1Wakoritho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana
waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
Katika kifungu hiki cha maneno
Paulo mtume anajaribu kuitimia historia ya Israel na safari yao ya jangwani kwa
kusudi la maonyo kwa Kanisa la korintho na kwa wakristo wote leo, Hata hivyo
ndani yake kuna maswala yamsingi ya kujifunza na moja wapo ya tukio Muhimu
linalotajwa hapa ni Israel kuunywea Mwamba wa Roho uliokuwa ukiwafuata, hili ni
moja ya tukio muhimu sana na ambalo lina kitu cha kujifunza.
Kwa mujibu wa tamaduni za
kiyahudi katika kitabu chao cha komentari ya kiyahudi kiitwacho “Haggada” Marabi wengi walikuwa wanaamini kuwa Waisrael
Jangwani walikuwa na Mwamba uliokuwa ukiwafuata na kuwapa maji, inaaminika kuwa
mwamba huu ulikuwa unaweza kuuimbia kwamba utoe maji nao uliweza kutoa maji
Hesabu 21: 16-18 “Kutoka huko wakasafiri kwenda Beeri; ni
kisima ambacho Bwana alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji.
Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu; Bubujika Ee kisima; kiimbieni; Kisima
walichokichimba wakuu, Ambacho wakuu wa watu wakakifukua, Kwa fimbo za enzi,
kwa fimbo zao.”
Hata hivyo Marabi wengine
wanaamini kuwa kulikuwa na kijito kilichokuwa kikitiririsha kuwafuata waisrael
na kutoka mlima Sinai kuhakikisha kuwa
unawapatia maji
Kumbukumbu 9:21 “Kisha nikaitwaa
ile dhambi yenu, huyo ndama mliyemfanya, nikamteketeza kwa moto, nikamponda,
nikamsaga tikitiki, hata akawa laini kama vumbi; nikalitupa vumbi lake katika
kijito kilichoshuka kutoka mlimani”
Na wengine wanaamini kuwa
kulikuwa na jiwe maalumu lililokuwa likidongoroka lenyewe kuwafuta na kuwapatia
maji tangu Musa alipoupiga mwamba, vyovyote iwavyo Paulo mtume aliitumia mifano
hii ya kiimani ya wayahudi kuonyesha jinsi ambavyo Mungu alikuwa akiwajali watu
wake, kwamba Yesu alikuweko Jangwani katika ulimwengu wa roho kuhakikisha kuwa
anawahudumia watu wake anatoisheleza mahitaji yao, anahakikisha kuwa
hawapungukiwi na kitu, kwamba anatimiza kiu yao, na kwamba anatimiza mahitaji
yao ya kila siku, kama jinsi ambavyo Mungu aliwalisha watu wake kwa mana
vilevile aliwalihakikisha kuwa wanakuwa na maji ya kunywa ya kutosha wao na
mifugo yao, Ni Mungu yuleyule anayeweza kuwapatia watu mahitaji yao wakiwa
jangwani ndiye ambaye anatoa neema wakati wa mahitaji yetu
Kristo ambaye ni Mwamba wa kiroho
kwetu yuko kuhakikisha kuwa anatimiza mahitaji yetu leo, atakutana na kiu ya
kila mmoja wetu, kama tunahitaji kufaulu, kupona, kutimiziwa mahitaji yetu yeye
yupo kutuhudumia na kutoa neema jangwani, anajua jangwa hili zito unalolipitia
anajua kuwa utakutana na kiu za aina mbalimbali, anajua kuwa aunahitaji
kushibishwana kuburudisha kutokana na uchovu wa safari, nisikilize Japokuwa
Mungu ameruhusu upite katika jangwa hilo yeye hatakuacha yuko pamoja nawe na
nakuhakikishia kuwa atakuwa wingu wakati wa Mchana, yaani atakuwekea uvuli
wakati wa hari wakati wa joto atakufunika jua lisikuumize, aidha atakuwa Nuru
kwako wakati wa usikum hutaita katika giza yeye atakuwa pamoja nawe, atakulisha
kwa mana jangwani lazkini atahakikisha wewe na nyimba ya baba yako na mlango wa
baba zako anawaburudhisha kwa maji ,kutoka katika mwamba huu na ni mwamba wa
ajabu kwani unakufuata katika safari yako ili kukuburudisha.
Tunapojikumbusha maneno haya ya
kihistoria na maonyo tunataka kuangalia neema ya Mungu kwa wanadamu na upendo
wake kwetu kuwa Mungu alijishughulisha sana na Israel na anajishughulisha sana
na mahitaji yetu pia.
Ujumbe. Na mkuu wa wajenzi mwenye
Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni