Zaburi 137:5,6 “Eee Yerusalem nikikusahau
wewe Mkono wangu wa kuume na usahau, Ulimi wangu na uganadamane na Kaakaa la
kinywa changu nisipokukumbuka, Nisipoikuza Yerusalemu zaidi ya furaha yangu
iliyo kuu”
Pichani Jiji la yerusalem Maarfuru kama old Jerusalem ikionekana katika utukufu wake
UMUHIMU WA KUIPENDA ISRAEL. (JERUSALEM)
Mji wa Yerusalem ambao ni
mji mkuu wa Israel ni mji muhimu sana katika maswala ya kisiasa kiimani na
kiusalama mjii huu ni picha ya mji halisi ulioko peponi au mbinguni ambao ni
makao makuu ya serikali ya Mungu Mbinguni,
Mungu ana mji ulioko Juu
mbinguni na mji huu unaitwa Yerusalem Wagalatia
4:25- 26 “Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na
Yerusalem wa sasa kwa kuwa anatumika pamoja na watoto, Bali Yerusalem wa juu ni
mwungwana naye ndiye mama yetu sisi”
Katika maandiko hayo Paulo mtume
anaonyesha kuwa kuna Yerusalem ya Duniani naya mbinguni miji yote hii ni makao
makuu ya serikali ya Mungu aliye hai, Yerusalem iliyoko Israel ni makao makuu
ya Mungu Duniani na Yerusalem ulioko mbinguni ni makao makuu ya serikali ya
Mungu.
Mji huu ni wa muhimu sana
wengi waliotambua siri ya umuhimu wa mji huu wanaupenda na watakatifu
waliotutangulia waliomba wasiisahau Yerusalem Zaburi 137:5,6 “Eee Yerusalem nikikusahau wewe Mkono wangu wa kuume na usahau,
Ulimi wangu na uganadamane na Kaakaa la kinywa changu nisipokukumbuka,
Nisipoikuza Yerusalemu zaidi ya furaha yangu iliyo kuu”
unaweza kuona Yerusalemu ni zaidi ya furaha ya
watakatifu
Kama ilivyo kwa almasi
katika kiti cha sofa ndivyo ulivyo mji wa Yerusalem mji huu ukokatikati ya
vilele vya Safu ya milima ya Yudea (Uyahudi) na kwa ujumla ni katikati ya Dunia
kijiografia, maisha na hatima ya wanadamu wote duniani iko au imefungamanishwa
na mji huu wa kipekee, Tangu wakati wa Ibrahim nabii Israel imekuwa ni makao
makuu ya ukombozi wa Mwanadamu, wakati huu dunia inapoelekea ukingoni Israel
inaanza kuwa ngome tena ya kufunua makusudi ya Utawala wa Mungu duniani na
ngoma ya kuchezwa mbele ya wanadamu na malaika.
Wakristo na hata wasio
wakristo wanapaswa kuwa na uelewa wa kutosha Kuhusu Israel na Jerusalem na
uhusiano wetu kiimani Biblia inaonyesha upekee wa hali ya juu kuhusu Israel na
Yerusalem na kukosa ufahamu huu kunaweza kutunyima Baraka za kipekee
zilizofichwa kuhusu inchi hii na mji huu
Nchi yangu na Mji wangu!
Zaburi ya 21:1 “Biblia inasema Nchi na
vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. “ unaweza kuona Biblia inatufundisha kuwa nchi na vyote
viijazavyo ni mali ya Bwana na Dunia yote na watu wote, hivyo kuna uweli kuwa
kila inchi ni ya Mungu na kila taifa ni la Mungu na watu wote ni wa Mungu
katika ujumla wake, lakini katika upekee wake Israel na mji wake mkuu Yerusalem
ni Mji mtakatifu wa Mungu na ushahidi wa kimaandiko upo kuthibitisha kuwa kuna
utofauti kwa nchi hii na mji huu
1.
Unaitwa mji Mtakatifu “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako
mazuri, Ee Yerusalemu, MJI MTAKATIFU; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako
Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.” Biblia
inasema katika Isaya 52:1
2.
Yesu mwenyewe aliupenda mji huu licha ya kuutolea Machozi katika
mafundisho yake aliuita mji wa Mfalme mkuu angalia Mathayo 5:35 “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila
mtimizie Bwana nyapo zako; 34. lakini
mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi
cha Mungu;35. wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa YERUSALEMU,
KWA MAANA NDIO MJI WA MFALME MKUU” Yesu
anatambua kuwa mji huu ndio makao yake makuu, mfalme mkuu ni yeye, mji huu ni
wake unawezaje kusema kuwa unampenda Yesu kisha unachukia mji wake na serikali
yake na makao yake makuu?
3.
Kiti cha enzi cha Mungu Yeremia
3:17 Wakati
ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha Bwana; na mataifa yote watakusanyika
huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la Bwana; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi
wa moyo wao mbaya.”
4.
Mungu aliahidi kuliweka Jina lake pale Yerusalem milele soma 2Nyakati 33:4 Biblia inasema ”Akajenga madhabahu katika
nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu litakuwako
jina langu milele”
5.
Maandiko yako wazi kuwa Mungu anajivunia Yerusalem angalia Zaburi 87:1-3 Biblia inasema “Msingi wake upo Juu ya
milima mitakatifu. Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za
Yakobo. Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu.”
6.
Yerusalem ni sababu ya Furaha Isaya
65:19 Nami
nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia
haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.”
7.
Isaya alisema kwaajili ya Yerusalem yaani sayuni sitanyamaza Isaya 62:3 “1. Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu
sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa
iwakayo. 2. Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu
wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. 3. Nawe
utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa
Mungu wako.” Unaweza kuona jinsi mji huu uliyounganishwa na shughuli za
kinabii na kiimani wote waliokuwa wakimpenda Mungu kwa dhati waliipenda Yerusalem
kwa dhati vilevile
8.
Unabii unaonyesha kuwa siku za mwisho watu wengi sana
wataitembelea Israel yaani wataitembelea Yerusalem makundi kwa makundi Isaya
2:3 “1. Hili ni
neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu. 2. Na
itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya
milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi
makundi. 3. Na mataifa mengi
watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu
wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake
maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. 4. Naye
atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao
watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua
upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. 5. Enyi wa
nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana”.Unaona unabii wa Isaya watu wote wataiendea Yerusalem huko ndiko
itokako amani ya watu wote huko ndio asili nya Neno la Mungu, huku ndio asili
ya mafundissho yote Yerusalem Yerusalem!
Mungu hajamaliza na
Yerusalem ya Asili
Ni muhimu kwa kila mkristo kuwa
na uelewa huu kuwa Mungu hajamaliza kazi yake na mji huu Yerusalem wa Duniani,
nasema hivi kwa sababu mtu anaweza kujenga Hoja za kimaandiko kuwa isis kama
Ibrahimu tunautazamia mji wenye misingi ambao mwenye kuujenga na kuubuni ni
Mungu, akiwa na maana ya Yerusalem ya Mbinguni
sawa na Waebrania 11:10
ambapo Biblia inasema “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali
pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 9. Kwa imani alikaa
ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika
hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10. Maana
alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni
Mungu.”
Maandiko yanaonyesha kuwa Ibrahim kwa Imani alikuwa
akiutazamia Mji wa Mbinguni kwa vyovyote vile Yerusalem wa Mbinguni, Pia
tunaweza kuona msisitizo wa Paulo Mtume kwa Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko
tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;” na tunaambiwa kuwa
Yerusalem wa Mbinguni ndio mama wa yote Waebrania
12:22 na kuwa kila aliyeamini ameungamanishwa na Sayuni ya Mbinguni au
Yerusalem ya Mbinguni “Bali ninyi
mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na
majeshi ya malaika elfu nyingi,”
Na Kama haitoshi Yesu mwenyewe alionyesha kuwa ndani ya agano jipya watu
wangefurahia uwepo wa Mungu katika roho na kweli ikiwa na maana ya ibada halisi
haitategemea Hekalu Yerusalem wala mlima Fulani kwa vile Mungu anataka
kuabudiwa katika roho na kweli angalia Yohana
4:21-24 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa
inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi
tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja,
nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli.
Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa
kumwabudu katika roho na kweli”.
Kama utaviangalia kwa makini vifungu
vyote vya maandiko hapo juu unaweza kudhani kuwa Mungu hana kazi tena na mji wa
Yerusalem wa sasa na Taifa la Israel, unaweza kufikiri kuwa makusudi yake
yamekwisha
Lakini turudi tena katika Mathayo 5: 35 Tena
mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo
zako; 34. lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana
ndicho kiti cha enzi cha Mungu;35. wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea
miguu yake; wala kwa YERUSALEMU, KWA MAANA NDIO MJI WA MFALME MKUU” Yesu anaonyesha kuwa
tusiape kwa Yerusalem kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu hii ina maana gani kwa
nini asiseme kwa vile ulikuwa mji wa mfalme mkuu? Kwanini Mungu Hajamaliza kazi
yeke na mji huu wa Yerusalem wa asili
Yesu
alisema Yerusalem utakanyagwa na mataifa kwa kitambo Luka 21:24 “…..Na
Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”
“Kama
Maandiko yametoa nafasi ya kukanyaga Israel na Yerusalem naamini ni vema
wakristo tukaitumia nafasi hiyo ya kwenda Israel na kutembelea nchi hiyo ya
kipekee kwani utakuja wakati itakuwa ngumu sana kuitembelea Israel hata kama
utakuwa na uwezo huo” huu ni mtazamo wa kinabii wa mkuu wa wajenzi hapa.
Maneno hayo ya
kinabii yanamaanisha kuwa mataifa wataukanyaga kwa muda na hatimeye mjii huu
utarejeshwa katika utukufu wake , Yesu Kristo atakaporudi katika utukufu wake
atasimamisha serikali yake kutoka mji huu na kutawala akiwa MFALMA WA WAFALME
NA BWANA WA MABWANA Kutoka Israel Yerusalem angalia
Zekaria
14:4, 9Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya
mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa
Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi;
litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande
wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. , Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana
atakuwa mmoja, na jina lake moja”
Kwa hiyo iko wazi
kuwa mjii huu bado uko na uhusiano mkubwa na maswala ya kiimani ni wazi kuwa
kuna Baraka za kimungu kama tunautakia mafanikio, na hata ingawa kunaweza
kusiwe na Uhusiano wa kiibada na Israel au Yerusalem lakini huwezi kukataa kuwa
kuna ahadi za mafanikio kwa wanaoiombea Israel na wamnaoutakia mema Yerusalem
Utakieni Yerusalem
Amani!
Zaburi
ya 122 :6-9 inasema hivi:- “Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe
wakupendao;. Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba
yako. Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe. Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu,
Nikutafutie mema”
Biblia inaamuru “Utakieni
Yerusalem Amani” na inaunganisha Baraka kubwa na wale waipendao Yerusalem
wafanikiwe wakupendao, Mema yataambatana na kila Mkristo na mtu aiye mkristo
anayeitakia Mema Israel na Yerusalem
Mungu anataka
tufurahi pamoja na Israel Isaya 65:18 , 19 a na 66:10-13
Biblia inasema haya
“18. Lakini
furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama,
naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. 19. Nami nitaufurahia
Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani
yake tena, wala sauti ya kuomboleza. 10. Furahini pamoja na Yerusalemu,
shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa
furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake; 11. mpate kunyonya, na kushibishwa
kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu
wake. 12. Maana Bwana asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na
utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa;
na juu ya magoti mtabembelezwa. 13. Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji,
ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu.”
Yesu aliipenda
Yerusalem kiasi cha kuulilia mji huu, Nehemia aliugua na kufunga na kuomba
kwaajili ya Yerusale, Yesu anaitamani Yerusalem mpango wake ni kuukumbatia ni
kuukusanya kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake! Mathayo 23:37 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga
kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja
watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa
yake, lakini hamkutaka! “ Yerusalem walikataa mapenzi ya Mungu kwa
kumkataa masihi na kumsulubisha nje ya mji huu, lakini Mungu anawatamani sana
Israel na ni mapenzi ya Mungu waokolewe na mjii huu kwa vyovyote vila ndio
utakuja kuwa makao makuu ya Masihi Yesu.
Siri
ya tai ya rangi ya blue katika shati Jeupe!
Kwa nini Viongozi
katika Israel na Marekani huvaa tai ya rangi ya Blue? Ngoja nikuambie siri ya tai
ya rangi ya blue na Nyekundu kwa Marekani, Bendera ya marekani ina rangi
nyeupe, Nyekundu na blue, Chama cha republican huwakilihwa na rangi nyekundu na
chama cha democratic huwakilishwa na rangi ya blue hii ni alama kubwa sana kwa
taifa lao, wanapovaa tai viongozi wao huvaa kuonyesha uzalendo wa taifa lao
katika maswala ya kitaifa
Pia kwa vile
wamarekani wana uhusiano mkubwa sana na Israel pia kuvaa tai ya blue kwao
humaanisha wazi kuipenda na kuiunga mkono Taifa la kiyahudi, Wayahudi bendera
yao ni yeupe na ina mistari ya blue na nyota ya Mfalme Daud iliwa na rangi ya
blue hivyo viongozi wa kitaifa kwao huvaa tai ya blue
Uganda bendera yao
ina rangi nyekundu,mkenya pia na nyeusi na njano, Rais Museven hupenda kuvaa
tai ya Manjano kwa vile ni rangi ya taifa lao katika bendera yao
Ukiona kiongozi wa
kitaifa katika taifa ambalo halijamwaga Damu amevaa tai nyekundu maana yake
huvaa tu bila kuzingatia amevaa kwa maana gani
Tai ya blue ikivaliwa
na mtu anayejua maandiko humaanisha wazi kuwa anaipenda Israel, scafu na
kadhalika kwa msingi huo kama unaipenda Israel katika kuonyesha mapenzi yako
kwa taifa hilo vaa tai ya blue kuna siri kubwa katika jambo hilo kwaajili ya
kuonyesha unaiunga mkono Israel
Kwa bahati njema kwa
watanzania tai ya blue pia itakuwa ni sehemu ya Bedera yetu katika zile rangi
nne mamarufu kwa hiyo tai ya blue itamaanisha uzalendo kwa taifa lako lakini
kiroho Israel, hii ni siahara nyingine ya kuipenda sayuni.
Ujumbe na Mkuu wa
wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni