Mathayo 28:18-19 “Yesu akaja
kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi,
enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba,
na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru
ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
Utangulizi:
Mojawapo ya jambo kubwa na Muhimu
sana katika kuyatenda mapenzi ya Mungu ni pamoja na kufanya kazi ya umisheni,
Kazi ya umisheni ndio mapenzi halisi ya Mungu, wakati wote kanisa linapaswa
kukumbuka kuwa mojawapo ya sehemu muhimu ya utekelezaji wa agizo kuu ni pamoja
na kazi ya umisheni na haya ndio mapenzi ya Mungu kwetu! Kusudi kubwa mataifa
yote wamjue Mungu na kumwamini mwana wa Mungu Yesu Kristo ili wawe na uzima wa
milele
Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee
wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
UMUHIMU WA KUFIKIRI KUHUSU ULIMWENGU.
ü
Mpango wa Mungu wa Wokovu hauhusu tu Utamaduni
mmoja au taifa moja pekee.
ü
Mungu hajawahi kufikiri kuhusu Mtu mmoja tu au
taifa moja pekee
ü
Mpango wa Mungu wa wokovu unahusu Ulimwengu
mzima, na unaanza na mtu mmoja, Familia, taifa na ulimwengu mzima
ü
Mungu anapokuita wewe na kukubariki kumbuka sio
kwaajili yako tu na Familia yako, au watu wako na taifa lako tu bali ni kwaajili ya ulimwengu mzima
ü
Kwa hiyo lolote ambalo Mungu amekuita kulifanya
na kulitenda ni kwaajili ya Ulimwengu mzima
MUNGU ALIPOMUITA IBRAHIMU.
Mwanzo 12:1-3
BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi
yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi
nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na
kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye
akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za DUNIA watabarikiwa.
MUNGU ALIPOMUITA YEREMIA.
Yeremia
1:4-5 Neno la Bwana lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
MUNGU ALIPOTUPA YESU KRISTO.
Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ULIMWENGU,
hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima
wa milele.
BIBLIA NA UMISHENI
ü
Biblia inazungumzia kuhusu Umisheni
ü
Umisheni ni nini?
ü
Umisheni ni agizo muhimu analopewa mtu au
watu, linalohusiana na kutoka au kuwaendea watu wa utamaduni tofauti kwa
kiyunani “APOSTOLOS” AU APOSTELLO yaani Utume
ü
Ni Sauti ya wito wa kiimani au kidini au
kimaandiko, au kidhehebu hususani Wakristo kutoka na kwenda kutimiza Agizo kuu
Duniani kwa kusambaza na Kuhubiri Habari njema za Bwana Yesu
ANGALIA AGIZO KUU
Mathayo
28:18-20 “Yesu akaja kwao, akasema nao,
akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni,
mkawafanye MATAIFA yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana,
na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha
kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku
zote, hata ukamilifu wa dahari.”
UMUHIMU WA UMISHENI
ü
Kwa sababu wanadamu wote Wamepotea
ü
Luka 19:10 “Kwa
kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea”
ü
Umisheni ndio mapenzi kamili ya Mungu
ü
Ni Agizo kuu kuhubiri injili Mathayo 28:18-20
“Yesu
akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la
Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru
ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
ü Kutakuwa
na kuwajibika kwaajili ya damu ya mtu mwovu kama hatutafanya sehemu yetu
Ezekieli 33:8-9
“Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika
utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya
huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye
asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.”
ZABURI 14:1-3
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo
yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana
aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.
Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
WATU WOTE WAMEFANYA DHAMBI
WARUMI
3:10-12, 23
kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. 23.kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
YESU NI KIELELEZO.
ü
Akizungumza juu ya Huduma aliyokuja kuifanya
Duniani Yesu yeye mwenyewe alisema wazi kwanini amekuja Ulimwenguni
ü
Luka 19:10 - Alikuja kuokoa na kutafuta
kilichopotea
ü
Mathayo 18:11- Alikuja kutafuta
kilichopotea
ü
Mathayo 18:14 – Mungu hataki awaye yote
apotee
ü
Mathayo 18:12-13 Mtu mmoja atubuye ni
muhimu kuliko 99 wasio na hitaji la toba
ü
Luka 15:7,10,32 – Kuna furaha kubwa
mbinguni kwaajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye
MUNGU NDIYE MWANZILISHI WA UMISHENI.
ü Mpango
wa Ukombozi uliandaliwa na Mungu ni yeye ndiye aliyemtafuta mwanadamu Mwanzo
3:8-9 “Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu,
akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya
miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia,
Uko wapi? ”
ü
Mungu hataki mtu yeyote apotee Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele.”
ü Alishuka
Wajati wana wa Israel wanaonewa Kutoka 3:7-10 “BWANA
akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia
kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami
nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata
nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani,
na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha
wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri
wanawatesa. Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu
wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”
ü
Anataka watu wote wafikilie Toba – 2Petro 3:9
“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine
wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee,
bali wote wafikilie toba.”
ü Baba
wa Mbinguni hafurahii awaye yote apotee Mathayo 18:12-14 “Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je!
Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?
Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa
na tisini wasiopotea. Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni
kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.”
WITO WA UMISHENI |
|
Yesu
ni Mfano wa Umisheni
|
Matendo 16:9-10
Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia
amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi
alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa
tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
UMISHENI
UNAHITAJI UTII
Yesu alikuwa mtii katika mapenzi ya Mungu
yote
Zaburi 40:7-8 “Ndipo
niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,) Kuyafanya
mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni
mwangu.”
Waebrania
10:5-7 “Kwa
hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili
uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;
Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa)
Niyafanye mapenzi yako, Mungu”
UMISHENI UNAHITAJI KUJIKANA
NAFSI
ü
Yesu alijikana nafsi
ü
Hakuna mahali popote ambapo Yesu alitumikia
umimi au kuonyesha au kunena kuhusu mambo yake
ü
Kila alichokifanya ilikuwa ni kwaajili ya
kumpendeza Mungu baba yake na kuwahudumia watu
ü
Majaribu yote yaliyomjia Yesu Kristo kutoka kwa
Shetani ilikuwa yalilenga kujihurumia yeye
ü Matthew
4:1-11, “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani,
ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona
njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe
haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Kisha Ibilisi akamchukua
mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe
Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na
mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu
akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Kisha Ibilisi
akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na
fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu
alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu
wako, umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja
malaika wakamtumikia.”
ü Mark
1:12-13, “Mara Roho akamtoa aende nyikani. Akawako
huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja
na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia.”
ü Luke 4:1-13 “Na
Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda
wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali
kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa
Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu
hataishi kwa mkate tu. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu
kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari
yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi,
wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia,
Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Akamwongoza
mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe
Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake
wakulinde; na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako
katika jiwe.Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Basi
alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.”
ü
Huu ni
ushahidi wa majaribu ambayo Yesu aliyashinda
UMISHENI UNAHITAJI HURUMA
ü
Yesu aliongozwa na huruma kubwa kwa wanaoteseka
na wanaopotea
ü Wakati
wote alisukumwa na huruma kwa wanadamu Mathayo 9:36-38 “Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa
wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. Ndipo alipowaambia
wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni
Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.”
ü
Alivuka mipaka na kwenda kuwahudumia watu
waliokataliwa na waliokuwa na dhambi Yohana
4:3-10. “aliacha
Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya. Naye alikuwa hana budi kupita
katikati ya Samaria. Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu
na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. Na hapo palikuwa na kisima
cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi
kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji.
Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini
kununua chakula. Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi
kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani
na Wasamaria.) Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye
ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji
yaliyo hai.”
ü Mtu
wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko aliyechukua mateso yetu Isaya 53:3-4 “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni
nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,
Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu,
na kuteswa.”
UMISHENI UNAHITAJI KUKAA KWENYE
KUSUDI LA MUNGU
ü
Yesu alihakikisha anakaa katika kusudi wakati
wote
ü
Mara kadhaa Yesu alijaribiwa na watu ili atoke
katika kusudi
ü
Kuna wakati watu walitaka kumfanya yeye kuwa
mfalme Yohana 6:15 “Kisha Yesu, hali akitambua
ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena
mlimani yeye peke yake.”
ü Na
kuna wakati Shetani alimtumia moja ya wanafunzi wake Kumzuia asiende msalabani Mathayo
16:22-23 “Petro akamchukua, akaanza kumkemea,
akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda
nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya
wanadamu.”
ü Ndugu
zake pia hawakumuelewa Mathayo 12:46-50 “Alipokuwa
katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama
nje, wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako
wamesimama nje, wanataka kusema nawe. Akajibu, akamwambia yule aliyempasha
habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? Akawanyoshea mkono
wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana ye yote
atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na
umbu langu, na mama yangu.”
John 7:3-9. “Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi,
wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna
mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo
haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hata nduguze hawakumwamini. Basi
Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi
naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi
sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. Naye
alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.”
UMISHENI UNAHITAJI NGUVU ZA MUNGU
ü
Umisheni
sio rahisi bila kuwa na nguvu za Mungu
ü
Musa hakuenda Misri bila nguvu za Mungu,
alikabiliana na Yane na Yambre wachawi wakubwa waliomsaidia Farao
2Timotheo 3:8, “Na kama vile Yane na Yambre
walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu
walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.”
ü Kutoka
7:20-22 “Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama BWANA
alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni,
mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika
mto yakageuzwa kuwa damu. Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto
ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa
katika nchi yote na Misri. Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa
uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama BWANA
alivyonena.”
ü Filipo alipambana na Simon Mchawi Matendo
8:5-21 “Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria,
akawahubiri Kristo. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale
yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa
maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na
watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji
ule. Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika
mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu
mkubwa. Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza
wa Mungu, ule Mkuu. Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa
uchawi wake. Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa
Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Na yeye
Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa
alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. Na mitume waliokuwako
Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu,
wakawapelekea Petro na Yohana; ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho
Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa
jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho
Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa
kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, Nipeni na mimi uwezo
huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Lakini
Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania
ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika
jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.”
ü Paulo mtume alipambana na Elima yule
Mchawi Matendo 13:6-12 “Walipokwisha kupita
katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo,
Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu
mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka
kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina
lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote,
mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana
zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu,
usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na
kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo yule liwali, alipoyaona
yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.”
ü Samsoni
dhidi ya wafilisti Waamuzi 15:14-16 “Alipofika
Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia
kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani
iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. Naye
akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa
huo; Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda
nimepiga watu elfu.”
ü Eliya
dhidi ya Manabii wa baali 1Wafalme 18:21-40 “Naye
Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili
hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya!
Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno. Ndipo Eliya akawaambia watu, Mimi
nimesalia, mimi peke yangu, nabii wa Bwana; lakini manabii wa Baali ni watu mia
nne na hamsini. Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie
ng'ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami
nitamtengeza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto
chini. Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana; na
Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu wakasema,
Maneno haya ni mazuri. Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe
mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu
wenu, wala msitie moto chini. Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza,
wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali,
utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya
madhabahu waliyoifanya. Ikawa, wakati wa
adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni
mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala,
sharti aamshwe. Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo
desturi yao, hata damu ikawachuruzika. Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita,
walitabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti,
wala aliyejibu, wala aliyeangalia. Kisha Eliya akawaambia watu wote,
Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya Bwana
iliyovunjika. Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana
wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la Bwana na kuambiwa, Jina lako litakuwa
Israeli. Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya
mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. Kisha
akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya
kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya
kuteketezwa, na juu ya kuni. Akasema,
Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya tatu.
Wakafanya mara ya tatu. Yale maji
yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji. Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu
ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa
Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli,
na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno
lako. Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana,
ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. Ndipo moto wa Bwana
ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi,
ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona,
wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu. Eliya
akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata;
na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.”
ü Tunapotumwa
katika umisheni tutakutana na watu, na serikali zinazotegemea nguzu za giza na
sio Mungu Mwanzo 41:1-8 “Ikawa, mwisho wa miaka
miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na
tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha
manyasini. Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni,
wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto.
Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono.
Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba
yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba,
yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke
membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka,
kumbe! Ni ndoto tu. Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita
waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia
ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.”
ü Huwezi kuigiza nguvu za Mungu Matendo
19:11-20 “Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo
miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka
mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. Baadhi ya
Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la
Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu,
yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi,
kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu
namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na
pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio
katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa. Habari hii ikajulikana na
Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la
Bwana Yesu likatukuzwa. Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama,
wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya
uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya
hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu.Hivyo
ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu.”
ü
Ni lazima tuwe na Nguvu za Mungu Waefeso
6:12, “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu
ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
ü
2Wakorintho 10:4, (maana
silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha
ngome;)
ü
Matendo 1:8, “Lakini
mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi.”
ü
Luka 24:49 “Na
tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata
mvikwe uwezo utokao juu.”
UMISHENI UNAHITAJI FEDHA
ü Kazi
ya umisheni inahitaji watu watakaoifadhili Warumi 10:13-15 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi
wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena
wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa,
Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”
ü Yesu
alikuwa na watu waliokuwa wakiifadhili huduma yake Luka 8:1-3 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika
miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale
Thenashara walikuwa pamoja naye, na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na
pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa
na pepo saba, na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine
wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.” Kama sisi hatuendi
tunaweza kwenda kwa njia ya maombi na ufadhili
ü
2 Wakorinthio8:9 “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu
Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili
kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.”
MAVUNO YAKO TAYARI
Yohana 4:35 “Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno?
Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha
kuwa meupe, tayari kwa mavuno.”
INUENI MACHO YENU MASHAMBA YAKO TAYARI
UMISHENI UNAWEZA KUFANYIKA
KATIKA KILA HALI
Binti aliyekuwa kijakazi huko Shamu 2Wafalme 5:1-14 “Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu,
alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa
mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa
vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua
mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe
Naamani. Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii
aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. Mtu mmoja akaingia, akamwambia
bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi
na hivi. Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa
Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za
fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi. Akampelekea mfalme wa
Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma
mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake. Ikawa, mfalme wa
Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! Mimi ni Mungu,
niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu nimponye ukoma wake? Fahamuni,
basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami. Ikawa, Elisha,
yule mtu wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake,
ndipo akatuma mtu kwa mfalme, akisema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje
sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli. Basi Naamani
akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha.
Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara
saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi. Lakini Naamani
akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu,
na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake
mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma. Je! Abana na Farpari,
mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani
yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira. Watumishi wake wakamkaribia,
wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo
kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi? Ndipo
akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu
wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto
mchanga, akawa safi.”
ü
Alikuwa ni binti kijana na mtumwa tu
ü
Alikuwa na busara na alionyesha upendo
ü
Alikumbuka Nguvu za Mungu wa Israel
ü
Alihubiri habari za uweza wa Mungu wa Israel kwa
mkuu wa Majeshi ya Syria
ü Mkuu
wa majeshi ya Syria alimuamini Mungu wa Israel 2Wafalme – 5:14-15 “Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani,
sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa
kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. Akamrudia yule mtu wa Mungu,
yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama,
najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba
upokee mbaraka kwa mtumwa wako.”
ü
Ni
kupitia Binti Mtumwa mjakazi mwenye ujasiri na Busara mtu mkubwa sana mkuu wa
majeshi wa Syria alimuamini Mungu wa Israel na kuponywa ukoma wake
Mfano wa vijana watatu
utumwani
Daniel
3:16-18 “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego,
wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno
hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile
iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo,
ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala
kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Hanania,
na Mishaeli, na Azaria, ni vijana waliochukuliwa utumwani kule Babeli, tamaduni
yao lugha yao majina yao yalibadilishwa Daniel 1:2-7 “Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono
wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka
nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika
nyumba ya hazina ya mungu wake.Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi
wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa
kiungwana; vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa
sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba
la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Huyo
mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa,
akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame
mbele ya mfalme. Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na
Hanania, na Mishaeli, na Azaria. Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita
Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita
Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.”
Walilazimishwa
kuabudu miungu ya huko, lakini kwa ujasiri mkubwa walishuhudia kuwa yuko Mungu
wa kweli Duniani Daniel 3:16-18 “Ndipo Shadraka,
na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna
haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza
kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.
Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu
yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Kupitia ujasiri wao na imani yao Waliweza
kumshawishi Mfalme kumuabudu Mungu wa Israel ona Daniel 3:28-29 “Nebukadreza
akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego;
aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza
neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala
kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe. Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila ya
watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya
huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na
nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna
hii.”
Mfano wa Daniel Kupitia Tundu
la Simba
Daniel
6:1-28 “Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali
mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na
Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate
hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa
roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli
kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa
maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. Ndipo
wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata
katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Basi wale mawaziri na maamiri
wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi
milele. Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na
maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga
marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa
mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa
katika tundu la simba. Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko
haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza
kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.
Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia
nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa
kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru
mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao
wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu
wake. Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku
ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua
kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini,
ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema,
Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza
kubadilika. Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja
wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile
marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku. Basi mfalme
aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya
Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa. Ndipo watu wale
wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya
kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku,
wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme. Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta
Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli,
Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya. Likaletwa jiwe, likawekwa
mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe,
na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za
Danieli. Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga;
na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa. Asubuhi mfalme
akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba. Naye
alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme
akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu
wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danieli
akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele. Mungu wangu amemtuma malaika wake,
naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi
nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. Basi
mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli
akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake,
kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake. Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale
watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto
wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande,
kabla hawajafika chini ya tundu. Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila
zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na
iongezeke kwenu. Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme
wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye
Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka
yake itadumu hata mwisho. Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu
mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba. Basi Danieli
huyo akafanikiwa katika enzi ya Dario, na katika enzi ya Koreshi, Mwajemi.”
Alikuwa bora kuliko mawaziri wote 120
Alihudumu
Katika utawala wa Dario mmedi Daniel 6:1-3 “Ilimpendeza
Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;
na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali
hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa
kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme
akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.”
Wenzake
walitafuta namna ya kupata sababu za kumshitaki Daniel 6:4-9 “Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za
kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona
sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala
hatia ndani yake. Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki
Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Basi wale
mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi,
Mfalme Dario, uishi milele. Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na
madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na
kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au
kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme
atatupwa katika tundu la simba. Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi
maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza
kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.”
Daniel
Hakuacha kuomba Daniel 6:10-16, “Hata Danieli,
alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani
mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili
Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za
Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika
pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake. Ndipo
wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme;
Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu
awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako,
Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili
ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika. Basi
wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale
waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia
sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku. Basi mfalme aliposikia maneno haya
alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha
kumwokoa hata jua likachwa. Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya
mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na
Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote
iliyowekwa na mfalme. Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa
katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako
unayemtumikia daima, yeye atakuponya.” na kwaajili hiyo alitupwa katikamtundu la
Simba
Mungu
alimuokoa Daniel na kuwa ushuhuda kwa mfalme na taifa zima Daniel 6:20-27 “Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa
sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa
Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba
hawa? Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.Mungu wangu
amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa
kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme,
sikukosa neno. Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile
tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote
halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake. Mfalme
akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika
tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda
wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu. Ndipo
mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote,
waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu. Mimi naweka amri, ya
kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za
Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme
wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho. Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na
maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.”
Mfano wa Nabii Yona huko Ninawi
Aliitwa na Mungu kwenda katika jiji la Ninawi – Yona 1:1 “Basi
neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema,”
Yona aliamua kukimbia kwenda nchi ya mbali zaidi
Yona 1:3 “Lakini Yona akaondoka akimbilie
Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona
merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende
pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana.”
Mungu
alisababisha tatizo kubwa lililopelekea yona kutupwa baharini Yona 1:4-10 “Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani
kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika. Basi wale mabaharia
wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena
iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka
hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. Basi nahodha
akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu
wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee. Wakasemezana kila mtu na
mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya
nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Ndipo wakamwambia,
Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi
yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa
kabila gani? Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu,
aliyeziumba bahari na nchi kavu. Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni
jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia,
ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha.”
Yona alitupwa baharini , na kumezwa na nyangumi Yona
1:12 “Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe
baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu
tufani hii imewapata.”
Mungu
alimuamuru Samaki mkubwa kumtapika Yona na kumuita mara ya pili, alitii na
kuhubiri mji wa Ninawi na mfalme na watu wote wakamgeukia Mungu Yona 3:4-10 “Yona
akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya
siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu;
wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata
aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti
chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika
majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya
mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi
ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na
wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa
nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio
mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha
hasira yake kali, ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha
njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema
atawatenda; asilitende.”
Mfano wa Mfalme Suleimani na Hekima yake
Mungu
alimpa Mfalme Suleimani Hekima kubwa sana 1Wafalme 10:1-5 “Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya
jina la Bwana, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo. Akaingia Yerusalemu
na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na
vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa
nayo moyoni. Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na
neno alilofichiwa mfalme asimwambie. Naye malkia wa Sheba alipoona hekima yote
ya Sulemani, na nyumba aliyokuwa ameijenga, na chakula cha mezani pake, na
watumishi wake walivyokaa, na kusimamia kwao wangoje wake, na mavazi yao, na
wanyweshaji wake, na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana, roho yake
ilizimia.”
Suleimani Mwana wa Daudi aliweka wazi kuwa
mpango wa Mungu ulikuwa ni kwa mataifa yote
Alijenga Nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa na
utikufu mkubwa sana uliovutia watu wa dunia nzima
Wafalme
wengi maarufu walikuja kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuisikia hekima ya
suleimani na kuona nyumba ya kifahari aliyoijenga, maalumu sana Malikia wa
Sheba (Ethiopia) alisema wazi kuwa habari alizosikia kuhusu Suleimani ni za
kweli na zaidi hata ya kile alichokisikia 1Wafalme 10:6-7“Akamwambia mfalme, Ndizo kweli habari zile nilizozisikia
katika nchi yangu za mambo yako na za hekima yako. Lakini mimi sikuzisadiki
habari hizo, hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; tena, tazama, sikuambiwa
nusu; wewe umezidi kwa hekima na kufanikiwa kuliko habari nilizozisikia.”
Mfano wa Hekalu la Mfalme Sulamani
Nyumba ya Mungu yenye Mvuto Mkubwa sana
1Wafalme 8: 41 -
43 “Hata
na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi
iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako; (maana watasikia habari za jina lako
kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa); atakapokuja
na kuomba kuielekea nyumba hii; basi, usikie huko mbinguni, makao yako,
ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia
wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya
kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako.”
William Ruto Rais wa Kenya
Shinzo Abe aliyewahi kuwa
waziri mkuu maarufu wa Japan
Waziri mkuu wa Israel Mwenyewe Benjamin Netanyahu
Pope Benedict wa 16
Pope Francis
Mfano wa Paulo na sila
Walikuwa
katika kazi ya umisheni wakafungwa – Matendo 16:23-31 “Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa
gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Naye akiisha kupata amri
hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini
panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia
nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata
misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya
wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango
ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa
wamekimbia. Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa
maana sisi sote tupo hapa. Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa
hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu,
yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe
utaokoka pamoja na nyumba yako.”
Walishambuliwa
na kupigwa kwaajili ya injili na wakatupwa gerezani, lakini waliitumia hali
hiyo Kuomba na kumuimbia Mungu wa Kweli, Mungu alisababisha Magereza
kutikisiaka Matendo 16:25-26 “Lakini panapo
usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za
kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko
kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango
ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”
Hali
ilimalizika kwa mkuu wa gereza kumuamini Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi na yeye
na nyumba yake kubatizwa Matendo 16:30-33 “kisha
akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Akawakaribisha
saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake
wote wakati uo huo.”
Mfano wa Mtumwa aliyemkimbia
Bwana wake
Onesmo
mtumwa wa Philemon alimkimbia bwana wake
na kufungwa Gerezani - Philemoni 1:1-9 “Paulo,
mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa
wetu, mtenda kazi pamoja nasi, na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari
mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako. Neema na iwe kwenu, na
amani, zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru
Mungu wangu sikuzote, nikikukumbuka katika maombi yangu; nikisikia habari za
upendo wako na imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote; ili
kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema
kilicho kwetu, katika Kristo. Maana nalikuwa na furaha nyingi na faraja kwa
sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu
yangu. Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo;
lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo mzee, na
sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia.”
Wakati huo Paulo Mtume alikuwa amefungwa
Gerezani, ndani ya gereza alikutana na Onesmo aliyemkimbia Bwana wake ambaye ni
Mwanafunzi wa Paulo mtume, Mwanafunzi huyo ni Filemoni
Paulo mtume alimuhubiri Onesmo ambaye
aliiamini injili, na alipokuwa anaachiwa paulo akliandika waraka wa kumuombea
Msamaha na kuwapatanisha Onesmo na Filemoni
Kwa
kuwa sasa amebadilika kupitia injili na mafundisho ya Mtume Paulo akiwa
kifungoni Philemoni Philemon 1:10-18 “Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika
vifungo vyangu, yaani, Onesimo; ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa
sana, wewe na mimi pia; niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu
hasa; ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika
vifungo vya Injili. Lakini sikutaka kutenda neno lo lote isipokuwa kwa shauri
lako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari. Maana, labda
ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele; tokea sasa, si
kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako
wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. Basi kama ukiniona mimi kuwa
mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi mwenyewe. Na kama amekudhulumu, au unamwia
kitu, ukiandike hicho juu yangu.”
Mfano wa Filipo na Towashi wa
Kushi (Ethiopia)
Filipo aqlielekezwa na Roho Mtakatifu kwa mtu
huyu Muhimu kutoka Ethiopia Matendo 8:26-40 alimshuhudia habari za
Kristo na injili ikafika nchini Ethiopia na bara la afrika mapema mnamo Karne
ya Kwanza.
Matendo 8:26-30 “Malaika wa Bwana akasema na Filipo,
akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka
Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona
mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi,
aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu,
akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. Roho akamwambia
Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. Basi Filipo akaenda mbio,
akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?”
WITO KATIMA UMISHENI
Tunapopitia maandiko tunagundua kuwa bado Mungu
anaita watu katika kazi ya umisheni
Na pia tunagundua kuwa kwa njia yoyote na katika
hali yoyote ile bado tunaweza kuihubiri habari njema kwa wengine, tunaweza
kuwahubiri watu habari njema kwa maneno yetu na matendo yetu kwa njia yoyote
Mungu ametuita ili tuwe baraka kwa wengine,
katika hali yoyote ile tunaweza kumtumikia Mungu au tunamtumikia Mungu, popote
tulipo sisi ni mabalozi wa Yesu 2Wakorintho 5:20 “Basi
tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu;
twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.”
Mathayo 28:18-20
“Yesu akaja kwao, akasema nao,
akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni,
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana,
na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na
tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
Matendo 1:8
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha
kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
1Nyakati 16:24
“Wahubirini mataifa habari za utukufu
wake, Na watu wote habari za maajabu yake.”
Yohana 20:21
“Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe
kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.”
Warumi 10:13-15
“kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la
Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye
wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa?
Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”
Isaya 52:7
“Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima
Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema
ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!”
Marko 16:15
“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni
mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.”
Yeremia 1:7-8
“Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi
ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila
neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe
nikuokoe, asema Bwana.”
Isaya 6:8
“Kisha nikaisikia sauti ya Bwana,
akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo
niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.”
2Timotheo 2:2
“Na mambo yale uliyoyasikia kwangu
mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa
kuwafundisha na wengine.”
Matendo 13:47
“Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na
Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.”
Mathayo 24:14
“Tena habari njema ya ufalme
itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo
ule mwisho utakapokuja.”
SWALI KWA KANISA LAKO
Ø
Je injili inahubiriwa ?
Ø
Je ni kanisa ambalo watu wanaamini katika
wokovu
Ø
Biblia inatambuliwa kama mamlaka ya mwisho na
neno la Mungu?
Ø
Waamini au washirika wanajazwa Roho
Mtakatifu?
Ø
Je mnatazamia kurudi kwa Yesu Kristo mara ya
Pili?
Ø
Je Kanisa linapaleka wamishionari?
Ø
Je wewe mwenyewe unajitathimini vipi?
RAMANI YA UMISHENI
Matendo 1:8
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho
Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi
wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
YERUSALEM
-
Kuimarisha kanisa la mahali pamoja, kanisa
litakaa katika mafundisho, watu watashuhudiwa, watu wataokoka na kubatizwa,
watu watazaliana watafundishwa chini ya walimu na wachungaji ili waweze
kuimarika na watamuomba Roho Mtakatifu kulizidisha kila wakati kwa idadi ya
watu wanaookolewa, ukuaji kibailojia, kiidadi na kiroho
-
Matendo 2:41-42
“Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku
ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la
mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.”
-
Matendo
5:28 “akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu,
msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho
yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.”
-
Matendo
2:47 “wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote.
Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”
YUDEA
-
Kuhubiri nje ya kanisa la mahali pamoja
-
Kufungua matawi katika maeneo mengine
-
kupanda kanisa jipya
-
Kuwafikiwa watu wa tamaduni tofauti kidogo mfano
Kenya na Tanzania
-
Kuwapelekea wachungaji na walimu kuwahudumia
-
Matendo
8:4 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na
huko wakilihubiri neno.”
SAMARIA NA HATA MWISHO WA NCHI
-
Hapa ndio Umisheni wenyewe
-
Hapa ni kuwafikiwa watu wa tamaduni tofauti
-
Hapa ni kuwafikia watu wa mabara tofauti
-
Kuwafikiwa watu wa dunia nzima
-
Kuwafikiwa watu wa Asia, watu wa Afrika, Ulaya
na America na sehemu zote duniani
Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni