different topics with all the texts related to each topic.

Mfano Nave’s topical Bible

Uwe na ATLASI ZA KIBIBLIA NA MSWALA YA KIHISTORIA (BIBLE ATLASS) & HISTORY

Kwa ajili ya kutambua sehemu Mbalimbali na umbali kwa kilomita za mraba n.k na vipimo kama homeri, yadi, mwendo wa sabato, Ridhaa n.k

·         Baker’s Bible Atlas

·         The Oxford Bible Atlas

Uwe na tabia ya kusoma Biblia, kusikiliza mahubiri ya wahubiri wengine, kuwa na akili ya kusoma vitabu mbalimbali na kupoanua maarifa kila wakati na kila siku, penda kujifunza na kufundisha na hakikisha kila wakati unakua na jambo jipya la kushirikiana na wengine

Na Rev. Innocent  Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

0718990796.