Alhamisi, 20 Novemba 2014

SOMO: Kwa Nini Wakristo Tunavaa Viatu Wakati Wa Ibada?

Nachukua nafasi hii kwa unyenyekevu mkubwa kujibu swali kwa nini wakristo tunavaa viatu wakati wa Ibada? Hili ni swali muhimu sana kwa vile linaulizwa na wakristo na waislamu hivyo nitalijibu kwa faida ya jamii nzima, lakini naomba kutoa angalizo, kuwa mada hii isitumike kwa kusudi la kukashifiana au kutukanana kwa vile nimeingia huku kwa kuwa nataka kujibu swala na sio kwa makusudi ya kuamsha mabishano ya Kidini Mimi ni mjenzi wa jamii na sio mmbomoaji ni mwalimu wa falsafa na nafundisha imani zote kwa makusudi mema ya kujenga na sio ya kubomoa
Ndugu zetu waislamu huwa wana huwa wanatulaumu kuwa huwa hatumueshimu Mungu kwa vile tunavaa viatu wakati wa ibada tofauti na wao ambao huvua viatu hasa pale wanapoingia Msikitini, waislamu hudai hayo kwa kunukuu Biblia (Kutoka 3;3-6 na Yoshua 5;13-15).vifungu ambavyo huonyesha Musa na Yoshua wakiambiwa wavue viatu. Kutoka 3: 3-6 Inasema …


3. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. 4. BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. 5. Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu…..”
Kwa ufupi ni kuwa hakuna aya yoyote katika quran ambayo inaunga mkono swala zima la kuvua viatu wakati wa kuswali, zaidi ya aya hizi mbili zinazopatikana katika Biblia yaani upande wa agano la kale, waisalamu wanaovua viatu wamepata mila hii kutoka katika Biblia kwa vile Historia inaonyesha kuwa hata waislamu walioishi kipindi cha Muhamad na muhamad mwenyewe waliswali wakiwa na viatu. Na hakuna agizo lolote kutoka katika Quran linaloagiza kuvaa viatu!


Ni muhimu kufahamu kuwa kwa waislamu wanaoifahamu quran, quran haiingilii maswala ya ibada za watu wengine kila umma umejaaliwa kawaida ya ibada wanayoishika soma (Surat al-Hajj-I 22; 67) kwa mujibu wa Pamfleti moja ya huduma ya biblia ni jibu Tanzania imenukuu kitabu kimoja kiitwacho Uislamu katika Biblia uk.20-21 kuna maneno yasemayo.


“Waislam wanapoingia pahala popote patakatifu kama vile msikitini huvua viatu, kinyume na wakristo…”Mwandishi wa pamfelti hilo anadai waislamu ni lazima wajiulize kuwa Musa alipoambiwa avue viatu maana pale alipokuwepo ni mahali patakatifu je mahali pale palikuwa mahali pa ibada kama msikiti? Kama mahali pale palikuwa patakatifu kwa kuwa Mungu alikuwepo pale je ni lini huyo Mungu amehamia msikitini? Mungu yuko mahali kote je Musa alipoambiwa avue viatu aliviweka upande gani ambapo Mungu hayupo?na kama Musa alivishika mkononi je havikuwa najisi kwake? Biblia inatufundisha kuwa utukufu wa Mungu umeijaa dunia nzima (Isaya 6;3) ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hakuwa na maana inayodhaniwa na waislamu bali alikuwa anawataka watu hao Musa na Yoshua kuwa wanyenyekevu,watii,wenyekujishusha,wenye hofu ya Mungu Viatu pia ilikuwa iashara ya kuwa na mamlaka lakini mamlaka tuliyo nayo kwa Mungu si kitu, si kila kinachotamkwa katika Biblia ufasiriwa kama mtu apendavyo kwa mfano Mungu asemapo “Tahirini govi za mioyo yenu”(kumbu 10;16). Je, Mungu humaanisha moyo utahiriwe? Je moyo unaonekana?, Una govi? Itamfaa nini mtu kuvua viatu wakati wa ibada huku moyoni ni mchafu ?


Ni muhimu kufahamu kuwa waislamu wanapovua viatu hawamfuati Muhamad ambaye yeye ni Ruwaza nzuri sawa na (surat Al-ahzab 33;1). Muhamad mwenyewe anasema “Alaa Yuminu ahadukum hattaa Yakuna Hawaahu Tab’an lima jitubihi” yaani haamini yeyote (katika ninyi waislamu)hata matamanio yake yawe yenye kufuata kile nilichokuja nacho(yaani kuvaa viatu ibadani). Kwanini kwa sababu Muhamad mwenyewe alivaa viatu ibadani, angalia uthibitisho;-.


• Muhamad alikuwa anaswali, huku amevaa viatu, Al-Mughira alijaribu kumkumbusha Muhamad hasa alipomuona anatawadha juu ya viatu na kuingia navyo msikitini Mughira akasema “Yaa Rasuwlala-hi Nasiyta”, (yaani ewe Mtume wa Allah Umesahau) Muhamad akajibu “Anta Nasityta Liannahuhadha Huwaamaratani rrabbu” (Yaani wewe ndiwe uliyesahau kwa maana hivi ndivyo alivyoniamuru Mungu) soma Miskat-al-Masabih,sura ya 10 sehemu ya III,Kitab-al-Wadhu) Kama Muhamad aliamuriwa asali na viatu je waislamu wametoa wapi swala la kuvua?


• Muhamad anaonekana tena akiswali na viatu katika (sahih-al-Muslim,I,hadith 555) hapa Saad bin Yazid (abu Maslama)alipokuwa anamuuliza Anas bin Maliki “Akana Rasula llaah (SAW) Yaswullay fiy l-Na’alay-hi?qala na’am” yaani Mtume wa Allah huswali huku amevaa viatu vyake? Anasi akajibu “Ndiyo”


• Sehemu nyinginezo nyingi ambazo Muhamad anaonekana akiswali na viatu na tena si kosa kufanya hivyo ni pale alipotawadha juu ya viatu na kuingia navyo msikitini na kuswalisha (Muwata-Imam malik sura ya 16-hadithi 69) pia soma sahih al-Bukhari I,hadith 388.,Sahih-al-Muslim I,hadith 1129,1130,nk).Pia Mishkat-a;-Masabihi vol ii hadith 766,Sunnan Abuu Dawud – Juzuu ya 1-uk,36-40 (Tafasiri ya Profesa Ahmad Hassan)nk. Katika kitabu hicho Abuu Said amemkariri Muhamad akisema baada ya kuulizwa swali.


“Mtu akifika msikitini na huku amevaa viatu vyake afanye nini?” kwa kiarabu “Idhaa jaa-a ahadukum lmasijid,Fal-yaqalab na’alayhifal-Yandwur fiy-himaa” Fiq-us-sunnah juzuu 1 uk 32,na muhamad akajibu
“Fa idhaa raa Khabathan,Fal-ya Masahu bii l-ardhhwi,Thumma liyu swalla fiy-himaa” yaani amesema mtume “Kama mmoja wenu amekuja msikitini, basi ageuze miguu yake kuona chini ya soli.akikuta kuna uchafu katika soli basi avifute katika ardhi (yaani aviburuze chini)Kisha aingie msikitini aswali navyo”
Ukweli ni kuwa kwa matendo yetu ya nje hatuwezi kumpendeza Mungu ambaye ni mtakatifu sana (Ebrania 12;14) haki ya mtu mbele ya Mungu inapatikana kwa imani tu (Galatia 3;11)

Waislamu ni lazima Wajifunze kutoka kwetu.

Quran 6;90. “Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza basi Fuata Uongozi wao”. Allah amewaamuru waislamu na Muhamad afuate uongozi ulio ndani ya injili kwa kuwa humo mna uongozi kwa wacha Mngu wote (quran 5;46), Waislamu ni lazima waisome Biblia kwa umakini na kujifunzaa yaliyomo humu ili siku ya hukumu wasiseme walikuwa hawana Habari ya yale yanayosomwa na Wayahudi na Wakristo (Soma Quran 6;156 soma ufafanuzi yaani Torati na injili).hakuna Mwislamu yeyote mwenye haki ya kumpinga Kristo kwani quran imeelekeza kufata uongozi humo ni lazima tuchukuwe nafasi hii kuwakumbusha waislamu kuwa atakaekuja kuuhukumu ulimwengu wote ni Yesu Kristo kwani ndiye aliyepewa Idhini hiyo hivyo kupingana na Mafundisho yake ni sawa na kubishana na Jaji (Quran 43;61-62, 78;38, Matendo 17;31).Muhamad mwenyewe aliwaonya waislamu na kuwakemea Kuwa mtakuwa katika hali gani(waislamu)atakapoteremka mwana wa Maryam na kuwa Mtawala au kiongozi Miongoni Mwenu?(sahih-al-Muslim IV,Kitab-al-Swifat-hadith 72 uk.2169)
Jambo la mwisho ni kuwa kila mtu na amuabudu Mungu wake vile anavyojisikia Mungu ni Baba wa wote na ana watoto tofauti wa tamaduni tofauti na aliyafanya yote kwa utukufu wake, yeye anapendezwa na kila mtoto wake anavyomuabudu kama alivyo hatupaswi kuhukumiana nani ana ibada sahii kuliko mwingine ibada sahii ni Mungu kuukubali moyo wako kama alivyokubali wa Habil na kukataa wa Kaini ingawa wote walikuwa wakiabudu ni wazi kuwa ibada ni mkao wa moyo na sio mtindo gani unautumia katika kuabudu


Ninapotaka kuzungumzia swala la uwasilishaji ibada nataka nikuonyeshe kwanza stori ya mtumishi mmoja wa Mungu ambaye alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa yaan Birthday mtumishi huyu alikuwa na watoto wanne wote walikuja kumpongeza baba yao na kumpa zawadi wa kwanza ambaye alikuwa na miaka 26 wa kike, alimpa zawadi ya Fedha baba yake kwa ajili ya kutembea kokote atakako kisha akambusu baba yake na kumwangalia kwa upendo, wa pili ambaye alikuwa na miaka 23 wa kike Yeye alichora picha nzuri sana na alimkabidhi baba yake kisha akambusu na kumkumbatia na kumnong’oneza kwa sauti ndogo nakupenda baba, kisha mtoto wa tatu mwenye miaka 21 wa kiume yeye alileta shati zuri kisha akamvalisha baba yake mabegani na kumwambia wewe ni baba wa pekee duniani na wa mwisho mwenye miaka 16 wa kiume alimpa baba yake saa aliyokuwa amenunua safarini na kisha akamwambia Baba yake najivunia kuwa na baba kama wewe bila shaka utaipenda zawadi hii. Unajifunza nini katika mfano huu? Kila mtoto anayo namna yake ya kuonyesha upendo na shukurani kwa baba yake na kama ambavyo kila zawadi ilikuwa tofauti hali kadhalika namna walivyoonyesha upendo na maneno waliyoyatoa yalikuwa tofauti je unafikiri kuna aliyempendeza baba yake zaidi kuliko mwingine? Bila shaka hapana wote walimpendeza hivyo ndivyo Mungu anavyopendezwa na kila mtu anayeonyesha upendo wake kwake na kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa kila ibada kama imeelekezwa kwa Mungu katika hali ya kumpenda basi hata kama ni tofauti na ile uliyoizoea Mungu anapendezwa nayo Hata hivyo Kibiblia Lazima kila Ibada Ipitie kwa Yesu Kristo tu
Maana Msingi mwingine hakuna mtu anayeweza kuuweka, isipokuwa uliokwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo. Wako mkuu wa wajenzi mwenye Hekima Rev. Innocent Mkombozi Innocent Kamote

Jumatatu, 17 Novemba 2014

Ujumbe: Tatizo La Yule Mwana Mkubwa!

Katika Luka 15: 11- 24,25-32.


KWA NINI YESU ALIFUNDISHA KWA MIFANO.


Ziko sababu kadhaa zilizopelekea Yesu kufundisha kwa mifano hii ni njia nzuri na kubwa aliyoitumia Mungu na Manabii na pia marabi lakini kwa Yesu kulikuwa na sababu kadhaa zilizopelekea kunena kwa mifano

1.       Alitumia mifano ili kukwepa mitego ya watu waliomwendea ili kumnasa kwa Maneno Marko 12;1-12.

2.       Alimtumia mifano ili kutofautisha watu walioitafuta kweli na waliofuata miujiza na mikate na pia kama hukumu kwa watu wenye mioyo migumu, Mathayo 13;10-17

3.       Alitumia mifano ili kukwepa au kuufikisha ukweli kwa waalimu wa torati waliofuatilia mafundisho yake (Mfano wanafunzi wa vyuo vya Biblia)

4.       Kupunguza ukali wa ujumbe ili kukwepa kupigwa mawe au kuuawa kabla ya wakati 2Samuel 12;1-6. Mungu huwapa Hekima Manabii wake namna ya kupeleka jumbe bila kupata madhara

5.       Kusaidia watu kuelewa kwa urahisi habari za ufalme wa Mungu


KANUNI YA KUTAFASIRI MIFANO


  Ni muhimu kufahamu kuwa mifano ya kibiblia hubeba maana moja tu na ambayo ndio kweli ya kiroho kwa hivyo ni marufuku kufasiri mstari mmoja mmoja ulio na mfano na kufafanua kwa maana za kiroho hii sio kanuni ya kutafasiri mifano na kwa kufanya hivyo huwezi kupata kweli iliyokusudiwa unapaswa kusoma mfano mzima na kuangalia unabeba nini Principle of Contents kisha uweze kuelezea kile kinachosemwa mfano Kwa mfano wa Msamaria Yesu alikuwa akifundisha Jirani wa kweli ni yupi.

Baba wa Mwenye Upendo akikimbia kumpokea mwanae aliyepotea kwa Furaha kwa vile amerudi Nyumbani

 TATIZO LA MWANA MKUBWA.



Tunaona hasara za mwana mpotevu jinsi alivyofanya mambo mabaya ya kusikitisha na jinsi alivyokosa amani na kurudi kwa Baba yake, na jinsi Baba yake alivyompokea lakini kwa namna ya kushangaza Yule mwana  mkubwa alipokea mambo kwa mtazamo wa tofauti.

Jinsi Mwana huyu mkubwa alivyopokea inatufundisha mambo ya msingi yafuatayo (Luka 15: 25- 32)



I.  ALIKUWA NI MTU WA KUJIHESABIA HAKI ( 29-30)


Huyu mwana  mkubwa alikuwa na tatizo kubwa sana lililohitaji msaada wa Mungu, Alikasirika alisusia, na alijiona kuwa ni mwema kuliko ndugu yake na kuwa yeye pekee ndiye mwenye haki ya kufanyiwa sherehe kuliko mwingine na  kuhukumu, hii ni tabia ya  Kifarisayo ambayo Mungu anapiga vita, ( Luka 18: 9- 14) Utoaji na  Baraka za  Mungu haziko katika wema au ubaya wa mtu ( Math 5: 45) Baraka za Mungu ziko kama  Mungu anavyoamua kwa yeye anayetaka kumrehemu  humrejeza ( Warumi 9: 11-16) Mungu angekuwaanabariki kwa matendo ya haki basi Yakobo  hangebarikiwa  kwani alikuwa mwenye  hila na muongo, lakini alibarikiwa kwa rehema za Mungu tu. Ni ukarimu na rehema za Yule baba aliamua afanye hivyo kwa mwana mpotevu ndugu mkubwa – Alijifanya ni  mtii zaidi kwa babaye, Alimhukumu nduguye.



II.  ALIKUWA HANA UPENDO BALI  CHUKI.(28- 30)


Mwana mkubwa alikuwa na tatizo la ubinafsi na chuki, mafundisho ya kristo  kupita  mitume  wake  yanpingana sana na tabia ya chuki yakitaka  tuwe na upendo,  watoto halisi  wa  Mungu wanajulikana kwa tabia ya upendo kwa wanzao.

(1 Yohana 3: 10- 12, 4: 20)


III.  ALIKUWA MTU WA KUTAFUTA MAKOSA (25- 38)


Huyu ndugu mkubwa anaonekana kuwa na tabia ya  mafarisayo, tabia ya kuhukumu au kuona kosa la Mwingine hii nayo ni tabia ambayo Yesu alikemea hadharani. (Luka 6: 41-42) Ndugu yake mkubwa alipaswa kwanza kushughulikia tatizo lake la ndani kabla ya kutoa shutuma na lawama  kwa mwenzie, yeye alihukumu na aliona kuwa hata baba yake  wa mbinguni ana  kosa.


IV. HAKURIDHIKA; ALIKUWA NA CHOYO NA ALIKOSA FURAHA. ( 31-32)


Mwana huyu mkubwa alikuwa na vyote, na  katika uaminifu wake ; angeweza kufanya karamu aifanyayo na rafiki zake na hangezuiwa, kwa kweli hakuridhika na  alihukumu  huruma ya baba yake kwa wengine, dhidi ya yote alikuwa na  choyo na  alitaka yeye awe yeye tu, choyo ilimkosesha  furaha,  babae alimtaka afurahi tu, Mungu anapobariki anataka tufurahi anapobariki wengine pia.

Mifano ya Yesu pia ilikuwa inatoa mwanga namna Mungu atakavyo hukumu kwa haki wale wanaojikinai na kufikiri kuwa ni wema na wamestahili kuliko wengine watakataliwa katika Ufalme wa Mungu uwe mwangalifu

Somo Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote

Jumamosi, 15 Novemba 2014

Nikadebwela Lifti kwa Saa Tatu!

Sitaki kutaja jina langu ingawa sio vibaya kufanya hivyo, Mimi ni kijana wa miaka 33 hivi Nilikuja Dar es Salaam kutoka Rufiji mwaka 1999 wakati huo nikiwa na miaka 27, kwa hiyo naweza kusema kwamba siifahamu Dar es Salaam vizuri, hata hivyo kutokufahamu Dar haina maana ya kutokufahamu mambo mengine ya kawaida ambayo kwa dunia ya sasa mtu anayeishi mjini kuyajua ni jambo muhimu, lakini pia la kawaida

Siku ninayotaka kuizungumzia ni Machi mwaka 2001 siku hiyo mjomba wangu ambaye ndiye aliyenilea  aliniita na kunituma , aliniambia niende mjini kwa jamaa yake mmoja nimpelekee fomu zake Fulani, huyo jamaa azishughulikie, alinielekeza ofisi za huyo jamaa zilipo, mjomba alinipa maagizo na kumtaja  huyo rafiki yake  ambaye nikimtaja pengine hata wewe utamfahamu ukifika pale’Panda lifti ghorofa  ya kumi ulizia ..’, Nilimkubalia na kuondoka ,nataka nikuambie jambo moja ni kwamba tangu kuja kwangu Dar nilikuwa nimepita majengo kadhaa wa kadhaa na kuona lifti Nasema kuona, basi nilipojua ni ghorofa ya kumi nilisema iko kazi, nilijiambia kuwa badala ya lifti ningetumia ngazi tu, Nilipofika kwenye jingo lenyewe ambalo lilikuwa bado jipya kabisa  wakati huo ilikuwa 2001 nilikwama baada ya kugundua kuwa hata njia ya kupandia ngazi kwa miguu sikuweza kuiona, Niliona aibu kuuliza kwa hofu ya kuonekana mshamba, Basi ilibidi nijiunge na watu wengine waliokuwa wakisubiri lifti na kupanda, sikuwa najua kuwa , nilifikiri labda kungekuwa na dereva na kondakta au mtu Fulani aliyeniendesha.


Nilioona watu wanadandia name nikadandia, niliona watu wanaboinyeza kitu Fulani kasha taa inawaka, Nilijinyamazia, na kiroho kilianza kunidunda, Lifti ikapanda watu wana shuka na kuingia, mwisho watu wote wakashuka na wakapanda wengine , nilihisi kama lifti ilikuwa inashuka lakini sikuwa na uhakika nilienda nayo huku nikijaribu kujiuliza maswal, Niliona watu waliopanda wakishuka tena na wengine wapya waliingia na lifti ikaondoka kuelekea  huko inakoelekea , Mimi nilibana tu,nilikuwa naangalia watu wanavyobonyeza lakini sikuwa na uhakika ni kitu gani hasa kinachofanyika , Nilitembea na hiyo lifti mpaka nikahisi  kama vile ninjaumwa  maradhi ya moyo au kitu kingine kibaya zaidi Nilikwenda na kurudi kwenda na kurudi  tangu kwenye saa tano na nilikuwa na uhakika kuwa imefika saa nane.
Lifti ni chombo kigeni sana katika miji mingi ya Tanzania pichani Lifti ya kwanza kuzinguliwa mjini Mbeya

Nikiwa nimefikia hatua ambayo sasa siwezi kuendelea kuwa bwege yaani kutaka kuuliza, Bwana mmoja mwenye mavazi ya kaki na bluu aliniuliza vipi hufiki unakokwenda? Tangu asubuhi uko ndani ya lifti, abiria wa lifti walivunja shingo zao kunitazama kama unavyojua watanzania masikio yako juujuu kama sungura kutaka kusikiliza ya watu, Nilibabaika lakini nilijikaza na kusema naenda ghorofa ya kumi lakini sipajui…” Yule jamaa ambaye kumbe alikuwa ni mesenja kwenye moja ya ofisi kwenye jingo lile alicheka na kusema ndio maana tangu saa tano hivi nakuona umo humu, naenda narudi nakuona mzee umo humu, nikadhani unataka kubwedela...” Abiria waliangua kicheko

Nilitazama chini hasa kwa kuzingatia kwamba kulikuwa na mademu wengi wakati huo mle kwenye lifti, Yule mesenja alikuwa kama amepata pa kuonyesha ujuaji wake ‘Ona ukitaka kwenda ghorofa ya kumi unabonyeza hapa..’ Halafu aliendelea kunifundisha mambo mengine ya lifti ni tuisheni ya bure lakini!

Nilishuka ghorofa ya kumi na kuulizia ofisi za Yule jamaa, Nilikuwa nahisi kizunguzugu mtindo mmoja, Niliambiwa huyo jamaa yake mjomba alikuwa ametoka Ilibidi nimsubiri hadi kwenye saa kumi aliporejea, Nilimkabidhi fomu na aliponiuliza sababu ya kuchelewa nilimwambia nilikuwa nimepotea jengo, unadhani wakati narudi nilipanda tena lifti? Kama unadhani hivyo shauri yako unadhani mbumbumbu niko peke yangu tuko chungu nzima 

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
ikamote@yahoo.com
0718990796
0784394550

Jumatano, 5 Novemba 2014

Nikajifunika Kusubiri Uroda!

Septemba 2003 nilikwenda kumsalimia mjomba wangu mjini Dodoma, Hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika Dodoma, Wakati huu nilikuwa nimemaliza kidato cha sita na nilikuwa nasubiri matokeo hali ya hewa ya Dodoma wakati huo ni mchanganyiko joto wakati wa mchana na Baridi kali wakati wa usiku.


Huyu mjomba wangu alikuwa mtu wa kinywaji sana na wanawake kwa sana, Lakini kwa sababu alikuwa anatengeneza hela za kutosha sisi wapwa wake tulimpenda sana tu,kwani haja yetu kubwa ahikuwa umjomba bali mshiko kutoka kwake, Nakumbuka nilipofika pale kwake mkewe yaani shangazi yangu alikuwa amesafiri kwenda  kwenye msiba kwao Tabora, Hapo nyumbani kwa hali hiyo alikuwepo mjomba na wanawe wane wa kike, hawa watoto wa mjomba walikuwa wakubwa  mmoja alikuwa kidato cha tano, wa pili cha nne, watatu kidato cha kwanza na wanne  darasa la sita.


Kama unavyojua watoto wa kike wanajisikia vizuri kuwa na kaka kwa hivyo nilipofika pale binamu zangu walifurahi sana na wakawa wanapenda sana kunipa good time. Nilikuwa naelewana sana nayule wa kidato cha nne kuliko wale wengine, kumbe huyu binamu nwangu alikuwa na buzi lake, ambalo lilikuwa linamsumbua sana, na mjomba na shangazi walisha litangazia hali ya hatari hilo libuzi lake, sikuwa najua jambo lile na hakuna ambaye angenijulisha kwani hakuna ahatujawahi hata mara moja kuzungumzia  maswala ya mapenzi.


Basi nakumbuka siku hiyo niko nyumbani jioni, nikamwona huyo mwizi akiingia chumbani mwa Yule binamu yangu mpendwa, alikaa huko kwa muda kabla hajatoka. Alipotoka name nikajitoma ndani nikakuta binamu yangu anavaa, kwa sababu ya balehe labda nilimwambia binamu yangu kama unataka nisiseme na mimi naomba maana nimeona kila kitu, Binamu yangu Yule aliniomba sana nisifanya hivyo, Tunasoma wote wala hatukuwa tunafanya jambo baya alisema kwa kujitetea, Niliomwambia unataka hutaki ni lazima nami nionje au niseme kwa mjomba. Baada ya kuona kuwa nimepenia sana, Yule binamu yangu alikubali, Nilikata kiu yangu kibabe na kuvinjari vilivyo siku ile.

Kumbe jambo lile lilimuuma sana kupindukia, ingawa hakuonyesha hivyo, siku ya tatu tangu tukio lile Yule binamu yangu alinifuata akiniomba tufanye naye tena jambo lile, Nilifurahi sana , huyu binamu yangu alikuwa akilala peke yake kwa sababu ya kusoma  kujiandaa kwaajili ya mitihani ya mwisho, hivyo aliniambia saa sita hivi wengine wakiwa wamelala niende chumbani mwake nilifurahi sana na kujisifu.


Basi usiku wa saa sita nikiwa nimetinga chumbani mwake tukiwa tunazungumza maswala ya mahaba, mara btulisikia gari Mjomba alukuwa amerudi, baada ya kusikia mlio huo wa gari  Yule binamu yangu aliniambia nimsubiri anakwenda kuzuga ili baba yake asijue kinachoendelea, aliniambia nizime taa nilale kwa kujifunika Nilifanya hivyo haraka haraka, Nilitulia hapo kitandani moyo ukinidunda, halafu nilisikia mlango ikifunguliwa na taa ikiwashwa, kabla sijajifunua kuangalia kinachoendelea nilishtukia kitu kikali kikinicharaza matakoni niliruka na kupiga yowe. Mijeledi ilizidi kuniangukia kama nilikuwa punda


Ghafla mpigaji alisita na kuniambia yaani wewe nakuchukulia kama mwanangu kumbe umekuja kuniharibia watoto nyama wee, mjomba akiwa na zinga la bakora alisema wewe unathubutu kuingia katika chumba na kuthubutu kumbaka dada yako nyama wee aliniongeza mijeledi kadhaa pale, Kisha aliniamuru kuvaa na kwenda chumbani kwangu kuchukua kila kilicho changu, Nakupeleka hotelini utalala huko na kesho urudi kwa mama yako, ibilisi wee, nilijaribu kujitetea kwamba tulipanga na mwanae tukutane lakini hakunielewa Yaani mpange halafu aje aniambie yeye ana kichaa?unadhani wanangu ni Malaya kama wewe?...


Ilibidi wale binamu zangu wengine waingilie kati kunitetea na kutetea kwao kulileta matunda ya kuhurumiwa  nilale hadi asubuhi ,ambapo niliambiwa utawahi basi la kwanza kurudi Dar kwa kweli niliaibika kwa kiasi cha kushindwa kuelezea, Hadi leo sijaweza kwenda kwa mjomba, ingawa ameomba sana niende kuwasalimia  lakini aibu niliyo nayo ni kubwa lakini bila shaka baada ya kuelezea kisa hiki huenda mjomba na watoto wake wengine watajua  ukweli ni kwamba Yule binamu yangu  alifanya vile ili kunikomoa  nami naona ni sawa tu kwani sikuwa nimemtendea haki. Kumbe alimjulisha baba yake tangu mchana kwamba nimekuwa nikimtongoza na wakakubaliana kuwa wanikomeshe.

Na. Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
0718990796
0784394550
e-mail ikamote@yahoo.com

Nikajimwaga Kwa Mwenye Mali!

Naitwa Salome Shemazua mkazi wa Pongwe Jijini Tanga nina umri wa kati ya miaka 35, ni mshichana mwenye umbo zuri la kibantu ambalo linaweza kumvutia mwanaume yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupenda wanawake wenye uasilia yaani wale wasiopenda wanawake vimbaumbau wale wanaoijifanya eti wana menteini na kukondesha vipaja vyao kaa kuku wa kisasa, mimi ni kibonge bwana umbo nambari nane lakini hata hivyo sijaolewa. Hiyo sio shida kwani wote tunajua kuwa kuolewa nako ni majaliwa.


Hata hivyo katika kubangaiza hapa na pale katika shughuli za maisha nilitokea kupendwa na baba mmoja hivi wa makamo sikuwa na muda hata wa kuuliza umri wake ingawa alionekana kama angeweza kunizaa na huenda pia ningeweza kuwa mwanae wa pili au watatu hivi, nilikutana na baba huyu pale Texas motel moja ya baa maarufu hapa Pongwe, baba huyu aliyekuwa anafanya kazi saruji kiwanda cha simenti kilichopo karibu na mji wa Pongwe alitupa ndoana yake kwangu nami bila ya fedheha sikuwa na hapana  nilimkubalia, wenyeji wangu walikwisha kunipa stori kuwa wanaume wa saruji wana pesa kama njugu kutokana na mishahara mizuri wanayolipwa na kiwanda hicho ambacho huchangia mapato ya kutosha katika jiji la Tanga niliona nami nimepata wangu wa kumchuna,

 Nilijitahidi sana kumpagawisha baba Yule kimapenzi kama unavyojua hapa Tanga waja leo waondoka leo  nilimpagawisha na mambo ya kipwani, nilijituma hasa nikijua kuwa hii ndio nafasi ya kumfanya baba huyu ajikite kwangu na kumsahau bi mkubwa,  hasa ukichukulia kuwa Alisha mwaga malalamiko kibao kuhusu bi mkubwa kuwa hajitumi na ni mshamba na kuwa hata kimaumbile mimi nimemzidi bi mkubwa kwa kila idara alidai mzee huyu kuwa bi mkubwa huyo ni kafupi na kamekomaa na ukikaona ni kuwa hata mkononi hakajai sikujua kwanini sasa alimuoa au alilazimishwa lakini niliona vyovyote iwavyo shuhuda hizi zinanipa ujasiri wa kujituma kuliko, na kumuonyesha kuwa na sisi wenye maumbile ya kibantu mchezoni nasi hatujambo nikijipindua hivi na vile kuonyesha manjonjo  kwa ujumla nilifanikiwa sana kumroga Baba Yule wa bara huko, hapa simaanishi maswala ya kishirikina namaanisha jinsi nilivyofanikiwa kumfisadi kimapenzi baba Yule,


Kujituma kwangu hakukuwa bure kwani alinihamisha kwenye nyumba ya kupanga na kunijengea kajumba kangu kazuri maeneo ya Ambangulu kwa wale wanaoijua Pongwe kule Tanga, nilijengewa kajumba potabo kwani kana vyumba vitatu na kila kitu ndani yaani selfu konteini  niliendelea kujidekeza na kupewa kila kitu nilichokitaka  ingawa nilimsikia Buzi wangu akilalamika kuwa ana maswala ya Ada ya watoto na kuwa na majukumu mengine huko kwa bi mkubwa, mi sikujali kwani niliendeleza ufisadi wangu bila kujali kuwa kuna kafamilia kanaumia  ingawa kaubinadamu kanaponijia  huwa najiuliza je ningelifanyiwa miye ingekuwaje? Lakini Mapepo ya ukatili yaliponivaa sikujali nilijitia moyo acha huyo bi mkubwa akome, 

Mungu ametuleta duniani tukomeshe wanawake wachovu wasiojituma kwa nini amtese baba wa watu ? mtu unapata bahati ya kuolewa halafu uinaichezea kweli upele anapewa asiye na kucha nilijitia moyo kuhalalisha upashikuna wangu na ufisadi kiwembe na nilitiwa moyo kwani wanawake wengi pale Pongwe hizo ndo issue zetu wengi ni nyumba ndogo.


Siku moja iliyopelekea kuelezea kisa hiki kama waswahili wasemavyo  “Mwizi zake arobaini” au za mwizi arubaini, Nilipatana na mzee wangu Yule  kwamba tukatese huko maeneo ya Raskazone njia ya kwenda hospital kuu ya Mkoa bombo karibu na daraja upande wa kulia ambako kuna hotel moja maarufu siku hizi nyuma kidogo ya shule ya sekondari ya mkwakwani sipendi kutaja jina la hoteli hiyo kwa maslahi ya mwenye hoteli hata hivyo kwa wenyeji wa Tanga watakuwa wamenipata vilivyo lakini hata kabla ya kwenda hoteli, Bwanangu Yule aliniambia nitangulie mjini na kupitia saluni kisha yeye angenipitia akitokea Saruji anakoishi  akiwa na usafiri wake, Nilitangulia na rafiki zangu kadhaa waliokuwa wakienda mjini nao kwenye mishemishe zao tuliingia saluni moja karibu na stendi kuu ya mji wa Tanga katika barabara maarufu kama Taifa rodi, saluni hii inapendwa na watu wengi sana hususani wakiwemo wale wanaotokea Pongwe hasa kwa sababu ya utaalamu wao pia wa kusuka rasta, na pia kuandaa maharusi, kama iliyo ada tulikutana na wanawake wengine kadhaa wengine wakihudumiwa na wengine wakisubiri, tulipofikia hatua ya kuhudumiwa  kama unavyojua mambo ya umbeya wa saluni tulianza na mada mbalimbali za kisiasa, umbeya udaku na mengineyo kedekede na baadaye ilikuja mada ya uchunaji mabuzi, hapo ndipo nilipodakia kama nimefikishwa kwani mimi sio mzuri sana kwenye maswala ya siasa za Tanzania nilizichoka kwani niliona kama tunazugwa tu  hivyo sikuwa na interesti na siasa tangu alipostaafu Mkapa na hata kufatilia Bunge nilifuatilia alipohutubia Kikwete ile hutuba yake ya bungeni ya kwanza kabisa, kwa hiyo eneo hili utafikiri nilipewa maiki nilieleza kuwa kuchuna mabuzi kunalipa, kulikuwa na mama mmoja mfupi aliyeonekana kama amekomaa hivi alionekana kupinga mada ya maswala ya waume za watu na kuonya kuwa inatesa sana wale walioolewa. Nilimkatisha mama huyo na kuanza kumsomesha kama mtoa mada mkuu huku nikiungwa mkono kwa herufi kubwa mada hii ilinigusa utafikiri ndio mwenyekiti wa kamati Fulani huko Bungeni  nilionyesha faida kadhaa za kufaidika kutokana na kuchuna mabuzi, huku nikitamba juu ya kajumba nilikojengewa  na aina ya simu maarufu kama blakiberi niliyonunuliwa na buzi na nilionyesha wazi jinsi wanaume wa saruji wanavyojua kuhonga na kuwa hata pale saluni buzi wangu atanipitia kwenda kutesa maeneo ya Rasikazone na kuwa atalipa hata hela ya gharama yote ya pale saluni, nilitoa mada siku hiyo utafikiri kungwi wa kicheni pati niliwaponda sana wanawake wachovu na kueleza pia kuwa buzi wangu anasema kuwa ka mwanamke kake kamekondeana na kukomaa kama nyigu na kuwa hata kwenye mkono hakajai hakana intateiniment na kwa mkwara mkubwa wakati mwingine niliwasiliana naye kumuulizia hani kuwa yuko wapi na mbona anachelewa ili mradi tu kuwapagawisha wanasaluni pale, Mama Yule kimbaumbau  aliyekuwa na nywele nzuri sana nyingi lakini kanyimwa nyama mwenye uso uliionekana kama ana mapito hivi kama wasemavyo watu wa dini Fulani ambao hujidai wanaimani kali,  alinyamaza kimya kama amelowa maji, nilimwaga sera na hatimaye alionekana kuunga mkono kama mbunge aliyepotea kutoka kambi ya upinzani, hilo lilinipa kichwa na kujiona kama ninatawala saluni kwa muda wana saluni wenyewe walikuwa bize kutushughulikia wakiwa kimya  na wengi walikuwa wakinisikiliza jinsi nilivyojimwaga na kumkandia mke mwenza ambaye nilikuwa simfahamu. Mwisho ikawa kama wote tumeshughulikiwa na wengine walikaa vitini kwaajili ya kuhudumiwa.


Niliinua simu yangu aina ya blakiberi niliyohongwa na kumjulisha dalingi wangu kuwa niko tayari na kuwa aje alipe tuondoke, kwa kawaida anaijua saluni hiyo kwani hiyo haikuwa mara ya kwanza, lakini kwa vile siku ile nilijimwaga sana kila mmoja alikuwa na hamu ya kumuona huyo buzi ni wa aina gani, alikuja mzee Yule na gari yake ya kifahari aina ya mark tu saluni grandi alipoteremka  aliingia mojakwamoja saluni na  nilimkimbilia kwa busu na mdeko wa nguvu “hai hani karibu umekuja nchukua eh njoo basi hani unlipie kisha ndo tuondoke”, jambo la kushangaza siku ile ni kuwa baba Yule katika hali isiyokuwa kawaida yake alikuwa kama ananitaaliza, au kunishushua kwa lugha za kitanga, Busu langu la siku ile lilikuwa pia limechanganyika na ishara ya kuwaonyesha kuwa huyu nitakayembusu ndiye kama vile alivyofanya mtume mmoja wa Bwana Yesu aliyeitwa Yuda Iskariote, lakini kama nilivyokugusia awali mwitikio wa shuga dady Yule ulikuwa kama amepigwa ganzi na ghafla mama Yule kimbaumbau alisimama kama afande  na kuanza kuteremsha matusi mazito sana  yakielekea kwa baba Yule  huku akilalamika kuwa watoto wamefukuzwa ada wameshindwa kwenda shule, nyumbani tunashindia dagaa na maharage tu kumbe wewe unajengea Malaya zako, kila mmoja alikuwa anashangaa na idadi ya watu ilianza kuongezeka pale saluni matusi yalimwagika kama mvua na hatimaye nikageukiwa miye na  yalimwagikia upande wangu  na nilipojaribu kujibu huku nikiwa nashangaa nilipokea mkong’oto mkali nikiambiwa Malaya wewe firauni mkubwa nikiambiwa ukome wewe kuchukua waume za watu nilishangaa mama huyu niliyekuwa naye saluni inakuwaje ana mamlaka kubwa kiasi hiki ndipo akili ilianza kunijia kuwa huku ndio kufumaniwa, Viungo vilinilegea kipondo kile kilipelekea kuchaniwa nguo  kiasi cha kuwa uchi, watu niliokuwa nao saluni walianza kupata majibu kuwa kumbe mwenye mali halisi alikuwa ni mwanamke Yule nilizomewa kama paka mwizi, ilikuwa ni aibu ya mwaka siwezi kusahau jamani  umbeya wa saluni bwana kumbe nilikuwa najimwaga kwa mwenye mali, wanaume za watu shoga nimekoma, unataka kujua yaliishije we mbeya sana mijimacho ka chura mbona ulipoacha kunyonya maziwa ya mamako mi sijakuuliza? Si uliacha bila kuambiwa sasa ulitaka niendelee kusumbua nyumba za watu mkong’oto ule ulikuwa kama zile stori za betina na zena katika magazeti ya sani zamani. kwa sasa nimeamua kujishughulisha na shughuli ndogondogo za kibiashara, nimeachana na maisha ya kupenda dezo kumbe bure ni gharama.

Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
0718990796
0784394550

Nikaalikwa Kama Mtoto wa Waziri

Mimi ni kijana wa umri wa miaka 34. Malezi na makuzi yangu yalikuwa ni ya wale wazazi ambao kwa siku hizi wangeitwa machekibobu, hawa ni wazazi ambao wanataka kujionyesha  kwa watu wengine kwamba  wao ni watu wenye fedha, waliotoka kwenye familia bora, waliosoma sana  ingawa sio kweli kwa hiyo name nilikuwa mtu wa aina hiyo mpaka niulipofunzwa na dunia.

Kwa ujumla ni kama nilifundishwa kujikataa kwamba siyo mimi na nilimudu sana kujikataa kwani katika kukua kwangu name nimekuwa mtu wa kujikweza mwaka 2000 ni kiwa nimemaliza masomo katika chuo cha biashara nilipata kibarua kwenye ofisi binafsi katika eneo la viwanda vingunguti nilianza kazi hapo nikiwa kama karani wa kawaida tu wa kutumwa shughuli za hapa na pale kujaza fomu za hesabu za fedha na mengine ya aina hiyo


Wakati nikiwapo hapo kazini nilikutana na msichana mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi kampuni ya jirani, nilikutana na msichana huytu wakati wa chakula cha mchana Lunch hapo eneo la viwanda. Kwa keli nilimpenda sana ghafla, yaani jicho la kwanza. Lakini Mungu si Athumani naye alionekana kunipenda ghafla pia, tulijikuta tukiwa marafiki baada ya mimi kumuanza ingawa kiuoga uoga kwani alikuwa mzuri sana na pia alikuwa anamiliki usafiri aina ya Rav4 ya milango mitatu, nilipochokoza alikubali kirahisi tofauti na nilivyotarajia.
 Kama kawaida yangu katika kujitambulisha mimi nilijitambulisha kwa  kujilambisha ujiko wa ajabu sana, mimi ni mwenyeji wa Tanga  na baba yangu anajuana na mtu mmoja mkubwa serikalini ambaye hadi sasa ni waziri. Badala ya kusema ukweli kuhusu baba yangu ambaye kwa maisha ya kichekibobu kama yangu alikuwa amesha chalala sana nilimtaja mkubwa huyo,


Yule binti aliniamini na huko nyumbani alitangaza bila shaka kwamba amepata mtu ampendaye ambaye baba yake ni mtu Fulani, siku hiyo binti alinialika niende nyumbani kwao kwaajili ya chakula cha mchana ilikuwa ni jumapili, nilijitahidi sana hadi nikamudu kukodi gari ya rafiki yangu kwa shilingi 40,000 ili niendenalo mwenyewe kule wajue kwamba nina gari unajua kitu gani kilitokea?


Nilipofika nyumbani kwao Yule binti nilimkuta mama yake, baba yake alikuwa amefariki zamani, lakini pia nilimkuta mtu mwengine, Hebu otea alikuwa nani? Alikuwa ni baba yangu, Nilibabaika sana  na kujiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu nilipigwa na butwaa kwa muda na baba baye pia, nilimsalimia mama wa binti yuile na baadaye kumsalimia baba na kumuuliza uko huku? Baba alisema nashangaa nawe unaijua familia hii Mama Lewisi tulikuwa naye kazini zamani. Siku nyingi sijamtembelea leo ndiyo nimeamua kuja kumwona….” Yuel mama mkwe wangu mtarajiwa aliuliza kwani mnajuana? Baba alisema huyu ni mwanangu wa kwanza” Halafu palizuka ukimya Yule mama kwaajili ya kuua soo alinikaribisha lakini ghafla Yule binti alikuwa amebadilika hakuwa na furaha tena.


Tulikula, lakini katika hali ya undavaundava tu, tulipomaliza  kula sikutaka kukaa zaidi kwani nilijua kuwa binti Yule na mama yake walikuwa wakinisanifu sana, du kutoka kuwa mtoto wa waziri hadi kuwa mtoto wa mzee aliyechezea maisha siku za nyuma, mbaya zaidi ni kuwa baba alikuwa amefika pale kwa nia  ya kuomba msaada, Niliaga nikimwacha baba akiendelea kupiga mabomu yake. Nilikuwa na uhakika kuwa baba aliambiwa ishu zangu zote, kwani jioni alinitembelea kwangu na kuniambia kwamba nimejisanifu sana kwa kujifanya mtoto wa waziri Unataka niendelee kukusimulia? Unataka kujua kuwa niliendelea na urafiki na Yule demu au La au nilitoa pua yangu kwa mama mkwe mtarajiwa? Hivi kichwa chako kiko sawasawa?

Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye hekima 
Rev. Innocent Mkombozi Kamote
e- mail ikamote@ yahoo.com
0718990796
0784394550

Wakurugenzi Wakaniita!

Sikumbuki tarehe wala mwezi lakini ilikuwa mwaka wa 1990 wakati huo nilikuwa nimeachishwa kazi katika kiwanda kimoja cha viatu, kilichokuwa barabara ya Pugu siku hizi Nyerere, nilikuwa nafanya kazi pale kama mlinzi mwaka huo ndio nilipata skendo na kuachishwa kazi


Nikawa nahangaika kutafuta kazi mjini, Nilifanikiwa mwaka huohuo kukutana na mtu ambaye alisoma na ndugu yangu, huyu Bwana aliamua kunisaidia kupata kazi mahali, aliponiuliza kuhusu elimu yangu nilimwambia nimemaliza kidato cha sita, ingawa ukweli ni kwamba nimesihia darasa la saba, Alinifanyia mpango nikapata kazi kwenye kiwanda kimoja hapohapo barabara ya Nyerere. Nilitafuta vyeti vya bandia  kutoka kwa rafiki yangu ambaye wakati huo alikuwa chuo kikuu, niliajiriwa kama karani waupokeaji wa mali ghafi na udhiinishaji wa  utokaji wa bidhaa, ilikuwa ni nafasi kubwa sana hata kwa mtu wa kidato cha sita, hata hivyo kwa sababu ilikuwa ni kazi yenye kuhitaji tu maelekezoili mtu kumudu kuifanya  niliielewa  kwa kiasi.

Bahati mbaya mwezi wa kwanza tu wa kazi, nikaanza kwa unoko sana, nilikuwa najifanya najua na nikawa nawazibia watu riziki zao, ili nipendwe na wenye kampuni, Kumbe katika unoko huo huo ndio ungeniponza, taarifa za kwamba mimi ni darasa la saba  na niliwahi kupata skendo zilifika pale kazini, Siku  hiyo nafika kazini kama kawaida, nikaitwa kwa mkurugenzi. Nikajua kuwa ninaenda kumwagiwa misifa kutokana na utendaji wangu wa kazi, kufika mkurugenzi akaniambaia, “tulikuajiri tukiamini kwamba kila ulilolisema kwetu lina ukweli, Hebu hasa jina lako na kiwango chako cha elimu na wapi uliwahi kufanya kazi kabla ya kuja hapa”

Nilihisi moyo ukianza kudunda kwa kasi na kwa nguvu, Nilijikaza na kusema  sijafanya kazi popote, tangu nimemaliza masomo ya kidato cha sita mwaka juzi, na jina langu ndilo hili ninalotumia, Wakurugenzi waliokuwa wamenizunguka walitabasamu kwa dharau hadi nikaogopa “Sasa bwana kuna mawili ama tukupeleke polisi sasa hivi kwa kudanganya na kufoji vyeti na jina la mtu  ambalo si lako au uondoke sasa hivi bila hata kipande cha karatasi yaani kama ulivyokuja, Hatuna haja ya kubishana nawe kwa sababu unaujua ukweli wote kuliko sisi”  Mkurugenzi mkuu alisema, Yule jamaa aliyenifanyia mpango wa kazi naye alikuwepo kwenye kikao kile, “Umeniangusha sana sikutegemea kabisa, kumbe hata sekondari hujakanyaga unakwenda kujipachika ufomu six wa bure! Kwa kweli hata tukionana njiani usinisalimie kabisa, Ungenisababishia kuharibu kazi yangu bure” Aliniambia.

Nilimwambia nimekosa nitaondoka sasa hivi na sitaki chochote, Nilijivuta polepole na kuanza kutoka nje, huko nje kumbe wafanya kazi wengine  walishapata  taarifa, kwa hiyo nilipokuwa nikikatiza mitaa walikuwa wakinicheka  na kunizomea, sikujibu chochote  kwa kweli ilikuwa fedheha  ya mwaka  unataka kujua nini kiliendelea we bwege nini? Mbona unapenda sana umbeya kwa taarifa yako sasa tukio hili lilinifanya niende kujisomea kwa machungu nikamaliza kidato cha sita na sasa nina stashahada ya uhasibu. Ilikuwa fedheha ambayo ililipa!. 

Fundisho na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
email. ikamote@yahoo.com
0784394550
0718990796

Jumapili, 2 Novemba 2014

Bible Geography (Jiografia ya inchi za Biblia)


UTANGULIZI:

I. Kulikuwa na wakati ni kwa uchache sana au nchi chache sana zilikuwa zinafahamika, kuliko zile zote zilizofunuliwa na Biblia.

II. Pamoja na matukio ya utaratibu wa kisasa wa:
A. Usafiri
B. Mawasiliano na
C. Vyombo vinavyobadilisha hali halisi ya asili - vimechunguzwa sana
D. Wakati wote neno la Mungu limethibitishwa kuwa kweli.

III. Biblia wakati wote ni sahihi na haina makosa ikiwa nipamoja na:
A. Maarifa -Ebr. 4:12.
B. Wakati
C. Ramani
D. Jedwali
E. Picha za rangi.

IV. Darasa hili litafurahia kwa ufahamu tutakaopata kwa kuzijua sehemu mbalimbali Kijiografia.

V. Ni kwa nini tunajifunza Jiografia ya Biblia? Ni kwa sababu tunaongeza ukubwa wa ufahamu wetu juu ya Biblia.

A. Kama ukisikia mji fulani wa zamani, ambao hujawahi kufika na kama Hujui ni wapi upo utakuwa na hamu ndogo tu kutaka kuelewa juu yake.

1. Inakuwa kinyume na kama umeyasikia mambo ya zamani yaliyowahi kuchukua nafasi pale - utakuwa na hamu sana.
B. Wengine wamelipuuzia sana somo hili la Jiographia ya Biblia matokeo yake Watu hawa wanajidanganya wenyewe na kushindwa kulifurahia neno la Mungu kama lilivyo, na kushindwa kuhubiri vizuri neno la Mungu.

C. Utakapojifunza somo hili utaiona Biblia ikiwa ina kuja kwako ikiwa hai:
1. Sio kozi ya vitu visivyo fahamika.
2. Utaona zile sehemu unazozisikia kama sio kweli, kuwa ni kweli.
D. Tujiandae vizuri kwa ajili ya kujifunza kozi hii, utakuwa na utajiri mkubwa
wa ufahamu, juu ya kitabu cha ajabu kuliko vyote duniani Biblia. 
  

SOMO LA KWANZA: ULIMWENGU WA AGANO LA KALE
 
I.                    Katika hali ya Kiroho Palestina au Kanaani ni Nchi ya Wakristo na Wayahudi vilevile
.
A. Matukio ya KiBiblia kihistoria yalichukua nafasi huko katika ulimwengu wa Agano la Kale.
1. Historia hiyo imeendelea kuwa changamoto kwa mwanadamu na ujumbe wa Mungu tuliopewa.
2. Mwanadamu ni kiumbe kinachohitaji Nafasi na Muda. Kwa hiyo Jiographia na Historia lazima viongezwe.
       PALESTINA MAHALI ILIPO, (ISRAELI)


 

       II. Palestina (Kanaani) ipo pembezoni mwa Bahari ya Mediteranea pwani ya mashaariki
A. Kuna njia au barabara nyingi za kibiashara kuingia na kutoka Afrika na Ulaya na Asia yote.
             B. Wakati wote umuhimu wa Palestina umejitokea.
1. Katika Agano la Kale.
2. Katika Agano Jipya.
C. Imekuwa na majirani ambao ni waarabu na kumekuwa na ugomvi wa muda mrefu kati ya    Taifa hili na Waarabu hivyo imekuwa ni sababu ya hofu ya Kule mashariki ya kati nzima.
D. Mataifa ya sasa ya mashariki ya kati yanajitahidi kujenga Nchi hiyo tasa kuwa atakufikia Nchi ijaayo "Maziwa na asali".
    III. Bahari Zinazopatikana Ulimwengu wa Agano la Kale.
A. Mediteranea: (Bahari kuu).
1. Kuna njia muhimu mno za baharini.
2. Ni mpaka wa Palestina kwa upande wa Magharibi, Yos.1:4.
3. Kuna bandari ya Joppa au Jaffa kwa sasa Tel Aviv.
B. Ghuba la Uajemi.
1. Ipo mashariki mwa Peninsula ya Uarabuni.
2. Waandishi wengi wanasema Bahari hii ya Ghuba ya Persia imesababishwa na mito miwili Tigris na Frati.
3. Mji wa Uru. Ulikuwa maili 100 kutoka katika kichwa cha hii bahari hapo zamani.
C. Bahari ya Kaspiani.
1. Bahari kubwa kabisa ulimwenguni iliyozungukwa na Nchi kavu.
2. Maji yake ni ya chumvi.
IV. Bahari ya Shamu Au Bahari Nyekundu.
A. Maji mengi yaliyo katika ufa wa bonde Yordani.
B. Ni mpaka kati ya Africa na Uarabuni.
C. Imezungukwa pande zote na Jangwa
V. Bahari Nyeusi.
A. Ni mpaka kati ya Ulaya na Asia.
B. Haionekani popote katika Agano la Kale.
VI. Bahari Ufi (Chumvi)
A. Bahari hii ni bahari ambayo maji yake yako chini sana.
B. Pia imeitwa
1. Bahari ya Chumvi, Mwa. 14:3.
2. Bahari ya Araba, Kum. 3:17.
3. Bahari ya Mashariki, Yoeli 2:20.
Mito Muhimu ni Mitano.
I. Tigris
A. Jina lingine unaitwa Hidekeli, Mwa.2:14.
B. Unatokea kwenye miinuko ya Armenia katika Asia ndogo na kuishia katika Bahari ya Ghuba la Persia.
C. Wakati wa zamani umuhimu wa miji ya Assyria ya Ashuru na Ninawi ilikuwa ukingoni mwa mto huu.
II. Frati
A. Chanzo chake ni mlima Taurus
III. Orente
A. Unaanzia Lebanon milimani unaishia Bahari ya Mediteranea.
IV. Mto Nili
A. Unaanzia Afrika mashariki katika ziwa Victoria au Nyanza mpaka Bahari ya
Mediteranea Misri.
B. Mto ulioleta ustaarabu wa Misri.
C. Wamisri waliufikiria mto huu kuwa Mungu.
V. Yordani
A. Ni mto mkubwa zaidi kule Palestina (Israeli)
B. Unaanzia katika mlima Hermon na kuishia Bahari mfu kwa kupitia Ziwa Galilaya hapo ndipo inapopotelea kwa jumla.
C. Wakati mwingine ulijulikana kama mto wa Jangwani, Amo. 6:14; Yos. 12:2, Yoh. 3:23.
VI. Majina matano ya Nchi ya Israeli.
A. Palestina
B. Kanaani
C. Ahadi
D. Maziwa na Asali
E. Takatifu.
Milima Mikubwa.
I.. Ararati- 14,000 fts kileleni 17, 000 fts.
A. Mahali ambapo safina ya Nuhu ilipotua baada ya Gharika, Mwa. 8:4.
B. Upo mashariki mwa Nchi ya Armenia kati ya Kaspiani na Bahari Nyeusi.
C. Jina lingine kufuatana historia kuitwa Mlima wa Nuhu.
II. Zagros: 9000 FTS.
A. Ni safu za milima mashariki mwa mto Tigris unatokea kaskazini kuenda kusini 4
B. Zamani ulikuwa ni mpaka wa Ashuru na Umedi.
III. Taurus: 12,250 fts.
A. Jina lingine ni Fedha - madini inayopatikana.
B. Kaskazini mwa mji wa Tarso.
IV. Lebanoni (Milima) - 10,200 ft. urefu.
A. Milima hii inafanywa na maendelezo ya Taurus.
V. Mlima Hermon - Kilele.
A. Maendelezo ya safu za milima ya Anti-Lebanoni uliyo upande wa pili wa miti Lebanoni.
VI. Mlima Sinai.
A. Upo kusini katika Peninsula ya Sinai kati ya mfereji wa Suez na Ghuba la Agaba.
B. Hapa mdipo Musa alipopokea sheria kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kut.20 ff)

SOMO LA PILI
Utangulizi:
I. Tumekwisha elezea mambo huhimu katika ulimwengu wa Agano la Kale.
A. Miili mikubwa ya maji - Bahari.
B. Mito.
C. Milima.
II. Sasa na tuendelee kuangalia Nchi Jinsi zilivyokuwa zinaonekana.
A. Hizi ni sehemu zinazoleta kumbukumbu tunapozisikia.
B. Ni sehemu zilizoleta utaratibu kama tujuavyo.
1. Zilikuwa na watu maarufu.
2. Vilevile matukio makubwa yaliyotendeka huko.
3. Baadhi yake Mungu alizitumia kukamilisha kusudi lake la milele, Efe. 3:10 -11.
III. Tupo hapa sasa ni kwa sababu ya matukio yaliyochukua nafasi katika nchi hizo katika maelezo ya miaka mingi iliyopita.
IV. Utakapoendelea kukua na kuzifahamu nchi hizo basi utaongeza ufahamu mkubwa katika kujifunza Biblia
Mwilli:
I. Historia fupi juu ya Mataifa.
A. Historia inagawanyika asili yake kama ilivyo Sayansi.
1. Wengine walishikiria ustaraabu wa Mesopotamia sasa Irag.
2. Wengine walifiria ni Misri ya zamani.
3. Bado wengine kudai kuwa ustaarabu huu ni kutokea mashariki ya mbali kama ndiko asili ya mwanadamu.
II. Mpangilio wa Mataifa.
A. Yaliyotokana na wana watatu wa Nuhu, Mwa. 10.
1. Yapheti - Mataifa 7
2. Hamu - Mataifa 4, Mwa. 10:1.
3. Shemu - Mataifa 5
B. Yaphet: (mst. 2-5).
1. Gomeri - Indo-Ulaya.
2. Magogu - Scyilians (Kas./Mash. Bahari Kaspiani)
3. Madai - Umedi (Kusini ya Kaspian)
4. Yavani - Ugriki (Mwisho wa kusini Balkan Peninsula)
5. Tubali - Haifahamiki.
6. Mesheki - Haifahamiki.
7. Tirasi - Thracians (Kati ya Uyanani na Bahari Nyeusi pwani)
C. Hamu: Ungua (mst. 6-14)
1. Kushi - Ethiopia.
2. Misri - (Mizraim) - Misri
3. Putu - Libya.
4. Kanaani - Palestina (Israeli - Uyahudi)
D. Shemu: Jina (mst. 21-31)
1. Elamu - Waelamu (Kasi ya Uajemi na Mash. ya Bahari)
2. Ashuru - Assyria (Kusi Magh - Asia)
3. Arfaksadi - Ukalidayo (Tigrisi na Ufrati chini)
4. Ludi - Lyalia (Magh - Asia ndogo)
5. Aramu - Shemu (kati ya Ashuru na Kanani)
III. Nchi kubwa za Kibilia ni Tatu.
A. Armenia - Nchi ya zamani ambapo safina ilitua, 2 Fal. 19:37; Isa. 37:38.
B. Mede - Mungu aliwatumia watu hawa kutimiza maandiko juu ya maandishi ukutani 2 Fal. 17:6; 18 :11; Dan. 5:25-31; 6:28.
C. Ujemi - Ujemi na Umedi - ndizo zilizofuata kutawala dunia. Dan. 2:36-39; 7:5; 8:3; 11:2; Est. 1:3.
1. Nchi zilizowahi kutawala dunia yote kila moja kwa wakati mmoja.
a. Misri.
b. Ashuru.
c. Alexander wa Makedonia, (Ulaya).
d. Babeli.
e. Umedi na Uajemi.
f. Rumi.
2. Dira ya mwelekeo wa dunia:

Kaskazini
Magharibi
Mashariki
Kusini
D. Duniani kuna Mabara 7.
1. Afrika.
2. Marekani ya Kaskazini.
3. Marekani ya Kusini.
4. Asia.
5. Australia
6. Antartica
7. Ulaya.
E. Kuna bahari kubwa 4 Duniani.
1. Uhindi.
2. Arctic.
3. Pacific.
4. Atlantic.
F. Historia ya Agano la Kale inachukua mabara mawili tu kati ya Saba.
1. Afrika - Kaskazini Afrika (Kas. na Kas. Mash.)
2. Asia - Asia Ndogo.
G. Historia ya Agano Jipya iko katika mabara 3 kati ya saba.
1. Afrika - Afrika Kaskazini.
2. Asia - Asia Ndogo
3. Ulaya.
Nchi zilizokuwa wazi ni 5.
1. Sumer - Sehemu ya zamani ya Babeli, Mwa. 14:1; 11:31, Dan. 1:1
2. Ashuru - Kati ya Babeli, Armenia, na Umedi - Tigri Mto, Mwa. 2:14; 25:18 Yoh. 1:2.
3. Mesopotamia - sehemu ya wazi kati Tigris na Ufrati, Mwa. 24:7 -10
4. Elamu - Kaskazini ya Ghuba ya Uajemi, Mwa. 10:23.
5. Arabu - Peninsula kati ya Afrika na Asia, 1 Fal. 10 :15; 2 Nya.17:11, Ez. 27:21.
Nchi zilizo zunguka mashariki mwa Bahari ya Mediterania 6.
1. Asia ndogo - ilijumuisha falme:
a. Lidia.
b. Ashuru
c. Hiti
2. Shemu mji mkuu ni Damaskus kwa Kiebrania - Aram. Ilikuwa katika Ashuru na kanaani, 2 Sam. 8:6; 15:8; Ez. 17:16; Lk. 2:2; Mdo. 15:23, 41.
3. Kanaani - Mabaki ya chini ya meditranea pwani na Bonde la Yordani.
a. Mabaki ya wasio wayahudi wote, Mwa. 10:18 -20; Hes. 13:29; Josh. 11:3.
4. Phoeniki - Mstali mwemba Kaskazini mwa mlima Karmel walizungumza Semitic lugha.
a. Miji yake mikubwa ni Tiro na Sidoni.
5. Philistina - Jina hili linatoka Palestina kuonyesha Nchi walipewa Waisrael Yoe.3:4; Ebr. 11: 9; Zak. 2:12.
6. Misri - Nyumba ya utumwa kwa Israel.
a. Nchi yenye rutuba kando ya mto Nili, Mw.12:10; 39:1; 42:1; 47:28; 29; Mdo. 7:23, 24.

Nchi ya Palestina au Kanani.
I. Kanaani ni Jina lililotumika katika A.K. kwa nchi hiyo iliyokuwa katikati ya Yordani na Mediterania kusini ilipakana na jagwa.
II. Kwa usahihi zaidi tunapozungumzia Palestina twaweza kuwa tunazungumzia mataifa mawili.
A. Nchi ya Wafilisti.
B. Nchi ziliyokaliwa na makabila 12 ya Israeli.
III. Migawanyo Yake ya Asili.
A. Uwanda wa Pwani.
B. Ukanda wa katikati.
C. Bonde la Yordani.
D. Ukanda wa mashariki.
E. Ukanda wa Jangwa (Mbele ya mashariki).
IV. Maji Yalivyo Katika Nchi ya Palestina.
A. Mto Yordani
B. Ziwa Hula.
C. Bahari ya Galilaya
D. Bahari Iliyokufa.
E. Mito mingine mingi midogo midogo.
V. Milima Ya Palestina.
A. Tabor - Debora na Baraka walitayarisha …. Wakanaani.
B. Gilboa - Sauli na Jonathani walikufa vitani na Wafilsti.
C. Karmeli - Nabii Eliya aliwashinda manabii na makuhani wa Baali.
D. Ebal na Gerzimu-
1. Baada ya wana Waisraeli kushinda Yoshua …. Amoc na Musa
2. Baraka zilitangazwa - kutoka mlima Gelizimu.
3. Laana zilingazwa kutoka mlima Ebal, Kum. 11:29.
4. Mwanamke Msamaria, Yosh. 8:33-35, Yoh. 4:1
E. Mlima Sayuni - kwa kawaida Sayuni lilikuwa ni Jina la Yerusalemu mji mtakatifu.
1. Mashariki mwa Yerusalemu Mlima Olivet au Olivus. (Mlima wa Mizeituni).
F. Mlima Hermon.
G. Mlima Gileadi - Gidioni alikusanya Jeshi (Waa. 7:3)
H. Mlima Nebo
1. Mahali Musa alipotazama nchi Ahadi.
2. Uko katika nchi ya Wamoabu.
3. Mahali alipofia Musa.
VI. Njia kuu 3.
A. Njia ya Pwani.
B. Njia za majini.
C. Njia kuu za wafalme.
MABABA WALIVYOSAFIRI.
Utangulizi:
I. Maelezo ya mapema kabisa ya Biblia kuhusu Maisha ya Mwanadamu.
II. Adamu maana yake "Mwanadamu"
III. Biblia inaeleza kuhusu mwanadamu juu mambo kadhaa.
A. Kuumbwa kwake.
B. Kuanguka
C. Gharika ambapo vyote hivi vimeelezwa juu ya mwamadamu kama ni jumla.
D. Kuitwa kwa Abraham (Ibrahimu na Uzao wake)
E. Rehema inaonyeshwa kwa watu kadhaa.
1. Rahabu, Yos. 2.
2. Ruth, Ruth. 1
3. Watu wa Ninawi, Yona.
IV. Lakini Mungu alitoa ufunuo kwa watu wake Israeli.
Mwili:
I. Kulikuwa na safari Tatu Kwa Mababa Watatu.
A. Ibrahimu
B. Isaka.
C. Yakobo.

II. Ibrahimu:
A. Historia ya Israeli inaanza na Ibrahimu.
B. Akaitwa " Baba wa Imani" Aliondoka Uru wa Ukaldayo kwenda asikokujua.
1. Uru wa Ukaldayo - (Mwa. 11:27-32)
2. Kutoka Uru mpaka Harani. (Mw. 11:27-12:4) Mesopotamia Kusinindipo palipokuwa nyumbani Ibrahimu.
3. Kanani - Mwa. 12:5-9 - Ibrahimu na mkewe Sara waliondolewa kutoka Harani. Kutoka harani waliambatana na Lutu Binamu yake- kwenda Kanani iliyokuwa chini ya Misri.
4. Misri, Mwa. 12:10-20.
a. Ibrahimu alienda kutafuta chakula.
b. Ibrahimu aliongopa - Sara ni dada yake.
c. Ibrahimu alifukuzwa na Farao baada ya kugundua.
d. Ibrahimu alirudi Betheli.
5. Hebroni - Mwa. 13:5-18.
a. Ibrahimu na binamu yake Lutu walitengana.
b. Lutu alichagua - Sodoma bonde ambalo lilileta baadaye maangamizi ya Sodoma na Gomora.
1. Lilikuwa ni bonde zuri kwa mifugo.
c. Ibrahimu alichukua sehemu za miinuko kuzunguka Hebroni.
1. Hapo ndipo alipokufa mkewe Sara.
2. Alinunua mahali pa kumzika mkewe kwa Efroni Mhiti.
3. Daudi alianza kutawala akiwa Mfalme katika Hebron.
4. Uasi mbaya wa Absolomu ulianzaa hapa.
5. Kwa mara ya pili Ibrahimu aliambiwa hapa kuwa ni "Rafiki" Mungu.
6. Vita vya wafalme, Mwa. 14.
7. Beersheba, Mwa. 20 - 25.
a. Baada ya maangamizi ya Sodoma na Gomora.
b. Hapa Ibrahimu aliungana na Abmeleki wa Gerali (Mwa. 26: 26-33).
c. Katika siku za za Ahabu na Jezebeli, Eliya alipata kutoa sadaka hapa baada ya ushindi wake dhidi ya manabii wa Baali, (1 Fal. 19:3-4).
8. Moria - Mwa. 22.
a. Mahali alipotolewa Isaka kama sadaka.
b. Mahali palipokuwa pametulia mbali na mikiki ya shughuli za watu.
c. Mapokeo hudai Ibrahimu alikuwa katika "Nchi ya Moria".
III. Safari za Isaka.
A. Maisha ya Isaka katika Biblia yameelezwa kwa ufupi zaidi kuliko mababa wengine.
1. Beer-Lahai-Rol (Mwa. 16:7, 13; 14; 24:62)
a. Hapa ni mahali Malaika wa Bwana alipomtokea Hajiri kijakazi wa Sara (Mama yake Isaka,) wakati Hajiri anamkimbia mkuu wake.
b. Yawezekana Isaka aliishi hapo.
2. Gerari (Mwa. 26:1-16)
a. Ni mahali ambapo Isaka alipata makaribisho mazuri kutoka kwa Mfalme wa Gerali Abimeleki.
b. Isaka aliongopa kuwa Rebeka ni Dada yake, mst. 7-11.
3. Rehobothi (Mwa. 26:23-33)
a. Isaka alifanya mapatano ya Amani na Wafilisti chini ya mfalme wao Abimeleki.
b. Mungu anarudia Ahadi yake juu ya Ibrahimu.
4. Hebroni (Mwa. 35:27).
a. Maisha yake ya mwisho aliyatumia akiwa HEBRONI.
b. Ni mahali alipofia na kuzikwa na wanawe Yakobo na Esau katika pango lilelile alilonunua Ibrahimu (makapela).
IV. Safari za Yakobo.
A. Jina lingene la Yakobo ni Isaraeli.
B. Baba wa makabila 12 ya Israeli.
MAISHA YAKE YAKO KAMA IFUATAVYO KWA UFUPI.
I. BEER -SHEBA: (Mwa. 26:33 - 27-46).
A. Yeye na pacha mwenzie walizaliwa (Esau)
B. Alidanganya na kupata baraka za uzaliwa wa kwanza watu aliowadanganya watu wawili nao ni:
1. Isaka.
2. Esau.
C. Alikimbilia Harani - Baada ya kugundulika kwa mjomba wake Labani.
II. BETHELI: (Mwa. 28).
A. Alikimbia kulipizwa kisasi na Esau.
B. Alipewa na Mungu maono ya kurudia kwa amani katika nchi aliyozaliwa.
C. Aliona ngazi kutoka Mbinguni.
D. Ndama kama mungu iliwekwa na Yeroboam I kuepusha watu kwenda Yerusalem hekaluni, Ufalme wa Isaraeli ulipogawanyika (Yuda na Israeli).
III. HARANI: (Mwa. 29:30).
A. Alitumia muda mwingi hapo.
1. Alitumia miaka 7 kwa msichana mzuri Raheli badala yake alipewa Lea ambaye hakuwa anavutiwa naye.
2. Alifanya miaka mingine 7 kwa ajili ya Raheli tena.
3. Alitumia maisha yake Harani kwa kuishi na mjomba wake Labani.
IV. MAHANAIMU: (Mwa. 32:1).

A. Alitiwa moyo na malaika baada ya kuogopa kulipizwa kisasi na nduguye aliye mkosea miaka ishirini mapema.
B. Ni mahali ambapo baadaye mwana wa Sauli Ishi - Bosheth alitawala, wakati Daudi akitawala Yuda kutoka Hebroni.
C. Ni mahali ambapo kilitokea kifo cha mateso cha mtoto mzuri sana wa Daudi Absalomu.
V. PENUELI (Mwa. 32:22 - 32).
A. Penueli maana yake ni "Sura ya Mungu."
B. Alipambana na Malaika, Yakobo alifanywa kilema na kupewa baraka.
VI. SUKOTHI (Mwa. 33:17).
A. Yakobo alipatana na nduguye Esau.
B. Alijenga madhabahu kwa ajili ya furaha ya kupatana na nduguye.
VII. SHEKEMU - (Mwa. 33:18-34:31).
A. Shekemu kwa sasa inajulikana kama - TELL-BALATA.
B. Dina binti Yakobo alibakwa na Shekemu.
C. Simeon na Lawi waliwaua wanaume wote wa Shekemu.
VIII. BETHELI: (Mwa. 35:1-15)
A. Jina lingine - "Nyumba ya Mungu."
B. Yakobo alirudia agano lake na Mungu.
IX. EFRATH.
A. Jina lingeni ni Bethlemu (Mwa. 35:16-21).
B. Maili 5 kusini ya Yerusalemu.
C. Ndipo alipokufa Raheli wakati anajifungua mtoto Benjamini mtoto wa mwisho
wa Yakobo.
X. HEBRON - (Mwa.35:27).
A. Ni mahali ambapo Ibrahimu na Isaka waliwahi kukaa.
B. Mahali ambapo Yusufu mwana mpendwa wa Yakobo aliuzwa na ndugu zake Utumwani kwa wa Ishimaili.
C. Kulikuwa na njia kutoka Damascus kwenda Misri.
XI. KULE MISRI (Mwa. 45-49)
A. Alikwenda kwa mwaliko wa Yusufu.
B. Yusufu alikuwa waziri mkuu wa Misri.
C. Aliishi katika Gosheni kule Misri - Sehemu ndogo lakini yenye rutuba sana.
D. Mwili wa Yakobo uliowekwa dawa ulihifadhiwa na kuchukuliwa kwenda kuzikwa Hebroni - Makapela.

SOMO LA TATU. MISRI NCHI YA UTUMWA.
I. Majina matano ya nchi.
A. Kemu - Jina la zamanil ililoonekana kumbukumbu za zamani.
B. Nchi ya Hamu - (Zab. 78; 51; 105:23; 106:22)
C. Mizraimu -Mwa. 12:10-14 ff ; 13:1.
D. Rahabu - (Kiburi au Jeuri) Zab. 87:4; 87:10.
E. Misri - Jina la sasa Jina iliyoitwa na Wayunani halikutumiwa kamwe hapo daima.
II. Historia yake ya nyuma.
A. Misri ni sehemu ya bonde refu la mto Nile.
B. Bonde hilo limegawanyika katika sehemu mbili au wilaya mbili zilizoitwa "Nomes".
C. Kila sehemu ilikuwa na mji mkuu wake ambao ulikuwa na hekalu la mungu kienyeji.
D. Lugha yao ni ile ya Kiarabu.
E. Farao wa kwanza kutawala pande zote mbili aliitwa Menesi na ndiye aliyeiunganisha nchi.
F. Wamisri walipenda sana desturi zilizofanya ustaarabu wao udumu. Kama maandishi yaliyo jumuisha maeneo matatu.
1. Logographic - kilaalama iliwakilisha neno.
2. Syllabic - Herufi alama iliwakilisha hefu.
3. Alphabetic - alama iliwakilisha sauti moja.
4. Mambo ya dini - miungu.
5. Katika ufalme wa 3 kulikuwa na kawaida ya kufanya "RE" kuwa ni mungu jua - Ilichukua miaka mingi kwa Wamisri. miungu mingi - kusherehekea Mungu mmoja.
6. Wafalme wa Misri walijulikana kwa jina la Farao.
III. JIOGRAFIA YA MISRI.
A. Mgawanyo wa nchi katika nyakati mbili za Wamisri zamani ulijulikana na Kufikiriwa vitu kamili. Historia yake ilianza wakati sehemu mbili zilipounganishwa na mfalme Menesi mwanzilishi wa ufalme kukawa na kuvaa taji mbili kuonyesha kuwa anatawala pande zote mbili za Misri.
1. Misri ya Kaskazini (Juu) ilikuwa mahali mto unapoingia baharini na ilikuwa pembetatu.
2. Misri ya Kusini (Chini) Bonde jembamba la mto Nile.
B. Misri inaanzia kwanza kwenye maanguko ya mto Nile kusini mwa Jimbo la Nubia.
C. Kwa upande mwingine wa mto Nile ni jangwa.
1. Jangwa Shuri linaloendelea mpaka Palestina ya kusini.
D. Ukubwa wa Misri ni 9,600 sq. mile kwa 13,000 sq mile.
E. Mipaka ya Misri.
1. Jangwa la Sahara - Magharibi.
2. Bahari ya Mediteranea - Kaskazini.
3. Nubia - Kusini.
4. Bahari Nyekundu - Mashariki na jangwa.
IV. MTO MKUBWA NILE.
A. Ukweli kuhusu mto Nile.
1. Ni mto mrefu kabisa katika Africa.
2. Unaweza kuwa na urefu wa maili 4,000.
B. Chanzo chake.
1. Ziwa Victoria lina mchango mkubwa katika chanzo cha mto Nile.
2. Vilevile kuna vianzo vyake toka kwenye maziwa ya Kas. Mashariki na Afrika ya kati.
a. Nile Nyeupe -mto wenyewe wa asili.
b. Sobati - Karibu na asili ya mto yenyewe.
c. Nile Nyeusi - inatokea maili 200 Khartoum.
d. Nile Blue - katika Ziwa Tana kule Ethiopia inayoungana na Nile Nyeupe kule Khartoum.
e. Unapoingilia Nile blue hakuna mwingine unaoingia katika mdomo huo.
C. Midomo ya Nile.
1. Nyakati za zamani kulikuwa na midomo 7 nyakati za saa iko midomo5 ya usafiri wa wazi Baharini.
2. Kuna milango mikuu miwili.
a. MASHARIKI - au Pelusiac.
b. MAGHARIBI - au Canaopic.
3. Gosheni - ilikuwa ni makao ya Waisraeli ilikuwa Kusini – Mashariki ya tawi la Pelusiac la Nile.
D. Zawadi ya Mto Nile.
1. Mara moja kwa mwaka hufurika.
a. Ndiyo chanzo cha maisha kule Misri.
b. Mahali popote maji yanapofika palikuwa na Neema.
c. Huwa mavuno tele na maji huwapo.
2. Mafuliko haya ya kila mwaka huanza 25/6 na yanadumu kwa muda wa miezi 3 maji kuwa juu ya nchi.
3. Mafuliko husababishwa na mvua za kila mwaka kutokea Afrika ya kati.
V. Sehemu muhimu katika Nchi ya Misri.
A. Misri ya Juu.
1. Memphis - Maili 10 kutoka Kairo ya sasa.
a. Mji mkuu wa zamani wa Misri.
b. Kuna maeneo muhimu ya Ki-Historia.
2. Heliopolis - au "ON"
a. Kama maili 20 kutoka Memphis.
b. Kiti cha kuabudia "mungu jua".
3. Rameses:
a. Mji katika jimbo la Gosheni.
b. Yawezekana mji huu ulijengwa na watumwa wa Ki-Israeli (Kut. 1:11).
c. Ulikuwa ni mji mkuu kati ya falme.
d. Pia uliitwa Zoan.
4. Pelusium:
a. Mashariki mwa mdomo wa mto Nile.
b. Maili za Mashariki mwa Bandari ya Saidi.
c. Iliaminiwa kuwa mji wa dhambi katika Biblia.
5. Alexandria:
a. Ulianzishwa na Alexander Mkuu mwaka 332 K.K.
b. Wayunani wengi waliozungumza Kiyahudi waliishi hapa.
c. Ndipo walilpotokea LXX (Septuagint).
1. Katika mji yote iliyoorodheshwa hapa ni Alexandria uliobakia hadi leo.
2. Ni moja ya maajabu saba ya dunia.
B. Misri ya Chini:
1. Thebes:
a. Pia unaitwa "NO" AU Hakuna au NO -AMON.
b. Mji mkuu wa Misri ya juu kwa muda mrefu.
c. Kulikuwa na hekalu la Amoni.

SOMO LA NNE: WANA WA ISRAEL. NCHI WALIZOSAFIRI NA SEHEMU WALIZOZUNGUKA.
Utangalizi:

I. Historia ya Misri inaanza pale ufalme wa juu na chini ulipoungana chini ya NAR - MER au MENES, farao wa kwanza wa Misri iliyoungana.
A. Mfalme alikuwa na Taji mbili kumaanisha kuwa ni mtawala wa Misri mbili.
II. Kwa kiebrania Misri ilijulikana kwa jina la MIZRAIM.
III. Yawezekana Waisraeli walianza kuondoka Misri mnamo mwaka wa 1225 -1447 BC.
IV. MEMPHIS, ni mji mkuu wa zamani wa Misri ambao sasa unajulikana ni KAIRO.
V. Mji maalumu wa kidini ulikuwani Heliopoli au "ON" kule Misri Jina hilo lilijulikana kama mji wa jua ulikuwa maalumu kwa mungu jua "RE".
VI. RAAMSES au RAMESES.
A. Mji wa kuanzia safari ya Waisraeli.
B. Ulikuwa katika jimbo la Gosheni.
C. Ulijengwa na watumwa wa Ki-Israeli.
D. Palikukuwa ni mahali Waisraeli walipoanzia safari kwenda Kanaani, (Kut. 12:37). Mwili:
I. Nyikani Walimozunguka Zunguka Waisrael.
A. Nyikani hapa yaweza kuwa inaelezea kila namba ya majangwa au nyika katika kuzunguka nchi za Biblia.
B. Kuna maana tofauti ya neno "nyika" kama lilivyo neno "jangwa" kuwa na maana tofauti za majangwa au nyika.
1. MIDBA - Nchi ya Nyika, (Mith. 21:19).
2. YESHIMONI - Nchi ya Ukame (Kum. 32:10).
3. ARABA - Nchi ya Chumvi, (Ayu. 39:6).
4. ISIYYAH - Nchi kavu isiyo zaa chochote, (Ayu. 30:3).
5. TOHU - Nyika msimo na njia, (Ayu. 12:24).
6. EREMIA -Ukame.
7. EREMO -Jangwa na Ukame.
II. Majangwa Waliyozunguka.
A. Mkono ya Sinai na Majangwa Yake.
1. Walitumia karibu miaka 39 au 38 kwa kuzungukazunguka eneo hili.
2. Kumbuka lipo kati ya Ghuba ya SUEZ na Ghuba ya Agaba katika mikono miwili ya Bahari ya Shamu au Nyekundu.
3. Ilikuwa na maeneo tofauti mawili.
a. TAMBARALE - (Table - Land) - Chokaa, kame jangwa.
b. MILIMANI au miinuko - liliitwa kwa jina lingine
Horeb au Sinai - kulikuwa na milima ya aina mbili
1. Kas- Magh - 679 fts.
2. Kundi la kati 7519 fts Mlima Sinai.
II. Maeneo ya Jangwa Au Nyikani.
A. Maeneo matano ya safari ya wana wa Israeli ni majangwa.
1. Shuri - Mashariki mwa Gosheni maana yake ni “Ukuta"
2. Zini - Kus/Magh mwa Bahari mfu lipo katika nchi ya Edom.
Iliyoitwa wana wa Israeli walinung'unika, Hes. 27:14, wapelelezi alitumiwa Kanaani, Hes. 13:21.
3. Sini - Iipo kati ya Elimu na mlima Sinai - Magharibi ya mkono mashariki kati ya mkono ya Sinai.
4. Parani - Ipo kati ya mpaka wa Araba na Ghuba ya Agaba, Hes. 10:12.
5. Etham - Kusini mwa jangwa la Shuri ni sehemu ya mkono ya ya Sinai.
B. Hizi nisehemu chache muhimu katika safari ya wana wa Israeli.
1. Zilikuwa sehemu ya Kaskazini na kati ya Peninsula.
2. Eneo hilo ni tambarale.
3. Kulikuwa na vyanzo vichache sana vya maji hata mto Wad- El- Arish (Mto wa Misri) unakauka karibu kwa mwaka mzima.
C. Mlima Sinai:
1. Unahusiana na jina la sehemu ya Sinai.
2. Horebu ipo sehemu ya kusini ya Peninsula ya Sinai.
3. Panajulikana kuwa ndipo mahali Musa alipopokea Sheria.
4. Kilele chake kimeitwa na wasomi wa Biblia kwa Kiarabu
"JEBEL MUSA" yaani "Mlima wa Musa."
D. ARABA:
1. Kutoka kusini mwishoni mwa Bahari mfu mpaka Ghuba ya Agaba.
2. Waamaleki waliishi hapa na kuishambulia Israeli, (Kum. 25:17 19; Kut.17:8-16. wana Esau, Mwa. 36:16, 12.
III. Nchi Ya Edom:
A. Mipaka yake.
1. Kusini mash, ya Palestina katika jimbo la Kusini mwa Bahari Mfu, kati ya mto Zeledi na ghuba ya Agaba.
2. Asili ya milima hiyo ya mashariki mwa Araba ilipewa jina Ki-Biblia "MILIMA YA SEIRI."
B. Majina ya Nchi yalikuwa Matatu (Mwa. 36:8, 20).
1. Esau au Edomu - Mwekundu.
2. Seiri - (Hairy) - Nywele nyingi.
3. Idumea- ilitumika katika A.J. kati ya Uyunani - Herode alikuwa Mfalme wa Idumea.
C. Miji mikubwa mitatu ya Edomu.
1. Bozra - ulikuwa mji mkuu hasa katika A.K.
2. Sela - uliitwa Petro (Jiwe) na Wayunani - ulikuja kuwa mji mkuu baadaye.
3. Ezioni - Geberi:
a. Kusini mwa Edomu katika Ghuba la Agaba.
b. Njia kuu za kibiashara zilikuwa huku.
c. Njia hizi zisababishwa na Biashara ya Misri na Bonde la Frati.
d. Sulemani alitumia mji huu kama Bandari.
D. Sura ya Nchi.
1. Magh - kulikuwa na miinuko ya mawe chokaa.
2. Mash - kulikuwa na Slop ya mawe ya chokaa mpaka jangwa.
3. Kati - Nchi ya milima na aina mbalimbali za mawe zaidi ni mawe ya chokaa.
E. Mwisho wa Taifa hili la Edomu.
1. Historia hii ya Waedomu ni ya kuvutia sana
a. Esau nduguye Yakobo alishinda na kuteka nchi.
2. Waisrael (Yakobo) walipotoka Misri Waedomu waliwakatalia wasipite katika nchi yao, Hes.20:17-21.
3. Daudi na Sulemani baadaye waliiunganisha nchi hii na miliki yao.
4. Kufuatia kipindi cha Ufalme uliogawanyika kati ya Israel na Yuda (Kas. na Kus.) Edomu ilifanywa sehemu ya Yuda.
5. Edomu iliasi na kujitawala wenyewe.
6. Babeli (Nebukadneza) alipoishambula Palestina Edomu ilimsaidia (Kitabu cha Obadia).
7. Wakati wa Makabayo Idumea au Wa-Edomu walilazimishwa kuungana tena na kuwa chini ya sheria za Wayahudi.
8. Haipo katika historia ya sasa kufuatia maangamizi ya Yerusalemu ya 1770. B.K. Mat.24:1-35.
a. Hakuna nchi inayoitwa Edomu leo.
IV. Njia na Vituo Vya Wana Wa Israeli - Kuzunguka Kwao Jangwani.
A. Kwa nini walikwenda kwa njia waliyoiendea? Kwa nini wasipite moja kwa moja kwenye pwani ya Mediteranea? Na kuvuka mto Wadi-el-Arishi (Mto wa Misri) na kutembea mpaka Kanaani? Kuna sababu 4 tunazoweza kuzielewa.
1. Ulikuwa ni mpango wa Mungu. (Kut.13:17, 18).
a. Wafilisti wangepigana na Israel … Kwa hiyo wangekata tamaa.
2. Njia ya Pwani ilikuwa na ngome nzito ya Askari wa maadui.
3. Jangwani ilikuwa imethibitishwa kwa safari.
4. Hawakuwa tayari kukabiliana na Wafilisti.
B. Njia zinazofanya kuwa Historia.
1. Rameses, Mahali walipoanzia katika Goshen, (Mwa.37:27; Kut. 12:37)
2. Sakothi - Israel walijiunganisha, (Kut. 12:37 -3:19) Hapa walikuwa wanaingia katika Jangwa la Ethamu.
3. Kwenye Pembe ya Jangwa la Ethamu.
4. Pi - Hahirothi - (karibu na Baal-Sefoni), Kut. 14:4-15:22
a. Farao aliwafuata alitaka kuwarudisha Misri.
b. Muujiza wa Mungu uliigawanya Bahari ya Shamu.
c. Vituo hivi vinne vyote vilikuwa katika nchi ya Misri na juu ya Bahari ya Reeds (Shamu).
d. Sasa katika Jangwa la Shuri.
5. Maji machungu ya Mara yaligeuzwa kuwa matamu, (Kut. 15:22-26)
6. Elimu:
a. Palikuwa na miti ya mitende 70.
b. Chemichemi ya visima 12, (Kut. 15:27). Sasa katika Jangwa la la Sini.
7. Walipofika hapa Sini watu walimnung'unikia Mungu na Musa na Mungu aliwalisha watu.
a. Mikate-manna.
b. Kwale-(Kut. 16:2-36)
8. Refidimu kwa sababu ya mateto mahali hapo Musa lipaita MASA NA MERIBA, (Kut. 17:7).
a. Maji kutoka katika mwamba.
b. Vita dhidi ya Wa-Amaleki.
c. Mikono ya Munsa ilitengenezwa na watu wawili.
1. Haruni.
2. Huri.
d. Mungu aliahidi kufuta kabisa Amaleki juu ya nchi.
e. Musa aliambiwa aandike kwa ajili ya Yoshua.
f. Musa alijenga madhabahu akaiita Yehova - Nisi maana yake Bwana ameapa kutakuwa na vita na Amaleki kizazi hadi kizazi Kut. 17:15-16.
9. Sinai, (Kut. 19:1-40:37)
a. Walawi wote na Hes, 1:1-10:11.
b. Sura ya 19- 24-Sheria zinatolewa.
c. Sura ya 25-31-Kielelezo cha Hema.
d. Sura ya 32- 34-Ibada ya sanamu.
e. Sura ya 35-40-Ujenzi wa Hema.
* Sasa tunaacha Sinai na kwenda kwenye kichwa cha Kadesh-Barnea.
10. Tabera (Unguza) Hes. 11:1-3.
a. Watu walinung'unika.
b. Moto wa Bwana uliwala baadhi yao.
11. Kibroth - Hataava - (Kaburi la Tamaa)
a. Wote waliotamani Misri Mungu aliwapiga hapa.
12. Haserothi-Hes. 11:4-34.
a. Miriamu na Haruni walimnenea vibaya Musa kwa sababu ya mkewe Mkushi.
b. Miriamu alipingwa na ukoma, Mst.10.
c. Haruni aliomba msamaha, Mst. 11.
* Sasa wanaingia katika Jangwa la Parani, Hes.12:16.
13. Kutoka Kadeshi- Barnea.
a. Wapelelezi 12 waliingia Kanaani.
1. Wapelelezi 10 waliaminiwa, (Hes.13:1-14:45; 13:26.
* Katika kipindi hiki walipita Jangwa la Sini mpaka Hamathi.
14. Kuna vituo 12 visivyofahamika.
a. Kwa miaka 38 walikuwa wakizunguka Jangwani.
b. Hes. 15-19. Biblia imenyamaza.
c. Vituo 12 vimeorodheshwa katika, Hes. 33:18-38.
1. Wanapewa maagizo na mwelekeo, Hes. 15.
2. Maasi yanatokea, Hes. 16-KoraDathanina Abiramu.
3. Fimbo ya Haruni inachipuka, Hes. 17:11, kuwa ushahidi
4. Kufuatana na makuhani na walawi, Hes. 18.
5. Maagizo ya mtamba mwekundu, Hes. 19.
15. Kadesh - Barnea: Hes. 20:1-20. (katika Jangwa la Zini.)
a. Mahali alipofia Mariamu, (dada yake Musa.)
b. Mahali Musa alipopiga Mwamba.
c. Baadhi ya walionungu'unika waliteketezwa kwa moto, Hes. 11:1-3.
d. Waedomu wanawazuia Israel wasipite katika nchi yao, Hes. 20:21.
16. Walifika mlima Hori.
a. Mahali alipofia Haruni.
b. Vita dhidi ya Wakaanani.
c. Watu walikufa moyo kwa sababu ya ile njia, Hes. 21:4.
1. Walitamani kurudi Misri.
2. Hawakutaka kufa jangwani.
3. Walikinahiwa na chakula kutoka kwa Bwana (Kware na mikatemaalumu Mana).
4. Nyoka wa moto waliwauma Mungu akamwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba.
5. Walirudi tena Bahari ya Shamu (Agaba).
17. Elathi:
a. Watu waliumwa na kufa kwa nyoka za moto, Hes. 21:4, 9; Kum.2:8.
18. Esion- Gebari: Kutoka hapa walianza kuizunguka Nchi ya Edomu mashariki mwa mto Jordani, Kum. 28.
19. Bonde la Moabu: Hes. 21:10-22, Mfululizo wa matukio tutayaona.
a. Musa na Haruni-wanadai kuwapa watu maji, Hes. 20:8-13.
b. Waliwaita watu enyi waasi, Hes. 20:10.
c. Baadala ya kuuambia mwamba Musa anaupiga, 20:11.
d. Bonde la Zeredi - Musa na Haruni hawakumtukuza Mungu.
e. Ng'ambo ya Arnoni.
1. Maji yaliitwa Meriba - Wana wa Israeli waliteta na Bwana.
f. Beer. Wanaomba ruhusa kwa Edomu kupita katika nchi yao.
g. Mattaha- Edomu anataka kupigana na Israeli.
h. Israel walibembeleza sana, hatuta kunywa maji yako wala mifugo yetu, mst. 18, bado Edomu hakuwa ruhusu.
i. Bonde la Moabu, Hes. 20:20; Yos. 4:19.
1. Sihoni - Mfalme wa Wa-Amori, Hes. 20:21-23 walishindwa na Israel Og - mfalme wa Bashani.
2. Uasi na manung'uniko, Hes. 22:1-26:1.
3. Watu walihesabiwa, Hes. 26:2 -26:65.
4. Sheria mbalimbali, Hes. 27:1-31:2.
5. Vita na Wamidiani, 31:3-54.
6. Marudio na mgawanyo wa Nchi, Hes. 32:1-36:13.
7. Kifo cha Musa, Kum. 34:1; Yos.1:2.
8. Kazi ya Yoshua, Yos. 1:3-18.
9. Kuipeleleza Nchi, Yos. 2:1-24.
10. Maji ya mto Yordani yalitindika. Miili 2 ya maji iliyowa kutindika.
a. Bahari ya Shamu.
b. Mto Yordani, Yos. 3:18.
j. Gilgali: Vita katika Kanaani mwisho wa safari ushindi uanaanza.
1. Vita katika Kanaani vinaanza.
2. Mwisho wa Safari (Kituo cha Mwisho).
3. Ushindi unaanza kupatikana.

SOMO LA TANO. USHINDI WA KANAANI.
UTANGULIZI:
I. Makabila yaliyokuwa Kanaani wakati wa Mababa na waliopaswa kushindwa na kutoka 20 mbele ya Israel, Kumb. 7:8 - sura ya 8.
A. Mhiti - Uria - 2 Sam.11:1-27; Heth, Mwa.10:15.
B. Mgirgashi.
C. Mwamori.
D. Mkanaani.
E. Mperizi - Vijijini.
F. Mhivi.
G. Myebusi - Wakaani walioshi Yerusalemu.
II. Makabila au mataifa yaliyokuwa yakiishi wakati Waisrael walipokuwa wanateka Kaanani.
A. Moabu - Mwa. 19:30-37 - Wajukuu wa Luthu.
1. Waliabudu. Kemoshi - Kuchoma watoto hai katika moto.
B. Ammoni - Hawa nao ni wale walitokana na Luthu, Mwa. 19:30- 38.
1. Mungu wao alikuwa. Moleki au Mikom.
III. Ushindi wa Kanaani ulikuwa kabla ya wana wa Israeli kufika katika kituo chao cha Mwisho.
A. Kituo chao cha mwisho kilikuwa - Gilgali.
B. Ilikuwa washinde mashariki ya Yordani kabla ya kuingia katika Nchi yenyewe.
C. Walipoiona Nchi waliigawanya miongoni mwa makabila.
Mwili:
I. Ushindi wa Mashariki, Hes. 31:54.
A. Vita dhidi ya Sihoni wa Gileadi - Hes. 21:21-31.
1. Mfalme wa Amorite (Mwamori) alikuwa mpinzani sana wa Israel.
2. Amorite (Waamori) waliwafukuza mbali Wamoabu.
3. Kulikuwa na makundi mawili ya Waamorite.
a. Geliadi -Sihoni.
b. Bashani - OG.
4. Kundi la Gileadi - lilikuwa kati ya Arnoni na Jabbok.
5. Mji wao mkuu ulikuwa - Hesh. - Boni au Eseboni.
B. Vita dhidi ya OG wa Bashani, Hes. 21:32- 35.
1. Kaskazini ya mto - Yamuku.
2. Mgawanyo wa Waamori.
3. Mtawala jina lake OG.
4. Vita vilipiganiwa Edrei.
5. Nchi ilisherehekea vitu vifuatavyo.
a. Ng'ombe.
b. Kondoo.
c. Mti wa ulaya unaoshi mufa mrefu.
C. Vita dhidi ya Moabu na Midiani, Hes. 22:31-37.
1. Moabu na midiani waliungana kijeshi, 22:4.
2. Moabu ilikuwepo kati ya Zeredi na Arnoni.
3. Midiani ilikuwa mbele ya kona ya Jangwa la Arabia.
4. Mji mkubwa - Kir-Moabu.
a. Wamoabu - Luthu - Binti mkubwa, Mwa.19:30-37.
b. Waamoni - Luthu - Binti mdogo, Mwa.19:30-37.
II. Magharibi (Kuyasukumia mbali), Yos. 1:1 - 11:23.
A. Vita vya katikati, Yos. 3 - 9.
1. Gilgali - kituo muhimu.
2. Yeriko - (mji wa mwezi au mji wa mitende).
3. Ai. - walishindwa kwa sababu ya dhambi ya Akani.
4. Bethel - (Ai waliamini kuwa ni kutuo chao cha kijeshi.
5. Milima Gerizimu na mlima Nebo, (Kum. 27:11 ff, Yos. 8:32).
B. Vita vya Kusini. (Yos.10:1- 43)
1. Kuanguka kwa Yeriko, Ai, Amani na Gibeoni kuwa Kanaani.
2. Ushirikiano ulioundwa ilikupigana na Israeli, Yosh. 10:5, 15-26.
3. Ushirikiano wa kumshambulia Gibeon.
4. Yoshua alikwenda kwa nguvu na kushambulia usiku, Yos. 12:9-24.
C. Vita vya Kaskazini, Yos.11:1-23.
1. Muungano mwengine wafalme uliongoozwa na Yabini mfalme wa Hazori uliundwa kupigana na Israeli.
2. Yoshua alikwenda kwa njia ya Bonde la Yordani akashambulia.
3. Yoshua aliuchoma mji wa Hazori na akaiacha miji mingine.
a. Kwa nini Hazor, Yoshua aliuchoma moto? Malme wake alikuwa mwanzilishi wa muungano wa kuipiga vita Israeli.
4. Ushindi kimsingi ulikuwa umefikiwa lakini ghasia ziliendelea, Yos. 11:15- 23.
III. Mgawanyo wa Nchi kati ya Makabila 12.
A. Mashariki ya Yordani- Makabila 2 na nusu, Yos. 13.
B. Magharibi ya Yordani - Makabila 9 na nusu, Yos. 14-19.
C. Miji ya Makimbilio sita.
1. Mtu aliye ua mtu.
2. Aliyeua bila kukusudia, Yos. 20.
3. Miji hiyo ilikuwa kama ifuatavyo.
a. Katika pande zote.
1. Upande wa Yordani Mashariki.
2. Upande wa Kusini.
3. Upande wa Kati.
4. Upande wa Kaskazini.
b. Yordani Mashariki, mst.8.
1. Bezeri - Rubeni.
2. Ramothi - Gadi.
3. Golani - Manase.
c. Magharibi ya Yordani, mst. 7.
1. Hebroni - Yuda.
2. Shekemu - nusu Manase.
3. Kadeshi - Naftali.
D. Miji ya Walawi, Yos. 21.
1. Ilikuwa 48, pamoja na miji 6 ya makimbilio.
2. Wastani ilikuwa miji 4 katika kila kabila.
E. Maelezo zaidi walivyokaa katika nchi, (mgawanyo wa nchi kufuatana na makabila).
1. Mashariki mwa mto Yordani yalipewa makabila 2 na nasu kukaa lakini ilikuwa wawasaidie waliobakia kushinda vita baadaye kurudia katika nchi yao, Yos. 22.
2. Makabila hayo yalikuwa:
a. Reubeni.
b. Gadi.
c. Nusu Manase.
3. Magharibi ya mto Yordani (Palestina halisi).
a. Kabila za kusini.
1. Yuda.
2. Simeon.
3. Benjamini.
4. Dani.
b. Kabila za kati kati.
1. Efraimu.
2. Nusu Manase.
3. Isakari.
c. Kabila za Kaskazini.
1. Asheri.
2. Zebuluni.
3. Naftali.



SOMO LA SITA. PALESTINA CHINI YA WAAMUZI.
Utangulizi:
I. Baada ya kifo cha Yoshua sehemu fulani ya Israeli walikuwa kawaida ya kujiingiza katika sanamu na kuabudu miungu kama walivyokuwa wanafanya majirani zao.
II. Tunajifunza katika historia kuwa Mungu aliwaokoa watu kutoka kwa maadui zao.
III. Mungu aliwainua viongozi ili kuwaokoa watu na wale waliokuwa wakiwatesa.
A. Viongozi hawa walijulikana kama waamuzi.
B. Walikuwa tofauti na wafalme waliokuwa wakiwaacha watoto wao kiti cha Ufalme.
Mwili:
I. Wakati wa maamuzi Israeli ilikuwa na vita vingi.
A. Vita kati yake na Mesopotamia - (Waa. 3:5-11).
1. Mwamuzi alikuwa Othnieli-Yos. 15:16-19; Waa. 3:9-10.
a. Ndugu yake Kalebu.
b. Amani ilikuwa miaka 40.
B. Vita na Wamoabu - (Waa. 3:12-30)
1. Mwamuzi alikuwa -Ehudi - kutoka kabila ya Benjamini Amani ilidumu miaka 80.
C. Vita na Wafilisti- Maa. 4- 5.
2. Mwamuzi au mwokozi - Shamgari (Maa. 3:31).
D. Vita na Wakanaani (Maa. 4-5)
1. Mwamuzi au mwokozi - Yabini - Yos. 11:1
E. Vita na Wakaanani tena - Maa. 4:4 ff.
1. Mwamuzi au mwokozi - Debora mwanamke pekee mwamuzi alisaidiwa na Baraka, Waam. 4:10, Debora na Baraka walifanya Israeli kukaa katika Bonde la Yezerel bila hofu ya Wakanani.
F. Vita na Wamidiani - Waa. 6-9, mwamuzi ni Gideoni.
1. Gideoni na watu 300 alilishinda jeshi kubwa la Wamidiani.
G. Vita wa - Ammoni - Wajukuu wa Luthu, (Maa. 10-11).
1. Mwamuzi alikuwa ni Yeftha.
H. Vita na Wafilisti tena: Maa. 13-16.
1. Mwamuzi alikuwa ni Samsoni.
I. Mwamuzi wa mwisho kati ya wengi wa Israeli alikuwa Samueli.
1. Israeli walitaka kuwa na mfalme kama majirani zao-mataifa, 1 Sam. 8:1 ff.
2. Kitu hiki hakikumpendeza Samweli hata Mungu hakupendezwa na madai yao.
II. Baada ya waamuzi wote kupita na Israeli kudai wawe na mfalme, bonde vita viliendelea moja baada ya vingine.
A. Sauli ndiye aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Israeli iliyo moja. (Monarch)
1. Alipakwa mafuta kule Ramatahaimu au Ramali kwa siri nyumbani kwa Samweli.
2. Alitokea katika kabila dogo sana la Benjamini.
3. Gibea- kulikuwa ni myumbani kwa Sauli na makao makuu ya mfalme wa kwanza wa Israeli.
4. Uko maili 4 kaskazini mwa Yerusalemu.
5. Mizpeh - Sauli alipokelewa kama mfalme.
6. Gilgali - kwa mara ya kwanza Sauli alipokilewa kama mfalme wa makabila yote ya Israeli.
III. Vita vya Sauli, (1 Sam. 11-15).
A. Vita vilikuwa kati ya mataifa yafuatayo:
1. Waamoni - 1 Sam. 11.
2. Vita vya kwanza na Wafilisti - (1 Sam. 13-14.)
3. Vita na wamoabu - 1 Sam. 14:47.
4. Vita na wa Edomu - 1 Sam. 14:47.
5. Vita na Shemu, 1 Sam. 14:47.
6. Vita na Waamaleki, 1 Sam.14:48 - 15:35, hasira za Samweli ziliinuka kwa sababu Sauli alimwacha Agagi mfalme wa Waamaleki aliwaacha ng'ombe wazuri, 1 Sam. 14:22-23.
7. Vita vya pili na Wafilisti, (1 Sam. 17:18).
B. Sauli aliuawa katika vita na Wafilisti pamoja na wana wake watatu akiwemo Yonathani katika mlima Giboa.
IV. Ufalme wa Daudi na Sulemani.
A. Daudi alipokuwa mfalme wa Israeli walikuwa na wajibu na miliki 6000 maili za mraba.
B. Aliacha maili 60,000 za mraba kwa mwanawe Sulemani.
C. Utawala wa Daudi juu ya Yuda, 1 Sam. 1-4.
1. Baada ya kifo cha Sauli, Daudi aliondoka kwenye mji wake wa ukimbizini wa Ziklag na kwenda Hebroni kule aliko tangazwa kuwa mfalme wa Yuda.
2. Wakati huo mwana wa Sauli Ish - Boshesh alikuwa anatawala makabila ya Kasikazini.
3. Mapigano yalizuka kati ya majemedari wa Daudi na Ish-boshesh. Aliuawa na watu wake pamoja na Jemedali wake hivyo Daudi akawa Mfalme wa Israeli yote.
V. Ushindi wa Daudi kwa Mataifa - Kigeni. (2 Sam.8:11).
A. Aliteka mji wa Wa-yebusi wa Yerusalemu akaufanya makao yake makuu.
B. Kisha alishinda Kaskazini ya Palestina (Kanani) miji aliyoteka Kaskazini ni kama ifutatavyo.
1. Megido.
2. Taanaki.
3. Beth-Sheani.
C. Aliteka tena nchi zifuatazo upande wa Mashariki ya Yordani.
1. Edomu, 2 Sam. 8:13-14.
2. Moabu, 2 Sam. 8:2.
3. Amoni, 2 Sam. 10-11.
D. Yawezekana hata wafilisti na wenyeji wa Aramu - Dameski walimtumikia Daudi, 2 Sam. 8:5, 6.
E. Aliteka Soba, 2 Sam. 3-5.
VI. Matatizo mbalimbali aliyoyampata Daudi baada ya Dhambi yake ya uzinzi na kumua Uria Mhiti, 2 Sam. 12-20; 24.
A. Uasia wa mwanawe Absalom.
1. Alimua nduguye kwa mama mwingine Amnoni.
2. Amnoni alilala na (kumbaka) Tamaria dadaye Absalomu.
B. Absalomu alijitangaza kuwa mfalme kule Hebroni wa Israeli kinyume na Baba yake Daudi.
C. Daudi alikimbia toka Jerusalemu mpaka mashariki ya Yordani, 2 Sam. 8:18.
D. Vita vilipingwa kati ya Daudi na Absalomu na Absalomu akauawa kule Mahanaimu, Daudi alirudi madarakani kwa huzuni ya kumpoteza mwanawe Absalome, 2 Sam. 17:24, 18:9-15.
1. Uasi wa Sheba, 2 Sam.20.

a. Aliuawa na mwanamke ili kuuokoa mji na Yoabu, mst.21.
2. Tauni - 2 Sam. 24:15-25.
3. Mwisho wa utawala wa Daudi, 1 Fal. 1:2, 1 Nya. 22-29.
a. Mtoto wake Adonija alijaribu kutwa kwa nguvu ufalme.
b. Daudi alifuata ushari wa Bath-Sheba na Nathani.
c. Sulemani akawa amepakwa mafuta kule Gihoni upande wa mashariki wa ukuta wa Yerusalemu.
VII. Utawala wa Sulemani.
A. Utawala wake wa mapema alikwenda Gibeoni pale Mungu aliko mwahidia Hekima kwa utawala wake kwa Israeli, 1 Fal. 3:4-15.
B. Haraka utawala wake ulijulikana na kusambaa katka majimbo 12, 1 Fal. 4:7-19
C. Yuda hauonekani, pengine ilitawaliwa moja kwa moja toka Yerusalemu.
D. Mipaka ya utawala wake ilikuwa kama ifuatavyo.
1. Kutoka mto Frati - hadi kwenye mpaka Misri, 1 Fal. 4:21.
2. Edomu na Moabu - vilevile waliwakilishwa kabila zao kule Yerusalemu chini ya Sulemoni.
E. Vyanzo vya Biashara.
1. Aliendeleza Israeli katika Biashara.
2. Kulikuwa na Amani.
3. Alijenga Hekalu, 2 Nya. 2.
4. Usafiri ulikuwa rahisi sana.
F. Uhusiano na Nchi zingine.
1. Alioa wake wa Kimisri, 1 Fal. 11:1-3.
2. Alioa wake Tiro na mataifa mengine.
3. Kutembelewa na malkia wa Sheba n.k.
G. Miaka ya mwisho ya utawala wa Sulemani.
1. Kumbuka Sulemani aliistawisha Israeli kiuchumi na Kisiasa.
H. Mambo yalibadirika na kuwa kinyume.
1. Misri wali mmuweka Farao kini asijekuwa rafiki wa Sulemani Hadadi. aliasi kabisa. 1 Fal. 11:14-22.
2. Rezoni - akachukua Damascus na kugoma kulipia kodi kwa utawala wa Sulemani baada ya kifo chake, alitawala Rehoboamu, mst. 4, 1 FF.
VIII. Mataizo yalijitokeza kutoka ndani.
A. Yeroboamu - aliyekuwa mkuu wa kukusanya, 1 Fal. 11:40. Kodi aliasi (alitoka kwa Yusufu Efraimu na Manase) aliitwa na watu wake yaani makabila 10 - Israeli au Kaskazini.
B. Rehoboamu - akabakiwa na makabila 2 urefu wa kusini (Yuda).


SOMO LA SABA ASIA NDOGO
UTANGULIZI:

A. Tumekwisha shugulika na eneo la ndani na kuzunguka hali ilivyokuwa na Mgawanyo wa nchi ya Palestina.
B. Katika somo hili tutarudisha mawazo yetu tena katika sehemu ya Asia ndogo.
C. Umuhimu wa eneo hili wakati mwingine umeisha sahaulika.
1. Ni sehemu ya Historia ya Biblia.
2. Ni sehemu muhimu mno hasa kwa Historia ya Agano Jipya.
I. Asia ndogo.
A. Maelezo.
1. Ina ukubwa wa maili Square, 156,000.
2. Wakati wa Biblia ijulikana kuwa Asia ndogo.
3. Wakati wa sasa hujulikana - Turkey- Uturuki
4. Mji mkuu wake wa zamani - Efeso.
5. Mji mkuu wake wa sasa ni Ankara.
a. Mlima Ararati unapatikana huko.
b. Milima ya Taurus pia ipo Asia Ndogo.
B. Mipaka yake (Asia Ndogo).
1. Kaskazini - Bahari Nyeusi.
2. Magharibi - Bahari ya Aegean.
3. Kusini - Bahari ya Mediterranea.
4. Mashariki:
a. Armeni -Urusi.
b. Mesopotamia - Iraq na Iran.
c. Shemu - Shemu.
C. Ilivyotumika Ki-Biblia.
1. Wakati wa A.J. Asia neno hili halikuwa na maana kama ilivyo leo.
2. Halikuwa kwa maana ya Asia yote bali kwa kawaida ni ndogo kama tujuavyo.
3. Hata hivyo sio Asia ndogo yote ilifikiriwa kuwa ni Asia lakini karibu
yote ilikuwa hivyo.
4. Weka mbali Mashariki ya mbali katika akili zako, weka au fikiria mashariki ya karibu.
II. Asia Ndogo kwa eneo.
A. Maeneo upande wa Bahari Nyeusi (Black Sea).
1. Ponto (Pontus) - chini ya Bahari Nyeusi katika Kasikazini, Mashariki
2. Ilipakana ma Armenia.
3. Kusini kulikuwa na Kapadokia.
4. Magharibi - Paphalagoni.
5. Baadaye lilikuja kuwa jimbo la Rumi.
a. Mdo. 2:9
b. Mdo. 18:2.
c. 1 Pet. 1:1.
6. Paphalagoni ulikuwa kati ya Ponto na Bithinia haimo katika Biblia.
7. Bithinia ipo chini ya Bahari ya marmara pamoja na Paphlogia upande
wa Mashariki kusini kulikuwa na Mysia na Phrgia.

a. Bithinia una utajiri sana wa historia
1. Iliungana na Ponto mwaka 63 B.K. na katika mwaka 103 B.K. Pliny alikuwa ndiye Gavana wa Bithinia.
b. Mdo. 16:7; 1 Pet. 1:1.
c. Kulikuwa na miji maarufu miwili.
1. Nikomedia - mji mkuu wa ufalme wote wa mashariki. mkutano wa baraza lililoamriwa na Constantine mkuu mwaka 325 A.D. mkutano wa maridhiano.
B. Eneo la Bahari ya Aegeani (uk. 14: Atlasia ya Biblia):
1. Mysia - ilikuwa mashariki mwa bahari hii na Bithinia ilikuwa kaskazini na Lydia kusini na Galatia ilikuwa Mashariki.
a. Kutoka Troa mji katika Mysia Paulo aliweza kuiona Ulaya kwa mbali. Hapo ndipo Paulo alipopokea maono ya Makedoni Mdo. 16:7, 8.
b. Miji maarufu kule Mysia.
1. Pergamos.
2. Troa.
2. Lydia - wakati wa A. J. ulikuwa chini ya Rumi.
a. Miji muhimu iliyokuwapo kule Lydia ni 4.
1. Efeso.
2. Saidi
3. Thiyatira.
4. Filadelfia.
3. Kara huu ulikuwa kusini magharibi kabisa na Lydia kaskazini na Lycia Kusini, Mashariki.
a. Haionekani popote sehemu hii katika A. J.
b. Kulikuwa na mji muhimu Mileto, Mdo. 15-17.
C. Maeneo ya Bahari ya Mediterranean.
1. Lycia - ilikuwa Kusini ya Milima ya Taurusi.
a. Likuwa eneo dogo lakini lenye Rutuba sana.
b. Mdo. 27:5.
2. Pamfilia - Mashariki mwa kilikia magaharibi mwa kilikia kusini ya Pisidia.
a. Perga ya pamfilia ulikuwa mji wa kwanza kumsikia Paulo, Mdo. 2:10; 13:13; 14:24; 15:38; 27:5.
b. Miji maarufu ya eneo hili 2.
1. Perga.
2. Atalia.
3. Kilikia katika ya Pamfilia na Shemu Kusini ya kapadokia.
a. Ulikuwa maarufu kwa utengenezaji wa nguo za maonyoa ya ya mbuzi.
b. Mdo. 6:9; 15:23, 41; 21:39; 22:3; 23:34; 27:5- 6; 1:21.
c. Mji maarufu ni Tarso.
D. Eneo la Milki.
1. Kapadokia - Kusini mwa Ponto na kusini Mashaki ya Galatika.
a. Maarufu kwa:
1. Farasi.
2. Chuma.
3. Fedha.
b. Mdo. 2:9.
2. Galatia - ilitokea Kaskazini na kusini katikati ya mkono mashariki ya eneo la Aegeani.
a. Mdo. 16:6; 18:23; 1 Kor. 16:1; Gal. 1:2; 4:10; 1 Pet. 1:1.
b. Miji maarufu 5:
1. Ikonia.
2. Derbe.
3. Lystra.
4. Pisidia.
5. Antiokia.
3. Likaonia (Mdo. 14:1-23).
a. Ilikwa sehemu ya Galatia.
b. Ilikuwa ni wilaya pamoja na Ikonia, Derbea, na Listra.
4. Pisidia Jimbo pamoja na Pamfilia upande wa Kusini Frijia upande wa Kasikazini.
a. Mji wake mkuu ulikuwa Antiokia, Mdo. 13:14; 14:24.
b. Pamoja na Galatia pia.
5. Frigia sehemu ya juu kati ya Lidia na Mysia Galatia na jina la eneo nasia jimbo.
a. Mdo. 16:6; 18:23- Paulo alisafiri kupiti eneo hili.
b. Miji muhimu.
1. Laodikia
2. Hierapolis.
3. Kolosai.
III. Miji ya Asia ndogo katika kitabu cha Ufunuo.
A. Makanisa saba ya Asia.
1. Efeso - Ufu. 2:1 - ulikuwa Lidia.
2. Smirna - Ufu. 2:8 - ulikuwa Lidia.
3. Pergamo - Ufu. 2:12 - ulikuwa Mysia.
4. Thyatira - Ufu. 2:18 - ulikuwa Lidia
5. Sardia - Ufu.3:1 -aulikuwa Lidia.
6. Filadelfia - Ufu. 3:7- ulikuwa Lidia.
7. Laodiakia - Ufu. 3:14- ulikuwa Frijia.

SOMO LA NANE. NCHI YA PALESTINA AU KANANI.
Utangulizi:
1. Tutashughulika na Nchi za Ki-Biblia na katika mawazo ya watu ya kidini.
A. Matukio makubwa yaliyochukuwa nafasi katika nchi hizo.
B. Watu waarufu, mawazo yao yalivyokuwa.
2. Tutaendelea kuona nchi ya Palestina yenye ukumbwa wa eneo mraba maili 12,000
Mwili:
I. Mgawanyo wa Asili wa Palestina.
A. Sehemu ya mashariki au Tambarale.
1. Bashani:
a. Mashariki mwa Yordani.
b. Ipo futi 2000 kutoka usawa wa bahari.
c. Ilisifika kwa uzalishaji wa Ng'ombe na eneo lenye rutuba, Zab. 22:13, Yer. 50:19; Amo. 4:1,2; 1 Fal. 10:33, Isa. 2:13. Mik. 7:14.)
2. Gileadi.
a. Ilikuwa usawa wa bahari 2,631.
b. Ilizungukwa na miti maarufu kwa dawa ya marhamu. (Mwa. 37:25; 2 Fal.11:7; Yer. 9:26; 2 Thes. 2:2).
3. Moabu.
a. Futi 300 kutoka usawa wa Bahari (Hes. 22:1; I fal 11:7; Yer. 9:26; Ruth. 2:2.
b. Bonde la Yordani.
1. Kaisaria Filipi futi 1292.
2. Bahari Mfu.
4. Bonde la Yordani ni la kipekee.
a. Hakuna usafiri wowote katika mto huo.
b. Kuna joto la ajabu. (kali)
c. Sehemu zingine ni matope matope.
d. Wakati wa A.K. wanyama pori wengi waliishi katika bonde hili.
e. Hakuna mji mkubwa uliowahi kujengwa upande wa kulia wa bonde hili.
5. Maisha ya viumbe wa asili ni ya kipekee.
a. Kuna aina 30 ya samaki wanapatikana 16 hawapatikanipenginepo duniani.
b. Kuna aina 45 za ndege kati ya hizo 23 ni za kipee.
c. Kuna mimea 162 na miti kati ya hiyo mimea na miti 135 inapatikana katika Africa.
C. Eneo la kati la Palestina.
1. Ni eneo la milimamilima iliyotanda karibu eneo lote kutokea Kaskazini mpaka Kusini na miinuko na vilele virefu.
2. Maeneo halisi ya kimsingi.
a. Galilaya ya juu wastani wa futi 2800.
b. Galilaya ya chini wastani wa futi 1800.
c. Miinuko ya Nchi ya Efraimu (Samaria) futi 2800.
d. Yudea.
e. Negebu.
D. Eneo la uwanda wa kati.
1. Eneo la wazi la Sharoni.
a. Eneo lililo kati ya Jopa (Tel - Aviv) na Mlima Karmeli.
b. Sehemu iliyojulikana katika A. K. rutuba na amani (1 Nyak. 27:29; Isa. 35:2; Wim. 2:10).
2. Eneo la wazi la Esdraelon.
a. Eneo kubwa la wazi lenye rutuba.
b. Lipo kati ya Galilaya na Samaria.
c. Katika Biblia linajulikana kama eneo la Yezreeli.
d. Sehemu maarufu kwa miji na matukio kama:
1. Waamu. 4 mahali alipofia mfalme mwema wa Yuda, Yosia.
2. Alipokuwa anapigana na Wamisiri.
II. Namna gani maji yalivyo - Palestina.
A. Mto Yordani.
1. Unakwenda kama maili 120 kutoka kwenye chanzo chake mpaka mwisho wake Bahari mfu.
a. Upana wake ni 80 mpka 180 fts.
b. Kina chake 5fts - 12 fts.
c. Kuna vyazo vyake 4 ambavyo ni vikuu.
1. Mashariki 3.
2. Magharibi 1.
2. Maana ya jina "Yordani" ni "shuka chini", au "telemka" (kwenda upande wa chini.
a. Vyanzo cyake 4 ni vifuatavyo.
1. Ziwa Hula.
2. Mlima Hermoni.
3. Na vyanzo vingine viwili vilivyojitokeza maeneo ya mbele ya vyanzo hivi vilivyotangulia.
4. Ni mto mkubwa kabisa Palestina, (Mwa. 13:10; Yos. 3:15; Yer.49:19; Zab. 114:3; Mt. 3:6; Yoh. 10:40).
B. Maziwa mbalimbali.
1. Hula ukubwa wake maili 20 kwa 5 futi 7 kutoka usawa wa bahari kwa sasa waisraeli wamelikausha na wanatumia eneo hili kwa kilimo.
a. Majina mawili ya ziwa hili (wakati huo):
1. Meromu.
2. Huleh.
2. Galilaya.
a. Majina matatu zaidi ya ziwa au bahari hii.
1. Chinerethi.
2. Tiberia.
3. Genesareti.
b. Lipo chini ya Ziwa Hula.
c. Ni ziwa zuri urefu wake ni maili 13 upana 3-8.
d. Kuonekana kweke futi 696 chini ya bahari, (Lk. 5:1, Hes. 34: 11, Mt. 4:18; Mk. 4:39.)
e. Miji mingine 9 yenye zaidi ya wakazi 15,000 ilikuwepo kando ya ziwa hili pamoja na Kapemaumu, (Mk. 1:29; Mt. 9:9).
3. Bahari au ziwa mfu.
a. Majina mawili mengine.
1. Chumvi.
2. Asfati.
b. Kimsingi inaitwa Bahari baada ya kuitwa ziwa.
C. Mito vijito.
1. Mto Zeredi - unatengeneza mapka kati ya Edomo na Moabu.
a. Unaingia kusini mash. Ya Bahari Mfu (Hes. 21:12; Kum. 2:13)
2. Arnon - mpaka wa kazini wa Moabu.
a. Unaishi Kas, Katikati ya Bahari Mfu.
b. Unaanzia uarabuni (Hes. 21:13; Waa. 11:18; 2 Fal. 10:33.
3. Yabboki - unaangukia katika Mto Yordani unapitia kati ya Bahari Mfu na Galilaya Bahari.
a. Ulikuwa ni mpaka mfalme Sihoni (Gilead Kask.).
b. Ni mto huu karibu ambapo Yakobo alishindana na malaika (milele), (Mwa. 32:22; Kum. 2:37; Waa. 11:22).
4. Yarmuk - mpaka wa Kusini wa Bashani (Og maili 6 mwa Bahari yaGalilaya).
5. Magharibi ya Yordani maji yaendayo Mashariki.
a. Qelt - unakwenda katika Yordani Kas, kidogo ya Bahari Mfu.
b. Qumran - upo Kas, Magh, ya Bahari Mfu (Chumvi).
1. Mahari DSS ilipatikana.
6. Kidroni.
a. Unaanzia katika bonde la Yerusalemu na kwenda Bahari MfuKusini mwa Qumran.
b. Kuna wakati unakauka, (2 Sam. 15:23; 1 Fal. 15:13; 2 Nya.32: 4; Yoh. 18:1).
7. Mito inayokwenda Bahari ya Mediterranean.
a. Leontesi - unatokea Kusini kati ya milima ya Lebanon kwenda Magh, na kuingia Tiro (katika Shemu).
b. Kishoni - Unaanzia kati ya Mlima Tabor na Mlima Gilboa kwenda Magh. kupitia Bonde la Jezreel.
Debora na Sisera walimshinda Jabini, Waamuzi. 4:5.
8. Zefathah:
a. (2 Nyak. 14:9- 15). upo Magh. Mwa Bahari Mfu (Chumvi).
b. Wadia-el-arish.
1. Mto wa Misri.
2. Kusini mwa mpaka wa nchi ya Ahadi (Mwa. 15:18; Hes 34:5).
III. Njia kuu za usafiri - Palestina.
A. Njia za pwani.
B. Njia za majini
C. Njia za wafalme.



SOMO LA NANE. SEHEMU LA PILI PALESTINA:
Utangulizi:
I. Sehemu ya kwanza ya Jiografia ya Palestina tumeona.
A. Mgawanyo wa asili.
B. Maji - Bahari, Mito, Maziwa, Vijito.
C. Njia za usafiri.
II. Katika somo hili tutaona Palestina katika A.J.
Mwili:
I. Majimbo ya Palestina.
A. Yudea.
1. Likuwa katika makabila ya:
a. Yuda.
b. Benjamini.
c. Dani.
d. Simioni.
2. Mipaka yake ilikuwa kama ifuatavyo.
a. Mto Yordani na Bahari Mfu upande wa Mashariki.
b. Negebu upande wa Kusini.
c. Bahari ya Mediterranean - Magharibi.
d. Samaria upande wa Kaskazini, (Mt. 2:1; Yoh.4:3; Mdo. 2:9; 8:1; 11:29: Gal. 1:22).
B. Samaria:
1. Sehemu ya eneo hili kati ya Yudea na Galilaya.
2. Lilikaliwa na watu (mchanganyiko wa damu), (Wayahudi + Assyria) walidharauliwa sana na Wayahudi.
3. Walijenga hekalu lao wenyewe katika mlima Gerizimu katika mwaka 400 KK (2 Fal. 17:29; Lk. 10:33; Yoh. 4:9, 39, Mdo. 8:25).
C. Galilaya:
1. Eneo linalojumsha kutoka Bahari ya Galilaya mpaka Bahari ya Mediterranean Mashariki na Magharibi, vilevile kutoka Mlima Karmeli mpaka Lebanon Kaskazini na Kusini (Yos. 20:7; Mt. 2:22 Yoh. 2:1; Mdo. 1:11; 13:31).
2. Ilikuwa imegawanyika sehemu mbili.
a. Galilaya ya juu.
b. Galilaya ya chini.
D. Perea.
1. Neno hili maana yake ni "Mbele ya".
2. Inachukulia nchi iliyo mbele ya mashariki ya Jordani mpaka jangwa na kuendelea Kaskazini na Kusini kati ya Arnon na karibu na Mashariki ya Bahari Mfu (Chumvi).
3. Jina hili halilpatikani katika Biblia labda linachukuliwa katika, Mt. 19:1, pia Yoh. 1:28; Mk. 10:1- 33.
E. Deacapolos.
1. Latokana na maneno mawili ya kiyunani "Dea" - 10 "Polis" - miji.
2. Jimbo katika Mashariki mwa Jordani kulikuwa na miji kumi miji hiyo ilikuwa.
1. Bethshan (Scythopolisi)
2. Dioni
3. Pela.
4. Kanatha.
5. Rafana
6. Hippos.
7. Gadara
8. Filadelfia.
9. Damaskusi
10. Gerasa,
a. (Mk. 5:1-20; Mt. 4:24, 25).
II. Maisha ya Yesu katika Palestina.
A. Tangu kuzaliwa mpaka ubatizo wake.
1. Bethlehemu.
a. Mahali Yesu lipozaliwa.
b. Maili 5 Kusini mwa Yerusalemu.
c. Upo katika miinuko ya Nchi ya Yuda katika njia kuu ya kutoka Yeruaslemu mpaka Hebron, (Lk. 2:1-20).
2. Yerusalemu.
a. Alipelekwa kwa Bwana katika hekalu pale alipokuwa na siku 40 tu.
b. Karibu maisha yake Kristo aliyatumia Galilaya.
c. Ni Yerusalemu Yesu alipouawa.
d. Kupaa kutoka Mlima wa Mizeituni, (Lk. 2:22-28; Mdo.1:10-11.
3. Misri.
a. Kwa sababu ya matisho ya Herode Mkuu Yesu alipelekwa Misri kwa kumkinga asiuawe.
b. Herode Mkuu alipokufa walirudi pamoja na walezi wale, (Mt. 2:1-8).
4. Nazarethi.
a. Yesu alitumia maisha yake ya ujana, (Mt. 2:19-23)
b. Ni miji usiopatikana katika A. K.
c. Hapa ndipo alipojifunza Yesu useremala, (Yoh. 1:46).
d. Kutoka hapa ndipo Yesu alipochukuliwa kwenda Yerusalemu akiwa na umri wa miaka 12, (Lk. 2:52).
5. Bethabara.
a. Mahali Yesu alipobatizwa.
b. Eneo kamili hali julikani, Yoh. 3:23.
6. Nyika ya Yudea.
a. Mahali Yesu alipojaribiwa na shetani ni mahali palipokuwa pamejaa wanyama mwitu, Mt. 4:1-11.
B. Huduma yake Galilaya.
1. Kana.
a. Karibu na Nazareti kwenye njia ya kwenda Tiberia.
b. Muujiza wa kwanza ulifanyika hapa, Yoh. 2:1-11.
2. Kapernaumu.
a. Ipo Magharibi pwani ya Bahari ya Galilaya.
b. Ndipo kilikokuwa kituo cha majehi ya Rumi toka Damascus kwenda Yerusalemu.
c. Hapa ndipo alipoitwa Mathayo na Yesu, Mt. 9:9.
d. Petro aliishi hapa, Mk. 9:35.
e. Inaaminika Kapernaumu yalikuwa makao ya Yesu, Mt. 9:1.
f. Kulikuwa na Sinagogi la Wayahudi hapa.
3. Sychar.
a. Ilikuwa katika Samaria karibu na Shekemu.
b. Ndipo kuwepo kisima cha Yakobo, Yoh. 4.
4. Pembe ya Hattini.
a. Ni milima miwili (Pair).
b. Karibu na Bahari ya Galilaya.
c. Yawezeka kuwa ndipo Yesu alipotoa "Hotuba ya Mlima."
5. Naini.
a. Katika Galilaya ya ni katika mteremko ya miinuko ya 6 Moreh katika Esnraelon.
b. Iko maili 6 Kus, Mash ya Nazerti.
c. Hapa Yesu alimponya mtu kipofu, Yoh. 8:22-26.
C. Huduma ya mwisho ya Yesu.
1. Foeniki.
a. Pwani ya Medeteranean kuvuka kutoka Galilaya.
b. Yesu alikuja katika Pwani ya Tiro na Sidoni, Mt. 15:22.
2. Decapoli, Mk. 7:31.
3. Kaisaria Filipo.
a. Ipo Kas. Mash. ya Bahari ya Galilaya upande wa mlima Hermon
b. Wengi wanaamini kuwa Yesu alibadirika karibu na hapa. (Lk.9:25-28).
4. Bethany.
a. Yerusalemu katika maanguko ya Mlima wa Mizeituni.
b. Hapa katika wakati wa Yesu ilikuwa ni njia ya kupitia kwa miguu kutoka Yerusalemu mpaka Bethany.
c. Hapa Yesu ndipo alipomfufua Lazaro, Yoh. 11:38-44.
5. Yerusalemu.
a. Wiki la mwisho la maisha ya Yesu aliitumia hapa.

III. Milima ya Palestina.
A. Magharibi ya Yordani.
1. Mlima - Lebanoni 2. Mlima Meiron.
3. Pembe ya Hattini 4. Mlima Tabor.
5. Miinuko ya Moreh 6. Mlima Gilboa.
7. Mlima Karmeli. 8. Mlima Ebal na Gerizimu.
9. Mlima Sayuni 10. Mlima wa Mizeituni. 11. Mlima Hebroni.
B. Mashariki ya Yordani.
1. Mlima Hermon.
2. Mlima Gileadi.
3. Mlima Nebo.

SOMO LA TISA. MJI WA YERUSALEMU.
Utangulizi:
I. Kujifunza kuhusu mji wa Yerusalemu kunavutia sana kwa sababu ya upekee wa asili yake.
A. Unafikiriwa kuwa ni "Kitovu" cha ulimwengu.
B. Mji huu umeteka hisia karibu za wanadamu wengine wote.
C. Japo kuwa uliweza kuangamizwa mara kadhaa bado uliendelea kujengwa tena na tena.
D. Histora ya Biblia imechukua nafasi katika.
1. Kuta zake.
2. Hekalu lake.
3. Mazingira yake.
II. Kwa hiyo tunahitaji kujifunza juuya mji huu kwa nguvu zote, ili kuijua vizuri Biblia.
Mwili:
I. Majina ya mji huu.
A. Urusalima - Wamisiri waliandika katika karne 19 katika (1900 kk.
B. Yerusalemu - Unaonekana wakati wa Melkezedeki, Mwa. 14:18; Zab. 76:2.
C. Yebusi - Uliitwa na Wayebusi waliokuwa wakikaa hapo, Waa. 19:10.
D. Mji wa Daudi - Mji ulipochukuliwa na Waisraeli karne 4 K.K. 1 Fal. 14:31.
1. Yerusalemu maana yake ni Mji wa Amani.
E. Mji mtakatifu - Mat. 4:5; 27:53.
II. Sehemu za miinuko za Yerusalemu.
A.     Mlima Sayuni.
1. Una urefu ea futi 2530 kutoka usawa wa bahari.
2. Upo Kusini Magh. mwa kona za Yerusalemu.
B. Mlima wa Hekalu.
1. Jina lingine uliitwa Moria.
2. Ibrahimu alipomtoa Isaka awe sadaka.
3. Hekalu la Sulemani lilikuwa hapo.
4. Urefu kutoka usawa wa bahari ni futi 2,432.
C. Ofel.
1. Ulikuwa na futi 2,490.
2. Ulisawazishwa zamani - kupata usawa wa mlima Hekalu.
D. Bezethi.
1. Upo Kas. mwa mlima Hekalu.
2. Herode Agripa aliungani shamlima huu na ukuta.
3. Bwawa la Bethesaida ndipo lilipokuwepo.
E. Mlima wa Mizeituni.
1. Urefu kutoka usawa wa bahari Futi. 2,665.
2. Karibu na Bonde la Kidroni.
3. Mahali alipopaa Yesu.
4. Chini yake kulikuwa na Bustani ya Gethsemani.
F.Mlima wa Makosa, (uovu)
1. Uliitwa kwa sababu ya ibada ya sanamu ilifanywa hapa na Sulemani 1 Fal. 11:7.
2. Upo kusini mwa Mlima wa Mizeituni.
3. Konde la damu lililo nunuliwa kwa vipande 30 alizopokea na kuvirudisha Yuda Iskariote.
III. Sehemu za mabonde za Yerusalemu.
A. Bonde la Kidroni.
1. Majina yake.
a. Kedroni.
b. Cedroni.
c. Bonde la Yehoshafati.
2. Kwa kawaida huwa kavu wakati wa kiangazi.
3. Wakati wa mvua kijito chake huenda mpaka Barahi Mfu (Chumvi).
4. Yesu alivuka Bonde hili karibu kila siku wakati Huduma yake anaimalizia, Yoeli. 3:2, 12; Yoh. 18:1.
B. Bonde la Turopoloni.
1. Limeitwa "Cheesmarker."
2. Linatenganisha Magharibi kutoka miinuko ya Mashariki karibu eneo la Hekalu.
3. Zamani lilikuwa chini zaidi kuliko hivi sasa lilivyo.
C. Bonde la Hinomu.
1. Mpaka wa Yerusalemu wa kusini.
2. Vilevile limeitwa:
a. Wana wa Hinomu.
b. Kuzimu (Gehenna) kueleza adhabu ya waovu.
3. Palikuwa na kiti cha kiji mungu Moleki kwa ibada.
4. Palitumika kama ni Jalala (damp) taka zilipochomwa, Yos. 15:8; 18:16; Mat. 23:15, 33; Yk. 3:6.
IV. Kuta za Yerusalemu.
A. Ukuta wa sasa umekuwa na maili 2 na nusu uliofanywa na mwawe minara 34 milango 8 ilijengwa wakati wa Sulemani.
B. Ukuta wa kwanza ulijengwa na Wayebusi kabla ya Daudi kuitaka sehemu hiyo.
C. Kuta zilizojengwa na Daudi na Sulemani zilizunguka, eneo la Mlima Sayuni Mlima Moria, na ukuta mwingine Bonde la Turopoinoni, Ulikuwa kama Heka 8.
V. Njia kuu 4 za Barabara za Yerusalemu ya zamani.
A. Barabara za Daudi.
1. Inatokea Yopa Mpaka Haramu.
2. Zinaitwa Barabara za Hekalu.
B. Kupitia Dolorosa.
1. Inakwenda magharibi Sambamba na Daudi Sreet.
C. Barabara za Mkristo.
1. Inakwenda Kas. na Kus. na kuunganishwa na Barabara ya Daudi kupitia Dolorosa.
D. Damascus Street.
1. Barabara ndefu kabisa katika Yerusalemu.
2. Inatokea Kus. kupita Yerusalemu mpaka lango Sayuni.
VI. Mabwawa ya Yerusalemu.
A. Bwana la Bikira.
1. Lipo - Bonde la Kidroni.
2. Linavutia kwa kuwa maji huenda na Kurudi tena.
3. Maji hujaa mara kwa mara kwa siku karibu kwa dakika 15 -30.
4. Limeitwa Bwawa la Bikira kwa sababu Mariamu alikuwa na destri kuosha nguo hapa.
B. Bwana la Siloamu.
1. Lipo karibu na mdomo wa Turopoioni (Bonde)
2. Maji ya bwawa hili hufikia futi 3 kwa kina.
3. Maji mengi yanayobaki humwangilia bustani, Yoh. 9:7.
C. En - Rogel - Yos. 15:7; 2 Sam. 17:17.
D. Gihon ya Juu.
1. Ukubwa wake ni meter 735 kutokea Lango la Magha, la Joppa.
2. Lina wastani wa futi 316 kwa 218.
3. Wastani wa urefu kina ni futi 20.
4. Kutoka hapa maji huchukuliwa katika Yerusalemu, (2 Fal. 18:17; Isa. 7:3; 36:2).
E. Gihoni ya juu.l
1. Kina chake futi 42.
2. Lilikuwa ng'ambo ya Bonde la Hinomu karibu na mlima Sayuni, Isa. 22:9.
F. Hezekia.
1. Bwana lilijazwa na gihoni ya juu.
2. Lipo kati ya Daudi na Mkristo mtaa, 2 Fal. 20:20; 2 Nya. 32:30.
G. Ni mji ulioharibiwa mara nyingi kuliko mji wowote ule duniani.
1. Mfalme - Zedekia - Nebuchadnezar, Yer. 39:6 -9.
2. 70 A.D - Wayahudi - Rumi, Mt. 24:1-35.
H. Ni nijio uliorudiwa kujengwa mara nyingi kuliko mji mwingine wowote duniani.
I. Ni mji uliotajwa, unatajwa kuliko mji wowote duniani katika Biblia.
J. Betheaida.
1. Karibu na lango la Stephen.
2. Linachukua kama eka na kina Futi. 80.
K. Mwanamke Mariamu.
1. Futi 150 Kas. mwa Lango la Stefano.
2. Ni bwawa lenye ukubwa wa futi 100 kwa 85 kina chake ni futi 80.
3. Hakuna Historia ya Biblia iliyounganishwa nalo.
L. Yeremia.
1. Karibu ukuta wa Kas. kati ya Lango la Herode na Kas. Mash. Mwa ukuta wa malaika.
2. Lina ukubwa wa futi za mraba 40, kina futi 10.
VII. Milango ya Yerusalemu.
A. Jopa - Magharibi lilitazamana na Hekalu.
B. Damaskusi - katika ukuta wa Kaskazini.
C. Herode - karibu na bwawa la Yeremia.
D. Stefano - ukuta wa Mashariki juu ya eneo la Hekalu.
E. Dhahabu - upande wa Mashariki kuingia eneo la Hekalu.
F. Madi - Kusini kukabili Kidroni (bonde)
G. Daudi - Kusini - mwishoni.
VIII. Kuhusu mji wa Yerusalemu.
A. Ni kituo cha dini kubwa 3.
1. Ukristo.
2. Uyahudi.
3. Uislamu.

SOMO LA KUMI: SAFARI TANO ZA UMISSIONARY KATIKA AGANO JIPYA.
Sehumu I.
Safari Tano Za Umissionary Katika Agano Jipya.
Utangulizi:
I. Historia ya mapema ya Kanisa, tunasoma safari tano za Umissionary.
A. Safari ya Filipo-(Mdo. 8:5-40).
B. Safari ya Paulo-(Mdo. 9:1 - 30).
C. Safari ya Petro-(Mdo. 9:32 -11:18).
D. Safari ya Barnaba-(Mdo. 11:22-26)
E. Safari ya Barnaba na Paulo-(Mdo. 11:26-30; 12:25).
Mwili:
I. Safari ya Filipo-Mdo. 8:5-40.
A. Alikuwa mmoja wa Mashemasi, (Mdo. 6:3-5).
B. Aliondoka mara moja Yerusalemu baada ya kifo cha Stefano, Mdo. 7.
1. Alihubiri - Samaria injili inafika mwisho wa nchi, Rum. 1:8.
2. Wayahudi walikuwa hawachangamani na Wasamaria.
C. Kutoka Samaria Filipo alikwenda chini ya Yerusalemu kule Gaza kulikokuwa jangwa, Mdo. 8:26.
1. Alikutana ma mtu wa Kushi (Etiopia) Towashi alimhubiri injili na kumbatiza, Mdo. 8:38.
D. Baadaye alionekana Azoto, katika Azoto A.K ni Ashidodi ilikuwa katika uwanda wa Filisti.
E. Huduma ya Filipo kule Samria, Mu - Ethiopia na katika miji ya Wafilisti ilileta taabu katika Kanisa ambapo baadhi ya wakristo walikuwa wanashikilia mapokeo ya dini ya Kiyahudi.
II. Safari ya Paulo Mdo. 9:1-30.
A. Paulo alizaliwa Tarso, ambao ulikuwa mji mkuu wa Kilikia, Kusini mwa Asia ndogo.
B. Alikuwa ni Mfarisayo, Ukristo aliouona kuwa Adui wa imani ya babu zake.
C. Alikuwa anakwenda Damaskasi-Shemu kuwatesa Wakristo ili warudie aina ya Kiyahudi.
D. Alikutana na Yesu njiani aliyebadirisha mwelekeo wa masiha yake yote.
E. Jina lake lilibadirishwa kutoka Sauli na kwa Paulo.
F. Alikwenda uarabuni baada ya kukaa muda Fulani Dameski.
1. Uarabuni -inaweza kuwa sehemu yoyote katika Peninsula.
2. Yaweza kuwa safari yake alipitia jangwani, Gal. 1:17.
G. Alirudia tena Damaski ambapo alikutana na mateso kwa mara ya kwanza, Mdo. 9:15-16.
1. Aliokolewa kwa kutoroshwa ndani ya kikapu.
H. Akarudi Yerusalemu ambako mapema lijifunza chini Rabbi Gamaliel – Paulo alipokelewa na kukaribishwa na Barnaba.
1. Barnaba alijua kuongolewa kwa Paulo.
2. Barnaba alimpeleka na kumtambulisha Paulo kwa mitume Petro na Yakobo, Gal. 2:1 10.
I. Alipokuwa anahubiri kule Yerusalemu, ghasia nyingi zilijitokeza na upinzani wa nguvu ulizuka, hivyo Paulo alichukuliwa kwa Bandari ya Bahari na kwenda Kaisari, kutoka hapo alikwenda Kusini ya Tarso.
J. Tarso ulikuwa mji wake wa nyumbani alikaa kwamiaka kdhaa miaka kabla ya kuanza mikiki - mikiki ya safari zake zote za Umissionari.
III. Safari ya Petro, Mdo. 9:32 - 11:18.
Kufuati kuongolewa kwa Paulo, yalianzisha makanisa mengi. Mateso ya Wakristo yalimfanya Petro aanze kusafiri na kuyatia moyo makanisa.
A. Alikwenda kule Lida iliyokuwa katika uwanda wa Sharoni njia ya moja kwa moja toka Yopa - Yerusalemu.
1. Alimponya - Ainea aliyeugua miaka 8 (amaepooza), Mdo. 9:32-35.
2. Alikwenda Yopa alimponya Dorkas, Mdo.9:36-42.
3. Alipokea maono - kupeleka injili kwa kornelio kule Kaisaria bado akiwa Yopa.
a. Kornelio - Mrumi Akida.
b. Kaisari ilikuwa mail 30 toka Yopa.
B. Viongozi wa Kanisa kule Yerusalemu walipokuwa wanatia mashaka kuongolewa kwa mataifa, Petro alirudia Yerusalemu na kujadiliana nao kuwa kazi ya kumwongoa kornelio ilikuwa kazi ya Mungu, Mdo. 11:1- 18.)

III. Safari za Barnaba, Mdo. 11:22 - 26.
Baada ya kifo cha kupingwa mawe kwa Stefano na kuingia kwa mateso idadi kubwa ya Wanafunzi walifukuzwa kutoka Yerusalemu.
A. Walisafiri Kas kupita Tirona sidoni na kufika mji wa Antiokia.
B. Walikuwa waaminifu kwa ukiri wao wa Ukristo na wakawa ni chanzo cha mbegu kwa kuanzisha makanisa.
1. Kule Antiokia (Shemu).
a. Wanafunzi waliitwa kwanza wakristo, Mdo. 11:26.
b. Kutoka katika mji huu Wamisionary walitumwa nje kuhubiri, Mdo 13:1-12, kama wahubiri wa injili.
c. Wasiwasi waliokuwa nao Wakristo Wayahudi juu ya Wakristo wa mataifa wapya.
1. Alisema hii kazi ni ya Roho Mtakatifu.
2. Moyo wake ulipenda na kuendalea kuwa na kanisa kule
Antiokia ili kuendelea kulisadia Kanisa.
2. Alisafiri kwenda Kaskazini kule Kilikia na akamshawishi Paulo kule
Tarso kuondoka naye mpaka Antiokia tena.
V. Safari ya Barnaba na Paulo, Mdo 11:26-30, 12:25.
A. Kutoka Taso Barnaba na Paulo walisafiri kwa njia ya Bahari mpka Seleusia Shemu.
B. Walikaa kwa mwaka mmoja Antiokia wakifanya kazi na Kanisa kufanya
Kanisa lilikokuja kuwa kituo cha Ukristo.
C. Wakati wa njaa kule Yudea, Kanisa la Antiokia liliwatuma Paulo na Barnaba pamoja na michango yao.
D. Waliporudia toka Yudea waliendelea kufanya kazi pale Antiokia mpaka walipoanza safari yao ya Umisirionary.
1. Ilitokana na nia zao na juhudi yao kupeleka Injili kwa wale wasio sikia bado Ukristo.

SOMO LA KUMI SAFARI ZA MTUME PAULO
Sehemu II
Safari Za Mtume Paulo .
Utangulizi:
I. Ni machache sana yanayofahamika kuhusu maisha ya mwisho ya mitume wa Bwana.
A. Petro anaonekana kuchukua mafasi katika sura za mwanzo za kitabu cha

Matendo.
B. Yohana alikuwa pamoja naye katika tukio moja, Mdo. 3:1.
C. Yakobo alichinjwa katika maisha ya mwanzo ya Mitume kwa amri ya Herode, Mdo. 12:2.
D. Maelekezo makubwa katika kitabu cha Mtendo ni safari kubwa za umisionari za mitume Paulo.
1. Wakati wa huduma yake Ukristo ulionekana kuwa ni wa kimataifa.
2. Paulo alipoanza huduma yake mataifa walikuwa huru kabisa kuingia au kuongezwa katika Kanisa.
3. Kabla ya kifo chake mtume Paulo, upande wote wa mashariki wa utawala wa Rumi ulikuwa umesikia ujumbe wa Injili kwa kiasi kikubwa.
Mwili:
I. Asia ndogo.
A. Safari ya mtume Paulo ya kwanza ya Umisionary ilichukua pia Asia ndogo.
1. Ukumbwa wake maili mraba 15,600.
B. Wilaya 4 magharibi mwa Asia Ndogo.
1. Karia.
2. Lidia.
3. Myasia.
4. Frigia.
a. Wilaya zote hizi ziliungana na kufanya Jimbo.
C. Majimbo ya Bithinia na Ponto yalikuwa ufukoni mwa Bahari Nyeusi.
D. Wilaya katika Bahari Nyeusi.
1. Ponto - (Mdo. 2:9; 18:2; 1 Pet. 1:1)
2. Paflagonia.
3. Bithinia - Mdo. 16:7; 1 Pet. 1:1.
E. Wilaya katika upande wa Bahari ya Aegean.
1. Mysia, Mdo. 16:7-8.
2. Liydia.
3. Karia.
F. Wilaya katika Bahari ya Mediterranean.
1. Lysia - Mdo. 27:5.
2. Pamfilia - Mdo. 13:13.
3. Cilisia (Kilikia) Mdo. 21:39.
G. Wilaya katika upande wa katikati (bara).
1. Galatia - Miji katika Galatia.
a. Ikoniamu.
b. Derbe.
c. Listra.
d. Antiokia ya Pisidia.
1. Katika miji hii Paulo aliteseka wakati akihubiri humo.
2. Kapadokia - Mdo. 2:9.
3. Lyconia - Mdo. 14:1-23.
4. Pisidia - Mdo. 13:14; 14:21.
5. Frigia - Mdo. 16:6; 18:23.
II. Safari ya kwanza ya Umisionary - Paulo.
A. Antiokia - Syria - Palikuwa ni mahali pa kuanzia safari.
B. Safari ya kwanza walikuwa watu 3.
1. Paulo.
2. Barnaba.
3. Yohana Marko.
4. Vituo vya safari hii ya kwanza ya Umisionary.
a. Antiokia Shemu.
b. Seleukia - Shemu - Bandari katika Shemu.
c. Kisiwa cha Cyprus.
5. Kulikuwa na vitu kadhaa kule Cyprus.
a. Salamis - Mdo 13:5, Mashariki ya Pwanai ya Cypus.
1. Hapa walihubiri katika sinagogi la Wayahudi.
2. Huu ni mji ulioanzishw na Wafoeniki.
b. Pafo (Paphos) - Mdo. 13:6.
1. Barnaba na Paulo - walikutana na mchawi aliyepingana nao alipigwa na upofu kwa muda aliyeitwa Bar - Yesu.
2. Ulikuwa ni mji maarufu ibada ya Aphrodite.
C. Asia Ndogo.
1. Walifika Perga - Mdo. 13:13.
a. Kulikuwa na kiji mungu cha kike Diana na hekalu lake la Artemi.
b. Hapa ndipo Yohana Marko aliporudia Yerusalemu na kuwaacha Paulo na Barnaba.
2. Antiokia Pisidia - Mdo. 13:14 - 48.
a. Paulo na Barnaba walipingwa na kutolewa nje ya mji Mdo. 13: 50 -51.
3. Ikoniamu kule Frigia.
a. Walipigwa na Paulo alikumbuka kuwa kipigo kilitaka kufikisha mwisho wa maisha yake, Mdo. 14:16; 2 Tim. 3:11.
4. Listra.
a. Ulijengwa na Augustino Kaisari karnea ya 6 KK.
b. Miujiza uilitendeka kwa kumponya mtu kiwete tangu kuzaliwa watu wa Listra waliwafanyia ibada Paulo na Barnaba na kutaka kuwafanaya miungu.
1. Paulo walimwita - Mercury Paulo alipingwa mawe karibu ya kufa.
2. Barnaba walimmita - Jupiter.
5. Derbe.
a. Walihubiri kwa nguvu baada ya mateso ya ya Listra.
b. Walihubiri njia ile ile ili kuwaimarisha Wakristo, Mdo. 14:22.
III. Safari ya pili ya Paulo.

A. Ilianza kwa kutokuwepo makubaliano kati ya Paulo na Barnaba kwa ajili ya Yohana Marko.
1. Waligawanyika kilamtu alimchukua anayemtaka.
a. Barnaba alimchukua Yohana Marko - Ciprus.
b. Paulo alimchukua Sila - Asia Ndogo.
B. Vituo walivyopita katika Asia Ndogo.
1. Antiokia Shemu.
2. Taso.
3. Derbe.
4. Listra - Timotheo aliungana nao hapa, Mdo. 16:1-4.
5. Ikoniamu.
6. Antiokia Pisidia.
7. Troa - Mdo. 16:6-8, Maono ya mtu wa Makedonia.
C. Vituo walivyopita katika Ulaya.
1. Neapolosi - Kituo cha kwanza kule Ulaya.
2. Filipi - Mdo. 16:14.
3. Amfipolis - Mdo. 17:1.
4. Apolonia.
5. Thessalonika - Mdo. 17:6, 8.
6. Beroya - Waungwana, Mdo. 17:10-13.
7. Athene - Wanamwabudu Mungu asiyejulikana.
8. Korintho
9. Kenkrea - Aliondoa nadhiri yake kwa kunyoa nyele zake.
10. Efeso- Mdo. 18:18-22 Asia Ndogo Palestina.
11. Kaisaria - Asia Ndogo Palestina.
12. Yerusalemu.
IV. Safari ya tatu ya Paulo.
A. Vituo kadhaa katika safari yake ya tatu.
1. Antiokia Syria - Kituo cha kuanzia, Mdo. 18:18-22.
2. Derbe.
3. Antiokia Pisidia.
4. Efeso.
5. Troa.
6. Neapoli.
7. Filipi.
8. Amfipoli.
9. Apolonia.
10. Thesslonika.
11. Beroya.
12. Korintho.
B. Wakati alipokuwa anarudia alitumia njia hiyo hiyo mpaka Troa.
1. Mitulano.
2. Samo.
3. Mileto.
4. Patara.
5. Tiro.
6. Tolemaisi.
7. Kaisaria.
8. Yerusalemu.
V. Safari ya Mtume Paulo kwenda Rumi, Mdo. 21:26; 28-31.
A. Kaisaria.
B. Damascus.
C. Myra - Lycia, Mdo. 27 :6.
D. Cnidus (Nido)
E. Lasea.
F. Kauda.
G. Kisiwa cha Malta.
H. Sirakusa.
I. Regio.
J. Putioli.
K. Soko la Apro.
L. Mikahawa mitatu (Three Taverns).
M. Roma.
SOMO LA KUMI: JIOGRAFIA YA KITABU CHA UFUNUO:
Sehemu Tatu
Jiografia ya Kitabu cha Ufunuo:
Utangulizi :
I. Kitabu cha mwisho kuandikwa kiliandikwa katika kisiwa kidogo cha Patmos, Kusini ya Magharibi ya Asia ndogo.
A. Patmo ipo maili 70 kusini magharibi ya Efeso.
1. Kuna miamba.
2. Mahari palipotengwa.
3. Pazuri kwa kuwaadhibu waharifu.
Mwili:
I. Makanisa saba ya Asia.
A. Sura ya Pili na tatu ya kitabu cha Ufunuo kuna barua kwa makanisa ya Asia.
B. Maeneo 4 yalikokuwako Makanisa 7.
1. Mysia.
2. Lidia.
3. Caria.
4. Frigia.
C. Barua hizo zilitumwa kama ifuatavyo.
1. Efeso, Ufu. 2:1.
a. Ulikuwa mji muhimu sana katika eneo hilo.
b. Ulikuwa mji mkuu wa Asia Ndogo wakati wa Rumi.
c. Paulo aliutembelea katika safari yake ya pili.
d. Safari ya yake ya tatu alikaa Efeso miaka 2.
2. Smyrna - Ufu. 2:8.
a. Kama maili 40 kuelekea Kaskazini ya Efeso.
b. Bandari muhimu katika Uturuki.
c. Kwa sasa mji unaitwa Izmir.
d. Ulijengwa mwaka 1200 KK na Aeolic Wayunani.
e. Ulikuja kuwa tajiri kati ya Asia na Magharibi.
f. Ulijengwa tena na Alexander Mkuu.
g. Umeandikwa katika kitabu cha Ufunuo tu.
h. Ulifanyika kuwa kituo muhimu wa Ukristo.
i. Polycarp alikuwa askofu wa Smyrna kabla ya kuuawa kwake 155 B.K.
j. Kanisa hili lilikuwa maskini na lilikuwa limeteseka sana kwa kukataa kuabudu ibada ya mtawala wa Rumi.
3. Pergamum (Pergamo), Ufu. 2:12.
a. Ulikuwa maili 60 kutoka Smyrna katika Mysia.
b. Kulikuwa na makitaba iliyokuwa na maandiko 200,000.
c. Kilikuwa ni kiti cha Shetani, Ufu. 2:13.
4. Thiyatira, Ufu. 2:18.
a. Ulikuwa mji katika Lidia katika ya kwenda Pergamo na Sardi.
b. Ulianzishwa na Seleucust mwaka 300 K.K.
c. Kanisa hili lilisifiwa kwa kazi nzuri.
1. Upendo.
2. Imani.
3. Uvumilivu.
d. Walionywa baadhi ya Wakristo kwa zinaa na kula vitu vilivyotolewa kwa sanamu, Ufu. 2:20.
e. Jina la sasa ni Akisa.
5. Sardi, Ufu. 3:1.
a. Ulikuwa mail 30 kusini ya Thiyatira.
b. Ulianzishwa mwaka 1200 K.K.
c. Utajiri wake ulikuwa ni kwa sababu ya Biashara.
d. Wachache walipewa sifa katika Sardi.
1. Walikuwa hawajachafua mavazi yao, Ufu. 3:4.
e. Baadaye ulifanyika kuwa kituo cha Ukristo katika Asia ndogo.
f. Mji huu uliangamizwa na mongol, Tamerlane mwaka 1500 B.K.
6. Filadelfia: (Ufu. 3:7.)
a. Ulikuwa kama maili 28 Kuskazini, Mashariki ya Sardi.
b. Mwanzilishi wake ni Attalus Filadelfia.
c. Uliharibiwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara.
d. Historia yake inaendelea kwa jina lingine la Alashehir.
e. Kanisa hili la Filadelfia lilisifiwa.
1. Kwa kutunza neno la Mungu.
2. Mungu atawatunza waaminifu wake walihakikishiwa katika saa ya kujaribiwa ulimwengu.
7. Laodikia, Ufu. 3:14.
a. Ulikuwa mji mkuu katika Frigia.
b. Ulikuwa kama maili 50 kutoka Filadelfia.
c. Ulipewa jina hili la Laodikia na mfalme wa Shemu Sleucus –II kwa kumpa heshima mkewe Laodice.
d. Ulikuwa maarufu kwa kutengeneza sufu za manyoa ya Kondoo.
e. Wajivuna kwa sababu ya kuwa na shule ya madawa ya macho, iliyojulikana kama unga wa Wa- Frigia.
f. Walipokea onyo kali.
1. Kwa sababu ya kuwa vuguvugu kwa Mungu kidogo na dunia kidogo. Mungu abariki kozi hii itumiwe na wote waliojifunza ipasavyo katika kuhubiri na kufundisha makusanyiko ya Mungu.