KWA NINI YESU ALIFUNDISHA KWA MIFANO.
Ziko sababu
kadhaa zilizopelekea Yesu kufundisha kwa mifano hii ni njia nzuri na kubwa
aliyoitumia Mungu na Manabii na pia marabi lakini kwa Yesu kulikuwa na sababu
kadhaa zilizopelekea kunena kwa mifano
1.
Alitumia mifano ili kukwepa mitego ya watu
waliomwendea ili kumnasa kwa Maneno Marko
12;1-12.
2.
Alimtumia mifano ili kutofautisha watu
walioitafuta kweli na waliofuata miujiza na mikate na pia kama hukumu kwa watu
wenye mioyo migumu, Mathayo 13;10-17
3.
Alitumia mifano ili kukwepa au kuufikisha ukweli
kwa waalimu wa torati waliofuatilia mafundisho yake (Mfano wanafunzi wa vyuo vya
Biblia)
4.
Kupunguza ukali wa ujumbe ili kukwepa kupigwa
mawe au kuuawa kabla ya wakati 2Samuel
12;1-6. Mungu huwapa Hekima Manabii wake namna ya kupeleka jumbe bila
kupata madhara
5.
Kusaidia watu kuelewa kwa urahisi habari za
ufalme wa Mungu
KANUNI YA KUTAFASIRI MIFANO
Ni muhimu kufahamu kuwa mifano ya kibiblia
hubeba maana moja tu na ambayo ndio kweli ya kiroho kwa hivyo ni marufuku
kufasiri mstari mmoja mmoja ulio na mfano na kufafanua kwa maana za kiroho hii
sio kanuni ya kutafasiri mifano na kwa kufanya hivyo huwezi kupata kweli
iliyokusudiwa unapaswa kusoma mfano mzima na kuangalia unabeba nini Principle
of Contents kisha uweze kuelezea kile kinachosemwa mfano Kwa mfano wa Msamaria
Yesu alikuwa akifundisha Jirani wa kweli ni yupi.
TATIZO LA MWANA MKUBWA.
Tunaona hasara za mwana mpotevu jinsi alivyofanya
mambo mabaya ya kusikitisha na jinsi alivyokosa amani na kurudi kwa Baba yake,
na jinsi Baba yake alivyompokea lakini kwa namna ya kushangaza Yule mwana mkubwa alipokea mambo kwa mtazamo wa tofauti.
Jinsi Mwana huyu mkubwa alivyopokea inatufundisha mambo ya msingi
yafuatayo (Luka 15: 25- 32)
I. ALIKUWA
NI MTU WA KUJIHESABIA HAKI ( 29-30)
Huyu mwana
mkubwa alikuwa na tatizo kubwa sana lililohitaji msaada wa Mungu,
Alikasirika alisusia, na alijiona kuwa ni mwema kuliko ndugu yake na kuwa yeye
pekee ndiye mwenye haki ya kufanyiwa sherehe kuliko mwingine na kuhukumu, hii ni tabia ya Kifarisayo ambayo Mungu anapiga vita, ( Luka 18: 9- 14) Utoaji na Baraka za
Mungu haziko katika wema au ubaya wa mtu ( Math 5: 45) Baraka za Mungu ziko kama Mungu anavyoamua kwa yeye anayetaka
kumrehemu humrejeza ( Warumi 9: 11-16) Mungu
angekuwaanabariki kwa matendo ya haki basi Yakobo hangebarikiwa
kwani alikuwa mwenye hila na
muongo, lakini alibarikiwa kwa rehema za Mungu tu. Ni ukarimu na rehema za Yule
baba aliamua afanye hivyo kwa mwana mpotevu ndugu mkubwa – Alijifanya ni mtii zaidi kwa babaye, Alimhukumu nduguye.
II. ALIKUWA
HANA UPENDO BALI CHUKI.(28- 30)
Mwana mkubwa alikuwa na tatizo la ubinafsi na
chuki, mafundisho ya kristo kupita mitume
wake yanpingana sana na tabia ya
chuki yakitaka tuwe na upendo, watoto halisi
wa Mungu wanajulikana kwa tabia
ya upendo kwa wanzao.
(1 Yohana 3:
10- 12, 4: 20)
III. ALIKUWA
MTU WA KUTAFUTA MAKOSA (25- 38)
Huyu ndugu mkubwa anaonekana kuwa na tabia ya mafarisayo, tabia ya kuhukumu au kuona kosa
la Mwingine hii nayo ni tabia ambayo Yesu alikemea hadharani. (Luka 6: 41-42) Ndugu yake mkubwa
alipaswa kwanza kushughulikia tatizo lake la ndani kabla ya kutoa shutuma na
lawama kwa mwenzie, yeye alihukumu na
aliona kuwa hata baba yake wa mbinguni
ana kosa.
IV. HAKURIDHIKA;
ALIKUWA NA CHOYO NA ALIKOSA FURAHA. ( 31-32)
Mwana huyu mkubwa alikuwa na vyote, na katika uaminifu wake ; angeweza kufanya
karamu aifanyayo na rafiki zake na hangezuiwa, kwa kweli hakuridhika na alihukumu
huruma ya baba yake kwa wengine, dhidi ya yote alikuwa na choyo na
alitaka yeye awe yeye tu, choyo ilimkosesha furaha,
babae alimtaka afurahi tu, Mungu anapobariki anataka tufurahi
anapobariki wengine pia.
Mifano ya Yesu pia ilikuwa inatoa mwanga namna Mungu atakavyo hukumu kwa haki wale wanaojikinai na kufikiri kuwa ni wema na wamestahili kuliko wengine watakataliwa katika Ufalme wa Mungu uwe mwangalifu
Somo Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni