Zaburi 52:8 “Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.”
Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu
katika hekima yake alipouumba ulimwengu, aliiuumba ili uwe zawadi kubwa kwa
wanadamu, na aliweka miti na mimea
kwaajili ya uhai na utatuzi wa matatizo ya kiafya kwa wanadamu, kwa msingi huo
basi utaweza kuona kuwa, Miti ina uhusiano mkubwa wa uhai maisha na hata nafsi
ya mwanadamu Lakini miti pia ina uhusiano wa kiroho na maisha ya mwanadamu. Mungu
aliitoa miti na mimea kama zawadi kwa wanadamu kwaajili ya kunufaisha maisha
yao ona Mwanzo 1:29 “Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu,
ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu;
vitakuwa ndivyo chakula chenu; “
Katika miti au miche ambayo ilitolewa kama zawadi kwa wanadamu moja ya mti wa ajabu sana wenye nguvu za mwilini na rohoni ni mti wa Mzeituni, mti huu ni malimbuko ya amani ya dunia ni ni mti wa kwanza kutajwa mara baada ya gharika wakati wa nabii Nuhu, ukiacha mti wa mtini ambao ulitajwa mapema sana mara baada ya anguko la mwanadamu ona Mwanzo 8:6-12 “Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani. Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.”
Mungu aliweka uwezo wa ajabu
katika mti huu, na miongoni mwa miti inayofanya kazi ya kuleta heshima kwa
Mungu na wanadamu Mzeituni ni mojawapo ni mti
wa kwanza katika miti hiyo maarufu ya kibiblia angalia Waamuzi 9:8-12 “Siku
moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti
mzeituni, Tawala wewe juu yetu. Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache
mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende
nikayonge-yonge juu ya miti? Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu
yetu. Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu
mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti? Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo
wewe, utawale juu yetu.”
Sifa za mti wa Mzeituni!
Moja ya sifa ya mti wa Mzeituni ni kuwa ni mti wenye uwezo mkubwa sana wa kustahimili ukame, lakini ni mti usioweza kufa, ni mti wenye uwezo wa kufufuka, mizizi yake ina uwezo mkubwa sana wa kwenda chini na kujiunganisha na maji, kwa sababu hiyo sio rahisi kuuua mzeituni, ukitaka kuuua lazima uchomoe mizizi yake na kuitenganisha na maji huko ardhini, hapo ndipo utaweza kuua, unaweza kuifyekelea mbali lakini baada ya muda fulani unachipua tena!
Mti huu ulitumika nyakati za Agano la kale kusimika watu waliokusudiwa kuwa watumishi wa Mungu katika Nyanja mbalimbali, kama Wafalme, Makuhani na manabii, ili mtu aweze kumtumikia Mungu katika nafasi hizo alipakwa mafuta ya mzeituni kwa maelekezo ya Mungu na maisha ya mtu huyo yalibadilika sana, Makanisa makubwa ya zamani kama Anglican na Kanisa Katoliki huyatumia mafuta ya mzeituni katika ibada za kipaimara na wakati wa kusimika viongozi wa kanisa wakiwemo makuhani wa madhehebu hayo, hii ni kwa sababu wanakumbuka huduma za kikuhani za kupoaka mafuta zilizokuwa zikifanywa na makuhani au manabii nyakati za agano la kale mifano ifuatayo itakusaidia kuelewa uhusiano wa kiroho ulioko kati ya mwanadamu na upako wa mafuta ya mzeituni unaokaribisha nguvu za Mungu Roho Mtakatifu! Ona
1Samuel 10:1-7 “Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu? Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri; na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE. Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.”
1Samuel 16:1-13 “Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako. Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani? Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu. Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu. Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na ROHO YA BWANA IKAMJILIA DAUDI KWA NGUVU tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.”
Katika Agano jipya ishara ya kupakwa mafuta inaweza kuwa mafuta halisi ya mzeituni au kuwekewa mikono na mtumishi wa Mungu aliyepakwa mafuta aliyewekwa wakfu, sio lazima yawe mafuta kama yale yaliyokaa katika pembe lakini Mchungaji aliyepakwa mafuta anaweza kukuwekea mikono na kutamka kusudi la kukuwekea mikono na ikawa sawa kabisa na kupakwa mafuta, lakini hata akikupaka mafuta halisi ya zeituni, bado uweza utakuwa uleule wa kuwekea mikono au kupakwa mafuta, Ndio maana Yesu hakuwekewa mikono lakini alipakwa mafuta na Mungu mwenyewe mara baada ya kubatizwa na Yohana Mbatizaji, mtu anapowekwa wakfu kwa kupakwa mafuta anakuwa mtu mwenye uweza wa kiungu ndani yake na kumfanya kuwa mtu wa tofauti! Ona tangazao la Yesu la kuwa mpakwa mafuta;-
Luka 4:18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu,
Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha
huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”
Mungu anaporuhusu katika kanuni
zake uwekewe mikono au upakwe mafuta unakuwa na uweza wa kiwokovu ndani yako na
mungu anakupoa neema inayokuwezesha kuwatetea wengina na kutimiza majukumu yako
ambayo Mungu anakuwa ameyakusudia
Mzeituni umeao katika
nyumba ya Mungu!
Zaburi 52:1-9
Kwa
nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.
Ulimi
wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
Umependa
mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.
Umependa
maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.
Lakini
Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako;
Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
Nao
wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka;
Kumbe!
Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake.
Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya
hodari kwa madhara yake.
Bali
mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu.
Nazitumainia
fadhili za Mungu milele na milele.
Nitakushukuru
milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya
wacha Mungu wako.
Katika msitari wetu wa Msingi Mwandishi anaonyesha ya kuwa yuko mtu wa hila, mtu mwenye kiburi mwenye uwezo wa kupoteza watu, muovu inaonekana mtu huyu ana madhara ni hodari na mwenye nguvu, anawaandama wanadamu anapigana nao ana hila bila shaka ni wazi kabisa mtu huyu ni Ibilisi anasimama kushindana na makusudi ya Mungu ndani ya kila mmoja wetu anataka kutuahribia anataka kutuumiza anataka kuweka jeraha katika mioyo yetu, anataka tushindwe, anazuia mafanikio yetu, anapoingana na makusudi ya mungu ndani yetu na ndani ya mwandishi wa zaburi hii ambaye ni Daudi. Mwandishi anamkumbusha mtu huyo (Shetani) kuwa Yuko Mungu mwenye nguvu kushinda yeye, anauwezo wa Kumuharibu milele, anauwezo wa kumfutilia mbali, na ana uwezo wa kumng’oa na Daudi anatabiri kuwa wenye haki watamcheka! Watashangaa kwanini mtu huyu wa kiburi hakumfanya Mungu kuwa nguvu yake? Kwa nini alitumainia mali zake na kujifanya hodari kumbe hana nguvu! Daudi anaeleza kuwa mtu anayemtegemea Mungu anayeutumainia wema wa Mungu anayetambua kuwa Mungu ni mwema siku zote yaani hata wakati wa nyakati ngumu au ndani ya jambo gumu bado Mungu ni mwema tu! Hao ni sawa na Mzeituni uliopandwa katika nyumba ya Mungu, yaani wale wanaomtegemea Mungu na kuzitumainia nguvu zake watamea katika nyumba ya Mungu yaani katika uwepo wa Mungu watastawi watahuishwa, kwa sababu wanategemea fadhili za Mungu wanalitizamia jina lile jema yaani jina la Yesu, hawa hawatatikiswa wala hawataogopa, wakikatwa wanachipua tena! huwezi kuwazibia wameunganishwa mizizi yao na chemichemi ya uzima na chanzo cha uhai ambaye ni Mungu!, watu walioungwa na chemichemu ya uzima wanautazamia wema wa Mungu siku zote Zaburi 52:1, hao hawawezi kutikiswa hawaogopi wana jina wanalolitumainia wanakaa katika uwepo wa Mungu wanazitumainia fadhili za Mungu milele na milele hawa ni watu wasiowezekana
Ndugu tunalo tumaini lisiloweza kutikiswa sisi ni kama Mzeituni unaomea katika nyumba ya Mungu. Kila anayemtegemea Mungu na anayezitegemea fadhili zake hapaswi kuogopa, hatupaswi kufadhaika maana sisi kama ilivvyo kwa daudi ni mzeituni unaomea katika Nyumba ya Mungu, Mizeituni huwa haifi, mizeituni huwa inadumu milele, mizizi yake imeungwa na chemic hemi za chini sana za maji, ili tutoweke ni mpaka wachomoe mizizi inayotuunganisha na fadhili za Mungu, Usiogope!
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni