Waamuzi 15:16 “Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu elfu.”
Then Samson said, "With a
donkey's jawbone I have made donkeys of them. With a donkey's jawbone I have
killed a thousand men
Ni Muhimu kufahamu kuwa ushindi
wetu katika mazingira ya aina yoyote ile na katika vita vya kiroho unatoka kwa
Mungu, Mungu alikwisha kutuahidi mapema sana katika torati kuwa atatupa
ushindi, bila kujali ni aina gani ya silaha inayotumiwa na adui, yeye anatia
moyo kuwa tusiogope wala mioyo yenu isizimie, Mungu asiyeonekana kwa macho ya
kibinadamu yuko nyuma ya watu wake kuwapa nguvu isiyoweza kuonekana na
kusababisha ushindi.
Kumbukumbu 20:1-4 “Utokapo kwenda
vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko
wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza
kutoka nchi ya Misri. Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na
kusema na watu, awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni
juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe
na hofu kwa ajili ya wao; kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda
kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.”
Mungu aliahidi kuwa atatupa
Ushindi, na kuwa ndani yetu ameweka uwezo wa kupiga watu elfu uwezo huu unatoka
kwake na sio wa mtu binafsi au kwa akili ya mtu binafsi Kumbukumbu 32:30 “Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu
kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?”
Ni wazi tu kuwa Samson alielewa
ahadi za Mungu na aliamua kutunga shairi na kutengeneza Fumbo kubwa sana la
siri ya nguvu zake kwamba ameweza kupiga watu elfu KWA TAYA LA PUNDA, lakini ukweli ulio wazi ni kuwa Samsoni
alijiliwa na ROHO WA MUNGU na ndiye
aliyempa ushindi huu na nguvu ya kupiga watu 1000
Tunajifunza wazi kuwa siri ya
ushindi wetu inatokana na NGUVU ZA ROHO
MTAKATIFU ambaye hapa Samson anamtaja kama taya la Punda, sio kweli kwamba
Samson aliwaangamiza maadui kwa Taya la punda bali nyuma ya taya la punda
ilikuweko nguvu isiyoonekana iliyomuwezesha Samson kupata ushindi
Waamuzi 15:14-20. Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana
naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya
mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake
vikaanguka mikononi mwake. Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa,
akapiga watu elfu kwa mfupa huo; Samsoni
akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu
elfu. Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena akautupa ule mfupa wa taya mkononi
mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi.Kisha akaona kiu sana, akamwita
Bwana akasema, Wewe umetupa wokovu huu kwa mkono wa mtumishi wako; na sasa
nitakufa kwa kiu, na kuanguka katika mikono ya watu wasiotahiriwa. Lakini Mungu
akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha
kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa
Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo.Naye akawa mwamuzi wa Israeli:
katika siku za Wafilisti muda wa miaka ishirini.”
Ushindi wa Samsoni haukuwa katika
mikono yake wala katika taya la punda bali ulitokana na nguvu za Roho wa Mungu
yaani Roho Mtakatifu,
Samson aliweza kusababisha
uharibifu mkubwa miongoni mwa maadui za Mungu Wafilisti, kwa kutumia Taya la
Punda huu ulikuwa ni muujiza mkubwa wenye maana ya kuwa Mungu hutumia mambo
manyonge na mapumbavu na yaliyodharaulika
ya dunia kudhihirisha Nguvu zake, kwa sababu hiyo ushindi huu ni dhahiri
kuwa haukutokana na aina ya silaha, wala mikono ya Samson Lakini alikuwa ni
Roho Mtakatifu aliyetumia Mkono pamoja na taya la punda kuleta ushindi, tunayaweza
yote katika yeye atutiaye Nguvu Wafilipi
4:13 “Nayaweza
mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Mungu anapokusudia kutupa
ushindi dhidi ya adui zetu ni lazima kuitunza ile nguvu ya asili inayotupa
ushindi nguvu hii ni Roho Mtakatifu.
Aidha ni muhimu kukumbuka
kuwa Pale “Ramoth lehi” Kulikuwa na hekalu la miungu ya kifilisti ambamo ndani
yake kulikuwa na alama ya taya la punda alama hii ilikuwa inawakilisha nguvu za
siri za miungu ya wafilisti ambao waliamini kuwa Mungu huyu aliwapa ushindi
dhidi nya adui zao, ni wazi kabisa na inawezekana kabisa kuwa watu wale 1000
waliopigwa na Samsoni huenda walikuwa ni makuhani wa miungu hiyo pale “Ramoth
lehi” Jina “Ramoth lehi” ni muungano wa Maneno mawili ya Kiebrania na wafilisti
Ramoth kwa Wafilisti ilimaanisha DRAGON
au Joka na LEHI maana yake
Palipotupwa mfupa wa Punda Taya la punda,
Nguvu ya joka iliyokuwa linaabudiwa na wafilisti katika eneo hili tendo
la Samsoni kuwapiga kwa kutumia taya la punda ilikuwa ni ishara ya wao kupigwa
na nguvu ya siri, na kwa sababu hawakuwa wametambua nguvu ya Samsoni bila shaka
wakati hu ndipo walipoanza uchunguzi wa kutaka kujua siri ya Nguvu ya Samsoni
ni nini?
Pichani Samsoni akiwa
amepiga watu wengi 1000 pale Ramoth lehi,
Samson alikuwa ametumiwa na Roho
Mtakatifu kwani nguvu za Mungu zilikuja juu yake kwa nguvu lakini maadui
hawakutambua, ndugu msomaji wangu ni muhimu ukafahamu kuwa iko nguvu ya siri
itakayosambaratisha kila anayekupinga na kukusaidia wakati nwa mahitaji yako
nguvu hii ni Roho Mtakatifu, Bwana atawasambaratisha wote wanaoshindana nawe kupitia
nguvu za Roho Mtakatifu, nguvu hii ya Mungu isiyoonekana kwa macho iliweza
kuwapa ujasiri watakatifu wote waliotutangulia na ndio itakayohusika na
inayohusika kuwashughulikia adui zako hata Leo, Kule Marekani watu fulani
hutumia alama ya vidole viwili, kwa kulaza vidole viwili vya katikati na
kusimamisha viwili, wakimaanisha nguvu ya siri nguvu hii inayowapa ushindi
inaweza kuwa ya Joka (Satanic Sign) au kwa Wakristo wanaomjua Mungu inaweza
kuwakilisha Heshima kwa Roho Mtakatifu aliyewapa ushindi dhidi ya adui zao
(Honor Sign) kwa hiyo taya la punda kwa
wafilisti ilikuwa nguvu ya siri ya Joka na kwa wayahudi taya la Punda ilitumika
kama alama ya Nguvu za siri za Roho wa Bwana.
Na. Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi wa mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni