Jumatatu, 29 Februari 2016

Mwitaliano Orijino Akaletwa Kwangu!


Nakumbuka mwaka lakini tarehe na mwezi umenitoka kidogo, lakini ilikuwa ni mwaka 2002 Nilikuwa nauza duka la jamaa yangu kule temeke wakati ule, nilikuwa ndiyo nimemeliza kidato cha sita , nasubiri kwenda zangu vyuoni  Nilifika hapo temeke nikitokea nyumbani Handeni, nilipofika hapo niliona nijifanye mimi kuwa mtoto wa mjini  ili nipokelewe vizuri na vijana wenzangu. Ni kweli nilijifanya najua vitu vingi sana, nilikuwa naawaambia rafiki zangu kuwa nimesoma sekondari nchini Namibia ambapo baba alikuwa akifanya kazi kwenye ofisi za FAO. 


Mwitaliano Orijino alitaka kujichanganya jamaa wakaniletea


Nilikuwanawaambia kwamba nilikuwa natembea kwenye inchi kadhaa  za ulaya kwani baba yangu alikuwa akipata tiketi za bure kila mwaka  kusafiri na familia yeke kwa kweli sio siri nilibaini kuwa vijana wa Dar ni washamba  kuliko wale wa vijijini, kwa nini niliamini hivyo? ni kwa sababu waliamini kila nilichokuwa nikiwaambia na kuonyesha kuvutiwa sana kiasi kwamba pale dukani pakawa ni kijiwe kilichositawi, mara nyingi nilikuwa napenda kusisitiza sana kuwa nchini Italia tulikaa kwa miaka mitatu  wakati baba anasoma ambapo aliruhusiwa kwenda na familia yake niliwaambia kuwa hata masomo nilikuwa nasoma kwa kiitaliano na kuwa ninakikumbuka sana.

Nilizidi kuwaambia kwamba huwa ninakwenda ubalozi wa Italia hapa nchini  kupiga stori na baadhi ya watumishi wa pale kwa kiitaliano, niliwaambia huwa nafanya hivyo ili nisikisahau, Walikubaliana name na  kunitazama kwa heshimna kubwa , siku hiyo ya tukio  nikiwa dukani  walikuja jamaa zangu wawili  na Mwitaliano mmoja ambaye gari lake lilikuwa limaharibika  na alikuwa anatafuta msaada na pia ilionekana kuwa kuna jambo linguine anataka kulijua , niliposikia hivyo mashuzi na jasho vilianza kunitoka niliona wazi wazi kuwa kuadhirika kumewasili, Niliwaambia kuwa wakati ule niko bize  siwezi kwenda kumwona muitaliano huyo, wale jamaa zangu walinishawishi wakisema ni jambo zuri kwangu kwenda kani litanipandishia ujiko zaidi,, niliwaambia ni sawa lakini nisingeweza kuacha duka peke yake wala kulifunga. 

Wale jamaa zangu waliridhika na kuondoka, lakini kiasi cha dakika kumi baadaye  niliwaona wakija na mzungu alipofika na wale jamaa zangu waliniambia kuwa Yule ni muitaliano,  nizungumze naye , sikuwa najua hata neno moja la kiitaliano  ilibidi nizuge kwa kusema kwamba Yule jamaa huenda anatoka Italia ya kusini ambapo kiitaliano chao hata wenzao hawakielewi, nilijifanya namsemesha Yule mzungu kiitaliano kwa kusema Fkorsia deminati maneno ambayo hata mimi nilikuwa siyajui maana yake mwitaliano alibaki ameshangaa  na kuonyesha ishara ya kuwa hanielewi, wakati huo huo alipiata mzee mmoja ambaye aliuliza kinachoendelea  na kuamua kuingilia kati  kwa kuzungumza na Yule mzungu , walielewana sana na Yule mzee akampa Yule muitaliano maelekezo, alipoondoka Yule mzee aliniuliza nilipokuwa ninaishi kule Italia Nilimwambia Rome aliniuliza mtaa nikakwama  aluniuliza mambo mengine ambayo wala sikuwa nayajua nikakwama kabisa jamaa zangu walianza kucheka hadi machozi yakawatoka , kwa kweli nilibaki nimeduwaa, Yule mzee alisema hujafika Italia hata kwa kusoma kitabuni, Halafu aliondoka Jamaa zangu hawakuwa na mbavu, ilinibidi nifunge duka siku ile  kwa muda , kilitokea kitu gani baada ya hapo? Unataka nikujibu subiri naomba unionyeshe cheti chenye kuthibitisha kuwa niliwahi kuishi Mirembe.

Ukawa ni ugeni wa kupiga deki !



Nilitoka huko kwetu liwetwe Songea mara baada ya kumaliza elimu ya msingi, shangazi yangu alimuomba kaka yake ambaye ni baba yangu anichukue huku Dar es Salaam ili nimsaidie shughuli zake za mama nitilie, tulipanda basi la shabiby hadi hapa Dar safari yetu haikuwa nzuri nilisikia kizunguzungu na kutapikaa nia nzima, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusafiri na kupanda basi kutoka kijiji chetu. 

 Mara yangu ya kwanza kupanda basi kutoka Songea kuja Dar es Salaam

Kijana niliyekuwa naye jirani alionekana kunihurumia sana kutokana na ile hali, Tulipofika ubungo kijana Yule alionesha wema kwangu kwani alitusaidia kushusha mizigo, tulipanda basi la ubungo mwenge – mbagala ili tufike keko shangazi alikokuwa anaishi.

Nilipenda sana mazingira ya keko kwani watu wa nyumbani walikuwa wengi hivyo sikuchelewa kuwa mwenyeji Shangazi alinichukua kwenye shughuli zake kutokana na ucheshi niliokuwa na adabu ya watu wa Songea hasa kitendo cha kuamkia watu, kuwapa chakula wateja na kuwakaribisha , kushukuru nikiwa nimepiga hatua  nikiwa nimepiga magoti kiliwafurahisha wateja . kati ya wateja waliokuwa wanajaza wateja wanajaza mgahawa wetu  ni pamoja na kijana niliyekaa naye siti moja wakati wa safari ya kutoka songea kuna vitu ambavyo  hutokea kwa njia ya ajabu  sana, tuilizidi kumpenda na kumuona ni ndugu yetu hasa, hatimaye kijana Yule aliutumia mwanya huo kumweleza shangazi nia yake ya kutaka tuwe wawili ili tuijaze dunia, sijui ni kwa nini  shangazi aliniruhusu kuhamia kwa Yule kijana kwani tulianza kuunganisha mwili na kuwatafuta hao watoto hata kabla ya ridhaa ya viongozi wa dini au wa mila  yetu na wazazi pia au alifanya hivyo ili kutoa muda kwetu wa kupimana tabia na mengineyo.

Siku ya nne baada ya kuhamia kwa huyo mshirika wangu, wifi yangu alikuja kunisalimia , aliniletea zawadi  ya unga mweupe wa muhogo  unaorowekwa kwenye maji, kule Songea tunaita kindowole na dagaa wa ziwa nyasa Niliushambulia ugali huo kama vile sina akili nzuri vile. Yaani niliula kwa pupa sana , Mshirika wangu siku ile alienda kazini  usikui ili arudi asubuhi. Hivyo ilipotimu majira ya saa sita hivi usiku nilisikia tumbo linauma kwa mtindo unaoashiria kuwa vyakula vyote vilivyomo tumboni vitoke nje Nilitoka chumbani kuelekea mlango wa kutoka nje  Mlango ulinishinda kufungua  na Uharo usiokuwa wa kawaida wala adabu ulinitoka, na kinyesi kilitapakaa pale mlangoni, kumbe inzi wa huku Dar hawalali waliamshana usiku ule na kushangilia neema ile iliyokuwa imewazukia. Wapangaji wenzangu  waliamshana na kusimama  kwenye milango ya vyumba vyao  huku wakiwa wameshangaa wazi na kunidharau, labda kwa kuniona mshamba . Kazi ya kupiga deki  ilianza usiku  huo huo Mpenzi wangu aliporudi kutoka kazini nilimsimulia yote yaliyotokea  na nilimuomba tuhame ila Mpenzi wangu hakuwa tayari kuhama  kwa wakati ule, kwa hiyo asubuhi ya silku ile  na siku zilizofuata zilikuwa ni za fedheha kwangu, Hatimaye hata hivyo tulihama, Hadi leo nikiona unga wa muhogo au ugali wa muhogo tumbo linafanya  fujo ya ghafla, kama vile kunipa tahadhari lakini huwa ninaula unapokuja kwenye anga zangu.  

Dada akaagiza tena Bwana!


Napenda watu wengine wajifunze kutokaa na uzoefu wangu na ndio maana naelezea kisa hiki najua wale wanaonifahamu watajua kwamba ni mimi, naomba hawa wachukulie kuwa nasimulia ili wengine wajifunze siyo kwa sababu nyingine, Mwaka 1996 nilikuwa nafanya kazi katika duka la vipuri vya magari lililokuwa eneo la msimbazi jijini Dar es Salaam, ukweli ni kwamba nilikuwa natengeneza pesa sana kwenye duka hili  zilikuwa ni fedha za wizi, labda ndio maana duka lenyewe halikudumu kwani lilifungwa mwaka 1996.

  
Nilikodolewa Mijimachi kila kona ya bar na Disco kwa kujifanya ninano kumbe ulofa tu!


Kwa hiyo baada ya duka kufungwa nikawa sina kazi, kwa sababu nilikuwa mtu wa matumizi sana, sikutaka kujishughulisha ghafla nilitaka kulinda hadhi na heshima yangu, kwa hiyo niliendelea na matanuzi yangu  nakumbuka ilikuwa juni 1997  yaliponikuta maswaiba haya 

Siku hiyo nilikwenda kwenye ukumbi mmoja maarufu wakati ule hapa Dar nasema wakati ule kwa sababu ndio ulikuwa unafunguliwa, nilikwenda pale kwa kupewa ofa ya kuingia ukumbini na rafiki yangu mmoja , aliniambia atanikatia tiketi  halafu maswala ya vinywaji ningejua mwenyewe, Nilikubali. Ni kweli baada ya kuingia ukumbini akamchukua bibi yake wakaenda kukaa kivyao, nilikuwa na shilingi 1000 mfukoni ambapo ningeweza kunywa bia kama mbili kwa wakati ule kwenye ukumbi kama ule, wakati naanza kunywa  bia niliyokuwa nimeagiza akaja msichana mmoja  ambaye awali sikuwa nimemtabua, baada ya kunisalimu kwa kunitaja nilimtambua  alikuwa ni msichana ambaye wakati nawika kwa fedha  niliwahi kufanya naye mapenzi, kwa bahati mbaya alisafiri kwenda Mauritius kwa kaka yake, haki ya Mungu leo nataka nikunywe hadi ukimbie nina hamu na pombe yako na mwili wako alisema, kabla sijajibu alimwita muhudumu  na kuagiza pombe kali nilijua kuwa ile oda moja tu ilihitaji 1000, nilijichangamsha na kujifaragua  lakini moyo wangu ulikwenda mbio nikianza kufikiria deni  la hiyo pombe nikiwa nafikiri aliagiza nyama choma, mazungumzo yalikuwa makali sana, huku binti Yule akinisanifu kwamba ninazo, nilijisikia vibaya ila sikuweza kusema, kufika saa sita usiku alikuwa amekunywa na kula kiasi cha shilingi 9000 mfukoni nilikuwa na 1000, bili ililetwa nilijua sina hela lakini ajabu sikusema hivyo, nilitulia huku nikitafakari, ingawa akili haikufanya kazi, baadaye kidogo  muhudumu alirudi kuchukua malipo. Alikuta sahani ya kuwekea hela iko tupu, aliondoka baadaye kidogo alirudi tena na kukuta sahani iko tupu haina kitu.

Aliuliza kwa upole ni nani anatakiwa kulipa , naomba malipo kwani namaliza shifti nilimwambia Yule mwanamke mwambie anayekupokea aje  nitamlipa yeye, Yule muhudumu alisema inanibidi nikamilishe hesabu ndipo niondoke, nilinyamaza halafu Yule msichana alianza kupayuka, alianza kunitukana na kunisimanga kwamba najifanya nina kitu wakati nimechoka, alinitukana hadi matusi ya nguoni, ilibidi watu waache burudani zao watupe macho na masikio kule kwetu na wengine walifika kabisa pale kwenye vurugu akiwemo na meneja wa ukumbi, kama unavyojua tena mitanzania kwa umbeya!

Nitalipa mimi achaneni na huyu bwege aende zake Pamoja na kuwa alikuwa amelewa nilijua alikuwa ananikomoa, nilitoka nje ya ukumbi kama aliyenyeshewa Nilikuja kugundua kuwa ile ilikuwa ni njama ya yule rafiki yangu aliyenipa ofa kunikomesha kujifanya bado nina pesa wakati nawapa shida wengine, ingawa haikuwa njia ya kiungwana kunifundisha lakini nashukuru kwani tangu wakati ule hadi leo maisha yangu sio ya kujionyesha bali naishi kama mimi. Cheki ulivyokodoa mimacho ishi kama Mungu alivyokujalia acha kujiinua!

Mtendeeni Yule Kijana Absalom kwa Upole kwaajili yangu!



Utangulizi
(2 SAMUEL 18:1-5) “1. Kisha Daudi akawahesabu watu waliokuwa pamoja naye, akaweka maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia juu yao. ,2. Daudi akawapeleka hao watu vitani, theluthi moja chini ya mkono wa Yoabu, na theluthi ya pili chini ya mkono wa Abishai, mwana wa Seruya nduguye Yoabu, na theluthi ya tatu chini ya mkono wa Itai, Mgiti. Mfalme akawaambia watu, Bila shaka mimi mwenyewe nami nitatoka pamoja nanyi. ,3. Lakini watu wakasema, Wewe usitoke nje; kwa maana tukikimbia, hawatatuona sisi kuwa kitu; au tukifa nusu yetu, hawatatuona kuwa kitu; lakini wewe u wa thamani kuliko watu elfu kumi katika sisi; kwa hivyo sasa ni afadhali ukae tayari kutusaidia toka mjini. 4. Mfalme akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa elfu zao na mia zao. 5. Mfalme akawaamuru Yoabu na Abishai na Itai, akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu. Nao watu wote wakasikia, mfalme alipowaagiza maakida wote katika habari za Absalomu.” 
  
 Uzuri wake Absalom na tamaa yake, moyo wa kisasi, hila, uchungu na kutenda kwa upumbavu viligharimu Maisha yake, Daudi alilia laiti ningelikufa mimi mwanangu Absalom
      
Moja ya maswala magumu sana katika maisha ni pamoja na kufanya maamuzi hususani wakati mtu unayempenda na kumthamini anapokufanyia jambo bay asana na jambo hilo ukawa umelithibitisha, katika nyakati kama hizo

·   Watu wengi huweza kutoa adhabu kali sana za kukomesha na kuangamiza pale wanapokuwa wamefanyiwa mambo mabaya,
    Tumeshuhudia watu wakiwachoma moto watoto wadogo kwa sababu tu wamechukua fedha ua wameiba
·       Wengine wamewaadhibu kwa kuwachapa vibaya kwa mikanda na kuwajeruhi wakosaji
·       Wengine wamemwagiwa tindi kali
·       Wengine wamepeleka taarifa katika vyombo vya habari na magazeti
Makanisani pia tunashuhudia watu wakitengwa na kufukuzwa utumishi bila malipo yoyote, wakinyimwa posho, kutengwa miezi kadhaa, kufungiwa huduma kuchafuliwa na kuwauia kihuduma ili yamkini ikiwezekana wasiinuke tena
Je unafanya nini wakati uwapendao, watoto, ndugu, jamaa, rafiki, na kadhalika wanapokuasi na kusimama kinyume nasi na kuanza kutubomoa, wale tuliowagharimia wanapotukosea tunafanya nini?
2 Samuel 18:1-5 Katika kifungu hiki Daudi analazimika kupigana vita, vita hii ni mbaya kuliko zote alizowahi kupigana katika maisha yake ni vita ngumu safari hii mfalme hapigani na wafilisti wala Goliath wala maadui za Bwana anapigana na ndugu zake mwenyewe Israel wakiongozwa na mwanaye mwenyewe
Hakuna vita mbaya duniani kama vita vya wenyewe kwa wenyewe, ni vita ngumu, ukisema ummalize adui ni kama unajimaliza mwenyewe Mathayo 12:25-26 Yesu anaonyesha ubaya wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vita hii ndio iliyokuwa ikimkabili Daudi wakati huu, hapa ilikuwa vita inayoweza kuleta ukiwa mkubwa sana
Vita yoyote ya Taifa kwa taifa yaani taifa lililogawanyika
Vita yoyote ya Familia iliyogawanyika
Vita yoyote ya mtu na mkewe au mtu na mumewe
Vita vya mtu na rafiki yake
Vita ya mtu na mchumba wake
Vita ya watoto na wazazi
Vita vya mtu uliyengharimia
Vita vya mchungaji na wachungaji wenzake au na wazee wa kanisa
Au wanakwaya kwa wanakwaya
Vita za namna hii zinakuwa mbaya sana na vinasababisha ukiwa mkubwa hasa inapotokea kuwa upande mmoja unakusudia kuumlaliza upande mwingine kabisa huku hakuna anayefaidika na vita hiyo
Haya ndiyo yaliyomkuta Daudi mara hii anapigana vita na mwanaye mpendwa mzuri aliyeitwa Absalom
Absalom alikuwa kijana wa mfalme aliyesifiwa sana , alikuwa mzuri namsafi, alipendeza na kuvutia  na alikuwa na ushawishi kwa watu, alikuwa na nywele nzuri na ndefu ambazo zlilikatwa mara tatu tu kwa mwaka , hakuwa na ila ya aina yoyote kwa habari ya uzuri, pia alikuwa na akili hata hivyo mambo kadhaa yalichangia kuharibu maisha ya kijana huyu
Alikuwa na Uchungu
 Alikuwa ni kisasi
Alikuwa na Hila
Alikuwa na kiburi na mwenye kukosa Subira pia hakuwa na msamaha
Mambo haya yalipelekea kijana huyu kumuasi baba yake na kujitangaza kuwa Mfaleme 2Samuel 14:25-26.

Kijana huyu alikuwa na uwezo wa kutumia hila na akili aliyonayo aliweza kuhadaa mioyo ya watu kwa muda wa miaka kama minne hivi 2Samuel 15:1-12, Safari hii uasi wake ulikuwa na nguvu ya kupita kawaida na alitaka kuithibitishia Isarael ya kuwa kweli amaemuasi baba yake 2Samuel 16:21-23 Mshauri wa Absalom alishauri kuwa anayepaswa kuuawa hapa ni Daudi peke yake na sio vinginevyo ili watu wakae katika amani 2Samuel 17:1-4
Unaweza kuona kuwa kijana wako uliyemzaa mwenyewe na ni Mashuhuri anakuasi waziwazi na anakusudia kukumaliza kabisa, amekuvunjia heshima yako hadharani amekudhalilisha  anakuweka katika wakati mgumu je katika hali kama hii unafanya nini hivi ndivyo Daudi alivyofanya nasi ni muhimu tukafanya

1.       Kubali kushuka
Watu wengi sana hususani vijana  na viongozi mbalimbali watu wao wanapowaasi, hawakubali kujishusha hata siku moja, wanataka kushughulikia matatizo wakiwa katika mamlaka yao ileile au katika mfumo wa cheo chao hujui mi mumeo, hujui mi askofu wako, Daudi alijua kuwa nia hii sio rahisi kufanikiwa kumpata mpendwa wake yeye aliamua kujishusha, aliachia ikulu na kukimbia pekupeku alijua kuwa hawezi kujiokoa wala kuwaokoa watu wake na mwanaye kama atabakia ikulu aliondoka 2samuel 15:14,30 Ili kumpata mwanadamu aliyeasi Yesu alikubali kuacha Enzi na utukufu, akanyenyekea kama mwanadamu mtumwa, watu wanavutiwa na mtu aliyejishusha, na sio Yule anayebaki ikulu, anayebaki katika haki yake na mamlaka yake , Absalom aliweza kuihadaa mioyo ya watu kwa sababu alijinyenyekeza kwao watu wakampenda 2Samuel 15:5-6, alifahamu kuwa ili aipate mioyo ya watu  hana budi kujishusha katika kiwango chao, ili kuipata mioyo ya watu jishushe katika kiwango chao,Kamwe usitumie mamlaka yako katika kutatua matatizo, hujui mimi ni mzazi wako?, hujui mimi ni mumeo? Hajui mimi ndiye Rais?, hujui mimi ndiye Askofu? Atanitambua atajua kuwa mimi ndiye mwenyeji, mimi ndiye mwangalizi, mimi ndiye alwatani, mimi ndiye nimeshika mpini. Daudi aliacha viatu, alichukua namna ya mtumwa, aliondoka ikulu, Kujishusha kunasaidia kutatua matatizo, 1Samuel 25:1-4, Mungu humwangalia mtu mnyonge, mwenye roho iliyopondeka na kumuinua Wafilipi 2:5-8, Hatuwezi kutatua matatizo yetu bila kuamua kujishusha, kujishusha na rohoya unyenyekevu kumesaidia kujenga maisha ya watu wengi sana , kiongozi anayekaa ofisini tu bila kujali wala kujua matatizo ya watu na mahitaji yao, hawezi kukubaliaka na kufaa kwa Mungu na watu.

2.       Rudisha sanduku la Mungu mahali pake 2Samuel 15:24-29
Sanduku la Agano la Mungu lilikuwa chombo muhimu sana chenye kuwakilisha uwepo wa Mungu, Ni chombo kinachoonekana kinachowakilisha uwepo wa Mungu asiyeonekana, Chombo hiki kilimwakilisha Yesu Kristo, aliye chapa ya mng’ao wa utukufu wa Mungu, Isarael waliamini kuwa hata ukiingia vitani na chombo hiki lazima utashinda, Viongozi wengi sana wanapokuwa madarakani, huwa wanasahau kuwa unaweza kuwepo madarakani lakini Mungu au uwepo wa Mungu ukawa hauko pamoja nawe, unaweza kuwa mpakwa mafutalakini Mungu akawa amekuacha , kama ilivyokuwa kwa Sauli mfalme, nNi lazima kwa nza ufahamu Mungu yuko upande wa nani unapokuwa na miggogoro, Absalom au wewe? Mungu yuko upande gani Hakuna mtu mwenye hati miliki ya uwepo wa Mungu, Mungu yuko kwaajili ya watu wote, si vema kuwahesabu wengina na kuwahukumu kama waasi tu, Daudi alitaka apate muda wa kupata na kusikia neno la bwana ili kujua kuwa Bwana amempa kibalia nani kati yake na Absalom, kama Bwana yuko na Absalom basi Absalom awe na uhuru nwa kuabudu kupitia sanduku la agano, na kama Bwana yuko naye basi atampa neema ya kuliona sanduku hilo tena lakini sio kuondoka nalo, halikuwa la kwake lilikuwa kwaajili ya watu wote wa Mungu,
·         Viongozi wengi sana wa kiroho nimeona wakiwatenga watu wanaodhani kuwa ni wenye dhambi na zaidi ya yote huwafukuza na kuwanyimba hata kuabudu, aku kufanya huduma fulanifulani kabisa wakiwahesabia dhambi na kuwapimia muda wa miezi na hata miaka lakini huwa wanasahau kuwa kipimo cha utii katika moyo wa Mwanadamu anacho Mungu tu, Mtu hapimwi kwa kumzuia asihubiri, asiombe au kutoa sadaka huko ni kuhukumu na kujichukulia madaraka makubwa
·         Au wanaweza kumzuia mtu asifanyie wengine maombezi, swala la Ibada kwa binadamu liko wazi kwa kila mtu,swala la ibada halina hakimiliki, kuabudu ni swala huru kwa kila mtu hata kama sio wa dhehebu lako, Mungu si wa dehebu Fulani au dini Fulani kila mtu anahaki ya kuabudu na anapaswa kuabudu, kila mtu anapewa nafasi na maandiko na anapewa haki ya kuufikia uwepo wa Bwana Luka 9:49-50, Matendo 4:18-20 Ni kwa kujua haya Daudi aliwaambia makuhani walirudishe sanduku la agano mahali pake, Mungu atusaidie kuwa na moo kama wa daudi wa kutambua kuwa uwepo wa Mungu sio hatimiliki  ya mtu gfulani, au kanisa Fulani au mchungaji Fulani au askofu Fulani kila mtu ana haki ya kuabudu.

3.       Fanya maombi ya kujidhili ( Kujishusha). 2samuel 15:30-32
Daudi alifanya maombi ya kujidhili yaani alijishuhsa, alilia, hakwenda mbele za Mungu kama mwanamume na mfalme bali alikwenda kama mjakazi wa kike , alijifunika kichwa alipokuwa akimuomba Mungu Kutoka 34:29-35, 1Korith0 11:3-7, Mwanamume hapaswa kufunika kichwa anapoingia katika uwepo wa Mungu, kuomba, hivyo maombi na dua za Daudi zilihusisha kujishusha kwa kiwango kikubwa na cha halia ya juu, Luka 18:9-14 Mungu hakubalia maombi ya watu wenye kujihesabia haki, Daudi alifahamu kuwa anahitaji maombi ya kujinyenyekesha wakati huu kupita kawaida ili hatimaye Mungu aweze kumuinua tena, alirusha michanga juu alitembea pekupeku alijifunika kichwa na kulia

4.       Panga vita (Mikakati) ya ukombozi
Nimuhimu kukumbuka kuwa hakuna vita ngumu duniani kama vita ya ndugu kwa ndugu, vita ya aina hii haina mshindi, ni ngumu na ni lazima  itaacha majeraha yanayoweza kudumu kwa muda mrefu, huwezi kupanga vita ya ndugu ikawa vita ya kumalizana, mwisho wa yote utalia mwenyewe, Ni lazima vita ya aina hii iwe vita ya ukombozi 2Samuel 18:1-5 Daudi aliona uzito wa vita hii kwani sasa hapigani na Mfilisti wala Goliath anapigana na mwanaye aliyetoka katika viuno vyake
Vita unayopigana na nduguyo ni lazima iwe vita ya ukombozi, Mara nyingi viongozi weni wa kiroho na Kikristo, kunapotokea shida za ikmahusiano mioyo yao hubadilika na kusahahu hili, mapambano yao na makusudi yao yanakuwa ni kukumaliza kabisa au kumlaiza nduguyo, kumpoteza, kufuta jina lake kumfanya akome, asione suluhu tena Daudi hakutaka kabisa kumpoteza Absalom aliagiza wazi mbele ya makamanda wote “MTENDEENI YULE KIJANA ABSALOM KWA UPOLE KWAAJILI YANGU” haya ni maneno mazito Daudi aliyasema haya hadharani, na watu wote walisikia , alikuwa na moyo, Daudi alikuwa na moyo wa kiungu, siku zote Mungu anapotuadhibu kwaajili ya makosa yetu na dhambi hutuadhibu kwa kusudi la kuturekebisha na kuturejesha, na sio kutuangamiza, Daudi alitambua udhaifu wa mwanawe Absalom kuwa ni ujana ndio unaomsumbua ni mchanga ni kuwa hajakomaa hajajua maisha, ni dasarindogondogo zinamsumbua na aliona ni afadhali angelikufa yeye badala ya mwanawe Asalom 2Samuel 18:33-19:4 Biblia inasemaje ndugu yako anapokukosea ni laazima arejeshwe kwa upole Wagalatia 6:1 Daudi alikuwa na moyo wa urejeshi huu ndio moyo wa Mungu ndio moyo wa mtu aliyekomaa kiroho
Mungu kamwe hafurahii kufa kwake mtu mwenye dhambi Ezekiel 33:11 Daudi hakufurahia kifi cha Absalom mwanawe, ambaye kwa vyovyote alikuwa hajaifikilia toba, Upendo wa kweli haufurahii udhalimu, Moyo wa daudi ulikuwa tayari, kufanya kitu kwaajili ya mtu muovu, kuliko watu wema waliokuwa upande wake 2Samuel 19:5-6 Ulikuwa ni moyo wa ajabu sana na upendo mwingi usioweza kupimika najua angaekuwa mtu mwingine angesema ndio afadhali kafa, Mungu kamlipizia kisasi, Mungu ameshughulikia adui zangu lakini huu haukuwa moyo wa Daudi na sio moyo wa Mungu.

5.       Mtendeeni kwa Upole
Ingawa Absalom alikuwa amekusudia kumuua baba yake na kuwaacha watu hai, Daudi alikusudia wazi kwamba Absalom aachwe hai, Daudi alitoa nafasi ya pili kwa mkosaji, alitoa nafasi ya tatu na ne na tano na kuendelea, ni vema kuwapa wakosaji nafasi nyingine tena nani ajuae kuwa mioyo yao itabadilika nani ajuaye kuwa watakuwa wamejifunza maswala kadhaa?
Daudi hakutaka kushindana na Absalom ni muhimu kufahamu kuwa hatupaswi kushindana na mtu aliye chini yako, Daudi hakuhesabu kuwa yuko vitani huwezi kupigana na mwanao hata kama yeye ni shetani, Mungu hapigani na shetani, hata siku moja ingawa yuko chini yake ni ujinga, daudi hakufurahia kufa kwa mwanaye, hakufurahia kifo cha kudhalilika cha mwanaye ingawa yeye alikuwa amedhalilishwana mwanaye, Daudi anaumia sana asiposamehe, alipenda kama angelipata nafasi ya kumtangazia mwanaye msamaha, alijuta kuikosa  nafasi hiyo alitamnani kama laity angelipata nafasi ya kumwambia mwanangu nimekusamehe, Dhambi ya Absalom ni maumivu kwa Daudi Isaya 43:25 Mungu anapotusamehe dhambi hutusamehe kwaajili yake mwenyewe upendo wake unamsukuma kusamehe na anaumia anapokosa nafasi ya kutusamehe, “Mtendeeni Yule kijana Absalom kwa upole kwaajili yangu” Tabia ya Daudi ni tabia ya uungu inayoonyesha ukomavu wa hali ya juu.
Daudi hakumuhukumu Absalom kwa vyovyote vile alimuachia Mungu ahukumu adui zakena wote waliomkataa na kumkana.
Mungu ndiye hakimu wa kweli atakayehukumu kwa haki dhidi nya maisha yetu
Mtazamo wako si ukweli kuhusu Mungu wakati wote.

Jumapili, 28 Februari 2016

Ufahamu kuhusu Saikolojia!



UTANGULIZI
     Kwa ujumla kujifunza kuhusu watu ni muhimu sana kuliko kujifunza kuhusu mambo mengine na kwa kuwa wanadamu wana umilele Mchungaji ni lazima awe na uwezo wa kuwashawishi na kuwavuta ili waufikie mwisho wao wa kimilele katika njia iliyo njema. Kadiri tunavyojifunza kuhusu watu ndivyo tunavyoweza kuwa na ujuzi wa kuwashawishi ingawaje kutegemea uwezo wetu tu wa kawaida bila kutegemea upande mwingine wa maisha yetu ni hatari sana na sio kusudio la somo hili lakini japo kwa kiwango kidogo ni muhimu kuwa na ujuzi kuhusu wanadamu Bila kuacha kumtegemea Mungu. 

    Ingawaje wanadamu wanatofautiana kulingana na mazingira na tamaduni kwa ujumla wana mambo ambayo kwa kawaida yanafanana sana au woote huyashiriki na tunapoona mwengine anaenenda Tofauti na tabia isiyokuwa ya kawaida  kama wengine tuna kuwa na mashaka kuwa ana maumbile Tofauti kisaikolojia lakini lazima utafiti wa kisaikolojia au Elimu ya viumbe yaani Baiolojia ifanyike kwa kulinganisha na jamii ya mtu huyo  mama yake kabila yake  na kadhalika ndipo ithibitike kuwa ni tabia tofauti kisaikolojia lakini zaidi ya hapo wanadamu katika ubinadamu tunafanana, Paulo Mtume alisema hivi Matendo 17;26 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja wakae juu ya uso wa inchi yote akiisha kuweka nyakati alizoziamurutangu zamani na mipaka ya makazi yao”

    Lakini ni muhimu kujibu swali moja la msingi kabla ya kuendelea je ni muhimu kusoma Saikolojia kwa wakristo? Baadhi ya watu huamini kuwa Saikolojia ni chombo cha shetani cha kudanganyia watu wenye mapenzi mema hii inaweza kuwa kweli kwa sababu wengi wa wasomi wakubwa wa Saikolojia ni watu wasio na wokovu hata hivyo siku hizi kuna watu wengi waliookoka waaminifu ambao ni wataalamu wa Saikolojia na wanapigia kelele umuhimu wa kujifunza Saikolojia wakidai kuwa wanafunzi wa Yesu wanaweza kufaidika kwa mengi kupitia kusomea Saikolojia katika mtazamo wa Kikristo
   Somo hili linafanya kazi hiyo na linaweka japo kwa Muhktasari yale ambayo ni muhimu kwa watumishi wa Mungu kuyajua na kuwasaidia wakati wa kuhubiri injili hivyo haina kusudi la kumfanya mtumishi wa Mungu kuwa mwana Saikolojia lakini kukutia moyo na kuyatumia katika maisha yako na kwa faida ya watu ambao Mungu amekupa uwahudumie hii itakuwa faida kubwa kwani tunaamini kuwa somo hili litakusaidia pia kuwahudumia watu ambao wanapitia misukosuko kadhaa ya kimaisha na tabia za binadamu

Kila sura ya kitabu hiki inatoa mwanga wa kiroho pia kwa aajili ya kweli Fulani za Kibiblia na mjadala wa kibiblia kuhusiana na jambo linalojadiliwa hapo kwa hiyo uwe na amani unapopitia somo hili na Mungu akubariki sana Sali sala hii pamoja nami 

“Bwana mwema wewe ulisema usimwache Elimu aende zake naomba unipe ujuzi huu lakini uufanye kuwa Baraka kwa mambo ya rohoni kwani Elimu zote na maarifa na Ufahamu na Hekima vyote vinatoka kwako nasi tunapokea ili tuvitumie kwa utukufu wako asante Mungu kwa kunipa neema hii ya kusoma somo hili ili niwe msaada kwa jamii ya watu uliowaita kwa faida ya ufalme wako asante Bwana Yesu kwani kupitia Roho Mtakatifu utapanua ufahamu wangu na kuzidi katika jina la Yesu Amen”


UFAHAMU KUHUSU SAIKOLOJIA NA ASILI YA SAIKOLOJIA
Kwa kawaida wanadamu wanatafuta faraja, maisha mazuri ya amani na utoshelevu hii ndio maana tunaona hata mtoto mdogo hulia anapokuwa anahitaji jambo Fulani na hufurahi anapokuwa ametimiziwa haja zake.kadiri mtoto huyo anapokuwa mkubwa hutoa kipaumbele kwa watu waliokaribu naye na wanaohakikisha anakuwa na mazingira mazuri. Lakini anapokuwa amekomaa zaidi kuwa mtu mzima anaanza kujitegemea na kuanza kushughulikia kufanya mambo ya wengine yaweze kuwa mazuri, Pamoja na umuhimu huu wa ukuaji na maendeleo ya mwanadamu kunakuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini mwanadamu anatenda hivi anavyotenda na kuunda aina ya ushiriki na hii inaonekana katika kila jamii na tamaduni.mambo haya ni ya muhimu katika msingi wa Ufahamu kuhusu Saikolojia

MAANA YA SAIKOLOJIA

Kuna maelezo mengi kuhusu Saikolojia na kila maelezo yanasisitiza sehemu Fulani ya ya Ufahamu kuhusu Saikolojia maelezo yafuatayo yatakuwa ni muhimu kwa mtazamo wa somo hili
Saikolojia ni Elimu kuhusu tabia za mwanadamu, uzoefu na maendeleo ya akili katika uhusiano wa jamii na mazingira yake.

Saikolojia ni sayansi inayohusu utendaji wa akili unaohusiana na tabia za mwanadamu katika kulenga kuielewa, kuona yajayo mbeleni na kuisahihisha hiyo tabia

Neno Saikolojia limetokana na neno Psychology la kiingereza kinachotokana na Kiyunani Psyche yaani nafsi na ology yaani logos Ufahamu kuhusu hivyo saikoloji ni somo lihusulo Ufahamu kuhusu nafsi. Hata hivyo kuna mkanganyiko kuhusu Saikolojia katika ulimwengu tulio nao wa leo hivyo ni muhimu kufahamu mambo amabayo sio Saikolojia 

·         Psychic Phenomena – Saikolojia sio kazi za kusoma Nyakati au utambuzi au usomaji wa nyota kama ifanywavyo na waganga wa kienyeji wanaodai kuwa na nguvu Fulani ya utambuzi watu hao hudanganya watu kwani ni kupitia uhusiano wao na mapepo ndipo huweza kutambua mambo fulani na sio Utafiti wa kisayansi katika shamba la Saikolojia.

·         Common Sense – Kuna uwezekano kabisa kupitia uzoefu Fulani mwepesi wa watu wenye fahamu au akili wanaweza kuelewa mambo Fulani kuhusu Saikolojia lakini kuna mipaka katika ujuzi wa kawaida wa kibinadamu ambao umegawanyika katika vipengele vikuu viwili 1. Utendaji wa kawaida wa kiakili mara chache hupitia vipimo vya kiutafiti vya kimaabara 2. Wote tuna ukungu Fulani wa kiufahamu katika mazingira Fulani ya kuwachunguza wengine na hivyo tunaweza kufikia hatima ya kuamua kitu Fulani kwa sababu Fulani kwa mfano katika hali ya kawaida wote tunaweza kukubali kuwa wanaume wana akili nyingi ukilinganisha na wanawake katika Ufahamu wa kawaida Common sense inaweza kuonekana kuwa sahihi lakini utafiti wa sayansi ya Saikolojia unagundua Tofauti yake kwamba wanawake wana akili kuliko wanaume

LENGO LA SAIKOLOJIA
 
Lengo kuu la msingi la Saikolojia ni mwanadamu kuyamudu mazingira yake au maisha.hii ina maana ya kuwa uwezo wa mtu na mali alizonazo hauwezi kuwa njia pekee ya kujitosheleza kuhimili migandamizo au msongo.Mtu huyu anaweza kuwa na umasikini wa kuhimili msongo au mgandamizo na hivyo akawa anatatizo la kushindwa kuhimili msongo “Maladjausted” hali hii inaweza kumlemea mtu, familia na hata jamii, kwa hiyo kazi ya Saikolojia kwa ujumla  ni kugundua kanuni nzuri za kumfanya mtu astahimili msongo au mgandamizo na kuzitumia kanuni hizo katika mahusiano ya wanadamu, inafanyika hivyo kwa kufundisha, Kuandika Vitabu au majarida na kwa kutoa ushauri au nasihi  kwa watu ili waweze kumudu mazingira yao kwa njia hii watu wengi wataweza kujimudu na kuchukuliana na maisha na kuzijenga jamii zao na kuwasaidia wengine katika jamii.

UHUSIANO WA SAIKOLOJIA NA SAYANSI.
 
Saikolojia inaweza kufikiriwa pia ni sayansi ya tabia “Behavioral science” lakini msingi wake ni wazi uko katika sayansi ya viumbe yaani Baiolojia na Filosofia ingawaje kuna mwingiliano kati ya Saikolojia na Nyanja hizi mbili za kisayansi  na Nyanja nyingine kama Elimu ya jamii Sosholojia na Anthropolojia na Elimu education.
Saikolojia ni sayansi ihusuyo tabia za mwanadamu kwa ujumla lengo kuu la sayansi likiwemo la Saikolojia ni 

·         Kufanya uchunguzi – Observation kuchunguza tabia ya mwanadamu kwa makini
·         Kufafanua Description – Kufafanua kile kilichochunguzwa
·         Kuelezea explanation – Kuelezea tabia katika msingi wa kufafanua kile ulichochunguza
·         Kukadiria Prediction - kuweza kukadiria au kutabiri kuhusu tabia hiyo baadaye katika msingi wa kile kilichoelezewa
·         Kudhibiti au kushawishi Influence or control – kutumia utabiri kushawishi tabia ya baadaye au kudhibiti ingawaje wana Saikolojia wengi wa kisasa wanapiga marufuku kudhibiti tabia ya mwanadamu mwengine.

Ili kufikia malengo wanasaikolojia wanatumia njia za kisayansi za kiutafiti, njia hii ndio njia halisi nzuri ya mbinu za kisayansi za kufanya uchunguzi unaofaa usio na kifungo “Unbiased” kwani njia za kisayansi zinachunguzika tena na tena na tena utafiti wa kisayansi lazima uwe wenye lengo, halisi na wenye hitimisho lisiloharibika ingawaje kwa bahati mbaya uchunguzi kuhusu mwanadamu ni mgumu kutokana na kutokusomeka moja kwa moja yaani mahitaji ya kiuchunguzi ni magumu lakini hii haimaanishi kuwa haiwezekani katika kufuata utafiti wa kisaikolojia.

SAIKOLOJIA KAMA SAYANSI.

Kuna njia kubwa mbili za utafiti wa kisaikolojia ya kwanza ni utafiti wa kimaelezo na ya pili ni utafiti wa kisayansi Experiment hapa tutajaribu kuzichambua kwa ufupi.

UTAFITI WA KIMAELEZO

Hii ni hali ya kutafiti kwa kuchunguza na kujifunza tabia ya mwanadamu, kumbuka umuhimu wa neno kujifunza na ni huku kujifunza kuna kusababisha uchunguzi wa kisaikolojia kuwa wenye kufanikiwa badala ya kumchunguza jirani yako. mchunguzaji wa utafiti wa kimaelezo huchagua tabia fulani kwa umakini zile anazotaka kuzichunguza na kisha anatafuta namna ya kutunza Kumbukumbu ya yale anayoyachunguza kwa utaratibu maalumu ingawaje utafiti huu hauna utafiti wa kisayansi au wa kimaabara lakini faida yake ni kupatikana kwa maelezo yawezayo kumfaa mtafiti kwa mfano tunataka kujua idadi ya watoto katika kanisa ili kujua kama kunahitajika mabadiliko fulani katika  madarasa ya shule ya Jumapili au kujua ni idadi gani ya wageni hutembelea kanisa  na kwa nini wanalitembelea kanisa na nini hutokea baada ya kutembelea Mchungaji anaweza akaliita jambo hili ufuatiliaji  lakini kwa mwanasaikolojia ni utafiti wa kimaelezo.

UTAFITI WA KISAYANSI "EXPERIMENT"

Tofauti na utafiti wa kimaelezo utafiti wa kisayansi hufanyika katika maabara za kisaikolojia vitu vingi muhimu vya kitaalamu vinapatikana humo kupima tabia fulani kisha kuitolea maelezo na kutafuta njia gani za kisayansi zinaweza kutumika kudhibiti kwa mfano ni wazi kuwa kama unataka kujua ni sababu gani hupelekea wanadamu kuwa na kiu unaposhughulika na watu utawauliza kuwa una kiu?  Lakini katika utafiti unaweza kumtumia mnyama ambao kwa kawaida huwezi kuwauliza hivyo maelezo kuhusu kiu kwa wanyama yatachukua muda wa kufuatilia ni kwa masaa mangapi au Dakika ngapi hujisikia kunywa maji utafiti wa kisaikolojia wa kimaabara ni wa muhimu kwa sababu unatupa kujifunza hii ni ya muhimu hata katika kusaidia kutafuta dawa ya tabia fulani ya mwanadamu, inaweza kutusaidia kujua mwendo wa Mapigo ya moyo kupumua na Shughuli nyingine za mwili na namna ya kutibu.

HISTORIA YA WANASAIKOLOJIA WA ZAMANI ZAIDI.
Kwa ujumla historia ya Saikolojia ni ya zamani sana tunaweza kusema ilianza tangu kuumbwa kwa mwanadamu  tangu wakati huo mwanadamu ametafuta kujitambua  na pia amejaribu kwa nia mbalimbali kutafuta kujua nini hatima ya tabia yake au nini kinafuata baadae katika tabia za kibinadamu  katika kutafuta hilo kuliibuka kuweko kwa falsafa mbalimbali.

1.      Mwanzo wa matazamo ya kifalsafa
Mwanafalsafa wa kiyunani Aristotle 485-322 K.K.  aliitwa na wengi kama mwanafalsafa wa kwanza na mwanasaikolojia mkubwa yeye aliamini kuwa mtu kuwa kichaa ni matokeo ya aina fulani ya maji katika ubongo kukosa kukaa sawa katika nafasi yake kutokana na utafiti huu ndipo ilipokuja kusaidia kupatikana kwa aina kubwa ya makundi ya watu duniani aina zile nne za makundi ya watu tutaziona mbeleni na kujifunza kwa kina kuhusu makundi hayo ya watu.

Mtakatifu Thomas Aquinas 1225-1274 B.K  aliandika katika matazamo wa kitheolojia  kuhusu tabia yeye aliamini kuwa  mwanadamu yuko huru kujiundia tabia, analo chaguo ambalo ni Jukumu la mwanadamu mwenyewe  na hivyo anawajibika kwa kila tendo atakalolifanya anajulikana pia kama baba wa Rational Psychology. Yaani Saikolojia ya ulinganifu 

2.      Viongozi wakuu wa kisayansi waanzilishi
Saikolojia haina mlengo mmoja tu na badala yake Viongozi wengi wakuu wa kisaikolojia waliweza kuendeleza mawazo yao kuhusu matazamo wao kuhusu tabia ingawaje hizi falsafa zao zinaweza zisikubaliane na hivi ndivyo shule nyingi za mkondo huu wa kisaikolojia zilipoanzia na shule hizi zinaelezewa pamoja na Viongozi waanzilishi wake

A.     Wilhelm Wundt 1832-1920

Huyu ndiye Mjerumani wa kwanza kuanzisha maabara ya kuchunguza tabia za wanadamu mwaka 1879 mrengo wake ulihusu mambo ya dhamiri na uzoefu, hisia na sura katika akili alimtumia mbinu za kiutafiti ziitwazo kitaalamu Introspection ambayo kwayo wachunguzi au watafiti watabia za wanadamu waliweka rekodi za mawazo yao na hisia zao mtindo huu uliitwa “Structualism





B.     William James 1842-1910



Ni mwanasaikolojia wa kwanza wa Marekani ambaye shule yake ilikazia katika mtazamo wa jinsi tabia inavyofanya kazi katika dhamiri, yeye pamoja na John Dewey walikuwa na ushawishi mkubwa katika swala la Elimu na kukazia kuwa chochote kinachofanya kazi ni muhimu kuliko kisichofanya kazi mlengo wao ni kujifunza




  
C. John Watson 1875-1958.


 
Alihisi kuwa wanasaikolojia wa wakati wake walihitaji utafiti wa kisayansi katika bongo zao na sio nje ya bongo zao yaani katika ulimwengu halisi hivyo alikazia katika kufanyia utafiti tabia zenye kuchunguzika tu na sio nini kina msisimua mwanadamu na kuhamasisha tabia au kuichochea pamoja na kuchunguza miundo ya mfumo wa fahamu, tezi na misuli kwa hivyo shule hii ilijihusisha na tabia tu na kuitwa Beheviorism.
  


D.     Wolfgang Kohler 1887- 1937.


Alikuwa mwanasayansi wa kijerumani aliyesomea maswala ya namna ya kuipokea mambo Perception mkazo wake ulikuwa ni jinsi gani akili inafanya kazi katika kutafasiri mambo kulingana na mazingira yetu hili lilimpatia umaarufu mkubwa hivyo ilisemekana kuwa mambo yote ni zaidi ya sehemu zake au wimbo ni zaidi ya kukusanya Maneno ya kuimba lakini tunauchukulia kuwa ni wimbo wote.






 E.     Humanism
Hii ni shule ya Saikolojia ambayo Haijulikani haina mwanzilishi lakini ni ya muhimu sana katika ufahamu kuhusu tabia za wanadamu na iligunduliwa huko Marekani kati ya mwaka 1950-1960 wakati wa mafanikio makubwa waandishi wake kama Carl Rogers walikazia katika matazamo chanya wa matazamio ya tabia ya mwanadamu hii ilijumuisha maswala kama ubunifu, uthamani, kukua na kujitosheleza ni moja ya shule za kifalsafa zilizodumu sana katika shamba la Saikolojia leo kwa sababu linalenga kupandisha juu kiwango cha  mwanadamu ambapo shule nyingine hazikuwahi kufanya

F.      Sigmund Freud 1856-1939

 
Hili jamaa lilikuwa daktari katika maswala ya madawa na utabibu alikuwa ni mtaalamu wa maswala ya akili aliamini kuwa tabia ya binadamu inasukumwa na misukumo “Drives” isiyozuilika kidhamiri au isiyokusudiwa kuelekea kwenye hitaji husika la kistarehe kama tendo la ngono na endapo halitatimizwa basi linamuacha mwanadamu huyu katika migogoro wa mtu na mazingira yake na kusababisha tatizo kisaikolojia.




MATAWI YA SAIKOLOJIA.

Saikolojia ina matawi yapatayo kumi na mbili hivi yoote ni muhimu kulingana na mazingira na eneo ambalo Saikolojia ya aina hiyo huitajika matawi hayo kitaalami huitwa Branches of Psychology.
a.       Saikolijia ya jamii Social Psychology – hii inahusu mwenendo wa mtu binafsi kuhusiana na jamii kwa ujumla kwani binadamu ni kiumbe kisichojitegemea Social being hakuumbwa awe mwenyewe
b.      Saikolojia ya maumbile Biological Psychology – hii inahusiana na Elimu ya viumbe kama mikondo mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu au mnyama na mifumo ya maumbile kama uzazi,urithi,magonjwa na madawa metabolism and Endrocine System,mfumo wa tezi n.k
c.       Children/adolcent/adult Psychology - hii ni Saikolojia ya hatua za binadamu na jinsi anavyoweza kutenda kulingana na umri wake nini kinamtokea wapi anajifunza nini Saikolojia hii ni ya watoto,vijana na watu wazima
d.      Clinical Psychology – Hii ni Saikolojia inayohusiana na matatizo ya magonjwa ya akili hapa wataalamu “Psychiatrists” wa magonjwa ya akili hutumia njia tatu katika kushughulikia maswala ya kutibu akili
·         Psychotherapy – hapa daktari bingwa wa magonjwa ya kisaikolojia hutimia njia ya mazungumzo na kujenga au kumtia moyo mpaka aweze Kujiamini au kukubali kukabiliana na hali halisi inayo mzunguka Reality Therapy n.k
·         During therapy – kutibu kwa kutumia madawa kama Trangulizers ili kumfanya mgonjwa awe mpole au aweze kulala na kupumzika kwa muda wa kutosha na kisha kusahau yanayomsibu kwa muda Fulani anajikuta amepona na anarudi katika hali yake.
·         Shock therapy – ni kutumia njia ya umeme  au mipira kushutua mgonjwa ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida
e.       Industrial Psychology – hii ni njia inayogusika na utumiaji au uchocheaji utumiaji nguvu ili kazi ifanyike katika viwanda, ngumi michezo na kadhalika man power
f.       Collective Psychology – hii ni Saikolojia inayohusu kurekebisha jamii katika makundi makubwa na madogo kubadilika kulingana au kutoka katika fasheni, kubadilika kitabia, kuonyesha mwitikio katika mambo mbalimbali mawazo na propaganda mfano  kura za maoni kama white paper iliyotumiwa na serikali kuingia katika vyama vingi 1992 ili kukuandaa kiakili kukubali
g.       Applied Psychology – hii ni njia ya kufanya utafiti wa kisayansi katika Saikolojia ili kutatua matatizo ya tabia mbaya za wanadamu katika jamii.
h.      Medical Psychology – hii ni Nyanja inayoshughulika na swala zima la matibabu ya kisaikolojia kwa ujumla.
i.        Education Psychology – hii ni Saikolojia ya Elimu ambayo kazi yake ni kuinua viwango vya Elimu, mbinu za ufundishaji, kutafuta vitendea kazi na kutatua matatizo kujifunza uwezo na maendeleo kwa ujumla
j.        Development Psychology – Hii ni Saikolojia ya kujifunza mabadiliko, misisimko, usomi na mahusiano ya jamii yanayotokea katika maisha ya mwanadamu  na maendeleo yake life pan
k.      Abnomal Psychology – hii ni Saikolojia inayohusika na tabia zilizoharibika na watu wasio wa kawaida kama vile mataahira, vichaa, wavuta unga na matatizo mengine yafananayo na haya n.k
l.        Military Psychology – hii ni Saikolojia ya mambo ya kijeshi inayohusika katika kuchochea moyo wa kivita Mfano Operation demokras, operation chakaza, mshike gaidi, Nduli, joka, nk.




MTAZAMO WA KIBIBLIA KUHUSIANA NA SWALA ZIMA LA SAIKOLOJIA
Je ni namna gani Ukristo unaweza kulinganishwa na sayansi katika mtazamo kuhusu mwanadamu na tabia? Kunamlingano katika swala ka kujifunza Saikolojia au tunaweza kusema kila mmoja anataoa matazamo wake na hakuna mgongano isipokuwa tunaweza kuona tofauti ndogo ndogo sana lakini mtu anapojifunza na kusoma zaidi kuhusu maswala ya Saikolojia utagundua kuwa tofauti ni ndogo sana na hitimisho huwa hivi kadiri tunavyojifunza Biblia zaidi ndivyo wakristo wanavyokuwa bora zaidi kuliko mahitimisho ya kisayansi lakini kwa ujumla wake tunawiana katika wigo mpana. Lakini ni muhimu kufahamu kuwa kadiri unavyojifunza kuhusu maoni yatolewayo na wanadamu wawe wakristo au wasio wakristo na tukapuuzia mtazamo wa kimungu ndipo tunapokuwa hatarini zaidi 2 Timotheo 2; 14- 16 Biblia inasema;-

Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema.”

Hatupaswi kujisahau na kuyategemea zaidi mawazo ya kibinadamu na tukasahahu kuwa sisi ni watu wa Mungu tunajifunza mengi kuhusu mawazo yetu, hisia, tamaa, misukumo nk. Kupitia katika neno la Mungu katika namna ambayo tunaweza kuwa na ufahamu mkubwa katika tafiti zinazofanywa na wana Saikolojia Ugunduzi unaonyesha kuwa wanasaikiolojia wa Kikristo wanauwezo mkubwa wa kutatua matatizo ya wanadamu kuliko hata wale wa kitabibu kwani wao hawagusi roho ya mwanadamu zingatia kielelezo kifuatacho kinaonyesha kuwa mwanadamu ana maeneo makuu matano





Mwanadamu ambaye tunashughulika naye ana mapito mengi na Saikolojia inaweza kugusa yote lakini inashindwa kugusa mahitaji ya kiroho ya mwanadamu ambapo hapo ndio chanzo cha matatizo yoote wanasaikolojia wa Kikristo wanaweza kugusa eneo hilo la muhimu, kwa vile mwanadamu ni zaidi ya mwili na akili


SAIKOLOJIA YA KUJIFUNZA
Tunaweza kuona kuwa ni mambo gani yanachochea mazingira ya tabia ya mwanadamu kupitia kusoma au kujua nini anajifunza na anajifunza vipi kwani karibu kila jambo katika tabia ya mwanadamu imechangiwa na tulivyojifunza, maarifa, mbinu, mtazamo, imani na tabia ya mchakato mzima wa mabadiliko ni matokeo ya kujifunza, mchakato huu wa kujifunza pia ni mchakato wa mabadiliko unaoanzia tangu wakati wa Kuzaliwa na unaendelea mpaka wakati wetu wote wa maisha ya duniani.

KUJIFUNZA NI NINI?

Kujifunza ni uhusiano wa kudumu wa mabadiliko ya tabia inayojitokeza kwetu kama matokeo ya mazoea.na msingi wa muhimu wa kujifunza ni kubadilika kwa mfano mwalimu anapoona wanafunzi wakionyesha muitikio wa maswali yake kwa ufahamu na maarifa anajua kuwa wanafunzi wake wamejifunza kwa sababu tabia hiyo ya ujibuji maswali kwa usahihi inaonyesha kuwa wamebadilika mchakato huu wa kujifunza unaweza kupimwa katika mazingira makuu matatu

1.      Kuendeleza mbinu mpya au kuboresha ile ya zamani
2.      Kuifundisha mbinu hiyo mpya kwa wengine na
3.      Kuendeleza mtazamo mpya na kuonyesha shauku ya kubadilika na kutumia mbinu mpya 

Ili mtu aweze kujifunza yako mambo ya msingi yanayosababisha kujifunza kuweza kutokea
·         Kuhamasika au kuwa na shauku motivation – mtu hawezi kuwa na moyo wa kujifunza kama hakuna hamasiko hii ni ile hamu kama ya kuwa na daraja zuri baada ya Kujisomea au kupania kufaulu au ujuzi kwanini unasoma hivyo shauku ikiwa juu  itakufanya uwe makini katika Kujisomea na kukumbuka kile ulichojifunza

·         Kushirikiana Association – unapokusanya vitu viwili au zaidi vinavyofanana na kusisimua katika akili huo ushirikiano kwa kweli ni moyo wa kujifunza kwa mfano nikitumia neno KUSOSA kumaanisha kanuni ya kula sana, soma sana na Sali sana neno hili kusosa ni ushirikianio wa neno hili kubwa hivyo maana halisi ya jambo hupatikana na hivyo kujifunza hutokea, kule kuweko katika jamii kunakufanya ujifunze, tabia za wanafunzi wa shule za kutwa zaweza kuwa tofauti na za wanafunzi wa bweni kutokana na kuwa na ushirikiano wanajifunza kitu cha ziada zaidi

·         Kuchochea reinforcement – hali ya kuchochea kitu ambacho umekwisha kujifunza inaleta matokeo ya kukifanyia kazi kile ulichojifunza hii ni kwa sababu wakati mwingine usipokichochea kitu kinaweza kisitokee tena lakini ukikichochea basi kitatokea hali ya kuchochea inaweza kufanya kazi katika mazingira yote mazuri na mabaya rafiki kazi nzuri endelea na kazi safi! Hii inachochea  wakati wa kampeni ni wakati wa kuchochea pia wakati wa mahubiri ya kiuamsho

Namna kuu tatu za kuelewa namna ya kujifunza
Haiwezekani kwakweli kufahamu kuhusu namna ya kujifunza bila kuelewa mambo machache kuhusu mawazo kuhusu kujifunza na utafiti unaolingana na mawazo hayo ingawaje hatuhitaji mawazo hayo au utafiti huo uweze kuathiri namna kuu tatu za kuelewa kujifunza

Kujifunza katika hali ya kawaida Classical condition
Hii ndio namna nyepesi zaidi ya kujifunza inahusisha mabadiliko katika kuakisi tabia nyepesi na hisia  mgunduzi wa mawazo haya ni Ivan Pavlov aliyegundua kanuni muhimu baada ya kufanyia utafiti kupitia mbwa na jinsi anavyoweza kudondosha ute  baada ya kumpima kuwa kila alipokuwa akimpa chakula alipiga kengele na siku moja kwa bahati mbaya kengele ililia na mbwa akatokwa na mate mengi akifikiri kuwa angeletewa chakula  hivyo mbwa alijifunza kutokana na hali ya kawaida  kwamba kula kwake kuliendana na mlio wa kengele hivyo ilipolia wakati hakuna chakula mate au ute ulimtoka kwa wingi . hali kama hii inaweza pia kuaathiri binadamu kwa mfano tunapoogopa mahali ambapo wala hapatishi kama vile tunapoona makaburi tumejifunza katika hali ya kawaida kuogopa au kama kuna wimbo unapigwa wakati sisi tukiwa katika hali fulani ya kihisia basi tunaweza kuwa na hisia zile kila tuusikiapo wimbo huo, kama ulikuwa wakati wa vita au lolote hisia zetu zitakuwa kama wakati huo na kwa hivyo tunaposisimuliwa na kitu ni kwa sababu tumejifunza katika hali ya kawaida inayotufanya sasa tujisikie kama vile tulipojifunza

Kujifunza kupitia Shughuli mbalimbali Operant condition
Dhana hii inaamiini kuwa tabia hujengeka kupitia Shughuli mbalimbali njia hii ni ngumu kwani inaingiza tabia kupitia nyenzo mbalimbali kwa mfano mbwa anaweza tena kufundishwa aokote kijiti na asipokiokota anachapwa kiboko na bwana wake na anapofanya vizuri anapewa zawadi chakula na upendo toka kwa bwana wake hivyo anajifunza kupitia Shughuli mbalimbali na wanadamu pia huweza kujifunza kupitia njia kama hizi kwa mfano watu wageni wanapokuja Kanisani wakapokelewa kwa furaha na kupewa zawadi wanaweza  kujifunza kuja Kanisani na kijijengea tabia kuanzia na wakati huo.

Kujifunza kupitia utambuzi au ufahamu au akili Cognitive learning
Dhana hii imegunduliwa na mwanasaikolojia wa kijerumani mapema katika karne hii yeye aliwafanyia watu utafiti na kugundua kuwa watu hujifunza au kuelewa vitu kutokana na mazingira yao hivyo alihitimisha kwa kusema kujifunza kunatokea mara mtu anapokuwa amepatwa na tatizo, ufahamu wa kuyajua mambo unatokana na uhusiano kati ya mambo mbalimbali yanayoungana kutengeneza picha nzima ya mambo kamili kwa mfano kama watu wameona Jengo kubwa kama Godauni na pakaweko Bwana shamba, Mchungaji na Dj wa muziki jengo hilo litatafasiriwa kwa haraka kulingana na ufahamu wa mtu Mchungaji ataliona linafaa kuwa kanisa,bwana shamba ataona linafaa kuwa ghala la kuwekea chakula na Dj ataona linafaa kuwa hall la kupigia muziki hii inatokana na utambuzi wao au ufahamu wao.

Kumbukumbu.
Tendo la kukumbuka linategemea na namna mtu anavyokuwa amejifunza, kujifunza kwenyewe kunategemeana na msukumo wenye kuleta athari kwa tabia hivyo kujifunza kunapokuwa kwa nguvu basi kunaifanya tabia ijengeke

Namna tabia inavyojengeka
Tunajua kuwa tabia imejengeka kutokana na tendo analolifanya mtu linapokuwa limejitokeza bila kupangwa katika hali kama hiyo tunasema tendo limekuwa tabia au mtu amejifunza  ingawaje tabia nyingine ni zile zisizo faa kama kuvuta sigara,  nyingi huwa tabia hasi au chanya  kama kutembea au kuchukua mazoezi, tabia nyingi huendelezwa pasipo kukusudia ingawaje nyingine zinapokelewa bahati mbaya katika kufanyia kazi mbinu mpya au ujuzi mpya, mazoea yanafaa kwa sababu hututoa katika kufikiria mambo madogo madogo na hivyo tuko huru kutoa muda wetu  na nguvu zetu katika vitendo vya ubunifu, na ni mpaka hali mpya inapoinuka usiyoitaka ya ina ile ya tabia  ndipo inaposhindwa kufanya kazi ipaswavyo na msukumo wa kidhamiri utahitajika.

Kukumbuka
Kukumbuka ni mchakato wa akili kutunza katika fahamu zetu Maneno, picha na mbinu na tunapokumbuka maana yake ni kuwa  akili inakurejesha katika ile picha au Maneno au mbinu uliyojifunza mwanzoni, kuna mabadiliko yanayoelezeka ya muundo wa mfumo wa ubongo na chembechembe zake ambao unahusika katika kufanya Kumbukumbu iweko mfumo huu unaitwa “Memory traces” kuhifadhi na kutafuta kilichohifadhiwa ndio unaofanya mchakato wa kukumbuka uweze kukamilika  kwa sababu ya muitikio wa chembechembe zinazo fanya  umoja uwepo wakati wa tendo la kukumbuka linapofanyika
     Lakini ni muhimu kufahamu kuwa kuna namna mbili kuu za kukumbuka Kumbukumbu za muda mfupi Short term memory na Kumbukumbu za muda mrefu  long term momory kwa mfano wengine kwa wanafunzi ni Hodari kuweka Kumbukumbu kwa ajili ya kujibu maswali katika mtihani lakini mara baada ya mtihani kila kitu kinayeyuka kwa sababu hakujifunza namna ya kuhifadhi katika mfumo wa kukumbuka wa muda mrefu lakini ili mtu awe na Kumbukumbu za muda mrefu anapaswa kuwa na  kujifunza zaidi Over learned au kurudia rudia  na kuyatumia kwa msingi huo mfumo wa Kumbukumbu wa muda mrefu utaumbika na ikifanikiwa hivyo basi kilichohifadhiwa hakiwezi kufutika kwa urahisi au kusahaulika kwa msingi huo basi ili mtu akumbuke ni muhimu kuwa na ufahamu kuhusu mambo ya msingi matatu yafuatayo
·         Recall hii ni Kumbukumbu ya kawaida na mwanafunzi anaweza kuigiza tabia na vituko vya mwalimu Darasani au kuweza kukariri kile alichojifunza kwa mwalimu wake amekariri tu!
·         Recognition hii ni kiwango cha juu sana katika kukumbuka wakati huu mtu huweza kutofautisha anachokijua na asichokijua na kufanya unyambulisho.
·         Relearning  ni jaribio la kukusanya mbinu au ujuzi wa jambo fulani ambalo umelisahau kabisa 

Kusahahu (forgetting).
Kusahau ni tatizo la ulimwengu mzima hii ni hali ya kushindwa kukikumbuka kitu ambacho ulijifunza, swala hili hutokea wakati mwingine kwa sababu ya upungufu wa vichocheo vinavyohitajika kuufanya mfumo wa Kumbukumbu kuwa kazini, na wakati mwingine hutokana na mwingiliano wa jambo jipya ambapo mtu anapokuwa amejifunza jambo jipya jambo hilo husababisha uwezo mdogo wa kukumbuka ya zamani tatizo hili huitwa retroactive inhibition au interference. Lakini unapojifunza lile la zamani kwa nguvu inakuwa ngumu pia kushika jambo jipya hii nayo inaitwa Proactive inhabition au interference wakati tukiwa tunalitafakari hili katika kanuni za ujumla tunaweza kusema yafuatayo
·         Watu wazima husahau zaidi kwa sababu wana mambo mengi ya kushughulikia katika maisha yao mengi yakiwa ni ya zamani na ni vigumu kwao kupokea jambo jipya.
·         Watu wazima wana tabia ya kufanyia kazi mambo yanayoonekana kama Yanastahili  na kushughulikia kidogo sana na mambo yanayoonekana kama hayastahili katika fahamu zao
·         Matatizo ya kihisia na kimwili pia yaweza kuchangia katika swala zima la kusahau mambo fulani  ili mtu akumbuke anatakiwa kushituliwa kwa umeme “Electric shock to the brain hii labda ni kwa sababu ya kuwa na msongo wa mawazo depression na mtu anaweza asikumbuke tukio lililomfanya akawa na msongo wa mawazo tiba yake ni hiyo.
·         Jambo lingine linaloweza kumfanya mtu akasahau ni kukandamiza Repression hii ni hali ya mtu kutokutaka kukumbuka jambo baya la kuumiza lililompata mtu kimaadili au kutishwa au kupitia uzoefu na hovyo anajaribu kulipotezea na anasahau linapokumbushwa kwake linakuwa ni la kuchukiza ama kutokana na kujeruhiwa nalo anakuwa mpiganaji wa tukio husika kuliko.
·         Jambo linguine ni suppression hii ni hali ya dhamiri kujaribu kusahahu au kujihadahari kukumbuka na hivyo anatumia nguvu nyingi ili asikumbuke jambo hilo na hii inaweza kufanyika bila mtu huyo kujitambua kuwa amejilazimisha kusahau tukio asilotaka likumbukwe.

Namna ya kujiendeleza au kukuza hali ya kujifunza Improving Learning Perfomance
1.      Kusoma katika makundi group discussion hii ni njia ya kujihamasisha kupitia wengine na kujichochea katika kuleta motisha ya Kujisomea.
2.      Kurudia rudia Recitation huu ni usomaji kwa sauti kubwa  ni usomaji mzuri kwani unahusisha na namna nyingine za milango ya fahamu kama kusikia  unaweza pia kujaribu kuelezea swala hilo kwa mwengine napo pia ni kujifunza kuliko kuzuri
3.      Kusudia kusoma kwa bidii mfano usilale wakati unaposikiliza kaseti fulani kwani hutajifunza
4.      Kujirekebisha soma kwa makini kisha jifanyie masahihisho kwa kurudia majibu sahihi
5.      Na namna ya Kujisomea kitabu kwa mfano kipitie kwanza kabla ya kukisoma, jiulize maswali, kisha soma, kariri au tamka kwa sauti, kisha pitia kwa upya hii ni njia nzuri. 

Mwanga wa kibiblia kuhusu kukuza hali ya kujifunza
Biblia ina mambo mengi ya kuzungumzia kuhusu swala la kujifunza hii inaonekana kwanza katika majukumu aliyopewa mzazi ya kuwafundisha watoto wake Kumbukumbu 6;6,7  wana Saikolojia wanasisitiza watu kujifunza wakiwa wamehamasika, kibiblia tunaambiwa kuwa wana wa Israel walikuwa na masikio lakini hawakusikia hii ina maana kuwa watu hawakuwa na hamasa ya kujifunza, lakini iko wazi kuwa alipokuja Kristo watu walikuwa wamehamasika kusikia habari njema za ufalme wa Mungu mwanadamu aweza kujifunza kivitendo hata kupitia mifano 1Koritho 4;16 Yohana 13;12-15 bado Biblia inaonyesha kuwa ili mtu ajifunze anahitaji bidii na kurudia tena na tena mpaka aweze kusema kama Daudi moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisikutende dhambi. Watumishi wa Mungu hawapaswi tu kuhubiri jumbe mpya kila wakati na kusahahu kuwakumbusha watu makusudi ya Mungu kwa kuyarudia tena na tena kwa namna nyingine.

Misingi ya maendeleo ya ufahamu na tabia ya mwanadamu
Jukumu la kutaka kujua maendeleo ya tabia ya mwanadamu ni Shughuli ya kila siku kwa mfano kama unataka kujua kwanini baadhi ya watu huwa na furaha kila siku na baadhi ni wakali au wahalifu au Walevi? Kujua jibu la maswala kama hayo inakupasa kwanza uanze kujifunza au kusoma kanuni za maendeleo ya mwanadamu tangu anapotungwa mimba anapokuwa mtoto mpaka anakuwa mtu mzima kadiri unavyo yafahamu mambo hayo ndivyo unavyopata ujuzi mzuri kuwahusu wanadamu na tofauti zao na kwa msingi huo ili tuweze kuelewa vema swala hili ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu juu ya maswala ya kurithi na mazingira yanayojiumba katika wiki za mwanzoni na miezi ya mwanzoni ya ukuaji katika tumbo la mama yake

Maswala ya kurithi Heredity
Huu ni ufahamu kuhusu maswala ya kibaiolojia ya namna kila mwanadamu anavyorithi kutoka kwa wazazi wake wakati anapokuwa anatungwa mimba, kwani uwezo wetu wa kimwili na kiakili  na upekee unaamuliwa na namna tunavyorithi,  hali hizo zitaamua tuwe na nywele za aina gani? Rangi gani? Macho ya rangi gani urefu au ufupi na mengineyo mengi huamuliwa na namna tunavyorithi kutoka kwa wazazi wetu aina hizi za urithi wa mambo kutoka kwa wazazi wetu unaamuliwa na chembechembe zinazobeba siri ya chembechembe za mwili zitakavyokua hizi huitwa “genes au genetics codes” DNAs deoxyribonucleic acid hizi huamua jinsi chapa ya mwili itakavyokua na kila chembechembe ya mwili itakavyokua hizi hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine hali hii ndiyo inayoamua mwili uweje na tabia pia inadaiwa na wataalamu kuwa karibu asilimia 80% ya uwezo wetu wa kiakili ni wa kuurithi hii haijalishi kuwa mtu ni masikini kiasi gani au ni tajiri kiasi gani kwani Elimu huchukua asilimia 20% tu ya maswala ya jinsi tulivyo huku tukizingatia kuwa mazingira pia yanachangia katika maendeleo ya mwanadamu

Maswala ya mazingira
Wakati ambapo wengi ni rahisi kufikiri kuwa mtoto anajifunza tabia anapokuwa amesha zaliwa au mara baada ya Kuzaliwa lakini ukweli unabaki kuwa mtoto anaanza kuathiriwa na mazingira hata tangu akiwa tumboni jambo hili kitaalamu huitwa Prenatal environment mtoto ambaye bado hajazaliwa anaanza kuathiriwa na kemikali za mabadiliko katika tumbo la mama yake kwa mfano kama mama anakunywa pombe, anavuta sigara, na mabadiliko yanayosababishwa na maumivu au migandamizo huweza kusababisha watoto wengine Kuzaliwa na athari za vilevi na baadhi ya magonjwa anayoambukizwa kutokana na mazingira ya mamaye mtoto akiwa tumboni. Inaaminika kuwa mtoto ambaye hajazaliwa anauwezo wa kuisikia sauti ya mama yake akiwa tumboni, mwanga, joto na maswala mengine ya mazingira ingawaje haikubaliki na wengi sana lakini wengi huamini kuwa pamoja na kuurithi mpaka mtu apatikane kuwa kama alivyo jamii familia tamaduni vina sehemu kubwa ya kuufanya utu wa mtu kuliko kuurithi.Lakini kisayansi inakubalika kuwa mtu hujifunza mambo tangu akiwa tumboni.

Maendeleo ya kimwili ya mwanadamu
Kuna dhana kama nne hivi zihusuzo ukuaji wa kimwili wa mwanadamu na hizi huanzia tangu wakati ule anapaokuwa anatungwa mimba mpaka anapokuwa mtu mzima

Kutoka kichwani mpaka mkiani
Inasadikiwa kuwa unapojifunza kuhusu ukuaji wa mtoto akiwa tumboni katika wiki za mwanzoni mtoto hukua kuanzia kichwani wakati huu kichwa ndicho huumbika kwanza kuliko kiwiliwili hivyo kiumbe ambacho hakija zaliwa huwa na kichwa kikubwa kuliko cha mtu mzima hivyo katika wakati huu basi ndio wakati wa makuzi ya ubongo kwani wenyewe ndio unaoongoza utendaji mzima wa mwili  kuanzia na Mapigo ya moyo na mzunguko wa damu hivyo ukuaji wa ubongo ndio unaoruhusu ukuaji wa mwili mzima na kuufanya ukue kwa asili hii ndio maana mtoto huweza kusema japo vitu visivyoeleweka kabla ya kujifunza kusema kabisa

Kutoka karibu kuelekea mbali.
Usemi huu kutoka karibu kuelekea hutumika kuelezea ukuaji wa viungo vilivyo karibu na uti wa mgongo ambavyo hukua kwa haraka zaidi kuliko mikono na miguu na baadhi ya viungo vya mbali zaidi kama vidole na viungo vingine hivyo ukuaji wa kichwa kuelekea kiwiliwili na ukuaji wa kutoka karibu kuelekea mbali unathibitisha kuwa mwanadamu huanza kukua viungo vile ambavyo ni muhimu kwa uhai kwanza kabla ya vile ambavyo vinatoa uimara na kumuwezesha au kuuwezesha mwili kutenda na kutembea 

 Mtoto wa miezi mitatu na nusu mpaka miezi minne tumboni anaweza kusikia na kujifunza kinachoendelea ulimwenguni


Tendo la kujitofautisha differentiation

Hii ni hatua ya tatu katika ukuaji wamwanadamu ambayo hutokea tangu mtu akiwa tumboni wakati ambapo viungo vidogo sana huanza kukua kwa kasi sana na kujichanganua katika namna ya kushangaza kwa mfano moyo huanza kama kijiungo kidogo sana kisicho na kazi lakini katika siku chache za ukuaji huko tumboni hukua kwa kasi na kuanza kujiumba katika maeneo yake makuu manne na kuanza kuongoza mtiririko wa damu inayoingia na kutoka

Ukuaji mwingineo Growth spurts
Katika namna ya kushangaza sana tangu kutungwa kwa mimba kunakuwa na ukuaji unaojitokeza na unaokwenda na mgawanyo sawia wa chembechembe za mwili katika kila sehemu lakini wakati huu zikiwemo sehemu za via vya uzazi via vya kike au kiume ukuaji wa viungo hivyo baadae huongezeka katika umri wa miaka miwili na kisha wakati wa ujana kati ya umri wa miaka 12 kijana huanza kuwa mrefu sana na kuanza kupevuka zaidi viungo vyake vya uzazi na kukoma kukua katika umri wa miaka 20

Maendeleo ya ukuaji wa kisaikolojia na kijamii Psycho-social Development
Mwanasaikolojia maarufu sana Erik K. Erikson alitoa maelezo ya kushangaza na kuvutia kuhusu hatua za ukuaji wa mwanadamu na namna unavyochukua nafasi yeye anatoa wazo linalobeba hali chanya na hasi katika kushughulikia ukuaji wa mwanadamu

Kujiamini na kutokujiamini trust & mistrust
Jambo hili hujifunza watu wa umri kati ya mwaka tangu Kuzaliwa mpaka mwaka mmoja au Kuzaliwa mpaka miezi 18 katika wakati huu mtoto huanza kupima ulimwengu kama ni mahali salama kwa ajili yake au la anapohisi kuna usalama anajijengea Kujiamini na inapokuwa anahisu si salama anajijengea kutokujiamini, Kujiamini hutokea pale mzazi anapomtimizia mtoto mahitaji yake yoote kama chakula na kumuonyesha upendo na wazazi wanapokuwa wanawasiliana kwa amani mtoto anahisi kuwa ulimwengu ni salama kwa ajili yake na anapohisi kinyume chake huanza kuingia hofu na kuhisi ulimwengu kuwa si salama kwa ajili yake lakini haitokei kuwa akajiamini au kutokujiamini kwa asilimia zote hili hutokea kiasi katika kipimo fulani lakini hili ndilo linaweka msingi wa maswala mengine yote ya kujiamini.

Kujitegemea na kuwa na mashaka Autonomy & doubt-Shame
 Jambo hili huanza kuumbika kutoka katika umri wa miezi kumi na nane mpaka miaka sita wakati huu ni wakati ambapo mtoto anaanza kujishughulisha na jamii wakati huu ndipo anapojifunza maswala ya kuvaa nguo na kuanza kufanya mambo mengine bila msaada wa mtu katika wakati huu mtoto atataka kufanya vitu vingi sana hata vile ambavyo haviwezi wazazi wakiwa makini wakati huu kumtia moyo kuwa anaweza anajijengea hali ya Kujiamini lakini anapokuwa anakemewa anaanza kuingia mashaka na kutokujiamini  na kuwa na aibu ya kufanya mambo 

Uwezo wa kuamua bila kumtegemea mtu na kuwa na hatia Initiative & Guilt
Jambo hili hutokea kati ya umriwa miaka 4 -5 katika wakati huu mtoto hujishughulisha katika vitendo zaidi vinavyo msaidia kujitegemea zaidi wakati huu anaongea anaongezeka nguvu na anatamani aujue ulimwengu zaidi na wakati huu wanakuwa na maswali mengi yakiwemo kuuliza mtoto anatoka wapi n.k wakati huu kama atajibiwa maswali yake kwa usahii basi mtoto ataendeleza tabia ya Kujiamini na kuwa na uwezo wa kuamua au kuanzisha kitu bila kutegemea msaada wa mtu lakini akivunjwa moyo huanza kuwa na hatia ya kujihisi kuwa anaweza kusema au kutenda kisichofaa na ataogopa kufanya mambo yake mwenyewe

Kujijenga na kuzalisha au kujiona duni na kushindwa Industry & inferiority
Jambo hili hujitokeza kati ya umri wa miaka 6-11 katika wakati huu mtoto huanza kusahau ndoto zake na matarajio yenye matumaini na kuanza kujishughulisha kubuni na kutenda kwa bidii ili kuzalisha anajitahidi kuwa bingwa wa kuanzisha jambo na mbinu zake hukua na huumbiwa shauku ya kutimiza mambo anajifunza kuchukuliana na matatizo au maswala ya kifamilia na shuleni anapotiwa moyo wakati huu anajijengea moyo wa kukamilisha yale aliyoanza na anapovunjwa moyo anajiona duni

Kujitambua au kujichanganya Identity & Role confusion
Hali hii huwapata watu wenye umri kati ya miaka 12-18 katika kipindi hiki kundi hili hukumbana na mapinduzi ya kisaikolojia katika wakati huu kijana huanza kujitambua na kwa kawaida huanza kujitenga mbali na wazazi na kujijumuisha na kundi rika la wenzake wakati huu wa mpito wao hujitahidi kujistawisha mwenyewe mbali na wazazi wakati huu kijana hujitambua kuwa ni mwanamke au ni mwanaume katika wakati huu kijana asiposaidika kujitambua vema atajichanganya katika kuelewa Jukumu lake na inaaminika na watafiti wengi kuwa hali ya usagaji au ushoga hujitokeza katika wakati huu katika kundi hili linaposhindwa kujitambua

Mwingiliano au upweke.  Intimacy & Isolation.
   Hali hii hujitokeza wakati wa ujana wakati huu kijana anahitaji kujichanganya na kuingiliana na vijana wenzake  mwingiliano huu pia hujengeka kutoka katika ngazi ya kujitambua ambapo kama ngazi ya kujitambua kwa kijana haijajengeka vema au akasumbuliwa katika kujua namna ya kujichanganya na watu wengine anaweza kupata tatizo la kuwa tayari kujitambua au kuingiliana na wengine na hivyo anaweza kushindwa kujichanganya hata na watu wa kundi la jinsia yake au ile nyingine na matokeo yake ni kuwa mpweke akijifunza vizuri anakuwa tayari kushiriki na wengine kimwili kimawazo na kihisia lakini inapokuwa kinyume chake mwingiliano na watu wengine litakuwa swala tishio kwake  na upweke utatokea hii haimaanishi kuwa mtu wa jinsi hii hataoa au kuolewa  lakini hata ndoa yake haitakua au kuendelea na hatakuwa na ukaribu na mwenzi wake matokeo kila mmoja atakuwa kivyakevyake

Kujumuisha na kujisahau Generativity & self-Absorption, au stagnation (Middle age)
    Hali hii hujitokeza katika umri wa kati wakati wa kazi za uzalishaji wakati huu akili inafikiri zaidi maswala ya kustawisha kizazi kijacho, atawaza zaidi juu ya familia yake na wengine kwa ujumla katika kufikia wawe na hali nzuri kwa ujumla wakati huu anaweza kuacha hata jambo la muhimu kwa ajili ya jambo analofikiri kuwa litakuwa la muhimu zaidi anakuwa na miaka mingi ya kazi na kusumbukia maisha jambo hili linaposhindikana mtu huyu anaathirika na kukata tamaa au kudumaa au kujidharau.

Kujikubali na kukata tamaa Integrity & Despair
    Hali hii hujitokeza katika umri wa utu uzima ambapo mtu hujikubali au hukubaliana na hali zilizoko za mizunguko ya maisha kwamba ndivyo yalivyotakiwa yawe katika wakati huu kama mtu hajafanya mambo ya maana huona kuwa muda ni mfupi kukamilisha jambo lolote na hivyo hukata tamaa na kuona kua amechelewa na wakati huu hujiandaa kuridhika na kujiandaa kwa safari ya kuondoka duniani wakati huu nguvu za kimwili zinakuwa zimepungua na anaanza kuakisi aina za maisha walizoishi enzi hizo kama alifanikiwa kujiandaa vizuri na kuwafanikisha wanawe atajiandaa kufa katika hali nzuri lakini kama hukufanya mambo vizuri anatamani angeongezewa muda ili arekebishe mambo lakini muda ndo hivyo tena katika wakati huu uzee wa mtu huyo utakuwa  uliojawa na uchungu na wenye kukatisha tamaa Paulo mtume aliyefanikisha kazi ya Mungu vema anasema katika 1Timotheo 4;7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri na kwa furaha anatazamia mwisho mwema, kwa walioshindwa wanabaki kusema ningelijua ningelijua! Huu ni wakati wa majuto wa aina za maisha Mwanzo 47;8-9.

Maendeleo ya uwezo wa akili za mtoto
Mwanasaikolijia wa Ki Swiss Jean Piaget alitoa mchango mkubwa sana wa ufahamu kuhusu makuaji ya watoto kiufahamu na kifikra alimtumia zaidi ya miaka 50 hivi katika utafiti wake na kwa umakini alichunguza watoto na ukuaji wao mchango wake una msingi mkubwa katika kuwafahamu watoto na kujua namna wanavyojifunza na kuwaelimisha yeye aligawanya vipindi vikuu vinne ambavyo haviwezi kujitokeza mpaka mtoto amefikia hatua ya tatu  ingawaje watoto hujifunza katika mtiririko wa maswala matatu Kibaiolojia, kihamasa na uzoefu wa kujifunza lakini yako mambo yanayoweza kuchangia kitu katika makuaji ya mtoto

Chati ifuatayo inaonyesha hatua za mtoto katika kukua kiakili


HATUA ZA UKUAJI KIAKILI

MUDA MUAFAKA
WA
KUJIFUNZA

SIFA ZA NAMNA ANAVYOJIFUNZA

Kipindi cha kuhisi sensorimental stage
Kuzaliwa – miezi 18
Wakati huu hugusa kile kinachoonekana mbele yake vinavyofichika hawezi kujua wala kuviona, hufuatilia lolote linalomjia au analoliona huweza kushika hiki au kuacha na kuamua kufuatilia kingine
Kipindi kabla ya kujishughulisha
Prioperation
Miaka 2- miaka 7
Hutatua tatizo kwa kujaribu na kushindwa, anafungwa na kile anachofikiri tu na kukiona  hawezi kutofautisha mambo baina ya vitu viwili mfano maji na chupa au chupa tupu
Kipindi cha kuumba au kuchanganuamambo
Concrete operations
Miaka 7-miaka 11
Anaanza kufikiri kwa usahihi  hata vitu vilivyochanganyika, kujua vipimo vya kitu au vitu kujaa au kupungua
Kipindi cha kujua
mambo kwa usahii zaidi
Formal operation
Kuanzia miaka 11 na
kuendelea
Anaweza kufumbua mafumbo na kuhusika na vitu na uchambuzi wa mambo anajifunza kufikiri kabla ya kutenda  na kupangilia au kuoanaisha

Maendeleo ya kimaadili ya mwanadamu

Mwanasaikolojia Lawrence Kohlberg naye alichanganua hatua sita za ukuaji wa kimaadili wa mwanadamu ambapo alidai kuwa kabla mwanadamu hajafikia hatua ya juu kabisa ya kimaadili lazima apitie hatua hizo mtu anapokuwa na hatua ya juu zaidi ndipo anapoweza kuonyesha sifa za hatua ya chini yake ingawaje mtu aweza kuwa na hatua ya juu zaidi kuliko nyingine lakini kadiri anavyokuwa katika hatua ya juu zaidi ndivyo anavyokuwa na uwezo wa chini wa kutambua hatua alizoziruka kimaadili

Hatua             Tabia na mahitaji                                              Umri husika
Hatua 0           Kabla ya kuwa na maadili                                     Miaka ya mapema
Hatua 0-a        Kipindi cha maadili                                             Mpaka miaka minne
Hatua 0-b        Maswali kuhusu maadili ubinafsi                        Miaka kuanzia sita
Hatua ya 1      Wakati wa kuiga maadili                                      Miaka 5-6 na mapema 7-8
Hatua ya 1      Adhabu na utii
                       Mafundisho kuhusu madhara na sio bahati mbaya
Hatua ya 2      Kugundua uhalisia                                                Miaka 7-8 na 9-10
                       Kufundishwa Matendo halisia
                       Kutosheleza mahitaji yake na tabia ya unyama
Hatua ya 2      Kipindi cha kuishi sawa na maadili                      Miaka 10-11 na 11-12
                       Kuona umuhimu wa kushirikiana kuhisi yuko kwa ajili ya jamii
Hatua ya 3      Kuishi sawa na maadili                                         Miaka 12-14  na 14-16
                       Sheria na utaratibu  kufanya majukumu yake
Hatua ya 4        kipindi cha kujitibu kitabia                                  wakati wa kuwa chuoni 20




SAIKOLOJIA YA ASILI YA MISUKUMO YA MWANADAMU
Tunawezaje kuelewa mahitaji, hamu, tamaa, matakwa na shauku zinazosababisha watu kuwa na tabia fulani? Kwa nini baadhi ya watu wana misukumo inayowahusisha na jamii au matakwa ya jamii na wengine wanaweza kuwa wahalifu na hata kupoteza maisha? Majibu ya maswali haya yanatupa au yanafunua nguvu au ugumu wa kuelewa misukumo ya mwanadamu katika maisha kwa msingi huo tunapojifunza kuhusu misukumo tunapaswa kujifunza katika Nyanja mbalimbali za maisha ikiwemo utendaji wa mawazo, misukumo, migawanyo ya mwili na utendaji mzima wa ubongo wa mwanadamu.

Misukumo na Mihemko
Kujifunza kuhusu misukumo ni kujifunza namna tabia inavyoanza kujijenga. Kimsingi hapa tunajifunza jinsi utendaji wa ndani wa mwili wa mwanadamu na mahitaji ya ndani ya kibaiolojia mihemko vichocheo vya kimazingira na  hamasa za ndani za mwanadamu  zinazo sababisha mwanadamu kuwa na tabia fulani ili kutimiliza mahitaji matakwa na malengo mengine ya baadaye
Mihemko hufanya kazi kama vichocheo vya ndani ambavyo huathiri uwezo wa kufukiri kuhisi na kutafasiri uthamani na kujenga tabia mihemko ya kibaiolojia inatokana na maumbile ya kawaida ya mwili kukosekana kwake kunachochea mwanadamu aweze kuwa na tabia fulani ambayo huamini kuwa itaondoa hali aliyo nayo, mihemko ya kijamii inaambatana na vichocheo vitokavyo katika mazingira kwa mfano kusikia harufu ya chakula kunaweza kusababisha wewe kusikia njaa hata kama bado ulikuwa hujasikia njaa

Ufahamu kuhusu mihemko yetu na mahitaji yetu  kutahamasisha kujitosheleza katika mahitaji yetu kama mtu atakuwa na uwezo na akafanikiwa kutosheleza mihemko yake  hisia za kupendeza zitafuatia na asipofanikiwa  atajijengea tabia ya kutoridhika na kuendelea kutafuta  kujitosheleza inagawaje mihemko hiyo na matakwa hayatakuruhusu  wakati wote kufanya mambo kwa usahii kwa mfano mtoto anaweza kulilia chakula hata kama ameshakula chakula cha kutosha tu na mtu mzima aweza kuvutiwa kununua nguo mpya hata kama anazo nguo za kutosha

Tendo hili linapojirudia rudia linaweza kujenga tabia na linaweza kutabirika kisaikolojia lakini likidumu zaidi linaweza kumsababishia desturi au mazoea ya kudumu ambayo ni vigumu kuyabadili lakini hili linategemeana pia na uwezo wa kiakili wa mwanadamu huyo na utayari wake katika kubadilika kwani kama mwanadamu hajataka kukubali kuibadilika hatuwezi kusaidia kubadilika kwake hivyo hapa tunaona mabadiliko au mchakato wa hali ya misukumo inavyoweza kupelekea tabia kujengeka
Hata hivo ni muhimu kufahamu kuwa misukumo haiwezi kuchunguzwa katika hali ya moja kwa moja bali inachunguzwa kwa kupitia tabia iliyozaliwa ingawaje kuna njia kuu tatu za kupima nguvu ya misukumo
·         Nguvu inayozalishwa – katika kumpatia mtu hali yoyote ya Shughuli je ni namna gani mtu huyo ni mgumu katika kutekeleza Jukumu fulani alilopewa kulikamilisha
·         Uvumilivu – Je pamoja na vikwazo anavokutana navyo je mtu huyu ni mvumulivu kiasi gani katika kukamilisha malengo aliyopewa?
·         Matumizi ya tabia mbalimbali na kuingilika – kama hizo za kwanza hazionyeshi matokeo je ni ubunifu kiasi gani alionao mtu katika kujaribu kuyafikia malengo?
Kama malengo ya chuo ni mtu kupata Diploma tunaweza kupima ni jinsi gani Mwanafunzi anajitihada kila wiki anaendeleaje katika kusoma ni mbunifu kiasi gani katika usomaji wake ili kufikia lengo la chuo? Lakini njia hii ya tatu itapimwa kama ile ya kwanza haijaonyesha matokeo 

Misukumo ya msingi na ya asili

Mwanadamu pamoja na wanyama woote wanayo misukumo ya kibaiolojia inayo usisimua, mfumo wa fahamu pale inapokosa kutimizwa au inapopungua hali ya kuhitaji hujitokeza misukumo hii inaweza kuzalisha tabia, mihemko, hisia au uhitaji misukumo hii ni kama vile;-
1.      Njaa – husababishwa na kemikali zinazozalishwa katika damu kupitia maumbile ya tumbo na hivyo kuzalisha hisia ya njaa au kuhitaji kula kutokana na taarifa hizo kuufikia ubongo.
2.      Kiu – Cell zote au chembechembe zote katika mwili wa mwanadamu zinahitaji maji hitaji hili linazalisha kusikia kiu au hitaji la maji mara kiwango cha mahitaji ya maji kinaposhuka au kuwa chini ya kiwango kinachohitajika taarifa huufikia ubongo na akili huanza kujua hitaji la maji
3.      Hali joto – mabadiliko katika mazingira lazima yatokeapo mwili huitaji kiasi cha joto lake kikae sawa kulingana na mazingira husuika hivyo mwili huzalisha hali ya kutaka kuweka hali joto ya mwili sawa kulingana na mazingira “Tempereture adjustiment mechanism” katika wakati huo mtu huweza kusikia joto au baridi n.k mishipa ya Damu hupanda juu kama kuna joto au kuzama chini kama kuna baridi, hizi ni hali zinazojizalisha zenyewe katika mwili bila kutumia akili.
4.      Kujisaidia – Mwili unahitaji kutoa uchafu au mabaki ya vitu visivyofaa baada ya matumizi yake au baada ya kuondoa virutubisho vinavyohitajiwa na mwili kutoka katika vitu tulivyokula vinapotaka kutoka mwanadamu hujisikia hali ya kutaka kujisaidia baada ya ubongo kufasiri
5.      Ngono – Tezi katika mwili wa mwanadamu huzalisha estrogen kwa mwanamke na androgen kwa mwanaume vinavyoamsha vichocheo katika mwili wa mtu na kuleta mhemko unaohitaji tendo la ngono ili kupunguza msukumo huo wa hitaji la kingono wakati mwingine vichocheo hivyo huweza kuamshwa kwa mazingira, mazungumzo, kuguswa au kusikia na ubongo kuelewa na kutafasiri hitaji hilo na kuzalisha nguvu za kutaka kutimiza shauku ya kingono.

Misukumo ya msingi ya kijamii
Kila mwanadamu anauhitaji wa kuwa na wanadamu wenzake kuliko kuwa peke yake hali hii huzalisha msukumo wenye nguvu wa kuwa na wengine, katika hali hii ya kuhitaji kujichanganya yako mahitaji ya msingi ya mwanadamu ya kimisukumo katika jamii misukumo hii ni kama ifuatavyo;-
·         Kutaka kuwa juu - hii ni hali ya kukataa kujiona duni miongoni mwa watu kwa mujibu wa Dr Alfred Adler aliamini kuwa  ni hali inayojitokeza ili kuziba ile hali ya kujiona duni au hisia zisizozuilika za kujiona duni na hii hutokea kimaumbile wala si kama watu watakavyo
·         Kutaka Kutambulika – hii ni hali ya kutaka wengine watambue kuwa tumefanya nini katika maisha yetu ili kukubalika au kusifiwa au wajue tu kuwa upo na wewe
·         Kutaka ulinzi – Dr Erick aliamini kuwa kuishi katika jamii ni asili ya mwanadamu katika maisha kwa ajili ya mahitaji ya kisaikolojia na kujihisi salama au kwa ajili ya usalama unaotokana na kuwa katika kundi au jamii

Matokeo ya mahitaji ya kuwa juu kimaendeleo
Inapotokea mtu amekuwa juu kimaendeleo kulingana na tamaduni za kila mahali zenye kumaanisha kuwa mtu amefanikiwa kuwa zaidi ya wengine kwani hili ni lengo la kila mwanadamu wanayo hulka ya kuataka kufikia kiwango fulani na wanapokuwa wamefanikiwa kukifikia, Winterbotton aliwasoma wanadamu mwaka 1953 na kugundua kuwa wanapokuwa wamefanikiwa wanakuwa na tabia ya kushindana kuzuri na kuwa na marafiki wengi lakini mambo haya pia hujitokeza
a.       Wanakuwa na tabia ya kujilinganisha need for social comparison
b.      Anahitaji la kusikilizwa na kuwa na au kujiunga katika kundi na haitaji kuwa peke yake
c.       Anahitaji kuwasaidia wengine hii ni tabia inayoumbika wakati mwingine kwa ajili ya kutaka sifa au kuitambulika au kutambua kuwa kuna wengine baada ya wewe kuwa umenusurika 2Falme 7;3-11
d.      Anatafuta kujilinganisha kulingana na uzito wake hii ni hali ya kuwa na jamii ya watu wenye hadhi kama yake kwa kawaida kama mtu amefanikiwa atahama manzese na kwenda masaki au mwakizaro kwenda Raskazone ili kujijumuisha na watu wa hadhi yake au kundi lake hii ipo hivyo kielimu na katika mafanikio mengine watu wenye degree hujitenga na wa diploma waalimu na wanafunzi ili kujazia ulinganifu wao

Kilele cha mahitaji ya msingi ya misukumo ya mwanadamu
     Kwa mujibu wa Dr. Abraham Maslow aliamini kwamba mahitaji ya mwanadamu yana jiorodhesha yenyewe hadi kileleni kama ngazi unayoweza kuipanda kutoka katika mahitaji muhimu mpaka kujitambua au kujitosheleza kwa maana nyingine ni kuwa wanadamu wana tabia ya kutafuta kujiridhisha katika hitaji moja la ngazi ya chini kabla ya kufikia lile la ngaji inayofuata kwa mfano kama mahitaji ya kimwili ya kawaida  kama chakula, maji,  hayajakamilishwa kwa kawaida nguvu kubwa ya mwanadamu itaelekezwa katika mahitaji hayo kwanza ambayo ni mahitaji ya kisaikolojia, (Psychological Needs) hayo yanapokuwa yametoshelezwa mwanadamu huamia katika hitaji lingine na kwa haraka atapata misukumo ya kutaka kuwa na mahali salama pa kukaa (Safety Need) na baada ya hilo kutimia ndipo linapokuja hitaji la kupenda watu wengine au mtu mwengine (Love Need) baada ya hapo ndipo mwanadamu huitaji kujiona kuwa anastahili/anajitambua (Esteen Need) na mwisho ndipo mwanadamu hujiona anaweza kufanya chochote awezacho kukifanya kupitia vipawa vyote na uwezo woote ambao Mungu amempa kwa nguvu zote hapa mwanadamu hujiona kuwa amejitosheleza  (Self Actualization Need). Hivyo katika mahitaji haya ya kilele cha mwanadamu tunaona jinsi mahitaji ya kimwili na kisaikolojia yanavyo chukua nguvu kubwa ya mahitaji ya misukumo ya mwanadamu na mahitaji yale mengine yanahitaji mwingiliano na watu wengine na hivyo huwa ni mahitaji ya kijamii zaidi na hivyo mengi ya nayozalishwa na tabia zetu yanalenga kufikia malengo hayo tuliyo nayo katika akili au fahamu zetu.








 Kilele cha ubora wajuu zaidi wa Mwanadamu ni kujitambua



Hivyo katika mahitaji haya ya kilele cha mwanadamu tunaona jinsi mahitaji ya kimwili na kisaikolojia yanavyo chukua nguvu kubwa zaidi ya mahitaji ya misukumo ya mwanadamu na mahitaji yale mengine yanahitaji mwingiliano na watu wengine na hivyo huwa ni mahitaji ya kijamii zaidi na hivyo mengi ya nayozalishwa na tabia zetu yanalenga kufikia malengo hayo tuliyo nayo katika akili au fahamu zetu.
Asili ya misisimko ya mwanadamu
Misisimko katika hali ya mwanadamu hutofautiana kutokana na mabadiliko ya mwili na hali ya akili misisimko inafanana sana na misukumo lakini misisimko ni ya ndani zaidi na inahusika zaidi katika kuyafikia malengo,Tunaweza kufikiri kuwa misisimko ni mahitaji ya kimwili na kisaikolojia mwili unabadilika hali kutokana na hali fulani zinazoamka katika vichocheo au kutokana na mabadiliko ya damu au hali fulani ya kiakili inapopata usumbufu lakini pia inaweza kusababisha mabadiliko katika hali ya kisaikolojia kwa mfano unaona umuhimu wa kumalizia sura hii ya kitabu lakini sina msukumo wa kuendelea hili linaweza kutokea kwa sababu ya kuchokozwa au kusumbuliwa kwa hisia
Maendeleo ya Misisimko
Kwa kawaida tunazaliwa tukiwa na uwezo kamili wa kuwa viumbe wenye misisimko lakini baadhi ya misisimko huchukua Muda kuumbika kwa mfano mtoto mdogo anazaliwa huku akiwa na uwezo wa kuonyesha kabisa kusisimkwa kimwili na kiasaikolojia lakini baada ya miezi kadhaa mtoto huanza kuonyesha mabadiliko ya kimsisimko kwa namna pana zaidi hii inatokana na ukuaji wa ubongo na kadiri mwanadamu anavyokua ndipo anapojifunza kiwango fulani cha kusisimkwa kutokana na yale aliyojifunza tangu mapema.
Mabadiliko ya mwili katika mabadiliko ya kihisia
 Ni wazi kuwa maswala ya misisimko si ya kisaikolojia tu bali ni ya kimwili pia kwa sababu hisia zinazo inuka juu ya mtu si zote zinachochewa na hali halisi za kimwili kama zifuatazo
·         Ukuaji wa moyo
·         Mfumo wa ulainishaji chakula kuwa chini au kutofanya kazi kabisa
·         Tezi zilizoko katika ini ziitwazo kitaalamu adrenal glands zinapofanya kazi kwa kasi sana na kuzalisha vilainisha chakula kwa wingi adrenalin
·         Mtiririko wa damu katika mikono na miguu unapoongezeka
Hali hizi zote za mabadiliko katika mwili zinaruhusu mchakato wa kumuinua mwanadamu katika hali fulani ya nguvu ya kuitikia mambo au misisimko katika wakati huo huo mtu huyo akihitaji mabadiliko kwa hivyo mwili utajiandaa kucheza au kufurahia au kujilinda au kufanya chochote kulingana na hali ambayo mwili unaokabiliana nayo ndipo tunapata vitu kama woga, hasira, au furaha n.k.

Hisia na Misisimko
Hisia na misisimko  ni nyanja zinazo angukia kwa wingi katika dimbwi la kisaikolojia zaidi kuliko kimwili ingawa vinaingiliana lakini vingine husababishwa na vichocheo fulani vinapoamshwa au kuchochewa hata hivyo utendaji huu mzima wakati mwingine una uhusiano na utendaji wa mfumo wa ubongo
Ufahamu wa jumla kuhusu ubongo
Una sehemu kuu tatu yaani
·         Medula Oblangata huu ni ubongo unaopokea taarifa kutoka katika mishipa ya fahamu Nevers kupitia katika uti wa mgongo
·         Cerebllum huu ni ubongo wa pili unaopokea taarifa kutoka ubongo wa kwanza na kuzirekebisha ili kuzipeleka katika ubongo wa tatu ili kutafasiri na kupata majawabu au nini cha kufanya
·         Cerebrum huu ni ubongo wa tatu unaopokea taarifa  toka ubongo wa pili Cerebllum na sehemu nyingine za karibu za ufahamu kama macho, pua na masikio na kutoa majawabu kwa kupeleka viashiria Signals kwa viungo husika ili kutafasiri au kutoa uamuzi nini kifanyike mfumo huu hufanya kazi kwa kasi ya ajabu kupitia mifumo miwili mikuu ifuatayo
·         Mfumo wa mishipa ya fahamu Nervours system mishipa hii iko kwa mamilioni ya nyuzinyuzi za nyama zinazopeleka taarifa kutoka kila eneo la mwili wa mwanadamu kwenda katika ubongo na kutoka katika ubongo kwenda katika viungo husika
·         Mfumo wa utendaji wa tezi Endrocine System hizi ni aina za tezi glands ambazo humwaga aina fulani ya dawa hormones na kusambaza katika mishipa ya damu ili kutayarisha mwili kwa huduma au tukio maalumu
Utendaji huu wa mfumo wa ubongo na mwili na mahitaji ya kisaikolojia vyote vinahusika katika utendaji wa hisia na misisimko





Woga.fear. Msisimko wa kihisia unaotokea ili kukabiliana na hali zenye kutosha au kuogopesha  kwa kawaida woga huwa tunazaliwa nao mfano mtoto mdogo anaposikia sauti ya kitu kikubwa ghafla au kilichoanguka na kutoa mlio huweza kuogopa huu ni woga wa Kuzaliwa hata hivyo Matendo mengine ya woga au yanayochangia woga  hivyo huo utakuwa ni woga wa kujifunza kutokana na mazingira ambao hujengeka hata kufikia hatua ya kuogopa kufanya jambo katika jamii kwa kuogopa kukosea lakini woga wa kuogopa kufa huu ni woga wa kawaida
Wasiwasi Anxiety. Tunasikia woga kwa sababu fulani au katika Matukio maalumu ya kututisha lakini tofauti na woga wasiwasi ni hali inayo fanana na woga ingawa wakati mwingine hali ya wasiwasi inaweza isiwe rahisi kuelezeka ni kama woga unaoelea hujulikani sababu au ni hisia za hofu inayotokana na jambo lililo tokea au litakalotokea  wasi wasi husababisha ubongo Cerebrum kuzalisha nguvu nyingi katika mfumo wa damu unaofanya damu nyingi kuhitajika katika kuendesha ubongo kuzalisha nguvu ya kisaikolojia kukabiliana na hali halisi pia huweza kusababisha Kuzaliwa kwa Hormones iitwayo adrenaline kuachiwa katika mishipa ya damu  na kumfanya mwanadamu kujiandaa kukabiliana na hatari au kukimbia hivyo kadiri mtu anavyokuwa na waoga au wasiwasi sana husababisha kuzalishwa kwa kemikali hiyo kwa wingi katika damu yake na matokeo yake huweza kusababisha tabia ya hofu au hasira na hatimaye muhusika huathiri afya yake ndio maana Biblia inasema furahini katika Bwana tena nasema furahini
Msongo wa mawazo Depression
Msongo wa mawazo ni moja ya matatizo makubwa sana kwa kizazi hiki kwa ujumla huu ni ugonjwa wa moja ya matatizo ya kiakili hujumuishwa na mchanganyiko wa matatizo mengine kama kukata tamaa, kujiona hufai, upweke hali ya kutokujisikia vizuri kwa ujumla ni hali ya kihisia inayohusisha kutokujisikia vizuri wakati mwingine huambatana na kilio au maumivu ya ndani ni kama inafanana na hali ya wasiwasi isipokuwa hii ni nzito
Hasira Anger
Ni msukumo wa ndani wa kukabiliana na hali iliyopo kutokana na kile tunachokiona kuwa ni haki yetu kuathiriwa yaani mtu anapata hasira kwa sababu fulanihasa kwa kuharibiwa lililo haki yake “Violate the rights of a Person” Hasira ziko za aina mbalimbali kwa mujibu wa Biblia Efeso 4; 31-32, hasira inatajwa katika ngazi tofauti tofauti “Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” wakati mwingine mtu mwenye wasiwasi huwa na hasira na mtu mwenye hasira huwa na wasiwasi kuna aina mbalimbali za hasira kama Biblia ilivyoainisha hapo juu
·         Uchungu “Bitterness” - hali ya kutaka kumfanyia mtu jambo baya au kutaka baya limtokee kama kisasi kwa mambo aliyokufanyia
·         Kuwa na kusudio ovu  Malice”au nia ya kutenda mabaya pia hutokana na kuchokozwa au kuingiliwa kile ambacho akili yako inakiona kuwa ni haki yako na malipo ni ubaya unaoukusudia
·         Mgomo “clamour”- hii ni hali ya kudai jambo kwa ghasia na kelele au kusababisha vurugu au kugoma  ni hasira itokanayo na kudhulumiwa,kukandamizwa au kile akili inachokiona kuwa ilikuwa haki yako kufanyiwa
·         Uchungu “Envy”- Ni uchungu unaotokana na mafanikio ya mtu mwingine
·         Kujisikia vibaya “Resentment”- kujisikia vibaya kwa sababu ya hali ya mtu au mafanikio yake
·         Kushindwa kuvumilia “Intolerance” – ni hali ya kushindwa kuvumilia  na kukubali kuwa tayari kutenda jambo litakaloleta madhara
·         Kukosoa “Criticism” - ni hali ya kusuta kwa Maneno ya hukumu au kukosoa  au kutafuta kosa katika kila jambo hata zuri likitendwa na mtu aliye na uhasama nawe
·         Kisasi “Revenge”- kujibu kwa kufanya jambo baya kwa sababu ulifanyiwa jambo baya kwa Maneno au kwa vitendo
·         Ghadhabu “Wrath”- Hasira kali au uchungu mzito ulio tayari kufanya jambo baya sana  au kitendo kiovu kikubwa
·         Chuki “Hatred”- hali ya kutokukipenda kitu au mtu  kutotaka hata kumuona au kujisikia vibaya unapomuona na wakati mwingine kumkusudia mabaya
·         Uchochezi “Sedition”- hutuba au mazungumzo yenye kuamsha hasira ili watu waasi au wagome au wachukue hatua kali dhidi ya kile kinachochochewa
·         Wivu “Jealousy”- hali ya chuki inayokusudia kumshinda mtu  au kumtakia mabaya au awe chini au akome wakati mwingine kwa sababu ana ubora unaozidi wako
·         Uvamizi “attack” – hali ya kumshambulia mtu kumuumiza au kumuangushia kipigo
·         Kusengenya “Gossip” – ni hali ya kumsenenga mtu kwa Maneno au kwa maandishi au kutumia nafasi uliyo nayo kukanadamiza
·          Kudhalilisha “sarcasm”- ni mazungumzo yenye uchungu yanayolenga kumdhalilisha ama kumuumiza mtu au kudhalilisha hata ingawaje yaweza kuzungumzwa kama utani
·         Kutokusamehe “unforgiveness”- hali ya kutokuweza kuachilia kabisa kutunza lawama moyoni siku zote kwa sababu ya jambo fulani ulilotendewa lenye kuumiza
Madhara yatokanayo na hasira
a.       Humfanya mtu aache kuwa mwenyewe na hivyo kuweza kutoa maamuzi ya kinyama au kufganya bvitendo hangeweza kufanya kama angekuwa hajakasirika
b.      Huumiza halui za kihisia na kuharibu amani na upendo
c.       Husababisha Stress au hormonies kuenea mwilini na kubaki kwa muda mrefu na huweza kujitokeza kutoka kazini kwenda nyumbani na kadhalika au hata makanisani na hii inakufanya uwe mtumwa wa yule mtu unayemchukia
d.      Husababisha matatizo ya kijamii hutatakiwa katika jamii yoyote wakati mwingine vita huweza kutokea kwa sababu ya watu wenye hasira
e.       Kunakuwa na madhara ya kiafya kwa mtu mwenye hasira asilimia 60% - 90% ya magonjwa ya moyo na Emotion disorders husababishwa na hasira hii huathiri utendaji wa mfumo wa fahamu na kuleta maafa kadhaa, kuathiri mzunguko wa damu na kudfhuru viungo kama fogo, nyongo, utumbo n.k kunaweza kuweko kwa madonda ya tumbo na maumivu ya kichwa au kukosa usingizi kwa sababu ya kusukumwa kwa damu nyingi kwenye ubongo kuliko inavyotakiwa
f.       Kuathiri uhusiano wako na Mungu kuathiri utendaji wa Roho Mtakatifu na kasi ya kutumiwa na Mungu au kuzuiliwa maombi yako
Furaha.
Hii ni hisia au Msisimko wa kihisia unaonyesha ya kuwa mambo ni mazuri na ya kufurahisha hii ni kinyume kabisa na mgandamizo wa mawazo au hasira mtu anapokuwa na furaha maisha huwa na maana na hujisikia vema anakuwa na matumaini na kunakuwa hakuna hofu wala hasira wala wasowasi matumaini ya mbele huwa mazuri wakati mwingine hali ya hisia za ndani huweza kujitokeza usoni lakini si kila wakati ikawa ni sahii 

  Furaha

 Huzuni


Hisia zetu za ndani zinaweza pia kuathiri ile tabia yetu yanje au muonekano wetu wa nje nyuso hizi mbili moja inaonyesha furaha na ya pili inaonyesha huzuni muonekano ho ni athari ya ndani ingawaje wanasaikolojia hawakubali kupima kwa muonekano tu wanataka kuenda ndani zaidi ya hapo

Muonekano wa kweli wa Hisia  
Muonekano wa kweli wa hisia za wanadamu hazionekani kupitia usoni pekee kwani wanasaikolojia wengi huamini kuwa uso unaweza kukudanganya na usipate usahii wa mambo wao wanapima hisia hizi kupitia njia zifuatazo
1.      Yakupendezayo na yasiyokupendeza 
2.      Yakuchukuayo na yasiyo kuchukua    

Wanasaikolojia wanaaminikuwa kupitia aina hizo mbili za misukumo unaweza kupima muonekano wa hisia za kweli kuliko kutegemea uso pekee ambao hauleti majibu ya kweli ya kihisia, ni wazi kuwa mtu akifurahi uso hushuka na tabasamu huonekana na mtu akikasirika uso hupanda na kuonyesha kutokufurahi hivyo kwa namna fulani mtu aweza kusoma Saikolojia ya tu usoni lakini hii ni sawa na kusoma box na kujua kilichomo ndani lakini wakati mwingine box hilo halina hicho kinachofikiriwa kuwa kimesomwa  hivyo kisaikolojia tunapaswa kwenda ndani zaidi ya uso wa mwanadamu

SAIKOLOJIA YA UFAHAMU AU TABIA ZINAZOJENGEKA KUPITIA MITAZAMO SENSES & PERCEPTIONS
Tunaufahamu ulimwengu huu na kufurahia jinsi ulivyo na rangi nzuri vivuli, sura mbalimbali za kupendeza milima kwa mabonde pia sauti nzuri na makelele baridi na joto ukavu na takataka maumivu na hali nzuri utamu na uchungu hii yote ni kupitia milango yetu mikuu mitano ya fahamu hivyo tunaujua ulimwengu huu kupitia milango hii mitano ya fahamu hivyo milango hii mitano ya fahamu ni ya muhimu sana katika maisha yetu kwani kwa hiyo ndiposa tunaweza kujua au kugundua mambo fulani yanayopelekea kusisismka


                          Kuona, Kusikia, Kuonja, kunusa na kugusa hukamilisha milango mitano ya fahamu

Milango mitano ya fahamu ni mfumo muhimu na maalumu sana wa viungo vya fahamu vinavyowekwa katika kundio hili ni viungo vyenye uwezo wa kutafasiri hisia za kawaida kuzipeleka katika hisia za kufahamu kwa mfumo wa fahamu uitwao Nerve impulses ambayo tungweza kusema lugha ya kiufahamu au midundo ya kiufahamu  katika mfumo wa ubongo kwa mfano kitu kinapogusa ngozi yako kinatafasiriwa katika midundo hiyo ya kiufahamu ili kwamba ubongo uweze kutambua na kurudisha tafasiri kwa kasi ya ajabu na ndipo ufahamu kamili wa hicho kilicho kugusa hujitokeza ufahamu huu hupitia mishipa ya fahamu mpaka kupitia katika uti  wa mgongo na kutumwa katika ubongo na ubongo kutafasiri na jibu la ulichokigusa kupatikana  na ndipo tunajua nini kinatuzunguka katika ulimwengu huu tulio nao 

Kusikia
 Ni moja ya kiungo cha ajabu sana na cha kipekee yaani sikio kinasafirisha au kutafasiri mawimbi ya sauti kutoka katika mazingira kupeleka katika midundo  na inapofikishwa katika ubongo ule wa kati hutafasiriwa na ndipo tunaweza kujua kile tunachokisikia kama ni mlio wa ndege radio n.k  mawimbi ya muungurumo fualani yanapoigia sikioni hugonga ngoma za masikio ziitwazo eardrum ni kama ngoma za kawaida lakini ni ndogo sana na laini sana na ziko makini sana  na hivyo ngoma hiyo hutikiswa na ndipo inapogeuza midundo hiyo nakuipeleka katika sikio la kati  ambalo lina vijifupa vitatu vidogo ambavyo hubeba mitetemo ile katika sikio la ndani na  sikio hilo hutafasiri ile midundo katika mtetemo wa midundo ya ufahamu ambayo hupeleka katika ubongo na kutafasiriwa ndipo sasa tunaposikia sauti ya asili ndani ya ubongo na sio huku nje hewani mambo haya hufanyika kwa kasi sana na kasi ya ajabu ni zaidi ya mara kumi kuliko sekunde kiasi cha kufikiri kuwa tunaisikia sauti hiyo moja kwa moja hii ni kwa sababu kuu mblili 

1. Namna ya muundo wa Umakini wa sikio na sikio la kati na la ndani
2. Ukaribu wa sikio la ndani na mfumo wa Fahamu nerve 

Aidha sikio la kati pia hufanya kazi za kumfanya mwanadamu asimame na kutembea wima bila kuanguka yani hutupatia Balansi huweka uwiano wa mwanadamu
Njia kuu tano za fahamu zilizo makini sana katika utendaji wa mwanadamu duara kubwa kabisa linaonyesha uwezo mkubwa kabisa wa ufahamu kupitia kiungo hicho na duara ndogo ni uwezo mdogo kwa kiungo hicho katika kutupatia fahamu kuujua ulimwengu

Kuona
Moja ya kiungo muhimu sana katika ufahamu wa mwanadamu ni kuona kuona ni kiungo muimu zaidi ya viungo vingine vyote vya fahamu, Jicho limejengwa kwa ufundi mkubwa wa viungo mbalimbali na limeumbwa duara kama mpira limejazwa kwa ute mzito unaolifanya liwe la mviringo limeumbwa kwa kusudi la kutafasiri mwanga na picha kwa kupitia mishipa ya mfumo wa fahamu na linafanya hivyo kwa njia ya kipekee sana 

      Picha hipitia katika mlango mwembamba sana wa duara uitwao kitaalamu pupil au mboni kwa Kiswahili,mwanga unaoruhusiwa kupita hudhibitiwa na kijinyama vinavyozunguka mboni viitwavyo Iris kijinyama hiki hufunguka sana kunapokuwa giza na hufunga kunakokuwa na mwanga mwingi mwanga hupita kulingana na ruhusa ya Iris na huingia katika lenzi (Lens) ambayo inafanana na ile lenzi ya kamera baada ya kufika hapo nguvu ya mwanga huo  inatupwa nyuma ya jicho huko husisimua cells za jicho ambazo ziko kwa wingi zaidi ya cells 130 milioni hizi ni seli maalumu za mfumo wa fahamu zinazotafasiri picha  kupeleka katika vijishipa vya fahamu impulses vijishipa hivyo vitumikavyo mchana huitwa Cones na vitumikavyo usiku huitwa rods mara zote Cones hufanya kazi ya kutafasiri vitu vya rangi mbalimbali na Rods hufanya kazi ya kutafasiri vitu vyeusi na vyeupe  vivuli na kijivu vijishipa hivi huipokea picha katika eneo liitwalo Retina ambako picha huangukia ikiwa kichwa chini miguu juu na hishafirisha kupitia mishipa maalumu ya kuonea vitu iitwayo optic nerves kuelekea katika ubongo huko picha hutafasiriwa na ndipo tunapoiona ikiwa sawasawa kwa rangi zake na aina yake kazi hii hufanyika kwa kasi sana na ndipo tunaposoma tunaona!
                   
       


 Muundo wa jicho la mwanadamu kama jinsi linavyoonekana kwa ndani

Kunusa na kuonja
Viungo vingine vya mfumo wa fahamu hufanya kazi kama ilivyo kwa sikio na jicho vifanyavyo aina fulani ya vichocheo huweza kuufanya nerves maalumu katika pua kwa kunusa na katika ulimi kwa kuonja na husafirishwa kupitia vijishipa vya fahamu katika ubongo na na kutafasiriwa kama utamu au harufu wanyama wana uwezo mkubwa zaidi ya wamwanadamu wa kunusa ili kuwinda au kujinusuru na kuwindwa na wanyama wenazao katika ulimi kuna aina fulani ya mishipa ya kiufahamu iitwayo test Buds ambayo ina uwezo wa kuhisi na kugundua aina nne za utamu yaani uchungu, utamu, uchumvichumvi na ungwadu.

Kugusa
Mishipa ya fahamu inayoweza kutafasiri mazingira ya asili kupeleka katika midundo ya mishipa iliyomo katika ngozi kila eneo huweza kusafirisha hisia hizo mpaka katika ubongo mishipa hii kama ulivyo utendaji katika ulimi huweza kuhisi katika mifumo mikuu minne
1.      Mitikisiko kama kuna mtikisiko wa kitu chochote
2.      Maumivu kama sindano ya daktari
3.      Baridi  kama mtu alalapo katika sakafu
4.      Joto kama wakati wakuota moto wakati wa baridi
Ingawaje mishipa hii ina kazi tofauti sawa na kazi hizo hapo juu katika kuhisi yoote hufanya kazi kwa pamoja kuuuambia ubongo nini kinatokea katika mwili na ndipo ubongo hutafasiri na kwa pamoja mwili unahisi kuna nini ulimwenguni jato au baridi au maumivi au mitikisiko na kadhalika

Mitazamo Perceptions
Ingawaje katika maisha tunasisimuliwa na vitu vingi sana aidha kupitia milango hii mitano ya fahamu lakini ni kwa ujumla wake ndio vinaleta maana inavyokusudiwa kwetu sasa jumla ya mkusanyiko huu wa kazi za milango yoote ya fahamu ndio unatupa kitu hiki kinachoitwa matazamo Perception hivyo milango ya fahamu ni milango ya ubongo katika kutupatia mtazamo ni ya muhimu katika kutupatia mtazamo wa ulimwengu wetu

Sifa za mitazamo
Matazamo ni mchakato wa ukusanyaji wa tafasiri kupitia mishipa ya fahamu kutuleta katika ujumla wa maana ya kitu fulani ni jumuisho la kazi za utendaji wa milango ya fahamu katika kutufunza mazingira yanayotuzunguka na kupata picha kamili ya kiufahamu, Mtazamo unaweza kujengeka kwa ghafla au taratibu kulingana na jinsi tunavyoathiriwa na mazingira yetu hii ni kwa mfano mtu kutoka ulaya anaposafiri kuja ngorongoro na kuona vumbi kubwa likitimka juu yeye anaweza kudhani kuwa ni Gari kubwa linakatiza katika barabara za Afrika zisizo na lami wakati mkazi wa ngorongoro aweza kudhani ni Tembo wanao pigana n.k kwa msingi huu tunaweza kuufahamu ulimwengu na kuwa na mtazamo fulani kwa sababu ya mtazamo wa mazingira tuliyokulia, kwa hivyo basi mtazamo hujumuisha ufahamu wa akili katika kutambua mambo watu,vitu na hali halisi lakini uwezo wetu wa kuipokea unatofautiana hata kama mishipa ya fahamu inafanya kazi vizuri na ubongo unafanaya kazi vizuri lakini mitazami yaweza kutofautiana kupitia  mazingira 

Mitazamo na mkazo au mvuto
Ni muhimu kufahamu kuwa matazamo pia huweza kuathiriwa na mikazo au mvuto wa kitu  hii inatufanya kila mmoja kuuona ulimwengu akiwa nadani ya miwani yake au kulingana na mahitaji ya mtu au yala yanayomvutia au anayoyakazia kwa hivyo hii ni hali ya kuangalia jambo wakati huo huo bila kupuuzia upande wa pili wa jambo hilo kadiri unavyokazia katika eneo moja bila kupuuzia yale mengine ndivyo unavyoweza kupata picha iliyo wazi wa kuelewa jambo lingine au lileliel kwa upana zaidi kwa hivyo ni muhimu kufahamu kuwa mvuto wa kitu huchangia katika kusaidia mtazamo ni wazi kuwa kuna vitu huvutia watu zaidi kwa mfano
1.      Picha – huvutia watu kwa kasi zaidi kuliko Maneno
2.      Mpangilio – kwa mfano inasemekana kitu kikipangwa mbele ya macho huonekana vizuri zaidi kuliko kilicho pangwa pembeni
3.      Upya – mlio mpya harufu mpya inavutia kwa haraka kuliko iliyo zoeleka
4.      Mtazamo – mlio au mwanga unagusa mwili na kuliko vichocheo vingine
5.      Mkazo – Mkazo wa sauti kubwa ,mwanga mkali, huvutia watu kwa haraka zaidi kuliko vingine
6.      Mwendo – vitu vitembeavyo huvutia kuliko visivyotembea
Mtazamo wa mtu unaweza kuathiriwa na mazingira mwana Saikolojia R. Chalks alijaribu kuchora mchoro wa glasi katika ubao mweusi na katika matazamo ya watu iliweza kutafasiriwa tofauti wakati mwingine tunaweza kuonyesha mkazo katika kuangalia rangi nyeusi zaidi kuliko nyeupe au nyeupe zaidi kuliko nyeusi na tukapata picha tofauti na iliyokusudiwa aidha michoro ya mishale inayopelekea nje na mishale inayopelekea ndani tunaweza kupata picha ya umbo refu au fupi zaidi kupitia matazamo hata kama vipimo vya umbile hilo viko sawa angalia picha zifuatazo

 




Pichani juu unweza kuona picha hii ni ya glasi au watu wawili wanaotazamana mtazamo wako utaamua kuwa unaweza kuona nini lakini ilikusudiwa kuchorwa glasi na sio watu wawili unaona!





   
                                                       A                                                   B

 Pichani juu ni michoro uliyochorwa kwa vipimo vinavyo fanana kabisa lakini ni rahisi kufikiri mchoro “a” kuwa ni mfupi zaid ya mchoro “b” kulingana na mtazamo wako ulivyozoezwa 

Mara nyingi tunaparaganya mambo kupitia matazamo yetu kwa kuwa matazamo yetu imezoea mambo fulani au imetoka kipaumbele katika jambo fulani basi tunashindwa kupata maana sahihi ya mambo kwa mfano kama unasoma kitabu na nia yako ni kupata kujifunza jambo fulani ni viguymu kuona makosa ya kitabu hicho hivyo uwezo wetu wa kuona mabo sio kwamba uko sahii wakati wote kwa msingi huo tunaweza kukosa maana ya jambo katika tafasiri ya mambo kwa sababu ya matazamo
Kwa msingi huu Biblia inaonya kuwa ili tusiweze kujichanganya katika mambo ya kufikiri isivyo sahihi ni muhimukuwa na tabia ya kutafakari mambo yaliyo mema Wafilipi 4; 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa njema, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye staha, ukiwako uzuri wo wote, pakiwepo cho chote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. Tito 1; 15 Kwa wale walio safi, kila kitu ni safi kwao. Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini, hakuna cho chote kilicho safi. Kwa kweli nia zao na dhamiri zao zimepotoka.  Kwa msingi huo basi mtazamo wa mtu unaweza kuwa mbaya pia kama mtu huyo ni mbaya na mtazamo wa mtu unaweza kuwa safi kama mtu huyo ni safi
Jinsi mitazamo inavyoathiri tabia
Kwa kawaida matazamo ina uwezo wa kuathiri tabia katika namna ya kutia nguvu hisia zetu ambazo kwa kawaida tunakuwa tumejifunza tangu tukiwa watoto na Tunaendelea kujifunza kwa kadiri tunavyoendelea katika maisha ya siku zote kwa njia mbalimbali kwa mfano propaganda na matangazo inaweza kuchangia kujenga matazamo yetu, kumbuka kuwa taarifa zinapotoka kwa mtu mwengine kuja kwa mwengine lazima ile taarifa itakuwa imeathiriwa na mtazamo wa mtu yule
Mitazamo ni hisia au mwelekeo uliotayari kufikiri au kutenda kuhusu watu, jamii hali, vyuo , taasisi,n.k. “mwanangu siku hizi hanionyeshi heshima “ vijana wa siku hizi hawana adabu kama vijana wa siku zetu, kanisa langu siku hizi hawanijali,siwezi kuishi bila kuabudu, hii ni baadhi ya matazamo ya watu ambayo mingine inachochea migogoro na mingine inahusisha hisia za faraja na usalama, kulingana na matazamo mtu anaweza kulichukia kabila fulani kwa sababu ya taarifa zisizo sahihi alizopokea toka vyanzo potovu
Matangazo ni tendo la kukusudia kivitendo kuwavutia watu katika jamii kujua jambo ili kuwaumbia ushawishi au mvuto ili waweze kununua bidhaa au kuja katika kanisa lako au vinginevyo hivyo kwa kutumia matangazo unaweza kubadilisha tabia ya mtu au mtazamo wake
Propaganda hii ni njia ya msukumo wenye kushawishi mwili wa mtu kukuunga mkono au kupokea aina fulani ya wazo, mtazamo au tendo ili kujijumuisha katika wazo lako au kusababisha kupinga la mwingine si kila wakati propaganda inaweza kuwa ya kweli lakini zinaundwa tu kwa lengo la kuishawishi jamii au chochote kukujengea tabia au mtazamo fulani na sio vinginevyo
Slogans ni misemo yenye kuubeba ujumbe wenye ushawishi wa kukuhamasisha ili utende au upige kura au kuhamasisha taifa,shule au kanisa au jamii kutenda jambo fulani au kuhamasika kupambana na jambo fulani aina hizo za slogan ni kama Maralia haikubaliki! Au Hari mpya nguvu mpya na kasi mpya.

SAIKOLOJIA YA TABIA NA UTU: JINSI UTU WA MTU UNAVYOCHANGIA TABIA ALIYO NAYO
Neno utu ni gumu kulielezea kwani watu huelewa utu katika matazamo mbalimbali kulingana na jinsi wanavyowaona watu na kuwa kila mtu ni tofauti na watu wengine wote, katika mitazamo tofauti tofauti kwa msingi huo tunaweza kusema kuna utu wa aina nyingi kwa sababu ya kuwa na watu tofauti tofauti ulimwenguni kwa msingi huo tunapochukua makundi ya watu na tabia walizonazo tunaweza kupata maana ya neno utu na pia kujaribu kutafasiri watu kulingana na utu wao kisha tunaweza kusema ni mpole au mtaratibu au mkali na kadhalika

Maana ya neno utu Presonality
Utu au personality ni jumla ya mtu na tabia zake, hii ina maana namna mtu huyo anavyo fikiri.anavyohisi, na anavyotenda na tabia zake kwa msingi huo utu ni mkusanyiko wa tabia zote za mwanadamu ni jumla ya sifa na ubora wa mtu katika uhusiano wake na wengine kwa maana nyingine utu wa mtu hudhihirika pale anapohusiana na wengine kwa hivyo hakuwezi kupatikana utu bila mtu kuhusiana na wengine kwa maana hiyo pasipo wengine katika maisha yetu utu hauwezi kuweko kabisa

Mahitaji ya afya ya utu
 Kila mtu ana mahitaji ya kisaikolojia ambayo kwa ujumla wake yana athiri afya au kutia nguvu utu mahitaji hayo yanapotimizwa maisha huonekana kuwa mazuri na tunapata afya hata katika muonekano lakini yasipotoshelezwa au yasipotimizwa matatizo ya afya ya akili hujijenga

Mahitaji makuu ya afya ya utu
1.      Kudhibiti mazingira yetu – hakuna mwanadamu anayependa  kuona anazidiwa na mambo au mabo yako juu ya uwezo wake inapo kuwa jambo liko juu ya uwezo wetu  hapa duniani tutahitaji anagalau tuyafahamu ni mpaka tuone utaratibu na jinsi jambo hilo linavyotabirika kudhibitiwa ndipo tunaweza kuzipumzisha akili zetu kuacha kushughulikia nalo
2.      Usalama – woote tunahitaji kuwa na uwezo wa kustahimili Migandamizo ya  ya maisha hivyo swala la usalama kadir tunavyoendelea linakuwa ni jambo la muhimu kila mtu anahitaji kujilinda kwa usalama wake
3.      Upendo na mahusiano – Hitaji la kupenda au kupendwa ni moja ya mambo ya muhimu katika kuendeleza utu  kama kuna jambo linavutia nyumbani ni wazazi kuonyesha wanampenda mto lakini hata hivyo hitaji la kuhusiana na watu wengine litaendelea kukua  na hii ndio maana watu hupenda kuwa na klabu au vyama vya kijamii
4.      Hitaji la kujitambua na kutambuliwa – kila mwanadamu ana hitaji la kujitambua au kujiona anastahili na zaidi ya hilo anahitaji kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake  kujitambua kwa mtu hata hivyo kunatokana na jamii inavyotoa uthamani  wa kiwango cha mtu huyo katika jamii  jinsi tunavyojifikiri sisi wenyewe ni moja ya kioo kikubwa cha wengine watakavyofikiri kutuhusu
5.      Uthamani maana na matumaini – kila mwanadamu analo hitaji la kutafuta uthamani wa maisha na kujikabidhi, katika hali kama hii ndipo tunapokutana na migandamizo fulani ya maisha na tunahitaji umaana na psipo maana maisha yanakuwa hayana matumaini na kunakuwa hakuna sababu ya kuishi inasemekana baadhi ya mateka au wafungwa wakati wa vita hufa kwa kukosa matumaini katika maisha na baadhi wanaoona umuhimu wa maisha hao huishi
6.      Kujitosheleza – hatuhitaji kuhakikisha ya kuwa tunaishi tu bali pia kujiendeleza wenyewe  kujiendeleza hata kufikia uwezo wa juu wa kiungu aliotupa kama watatwala wa viumbe vyote  hapo ndipo mwanadamu anapotafuta kujitosheleza  hali hii iligunduliwa na Dr. Abrahamu Maslow ambaye aliorodhesha mambo kadhaa chini kama sifa za mtu aliye jitosheleza
·         Anakubaliana na hali halisi bila kutafuta kujiridhisha
·         Hufikia ngazi ya juu kabisa ya kujikubali
·         Anaishi kwa kujitosheleza badala ya kupambana na maisha
·         Anahitaji kukaa peke yake ingawa hachukizwi kuwa na watu
·         Anakuwa na viwango vya juu vya ufahamu na hubakia kuwa mkeli kwa nafsi yake
·         Anakuwa na urafiki wa karibu na marafiki wa karibu au mpenzi wake
·         Anakuwa na ucheshi
·         Anakuwa amekomaa kimaadili na kitabia
·         Anakuwa na uwezo wa kubuni na kugundua
       Mtu aliyejitosheleza au kuridhika katika Saikolojia ndiye mwenye afya nzuri kisaikolojia katika hali fulani za maisha ni vigumu kuwa na uwezo wa kuridhika au kujitosheleza hususani wakati wa migandamizo, matatizo, maumivu, kutishiwa, katika wakati kama huo tunajaribu kujilinda lakini kuridhika kunabaki kuwa lengo lenye maana la maisha la kila mmoja wetu.

SAIKOLOJIA YA AKILI NA MASWALA YA KUJIWEKA SAWA KWA MAPAMBANO YA KIAKILI
Wataalamu wa maswala ya Saikolojia wanaamini kuwa mwanadamu wakati wote yuko katika vita au mapambano na Yeye mwenyewe au na mazingira yake kiakili lakini wengine wanaamini kuwa mwanadamu aweza kuishi kwa amani na Yeye mwenyewe na wengine lakini tofauti hii ni kubwa kwani ni lazima mwanadamu ajiweke sawa kwa namna fulani katika mapambano ya kiakili ili aweze kumudu kuchukuliana na mengi katika ulimwengu

Kujiweka sawa kunahusu tabia,mawazo na maswala yote ambayo watu waweza kuchukuliana nayo katika mazingira, inaaminika kuwa kila mwanadanmu huweza kujiweka sawa katika aina fulani ya mazingira  na migandamizo tunayokutana nayo katika maisha lakini ni kitu gani kiaweza kumfanya mwanadamu kujiweka sawa?Baadhi ya waandishi wanasema  ili kujua kuwa mwanadamu ana afya nzuri kiakili muulize swali jepesi  JE UNA FURAHA? Kama tunalenga furaha kama lengo la maisha ndipo tunaweza kujua kuwa mtu yuko sawa au la kama mtu huyo anaweza kuwa na uhusiano mzuri na wengine na kuonyesha kua anajitambua na kuwa na matumaini katika maisha mtu huyo aweza kujibu ndiyo katika swali hili muhimu je una furaha

Kujitambua/kustahili kama moja ya njia muhimu ya kujiweka sawa kisaikolojia
Wengi wa wanasaikolojia wanaamini kuwa moja ya njia muhimu sana za kujiweka sawa katika maisha ni kujitambua hii ndio inaonekana kuwa msingi mkubwa wa kuridhika aku kujitosheleza Dr.Stanley Coopersmith aliandika kuwa  kujitambua ni njia rahisi ya uhakika na uaminifu wa nafsi ya mwanadamu lakini pia ni kama dhambi ya kiburi

Sambamba na hilo hapo juu upendo usio na sababu ni moja ya mambo yanayokuwa dawa kwa kujiweka sawa kisaikolojia huu ni upendo kama ule unaotolewa kwa wazazi kwa mtoto wao kwa sababu ni sehemu ya familia  athari ya upendo huo unaotolewa bure bila mipaka au sababu unaumba kukubalika kwa wazazi  na familia na ndipo unamsaidia mtoto  kujikubali na kuridhika hata hivyo si kila mtu anaweza kuridhika katika kujiweka sawa kwa maisha  mtu mmoja alitoa dalili za watu wlio ridhika na wasioridhika au watu walio na uwezo wa kujiweka sawa kiakili na watu wasioweza kujiweka sawa kiakili 

Sifa za watu wenye uwezo wa kujiweka sawa kiakili na wasio na uwezo wa kujiweka sawa kiakili 

Wanashughulika katika maisha
Wanakata tamaa katika maisha
Wanadhamiri safi
Wanadhamiri iliyojikunyata
Wanjihisi wanaweza
Wanajihisi kutokuweza
Wanamudu hisia
Hawana hisia zilizo imara
Ni rafiki wazuri
Hawana urafiki mzuri
Wanajilaumu wenyewe kwa matatizo
Wanalaumu wengine kwa matatizo
Wanafurahia maisha
Hawafurahii sana maisha

Migogoro ya migandamizo na ujiwekaji sawa kisaikolojia
Uwezo wa mtu kujiweka sawa kisaikolojia unaweza kuonekana mtu huyo anapopatwa na matatizo na migogoro mtu huyo anapoweza kustahimili hali halisi na kutumia vyanzo vilivyoko kujiweka sawa tunasema mtu huyo ana uwezo wa kujiweka sawa kisaikolojia kama migogoro na matatizo yatampelekea mtu huyo kuwa na tabia tofauti  na hisia tofauti tunaweza kusema kuwa mtu huyo hana uwezo wa kujiweka sawa kisaikolojia kwa hivyo swala linakuwa katika kujiweka sawa na kutokujiweka sawa hili pia linaweza kuonekana kwa mtu anapotoka katika tamaduni moja kuelekea katika tamaduni nyingine kama wamishionari,au inaweza kuonekana kwa Mwanafunzi anapotoka nyumbani kwenda kuishi maisha ya shuleni kwani katika hali ya kawaida kwa mazingira ya kawaida mtu hutimia mbinu zake za kawaida kukutana na mahitaji yake lakini katika mazingira mapya mtu anahitaji mbinu mpya kukabiliana na mahitaji na kushinda vikwazo vipya akiweza hilo tunasema pia kuwa anao uwezo wa kukabiliana na migandamizo na kujiweka sawa kisaikolojia

Hali za kukatisha tamaa (Frustration)
Hii ni hali ya mtu kutakuwa na uwezo wa kufikia malengo kwa sababu ya hisia fulani kwa mfano mtu mwenye njaa anapokosa chakula  na kwa kuwa hana njia nyingine labda hana Fedha  basi anaweza kukasirika na kukata tamaa kwa msingi huo hali za kukatisha tamaa huweza kutokea pale mahitaji yetu na tamaa zetu  zinakosa kutimilizwa na hapo ndipo mtu hukata tamaa ikiwa ataendelea kutafuta namna nyingine ya kutimiliza mahitaji yake basi kisaikolojia tunasema mtu huyo anauwezo wa kujiweka sawa kukabiliana na vikwazo au migogoro katika maisha  lakini anapoonyesha kukata tamaa na kutamani au kuona maisha hayana maana tunasema mtu huyo anauwezo mdogo wa kujiweka sawa kukabiliana na mabo magumu au napoanza kuwa na tabia zisizo fanana na alivyotakiwa kuwa kitaalamu watu hao huitwa “Poor adjustiment Person” na wale wenye uwezo wa kujiweka sawa tunawaita “well au Good adjustiment Person”

Hali za mapambano au migogoro (Conflict)
Hali hii haitofautiani sana na hali ya hapo juu lakini mgogoro hapa ni matokeo ya vitu zaidi ya viwili au zaidi ya malengo au mahitaji au mwelekeo wa maisha haya ni mapambano ya kimaisha yanayoweza kumfanya mtu asukumwe katika mwelekeo mwingine au hali inayo mfanya mtu ashindwe kuchagua mwelekeo mwingine kwa mfano mtu amekusudia kuoa mwanamke mzuri basi hawezi tena kuwa na uwezo wa kuamua kuoa mwanamke mwengine aliye mzuri na anayemvutia huu ni migogoro au kijana anataka kwenda chouni lakini anaogopa kuiacha familia hii pia tunaweza kuiita migogoro,kwa hivyo migogoro hutokea tunapokuwa na mawazo mchanganyiko kwa mfano shauku na woga au hofu hizi ni hali za migogoro kisaikolojia

Kuchukuliana na kujiweka sawa
Mwanadamu anapokutana na hali za mapambano naq migogoro kwa kawaidea atajaribu kutafuta njia za kutatua tatizo hilo mwenye njaa aweza kutafuta Fedha  ili kununua chakula au kutafuta chakula kwa njia nyingine lakini kuna wakati amabapo mbinu zetu haziwezi kukidhi hali halisi katika wakati huo ndopo tunaunda uwezo wa kuchukuliana na tatizo tulilonalo ili kufanya fidia fulani ya kiakili, fidia hizo kwa asili huzalishwa kwa kusudi la kujilinda Defensive  hizi ni fidia za kujilinda kisaikolojia ambazo kitaalamu huitwa “Cognitive Defense Mechanism” hizi ni mbinu za kibinadamu za kuchukuliana au kutafuta kuziba pengo la tatizo lililoshindwa kutatulika kwa kawaida nyingine ni za kawaida na nyingine si za kawaida lakini ni matatizo ya kiakili yanayo ziba hali ya tatizo fulani ili kufidia au kujiweka sawa au kuchukuliana na matatizo halisi miongoni mwao chache tutazijadili hapa chini kama ifuatavyo;-

1.      Kukandamiza (repression) Hii ni hali ya kufidia kitu usichokipenda au wazo la kitu usichokipenda ambacho kinaweza kukujia hata katika mawazo lakini hutaki kukipa kipaumbele si kuwa hutaki kukiwaza tu lakini hutaki hata kukumbuka tukio hilo kabisa na kutaka kusahau hata kuwa umekisahau yaani unaweza kukumbuka kuwa kuna shida fulani lakini hutaki hata au huwezi hata kukumbuka namna ilivyotokea mwizi anapokamatwa anaweza kuuawa na wezi wenzake walioko katika jamii kwa kupigwa mawe ili kukandamiza miongoni mwa jamii wasionekane kuwa nao ni wezi bali wanachukizwa na wizi huo kwa kisi kikubwa katika hali halisi wao ni waizi lakini hawataki hali hiyo wasije nao wakaonekana kuwa ni wezi

2.      Kukanusha (Denial) hii ni hali ya kufidia kwa kukataa hali halisi ya jambo ambalo limetokea kwa dhati,kwa hiyo ni hali ya kujaribu kukataa kabisa hali fulani ambayo kwa kawaida imetokea kweli kwa mfano ni rahisi baadhi ya watu kukataa tukio la kweli la habari za kufa kwa mtu unayemfahamu sana kwa watu wenye uwezo wa kuchukuliana vema jambo hili linaweza kutokea kwa muda kisha akakubaliana na hali halisi lakini mwenye tatizo la kuchukuliana ataendelea kukataa ili kuondokana na tukio hilo lenye maumivu

3.      Ndoto za mchana (Fantasy) hii ni hali ya kufidia ambapo mtu asiyeweza au aliyeshindwa kufikia mafanikio fulani hubaki na mawazo amabayo tunayaita ndoto za mchana akiifurahisha akili yake kwa kamchezo ka kujifurahisha kujiona bingwa au shujaa kwa kutengeneza picha tu akilini .aweza kujiona kuwa amaekuwa Rais, au yuko kama Yesu au kiongozi yeyote mkubwa ulimwenguni mtu wa jinsi hii huweza kuwaza kuwa amejenga ghorofa anamiliki gari au yuko mahali fulani katika inchi iliyoendelea n.k kwa ujumla huyu haishi katika ulimwengu halisi kwani katika ulimwengu halisi tatizo liko palepale ingawaje hata wale wenye uwezo wa kuchukuliana wanaweza kuwa na ndoto hizi kabla ya kuzifanya ziwe halisi kivitendo lakini wagonjwa hubaki na wakati mgumu

4.      Kutafuta sababu (Rationalization) hii ni hali ya kufidia tatizo kwa kutafuta sababu au kusingizia  kwa mfano Mwanafunzi wa chuo cha Biblia aweza kuacha kwenda Kanisani kwa kisingizio kuwa amekuja kusoma na sio kufanya ibada hali ya kutafuta sababu pia hutumika katika kuwepa migogoro kwa mfano  kijana anapotaka kuoa na ana wasichana wawili aliowapenda na mmoja kati yao ana mchukia ili apate sababu ya kumuachia anasingizia kuwa hana tabia nzuri ili kuhalalalisha kuwa huyo aliyemuoa ndio uchaguzi sahihi na sio vinginevyo

5.      Kulaumu wengine (Projection) hili ni tendo la kufidia ambapo mtu hulaumu watu wengine kama njia ya kujitetea katika hali fulani aidha projection ni tatizo liwezalo kufanyika kivitendo kwa mtu kuamua kuudhi wengine kwa sababu yeye ameudhiwa hii ina maana ya kuwa kama Bosi kazini alikuwa mkali baba anaporudi nyumbani anakuwa mkali kwa mkewe na mke kwa watoto na watoto waweza kumalizia hasira zao kwa paka  ni tendo la kuamini kuwa watu wengine ndio walio na hali ya kumkataa mwingine kihisia na kimawazo hivyo muathirika huwalaumu wao kama njia ya kujilinda

6.      Kujiondoa (Withdrwal) ni hali ya kufidia kisaikolojia ambapo mtu hujitoa katika hali inayoonyesha kuwa kuna migogoro anawea kufanya hivyo kwa kuondoka kabisa katika eneo husika au kwa kujifanya haoni wala hasikii ili asihusishwe kwenye matatizo hayo au migogoro huo ni kama anawsema mimi simo kivitendo au kisaikolojia.

7.      Kujilinganisha (Identification) ni hali ya mtu lijaribu bila kukusudia yaani sio kwa Makusudi,kujifanya kama mwingine au ni kuiga tabia za mwingine, au kujifananisha na jamii ya watu wengine na kuficha ya kwake ili asionekane duni kwa mfano mtu anaweza kuwa mmbugu akajifanya msambaa,au kujifanya ni moja ya wanafamilia ya mtu mmoja mkubwa serekalini au rafiki wa mtoto wa mtu mkubwa n.k hata hivyo tabia hii hujitokeza zaidi sana wakati wa utoto au ujana

8.      Kutafuta visingizio (Dispaced Agrgession) ni hali ya kufidia kisaikolojia kwa mtu aliye sababisha tatizo kwenda kwa mtu au kitu kingine au kujilaumu mwenyewe mtindo huu unapokuwa endelevu unatengeneza hali ya kujificha katika kitu kingine Scape goating wakati mwingine mtu anaweza eti hata kutishia kuwa atajiua

Hali ya kushindwa kuchukuliana na kujiweka sawa (Maladjustment)
Ingawa tunapenda isiwe hivyo lakini wako watu wengine ambao hawawezi kuchukuliana na kujiweka sawa wanapopatwa na matatizo watu hao huteseka sanqa kihisia na maisha kwa ujumla wake kwao hayana maana tungetamani kuwa kila mkristo asiwe na tatizo la kushindwa kuchukuliana ingawaje tunajua kuwa baadhi hufanya hivyo
Woote tunajua kuwa kinyume cha afya nzuri ya akili ni afya mbaya ya akili lakini wanasaikolojia wengi na matabibu wa maswala ya kisaikolojia  au matatizo ya akili  humchukulia mtu yeyote anayeshindwa kuchukuliana na kujiweka sawa kuwa ana matatizo ya kiakili ingawaje watu hao wanaosumbuliwa hawapendi kuitwa watu wenye matatizo ya akili au vichaa watawaita tu watu wasio weza kuchukuliana au wasiojitambua kuna matatizo mengi sana ya kiakili kwa wanadamu lakini muda hautoshi kuweza kuyaangalia moja baada ya jingine lakini tunaweza kujadili kwa mukhtasari machache kati ya hayo kwa ujumla wake kuna  matatizo ya kihisia makuu matatu yaani kuchanganyikiwa kiasi  Affective disorders, kichaa,au kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwakidogo Neuroses, na kuchanganyikiwa kukubwa zaidi kisaikolojia Psychoses.

Kuchanganyikiwa kiasi affective disorders
 Hii ni hali ya kuwa katika hali isiyo ya kawaida kihisia katika hali fulani mtu anaweza kujikuta anaharakisha kufanya mambo bila kufikiri au kwa nguvu kubwa tatizo hili huitwa mania watu wa jinsi hii wanapenda juu kwa jazba na kitabia na inaweza kuchukua muda kuwa katika hali ya kawaida wanakosa usingizi hawaoni uhalisia na hawako katika hali ya kawaida mania ni hali ya migandamizo depression hali hii huwapata sana watu wa magharibi kuliko Afrika ingawaje watu wa Afrika wanapenda kuiga tabia ya watu wa magharibi hivyo migandfamizo iatakuwa sehemu ya maisha yao waigizaji watu wa jinsi hii wanavunjika moyo,hawawi kawaida mood wanajitenga na jamii hawali vizuri wala hawalali vizuri maisha ya baadaye kwao si ya matumaini na takwimu zinaonyesha kuwa 75% ya watu wanao teseka mateso hayo hufikiri kuwa hawataweza kupona wengi hufikia hatua ya kujiua kwa kukata tamaa


Kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwa kidogo neuroses
Hii ni hali mbaya zaidi ya hiyo ya kwanza ni usumbufu mkubwa wa akili na kihisia na huwapata watu wasioweza kustahimili au kuchukuliana watu wa jinsi hii wanaweza kuwa na hali ya kuhofia kila wakati anxiety bila sababu na wanaweza kuwa nje tu wakati mwingi au anaweza kuwa na woga wa kupita kawaida Phobias watu wa jinsi hii ni vigumu sana kuwatibu maumivu yao wanaweza kujikuta wananawa mikono mara nyingi au kula saa wanaweza kususa kukaa endapo atakuta mtu amekalia kiti chake wanasaikolojia hudai kuwa hali hii inaweza kutupata watu wote au watui wote tunayo lakini kila mmoja ananjia yake isiyo ya kawaida ya kupambana na hali hizi na kwa ajili ya kujitambua watu wenye kustahimili hurejea katika hali ya kawaida lakini viwango havifanani hivyo wale wanaozidiwa wanaoitwa wagonjwa kisaikolojia na hawa hudhani kuwa hawawezi kustahimili hali iliyowakuta hivyo hujaribu kujilinda wenyewe na hali ya maumuvi ya ulimwengu huu kumbe wanajikuta wamechanganyikiwa

Kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwa Psychoses
Hii ndio hali mbaya na ya juu zaidi kuliko hizo mbili hapo juu , kuna aina nyingi za usumbufu wa aina hii  lakini hii inakuwa nje zaidi ya uhalisia ulimwengu kwao unakuwa ni sehemu ya maumivu na kutosha na wakati mwingine hufuikia hatua ya kusikia makelele ambayo huwezi kuyaona au kuyasikia wala sio halisi lakini yeye huyasikia hali hii huitwa Hallucinations, wakati mwingine hali hii huweza kufikia kiwango cha mtu kushindwa kujua nini kinaendelea katika mwili wake au kujijali anaweza kujisaidia kuvua nguo kuchora chora n.k kwa ujumla watu wa naman hii hutakiwa kulazwa hospitalini chini ya uangalizi wa madaktari Kikristo wengi wwenye hali hizi huweza kudhaniwa kuwa wana mapepo lakini hata hivyo wanasaikolojiwa wa Kikristo wanasema si kila wakati wanaochanganyikiwa kiwango hiki wana mapepo hivyo wanapaswa kuwa na uwezo wa kupambanua kati ya mapepo na ukichaa wa kawaida ingawa ukweli unabaki kuwa tiba ya kiroho ya watu wengi wenye matatizo ya kisaikolojia ni ya muhimu sana kwani mtu anapoungama na kutubu dhambi zake kisha kuombewa anaweza kuwa na maendeleo mazuri ya afya ya kiakili na kuwa na matumaini kanisa lina nyenzo kubwa sana ya uponyaji wa mwanadamu kwa ukamilifu wake kumtoa katika ulimwengu wa maumivu kuliko tiba nyingine

Viwango vya athari na maumivu wayapatayo watu LCU.
Kwa mujibu wa Dr.Thomas H Holmes na timu ya wenzake katika chuo kikuu cha Washington school of medicine walijaribu kufanya utafiti wa maumivu yanayowapata watu na kusababisha athari ya mgandamizo wa mawazo au msongo na kuupa jina la kipimo cha mabadiliko ya maisha na miganadamizo yake yaani LCU “Life Change Units” na kugundua ya kuwa kama kiwango hicho kitafikia asilimia 300 LCU kwa miaka miwili Mfululizo kwa mwanadamu mmoja kuna uwezekano wa mtu huyo kupatwa na ugonjwa mkubwa sana wa kisaikolojia
Tukio
Kiwango LCU
Tukio
Kiwango LCU
Kufiwa & mpenzi
100%
MtotoShuleni
29%
Takaka
73%
Shida kisheria
29%
Watoto  wapweke
65%
Mke kuacha kazi
26%
Kufungwa
63%
Hali ya hewa tofauti
25%
Kufiwa na ndugu
63%
Kupitia tabia
24%
Kujiumiza
53%
Boss mkali
23%
Shughuli za ndoa
50%
Kubadili saa za kazi
20%
Kufokewa kazini
47%
Mabadiliko shule
20%
Ndoakupatanisha
45%
kuhama
20%
Kujiuzulu
45%
Mabadiliko Kanisani
19%
Afya mbaya
44%
…”…kulala
19%
Mimba
40%
…….kula
15%
Ugumu ktk sex
39%
sikukuu
13%
Mtoto mpya
39%
likizo
13%
Biashara mbaya
39%
Ukiukaji mdogo wa sheria
11%
kuchacha
38%


Kifo cha rafiki
37%


Kuhamishwa
36%


_____________ Used by Permission of Holmes,T.H & Rahe,R.H.The Social readjustment rating Scale.Jounal of Psychosomatic Research II:213-218,1967.
SAIKOLOJIA YA MIGANDAMIZO DEPRESSION PSYCHOLOGY
Ni moja ya matatizo makubwa sana ya kiakili ambapo mtu huhemewa au huelemewa na huzuni kubwa na ya ndani kiasi cha hata kufanya jambo lolote isipokuwa kukata tamaa watu wa jinsi hii hujisikia upweke, kukataliwa, kutokustahili na kukata tamaa na mwisho wa yote watu wa jinsi hii hutamani hata kujiua gonjwa hili la akili pia liko katika migawanyiko ile mitatu ya nafuu, wastani na hatari kabisa kwa wanansaikolojia hili ni tatizo kamili la kiakili linalohitaji tiba. Tatizo hili halijali jinsia ya kike au ya kiume inamsumbua mtu yoyote
Athari za saikolojia ya mgandamizo
A.     Mabadiliko katika kupata Usingizi
Mtu mwenye migandamizo mara nyingi matatizo yake ya hamu ya kitu huweza kuongezeka sana au kupungua ingawaje mara nyingi hupungua Kwa mfano tabia ya mabadiliko katika kulala watu wenge Migandamizo wanaweza aidha kulala sana au zaidi sana kukosa usingizi au kulala muda mfupi, Mtu mwenye migandamizo anaweza kuchelewa sana kwenda kulala na anaweza kuamka mapema kama saa 11 alfajiri na usingizi wake ni wa man’gamung’amu au aweza kuamka asubuhi akiwa amechoka sana na hivyo kwa watu wengi wenye tatizo hili asubuhi huwa ni wakati wa huzuni kwao
B.     Mabadiliko katika Nguvu
Migandamizo hii pia husababisha mabadiliko katika nguvu za muathirika baadhi yao hujisikia kutokupumzika na hijitia katika Shughuli nyingi sana na hawapendi kula wengine hujisikia uvivu na kutokutaka kufanya lolote hujisikia wamechoka sana na nguvu zimepungua na au kujisikia kama watu waliobeba mzigo mzito sana wanapunguza uwezo wa kufikiri na hawawezi kuwa makini kusikiliza jambo moja Poor concentration na pia huwa na matatizo ya kukumbuka vizuri
C.     Uwezo duni wa kujitambua au kujiona anastahili
Watu wenye miganadamizo mara nyingi hujiona kuwa hawastahili kabisa,hukosa matumaini na kujilaumu wanaweza kutafasiri jambo dogo tu au kushindwa kidogo tu kama njia ya kutokuwezekana kabisa na wanaweza kutafasiri kukosolewa kidogo tu kama wamehukumiwa wengine hujilaumu kuwa wamekufa kiroho au kimaadili na kioo kwao wanapojiangalia huona uso mbaya au wenye hatia ya kudanganya wengine watu wenye migandamizo mikali zaidi huamua kujiua kwani migandamizo husababisha maumivu ya kihisia asilimia 15% ya watu wenye migandamizo huishia kujiua au wengu wamejaribu kujiua
D.     Matatizo ya kuufahamu
Wakati mwingine watu wenye matatizo haya wanaweza kuona picha za Matukio mbalimbali zikiwajia ambazo kitaalamu tunaziita False beliefs & Hallucinatios ambapo mtu huona matazamo isiyo sahii hali inapokuwa hivi tatizo hili la migandamizo ujue limekuwa baya zaidi Psychotic symtoms tayari ni ugonjwa mbaya wa kiakili,hwana raha,na hujisikia kujiuua hata baada ya kulazwa hospitalini kwa muda mrefu

Sababu kubwa za Matatizo ya Migandamizo
Baadhi ya migandamizo inatokana na haliza uchovu tu hata kama mtu hana matatizo yoyote na mabo yako vizuri tu, lakini wengi hupatwa na matatizo haya kwa sababu za matatizo ya unyumba ndani ya ndoa kama hakuna amani,Maswala ya kifedha kuwa mabaya,kushindwa vibaya kwa mfano anguko la kiroho,kushushwa cheo kushindwa uchaguzi, ingawaje baadhi ya wanasaikolojia pia huamini kuwa matatizo haya pia husababishwa na matokeo ya mtu aliyetoka katika maishauonevu na mateso kwa hivyo muingiliano wa mambo fulani na mtu wa namna hiyo unaweza kusababisha matatizo haya ya kisaikolojia, aidha utafiti mwingine unabainisha kuwa unaweza kusababishwa na maswala ya kibaiolojia kwa mfano watu waliozaliwa mapacha baada ya kufanyiwa utafiti wengi wananonekana kuwa na migandamizo, hivyo kuna uwezekano wa kuurithi kibaiolojia migandamizo pia inasadikiwa kuwa wengi waliopitia hali hii huweza kuwaganadamiza wengine,sababu nyingine ni kutakuwa sawa kwa kemikali za ubongo zinazo shughulika na maswala ya hisia ya mwanadamu ziitwazo kitaalamu Neurotransmitters na matatizo ya homoni  “An imbalance of hormones” yanaweza kuchangia tatizo hilo,aidha matumizi ya baadhi ya madawa kama vitamin B6, vitamin B12, and folic acid na mengineyo huweza kusababisha migandamizo depression na matatizo yenye kuumiza au Matukio yenye kuumiza kama kufiwa na mpenzi au mtu unayempenda inaweza kusababisha matatizo kama hayo tatizo la kufiwa na mpenzi huweza kuchukua 100 LCU hivyo ni tatizo la juu sana kama tulivyoona mwanzoni huko juu

Matibabu ya matatizo ya migandamizo
Kwa watu wenye matatizo makubwa kabisa ya migandamizo ya kisaikolojia mara nyingi ni vigumu kutibika kwa kupewa ushauri wa kawaida tu  lakini kuna njia kama nne hivi zinazoweza kufaa katika kutibu matatizo makubwa kiasi hiki ,kuna vidonge vinavyotenda kazi kinyume na miganadamizo ambazo kitaalamu huitwa  Antidepressant Drugs , halafu uponyaji wa kisaikolojia Psychotherapy, ambao wakati mwingine huambatana pamoja na vidonge au njia nyingine ya kutumia umeme iitwayo kitaalamu Electroconvulsive therapy ambayo muathirika huvurugwa akili ili zianze kwa upya kwa kutumia kifaa maalumu hii hufanyika njia nyingine zinapokuwa zimeshindikana aidha pia maombezi na ushauri wa kichungaji nao umekuwa na matokeo mazuri na makubwa katika maswala ya kutibu matatizo ya migandamizo

SAIKOLOJIA YA MIGANDAMIZO YA MSONGO WA MAWAZO MSONGO STRESS
Stress (psychology)
Msongo wa mawazo au stress ni hali isiyopendeza ya kisaikolojia ambayo watu hujisikia kulingana na hali wanazozipokea aidha zenye kuashiria hatari kuwatishia au kuwafanya wasijisikie vizuri hata hivyo msongo unaweza kuwa na maana nyingine kwa sababu tofauti wengine huuelezea msongo kama tukio la hali inayomsababishia mtu kujisikia yuko juu juu, pressure inapanda na kushika au kuogopa hofu na hali zisizoweza kuelezeka mara nyingi hili huchangia pia kuleta mabadiloko ya Mapigo ya moyo na hivyo pia husababisha mpanuko wa misuli ya Mapigo ya moyo na mababdiliko ya tabia za kihisia hata hivyo msongo unategemeana sana na hali halisi za tafasiri za mtu binafsi na hali ananzokutana nazo hivyo si rahisi kuelezea kwa wazi kuwa
Ni muhimu kufahamu kuwa pia msongo ni hali ya kawaida tunayokutana nayo kila siku inaweza kukupata unapokuwa na Shughuli nyingi, au tunapokuwa na jambo la muhimu sana la kutimiza na ukawa na muda mfupi sana wa kutimiza hapo msongo unaweza kutokea.msongo unaweza kutokea pia kwa sababu ya matatizo kazini au kautokana na mahusiano mabaya katika jamii muingiliano na marafiki n.k aidha Matukio yenye kuumiza katika maisha kama kifo cha mtu uliyempenda sana na kuogopa maeneo ya kawaida yanayotisha n.k huweza kusababisha msongo. Msongo unaweza kuleta athari nzuri au athari mbaya mtu anapotishiwa na jambo anaweza kuzalisha nguvu mbili kujilinda au kuepuka msongo unaweza kusababisha utimize jambo fulani na pia unaweza usababishe kushindwa lakini katika upande mbaya Msongo unaweza kusababisha tatizo kubwa sana

Vyanzo vya msongo
Msongo unaweza kusababiswa na sababu mbalimbali ziitwazo Stressors lakini sababu kuu hizo hugawanywa katika maeneo makuu matatu Matukio ya ghafla Catastrophes hii huweza kusababishwa na uvamizi,ajali,vitana kadhalika Matukio yenye kuhusisha mabadiliko makubwa ya kimaisha Mojor life changes haya ni Matukio kama ya talaka,kufungwa kwa baba au mama,kuuguliwa kufiwa na baba au mama,mipango ya kuoa nk chanzo cha tatu ni Matukio ya kila siku katika maisha haya ni msongo unaotokana na mwingiliano wa maisha ya kila siku kazini ndugu jamaa nk.

Athari za msongo
·         Kutokuwa na Kumbukumbu nzuri
·         Kutokuweza kumudu kazi zako kama inavyopaswa au katika hali ya kawaida
·         Kupatwa na magonjwa ya moyo na athari za viungo vingine

SAIKOLOJIA YA UTU NA MAUMBILE YANAVYOUNDA TABIA YA MWANADAMU
Mwana Saikolojia wa zamani sana aitwaye Galen alijaribu kugawa mafungu makuu manne ya aina za utu ambazo huumba tabia kutokana na maumbile yao aina hizo nne za utu ni Sanguine, Phlegimatic, choleric na melancholic aliyagawa makundi haya makuu manne kutokana na maumbile ya mkao wa maji Body Fluids unaomkalia kila mtu mafungu hayo manne ya watu yanaungwa mkono na Biblia katika Mithali 30; 11-14 katika muonekano wao waloonekana hivi;-




      Kutoka kushoto Sanguine, Phlegmatic,  Chini choleric na melancholic katika picha kama wanavyoonekana kwa mujibu wa mwanasaikolojia Galen haya ndio makundi makuu manne ya watu

Jinsi ya kuchukuliana na watu tofauti tofauti
    Kuna wakati inatulazimu katika maisha kuvunja urafiki na baadhi ya watu kutokana na kushindwa kuchukuliana nao au kushindwa kuwaelewa wewnzetu kuwa ni watu wa namna gani na ni wa kundi gani katika tabia sehemu hii itatusaidia kufahamiana na pia kijifahamu ili iwe rahisi kwako kuchukuliana na watu woote rafiki aliyekomaa hawezi kupoteza marafiki kwani anawajua rafiki zake nguvu zao na udhaifu wao Biblia ina tuambia kuna aina nne za watu ona (Mithali 30;11-14).jamii hizi kisaikolojia huitwa Melancholic (mst 11), Phlegimatic (mst 12), Sanguine (mst 13) na Colerich (mst 14). Jamii hizi zina sifa na madhaifu, mbalimbali ambazo ni taa ya kutuonyesha sifa zao Sifa hizo ni kama ifuatavyo;-

Melancholy Kundi la watu wenye Nafsi inayoumia.
Kwa kawaida hili ni kundi la watu makini, wenye kuweza kunyambulisha mambo,ni wenye kupendelea ukamilifu,wana mpangilio wa mambo wana mawazo mazuri na wenye kujitoa jamii hii ya watu wengi wamekuwa wanasayansi wasanii wanafalsafa na wagunduzi wa kubwa pia ni wachoraji,Hata hivyo ni kundi la watu wasiojichanganya na jamii wapweke na wanaoumia mioyo,wanatazamia mambo ya kuumiza ni wabinafsi,hana ushirikiano anatunza visasi wanahitaji tunda la roho la furaha na amani.

Phlegmatic. Kundi la watu wenye Nafsi iliyotuliana taratibu.
Hili ni kundi la watu wanaojiamini,wanaojitegemea na kujitosheleza na ni wapenda amani,kundi hili ni la watu wasioweza kubadilika kwa haraka na hupenda kusanifu mambo,hata hivyo kundi hili hupenda kujilinda ni waoga,wachoyo hawahamasiki na ni wavivu wanapenda usingizi na mambo yao ni polepole na ni wachokozi chinichini hufanya chochote wanachoshauriwa

Sanguine. Kundi la watu wenye Nafsi Changamfu.
Kundi hili ni kundi la watu wachangamfu sana wanaweza kufanya marafiki kwa haraka sana ni waigizaji wazuri na wasanii,ni wasemaji sana ,wacheshi,ni marafikihawatulii na wasiojitegemea,hata hivyo sanguini ni wadhaifu,wanaonekana kama hawana nidhamu waoga,wana haraka.

Choleric .Kundi la watu wenye Nafsi Katili.
Kundi hili ni kundi la watu jasiri,wanaojiamoni,ni viongozi hufanya mambo yatokee ni watendaji wanaona mbali wanaweza kufanya maamuzi lakini ni wenye hasira ,hila,kujigamba,hana hisia za huruma,ni katili anajitoa sadaka kwa kufanya kazi kupita kawaida.
Kuna uwezekano wa kujijua kuwa uko kundi gani kwa kuangalia sifa za makundi hayo nzuri na dhaifu kisha unachukua idadi ya sifa utakazozipata unazidisha kwa mia na kugawa kwa idadi ya sifa zote hapo utajijua.

Mfano tunamjadili Kamote kujua kuwa Yeye ni kundi gani hivi ndivyo tutakavyofanya
Melancholy


Phlegmatic


Sanguine


Choleric


Anauchungu                                                                                 

Anajiamini


Mcheshi


Ni katili


Ana jitoa

ü   
Mtaratibu


Msemaji

Anahasira


Ana kipawa                                


Anajitosheleza


Muigizaji


Jasiri


Ni mkamilifu


Habadiliki

Anakelele

Mzalishaji


Mbunifu


Hahamasiki

Muoga


Mtendaji


Makini


Ana sanifu

Muongo

Kiongozi


Hashirikiani

Mvivu

Muhamsishaji


Anaamua


Hanaharaka

Ana choyo

Hana aibu


Anakisasi


Mgunduzi


Hana haraka


Si mtendaji


Hujisifu


Mchoraji


Hujilinda


Kigeugeu

Ana hila


hunyambulisha


Hupendaamani


Ana haraka


hajihurumii



Unaweza kuona kuwa alama za x zinaonyesha sifa ambazo Kamote hana hivyo katika Melancholy Kamote hana alama tatu  na alama nane zilizo tupu ni sifa alizo nazo sifa zitakazopatikana utazigawa kwa 12 sawa na jumla ya sifa zote za kila sifa hivyo katika melancholy Kamote ana sifa nane na anakosa tatu hii ni kusema kuwa katika melancholy na sifa nnyingine Kamote atakuwa na sifa zifuatazo kwa kila moja ile itakayokuwa na asilimia kubwa zaidi ya wengine ndiyo sifa ya mtu huyo mfano mzuri ni huo hapo chini 

Melancholy kwa Kamote ni = 8/12 X 100=66 %
Phlegmatic kwa Kamote ni= 7/12 X 100=58%
Sanguine kwa Kamote ni=7/12 X 100=58%
Choleric kwa Kamote ni = 12/12 X 100=100%

Hivyo Kamote ni Choleric kwa asilimia 100 lakini anazo sifa nyingine kutoka katika makundi mengine na kwa kawaida zile zinazojitokeza kwa wingi zaidi zile mbili hutabiri wazazi wa Kamote kuwa mmoja ni Melacholy na mwingine ni Choleric na kwa kawaida  Melancholy akioana na choleric melancholic huumizwa hivyo mmoja wa wazazi wa Kamote katika ndoa alikuwa ni nafsi iliyoumizwa na kitaalamu Yule anayeumia hufa haraka na ni kweli mzazi mmoja wa Kamote yaani mama yangu alikufa mwaka wa 1984 hivyo chati hizi husaidia hata kujua sifa za wazazi na taabu zao katika ndoa na kama mmoja yuko hai au lapia unaweza kufanya utabiri usiorasmi


Jinsi ya kufanya majaribio mengine ya kisaikolojia
Saikolojia ni sayansi hivyo inahitaji majaribio wakati mwingine unaweza kupima uwezo wa mtu wa kiakili na utendaji wake au kupima aina kuu za watu yaani yale mafungu manne na utendaji wao wa ubongo lakini kabla hatujaonyesha namna majaribio hayao yawezavyo kufanyika ni muhimu tukajifunza kwanza uwezo wa utendaji wa ubongo Intelligence
Intelligence inapimwa katika kipimo cha uwezo wa akili mara mia kugawanya kwa umri wa muhusika ndipo unapata uwezo wa utendaji wa akili ambao kitaalamu unaitwa intelligence Qutient (IQ) hivyo
                 IQ Intelligence Quotient            =     Uwezo wa kiakili X 100
                                                                                  Umri husika
Matokeo ya kipimo hiki yatakuonyesha kuwa watu wenye uwezo mkubwa kiakili watakuwa hivi;-
Watu wenye IQ kutoka 50 - 75 wanaitwa Morons
Watu wenye IQ kutoka 25 – 50 wanaitwa Imbeciles
Watu wenye IQ kutoka 0 - 25 wanaitwa Idiots
Watu wenye IQ kutoka 75 -100 wanaitwa Nomal
Watu wenye IQ kutoka 100- na zaidi ni Geniases

 Aidha mazoezi ya kisaikolojia ya kupima ubongo wa mwanadamu unaweza kufanyika kwa zoezi kama lifuatalo
Maelekezo chagua Fedha kama za sarafu sio za note kama kumi kisha zitengeneze katika mfano wa Piramidi au umbile la pembe tatu mfano huu

 





Baada ya kuwa na kiasi hiki cha Fedha  zilizo katika mtindo wa umbo la pembe tatu wajaribu wahusika kama kumi hivi watano wa kike na watano wa kiume waambie wanaruhusiwa kugusa sarafu tatu tu ili kubadili umbile la pembe tatu ielekee chini wakati huu utakuwa unahifadhi Kumbukumbu za utendaji wao na zoezi litafanyika kwa Dakika tatu tu  kama atashindwa mzuie kuendelea na rudisha piramidi katika hali ya kawaida na jaribu watu wengine unaweza kufganya hata kwa watu 15-20 nusu wawe wanawake na nusu wanaume  majibu utakayo pata yatakusaidia kujua uwezo wa mtu kiakili na utaweka Kumbukumbu katika namna ifuatayo

Jina…………………………………………………….Jinsia……………………………………………...
Muda aliotumia…………………….Dakika………………….Sekunde………………………………..
Je alikuwa na shauku yoyote kuhusu somo au kazi uliyompa………………………………………..
………………………………………………………………………………………………………………

Baada ya zoezi jumlisha muda woote uliotumika gawanya kwa idadi ya watu uliowafanyia zoezi la somo, kisha tafuta wastani wa muda uluiotuiwa na wanaume na kisha wastani wa muda ulio tumiwa na wanawake kisha jibu maswali haya ukikumbuka kuwa lengo ni….Kujua utendaji wa akili za wanawake na wanaume, ukikumbuka idadi ya watu uliowafanyia zoezi wanawake wangapi na wanaume wangapi ni nini wastani wa Muda uluiotumika kwa pande zote kisha kwa wote, kisha ni kundi ganimliko juu wanawake au wanaume? Kisha umejifunza nini katika kupima bongo za wanawake na wanaume kisaikolojia au hata mtu moja moja.


UHUSIANO WA SAIKOLOJIA NA ANTHROPOLOJIA (ANTHROPOLOGY & PSYCHOLOGY)
Maana ya Jumla
Anthropology ni neno lenye asili yake katika lugha ya Kiyunani/Kigiriki. Neno hili ni muungano wa maneno mawili: anthropos na logia. Anthropos maana yake ni mwanadamu na Logia maana yake ni elimu juu ya jambo fulani. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa anthropology ni elimu inayohusu mwanadamu na Nyanja mbalimbali za maisha maisha yake.
Kwa ujumla anthropology inajaribu kuchunguza mambo yanayomhusu mwanadamu kama vile; jinsi watu wanavyoishi, wanavyofikiri, wanazalisha nini na kwa jinsi gani watu hao wanaishi katika mazingira waliyomo. Pia wanataalamu wa anthropology (anthropologists) wanachunguza tofauti kati ya watu na watu na mambo ambayo watu hao wanayo kwa pamoja (diversity and what they have in common). Anthropologists wanafanya utafiti wao kwa kujiuliza maswali kama vile lini, wapi na jinsi gani mwanadamu ameanza na kuendelea (evolve)? Kwa jinsi gani jamii zimeanza na kuendelea tangu zama za kale hadi leo hii?

Anthropologia ya Kikristo (Christian Anthropology)
Anthropologia ya Kikristo ni elimu juu ya mwanadamu na uhusiano wake na Mungu. Inatofautiana na anthropologia ya elimu jamii kwa kuwa yenyewe inajifunza habari za mwanadamu kwa kutumia kipimo cha theologia ya Kikristo. Anthropologia hii inachunguza juu ya asili ya mwanadamu au vitu vinavyofanya mwanadamu awe mwanadamu.Inajishughulisha na uhusiano uliopo kati ya mawazo makuu kama vile mwili, nafsi na roho vitu ambavyo muungano wake kwa pamoja ndivyo vinavyotengeneza mwanadamu. Vinachunguza mambo mambo kwa kuweka msingi wake katika maandiko matakatifu, yaani Biblia.

Mwili, Nafsi na Roho
Tunapojifunza juu ya anthropologia ni muhimu sana kuchunguza juu ya mambo hayo matatu.
        i.            Mwili: Hii inatokana na neno la Kiyunani lijulikanalo kama Soma .Hii ni sehemu ile ya mwili ambayo inaonekana na inaweza kuguswa kwa mikono ya nyama. Hii ni sehemu ambayo huoza na kuharibika wakati mwanadamu anapokufa. Lakini Kanisa kulingana na mapokeo ya Kanisa ni kuwa mwili utafufuliwa katika mwisho wa duni.

      ii.            Nafsi: Neno hili linaelezwa vizuri na dhana mbili; moja ya Kiyahudi na nyingine ya Kiyunani. Kwa Kiebrania Nafsi ni Nephes. Kwa kiyunani neno hili lina julikana kama Psyche. Neno hilo ndiko neno Psychology linapotokea. Katika Kiebrania Nephes ina maana inayokaribia na pumzi au kiumbe kinachopumua. Katika upana wake nephes ina maana ya uhai kamili wa kiumbe. Hapo zamani neno hili halikuwa na maana kama tuliyonayo leo ya roho isiyokufa hata kama mwili utakufa. Neno hili lilimaanisha mwadamu katika ujumla wake. Agano Jipya ambalo liliandikwa Kigiriki limetumia neno Psyche. Wayunani waliona kuwa Psyche ni nguvu isiyoonekana iliyomo ndani ya kiumbe hai ambayo inakipa nguvu na mwendo. Kumekuwa na mabishano kuwa je mwanadamu ana nafsi au yeye mwenyewe ndiye nafsi. Kulinga na mwanzo 2:7 mwandamu yeye mwenyewe ndiye nafsi hai.

    iii.            Roho: Katika Kiebrania neno hili linajulikana kama Ruah na katika Kiyunani neno hilo linajulikana kama Pneuma. Neno hilo lina mana ya pumzi. Ni sehemu ya mwanadamu ambayo haionekani kwa macho ya nyama. Kuna baadhi ya wasomi wanaamini kuwa roho na nafsi ni kitu kimoja na wengine wanaona kuwa roho na nafsi ni vitu viwili tofauti. 

Mwanadamu ni Nini
Historia inaonenyesha kuwa watheologia wa Kikristo wanekuwa katika mabishano bila ya kukubaliana juu ya suala la kuwa mwanadamu ni muunganiko wa mambo gani au mwanadamu amegawanyika katika sehemu ngapi? Kwa ujumla yapo mawazo ya aina kuu tatu ya mgawanyo wa mwanadamu. Mawazo hayo ni Dichotomism, Trichotomism na Monism.
        i.            Dichotomism (sehemu mbili): Wanazuoni wa kundi hili wanasema kuwa mwanadamu amegawanyika katika sehemu kuu mbili: Mwili na nafsi au roho(roho na nafsi kwa watu hawa ni kitu kimoja). Mwili ni sehemu inayoonekana na kushikika (material) na roho au nafsi ni sehemu isiyoonekana au kushikika (spiritual). Haya ni mawazo yanayoungwa mkono na watu wengi. Kulingana na mawazo hayo, roho au nafsi vinakaa ndani ya mwili. Roho na nafsi huondoka katika mwili mtu anapokufa. Lakini vitarudi tena katika mwili wake siku ya ufufuko.
      ii.            Trichotomism (sehemu tatu): Watheologia wachache wanaamini kuwa mwanadamu amegawanyika katika sehemu tatu yaani mwili na roho na nafsi. Watheologia hawa wanatumia vifungu vituatavyo vya Biblia kuelezea jambo hilo; 1Thes. 5:23 na Ebr 2:12.
    iii.            Monism (sehemu moja): Wanatheologia wa kisasa (modern) wanashikilia msimamo kuwa mwanadamu ni sehemu moja tu. Mwanadamu hawezi kugawanyika (holism).Kwa hiyo hao wanataka mwanadamu achukuliwe kama mtu bila ya kumgawanya.

Asili/Chanzo(origin) cha Mwanadamu
Swali juu ya asili ya mwanadamu limesumbua wasomi wengi duniani tangu kale hadi hivi leo. Mila, desturi, ustaarabu na dini mbalimbali zina hadithi au hekaya tofouti juu ya wapi mwanadamu ametoka au jinsi gani mwanadamu amepata kuwepo duniani. Elimu juu ya asili ya mwanadamu na maendeleo yake ya kibailojia ni tawi la anthropologia linalojulikana kitaalam kama paleoanthropology.  Tawi hili la anthropologia linachunguza juu ya mila na desturi za watu, jamii, na yaliyomo katika bailogia ya mwanadamu. Paleoanthropology inachunguza zaidi juu ya tabia za kibaologioa na tabia za nje za mwanadamu (physical traits and behaviors). Kwakifupi tunaweza kusema kusema kuwa paleoanthropology inachunguza juu ya evolution. Kwa kufanya hivyo uwanja huo wa elimu unaangalia juu ya uhusiano wa kitabia uliopo kati ya mwanadamu na viumbe wengine duniani.
Yapo mawazo mbalimbali na mapokeo mengi yanayozungumzia suala la asili ya mwanadamu, kati ya mawazo hayo nadharia mbili ndizo zinazotumiwa na kuelezea asili ya mwanadamu. Nadharia hizo evolution theory na creation theory.
        i.            Evolution Theory
Wataalamu wanaofundisha asili ya mwanadamu kutumia nadharia hii wanasema kuwa mwanadamu alibadilika kutoka katika viumbe rahisi (simple) kwenda katika viumbe vigumu zaidi (complex). Wao wanaamini kuwa mwanadamu alibadilika kutokana na mazingira na mahitaji hadi kufikia katika hali aliyonayo sasa.
Watu hawa wanaamini kuwa mwanadamu yupo katika kundi moja na wanyama wa jamii ya nyani (chimpanzee) wote wanatoka katika genus iitwayo homo. Kwamba mwanadamu na nyani wanatoka katika wazazi (ancestors) wa aina moja. Walitoka katika babu hao kiasi cha miaka milioni tano hadi saba iliyopita.  Watalaamu hao wanasema kuliwahi kuwepo na species nyingi sana za homo lakini zimetoweka zamani sana. Miongoni mwao ni Homo erectus ambayo ilipatikana kule Asia, Homo Neanderthalensia ambaye alikuwa anapatika huko Ulaya na Homo Sapeans ambao walipatikana hapa Afrika. Inasemekana kuwa Homo Sapeans walikuwepo duniani kati ya miaka Laki nne na Hamsini elfu iliyopita.
Wataalamu wanasema kuwa mwanadamu aliyepo duniani leo hii ni matokeo ya Homo Sapean. Wanasayansi wanaamini kuwa bara la Afrika ndilo asili ya wanadamu ulimwengu.  Hii ni kwa sababu Homo Sapean aliishi Afrika alihamia katika bara la Asia na Ulaya na kuchukua nafasi ya Homo erectu na Homo Neanderthelensia.
Hata hivyo nadharia hiyo inashindwa kuonyesha asili ya uhai. Kumekuwa na mawazo kuwa uhai ulianzia majini kwa wanyama wadogo sana hadi kufikia wanayama wakubwa. Lakini bado haijafamika kuwa uhai huo uliokuwa majini unatoka wapi. Wazo la msingi hapa ni wanasayansi wameshindwa kufahamu asili ya DNA. Kwa hiyo bado kunahitajika njia nyingine ya kuelezea kuwepo wa uhai ulimwenguni. Haja hiyo ndiyo inayoleta suala la nadharia ya uumbaji.
Hatari ya mawazo hayo ni kuwa yanapunguza heshima ya mwanadamu. Pia yanaondoa uwepo wa muumbaji. Zaidi ya yote yanataka kusema kuwa mwanadamu hawajibiki kwa mtu yoyote.
      ii.            Creation Theory
Imani juu ya uumbaji inajulikana kama creationism. Nadharia ya uumbaji inaonyesha kuwa dunia na viumbe vilivyomo vimeumbwa na muumbaji na kuwekewa utaratibu wa jinsi ya kuenenda. Uumbaji huu unajulikana kama exnihilo. Hii maana yake ni kuwa uumbaji huo ulifanyika pasipokuwa na kitu cha kuumbia. Yaani uumbaji ulifanyika kutoka katika hakuna kwenda katika kuwepo (from nothing to something). Mawazo haya yanapingana na mawazo yanayosema kuwa mwanadamu hakuwaameumbwa kama alivyo leo bali alikuwa mnyama kama nyani hapo zamani. Nadharia hii inaonyesha kuwa mwanadamu ameumbwa na mamlaka kubwa kuliko yeye. Tena anaowajibu wa kufuata kile ambacho muumbaji wake anataka kifuatwe na mwanadamu.
Kulingana na Biblia (Mwa 1:26, 27/2:7) mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Kulingana na maandiko kuna mambo makuu matatu katika uumbaji wa mwanadamu: mavumbi ya ardhi, Pumzi na Nafsi hai.Mwanadamu ameumbwa (kwa mfano na sura ya Mungu, Image and likeness of God). Kwa kuwa wanadamu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu, wanadamu wote ni sawa na wote wanahitaji heshima sana. Wanadamu wote wana haki sawa.
Umoja wa tabia ya Binadamu
Ushahidi unaonyesha kuwa wanadamu wote duniani wanafanana katika tabia zao.Tofauti zao za rangi, taifa sio kitu. Ndani yao ni sawa katika mahitaji na tabia zao ja jumla (Mdo. 17:26; Rum5:12,19; 1Kor.25:21,22). Kuna aina nne za ushahidi unaothibitisha jambo hilo. Ushahidi wa kihistoria, ushahidi wa lugha, ushahidi wa saikolojia na ushahidi wa asili au maumbile ya kimwili ya wanadamu.
Swali kuhusu asili ya roho ya Mwanadamu
Wanatheologia wakubwa wamekuwa katika mabishano makali juu ya nini asili ya roho ya mwanadamu. Yapo mawazo makuu matatu yanayoshughulikia swali hilo.
        i.            Kabla ya uumbaji: Watheologia wanaunga mkono wazo hili ni pamoja Origen ambaye ametumia mawazo ya Plato. Wao wanasema kuwa roho ya mwanadamu ilikuwepo kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu. Wao waliamini kuwa roho ya mwanadamu ilikuwepo duniani na unapofika wakati wake inazaliwa duniani.

      ii.            Kurithi Kutoka kwa wazazi: Miongoni mwa watheologia wanaoamini nadharia hii ni Tertuliano, Marthini Luther. Wao wanaona kuwa ni kweli Mungu amemuumba mwanadamu. Lakini Mungu aliumba roho mara moja na kuiweka ndani ya Adamu na Hawa. Baada ya hapo wanadamu wanarithi roho zao kutoka kwa wazazi wao. Yaani wengine huzaliwa na roho zao.
    iii.            Uumbaji katika wakati: John Calvin na Jerome ni miongoni mwa watheologia wanaounga mkono wazo hili. Wao wanaamini katika wakati Fulani wa maisha ya mtu roho yake inaumbwa na kuwepo duniani.
DHAMBI
Tawi la theologia linaloshughulika na masuala ya dhambi linajulikana kitaalam kama hamartiology. Elimu hiyo inashughulika na asili ya dhambi, madhara yake kwa mwanadamu matokeo yake na jinsi ya kuepukana na dhambi.
Dhambi ni neno la kawaida sana katika maisha ya kila siku. Lakini ni neno gumu sana kuelezea mana yake. Pia ni vigumu sana kusema ni tendo gani au jambo gani linapofanywa huwa dhambi au sio dhambi. Pia ni vigumu sana kufahamu kuwa jambo gani au tendo gani hugeuka wakati gani kuwa dhambi.
Lakini sisi kama Wakristo tunacho kipimo cha kupimia dhambi, yaani Neno la Mungu. Lakini pia pamoja na kuwa na kipimo hicho cha kupimia dhambi, bado hatuwezi kuwa njia moja tu ya kuelezea dhambi. Mahali pengine dhambi inategemea mazingira na mapokeo ya watu husika. Kwa hiyo hata suala la dhambi linahitaji kufanyiwa Contextualization.
Mtazamo wa Biblia Kuhusu Dhambi
Mtazamo wa Biblia kuhusu dhambi umegawanyika katika sehemu kuu mbili kama Biblia yenyewe ilivyogawanyika. Upo mtazamo wa Agano la Kale ambao ni mtazamo wa Kiyahudi na mtazamo wa Agano Jipya ambao ni mtazamo wa Kiyunani.

        i.            Mtazamo wa Dhambi katika Agano la Kale.
Kwa mtazamo wa Kiyahudi, dhambi ni kitu chochote kile kinachokwenda kinyume amri takatifu za Mungu. Wayahudi walifundisha kuwa dhambi ni tendo la wala siyo hali. Katika lugha ya Kiebrania dhambi inajulikana kama avera. Kwa Wayahudi dhambi ipo katika viwango vitatu. Kwanza mtu afanye dhambi kwa kukusudia (B’mezid). Hii ni aina mbaya zaidi ya dhambi. Pili ni mtu anayefanya dhambi bila ya kukusudia (B’shogeg). Mtu huyu atawajibika kutokana na dhambi yake, lakini dhambi hii inachukuliwa kama dhambi ndogo.Na aina ya mwisho ni dhambi anayoifanya mtu kwa kuwa amekulia katika mazingira ambayo siyo ya Kiyahudi na hivyo akajikuta amevunja sheria. Mtu huyo alijulikana kama Tinok Shenishba. Mtu huyu hawajibiki kwa dhambi yake aliyofanya.

      ii.            Mtazamo wa Agano Jipya Kuhusu dhambi
Kwa Wakristo dhambi ni uvunjaji wa sheria. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa kama dhambi linaitwa Hamartia. Hamartia maana yake ni kupita njia isiyo sahihi au kukatiza njia. Maana nyingine ya dhambi ni kukosea shabaha. Kwa kifupi dhambi ni uasi (1Yoh.3:4). Missing the mark kuacha alama ya mstari au kupuuzia alama za barabarani katika hali kama hii kile kilichokatazwa katika agano jipya na mtu akakikiuka anakuwa amefanya dhambi hata hivyo dhambi hutendwa kumuelekea Mungu