Waebrania 5:7 “Yeye, siku hizo za
mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na
dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha
Mungu;”
Utangulizi:
Tunajifunza
kutoka katika maandiko kuwa kwa kila jambo kuna majira yake Muhubiri 3:1-4 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa
kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa
kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;
Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa
kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati
wa kucheza;” kwa msingi huo kila mwanadamu ana wakati wa kulia na
kuna wakati wa kufurahi na kadhalika hata hivyo kwa kuwa nazungumzia kuhusu
kulia kila mwanadamu ana wakati wake wa kulia na wakati wa kucheka, yako mambo ambayo katika maisha
ama watu wanaotuzungunga na ama aina ya mapito
tunayoyapitiatyanaweza kukufikisha katika point ambayo kwa vyovyote vile
tunaweza kulia.
Dunia huwa
inasema kuwa wanaume hawalii, Lakini maandiko yanatuambia watu wakubwa sana wa
Mungu walilia, watu ambao ni majasiri na wenye nguvu na mashujaa pia wakati
fulani walilia, Hata Yesu Kristo ambaye ni Mungu alipokuwa katika mwili duniani
alilia, Wakati fulani katika ulimwengu huu itatupasa kulia na kuliitia jina la
Mungu kwaajili ya maswahibu mbalimbali na Mungu yule tumuabuduye atatupa amani,
atatufariji na kutokeza msaada kwa nini kwa sababu maandiko yanaonyesha kuwa
iko nguvu kubwa sana katika machozi.
Mungu anawajali sana wanadamu.
Ni muhimu sana
kufahamu kuwa Mungu anawajali sana wanadamu ni jambo la kushangaza kuwa
mwandishi wa kitabu cha waebrabia
alihoji kuwa mwanadamu ni nani hata umkumbuke Waebrania 2:6 “Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata
umwangalie? “ Mungu anatamini sana wanadamu kiasi ambacho tukiomba
anatusikia na ni Mungu mwenye kujishughulisha sana na mambo yetu 1Petro 5:6-7 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio
hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa
maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”Unaweza kuona
tunamuabudu Mungu ambaye anajishugulisha sana na wanadamu anatujali mno,
maandiko yanasema anajishughulisha sana na mambo yetu, sisi hatupaswi
kunung’unika tunapaswa kumuomba na kumkabidhi njia zetu zote, hivyo ndivyo
maandiko yanavyotufunza angalia katika Zaburi
37:5 “Umkabidhi
Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.” Unaona kwa msingi
huo tunaweza kumkabidhi Mungu mahitaji yetu yote, naye atashughulika nayo, kwa
sababu hiyo maandiko yanatutia moyo kwamba hatupaswi kufadhaika Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila
neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia
zenu katika Kristo Yesu.”Mungu huwa ndio kimbilio letu na ni asili
ya nguvu zetu na yuko tayari kutusaidia wakati wa mahitaji hususani Mateso kama
tukimuomba Zaburi 46:1 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana
tele wakati wa mateso.” Hata tunapopitia mateso na mapito ya aina
mbalimbali Mungu bado ni ngao yetu Zaburi
9:9 “Bwana
atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida.” Wakati
wote tupitiapo shida na kuonewa Mungu anakuwa ngoime yetu ba anatoa msaada
unaotatikana au unaohitajika, kwa msingi huo maandiko yanataka tusiogope kwa
sababu Mungu atatusaidia Isaya 41:10
“usiogope, kwa
maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia
nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”
Kwa hivyo tupitapo katika majaribu hatupaswi kuona kuwa cha ajabu na kama
ikiwezekana tunapaswa kufurahia Yakobo
1:2-4 “Ndugu
zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na
kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.”Hata hivyo pamoja na maandiko kututia Moyo
kuhusu maombi na namna Mungu anavyojali maisha yetu na namna anavyojihusisha
nayo mamandiko yanatuonyesha kuwa liko jambo lingine kubwa na la ziada ambalo
likiambatanishwa na maombi Mambo makubwa sana hutokea jambo hilo Mungu analithamini
sana na hili sio lingine ni Maombi yanapoambaanishwa na Machozi, Mungu
anayathamini sana machozi, machozi yana faida kubwa sana kisayansi na kiroho,
leo tutachukua Muda kuangalia nguvu ya machozi na kujibu swali kwa nini Mungu
anayathamini sana Machozi!
Mungu anathamini sana Machozi!
Utafiti usio
rasmi wa kisayansi umebaini kwamba kulia machozi kunampa mwanadamu nafasi ya
juu zaidi ya kujitibu kutoka katika mgandamizo mkubwa wa mawazo yaani stresses,
Hii ni kwa sababu wakati mtu analia anatoa chemikali iitwayo Oxytocin na Endorphins, Chemikali hizi zinapotoka zinaleta unafuu kwa mwanadamu
na kumfanya ajisikie vizuri kimwili na kihisia na kuondoa maumivu ya moyo na
kwa sababu hiyo inakubalika kuwa kisayanzi kulia kunaondoa uchungu na kuleta
unafuu wa roho.
Wanadamu hulia
machozi kutokana na hisia za hali ya juu tofauti tofauti katika nafsi zao,
Machozi yanabeba hisia za juu kabisa za homoni kuliko aina nyingine yoyote ya
chemikali za homoni, kutoa machozi kuna faida kubwa sana kiafya. Na Endapo mtu
atapatwa na jambo lenye kuumiza sana hisia zake na kujizuia kutokulia atakuwa
amejeruhika kwa kiwango kikubwa nafsini mwake.
Katika namna
isiyoweza kuelezeka ulimwengu wa kiroho nao unathamini sana machozi, Mungu
anayaangalia sana machozi, kiasi ambacho hawezi kuyadharau kwa namna yoyote,
Machozi huwa yana nguvu kubwa sana katika ulimwengu wa Kiroho, wakati wowote
watu walipolia na kuugua Mungu hakuweza kuvumilia alishuka na kuleta wokovu au
msaada Zaburi 107:4-6 “Walitanga-tanga
jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa. Waliona njaa, waliona na
kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. Wakamlilia Bwana katika dhiki zao,
Akawaponya na shida zao.” Zaburi 107:19 “Wakamlilia
Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.” Zaburi 34:17 “Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na
taabu zao zote.” Mungu anazingatia sana Machozi ya mwanadamu, mtu
anapolia maana yake amefikia kiwango cha juu zaidi cha kukata tamaa katika
maisha yake, hana mlango mwingine wa msaada zaidi ya Mungu, hana namna ya kujieleza
tena, hakuna mtu anaweza kumuelewa hakuna mtu anaweza kumtetea, amebanwa hakuna
njia nyingine isipokuwa Mungu mwenyewe aingilie kati na ndio maana wakati wote
wanadamu wanapoteseka wakilia Mungu hawezi kuyapuuzia machozi yao, Machozi yana
uwezo mkubwa sana wa kumvuta Mungu karibu, yana nguvu ya kumfanya Mungu
kuingilia kati na kubadili mambo
Nguvu ya Machozi:
-
Machozi yana uwezo wa kumuokoa mtu na Mauti.
Biblia inaonyesha kuwa Mungu alimfufua Yesu siku ya tatu, kwa sababu
aliomba, Mara kadhaa pia tunaona kuwa wako watu waliahirishiwa mauti yaani kifo
kwa sababu walilia sana Waebrania 5:7
“Yeye, siku hizo
za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi
na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha
Mungu;” Unaona Yesu Mwana wa Mungu
aliomba, alifanya dua na aliiambatanisha na machozi na alisikilizwa na
kufufuliwa siku ya tatu Mungu hakumuacha Kaburini aone uharibifu, kumbe maombi
yana nguvu ya kuhairisha mauti, Katila injili ya Luka 7 tunaelezwa habari ya
mjane mmoja katika mji wa Naini mjana huyu alikuwa na mtoto mmoja tu na mtoto
huyo alikufa watu wengi sana walijitokeza kumfariji mjane yule na walikuwa
tayari kushiriki mazishi ya kijana huyo wa pekee wa mwanamke mjane na bila
shaka mjane yule inaonekana alilia sana, Maombi yake na kulia kwake kulimgusa
sana Bwana Yesu na kutokana na machozi
yale Yesu alihairisha msiba ule ona Katika Luka
7:11-15 “
Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake
walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. Na alipolikaribia lango la mji, hapo
palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane,
na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.
Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. Akakaribia,
akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana,
nakuambia, Inuka. Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama
yake.” Unawezaje kujua kuwa mwanamke yule mjane alikuwa analia ni
neno moja tu la Yesu, Alimuonea huruma akamwambia “USILIE” ni kwa nini huruma za Mungu zilikuja juu ya mwanamke huyu
mjane ni kwasababu yule alikuwa kijana wake wa pekee kwa hiyo msiba wake mama
huyu mjane ulikuwa mkubwa sana moyoni mwake na hapa Yesu aliiahirisha mauti,
tunapolia machozi Mungu huweza kutuokoa na mauti, ona vilevile yakwamba Mungu
alimuongeza Hezekia miaka 15 ya maisha yake japo ni yeye aliye mtum anabii
isaya akamtangazie kufa Isaya 38:1-5 “Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari
ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana
asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi
Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana, akasema, Ee
Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa
moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana,
Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona
machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.” Katika namna ya kushangaza sana wote tunafahamu
namna na jinsi Nabii Isaya alivyokua mkali na sirias na hapa Mungu alimtuma
amwambie Hezekia ajiandae kufa Hezekia hakuwa na jinsi isipokuwa kumgeukia
Mungu na tunaambiwa kua Hezekia AKALIA
SANA SANA na vilevile tunaambiwa kuwa Mungu alimjibu kuwa amesikia maombi
yake lakini AMEYAONA MACHOZI YAKE,
hapa tena tunaona nguvu kubwa iliyomo katika machozi ikimkinga mtu na kifo,
Kaka yangu na dada yangu, maombi yako yakiambatana na hisia kali na machozi kwa
dhati kutoka moyoni Mungu huyaona na kuyafanyia kazi, usipende kulia tu bila
kuambatanisha maombi yako na Machozi.
Aidha maandiko yanaonyesha kuwa Mauti ya rafiki wa Yesu aliyeitwa
Lazaro iliahirishwa kwa sababu ya mtiririko wa machozi ya watu kadhaa yakiwemo
ya Yesu Kristo mwenyewe ona Yohana
11:32-35,43-44 “Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo
Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo
hapa, ndugu yangu hangalikufa. Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi
waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, akasema,
Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi”.
43-44 “Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu,
Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na
mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache
aende zake.”
Eneo lingine ambalo tunaona Mungu akihairisha kifo kwa sababu ya
machozzi ni pamoja na eneo ambalo Yona alimezwa na Nyangumi kwa ujumla hali
hiii ni ngumu sana kuelezea namna ilivyokuwa sidhani kama mtu katika tumbo la
nyangumi anaweza kuwa hai ukweli ni kuwa Mungu alimpa neema Yona katika Tumbo
la Nyangumi angalau kusema maneno kadhaa ambayo yalimfanya Mungu amkumbuke na
samaki akaona kuwa sio sahihi kumeza Yona na akamtapika Yona 2:1-6, 10 “Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule
samaki, Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia;
Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa
vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;
Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. Nami nikasema,
Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako
takatifu. Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani
ulikizinga kichwa changu; Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na
mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka
shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,” 10 “Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika
Yona pwani.”
-
Machozi yana nguvu ya kumfanya Mungu kushuka.
Biblia inaonyesha kuwa mara kadhaa vilevile watu walipopata shida za
aina mbalimbali na mateso na wakalia, licha ya kuwa Mungu alisikia na licha ya
kuwa Mungu yuko mahali kote Mungu vilevile hushuka na kujishughulisha na maisha
ya watu wanaolia na kuugua kwa kusudi la kuleta msaada Kutoka 3:7-9 “BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko
Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua
maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe
kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata
mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo
mateso ambayo Wamisri wanawatesa.”
Unaweza kuona pia Katika Matendo 7:34
“Yakini nimeona
mateso ya watu wangu waliomo Misri, nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka
niwatoe. Basi sasa, nitakutuma mpaka Misri.” Mtu anapolia kwa kuugua
Mungu huguswa kwa namna ya ajabu sana na hushuka kwaajili ya kutoa msaada
husika Bwana na ampe neema kila mmoja wetu, kumlilia Mungu kila tunapokumbwa na
maswaibu ya namna mbalimbali ili uwepo wake ushuke kuja kutusaidia.
-
Machozi humfanya Yesu ajifunue kwetu
Mara baada ya kufa kwa Yesu na kuzikwa siku ya tatu alfajiri na
Mapema Wanawake wanaompenda Yesu walijihimu Kaburini bila shaka kwa kusudi la
kuuhudumia mwili wa Bwana Yesu ili kuuhudumia usiharibika, katika namna ya
kushangaza sana hawakuweza kuuona mwili huo na kwa vile Kaburi lilikuwa wazi na
jiwe nlimeondolewa Mariam Magdalene alikata tamaa akijua kuwa mwili huo wa
Bwana Yesu umeondolewa na kwa sababu alimpenda sana Yesu alilia kwa uchungu
mkubwa sana kwa sababu ya Machozi Yesu
alijifunua kwake Yohana 20:11-15 “Lakini Mariamu
alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi,
aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. Akaona malaika wawili, wenye mavazi
meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake
Yesu. Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa
Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.
Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama,
asijue ya kuwa ni Yesu. Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani?
Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa
umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. Yesu akamwambia,
Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu
wangu).” Unaona Malaika wa
Mungu unapolia wanaguswa mno na Yesu alipoona Mariam analia alijifunua kwake,
kumbe endapo tunataka Yesu ajifunue kwetu hatuna budu kuambatanisha Maombi yetu
pamoja na kulia sana na Machozi na Bwana atatutokea katika maisha yetu!
-
Machozi hufanya Mungu akuone
Biblia inatuonyesha kuwa moja ya watu waliopitaia mateso ni Pamoja
na Hajiri na Ishamel tangu akiwa tumboni, Lakini mara kadhaa Mungu alionyesha
kujali kwa sababu ya machozi yao, Hajiri alipoteswa na Sarai alikimbia jangwani
akiwa amekata tamaa, ukweli ulio wazi ni kuwa alikuwa analia, Mwanadamu
anapolia au kutoa machizi maana yake amefikia kilele cha juu kabisa cha hisia
zenye kuumiza na kuhitaji msaada, Mungu alimtokea Hajiri na kumthibitishia kuwa
amesikia kilio cha Mateso yake ona
Mwanzo 16:6-13 “Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi
mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka
mbele yake. Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa,
chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri, wewe
mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi
kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi
yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika
nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume,
nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.
Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote
na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake
wote. Akaliita jina la BWANA aliyesema
naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?
”
Aidha Hajiri yuleyule akiwa sasa na kijana wake Ishmael
walipofukuzwa na kuishia Jangwani maji yaliwaishia na Mama alijikuta anakata
tamaa sana alimtupa mtoto chini ya kijimti, ili ikiwezekana asishuhudie mtoto
huyo anavyokufa bila shaka Hajiri alipaza sauti alilia lakini vilevile Ishamel
alilia sana jambo hili lilipelekea Mungu kusikia na kufanya muujiza wa
kupatikana kwa maji. Unaweza kuona katika maandiko yafuatayo
Mwanzo 21:12-20 “Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni
pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara,
sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. Naye mwana wa
mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako. Ibrahimu akaamka
asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika
begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la
Beer-sheba. Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti
kimoja. Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana
alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake,
akalia. Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka
mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya
kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa
nitamfanya kuwa taifa kubwa. Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha
maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Mungu akawa pamoja na
huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.”
Hii maana yake ni nini? Neno la Mungu limejawa na shuhuda nyingi
sana zinazoashiria kuwa Mungu atakutokea na kufanya muujiza, Mungu anaposikia
mama analia, Mungu anachungulia anaposikia mtoto analia, Mungu husikia kilio
cha mtu aliyekosa matumaini, maombi ya kulia humfanya Mungu kuona na kusikiliza
haraka!
-
Machozi humfanya Mungu akukumbuke!
Ni muhimu kufahamu kuwa kibiblia neno kukumbuka maana yake ni “KUTOA KIPAUMBELE” first priority Neno
hili kukumbuka kwa kiebrania maana yake ni “Zakar” to bring someone to mind and then act upon that person's
behalf." Maana yake kuweka akilini na kushughulika naye kwa haraka kabla
hajakata tamaa Neno hili limetumika katika Mwanzo
8:1 “Na
Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja
naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua; “
na Mwanzo 30:22 “Mungu akamkumbuka
Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.” Sasa kwa kawaida kutokana na Maumbile ya
wanadamu ni vigumu wanadamu kutoa kipaumbele kwa wanadamu wengine ni vigumu wanadamu kukumbuka wenzao ona Mwanzo 40:14 “Ila
unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa
Farao, na kunitoa katika nyumba hii.” Yusufu
alijiombea neno hili kwa rafiki yake aliyemtafasiria ndoto kwa kumuomba
amkumbuke hata hivyo baada yamafanikio rafiki yake Yusufu alimsahau Mwanzo 40:23 “Lakini
huyo mkuu wa wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahau” sasa basi
Mungu katika mpango wake hawezi kusahu yeye anasema mama anaweza kumsahau mtoto
anayenyonya lakini Mungu hatakusahau wewe Isaya
49:15-16 “Je!
Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo
lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. Tazama,
nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima. “
Kumbe Mungu hawezi kukusahau wajibu wetu sisi ni kumuomba tu atukumbuke aweke
kipaumbele akuangalie Zaburi 106:4 “Ee Bwana,
unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako”,
Moja ya jambo ambalo linaumiza sana katika jamii, ni Pamoja na kukosekana
kwa uzao, hali hii katika biblia inatajwa kama sababu kubwa ya uchungu mkubwa
kwa watu wengi hususani wanawake, katika jamii ya Israel utasa ulifikiriwa kama
laana, ulifikiriwa kama hali ya kutokuwa na faida au kuzalisha, Hali hii
ilimuumiza sana mwanamke aliyeitwa Hana ambaye alikuwa akisanifiwa na
kuchokozwanamwanamke mwenzake mke mwenza kwa
sababu yeye alikuwa anazaa na Hana akuwa na mtoto, hali hii ilimuumiza
sana Hana kiasi ambacho aliamua kuambatanisha maombi yake na machozi Biblia
inaonyesha kuwa kutokana na maombi yake yaliyoambatana na machozi Munguhatimaye
alimkumbuka na kumpa Mtoto aliyeitwa Samuel ambaye alikuja kuwa Nabii mkubwa,
mwamuzi, kuhani na kiongozi mkubwa wa Taifa la Israel, maombi ya kulia machozi
humfanya Mungu atukumbuke ona;-
1Samuel 1:5-10 “lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana,
ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Ila mwenzake humchokoza sana, hata
kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Tena mumewe akafanya
hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana,
ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula. Elkana
mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako
una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? Ndipo Hana akainuka,
walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi
kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana. Naye huyo mwanamke alikuwa na
uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana.”
1Samuel 1:19 “Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha
wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye
Bwana akamkumbuka.”
Unaona ndugu yangu Mungu hukumbuka machozi, huyahifadhi hayataachwa
bure, machozi ni kama Damu machozi ni sadaka ya thamani sana yako mambo mengi
sana duniani yanayoweza kutufanya tulie, wakati mwingine kwa sababu ya mawimbi
ya maisha au kwa sababu ya matatizo na majanga sugu, yanayoyakumba maisha yetu,
ndoa zisizo na amani, watoto wasiotii, kudhulumiwa, misiba isiyotarajiwa, na
wakati mwingine tunaweza kulia hata pasipokujua sababu hii yote hutokana na
uchungu wa maisha lakini kumbuka Mungu atayafuatilia machoziyako atayakumbuka
-
Machozi humfanya Mungu akuokoe na majanga.
Nabii Yona alikataa wito wa Mungu na kuamua kukimbilia Tarshish, kwa
mujibu wa wanajiopgrafia Ninawi mji alikotumwa Yona ulikuwa ni katika nchi ya
Syria au Iraq lakini mjia aliokuwa akikimbilia uko katika nchi ya Spain leo na
unaambiwa kuwa alilipa Nauli, kutokana na kuukimbia uso wa Mungu safari ile
ilikuwa na dhuruba nyingi mno na hivyo kiasi ambacho mabaharia walipata Hasara
kubwa sana na kutupa shehena za mizigo ili kujaribu kujiokoa lakini dhuruba
haikutulia waliamua kupiga kura ili kujua sababu na mtu aliyesababisha majanga
yale na kura ilimuangukia Yona, kwa kweli hakukuwa na jinsi kwani ililazimu
atupwe kilindini mwa bahari na mara akamezwa na Nyangumi, hii ilikuwa ni kama
kifo kwa Yona ni kama alitumbukia kuzimu Yona alilia ndani ya tumbo la Nyangumi
na Bwana akasema na Nyangumi yule na akamtapika Yona angalia.
Yona 2:1-10 “Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule
samaki, Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia;
Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa
vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;
Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. Nami nikasema,
Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako
takatifu. Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani
ulikizinga kichwa changu; Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na
mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka
shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka
Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao
mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; Lakini mimi
nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu
hutoka kwa Bwana. Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.”
-
Machozi yanaleta wokovu na
Neema na huruma za Mungu
Kitabu cha waamuzi ni moja ya mfano wa watu walioteseka sana wakati
wa mpito wa uongozi kutoka yoshua mpaka mfalme wa Kwanza Israel walikuwa na
viongozi walioteuliwa na Mungu kuwaamua viongozi hao waliitwa kuwaokoa pale
walipomlilia na kumuomba kutokana na mateso waliyokuwa wakiyapitia, Mungu
alileta neema wokovu na msaada kutokana na israel kumlilia Mungu, ni wazi kuwa
tunapopitia aina mbalimbali za majaribu na mapito kisha tu7kamkumbuka Mungu na
kumlilia mara moja Bwana ataonyesha uwezo wake kwetu na kutuhurumia na kutupa
msaada kama alivyofanya nyakati za waamuzi
Waamuzi 3:14-15 “Wana wa Israeli walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa
miaka kumi na minane.Lakini wana wa Israeli walipomlilia Bwana, Bwana
akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye
shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa
huyo Ehudi.”
Waamuzi6:6-14 ”Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa
Israeli wakamlilia Bwana. Kisha ikawa, hapo wana wa Israeli walipomlilia Bwana
kwa sababu ya Midiani, Bwana akamtuma nabii aende kwa hao wana wa Israeli; naye
akawaambia, Bwana, yeye Mungu wa Israeli, asema hivi, Mimi niliwaleta ninyi
mkwee kutoka Misri, nikawatoa katika nyumba ya utumwa; nami niliwaokoa na
mikono ya Wamisri, na mikono ya wote waliokuwa wakiwaonea, nami niliwafukuza
watoke mbele zenu, nami niliwapa ninyi nchi yao; kisha niliwaambia, Mimi ndimi
Bwana, Mungu wenu; msiiche miungu ya Waamori, ambayo mwaketi katika nchi yao;
lakini hamkuitii sauti yangu. Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni
uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni
alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.
Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo
haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba
zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa
ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.Bwana akamtazama, akasema,
Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi
ninayekutuma?“
Mashujaa wa machozi.
Machozi
yanaashiria upendo mkubwa na uchungu alionao mtu wakati mwingine kutokana na
mateso au aina ya mapito waliyopitia, jamii kubwa sana ya watu wa zamani
walikuwa na tabia ya kusalimiana na kupeana taarifa kwa zamu na kisha kila
walipopeana taarifa kuhusu mtu fulani aidha aliumwa au alikufa au wamefarakana
muda mrefu walikatika maongezi nhayo na kulia Jambo hili lilionyesha nupendo na
kujali kuliko kukubwa sana , upweke na mateso waliyonayo wanadamu unaweza
kuwafanya wao kulia sana Katika biblia wako watu wengi sana walilia na kisha
Mungu baadaye aliyabadilisha maisha yao
Shujaa wa kwanza wa machozi alikuwa Yusufu
Ona katiika
maandiko mkadhaa akitajwa kama mtu aliyelia mara kwa mara kulia kwake
kuliashiria kujali na upendo aliokuwanao kwa ndugu zake na jamaa zake na baba
yake na wana wa baba yake, kwanza maisha yake ya kupotea Huko Misri
yalisababisha baba yake kumlilia siku zakeo zote akikataa kufarijiwa kwa sababu
alikuwa ni mwana wake aliyempenda angalia Mwanzo
37:34-35 “Yakobo
akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi.
Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa
kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba
yake akamlilia.” Uaona kutokana na upendo Yakobo aliokuwa nao kwa
Yusufu Biblia inaonyesha ya kuwa babaye alimlilia siku nyingi kwa nini kwa
sababu alikuwa ni mwana mwenye utii mwenye kupendeza mwenye heshima na adamu na
mwaminifu kwa babaye na aliyekuwa na maono makubwa kwaajili ya familia yake,
Maisha yake yaliyokuwa yamejaa upedno yalisababisha na yeye kuwa mtu wa machozi
mara kwa mara hasa kwaajili ya ndugu zake Mwanzo
42:24 “Akajitenga nao akalia. Kisha akawarudia, na
kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao.”
Mwanzo 43:30 “Yusufu
akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa
kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo. Akanawa uso, akatoka, akajizuia,
akasema, Leteni chakula.” Mwanzo 45:2 “Hapo
Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga
kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja
naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. Akapaza sauti yake akalia, nao
Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia.” Mwanzo 45:14-15 “Akaanguka
shingoni mwa ndugu yake Benyamini, akalia; Benyamini naye akalia shingoni
mwake. Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze
wakazungumza naye” Mwanzo 46:29-30 “Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda
kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia
shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kizima. Israeli akamwambia Yusufu, Na
nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai.” Mwanzo 50:1-6 “Yusufu
akamwangukia babaye usoni, akamlilila, akambusu. Yusufu akawaagiza watumishi wake waganga,
kwamba wampake baba yake dawa asioze. Waganga wakampaka dawa Israeli. Siku zake arobaini zikaisha, maana hivyo
hutimizwa siku za kupaka dawa. Wamisri wakamlilia siku sabini. Siku za kumlilia
zilipopita, Yusufu alisema na watu wa nyumba ya Farao, akinena, Kama nimeona
neema machoni penu, tafadhalini mkaseme masikioni mwa Farao, mkinena, Baba
yangu aliniapisha, akisema, Mimi ni katika kufa, unizike katika kaburi langu
nililojichimbia katika nchi ya Kanaani. Basi tafadhali uniruhusu niende sasa
nikamzike babangu, nami nitarudi. Farao akasema, Uende, ukamzike baba yako,
kama alivyokuapisha” Mwanzo
50:17 “Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu
zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba
utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema
naye.” Maisha ya Yusufu yalijaa machozi alikuwa mtu wa machozi
pamoja na mafanikio makubwa na heshima kubwa aliyokuwa nayo machozi
yaliambatana na maisha yake lakini wakati wote maisha ya machozi ya Yusufu
yalikuwa na muunganiko kuhusu Ndugu zake upendo wake kwa Israel .
Shujaa mwingine wa kulia ni Daudi.
Daudi ndiye
shujaa wa juu bzaidi nkatika swala la kulia machozi yeye alimujuanmUngu vema
sana kwa sababu hiyo mara nyingi katika dua na maombi yake alilia sana na
machozi utaweza kugundua njambo hili unapopata nafasi ya kuzipitia zaburi
mbalimbali Mwenyewe anasema Zaburi 6:6-9
“ Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza
kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. Jicho langu
limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. Ondokeni
kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa Bwana ameisikia sauti ya kilio changu.
Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu.” Unaweza
kuona pia katika Zaburi 69:3 “. Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu
yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu.” Ni kupitia machozi Daudi
alimlilia Mungu na kumuimbia zaburi kadhaa wa kadhaa, ushaujaa wa Daudi na
uanajeshi wake haukumfanya asiwe mwenye kuklia mbele za Mungu wake maombia yake
na dua zake zilijawa na machozi ni machozi pekee yanayoweza kutuinua juu, kwani
machozi ni Ishara ya kushuka kwetu chini nana kuinyesha namna na jinsi
tunavyomuhitaji Mungu, Na Mungu kamwe hatakuja ayadaharu machozi yetu, Hisia zetu
ni sehemu kamili ya hali zetu za kiroho pia na zinaweza kutumika katika maombi
na kuabudu, ni shara ya kuwa tunaweza kuzama ndani nzaidi na kujielezea na
kujipambanua kwa Mungu wetu, Mungu huyaiona machozi yetu na anasukumwa kufanya
jambo, na siku moja atayafuta machozi yetu yote kwa hiyo hatupaswi kuona aibu
kulia lakini tuyatoe machozi yetu kwa imani na Mungu atayageuza machozi yetu
kuwa kichezo.
1Samuel 20:41 “Basi mara
alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na
kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana,
wakaliliana, hata Daudi akazidi.” Daudi alikuwa na upendio wa ajabu
sana yeye a rafiki yake Yionatahan walipokuwa wakiagana walilia lakini Daudi
alilia zaidi
1Samuel 24:12-16 “Bwana
atuamue, mimi na wewe, na Bwana anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono
wangu hautakuwa juu yako.Kama vile walivyosema watu wa kale katika mithali yao,
Katika waovu hutoka uovu; ila mkono wangu hautakuwa juu yako. Na mfalme wa
Israeli ametoka ili kumfuatia nani? Unamwinda nani? Ni kuwinda mbwa mfu, au
kiroboto. Basi Bwana atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno
langu, akaniokoe na mkono wako. Ikawa, Daudi alipokwisha kumwambia Sauli maneno
hayo Sauli alisema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Naye Sauli akapaza
sauti yake, akalia.” Daudi alikuwa na uwezo wa kujieleza na kusimamia haki katika
kiwango ambacho kingeweza kumfanya mtu alie machozi Sauli alilia kwa sababu
Daudi alikuwa amemueleza ukweli kile ambacho angewza kumfanyia lakini alikuwa
amemuachia Mungu aingilie kati uadui wao.
1Samuel 30:1-8 “Ikawa, Daudi na
watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa
wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; nao
wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo
wote, ila wakawachukua, wakaenda zao. Basi Daudi na watu wake walipoufikilia
mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa
wake, wamechukuliwa mateka. Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua
sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. Na hao wake
wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na
Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. Naye Daudi akafadhaika sana; kwa
sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao
watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini
Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. Kisha Daudi akamwambia
Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera.
Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. Daudi akauliza kwa Bwana, akasema,
Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika
utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.” Daudi alipopatwa na fadhaa alilia lakini npia
alimuomba Mungu na kupata suluhu ya mahitaji yake alijua umuhimu wa Machozi
kama atayaunganisjha na maombi alijitia nguvu na Mungu alimsikia na kujibu
maombi yake
Daudi alilia
sana siku alipokufa Sauli na Yonathan na
kufunga kwaajili ya kuomboleza
2Samuel 1:11-12 “Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.”
2Samuel 1:11-12 “Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.”
Daudi alilia
machozi siku alipokufa Abneri 2Samuel
3:31-33 “Kisha
Daudi alimwambia Yoabu, na watu wote waliokuwa pamoja naye, Rarueni nguo zenu,
mkajivike nguo za magunia, mkamlilie Abneri. Naye mfalme Daudi akaifuata
jeneza. Wakamzika Abneri
katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao
watu wote wakalia. Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje
Abneri kufa afavyo mpumbavu?”
Daudi alilia
machozi alipokuwa akipambana kivita na mwanae Absalom na Mungu alisikia dua
yake 2Samuel 15:30 “Daudi akapanda
akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye
alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa
pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia
walipopanda”.
Daudi alilia
vilevile aliposikia ya kuwa mwanae amefariki
2Samuel 18: 33 “Naye mfalme
akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango,
akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu!
Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!”
Lia kwa Mujibu wa Kanuni za Mungu
Kama ukikiuka
kanuni za kimungu kisha ukalia tu kuna aina za kilio Mungu hatasikiliza mfano Esau
aliuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kisha baadaye akaanza kuulilia Mungu
hakumsikiliza, Kwa sababu Mungu alikuwa ni shahidi wa Mwanzo 27:34-35 “Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha
uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu. Akasema,
Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako”. Esau alikuwa
maeuza urithi wake wa mzazliwa wake wa kwanza na alimuapia Yakobo kwa Mungu
hivyo Mungu alikuwa ni shahidi wa kile alichokifanya hivyo kilio cha Esau
kilikuwa kiko na kinyume na maswala ya haki kwa kile alichokifanya, aidha kama
tutadumu sana katika dhambi na kuwa na tabia ya kurudia rudia makosa yale yale
unaweza ukafika wakati Waamuzi 10:10-16 ”Ndipo wana wa Israeli wakamlilia Bwana, wakisema, Sisi
tumekufanyia dhambi, kwa sababu tumemwacha Mungu wetu, na kuyatumikia Mabaali. Naye
Bwana akawaambia wana wa Israeli, Je! Sikuwaokoa ninyi na hao Wamisri, na
Waamori, na wana wa Amoni, na Wafilisti? Hao Wasidoni nao, na Waamaleki, na
Wamaoni, waliwaonea, nanyi mlinililia, nami niliwaokoa na mikono yao. Lakini
mmeniacha mimi, na kuitumikia miungu mingine; basi kwa ajili ya hayo mimi
sitawaokoa tena. Haya, endeni mkaililie hiyo miungu mliyoichagua; na hiyo iwaokoe
wakati wa kusumbuka kwenu. Wana wa
Israeli wakamwambia Bwana Tumefanya dhambi; utufanyie yote uyaonayo kuwa ni
mema; lakini tuokoe, twakusihi, siku hii ya leo, haya tu. Nao wakaiondoa hiyo
miungu ya kigeni iliyokuwa kati yao, nao wakamtumikia Bwana; na roho yake
ilihuzunika kwa sababu ya msiba wa Israeli.” Kama tunataka kumuona
Mungu katika maisha yetu kupitia machozi yetu ambayo Mungu huyaheshimu sana ni
lazima tuhakikishe kuwa tunalia katika kanuni za Mungu yaani tutubu na kuyaacha
makosa yetu na kukaa katika kanuni zake kisha yanapoibuka maswala magumu na
kuliitia jina la Mungu, Mungu ataonekana katika maisha yetu na kututokea na ile
nguvu ya machozi tutaiona waziwazi.
Siri
iliyofichikakatika machozi.
Mungu hatakuja
kuyadgarau machozi yetu tunapougua Zaburi
51:17 “Dhabihu
za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu,
hutaudharau.”
Mwisho wa Machozi:
Ufunuo
21:4-5 “Naye atafuta kila
chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala
kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha
kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya
yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.”
Na Rev, Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Maoni 2 :
Asante mchungaji umeigusa nafsi angu mungu akutie nguvu
Asante Mungu akubariki mtumishi
Chapisha Maoni