Wengi wetu tutakuwa tunafahamu kuwa Mungu wetu ana tabia ya uaminifu na mkweli anapokuwa ameahidi jambo ni muhimu kufahamu kuwa atalifanya (2 Koritho 1;20,)Biblia inasema hivi:-
“Maana
ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni
Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.”
Tabia za Mungu kamwe haziwezi
kufananishwa na za wanadamu ambao wao hugeuka geuka kwa sababu ya kigeugeu
(Yakobo 1;17)Biblia inasema hivi:- “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili,
hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli
cha kugeuka-geuka.”
Kwa msingi huo basi hatupaswi hatupaswi kumdhani Mungu kuwa ni kama
mwanadamu yeye anapohaidi au kusema ni lazima atatenda na kulifikiliza na kamwe hawezi kujuta kama
mwanadamu kuwa kwanini alihaidi YEYE SI
MTU HATA ASEME UONGO Hesabu 23;19,katika
kujifunza kwetu kuhusu uaminifu wa Mungu leo tutaangalia mfano wa maisha ya
Yusufu tangu Mungu alipomuahidi kwa ndoto kuwa atawatawala ndugu zake Hali ilikuwa tofauti kana kwamba ndoto za
Yusufu zinakwenda kupotelea mbali je mambo yalikuaje? Miaka kumi na mitatu
ilipita na ahadi za Mungu zikatimizwa angalia mchoro huu.
Maelezo kutoka katika picha ya
Grafu ya maisha ya Yusufu
·
Mwanzo
37;5-11- Yusufu alipewa Ndoto Na Mungu kuwa atakuwa Kiongozi mkubwa
kiasi ambacho Nduguze watamuinamia
·
Mwanzo
37;18-22 – Ndugu wa Yusufu kwa wivu uliosukumwa na Ibilisi walitaka kumuua
·
Mwanzo
37;26-27- Mungu alimuokoa Yusufu na Kifo kwa wazo la Yuda la kumuuza Ndugu yao
·
Mwanzo
39;2-6 - Yusufu alinunuliwa na Potifa
Kamanda wa Jeshi la farao na kuwa mkubwa
·
Mwanzo
39;7-20 - Majaribu Makubwa yalimpata kwa
kusingiziwa kubaka na akafungwa
·
Mwanzo
39;21-23 - Mungu aliyatunza maisha yake
Gerezani akawa kiongozi wa wafungwa
· Mwanzo 41;40,42,42;5-6,43;26 – Mungu aliiitimiza
Ndoto ya Yusufu Na akawa mkubwa na nduguze walimsujudia ilichukua miaka 13 kwa
ndoto ya Yusufu kuwa kweli, Mungu alitunza ahadi yake Mungu si Mtu hata aseme
uongo
Kijana Yusufu akiwa anatupwa shimoni kwa kusudi la mkuuawa, na kijana Yusufu akiwa anauzwa utumwani
Yusufu akisimikwa kumsaidia farao kama makamu wa rais wa Taifa kubwa Duniani nyakati hizo
Mambo yatupasayo Kufanya
1. Kuendelea Kumuamini Mungu ( Yusufu alimuamini Mungu katika maisha yake)
2. Kuendelea kuwa mwaminifu Yusufu hakutaka kumtenda Mungu dhambi ambazo zingeweza kuharibu Ndoto yake, hata ingawa Mungu ni Mwaminifu katika upande wetu sisi nasi tunahitaji kutunza uaminifu wetu kwake kusudi aweze kutubariki
3. Ni lazima tuwe wavumilivu hakuna ahadi ya Mungu ambayo haitatimizwa kwetu, lakini kwa uvumilivu tutazipata ahadi, ni lazima tuwe kama wakulima ambao huvumilia tangu mvua ya kwanza
Waebrania
6:13-18 "13. Kwa maana Mungu, alipompa
Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa,
aliapa kwa nafsi yake, 14.akisema, Hakikayangu kubariki nitakubariki, na
kuongeza nitakuongeza. 15. Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. 16.
Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa
mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha. 17. Katika neno
hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri
yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; 18. ili kwa vitu
viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo,
tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale
yawekwayo mbele yetu;"
Yakobo 5:7-8."7. Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. 8. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni