Uhuru Muigai Kenyatta.
Uhuru Kenyata alizaliwa tarehe 26
October 1961 ni moja ya wanasiasa mahiri na raisi wa awamu ya nne wa jamhuri ya Kenya.
Mheshimiwa Kenyatta amewahi kuwa
mbunge wa Jimbo la Gatundu ya kusini kati ya mwaka 2002 mpaka 2013, Kenyatta ni
mtu aliyejaa upendo, imani, na mwenye kuheshimu utu, ni mpole na mnyenyekevu,
ni mpenda maendeleo na ni mtu anayeipenda Afrika kwa dhati na mwenye moyo wa
Kumcha Mungu.
Kabla ya kuwa raisi wa awamu ya
nne wa Kenya ndugu Kenyata amewahi kuwa mwanachama wa Kenya African National
Union, chama ambacho kilihusika kudai Uhuru wa Kenya chini ya baba yake Mzee
Jomo Kenyatta. Kwa sasa Kenyatta ameingia madarakani kwa tiketi ya chama cha “Jubilee” jina ambalo kwa asili ni la
kibiblia lenye kuzungumzia mwaka wa Bwana wa kuwaweka huru watu wake sawa na
Luka 4:18-19. “Roho
wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari
njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona
tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” Neno mwaka wa Bwana uliokubaliwa kibiblia
ndio ulijulikana kama Jubilee.
Uhuru Kenyatta ni moja ya watoto
wa kiume wa aliyekuwa rais wa Kwanza wa jamhuri ya Kenya na mama yake Mama
Ngina Kenyatta ambaye kwa bahati nzuri bado yu hai, Mheshimiwa Uhuru alishinda
Uchaguzi kwa mara ya pili August 2017
katika uchaguzi mkuu na kupata ushindi kwa asililia 54% kupitia kura za wakenya
wote waliokuwa wamejiandikisha, Hata hivyo ushindi huu uliokuwa umetangazwa na
mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi wa nchi hiyo “Independent Electoral and
Boundaries Commission” Ndugu Wafula Chebukati. Ushindi huu ulipingwa kisheria
na mahakama kuu nchini humo baada ya kuzingatia madai ya muungano wa vyama
pinzani unaojulikana kwa ufupi kama NASA uonaoongozwa na “Raila Odinga” kwa
kuzingatia madai kadhaa tarehe 1 September 2017 Mahakama kuu ilibatilisha
matokeo hayo na kuamuru kuwa uchanguzi urudiwe tena tarehe 26 October 2017
yaani ndani ya siku 60 tangu kutanguliwa kwake, hata nhivyo katika namna ya
kushangaza uchaguzi huu wa marudio ulipingwa na kukosolewa vibaya na wapinzani na watu wa maswala ya haki za
binadamu, Huku mpinzani mku Raila Amolo Odinga akisusia uchaguzi huo.
Maswala kadhaa ya ya uvunjifu wa
amani yalijitokeza kwaajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliorudiwa kwa
mara ya pili, huku wafuasi wa raila wakiandamana katika mitaa kama
Kawangware, Nairobi na maeneo mengine
wakipinga vikali na kuchoma moto maduka na kuchoma matairi, watu kadhaa walijeruhiwa
na wengine kufariki dunia, waandamanaji walikuwa wakimtaka Raila kuchukua
hatua, kabla ya kura kurudiwa tena, Huku
yeye mwenyewe akiwachochea wafanye fujo na kupinga uchaguzi huo kwa madai kuwa
hakukuwa na uwanja huru na wa haki wa ufanyikaji wa uchaguzi huo, Na baadaya
bwana Odinga alijitoa katika kinyanganyiro hicho cha uchaguzi wa mara ya pili,
kutokana na tukio hilo Muheshimiwa Kenyatta alipata nafasi ya kushinda uchaguzi
wa Marudio kwa njia iliyo laini zaidi na hivyo kumpa nafasi ya kuiongoza Kenya
kwa miaka mitano ijayo.
Katika uchaguzi huo wa Marudia muheshimiwa Uhuru Kenyatta alipata
ushindi mkubwa wa kishindo kwa asilimia 98% ya kura zote zilizopigwa, Wakati
akiapishwa Rais Kenyata aliahidi kuwa daraja la maendeleo lenye kuwaunganisha
wakenya kuwa kitu kimoja na kusonga mbele huku akiweka moyo wake wote, katika
Hutuba yake iliyojawa na utukufu wa Mungu Mheshimiwa Kenyata alisoma andiko na
Nabii Isaya akihusisha tukio la
kuapishwa kwake tarehe 28/11/2017 kuwa bila Mungu haikuwa rahisi namnukuu
“Today is yet another
historic day for our great motherland. First and foremost, our gratitude
is to our Almighty God. The Prophet Isaiah proclaimed: When you pass through
the waters, I shall be with you. When you pass through the rivers, they shall
not overwhelm you. When you walk through fire, the flames will not consume you, Our
God is faithful. He heard our voices when we cried out to Him. He
listened, and answered our prayers. He has brought us thus far, and He
will take us even further.This is the testimony of our country today; and for
this we thank Him”
Tafasiri isiyo rasmi Leo ni siku
nyingine ya kihistoria katika ardhi mama yetu, Kwanza ningependa kumshukuru
Mwenyezi Mungu, Nabii Isaya alisema, “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika
mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto
hautakuunguza.” Mungu wetu ni mwaminifu, amesikia sauti zetu
tulipomlilia na kuhitaji msaada wake. Amesikia na kuyajibu maombi yetu,
ametufikisha hapa leo na atatuvusha zaidi ya hapa na huu ni suhahidi ulio wazi
leo na kwaajili ya hili tunamshukuru mwisho wa kumnukuu
Maandiko yaliyotumiwa na Mheshimiwa
Kenyatta ni Isaya 43:2, Ni wazi kuwa
Kenyatta hakunukuu maandiko haya hivihivi tu Kenyata pamoja na willium Rutto
ambaye siku ile Kenyata alimuita Pastor ni wazi kuwa walimtegemea Mungu, ni
wazi kuwa walimtanguliza Mungu mbele, ni wazi kuwa walikuwa na timu kubwa ya
watu walioomba pamoja nao na kwaajili yao mapema waimbaji kadhaa walisikika
katika uwanja ule wakiimba kuwa sio uchawi ni Maombi, hii ilikuwa ni ushahidi
wazi kuwa kuna watu walikuwa wakiomba kwaajili ya wakenya.
Kwanini naandika makala haya, ?
wanafunzi wangu wote waliosoma Living Stone Boys’ Seminary ni mashahidi kuwa
kwa neema aliyonipa Mungu niliweza kuwatabiria maraisi kadhaa na wakawa katika
nafasi nilizowatabiria, akiwepo Rais John Pombe Magufuli, Rais Trump na
Kenyatta, Niliwaambia wazi wanafunzi wangukwa vile tulikuwa tunaomba pamoja
mara kadhaa nilitaka wayajue mapenzi ya Mungu niliwaambia kuhusu ujio wa
maraisi hao madarakani na ikawa kama nilivyowaambia, niliwaambia kuwa mimi sio
Muhubiri mkubwa sana kwa maana ya umarufu, wala sijiiti nabii lakini nilimsikia
nabii mmoja mkubwa mwenye kituo kikubwa cha tv huko Dar es Salaam akisema wazi
kuwa anamuona Raila Ikulu, mimi hapohapo nmilimwambia mke wangu hapana mimi
namuona Kenyetta Ikulu, na jiono nilipokwenda kuomba niliwaambia wanafunzi
waziwazi kuwa yuko nabii mwenye kituo cha TV huko Dar es Salaam amesema kuwa amemuona
Raila akiwa ikulu mimi naomba nieleze wazi kwamba tuiombee Kenya kwani nimeona
Moto katikati ya mji, na moshi mkubwa karibu na jengo moja refu sana nchini
humo, na tukiomba vema moto huo unaweza kuzimishwa lakini mimi simuoni Raila
Ikulu namuona Kenyatta.
Leo ninapoandika naandika mambo haya
yakiwa yametimia lakini kwa nini nataka kuandika hili leo nataka kukiri Mbele
za Mungu kuwa Kenyatta yuko Kihalali madarakani, si kwa sababu ya uchaguzi
kurudiwa, si kwa sababu, ameapishwa lakini kwa sababu Mungu amemchagua na
kukusudia awepo na nataka kuitumia nafasi hii kutoa maonyo kwa raila Odinga,
kuwa ajihadharina jaribio la kutaka kujiapisha kuwa Rais kwani tukio hili licha
ya kuwa na madhara kwa wafuasi wake kadhaa lina madhara makubwa sana kwake mwenyewe,
huu ndio utakuwa mwisho wa Raila, kisiasa, kiimani na kwa heshima aliyonayo,
litakuwa tukio la aibu kubwa sana kwake na lenye kufedhehesha, kwani licha ya
kuwa kinyume cha sheria liko kinyume na Mungu, Mungu hakukuchagua Raila, wala
hatakuchagua tena kuwa Rais wa Kenya wakati wowote na nataka kuweka wazi wazi
wazi kuwa Rais ajaye wa Kenya mara baada ya Kenyata atakuwa Mcha Mungu zaidi
mara mbili ya Kenyatta atalitaja jina la Mungu maradufu zaidi na atatokea
Jubelee tena na Raila hataonekana tena.
Katika Historia ya mageuzi nchini Kenya.
Wito kwa wakenya wote tusikubali kamwe
kumwaga Damu, tusikubali kushawishiwa na wapinga maendeleo na wapinzani na
maadui wa Kenya walioko ndani na nje, Kenyatta anaweza asiwe mkali kama
Magufuli, watu hawafanani, lakini moyo wake una mapenzi mema kwa wakenya na
Afrika kwa ujumla, Mimi ni Mtanzania sina asili yoyote ya Kenya, lakini nabii
hana mipaka kwa vile Mungu ni wa watu wote, lakini Kenya ikiendelea ni Afrika
imeendelea, uchumi wa Kenya ukikua ni uchumi wa Afrika umekua,
Naitakia Kenya wakati wa utulivu na
wakati wa kufanya kazi na kuachana na aina yoyote ya ushawishi ulio na nia ovu
wa kutokuitambua serikali halali iliyoko Madarakani, niwaonye wakenya wote
kutokujitokeza tarehe 12 kwaajili ya kuapisha mtu asiyehusika na wamuache mwenyewe aidha serikali ya Kenya
iliyoko madarakani ichukue hatua stahiki na kali za kisheria kwa jaribio hilo
la kipumbavu litakalojaribiwa kufanya na uongozi wa Nasa.
Mungu Ibariki Kenya
Mungu Ibariki Afrika
Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi
mwenye Hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni