Nikawa
nahangaika kutafuta kazi mjini, Nilifanikiwa mwaka huohuo kukutana na mtu
ambaye alisoma na ndugu yangu, huyu Bwana aliamua kunisaidia kupata kazi
mahali, aliponiuliza kuhusu elimu yangu nilimwambia nimemaliza kidato cha sita,
ingawa ukweli ni kwamba nimesihia darasa la saba, Alinifanyia mpango nikapata
kazi kwenye kiwanda kimoja hapohapo barabara ya Nyerere. Nilitafuta vyeti vya
bandia kutoka kwa rafiki yangu ambaye
wakati huo alikuwa chuo kikuu, niliajiriwa kama karani waupokeaji wa mali ghafi
na udhiinishaji wa utokaji wa bidhaa,
ilikuwa ni nafasi kubwa sana hata kwa mtu wa kidato cha sita, hata hivyo kwa
sababu ilikuwa ni kazi yenye kuhitaji tu maelekezoili mtu kumudu kuifanya niliielewa
kwa kiasi.
Bahati mbaya
mwezi wa kwanza tu wa kazi, nikaanza kwa unoko sana, nilikuwa najifanya najua
na nikawa nawazibia watu riziki zao, ili nipendwe na wenye kampuni, Kumbe
katika unoko huo huo ndio ungeniponza, taarifa za kwamba mimi ni darasa la saba na niliwahi kupata skendo zilifika pale
kazini, Siku hiyo nafika kazini kama
kawaida, nikaitwa kwa mkurugenzi. Nikajua kuwa ninaenda kumwagiwa misifa
kutokana na utendaji wangu wa kazi, kufika mkurugenzi akaniambaia, “tulikuajiri
tukiamini kwamba kila ulilolisema kwetu lina ukweli, Hebu hasa jina lako na
kiwango chako cha elimu na wapi uliwahi kufanya kazi kabla ya kuja hapa”
Nilihisi moyo
ukianza kudunda kwa kasi na kwa nguvu, Nilijikaza na kusema sijafanya kazi popote, tangu nimemaliza
masomo ya kidato cha sita mwaka juzi, na jina langu ndilo hili ninalotumia,
Wakurugenzi waliokuwa wamenizunguka walitabasamu kwa dharau hadi nikaogopa
“Sasa bwana kuna mawili ama tukupeleke polisi sasa hivi kwa kudanganya na
kufoji vyeti na jina la mtu ambalo si
lako au uondoke sasa hivi bila hata kipande cha karatasi yaani kama ulivyokuja, Hatuna haja ya kubishana nawe kwa sababu unaujua ukweli wote kuliko
sisi” Mkurugenzi mkuu alisema, Yule
jamaa aliyenifanyia mpango wa kazi naye alikuwepo kwenye kikao kile,
“Umeniangusha sana sikutegemea kabisa, kumbe hata sekondari hujakanyaga
unakwenda kujipachika ufomu six wa bure! Kwa kweli hata tukionana njiani
usinisalimie kabisa, Ungenisababishia kuharibu kazi yangu bure” Aliniambia.
Nilimwambia nimekosa nitaondoka
sasa hivi na sitaki chochote, Nilijivuta polepole na kuanza kutoka nje, huko
nje kumbe wafanya kazi wengine
walishapata taarifa, kwa hiyo
nilipokuwa nikikatiza mitaa walikuwa wakinicheka na kunizomea, sikujibu chochote kwa kweli ilikuwa fedheha ya mwaka
unataka kujua nini kiliendelea we bwege nini? Mbona unapenda sana umbeya
kwa taarifa yako sasa tukio hili lilinifanya niende kujisomea kwa machungu
nikamaliza kidato cha sita na sasa nina stashahada ya uhasibu. Ilikuwa fedheha
ambayo ililipa!.
Fundisho na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
email. ikamote@yahoo.com
0784394550
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni