Jumamosi, 15 Novemba 2014

Nikadebwela Lifti kwa Saa Tatu!

Sitaki kutaja jina langu ingawa sio vibaya kufanya hivyo, Mimi ni kijana wa miaka 33 hivi Nilikuja Dar es Salaam kutoka Rufiji mwaka 1999 wakati huo nikiwa na miaka 27, kwa hiyo naweza kusema kwamba siifahamu Dar es Salaam vizuri, hata hivyo kutokufahamu Dar haina maana ya kutokufahamu mambo mengine ya kawaida ambayo kwa dunia ya sasa mtu anayeishi mjini kuyajua ni jambo muhimu, lakini pia la kawaida

Siku ninayotaka kuizungumzia ni Machi mwaka 2001 siku hiyo mjomba wangu ambaye ndiye aliyenilea  aliniita na kunituma , aliniambia niende mjini kwa jamaa yake mmoja nimpelekee fomu zake Fulani, huyo jamaa azishughulikie, alinielekeza ofisi za huyo jamaa zilipo, mjomba alinipa maagizo na kumtaja  huyo rafiki yake  ambaye nikimtaja pengine hata wewe utamfahamu ukifika pale’Panda lifti ghorofa  ya kumi ulizia ..’, Nilimkubalia na kuondoka ,nataka nikuambie jambo moja ni kwamba tangu kuja kwangu Dar nilikuwa nimepita majengo kadhaa wa kadhaa na kuona lifti Nasema kuona, basi nilipojua ni ghorofa ya kumi nilisema iko kazi, nilijiambia kuwa badala ya lifti ningetumia ngazi tu, Nilipofika kwenye jingo lenyewe ambalo lilikuwa bado jipya kabisa  wakati huo ilikuwa 2001 nilikwama baada ya kugundua kuwa hata njia ya kupandia ngazi kwa miguu sikuweza kuiona, Niliona aibu kuuliza kwa hofu ya kuonekana mshamba, Basi ilibidi nijiunge na watu wengine waliokuwa wakisubiri lifti na kupanda, sikuwa najua kuwa , nilifikiri labda kungekuwa na dereva na kondakta au mtu Fulani aliyeniendesha.


Nilioona watu wanadandia name nikadandia, niliona watu wanaboinyeza kitu Fulani kasha taa inawaka, Nilijinyamazia, na kiroho kilianza kunidunda, Lifti ikapanda watu wana shuka na kuingia, mwisho watu wote wakashuka na wakapanda wengine , nilihisi kama lifti ilikuwa inashuka lakini sikuwa na uhakika nilienda nayo huku nikijaribu kujiuliza maswal, Niliona watu waliopanda wakishuka tena na wengine wapya waliingia na lifti ikaondoka kuelekea  huko inakoelekea , Mimi nilibana tu,nilikuwa naangalia watu wanavyobonyeza lakini sikuwa na uhakika ni kitu gani hasa kinachofanyika , Nilitembea na hiyo lifti mpaka nikahisi  kama vile ninjaumwa  maradhi ya moyo au kitu kingine kibaya zaidi Nilikwenda na kurudi kwenda na kurudi  tangu kwenye saa tano na nilikuwa na uhakika kuwa imefika saa nane.
Lifti ni chombo kigeni sana katika miji mingi ya Tanzania pichani Lifti ya kwanza kuzinguliwa mjini Mbeya

Nikiwa nimefikia hatua ambayo sasa siwezi kuendelea kuwa bwege yaani kutaka kuuliza, Bwana mmoja mwenye mavazi ya kaki na bluu aliniuliza vipi hufiki unakokwenda? Tangu asubuhi uko ndani ya lifti, abiria wa lifti walivunja shingo zao kunitazama kama unavyojua watanzania masikio yako juujuu kama sungura kutaka kusikiliza ya watu, Nilibabaika lakini nilijikaza na kusema naenda ghorofa ya kumi lakini sipajui…” Yule jamaa ambaye kumbe alikuwa ni mesenja kwenye moja ya ofisi kwenye jingo lile alicheka na kusema ndio maana tangu saa tano hivi nakuona umo humu, naenda narudi nakuona mzee umo humu, nikadhani unataka kubwedela...” Abiria waliangua kicheko

Nilitazama chini hasa kwa kuzingatia kwamba kulikuwa na mademu wengi wakati huo mle kwenye lifti, Yule mesenja alikuwa kama amepata pa kuonyesha ujuaji wake ‘Ona ukitaka kwenda ghorofa ya kumi unabonyeza hapa..’ Halafu aliendelea kunifundisha mambo mengine ya lifti ni tuisheni ya bure lakini!

Nilishuka ghorofa ya kumi na kuulizia ofisi za Yule jamaa, Nilikuwa nahisi kizunguzugu mtindo mmoja, Niliambiwa huyo jamaa yake mjomba alikuwa ametoka Ilibidi nimsubiri hadi kwenye saa kumi aliporejea, Nilimkabidhi fomu na aliponiuliza sababu ya kuchelewa nilimwambia nilikuwa nimepotea jengo, unadhani wakati narudi nilipanda tena lifti? Kama unadhani hivyo shauri yako unadhani mbumbumbu niko peke yangu tuko chungu nzima 

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
ikamote@yahoo.com
0718990796
0784394550

Hakuna maoni: