Matendo 27:23-25 “Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye
mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia,
Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu
amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu
namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.”
Utangulizi:
Ni muhimu
kufahamu kwamba ustawi wa nafsi zetu na usalama wa roho zetu ulinzi na muelekeo
wa maisha yetu unategemeana sana na Mungu yule Tunayemuabudu! Hili ninjambo la msingi sana, tunaweza kuwa
na mtazamo tofauti, tabia tofauti na mwenendo tofauti, na tukawa tunajiamini
sana au tukawa na hofu lakini kwa vyovyote vile kila kitu na kila jambo matumaini yetu na kujiamini kwetu kwenye
kupita kawaida kunategemeana sana na Mungu tunayemuabudu, au kwa lugha nyingine
uhusiano wetu na Mungu tunayemuabudu! Angalia maandiko yafuatayo kisha kuna
kitu utagundua!
1.
Mwanzo 15:1 ” Baada
ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope,
Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”
2.
Mwanzo 31:24 “Mungu akamjia Labani,
Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno
la heri wala la shari.”
3.
Matendo 8:9-10 “Bwana akamwambia Paulo
kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa kuwa mimi ni pamoja
nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina
watu wengi katika mji huu.”
4.
Matendo 23:11 “Usiku ule Bwana
akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama
ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo
Rumi nako.”
5.
Zaburi 27:1-4 “Bwana ni nuru yangu na
wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama
yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga
kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo
nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae
nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na
kutafakari hekaluni mwake.”
Maandiko yote hapo Juu pamoja na
andiko la msingi yanatufundisha kwamba watakatifu waliotutangulia walikuwa na
ujasiri mkubwa sana, walijiamini, walithibitishiwa usalama wao, kwa miili yao
nafsi zao, ulinzi na kujaliwa kwa sababu walikuwa na uhusiano wa karibu na
Mungu wa kweli aliye hai na mwenye uwezo na nguvu za kuwalinda kuwatetea
kuwabariki na kutangaza hatima yao, hii maana yake ni nini? Maana yake ni
kwamba ustawi wetu katika Nyanja zote za maisha yetu unategemeana sana na Mungu
tunayemuabudu!. Paulo mtume alipookuwa safarini Rumi safari ambayo ilikuwa
imejawa na misukosuko mingi na hatari ya
kifo, Mungu ambaye Paulo anamuabudu na kumtumikia, Mungu wake alimtuma malaika
wake na malaika yule alimthibitishia usalama Paulo pamoja na watu wote aliokuwa
nao chomboni ona hii Matendo 27:23-25 “Kwa maana usiku huu wa leo MALAIKA WA MUNGU YULE AMBAYE
MIMI NI WAKE, NAYE NDIYE NIMWABUDUYE, alisimama karibu nami, akaniambia,
Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu
amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa
sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.”
Unaona Mtume Paulo ana uhakika wa kile alichoelezwa na malaika wa MUNGU YULE AMBAYE YEYE NI WAKE NAYE NDIYE
AMUABUDIYE kwa nini Paulo ansema haya kwa watu wale? Watu wale walikuwa
hawamjui Mungu ambaye Paulo anamuabudu
na kumtumikia, walikuwa wanaabudu miungu mingine, kwa hiyo hofu ya kifo na
mauti, kuhisi nuksi mikosi na balaa kuliwajaa kwa sababu hawakuwa na ufahamu
kwa habari ya Mungu aliye hai ambaye Paulo anamuita Mungu wake, na tena Mungu
ambaye yeye anamuabudu na kumtumikia, Mungu huyu sio tu aliyatunza maisha ya
Paulo lakini alimpa na maisha ya watu wote waliokuwa pamoja naye na hivyo
kwaajili ya Paulo nao walikuwa salama kwa sababu ya uhusiano uliokuwepo kati ya
Paulo na Mungu huyo!
Hii maana
yake ni nini ? maana yake ni lazima kila mmoja wetu awe na uhakika na Mungu yule
anayemuabudu, Maandiko yanakubali kuwa kuna miungu Mingi, Na Mungu mwenyewe
amewaonya watu wake kutokuwa na Mungu mwingine zaidi yake ona Kutoka 20:2-3 “Mimi
ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya
utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Unaona kama maandiko
yanakiri kuweko kwa miungu mingi, basi
kuna miungu mingi, lakini anayepaswa kuabudiwa ni Mungu mmoja wa kweli, kama
mwanadamu awaye yote atakuwa na uhusiano zege yaani uhusiano mzuri na mwema na
Mungu huyu wa kweli atakuwa salama katika ulimwengu huu na ule ujao
Je ni kweli Mungu yupo?
Ni muhimu
kufahamu kuwa Maandiko hususani neno la Mungu halifanyi kazi ya kuthibitisha
kuwa Mungu yupo au hapana, Neno la Mungu linatuhakikishia moja kwa moja kuwa
Mungu yupo na neno la Mungu linasema mtu anayewaza kuwa hakuna Mungu ni
mpumbavu Zaburi 14:1-2 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo
yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana
aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.”
Hakuna jaribio lolote katika maandiko linalojaribu kuithibitisha kuwa Mungu
yupo, kila amahali neno la Mungu limethibitisha kuwa Mungu anajulikana labda
mtu awaze upumbavu tu moyoni mwake Zaburi
53:1-2 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;
Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni
MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye
Mungu.”
Sasa basi
kama Neno la Mungu linaonyesha wazi kuwa asemaye au awazaye moyoni kuwa hakuna
Mungu ni mpumbavu tunawezaje kujua sasa ya kuwa Mungu yupo? Neno la Mungu
linaweza kutusaidia namna ya kujua uwepo wa Mungu na namna ya kutthibitishia
watu kwamba yeye yupo
1.
Kupitia uumbaji
Moja ya vitu ambavyo ninashangaza sana
wanadamu hata wale walio wabishi kuhusu uwepo wa Mungu ni uumbaji, uumbaji ni
uthibitisho wa wazi kuwa namna ulivyoumbwa na namna ulivyopangiliwa na ustadi
wake ni wazi kuwa uumbaji unatangaza uweza nguvu na utukufu wa Mungu maandiko yanasema Mbingu yaani solar system
inatangaza utukufu wa Mungu ona Zaburi
19:1-6 “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga
laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea
usiku maarifa. Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Sauti yao
imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo
ameliwekea jua hema, Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake, Lafurahi kama mtu
aliye hodari Kwenda mbio katika njia yake.Kutoka kwake lautoka mwisho wa
mbingu, Na kuzunguka kwake hata miisho yake, Wala kwa hari yake Hakuna kitu
kilichositirika.” Mwandishi anataka kutuelezea wazi kuwa mfumo wa
jua na mbingu na anga kama ukiuchunguza unaonyesha utukufu wa Mungu, yaani kama
vile tunavyoweza kuona na kushangaa vitu vilivyotengenezwa na wanadamu, na
tukavihusudu ni wazi kabisa kuwa tunaweza kuhusudu kazi na utendaji wa Mungu
wetu namna alivyoumba ulimwengu na hasa maswala ya anga
Uumbaji ni wenye kushangaza sana anga pekee
limewafanya watafiti kujikuta wakishangaa kwa miaka mingi, Mungu ameweka utaratibu
wa ajabu sana mawinguni ambao unawapa wanasayansi wakati mzuri wa kufanya
utafiti wa again kujifunza na kujua mwenendo wa kazi na utendaji wa Mungu ambao
ni dhahiri kila mtu anakubali kuwa ahuwezi kutokea kwa bahati mbaya tu!, ni
wazi kuwa kadiri wanasayansi wanavyofanya uchunguzi wa kina wanabaini na
kukubaliana na maneno ya mwandishi wa Zaburi 19:1 kwamba ni kweli Mbingu
zinahubiri utukufu wa Mungu!
Watafiti wa kisayansi wa chuo cha
Harvard wanasema mpaka sasa wamegundua
na kukubali kuwa kuna zaidi ya Galaxy yaani mfumo wa nyota au majua yaliyoko
katika mpangilio ambao unaonekana kama vumbi wa zaidi ya miliono 500 milions
Jua ambalo ni nyota iliyoko karibu na Dunia
ina kipenyo kinachokadiriwa kuwa na kilomita 1,392,000 na jua hilo linazunguikwa na sayari
zilizothibitishwa zipatazo nane na ya tisa ambayo iko mbali sana na mwenendo
wake bado unawachanganya watafiti kuibainisha kuwa ni sayari sayari hizo ni
pamoja na
Jina la sayari
|
Umbali kutoka juani
|
Muda wa kuzunguka jua Revolution
|
Muda wa siku Rotation
|
Number of Moons
|
Mercury
|
57.9 million km
|
87.96 siku
za dunia
|
58.7 siku
za dunia
|
0
|
Venus
|
108.2 million km
|
224.68
siku za dunia
|
243 siku
za dunia
|
0
|
Earth
|
149.6 million km
|
365.26
siku
|
24 hours
|
1
|
Mars
|
227.9 million km
|
686.98
siku za dunia
|
24.6 masaa
ya dunia
=1.026 siku ya dunia
|
2
|
Jupiter
|
778.3 million km
|
11.862
siku za dunia
|
9.84 saa
za dunia
|
67 (18
named plus many smaller ones)
|
Saturn
|
1,427.0 million km
|
29.456
siku za dunia
|
10.2 saa
za dunia
|
62 (30
unnamed)
|
Uranus
|
2,871.0 million km
|
84.07 siku
za dunia
|
17.9 saa
za dunia
|
27 (6
unnamed)
|
Neptune
|
4,497.1 million km
|
164.81
siku za dunia
|
19.1 saa
za dunia
|
13
|
Pluto
|
5,913 million km
|
247.7
miaka ya dunia
|
6.39 saa
za dunia
|
4
|
Unaweza
kuona itakuwa ni ujinga kama sio upumbavu mkubwa kudhani ya kuwa mfumo huu
umejiumba wenyewe Na ndio maana neno la
Mungu linaanza kwa kusema wazi kuwa Hapo mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na nchi
ona Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.”
Hii maana yake ni nini lazima kila mwadamu afikie kwenye hitimisho ya kuwa
yuko Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, haiwezekani kwa namna yoyote ile kwamba
itokee kwamba ulimwengu ulijiumba wenyewe baada ya miaka milioni nyingi sana
kama watu Fulani wanavyodhani
Kwa hiyo
unaweza kuwaza pale unaposema namwamini Mungu baba mwenyezi muumba wa mbingu na
inchi unaweza kupata picha ya Mungu yule tunayemuabudu na kumtumikia na kama
una uhusiano naye Mungu yule ambaye mimi/wewe ni wake “THE GOD WHOM I/YOU BELONG TO HIM” kwa hiyo tunaweza kutambua kuwa
Mungu yuko kwa kupitia uumbaji wake
2.
Kupitia Historia
Matukio mengo ya kihistoria duniani ni
ushahidi ya kuwa nyuma ya kila historia ziko nguvu za Mungu aliyehai, adhai
historia yote ya kibiblia imeandikwa kwa ajili ya kufunua nguvu na uweza wa
Mungu wa kweli, Mungu wa kweli amejifunua kwetu kupitria taifa la Israel kwa
hiyo ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa uwepo wa taifa hili ni ushahidi wa uwepo
wa Mungu, kutoka Israel kanisa lilizaliwa na neno la Mungu lilienea duniani
kote na ndio maana katika namna yenye kushangaza shetani amewahi kuwashawishi
mataifa kadhaa kutaka kujaribu kuiangamiza Israel au kuifuta Israel katika
ramani ya dunia, lakini mara kadhaa mataifa hayo yameshuhudia kushindwa vibaya
Israel ni kijiti inachowaka moto lakini hakiteketei ona Kutoka 3:2-3 “Malaika wa BWANA akamtokea,
katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile
kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa,
niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.” Maono
haya kitaalamu yalikuwa ni picha ya kinabii pia ya hali ya Israel ambayo
inapitia matesio ya aina mbalimbali lakini haiwezi kuteketezwa kwa sababu kile
kinazozaniwa kuwa moto, kibinadamu ni kwa sababu Israel imefunikwa na utukufu
wa Mungu;- tuangalie kwa ufupi historia
fupi ya vita mbalimbali za anga za Israel ambazo walishinda kwa sababu ya uwepo
na ulinzi wa Mungu Mungu amewafanya Israel kuwa hodari kweli kweli unaweza
kuona data hizo kutoka (www.israelairforec.org).
1948 –
wayahudi walipopata uhuru wakiwa kiasi cha wayahudi laki sita hivi kuhesabu
wanawake na watoto Waarabu wakiwa milion 80 walikusudia kuwa futilia mbali
lakini kwa uweza wa ajabu Israel Iliwapiga vibaya waarabu na kufanikiwa kupanua
mipaka yao kutoka Tell Avivi Jaffa mpaka ukanda wa gaza, milima ya Golan, na
kuuteka mji wa Yerusalem
1950 –
Wafaransa walikuwa ndio wafadhili wakubwa wa kuuza ndege za kivita kwa Israel lakini
katika vita ya Six days War Israel walionyesha kipigo kikali sana kwa maadui
ambacho wafaransa walisema kipigo hicho hakiwezi kusababishwa na ndege zao kwa
hivyo uhusiano na Israel kijeshi ulisimama kwani Israel walikuwa wakiziboresha
ndege hizo na zikatoa kichapo kikali
June 5 1967
– Israel kwa dakika 3 tu walizipiga ndege za maadui 451 zilizokuwa zimeandaliwa
kwa ajili ya kuifuta Israel ndege hizo mpya zilizonunuliwa na wamisri na
nyingine za Jordani na Syria
zilitandikwa vibaya na hivyo kupelekea Misri na Jordani kuweka mkataba
wa kudumu wa amani na Israel kuwa hawatapigana tena milele, mkataba huu
uliwafanya Israel kuipa Misri Jangwa la mlima Sinai, kwa masharti kuwa
hawatapigana milele
1969-1970 –
Ndege 111 za maadui ziliwekwa chini pamoja na msaada wa warusi katika vita hiyo
waarabu waliaibika
Jeshi la
anga la Israel limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na katika operation
mbalimbali waliweza kuwalenga viongozi wa kigaidi wa palestina kwa vipimo
vilivyoweza kuwapata na kuwaua mmoja mmoja viongozi hao ni pamoja na Abu ali
Mustafa, Ahmed Yasini na Abed al azizi Rant iss aliyeuawa punde akitokea
msikitini wakati wa ibada ya ijumaa
1976
walifanikiwa kuokoa wayahudi kadhaa
waliokuwa wakitishiwa kuuawa na Iddi amini dikteta aliyetawala Uganda katika operation
iliyoitwa operation Entebe
1991 – Jeshi
la anga la Israel lilifanikiwa kuwaokoa wayahudi wenye asili ya kiafrika huko
Ethiopia wanaoshukiwa kuwa ni watoto wa mfalme suleimani Katika operation iliyoitwa operation Solomon
Hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa Mungu yuko
nyuma ya mambo, Mungu amewahi kuwapigania Israel katika vita mbalimbali kwa
miujiza mikubwa sana, hii yote I nawatokea kwa sababu wanamuamini Mungu aliye
hai, aidha unaweza kusoma miujiza 17 ambayo Mungu amewafanyia jeshi la ulinzi
la Israel katika https://www.jewishvirtuallibrary.org/ Mungu
aidha anahusika pia katika kazi ya kuwekaau kuinua viongozi na kuwashusha
maandiko yana ushahidi kuwa hili ni swala pakee ambalo linafanywa na Mungu
nyuma ya kura na matakwa ya kawaida ya kibinadamu, Mungu anafanya kazi nyuma ya
historia, viongozi wa kisiasa na taasisi zozote duniani wanaonywa kuwa na
unyenyekevu na utambuzi ulio wazi kuwa Mungu yuko nyuma ya uwepo wao au
kutokuwepo kwao ona Zaburi ya 75:5-7 “Msiiinue
pembe yenu juu, Wala msinene kwa shingo ya kiburi. Maana siko mashariki wala
magharibi, Wala nyikani itokako heshima. Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili
huyu na kumwinua huyu.”
Daniel
2:20-22” Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe
jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili
majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima
wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; yeye hufunua mambo ya fumbo na ya
siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.”
Daniel
5:18-21 “Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye
juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu; na
kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha,
wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka
kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka
kumshusha, alimshusha. Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa
ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao
wakamwondolea utukufu wake. Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa
kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa
majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata
alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu,
na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.” Mungu yuko
nyuma ya kila Historia, Historia yoyote ile duniani ni Historia ya Mungu.
3.
Tunaweza kumjua Mungu kupitia jina lake!
Ni vigumu sana kumuelezea Mungu na
tukamuelewa vema bila kwanza kujua kuwa njia pakee ya kumjua Mungu ni kwa njia
ya imani Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu
amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale
wamtafutao.” Ni ili uweze kuwa na imani maandiko yanatuambia kuwa
imani chanzo chake ni kusikia yaani lazima usikilize mafundisho na sio kila
mafundisho yanaweza kuwa sahihi bali mafundisho kuhusu Kristo kwa sababu yeye
pekee ndiye anayeweza kumfunua Mungu kwetu ona Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni
kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Kwa hiyo ni neno la
Mungu pekee tena likifundishwa kwa usahihi linaloweza kutusaidia kumfahamu
Mungu na kumuamini, Mungu anazo sifa nyingi sana na amajifunua kwa wanadamu kwa
namna mbalimbali, na wanadamu walimpa Mungu majina kutokana na ufunuo ambao kwa
huo Mungu alijifunua kwao Westminster Catechism inamuelezea Mungu kuwa ni Roho,
Aelezeki, habadiliki, anajua yote, ana hekima yote, ana nguvu zote, ni
mtakatifu, ni mwema, ni mwenye haki, ni mkweli na kadhalika. Maandiko
yanamfunua Mungu kwa majina mbalimbali kutokana na aina ya jambo au kitu au
tukio ambalo Mungu alilifanya kwa mwanadamu au wanadamu Fulani kwa wakati huo,
nay eye mwenyewe amejidhihirisha kwa jina YAHWH
katika maandiko jina ambalo hata Ibrahimu na Isaka na yakobo hawakuwahi kulijua
wala kulipata ona
Kutoka 6:2-3
“Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni
YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi,
bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.” Mungu anajifunua kwa mara ya kwanza kwa jina
hili kwa Musa kwa sababu hapa alishuka kwa kazi maalumu ya UKOMBOZI hivyo jina
hili linadhihirisha kuwa yeye ni Mwokozi na hapa alikuwa ameshuka kuwasaidia
mwana wa Israel kukombolewa kutoka katika hali ya utumwa huko Misri Kutoka 3:6-9 “Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa
Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana
aliogopa kumwangalia Mungu. BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu
walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana
nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri,
niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa
na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi,
na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena
nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.” Ni wazi kuwa Musa
alitamani sana kumjua Mungu kwa kina na mapana na Marefu hata pamoja na ufunuo
huu aliomba amjue Mungu kwa undani zaidi lakini Mungu alimtangazia jina pana
zaidi ona Kutoka 34:5-7” BWANA akashuka
ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la BWANA.
BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma,
mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye
kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala
si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto
uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.“
kwa msingi huo ni wazi kuwa katika agano la kale jina la Mungu lilifichwa
na ilikuwa ngumu sana kwao kulitaja jina la Mungu au kulitumia bure au kukufuru
kwa jina hilo wayahudi waliliogopa na jina hili lilifichwa kwa kuwa Mungu
alikuwa anajifunua kwao kidogo kidogo Kutoka
20:7 “Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako,
maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.”
Walawi 18:21
“Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapitisha
kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.”
Walawi 24:16 “Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA
hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama
ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la BWANA atauawa”
Amri ya kuhakikisha kuwa jina la Mungu
linatukuzwa sio wayahudi pekee walioamriwa bali hata wakati wa agano jipya
katika mafundisho yake Yesu anataka jina hilo litukuzwe Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba
yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,”
Jina la Mungu lina uwezo wa kulinda watu wake
lima uwezo wa kuinua, lina uwezo wa kubariki Zaburi 20:1-6 “Bwana akujibu siku ya
dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu
pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali
dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri
yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke
bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote. Sasa najua kuwa Bwana amwokoa
masihi wake; Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu.Hawa wanataja magari na hawa
farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.” Na kwaajili
ya jina lake hawezi kuwatupa watu wake
1Samuel 12:21-22 “Wala msigeuke upande, maana,
kufuata vitu vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai
kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa
imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.” Kwa msingi huu tunaweza kuona umuhimu wa
jina la Bwana Mungu wetu na zaidi ya yote unaweza matumizi ya jina lake kwamba
ni lenye nguvu kubwa sana na msaada mkubwa kwa maisha yetu, Maandiko
yanaionyesha jinsi watu walibyimuita Mungu majina mbalimbali kwa sababu ya
ufunuo aliojifunua kwa watu wake
a. Elohim – Ni jina ambalo watu walimpa Mungu wakimtambua
kama Mungu mwenyezi muumba wa mbingu na ardhi ni jina la Mungu muumba jina hili
linatumika kwa wingi likionyesha kuwa Bwana Mungu yu katika wingi na huu ni
ufunuo kuhusu utatu wa Mungu elohimu inatumika katika maeneo kadhaa yafuatayo
mfano Mwanzo 1:26 “ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura
yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi
yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Na
limetumika pia katika eneo linguine Mwanzo
11:6-7. “BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa
moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa
hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie
usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao”
b. Yehovah – Ni jina ambalo Mungu mwenyewe alijitambulisha
kwa Musa alipokuwa ameshuka katika uwepo maalumu ili kuwasaidia wana wa Israel
kutoka utumwani,ukiacha kuwa ni jina la ukombozi pia linaonyesha kuwa ni Mungu
ashikaye maagano hasa kwa sababu ya utambulisho wake kama Mungu wa Ibrahimu,
Isaka na yakobo, jina hili pia lina maana ya aliyekuwako, aliyeko na
atatakayekuwako au niko ambaye niko kuonyesha umilelel wake Kutoka 6:2-3 “Kisha Mungu akasema na Musa,
akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama
Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.” Jina
hili Yehovah hata hivyo linasimamam na uaminifu au utendaji wa Mungu katika
kutoa neema na msaada kwenye eneo Fulani la maisha pale Mungu anapoleta msaada
kwa hivyo lilikuwa ni jina lisiloweza kusimama lenyewe bali lilionyesha
ukombozi katika eneo ambalo Mungu anataka kukusaidia au alikusaidia
c. Yehovah
Rapha – Ni jina linalotumika Pale Mungu
anapojifunua kwetu kama Mungu mponyaji
Kutoka 15:26 “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa
bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na
kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako
maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.”
d. Yehovah
Nissi – Ni jina linalohusiana na uwezo
wake wa kutupigania vitani, tunapokabiliwa na maadui au lolote lenye kuzia
makusudi ya Mungu kwetu Mungu kama Yehovah Nissi ataingilia kati na kutupigania
kwa namna ya kipekee, yeye ameahidi kutupigania milele, awaye yote
atakayejifabya adui kwetu Mungu atakuwa adui kwake na atatusaidia katika vita
maana yeye ni Bwan wa vita ona Kutoka
17:8-16 “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana
na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke
upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya
Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa
alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya
kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha
mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi
wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza
mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika
hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa
upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho,
kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki
kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake
Yehova-nisi; akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi
baada ya kizazi.”
e. Yehovah
Shalom – Ni jina la Mungu lenye uhusiano
na kujali kwa mungu na namna Mungu anavyotoa ustawi wa mwanadamu, ni Mungu anapojihusisha
na kutupa amani Waamuzi 6:24 “Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita
jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”
f.
Yehovah Ra’ah – Ni jina la Mungu anapojihusisha na kuyalinda
maisha yetu, na kujihusisha na utoshelevu wetu Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.”
g. Yehovah
tsidkenu – Jina linalotumika pale watu
wanapotuhukumu na kutuona kama wenye hatia kwa sababu kadhaa au pale dhamiri
zetu zinapohitaji kutiwa moyo kutoka katika hatia Mungu hufanyika kuwa haki
yetu Yeremia 23:6 “Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa
salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.”
h. Yehovah Yire
– Ni jina la Mungu
anapojidhihirisha kama Mungu ambaye anakutana na mahitaji yetu Mwanzo 22:14 “Ibrahimu
akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa
BWANA itapatikana.”
i.
Yehovah Shammah – Ni jina la Mungu linalodhihirisha uwepo wake
BWANA YUPO HAPA Ezekiel 48:35 “Kuuzunguka ni mianzi kumi na nane elfu; na jina la mji
huo tangu siku hiyo litakuwa hili, Bwana yupo hapa.”
Ni muhimu kufahamu kuwa pia jina
El ambalo pia hutumika kwa utukufu wa Mungu pia ni jina lisiloweza kusimama
lenyewe El ni Mungu lakini hutumika na muunganiko wa maneno mengina katika
kulikamilisha kama ilivyo kwa jina lile Yehovah
j.
El-Elyon – Mungu
aliye juu sana Mwanzo 14:18-20 18. “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai,
naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na
abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye
juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la
vitu vyote.”
k. El-Shaddai –
Mungu muweza yote mwenye
kutekeleza mahitaji ya watu wake Kutoka
6:6-7 “Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni
YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa
na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa
mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.”
l.
El-Olam – Mungu
wa Milele Mwanzo 21:33 “Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko
jina la BWANA Mungu wa milele.” Aidha majina mengine ya Mungu ni
pamoja na
m. Adonai –
maana yake Bwana au mttawala Kutoka 23:17 “Mara
tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya BWANA MUNGU.”
n. Baba – Abba
Mwanzilishi wa kila kitu Muumba au sababu ya kuwepo kwetu Matendo 17:28 Kwa
maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile
mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Japo hii haituhakikishii wokovu bila kufuata
kanuni ya kumuamini Yohana 1:12-13 “Bali
wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili,
wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”
SIFA ZA
MUNGU
1. Mungu
anatajwa katika maandiko kuwa ni roho
Yohana 4:24 “Mungu
ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
Tunaposema kuwa Mungu ni roho
maana yake ni kuwa Mungu Baba hana mwili wa kibinadamu, Lakini mwana wa Mungu
Yesu Kristo alikuja Duniani akiwa katika mwili ona Yohana 1:1-2, 14 “Hapo mwanzo kulikuwako
Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo
alikuwako kwa Mungu. 14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona
utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na
kweli.” Kutokana na tendo hiliLa Mungu mwana kuwa na mwili wa
kibinadamu Yeye amejulikana kama Emmanuel yaani Mungu pamoja nasi Mathayo 1:23 “Tazama,
bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli;
Yaani, Mungu pamoja nasi. “
Mungu anapopewa sifa za
kibinadamu hutumika lugha inayoitwa Anthromorphism – ili kusaidia kuleta uelewa
kwa wanadamu, kwa msingi huo Biblia inatoa aina Fulani ya matamshi yenye
kuashiria au kumfananisha Mungu na utendaji wa kibinadamu!
Mfano Isaya 59:1-“Tazama, mkono wa Bwana
haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze
kusikia;” hapo Munu anatajwa kama ana mkono na ana sikio
2Nyakati 16:9 “Kwa
maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu
kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda
upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.” Na pia
Kumbukumbu 33:27 “Mungu wa milele ndiye makazi
yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui;
Akasema, Angamiza.” Lugha hizi zote ni lufgha zenye kumuelezea Mungu
katika namna ya kibinadamu ili kutusaidia kumuelewa Lakini Mungu ni Roho na si
mwanadamu!
2. Mungu hana
mipaka “infinite” no limitation
Ni mungu ambaye yuko mahali kote
kwa wakati mmoja kwa msingi huo hawezi kutenganishwa na umbali au mahali 1Wafalme 8:27 “Lakini
Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala
mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga! “ Lakini neno hilo pia
linatumika kumuelezea Mungu kama Mungu wa milele Muda hauna uwezo wa kumfunga
yeye yuko tangu milele na milele ona Kutoka
15:18 “BWANA atatawala milele na milele.” Kumbukumbu
33:27 “Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono
ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema,
Angamiza.” Zaburi 90:2 “Kabla haijazaliwa
milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.”
3. Mungu ni
mwema
-
Ni mwenye
upendo na huruma isiyoweza kuelezeka
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele”.
-
Zaburi 69:16 Ee “Bwana,
unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee”.
-
Warumi 8:38-39 “Kwa
maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika,
wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala
kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika
Kristo Yesu Bwana wetu.”
4. Mungu ni
Mtakatifu!
-
Sifa ya
utakatifu ni suifa ya Mungu pekee, hakuna mwanadamu mtakatifu wala mkamilifu
wanadamu wote wana mapungufu Muhubiri
7:20 “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa
duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.”
-
Hakuna
mwanadamu mwenye haki hata mmoja mbele za Mungu mpaka kwa neema yake tu ona Warumi 3:10-12, 23-24 “kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata
mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote
pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. 23. kwa sababu wote wamefanya dhambi,
na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24. wanahesabiwa haki bure kwa neema yake,
kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;” Ni Bwana Mungu wetu
tunayemuabudu aliye mtakatiu sana ona
Isaya 6:1-4 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia
nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa
sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. Juu yake walisimama maserafi;
kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili
alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. Wakaitana, kila mmoja na mwenzake,
wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote
imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti
yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.” Ufunuo 15:4 “Ni
nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u
Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa
matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.”
-
Maandiko
yanatoa wito kwa watu wote kuwa watakatifu kama Baba Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa
na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao; 1Petro 1:15-16 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi
iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa
watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”
5. Mungu ni
Mungu mwenye haki (Righteous and Just)
-
Kutokana na
haki yake hataruhusu wadhalimu kuingia katika ufalme wake 1Wakoritho 6:9-10 9. “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu?
Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu,
wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala
walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.”
6. Mungu ni
mkweli na Muaminifu
-
Isaya 25:1 “Ee
Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa
umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.”
-
Ufunuo 3:14 “Na
kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye
Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.”
-
Warumi 3:4 “Hasha!
Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike
kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu”.
-
Ahadi zake zote ni ndio na kweli Waebrania
10:23 “Na mlishike sana ungamo la tumaini letu,
lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;”
7. Mungu ni
mtoaji (He is a giving God)
-
Mungu ametupa kila kitu, kila kitu duniani ni
chetu, Mwanzo 1:28-31 “Mungu akawabarikia, Mungu
akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki
wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya
nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa
nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo
chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani,
na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche,
ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu
akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa
asubuhi, siku ya sita.”
-
Ametupa maandiko 2Timotheo 3:16. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,
na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika
haki;”
-
Ametupa mwana wake wa pekee Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele. Ona pia Warumi 8:32”Yeye asiyemwachilia
Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje
kutukirimia na mambo yote pamoja naye? “
-
Anatupa Roho wake Mtakatifu Luka 11:13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu
vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao
wamwombao?
-
Nguvu za kupata utajiri Kumbukumbu 8:18 “Bali utamkumbuka
Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye
imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo”-
-
Anatoa neema kwa wanyenyekevu 1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi
nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga
wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
-
Hutupa Hekima kama tukihitaji Daniel 2:23 “Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu,
uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana
umetujulisha neno lile la mfalme. “
-
Mungu ni mkuu
a. Anajua yote
Omniscient – Warumi 16:27 “ Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa
Yesu Kristo, milele na milele. Amina. 1Samuel 2:3 Msizidi kunena kwa kutakabari
hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na
matendo hupimwa na yeye kwa mizani.”
b. Yu mahali
kote Omnipresent – Zaburi 139:7-12 “Niende wapi
nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na
kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono
wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru
inizungukayo ingekuwa usiku; Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza
kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa. “
Yeremia 23:24“Je,
mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu
na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana.”
c. Mungu ni
mwenye nguvu zote Omnipotent – all powerful
o
Nguvu za uumbaji Power of Creation Mwanzo 1:1
“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Wakolosai 1:16-17 “Kwa
kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,
vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi,
au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye
amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye”.
o
Ana nguvu za kuokoa - Isaya 50:2-3 “ Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona
hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa?
Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari,
mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji,
nao wafa kwa kiu. Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa
kifuniko chao.” Mungu ni
mwenye uwezo wa kuokoa na ni mwenye uwezo
wa kutukomboa, anasema katika Isaya kuwa ana uwezo wa kuikemea hata
bahari jambo ambalo liliwatishia sana
wanafunzi wa Yesu waliokuwa wanalijua andiko hili vema na kisha Masihi
akaikemea bahari mbele yao nayo ikatii ona
– Marko 4:39-41 ”Akaamka, akaukemea upepo,
akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Wakaingiwa na hofu kuu,
wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?”
o
Hakuna jambo
lolote lililo gumu la Kumshinda yeye
Yeremia 32:17 “Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe
umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa;
hapana neno lililo gumu usiloliweza;”
d. Mungu ni wa
milele
o
Amekuweko tokea enzi na enzi ona Zaburi
90:1-2 “Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi
baada ya kizazi.Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele
hata milele ndiwe Mungu.”
o
Yeye ni Mwanzo na mwisho Alfa na omega Ufunuo
22:13 ” Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa
kwanza na wa mwisho.”
o
Yeye
mwenyewe anasema kabla yake na baada yake hakuna mwingine ona Isaya 43:10-11 ”Ninyi
ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na
kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote,
wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi
yangu mimi hapana mwokozi.”
e. Mungu hana
kigeugeu
o
Waebrania 13:8 “Yesu
Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.”
o
Yeye sio kama kivuli kinageuka geuka Yakobo
1:17 “ Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho
kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna
kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. “
8. Mungu ni
Mkamilifu!
Tuwapo duniani kama wanadamu na
kutokana na hitilafu ya kuwepo kwa dhambi Duniani kumekuwepo na mapungufu mengi
sana wakati mwingine tunaweza kufikiri kuwa labda huenda muumba amekosea au
kuna namna anakosa ukamilifu, Lakini sivyo maandiko yanavyotusimulia kuhusu
Mungu, Mungu ni mkamilifu katika kazi zake zote na hakuna lolote analoweza
kukosea au kujuata, wala hakuna kutokukamilika kokote ambako amekuficha ni
mkamilifu katika sifa zako zote
-
Amekamilika
katika maarifa na ujuzi wake wote ona
Ayubu 37:16 “Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa
sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?”
-
Hakuna
lolote asilolijua ama linaloweza kufichika kwake lolote tulifanyalo hata kwa
siri sana anajua yote na anakumbuka vema mno anajua mpaka mawazo yetu na
Mapenzi yake ni kamili Warumi 12:2 “Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate
kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
-
Sheria yake pia ni kamilifu haina mapungufu
Zaburi 19:7 “Sheria ya Bwana ni kamilifu,
Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima.
-
Njia zake ni kamilifu Zaburi 18:30 “ Mungu,
njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote
wanaomkimbilia.”
-
Kazi zake ni kamilifu Kumbukumbu 32:4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote
ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.
-
Neno Ukamilifu “Perfect katika Kiebrania
linatumika neno “TAMIYM” Ambalo maana
yake isiyolaumika , isiyo na lawama without Blemish Katika kiyunani ni “TELIOS” maana yake Kamilifu
sawa na Sadaka ya mnyama ambayo Mungu aliagiza itolewe katika Walawi 23:17-18 17.” Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa,
itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na
chachu, iwe malimbuko kwa BWANA. Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza
wana-kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng'ombe mume mmoja,
na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA, pamoja na
sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza
iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.”
Faida za Kumjua Mungu!
Kwa nini
tunajifunza kuhusu Mungu? Kuna faida gani ya kujifunza kuhusu Mungu, Nguvu zake
na uwezo wake? Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema
yatakavyokujia.” Tunapopata nafasi ya kumtambua Mungu inakuwa rahisi
kwetu kustawisha uhusiano wetu na Mungu jambo ambalo litatufanya tuwe na uwezo
wa kutambua uwepo wake, kumuheshimu na kumuabudu na kujenga uhusiano mkubwa
sana na yeye! Paulo Mtume alikuwa na uhusiano mkubwa sana na Mungu jambo
lililopelekea awe na uwezo wa kupata taarifa za usalama wake kutoka kwa Malaika
wa Mungu, huku akizungumza wazi kwa wapagani, kuwa mungu huyo ni wake na ndiye
anayemtumikia Matendo 27:23-25 “Kwa maana usiku
huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye,
alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya
Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi,
wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile
kama nilivyoambiwa.”
1.
Kumjua Mungu na kumtumikia kunatupa imani
thabiti isiyo na shaka juu ya uwezo wake Daniel 3:16 -18 “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu,
wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama
ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto;
naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme,
ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya
dhahabu uliyoisimamisha.”
2.
Kumjua Mungu na kumtumikia yeye kunatupa
tofauti kati yetu na wapagani au watu wasiomjua Mungu Zaburi 20:7-8 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja
jina la Bwana, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na
kusimama.” Zaburi 46:1-2 “Mungu kwetu sisi
ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo
hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.”
3.
Uhusiano wetu na Mungu utaimarika atakuwa
Mungu wetu na tutakuwa watu wake ona Yeremia 30:19-22 “Tena
kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala
hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.Watoto wao nao
watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami
nitawaadhibu wote wawaoneao. Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye
mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye
atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema
Bwana. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”
4.
Kumjua Mungu kutafungua ukurasa wa maarifa
ambayo wengine hawana, ujuzi
kuhusu Mungu unauwezo wa kutupa aina ya maarifa ambayo wengine hawana Petro
aliwahi kupokea maarifa ya kipekee ambayo kwayo Yesu alijua isingekuwa rahisi
kuyajua au kuyapokea Bila kuwa na uhusiano na Mungu ona Mathayo 16:13-17 “Basi Yesu akaenda
pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana
wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine
Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena
mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa
Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa
mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”
5.
Kumjua Mungu kutatupelekea kufanya mambo
makubwa ya ajabu Zaburi 108:12-13 “Utuletee msaada
juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai. Kwa msaada wa Mungu tutatenda
makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu” Daniel 11:32 “Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa
maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na
kutenda mambo makuu.”
6.
Kumjua Mungu na kumtegemea Yeye kunatupa
uhakika wa usalama wetu Zaburi 91:1-,7 “Aketiye
mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.Nitasema, Bwana
ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye
atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake
atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na
kigao. Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo
gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako.
Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.”
7. Kumjua Mungu na kuwa naye kunatupa ujasiri
Yoshua 1:5 “Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza
kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa,
ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.”
Na Rev.
Innocent Kamote
Mkuu wa
wajenzi Mwenye Hekima!