Kumbukumbu 25:17-19 “Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.”
Moja ya matukio mabaya sana
ambayo Israel walitakiwa kuyakumbuka Daima ni pamoja na ukatili mkubwa waliofanyiwa
na wana wa amaleki (Amaleki). Musa analikumbuka sana tukio hili baya na la
kinyama na anawaandikia Israel na kumkumbusha Joshua kutokulisahau tukio hili
baya na la kinyama lililopata kufanywa
na Wamaleki!. Wana wa Israel walikuwa wamefanyiwa mambo ya kikatili sana katika
nchi ya Misri, waliteswa na kutumikishwa katika utumwa mkubwa na mzito kwa muda
wa zaidi ya miaka 400, waliugua na kulia na kibinadamu haingekuwa rahisi mtu
awaye yote kuwaondoa katika utumwa huo mzito isipokuwa tu pale ambapo Mungu
alikuja kuingilia kati unawezakuona.
Kutoka 3;7-10 “BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu
walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana
nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri,
niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa
na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi,
na Myebusi.Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena
nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. Haya, basi, nitakutuma sasa
kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”
Huu ndio ulikuwa mpango wa Mungu
na mapenzi kamili ya Mungu, kwamba awakomboe wana wa Israel na kuwafikisha
katika nchi ya mkanaani nchi iliyojawa maziwa na asali, aweze kuwafariji na
kuwafundisha mapenzi yake ili kwamba kupitia wao jamaa zote za dunia zipate
kubarikiwa kupitia mwana wake mpendwa Yesu Kristo ambaye kinabii angetokea
Israel na kuwa ishara ya kuaminiwa duniani kote, kwa hiyo Taifa hili lilikuwa
limebeba mpango na mapenzi kamili ya Mungu, Mungu aliwapitisha katika jangwa
hili zito na la kutisha apate kuwafundisha imani na kumtegemea yeye ili wawe
watu wake Lakini wakiwa njiani pamoja na vikwazo vingi walivyokuwa wamekutana
navyo walitokewa kabila hili la jangwani waliojulikana kama Amaleki watu hawa
walifanya vita na Israel, Kitabu cha kutoka kimetuficha sababu ya vita hii
kinaeleza tu walivyotokea na kupigana na Israel na Yoshua akatumwa kuwapiga kwa
msaada wa maombi ya Musa unawezakuona katika
Aliyoyafanya Amaleki:-
Kutoka 17:8-14 “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli
huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na
Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa
nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na
Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa
alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki
walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe,
wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake,
mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua
lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.
BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha
ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa,
usiwe tena”
Mungu anakasirishwa sana na tendo
la Amaleki kushindana na Israel na akaagiza kuwa Musa ni lazima alihubiri jambo
hili kwa Yoshua na wana wa Israel
walikumbuke tukio hili milele, aliambiwa aliweke tukio hili katika kitabu cha
kumbukumbu ukumbusho kuwa kizazi cha Amaleki kitashughulikiwa siku zote mpaka
kifutike kabisa duniani, sababu kubwa ni kuwa kilikuwa kizazi cha watu katili
sana hawakuwa na huruma hawakuwaonea huruma watu waliotoka katika mateso kwa
muda mrefu sana waliotakiwa kuhurumiwa waliostahili kuhurumiwa na waliokuwa wanahitaji msaada, watu waliokuwa
wanahitaji msaada na huruma na huduma na kutiwa moyo na msaada wa kibinadamu
ambao Mungu alikuwa amefungua mlango kuwatoa katika mateso amaleki walikosa utu
kabisa hawakuwahurumia watu ambao walistahili kibinadamu kuhurumiwa,
hawakuwahurumia wanyonge, hawakuwahurumia watu waliokuwa wamechoka na kuzimia
wala hawakumuhofu Mungu na kwa tukio hili Musa analiweka vizuri katika kitabu
cha kumbukumbu la Torati kwamba Amaleki kwamba Israel walikuwa wamewaacha nyuma
watu wanyonge wagonjwa na wenye uhitaji wa namna mbalimbali ili labda huenda
wapate huduma za kitabibu, maji na huduma nyinginezo lakini Amaleki aliwapiga
bila kujali ilihali wakijua kuwa ni watu wanaohitaji huduma na msaada wa
kibinadamu ona.
Kumbukumbu 25:18. “jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako
walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na
kuzimia; wala asimche Mungu“
Tukio hili halikuwa tukio
lenye kuheshimu ubinadamu, watu wanapokuwa vitani sharia za kivita zinakataza
kushambulia maeneo ya kiraia, lakini mbaya zaidi kushambulia hospitali au
sehemu zinazotoa huduma za kijamii, wanawake watoto na raia, lakini sio hivyo
tu wakati wa vita taifa lile linalopigana linapaswa kuhakikisha kuwa wanajali
utu na ndio maana utaweza kuona baadhi ya mataifa wanapokuwa na vita na
wananchi wakapata shida ya njaa huwa wanatoa msaada wa chakula na madawa,
Katika ulimwengu huu ulio haribika ni dhambi kubwa sana kumuongezea mtu tatizo
ilihali yeye mwenyewe ana tatizo au anatoka katika matataizo, kwaajili ya shida
zetu, wamekuwepo watu katika jamii ambao matendo yao ni kama waamaleki, badala
ya kuwasaidia watu wanyonge wenyewe wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwa watu hao wanyonge, mtu ni mgonjwa
anahitaji msaada ana matatizo wanaweza kuwako hata wahubiri au watoa huduma
kama hospitalini ambao watadai fedha kutokana na huduma wanayoitoa, mtu anaweza
kuwa mlemavu lakini watu wakamuhuzunisha na kumjeruhi roho yake kwa kumuongezea
masimango, mtu anaweza kuwa mjamzito akakutana na huduma na maneno ya kukatisha
tamaa huko leba wanakojifungulia, mtu anaweza kuwa yatima watu wakawatumia
yatima hao kwa manufaa yao, mtu anaweza kuwa mlemavu, kipofu au mwenye ualbino
na watu wakawatumia hao kwa manufaa yao wenyewe, mtu anaweza kuwa mjane anahitaji msaada lakini ujane wake ukatumika
kwa manufaa ya wengine, ukatili wa kijinsia, uonevu kwa wanyonge kutokujali,
kukosa utu na lugha mbovu sehemu za huduma ni maswala ambayo yanaweza kufanywa
na watu ambao wanaweka kwazo kama walivyo Amaleki ambao kwa makusudi kabisa
walishindana na kusudi la Mungu la kuwapeleka watu katika nchi ya mkanaani
lakini pia kwa kuwaonea wanyinge, jambo hili linahifadhiwa katika kumbukumbu za
Mungu na ndipo Mungu hujitakia kisasi, na kuwa na vita na jamii ya watu hao
milele, dhuluma na uonevu unawekwa katika kumbukumbu za Mungu na ni lazima
vilipiwe ni kwaajili ya haya miaka mingi baadaye Mungu alimtaka mfalme Sauli
kuwafutilia mbali Amaleki kwa sababu ya uovu wao lakini hata hivyo Mfalme Sauli
alimuudhi sana Mungu kwa sababu alishindwa kuyatii maneno ya Musa mtumishi wake
na agizo la Mungu na mapenzi yake ya kutaka kujilipizia kisasi dhidi ya Amaleki
Muhukumu wa ulimwengu lazima atende haki;-
1Samuel 15:1-19 “Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka
nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na
maneno ya Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo
hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo
walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu
kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na
mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. Ndipo Sauli
akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu,
na watu wa Yuda kumi elfu. Sauli
akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. Sauli akawaambia Wakeni, Haya!
Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi
pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri.
Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. Sauli akawapiga
Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. Akamkamata Agagi,
mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. Lakini
Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na
ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala
hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho
walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, Najuta
kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala
hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha. Samweli
akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba,
Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita,
akatelemkia Gilgali. Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe
na Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. Samweli akasema, Maana yake nini, basi,
hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Sauli
akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na
ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia
tumewaangamiza kabisa. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia
neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. Basi Samweli
akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa
cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. Kisha
Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki
wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. Mbona, basi, hukuitii sauti ya
Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana? ”
Onyo kwa watu wenye dhukluma:-
Kuwatumiwa wanyonge kwa manufaa
yakio mwenyewe ni dhambi kubwa sana, Mungu anachukizwa na udhalimu wa kila
namna maandiko yanasema wala wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu, Kitendo
cha waameleki kuwazuia Israel wasiende kulitimiza kusudl la Mungu kilikuwa ni
kitendo cha kutokujali mpangio wa Mungu, laziki tendo la kuwaonea watu wanyonge
na kuwatendea uahlifu liliwekwa katika kumbukumbu za Mungu, lakini tendo la
kuwahurumia amaleki na kutiokuangamiza au kumlipizia Bwana kisasi sawasawa na
neno lake kulikofanywa na Sauli kulimuudhi sana Mungu, Maana yake ni kuwa Mungu
hatakubali mtu awaye yote aliye mnyonge na mnyenyekevu aonewe kupita kawaida,
ni lazima ataliweka jambo hilo katika kumbukumbu na kujitakia kisasi milele,
Warumi 12:19 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya
Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.”
Mungu alitunza uovu wa wana wa
Amekeli na alikusudia kujilipizia kisasi, na ole wake mtu yule ambaye atawaacha
waameleki, Dhambi yao ilikuwa kubwa , walikuwa waonevu, walikuwa wenye dhuluma,
walikuwa wasiojali utu, waliwaonea wanyinge, walishindana na kusudi la Mungu,
kuna mambo unaweza kuyafanya kuna ukatili unaweza kuufanya lakini sio kwa watu
wanyonge ambao maisha yao yalikuwa ya taabu na Mungu aliwasaidia dhidi ya
wamisri, watu waliohitaji huruma
kufarijiwa kuinuliwa na kutiwa moyo, Mungu asingeliweza kupuuzia hata kidogo,
Lazima atawangalia wanyonge
Isaya 66:2 “Maana
mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema
Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho
iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.”
Mungu ni lazima atatenda haki Mwanzo 18:25b ………. "Hasha: Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? ”
Mungu atakulipa endapo unaonewa
kwa haki na kudhukumiwa hebu mlilie Mungu lalama mbele zake omba na kuliitia
jina lake na kisha utaona ukuu wa Mungu katika maisha yako, wale wanaoowatumia
wanyionge kwa manufaa yao tubu na achana na unevu wa kila namna Mungu asije
akakuhukumu!
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni