2Timotheo 4:9-11 “Jitahidi kuja kwangu
upesi. Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda
Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. Luka peke yake
yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa
utumishi.”
Utangulizi:
Ni maneno ya huzuni na masikitiko
makubwa sana kutoka kwa mtume Paulo, akiwa kifungoni katika siku zake za
mwisho, kabla kidogo ya kuhukumiwa kifo. Akiwa katika gereza lenye kutisha liitwalo
“Mamertine Prison” akisubiria hukumu
yake ya kifo, Katika wakati huo Mgumu anaachwa na mtenda kazi maarufu sana
aliyewahi kuwa karibu sana na mtendakazi pamoja naye katika kazi ya injili
aliyejulikana kwa jina la Dema, Ni katika namna ya kusikitisha sana Paulo akiwa
katika maumivu hayo Dema anaamua kuachana na injili na kwenda katika jiji la
Thesalonike Ugiriki ya leo, kwenda kuishi maisha ya kutanua na kustarehe, “Dema aliniacha akiupenda ulimwengu huu wa
sasa”, ni ujumbe unaobeba fundisho muhimu sana kuhusu hatari ya kuanza
vizuri na kumaliza vibaya! Wakati Paulo akiwa anafurahia kumaliza vizuri huduma
yake Dema anamaliza vibaya kwa kurudi nyuma na kwenda kujirusha duniani.
Matendo 20:22-24 “Basi sasa, angalieni,
nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo
yatakayonikuta huko; isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema,
ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu
cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa
Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.”
Tuitajifunza somo hili Dema
aliniacha akiupenda ulimwengu huu wa sasa kwa kuzingatia vipengele vitatu
vifuatavyo:-
·
Dema ni
nani na alikuwa nani?
·
Dema
aliniacha akiupenda ulimwengu huu wa sasa.
·
Mambo ya
kujifunza kutoka kwa Dema.
Dema ni nani na alikuwa nani?
Jina Dema kwa asili limetokana na
jina la Kiyunani Dēmos ambalo maana yake kwa
kiingereza ni “The people” mzizi mmoja na jina Nicodemus ambalo kwa kiingereza ni “Victory of the people” kwa hiyo jina Dema maana yake ni watu. Na Nicodemo maana yake ushindi wa watu. Dema
hakuwa mshirika wa kawaida tu kanisani na katika huduma, Yeye alikuwa ni
Mtumishi wa Mungu katika timu ya umisheni pamoja na Paulo Mtume na anatajwa pamoja na Luka yule tabibu
mpendwa, mwandishi wa Injili ya Luka na kitabu cha Matendo ya mitume pamoja na
kina Epafra mwanzilishi wa makanisa ya Kolosai, Laodikia na Hierapoli.
Wakolosai 4:12-14 “Epafra, aliye mtu wa
kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili
yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana
katika mapenzi yote ya Mungu. Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa
ajili yenu, na kwa ajili ya hao walioko Laodikia, na kwa ajili ya hao walioko
Hierapoli. Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.”
Maandiko yanamtaja Dema pamoja na
watumishi wa Mungu wa ngazi ya juu kabisa wenye sifa njema, na wote tunajua
jinsi ambavyo Paulo mtume alikuwa makini sana katika kuchagua watu wema wa kuambatana
naye katika kazi ya injili, kwa hiyo iko wazi kuwa Dema alikuwa sehemu muhimu
ya timu ya wamishionari na mtendakazi, Pamoja na Paulo mtume. Na alijulikana
sana kuwa aliitenda kazi ya Mungu pamoja na watu wengine maarufu katika
watendakazi wenza pamoja na Paulo mtume, Dema alikuwa pia katika timu moja na
Marko mwandishi wa Injili ya Marko na pia Aristrarko, na wengineo, alikuwa
muhubiri wa injili, alikuwa mmishionari, alikuwa mpanda makanisa kwa hiyo ni dhahiri
kuwa alikuwa mtendakazi aliyeweza kustahimili magumu mengi katika safari ya
injili, kimsingi aliianza kazi hii vizuri.
Filemoni 1:22-24 “Na pamoja na hayo
uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana nataraji ya kwamba kwa maombi yenu
mtajaliwa kunipata. Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu,
akusalimu; na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami.”
Hata hivyo katika mazingira ya
kustaajabisha na ya kusikitisha sana mtumishi huyu wa Mungu maarufu namna hii
tunataarifiwa kuwa alirudi nyuma alimuacha Mtume Paulo akiwa gerezani kisha
akaenda zake jijini Thesalonike kwenda kufanya biashara zake akiupenda
ulimwengu wa sasa hii maana yake ni nini? Hilo linatupa nafasi kutafakari
kipengele cha pili cha somo hili Dema aliniacha akiupenda ulimwengu huu wa
sasa, kama Dema angemuacha Paulo mtume na kwenda kuhubiri sehemu nyingine hiyo
ingekuwa njema na Paulo asingelihuzunika lakini Dema aliupenda ulimwengu huu ni
msiba hasa kwa Paulo kwa kuwa Dema hakwenda kuihubiri injili bali alirudi
duniani huko Ugiriki.
Dema aliniacha akiupenda ulimwengu huu wa sasa.
Biblia haitoi maelezo mengi
kwanini Dema alirejea nyuma, akiiacha kazi ya Mungu na mateso ya Mtume Paulo
gerezani, lakini ufafanuzi wa maneno ya Paulo unatupa picha kubwa na ya kutisha
na kusikitisha kuhusu mkasa wa Dema,
Kimsingi mstari wa “10” 2Timotheo 4:10 “Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa,
akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.”
Unasomeka hivi katika Kiyunani “yáp Dēmas
egkataleipō, agapaō ton nun aiona” Katika maneno hayo ya Kiyunani neno Agapaō
linamaanisha “sacrificial love” kujidhabihu
kwa hiyo Dema alikuwa amejidhabihu kwa dunia badala ya kazi ya Mungu, hii maana
yake aliipenda sana dunia, alikubali kuvutiwa nayo, alishikamana na dunia kwa
moyo wake wote na neno “Aiona” yaani ulimwengu wa sasa
linamaanisha alishikamana na mfumo wa sasa wa dunia hii ikimaanisha kutafuta
Heshima, kutafuta mali, na usalama wa kidunia Dema aliamua kufanya hivyo kwa
sababu wakati huu ulikuwa ni wakati wa hatari sana kujitoa kwaajili ya injili,
mateso kutoka utawala wa kirumi yalikuwa yamepamba moto kinyume na Ukristo na
injili yake, wakristo walikuwa wanateswa, kuuawa na hata kufungwa kwa hiyo Dema
aliogopa alikimbilia katika jiji kubwa la kibiashara la Thesalonike huko Ulaya Ugiriki ambako kulikuwa na kanisa letu huko
lakini hakurudi kanisani na badala yake alirudi katika maisha yake ya kawaida
na kufanya biashara akiishi maisha ya kawaida akiachana na huduma ambayo kimsingi ilikuwa inagharimu
maisha ya watu, aliogopa kuifia injili.
1Yohana 2:15-17 “Msiipende dunia, wala
mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani
yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho,
na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia
inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata
milele.”
Warumi 12:1-2 “Basi, ndugu zangu, nawasihi,
kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya
kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya
dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi
ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
Dema hakuwa mshirika wa kawaida
alikuwa mtumishi wa Mungu alishiriki katika kazi ya injili, sio wakati wote
mazingira yalikuwa rahisi lakini alivumilia kurudi nyuma kwa Mtumishi wa Mungu
kama Dema ni swala la kusikitisha sana na ni swala lenye kuogopesha, Dema
alikuwa askari wa mstari wa mbele, Kadiri tunavyokua na kuinuliwa katika imani na kushinka nafasi za kitumishi hatunabudi kuongeza
kiwango chetu cha kujitoa kwa Mungu na kumpenda Yesu, Shetani haogopi kuwa
umefikia ngazi gani ya kiroho anaweza kukurejesha Duniani, kwa uwazi au kimya
kimya.
Mambo ya kujifunza kutoka kwa Dema
Kumfuata Yesu
kunahitaji kujikana nafsi – Leo tunamuhubiri Kristo na tunaweza tusisikie
wahubiri wakirudi nyuma kwa sababu kwanza injili inalipa, watu wengi sana
wamebarikiwa kutokana na kuihubiri injili katika wakati huu wa Amani, lakini
yako mazingira ambapo mambo yanaweza kuwa magumu na mateso yakazidi hapo waoga
wote wataondoka kwenye mfumo, tujikumbushe kuwa kumfuata Yesu kunahitaji
kujikana na kubeba Msalaba
Luka 9:23-25 “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na
ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu
atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake
kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata
ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?”
Kumfuata Yesu
kunahitaji kuhesabu gharama – Yesu anawataka wanafunzi wake watambue kuwa
kumfuata Yesu ni gharama ni sawa na mtu anayetaka kujenga mnara, ni lazima ukae
upige hesabu na kufanya maandalizi ya kutosha ili usije ukawa dhihaka kwa kushindwa
kukamilisha mradi wako, Dema alishindwa kukamilisha mradi.
Luka 14:28-30 “Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara,
asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije
akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza
kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.”
Kumfuata Yesu
ni kama kuanzisha vita – taifa lolote linapoanzisha vita na taifa lingine
au ufalme wowote unapoanzisha vita na ufalme mwingine ni lazima taifa hilo au
ufalme huo ukae chini na kupiga hesabu zake vizuri na kufanya mashauri au
upelelezi wa kutosha kama unaweza kupigana na upande wa pili na kupata ushindi
na ukiona vita inakuwia ngumu basi omba agano la Amani
Luka 14:31-33 “Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme
mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu
kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? Na kama
akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa
mwanafunzi wangu.”
Kumfuata Yesu
ni kama kulima kwa jembe la kukokotwa na wanyama – Jembe la kukokotwa na
wanyama kama ng’ombe kwa kawaida mtu anapolitumia kwenye kulima haliruhusu
kusimama au kuangalia nyuma, mkulima wa jembe la kukokotwa na ngombe ni lazima
aangalie pale anapolima ni lazima aangalie mbele asiondoe mawazo yake katika
shughuli hiyo kwani kuangalia nyuma kunapoteza sifa ya mkulima wa aina hiyo
hali kadhalika mtu anayemfuata Yesu
Luka 9:61-62 “Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini,
nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, Mtu
aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.”
Kumfuata Yesu
kunahitaji uaminifu hata kufa – Mungu kweli atatukoa wakati mwingine katika
mitego ya adui, na vita za aina mbalimbali kama ilivyokuwa kwa Dema, tunakuwa
salama wakati wote Bwana akiwa upande wetu hata hivyo yako mazingira kama haya
ambayo Paulo mtume alikuwa anakabiliwa na kifo ni ukweli ulio wazi wengi
walimuacha, kuna wakati tunapaswa kuwa waaminifu hata kufa lakini sio kila mtu
anataka kifo, kuwa tayari kwa hilo kwaajili ya Kristo ni dhabihu ya hali ya juu
sana ni kukubali kuwa shahidi wa Yesu Kristo uliye mwaminifu
2Timotheo 4:16-17
“Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu
aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa
jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi
yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami
nikaokolewa katika kinywa cha simba.”
Ufunuo 2:9-10 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)
najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi
la Shetani. Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa
baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe
mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
Matendo
21:10-14 “Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi,
nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. Alipotufikia akautwaa
mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema
hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi
huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa. Basi tuliposikia haya, sisi
na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu. Ndipo Paulo
alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya
kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana
Yesu. Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na
yatendeke.”
Kumfuata Yesu
kunahitaji uwe imara – Kila mwanafunzi wa Yesu anapaswa kukumbuka wakati
wote kujiimarisha katika Imani ili kuhakikisha kuwa kila siku tunapiga hatua na
kukua kiroho, hata pamoja na kuwa tunamtumikia Mungu, Dema alijisahau, Paulo
mtume anasema hakujihesabu kuwa amefika lakini kila wakati alikuwa akiendelea
na mazoezi muhimu ya kiroho ili asifanye kazi ya kuhubiri tu wengine kisha yeye
akawa mtu wa kukataliwa, uzoefu na kurudi nyuma kwa Dema kunatukumbusha kwamba
tunapaswa kuhakikisha kuwa tunajiimarisha kila iitwapo leo
Wafilipi
3:12-14 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha
kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa
ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba
nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma,
nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya
mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.”
Mathayo 7:2-27
“Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye,
atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua
ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka;
nalo anguko lake likawa kubwa.”
Mathayo
13:20-21 “Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye
alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake,
bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara
huchukizwa.”
Watu wa Mungu tunaowajibu wa kuhakikisha kuwa
tunamaliza vizuri, inasikitisha sana kuona mtu mkubwa aliyembatana na muhubiri
mkubwa kama Dema akirudi nyuma, na kuipenda dunia, Shetani haogopi kuwa
umefikia ngazi gani ya kiroho, kwa sababu hiyo kila wakati tujilinde katika
neema ya Mungu, na kuendelea kujidhabihu na kutokukata tamaa kwa sababu ya
dhiki na mambo mengineyo, na badala yake tujiimarishe katika Bwana ili kila mmoja
wetu aweze kumaliza vizuri, tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima
kipo na ni rahisi kuvutwa kwenye ulimwengu huu kama hatutashikamana na
utimilifu wetu wa Imani mpaka mwisho.
Na. Rev.
Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye
Hekima

Maoni 2 :
Ukiwa umefanya kazi maisha yako yote kujenga familia na urithi, huwezi kuruhusu kivuli cha mtu wa tatu kiiharibu katika miezi michache tu. Niligundua kuwa mabadiliko ya ghafla ya tabia ya mume wangu yalikuwa kuingiliwa kiroho, si tu mgogoro wa katikati ya maisha.
Niliwasiliana na Mystic Kakaa kwa ajili ya uingiliaji kati wa kibinafsi. Kazi yake ilikuwa ya upasuaji. Alitambua kivuli na kukiondoa kabisa bila drama yoyote ya umma. Ndani ya siku 5, umakini wa mume wangu ulirudi nyumbani kwetu na katika mustakabali wetu. Ikiwa unalinda maisha yenye thamani kubwa na unahitaji bwana anayeelewa busara, wasiliana naye kwa: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159
Yeye ndiye kiwango cha dhahabu.
Kwa uchawi wa upatanisho wa uhusiano/ndoa.
Uchawi wa kumfanya mpenzi wako wa zamani/mwenzi wako aombe msamaha.
Uchawi wa kumrudisha mpenzi wako/kumvutia mpenzi mpya.
Uchawi wa kurejesha mali/pesa zilizoibiwa.
Mabadiliko ya umbo/Uchawi wa kutoweka.
Uchawi wa kushinda bahati nasibu/kesi ya mahakama. Na zaidi
Nataka kutoa ushuhuda kuhusu jinsi nilivyopona kutokana na Virusi vya Herpes. Miezi michache iliyopita nilikuwa na dalili kadhaa. Nilienda kumuona daktari na vipimo vingi vya damu vilifanywa kwangu, baadaye niliambiwa nilikuwa na Herpes. Daktari wangu aliniambia kwamba hakuna tiba ya Herpes. Nilijisikia vibaya, niliingia mtandaoni nikitafuta tiba inayowezekana ya Virusi vya Herpes, niliona chapisho la Dkt. Dawn, daktari wa mitishamba anayewasaidia watu kupona kutokana na Herpes. Saratani. VVU na mengineyo. Niliwasiliana naye na kumwambia jinsi ninavyohisi. Alisema dawa yake ya mitishamba inaweza kuniponya. Alinitumia dawa kupitia huduma ya utoaji wa UPS na nilipokea dawa siku 6 baada ya kuituma, nilichukua dawa kama alivyoniagiza. Kabla sijakamilisha dawa dalili zilisimama. Nilienda kwa daktari na kufanya kipimo kingine cha damu, cha kushangaza nilikuwa hasi. Sijapata dalili tena. Dkt. Dawn ni mzuri na unaweza
kuwasiliana kwenye WhatsApp: +2349046229159
Gmail ( dawnacuna314@gmail.com )
Ikiwa unahitaji dawa za mitishamba kutibu magonjwa yoyote sugu au ya zinaa kama.
HERPES.
SARATANI.
VVU/UKIMWI na zaidi
Chapisha Maoni