Jumanne, 28 Septemba 2021

Msikilizeni Israel, Baba yenu!


Mstari wa Msingi:- Mwanzo 49:1-2 “Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.”


Utangulizi:

Wakati huu ulikuwa ni wakati Muhimu sana kwa Yakobo, kuhitimisha maisha yake na kazi yake hapa Duniani, Yakobo kama mrihi wa Baraka za Ibrahim na Isaka sasa ana watoto wengi na sasa anataka kuwabariki, kulingana na kile Mungu alichokikusudia katika maisha yao ya baadaye, lakini kukiwa kwa kiwango Fulani kimeathiriwa na mwenendo na tabia zao za maisha ya awali, sio tu Yakobo anataka kuwabariki lakini, Yakobo anataka kutoa neno la kinabii kwa watoto wake wote, yale atakayoyasema sio tu yana maana kubwa kwa wana wa Israel na kabila zile kumi na mbili za wana wa Israel bali yana maana pana sana kwa kila mmoja wetu hebu turudie tena kile ambacho neno la Mungu limekisema:-

Mwanzo 49:1-2Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.”

a.       Yakobo anaanza kwa kuwaita wanae ili aweze kuwatabiria na kuwaambia yale yatakayotokea katika maisha yao siku za baadaye, jambo ambalo pia linaweza kumtokea kila mmoja wetu, sisi ni wana wa Israel kwa njia ya imani ni watoto wa Ibrahimu na warithi wa ahadi za Mungu kama ilivyo kwa Isaka na Yakobo, kwa hivyo Yakobo ameita mtoto mmoja baada ya mwingine ili aweze kuwabariki na kuwatamkia Baraka sawasawa na matendo yao. Baraka hizo kimsingi zinamuhusu kila mmoja wetu sawasawa na matendo yake na kwa kadiri ya neema ya Mungu, hivyo kwa kadiri unavyotenda na kwa kadiri Mungu anavyousoma moyo wako ndio utakavyoona Baraka zako na namna unavyoyaandaa maisha yako ya baadaye ama namna na jinsi unavyoweza kuamua kubadilika.

 

b.       Kabla ya kuanza kuangalia jumbe zile za muhimu sana kuwahusu wana wa Israel ni vema kwanza tukajua idadi yao na namna wana wa Israel walivyozaliwa.

 

Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili (12) kwa mujibu wa maandiko na binti mmoja aitwae Dina, Mwanzo 35:23-26, Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni. Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini. Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali. Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu. watoto wake walitokana na wake zake wawili pamoja na masuria wake wawili ambao kwa jumla yao ndio walimpatia watoto wale kumi na mbili 12” Kwa hivyo tumeona maandiko yakituelekeza wana wa Israel 12 pamoja na mama zao:-

 

a.       Kutoka kwa Lea ni Reuben, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabulon

b.       Kutokwa kwa Raheli ni Yusufu na Benjamin

c.       Kutoka kwa suria kijakazi wa Lea Zilpah ni Gad na Asheri

d.       Kutoka kwa suria kijakazi wa Raheli ni Dani na Naftali

 

c.       Maana za majina ya wana wa Israel.

 

-      Reuben – ni kijana wa kwanza wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:32 “Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda.” – Maana ya jina Bwana meona teso langu

-      Simeon – ni kijana wa pili wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:33 “Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.” – Maana ya jina Bwana amesikia teso langu

-      Lawi – ni jina la kijana wa tatu wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:34 “Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.” – Maana ya jina Bwana ataungana nami

-      Yuda – ni jina la kijana wan ne wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:35 “Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.” – maana ya jina Mara hii nitamsifu Bwana

-      Dani – ni jina la kijana wa tano wa Yakobo kwa Bilhah mjakazi wa Raheli Mwanzo 30:6 “Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.” – Maana ya jina lake Bwana amenipa haki yangu

-      Naphtali – ni jina la kijana wa sita wa Yakobo kwa Bilha mjakazi wa Raheli Mwanzo 30:8 Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.” – Bwana amenipa Ushindi

-      Gadi – ni kijana wa saba wa Yakobo kwa Zilpa mjakazi wa Leah Mwanzo 30:11 “Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.” – Bahati njema

-      Asheri – ni kijana wa nane wa Yakobo kwa Zilpa mjakazi wa Leah Mwanzo 30:13 “Lea akasema, Ni heri mimi, maana wanawake wataniita heri. Akamwita jina lake Asheri.” Maana ya jina lake – Nimebarikiwa

-      Issakari – ni kijana wa tisa wa Yakobo kwa Leah, na kijana wa tano kwa Leah Mwanzo 30:18 “Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari.” Maana ya jina lake Mungu amenilipa.

-      Zabuloni – ni kijana wa kumi wa Yakobo na mwana wa sita kwa Leah Mwanzo 30:20 “Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni.” Maana ya jina lake Bwana atakaa nami

-      Yusufu – ni kijana wa kumi na moja kwa Yakobo mzaliwa wa kwanza kwa Raheli Mwanzo 30:24 “Akamwita jina lake Yusufu, akisema, BWANA aniongeze mwana mwingine.” Maana ya jina lake Bwana aniongeze.

-      Benjamini – Ni kijana wa kumi na moja wa Yakobo mzaliwa wa pili wa Raheli Mwanzo35: 18 “Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.” Maana ya jina lake mwana wa mkono wangu wa kuume.

Yakobo anawaita wanawe:

Inawezekana ilikuwa ni desturi yake Yakobo kama Kuhani wa Bwana na Kiongozi mkuu wa familia kuwakusanya wanae, lakini kusanyiko hili lilikuwa na upekee, lilikuwa na upekee kwa wana wa Israel lakini vilevile lina upakee kwa kila mmoja wetu leo, Hapa Yakobo hakuwa ametoa wito wa kawaida tu, hili huenda lilikuwa kusanyiko lake la muhimu na la mwisho, lakini vilevile lilikuwa ni kusanyiko maalumu la kinabii, Yakobo alikuwa anatangaza Baraka kwa watoto wake mmoja baada ya mwingine wote walibarikiwa na pia kutabiriwa sawasawa na jinsi baba yao alivyoona vema na vilevile sawasawa na Matendo yao, baba yao hakuwa mwenyewe tu Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye, halikuwa kusanyiko aliloliita yeye tu lilikuwa ni kusanyiko ambalo uwepo wa Mungu vilevile ulikuwepo ili kuwabariki na kuwatamkia wana wa Israel Baraka zao na kuwakemea na kuwaonya, Huku kwa kiwango kikubwa matendo yao yakichangia kwa kiwango kikubwa Baraka zao na utabiri wa nini kinaenda kuwatokea wao katika siku za mbele ni ukweli ulio wazi kuwa Yakobo anatufundisha kuwa iko siku Bwana atazihukumu siri za wanadamu kama Yeye alivyohukumu maisha ya wanawe sawa na matendo yao waliyoyafanya iwe wazi au sirini na kwa kadiri ya mabadiliko na ukomavu wa mioyo yao, Bwana atazihukumu siri za wanadamu kwa kadiri ya injili tuliyoipokea ona

Warumi 2:16 “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.”

Muhubiri 12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”

Wito wa Yakobo kwa watoto wake unatukumbusha kuwa kila mmoja anapaswa kujiangalia namna anavyoenenda kwani hata kama inaonekana kama Mungu yuko Kimya anahukumu sawa na kutenda kwetu, ni wito wa Mungu kwa kila mmoja kutenda vema na Mungu amemkusudia kila mmoja atende vema ili aweze kumkubali na kumbariki na kumtakabali bila upendeleo:-

Mwanzo 4:6-7 “BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”

Mungu anatoa wito kwa kila mmoja wetu kushinda uovu na kutenda vyema, ni ukweli ulio wazi kuwa tukitenda vyema Mungu yuko tayari kukubariki, lakini pia matendo yako yanaweza kuamua au kugharimu hatima yako, hiki ndio kinachotokea kwa wana wa Israel mbele ya Yakobo katika siku hii, Ilikuwa ni siku ya kila mmoja kusikiliza hukumu yake, makemeo yake na ujira wake kutokana na kile kilichowapata., lakini vilevile kujua hatima yao.               

Yatakayowapata siku za Mwisho:!

Ni ukweli ulio wazi kuwa Israel alikuwa akisema na watoto wake mmoja baada ya mwingine, alikuwa anawabariki, anawakemea na kuwaonya lakini alikuwa akiwatabiria yatakayowapata siku zao za mwisho, sio tu Yakobo alikuwa akitabiri, lakini alikuwa akiyaona yale Mungu atakayowafanyia kabila moja baada ya jingine katika Israel, lakini sio wao tu Mungu alikuwa anasema kwa kinywa cha Yakobo yale yatakayotupata wewe na mimi, tabia zetu na matendo yetu ni ukweli ulio wazi kuwa yanatuunganisha katika kabila hizi, kila mmoja anaungwa katika kabila mojawapo kutokana na kutenda kwake na hivyo endapo katika maisha yako, utakuwa kama mmojawapo wa wana hawa wa Yakobo kitabia Basi Msikilize Israel baba yako anavyokuambia, unabii sio lazima uje kwa mtu kujaa roho na kuanza kutetemeka au kwa mbwembwe nyingi na makelele ya the major one kama ilivyo leo au kelele za Prophesy!!!!  ni ukweli ulio wazi kuwa Yakobo alikuwa ameketi kwa utulivu na kusoma tabia za wanawe na alikusanya hata taarifa zao na maswala mengine aliyaweka moyoni, kule kutenda kwao kwa mujibu wa Yakobo kulitabiri maswala kadhaa yanayowajia baadaye, Yakobo aliitisha mkutano na kuwaambia wanawe kusanyikeni niwaambie mambo yatakayowapata siku za mwisho hii ilikuwa ni muda wa kuwatolea unabii ulio wazi wazi bila mbwembwe, leo na mimi nitakutolea unabii ulio wazi wazi kwa neno hili bila mbwembwe zozote, Yakobo aliweza kuwaelezea siri kubwa na za wazi kuhusu siku zao za mwisho na namna itakavyokuwa katika maisha yao, uwepo wa Mungu ulikuwepo kumfunulia na alijua wazi kuwa anakwenda kuzungumza nao waziwazi na kuwa mambo hayo yangetokea!

Msikilizeni Israel Baba Yenu!

Hili ndio eneo muhimu ambalo kila mmoja anapaswa kusikiliza kwa makini, sio Reuben tu, au Simeoni, au Lawi au Yuda au Isakari, au Yusufu na kadhalika kila mmoja anapaswa kusikiliza kwa makini sana, Yakobo  anawaita wanawe na ni wazi kuwa anazungumzia ubinadamu wake ambao kila mtu anao, matendo yetu yote tunayoyafanya wakati mwingine yanafanyika kwa sababu ya ubinadamu wetu, sisi ni wana wa Yakobo ni wana wa Adamu sisi ni binadamu hatupaswi kujilaumu kwa sababu ya ubinadamu wetu, Lakini ubinadamu wetu una nafasi kubwa sana ya kuamua hatima yaetu ya Kiroho na kama tukikubali tutabadilika kwa msingi huo tusikubali kamwe kuendeshwa na mwili 1Thessalonike 4:4 “kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;Yakobo anapojiita Yakobo alikuwa anakumbuka ubinadamu wake anafahamu kuwa hata watoto wake wanafahamu kuwa yeye ni binadamu, Lakini Yakobo anaongezea kuwa wamsikilize tu sio kama Yakobo lakini vilevile kama Baba yao, akiwa kama Yakobo hata wanawe waliweza kumdanganya, walifahamu historia ya maisha yake hivyo ni vigumu kumsikiliza sana kama yakobo Yakobo, Yakobo ni mwili, Yakobo ni kipindi cha mapambano, sasa wamsikilize kama Mtu aliyebadilishwa na Mungu Msikilizeni Israel, huyu alikuwa ni Yakobo aliyebadilika lakini pia mtu mwenye uzoefu aliyeona mengi hivvyo wamsikilize kama baba pia kama kiongozi wa familia yao aliyetembea  na Mungu!


1.      Rubeni (Bwana ameona teso langu)

 

Mwanzo 49:3-4 “Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.”

 

Yakobo anataka kumbariki Reubeni na anatambua wazi kuwa huyu ndiye kijana wake wa kwanza mzaliwa wake wa kwanza ni malimbuko yake Duniani, ni mwenye nguvu na ni mkubwa kuliko wengine lakini Yakobo anaondoa mamlaka kwake, kwa mujibu wa tamaduni za Israel huyu ni mrithi halali wa Yakobo,  na wazaliwa wa kwanza walikuwa na kibali maalumu kutoka kwa Mungu cha kubeba kusudi lake, Hata kama ni ujio wa Masihi unapaswa kupitia kwake hata utawala pia Lakini Yakobo anamkataa kwa sababu kadhaa, Reubeni alikuwa na tatizo, alikuwa hana uadilifu, alikuwa hana adabu, lakini sio hivyo tu alikuwa ni mtu asiye na nidhamu na asiyeweza kujizuia, alikuwa ni mtu aliyeshindwa kudhibiti tamaa, na mihemko yake, na hisia zake, Hivyo hangeweza kuwa kuhani wala hangeweza kuwa mfalme, hawezi kuwa kiongozi wa kiroho wala wa kijamii wala wa kisiasa kwa sababu alikuwa mwenye tamaa aliweza kutembea hata na suria wa baba yake hakuweza kujizuia, hakuwa na adabu aliruka mpaka ona

 

Mwanzo 35:21-22 “Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi.Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.”

 

Unaona Mungu katika hekima yake aliamua kuuondoa Ukuhani, Unabii na Ufalme kwa Reuben na kuwapa wengine, Reuben alilipa gharama kubwa ya uovu wake na haki yake ya kukosa uadilifu, kwa vyovyote vile Mungu haitaji watu wanaovuka mpaka kama maji, Dhambi aliyoifanya ilikuwa sio ya kawaida ilikuwa amepitiliza ule mstari wa kawaida wa utendaji dhambi ni dhambi ambayo ikifanyika hata kwa wapagani huwa inaweza kuwapa watu taharuki Lakini Reuben alikuwa ni mtu aliyeshindwa kujizuia  lilipokuja swala la tamaa na uwezo wa kustahimili mihemko yake! Hivyo alimvinjia heshima baba yake!

 

1Wakoritho 5:12 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.”

 

Reuben alifanya zinaa na mke wa baba yake, hii ilikuwa dhambi iliyopitiliza katika uadilifu, kwa hiyo ni mwana mkubwa wa Yakobo, Malimbuko ya Israel lakini hana nidhamu, hana adabu, watu wasio na nidhamu, watu wasioeleweka watu wasiotulia, watu wasio na misimamo, ni kama maji yanayotokota, ni kama mawimbi ya bahari hawana utulivu hawa hawawezi kuwa viongozi, hawawezi kuwa watumishi wa Mungu, ukweli ni kuwa hakuna kuhani, wala nabii, wala mwamuzi aliyetokea kabila la Reubeni  unapoyachunguza maandiko, Yeye ni mfano wa watu wote wenye tabia mbaya, watu wagomvi, watu wasio na busara, watu wasio na adabu watu wasiojiheshimu, watu wanaoshindwa kuidhibiti mihemko yao, watu wanaoshindwa kuheshimu wazazi,  Biblia inaagiza wazi kwamba mtu asilale na mke wa baba yake awe mkubwa au mdogo hiyo ni sawa na kulala na mama yako, aidha maandiko yameonyesha watu wa karibu ambao kwa uadilifu haikuwa vema kushirikiana nao tendo la Ndoa ona

 

Mambo ya walawi 18:5-18  Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA. Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai.

 

Tofauti kubwa kati ya binadamu na mnyama ni kuwa wanadamu wana utashi na wanaweza kutumia vema utashi wao na kuamua kwa busara, haikuwa jambo jema mwanamke aliyezaa na baba yako wewe ukaingia, Reuben anawakilisha watu ambao wangekuwa na uwezo wa kuwa na nafasi kubwa lakini wanapoteza nafasi zao kwa sababu ya kukosa uvumilivu na kukosa adabu, huenda wangekuwa watu wakubwa sana lakini kwaajili ya tabia zao zisizotabirika wamepoteza nafasi zao, sote hatujui Mungu ametukusudia kuwa watu wa namna gani baadaye kwa msingi huo tangu sasa ni lazima tuhakikishe tunaishi kwa uadilifu, hususani katika nyakati hizi ambapo vyombo vya habari, na teknolojia vinauwezo wa kutunza kumbukumbu zetu nzuri na mbaya pia, kama utakuja kuwa kiongozi mkubwa sana huna budi kuyatunza maisha yako kuanzia sasa,  Mungu atupe neema ya kutunza tabia zetu. Ni wazi kuwa sifa za mtu anayetakiwa kuja kuwa askofu hazianzi akiwa askofu bali zinaanza akiwa mtu wa kawaida, na mkristo wa kawaida ndipo anapokuja kuwa na uwezo wa kufiti katika mazingira yanayokusudiwa baadaye na Mungu! Usifanye mambo ya kijinga wala usipige picha za kijinga kwa sababu hujui utakuja kuwa nani baadaye!, Reuben alipoteza sifa za kuwa kiongozi wa kifamilia, kiroho na kisiasa alijiingiza chini ya laana yeye mwenyewe, kwa kulala na mke wa baba yake alijiletea  laana ona

 

Kumbukumbu la Torati 27:20 “Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina. Aidha tabia ya Rubeni inawakilisjha watu wasioshehimu wakubwa zao kiumri, kazini na popote pale kutokuwaheshimu wazazi na wakubwa kunatuondolea Baraka Mungu alizozikusudia kwetu ona Waefeso 6:2-3 “Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.” Kuwaheshimu wazazi wetu au watu waliotuzidi umri ni pamoja na kuwathamini, kutambua mamlaka yao,kuwatendea kwa heshima, na kuwahifadhi, Reuben alivuka mpaka huo

 

Reuben alijiletea shida Roho Mtakatifua alikumbuka tukio lake na Israel aliliweka moyoni na hivyo alipoteza Baraka iliyokusudiwa kwake, Biblia ya kiingereza inatumia maneno YOU WILL NO LONGER EXCEL neno Excel katika Kamusi ya kiingereza ya American Dictionary  linasomeka to do something very well or be highly skilled and be better than most others or to be extrimly good at something, Kwa hiyo Yakobo aliposema Reuben usiwe na ukuu, ni kama alikuwa anamaanisha hakutoakuwa na lolote jema kutoka kwake, Reuben anapoteza haki ya mzaliwa wa kwanza, anapoteza nafasi ya uongozi, anapoteza heshima, anapoteza mamlaka, kwa sababu ya kukosa uadilifu, kwa msingi huo kupoteza sifa za uadilifu na kutokujitia nidhamu kunaweza kutufanya tupoteze nafasi zetu kama viongozi, mbaya zaidi unapoteza kibali kwa Bwana!, Katika nyakati za Kanisa la kwanza mtu alipokuwa anataka kujitoa kwaajili ya maongozi ya kanisa ziko sifa ambazo mtu anapaswa kuwa nazo za uadilifu, ni kweli kuwa sisi ni binadamu lakini maandiko yanatufundisha kutunza uadilifu ili kupata Baraka za kiungu za kuwa kiongozi wa wengine kazi ambayo ina heshima kubwa sana kwa Mungu.

 

1Timotheo 3:2-7 “Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi

 

Katika nyakati za leo tunao kina Reuben wengi hauhitaji kutafuta unabii kwanini hufanikiwi sababu ziko wazi katika maandiko, huitaji kutafuta nani amekuroga sababu ziko wazi, kama unashindwa kujidhibiti, una hasira, unagombana na kila mtu, huwezi kuzuia tamaa zako, huna adabu, unatembea na mijimama mikubwa kuliko umri wako ambao wangestahili kuwa  wake za baba zako, hueshimu huyu ni mke wa nani usitegemee kuwa na ukuu Yakobo anasema, hivyo ni onyo kwa kanisa vilevile kwamba wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho hatupaswi kujivunia lolote, hatupaswi kujiamini kupita kawaida, hatupaswi, hatupaswi kujikweza, Mungu anaweza kuinua yeyote na kushusha yeyote

 

Mathayo 19:30 “Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”

 

Tabia ya kupenda ukubwa na kujiamini kupita kawaida na hata kujikweza itawafanya wengi kushushwa na Mungu, wako watu hawana adabu kwa wale waliowazidi umri na wakati mwingine wako tayari hata kuwadhalilisha na kuwakosea adabu au kuwafanya waumbuke hao ni wa kabila la Reuben ni watu ambao hawatatoboa katika ukuu Mungu atawashusha

 

Luka 14:11 “Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.” 1Petro 5:5-6 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;”

 

Kama tutajirekebisha na kukataa kuwa Reuben leo Mungu atatuinua kwa wakati wake, wewe kama ni muisraeli leo nasema msikilizieni Israel Baba yenu, Reuben hakuwa na nafasi tena ya kujirekebisha lakini wewe unaweza kuwa na nafasi ya kutubu na kuachana kabisa na kabila la Reuben, Bwana akupe neema ya kumsikiliza Israel baba yetu katika jina la Yesu amen! Reuben alihukumiwa kwa kutokumuheshimu baba yake lakini kwa habari ya uhusiano na Yusufu Reuben alikuwa na mpango wa Kumuokoa Yusufu, ila mpango wake wa wokovu haukufanikiwa  Israel aliwabariki watoto wake na kuwadhibu kutokna na namna walivyomtendea yeye au Yusufu au watu wengine, Mungu atatuhukumu kwa kadiri tulivyomtendea yeye na watu wengine ona

 

Mwanzo 37:19-22 “Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.Reubeni akasikia akamwokoa katika mikono yao, akasema, Tusimwue. Reubeni akawaambia, Msimwage damu; mtupeni katika birika hii iliyopo nyikani, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake.”

 

Sio kila mtu mbaya ana mambo mabaya wakati mwingine yako mema vilevile Yakobo alikuwa akiwahukumu watoto wake kulingana na uhusiano wakliokuwa nao kwake kama baba na kwa wenzake ndugu zao kama Yusufu, na kwa watu wengine, Mungu atahukumu sawasawa na jinsi tunavyojali mahusiano yetu kwake na halikadhalika mahusiano yetu na watu wengine,

 

1Yohana 4:20-21 “Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.”

 

2.      Simeon (Bwana amesikia teso langu) na Lawi (Bwana ataungana nami).

 

Mwanzo 49: 5-7 “Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri. Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe; Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.”

 

Simeoni na Lawi wote wanapokea unabii unaofanana Israel pamoja na Roho Mtakatifu wanawatawanya hawa, hawapewi ukubwa hata kidogo, wao wanaitwa vyombo vya ghadhabu au ukatili, Israel anailaani Hasira kali waliyokuwa nayo, wameshindwa kujizuia wako tayari hata kuua mtu, walikasirika sana aliponajisiwa dada yao Dina, hata watu wale walipotaka amani nao wao walikuwa na mpango wa kuwafutilia mbali watu waliojisalimisha kwao waliwaua kwa makali ya upanga wala hawakuwa na huruma walikuwa katili, wala hawakutaka ushauri wa baba yao, wao walikuwa na Hasira kali kiasi ambacho walisahau vilevile kuwa Mungu ni wa rehema Yakobo 1:20 “kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.” Ni jambo la kusikitisha sana kuwa wako watu wengi wa Mungu wanasumbuliwa na hasira na wanadhani wanastahili Baraka za Mungu ilihali wanayo maeneo ya kutengeneza, kwa sababu ya hasira wengi tumewatamkia maneno mabaya wengine, tumekimbilia kuwatenga watu na kuwahukumu na kutoa adhabu mbaya hata bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza na hata bila kujali kuwa wako watu hawawezi kujieleza, Simeoni na Lawi walifanya hila na kwa hasira waliwaua washekemu jambo ambalo Israel alilikumbuka na Roho Mtakatifu alilikumbuka ona ilivyokua

 

Mwanzo 34:1-31 “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi. Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri. Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu. Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja. Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka.Hamori akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe. Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu. Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo. Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa. Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu.Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu Dina, umbu lao, wakawaambia, Hatuwezi kufanya neno hili, tumpe umbu letu mtu asiyetahiriwa; ingekuwa aibu kwetu. Lakini kwa sharti hii tu tutapatana nanyi; mkiwa kama sisi, akitahiriwa kila mwanamume wenu, ndipo tutawapa ninyi binti yetu, na sisi tutatwaa binti zenu tutakaa pamoja nanyi, nasi tutakuwa watu wamoja. Lakini kama hamtusikii na kutahiriwa, basi tutamtwaa umbu letu, nasi tutakwenda zetu. Maneno yao yakawa mema machoni pa Hamori, na machoni pa Shekemu, mwana wa Hamori. Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye. Hamori, na Shekemu mwanawe, wakaja langoni pa mji wao, wakasema na watu wa mji wao, wakinena, Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao. Lakini kwa sharti hiyo moja tu watapatana nasi wakae wote kwetu, tuwe watu wamoja, kama tukitahiriwa kila mwanamume, kama hawa walivyotahiriwa. Je! Kondoo zao, na mali zao, na wanyama wao wote hawatakuwa mali zetu? Basi na tupatane nao tu, nao watakaa kwetu. Wakawasikia Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake. Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote. Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka.Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao. Wakachukua kondoo zao, na ng'ombe zao, na punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni. Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka. Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu. Nao wakasema, Je! Ni vema amtendee umbu letu kama kahaba? unaona jamaa hawa walikuwa na Hasira na wanaitwa vyombo vya hasira na Israel anasema anawatawanya, hataki kujulikana kupitia wao, Israel hataitwa kwa jina la watu wenye Hasira kiasi hiki, hawa ni vyombo vya dola, tatizo kubwa la Simeon na Lawi ni hasira hasira yao iliwafanya wafanye dhambi, wafanye hata yale ambayo Mungu hakuwa ameyakusudia Waefeso 4:26 Biblia inasema  Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;” Maandiko yanatutaka tuwe mbali na hasira, uchungu na ghadhabu na hasira ni mbaya  Wasimeoni hawakupewa ukubwa kwa sababu ya hasira yao Waefeso 4:31 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;” Israel aliwatawanya wawe watumishi wa jamii kokote waliko, tena wasiwe na urithi katika Israel, unabii wa kuwatawanya na kuwagawa haukuwa mwema kwao, kabila la Simeoni ndio lilikuwa dhaifu kuliko yote katika Israel walikuwa wengi walipotoka misri lakini Mungu aliwapunguza sana Hesabu 1:23 “wale waliohesabiwa katika kabila ya Simeoni, walikuwa watu hamsini na kenda elfu na mia tatu” (59,300), lakini walipofika Kanaani miaka 35 baadaye walikuwa wachache mno Hesabu 26:14 “Hizi ndizo jamaa za Wasimeoni, watu ishirini na mbili elfu na mia mbili.” (22,200) kwa hiyo kabila la Simeoni lilitoweka na kuchanganywa na Yuda. Ona katika  Yoshua 19:1  Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda. Nitawagawa nitawatawanya katika Israel unabii huu ulitimia kwani kabila ya Simeoni ilitoweka na walawi walipata Baraka ya kuwa watumishi wa Mungu tu, wao waliponea chupuchupu baada ya kuonyesha utii kwa Mungu wakati kabila nyingine zilipoasi jangwani Kutoka 32:26-28 “Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe dhihaka kati ya adui zao, ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, Mtu awaye yote aliye upande wa BWANA, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake. Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.” Walawi waliweza kujiokoa kwa kumsogelea Mungu, Lakini kabila ya Simeoni ilitawanyika na kupotea, kila mmoja anaweza kuwa ni mwana wa Israel kila mmoja anaweza kuwa mwamini, tunaweza kuwa kabisa hatunywi, pombe, hatufanyi zinaa, wala uasherati, wala sio wadhulumaji na ama watenda maovu mengine lakini Maandiko yanatufundisha kuwa Haisra ni mbaya mno, ni kwaajili ya Hasira Musa alizuiliwa asiingie katika nchi ya kanaani, kumbuka Musa ni wa kabila ya walawi, Zaburi 106: 32-33 “Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao, Kwa sababu waliiasi roho yake, Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.” Hasira na ghadhau zinaweza kuwakosesha watu wengi wa Mungu mbingu, hatuna budi kumuomba Mungu atuwezeshe tusitawanywe na kufutiliwa mbali na Mungu na kunyimwa urithi kama ilivyokuwa kwa Simeoni na Lawi kwa sababu ya Hasira Yakobo anailaani hasira ya vijana hawa kwa kiingereza CURSED BE THEIR ANGER, Ghadhabu yao na ilaaniwe! Kwanini Israel anawaweka Simeoni pamoja na Lawi, hawa walikuwa ni ndugu na marafiki, ndugu-rafiki, mkubwa alikuwa Simeon na mdogo wake ni Lawi, walipendana na walikuwa na mtindo wao wa maisha wanasikilizana mno na wakiamua lao wameamua, Lawi kwa vile alikuwa mdogo alimsikiliza sana Simeon, kwa hivyo walikuwa watu wenye mambo yao uhusiano wao na baba yao ni kuwa hawakumsikiliza baba yao walidharau ile hali ya moyo wa baba yao hawakusikiliza Kumbukumbu la Torati 27:16 “Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.” Katika uhusiano wao na baba hawakumsikiliza, walijiamulia mambo yao wenyewe, Katika uhusiano wao kwa wengine na hasa Yusufu Simeon ndiye aliyetoa wazo la kumuangamiza ndugu yao tena akimuita bwana ndoto ona Mwanzo 37:18-20 “Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwajemtu mmoja ataniuliza swali tunawezaje kujua kama Simeon ndiye anahusika moja kwa moja na mpango ule, Reuben hakukubali Yusufu auawe, alitaka kumuokoa baadaye amrejeshe kwa baba yake, lakini Simon na wengine walikuwa na nia thabiti ya kutekeleza jambo hilo ona Yusufu aliweza kuwaelewa wote alipowasumbua na kuwababaisha na kumtia ndani mmoja wao ona Mwanzo 42:15-24 “Mtabainika kwa njia hii; aishivyo Farao, hamtoki hapa, asipokuja huku huyo ndugu yenu mdogo. Mpelekeni mmoja wenu, aende akamlete ndugu yenu, na ninyi mtafungwa, hata maneno yenu yahakikishwe, kama mna kweli ninyi; ikiwa sivyo, aishivyo Farao, ninyi ni wapelelezi. Akawatia wote gerezani siku tatu. Yusufu akawaambia siku ya tatu, Fanyeni hivi, mkaishi, maana mimi namcha Mungu. Kama ni wa kweli ninyi ndugu yenu mmoja na afungwe gerezani, nanyi nendeni mkachukue nafaka kwa njaa ya nyumba zenu, mkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa. Ndivyo walivyofanya. Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosa ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia kwa hiyo shida hii imetupata. Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, msimkose kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo damu yake inatakwa tena. Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alikuwapo mkalimani kati yao. Akajitenga nao akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao.”

 

Yusufu alifanya upelelezi wa kutosha na wote walibainika namna walivyojihusisha na maisha yake na Yusufu alipata Muda wa kuelezea upelelezi wake kwa baba yake kila kilichofanyika kwa hivyo unaweza kuona kitendo cha kumfunga Simeon na kuruhusu wengine ilikuwa wazi kuwa mwanzilishi wa wazo lile ovu alikuwa ni huyu Bwana,  Mungu yuko tayari kumbariki yeyote anayefanya vema, watu wa kabila la Lawi baadaye walijifunza kuwa upende wa Mungu, walibadilika na kuwa watu wenye kushika sharia na uadilifu na hivyo ingawa walikuwa wametawanywa, wao walifawanywa kama watumishi wa Mungu, Walawi walijiokoa na laana hii baadaye kwa kusimama upande wa Mungu, ahadi za Mungu na hata laana za wazazi wetu zinaweza kubadilika kwetu kwa toba na kubadili mwenendo wetu usiofaa, Bwana ampe neema kila mmoja wetu, kubadilika ili kujilinda na mawaa na kupata Baraka alizokusudia Mungu katika maisha yetu katika jina la Yesu ameeen!

 

3.      Yuda (Mara hii nitamsifu Bwana)

 

Mwanzo 49:8-12 “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.”

 

Yuda hakuwa mwema kuliko kaka zake, kila mmoja ana udhaifu wake kama baba yao alivyojieleza kuwa yeye ni Yakobo, lakini pia ni Israel na ni Baba yao, lakini Yuda  alikuwa na moyo wa kukubali kujitoa kwaajili ya familia yake baba yake na maisha ya Yusufu, Benjamin na baba yake pia, Mpango wa kwanza wa ukombozi kwa Yuda unaonekana kwanza kwa Yusufu akiwa na mpango tofauti na nduguze hakutaka auawe alikuwa mwema kwa Yusufu alitafuta kuokoa maisha yake Mwanzo 37:26 “Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake?Yuda aidha alikuwa tayari kuyatoa maisha yake kwaajili ya Benjamin na kwaajili ya Maisha ya baba yake ona Mwanzo 44:1-34 “Akamwamuru yule msimamizi wa nyumba yake akisema, Jaza magunia ya watu hawa chakula kwa kadiri wawezavyo kuchukua, utie na fedha ya kila mtu kinywani mwa gunia lake. Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu. Asubuhi kulipopambazuka, hao watu wakapewa ruhusa, wao na punda zao. Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema? Je! Kikombe hiki, sicho anyweacho bwana wangu? Naye hufanya uaguzi kwa hicho. Mmefanya vibaya kwa kufanya hivi.  Akawafuata, akawapata, na kuwaambia maneno hayo. Wakamwambia, Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu? Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu. Akasema, Basi na iwe hivyo kama mlivyosema, Mtu atakayeonekana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu, na ninyi mtakuwa hamna hatia. Wakafanya haraka, wakashusha kila mtu gunia lake, na kufungua kila mtu gunia lake. Naye akatafuta, akaanza kwa mkubwa na kuisha kwa mdogo. Kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini. Wakararua nguo zao, wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini. Akaja Yuda na ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia kifudifudi. Yusufu akawaambia, Ni tendo gani hili mlilolitenda? Hamkujua ya kwamba mtu kama mimi naweza kufanya uaguzi? Yuda akasema,Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake. Akasema, Hasha! Nisifanye hivi; mtu ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake, ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Nanyi enendeni zenu kwa amani kwa baba yenu. Ndipo Yuda akamkaribia, akasema, Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na aseme neno moja masikioni mwa bwana wangu, wala hasira yako isimwakie mtumwa wako, maana wewe u kama Farao. Wewe, bwana wangu, ulituuliza watumwa wako, ukisema, Je! Mnaye baba, au ndugu? Tukakuambia wewe, bwana wangu, Tunaye baba, naye ni mzee, na mwana wa uzee wake ni mdogo, na nduguye amekufa; amebaki yeye peke yake wa katika tumbo la mamaye, na baba yake anampenda. Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie. Tukakuambia, bwana wangu, Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa. Ukatuambia watumwa wako, Asiposhuka ndugu yenu mdogo pamoja nanyi, hamtaniona uso wangu tena Ikawa tulipokwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamwarifu maneno yako, bwana wangu. Kisha baba yetu akanena, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo. Tukasema, Hatuwezi kwenda; ndugu yetu mdogo akiwapo pamoja nasi, tutashuka, maana hatutaweza kuuona uso wa mtu huyo, ndugu yetu mdogo asipokuwa pamoja nasi. Mtumwa wako, baba yangu, akatuambia, Mnajua ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili; mmoja alitoka kwangu, nikasema, Bila shaka ameraruliwa, wala sikumwona tangu hapo. Na mkiniondolea huyu naye, na madhara yakimpata, mtashusha mvi zangu na msiba kaburini. Basi, nikienda kwa mtumwa wako, baba yangu, na huyu kijana hayupo pamoja nasi, iwapo roho yake imeshikamana na roho ya kijana; itakuwa atakapoona ya kwamba huyu kijana hayuko, atakufa; na watumwa wako watashusha mvi za mtumwa wako, baba yetu, kwa huzuni kaburini. Kwa maana mtumwa wako alijifanya mdhamini wa huyu kijana kwa baba yangu, nikisema, Nisipomrudisha kwako, nitakuwa na hatia kwa baba yangu sikuzote. Basi, sasa nakusihi, uniache mimi mtumwa wako nikae badala ya huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu; na huyu kijana umwache aende pamoja na nduguze. Kwa maana nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.”

 

Israel pamoja na Roho wa Mungu walichunguza moyo wa Yuda na kugundua kuwa ndani mwake kulikuwa na Roho ya wokovu, alikuwa yuko tayari kuyatoa maisha yake kwaajili yaw engine kwa msingi huo ingawa Yuda anaoenekana kuwa na madhaifu ya kawaida ya kibinadamu kama kutokutaka kutimiza haki kwa mkwewe tamari na hata kulala naye kama kahaba

 

 Mwanzo 38:24-26 “Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe. Alipotolewa, alipeleka watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii. Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.”

 

Mungu aliangalia moyo wake na kuona kuwa ni moyo wa tofauti, Baraka zote hizo Mungu alizitoa kwa neema na kulingana na matendo yao, udhaifu wa maswala Binafsi ya Yuda haukuwa, sababu ya Mungu kupuuza uwezo wake mkubwa wa kuwapenda ndugu zake na kuwa tayari kufa kwaajili yao na kwaajili hii unabii kuhusu kuja kwa Masihi umeunganishwa na moja kwa moja kabila la Yuda hivyo

 

a.      Yuda Ndugu zake watamsifu – kutokana na wokovu wake mkubwa kwa jamii yake na kuwafanya ndugu zake wasiingia katika dhambi na kumwaga Damu ya ndugu yao, kumlinda Benjamin na kumlinda na kujali moyo wa baba yao na kumlinda Yusufu, wazo lake na mpangio wake ulikubalika katika jamii yake na alisifiwa kama sababu ya ukombozi wa wanadamu wote.

 

b.      Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii, ni wazi kuwa watawala wengi na manabii wengi na wafalme wengi walitoka katika kabila hili lakini vilevile Masihi anaunganishwa kuwa ni wa kabila la Yuda Ufunuo 5:5 “Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.” Baada ya miaka kama 640 hivi alitokea Kiongozi maarufu sana wa kabila la Yuda aliyeitwa Daudi na baada ya miaka kama 1600 alitokea Yesu Kristo yeye ambaye mataifa watamtii (Shiloh) Watu wa kabila hili hawaangalii maslahi yao, ni watu ambao hawana ubinafsi, pamoja na madhaifu yao lakini marazote wako tayari kufa kwaajili ya wengine wako tayari kujitoa dhabihu, Mungu anaweza kumtumia mtu kuwa kiongozi, mtu kuwa nabiii, mtu kuwa kuhani kama mtu huyo anamoyo wa huduma kwa wengine ni watu wenye kujali wengine na kuwa tayari kuokoa wengina kuwasaidia wengine kujitoa kuwa mbadala wa wengine kuwatetea wengine ndio ambao wanaweza kutumiwa na Mungu katika Baraka kubwa anazozikusudia kwa watu wake!

 

4.      Zabuloni (Bwana atakaa nami).

 

Mwanzo 49:13 “Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.” Yakobo anaruka utaratibu (Itifaki) ya mfululizo wa uzaliwa na anakwenda kwa kijana wake wa kumi kwa kuzaliwa na kijana wake wa tisa lakini akiwa anazingatia watoto wake kwa Leah, Kabila hili wanatabiriwa kua askari, ni kabila maarufu sana wakati wa utawala wa Daudi, walitoa askari wengi zaidi kuliko kabila nyingine, wanasifiwa kuwa ni wanajeshi bora nan i hiodari wa kupanga vita, na hawana kusitasita 1Nyakati 12:33 “Wa Zabuloni, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila namna, hamsini elfu; askari wastadi wasiokuwa wenye moyo wa kusita-sita.”  Licha ya kuwaona kuwa watakuwa watu wa namna gani vilevile Israel anaona ni eneo gani la nchi ya kanaani watairithi siku za usoni kwamba watakaa upande wa bahari mashariki na magharibi kuikabili bahari, Watu wa kabila hili ni watu wenye moyo wa ujasir, wanaojua kupigana vita vya kiroho, kupanga mashambulizi na walio na imani wasiositasita katika mipango yao, watu ambao wako tayari kushiriki tabu pamoja na Daudi kwa faida ya taifa  Waebrania 10:38 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.” 2Timotheo 2:3 “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine. Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo YesuNi ukweli uolio wazi kuwa Mungu hata sasa anahitaji wapiganaji hodari wa Kiroho, Biblia inawataka watu stadi wanaojua kupigana vita vya kiroho na kutumia silaha za Mungu ili kuweza kuzipinga hila za Yule muovu ona Waefeso 6:10-13 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Zabuloni walimsaidia sana Daudi wakati wa vita, walijua kupanga vita, walikuwa mashujaa hawakusitasita, Mungu anatutaka sisis nasi kupambana katika ulimwengu nwa roho kwaajili ya kazi za mfalme wetu samba wa kabila la Yuda yaani Yesu Kristo, wale wote wanaopambana kwaajili ya injili na maombi ni askari wema wa yesu Kristo!

 

5.      Isakari (Mungu amenilipa)

 

Mwanzo 49:14-15Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.

 

Isakari wanatajwa kuwa watu wenye nguvu, na watulivu mfano wa punda, lakini ni watu wenye kuona wanajua nchi na wanajua nyakati, Kabila la Isakari likikuwa ni moja ya makabila makubwa sana katika Israel kwa mujibu wa sensa katika kitabu cha hesabu ndio ilikuwa kabila ya tatu kwa ukubwa

 

Hesabu 26: 25. “Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu.”

 

Na kutokana na wingi wao pia walitumiwa mara kadhaa kukabiliana na majeshi ya wageni yaliokuwa yanataka kuwasulubu Israel kwa hiyo walikubali kuwa walinzi na wanajeshi wa taifa Lakini kabila hili lilikuwa na wataalamu wenye kujua nyakati na kujua Israel wanapaswa kufanya nini hivyo lilikuwa na viongozi wengi sana wakati wa Daudi waliotegemewa

 

1Nyakati12:31-32Na wa nusu kabila ya Manase, kumi na nane elfu, waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme. Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.

 

Watu wa Kabila hili ni watu wenye akili, wenye kujua majira na nyakati, na kujua Israel wanapaswa kufanya nini walikuwa ni wenye uwezo na viongozi wakubwa na watu waliwasikiliza, Ni kabila ambalo walijua nyakati na walijua na mna ya kuzitumia nyakati lakini pia walikuwa ni watu wenye kuwajulisha wengine nini cha kufanya na nini kimetokea, ukweli huu unazihirika wazi kuwa watu hawa walikuwa ni watu wa namna Na ni kitu gani Israel wanapaswa kukifanya, Lilikuwa ni kundi la watu pekee waliokuwa wanajua nini cha kufanya na wakati wa kufanya, walikuwa na hekima na maono jambo ambalo lilifanya taifa zima kuwasikiliza,  Majira na nyakati za zamani zlikuwa zinategemea mwandamo wa mwezi, kwa hiyo wana wa isakari walikuwa na ujuzi huo, walitambua mwenendo wa jua na sayari, walijua ni wakati gani wa kuabudu na ni wakati gani waweke mfalme walijua kutafasiri nyakati na matukio, walijua majira ya kisiasa nay a kiroho, walijua ni wakati gani Mungu anataka nini na anafanya nini, alikini vile vile waliijua sharia ya Mungu sana, walikuwa na hekima na maarifa na walijua kweli za Mungu ni hatari sana kuishi maisha yasiyo na muelekeo Mithali 29:18 “Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.” Watu wengi wamefeli masomo kwa sababu hawana maono, wengi wamepoteza kazi kwa sababu hawana maono, wengi wameshuindwa kukabiliana na wakati ujao kwa sababu hawajui nini liwapasalo kulifanya mtu asiyejua nini kinakuja mbeleni huwa hajizuii, kuna faida kubwa sana za kujua majira na nyakati na nini cha kufanya kwa sababu

a.       Kila kitu katika maisha yetu kitaamuliwa na Muda

b.    Muda ni moja ya jambo la thamani na la muhimu kwa sababu ukiupoteza hautakuja urudi tena

c.       Kila mtu ana muda wake kwa kila jambo, usijifananishe ne mwingine

d.       Hakuna mtu anayejua muda wake aliowekewa

e.       Muda ukiutumia vibnaya utajuta

f.     Muda ni kama Mwalimu utakufundisha kama ulikuwa na hekima au ulikuwa mjinga ni lazima ujue muda wako na uhuheshimu, Isakari waliheshimiwa sana na kabila zote na walimsaidia sana mfalme kwa sababu walikuwa wanajua nini cha kufanya na wakati wa kufanya

Muhubiri 3:1-11Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani. Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo? Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.” Moja ya jambo ambalo litakuja kuwafanya watu wengi wajute katika maisha yao baadaye ni kutokujua majira na nyakati na nini mtu anapaswa au alitakiwa kukifanya Luka 19:41-44 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.” Watu wanaojua majira na nyakati nwanaitwa wise man au wenye hekima!                 

6.      Dani (Bwana amenipa haki yangu).

 

Mwanzo 49:16-18 “Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.” Ni moja ya kabila iliyotoa Mwamuzi muhimu na mkubwa mwenye historoa ya kipekee aitwaye Samsoni Waamuzi 13:1-24 “Wana wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya Bwana, Bwana akawatia katika mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arobaini.Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi; kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti. Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala hakuniambia jina lake;lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake. Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa. Mungu akasikiza sauti ya Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye. Basi huyo mwanamke akaenda haraka, akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama, huyo mtu amenitokea, huyo aliyenijilia siku ile. Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi. Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini? Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, Katika hayo yote niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari. Asile kitu cho chote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze. Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Nakuomba, tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako. Lakini malaika wa Bwana akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea Bwana. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa Bwana. Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia nipate kukutukuza? Huyo malaika wa Bwana akamwambia, Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa kuwa jina hilo ni la ajabu?Basi Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea Bwana hapo juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia.Kwa maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa Bwana akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakainama kifudifudi. Lakini malaika wa Bwana hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa Bwana. Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu tumemwona Mungu. Lakini mkewe akamwambia, Kama Bwana angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu. Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, Bwana akambarikia.” Unabii wa Israel unatimizwa kupitia maisha ya Samsoni aliyewaamua watu wake vema Dani atawaamua au kuhukumu watu wake hili lilifanikiwa kwa kiwango cha juu wakati wa maisha ya Samson, Lakini Israel pia anaeleza jambo la tofauti kidogo kuhusu Dani, Dani atakuwa nyoka! Hii ni tabia ya kishetani, ni tabia ya ushirikina, Kabila hili linaonekana kuwa na tabia ya kumshirikisha Mungu na miungu mingine

 

Waamuzi 18:30-31Kisha wana wa Dani wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga; na Yonathani mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa ni makuhani katika kabila ya Wadani hata siku ya kuchukuliwa mateka hiyo nchi. Basi wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga aliyoifanya Mika, wakati wote ile nyumba ya Mungu ilipokuwako huko Shilo.”

 

Tunaona katika habari ya kuabudu sanamu watu wa Kabila ya dani wakiwa wa kwanza kufanya hayo, Kabila hili likawa kiini cha ibada za sanamu hata katika wakati wa utawala wa Yeroboamu 1Wafalme 12:26-30 “Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. Kama watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani. Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani.

 

Tabia hii iliendelea mpaka wakati nabii Amosi alipotangaza hukumu ya kukomesha ibada ya sanamu katika Israel na kutangaza kuleta kiu ya neno la Mungu ona

 

Amosi 8:11-14 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione. Siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kwa kiu. Na hao waapao kwa dhambi ya Samaria, na kusema, Kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na, Kama iishivyo njia ya Beer-sheba, hao nao wataanguka, wasiinuke tena.” Israel anamuona Dani kuwa licha ya kuwa angekuwa mwamuzi mzuri lakini vilevile angekuwa nyoka miongoni mwa nduguze hasa kwa sababu ya ibada za sanamu lakini sio hivyo tu wana theolojia wengi wanaamini ya kuwa huenda mpinga Ksristo atatokea katika kabila la Dani sawa na unabii wa

 

Daniel 11:36-37 “Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa yatafanyika. Wala hataijali miungu ya baba zake; wala yeye aliyetamaniwa na wanawake; wala hatamjali mungu awaye yote; maana atajitukuza mwenyewe juu ya wote.” Na vilevile unabii wa Yeremia 8:16Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi zake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi zake za vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.”

 

Hata hivyo Yakobo aliamini ya kuwa hatimaye Mungu takuja kumkomboa mwanae pia na jamii ya kabila la Dani kwa kulia kuwa Wokovu wako nimeungoja ee Bwana, Hapa aliunganisha taabu za vijana wake na ule mpango wa Mungu wa ukombozi, na bila shaka anamuona masihi!, Watu wa jamii ya kabila hili ni wenye nguvu kama samsoni ni watu wazuri, wana moyo wa kusaidia wanampenda Mungu lakini wana tatizo la ushirikina, Mungu anataka tumtegemee yeye na kumtumikia yeye kwa nguvu zetu zote

 

1Wakoritho 10:1-21 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa mbali na tabia ya kumshirikisha Mungu na miungu, au ushirikina au kuabudu sanamu, na kutupa kuwa na uhusiano bora nayeye!

 

7.      Gadi (Bahati njema)

 

Mwanzo 49: 19 “Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino.” Israel anamtaja Gadi kama mwanajeshi ni mpambanaji atashambuliwa lakini vilevile atashambulia na kupata ushindi, Musa aliongezea unabii huu kuwa kila atakayemgusa Gadi atararuliwa mpaka utosi wa kichwa ona Kumbukumbu la Torati 33:20 “Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.  Kabila hili linaonekana baadaye kujitoa kijeshi wakati wa utawala wa Daudi na walimsaidia sana Daudi wengi wa wagadi walikuwa ni makomandoo na walikuwa hodari na wajuzi wa vita sana hawakuogopa chochote na walikuwa wepesi na wenye uzoefu mkubwa katika medani za kivita sio hivyo tu walikuwa na ujuzi wa kutumia silaha walizokuwa nazo nyakati hizo 1Nyakati 12:8-16 “Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima; Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu; Mishmana wa nne, Yeremia wa tano; Atai wa sita, Elieli wa saba; Yohana wa nane, Elzabadi wa kenda; Yeremia wa kumi, Makbanai wa kumi na moja. Hao wa wana wa Gadi walikuwa maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu. Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.Tena wakafika ngomeni kwa Daudi baadhi ya wana wa Benyamini na Yuda.” Wagadi walikuwa ni watu wasioshindwa vita wanaweza kuvamiwa kivita lakini lazima waibuke washindi tu Yeremia 49:1 “Habari za wana wa Amoni. Bwana asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake? Hii ni Baraka kubwa sana kwamba unakuwa na watu mashujaa, wanaweza kuvamiwa na maadui lakini hawakati tamaa mwisho lazima wawe washindi tu. Kumbuka Gadi ni mwana wa Zilpa kijakazi cha Lea, hatupaswi kuwa watu wa kukata tamaa, tunapaswa kuwa hodari katika bwana na katika uweza wa nguvu zake, tunapaswa kujua namna ya kutumia silaha za kiroho na kuhakikisha kuwa tunashinda vita zote hata kama kuna wakati tutazidiwa Kabila la Gadi walikuwa hodari katika vita, na hawakuwahi kushindwa kivita, Katika agano jipya Maandiko yanatuasa kuwa hodari katika bwana kuhakikisha kuwa tunashinda Waefeso 6:10-13 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.Ni muhumu kwa kila mmoja wetu kuhakikisha ya kuwa anakuwa mpambanaji katika maisha yake, tumia kila nafasi uliyonayo kuwashinda maadui zako, na kushinda kila aina ya kikwazo unachokutana nacho, hakikisha ya kuwa unatoboa na kupata mpenyo katika kila eneo la maisha yako usikubali kuwa “defeated” usikubali kushindwa vita yoyote iliyoko mbele zako Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.”  Mashujaa wote wa imani nyakati za Biblia walishinda kila aina ya kikwazo kilichowakabili mbele yao, sisi nasi Bwana na atupe neema ya kuwa washindi na watu tusioshindwa na lolote katika jina la Yesu Kristo amen!              

 

8.      Asheri (Nimebarikiwa/nina furaha).

 

Mwanzo 49:20“Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalmeAsheri alikuwa ni mwana wa pili wa Zilpa kijakazi wa Lea, tunaona tena maneno mazuri sana kutoka kwa Yakobo kuelekea wana wa Leah huenda kulikuwa na malezi mazuri mno, Asheri anatabiriwa kukaa sehemu yenye hazina za kifalme ni kama ardhi yenye madini na starehe zinatabiriwa kwake na hawatakuwa na taabu Musa anaongezea hilo katika Kumbukumbu la Torati 33:24 -29 “Na Asheri akamnena, Na abarikiwe Asheri kwa watoto; Na akubaliwe katika nduguze, Na achovye mguu wake katika mafuta. Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako. Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake. Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza. Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande. Uheri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.” Hawa walikuwa watu imara na wenye nguvu, wataratibu na wasiopigika, adui akija juu yao lazima atiishwe vita vyao ni Mungu ndiye anayesaidia, unono umetajwa kuunganishwa na kabila hili, katika agano jipya mwanamke mmoja anatajwa kutokea Kabila hii alikuwa hodari wa kufunga na muombaji wa kiwango cha juu sana Luka 2:36-38 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu,na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.

Kabila hili Yakobo anasema litatoa tunu za kifalme kwa mujibu wa maelezo ya marabi, ni kuwa kabila hili lilikuwa na mabinti wazuri mno na wenye adabu, na makuhani wengi na wafalme walikwenda kuoa katika kabila hili.

 

Aidha Kabila la Asheri walipata ardhi nzuri sana na hivyo ardhi waliyoipata iliweza kuwapa utajiri wa madini na chakula wao walipata ardhi nzuri katika nchi ya kanaani karibu na bahari ya mediteraniani Yoshua 19:24-31Kisha kura ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao. Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, na Hali, na Beteni, na Akishafu; na Alameleki, na Amadi, na Mishali; nao ukafikilia hata Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Shihor-libnathi; kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikilia hata Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hata Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hata Kabuli upande wa kushoto; na Ebroni, na Rehobu, na Hamoni, na Kana, hata kufikilia Sidoni mkuu;kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu; na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.”

Mungu anapokuwa amekubariki wakati wote unakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji na kamwe hautakuja ukauke ona, Asheri walikuwa wamebarikiwa sana na walistawi na walikuwa na furaha, na walifanikiwa sana  

 

Zaburi 1:1-3 “Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”

 

Isaya 44:3-4 “Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa; nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji.”

 

Yeremiah 17:7-8 “Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.”    

 

9.      Naftali (Bwana amenipa Ushindi)

Mwanzo 49:21“Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri.” Yakobo anaitaja kabila hii kama uwakilishi wa watu waungwana sana na wanaozungumza vizuri, hawala lugha mbaya wana mvuto wazuri kama ayala (Paa) na watu walio huru, Ardhi ya watu hawa ilikuwa karibu na Pwani ya Galilaya maeneo ambayo Masihi aliyatembelea sana Musa alionyesha kinabii kuwa Naftali ni watu walioshiba fadhili na kujaa Baraka ona Kumbukumbu la Torati 33:23 “Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na baraka ya Bwana; Umiliki magharibi na kusini.”ni ukweli usiopingika kuwa Yesu alitembelea na kufundisha na kufanya miujiza mingi sana katika nchi ya Naftali ona Mathayo 4:12-16 “Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa,Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.Naftali ni mtoto wa mwisho wa kijakazi wa raheli. Maandiko yanatutaka tuwe waungwana, tuwe na maneno mazuri, lugha nzuri, Wafilipi 2:1-4 “Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.” Tofauti na nduguze karibu wote wa upande wa Raheli Naftali walikuwa huru, lakini hawakuutumia uhuru wao vibaya, walitoa maneno mazuri, walikuwa waungwana hivi ndio wakristo wanavyopaswa kuwa, wakristo ni watu huru, sio watumwa lakini nhawapaswi kuutumia uhuru wao kwa kukosa kiasi au nidhamu wakristo wanapaswa kuwa waungwana katika uzungumzaji, na kujali watu Wakolosai 4:5-6 “Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.”.  Waebrania 13:1-2 “Upendano wa ndugu na udumu. Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.” Tabia ya ukarimu na lugha njema zinaweza kuleta mafanikio makubwa katika biashara, kazi na kujenga mahusiano, watu wa Mungu waliobarikiwa na waliowaungwana hawapaswi kuwa na lugha mbovu, lazima tuwajibu watu wote kwa upole na kuacha majivuno, Mungu atatupa mlango uliofunguka kama Naftali, tutakuwa huru na tuliojawa na uungwana na kupendeza.

 

10. Yusufu (Bwana aniongeze)

 

Mwanzo 49:22-26 “Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matawi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli, Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba. Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake.”       

 

a.      Mti Mchanga wenye kuzaa, Yusufu Baraka hizo zinamhusu yeye binafsi na vijana wake ambao Yakobo alikwisha kuwabariki katika Mwanzo 48

 

b.    Anasifiwa kwa kuwa na uhusiano mkubwa na Mungu na hivyo alibarikiwa sana alikuwa mtumishi wa Mungu na alikuwa Baraka kubwa kwa familia yake ndugu zake na dunia ya wakati ule, alisalitiwa na ndugu zake na kufanyiwa mambo machungu Lakini Mungu alimtia nguvu na kumpa akili na weledi Mungu alikuwa pamoja naye hata kama hakuwa anajua hilo, alibarikiwa maradufu na kupokea urithi mara mbili kama mzaliwa wa kwanza na kupandishwa cheo kuwa mojawapo ya mababa wa Israel na wanawe kuwa makabila ya Israel kuziba nafasi ya Simeoni na lawi ambao Israel aliwatawanya, Mibaraka aliyopewa Yusufu ilikuwa ile ambayo baba zake waliipata, Yakobo anamtaja Mungu wa Yakobo yaani Mungu wake kwa Majina makubwa sana anapotoa Baraka kwa Yusufu

a.       Mwenye enzi wa Yakobo

b.       Mchungaji

c.       Jiwe la Israel

d.       Mungu wa baba yako

e.       Mwenye Nguvu

Ujuzi kuhusu Mungu sasa unajulikana vema kwa Yakobo kutokana na uhusiano wake na Mungu na yale aliyoyafanya kwa Yusufu tofauti na ujuzi ule wa Mungu wa Ibrahimu, na Isaka Mwanzo 31:53 “Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu.” Yusufu alikuwa na tabia njema tangu mwanzo, alipendwa na baba yake, Mungu alisema naye kuhusu maisha yake ya baadaye, aliamua kuwa mwaminifu kwa Mungu, alipitia magumu mengi, lakini Mungu alikuwa pamoja naye alijifunza kujua Mungu ni nani, alitambua mapenzi ya Mungu hata wakati wa mambo magumu, alijifunza kusamehe na kumuelewa Mungu vizuri, watu wa kabila hii ni jamii ya watu wanaoyajua makusudi ya Mungu na kuyafahamu mapenzi yake huku wakiwa na ujuzi kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi na wale wampendao  katika kuwapati mema Warumi 8:28-30 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.”

Yusufu ni mfano mzuri wa mtu aliyekuwa katika imani na uadilifu, aliyajua makusudi ya Mungu na alihakikisha kuwa anawasamehe nduguze na kuwatunza ona Mwanzo 50:15-21 “Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema, Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.Nduguze wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako. Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.”

Yusufu anapata uristhi maradufu miongoni mwa ndugu zake, watoto wake wawili wanafanyika kuwa wana wa Israel wakichukua nafasi ya simeoni na lawi ambao Israel aliwagawa kwa kuwa hawakuwa na rehema Mwanzo 48:3-5 “Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki, akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako nchi hii baada yako, iwe milki ya milele. Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.”  Kwa msingi huo Yusufu anaingia katika orodha ya mababa Ibrahimu, Isaka, Yakobo na yusufu na watoto wake wanaingia katika kabila za Israel, Mtu awaye yote aklifanya vema Mungu atambarikia.


11. Benjamin (Mwana wa mkono wangu wa kuume).

 

Mwanzo 49:27 “Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua, Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.” Hili lilikuwa ni kabila lenye watu wakali wasiotetereka (aggressive) walikuwa wakatili na wapambanaji na wakati wote walitafuta kuwa washindi Ehud ni moja ya waamuzi aliyetoka kabila hili Waamuzi 3:15-23 “Lakini wana wa Israeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi. Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kuume. Kisha akamsongezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyewanda sana.Naye hapo alipokuwa amekwisha kuisongeza hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua tunu, wakaenda zao. Lakini yeye mwenyewe akageuka kutoka huko kwenye sanamu zilizokuwa karibu na Gilgali, akasema, Mimi nina ujumbe wa siri kwako wewe, Ee mfalme. Naye akasema, Nyamazeni kimya. Watu wote waliokuwa wanasimama karibu naye wakatoka na kumwacha. Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake. Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia tumboni mwake; hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma. Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo.” Aidha ni kabila lililotoa mfalme wa kwanza kabisa kuitawala Israel 1Samuel 9:1 “Basi, kulikuwa na mtu mmoja wa Benyamini, jina lake akiitwa Kishi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa, mwenye nguvu.” Mfalme huyu alikuwa hodari sana katika vita 1Samuel 14:47-52 “Basi Sauli alipokwisha kuutwaa ufalme juu ya Israeli, alipigana na adui zake zote pande zote, juu ya Moabu, na juu ya wana wa Amoni, na juu ya Edomu, na juu ya wafalme wa Soba, na juu ya Wafilisti; na po pote alipogeukia, akawashinda. Naye akatenda kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli katika mikono yao waliowateka nyara. Basi, wana wa Sauli walikuwa ni hawa, Yonathani, na Ishvi, na Malkishua; na majina ya binti zake wawili yalikuwa haya; jina lake wa kwanza aliitwa Merabu, na jina lake mdogo aliitwa Mikali; na jina lake mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu, binti Ahimaasi. Tena, jina la jemadari wa jeshi lake aliitwa Abneri, mwana wa Neri, aliyekuwa baba mdogo wa Sauli. Na Kishi, babaye Sauli, na Neri, babaye Abneri, walikuwa wana wa Abieli. Tena, kulikuwa na vita vikali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu ye yote aliyekuwa hodari, au mtu ye yote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.” Katika agano jipya tunaelezwa habari za Sauli au Paulo mtume namna alivyokuwa na hatimaye baadaye Mungu alimtumia sana na akafanya kazi kuliko mitume wote Matendo 8:1-3 “Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.” Israel anamfananisha Benjamin na Mbwa mwitu kwamba mbwa hawa ni wadogo, lakini wako makini nan i wawindaji wazuri na wakali hawana mchezo wanauwezo wa kurarua rarua wana umoja na huwinda kwa kufunga mtaa wanaogopwa na wanyama wengi hata wakubwa, mbwa mwitu hakubali kushindwa, anaamini katika ujamaa, wanapiga kazi na hawachoki, wakishiba wao hushinda wanacheza na kufutrahi, na ukitaka vita nao gusa watoto wake, watu wenye Kabila hii wanafanikiwa katika kila wanachokitamani na kutimiza kila jukumu wanalopewa na kulifanikisha

 

Yakobo Anakamilisha kazi yake Duniani

 

Baada ya Israel Kumaliza kuwabariki vijana wake kazi yake ikawa imekamilika aliagiza azikwe Israel katika mji wa Hebron Pale pale walipozikwa wazee wake, kwanini alikifumbua kinywa chake alitaka kuwabariki, alitaka kuwatabiria, tabia zetu na mwenendo wetu utaamua kuwa sisi tuwe watu wa aina gani, Kila mmoja alikuwa na mambo yake mazuri na kila mmoja alikuwa na mapungufu yake, lakini tunahitaji neema ya Mungu kuiga mazuri kwa maana sisi sasa ndio hao wana wa Israel, Leo hii hayuko Benjamin, hayuko Asheri wala Gadi watu hao ni mimi na wewe je unayasikiliza mausia ya Yakobo? Je unasikiliza Israel baba yako, neno la Mungu ndio mausia yetu leo, endapo tutalisghika na kulitii na kuliishi litaamua hatima yetu

 

Mwanzo 49: 28-33. “Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki. Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi. Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake

Bwana na ampe neema kila mmoja kubwarikiwa na Roho Mtakatifu, tunapolishika neno lake na kubadili matendo yetu ili tupate thawabu zinazokusudiwa kwetu amen uongezewe neema

 

Rev. Innocent Kamote.

 

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!

 

~0718990796~