Mstari wa Msingi Kutoka 3: 7- 11
Biblia inasema hivi katika
Mistari hiyo hapo “BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko
Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua
maumivu yao; 8. NAMI NIMESHUKA ILI NIWAOKOE NA MIKONO YA WAMISRI, niwapandishe
kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata
mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 9.
Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo
mateso ambayo Wamisri wanawatesa. 10.
Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana
wa Israeli, katika Misri. 11.
MUSA AKAMWAMBIA MUNGU, MIMI NI NANI, HATA NIENDE KWA FARAO, NIKAWATOE WANA WA
ISRAELI WATOKE MISRI?”
Wengi wetu tunaposikia kitabu cha
kutoka na kujifunza unapoambiwa uelezee maana ya kitabu hiki kutoka ni rahisi
kujibu kuwa kutoka ni jina la mojawapo ya kitabu kilichoandikwa na Musa kati ya
vitabu vyake vitano viitwavyo Pentateuch kitabu hiki kiliitwa kwa Kilatini Exodus
kutokana na tafasiri ya kiyunani ya neon “Exodos”au English Exodus na maana
yake ni Kutoka, “Going Out” “Exit”au “departure” Hii ni tafasiri rahisi sana na
haitoi maana kamili ya kazi ya Mungu aliyoifanya Kule Misri inapunja utendaji
wake na kuufedhehi!
Hiwezekani Mungu ASHUKE tu kwa jambo rahisi kiasi hicho!
Haiwezekani! Popote unaposikia au kuona Biblia inasema kuwa Mungu ALISHUKA ni
lazima uelewe kuwa kulikuwa na uzito mkubwa sana wa jambo au tukio na Mungu anaposhuka ujue analokwenda kulifanya
ni la kihistoria na ni la kupita kawaida!
Kwa halali kabisa kitabu hiki
kinafunua mambo kadhaa muhimu sana kuhusu Mungu
1. Kinamfunua
Mungu kama “Yehova” IAM who IAM Yeye alijulikana kama Mungu muumba katika
kitabu cha Mwanzo sasa ni Mungu Mwokozi he is going to perform great Redemption
2. Kinafunua
tabia ya uungu ya kupinga uonevu, kwa taifa moja lenye nguvu kuwanyonya
wanyonge kwa ufupi Mungu ndiye aliyekuwa wa kwanza kupinga na kukomesha utumwa
3. Kinafunua
juu ya uongozi wa kweli wa Mungu kwa wanadamu kwa kuwapa sheria
4. Na
kinaelekeza namna Mungu navyoweza kufikiwa na wanadamu kwa njia ya Ibada
Iwapo ningepewa
nafasi ya kutoa jina kwa kitabu hiki mimi ningekiita “Redemption” simply!
Baada ya kutoa utangulizi huo
sasa - Ni muhimu kuwa na Ufahamu kuwa Misri lilikuwa ni taifa la namna gani ili
uweze kupata picha kwanini Mungu alishuka kuwaokoa wana wa Israel yeye
mwenyewe?
·
Misri lilikuwa ndio taifa la kwanza lenye jamii
yenye maendeleo makubwa sana “Civilization”
·
Kihistoria jamii ya wamisri ilikusanyika kwa
wingi kutokana na kukua kwa jangwa la sahara kati ya mwaka wa 7000 mpaka wa
5000 (K.K.)kabla ya Kristo
·
Jamii ya watu waliokusanyika waliweza kuwa na
maendeleo makubwa sana kutokana na matumizi ya maji ya mto Nile kwa kilimo na
umwagiliaji
·
Bonde la mto nile lilikuwa na rutuba ya kutosha
kutokana na kutiririka kwa mbolea toka Ethiopia na maeneo mengine yenye asili
ya mto nile
·
Kutoakana na kuwepo kwa rutuba hii kuliwafanya
watu wengi kufanya makazi ya kudumu pale Misri na kukawa na maendeleo makubwa
katika sekta ya kilimo
·
Misri ilianza kuwa taifa kamili kutokana na
kuweko kwa jamii mbalimbali na falme ndogondogo zilizoungana na baadaye kuwa na
mataifa makubwa mawili yaani Upper Egypt na Lower Egypt au Delta Nile maendeleo
haya yalitokea karne nne kabla ya Kristo, mwaka wa 3200 baadaye falme hizi
mbili ziliungana na kuwa ufalme mmoja chini ya watawala waliojulikana kama
farao
·
Kutokana na ugunduzi wa chuma uliokuweko miaka
mingi wamisri waliweza kuendeleza teknolojia ya vifaa mbalimbali kwa kilimo
huku wakiwa na kiu ya ujuzi na maarifa na sanaa na taaluma mbalimbali, Misri
ilipata neema ya kuwa na watu wengi, Uongozi imara na kukua kwa maarifa,
wamisriwalikuwa na maarifa makubwa ambayo mengina yanatumika na ulimwengu huu
wa leo tulio nao:-
Kulikuwa na ujuzi wa kuandika katika magombo ya
karatasi ziitwazo “papyrus”
Walikuwa ndio watu wa kwanza kugundua na kutumia
kalenda yenye siku 365
Walikuwa na ujuzi wa maswala ya nyota na unajimu
Uwezo mkubwa wa uhandisi na ujenzi kwa kutumia
Mawe na ujuzi wa kutumia shaba na dhahabu, walikuwa na ujuzi wa Mathematics na
Geometric
Wamisri walikuwa hodari katika maswala ya
upasuaji na utabibu na hata kutunza maiti isiozekwa muda mrefu
Tawala za kisiasa zenye nguvu za kifarao ambazo
zimedumu kwa zaidi ya miaka 3000 inasemakena ya kuwa Misri ndio taifa
lililojiunda katika mfumo wa taifa na maendeleo kwa muda mrefu zaidi kuliko
yote duniani
Kutokana na utaalamu huo waliweza kuwa na Jeshi
kali lenye silaha na ujuzi wa kutumia farasi na wanyama wengineo
Utawala wa farao inaaminika kuwa ulidumu kwa
miaka 3200 KK mpaka 352KK, kabla ya Kristo.
Hata hivyo kiroho Misri waliabudu miungu mingi
sana miungu mikuu ilikuwa karibu kumi na Pharao mwenyewe na ukoo wake
alihezabika kama uzao uliotoka kwa mungu hivyo farao alikuwa mungu
Ni katika mazingira haya ni wazi
kuwa uwezo wa Misri ulikuwa mkubwa sana, na wenye fahari kubwa sana hakuna
utawala ungeweza kuingo’oa Misri ni katika mazingira kama hayo Musa alikuwa na
uelewa kamili kuwa jambo ambalo Munguanamtaka akalifanye lilikuwa gumu na
lisilowezekana kamwe,Kumbuka maneno ya Musa “MUSA AKAMWAMBIA MUNGU, MIMI NI NANI, HATA NIENDE KWA FARAO, NIKAWATOE
WANA WA ISRAELI WATOKE MISRI” lakini
wakati huo huo wana wa Israel wanafanyika kuwa watumwa katika misri na wanalia
na kutaka ukombozi katika mazingira yasiyowezekana! Hili lilikuwa jambo gumu
sana Biblia inasema hivi katika Kutoka
2:23-25,
“Hata baada ya siku zile nyingi
mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa,
wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. 24. Mungu
akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na
Isaka na Yakobo. 25. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia”.
Ni muhimu kufahamu mazingira na
Lugha ya kibiblia ni vema ikaeleweka wazi kuwatoa Israel Misri halikuwa jambo
jepesi, haikuwa hadithi ya kupendeza watu tu ulikuwa ni utendaji wa Mungu ulio
mkubwa sana ulikuwa ni mkono wa Mungu uliohodari!
Biblia ina maneno kadhaa kuhusu
kutolewa kwa wana Israel Misri ziko lugha kama
Kutoka 13:3 “ …Kwa
kuwa bwana aliwatoa Mahali hapa(Misri) kwa
nguvu za mkono wake…” Unaona!
Kutoka 7:
4-5…Nitaweka mkono wangu juu ya
Misri na kuyatoa majeshi yangu…watoke Misri kwa hukumu zilizo kuu na wamisri
watajua kuwa ndimi Bwana! Unaweza Kuona!
Mungu hangeweza kutafuta utukufu
kwa kitu cha Hovyo hovyo,Misri ilikuwa na uwezo mkubwa na Mungu alitaka
kuonyesha uweza wake ulio mkuu ili yamkini hata wamisri wajua ya kuwa Mungu
ndiye Bwana!
Ni kwa sababu hii Mungu aliamua
kuacha kiti chake cha Enzi mbinguni na KUSHUKA! Ili aje kuwaokoa wana wa Israel
Msomaji wangu mpendwa wote tunafahamu uweza wa Mungu ni mkuu na kuwa Mungu yuko
mahali pote kwa wakati mmoja hata hivyo tunaambiwa kuwa makazi yake makuu ni
mbinguninlakini katika mazingira Fulani HUSHUKA apate kuleta msaada kwa
wanadamu,
Inawezekana unapitia wakati
mgumu, unaugua, na unalia unaliona tatizo lako katika ndoa yako, kazini,
shuleni na kadhalika, kuwa ni kubwa
nataka nikuhakikishie kuwa Mungu amesikia kilio chako na hawezi
kuvumilia tena na ili dunia ijue ya kuwa Yeye ni Bwana atanyoosha mkono wake
ulio hodari kukuokoa ataacha makao yake kuja kushughulikia Upweke ulio nao,
utumwa ulionao, atashughulika na wewe na kukuponya na kukuokoa na kukupa kila
unachomlilia
Hatakama adui amejenga ngome,
ameendelea kitaalamu kama Misri ana miaka Miingi na ujuzi mkubwa Mungu kwa
neema yake atashughulika na kila kinachokusumbua nawe utaimba Bwana ni Nuru
yangu na wokovu wangu Nimuogope nani? Kama alivyowaokoa Israel atakuokoa wewe
nawe!
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni