Ni muhimu kufahamu kuwa nyakati
hizi tulizonazo ni nyakati za mwisho, Yeye ajaye anakuja wala hatakawia. Waebrania 10:37
“Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.”
Katika nyakati hizi ambazo maandiko yanaziita za hatari; ni muhimu kuwa na
ufahamu wa rohoni na kuwa na macho ya rohoni ili kwamba tuweze kujua majira na
nyakati na kujiandaa vema na kurudi kwa Bwana Yesu, na ili kwamba pia tusiwe
miongoni mwa hao wanaopotea.
Katika nyakati za kizazi cha leo
tumekuwa tukisikia sana neno “Demokrasia”
au utawala wa kidemokrasia na tumeona jinsi ambavyo kupitia utawala huu wa
kidemokrasia kumekuwepo na mwamko mkubwa sana wa watu kutaka kuwa na uhuru,
uhuru wa kuzungumza, uhuru wa kutoa au kupokea habari, uhuru wa kuchagua lolote
mtu atakalo, uhuru wa kuamua, kumuoa au kuolewa na yeyote umtakaye uhuru wa
kuabudu,Usawa wa kijinsia, vurugu na ugaidi pamoja na Haki za watoto, Hakiza
Binadamu na aina nyingine za usawa na maswala yanayofanana na hayo, Yote yakiwa
yamekuja na kifurushi hiki kiitwacho demokrasia kwa nini neno demokrasia
linapata nguvu sana katika nyakati zetu, na linaonekana kuwa na washabiki wengi
sana duniani? Leo tutachukua Muda kulitafakari neno hilo chini ya somo hili
Muhimu Neno la Mungu na utawala wa kidemokrasia, na tutajifunza somo hili kwa
kuzingatia vipengele muhimu vifuatavyo:-
·
Maana ya neno Demokrasia
·
Mifumo ya utawala wa dunia na serikali za
wanadamu duniani
·
Neno la Mungu na utawala wa kidemokrasia
·
Hatari ya uhuru uliokithiri chini ya mfumo wa
Kidemokrasia
Maana ya neno
Demokrasia.
Neno Demokrasi limetokana na neno
la kiyunani “DemosKratein” ambalo ni
muunganiko wa maneno mawili ya kiyunani Demos
– ambalo maana yake ni watu na Kratein- ambalo maana yake kutawala au utawala, Kwa msingi huo neno Demokrasia
maana yke ni Utawala unaotokana na nguvu ya watu au nguvu ya umma, Demokrasia
ni mfumo wa siasa za dunia ambao unatoa mamlaka makubwa kwa watu kuamua, nani
awaongoze, waongozwe vipi, wawajibike vipi, na kadhalika, Katika tawala za
kidemokrasia viongozi nyeti kabisa huchaguliwa na watu, hivyo watu ndio wenye
nguvu kuu ya maamuzi katika mifumo ya tawala za kidemokrasia, sio hivyo tu watu
ndio wenye maamuzi ya kumkataa kiongozi na hata kumuwajibisha, Mfumo huu wa utawala umepata nguvu kubwa sana
katika nyakati hizi za mwisho wa dunia kuliko nyakati za tawala nyingine za
kihistoria ambazo zimewahi kuitawala dunia, Katika maswala ya kiimani mfumo huu
ni hatari zaidi kwa maisha ya kiroho na kanisa kuliko tunavyofikiri ingawa unaonekana
kuwa unakubalika zaidi katika maisha ya wanadamu na unaungwa mkono zaidi
duniani, na wakati mwingine tunaweza kusema kuwa una nguvu na umeangusha aina
nyingine za tawala kwa vile zinaonekana kuwa za kizamani. Kabla hatujaona kwa
undani hatari zake ni vema tukaangalia namna maandiko yalivyoweka wazi aina za
tawala za serikali za wanadamu zilizotawala Dunia, kabla haujaa utawala wa
Ufalme wa Mungu.
Mifumo ya utawala wa dunia na serikali za wanadamu duniani
Ni muhimu kufahamu kuwa mfumo wa
utawala wa kidemokrasia na tawala nyingine duniani, sio kitu kigeni kwa
wataalamu wa maandiko, Mungu ndiye ayatetawala Daniel 4:17 “Hukumu hii imekuja kwa agizo
la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua
ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye,
tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.” Kwa kuwa Mungu ndiye
anayetawala ulimwengu na ndiye anayeruhusu nani atawale na aina za utawala,
Mungu anajua yote na hivyo aliwafunulia watumishi wake Tangu nyakati za
Nebukadneza na Daniel ili kutujulisha majira na nyakati tangu wakati huo hata
ufalme wa Mungu utakapotawala duniani, Unabii kuhusu mifumo ya serikali za
dunia uko katika maono na ndoto aliyoota Nebukadreza na ikatafasiriwa na nabii
Daniel kwa ajili ya vizazi vyote ili tuweze kuwa na akili ya kile
kinachoendelea katika nyakati zetu, Unabii huu ulionyeshwa kwa njia ya Sanamu
ya ajabu ambayo tutaiangalia na kupata uchanganuzi wake kama ifuatavyo:-
Daniel 2:1- 49. “Hata katika mwaka wa pili
wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake
ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga,
na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi
wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho
yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake. Ndipo hao Wakaldayo wakamwambia
mfalme, kwa lugha ya Kiaramu, Ee Mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi
wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu, akawaambia Wakaldayo, Neno lenyewe
limeniondoka; msiponijulisha ile ndoto na tafsiri yake, mtakatwa vipande
vipande, na nyumba zenu zitafanywa jaa. Bali kama mkinionyesha ile ndoto na
tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionyesheni
ile ndoto na tafsiri yake. Wakajibu mara ya pili, wakasema, Mfalme na atuambie
sisi watumishi wake ile ndoto, nasi tutamwonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu,
akasema, Najua hakika ya kuwa mnataka kupata nafasi, kwa sababu mmeona ya kuwa
lile neno lenyewe limeniondoka. Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja
tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele
yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya
kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake. Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme,
wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana
hapana mfalme, wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kama hili kwa mganga,
wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo. Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme,
wala hapana mwingine awezaye kumwonyesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na
kikao pamoja na wenye mwili. Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona
hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli. Basi ile
amri ikatangazwa, na hao wenye hekima walikuwa karibu na kuuawa; watu
wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauawe. Ndipo Danieli kwa busara na hadhari
akamjibu Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, aliyekuwa ametoka ili kuwaua wenye
hekima wa Babeli; alijibu, akamwambia Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, Mbona
amri hii ya mfalme ina ukali namna hii? Ndipo Arioko akamwarifu Danieli habari
ile. Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha
mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari
kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake;
ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili
kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo
Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi
Mungu wa mbinguni. Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele
na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili majira na nyakati;
huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa
wenye ufahamu maarifa; yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo
gizani, na nuru hukaa kwake. Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu,
uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana
umetujulisha neno lile la mfalme. Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa
na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi,
Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami
nitamwonyesha mfalme ile tafsiri. Ndipo Arioko akamwingiza Danieli mbele ya
mfalme kwa haraka, akamwambia hivi, Nimemwona mtu wa hao wana wa Yuda
waliohamishwa, atakayemjulisha mfalme ile tafsiri. Mfalme akajibu, akamwambia
Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto
niliyoiona, na tafsiri yake. Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri
aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala
waganga, wala wanajimu; lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye
amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako,
na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi; Wewe, Ee mfalme,
mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu;
na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa. Lakini mimi,
sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu
wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua
mawazo ya moyo wako. Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana.
Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele
yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa
ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na
viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu
ya chuma na nusu ya udongo. Nawe
ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga
sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.
Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu,
vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea
wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe
lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote. Hii ndiyo
ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. Wewe, Ee mfalme, u
mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na
utukufu; na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani
amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile
cha dhahabu. Na baada ya zamani zako
utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa
shaba, utakaoitawala dunia yote. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa
chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma
kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. Na kama vile
ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi,
na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake
zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na
udongo wa matope. Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo,
kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika. Na
kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope,
watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama
vile chuma kisivyoshikamana na udongo. Na katika siku za wafalme hao Mungu wa
mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine
hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na
kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe
lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma,
na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu
amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na
tafsiri yake ni thabiti. Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi,
akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba. Mfalme
akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana
wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.
Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa
mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye
hekima wa Babeli. Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na
Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo
Danieli alikuwa akiketi katika lango la mfalme.”
Ukiangalia kwa undani kuhusu
tafasiri ya Daniel kutokana na ndoto aliyoiiota Nebukadreza ambayo ilikuwa
ikionyesha dalili za kuja kwa ufalme wa Mungu tangu wakati wa utawala wa
nebukadreza unabii huu unatuonyesha mifumo ya serikali za dunia kabla haijaja
ile serikali ua utawala wa Masihi, Mungu ametaka kutujua sisi kuhusu wakati
ujao, kwa kuchambua sasa tawala hizi ndoto hii ilikuwa na ujumbe ufuatao
1.
Kichwa
cha Dhahabu – kiliwakilisha utawala wa Babeli uliokuwa chini ya Nebukadneza
Nebuchadnezzar
alitawala kati ya mwaka wa 605-562 hivi kabla ya Kristo alikuwa ni mtawala
mkubwa sana wa ufalme katika ufalme wa kabila za Wakaldayo, aliyeshinda falme
kuu za Asia na asia ya kusini mashariki na utawala wa Dunia ya wakati huo,
alijulikana kwa uhodari mkubwa wa ujenzi kwani alijenga miji mikubwa sana
ukiwemo mji wa Babeli ambao ulikuwa wa kifahari sana, alikuwa ni mtawala mwenye
nguvu aliyeruhusiwa na Mungu kuharibu Yerusalem na kuchukua mateka Wayahudi na
hata kuwapeleka utumwani na kuwafanya watumwa wake, Utawala wake ulikuwa
unawakilisha mfumo wa kidikteta kuitawala dunia ya wakati huo, Yaani wafalme au
mfalme alikuwa na nguvu kuliko kitu chochote, mtu yoyote na sheria yoyote
alichokiamuru yeye ndio kilikuwa jambo la mwisho na hakuna wa kumpinga Dunia ya
wakati wake iliongozwa na Mfumo wa utawala wa Kidikteta
Utawala wa
kidikteta ni mfumo wa utawala ambao mtawala anatumia nguvu ya dola kutawala,
mamlaka nguvu na utawala anakuwa navyo yeye na huwezi kumpinga, Mtawala
anajifikiri kuwa ana mamlaka yote juu ya kila kitu hata maisha ya watu,
kumpinga kwako kungeweza kuhatarisha maisha, watu walipaswa kumuogopa na kumtii
mtawala katika mazingira yoyote yale, utawala huu uliwakilisha aina za serikali
za zamani za kifalme na watemi, utawala wakeulidumu kwa miaka kama 70 hivi na
baadaye mifumo ya serikali za aina hii ilikuwepo duniani na kuondoka
kidogokidogo.
2.
Kifua
cha Fedha – kiliwakilisha utawala wa uamedi
na uajemi utawala wa sheria
Baada ya anguko
la utawala wa kidikteta uliowakilisha na Nebukadneza mfumo wa utawala na
serikali uliofuata uliigawanya babeli vipande viwili na kukaweko utawala wa
waamedi na waajemi ambazo ni sawa na Iran na Iraq ya leo, utawala huu ulidumu
kwa miaka 206 (536KK-330 KK) Utawala huu unawakilisha na madini ya Fedha maana
yake hakukuwa bora sana ukilinganishwa na Madini ya dhahabu, utawala huu
ulikuwa wa kisheria na hakuna aliyekuwa juu ya sheria utawala huu, Sheria
iliheshimika zaidi na hata wafalme walitakiwa kuzitii, sheria iliheshimika sana
ikiwekwa imewekwa na kila mtu alipaswa kuitii ni mara chache sana mfalme
aliweza kutangua lakini hata hivyo wakati huu Hakuna mtu aliyekuwa juu ya
sheria, hii inawakilisha mfumo wa serikali zilizofuata duniani baada ya ule wa
kidikteta.
3. Tumbo la Shaba – linawakilisha utawala ugiriki
au uyunani chini ya Aleksandria
Utawala wa
kiyunani au kigiriki unawakilishwa na madini ya shaba na ni sehemu ya tumbo,
ulikuwa ni utawala wa kijeshi chini ya mfalme Alexander mkuu, utawala hu wa
kiyunani ulidumu kwa miaka 300 (330KK-30KK), kinabii tawala za kijeshi
zilifanana kiasi na tawala za kidikteta, shaba inafanana na dhahabu kwa kiwango
fulani lakini si bora wala ya thamani kama Dhahabu na fredha huu ni mfumo wa
nyakati za serikali za kijeshi zilizotawala sehemu mbalimbali duniani, Nguvu
yako yamkijeshi ndiyo ingekuwezesha kuitawala Dunia.
4.
Miguu
ya Chuma –Inawakilisha utawala wa warumi chini ya mataifa ya ulaya. Utawala wa
kikoloni.
Aina hii ya
utawala ilianzia huko ulaya ambapo wao hawakuwa wanachukua watu na kuwapeleka
utumwani lakini badala yake waliwatawala watu hukohuko katika inchi zao.
Kulikuwa na mabadiliko mengi sana nyakati za utawala huu, Utawala wa kikoloni
ni utawala ambapo taifa kubwa na lenye nguvu Super power Nations, linaondoka na
kwenda kuwatawala wengine kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kitamaduni.
Utawala wa chuma
unawakilisha utawala wa Kirumi ambao ulikuwa na unaowakilishwa na miguu ya chuma
katika sanamu kabla haujagawanyika miguu miwili inawakilisha kugawanyika katika
maeneo makuu mawili, mguu mmoja unawakilisha ubepari Magharibi chini ya ushawishi wa papa na kanisa lake na mguu mwingine unawakilisha Ujamaa mashariki, chini ya utawala au
ushawishi wa kiyunani Kanisa la Othodox,
Ukoloni ilikuwa ni sehemu ya utawala wa mataifa yote yanayowakilishwa na mguu
wa kulia na wa kushoto, yaani magharibi na mashariki mpaka wakati wa mataifa
yote kuwa huru na kujitegemea,
Kuchanua kwa mtini
na miti mingine kunawakilishwa kinabii na swala zima la kupata uhuru kwa
mataifa yaliyokuwa chini ya ukoloni Kama alivyoeleza Yesu katika unabii wake Luka 21:29-33 “Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti
mingine yote. Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba
majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo
yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Amin,
nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie..”
Tawala kubwa ni
tawala ambazo zilipanua utawala wake mpaka katika mataifa mengine, tawala hizi
kubwa zilidumu kwa karne nyingi na zilikuwa na hatua za maendeleo
zilizowafuatiwa nazo, Ukoloni na ubepari
uliletwa na tawala hizi kubwa, Twala kuu zilidumu mpaka mwaka wa 30 KK – 1453
BK, Mtawala mkuu wa kwanza aliku kaisari Augusto. Yesu Kristo alizaliwa wakati
wa mtawala huyu, watawala wengi waliofanikiwa walitawala wakati wa utawala wa
rumi na waliwatesa sana wakristo, Mshauri wa Mtawala aliyeitwa Pliny na barua
yake aliyoiandika kumshawishi Mtawala Trajan katika mwaka 112 jinsi ya
kuwashughulikia wakristo ilikuwa na mchango mkubwa sana katika swala hili,
ilipofika mwaka 117 wakati utawala wa Rumi ukiwa bado uko chini ya Trajan
Ukristo ulikuwa na kuwa dini kubwa sana ulimwenguni yenye ushawishi mkubwa
katika uatwala wa Rumi, Mtawala wa rumi alianzisha ibada za miungu ya Rumi na
sanamu zake
Utawala huu
uliweka sheria zenye lengo la kukandamiza na kutiisha, ili kuendeleza ulimwengu
na jamii za ulimwengu na pia walianzisha maswala ya kuhamisha watu na maswala
ya kutokuwatendea watu haki kama sehemu ya swala hilo, Baadaye swala hili
linasemekana ndilo lililochochea kuweko kwa ukoloni na utumwa, Wanadamu waliaza
kufanywa watumwa na kuwa kama bidhaa, wanadamu wengine wakiwanunua na wengine
wakiwamiliki bila wao kuwa na uchaguzi wa nini cha kufanya na kuwatumikia
mabwana zao, Mswada wa kukomesha
biashara ya utumwa ulipitishwa mwaka 1807 na Bunge la Waingereza, Lakini
huko Zanzibar Afrika Mashariki ambako
ilikuwa bandari na soko kuu la utumwa na
chini ya utawala wa Waarabu wa Oman biashara iliendelea mpaka karne ya
19, na hii inafunua jinsi ambavyo wanadamu ni waovu na wabaya pasipo na Mungu.
Ubepari ambao
ulitawala magharibi unaweza kuelezewa kuwa ni mfumo wa kisiasa wenye misingi ya
haki za binadamu za mtu au shirika kuwa na uwezo wa kimiliki mali.
Ukomonisti ambao
ulitawala Mashariki ni wazo kutoka ugiriki ya kale, lililoelezewa na Plato kama
wazo lenye daraja za ushirikiano na umiliki wa pamoja wa mali, hiki ndicho
kilichikuja kuzaa ukomonisti, na usoshalisti, lengo likiwa ni kuwa na serikali
ambazo watu wake wanashirikiana mali na ikawa kinyume na ubepari, Katika
nyakati hizi baada ya kuchanua kwa Mtini yaani Israel na mataifa mengine yaani
kupata uhuru athari za tawala hizi zilisalia katika mataifa mbalimbali hata leo
na umeishababisha dunia kutokuwa na mshikamano hata sasa
5.
Chuma
na Udongo.Inawakilisha mfumo wa serikali za Kidemokrasia ukoloni mambo leo na
sharia Mchanganyiko wa mambo.
Inawakilisha
tawala za kidemokrasia zinazoendelea lakini dhaifu, kwa mujibu wa unabii hii ni
aina ya mwisho wa tawala za kibinadamu duniani na ni wa muda mfupi, utakuwa na
uhuru mkubwa wa kupita kawaida kwa dhambi na uovu ambao utaenea dunaini,
Uislamu udongo ukiwa na mgogoro mkubwa na mifumo ya serikali hizo kwa kuwa
watafanya kazi ya kutafuta kuwa na mfumo waserikali zinazotaka kuwa na nguvu
dhidi ya Kanisa. Uislamu umekuwa ukiendeleza chuki za wazi dhidi ya wayahudi na
kanisa na kuandaa njia ya ujio wa Mpinga
Kristo, Chuma kinawakilisha tawala ambazo zina ushawishi wa Kikristo na udongo
unawakilisha tawala zenye ushawishi wa kiislamu chini ya utawala wa Sharia, mtu
anaweza asikubaliane na tafasiri hii lakini angalia kile kinachoendelea sasa
duniani katika jamii yatu ya sasa utaelewa. Kuwa unabii wa maandiko unatimizwa. Tawala za Chuma na
Udongo haziwezi kushikamana na udongo ni dhaifu, inawakilisha tawala za
Demokrasia na Sharia, kutokana na mkazo wa kukua kwa demokrasia na uhuru wa
watu kuwa na sauti duniani na uhuru wa kuabudu, kutatokea kutokuelewana kukubwa
sana katika jamii na mchanganyiko usioshikamana , huu utakuwa ni wakati wa
kilele cha uovu wa aina binadamu na serikali chafu sana kutokana na kivuli cha
Demokrasia kama tukakavyojadili kwa undani zaidi.
6.
Jiwe lisilochongwa
kwa mikono ya kibinadamu linawakilisha Ufalme wa Mungu chini ya Yesu Kristo
THEOCRACIA
huu ni utawala wa Mungu, Utawala ambao Yesu Kristo baada ya kurudi kwake mara ya pili
Duniani ataitawala dunia nzima, utakuwa utawala wa amani juu ya mataifa kwa
miaka 1000, Hili jiwe ni Yesu Kristo atakapokuja mara ya pili duniani, ambaye
atakomesha vita vya harmagedon, na
migogoro yote mikubwa duniani na kufikisha mwisho aina zote za serikali za
kibinadamu ambazo zinamalizikia na tawala za kidemokrasia, Atasitawisha amani
na ufalme wake kwa kuyashinda mataifa yatakayokusanyika kwaajili ya vita vya
Harmagedoni, Wayahudi na waisrael wote wakati huu watamkubali Yesu Kristo yeye
waliyemchoma kuwa Ndiye Masihi Mfalme wa wafalme. Utakuwa ni ufalme wa utulivu
na amani SHALOM au Irene itatawala Duniani. Huu ndio ufalme ambao Israel
wanautazamaia makao makuu ya utawala huu yatakuwa Israel na mji mkuu utakuwa
Yerusalem.
Neno la Mungu na utawala wa Kidemokrasi.
Historia inaonyesha kuwa kila
aina ya utawala na mifumo ya kiserikali ilikuwa na faida zake na hasara zake,
Mungu aliwaacha wanadamu wajitawale, baada ya kuwa wanadamu waliukataa utawala
wake na kutaka kuwa huru kufanya kila wanaliloiona kuwa jema machoni pao, Mara
kadhaa Mungu aliadhubu na kukemea wanadamu lakini walikuwa ni wenye shingo
Ngumu Mwanzo 6:3 “BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu
milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na
ishirini.”
Mungu aliona kuwa wanadamu
wamekuwa na desturi ya kukataa ufalme wake na utawala wake na kwa sababu hiyo
amewacha wafuate kila wanachikitaka, katika nyakati hizi za tawala za Kidemokrasia
maovu yataongezeka mno kwa sababu madai makuu ya wanadamu yatakuwa kwenye uhuru
wa kujifanyia kila wanaloliona jema machoni pao, wanadamu watakuwa wamechoka
kuingiliwa na kila mtu ataona anahitaji
kuliamulia anachoweza kujiamulia na kwa sababu ya kukataa kuwa na Mungu, Mungu
atawaacha wanadamu wafuate njia zao za uharibifu na kujiletea hukumu
Warumi 1:18-25 “Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa
kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana
Mungu aliwadhihirishia.Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa
ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele
na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu
hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi
wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima
walipumbazika; wakaubadili
utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na
uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo
Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana
heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo,
wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina”
Huu ndio wakati ambapo watu
watalikataa neno la Mungu na kufuata na kujitafutia waalimu kutokana na
kuwawatafiti watafuata khadhithi na kulikataa neno la Mungu, katika nyakati
hizi ndio watu wa Mungu tunatiwa moyo kwa maandiko kukemea kukaripia kuonya na
kufundisha kwa bidii
2Timotheo 4:1-5 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu,
atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme
wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia,
kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati
watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe
watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;nao
watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Bali wewe,
uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa
Injili, timiliza huduma yako.”
Mfumo
wa utawala wa Kidemokrasia umeharibu sana jamii, muhubiri wa Kimarekani mwenye
asili ya Afrika “Creflo Dollar” aliwahi kuitwa polisi kutoa maelezo ya kumchapa
kibao binti yake, kumekuwapo na sheria za kijinga kiasi ambacho huwezi kumuonya
mtu, kumpiga mtoto ni kosa kubwa, wanawake wnahisi kuwa walikandamizwa kwa
miaka mingi na sasa wanataka kuwa na sauti na maamuzi yao, kuwatii waume zao sawa
na maandiko limeonekana kuwa swala la utumwa, kudaiwa kwa haki na usawa wa kijinsia, ndoa za
jinsia moja ambazo zinatiwa moyo na
mataifa yote ya kidemokrasia ambayo yanafikiri kuwa yameendelea sana, uhuru wa
kuabudu uliokithiri kiasi ambacho watu wanaweza kufanya lolote kwa jina la
Mungu, vikundi vya kigaidi vya watu wenye kuua wenzao kwa misingi ya chuki na
visingizio vya dini zenye siasa kali, machafuko ya kila aina uhuru wa kutoa au
kupokea habari, uhalifu wa kimtandao, wizi, udanganyifu na utapeli ufisadi na
kadhalika ni matukio ambayo yametawala katika nyakati hizi za utawala wa chuma
na udongo kabla haujaja utawala wenye nguvu wa Yesu Kristo, hizi ni dalili za
ujio wa mpinga Kristo na kunyakuliwa kwa kanisa ambako wengi wataacha kutokana
na kuvutiwa na uovu na anasa na tamaa za dunia hii
Yesu anaonya kwamba katika wakati
huu watu wajihadhari
Luka 21:34-36. “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi,
na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego
unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia
nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya
yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
Yesu ataikuta dunia iko katika
hali mbaya sana kutokana na kuwepo kwa serikali ovu na legevu, ni lazima kanisa
liwe macho na kutokukubali kuifuatisha namna ya ulimwengu huu
Hatari ya uhuru uliokithiri chini ya mfumo wa kidemokrasia.
Uhuru wa kupita kawaida sio
mpango wa Mungu kabisa tangu pale alipomuumba mwanadamu, Mungu alipomuumba
mwanadamu aliweka mipaka ili kutokuruhusu uhuru uliokithiri, uhuru ambao
ungemuongoza mwanadamu katika kumtenda Mungu dhambi, uhuru bila mipaka sio mpango wa Mungu, kizazi
tulicho nacho kwa bahati mbaya kinataka uhuru huo chini ya kifurushi cha
maendeleo na demokrasi.
Kwa Adamu na Hawa Mungu hakuwapa
uhuru bila mipaka Mwanzo 2:16-17
inasema “BWANA
Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku
utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”
Kwa wana wa Israel Mungu
hakuruhusu wawe na uhuru wa kujifanyia kila wanachokitaka kwani wangefanya
dhambi aliwapa amri kumi na sheria nyingine ndogondogo ili waweze kuzizingatia,
Kutoka 20-40, amri hizi zilipelekea
wana wa Israel waweze kudumisha uhusiano wao na MUngu na watu wengine
wanaowazunguka
Kutoka 20:1-17 “Mungu akanena
maneno haya yote akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya
Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie
sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala
kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu;
nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha
wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana
hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita
fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA,
Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti
yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala
mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu,
na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA
akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. Waheshimu baba yako na mama yako; siku
zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako. Usiue.
Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo.
Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa
wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote
alicho nacho jirani yako.”
Kwa kanisa zaidi ya kuangalia amri
kumi Yesu Kristo katika hutuba yake ya
mlimani aliweza kutoa muongozo wa kiroho ili kila mmoja aweze kuzingatia na ili
aweze kuwasehemu ya ufalme wa Mungu,
katika injili ya Mathayo 5-7, Yesu alitoa na kuorodhesha sifa za kiroho ambazo
mtu anapaswa kuwa nazo ili aweze kuwa na uhusiano na Mungu na kuurithi uzima wa
milele. Aidha sheria maarufu ya Yesu Kristo iitwayo sheria ya dhahabu ni smingi
muhimu katika kuishi kwa utaratibu Mathayo
7:12 “Basi
yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo
ndiyo torati na manabii.”
Jambo la muhimu ninalotaka
kulizungumzia hapa ni kwamba mfumo wa serikali za kidemokrasia unaoonekana kuwa
ni mzuri zaidi na kupendwa ndio mfumo mbaya
na muovu na unaoharibu hali ya kiroho na kudhoofisha uadilifu wa watu na Kanisa na ndio mfumo wenye
kuvumilia dhambi kwa kiwango kikubwa na cha uhuru uliopitiliza, msisitizo wa
kisheria unaendelea kuwa dhaifu kila siku, watu wanataka uhuru zaidi na wako
tayari hata kuasi, viongozi wakubwa wa mataifa ya dunia wamekuwa wakichukuliana
na kila kinachoonekana kuwa ni sawa na kwa ujumla wamelemazwa na mfumo huu.
Mfumo huu wa kisiasa una nguvu ya shetani na wanadamu na hivyo kila kiongozi
duniani atakayeonekana ana viashiria vya kidikteta anapigwa anadhoofishwa na
Demokrasia inatawala kisha uovu mkuu unafuata hii ni sihara kuwa muda wa ile sanamu
ya Nebukadreza umekamilika na sasa tunasubiri utawala wa Jiwe lisilochongwa kwa
mikono Utawala wa Yesu Kristo duniani.
Asomaye na afahamu
Na mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.