Mstari wa Msingi: Warumi 16:19 “Maana utii wenu umewafikilia watu wote;
basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika
mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.”
Ni lazima watoto walelelwe katika njia iwapasayo kabla mioyo yao haijawa zege iliyokauka na Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Utangulizi.
Ni muhimu kufahamu kuwa tunaishi
katika nyakati za mwisho zaidi na katika nyakati hizi nza mwisho Shetani
amekusudia kuharibu kanisa na kuiharibu jamii kupitia mmomonyoko wa maadili, na
ili aweze kufanikiwa kuharibu jamii anaweza kupata mafanikio makubwa kama
atakusudia kuwaharibu watoto ambao ndio kanisa na taifa la kizazi kijacho.
Kwa muda mrefu katika jamii ya
wasomi wa Kikristo kumekuwako na mijadala mikubwa miwili, mmoja ni msimamo
mkali unaolenga kuwa watoto ni lazima wafundishwe njia za Mungu mapema kabisa
katika maisha yao ili neno la Mungu likae ndani yao kwa iwngi kabla ya kuwa
watu wazima, lakini wazazi wengine na baadhi ya wanatheolojia wa kikristo
wanapinga kwa madai kuwa watoto hawawezi kuzaliwa na Ukristo wetu hivyo ni
muhimu wakaachwa na kujifunza mema na mabaya na kuijua Dunia kisha wakutane na
Mungu wao binafsi ndipo watakuwa na imani ya kweli, hata hivyo wazo hili la
pili ingawa linaweza kuonekana kama lenye hekima ni wazo baya zaidi kupata
kutokea duniani kwani liko kinyume na maandiko.
Biblia imeagiza kuwa ni lazima
watoto waelekezwe na kukua katika njia ya Mungu,
Kumbukumbu la torati 6:1-9 “Na hii
ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu wenu, mfundishwe,
mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; upate kumcha Bwana,
Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na
mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda;
upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako,
alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu
wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na
kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo,
yatakuwa katika moyo wako; nawe
uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na
utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati
ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango
yako.”
Biblia inaonyesha kuwa watoto
wakifundishwa vema njia ya Mungu hawataiacha hata watakapokuwa watu wazima
Mithali 22:6 “Mlee
mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”
Kutokuwalea watoto katika njia
iliyonyooka na kosa kubwa sana katika mapenzi ya Mungu Nyakati za Biblia
hususani wakati wa waamuzi kulitokea kizazi ambacho hakimjua Mungu wala njia
zake na hivyo waliishi kwa kutenda kila aina ya uovu
Waamuzi 2:10-11 “Tena watu wote wa
kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine
nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa
ameitenda kwa ajili ya Israeli. Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu
mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.”
Kwa sababu hiyo ni
jukumu la Wachungaji walimu na wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanaikulia njia
ya Mungu, na hawajifunzi uovu kutoka kwetu, na kuhakikisha kuwa tunawasaidia
kwa namna yoyote ile kukua kiakili, kimwili, kitaaluma na kiroho, huiku wakiwa
wenye nidhamu thabiti, Yesu alitangaza hukumu kubwa sana kwa watu
watakaowakwaza watoto na kuwafanya wakengeuke alisema yafaa wafungiwe jiwe
kubwa la kusagia na kutoswa katika kilindi cha bahari
Mathayo 18:6 “bali atakayemkosesha
mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la
kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.”
Mungu alimchagua Ibrahimu na
kumfanya kuwa Baraka kubwa sana Duniani lakini sababu kuu ya kumchagua Ibrahimu
Mungu anaieleza katika
Mwanzo 18:17-19
“BWANA akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo
nilifanyalo, akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa
yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na
nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili
kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.”
Kumbe ni kwa kusudi hili katika
andiko la Msingi Paulo mtume anatoa wito kwa kanisa la rumi kuwa na hekima
Yaani ujuzi wa kutosha katika mambo mema na kuwa wajinga katika mambo mabaya
neno kuwa wajinga katika biblia ya kiyunani linasomeka kama “AKERAIOS” Ambalo maana yake kuwa
incorruptible au kuwa Innocent, kwa
Kiswahili ni kuwa safi kabisa, wasiochanganywa, kutokuujua kabisa uovu wala
mwenendo wa Dunia, Biblia inatumia neno hilo pia katika
1Wakoritho 14:20 “Ndugu zangu, msiwe
watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali
katika akili zenu mkawe watu wazima.”
Unaweza kuona kwa msingi huo basi
Msingi wa kibiblia haufudnishi kuwaachia huru watoto, Bibloia inataka watoto
wabanwe katika sheria, waelekezwe nini cha kufanya na nini sio cha kufanya ,
haiwezekani watoto waachiwe kufanya lolote wanalojisikia kilifanya,
tusiwaruhusu kukaa katika njia ya shetani eti ili nao wakutane na neema ya
Mungu binafsi, ni lazima sisi tutumike kama chombo cha kuwanyoosha wakae katika
njia iliyonyooka, kujua maovu kuna mateso mengi sana ni waarabu na wayahudi tu
Duniani ndio wanaojua kuwalea watoto wao na kuwafanya wafuate imani zao kwa
uthabiti na kuwarithisha kama Ibrahimu, sehemu nyingi duniani na wakristo
wameshindwa kabisa kufanya wajibu huu
Hatupaswi kuwaacha watoto
wakajikulia tu kana kwamba kuna bahati nasibu ya kukua kwao, lazima tuhusike
katika kuwajenga na kuwalea watu wengi sana wanatumia mamilioni ya fedha
duniani kusomesha wachungaji, walimu madaktari na wataalamu mbalimbali na hata
makanisani lakini hakuna watu wanaofanya utafiti wa kutosha kuhusu watoto zaidi
tu tunasoma kina “Maria Montessori”
mwana falsafa wa zamani tu wakizungumza kuhusu watoto na namna yao ya
kujifunza, Zamani kulikuwa na kozi katika chuo cha biblia Inaitwa “Children Ministry” mimi niliisoma
katika ngazi ya Diploma zamani sijui kama mkozi hii siku hizi ipo lakini kanisa
limepuuza kabisa huduma ya watoto na ukiwauliza Wachungaji wengi watakuambia
kuwa tatizo watoto hawana mafungu ya kumi,
Ni lazima tufanye kila jitihada
ya kuwalinda watoto wetu katika udanganyifu wa dhambi na maasi ili kuwalinda
watoto wetu na uovu duniani Roho mtakatifu anataka wawe wajinga katika mambo ya
uovu
Tukiwaachia watoto wetu waijue
dunia watabikiriwa kama Dinah binti Lea wa Yakobo Mwanzo 34:1-2, 7 Wana wa Yakobo waliposikia walikasirika sana na
walisikitika waliona kuwa dada yao amefanyiwa mambo ya kipumbavu kwa nini hii
ni kwa sababu Yakobo alikaa na watu wabaya karibu nao ni lazima tuwalinde
watoto wetu, Naamini ya kuwa hukuchagua mahali hapa kwa bahati mbaya, wazazi
waliochagua mahali hapa wanajua kuwa watoto wao wako katika mikono salama na
hatutaruhusu mambo ya kipumbavu yatokee Katika jina la Yesu amen
“Songs “Bless the Lord” Rebbeca Malope”
Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa Wajenzi mwenye hekima