Jumatatu, 27 Februari 2017

Mkono wa Bwana!


Mstari wa Msingi: Isaya 53:1Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”


Kware kama wanavyoonekana Pichani ni ndege watamu sana na wenye afya ya ajabu 

Utangulizi:

Neno mkono linapotumika katika maandiko humaanisha utendaji au uweza, Na tunapoona neno Mkono wa Mungu moja kwa moja humaanisha uweza na utendaji wa Mungu, yako mambo kadhaa katika maisha yetu hayawezi kufanikiwa kama mkono wa Mungu hautakuwa juu yako ama kuwa pamoja nawe, Katika maandiko tunamuona Naomi akilia akiamini kuwa alipatwa na mikasa mbalimbali mibaya kwa sababu Bwana ameondoa mkono wake juu yake 

(Ruthu 1:11-13) “Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, mrejee; kwani kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume;  je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa Bwana umetoka juu yangu”.  
     
kwa msingi huo Nyakati za Biblia watu wengi waliofanikiwa walifahamu kuwa mkono wa Bwana uko pamoja nao, Hakuwezi kuwa na mafanikio ya aina yoyote kama Mkono wa Bwana ukitupungukia, lakini uko ushindi mkubwa sana kama Mungu akiunyoosha mkono wake kutenda jambo.

Uweza wa mkono wa Bwana

·         Mkono wa Mungu ukinyoosha kila kilicho kigumu kinashughulikiwa Kutoka 3:19-20 Biblia inasema hivi “19. Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu. Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.” 

·         Mkono wa Bwana ukinyooshwa hakuna jambo gumu la kumshinda Hesabu 11:4-15, 18-23, 31-32. “4. Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N'nani atakayetupa nyama tule? 5. Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; 6. lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. 7. Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola. 8. Watu wakazunguka-zunguka na kuikusanya, kisha wakaisaga kwa mawe ya kusagia, au kuitwanga katika vinu, kisha wakaitokosa nyunguni, na kuandaa mikate; na tamu yake ilikuwa kama tamu ya mafuta mapya. 9. Umande ulipoyaangukia marago wakati wa usiku, hiyo mana ilianguka pamoja nao. 10. Basi Musa akawasikia watu wakilia katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema yake; na hasira za Bwana zikawaka sana; Musa naye akakasirika. 11. Musa akamwambia Bwana, Mbona umenitenda uovu mimi mtumishi wako? Kwa nini sikupata neema machoni pako, hata ukanitwika mzigo wa watu hawa wote juu yangu? 12. Je! Ni mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote je! Ni mimi niliyewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto anyonyaye, uende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao? 13. Nipate wapi nyama ya kuwapa watu hawa wote? Kwani wanililia, wakisema Tupe nyama, tupate kula. 14. Mimi siwezi kuwachukua watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa kunishinda. 15. Na kama ukinitenda hivi, nakuomba uniulie mbali, kwamba nimepata fadhili mbele ya macho yako; nami nisiyaone haya mashaka yangu.”

“18. Kisha uwaambie watu hawa, Jitakaseni nafsi zenu kabla ya kesho, nanyi mtakula nyama; kwa maana mmelia masikioni mwa Bwana, mkisema, Ni nani atakayetupa nyama, tule? Maana huko Misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo Bwana atawapa nyama, nanyi mtakula. 19. Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala siku kumi, wala siku ishirini; 20. lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hata hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa Bwana aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani? 21. Musa akasema, Watu hawa ambao mimi ni kati yao, ni watu sita mia elfu waendao kwa miguu; nawe umesema, Nitawapa nyama, ili wale muda wa mwezi mzima. 22. Je! Makundi ya kondoo na ng'ombe yatachinjwa kwa ajili yao, ili kuwatosha? Au samaki wote wa baharini watakusanywa pamoja kwa ajili yao, ili kuwatosha? 23. Bwana akamwambia Musa, Je! Mkono wa Bwana umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako, au sivyo.”

“31. Kisha upepo ukavuma kutoka kwa Bwana, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao ukawaacha wakaanguka karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, na kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, kuizunguka, nao wakafikilia kiasi cha dhiraa mbili juu ya uso wa nchi. 32. Watu wakaondoka mchana huo wote, na usiku huo wote, na siku ya pili yote, kuwakusanya hao kware; yeye aliyepata ya upungufu kuliko wenziwe alipata kiasi cha homeri kumi; nao wakawaanika wote kando-kando ya kambi kuizunguka pande zote.”            

Dhiraa mbili  (2 Cubic )ni sawa na Futi Tatu kwenda juu au mita moja, na mwendo wa siku nzima ni sawa na KM.

Siri ya Mkono wa Bwana

·         Isaya anauliza Ni nani aliyesadiki Habari tuliyoileta na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Kisha isaya anaeleza habari za Yesu Kristo na mateso yake ambayo yameleta ukombozi mkuu kwa wanadamu

·         Ni wazi kuwa Biblia inapozungumzia juu ya mkono wa Bwana inaeleza siri iliyo wazi kuwa Yesu ndio mkono wa Bwana ni wazi kuwa ukiiamini injili, Habari njema na kuiamini kazi iliyofanyika msalabani kwamba ni kwaajili yetu, na kuwa Yesu ametunukiwa jina kuu kuliko yote nay a kuwa tukiliitia jina lake tunaokolewa

·         Hakuna jambo litakalokuwa Gumu kwetu, hakuna jambo linaloshindikana Mkono wa Bwana utafunuliwa kwako tu, mweke Yesu mbele, kubali kazi zake usimkatae Yesu utauona uwezo wake, Musa alilia alikata tamaa wanataka Nyama, nitoe wapi nyama Kama nimepata fadhili machoni pako inatosha Heri nife, inawezekana umefikia pointi ngumu sana katika maisha yako, kwamba sasa Mungu uko wapi, kwanini haya yanatokea, heri uniuwe kabala ya aibu hii, yatosha baba lakini nakuthibitishia leo kuwa Mkoo wa Bwana haujapunguka urefu wake

·         Yeye alisema niite nami nitakuitika na kukuonyesha Mambo makubwa na Magumu usiyoyajua

Kizuizi kwa Mkono wa Bwana
·         Isaya 59:1-2 1. “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2. lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”. 

 Biblia inaonyesha wazi kuwa ni dhambi tu ndio inaweza kumfanya Mungu aionyeshe mkono wake na ni maovu tu ndio yanayoweze kumfanya asisikie sasa dawa ya hili ni rahisi, lazima tukubali kutubu na Yesu anatusubiri na tukiungama yeye ni mwaminifu na atatusamehe kabisa 1Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”

Na Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.

Hakuna maoni: