WAAMUZI 9:1-6, 7-15
Biblia Inasema katika Mistari hii
ya msingi “1. Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda Shekemu kwa ndugu za mama
yake, akanena nao, na wote waliokuwa wa nyumba ya baba ya mama yake, akasema, 2. Haya, neneni tafadhali
masikioni mwa waume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo jema kwenu,
kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, watawale juu yenu, au
kwamba mtu mmoja atawale juu yenu? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na
nyama yenu. 3. Hao ndugu za mama yake
wakanena habari zake masikioni mwa hao watu wote wa Shekemu maneno hayo yote;
na mioyo yao ikaelekea kumwandama Abimeleki; kwa kuwa walisema, Huyu ni ndugu
yetu. 4. Wakampa vipande vya fedha sabini vilivyotoka katika nyumba ya
Baal-berithi, na kwa fedha hizo Abimeleki akaajiri watu wapuuzi mabaradhuli,
wafuatane naye. 5. Kisha akaenda nyumbani kwa babaye huko Ofra, akawaua
nduguze, hao wana wa Yerubaali, watu sabini, akawaua juu ya jiwe moja; lakini
Yothamu, mwana mdogo wa Yerubaali, alisalia; kwa maana alijificha. 6. Kisha hao
watu wote wa Shekemu wakakusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na
kumtawaza Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo
katika Shekemu. “
7. Kisha walipomwambia huyo
Yothamu, yeye akaenda, akasimama juu ya kilele cha kilima cha Gerizimu, akapaza
sauti yake, akapiga kelele, na kuwaambia, Nisikieni mimi, enyi watu wa Shekemu,
ili kwamba Mungu naye apate kuwasikia ninyi. 8. Siku moja miti ilitoka ili
kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu
yetu. 9. Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu
mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti?
10. Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu. 11. Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache
utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti? 12. Kisha miti ikauambia mzabibu,
Njoo wewe, utawale juu yetu. 13. Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai
yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya
miti? 14. Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu
yetu. 15. Huo mti wa miiba ukaiambia
miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli, basi njoni
mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na
kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.
Moja ya mahitaji makubwa ya
wanadamu na watu wa Mungu kokote duniani ni kuwa na “ KIONGOZI MTUMISHI” Viongozi watumishi ni watu
wanaojishughulisha na kutoa huduma yenye kuwafanya watu waliokataliwa kuwa na
Heshima na kamwe wao wenyewe hawajishughulishi na kuitafuta heshima, Dunia ya
leo ina tatizo kubwa sana la aina hii ya viongozi ni adimu mmno na hawapatikani
kirahisi
Kitabu cha waamuzi ni kitabu cha
uongozi wa mpito kutoka Yoshua kuelekea kuwa na Wafalme, Katika kipindi hiki
Mungu mwenyewe aliwaongoza Israel akitumia viongozi walioitwa waamuzi hawa
walikuwa mahakimu na viongozi wa kijeshi na washauri wa taifa viongozi hawa
waliinuliwa na Mungu mwenyewe kwa nyakati tofautitofauti
Katika kisa tulichokisoma leo
katika Mistari ile pale Juu kuna maswala mengi muhimu ya kujifunza kuhusu
kanuni za uongozi wa kawaida na kiroho hasa kupitia Muamuzi aliyeitwa Abimeleki
1. Uongozi
hautafutwi kwa fitina na tamaa (Waamuzi 9:1-6)
Biblia
inatufundisha kuwa katika maswala ya uongozi wa kawaida na wa Kiroho namna mtu
anavyoingia au anavyotafuta namna ya kuingia madarakani inatupa ishara za
msingi sana na kutuelekeza kuwa namna anavyoingia ndivyo atakavyotoka
Uongozi wa
Kiroho na wa kawaida unatoka kwa MUngu na kwa kawaida hauendani na matakwa ya
kibinadamu, Abimeleki aliingia Madarakani kwa tama yake mwenyewe na sio kwa
mapenzi ya Mungu, aliingia kwa mauaji ya kuua ndugu zake, Kwa ujuzi wa hali ya
juu na Hekima watu waelewa huwa hawatamani madaraka ya juu na mara nyingi
hukataa majukumu ya kiutawala sikun zote Mungu anapowaita, hawathubutu hata
kidogo kuyachukua kwa nguvu, kwa hila au kwa kampeni chafu au kwa kusukumwa kwa
mtu mwingine ili wao waingie (1Samuel 24:1-6,26:7-11). Daudi alikuwa na uelewa
wa hali ya juu sana , kuwa aina yoyote ya kutwaa uongozi kwa fitina utakufanya
uishie kwa fitina Abimeleki hakuielewa kanuni hii lakini akiongozwa na tama na
uchu wa madaraka na utukufu wa wanadamu alikuwa radhi kuua wengine ili yeye awe
Kiongozi, Msomaji wangu mpendwa Je hujawahi kuona watu wa aina hii ambao
walipokuwaq nje ya uongozi na hata walipoingia madarakani hawana kazi nyingine
zaidi ya kuchafua, kuponda na kuharibu watu wengine ili wao waonekane kuwa Bora
zaidi? Viongozi wa aina hii hugombana na kila mtu hata wale ambao hawawawazii
mabaya wao huwaponda na kuwaua!
2. Watu
wenye Hekima hawatafuti Utawala (Waamuzi 9:7-15)
Maneno ya Yotham
na mfano wake unatufundisha kanuni nyingine kubwa sana za huduma za uongozi wa
kawaida na Kiroho Daniel 4:17 Utawala hutoka kwa Mungu na Mungu huwapa watu
wanyenyekevu!
Jothamu alitoa
mfano wa miti iliyokataa uongozi
a.
Mzeituni
Waamuzi 9:8-9 Mti -uliohusika kupaka watu mafuta
b.
Mtini Waamuzi 9: 10-11 ulitumika kufunika uchi
kwa Adamu na Eva na matunda
c.
Mzabibu Waamuzu 9: 12-13 Uponyaji na
kuchangamsha mwili na Roho
Miti hiiyohapo
juu ilitumika kuleta Heshima kwa wanadamu na ilikataaa maswala ya utawala, ni
miti iliyotumika kuleta heshima kwa wanadamu na iliridhika na kazi hizo, miti
hii ni kimbilio na imetumika kurejesha heshima kwa wanadamu
kinabii miti hii huzungumzia
- 1. Mzeituni- wokovu wa Israel Warumi 11
- 2. Mtini Taifa la Israel Mathayo 24
- 3. Mzabibu - Hali ya kiroho ya Israel Isaya 5
Baba yake
Abimeleki Gideon aliwaokoa watu waliokuwa wamegandamizwa katika utumwa wa
wamidian, waliokuwa wamegandamizwa kwa uchungu, alitumwa na Mungu kuwakomboa
Waamuzi 6:11-14, Baada ya kuifanya kazi hiyo na kuitimiza watu walitaka
kumfanya kuwa Mfalme lakini alikataa Waamuzi 8:22-23 Gideoni alielewa kuwa
Jukumu lake kubwa ni kuwaletea wanadamu Heshima na sio kuwatawala alijua kuwa
swala la utawala ni la Mungu, yeye alikuwa ni mfano wa Miti ile yenye hekima
3. Kutiwa
mafuta kwa mti wa Miiba Waamuzi 9:14-15
Baada ya miti
mingine kukataa utawala Mti wa miiba (Abimeleki) aliamua kutawala sawa na mfano
wa Yotham waamuzi 6:14
Mti wa miiba
kihistoria ni mti wa laana, ulikuja duniani kama matokeo ya dhambi na kama
adhabu kwa wanadamu walioasi ni mti usio na matunda yenye manufaa kwa wanadamu,
ni mti unaojinufaisha wenyewe, hauwezi hata kutoa kivuli lakini unajiamini, una
majigambo na kiburi na haujali kuwa unatoa shida kwa wengine na hudhalilisha
wanadamu, wakati wa Kusulubiwa kwa Yesu Mti wa Miiba ulitumika kumuumiza Kristo
kichwani na kumdhalilisha kama mfalme asiyena utukufu kwa wayahudi, Mti wa
miiba ukichomwa moto huwaka kwa haraka sana na kusababisha madhara kwa miti
yote
Taifa na kanisa
ni lazima liwe makini na aina hii ya viongozi, kwamba tunachagua na kuweka
viongozi wa aina gani ni lazima tumuombe Mungu atupe viongozi watakaotujali na
kurudisha heshima ya wanadamu
Yesu Kristo ni
Mfano katika Viongozi wakubwa sana Duniani
·
Hakuhitaji Kanisa ili awe Mchungaji nalikuwa
Mchungaji tayari
·
Hakuhitaji Darasa ili awe mwalimu lakini watu
walimsikiliza
·
Hakupokonya Hospitali ili awe mganga mkuu lakini
watu walimfuata ili awaponye
·
Hakupindua ufalme wa Mtu lakini watu walitaka
kumfanya kuwa mfalme na ndivyo alivyo
·
Kiongozi mzuri hawi mzuri anapokuwaq madarakani,
ni kiongozi tu hata asipokuwa madarakani
·
Kiongozi mwema wakati wote huwa ni kimbilio la
wanyonge na wenye madeni 1samuel 22:1-2
·
Kristo yesu alikuja Duniani kuleta Heshima kwa
wanadamu waliokataliwa na kudharaulika, hakuwa na ubaguzi na watu walimpenda
Viongozi ambao
ni mti wa miiba huendeleza mafarakano chuki na wivu na kila mtu huwa mbaya
kwake hata wale waliomuunga mkono huwageuka na kuwajeruhi
Kila mtu na
ajipime mwenyewe kuwa Yeye ni kiongozi wa aina gani na uhusiano wako na
wanaokuzunguka ukoje jihoji je unaua wengine na kuwabomoa kwa maneno eti ili
wewe uonekane kuwa Bora zaidi? Una wivu wenye uchungu? Unapenda Heshima na
hutaki kushughulishwa na mabo manyonye ? Mungu atupe neema ili tusiwe kama mti
wa Miiba katika jina la Yesu
Mkuu wa Wajenzi
Mwenye Hekima
Rev. Innocent
Kamote.
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni