Jumanne, 20 Aprili 2021

Mtetezi wangu yu hai

Mstari wa msingi: Ayubu 19:25-27Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu


.”


Utangulizi:

Lakini mimi najua mteteaji wangu yu hai - ni moja ya vifungu vilivyojipoatia umaarufu mkubwa sana katika Biblia na kuvutia mioyo ya watu wengi sana na kutolewa maoni mbalimbali, na wataalamu mbalimbali wa neno la Mungu na watafasiri wengi wa Biblia, huku wengi wakivutiwa na kifungu hiki cha Ayubu 19:25-27 hasa kwa vile kifungu hiki kina uhusiano mkubwa sana na unabii wa kuja Masihi. Lakini sio hivyo tu kifungu hiki kina mvuto mkubwa saa kwa sababu kinapandisha imani zetu. Leo tutachukua muda kwa ufupi kujifunza kuhusiana na kile ambacho Mungu anataka kusema nasi kupitia kifungu hiki.


Kimsingi kitabu cha  Ayubu ni kitabu cha kwanza kati ya vitabu vya Mashairi ya kiibrania, kikifuatiwa na Zaburi, Mithali, Muhubiri na Wimbo uliobora Lakini vitabu hivi pia  ni vitabu vya  Kifalsafa.  Kitabu cha Ayubu chenyewe kina uhusiano mkubwa sana na falsafa ya Mateso na hasa kikiwa na maswali kwa nini mwenye haki ateseke? Lakini kama haitoshi pia kinatabiri mateso ya Yesu ambaye hakuwa na dhambi lakini aliteseka kwa kusudi la kuwakomboa wanadamu, Katika kitabu hiki tunaona kwa undani sana mateso mazito yaliyompata Ayubu na kimsingi Mateso haya yalikuwa na sababu ambayo kwa wakati huo wa Ayubu hakuwa anajua nini kilikuwa kinaendelea katika ulimwengu wa roho, Mateso yake kwa kiwango kikubwa yalichangiwa na wivu, dhuluma na uonevu wa shetani, kama tunavyotahadharishwa leo katika maandiko  Ona 1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.” Shetani alileta uonevu huu kwa mtu wa Mungu hata pamoja na kuwa mtu huyu aliishi maisha ya haki, Maandiko yanaonyesha wazi kuwa Ayubu alikuwa mtu wa haki na kwa sababu hiyo mateso yake hayakuwa kwamba ni kwa sababu amemkosea Mungu! Lakini maandiko yanaonyesha wazi kuwa ni kwa sababu ya mshitaki wetu shetani namna na jinsi anavyofanya kazi katika ulimwengu wa roho!


Mateso ya Ayubu:-

 

Ø  Ayubu aliishi maisha ya haki ona Ayubu 1:1-3Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.      

 

Ø  Asili ya Mateso ya Ayubu yalitokana na mashitaka ya Shetani katika ulimwengu wa roho ona Ayubu 1:6-12Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.”

 

Ø  Shetani alimuonea Ayubu kupitia mali zake ona Ayubu 1:13-19Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.

 

Ø  Shetani alimuonea Ayubu kupitia afya yake aliiharibu kabisa afya ya Ayubu kwa sababu Ayubu alikuwa ma majipu mabaya yaliyokuwa yakioza na kufumba na kupasuka kila eneo la mwili wake  

     Ayubu 2:7-10 “Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni. Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe. Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.”           

Ø  Watu na rafiki zake Ayubu waliposikia yaliyompata walifunga safari kuja kumtia moyo lakini walipoona kwa mbali hali halisi ya maisha ya Ayubu waliomboleza kwa kulia sana na kurarua mavazi yao, huku wakirusha michanga juu, inasemekana kwa siku saba wote walikaa kimya na hakuna aliyeweza kuzungumza lolote yaani walishindwa unaanzia wapi kumfariji kwani yaoikuwa ni majanga makubwa mno ona  


Ayubu 2:11-13 “Basi ikawa hao rafikize Ayubu watatu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikilia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumlilia Ayubu na kumtuliza moyo. Basi walipovua macho yao, nao wakali mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho yake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni. Kisha wakaketi nchi pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lo lote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno.”    

 

Ø  Mateso ya Ayubu yalizidi kiasi cha kufikia kiwango cha kuilaani siku yake ya kuzaliwa ona Ayubu 3:1-4 “Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake. Ayubu akajibu, na kusema; Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto mume ametungishwa mimba. Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie.”Ayubu alitamani kama angekufa tangu tumboni ili aweze kupumzika aliyaona maisha ya dunia hii kuwa ni maisha yasiyofaa hata kidogo Mstari wa 11-13 unasema hivi “Mbona si kufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni? Mbona hayo magoti kunipokea? Au hayo maziwa, hata nikanyonya? Maana hapo ningelala na kutulia; Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;

 

Ø  Pamoja na mates ohayo yote inasemekana kuwa Ayubu alikimbiwa na watu wote waliokuwa karibu naye tunaelezwa wazi mwanzoni kuwa watu wengi sana walimjia Ayubu alipokuwa na uwezo ona Ayubu 1:3 “Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.” Lakini Ayubu alipopatwa na majanga na umasikini kila mtu alimkimbia ona Ayubu 19:13-21 “Amewaweka ndugu zangu mbali nami, Na wanijuao wametengwa nami kabisa. Watu wa mbari yangu wamekoma, Na rafiki zangu niwapendao wamenisahau. Wakaao nyumbani mwangu, na vijakazi vyangu, wanihesabu kuwa mgeni; Mimi ni mgeni machoni pao. Namwita mtumishi wangu, wala haniitikii, Ingawa namsihi kwa kinywa changu. Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu, Nami ni machukizo kwa ndugu zangu. Hata watoto wadogo hunidharau; Nikiondoka, huninena. Wasiri wangu wote wanichukia; Na hao niliowapenda wamenigeukia. Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu, Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu. Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu, Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa.”

 

Ø  Ayubu alikuwa na Machungu mengi sana Moyoni na alifikiri kuwa mambo yote hayo maovu na mabaya yanatoka kwa Mungu alimlaumu muumba wake ona Ayubu 6:2-4 “ Laiti uchungu wangu ungepimwa, Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja! Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari; Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka. Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi i ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.

 

Mtetezi wangu yu hai!:-

Kutokana na uoenvu huu wa shetani Ayubu alielewa kuwa alikuwa anaonewa na kudhulumiwa na Ibilisi alifahamu kuwa nimshitaki wetu yuko kazini na anamchochea Muumba ilia pate kufanya haya aliyoyafanya shetani, hata hivyo pamoja na changamoto zote hizo imani yake Ayubu haikutindika aliamini ya kuwa mteteaji wake yu hai nay a kuwa hatimaye ataismama juu ya nchi kumtetea

Ni muhimu kufahamu kuwa neno linalotrumika hapa kwa Mteteaji wangu katika kiingereza linasomeka kama “redeemer” katika lugha ya kiebrania neno linalotumika hapo ni ni Ga’al au Go’ al ambalo lilitumika kumaanisha mtu mwenye kulipia gharama ya hasara zote ulizozipata, au aliyekulipia gharama za shamba lililouzwa, au mali iliyopotea, au anayekukomboa kutoka katika umasikini kwa mfano ulipoteza shamba lako kwa umasikini kisha akaja ndugu yako aliye karibu akalilipia na kukurudishia huyu sasa ndiye aliyeitwa Ga’al au Go’ al   kwa kizigua Mkombozi, ona kwa mfano Mambo ya walawi 25:25-26 “Kwamba nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa;” Neno hilo pia lilitumika kwa mtu aliyechukuliwa utumwani kisha mtu akaja kumnunua kwa kusudi la kumkomboa unaweza kuliona katika Kutoka 6:6 na Isaya 43:1 ona Kutoka 6:6 “Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;” pia angalia Isaya 43:1 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.”

Mpendwa haijalishi umekosa furaha na amani mara ngapi, haijalishi umedhulumiwa mara ngapi, haujalishi umefanyiwa fitina mara ngapi, haijalishi umeteseka kwa muda gani, hajalishi shetani amekuonea kwa kiwango gani, haijalishi kwamba una onewa na magonjwa na mateso kwa kiwango gani , haijalishi wazee wa kanisa nwanakukandamiza kwa kiwango gani, hajalishi manabii wamekudhulumu kwa kiwango gani, hajalishi unapitia changamoto za aina gani, haijalishi umeibiwa mara ngapi, haijalishi umelizwa mara ngapi, haijalishi una huzuni kwa kiasi gani  leo natangaza ya kuwa Mkombozi wetu yu hai, Ayubu aliamini ya kuwa siku moja atasimama atatokea juu ya uso wa nchi na kumtetea mimi natangaza kuwa amekwishakutokea, namtangaza metetaji wetu yuko hai na kuwa ameketi mkono wa kuume wa nguvu; Mbinguni na anafuatulia kwa ukaribu maumivu na mateso unayoyapitia, nakutaarifu kuwa mbingu zina taarifa ya kile unapitia, Mbingu zinataarifa ya kile familia yako inapitia, mama yako na baba yako na wazazi wako na ndugu zako kila wanalolipitia na kile unapitia katika ndoa yako na popote pale nakutangazia kuwa Yuko mkombozi yuko mtetezi haijalishi ni huzuni kiasi gani tunapitia lakini nataka tumuamini kuwa anajua hali zetu na kuwa hatupaswi kuogopa lolote,  na kuwa atalipa atatulipia machungu yote na machozi yote na huzuni zote tutalipiwa tu Mungu yuko atatulipia, Mtetezi wetu yu hai aatashughulika hatupaswi kuogopa ametuita kwa jina lake ametukomboa kwa mkono wake yu haiiiiii!

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima   


Hakuna maoni: