Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa
mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani,
na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa moja ya
siri ya mafanikio makubwa sana ya mwanadamu, ni pamoja na kuwa katika
mfano na sura ya Mungu, (Image and likeness). Mwanadamu wa
kwanza kabisa katika bustani ya Edeni hakuwa mtu wa kawaida alikuwa mkamilifu
na mtakatifu, alikuwa ameumbwa tayari kwa kuutawala ulimwengu na kila kilichomo
ndani yake, hakuwa amekusudiwa afe, augue au akose kitu au apoteze uhusiano
wake na Mungu hakukusudiwa akose amani na furaha au akose utoshelevu, Chini ya
uwepo wa Mungu mwanadamu aliumbwa afanikiwe katika kila jambo, Afanikiwe katika
mambo yote, aweke mambo yote chini ya miguu yake, atawale atiishe,awe na
mamlaka na uweza chini ya uwepo wa Mungu, Hata hivyo Biblia inaonyesha Katika
mwanzo 3 kuwa kila kitu kiliharibika mara baada ya anguko, mwanadamu alipoteza
sura na mfano wa Mungu, alipungukiwa na utukufu wa Mungu,
Warumi 3:10-12,23 “10. kama ilivyoandikwa, ya
kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. 11. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye
Mungu. 12. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata
mmoja. 23.
kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;”
Matokeo yake ni kuwa mwanadamu
alitawaliwa na Mazingira yake, alipoteza hekima ya kuyatawala mazingira yake,
alipoteza ukamilifu, uwezo wa kuutawala ulimwengu ulipungua, na mwanadamu
amepoteza tumaini na Mfano na sura ya Mungu iliharibiwa, Ili mwanadamu aweze
kuwa na mafanikio makubwa na kuwa na nguvu kama ile iliyokusudiwa kwa Adamu, ni
muhimu sana akarejea katika Mfano na sura ya Mungu.
Kwa mfano wetu na kwa sura yetu.
Katika moja ya mistari ya Msingi
na ya Muhimu sana katika kitabu cha mwanzo Mstari wa Mwanzo 1: 26, Mstari huu una nguvu kubwa sana, Uelewa wa kutosha
katika mstari huu utatufanya tuweze kuona ubora wa mwanadamu na kumtukuza Mungu
hata kwa jinsi alivyotuumba na kisha kuendelea kumtegemea Mungu kwa asilimia
100 na kuacha kujivuna.
Kwa mfano wetu na kwa sura yetu.
(in our image, in our Likeness)
Kwa sura wetu – in our image
– A representation of the external form of a person- Muonekano wa nje
Kwa mfano wetu – in our
likeness – The fact or quality of being alike, similarity - mfanano wa kitabia na uadilifu.
Kwa msingi huo ni wazi kuwa
mwanadamu aliumbwa akiwa anafanana na Mungu kimaumbile, kitabiana kimaadili.
Hivyo basi mafundisho yoyote au theory yoyote inayoshusha thamani ya mwanadamu,
au tabia au mwenendo wowote unaoshusha thamani ya mwanadamu kimaandiko
unamkosea sana Mungu na kumdhalilisha Mungu na ubora wa uumbaji wake, katika
mstari huu tunajifunza sasa kwamba;-
1. Unaonyesha
wazi kabisa kuwa Mwanadamu aliumbwa na Mungu na kuwa hakutokana na mabadiliko
ya tabia ya nchi, “Evolution theory” Mwanzo
1;27, Mathayo 19:4, Marko 10:6 Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa
Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Mathayo
19:4 “Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye
aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,” Marko 10:6 “Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na
mke.”
Mistari hii ya Musa na maneno
ya Yesu inatuthibitishia wazi kuwa mwanadamu anatokana na kuweko kwa kusudi la
Mungu, Mwanadamu sio kiumbe cha kawaida, Mungu amemtukuza mwanadamu na
kumtawaza juu ya kazi zake zote, na kamwe mwanadamu sio matokeo ya bahati mbaya
wala mabadiliko ya tabia ya nchi, mwanadamu ni kiumbe cha juu zaidi katika kazi
na utendaji wa Mungu, sio kiumbe cha kudharauliwa wala kuvunjiwa heshima, sio
kiumbe kilichoumbwa kuwa mtumwa wa mtu au mazingira, sio bidhaa inayoweza
kuuzwa kama ng’ombe kila mtu anapaswa kuelewa kuwa anaposhughulika na mwanadamu
anashughulika na kiumbe ambacho Mungu amekitukuza mno, uhai wake haupaswi
kutolewa kijinga na kirahisi, maisha ya kiumbe hiki hayapaswi kupuuziwa na
kuachwa yapotee kirahisi, Mwanadamu ni wa thamani, ametoka katika wazo na
mpango kamili wa Mungu.
2. Mwanadamu
ndio kiumbe pekee kilichoumbwa kuwa na ushirika wa karibu zaidi sana na Mungu,
hata kama viumbe vyote vimeumbwa kwaajili ya utukufu wa Mungu ili vipate
kumuabudu Mungu, Mwanadamu ndie kiumbe bora zaidi ambaye Mungu anapendezwa
naye, anafurahia kuabudiwa naye, Mungu alikusudia kuwa na ushirika wa karibu na
mshikamanifu sana na Mwanadamu kuliko kiumbe kingine chochote Waebrania 2:6 “Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa
binadamu, hata umwangalie?” linapokuja swala kuhusu Mwanadamu Mungu
huwezi kumwambia kitu, yuko tayari kumkumbuka yuko tayari kumwangalia, Historia
ya mwanadamu inaonekana hapa kwamba alikuwa na ushirika “mgumu” “Athletic fellowship” na Mungu, walikuwa na uadilifu wa hali ya juu,
walikuwa wakamilifu, hawakuwa na dhambi, walikuwa watakatifu, wenye hekima,
moyo wa ujasiri, waliokuwa na upendo kamili, ukarimu na wasiokuwa na ubinafsi
wala choyo, na uamuzi uliweza kutumika kufanya maamuzi yaliyo sahihi, Mungu
alikusudia nawe na ushirika wa karibu zaidi na mwanadamu unaozidi undugu na
kwamba mwanadamu amtegemee yeye.
3. Walipewa
neema ya kuwa mfano na sura ya Mungu, Hili nalo ni moja ya jambo muhimu sana
ambalo wasomi wengi wa kimaandiko hawaelewi uzito wa andiko hili, Swali kubwa
la kujiuliza linalozaliwa na Mwanzo 1:26
ni kuwa sisi tuliumbwa kwa mfano na sura yake Mungu, hii ina maana gani? Andiko
hili lina maana kubwa sana kinabii kwamba Mungu mwenyewe aliwapa wanadamu Mwili
(Sura, Umbile Muonekano) ambao yeye mwenyewe angeweza kuja kujitokeza na
kuonekana kwao, na kuwa wenzake
Mwanzo
18:1-14 “1.BWANA
akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa
hema yake mchana wakati wa hari. 2. Akainua macho yake akaona, na tazama, watu
watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka
mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, 3. akasema, BWANA wangu, kama nimeona
fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. 4. Na yaletwe
basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. 5. Nami nitaleta
chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa
wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. 6. Basi Ibrahimu akaenda hima
hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye
mikate. 7. Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye
laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. 8. Akatwaa siagi na
maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao
chini ya mti, nao wakala. 9. Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo
hemani. 10. Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama,
Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo
nyuma yake. 11. Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na
Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12. Kwa hiyo Sara akacheka
moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?
13. BWANA akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa
mwana, nami ni mzee? 14.
Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia,
wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume” Unaweza
kuona Mungu aliweza kujitokeza kwa Abrahhamu na kufanya mazungumzo naye katika
namna ya kawaida kabisa kwa mwili ule ambao Mungu alikuwa nao; Zaidi ya yote
Mungu alikuwa anamaanisha kuwa kinabii angekuja na kujitokeza kwa wanadamu akiwa
na mwili sawa na ule wanaoutumia wanadamu ili awaonyeshe njia mwili ambao Yesu
alikuwa nao Luka 1:35 “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu
yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho
kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” Kimsingi Mungu
alipokuwa akimuumba mwanadamu alikuwa na wazo la Yesu, au wazo lake yeye
mwenyewe, kwa hiyo basi mwanadamu kuwa na mfano na sura ya Mungu maana yake ni
kuwa kama Yesu, ambaye ni Mungu na alikuja duniani kwa nia ya kuutwaa mwili Yohana 1;1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno
alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa MunguNaye Neno alifanyika mwili, akakaa
kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa
Baba; amejaa neema na kweli.” Mungu amekusudia wote tuwe kama Yesu
tangu mwanzo, tofauti yetu ni kuwa sisi na baba yetu Adamu alipoteza hali ya
kuwa na mfano na sura ya Mungu (Likeness)
tunapokuwa tumeokolewa na kumuamini Yesu Mungu anaturatajia turejee na kuwa
wakamilifu kama yeye mwenyewe kwa kuufuata mfano wa Yesu Kristo “Kwa mfano wetu
na kwa sura yetu” tunapomuamini Yesu kwa imani tunakuwa kama Yesu Mungu
anatukubali kwa neema na kututazama kama yeye mwenyewe na kuwa na ushirika nasi
kama atakavyo yeye, inahitajikia neema ya Mungu kulielewa hili. Na Mungu akupe
neema hiyo katika jina la Yesu.
4. Mstari
huu Mwanzo 1;26 unatukumhbusha sisi
asili yetu Kimaadili, kwamba tulikuwa wakamilifu kama Mungu, lakini tumepoteza
ile hali yabuadilifu ya kuwa kama Mungu, sio hilo tu tumepoteza hali ya kuwa na
ushirika na Mungu, kuja kwa Yesu Duniani kulikuwa na kusudi la kutujenga tena
katika ule uadilifu, na hivyo Yesu ametuachia kielelezo tukifuate Yohana 13:15 “Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea,
nanyi mtende vivyo.”
Madhara ya kupoteza sura na mfano wa Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa ili
tuweze kuwa na ushirika wa karibu na Mungu ni lazima tushughulikie sana swala
la kufanana na Mungu “likeness”
ambalo mwanadamu amelipoteza, hili ndio jambo la msingi, tunapokuwa na
watumishi wa Mungu walioitwa kwa makusudi mbalimbali ya kuujenga mwili wa Kristo
lazima ikumbukwe kuwa kusudi letu kuu ni kuwa kama Kristo, Adamu wa kwanza
alikuwa kama Kristo lakini alipoteza, na kuathiri jamii nzima ya iana binadamu,
sasa basi ni lazima tulenge kuwa kama Kristo Waefeso 4:11-13 “Naye alitoa wengine kuwa
mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa
wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya
huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia
umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata
kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo” Hili ndio Jambo
la msingi na la muhimu mno Yesu amekuwa kielelezo chetu tunapaswa kumfuata
tunapaswa kumuigiza tunapaswa kuwa kama yeye, kila mmoja wetu anapaswa
kujiuliza kama anafanana na Yesu, Ushirika wa karibu na wenye nguvu na Mungu
utategemea namna na jinsi tunavyomtegemea yeye, kwa nguvu zetu hatuwezi lakini
chini ya neema yake tunaweza kujitegemeza kwake na sura na mfano wa Mungu
ukawepo ndani yetu. Hili ni jambo la Muhimu
Mwaka 1972 wakati wa uchaguzi wa
Rais Huko Marekani, wagombea wawili maarufu sana waipambana kuwania kiti cha
urais, 1 aliitwa Richard Nixon, aliyetokea California akiwakilisha chama cha
the republican na Mpinzani wake aliitwa George McGovern, aliyetokea jimbo la
South Dakota akiwakilisha chama cha Democratic Katika uchjaguzi huo George
McGovern alishindwa vibaya, Kura za turufu za Marekani Electoral vote Nixon
alipata 520 na George alipata 17, Inaelezwa moja ya sababu kubwa ya kushindwa
kwa George ni kuwa wakati walipofanya kampeni zao kwa njia ya Radio kila mtu
alivutiwa sana na George Sauti yake ilikuwa yenye mvuto mkubwa sana na yenye
ushawishi ukilinganisha na Nixon hata hivyo mara walipokuja kuonekana kwa njia
ya Television Muonekano wao ulikuwa tofauti sana George alikuwa ametoka kuugua,
na hivyo alikuja studia akiwa amejifunika koti na sweta, alionekana kuchoka
sana na muonekanao wa afya yake pia haukuwa mzuri, alikataa kufanyiwa make –up
na kupakwa poda na kufanyiwa maandalizi ya kurushwa katika televisheni huku
Nixon alionekana mwenye afya njema na aliyekuwa amefanyiwa make up ili
muonekano wake uwe Mzuri, kumhbuka hii ilikuwa debate ya mwisho, watu walikata
tamaa sana walipoona muonekano wa George na hivyo Nixon ambaye hakuwa mnenaji
Mzuri alichaguliwa kura rais wa marekani.
George McGovern Kushoto – Democratic na Richard Nixon Kulia- Republican
Nini kilimpa Nixon ushindi mkubwa
ilikuwa ni Sura yake, muonekano wake, nini kitatupa ushindi katika maisha yetu,
ni kitu gani kitatufanya tukubaliwe na Mungu na wanadamu, nini kitatufanya tuwe
na mvuto na ushirika wa karibu sana na Mungu ni Sura na mfano wa Mungu,
Mwanadamu atakuwa kiumbe chenye utukufu mkubwa anapokuwa anazishika njia za
Mungu, atakuwa na ukaribu naMungu akijitahidi kuwa kama Yesu, Ni lazima kila
mmoja wetu akubali kumwamini Yesu na kujifunza kuwa kama Yeye ili tuweze kupata
kibali kwa Mungu, Shetani atakosa la kutushitaki ikiwa tutamfanania Mungu,
Bwana na ampe neema kila mmoja wetu kuwa na sura na mfano wa Mungu ili tuweze
kupata kibali mbele za Mungu. Lazima tujitahidi kujionyesha kuwa tumekubaliwa
na Mungu 2Timotheo 2;15
Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!
Endapo umebarikiwa na Masomo yangu tafadhali usisite kunijulisha namna na jinsi ulivyobarikiwa kama wafanyavyo wengine sms au whatsapp me kwa +255 718 990 796