Mithali 25:24, “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika
nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.” Mithali 21:9 “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika
nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.”
Utangulizi:
Mithali ni mojawapo ya kitabu
muhimu katika vitabu vya mashairi ya kiebrania, kama wengi wetu tunavyofahamu
kuwa katika tamaduni nyingi kwenye misemo na mashairi au nyimbo, watunzi wengi
huifadhi maneno ya maana na yenye uadilifu fulani kwa kusudi la kupeleka
mafunzo fulani katika jamii, kama Jinsi ambavyo tumeona hapa katika kitabu cha
Mithali, hapo juu, Katika kifungu au vifungu hivyo, Walengwa wa kifungu hiki
hasa wanaweza kuwa wanaume na wanawake pia! Na hasa vifungu vinaweza kuwa na
kusudi la kutoa ushauri au kuwafundisha wanaume ni mwanamke wa aina gani
anaweza kumuoa na wanawake jinsi gani na namna wanaweza kutumia ndimi zao na
kutunza hisia zao “TEMPER” zinazoweza kuondoa amani na utulivu katika
nyumba na sehemu nyinginezo, Tunapoendelea kujifunza somo hili AFADHALI
KAUKAA KATIKA PEMBE YA DARINI, Utagundua kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa
kila mwanamke kuchunga kauli zake katika mahusiano ya aina yoyote ile! Lakini
zaidi sana uhusiano wake katika ndoa. Lakini vilevile kuna maonyo makubwa sana
kwa wanaume kuwa kama kuna kitu ukikikosea wakati unakusudia kuoa kuna jambo
utakutana nalo. Kwa ufupi matumizi ya ulimi na udhbiti wa hisia zetu una faida
na ama hasara kubwa sana katika swala zima la mahusiano. tutajifunza somo hili
kwa kuzngatia vipengele kadhaa vifuatacyo:-
·
Maana ya Pembe ya darini
·
Afadhali kukaa katika Pembe ya darini
·
Mwanamke mgomvi!
·
Umuhimu wa kutunza amani ya moyo!
Maana ya pembe ya darini
Katika tamaduni za ujenzi wa kale
hasa katika jamii ya waarabu na wayahudi, walijenga nyumba za ghorofa ambazo
juu zilikuwa na dari au sehemu maalumu za kupumzikia, ambayo ilijengwa kwa
kusawazishwa juu, Pwani ya Afrika mashariki watakuwa na ufahamu kuhusu aina hii
ya ujenzi kwa sababu waarabu walipokuja mapema sana katika miji ya Kilwa,
Malindi, Mombasa, Zanzibar, Mafia na Sofala waliacha urithi wa aina hizo za
majengo na ambazo wenyeji pia waliigiza, Katika ujenzi huo juu waliweka dari na
dari iliweza kuwekwa aina fulani ya lami
na hivyo kupata eneo zuri na salama la kupumzikia, hata hivyo wakati
muafaka wa kukaa katika Pembe ya dari ulikuwa ni wakati wa hari yaani wakati wa
joto, wakati wa tufani, pepo kali na mvua na radi eneo hilo halingeweza kufaa
kwa kupumzikia.
Afadhali kukaa katika Pembe ya
Darini
Mwandishi wa kitabu hiki cha
Hekima anaona ni heri kukaa katika Pembe ya dari kuliko kukaa na mwanamke
mwenye kelele, Yeye mtazamo wake ni kuwa pale kwenye pembe ya darini pana
afadhali kukaa wakati wote ikiwa ni pamoja na wakati wa tufani na joto kali na
hata wakati wa mvua na radi kuliko kukaa katika nyumba pana na mwanamke mwenye
kelele, Nyumba pana inayozungumzwa hapa
ni zile ambazo ni kubwa na zina vyumba vingi na familia kubwa nyumba ya jamii, nyumba ambayo familia kubwa
wanaweza kukaa na kushirikiana nyumba ambayo ina mume mke na watoto yeye
anaiona nyumba hiyo kuwa ni nyumba isiyofaa kabisa kama atakuwepo mwanamke
mwenye kelele, yaani mwanamke mtawala, mkaidi, kimbelembele asiye na uvumilivu
mdadisi, mchunguzi mwenye kushuku, mchoyo, asiye na ushirikiano katika tendo la
ndoa mgomvi, mwenye luigha mbaya mwenye matumizi mabaya ya ulimi, kwa mwandishi
wa kitabu cha Mithali Mfalme solomoni anaona ni Kheri kukaa katika pemba ya
dari kuliko kukaa na aina hii ya mwanamke katika jumba la kifahari au wakati mwingine ni afhadhali uende nyikani
au jangwani kuliko kukaa na mwanamke huyo mgomvui ona
Mithali 21:19 “Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na
mwanamke mgomvi, mchokozi.” Mwandishi pia anaona afadhali kula ukoko
wa wali au ukoko wa mkate kuliko kwenye nyumba yenye karamu nyingi lakini haina
amani ona
Mithali 17:1 “Afadhali mego kavu
pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.”
aidha katiika
Mithali 19: 13 Biblia inasema hivi “Mwana
mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.”
Mwandishi
anazungumzia hapo ugomvi wa mke yaani mwanamke mwenye kelele ni kama kutona
tona neno hilo kutona tona katika biblia ya kiingereza ya The Amplified
Bible linatumika neno “continual
dripping” hali hii ni ngumu kuielezea kwa kizazi cha leo ambao wanaishi
kwenye nyumba nzuri zilizosakafiwa vema kila mahali lakini wale wenye umri wa
miaka kadhaa na waliowahi kuishi vijijini wanafahamu taabu ya nyumba inayovuja
hasa zile za nyasi au za makuti, unafahamu karaha ya kuishi katika nyumba
ambayo hapa panavuja na pale panavuja na kadhalika ile taabu ya kuishi kwenye
nyumba inayovuja daima ndio inaitwa kutona tona kwa hiyo kimsingi Sulemani
anaonyesha yale maudhi ya kukaa katika nyumba inayovuja ile hali ya kuishi kwa
mashaka na wasiwasi katika nyumba inayovuja inalingana kabisa na kuishi na
mwanamke mgomvi
Mwanamke mgomvi ni wa namna
gani?
Mithali hii ina maswala ya msingi
ya kuzingatia sana ona mwanamume aliyeoa hapa anatamani kukaa katika Pembe ya
darini au anaona ni afhadhali kukaa katika pembe ya darini juu npeke yake kuliko kukaa na mwanamke mwenye kelele au
mgomvi Mithali inaonekana kuwa yenye kutaka kuchukua ufahamu wetu wote uelekee
kwenye kitu kigeni na cha muhimu kwetu kujifunza yaani iweje jamaa aone kuwa
kwenye kona ya darini peke yake ni pazuri kuliko kukaa na mwanamke mwenye
kelele mgomvi, kuna tatizo kukaa katika kona ya darini ni maisha gani je ni
kweli panaweza kuwa na faraja? Bila shaka ni lugha ya kukuza jambo ili kutoa
umuhimu kwenye kitu mwandishi anataka kukiwasilisha na hiki si kingine ni
mwanamke mgomvi ni mwanamke mwenye kelelel huyu ni mwanamke wa namna gani?
Biblia ya kiebrania inatumia neno “MADON” inamaanisha mtu aliyejawa na
uchungu Biblia ya kiingereza inatumia neno
strife dissension yaani muasi, mwenye uchungu na asiyekubaliana au mwenye
mijadala na mpinzani unaweza kuona kwa
hiyo unapokuwa naye wakati wote kunakuwa
na mafuriko ya ugomvi
Mithali 17:14 “Mwanzo wa
ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.”
au kunapotokea ugomvi na kutokuelewana yeye hamalizi kwa haraka haachilii
hawezi kuacha kubwatuka na kusema na kusengenya
yuko kwaajili ya mashindano yuko kwaajili ya kulipiza kisasi ona
Mithali 18:19 “Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko
mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.” yaani ni aina
ya mwanamke ambaye wakati wote anakwaza au anakuwekea vikwazo na hii
inaambatana na ubovu wa moyo alionao na hisia mbaya, acha ya kuwa atakukwaza
kiasi ambacho hutakuwa na hamu ya kushirikiana naye hata tendo la ndoa,
atajificha katika silaha ya kulia na kujibanza kwenye kuamua kufungasha au
kukuletea aibu miongoni mwa watu wanaokuheshimu, atataka akuweke vikao
akupeleke kwa wachungaji au wazee wa kanisa au kwa wakwe kule ukasutwe mpaka
aonekane yeye ndio mshindi, ni aina ya
mwanamke mwenye wivu mkali sana akikuona umesimama na mwanamke tu hata bila
kujali ni wa rika gani na wa aina gani na mnazungumza nini mtajikuta mnaingia
katika ugomvi mkubwa , huyu kila kitu ni ugomvi hii ni dhambi mbaya sana ni
katika aina hii ya mwanamke ndio inaonekana kuwa ni afadhali kukaa katika pembe
ya darini na kuvumilia dhuruba na upepo na upweke kuliko jumba kubwa la karamu
na sherehe lakini na aina ya mwanamke kama huyu, aina hii ya mwanamke kwa
mujibu wa Sulemani ni msiba ukikaa naye, badala ya kuwa mpole na mwenye
kujinyenyekeza na mtii kwa mumewe kama maandiko yanavyoelekeza huyu ni mwanamke
mtawala, mwenye hasiram asiye na utulivu hawezi kuzuia hisia zake amejaa chuki na wakati wowote roho yake iko
tayari kwa majibu ya hovyo na kupambana na mumewe, ukiwa na aina hiyo ya
mwanamke ni heri kukaa katika pembe ya dari, eneo ambalo utatulia kimyaa na
utajisikilizia moyo wako kuliko kuwa na misiba kila wakati na majanga kila
wakati!
Mungu alimkusudia mwanamke awe
msaada mkubwa wa mumewe MSAIDIZI Neno Msaidizi limetumika pia kuelezea
ukaribu wetu na msaada tunaoupata kutoka kwa Mungu ROHO MTAKATIFU yeye hutusaidia, hujaziliza madhaifu yetu,
hutushauri hutuombea na kuleta msaada mwingi, kututeteta na kututia nguvu, kwa maana nyingine Mwanamke anatakiwa kuwa
msaada Mkubwa kama alivyo Roho Mtakatifu katika maisha yetu, kama umeokoka
unapojazwa Roho Mtakatifu unakuwa na ujasiri na unapokea nguvu ya ajabu na
mambo mengi yanaonekana kurahisishwa hata ukipitia magumu kwa uwepo wa Roho
Mtakatifu, wanaume hawapaswi kufikia
hatua ya kuamua kushinda ofisini, au kwenda kunywa kahawa na tangawizi mbali
kama watakuwa na mwanamke mwenye kuvutia,
Mithali hii inatufunza kwamba Lugha na matumizi ya ulimi na udhibiti wa
hisia kwa mwanamke ni jambo la maana sana mwanamke aliyepewa mume ni muhimu
sana kwa mumewe, kwamba mumeo atakuelewa au hata kuelewa maneno yako ni ya
muhimu sana na matendo yako pia wakati wote unapomkwaza mumeo na kuzungumza
maneno ya kejeli na kumkatisha tamaa unamuharibu mumeo kabisa kabisa na kumbomoa
mara 1000 kuliko mtu yeyote yule , sababu ya mtu yule kuona umuhimu wa kutulia
katika pembe ya dari ni kwa sababu anajisikia kuumizwa, anajisikia vibaya
anajisikia kuvnjika moyo, anakosa faraja ya kweli anaumizwa badala ya kupata
faraja kutoka kwa mwanamke, kusema kweli amani katika nyumba na ndoa yoyote ile
inaweza kupokea mabadiliko kama wanawake watajua nafasi zao, inawezekana ukawa
unasoma hapa halafu ukasema mkuu wa wajenzi anasema tu huyu hajui aina ya
mwanaume niliye naye! Angejua ! inawezekana kweli anakuudhi kweli ni kama
hakufai lakini alikufaa mpaka mkaoana na kuchumbiana najua kuwa kuna weza kuwa na maudhi ya hapa
na pale lakini hapa Biblia inamtaka mwanamke
awe mtulivu, amtiii amtie moyo na awe na lugyha nzuri hii itamuondoa
mumeo katika pembe ya dari, wengi waume zenu wako katika pembe ya dari,
hawataki hata kuwasikiliza, wako tayari kusikiliza mpira na kuzungumza na
wengine katika magroup ya mitandao ya kijamii wako tayari kuzungumza na wengine
kwa lugha ya upole na ubembelezi lakini kwako wanasubiri kufyaua maneno kama
risasi ili kujeruhiana, mimi nilikuwa nagombana sana na mke wangu mapaka wakati
mwingine nikawa nimezoea maisha ya ugomvi, mpaka nikawa mchokozi nasubiri
arushe neno moja tu nimtapikie mpaka anyauke ndio alinizoesha mwenyewe!, Lakini
nataka nikuhakikishie mwanamke akibadilika akawa katika nafasi yake ya ulaini
wa moyo, ulaini wa lugha ulaini wa ngozi ulaini wa sauti ulaini wa mapishi
ulaini wa kujali ulaini wa kukupmkea ulaini wa kila kitu mwanamke akikaa katika
uanawake kwelikweli Mwanaume atatoka gerezani, atatoka fgereji atatoka pangoni
atatoka kazini atatoka kwenye mpira atatoka kanisani, atatioka kwenye jumuia
atatoka kwenye simu na redio na television
ataondoka kwenye pembe ya dari na kuja kutulia na mkewe, haiwezekani nyumba
iwe kama ina wanaume wawili ndani haiwezi kuwa nyumba yenye kufaa tafadhali
wanawake kuweni wanawake kweli na sisi tutashuka darini na kuwasogelea!
Umuhimu wa kutunza amani ya
moyo!
Mithali hii pia inatumika kama
mafunzo kwa vijana hasa wale ambao hawajaoa inawakumbusha kuwa ni jambo baya
sana kuwa peke yako, Upweke na kuwa mwenyewe ni jambo baya kimaandiko Biblia
inasema si vema huyo mtu awe peke yake ona
Mwanzo 2;18 “BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake,
nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” ingawa sio vema mtu kuwa
mpweke lakini ni mbaya zaidia kama utaona mwanamke mgomvi mwenye kelele,
anayetajwa katika mithali hii, kwa hiyo mithali hii inakutaka ujiokoe mwenyewe
kuoa mwanamke mgumu kunaweza kuleta huzuni kubwa zaidi kuliko unavyoweza
kuwaza, usimkaribie kabisa mwanamke jeuri mwenye mijadala na asiyeweza kuzuia
hisia zake, Kuna namna ambayo Mungu ameumba wanakwake na kuna namna neno la
Mungu linavyomtarajia mwanamke awe Sulaimani ambaye amewahi kuwa na wanawake
wengi aliowaoa anaandika mithali hiii akiwaonya wanaume kujihadhari na mwanamke
wa aina hii, wanawake wengi wameharibu huduma za waume zao, maisha ya waume
zao, kazi za waume zao heshima za waume zao kwa sababu ya tabia mbaya isiyokuwa
ya kimaandiko
Mithali 12:4 “Mwanamke mwema ni taji ya mumewe; Bali aaibishaye ni kama
kuoza mifupani mwake.“
Mithali 14:1 “Kila
mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa
mikono yake mwenyewe”
Mithali 27:15-16
“Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na
mwanamke mgomvi ni sawasawa; Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake
wa kuume hukuta mafuta.”
Mithali 30:21-23 “Kwa
ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi
kuvumilia. Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula;Mwanamke
mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.”
~
Mithali 31:10-12 “Mke mwema, ni nani awezaye
kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.”
Mfalme Sulemani anaelewa
anachokiandika alikuwa na wake 700 na masuria 300, anajua namna mwanamke mkorofi anavyokua
anaonya vijana kuwa makini unapofika wakati wa kufabnya maamuzi ya kuoa siku
moja ya majuto na hasira za mwanamke inaweza kukuokoa wewe unayetaka kuoa, Ndoa
inaweza kuwa kaburi na ukajuta na
kutamani kutoka na kuwa single tena kuwa na mwanamke mkorofi ni msalaba mkubwa
sana mwanamke mgomvi, mwanamke mwenye
kukosoa kila kitu hana jema, mwanamke anayependa kugombana anayependa kukupinga
anayependa kushindana nawewe, asiyeridhika na kitu chochote, mwenye maswali ya
kila aina, mwenye kukukumbusha makosa ya nyuma, mwenye kisasi asiyesamehe,
mwanamke mwenye kumlaani mumewe, asiyetia moyo asiye na adabu, mwenye kiburi
mtawala Biblia inatoa maonyo kwamba ni afadhali kukaa kwenye pembe ya dari,
mwanamke yeyote utakayeoa na ukagundua kuwa hali yako ya kiroho inaharibika
baada ya kumpata, hali yako ya kuomba na kuabudu na upendo unaondoka na kuanza
kuwa katili mwanamke anayekufabnya ujute kwanini umeaoa ? huyo ndio mwanamke
ambaye biblia inasema hafai, huyu ni mwanamke asiyeweza kuitawala roho
yake anayependa kugombana na kusema leo
na mimi nimemkomesha ukizungumza naye anazungumza ukimweleza anakuja juu, sauti
yake inapanda kwa kiasi ambacho hata walio nje wanasikia mnavyozozana au
anaweza kuwa na kiburi mpaka ukatamani umpige , mwanmake asiyetosheka
aliyekinyume na kila kitu, na kila tukio na kuzungumzia vibaya kila kitu,
mgumu, hawapendi hata ndugu zako, wakati wote yeye ni kulaumu kila kitu
Mwanamke wa namna hiyo Biblia inasema hakufai na kwa vyovyote vila atakupeleka
kwenye pembe ya dari, hawa ni wanawake
watawala kama utakuwa umeoa mwanamke wa aina hii utakuwa umechelewa kujiokoa na
kifo na hasara vinakuhusu na ndio maana Sulemani anaonya kuwa wanaweza
kuionekana kuwa nadhifu na wazuri wakati wa uchumba lakini utakapoingia kwenye
agano naye umekwisha hawa kutokana na utawala wao wanaweza kukufanya ukashindwa
hata kumudu tendo la ndoa, Maisha yako ni ya muhimu sana jifunze kutokana na
maonyo, mke gani anashinda kwenye TV daima , mke gani anashinda anachati tu,
simu jmemnunulia wewe, vocha unaweka wewe na simu hiyohiyo na vocha hiyo hiyo
inatumika kukutukana jiokoe na maumivu, jiokoe na viumbe wa aina hiyo, ogopa
maumivu ya maisha, mwanagalie mama yake ni mwanamke wa namna gani, waulize
waliooa , kuwaa mwangalifu na kwanini uishi miaka karibu 50 na mtu
atakayeshinda anakuumiza tu tunza amani ya moyo wako!
Mwanamke wa Kikristo anapaswa
kujifunza na kuishi kwa upendo, na anapaswa kujua namna ya kujinyenyekeza kwa
mumewe anajua nafasi yake kimaandiko
1Wakoritho 11:8-9 “Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke
katika mwanamume.Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke
kwa ajili ya mwanamume.” Mwanaume hakuumbwa kwaajili ya mwanamke
bali mwanamke kwaajili ya mwanaume hivyo mwanamke wa Kikristo anapaswa kujua
wajibu wake anapaswa kuishi maisha ya kumpendeza mumewe ona
1Timotheo 2:13 “Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye”
Mungu alimuumba mwanaume kwaajili yake na wala sio kwaajili ya mwanamke hivyo
mwanamke wa kikristo anapaswa kuwa anayejipendekeza nakazia tena
anayejipendekeza kwa mumewe, ni lazima wakati wote ahakikishe anajiweka vizuri
anajaa neema ili aweze kuwa mwenye mvuto na mwenye kumpendeza mumewe
Mithali
11:16 “ Mwanamke
wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. “
mwanamke ni adabu bwana ! mwanamke unyenyekevu jifunze kutoka kwa Abigaili anajua kubembeleza mpaka mwanaume shujaa mwenye
hasira anayetaka kuua anakuwa mpole huu ndio uzuri ambao wanaume wa kweli
wanautafuta
1Samuel 25:21-35 “Basi Daudi
alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo
mtu huyu, asipotewe na kitu cho chote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya
badala ya mema. Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi,
nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka
asubuhi. Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya
punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi. Akamwangukia
miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu;
tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya
mjakazi wako. Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa,
yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake
ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana
wa bwana wangu aliowatuma. Basi sasa, bwana wangu, aishivyo Bwana, na iishivyo
nafsi yako, kwa kuwa Bwana amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi
mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya,
wawe kama Nabali. Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na
wapewe vijana wamfuatao bwana wangu. Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako,
kwa kuwa hakika Bwana atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu
bwana wangu anavipiga vita vya Bwana; tena uovu hautaonekana ndani yako siku
zako zote. Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi
yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na
Bwana, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka
kati ya teo.Tena itakuwa, hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu
sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli; hili
halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga
damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo Bwana
atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako. Naye
Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye
amekuleta hivi leo kunilaki; na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe,
uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu
mwenyewe. Kwa kuwa ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia
nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali
asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. Basi Daudi
akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani
kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso
wako”. Wanawake wacha Mungu sio kuwa wanapendezwa na kufurahishwa na
kila kitu kuhusu waume zao hapana wanawatii, wanawanyenyekea, wanawaheshimu
wanatumia busara kuishi nao, hawashindani nao ndio biblia inavyoagiza
Waefeso5:22-24
“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii
Bwana wetu.Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha
Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo
hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo”
Tito 2:3-5 “Vivyo hivyo na
wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye
kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana
akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa
safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili
neno la Mungu lisitukanwe.” Wanawake wacha Mungu sio wagomvi wala
jeuri wanajua kuutumia ulimi wao ona
Mithali
31:26 “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria
ya wema i katika ulimi wake.” 1Petro 3:1-4 “Kadhalika
ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa
mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa
hofu.Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na
kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika
mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu
mbele za Mungu”.
Ni wajibu wa kila mzazi wa
kikristo na mwenye kupenda uadilifu kumfunza mtoto wake wa kike nawa kiume
namna anavyotakiwa kuwa kupitia Mithali za Suleimani kwenye mithali kuna hekina
na maarifa na ujuzi utakaosaidia jamii katika maisha ya kawaida na ya kiroho,
kila kijana ajifunze kuhusu mke mwema na kujua anapaswa kuoa mwanamke wa namna
gani na kila mwanamke anapaswa kujivunza na kujikosoa au kumuiomba Mungu
ambadilishe ili asimpeleke mumewe kwenye pembe ya dari kuna faida kubwa sana za
kujifunza kupitia mithali za solomon
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni