Mstari wa Msingi:- Matendo 5:29 “Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa
kumtii Mungu kuliko wanadamu.”
Mstari wa Somo:- Kutoka 1:15-21 “Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa
Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa
Pua; akasema, Wakati mwazalishapo
wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume,
basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. Lakini wale wazalisha
walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri,
lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. Basi mfalme wa Misri akawaita wale
wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto
waume wawe hai? Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa
Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla
mzalisha hajapata kuwafikilia. Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na
hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. Ilikuwa
kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa wako watu
ambao wametajwa katika maandiko kwa ufupi sana lakini wanatufundisha somo pana
sana lenye kuweza kutufaa katika nyakati zetu, Miongoni mwa watu hao ni
Shiphrah na Puah ambao wanatufundisha mambo ya msingi katika kumpendeza Mungu,
Leo tutachukua muda kujifunza kuwa wao ni nani na mambo muhimu ya kujifunza
kutoka kwao:-
Shiphra na Puah ni nani?
Tofauti na Mashujaa wengine
katika maandiko Shiphra na Puah wanatajwa kwa kifupi sana katika maandiko
katika kitabu cha Kutoka 1:15-21,
Hawa walikuwa wanawake waliookoa maisha ya wengi kabla ya kuzaliwa kwa Musa
huko Misri, wanawake hawa walikuwa ni wakunga, (Wauguzi wanaohusika na
kuzalisha wanawake wajawazito)
Wanatheolojia wanapata utata
mkubwa sana kugundua asili ya Shiphrah na Puah kwamba walikuwa Waebrania au
walikuwa Wamisri, hii ni kwa sababu Biblia ya kiyahudi inawaita wazalisha wa
kiibrania “Hebrew Midwives” kwa kiibrania “ Meyaldot Haiviyot” “Meyaldot
Haiviyot” Wataalamu wa maandiko wa kiyahudi akiwemo Rabbi Abrabanel ameweka wazi katika mawazo yake kuwa wanawake
hao walikuwa wamisri isipokuwa waliokuwa wanamcha Mungu, kama wangekuwa
waebrania neno Mcha Mungu lisingeliweza kutumika hapo, lakini neno hilo ndilo
linalosaidia kujua kuwa wanawake hao walikuwa wamisri, kwa vile neno wacha
Mungu mara nyingi lilitumika katika biblia kumaanisha mataifa waliomuamini au
waliomcha Mungu wa waebrania, sasa swali linaweza kuja kwa nini waliitwa
wazalisha wa kiibrania lugha hii inaweza kuwa na maana ya “Wakunga waliokuwa
wakiwazalisha waebrania” na kwa sababu hiyo haikuwa na ulazima sana wao wenyewe
wawe waebrania Kama hivyo ndivyo basi, Shiphra na Puah wanakuwa watu wa kwanza
wasiokuwa waenrabia kuhatarisha maisha yao kwaajili ya Wayahudi. Msomi mmoja wa
kiyahudi ambaye ni mwalimu mwenye kuheshimika sana ajulikanaye kama Nechama Leibowitaz anasema kama wanawake hao walikuwa wamisri
hapo ndipo somo hili linapokuwa tamu na kupata maana iliyo njema zaidi, na somo
kuu tunajifunza kuwa mtu yeyote yule wa taifa lolote lile na jamii yeyote ile
anaweza kusimama katika kweli linapokuja sala la kusimamia haki, bila kujali
kuwa anatoka katika historia gani.
Ni wanawake waliompendeza Mungu.
Wanawake hawa mashujaa waliagizwa
kwa amri ya mfalme katika Kutoka 1:15-17
“Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa
Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;
akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa,
ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.
Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na
huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.” Unaona
Maandiko yanasema wanawake wale walikuwa wacha Mungu na hivyo hawakufanya kama
ilivyokuwa amri ya mfalme, wao kwa imani waliamua kumtii Mungu kuliko kuwatii
wanadamu waliwatunza wayahudi bila kujalia amri ya mfalme jambo hili
lilihatarisha sana maisha yao, zamani ilikuwa usipotii amri ya mfalme ilikuwa
lazima uuawe, lakini wanwake hawa walisimama katika kweli walisimama katika
haki na Mungu aliwatetea, Ziko
nyakati katika maisha yetu ambazo tunatakiwa kuwa na msimamo thabiti kwamba
heri ya lawama kuliko fedhea kuwa tayari kuhatarisha maisha yetu kwaajili ya
utii wetu kwa Mungu, hili ni somo ambalo wanawake hao wanatufunza leo, walikuwa
na ujasiri, hawakuogopa, walifanya yaliyo wajibu wao, sawa na Petro alivyojibu
wakati baraza la wazee wa kiyahudi wakiwapiga marufuku wasihubiri injili, Petro
alijibu kwa ujasiri “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”
Somo kutoka kwa Shiphra na Puah
1. Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu
– wanawake hao walihatarisha maisha yao kwaajili ya kuikiuka amri ya mfalme kwa
kweli walipaswa kukatwa shingo, lakini walikuwa tayari kupoteza kila kitu kwa
sababu WALIKUWA WANAMCHA MUNGU tunajifunza kuwa kama tunamcha Mungu kama
tunamuogopa Mungu tunaweza kusimama na kupingana na dhuluma na udhalilishaji wa
aina yoyote ile bila kujali nini kitatukuta ila kwa sababu kubwa moja tu
tunamcha Mungu.
2. Walitamini umuhimu wa uhai na maisha - Bila
kujali kuwa wanaozalishwa ni wamisri au wayahudi wanawake hawa walionyesha kuwa
wanathamini uhai na kuwa wako tayari kutoa uhai kwaajili ya uhai, hawakuogopa
waliwahurumia watoto hao wachanga walioma huruma jinsi ambavyo mama amebeba
mimba miezi tisa na sasa anataka kuunganishwa na mwanaye na kitoto kipya
kinakuja ulimwenguni bado hakujaunganishwa na mama yake, bila kujali ni wa aina
gani ni wakabila gani uhai wa mwanadamu una thamani kuwa sana, wao walijua kuwa
wameapa kuokoa uhai wa mwanadamu na hivyo walikuwa wana haki ya kuhakikisha
kuwa wanafanya hivyo bila kujali nani ameagiza vitoto visivyo na hatia viuawe,
siku nhizi watu hawathamini uhai unaweza kusikia watu wakiwaxchinja wake zao,
au kuua vitoto na kuwachoma moto wezi kabla hata ya kuwafikisha katika vyombo
vya kisheria kuua limekuwa jambo la kawaida tu Mithali 31:8-9 inasema “Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu
wote walioachwa peke yao; Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie
maskini na wahitaji haki yao” Neno la Mungu linatutaka tuseme kwa
aajili ya wale wasiosema, tuwatetee wasioweza kujitetea, tusimame katika haki
na kuhakikisha kuwa masikini wanapata haki zao, Hii ndio kazi iliyofanywa na
Shiphrah na Puah, walisimama kwa niaba ya wanyonge na masikini vitoto
visivyoweza kujitetea, watu wengine kwa kuwa Mungu amekuweka katika mikono yake
basi ndio utaipata fresh.
3. Mungu anaona Mawazo yetu na Matendo yetu
– Hwa wanawake wakunga walikataa kutii amri ya mfalme wao muovu, na
kutokukubalia kuuwa watoto wasio na hatia na Mungu aliona na kuwabariki, Sio tu
kuwa mungu aliona matendo yao hapa lakini pia aliisoma nia yao namawazo yao, Zaburi 139:1-4 “Ee
Bwana, umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote. Maana
hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, Bwana.” Kumbe Mungu
anaona na anayajua mawazo yetu anatufahamu kwa undani zaidi hakuna cha
kujificha katika mawazo yetu wala katika ulimi wetu, hivyo ni muhimu katika
maisha yetu kuishi maisha ya kupendeza yeye popote tulipo na kisimama upande
wake hata kama lile tunalolisimamia litahatarisha maisha yetu, hatuna budi
kuisimiamia kwaajili ya Mungu.
4. Lazima tusimame na Israel. – Shiphra na
Puah hawakuwa Wayahudi, lakini waliwahudumia waliwalinda na kutokana na matendo
yao mema Mungu aliwabariki aliwasimamishia nyumba , walipate neema waliolewa,
walikuwa na familia nzuri. Walibarikiwa, Bilia ina ahadi nyingi kuhusu kusimama
na Israel, Bila kujali wewe ni mtu wa namna gani, ni wa asili ipi ni wa imani
ipi linapokuja swala la mtu anataka kuiharibu Israel simama na Israel simama na
watu wa Mungu, hata siku moja usithubutu kuwashutumu na kuwazomea na kuwalaani
Mwanzo 12: 1-3 “BWANA
akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba
yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa
kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki
wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia
watabarikiwa.”
Isaya 62:1 “Kwa
ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki
yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.”
Isaya 62:6-7 “Nimeweka
walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi
wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;
wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na
kuufanya kuwa sifa duniani.”
Zaburi 122:6 “Utakieni
Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;
Warumi 15:27 “Naam,
imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki
mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili.
Shiphrah na Puah
walisimam na wayahudi na wakabarikiwa, kila taifa linapaswa kuwa na uelewa na
kujifunza na kufahamu kuwa mataifa mengi yaliyobarikiwa na Mungu na watu wengi
waliofanikiwa sana ni wale wanaosimama na Israel, viongozi wa taifa letu ni
lazima wahakikishe kuwa linapokuja swala la Israel kama huna cha kusema ni
afadhali kunyamaza kimya, kuna uhusiano mkubwa wa Baraka za watu wote Duniani
na mataifa yote Duniani kubarikiwa kutokana na msimamo wako katika Israel,
Marekani na mataifa mengine makubwa yanaifahamu siri hii na ndio maana unawaona
kama wanaojipendekeza kwa wayahudi, Kupitia wanawake wale wakunga waliosiamama
na Waisrael nataka kumuonya kila mtu kuhakikisha kuwa katika maisha yake ili
kuzivuta Baraka waza mema na watakie heri Israel waombee amani, fanya amani nao
na utaona Baraka alizoahidiwa Ibrahimu zikimiminika katika maisha yako Shipra
na pua walifanya hivyo walisimama na Israel licha ya kuwa wao hawakuwa
waebrania.
I stand with
Israel forever
Rev. Innocent
Kamote
Mkuu wa wajenzi
mwenye Hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni