Waamuzi 4:1-9 “Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu
tena mbele za macho ya Bwana. Bwana akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini,
mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika
Haroshethi wa Mataifa, alikuwa amiri wa jeshi lake. Wana wa Israeli wakamlilia
Bwana; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea
wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini. Basi Debora, nabii mke, mkewe
Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Naye alikaa chini ya
mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya
Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue. Huyo akatuma mtu akamwita
Baraka wa Abinoamu toka Kedesh-Naftali, akamwambia, Je! Bwana, Mungu wa
Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawavute kwako, huko katika mlima wa
Tabori, watu elfu kumi wa wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni? Nami
nitakuvutia Sisera, amiri wa jeshi lake Yabini, hata mto wa Kishoni, pamoja na
magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako. Baraka
akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi
pamoja nami, mimi siendi. Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini
safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana Bwana atamwuza Sisera
katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka
Kedeshi.”
Utangulizi:-
Ni muhimu kufahamu kuwa katika
kanuni za Mungu, Mungu hufanya kazi kwa njia tofauti na njia za wanadamu, na
kwa mawazo tofauti na mawazo ya wanadamu, na hata kwa uzoefu tofauti na uzoefu
wa wanadamu, Biblia inaonyesha hekima hii ya Mungu na namna yake katika utendaji
nwake wa kazi ona:-
1Wakoritho 1:26-29 “Maana, ndugu zangu,
angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi
wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo
mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu
vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya
dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile
vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu”
Katika kitabu cha waamuzi Yaeli
ni mojawapo ya mfano wa watu dhaifu ambao MUngu aliweza kuwatumia kuleta
ushindi mkubwa kwa wana wa Israel waliokuwa wakionewa na wakanaani chini ya
Mfalme Yabin kwa zaidi ya miaka 20, wanawake kumbuka katika jamii ya kiyahudi
walikuwa hawapewi umuhimu mkubwa sana waoa hata kuhesabiwa walikuwa
hawahesabiki, lakini tunaona Mungu akiwatumia baadhi yao kwa utukufu wake.
Yaeli alikuwa moja ya wanawake
ambao Biblia haijawahi kuzungumza habari zao kwa undani, tunajua tu kuwa alikuwa
miongoni mwa ma bedui walioishi jangwani na aliyeolewa katika Familia ya Heber
mkenizi au mkeni. Mwanamke huyu ndiye aliyetumiwa kukamilisha ushindi wakati wa
waamuzi Debora na Baraka.
Israel katika Shida na dhiki.
Ushindi dhidi ya wakanaani
ulikuja wakati wana wa Israel wamechoswa na mateso yaliyokuwa yakiwakabili
kutoka kwa mfalme wa kanaani Yabin mfalme huyu alikuwa anatawala kanaani na
Biblia inasema kuwa alikuwa na Mkuu wa majeshi (Amiri wa majeshi) aliyejulikana
kama Sisera, hawa walikuwa na jeshi kali sana Biblia inaeleza kuwa alikuwa na
Magari ya chuma mia tisa, na aliweza
kuwaonea sana Israel tena biblia inasema aliwaonea kwa nguvu muda wa miaka 20,
halki hii ilikuwa ngumu, Mungu alikuwa kama amewauza yaani ameruhusu wateseke
kutokana na kumsahau yeye ingawa yeye hangeliweza kulisahahu Agano lake, hali
hii ilipelekea wana wa Israel kulia na kuuugua kwa sababu ya msiba ule wa
mateso.
Israel walipolia kwaajili ya
mateso yale Maandiko yanaeleza kuwa alikuwepo nabii mke jina lake Deborah
aliyekuwa akiwaamua Israel, yeye alijaa Roho na kuambiwa na Bwana amuite mtu
anaitwa Baraka ambaye Mungu alimchagua aweze kuyakabili majeshi ya Yabin na
kamanda wake Sisera, aliyekuwa Hodari na katili sana na aliyewatesa sana wana
wa Israel
Hata hivyo katika namna ya kushangaza
Baraka alisisitiza kuwa hawezi kwenda bila Deborah kumbuka Debora alikuwa
mwanamke Waamuzi 4:6-9 “Huyo akatuma mtu
akamwita Baraka wa Abinoamu toka Kedesh-Naftali, akamwambia, Je! Bwana, Mungu
wa Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawavute kwako, huko katika mlima
wa Tabori, watu elfu kumi wa wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni? Nami
nitakuvutia Sisera, amiri wa jeshi lake Yabini, hata mto wa Kishoni, pamoja na
magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako. Baraka
akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi
pamoja nami, mimi siendi. Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini
safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana Bwana atamwuza Sisera
katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka
Kedeshi”.
Bwana atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke!
Debora alikubali ombi la Baraka
lakini alimueleza wazi kuwa kutokana na ktaka kwenda vitani na mwanamke ili
halinyeye ni mwanaume basi Sisera atauawa na mwanmke na mwanamke huyo ndiye Yael, Majeshi ya
Baraka yalijipanga huku Debora nabii akiwa pamoja naye na bwana alianza
kuyafadhaisha majeshi ya Sisera na kuanza kuwapiga vibaya jambo lililopelekea
Sisera kukimbia ili kuayasalimisha maisha yake, alikimbilia kwa Yael ambaye
nyumba yake iliuwa na mani nay eye hivyo alifikiri kuwa atasalimika alifunikwa
na nguo nzito ili kujipumzisha na alipoomba maji ya kunywa alipewa maziwa,
maziwa huwa yana tabia ya kuleta usingizi mzito sana na yael alipoona Sisera
amelala alichukua mambo na nyundo na kuipigilia kichwani mpaka ardhini na
kumuua.
Waamuzi 4:21-24 “Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika
nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji
chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito
ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa. Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera;
Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonyesha yule mtu
unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na
hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake.
Basi hivyo Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani mbele ya wana wa
Israeli siku hiyo. Mkono wa wana wa Israeli ukazidi kupata nguvu juu ya Yabini,
mfalme wa Kanaani, hata walipokuwa wamemwangamiza Yabini, mfalme wa Kanaani.”
Njia za Mungu sio njia zetu, ni
muhimu kufahamu kuwa Nabii katika Biblia anasimama kwa niaba ya watu wa Mungu
na Mwanamke anasimama kwa niaba ya kanisa, Kanisa likiomba ni lazima ifahamike
kuwa kuna nguvu kubwa sana ya ajabu iliyofichika katika kanisa lake kila mtu
anaweza kujipatia ushindi mkubwa kupitia Yesu Kristo, yeye hataweza kulisahahu agano
lake alilolifanya nasi pale msalabani atatupa ushindi kwa dhahiri,
·
Ushindi wako hautakuja katika njia ya kawaida
unayoidhani Mungu anakwenda kufanya jambo jipya litakalokushangaza
·
Mungu atatumia ulicho nacho katika mkono wako
kukupa ushindi nalitumia nyundo na mambo tu kumaliza tatizo kubwa lililodumu
kwa miaka 20
·
Haijalishi kuwa tatizo lako lilikuwa baya au ni
baya kiasi gani na limekugharimu miaka mingapi leo kwa neno la kinabii kama la
Debora ninatamka muujiza na uponyaji kwaajili yako katika jina la Yesu
·
Haijalishi adui yako ana nguvu kiasi gani Sisera
alikuwa na magari ya chuma mia tisa lakini alikimbia mbele ya upanga wa Baraka
nataka nikuambie na nkukutamkia kinabii leo kuwa kwa jina la Yesu Kristo aliye
hai tatizo lako lazima likimbie mbele yako bila kujali kuwa lina nguvu kiasi
gani
·
Haijalishi kuwa hujajibiwa mamombi kwa muda gani
lakini leo natabiri kwako katika jina la Yesu Kristo Israel waliteseka kwa
miaka 20 lakini ka neno la Nabii Debora na na upanga wa Baraka siku moja tu
ilileta ushindi mkubwa katika maisha ya Israel na kuwafanya salama leo
ninatangaza usalama wako natangaza kwa neno la kinabii na uweza wa jina la Yesu
kuwa utajibiwa maombi yako
·
Mungu anakwenda kuzigeuza fadhaa zako kuwa
furaha, adui zako kuwa watumwa wako, watesi wako kuwa wakimbizi, waoneziwako
kuwa waonewa, waliokutisha kuwa waoga, natangaza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya
nguvu za giza, dhidi ya majeshi yanpopi wabaya katika ulimwengu wa Roho kwa
jina laYesu Kristo na kwa njia ya imani natanmka ushindi dhidi ya msomaji wangu
namsikilizaji wangu awekwe huru na amani idumu kwake
·
Hajalishi kuwa kesi yako imesumbua kwa miaka
mingapi, wanaokudai hawajarudisha madeni, waliokudhulumu na kukuonea
Nasimamisha mwamuzi leo, tunaye muamuzi leo,. Muamuzi wetu leo sio Baraka wala
sio Debora wala sio Yael Yuko muamuzi
mwenye haki aliyetupa ushindi kwa njia ya Msalaba huyu ni mwanaume
anaitwa Yesu, na akuweke huru leo na akutetee na akutegemeze na akukomboe na
akupe furaha na akufungue na akukumbuke na akutazame na akusikie na akufariji
na akuinue dhidi ya udhalimu wa kila aina katika masiha yako!
·
Yail hakutumia nguvu hakuwa na uzoefu wa vita
hakwenda hata vitani hajui hata kupigana lakini ndiye aliyeu Shujaa aliyesumbua
Israel kwa miaka 20, Ndugu zangu neema ya Mungu ikiwa juu yako hakuna
kitakachoweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako!
Ramakarashat! Rimasakarutarama!
sakatarino, trembeshederengendebe! rimosakarapati yetereseka yatoroseka
yakarakata yatoromoskomoli, yenderebisakuramato rimamama sakarenderebe katabash
karabakat yerekerebeshe masokolipatei birikuromoto sakarambat.
Nakuombea neema ya Mungu kila
amwaminieye hatatahayarika atakupa
kushinda, na kukutetea na kukufungua uwe mtu wa kipekee mtu wa tofauti mtu wa
kushangaza na kwa njia laini bwana ana atende na kukutetea dhidi ya uonevu wa
kila namna katika jina la Yesu amen. Adui yako na auzwe kwenye mkono wa
mwanamke tu. Na aaaibike kwa namna ya ajabu katika Jina la Yesu, amen. Mungu
bhatafanya kwa sababu ya ujuzi wetu, uzoefu wetu, elimu yetu bali atafanya kwa
sababu ya neema siri ya ushindi wa kanisa ni neema sio mazoezi, sio nguvu, sio
uwezo ni neema yake neema yake na iwe juu yako kama ilivyokuwa kwa Yael
Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima.