Nyakati hizi tulizo nazo ni nyakati za mwisho sana, Biblia inaziita nyakati hizi kama nyakati za hatari “2Timotheo 3:1-5”Katika nyakati hizi za mwisho moja ya matatizo makubwa sana yatakayosumbua ulimwengu ni pamoja na matatizo ya kifamilia, ni muhimu kufahamu kuwa nshetani atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa anazishambulia familia kwa kadiri awezavyo ili kuwavuruga wanadamu na kuharibu mpango na makusudi ya Mungu. Tutajifunza somo hili FAMILIA CHINI YA UVAMIZI kwakuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-
- · Familia ni Mpango wa MUngu.
- · Uvamizi Katika Familia (Family Under Siege).
- · Jinsi ya Kuilinda na kuiponya Familia.
Familia ni Mpango wa Mungu
Kabla hatujaanza kuangalia kwa
undani kuhusu uvamizi katika familia ; ni muhimu kwa kila mmoja kuwa na ufahamu
kuwa Familia ni Mpango wa Mungu, kutokana na vipingmizi mbalimbali
tunavyokutana navyo wanadamu tunaweza kufikiri kuwa labda sio mpango wa Mungu
kwangu au kwetu kuwa na familia, lakini ni muhimu kuyajua maandiko ambayo
yanatukumbusha kuwa familia ni Mpango wa Mungu.
Kaini akimuua Habili Nduguye
1. Ni
muhimu kufahamu kuwa Mungu ndiyi aliyemuumba Mwanadamu Mwanzo 1:26-27
2. Mungu
alimuumba mwanadamu ili awe na uhusiano Mwanzo 2:18
3. Mungu
alimuumba Mwanadamu ili awe na uhusiano naye Mwanzo 3:8
4. Mungu
alikusudia mwanadamu awe na Hisia kali dhidi ya jamii yake Mathayo 19:4-6
5. Mungu
alikusudia Jamii iongezeke Mwanzo 1:28, Zaburi 27:3-5
6. Mungu
alikusudia watoto walelewe na familia na sio mitaani 1Timotheo 5:8
7. Mungu
alikusudia Familia iwe ndio shule ya kwanza ya kujifunza uadilifu Mwanzo
18:17-19
Hata hivyo kwa kufahamu kuwa
familia ni taasisi muhimu, shetani amekuwa akizishambulia familia na kuziweka
chini ya ulizni wake kwa kujua kua akifanya hivyo ataharibu Jamii, taasisi.
Kanisa, taifa na ulimwengu kwa ujumla!
Uvamizi Katika Familia
Tunapozungumzia uvamizi katika
Familia tunazungumzia Kiswahili cha zamani KUHUSURU kwa kiingereza SIEGE.
Kuhusuru ni uvamizi unaofanywa na jeshi katika vita za zamani ili kuwabana watu
walioko mjini kwa muda mrefu wasiweze kutoka au kuingia mpaka wadhoofike na
hatimaye kuwangamiza kabisa kwa urahisi!
SIEGE - “According to Oxford Advanced Learners
dictionary is A military Operation in
which an army tries to capture a town by surrounding it and stopping the supply
of food etc to the people”
Shetani makusudio yake kwa
familia ni mabaya, analeta mashambulizi na kuzibana familia kila kona ili
kuleta uharibifu mkubwa,
Shetani katika karne hii
amafanikiwa kuharibu familia kiasi ambacho miaka michache ijayo kutakuwa na hali
mbaya zaidi
Amefanikiwa
·
Kuwafanya wazazi kuwa mbali na watoto wao
·
Amefanikiwa kuharibu utawala na Mamlaka katika
familia kupitia Usawa na haki
·
Amefanikiwa kuwafanya wanaume kwa wanawake kuwa
na pilikapilika za kutafuta maisha
·
Misuguano katika maswala ya fedha
·
Amefanikiwa kuwafanya watoto wengi sana waishi
mitaani na kukosa malezi
·
Amefanikiwa kuwaangamiza wengine mapema kwa
kusababisha n utoaji wa mimba
·
Ameingiza utasa na ugumba katika familia nyingi
kinyume na Baraka za Mungu
·
Amefanikiwa kuwafanya watoto wengi wasitii,
ameleta magonjwa,Hofu, kutokuaminiana,ubinafsi, choyo, umimi, na kukosa uaminifu
Shetani katika mpango wake huo
amekusudia kuharibu mpango wote wa Mungu kabisa na kuwa kinyume na familia
Biblia inatukumbusha kuwa tutapoyaona hayo hatupaswi kufikiri kuwa ni kitu
Kigeni 1Petro 4:12 Biblia imejaa mifano mingi ya watu ambao shetani alizivuruga
familia zao hata pamoja na kuwa walikuwa watu wa Mungu!
-
Familia ya kwanza ilikuwa ya wana wa Mungu
mwenyewe Adamu na Eva wao walikuwa wa kwanza kumuasi Mungu ambaye alikuwa ni
Baba yao
-
Adamu na Eva walikuwa na watoto wao wa pekee
Kaini na Habil lakini walijaa wivu na kuchukiana na kaini aliamua kumua
nduguye?
-
Nuhu alikuwa Mtu wa haki alikuwa na wana watatu
Hamue, Japhet na Shemu Lakini Hamu alimvinjia Heshima Baba Yake
-
Ibarahimu alikuwa na Ishmael na Isaka lakini
Ishamel alimnyanyasa na kumdhihaki nduguye
-
Lutu alizaa na Binti zake
-
Isaka alimpenda Esau Rebeka akampenda Yakobo na
kusababisha mgawanyiko katika familia
-
Esau na Yakobo walifanyiana mambo ya hiyana na
Esau alikusudia kumuua nduguye
-
Reuben alimkosea Heshima Baba Yake, Pia wana wa
Isarael walitaka kumuua Yusufu Ndugu yao na kuamua kumuuza huko Misri
-
Musa, Mkewe alishambuliwa na wifi yake na
shemeji yake yaani Miriam na Haruni
-
Daudi alikuwa shujaa lakini hakuwa shujaa wa
kuilinda familia yake aliidekeza na kushindwa kusimamia uadilifu katika familia
Huu ni Uvamizi katika Familia,
hali ni mbaya leo ziko familia zinagombania Urithi, Mali na kadhalika, watu
hawajifunzi kuwa na vyao, ziko familia nyingine watu wanaombea mpaka maiti, au
watu wanaapizana usiisogelee maiti yangu, au uaduia kati ya ndugu na ndugu,
watoto wasiotii, leo hii wengine wazazi wanawaogopa watoto wao hufu na wasiwasi
umeingia katika Familia hakuna kuaminiana magomvi na Vitimvi, Tendo la Ndoa
baya, watu wananyimana, hii yote ni Uvamizi katika Familia! Ni namna Gani
tunaweza kupata Uponyaji?
Jinsi ya Kuilinda na kuiponya familia
Kwa kuwa Familia ni Mpango wa
Mungu hii ndio zawadi yetu ya Kwanza na ni Mungu ndiye aliyetuchagulia
1. Ni
lazima Mamlaka na Utawala katika Familia Ukawa chini ya Baba Mwanzo 3:16
2. Lazima
watoto wajitiishe chini ya wazazi wao Kutoka 20:12, Efeso 6:1
3. Lazima
Wazai wawafundishe watoto wao njia za Mungu Kumukumbu 6:6-7 Mithali 22:6
4. Lazima
wakubwa wote nyumbani wawe mfano na kielelezo cha kuigwa 2Nyakati 26:3-4
5. Tuache
kujifikiri kuwa tunaweza kuwa na akili kumshinda Mungu ni lazima tulifuate neno
lake huu ndio Muongozo wake unaoweza kutusaidia
6. Mpinge
Ibilisi na wala msimpe nafasi, Kemea kila unachokiona sio cha kawaida, Mafno
haiwezekani Binti mdogo miaka 9 akaanza kuota maziwa ni lazima ujiulize ya
nini? Ni mapema sana
7. Kemea
na kuwa na maombi maalumu ya kifamilia na kama mnaweza kuwa na Ibada za
Kifamilia anzisha Ibada
8. Kuwa
na Muda na Familia yako, Mumeo au Mkeo na zungumza naye kwa Lugha njema na
tuwaheshimu wazazi wetu na kuwatunza.
9. Pinga
sheria mbaya zinazopitishwa na mataifa makubwa mfano ndoa za jinsia Moja, Haki
za utoaji wa Mimba , haki za watoto na wanawake, ni lazima zipimwe kwa neno la
Mungu kwanza pamoja na mila na tamaduni zetu zilizo nzuri.
Mungu amekupa
wajibu wa Kuilinda na kuitetea Familia yako itetee, ukiyajua Hayo Heri wewe
Ukiyatenda
Mkuu wa Wajenzi
mwenye Hekima Rev. Innocent Kamote.