Kumbukumbu la Torati 31: 6 “Iweni hodari na
moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye
ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.”
Utangulizi:
Neno la Mungu linamtaka kila mmoja wetu kuwa na moyo wa ushujaa, na kwamba tuwe hodari na kamwe tusiogope, na zaidi ya yote linatuhakikishia kuwa Mungu wetu atakuwa pamoja nasi katika yote tunayokabiliana nayo iwe jua iwe mvua neema ya Mungu inatosha kabisa katika kutufikisha katika mafanikio yote ya kimwili na kiroho tunayoyahitaji. Mungu huyu huyu aliyekuwa na wana wa Israel Jangwani kumbuka yuko pamoja nasi hata ukamIlifu wa dahari, Yuko pamoja nasi na zaidi ya yote amemuachilia Roho wake Mtakatifu mno eti akae ndani yetu, na kutuongoza na kutufariji na kutupa nguvu wakati wa mahitaji, kwa msingi huo hatupaswi kusitasita wala kuhofia au kuogopa jambo lolote zaidi ya kuwa na Moyo wa ushujaa! Biblia ya Septuajint version maneno moyo wa ushujaa yanasomeka hivi “Play the men and be strong” au “Prove yourself a man” ambalo kwa tafasiri nzuri lingeweza kusomeka hivi “fanyeni kiume iweni na moyo wa ushujaa” unaweza kuona mfano katika
1Wakoritho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.” Ni sawa na maneno ambayo Daudi alimuusia mwanaye Suleimani katika 1Wafalme 2:2-3 “Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume; uyashike mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;”
Hatuwezi kuwa na mafanikio yoyote
yale katika mwili na katika roho kama hatutakuwa na Moyo wa ushujaa. Maneno ya
Mungu kupitia Musa mtumishi wake kwa wana wa Israel yalikuwa iweni na moyo wa ushujaa, simameni kiume, sina shaka kama jinsi
ambavyo watu wote hawana shaka kuwa Mungu akisema yuko pamoja nasi basi yuko
pamoja nasi kweli kweli, yeye sio kama rafiki zetu ambao wanaweza kukuambia tuko
pamoja mzee lakini zinapotokea changamoto katika maisha yetu wanayeyuka, Mungu
yuko Pamoja nasi kweli kweli, Lakini kama Mungu yuko pamoja nasi na anaendelea
kuwa pamoja nasi, kwanini niwe au tuwe na moyo wa ushujaa?, kwanini maandiko
yanatutaka tuwe na moyo wa ushujaa? Bila shaka hapa ndio kuliko na siri ya
ushindi.
Israel walikuwa wanakaribia kabisa nchi ya kanaani, ilikuwa nchi njema kama Mungu alivyowaaminisha, Hata kama Israel ni jangwa kwa sehemu kubwa lakini ni nchi ambayo Mungu aliichagua ili aliweke jina lake na kutukuzwa kutoka hapo kwa dunia nzima kwa hiyo popote ambapo Mungu anasema ni pazuri ni pazuri, nchi hii ilikuwa njema, ilikuwa imejaa maziwa na asali, mizabibu na tini tende, na kadhalika na eneo zuri kwa malisho ya wanyama, lakini ilikuwa inakaliwa na wakanaani, na wakaani walikuwa hodari, walionekana kuwa majitu, na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maendeleo makubwa sana ikiwa imezungukwa na ngome zenye kutisha, walikuwa na utaratibu maalumu wa kiserikali walikuwa na wafalme na majeshi, walikuwa wameendelea kitaaluma kwa hiyo ni wazi kuwa Israeli walikuwa wakijilinganisha kwa namna yoyote ile na wakanaani, walijiona sio kitu, Lakini Mungu Yehova alikuwa amewaahidi kuwa atakuwa pamoja nao na kuwa wasiogope na kuwa hatawapungukia wala hatawaacha lakini jambo kubwa ilikuwa wawe na moyo wa ushujaa! Hilo tu ili kumiliki yale tunayopaswa kuyamiliki katika ulimwengu huu tunahitaji tu kuwa na moyo wa ushujaa ona
Yoshua 1:6- 7 na 9 “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe
utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.Uwe
hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote
aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa
kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. 9Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe
hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu
wako, yu pamoja nawe kila uendako.”
Maana ya moyo wa ushujaa!
Kuwa na moyo wa ushujaa katika
lugha ya kiibrania kulikuwa na maana ya kusimama kiume, au kuonyesha uanaume
kweli kweli kwa kiingereza “Courage”
ability to do something that which is frightens; bravery ambalo maana yake
ni uwezo wa kufanya jambo lenye kutisha kwa werevu. Au kwa weledi, au nguvu ya
kukabiliana na jambo lenye kutisha au kuogopesha au hatarishi kwa ushujaa
mkubwa, ni uwezo wa kuamua kupambana na maumivu, tishio, mateso, hatari, au
jambo lenye kutisha bila woga wowote, wala hofu yoyote, Ni uwezo wa kuthubutu
kufanya au kukabiliana na jambo ambalo kwa akili za kibinadamu linaonekana kuwa
gumu kwa imani kuwa utalifanikisha iwe mvua ama jua, kibiblia ushujaa huu
unaambatana na kumuamini Mungu, ndio maana Mungu ameambatanisha na kuwa pamoja
nasi, na ili kuiifikia ile ndoto, au lile tumaini au ile ahadi Waebrania 10:35-36 “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji
saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.” Kwa
hiyo tunapokuwa na moyo wa ushujaa ndipo tunapoweza kupokea thawabu kuu na
kutimiza mapenzi ya Mungu na kuifikia ile ahadi au ile ndoto au lile lengo
tulilolonalo ambalo ni mapenzi ya Mungu, Katika ulimwengu huu vilevile ili
tuweze kufikia malengo yetu ya kawaida hatuna budi kuhakikisha kuwa tunavaa
moyo huu wa kijasiri, nina mshirika wangu mmoja anaishi maisha duni na yakawaida
kabisa lakini ananiambia mchungaji mimi sitaki kuomba kwangu kuomba ni aibu
kubwa hivyo napambana katika maisha, yeye anapambana kwa kuzunguka mitaani na
kuuza mahindi ya kuchemsha na anapozunguka hazunguki kimya kimya anapiga kelele
aiiiiimahindi ya kuchemshaaa kwa hivyo mimi nilimuhurumia lakini sikuwa na
namna ya kumsaidia nilimnunuza mahindi matano ya kuchemsha na niliyagawa kwa
watu waliokuwa mtaani ili wale nami nilikula moja tu, lakini nilitaka kumtia
moyo kwa kununua mahindi yake kwa sababu nilifuarahia ujasiri alio nao, anapata
ridhiki yake kwa sababu haoni aibu, ni mwanamke mzuri wa makamo hivi, ni mzuri,
uzuri wake na biashara anayoifanya ni kama haviendani hivi, Lakini ndio njia
ambayo Mungu amempa kupata ridhiki yake, yako mambo duniani ambayo ili tuweze
kutoka katika hayo hatuna budi kuwa na moyo huu na kutokuogopa lolote hata kama
ni kuangamia lakini tukiwa na kusudi la kukaa na kutimiza mapenzi ya Mungu,
tunahitaji Moyo huu, ni moyo huu ndio unaoweza kutufanya tukasimama sokoni,
viwanjani na kumuhubiri Yesu, ni moyo wa aina hii unaoweza kumfanya mtu
akakubali kuwa Kondakta wa basi na kupata ridhiki yake, kuhutubia watu na kila
jambo, kusoma, kujifunza na kufundisha kote kunahitaji moyo wa ushujaa, bila
moyo huo ni vigumu kuyafikia malengo yetu na mapenzi ya Mungu, sasa tunawezaje
kujifunza kuwa na moyo wa ushujaa? Hilo sasa linatuleta sasa katika kutafakari
kipengele muhimu jinsi ya kuwa na moyo wa ushujaa:-
Jinsi ya kuwa na Moyo wa ushujaa!
Kuwa na moyo wa ushujaa ni swala
la kujizoeza, na ndio maana maandiko yanatuamuru tuwe na moyo wa ushujaa,ushujaa
hautoki kwa Mungu unatoka mioyoni mwetu pale tunapomuamini na kumtegemea Mungu,
hivyo ni lazima kuamua kutoka moyoni ili kukabiliana na kile ambacho tunataka
kukabiliana nacho, lakini tunawezaje kujua au kujipima au kujizoeza kuwa na
moyo wa ushujaa yafuatayo ni maswala ya msingi sana yanayoweza kutusaidia kuwa
na moyo wa ushujaa na kwa ufupi ukiwa na mambo haya na kuyafanyia kazi katika
maisha yako utakuwa na moyo wa ushujaa;-
1. Mtu
mwenye moyo wa ushujaa hapaswi
kujihurumia - Moyo wa ushujaa na
mafanikio yake hauwezi kuwepo kwa mtu anayejihurumia, wengi tumeweza kuangamiza
nafsi zetu kwa sababu ya kujihurumia, tumeshindwa wakati mwingine kufikia ndoto
kadhaa kwa sababu tuna tabia ya kujihurumia, mtu anapojiandikisha kuwa askari
ni kama mtu anayejiandikisha kuangamiza nafsi yake kwaajili ya nchi yake,kujiandikisha
kuwa askari ni kujiandikisha kufa! huwezi kuwa mpiganani mzuri kama unajionea
huruma, wala huwezi kuwa mwanafunzi mwema wa Yesu Kristo kama unajihurumia,
wala huwezi kutoboa katika maswala kadhaa wa kadhaa ya maisha kama utajihurumia
Mathayo 16:24-25 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote
akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa
kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi
yake kwa ajili yangu, ataiona.” Kwa hiyo kuwa mwanafunzi wa Yesu
lazima uwe kama mtu unayepoteza maisha, unayekubali kuangamia, unayekataa nafsi
yako kujifurahisha, watu wanaojihurumia hawawezi kamwe kuwa wanafunzi wa Yesu,
lakini sio hivyo tu watu wanaojihurumia hawawezi kutoboa katika maisha haya! Nyakati
za torati katika agano la kale wanajeshi wote waliokuwa wameoa hivi karibuni au
mtu aliyenunua shamba jipya na kadhalika Mungu aliagiza wasiende vitani, kwa
sababu mawazo yao hayatakuwa tayari kuangamia na kuacha mke mpya nyumbani hivyo
watu wote waliokuwa na mioyo ya hofu na sababu zinazoweza kuwafanya wasijikane
nafsi walipaswa kuchujwa ili wasiende vitani ona Kumbukumbu la Torati 24 :5 “Mtu atwaapo mke
mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote;
akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.”
Au wale waliokuwa na hofu au woga walipaswa kurudi nyumbani Waamuzi 7:3 “Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa,
na kusema, Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika
mlima wa Gileadi. Ndipo watu ishirini na mbili elfu wakarudi katika watu hao,
wakabaki watu elfu kumi.” Unaona Mungu hakuhitaji watu wenye hofu au
wanaotetemeka wanaoogopa vita wanaojihurumia wenye ndoa mpya hawa walitakiwa
kurudi nyumbani, awaye yote ambaye anataka kufanikiwa lazima avae moyo wa
ushujaa asijihurumie kamwe apambane kiume awe na moyo wa ushujaa #
2. Mtu
mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuchoka
– ili tufanikiwe katika maisha yetu lazima tuwe na mioyo migumu, hatupaswi
kuchoka, Biblia inamtaja punda milia au punda mwitu kama mnyama asiyechoka,
aliyeizoelea nyika na ukijaribu kumtafuta utachoka wewe na hutaweza kumkamata
au kumgeuza ona Yeremia 2:24 “punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo
katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao
hawatajichokesha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.” Mtu mwenye
moyo wa ushujaa moyo wake hauchoki haukati tamaa, unaendelea mbele hata kutokee
vihunzi vya namna gani moyo unaendelea tena na tena katika kuyafikia malengo
yake, watu wote mashujaa katika maandiko waliofanikiwa katika Nyanja mbalimbali
walikuwa watu wasiochoka, watu wengi ambao wanachoka wanakata tamaa na kuishia
njiani, kwa msingi huo hatupaswi kuchoka katika kutia bidii kwenye kila kitu
tunachokifanya kwaajili ya utukufu wa Mungu, tusichoke katika kutenda mema na
pia tusichoke katiika kumgojea bwana naye atatutokea na kututia nguvu Wagalatia 6:9 “Tena
tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”.
Isaya 40:31 “bali wao wamngojeao Bwana watapata
nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka;
watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”
Watu wengi wenye mafanikio katika Nyanja mbalimbali ni wale
wasiokuwa na moyo wenye kuchoka, maisha ya kwenda mbinguni na maisha ya
kumngojea bwana yanawezwa na wale wasiochoka, Lakini vilevile tukitaka
mafanikio ya aina mbalimbali basi hatupaswi kuchoka. #
3. Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa kubaki peke yake - Moja ya mambo ambayo yanaweza kumvunja mtu
moyo ni pamoja na kuachwa peke yako, watu wengi sana hukata tamaa wanapobaki
wenyewe, mtu mwenye moyo wa ushujaa wakati wote anakuwa tayari kupambana hata
anapobaki peke yake, hayuko tayari kwenda kwa mkumbo au kufuata mkumbo, Hesabu 14:6-10 “Na
Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao
walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa
Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema
mno ya ajabu. Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe
yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi Bwana, wala
msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu
yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope. Lakini mkutano wote
wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya
kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote”. Yoshua 24:15 “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni
hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia
ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi
yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.” Yoshua ni moja
ya viongozi walioambiwa na Mungu moja kwa moja wawe na moyo wa ushujaa, wawe
hodari na wasiogope, katika maisha yake anadhihirisha kuwa yuko tayari kusimama
na jambo lililo jema na katika mapenzi ya Mungu hata kama atabaki yeye mwenyewe
na nyumba yake, ukiisha kuyajua mapenzi ya Mungu na kujua lile kusudi lililoko
kwako kamwe usikubali kufuata mkumbo katika kufanya ujinga wewe lenga katika
kuyafanya mapenzi ya Mungu, hata kama inatokea migomo mashuleni vyuoni na
kadhalika, wewe kama unajua kuwa mgomo huo hauna maslahi kwako na kwa Mungu
simama mwenyewe ni wewe peke yako unayeweza kumdhihirisha Mungu wa kweli, Mungu
sio mwanademokrasia kwamba anaangalia wengi wape yeye ni mwanatheocracia
anaangalia wanaosimama upande wake, Nuhu alisimama na Mungu wakati mkumbo wa
ulimwengu wa nyakati zake watu waliishi kwa anasa na kutokujali, Lutu aliishi
kwa kumtii Mungu wakati watu wa miji ya Sodoma na Gomora walipokuwa wakiendekeza dhuluma uovu uozo na
mapenzi ya jinsia moja, Eliya alisimama mwenyewe wakati Israel walipokuwa
wakimtumikia baali na yeye pekee nabii wa Bwana alisimama ona 1Wafalme 18:22-39 “ Ndipo Eliya akawaambia watu, Mimi nimesalia, mimi peke yangu, nabii wa
Bwana; lakini manabii wa Baali ni watu mia nne na hamsini. Kwa hiyo na
watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie ng'ombe mmoja, wamkate-kate na
kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza huyo ng'ombe wa
pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini. Nanyi ombeni kwa jina la
mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na
awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu wakasema, Maneno haya ni mazuri. Eliya
akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza;
maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini.
Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu
asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti,
wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya. Ikawa, wakati
wa adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana
ni mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda
amelala, sharti aamshwe. Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe
kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika. Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita,
walitabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti,
wala aliyejibu, wala aliyeangalia.Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni
mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya Bwana iliyovunjika.
Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo,
aliyejiliwa na neno la Bwana na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli. Naye
akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama
wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. Kisha akazipanga zile kuni,
akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni
mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni.
Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya
tatu. Wakafanya mara ya tatu. Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza
mfereji maji. Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia,
akasema, Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane
leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako,
na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee Bwana,
unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe
umewageuza moyo wakurudie. Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya
kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo
katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana
ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu.” Mungu hupendezwa na mtu
anayejitambua na kutambua mapenzi ya Mungu, ili uweze kufabnikiwa huna budi
kusimama mwenyewe, katika kutimiza kusudi lile ambalo Mungu amekuitia Biblia
inasema usiandamane na mkutano kutenda uovu, maana yake usikubali kufuata wingi
wa watu hususani kama watu hao wamepotea na kupotoka, kanuni hii inafanya kazi
sio katika mazingira ya uovu tu na kumcha Mungu lakini inafanya kazi katika
kuyafikia mafanikio ambayo lengo lake Mungu ameweka moyoni mwako kwa kuwa wewe
ndiwe unayelitambua kusudi hilo simama mwenyewe, usikubali kufuata mkumbo, hata
kama dunia itakuacha peke yako Kutoka
23:2 “Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala
usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na
mkutano ili kupotoa hukumu; ”
4. Mtu
mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kupoteza
nguvu zake – Kumbuka kuwa tunazungumzia Moyo wa ushujaa na hivyo hapa
hatuzungumzii kamwe nguvu za kimwili, shetani anajua kuwa ili aweze kutukwamisha
anajua wazi kuwa anapaswa kuujeruhi moyo, moyo wako ukiisha kukubali kujeruhika
basi umepoteza nguvu zako, hata kama mtu ana miguvu kiasi gani ushindi wa mtu
hatokanani na muonekano wake wa kimwili bali mtazamo wake wa moyoni, yako mambo
ambayo ibilisi anaweza kuyatumia kujeruhi mioyo yetu ili tupoteze nguvu zetu
watu wenye moyo wa ushujaa hawapaswi kupoteza nguvu zao!huwezi kuwa na nguvu
kama utakubali shetani na watu waudhibiti moyo wako, na hisia zake mtu
akifanikiwa kuudhibiti moyo wako na hisia zako amekupunguzia nguvu ya moyo
wenye ushujaa, unajua ni kwanini maandiko yanatuasa kusamehe au kuwa na subira
kwa sababu mtu asiyesamehe anapoteza nguvu unapoteza muda kumfikiri mtu
anayekukwaza kuliko kufikiri unachopaswa kukifanya Mathayo 18:21-35 “Kisha Petro akamwendea
akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara
saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya
hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta
elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe
na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia
akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule
akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona
mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata, akamshika koo,akisema
Nilipe uwiwacho.Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema,
Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa
kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona
yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote
yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu,
nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu
mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika,
akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu
wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu
yake.” Kumbe kutokuachia ni kutokujiachilia, hatupaswi kukaa chini
na kuwafikiri wale waliotuumiza kwa vile watachelewesha kusonga kwetu mbele,
sisi hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaachilia kutokuachilia kutatufanya
tupoteze nguvu, kuachilia ni nguvu kubwa katika maisha yetu.
·
Mfano umeumizwa na unakaa chini kusikilizia
maumivu yale badala ya kusamehe na kusonga mbele
·
Watu wanakusema vibaya au wanakosoa vikali kile
unachokifanya unakaa kusikiliza maneno yao
·
Umedhulumiwa usipoteze muda kutafuta kurudishiwa
tafuta njia mpya ya kupata kilichopotea mara dufu zaidi,
·
Mtu anafanya mambo ya kuumiza moyo wako nawe
unasikilizia badala ya kupuuza, unabadili mtazamo wako na malengo yako kwa
sababu ya maneno ya watu au vitisho, hakikisha unasahau unaachilia na kusonga
mbele ukijihakikishia furaha katika maisha yako
·
Unapoteza muda kukaa chini na kulalamikia watu
au mazingira kuwa ndio sababu ya kushindwa kwako,
·
Unasikitikia mambo yote uliyoshindwa kuyatimiza
katika mipango yako, au unaketi chini kukumbuka mambio ya kushindwa kwako
yaliyopita
Mtu wa Mungu
unapokaa chini na kuanza kufikiria kile watu wanasema au wanakufanyia hutaweza
kutoboa kumbuka kuwa hao wanakupotezea nguvu zako, unachotakiwa kukifanya ni
kusonga mbele na kutokupoteza nguvu zako, wakati mwingine huhitaji hata
kuwajibu wanaokushambulia Nehemia 4:1-3
“Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba
tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana,
akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria,
akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa
dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu
hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa
karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa
ukuta wao wa mawe.”Wakati wote usikubali kukaa katika mambo ambayo
yatakupotezea nguvu hakikisha kuwa unasonga mbele, usikubali kitu au jambo
likukalishe chini, unapokuwa unakubali watu au mtu Fulani aushike moyo wako
maana yake utahitaji watu wa kukutia moyo, wa kukusiafia ili ujisikie vizuri, utashindwa
kukabiliana na wajibu muhimu ulioko mbele yako na mazingira yatakutawala na
kukukalisha chini na kukuchelewesha, inuka songe mbele, usipoteze nguvu zako, acha
kazi zako zijibu hoja za wapinzani wako!
5. Mtu
mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuangalia
nyuma – Marrianne Williamsone aliwahi kusema hivi nanukuu “we do not heal the past by dwelling there,
we heal the past by living fully in the present” kwa tafasiri isiyo rasmi ni
kama anasema hivi hatuwezi kujiponya na mambo ya nyuma kwa kukaa na kuyakumbuka
tunaweza kujiponya na mambo ya nyuma kwa kuishi sasa, kwa lugha nyepesi wakati
wote tunapaswa kuyasahau yaliyo nyuma na kuyaangalia yaliyo mbele Wafilipi 3:12-14 “Si
kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo
ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja
tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo,
niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.”
Mtu mwenye moyo wa ushujaa wakati wote ataangalia mbele, hatupaswi kuangalia
nyuma aidha kulikuwa na mafanikio au tulishindwa, wakati wote tuwaze kufikia
malengo makubwa na kuyatimiza kwa ubora zaidi,
wachungaji wengi wakifikisha kanisa lina watu 200 tayari wanadhani
wamefikia mahali pa kupumzika, mwanafunzi ana maksi tisini au themanini
amepitisha kiwango cha matokeo yaliyowekwa na shule anaridhika, Mwalimu
amefaulisha au shule na imashika nafasi Fulani njema mtu anadhani amefika,
hatuna budi wakati wote kuhakikisha kuwa haturidhishwi na mafanikio madogo
tunayoyapata ilihali tunaweza kwenda zaidi ya vile kwaajili ya hayo ndugu zangu ni muhimu sana
kuhakikisha kuwa tunaangaluia mbele, Mtume Paulo alikuwa ni mtume aliyefanya
kazi kubwa kuliko wote, alikuwa muombaji na mwenye uwezo mkubwa sana wa kunena
kwa lugha kuliko watu wote, alihubiri injili na kuupindua ulimwengu wa wakati
wake. Aliishi maisha matakatifu na kuwa kielelezo, hata cha kuwataka watu
wanfuate yeye kama anavyomfuata Kristo, alipewa mafunuo makubwa sana lakini
anasema anasahau yaliyo nyuma na anayachuchumilia yaliyo mbele, kila wakati
tuhakikishe kuwa tunaongeza viwango na kuachana na mafanikio madogo ya nyuma.
6. Mwenye
moyo wa uhujaa hapaswi kuwaogopa
wanadamu – inasemekana kuwa
mwanadamu ndiye mnyama anayetisha zaidi kuliko wanyama wote, ili uwe na moyo wa
ushujaa ni lazima ujifunze kutokuwaogopa wanadamu, wao ndio viumbe
tunaoshindana nao katika mambo yote ndio wanaoweza kutumiwa na Mungu kwa
mafanikio yako lakini vilevile ndio wanaoweza kutumiwa na ibilisi wakasimama
kama vikwazo ili uweze kutoboa katika maisha yako usiwaogope wanadamu Kumbukumbu la torati 3:21-22 “Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako
yameona yote aliyowatenda Bwana, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo
atakavyoutenda Bwana kila ufalme huko uvukiako. Msiwache, kwa kuwa Bwana, Mungu
wenu, ndiye awapiganiaye.” Ili uwe shujaa Mungu anataka kuona
ukimuogopa yeye tu peke yake wale tunaoshindana nao ni wanadamu tu kama sisi,
kwa msingi huo hatupaswi kwa namna yoyote kuwaogopa kwa kuwa wewe unapiganiwa
na Mungu wako, Mungu akiisha kusema nawe na akiisha kukupa wazo la kufanya
katika Nyanja yoyote lifanye maana Mungu yuko pamoja nawe na amekupa watu kwa
msingi huo usiwaogope watu Yoshua 8:1 “Kisha Bwana akamwambia Yoshua, Usiche, wala usifadhaike;
wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai,
angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji
wake, na nchi yake;” kwa kawaida Mungu anakupa ushindi wa vita hata
kabla hujaingia katika vita vyenyewe, na kwa sababu hiyo haitakuwa vema kabisa
kuogopa, unapoogopa watu na kufadhaika
unaondoa uwepo wa Mungu maana yake unashindwa kumfanya Mungu atende kazi na
wewe na kwa sababu hiyo utaleta kushindwa, Zaburi
56:11 “Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu
atanitenda nini?” Mwandishi wa zaburi hii ana ushahidi wa kushangaza
yeye nguvu zake ziko katika kumtegemea Mungu kiasi ambacho anajua kabisa kuwa akama ukiweka tumaini lako
kwa Mungu ni dhahiri hofu taondoaka na hautaogopa chochote, kujifanya tu uko
vizuri huku humtegemei Mungu ni kiburi,
Lakini kuweka tumaini kwa Mungu kunakupa ujasiri sio kusema tu humuogopi
mwanadamu lakini hata majeshi yakijipanga kwa mtu anayemtegemea Mungu bado
hawezi kuogopa ona Zaburi 27:1-3 “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia,
Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi
lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata
hapo nitatumaini.” Kama utajifunza kutokuwaogopa wanadamu na
kuangalia imani yako na kuweka tegemeo lako na tumaini lako kwa Mungu lazima
ukumbuke kuwa ni Mungu ndiye atakayekupigania na kukusaidia na kukushuindia
hivyo hupoaswi kuoopa changamoto ya aina yoyote ile na hupaswi kuwa na moyo wa
unyonge, wewe utamwangalia Mungu tu.
7. Mwenye
moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa
mabadiliko - Tunaishi katika
ulimwengu ambao mambo yanabadilika kwa haraka sana kutokana na maendeleo
makubwa ya sayansi na teknoliojia, lakini moja ya maswala ambayo yanawatishia
watu ni pamoja na mabadiliko watu wengi wanaogopa mabadiliko, kwa sababu hiyo
wanapingana nayo, kwa mfano moja ya jambo ambalo watu wengi wanaliogopa katika
taifa letu ni pamoja na mabadiliko ya katiba, watu wanaogopa sana lakini
mabadiliko ya katiba hayaogopeshi kama yalivyo mabadiliko ya viongozi, kama
tunaweza kubadili viongozi wetu kwa amani basi vilevile tunaweza kuibadilisha
katiba yetu kwa amani, jambo la msingi tu ni kwa wale wanaoona hitaji la katiba
mpya watoe Elimu ya kutosha kuinyesha kwanini sasa tunahitaji mabadiliko ya
katiba, ili waoogopa wajue kwanini tunahitaji katiba mpya, dhambi ni
kushinikiza tu kuwa ni lazima tuwe na katiba mpya huku hata wapiga kura wakiwa
hawajui kwanini tuwe na kaiba mpya, tukiipata itatunufaisha nini ina manufaa
gani, hakuna sababu ya kuogopa, kwa msingi huohuo watu wanaoweza kuleta
mabadiliko na kutoboa ni wale ambao kwa namna Fulani hawaogopi kubadilika kwa
mambo, ukiogopa mabadiliko utapoteza nafasi nyingi za muhimu ambazo
zingekujilia kuliko kuogopa Zaburi
46:1-3 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika
nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka,
Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.” Unaona mwandishi wa zaburi hii aonyesha kuwa
haogopi mabadiliko, lazima akili ya mtu shujaa ijiandae kwa mabadiliko, na
kukubaliana nayo, kama tumemtegemea Mungu tujue tu katika maisha yetu pia
kwamba kuna kupanda na kushuka, kuna wakati kwa kila jambo, kuna kudhiliwa,
kuna wakati wa magumu na kwa vyovyote vile hali yoyote ya mabadiliko haipaswi
kuwa sababu ya kuondoa ujasiri katika maisha yetu Warumi 8:35-39 “Ni nani atakayetutenga na
upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari,
au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa,
Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote
tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha
kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye
mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu,
wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo
wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”Mwandishi anaonyesha
kuwa hakuna kitu maana yake hakuna aina ya mabadiliko ya maisha
itakayomtenganisha na Yesu Kristo, iwe dhiki, au shida, au njaa, au uchi au
hatari au upanga hata kama tunauawa iwe jua iwe mvua atabaki katika imani bila
kujali hali ikoje? Wako watu wengine haki yao ya wokovu inategemeana na hali ya
hewa, hali yao ya kumuamini Mungu, inategemeana na hali ya hewa na mazingira
kukiwa na shida anamuacha Yesu, hawa ni watu wanaoogopa mabadiliko, unasikia
watu wanasema wokovu wa siku hizi, kumbe kuna wokovu wa zamani, wa siku hizi je
wa siku zijazo utakuwaje maandiko yanatuambia kuwa Yesu ni yeye yule jana leo
na hata milele, Neno la Mungu linatuonyesha kuwa watru wenye moyo wa ushujaa wanaendelea
kubaki vilevile bila kujali kuwa mazingira yakoje hawaogopeshwi na mabadiliko,
wakati wote huyatumia mabadiliko kama wimbi la kuelekea katika Nyanja nyingine,
nimeona kuna wanafunzi wanaogopa mabadiliko, Mwalimu fulani hayuko sijui
itakuwaje, fomart ya mitihani imebadilika sijui itakuwaje, syllabus imebadilika
sijui itakuwaje, bei ya hiki na kile imepanda sijui itakuwaje kwani ilipokuwa
nafuu ulifanya nini? Ndugu zangu mwenye moyo wa ujasiri haogopi mabadiliko!.
8.
Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa Kushindwa! – Kushindwa
ni sehemu ya maisha tunajifunza mengi mazuri kwa watu waluioshindwa kuliko hata
washindi, Biblia imejaa mifano ya watu wengi wanaoitwa mashujaa wa imani ambao
maisha yao yamejaa ushindi kwa msaada wa Mungu hata hivyo Roho Mtakatifu
hajaacha kuonyesha kushindwa kwa watu hao, tunawaonaga wachezaji wakikatwa
mtama na kutibiwa na hatuimaye kuinuka tena na kuendelea na kucheza hawakati
tamaa kwa sababu wameshindwa, shule za Private zamani zilikuwa ni shule za watu
walioshindwa ndio wanachukuliwa na kuandaliwa na kufanywa washindi tena!,
kushindwa ni moja ya changamoto kubwa sana katika maisha ya wanadamu na
inaogopewa na watu wengi sana wengine hawataki hata kujaribu kwa sababu
wanafikiri watashindwa! Kama
ingekuwa unaweza kuchagua aina za washirika wa kuchunga kama mchungaji mimi
ningetamani sana kuchunga watu walioshindikana, walioanguka, wenye madeni,
wanyonge hao ndio ningetamani wanijie alafu nionyeshe uwezo wangu wa kichungaji
na niwawezeshe wao kuonyesha uwezo wao na uzoefu wao wa kushindwa ulivyo wa
muhimu sana na unavyoweza kuwaletea ushindi dhidi ya wale wanaofikiri wanaweza!
1Wakoritho 1:26-31 “Maana, ndugu zangu,
angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi
wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo
mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu
vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya
dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile
vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa
yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo
kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye
aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.” Mungu huwa haogopi
kushindwa kwa hiyo ana chagua vitu au watu dhaifu kisha anawatumia kwa utukufu
wake, kushindwa kwetu katika maeneo mbalimbali hakukufanyi wewe uwe dhaifu bali
kunakufanya wewe ujue ni changamoto gani unaweza kuziepuka na ukaleta ushindi,
kwa hiyo lazima tujaribu tena na tena, Daudi
jeshi lake lilikuwa na watu hodari sana lakini wengi waliomwendea na kujiunga
naye walikuwa watu duni ona 1Samuel 22:1-2 “Basi
Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote
wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. Na kila mtu
aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote
wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao
waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne.” Inashangaza sana
kuona kwamba Daudi alikuwa jemedari yaani ni mkuu wa majeshi lakini tunaambiwa
jeshi lake liliundwa na watu duni, watu waliokuwa na dhiki, waliokuwa na madeni
tena wameshindwa kuyalipa huko watu waliojaribu maisha wakashindwa hao ndio
wanaunda jeshi la Daudi unaweza kuona, lakini
katika namna ya kushangaza sana hawa ndio waliotumiwa na Mungu na kuleta
ushindi mkubwa, hawaogopi kushindwa kwa sababu inaonekana walishashindwa mara
nyingi, Waamuzi 11:1-3 “Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye
alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha.Mkewe huyo Gileadi
akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa
Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe
u mwana wa mwanamke mwingine. Ndipo Yeftha akawakimbia hao nduguze, akakaa
katika nchi ya Tobu; na watu mabaradhuli walikwenda na kutangamana na Yeftha,
wakatoka kwenda pamoja naye.” Ni katika hali kama hiyo Yeftha pia
tunaelezwa kuwa alikuwa mtu shujaa yaani jemadari na jeshi lake liliundwa na
watu mabaradhuli, hii ni jamii ya watu walioshindwa maisha lakini baadaye
walileta ushindi mkubwa, mtu anayeogopa kushindwa hawezi hajta kujaribu,
tunaweza kukwepa mambo kadhaa wa kadhaa na hatimaye tukakosa mambo ya msingi na
ya muhimu kwa sababu tu tunaogopa kujaribu kwa sababu ya kuogopa kushindwa!
Kumbe kushindwa kunaweza kutupa uzoefu utakaotuletea ushindi wa kweli,
tunajifunza vitu vingi kwa namna ya kushindwa, watoto kusimamam na kutembea na
kujua mambo mengi kwa kujaribu na kushindwa, baiskeli kwa namna ya kuanguka na
kuumia, lugha kwa namna ya kuanguka na kuumia, na hali ya kiroho wakati
mwingine kwa kuanguka na kuinuka tena hatimeye kusimama
9.
Mtu mwenye moyo wa ushujaa haogopi kukataliwa - watu wengi sana wanajiepusha na mambo Fulani
kwa sababu wanaogopa kukataliwa, mtu anaweza kuona binti mzuri na akampenda
lakini akashindwa kusema chochote kwa sababu anaogopa kukataliwa, hata wanandoa
mtu anaweza kuogopa kuomba jambo Fulani kwa mwenzi wake kwa kudhani kuwa
atakataliwa, kwa sababu ya kuogopa kukataliwa wakati mwingine katika maisha
yetu tunabakia palepale na hatusiongi mbele Biblia imejaa ushahidi wa watu
wengi ambao walikuja kufanya vizuri katika nafasi zao lakini mwanzoni
walikataliwa Mwanzo 37:18-20 “Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya
shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa
ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi
tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.”
Yusufu alikuwa na ndoto ambayo ingekuja kuwafaa ndugu zake lakini
alipowasimulia hawakufurahi, walikusudia kumuangamiza ili waone ndoto zake
zitakuwaje mkono wa mungu ulikuwa pamoja naye na akatoboa Matendo 7:9-10 “Wale wazee wetu wakimwonea
wivu Yusufu, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja naye, akamtoa katika
dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye
akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.” Unapokataliwa
huo sio mwisho wa maisha Oprah Winfrey
alikuwa ni mtangazaji wa taarifa za habari jioni katika televisheni Fulani na
alifukuzwa kazi kwa sababu hakuweza kuzuia hisia zake wakati akitoa habari, kwa
hiyo alitimuliwa kama mtanzagaji asiyefaa, alianzisha kipindi chake kiitwacho
Oprah Winfrey show na kuwa mtu maarufu sana na baadaye kuwa tajiri mkubwa na
mtu mwenye kibali ambaye unaweza kusimama naye wakati wa kampeni za kisiasa,
sasa ni moja ya watu wenye ushawishi mkubwa nchini Marekani, Msanii Harmonize ambaye alitokea WCB au wasafi hapa Tanzania unapomuona
anaonekana kama kituko flani hivi na ndio hali halisi, lakini wakati anaanza
sanaa alikataliwa na watu wanaohusika na kuinua vipaji katika mashindano
maarufu yajulikanayo kama Bongo Star search, kwamba hafai na ajaribi fani
nyingine, leo hii Harmonize ni moto wa kuotea mbali, hakujali kukataliwa, hakukata
tamaa, alipambana kupigania ndoto zake kwa nguvu zake zote leo hii Harmonize ni
next level kwa hiyo neno la Mungu, kwa
msingi huo mtu kukuambia haufai au kukukataa haimaniishi kuwa huwezi kuachieve
au kufikia kile unachotaka kukifikia, hakikisha wakati wote unapambana kuifikia
ndoto yako Yefta alikataliwa na ndugu zake lakini walipoozidiwa walienda
kumuomba yeye awe mwamuzi juu yao
Waamuzi 11:1-2 “Basi huyo
Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke
kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha. Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana
wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe
hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke
mwingine.” Unaona hapa Yefta anakataliwa laiki mtu huyu alikuwa ni
shujaa mno na baadaye wale walimkataa yalipowakuta walienda kumuomba aje
awasaidie na akakubali kurudi na kuwasaidia watu wake ona Waamuzi 11:4-11 “Ikawa baadaye, wana wa
Amoni wakapigana na Israeli. Ikatukia, hapo wana wa Amoni walipopigana na
Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu;
wakamwambia Yeftha, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa
Amoni. Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na
kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa
wakati mlio katika taabu? Wazee wa
Gileadi wakamwambia Yeftha, Kwa ajili ya hayo sasa tumegeuka kukuelekea wewe
tena, ili uende pamoja nasi na kupigana na wana wa Amoni, nawe utakuwa kichwa
chetu juu ya wenyeji wote wa Gileadi. Basi Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi
Kwamba mwanirejeza kwetu tena ili kupigana na wana wa Amoni, naye Bwana
akiwatoa mbele yangu, je! Mimi nitakuwa kichwa chenu? Wazee wa Gileadi
wakamwambia Yeftha, Yeye Bwana atakuwa shahidi kati yetu; hakika yetu tutafanya
sawasawa na neno lako. Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao
watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake
yote mbele ya Bwana huko Mispa.”
10.
Mtu
mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuwa na
mashaka – ni ukweli ulio wazi kuwa watu wengi huogopa kujaribu mambo kwa
sababu wanaona shaka, watu wana mashaka ya kujaribu kitu kingine, wanaogopa
kuwa labda kujaribu kitu kingine kunaweza kusiwaletee maisha mazuri, lakini
kukaa tu bila kujaribu kwa sababu ya mashaka kutakufanya udumae na Yesu
aliwakemea wanafunzi wake mara kadhaa kutikana na kuwa na mashaka Mathayo 14:25-31 “Hata
wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya
bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni
kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni
mimi; msiogope. Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije
kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro
akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini
alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana,
niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani
haba, mbona uliona shaka? ” Yesu anatuonyesha wazi kuwa hakuna
lisuilowezekana kwa mtu anayeondoa shaka ukiweka mashaka utashindwa lakini
ukiondoa shaka utashinda angalia Marko
11:23-24 “Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia
mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini
kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote
myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Mashaka
yatakuondoa kwenye malengo, mashaka yatakuondoa kwenye imani, amshaka
yatakutupa nje ya mpango wa Mungu, mashaka yatakufungia mafanikio yako Yakobo 1:5-7 “Lakini
mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa
ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo
yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na
kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu
kwa Bwana.”
11.
Mtu mwenye moyo wa ushujaa hapaswi kuogopa kukosolewa “Critics”
- kwa kawaida kukosolewa na au
kuhukumiwa na wanadamu katika mambo tunayoyafanya, kukosolewa au kuhukumiwa na
wanadamu katima maswala tuyafanyayo ni jambo la Muhimu sana, nani kawaiada hivyo hatupaswi kuogopa kukosolewa wala
kuhukumiwa wala, ukweli ni kuwa watu watakuhukumu na wakati mwingine kwa maneno
makali, lakini ukiwa na moyo wa ushujaa utaishi sawa na thamani ya vile ulivyo,
na hiyio ndio njia ya mafanikio ya kufanikiwa kwako, unaposoama sana ni rahisi
wenzako kukuambia umetumwa na kijiji, unapojituma sana ni rahisi kuambiwa na
wenzako unajipendekeza, Yesu alikosolewa katika kila anachokifanya na hata
alipotoa Pepo walisema anatumia nguvu za giza za mkuu wa pepo Belizebul Mathayo 12: 22-24 “Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya,
hata yule bubu akanena na kuona. Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye
mwana wa Daudi? Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila
kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.” Paulo mtume alihakikisha kuwa wakati
wote anakubali kila aina ya udhaifu, dharau, taabu udhalimu na mateso kwaajili
ya Kristo Yeye alikuwa mtu mkubwa sana katia ulimwengu war oho alipata mafunuo
makubwa sana kuliko mtu awaye yote lakini hakuwahi kujisifu, na alikubali
kukosolewa wala hakukumtisha kwa sababu alimuweka Kristo mbele 2Wakoritho 12:1-10 “Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na
mafunuo ya Bwana.Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na
minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui;
Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu
huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui;
Mungu ajua);ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika,
ambayo haijuzu mwanadamu ayanene. Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu;
lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu
wangu. Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema
kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au
kuyasikia kwangu. Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa
mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije
nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu
kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu
hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi,
ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na
ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo
dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” Lengo lake yeye ilikuwa Yesu atukuzwe
katika mazingira yote, kwa msingio huo basi hatuna budi kuhakikisha kuwa
tunakabiliana na kutikuogopa aina yoyote ya kukosolewa tukijua ya kuwa kuna
lengo tunakusudia kulifikia .
12. Watu
wenye moyo wa ushujaa hawaogopi kupoteza
maslahi yao – Kupoteza maslahi ni moja ya hofu inayowakumba watu wengi
sana, kwa mfano kutokana na kujiunga na chama Fulani cha kisiasa na kupoinzana
na kingine unaweza kujikuta unapoteza maslahi, kumfuata Yesu na kuacha dini
nyingine inaweza kukufanya upoteze maslahi, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
alipoteza nafasi ya kuwa Mwalimu wakati wa ukoloni alipoanzisha TANU ili
kuwaunganisha watanganyika wapiganie uhuru, kwa hiyo ni wazi kuwa wakati
mwingine ili uelekee katika manufaa Fulani huna budi kukubali kupoteza maslahi
yako, Wafilipi 3:7-11 “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu
kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote
kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana
wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa
kama mavi ili nipate Kristo;tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu
mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika
Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na
ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo
yote kuifikia kiyama ya wafu.” Watu wanaowekeza katika biashara, na
maswala mengine mara nyingi ni risk takers wako tayari kujilipua, lakini wakati
mwingine tunaweza kuchukua hasara kwaajili ya kuwatetea wengine.
Hili ndilo jambo la msingi zaidi
ambalo mwanadamu anaweza kulifanya ili Mungu awe pamoja na kumfanikisha katika
kila jambo ni kuwa na moyo wa ushujaa, bila moyo wa haina hii huwezi kuitomboa
katika Nyanja ya aina yoyote ile
Ujumbe: Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni