Jumatano, 24 Februari 2016

Ufahamu Kuhusu Kitabu Cha Waraka Kwa Waebrania



Utangulizi;

     Kitabu cha Waebrania  au waraka kwa Waebrania uliandikwa kwa Wakristo wa Kiyahudi waliokuwa kwenye mateso na kukatishwa tamaa, Mwandishi  aliongozwa na Roho wa Mungu kuandika waraka huu kwa kusudi la kuimarisha Imani yao katika Kristo.

    Mwandishi anaelezea kwa makini ukuu wa Yesu Kristo na Ubora alionao na hitimisho la ufunuo na ukombozi wa Mungu katika yeye.

     Kwa ujumla waraka huu umekaa kimahubiri zaidi kuliko kiwaraka na hata hivyo unafaa sana kwa wainjilisti lakini zaidi sana kwa kuimarisha wakristo, Kitabu hiki kinakemea ile hali ya kudumaa kiroho na kinatoa maonyo kuhusu kukengeuka! Hasa baada ya kuwa washirika wa Yesu Kristo.Kitabu kinatia moyo kustahimili katika wokovu kwa gharama yoyote ile kikitia moyo kutokuiacha imani kukubali mateso na kuishi maisha matakatifu pia kinatia moyo maeneo mbalimbali ya kihuduma.

    Waraka kwa waebrania ni moja ya kitabu kinachotoa maana pana zaidi ya mambo unayoyasoma katika Agano la kale  hususani vitabu vile vitano vya Musa (Pentateuch) na pia vitabu vingine vya Manabii,Mashairi na vile vya kihistoria,Lakini zaidi sana unaweza kukielewa vema kitabu hiki endapo utakisoma pamoja au baada ya kusoma kitabu cha mambo ya Walawi,Kuna fafanuzi nzuri kuhusu kurudi nyuma na kukengeuka tofauti na wahubiri wengi wanavyopotosha kitabu hiki kinavyomaanisha , Kinapanua ufahamu mkubwa wa kutosha kumhusu Yesu Kristo na kinakuandaa kuwa mshindania imani mzuri katika kristo endapo utakielewa na ni maombi yangu kuwa Mungu akusaidie kukielewa katika namna iliyo nyepesi zaidi, Kitabu kitakusaidia kuelewa kwa Upana maana ya imani katika pande zake zote Mbili kwani wahubiri wengi huubiri upande mmoja tu wa Imani tofauti pia na kitabu hiki au mwandishi wa kitabu hiki alivyomaanisha,Ndani ya kitabu hiki utalihisi pendo la Mungu lilivyo kuu kwetu na utakubaliana nami kuwa Mungu ametuandalia mambo yaliyo bora zaidi neno hili bora zaidi ndio neno kuu la msingi la kitabu hiki cha Waebrania.

    Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote akiwa amejaa neema ya Mungu ameandaa somo hili katika mtindo utakaowafaa wanafunzi wa chuo cha Biblia, waalimu na wakristo wa kawaida na hata wasio wakristo ila wana mapenzi mema katika kutaka kujifunza maneno ya Mungu, Kilipoandikwa mara ya kwanza mwaka  mwezi January 2003 kiliandikwa kwa kusudi la kufundishia tu, lakini kwa kuwa watu wengi waliomba nikiweke katika mtindo wa kitabu cha kawaida nitajitahidi kukiweka katika mtindo utakao msaidia msomaji wa kawaida kuelewa. Ni matumaini yangu kuwa utakielewa kitabu hiki vizuri na utakitumia kwa utukufu wa Mungu basi kama kitabu hiki kinakubariki mpe Mungu utukufu na tuombee sisi waalimu kusudi tuweze kuleta tafasiri halali za neno la Mungu ili tusipate hukumu bali thawabu kwa kuwasaidia watu kulielewa Neno lake hili ndilo kusudi langu siku zote, Tuendelee katika Imani, Tuukulie wokovu na kusiwepo wepesi wa kurudi nyuma baada ya kuwa tumemjua Yesu Kristo Bwana wetu namna hii 

   Mungu na akubariki unapopitia kitabu hiki kikujenge kiroho na kikuelimishe na kukufungua katika maeneo mbalimbali ya maisha ya kikristo nakutakia kila la heri unapopitia kitabu hiki..Neema na upendo na amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.Amen.

                                            Hekalu la Yerusalem wakati wa Yesu

Muhtasari wa Kitabu Waraka kwa Waebrania.

       Kitabu cha waebrania kimegawanyika katika maeneo makuu mawili. Mafundisho kuhusu Ubora wa Yesu Kristo na mafundisho Kuhusu ubora katika maisha mapya ndani ya Yesu Kristo kwa msingi huo  utaweza kuona migawanyiko mikuu miwili katika sura ya 1-10 na 10-13.

1. “1-10” Ubora wa Yesu Kristo
2. “10-13”Ubora katika maisha mapya ndani ya Yesu Kristo.

I  Ubora wa Yesu Kristo.(Waebrania 1;1-10;31)
      A. Jinsi Yesu Kristo alivyo Bora zaidi.(Waebrania 1;1-4-13)
           a). Ufunuo ulio Bora zaidi wa asili ya Mungu (Waebrania 1;1-3)
           b). Ubora wake kama mwana pekee wa Mungu.(Waebrania1;4-2;18)
           c). Ubora wake zaidi kuliko Musa.(Waebrania 3;1-19)
           d). Ubora wake zaidi kuliko Yoshua (Waebrania 4;1-13).
      B.Yesu Kristo Kama kuhani mkuu aliye Bora zaidi. (Waebrania 4;14-10;31)
           a). Kuhani mkuu aliye Bora zaidi (Waebrania  4;14-5;10).
           b). Kuhani mkuu mkamilifu wa kudumu (Waebrania 7;1-28)
           c). Mhudumu wa Agano jipya lililobora zaidi (Waebrania 8;1-9;28)
           d). Ubora wa sadaka iliyo bora zaidi (Waebrania 10;1-31).
II. Ubora Katika maisha mapya ndani ya Yesu Kristo.(Waebrania 10-32-13;25).
           a). Njia iliyo Bora (Waebrania 10;32-11;40)
           b). Nidhamu iliyobora zaidi (Waebrania 12;1-29).
           c). Maisha yaliyo bora zaidi (Waebrania 13;1-25).

Kwa nini Tunasoma kitabu cha waebrania.

    Kwa nini tunasoma kitabu cha Waebrania,Kinatusaidia nini kitabu kilichoandikwa miaka karibu 2000 iliyopita kwa jamii ya wakristo wa kiyahudi kinaweza kutusaidia nini sisi leo? Maswala yafuatayo yaweza kutusidia kufahamu umuhimu wa kusoma kitabu hiki cha waebrania.
  • Kitabu hiki ni Sehemu ya Neno la Mungu ambalo limevuviwa (2Timotheo 3;16) .Kama neno la Mungu litatufanya kuwa wakristo wazuri na watumishi wazuri.
  • Kitabu kinafafanua ukweli wa kutimizwa kwa sadaka za kuteketezwa na sikukuu zilizotumika kama kivuli, katika agano la kale kumhusu Yesu Kristo.
  • Kina maonyo na mafundisho yenye kujenga ambayo ni muhimu kwetu katika siku za leo
  • Kinaonya na kuwajenga wakristo walio katika mateso na kuwatia moyo kuwa wasikate tamaa huku kikionyesha faida za kuendelea kumshika Kristo na hasara za kuiacha imani.
  • Kinabariki wasomaji na tunaweza kukitumia kwa mafundisho na mahubiri katika kuujenga mwili wa Kristo na Ufalme wa Mungu
  • Kitabu cha waebrania kinaweza kufanya kazi nzuri ya utetezi wa imani kwa wote wanaopinga ukuu wa Yesu Kristo na kupinga uungu wake,kinathibitisha kuwa Yesu Kristo ni Ufunuo wa Mwisho kabisa wa Mungu,na kuwa ni muumba ni mwenye amri na uwezo woote na ni mwenye kusamehe dhambi.
  • Kinaweza kutumika kama kemeo la ile Tabia ya kuuzoelea Ukristo na kudumaa kiroho kitabu hiki kinatia moyo swala zima la  kuukulia  wokovu .
Muundo wa kitabu cha Waebrania

  Kitabu hiki  kina nukuu nyingi sana kutoka katika Agano la kale  na kwa msingi huu kinatuthibitishia lile wazo sahii kuwa neno la Mungu limevuviwa kwani ingawa limeandikwa na watu tofautitofauti kiini chake ni kimoja tu wokovu wa mwanadamu
  •   Kitabu hiki kinafaa kusomwa sambamba na Vitabu vitano vya Musa na hususani kitabu kile cha mambo ya walawi,kitabu kina nukuu nyingi kutoka katika vitabu vya mashairi,Kihistoria na vitabu vya manabii kina maelezo mazuri ya kutimia kwa nabii mbalimbali kumhusu Yesu Kristo
  • Kitabu kinatumia Mafundisho ya agano la kale kama msingi wake katika kumuelezea Yesu Kristo,kinatumia watu na matukio katika agano la kale  kama mifano ya mafundisho yake,Kinaelezea kwa ufasaha matukio vivuli (Typology)  za dini ya kiyahudi zinazo muhusu Masihi Yesu.
Kiini kikuu cha kitabu cha Waebrania

  • Kiini kikuu katika kitabu hiki ni UKUU WA YESU KRISTO au UBORA WA YESU KRISTO.
  • Kitabu kinaonyesha jinsi ambavyo Kristo ni Ufunuo kamili wa mwisho wa Mungu kwa mwanadamu na hivyo ni Bora kuliko manabii (1;1-3)
  • Yesu anafunuliwa kama mkuu au bora kuliko Malaika (1;4-2;18)
  • Yesu anafunuliwa jinsi alivyo mkuu au bora kuliko Musa (3;1-6)
  • Yesu anafunuliwa jinsi alivyo mkuu au bora kuliko Yoshua (4;1-11)
  • Yesu anafunuliwa kama kuhani mkuu ambaye sifa zake,Tabia zake,huduma yake, na ukuhani wake ni mkamilifu na wa milele ulio bora kuliko walawi makuhani waliotangulia    na ni kwa mfano wa Melk- zedeki (4;14-10;18)
Neno kuu na Mstari mkuu katika Waebrania.  

      Mstari mkuu ni muhktasari wa kiini na kusudi kuu la kitabu cha Waebrania, neno kuu tunaweza kulipata au kuliona kwa urahisi kwa kuwa linajirudia rudia kama kiini kikuu cha kitabu kilivyo
  • Kulingana na maoni ya George A.C mwandishi wa studies in Hebrew kwake mstari mkuu ni Waebrania 13;8  Yesu Kristo ni Yeye Yule jana leo na hata milele”Yeye anauona mstari huu kama umekamilisha swala zima la Yesu asiyebadilika na kwamba unakamilisha ile dhana nzima ya Ubora wa Yesu Kristo.
  • Neno kuu la kitabu hiki ni UBORA WA YESU KRISTO hivyo neno Bora zaidi hujitokeza katika kitabu hiki likimuinua Kristo
  • Mstari mkuu hauwezi kuwa mmoja kulingana na kujirudia kwa neno hilo mara kadhaa hata hivyo mistari hii ifuatayo yoote huelezea jinsi Kristo alivyo bora zaidi kulingana na eneo husika .
         a). 1:4.................................   e).  7:22 ........................................... i). 11:16....................................
         b). 6:9................................    f).   8:6 ............................................  j).11:35………………………
         c). 7:7…………………...    g).   9:23 ............................................ k).11:40………………………
         d). 7:19..............................   h).10:34………………………………  l). 12:24……………………

Mwandishi wa kitabu cha Waebrania 

I.   Hakuna ajuaye kwa uhakika nani ni muandishi wa kitabu cha waebrania.wasomi wengi wamekuja na maoni na hisia mbalimbali kumhusu mwandishi wa kitabu cha Waebrania.
·         Clement wa Alexandria  aliamini kuwa waraka huu uliandikwa na Paulo mtume kwa Lugha ya kiebrania na kuwa Luka aliutafasiri katika Lugha ya Kiyunani.
·         Tertullian wa Afrika ya kaskazini  anaamini na kuelezea kuwa Barnaba mwana wa faraja atakuwa ndiye aliyeandika waraka huu wa waebrania na hizi ndizo sababu alizotoa katika kutetea hoja yake
    • Barnaba alikuwa ni mwenyeji wa Cyprus na kuwa wakazi wa Cyprus walikuwa Hodari sana katika ujuzi wa lugha ya Kiebrania na Kiyunani.
    • Barnaba alikuwa mlawi (Matendo 4:36). Kwa hivyo alikuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu ukuhani na sadaka za kuteketezwa na mtazamo mzima uliomo katika kitabu hiki cha waebrania.
    • Barnaba alikuwa mwana wa faraja “paraklesis” na kwa kuwa waraka kwa waebrania unafanya kazi ya kufariji huenda ikawa ni kazi ya Barnaba (13:22).  Na kwa hiyo hapa anawatia moyo waamini kubaki katika imani bila kujali ni aina gani ya mateso wanapitia
    • Barnaba alikuwa anakubalika na kuheshimika na wayahudi na wayunani kwa msingi huuo aweza kuwa mwandishi wa kitabu hiki.
  • Martin Luther aliamini kuwa Appolo huenda ndie mwandishi wa kitabu hiki .kwa nini?
a)       Appolos alikuwa myahudi mzaliwa wa Alexandria na namna mwandishi anavyotoa hoja zake ni wazi kuwa  ni kama alikulia katika ulimwengu wa ki Alexandria
b)       Alikuwa ni mtu anayejua kujieleza (Matendo18:24-25) Mtu anayejua kujieleza namna hii yamkini anaweza kuwa mwandishi wa kitabu hiki.
c)       Appolo alikuwa Msomi na mjuzi au hodari  katika maandiko (Matendo 18;24-25),Mtu mwenye ujuzi katika maandiko anaweza kuwa mwandishi wa kitabu hiki
  • Wasomi wengine wanaamini kuwa huenda Prisila na Akila wakawa ndio waandishi wa waraka huu kwa Waebrania wanaamini hivyo kwa sababu;-
a)       Prisila na Akila walikuwa ni waalimu hodari sana (Matendo 18:26) na wenye ujuzi katika maandiko.
b)       Nyumba yao kule Rumi ilikuwa ni kanisa (Rumi 16:5) na mwandishi wa kitabu hiki anatoa salamu kutoka Rumi au Italia (Ebra 13:24).
c)       Kwakuwa Prisila alikuwa mwanamke na wayahudi isingekuwa rahisi kumkubali mwanamke ndio maana hawakuweka jina la mwandishi katika waraka wao
  • Kwa mujibu wa tamaduni na wasomo wengi katika karne ya 19thc na 20thc wanaamini kuwa mawazo ya Paulo mtume yanaonekana kwa wingi katika waraka huu na hivyo wanaonyesha hisia zao kuwa Paulo ndiye mwandishi wa Kitabu hiki Waraka kwa waebrania, aitha tafasiri ya zamani ya biblia ya kiingereza KJV humtaja Paulo kama mwandishi wa waraka huo.
Mawazo ya wale wanaoamini kuwa Paulo ndie mwandishi wa Waraka huu

Wale wanaoamini na kutetea kuwa Paulo mtume ndie mwandishi wa kitabu hiki wana maoni haya kutetea hisia zao
  1. Wazo halitofautiani na lile la Paulo imani katika kristo
  2. Muundo na mtindo wa uandishi ni wa Paulo isipokuwa tu utangulizi wake
  3. Timotheo ametajwa kama mtendakazi wa karibu sana wa Paulo mtume
  4. Namna anavyomuelezea Kristo na ufafanuzi kuhusu ubora wake ni kiini katika nyaraka nyingine za paulo
  5. Mtazamo kuhusu sheria ya Musa na jinsi ilivyokamilishwa katika agano jipya
  6.  Msisitizo wa imani na namna anavyonukuu Agano la kale mfano mwenye haki ataishi kwa imani Ebrania 10;38 Rumi 1;17 na Galatia 3;11 ni mikazo ya Ki Paulo kabisa katika nyaraka zake
  7. mwangwi wa mzigo wa Paulo aliokuwa nao kwa Wayahudi na wakristo unaonekana katika waraka huu.
Mawazo ya wale wanaokataa kuwa Paulo sie mwandishi wa Waraka huu

  1. Mtindo na msamiati si wa Paulo
  2. Jinsi Paulo anavyoanza katika utangulizi wa nyaraka zake ni tofaut na huu
  3. Mtindo wa sheria,mawazo ya kiimani na ujuzi wa ukuhani kuhusu Kristo pekee ndio wa Ki Paulo.
  4. Waraka una alama za mtu msomi sana
  5. Wraka haubebi jina la Paulo kama ilivyo desturi yake
Hitimisho:  Mungu mwenyewe anajua mwandishi ni nani tunachotakiwa kushukuru na kufurahia ni kuwa tunalo neno lake zuri linalotutosheleza kwetu leo katika kumjua Kristo

Walengwa kwa waraka wa waebrania.

     Waraka unawalenga  wakristo wa kiyahudi waliokuwako katika maeneo mbalimbali huenda Rumi,au Yerusalem au Alexandria lakini mahali rasmi hapajulikani hata hivyo wanazuoni wengi wanaamini kuwa waraka huu uliwahusu waebrania waliokuwako Yerusalem pale Israel na hizi ndizo sababu wanazozitoa
  • Jina waebrania linawahusu waebrania ambao kwa asili waliishi Israel na jina Eber ni la asili ya baba za Ibrahimu na linawahusu wayahudi (Mwanzo 14: 13, 40:15).
  • Yerusalem ndio palikuwa kanisa hisika la Nyumbani la kuabudia wakristo wenye asili ya kiebrania
  • Maswala ya ukuhani,sadaka za kuteketezwa na mambo ya sheria aliyonukuu mwandishi hayangekuwa na maana sehemu ambako hakuna hekalu wala maswala hayo
  • Mitume inaonekana kuwa waliwahubiri (Ebrania 2:3-4)
Hali halisi ya wakristo hao wa Kiebrania

  • Inaonekana walikuwa wachanga sana kiroho na walikuwa wamekosa mafundisho
  • Inaonekana walikuwa na muda mrefu katika ukristo lakini walikuwa wachanga au walidumaa kiroho jambo lililowafanya kubaki wachanga10:32, 5:11
  • Hali ya mateso kwa ajili ya imani ilkuwa mbaya kiasi cha watu kumwaga damu
  • Inaonekana shughuli za kikuhani zilikuwa zinaendelea kwani hekalu lilibomolewa kati ya mwaka 70 baada ya Kristo
  • Inaonekana shauku yao kumhusu kristo ilikuwa imeshuka
  • Na wakristo hawa walikuwa wamefunzwa vizuri maswala ye sheria ya Musa
Tarehe ya Uandishi

  • Inaonekana kuwa waraka huu uliandikwa kabla ya hekalu kubomolewa mwaka wa 70.AD.
  • Huduma za kikuhani na sadaka za kuteketezwa zilikuwa zinaendelea Inaonekana ulikuwa wakati wa mateso na huenda ni wakati wa mtawala katili aitwae Nero kati ya 64-66 AD.
Makusudi ya kitabu cha waebrania 

    1. Kiliandikwa ili kwatia moyo wakristo wa kiyahudi wakati wa mateso
    2. Kuwaonya wakristo wakae katika imani Bora waliyoipokea
    3. kuwaonyesha jinsi Kristo alivyo bora ili kuwakinga wasirudi katika imani yao ya kiyahudi ya mwanzo
    4. kuwatia moyo waishi katika imani na kukabiliana na mateso
    5. na kuwaonyesha jinsi Maisha ndani ya Kristo yalivyo bora zaidi.
Hali halisi ya Wakristo wa Kiyahudi wakati ule

      Wakristo wa kiebrania wakati huu walikuwa njia panda, walikuwa wanakabiliwa na changamoto za kiimani na mateso, Uchanga wao uliwafanya wasione umuhimu wa kuendelea na imani ya Kikristo, walinyanyaswa na wayahudi wenzao kwa sababu ya kumfuata kristo, walisumbuliwa na kuachwa njia panda kama wamfuate Kristo au sheria ya Musa na wayahudi wenzao walikuwa katika kibano cha kumuabudu mtawala wa kirumi,aidha kulikuwa na imani nyingine potofu zilizokuwa zikiwakabili hivyo walikuwa njia panda. Na imani hizi ndizo zilizowaweka njia Panda;-

  •  Kulikuweko imani kama Legalism walioamini wokovu ni mpaka ushike sheria
  •   Kulikuweko imani ya  Sacredotalism walioamini wokovu kupitia sadaka  za Kikuhani 
  •    Kulikuweko imani ya  Gnosticism  walioamini wokovu kupitia maarifa au ujuzi hawa walikata uungu wa Yesu waliona kuwa haiingii akilini Yesu kuwa Mungu
  •  Kulikuwako na imani ya Antinomianism  walioamini kuwa mtu anatakiwa ajiishie vile anavyotaka bila kufuata sheria yoyote

Kwa hivyo waraka ulilenga kuwasaidia watu katika maeneo makuu mawili kitheolojia (elimu kuhusu Mungu) na kipolemics (Utetezi) kumhusu Kristo, kuhusu malaika, uanadamu na maswala ya Mambo yajayo. Na kusudi la kiutetezi kuwa wakristo wanapaswa kujua imani potofu zinazo wazunguka na kujua namna ya kuzikabili na kubaki katika imani ya Yesu Kristo.

SOMO LA KWANZA

UFUNUO ULIOBORA ZAIDI WA ASILI YA MUNGU.
     Mwandishi anaanza somo moja kwa moja kwa kufunua ubora alionao Yesu Kristo kwa kutaka kutuonyesha jinsi Yesu  alivyo bora zaidi kuliko manabii ambao mwanzoni walikuwa ndio njia ya mungu kujifunua kwa wanadamu,Kristo sasa ndio ufunuo ulio bora zaidi wa asili ya Mungu na ukamilifu wa Ufunuo wa Mungu. Kwa maana hii Mungu amejifunua kwa njia iliyo bora zaidi kupitia mwanae wa pekee Yesu kristo kuliko nyakati za manabii wa agano la kale na kwa njia ya Ajabu manabii wote walizungumza habari za kuja kwake katika somo la kwanza tutajifunza kwa kuzingatia vipengele vinne muhimu vifuatavyo;-

  • Mwana ni bora zaidi kuliko Manabii (Waebrania 1;1-3)
  • Mwana ni bora zaidi kuliko Malaika (Waebrania 1;4-2;18)
  • Mwana ni bora  zaidi kuliko Musa nabii (Waebrania 3;1-6)
  • Mwana ni bora zaidi kuliko Yoshua nabii ((Waebrania 4;1-13)
  • Maonyo ya kutokumpuuzia Kristo na maonyo dhidi ya kutokuamini (Ebr 2;1-4,3;7-19).
Mwana ni bora zaidi kuliko Manabii (Waebrania 1;1-3).

   Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi (Mstari 1) mwandishi anadokeza kuwa Mungu anasema na kuwa alisema na manabii kwa njia nyingi Je ni kweli Mungu husema naam ndio Mungu husema na hutumia njia nyingi inaaminika kuwa ziko njia zaidi ya 38 ambazo Mungu huzitumia kuzungumza nasi au alizitumia kuzungumza na manabii zifuatazo ni baadhi;-
  1. Huzungumza kwa sauti kubwa ya kusikika. Alifanya hivyo kwa watu kama Samuel, Abraham.n.k.
  2. Huzungumza kupitia asili= Uumbaji wake
  3. Huzungumza kupitia matukio ya kihisto = mfano kifocha Anania
  4. Huzungumza kupitia Roho wake = kwa sauti na msukumo wa ndani
  5. Huzungumza kupitia neno lake =  Biblia
  6. Huzungumza kupitia dhamiri zetu
  7. Huzungumza kupitia ndoto na maono
  8. Huzungumza kupitia Mazingira=.Baraka, adhabu, kufungua mlango au kufunga mlango,na hukumu,kwa kujibu maombi,miujiza au zawadi,uwepo wake n.k.
  9. Huzungumza kupitia Malaika zake
  10. Huzungumza kupitia watu wa kawaida waliookoka au hata wasiookoka.
Mwisho wa siku hizi Mungu amezungumza nasi kupitia Mwana wake, Huu ndio ufunuo wa juu kabisa wa Mungu kujifunua kwa wanadamu na ni ufunuo wa mwisho.Tukumbuke kuwa manabii wote wa Agano la kale walizungumza habari kumhusu yeye.Mungu alizungumza habari zake kupitia Henoko (Yuda 1;14-15) miaka mingi sana, Alimtumia Musa miaka 1400 K.K. Kutabiri habari zake (torati 18;15),Alimtumia Daudi  miaka 400 baada ya Musa na 1000 hivi K.K akisema habari zake (Zaburi 22) alimtumia Isaya nabii 750 K.K. kuzungumza habari za kuzaliwa,kutwaa mwili na mateso yake ya ukombozi (Isaya 7;14,9;6-7,53;1-12) na Mika 700 K.K kutaja mji atakaozaliwa masihi (Mika 5;2) hili linamaanisha wazi kuwa yesu ni Bora kuliko Manabii.

Sifa kumi za Yesu Kristo katika Waebrania 1;2-4.

  • Ni mwana wa Mungu
  • Mrithi wa Yoote.
  • Muumba ulimwengu
  • Mng’ao wa utukufu wa Mungu
  • Chapa ya nafsi ya Mungu
  • Mwenye kumiliki vyoote.
  • Mwenye amri na uwezo.
  • Aliyeleta utakaso wa dhambi.
  • Yuko mkono wa kuume wa Mungu
  • Ambaye Mungu amesema nasi
Sifa alizopewa Kristo hapa zina maanisha kuwa mwandishi alikuwa na lile wazo kamili la utatu wa kimungu na anmpa Yesu heshima ya uungu kabisa hii inakubaliana na umoja wa fundisho hili katika vitabu vingine vya agano jipya na hivyo ingawa mwandishi wa waraka huu hajulikani fundisho lake ni sahii na linakubaliana na wazo la kibiblia na dnio maana kiliingizwa katika kanuni za kimaandiko na kukubalika

Mwana ni bora zaidi kuliko Malaika (Waebrania 1;4-2;18).

      Katika Eneo hili mwandishi anaonyesha ubora alionao Yesu Kristo dhidi ya malaika kwani wakati huu ilikuweko imani ya Gnosticism ambao waliamoni  kuwa Yesu aliumbwa na kuwa yuko chini ya  Mungu na juu ya mwanadamu ila yuko sawa na malaika tu,Mwandishi alitaka kuwasaidia waamini kuelewa na kuikanusha dhana hii na kuonyesha kuwa Kristo ni Bora zaidi ya malaika

 Yesu Kristo Ni bora na mkuu zaidi ya Malaika


Malaika na Yesu Kristo wako katoka daraja moja na woote ni waombezi wa wanadamu kwa Mungu,Mwanadamu yuko chini kidogo ukilinganisha na yesu na malaika Hivi ndivyo walivyoamini agnosticism ndivyo wanavyoamini Mashahidi wa Yehova leo. Kuwa Yesu ni mwanadamu aliyetukuzwa kama malaika tu kwa ajili ya mwaisha yake.

   Dhana hii siyo sahii hata kidogo kwani mwandishi alitaka kuwaonyesha wakristo wa liiebrania wasijivunie mafundisho potofu yenye kumshusha hadhi Kristo iko tofauti kubwa kati ya Kristo na malaika kama jedwaqli lifuatalo linavyoonyesha;-

Malaika
Yesu Kristo
Malaika ni viumbe
Yesu Kristo ni Muumba
Hawakuweko Tangu mwanzo
Yuko tangu milele “Jana leo na milele”
Ni wadogo kwa Mungu
Yuko sawa na Mungu
Wana wahudumia waliookolewa
Ndiye Mwokozi
Ni watumishi wa Mungu
Ni mwana wa Mungu wa pekee
Wanamwabudu Mwana wa Mungu
Anaabudiwa na wanadamu na Malaika
Ni wajumbe
Ni mfalme

Nini maana ya kufanyika mdogo Punde kuliko malaika (Waebrania 2;9-10)

Mahali hapa mwandishi anashughulikia swala la kitheolojia ambapo Mungu alichukua mwili wa kibinadamu na kuwa kama mwanadamu (incarnation),Mwili wa kibinadamu ukilinganishwa na mwili wa malaika ya malaika ni bora zaidi na haina mupaka ,kitendo cha Yesu kristo kuwa mwanadamu kulimfanya awe  mdogo ukilinganisha na malaika kwa muda (Punde) ni kwa jinsi gani Yesu alifanyika mdogo punde kuliko malaika?
  • Alifanyika mwanadamu-malaika wana miili bora zaidi kuliko binadamu
  • Alikuwa na mwili wenye mipaka-malaika miili yao haoina mipaka.
  • Alichukua dhambi za wanadamu-malaika hawajui dhambi
  • Alikufa msalabani-malaika hawafi wala hawakuwahi kufa
  • Aliteseka msalabani -malaika hawawezi kuteseka
  • Alisikia njaa na kuchoka ,kukua– malaika hawasikii njaa wala hawachoki,wala hawakui.
Mwandishi wa waraka wa waebrania katika dhana hii anaona kuwa Yesu alifanyika mdogio punde kuliko malaika lakini aliadhimishwa mno  na hivyo malaika woote walipaswa kumsujudu na kumuadhimisha na amewekwa mkono wa kuume wa uweza wa Mungu.

Nini maana ya Neno Incanation (Tendo la kinyenyekevu (Mstari wa2; 5-18) .

  • Ni tendo la Mungu halisi kuutwaa mwili wa kibinadamu na kuwa Mwanadamu kamili kwa asilimia100% na wakati huohuo Mungu kamili kwa asilimia 100%
  • Kusudi lake ni kumfunua mungu kwa wanadamu na kukamilisha kazi ya ukombozi wa mwanadamu
  • Tendo hili lilifanyika kwa uwezo wa Roho mtakatifu kupitia Bikira Mariam luka 1;26-35,Mathayo 1;22-23.
  • Mungu kuuvaa mwili na kuwa mwanadamu ni tendo la unyenyekevu kwa nini? Kwa sababu aliacha enzi na utukufu na kuuchukua mwili huu dhaifu wa kibinadamu na kuonekana na umbo la kibinadamu fundisho hili huitwa (The Doctine of kenosis Filipi 2;5-11).
  • Kupitia tendo hili la incarnation Yesu aliweza kutuweka huru (2;14-15) kutoka kwa aliyekuwa na nguvu za mauti yaani ibilisi na kuwaweka huru watumwa wa hofu ya mauti
Nini faida za Yesu kuutwaa mwili wa kibinadamu Incarnation?
  • Alimshinda yeye aliyekuwa na nguvu za mauti shetani.
  • Alizuhubiri roho zilizokuwa kifungoni (1Petro 3;18-19),neno linalotumika katika Petro kuhusu kuzihubiri roho zilizokuwa kifungoni katika biblia ya kiyunani ni “Kerussen” amabalo maana yake ni kutangaza announce na sio kuhubiri kule tunakofikiri au tulikozoea
  • Kwa kuuvaa mwili amefaa kuwa kuhani mkuu mwenye rehema na mwaminifu katika mambo ya Mungu (Waebrania 2;17-18).Yeye anawajua wanadamu na anamjua Mungu hivyo yu afaa kuwa kuhani mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu.
  • Alijaribiwa sawa na sisi katika mambo yoote bila kufanya dhambi na kwa sababu ya ukamilifu wake tunaweza kuyategemea maombi yake,msaada wake na tunapata ujasiri wa kumuendea maana anatujua vizuri,mara nyingi tumewaeleza wanadamu shida zetu na hisia zetu na wakaishia kutuumiza zaidi kuhani anayefaa zaidi na mtu wa kumueleza shida zetu na hisia zetu ni Yesu Kristo pekee yake.
Nini maana ya Yesu Kristo kuwa mwana?
  1. Kule kuitwa mwana kunahusu ile asili ya uungu aliyonayo Yesu Kristo na ule uhusiano kuwa alikuwa na Mungu Baba siku zote hivyo ni tofauti na mwana wa mungu inavyotumika kwa wengine (Math.17: 5; 3:17 Yohana 1;14)
    • Neno mwana wa Mungu hutumika kwa makundi yafuatayo
Ø  Adamu mwana wa Mungu kwa kuumbwa (Created)
Ø  Malaika wana wa Mungu kwa kuumbwa (Created) Ayubu 2;1.6.
Ø  Waamini wana wa Mungu kwa kuwezeshwa (Adopted) Yoh 1;12
Ø  Yesu Kristo ni Mwana wa pekee (Yohana 1;14,3;16 Zaburi 2;7) Neno mwana wa pekee hutumika kama “Monogene” kiyunani ambalo maana yake wa asili moja na Baba hii maana yake Ni Mungu,ni wa milele,Hakuumbwa,Bali amekuwepo pamoja na Baba tangu milele ni wa asili moja (Filipi 2;5-8).

  1. Waebrania 1:2-3 Inaonyesha kuwa Mwana ni ;-
    • Muumba wa ulimwengu
    • Mrithi wa Vitu vyoote.
    • Mwenye kushikilia vyoote
    • Mng’ao wa utukufu wa Mungu
    • Chapa ya nafsi ya Mungu
    • Mwenye kufanya utakaso kwa dhambi
    • Aliketi mkono wa kuume wa ukuu huko juu
    • Mungu amesema nasi kupitia huyo
Maonyo ya kuto kumpuuzia Kristo (Waebrania 2;1-4).

     Mwandishi aliendelea kufafanua kuhusu Ubora wa Yesu kristo huku akisisitiza na kuonya kutokumpuuzia Yesu kristo na kuudharau wokovu tulioupata kwa yeye (Mstari 3) “Sisi je tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii? Kwa nini mwandishi anauona wokovu kuwa ni mkuu kwa sababu muhimu zifuatazo;-
Ulinenwa na Bwana nwenyewe,Umethibitishwa ndani yetu,Umethibitishwa kwa ishara na miujiza na Roho Myakatifu, Umegharimu maisha ya mwana wa mungu, Unatupa Uzima wa milele unatuokoa na dhambi mauti na kuzimu

Mwana ni bora  zaidi kuliko Musa nabii (Waebrania 3;1-6)

     Mwandishi anataka kuwaonya wakristo wa Kiebrania  kumtafakari Yesu kristo kama mtume na kuhani mkuu aliye mwaminifu na kuonyesha kuwa amestahili neshima kuliko Musa, huenda alitoa wito huu ili kuwalinda waebrania waliomwamini Yesu kutokurejea katika imani yao ya awali ya kiyahudi inayoamini katika sheria za Musa mwandishi anaonyesha ubora wa Yesu unavyozidi ule wa Musa kwa mtindo huu;-
  • Musa alikuwa kama mtumishi mwaminifu katika nyumba ya Mungu wakati Yesu Kristo ni  Mwana muaminifu katika nyumba ya Mungu.(2,5-6)
  • Musa kulinganishwa na Kristo ni sawa na kulinganisha  nyumba na mjenzi wa Nyumba Yesu ndiye mjenzi wa nyumba na ni Mungu (Mst 3-4)
  • Mwandishi hana mpango wa kumvunjia Musa heshima bali kuonyesha jinsi Yesu alivyo mkuu kuliko Musa maisha ya Musa na mapito yanafanana nay a Kristo katika hali kama hii;-   
  • Ukuu wa Nabii Musa.
Ø  Alikuwa mtoto wa kifalme (Nyumbani kwa Farao Misri)
Mrithi mtarajiwa wa Farao
Aliishi kama mtu maalumu (Prince) miaka 40 ikulu
Ø  Alikuwa mchungaji wa kondoo jangwani
Alijinyenyekeza
Alipata mateso magumu ya jangwani,upweke na kuwa mbali na ndugu
Aliishi kama tu duni miakla 40 jangwani
Ø  Alikuwa kiongozi wa taifa la Israel
Aliishi kama Mtumishi wa Mungu miaka 40.
Alionyesha njia,Nguvu za Mungu
Aliandika neno la Mungu (Sheria) Mungu ana tumia mtu duni.
  • Ukuu wa Yesu Kristo
Ø  Alikuwa mtoto wa kifalme Mbinguni
Mrithi wa Mungu
Alikuwako tangu milele na milele
Ø  Alijinyenyekeza Duniani
Aliteswa Msalabani,alikuwa mpweke mpaka msalabani
Aliishi  kama mtu duni
Ø  Amekuwa kichwa cha Kanisa
Ametunukiwa jina lipitalo majina yoote
Ametupa Neno la uzima wa milele (Injili)..

Kufanana Kwa Musa na Yesu Kristo Kihuduma na kimapito

1.       Woote wlikuwa viongozi
2.       Woote walikataliwa na watu wao (Kutoka 2: 15, Yohana 1:11)
3.       Woote walijaribiwa jangwani (Hesabu .20, Luka 4)
4.       Woote waliitwa Manabii (Torati 18: 5, Luka 24:19)
5.       Woote walikuwa wajenzi – Musa alijenga hema(Kutoka  40:1-33) -Yesu analijenga kanisa (Math. 16:18)
6.       Woote walifanya miujiza  (Kutoka 7, Matendo:22)
7.       Woote waliombea watu  (Hesabu 21:7, Yohana 17)
Pamoja na kuwa Yesu ana maswala yanayofanana na Musa kihuduma ama kimapito Bado mwandishi wa kitabu cha waebrania anawaonyesha wakristo wa kiebrania kuwa Yesu ni Bora zaidi ya Musa.

Maonyo dhidi ya kutokuamini (Waebrania 3;7-19)

  • Chanzo kikubwa cha watu wengi kurudi nyuma na kuacha wokovu ni kuto kuamini
  • Wana wa Israel waliifanya mioyo yao kuwa migumu (Zaburi 95;7-11)
  • Hali ya kutokuamini huzaa hali ya kuto kutii
  • Wengi wa wana wa Israel walioasi hawakuingia  katika inchi ya ahadi.
  • Mwandishi anataka tujifunze kutoka kwao na kuacha tabia ya kutokuamini.
  • Ugumu wa moyo na kutokuamini kunaweza kuzaa ukengeufu wa nafsi
  • Kuna uwezekano wa kupoteza wokovu kama mtu hatautunza na kuvumilia mpaka mwisho
Mwana ni bora zaidi kuliko Yoshua nabii ((Waebrania 4;1-13).

     Yoshua alikuwa mrithi wa Musa aliyewaongoza wana wa Israel baada yake alikuwa ni kijana jemadari wa Jeshi aliyewapigania watu wake kuhakikisha wanairithi raha ya kanaani kifo cha Musa  na uongozi wake wa sheria haungafaa kuwapa watu ushindi na kuwapa kustarehe huko kanaani hili linatufundisha kuwa sheria kamwe haiwezi kuwaongoza watu katika Raha. Yoshua aliwaongoza watu katika raha ya kanaani ni mfano wa Yesu kristo kutuongoza katika raha ya kweli ya moyoni.Waisrael walishindwa kumuamini Mungu jangwani kabla hawajaipata raha ya kanaani mwandishi anaona waebrania wanaokata tamaa kama wanaoacha kuamini na kutaka kujikosesha raha ya Kristo ya milele iliyoahidiwa.
     Mwandishi alitaka kuonyesha kuwa Yoshua ni kiongozi mwaminifu aliyeheshimika sana na wayahudi kwa kuwapigania na kuwapa raha ya kanaani,Lakini alitaka kuwaonyesha kuwa yesu Kristo ni mkuu zaidi ya Yoshua na kuwa anatoa raha iliyo bora zaidi na ya milele kuliko ile ya Yoshua ambayo kwa ukweli haikudumu .
Biblia inataja aina kuu nne za Raha;-

  • Raha ya sabato- Kupumzika kutoka katika kufanya kazi.
  • Raha ya Kanaani-Kupumzika kutoka katika safari ndefu ya Jangwani.
  • Raha ya utiii- Raha inayotokana na kumwamini Yesu
  • Raha ya Mbinguni-Raha ya kuingia katika ufalme wa mbinguni milele na milele.
Yoshua alitoa raha ya kanaani kwa kuwarithisha wana wa Israel nchi ile ya kikanaani na Yesu anatoa raha ya nafsi na raha ya kuwa na uhusiano na Mungu moja kwa moja na raha ya Roho mtakatifu neno la Mungu likiwa kipimo kikuu cha kuirithi raha hiyo.

Yoshua
  Yesu Masihi  
1. Jina Yoshua maana yake ni mwokozi
Jina Yesu maana yake ni Mwokozi
2. Ni Mwokozi wa Israel
Ni Mwokozi wa Ulimwengu
3. Alitoa urithi kwa ardhi ya kanaani
Anatoa Urithi wa uzima wa milele
4. Alitoa raha baada ya taabu ya jangwani na kuwashindia vita
Anatoa raha kutokana na mizigo ya dhambi na kuwapa watu ushindi
5. Aliwashinda maadui wa kawaida
Aliwashinda maadui wa ulimwengu shetani na jeshi lake
6. hakuwafuta maadui woote
Ametoa ushindi kamili dhidi ya Adui.
7. Alitoa raha ya Muda haikudumu
Ametuahidi Raha kamili isiyoisha (2:10)


SOMO LA PILI;

Yesu Kristo Kama kuhani mkuu aliye Bora zaidi. (Waebrania 4;14-10;31)

     Katika eneo hili mwandishi wa kitabu cha waebrania anajaribu kuonyesha jinsi Kristo alivyo kuhani mkuu aliye bora zaidi, mkamilifu na kuwa viwango vyake ni vya juu zaidi huduma yake ni kamilifu nay a milele iliyo bora zaidi na kasha anaonya ile hali ya kuendelea kudumaa kiroho na kuanguka katika wokovu baada ya neema na hatimaye anawajenga wakristo.

Ofisi za Masihi aliyekuwa anatarajiwa na Wayahudi.

     Masihi alitarajiwa kuwa kiongozi atakayetimiza majukumu ya ofisi kuu zipatazo tatu katika utu wake na kitabu cha waebrania kinaonyesha kuwa hayo yoote matatu masihi Yesu Kristo aliweza kuyakamilisha  ofisi hiizo ni kama ifuatavyo;-
  • Kama nabii (Ebr 1;1-3) Alitimiza huduma hii akiwa hapa duniani alifundisha ,alitabiri mambo yajayo na kufanya miujiza (Luka 24;19)
  • Kama kuhani (Ebr 2;14-16) Kutoka Calvary hata atakaporudi mara ya pili.
  • Kama Mfalme (Ebr 1;8). Alitoka katika ukoo wa kifalme (Mathayo 1;1-16) na atatawala dunia  wakati wa miaka 1000 ya utawala wake (Ufunuo 19;16).
Sifa za Yesu Kristo kama Kuhani mkuu

Basi iwapo tunaye Kuhani mkuu... Waebrania 4;14a.
Nabii ni mjumbe wa Mungu kwa watu wake ni msemaji kwa niaba ya Mungu  ”Nabi” Nabii huzungumza Neno la Mungu.
Kuhani ni muwakilishi wa watu Mbele za Mungu ni mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Kuhani hutoa sadaka za kuteketeza kwa mungu kwa niaba ya watu wa Mungu. Hivyo Kristo ni kuhani wetu mkuu ni mapatanishi wetu kwa Mungu. Makuhani pia walifanya kazi ya kuwakilisha mahitaji ya watu kwa Mungu,kuwaombea na kutoa sadaka ya dhambi kwa ajili yao ili wapatanishwe na Mungu ,walifanya kazi ya kufundisha na kuonya na kurejeza wapoteao walifanya kazi ya kusifu na kuabudu hivyo kusifu na kuabudu ni huduma ya kikuhani

Ukuhani Kabla ya sheria 

Kabla ya sheria makuhani walikuwepo wakati huu baba alikuwa ndiye kuhani kwa ajili ya familia yake. (Ayubu 1;5).
  • Alitakiwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya familia yake
  • Alitakiwa kuombakwa Mungu kwa ajili ya familia yake
  • Alitakiwa kuifundisha familia yake njia za Mungu na habari kuhusu Mungu
  • Mfano ni Adamu,Nuhu, Abrahamu Ayubu  na mifano mingineyo.
Ukuhani wakati wa Sheria.

  Kuhani alitakiwa kuwa na sifa za mwilini zenye ukamilifu wa hali ya juu (Lawi 21;1-24)  wakati huu Mungu alichagua kabila moja tu ya walawi na kuwaweka wakfu ili waifanye kazi hii  na walifanya hivyo kwa niaba ya waisrael pekee tu.

Yesu Kristo kuhani mkuu mkamilifu (Waebrania 4;14-5;10)

Kule kuwa Mungu na kuwa mwanadamu kunamfanya Yesu awe kuhani mkuu aliye bora zaidi
  • Anamjua Mungu na ana wajua wanadamu hivyo anafaa kuwa mpatanishi
  • Anafaa kuchukuana nasi maana anatujua udhaifu wetu na yuko tayari kutusaidia
  • Kama Mungu ana sifa ya Kutusamehe,kutuokoa na kutupa msaada
  • Anaweza kutekeleza mahitaji yetu na kutuwakilisha vema kwa Baba kwa kututetea kwa sadaka yake aliyojitoa Msalabani sadaka kamilifu ya kumpendeza Myngu ya kudumu
  • Kama mwanadamu aweza kuchukuliana nasi na kama Mungu  anatupa ujasiri na kututia nguvu
Ukuhani wa Haruni ni Tofauti na wa Yesu Kristo.

  • Yesu ndiye kuhani wetu mkuu kupitia uchaguzi wa kimungu ambaye amekamilisha matakwa yoote ya ukuhani mkuu ambayo Haruni hangeweza
  • Haruni angehitaji kupaingia patakatifu mara moja tu kwa mwaka Yesu ameingia maramoja kwa ujumla
  • Haruni alikuwa mwenye dhambi Yesu hakuwa na dhambi kwa hivyo ukuhani wa Yesu ni Bora zaidi kuliko wa haruni.
  • Yesu alikuwa mungu na alikuwa mwanadamu hivyo aliweza kumwakilisha mwanadamu ipaswavyo na Mungu ipaswavyo jambo ambalo Haruni hangeweza.
  • Sadaka za haruni hazikuweza kuondoa dhambi.Sadaka ya Kristo ni kamilifu na ni chanzo cha wokovu wetu milele.
Kuhani mkuu Bora zaidi kwa Mfano wa Melkzedeki (Waebrania 5;5-10,& 7;1-7 )

     Kumekuwa na utata wa kutosha miongoni mwa wana theolojia kumhusu Melkizedeki wengi wakimfikiri kuwa ni mtu wa namna gani na labda pengine ni Yesu Kristo mwenyewe miongoni mwa waliotoa maoni yao ni pamoja na ;-
  • Origen-Alitoa maoni kuwa Melkizedeki ni malaika
  • Hicracas-Alitoa maoni kuwa Melkizedeki ni Roho mtakatifu.
  • Ambrose Alitoa maoni kuwa Melkizedeki ni malaika wa Bwana yaani Kristo
  • Martin Luther  alitoa maoni kuwa Melkzedeki ni Shem.
  • Wengine- Mfalme wa nchi ya kanaani,Mungu mwenyewe au kristo mwenyewe.
Mwisho wa Utata kuhusu Melkizedeki

      Melkizedeki alikuwa mfalme wa wa kanaani mji wa Salem ambao sasa ni Yesrusalem na alikuwa kuhani wa mungu (Mwanzo 14;17-18) Yeye aliishi wakati uleule Ibrahimu alipokuwa anaishi,kama kuhani alikuwa na uwezo wa kubariki,kupokea fungu la kumi na alikuwa wa kabila nyingine,Ibrahimu hakumuabudu bali alimpa zaka kama nafasi ya kuonyesha heshima kwa watumishi wa Mungu kwa ujumla Mwandishi wa kitabu cha waebrania anamtumia kama mfano wa Yesu Kristo huenda ni kwa vile  alivyo na ofisi zifananazo na Kristo Mfalme na Kuhani na Pia kutoka kabila nyingine sio ya walawi.
Hana baba ,Hana mama
      Hii haina maana kuwa melkizedeki hakuwa na baba au mama au familia  wala hakuwa malaika  maandiko hayakuandika kizazi chake huenda Roho mtakatifu aliruhusu hilo ili awe mfano wa kumzungumzia Kristo, Jina lake MEHLECHZEHDEK maana yake ni mfalme wa haki,mfalme wa amani,hana baba wala mama hana mwanzo wa siku zake wala mwisho wa siku zake amefananishwa na mwana wa Mungu. Hii ni sawa na mimi mwandishi wa kitabu hiki naitwa Innocent mkombozi kamote.Jina Inoocent maana yake Asiye na Hatia au dhambi .hii ni maana tu ya jina langu hii haimaanishi kuwa sina dhambi au sikuwahi kuwa nadhambi hivyo maana ya jina inaweza kuwa tofauti na hali halisi,ndivyo lilivyo jina Melkizedeki Soma vizuri  (Waerbrania 7;1-3)

Yesu ni kuhani mkuu aliye bora zaidi kuliko Melkizedeki.

§  Yeye ni mfalme wa Yerusalem ya Mbinguni
§  Ni kuhani mkuu milele asiyekufa
§  Anasamehe dhambi
§  Alitokea kabila la Yuda/ Amechaguliwas na Mungu
§  Anaabudiwa na wanadamu na malaika
§  Wanaomtumikia hupokea sehemu ya kumi

Tofauti ya ukuhani wa makuhani Walawi na Ukuhani wa Yesu Kristo

Wajibu
Makuhani wa Kilawi
Kuhani mkuu Yesu Kristo
Watu wake
Waisrael tu
Ulimwengu mzima
Anawakilisha
Waisrael tu
Ulimwengu mzima
Maombezi ya
Waisrael tu
Ulimwengu mzima
Eneo la kazi
Katika Hema na Hekaluni
Kanisa na ktka mioyo .
Shughuli za uongozi
Ibada ,
Ibada katika roho na kweli
Sadaka
Wanyama
Yeye mwenyewe
Maombi
Duniani
Mbinguni
Kutia moyo
Jeshi
Watu wake
Hukumu
Baadhi ya matatizo
Ulimwengu mzima
hema
Ya kidunia
Ya Mbinguni
mafundisho
Sheria ya Musa
Injili
Usafi
Wa Nje
Wa mwili nafsi na roho

Wito wa kuikulia Imani (Waebrania 5;11-6;20).

     Mwandishi wa kitabu cha waebrania  kama ilivyo desturi  yake anapomaliza kumwelezea Kristo katika eneo Fulani  hutoa maonyo au mafundisho hapa anasisitiza  wajibu wa kuikulia imani ,mwandishi ana chukizwa na tabia ya  wakristo kudumaa kiroho (1koritho 3;1-3).

Ishara za Mtu aliyedumaa kiroho (Waebrania 5;11-14).
  • Uvivu wa kusikia au kuelewa
  • Kusahau mafundisho ya msingi
  • Kutokujua neno la haki
  • Kutokutendea kazi yale tunayojifunza
  • Kutokujua kupambanua mema na mabaya
  • Kutokuweza kufundisha
  • Kuwa na tabia ya kufarakana, migongano,na kuhusudu wanadamu.
  • Kutokuwa tayari kwa mafundisho zaidi.
Tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya kristo (Waebrania 6;1-3)

 Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu cha waebrania mafundisho ya kwanza ya Kristo ni yale yanayohusu;-
  • Toba kwa ajili ya dhambi
  • Kuwa na imani kwa Mungu
  • Mafundisho ya mabatizo.
  • Kuwekea mikono
  • Kufufuliwa wafu
  • Na hukumu ya milele
Mafundisho hayo hapo juu kwa mujibu wa mwandishi ni mafundisho ya watoto wachanga kiroho,wao huitaji kuongozwa sala ya toba kila wakati na huishi katika vifungo vya dhambi na kushindwa kujisamehe, Huitaji kutiwa moyo wamuamini Mungu ili kupokea miujiza yao na wasipoona miujiza hufikiri kuwa wameachwa na Mungu, wanahitaji mafundisho kuhusu mabatizo tutayachambua hapo chini na kutiwa moyo kwa kuwekewa mikono,kuwaelezea kuhusu ufufuo kwa sababu wanaogopa kifo na kuwatishia hukumu ya milele ili waishi kitakatifu.Agizo la Mungu ni pana kuliko mafundisho hayo tu hiki ndicho mwandishi anacho kimaanisha kwa watu waliodumaa kiroho au wachanga.

Aina za mabatizo.

     Biblia inaonyesha kuwa kuna aina mbalimbali za Ubatizo au mabatizo hapa tutaangalia aina nne tofauti zifuatazo;-
  • Ubatizo wa maji huu hufanyika mtu anapokua ameamini (Mathayo 28;19)
  • Ubatizo wa Roho mtakatifu hii ni ahadi ya kujazwa Roho (Matendo 1;8)
  • Ubatizo katika mwili wa Kristo hii hutokea mtu anapoamini (1Koritho 12;13)
  • Ubatizo wa Mateso huu ni ubatizo wa mapito mbalimbali kutokana na imani ndani ya kristo (Wafilipi 1;29,Marko 10;35-39)
Mafundisho + Kutendea kazi = Kukua kiroho.

Maonyo makali zaidi ni Onyo la kuto kukengeuka. (Waebrania 6;3-12) 

  • Swala la kukengeuka linauhusiano na kukataa kazi za Roho mtakatifu huku tukiwa tunajua wazi swala zima la utendaji wake (Mathayo 12;24-32,Yoh 16;8).
  • Ni rahisi kubaki na Ukristo pasipo imani.
  • Waamini wengi hujikwaa,wapatapo majaribu,wanaweza kufanya dhambi zisizo endelevu,wana hasira wivu,magombano Matendo ya mwili (Galatia 5;19-21) wafanyapo mambo kama hayo wameanguka , lakini hawajakengeuka.
  • Kukengeuka ni kuiacha kabisa Imani ni kuikana imani na ni vigumu sana kujua ni wakati gani ukengeufu umetokea Mungu mwenyewe ndie anayejua tunaweza tu kuona dadlili fulani lakini tusiwe na uhakika
  • Katika wakati huu Roho mtakatifu huwa hasemi na mtu huyo,dhamiri yake inakufa kabisa,hawi na tumaini la toba wala hawezi kutubu ukengeufu ni dhambi ya mauti (1Yohana 5;16-17) ni dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu
Bishano la Wakelvin na Waarminian linawekwa sawa na mwandishi wa Waebrania

  Mwandishi wa kitabu cha waebrania ingawa aliishi kabla ya bisha no la wakelvin na waarminian hapa ni kama anatumiwa na Roho wa Mungu kusaidia kuweka sawia mafundisho ya imani hizi mbili.
  • Wakelvin – Wanaamini kuwa mkristo wa kweli hawezi kupoteza wokovu na kuwa endapo imetokea hivyo basi alikuwa hajaokoka “Once saved forever saved”
  • Waarminian- Wanaamini kuwa mkristo anaweza kupoteza wokovu endapo hatautunza lakini pia aweza kutubu na kurejea.
Tumeamini Mambo yaliyo mazuri zaidi au Bora zaidi (Waebrania 6;9-20.).

   Mwandishi sio tu alikuwa anashindilia maonyo na mafundisho tu lakini pia bado anawasifu waamini kwa kuwatia moyo kuwa tumeamini mambo yaliyo mazuri zaidi ya wokovu waebrania nao walikuwa na mambo mema pia.
  • Mungu si dhalimu ni mwenye haki anakumbuka mambo mema wayatendayo watu na anatoa thawabu hivyo atawalipa wakristo wa kiebrania kwa ukarimu wao wakuwahudumia watakatifu.
  • Anawatia moyo kuwa na bidii na kuwa waidhihirishe mpaka mwisho(Mst 11)
  • Anawatia moyo wasiwe wavivu  bali wafuasi wa imani na uvumilivu kama kina Ibrahimu (mst 12).
  • Ahadi za mungu ni za kuaminika kwakuwa amejifunga kwa kiapo (Msta 13-18)
  • Tunaye mwokozi nanga yetu,Kuhani wetu mkuu na ni usalama wetu wenye nguvu (Mst 19-20).

SOMO LA TATU.
Huduma Bora zaidi Katika hema bora zaidi



     Katika sura ya 8-10 hivi mwandishi wa kitabu cha waebrania anazungumzia Huduma bora zaidi katika hema bora zaidi  hii ni hema ya kukutania ya kimbinguni,anazungumzia pia kuhusu agano lililo bora zaidi na huduma ya sadaka ya kuteketeza iliyo bora zaidi akimaanisha damu ya Yesu tofauti na damu ya Mafahari na mwishoni anatumia muda wa kutoa maonyo kwa wakristo tena. Ni kama Eneo hili limegawanyika katika vipengele vinne vifuatavyo
A.       Huduma katika hema iliyobora zaidi ya kukutania (8;1-5,9;1-28)
B.       Agano lililobora zaidi (8;6-13,9;1)
C.      Huduma na sadaka iliyo bora zaidi (9;1-23,10;18)
D.      Maonyo ya kutokufanya dhambi kusudi (10;19-39)

A. Huduma katika hema iliyobora zaidi ya kukutania (8;1-5,9;1-28).

Makuhani walifanya huduma zao katika hema ya kukutania ya kidunia iliyojengwa kwa mikono ya wanadamu wakiojazwa na Roho Mtakatifu ili kuwakilisha mambo muhimu sana ya hema halisi ya mbinguni.

Ufahamu kuhusu ile hema ya kukutania.

               I.      Hema hii iliitwa Patakatifu (kutoka 25;8) huenda ni kwa sababu ya uwepo wa Mungu
              II.      Iliitwa pia maskani (Kutoka 25;9)huenda kwa vile ilihesabiwa kama mahali akaapo Mungu
            III.      Iliitwa hema ya kukutania (Kutoka 40;2-3) huenda kwa sababu mungu alikuwa akikutana na watu kupitia hema hii.
           IV.      Iliitwa pia hema ya ushuhuda (Hesabu 17;8) huenda ni kwa sababu ndani yake kulikuwa na  sanduku la agano ambalo ndani lilikua na amri kumi za mungu zilizokuwa katika mbao mbili zilizoitwa za ushuhuda (kutoka 31;18,34;29).
             V.      Wakati wa zama za waamuzi ile hema iliitwa Nyumba ya Mungu (waamuzi 18;31).

Mafundisho muhimu kutoka katika hema ya kukutania na lile sanduku la agano

Hema ya kukutania na sanduku la agano liliwafundisha wana wa Israel mambo muhimu ya msingi kumuhusu mungu,tabia zake na namna ya kumkaribia yafuatayo ni muhktasari tu way ale ambayo hema inatufundisha;-
  1. Mungu ni mtakatifu sana na hakuna mwanadamu anaweza kumkaribia (kuta zile za pazia zilimaanisha haya)
  2. Wanadamu ni wenye dhambi na hivyo dhambi imewatenga wao mbali na Mungu
  3. Njia pekee ya kumfikia mungu ni kupitia kumwagika damu (damu zile za mafahari waliochinjwa)
  4. Mungu alikuwa anataka kukamilisha mpango wake wa kukaa kati ya wanadamu Mungu pamoja nai.
Utatu wa Mungu katika hema ya kukutania

 Maagizo ya ujenzi wa ile hema ya kukutania yalikwenda sambamba na maagizo ya ujenzi wa lile sanduku la agano.Sanduku la agano kilikuwa ni chombo kitakatifu sana kilifunikwa kwa dhahabu tupu iliyo safi,Urefu wake ulikuwa sentimita  kama 110 na upana 66 pia kwenda juu kwake 66,juu kulikuwa na kifuniko  kilichopambwa na sanamu za makerubi (malaika wa ngazi ya juu wa kivita) makerubi hao wawili walifunika kiti cha rehema kwa mbawa zao.

I.                     Hema ya kukutania ilikuwa na sehemu kuu tatu.
·         Ua wa nje.
·         Patakatifu
·         Patakatifu pa patakatifu (au patakatifu sana)
II.                    Hema ya kukutania ilikuwa na milango mitatu
·         Lango la ua wa nje
·         Lango la patakatifu (kwa pazia)
·         Lango la patakaifu pa patakatifu ( kwa pazia)
III.                  Hema ya kukutania ilikuwa ikiangazwa kwa aina tatu za mianga
·         Mwanga wa jua kwa ua wa nje
·         Mwanga wa taa yenye vinara saba kwa patakatifu.
·         Mwanga wa wingu la utukufu wa Mungu (shekinah) kwa patakatifu pa patakatifu.
IV.                 Hema ilikuwa na madhabahu kuu tatu za kunyunyizia damu ya upatanisho.
·         Madhabahu ya shaba katika ua wa nje.
·         Madhabahu ya dhahabu katika patakatifu
·         Na katika kiti cha rehema pale patakatifu pa patakatifu.
V.                   Hema ya kukutania ilipambwa kwa aina tatu za madini
·         Dhahabu- ambayo inafundisha uwepo wa Mungu
·         Fedha – ambayo inafundisha ukombozi.
·         Shaba – ambayo inafundisha juu ya hukumu
VI.                 Hema ya kukutania ilipambwa kwa aina tatu za rangi katika mapazia yake
·         Damu yam zee –inayofundisha upatanisho
·         Rangi ya bluu- inayofundisha ufalme wa mbinguni
·         Rangi ya zambarau inayofundisha kuhusu ufalme wa Mungu.

Utaratibu wa kupiga kambi kuzunguka hema na wakati wa Kutemmbea

Wana wa Israel walipokuwa jangwani walikuwa na utarartibu maalumu wa kutembea na pia wa kupiga kambi kuzunguka hema ya kukutania ,hawakujitembelea au kupiga kambi bila utaratibu mungu aliwawekea utaratibu maalum.

Wakati wa kupiga kambi utaratibu ulikuwa hivi;- Hesabu 2;1-31.

                                                                                                                     
Hivi ndivyo Israel walivyojipanga kuzunguka hema “H” Kabila nyingine na jinsi zilivyojipanga zinawakilishwa kwa Herufi zake N-naftali,A-asheri,D-dani,E-efraimu.M-manase,B-benjamin.G-gadi,S-simeon.R-ruben,Y-yuda.I-isakari.Z-zabuyloni. Kabila ya lawi ambao ni wahudumu waliishi karibu na hema ya kukutania

    Wakati wa kuondoka Musa alisema maneno haya “Inuka Bwana maadui zako watawanyike wakuchukiao” (Hesabu 10;35) na wakati wa kupiga kambi  Musa alisema maneno haya “:Ee Bwana uwarudie maelfu ya Israel” (Hesabu 10;36).

     Fundisho kuu tunalolipata hapa  ni kuwa Mungu anapaswa kuwa katikati ya maisha ya mwanadamu na ni lazima apewe kipaumbele au nafasi ya kwanza, ni muhimu kuanza siku na mungu na kumaliza na Mungu,pia mungu ndiye aongozaye watu na sio watu wamuongoze Mungu hivyo ni vema usiamue jambo kasha kumlazimisha mungu afanye. Mpangilio huu mzima unatukumbusha kuwa Mungu ni Mungu wa Utaratibu.

Wakati wa kutembea Utaratibu ulikuwa hivi Hesabu 10;11-33



                                                                                                                                     Walawi walibeba
                                                                                                                                    Sanduku la Agano
                           Wana wa kora                Wana wa Gershon na merari
                        Walibeba fanicha                  walibeba hema yenyewe
                              Za Hema

Hivi ndivyo wana wa Israel walivyokuwa wakitembea wakati wa safari ya jangwani walitembea kwa utaratibu maalumu sana wakifuata mpangilio wa kabila zao hapo juu.

Hema ya kukutania na maana zake Waebrania 9;1-12.

               I.      Ua wa nje . ua wa nje ulikuwa na;-
·         Birika la shaba .
Ø  Lilikuwa linahusika na maswala ya kutawadha kabla ya ibada
Ø  Inatufundisha umuhimu wa kutakaswa kwa neno la Mungu
Ø  Inatufundisha wajibu wa kujitakasa kila tunapokwenda mbele za bwana au kumfanyia bwana ibada au maombi.
·         Madhabahu ya shaba ya sadaka ya kuteketezwa
Ø  Inatufundisha Upatanisha kwa ajili ya dhambi
Ø  Inatukumbusha au kutoa unabii juu ya kusulubiwa kwa Yesu nje ya mji kalvary
Ø  Inatukumbusha kuwa Yesu ni mwanakondoo wa Mungu aliyechinjwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.

              II.      Patakatifu Mahali pa huduma ya makuhani
·         Taa ya vinara saba
Ø  Inatukumbusha ule ujumbe kuwa Yesu ni nuru ya ulimwengu.
Ø  Inatukumbusha waqjibu wetu wa kuwa nuru kwa ulimwengu.
Ø  Inatukumbusha swala zima kuangaza kupitia maisha yetu
      (Yohana 8;12,mathayo 5;14-16).
·         Meza ya mikate ya wonyesho.
Ø  Inatukumbusha ule ujumbe kuwa Yesu ni mkate wa uzima.
Ø  Inatukumbusha ule ushirika wa kiroho
Ø  Na ule ujumbe wa yesu aulaye mwili wangu.
·         Madhabahu ya dhahabu ya kufukiza uvumba.
Ø  Uvumba ulifukizwa hapa mara mbili kwa siku na harufu yake ilidumu kwa kutwa nzima
Ø  Inatufundisha kuabudu na umuhimu wa maombi
Ø  Inatukumbusha kuwa mtu muombaji yuko karibu sana na Mungu kama madhabahu hii ilivyokua karibu na patakatifu pa patakatifu

            III.      Patakatifu pa patakatifu (au patakatifu sana).
·         Palikuwa na shekina  au wingu la utukufu wa Mungu ulioonekana
Ø  Kuhani mkuu aliingia mahali hapa maramoja tu kwa mwaka(Lawi 16 na 23).
Ø  Siku hii ilikuwasiku muhimuna makini kwa utakaso
Ø  Watu woote walifunga masaa 24.
Ø  Kuhani mkuu alijitakasa  siku saba kwenye chumba maalum mbali na nyumbani kabla ya siku hii ya upatanisho
Ø  Mahali hapa palitengwa kwa pazia  jeupe la kitani safi lenye unene wa inchi nne na kupambwa kwa rangi mbalimbali ,blue zambarau na damu ya mzee
Ø  Pazia hili liliwatenga watu na uwepo wa Mungu (Kwa sababu ya dhambi ).na linawakilisha mwili wa Kristo (Mathayo 27;51).

Sanduku la dhahabu Agano
Sanduku linawakilisha uwepo wa Mungu,ni ishara inayoonekana ya Mungu asiyeonekana  hii  ina maana ya kuwa sanduku linamwakilisha Yesu Kristo mwenyewe  yeye ni chapa ya mng’ao wa utukufu wa Mungu (Waebrania 1;3).


 Sanduku la Agano la Bwana Mungu wa Israel
 

Sanduku la agano lilikuwa na vitu Vifuatavyo
§  Kopo la dhahabu lililokuwa na mana iliyohifadhiwa
Ø  Neno mana maana yake Cha Ajabu
Ø  Mana inatukumbusha ujumbe Yesu ni mkate wa uzima
Ø  Inatukumbusha kuwa Mungu ni wa fadhili na anajishughulisha na mambo yetu.
§  Fimbo ya haruni iliyochipuka.
Ø  Ishara ya kukomesha manung’uniko dhidi ya uteuzi wa Mungu(Hesabu 17;1-11)
Ø  Inawakilisha Ishara ya mamlaka ya Kimungu.
Ø  Ishara ya ufufuo ( Kitu kikavu kinapochipuka?)
§    Mbao mbili za sheria (Agano).
Ø   Ni ishara ya utawala wa Mungu,haki na hukumu.
Ø   Pasipo sheria hakuna dhambi,mungu alitaka Israel wajue kuwa wao ni wenye dhambi.

§          Juu ya sanduku la Agano kulikuwa na ;-
Ø  Kiti cha rehema  na makerubi wawili
Ø  Makerubi ni Ishara ya utii malaika ni watii sana
Ø  Kiti cha rehema ,haki,hukumu na neema
Ø  Damu ilinyunyizwa Ku “covering” kufunika kiebrania na kufanya upatanisho (rumi 3;25,1yohana 2;2)
Ø  Yesu amaetupatanisha na mungu kwa damu yake (1Yohana 2;2)..


Mpangilio wa vifaa katika Hema ya kukutania .




Inashangaza kwamba mpangilio  wa fanicha za ndani ya hema ya kukutania kwa ndani iko katika alama ya msalaba. Kama unavyoona katia kilelezo hapo juu.


Ubora wa hema mpya ya kimbinguni ya kukutania.

Ile ya agano la kale;-

Hema ile ya kimbinguni
Ni ya ulimwengu huu

Ni ya mbinguni.
Ni kivuli au ishara  ya ile halisi

Ni hema halisi naya kweli
Ilikuwa na mipaka kuhani tu aliruhusiwa kuingia katika patakatifu
Yenye kuharibika

Ni kwa watu woote kila mtu anao ujasiri wa kupaingia patakatifu pa patakatifu na kupataneema
Makuhani wake walikuwa dhaifu

Kuhani wake ni mkamilifu
Ilikuwa ya Muda

Ni ya milele
Dhahabu yake na madini yake ni ya kidunia

Dhahabu yake na madini ni ya kimbinguni.
Ni yenye kuharibika
Isiyo haribika

Agano lililo bora zaidi

Ø  Agano jipya ni njia ya Mungu kutuletea watu wake katika uhusiano mpya na yeye,agano la kale  lilikuwa na mipaka na lilishindwa kutuletea nguvu ya kuzitii sheria za Mungu (Waebrania 8;1-13).
Ø  Agano la kale lilitumika kama kivuli cha agano jipya  agano lililobora zaidi (Waebrania 8;1-5).
Ø  Ahadi nzuri katika agano jipya  ni pamoja na uhusiano mpya na Mungu (Waebrania 8;8-12).Nabii yeremia alitabiri habari za agano hilo jipya (Yeremia 31;31-34).
Ø  La kale liliandikwa katika mbao hili liliandikwa katika mioyo ya watu. Lile lilikemea dhambi bila kutoa njia ya ushindi hili  limetoa suluhisho na nguvu ya ushindi (ebrania 9;15-28)

Huduma na sadaka iliyo bora zaidi (9;1-23,10;18).
     Damu ya Yesu ndilo chimbuko na sadaka iliyo bora zaidi  na ndio kiini cha ukombozi na agano jipya (1Koritho 10;16,11;27,Efeso 2;13 1Petro 1;2,Ufunuo 2;8) .
Ø  Damu yake inasafisha kwa yeyote anaye mjia kwa toba
Ø  Inaweka huru kutoka nguvu za shetani na roho chafu
Ø  Inatufanya tuhesabiwe haki
Ø  Inaondoa hatia na kutupa ujasiri  wa kumtumikia,inatakasa watu wa Mungu
Ø  Inafungua njia ya kumuendea yeye moja kwa moja
Ø  Inatuthibitishia kuurithi ahadi zote ktk agano jipya
Ø  Imetuweka huru kutoka katikashughuli ya kuchinjachinja wanyama
Ø  Inatunenea mema kuliko ile ya habili iliyotaka kisasi.
     Damu ya mafahari ya mbuzi ilikuwa ni kivuli cha muda tu ili kusubiri wakati mkamilifu ije damu halisi ya Kristo iliyomwagika kwa ajili ya wengi
Ø  Ilihitajika damu ya mwanadamu aliye mkamilifu kwa ajili ya ukombozi
Ø  Damu ya wanadamu wengine zinapomwagika zinzlilia kisasi  hii rehema
Ø  Ilihitajika mtu aliye mbali na dhambi
Ø  Damu hii haidai kisasi inatoa msamaha
Ø  Yesu alijitoa kwa hiari yake mwenyewe mafahari walilazimika kuchinjwa bila hiyari yao
Ø  Mafahari walihitaji kuchinjwa mara kwa mara Kristo mara moja tu kwa mara zoote kwa sdaka ya milele
Muhktasari
Waebrania
Sifa/asili
Agano la kale
Agano Jipya
8;5-6,15
Mpatanishi
Musa
Yesu
8;6
Ahadi
Mkazo mwilini
Mkazo rohoni
8;9-14,15.
Kuokolewa
Toka misri
Toka dhambini
8;9,12-15.
Hali ya wokovu
Kushika sheria
Kumwamini Yesu
8;7-10,9-10.14
Nguvu
Dhaifu
Roho wa mungu
9;1,9-14
Kuabudu
Kwa nje /kwa muda
Katika rohona kweli
9;1-12,23-25
Patakatifu
Pa Kidunia
Pa kimbinguni
9;8.
Patakatifu zaidi
Palifungwa
Pamefunguliwa
9;12-23
upatanisho
Damu ya mafahari
Damu ya Yesu

Maonyo dhidi ya kufanya dhambi kusudi (Waebrania 9;10,19-39).

      Mwandishi hapa anaonya tena kuhusu tabia yenye kuelekea katika ukengeufu (6;4-8). Biblia ya Kiswahili inatumia neno kufanya dhambi kusudi lakini NIV. Inatumia neno “ If we deliberately keep on sinning” hii inamaanisha tabiya ya kufanya dhambi endelevu hapa  inamaanisha tabia yenye kudumu katika kutenda dhambi bila kumaanisha kuziacha hii ni tabia mbaya sana na inaelekea katika ukengeufu .
      Aidha inawezekana watafasiri wa Biblia ya Kiswahili wamatumia neno kusudi kutokana na ukweli kuwa kulikuwa na namna ya kuuthibitishia umma wa wakati ule kama umemkana Yesu hadahrani ulitakiwa kuonyesha kivitendo kwa kuruka damu ya fahari iuliyochinjwa na kumwaga katika shimo ili kuthibitisha kuwa hutashikamana na Yesu tena jambi hili mwandishi analiita kusudi nalo pia ni swala linaloongoza katika ukengeufu.
        Dhambi ya ukengeufu kwa kawaida inafanyika kukiwepo ujuzi wa kutosha kayika swala lile ambalo mtu amelielewa vema na kwa kutokujali au kwa jeuri anapuuzia na anakataa maonyo na kukataa ukweli kuhusu Mungu jambo kama hili lilikuwa wazi kwa mafarisayo amabao walijua kwa hakika Yesu alikuwa akitoa Pepo kwa Roho wa Mungu lakini kwa jeuri na kejeli walitaka kuudanganya umma kuwa Yeye anafanya hivyo akitumia mkuu wa pepo.
     Tabia ya kupenda kumpinga roho mtakatifu ambaye kwa kawaida ndio chanzo kikuu cha kutuvuta katika toba kinaleta ugomvi usiokuwa na mpatanishi kwani ukiisha kukosana naye katika nafsi tatu hakuna nyingine inayoweza kufanya kazi hiiyo ya kukupatanisha kwa mungu hata ufikie toba,aidha tabia hii mwandishi ameeiita Kumkanyaga Kristo na kumsulubisha tena,kuhesabu damu aliyoimwaga kuwa ni kitu ovyo na kumuasi roho mtakatifu atoaye Neema ya toba. Inatisha kuanguka katika mikono ya mungu aliye hai.
Ø  Mwandishi anahitimisha kwa kuonya kuwa tusifanye dhambi kusudi 32-36
Ø  Tuzikumbuke siku za kwanza Tulipokwisha kutiwa nuru hiki ni kipimo kizuri cha upendo mkuu tuliokua nao kwa Mungu hata kama tulikua wajinga bado hatukua na upendo mdogo tulikuwa na pendo kuu sana hivyo tukumbuke wakati ule na tuufuate (32-34)
Ø  Tusiutupe ule ujasiri wetu maana una thawabu ili kuwa na subira tupate ile ahadi ahadai za Mungu zinategemea uvumilivu wetu na subira.
Ø  Mwandishi anahitimisha kwa kuwakumbusha kuwa Yesu anarudi (37)
Ø  Na kuwa mwenye haki ataishi kwa imani (38)
Ø  Na anawaaminisha kuwa sisi si miongoni mwa hao waiona imani wanaosita na kupotea bali ni miongoni mwa walio na imani ya kuokolewa kwa Roho zetu.

SOMO LA NNE

      Ubora Katika maisha mapya ndani ya Yesu Kristo.(Waebrania 10-32-13;25).

Mwandishi anamalizia somo laka kwa kuonyesha kuwa maisha ya imani ndani ya Kristo ni ya Muhimu na ni bora zaidi bila kujalikuwa ni mapito gani tunayapitia  aidha alitaka kwaamini kuwa tayari kupokea maonyo na adhabu anazotupa mungu na umuhimu wa kuheshimu ndoa na kuishi maisha ya utakatifu ambayo ni bora zaidi hivyo eneo hili limegawanyika katika vipengele vitatu vifuatavyo;-

           a). Njia iliyo Bora (Waebrania 10;32-11;40)
           b). Nidhamu iliyobora zaidi (Waebrania 12;1-29).
           c). Maisha yaliyo bora zaidi (Waebrania 13;1-25

Njia iliyo Bora (Waebrania 10;32-11;40)

Mfano wa kustahimili mabaya   na kuishi kwa Imani sura 11
Neno imani liko katika maeneo makuu mawili “Hupomone” Gk yaani imani ina pande zake mbili Imani iletayo ukombozi na imani ya kustahimili mabaya kwa uaminifu hata kufa bahati mbaya wahubiri wengi hupenda kuhubiri upande mmoja wa imani ya mafanikio na ukombozi mwandishi wa kitabu cha webrania anazionyesha imani kwa pande zake zote mbili  Kwamab  wakati mwingine inatugharimu hata kufa nab ado tukahaesbiwa na Mungu kuwa tu watu wa imani

Imani iokoayao ya ukombozi mifano

Ø  Daniel toka katika tundu la simba
Ø  Shadrak,Mesheki na Aberdnego kutoka katika miale ya moto
Ø  Daudi kutoka katika makali ya upanga au mkuki wa Sauli.

Imani ya kustahimili mabaya kwa uaminifu hta kufa (hupomone)
Ø  Isaya kukatwa kwa misumono hata kufa
Ø  Yakobo tume kukatwa kichwa
Ø  Stefano kuuawa kwa kupigwa mawe.
Kibiblia hawa woote ni mashujaa wa imani haina maana kuwa Mungu anapotuacha tuangamie katika mateso ndio amepungua uwezo Yeye hubaki kuwa Mungu tu na hufaa kuaminiwa kwa gharama yoyote wahubiri ni muhimu kuhubiri kwa kubalansi maandiko.

Msaada kutoka kwa wingu kubwa la Mashahidi. (12;1-12)
Wingu kubwa la mashahidi ni akina nani umewahi kujiuliza? Watu wengi huchanganyikiwa,zamani biblia ilipokuwa inaandikwa haikuwa na sura wala aya hizi ziliwekwa baadae na wataalamu ili kutusaidia kuisoma kwa urahisi bila kupotea hivyo wakati mwingine kifungu Fulani kinaweza kuwa na uhusiano na kifungu Fulani cha juu au chini kama ilivy mahali hapa wingu ni mashujaa waimani waliotajwa katika sura ya 11
Ø  Wingu nimashujaa waimani waliotumika kututia moyo
Ø  Wanatutia moyo kuishi kwa imani aidha kwa mema au kwa mabaya au kwa kusubiri sana au kwa uvumilivu au hata kwa kutokuipokea ahadi kwa wakati
Ø  Nani anaweza kuwa wingu la mashujaa leo?
§  Mashujaa wa imani katika Biblia
§  Mashujaa wa imani katika historia ya kanisa
§  Mashujaa katika nyakati zetu
§  Mkristo yoyote aliyekutia moyo kivitendo
Kama wako watu walioweza kustahimili namna hii wa Agano la kale je sisi wa agano jipya tunashindwaje kustahimili katika ubora huu wa maisha mapya? Tufanye nini basi
  • Tuweke mbali mizigo yoote 12;1
  • Tujilinde na dhambi ile ituzingayo kwa upesi
  • Tupige mbio kwa saburi
  • Tumtazame Yesu kiongozi mkuu wa wokovu wetu12;2
  • Tushindane kabisa na dhambi hata ikiwezekana kumwagika Damu
  • Tukubali maonyo na marudia ya Bwana yakiwemo majaribu.
Nidhamu iliyobora zaidi (Waebrania 12;1-29)
Nidaamu na kurudiwa ni sehemu kabisa ya ukristo wengi ambao wamekuwa wakiadhibiwa na kuwekwa chini ya nidhamu kisha wakanyenyekea wamekuwa watu  wazuri na wakubwa sana katika Imani Petro alikemewa sana na Bwana,Tito alipokea maonyo na baadae kuwa kiongozi mkubwa sana 2koritho 8;16-17 Adhabu na maonyo vina faida sana ingawa wakati unapitia inaonekana kama mzigo na wakati usiofaa hata hivyo adhabu zinatakiwa kuwa zenye lengo la kurejeza na sio kuua kama wafanyavyo baadhi ya viongozi wa kidini mungu alitoa adhabu kama baba aliyekua akimuonya mtoto wao hutoa adhabu kama sehemu ya kuua huduma changa zilizo tishio dhidi yao wakiwa wamejaa wivu wasiwasi na mashaka ya vyeo walivyo navyo huku wakiwa wanakuhesabu kama mtu usiyefaa tena au usiyeweza kupona hii ni dhambi na mungu atawarudia na kuwalipa kwa wakati wake 

Nidhamu au marudio yana faida gani?
  • Yana tujengea imani kubwa
  • Yanatufundisha utii
  • Yanatufundisha kuwavumilia wengine
  • Yanatufundisha kumjua Kristo katika mapito aliyoyapitia
  • Tanatujengea kujaa neema na faraja ya kimungu
  • Yana turekebisha kutoka katika tabia zisizofaa
  • Yanatupatia thawabu  mbinguni
  • Yanatua kukua kiroho
  • Yanakufanya utambue upande wa pili wa watu wanaokuzunguuka
  • Yanatutengenezea mafunzo,Amani,na kutupa kuhesabiwa haki
 TUFANYE NINI TUNAPOPATWA NA MABAYA AU MAGUMU?
     Tufurahi tukijua kuwa Mungu amaruhusu tumuombe kwa imani tukitarajia ukombozi au uvumilivu.falsafa kuhusu mateso ni mjadala wa muda mrefu na wa siku nyingi dini nyingi zina maoni mbalimbali kuhusu mateso;
  • BUDHA-Wanaamini  kuwa chanzo cha mateso yoote ni tama,watu huteseka kwa sababu ya tama,kwa sababu anatamani kitu Fulani akiridhika mateso hukoma
  • WAHINDU- Wanaamini mateso ni matokeo ya  matendo mabaya Karma hii ni kama ul;ipokuwa mwanadamu wa kudni Fulani hukuishi vizuri ukizaliwa mwanadamu tena au kiumbe kingine unavuna yale uliyoyatenda
  • WAISLAM- Wanaamini kuwa kila linalokutokea ni majaliwa ya mwenyezi Mungu mwenye kutoa neema kubwakubwa na ndogondogo na hivyo tunatakiwa kukubali majaliwa hayo ya Allah
  • WAYAHUDI- wanaamini  mateso ni matokeo ya dhambi yako binafsi au ya wazazi wako (Yohana 9;2)
Ziko sababu mbalimbali za mateso
  • Kwa sababu ya asili ya dhambi ya Adamu
  • Kwa sababu ya dhambi za watu wengine ,Vita,magonjwa ubinafsi,ulevi n.k
  • Mungu anapokuwa ameruhusu kwa sababu mbalimbali
  • Mambo ya asili, uchafuzi wa mazingira,ajali,
  • Kutokutumia akili tulizopewa na Mungu
  • Shetani kwa ajili ya uvamizi, mashambulizi, kutujaribu, wivu wake n.k.
  • Kutiwa nidhamu na Bwana kwa ajili ya kutuimarisha, kuturekebisha, kutufanya tukue n.k.
Mikono iliyolegea na magoti yaliyoopooza. (Waebrania 12;12-13).

   Huenda mwandishi hapa anazungumzia wajibu wa kuwatia moyo watu dhaifu katika kazi ya Mungu,watu dhaifu katika maadili ya kikristo,watu waliokata tama au kuvunjika moyo ya kuwa tusiache kuwasaidia na kuwatia moyo badala ya kuwakatisha tama na kuwaua kiroho hii ndiyo huduma ya kimasihi haikuja kuangamiza bali kuponya.

Umuhimu wa kuwa na Mahusiano Bora (Waebrania 12;18-28)

     Hakuna jambo la msingi duniani kama kuwa na uhusiano mzuri na kila mtu, Biblia inatutaka tuwe na amani na watu woote , Shina la uchungu ni chuki kali na hasira ambazo zinaweza kusababishwa na mahusiano mabaya na kuharibu wengi.Kwa sababu ya uchungu watu wengi sana wameweza kuliharibu kanisa la Mungu na kuunajisi utakatifu hivyo tunataadharishwa mfano wa Esau ni mfano wa tabia hizo nah ii ilipelekea neema kupunguka kwake na kupoteza mambo mazuri aliyoyalilia sana baadae asiyapate.

 Mjadala kuhusu mlima Sinai na mlima sayuni (Waebrania 12;18-29)

     Hofu katika mlima Sinai
  • Mungu alitumia njia ya kutisha sana katika mlima Sinai (Kutoka 20;20)
  • Ili hofu ya Mungu iwasaidie Israel Kumcha yeye na kuishi maisha matakatifu
  • Mungu aliwapa Amri kumi na kufanya Agano nao kupitia Musa
  • Mlima Sinai unatufundisha  hasira ya sheria kuwa haina huruma
  • Wale woote wanaotaka kuishi maisha ya sheria wanataka kuishi chini ya hofu na amri nah ii ina maana kwa kushika sheria bado hakuna mwanadamu awezae kumkaribia Mungu watu waliookolewa hawako chini yam lima wa Sinai
   Furaha katika mlima wa Sayuni
  • Sayuni ni mlima wa amani na mapumziko baada ya taabu nyingi,katika Yerusalem kiko kilima kilichoitwa sayuni ambayo yalikuwa ni makazi ya mfalme mkuu Daudi mji huu utakuwa makao makuu ya masihi atakapokuja
  • Mwandishi anaashiria kuwa iko sayuni ya kimbinguni ya dunia ni nyumba ya Mungu ya kidunia na ya mbinguni ni nyumba ya Mungu ya mbinguni waliokolewa makazi yao mlima wao ni wa mapumziko na furaha ,majina yetu yameandikwa huko na Kristo ndiye kiongozi wetu na usalama ni kamili kwa ajili ya majeshi ya malaika elfu nyingi
  • Hivyo tuwe waangalifu tusimkatae yeye kwani Yeye pia ni moto ulao  tumtolee ibada ya kumpendeza na  Mst 25-29)
Maisha yaliyo bora zaidi (Waebrania 13;1-25)
  Mwandishi anakamilisha kazi yake kwa kuwaasa wakristo waishi maisha yaliyo bora zaidi .Wakristo wanaweza je kuishi maisha hayo yaliyo bora zaidi ni kwa utakatifu na kwa kudumisha upendo wa ndugu.

Upendo wa ndugu na udumu
  • Utatusaidia kusaidiana sisi kwa sisi
  • Inatutia moyo.
  • Itawafanya wtu wasirudi nyuma na pia wavutiwe na upendo wetu,
  • Itafanya mungu ashughulikie mambo yetu tunaposhughulkia na wengine
Kuwafadhili wageni
     Ziko sababu saba kwa nini tuwafadhili wageni
  • Wanahitaji msaada wetu wa kimwili na kiroho
  • Watavutwa na upendo wetu na kuamini
  • Wanaeza kuwa waamini wanaohitaji marafiki.
  • Wakati mwingine tunaweza kupokea malaika waliotumwa kwetu
  • Kunasaidia kutukuza kiroho
  • Mungu atatulipa kwa ni ni sehemu ya ukarimu.
Umuhimu wa kuheshimu ndoa 13;4
  • Ni lazima malazi yawe safi  neno malazi maana yake ni Koite Gk coitus Eng
  • Neno malazi limetumika kama lugha ya mficho.  “Euphenisim”
  • Neno hili humaanisha Tendo la ndoa , hili hubeba nguvu ya familia yoyote na kam ndoa itachezewa basi nguvu ya familia inachezewa na kuharibiwa.
Kusudi la Mwandishi kuzungumzia ndoa.
  • Mwandishi alitaka kuondoa dhana mbili potofu zilizokuwa zimejengeka katika wakati ule kuhusu ndoa
  • ASCETICISM- hii ni jamii ya watu walioamioni kuwa na kiasi katika raha zozozte za mwili hivyo waliitesa miili yao (1Koritho 7;5)
  • Gnosticism –Tawi mama la imani hiyo hapo juu waliamini kuwa kila kitu nidhambi likiwemo tendo la ndoa,walikula chakula cha kawaida na kuitesa miili Tendo la ndoa ndani ya ndoa lilifikiriwa kuwa ni dhambi hivyo walinyimana
  • Wengine walijitenga na familia zao na kuishi maisha ya kitawa
  • Dini nyingi ikiwemo katholic waliiga imani hizi
  • Mungu alianzisha ndoa Yeye mwenyewe hivyo swala la tendo la ndoa katika ndoa ni halali Makuhani katika agano la kale waliruhusiwa kuoa
  • Imani nyingine mwandishi alikuwa anaishughulikia ni imani ya ANTINOMIANISM neno hili maana ya ke ni kinyume cha sheria
  • Hawa waliamini mtu akiwa ndani ya Yesu hayuko chini ya sheria byuko huru lakini hata hivyo uhuruwao ulipita mipaka
  • Waliamini kuwa unaweza kufanya lolote lile ukiwa umeokoka nahaina madhara wala hufungwi
  • Waliweza kutoa talaka,kuazimana wanawake kubadilishana waume na kufanya uasherati  Mwandishi anakemea tabia hii akitaka ndoa iheshimiwe. Kwani Mungu angewahukumu waasherati.
Kutokuheshimu ndoa maana yake ni nini ?

  • Imani hizi zoote mbili hazikuheshimu maana ya ndoa na zilikuwa na mawazo mabaya
  • Zilifungua mlangowa zinaa na uasherati
  • Zilipelekea zinaa za jinsia mojaq na matumizi yasiyo ya asili na utoaji wa talaka hovyo
  • Mwandishi anaona sio sahii swala hili na anaonya kuwa ni kinyume na maisha yaliyobora ndani ya Kristo na kuwa huko ndio kutokuheshimu ndoa.
  Mausia ya mwisho
§  Kuwakumbuka wale waliokuwa wakituongoza na kuiiga imani yao 7
§  Kristo Yesu habadiliki 8
§  Kukataa mafundisho ya kigeni yaliyo potofu 9-14
§  Kuwatii wenye kutuongoza kama watu watakaotoa hesabu tuwaombee 15-19
§  Salamu za mwisho 20-25.
 Mungu akubariki unapoendelea kujifunza kutoka Blog Hii Ndimi Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima. Rev. Innocent Kamote.


Hakuna maoni: