Katika maandiko haya,(HESABU 13:25-33; 14:1-12,26-32),
Hesabu 14:26-32 “Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na
kuwaambia, Je! Nichukuane na mkutano
mwovu huu uninung'unikiao hata lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli,
waninung'unikiayo. Waambieni, Kama
niishivyo, asema Bwana, hakika yangu
kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;”
Hesabu 13:25-33 “Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa
siku arobaini. . Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote
wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari,
wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi. Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile
uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya
ndiyo matunda yake. Lakini watu wanaokaa
katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na
pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko. Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na
Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu
na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani. Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa,
akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali
wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu
hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya
ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili
kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani
yake ni watu warefu mno. Kisha, huko
tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi
zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.”
Hesabu 14:1-12 “1. Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu
wakatoka machozi usiku ule. Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na
Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya
Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. Mbona Bwana
anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu
watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? Wakaambiana, Na tumweke mtu
mmoja awe akida, tukarudi Misri.Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi
mbele ya mkutano wa kusanyiko la wana wa Israeli. Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa
Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena
na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili
kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika
nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini
msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula
kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi;
msiwaogope. Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa
Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote. Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu
hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara
hizo zote kati yao. Nitawapiga kwa
tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha
yenye nguvu kuliko wao.
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa ulimi wa
Mwanadamu una nguvu ya kusababisha madhara makubwa na pia kuleta uponyaji
mkubwa, kwa kuwa wanadamu wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, Mungu aliuumba
ulimwengu kwa Neno tu alitamka na ikawa, wakati wote utendaji wetu na matukio
yetu katika maisha yanatokana nay ale tunayoyazungumza Mithali 18:20-21 “Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba
mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao
waupendao watakula matunda yake”Kama hivi ndivyo ni jambo la msingi
sana kujichunga ni kitu gani tunakizungumza na kukitamka kwa vile tunaweza
kuumba jambo hilo.
Kumbuka hata wokovu wetu
unapatikana kwa kumuamini Yesu moyoni na kwa kumkiri kwa kinywa na ni kwa
kinywa tu tunaweza kuliitia jina la Bwana na kupata msaada Warumi 10:9-13 “Kwa sababu,
ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata
kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye
hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti
ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa
wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.”
Kwa msingi huo kama tunataka kuwa mbali na mauti na kama tunataka
kuleta uzima katika maisha yetu ni lazima tuwe na semi zilizo na manufaa katika
maisha yetu na hata ya wengine
Jambo la kujifunza:
Wana wa Israeli wanatumia ulimi
kuzungumza maneno kama haya "AHERI
TUNGALIKUFA KATIKA JANGWA HILI" na maneno kama "HATUWEZI".Mungu akasema
atawafanyia hivyo walivyosema na kweli walikufa katika jangwa hilo.
Kalebu Mwana wa Yefune na Yoshua
Mwana wa Nuni walisema maneno ya ushindi kama haya "TWAWEZA KUSHINDA BILA SHAKA na BWANA
YU PAMOJA NASI".
Tunajifunza juu ya makundi
mawili.Kundi la kwanza ambao ndio wengi wanazungumza maneno HASI NA YA
KUSHINDWA na kweli walishindwa.
Kundi la pili ambao ni wachache
sana wanazungumza maneno ya CHANYA YA KUSHINDA na kweli walishinda na kuingia
nchi ya ahadi.
Watu wa Mungu ikiwa Mungu
anatufanyia jambo sawa na ukiri wetu, ikiwa uzima na mauti uko katika uwezo wa
ulimi wetu, ikiwa kwa ulimi tunaweza kukiri na hata kupata wokovu ni muhimu
kwetu ,KWA KILA JAMBO TUZUNGUMZE MANENO CHANYA
YA KUSHINDA sawasawa na Neno la Mungu,NA BWANA mwenye kutushindia
atakuwa pamoja nasi kufanikisha yote kiroho na kimwili.
MANENO TUNAYOSEMA NDIYO BWANA
ANAYOTUFANYIA YAWE MEMA AU MABAYA!Maana anasema CHAGUENI HIVI LEO!(YOSHUA
24:14-15;WAFILIPI 2:13;WARUMI 8:31-32,37-39;WAFILIPI 4:13).Mungu aweke mlinzi
vinywani mwetu ili sikuzote tuzungumze maneno ya kuumba ushindi katika Jina la
Yesu Kristo.(ZABURI 141:1-3)
Ni imani yangu kuwa Tangu sasa
utatumia kinywa chako vema na kujizungumzia ushindi, acha kujizungumzia kukata
tamaa, jizungumzie mambo mema wazungumzie wengine mema Na mungu atatubariki sawasawa na ukiri wetu.
Sources. Rev.George Swenya Full
Gospel Bible Fellowship Church Tanga.
Ukarabati: Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni