Alhamisi, 23 Februari 2017

WALIO PAMOJA NASI NI WENGI KULIKO WALE WALIO PAMOJA NAO.



ANDIKO LA MSINGI: 2WAFALME 6:15-16 “.Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?  Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.”

Utangulizi:

Ni muhimu kwa kila Mkristo kuwa na ufahamu kwamba ulimwengu wa kiroho ni halisi, na kuwa kama tulivyojifunza, kwamba kuna vita vya kiroho katika ulimwengu wa roho, kwamba ziko pande mbili zinazoshindana, upande wa Mungu na Shetani na kuwa wakati mwingine vita hii hujitokeza katika hali halisi ya mwilini.

Ili ushindi wetu uweze kuwa Dhahiri,ni muhimu kuwa na uelewa wa kutosha namna na jinsi ambavyo ulimwengu war oho unavyotenda kazi, ujuzi huu wakati wote utakufanya utembee katika ushindi na kuwa mbali na hofu ya jambo lolote linalohsindana nawe.
Nabii Elisha alikuwa moja ya manabii muhimu sana katika Israel, hii ilitokana na uwezo wake mkubwa sana katika kuuona ulimwengu war oho na kujua kila kinachoendelea upande wa maadui wa Israel, kutokana na umuhimu wake siku alipougua na kukaribia kufa, mfalme alilia san asana na kusema “ Baba yangu baba yangu Gagari la Israel na Mpanda farasi wake” 2 Wafalme 13:14 Biblia inesema

Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!

Kilio hiki kilikuwa kina maanisha mtu huyu anayekufa alikuwa ni wa muhimu kwa Israel kuliko jeshi zima, Elisha alikuwa ametumiwa na Mungu sio tu kama Nabii lakini pia kama Mlinzi na mtetezi wa Izrael na Mfalme pia, Mfalme alijua kuwa kufa kwa Elisha ni sawa na kutoweka kwa Jeshi la Ulinzi la Israel kwa sababu kadhaa wa kadhaa.

·         Elisha alikuwa ni zaidi ya Idara ya Usalama wa taifa kwa Marekani, tunaweza kusema alikuwa ni zaidi ya FBI au CIA, alikuwa na uwezo wa kuona maadui na mipango yao zaidi ya rada kali sana katika Israel inayoitwa “GREEN PINE” Rada hii ina uwezo wa kuhisi hatari kwa zaidi ya KM 400, Elisha alikuwa ni zaidi ya Green Pine”


Pichani ni Rada aina ya Green Pine ambayo imegunduliwa na kuundwa na Jeshi la Israel pekee

·         Ulinzi wa Elisha ulikuwa ni zaidi ya “IRON DOME” hii ni silaha nzito yenye uwezo wa kuhisi mashambilizi ya adui na kufyatua makombora ya kudhoofisha makombora ya adui kabla hayajaleta madhara

 Pichani ni silaha aina ya Irone Dome ni silaha iliyogunduliwa Israel ina uwezo mkubwa sana wa kulinda na kuharibu mashambulizi dhidi ya silaha za adui na vituo vyao

·         Elisha alikuwa ni zaidi ya “DELILAH CRUISE MISSILE” yenye uwezo wa kupiga km 250 ikiwa na uzito wa kg 187 au “PROTECTOR USV RAFAEL” ambazo ni boti zenye uwezo wa kufanya kazi ya boti 9-11 za kijeshi na inauwzo wa kutumiwa na watu sita na kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja, umuhimu wa silaha hizo zote nzito zinazotumiwa na Jeshi la Israel kwa wakati wa sasa zilikuwa sawa na Elisha mmoja tu umuhimu wake kwa ufahamu kuhusu silaha hizo Google Top 10 Most Powerful weapons of Israel pia unaweza kupitia Defencyclopedia.com)

Pichani ni Israel Rafael Protector USV ni chombo chenye uwezo mkubwa sana na chenye kufanya kazi nyingi katika Jeshi la Israel

 Kwa nini Elisha alikuwa wa Muhimu kiasi hicho?

2Wafalme 6:8-14 Biblia inasema “Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu kitakuwapo mahali fulani. Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami. Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili. Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?, Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.  Akasema, Enendeni, mkamwangalie aliko, nipate kupeleka watu kwenda kumchukua. Akaambiwa ya kwamba, Tazama, yuko Dothani. Kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote.”

Unaposona kifungu hicho utaweza kuona umuhimu wa Elisha kwa Israel uwezo wake wa kuona mambo katika ulimwengu war oho ulimpa ujasiri mkubwa kiasi cha kuliteka Jeshi zima la madui wa Shamu, Kijana wake Elisha alikuwa haoini katika ulimwengu wa Kiroho na hiyo aliogopa sana lakini Elisha alimtia moyo asiogope

Kuna watu wengi sana wanaogopa tena wanaogopa nguvu za giza, au wanapoona mapambano ya vita za aina mbalimbali kwa jinsi ya mwili wanaogopa sana woga wao ni kama wa mtumishi wa Elisha shida yao ni kutokuujua ulimwengu wa Kiroho ulivyo

-          Mtu anaweza kuogopa Hirizi tu
-          Mtu anweza kuogopa kuwa ametumiwa njiwa
-          Mtu anwexza kuogopa milio ya Bundi tu wakati wa usiku
-          Mtu anaweza kuogopa akisikia vitu vinatembea juu ya dali au bati
-          Mtu anaweza kuogopa kusikia milio ya Mapaka
-          Mtu anaweza kuogopa kwa sababu tu ameota ndoto mbaya
-          Mtu anaweza kuogopa kwa sababu tu ya nguvu za giza au wachawi na wapiga madogoli
-          Mtu anaweza kuogopa kwa sababu ya vitisho vya aina mbalimbali duniani

Ukijujua ulimwengu wa Roho kwamba tunazungukwa na majeshi ya Malaika hutaweza kuogopa Elisha alikuwa anajua kuwa analindwa na nguvu za kupita kawaida, Malaika wenye farasi za moto walikuwa wamemzingira pande zote, ikiwa Elisha wa agano la kale alikuwa analindwa kiasi hiki sisi nasi tunalindwa na nguvu za Mungu, Zaburi 3:5-6, 27:3 Waebrania 1:14 Roho watumikao kuwahudumia wale watakaourithi wokovu wapo kutuhudumia na kutulinda hivyo hatupaswi kuogopa

 2Wafalme 6; 16-17 “Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.”
 Pichani ni silaha ya Mashambulizi iliyogunduliwa Israel iitwayo "Delilah Cruise Missile"

Mungu akikufungua macho ukaona namna unavyolindwa na majeshi ya Malaika hutaweza kuogopa Daudi akasema Jeshi lijapojipanga kupigana name Moyo wangu hautaogopa”

Maoni 6 :

Unknown alisema ...

Mungu na akubariki kwa jumbe na mafundisho mazuri.

Unknown alisema ...

Mungu akubariki sana nafurahia mafundisho yako na yanijenga sana.

Unknown alisema ...

Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu. Asante kwa mafundisho, ukweli yanibadilisha sana. Naomba kuuliza pia je, una vitabu? Asante kwa huduma hii ya Ki-Ungu, Mungu akubariki sana.

Unknown alisema ...

Bwana Yesu asifiwe sana. Asante kwa mafundisho mazuri, kwa kweli yananibadilisha sana. Asante na Mungu akubariki sana.

Unknown alisema ...

Bwana Yesu asifiwe sana. Asante kwa mafundisho mazuri, kwa kweli yananibadilisha sana. Asante na Mungu akubariki sana.

Unknown alisema ...

Bwana Yesu asifiwe sana. Mungu akubariki sana kwa mafundisho. Binafsi ninajengwa na ninabadilishwa sana na masomo haya. Asante sana Mtu wa Mungu.