Alhamisi, 17 Mei 2018

Pembe ya Wokovu wangu!



Mstari wa Msingi: Zaburi 18:2-8Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na PEMBE YA WOKOVU wangu, na ngome yangu. Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu. Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.  Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala, Makaa yakawashwa nao.”


Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-

1.       Maana ya neno Pembe
2.       Maana ya pembe ya wokovu


Maana ya  neno Pembe. 

Neno Pembe ya wokovu limetajwa mara nytingi sana katika sehemu mbalimbali za Maandiko Matakatifu yaani Biblia, Lakini itakuwa muhimu zaidi kama tutafahamu kwa pamoja kwa kina na mapana na marefu maana ya Pembe ya wokovu, neno Pembe na uhusiano wake katika wokovu.

Neno Pembe katika Biblia waebrania wanaiita “SHOFAR” imetumika katika maandiko kuelezea mambo mengi sana, katika namna nyepesi wote tunafahamu kuwa Pepmbe ni aina mfupa mgumu unaojitokeza na kukua katika kichwa cha mnyama, Mwanzo 22:13, Pembe ya mnyama hususani kondoo mume inatumika kama silaha ya Kushambulia, Kulinda, kuonyesha mamlaka na utawala na kuleta Hofu, ni ishara ya nguvu, uweza na ushindi, kwa Msingi huo maandiko yanapotaja Pembe mara nyingi hutumika kuelezea uweza na nguvu.

Kwa lugha nyingine ya kinabii neno Pembe pia linatumika kuelezea kuhusu Serikali, au ufalme au nguvu ya dola yaani nguvu za ufalme huo unaweza kuona katika  Daniel 7:7, 24Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.; 24  Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Unaweza kuona hivyo Pembe huzungumzia NGUVU au uweza wa KIJESHI Dolla, kwa msingi huo taifa au kabila fulani linapoondolewa ngvu zake lugha ya kibiblia maana yake pembe zake zimekatiliwa mbali Yeremia 48:25Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema Bwana. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya Bwana                                            

Pembe pia hutumika kuelegea nguvu ya Upako yaani uwezo wa Roho Mtakatifu,Pembe katika agano la kale zilitumika pia kuweka mafuta maalumu ya upako ambao wangepakwa watu kama makuhani, manabii na wafalme kwa kusudi la kutimiza mapenzi ya Mungu mfano 1. Samuel 16:1-3 “Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako, 13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.” Aidha Pembe zilitumika kama tarumbeta za kumsifu Mungu na zilipopulizwa pembe kwaajili ya utukufu wa Mungu ngome za adui zilianguka na kusambatratika kabisa Yoshua 6:1-5Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili.


Tafasiri nyingine ya kibiblia ilihusu pembe za madhabau  kwa maana ya kuwa kila kona ya madhabau kulikuwa na pembe nne, pembe hizi zilivyunyiziwa damu wakati wa kutoa dhabihu ili kwamba watu waweze kufanyiwa upatanisho kwa mungu na kupata rehema, sehemu hii ya pembe pia ilitumika kwa ibada ya upatanisho kati ya Mungu na wanadamu Walawi 8:15Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.”  Eneo hili la pembe za madhabahu lilitumika pia kumaanisha MAKIMBILIO au kujisalimisha endapo mtu angekuwa na tatizo linalohitaji kujihami, au kujitakia rehema hususani alipataka kuuawa 1Wafalme 1:50Adonia naye akaogopa mbele ya Sulemani; akaondoka, akaenda, akazishika pembe za madhabahu.” Kwa hivyo kimsingi hizo ndizo maana ya Pembe kibiblia.

Maana ya Pembe ya wokovu!

Kama tulivyoweza kuona kwa uapana na kina na urefu kuhusu maana ya neno Pembe sasa ni muhimu kwetu tukarejea katika andiko letu la Msingi Zaburi 18: 2 “Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na PEMBE YA WOKOVU WANGU, na ngome yangu.” Hapo sasa utaweza kumuelewa vema mwandishi wa zaburi anapozungumzia kuhusu Pembe ya wokovu wake, kwamba ana maanisha nini, Pembe kwa msingi huo ilitumika kuelezea WOKOVU neno wokovu katika kiyunani ni SOTERIA  ambalo maana yake ni Nguvu ya kuweka Huru, Nguvu ya kukuondoa Hatarini, Nguvu ya kukulinda na Hatari, Nguvu ya ukombozi, Nguvu ya kuharibu mipango ya adui, Nguvu ya kusambaratisha nguvu za adui yako Zaburi 75:10 “Pembe zote za wasio haki nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka” Kazi hii ya ukombozi Israel walikuwa na ufahamu na Roho Mtakatifu aliwafunulia wazi kuwa Dola hii au nguvu au serikali hii inayoweza kuleta ukombozi, inayoweza kuvunja vunja nguvu za adui zako, inayoweza kuharibu kila aina ya nguvu za upinzani, inayoweza kukulinda, inayoweza kukuokoa, inayoweza kukupa rehema na neema, inayoweza kukutetea dhidi ya adui zako dhidi ya waliokudhulumu, dhidi ya waonevu, dhidi ya magonjwa, dhidi ya masononeko, dhidi ya ufisadi, dhidi ya fitina, faraka , masengenyo mateto kunenwa vibaya, kusingiziwa, kuvunja nuksi mikosi na balaa, kukuweka huru nguvu hii inaitwa PEMBE YA WOKOVU LUKA 1:67-75 “. Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema,  Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.  Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;  Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu; Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu, Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,  Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote.”(my god mya god ribasakarabashanda! Rebosokoroboshi ribabababaskataritoli yenderebekisha sanda) Zekaria akajazwa Roho Mtakatifu kwa msingi huo maneno hayo ni ya Roho Mtakatifu, Na hapo yanamtaja “YESU KRISTO” ndni yake kuna ukombozi, ndani yake kuna kuokolewa na adui zetu ndani yake kuna kutolewa mikononi mwa wanaotuchukia Mungu wangu, kumbe kwaajili ya amani yetu na ulinzi wetu hatuhitaji pembe za waganga wa kienyeji, kwa sababu tunayo pembe tumesimamishiwa Pembe ya wokovu, Jina Yesu maana yake ni wokovu, Yesu ni mwenye nguvum kama zilivyo nguvu za Pembe za wanyama wakali, wenye nguvu Yuko mwenye nguvu kuliko vyote yeye ni pembe ya wokovu wangu, yeye ndio kimbilio letu yeye ndio mahali sahihi pa kujisalimisha mmmmmhmmmm my God najisikia kuhubiri hapa kuna mtu nasema naye hapa viti haviwezi kukalila maana nimempata Yesu, nimepata nguvu nina upako nina ulinzi wa ajabu sio kitu kingine ni Yesu mwana wa Mungu aliye hai pambe ya wokovu wangu! 

Mungu akubariki tafadhali si mbaya ukinijuza jinsi ulivyobarikiwa na somo hili  sms or whatsapp 0718990796

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Maoni 2 :

Unknown alisema ...

Barikiwa sana Mkuu wa wajenzi

Bila jina alisema ...

Nimebarikiwa sana, kwa mafundisho haya,nilipoyatafuta na nikaelewa vizuri,,asante sana 🙏