Zaburi 61:1-8 “Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu.
Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba
nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui
asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako
Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina
lako. Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. Atakaa
mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi. Ndivyo
nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.”
Utangulizi:
Zaburi ya 61 Ni mojawapo ya
zaburi iliyoandikwa na Mfalme Daudi wakati alipokuwa amekimbia ikulu na akiwa
katika hali ya kutokuwa salama, wakati huu inaonekana Daudi anaaanza kwa
kulia na huku akiwa amezimia moyo yaani
amevunjika moyo au amekata tamaa mno, na anaamua kuliitia jina la Mungu wake
katika Maombi, kwa nini anamuitia Mungu kwa sababu wakati huu anaona wazi
kabisa kuwa njia pekee ambayo kwayo anaweza kuwa salama na kutiwa moyo ni kwa
mwamba wa wokovu wake ambaye ni Mungu na ya kuwa yeye pekee naweza kumuinua na
kumuweka juu ya mwamba asioweza kuupanda naye atakuwa salama dhidi ya adui zake
Unapoifanyia uchunguzi wa kina zaburi
hii unaweza kuona wazi kuwa iliandikwa wakati Daudi akiwa mfalme ona msatri
wa Zaburi
61:6 “Utaziongeza
siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.” Unaona wakati
huu inaonekana wazi kuwa Daudi alikuwa amelazimika kukimbia ikulu, lakini pia
kwenda mbali na hema ya kukutania ambayo ilikuwa ni ishara inayoonekana ya
Mungu asiyeonekana kwa hiyo ni wazi hiki kilikuwa ni kipindi Daudi alipinduliwa
kwa Muda na mwanae mpendwa Absalom wakati alipomuasi baba yake, unaweza
kuigundua siri hii wazi kama mwanafunzi wa neno lake.
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na
wakati ambapo anapitia Mambo magumu, vita au mateso na mapambano ambayo wakati
mwingine yanaweza kumuumiza moyo kwa kiwango cha kuzimia Moyo, ni muhimu
kukumbuka kuwa wewe sio wakwanza sio wewe peke yako unayepitia hali kama hizo
sote tunapitishwa, sote tunavunjika moyo sote kuna wakati tunazimia Moyo hata
kama kwa nje watu wanatuona kama wafalme, lakini sisi tunaopitia katika dhiki
na mapito na mateso hayo kwa kweli wakati mwingine tunalemewa sana kiasi cha
kukosa matumaini na kulia au kuvunjika moyo, hali hii ndiyo iliyompata mfalme
Daudi wakati huu ona
2Samuel 15:14,30 “Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate Kwa upesi, Na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga., Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda.“
Daudi anaonyesha kuwa kuna wakati mashujaa wanakata tamaa na hata yeye alikuwa na wakati mgumu mno wakati huu lakini pamoja na magumu hayo yote alijitia moyo kwa namna ambayo itatutia moyo sisi nasi
2Samuel 15:14,30 “Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate Kwa upesi, Na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga., Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda.“
Daudi anaonyesha kuwa kuna wakati mashujaa wanakata tamaa na hata yeye alikuwa na wakati mgumu mno wakati huu lakini pamoja na magumu hayo yote alijitia moyo kwa namna ambayo itatutia moyo sisi nasi
1.
Alimlilia
Mungu, aliomba na alimsihi Mungu asikie Dua zake, inawezekana alichanganya
na toba katika maombi yake alimsihi Mungu, alimwambia Mungu kuwa hata kama
angepelekwa uhamishoni utumwani ambao wana wa Israel zamani waliita mwisho
wanchi yaani mahali ambapo huwezi kujikomboa wala kujitoa ni eneo la mashaka
bado aliamini Mungu kuwa anaweza kumtoa huko nako yeye alikuwa amejaa shuhuda
kuwa tangu zamani Mungu amekuwa kimbilio lake na wokovu wake anajua na kuamini
kuwa Mungu atamtoa katika hakli anayoipitia na atampandisha juu mahali pa juu
kwenye mwamba asioweza kuupanda ni Mungu pekee anayeweza kuzihuisha nafsi zetu
tunapokuwa tumekata tamaa na kwa sababu hiyo ni muhimu kwetu tukamlilia yeye
kwa dua na maombi Zaburi 23:3 “Hunihuisha nafsi
yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.”
2.
Alimsihi Mungu amuweke mbali na jaribu anasema hivi Zaburi 61:2b “Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.” Hapa kuna mambo ya msingi mawili Mwamba asioweza
kuupanda inaweza kumaanisha kwanza Mungu ampe kulishinda jambo gumu ambalo yeye
kwa akili zake na ujuzi wake na utaalamu wake ilikuwa ngumu sana kupambana
nalo, wakati mwingine tunakutana na mambo magumu sana duniani ambayo wataalamu,
watumishi wa Mungu, makuhani manabii,madaktari na wanasiasa, na watawala
wanasaikolojia na wanafalsafa huwa wanakosa majibu, kumbuka Daud alikuwa
jemadari wa vita, mtaalamu na mtu hodari lakini hapa majemadari wengine
walikuwa upande wa mwanae Absalom na yeye hawezi kupigana kumuua mwanae na
huwezi kupigana vita ngumu ya namna hii, unawezaje kumuua mwanao mrithi wako
kisha ukajiita shujaa? Unawezaje kumuua mtu ambaye wengine wanampenda na
kumuheshimu na kumuona kiongozi? Kama hutaonekana una wivu? Ulikuwa ni mwamba
usioweza kupandika ilikuwa ni lazima akate tamaa na kuzimia moyo, ziko vita
vyingine unapambana mpaka unazimia moyo, unashindwa kujua utapenya namna gani
na ni Mungu pakee anayebaki kujua hatima yako, usiogope endelea kuliitia jina
la Bwana Mungu wako, Yeye alimsihi Mungu amuweke mbali na jaribu! Ambalo yeye
aliliona kuwa hawezi kulikabili, kila tunapokabniliana na jambo tusiloweza
kulikabili duniani basi ni vema tumkabidhi Bwana Mungu wetu!
3.
Alimtambua
Mungu kama Ngome yenye nguvu
Zaburi 61:3-5“Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye
nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya
mbawa zako Maana Wewe, Mungu umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina
lako” Tunapomuendea Mungu kwa magumu yoyote tunayokabiliana nayo ni
lazima tukubali na kutambua yuko Mungu ambaye ni mkuu mno kuliko jaribu
tunalolipitia, Japo Daudi alitambua ukubwa na ugumu wa yale aliyoyapitia lakini
alitambua Kuwa Mungu ni ngome yake yenye nguvu na tena amekuwa kimbilio lake na
ni ngome yake na hivyo adui hatampata, hii sio tu itatokea katika jaribu hili
lakini imekuwa kama shuhuda ya historia ya maisha yake, wakati mwingine ni
muhimu kukumbuka kuwa Mungu alitufanyia nini alituvusha katika magumu ya namna
gani na tukubali na kutambua kuwa atatuvusha katika hili pia linalotukabili.
Wakati huu dunia
inapokbaliana na adui Corona (COVID 19) kila mtu anayeliogopa jina la Mungu
atapata urithi, Mungu atakutunza haijalishi corona inatishia kwa kiwango gani
vyovyote iwavyo tuihesabu kuwa ni adui kwa maisha yetu, lakini haiba nguvu kama
alivyo Mungu wetu yeye aliyetuhifadhi maisha yetu katika namna nyingi na kwa
njia nyingi atatupitisha pia katika janga hili na kutuweka mahali salama,
usiogope wala usizimie moyo!
4.
Aliagiza
fadhili za Mungu zimhifadhi!
Zaburi 61:6-8 “Utaziongeza
siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili
na kweli zimhifadhi. Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe
nadhiri zangu kila siku” Daud alijiombea aongezewe siku nyingi,
alijiombea kukaa katika uwepo wa Mungu milele lakini alimsihi Mungu aagize
Fadhili zake zimhifadhi, kuwepo kwetu duniani hakutokani na nguvu zetu, kuwa
kwetu kwenye cheo chochote hakutokani na nguvu zetu, Ni fadhili za Mungu tu,
Mungu alimuongezea Daudi siku za ufalme kweli alikuwa amekimbia ikulu, kweli
mwanaye mwenyewe alikusudia kumuua, lakini dua hii ilisikiwa aliziomba fadhili
za Mungu zimhifadhi, Ni lazima tumtegemee Mungutu lazima tuzitegemee fadhili
zake, fedha na nguvu na madaraka na ukuu si kitu bila fadhili za Mungu, kule
Italy watu walitupa fedha zao, walikuwa wamebaini kuwa fedha haiwezi kukusaidia
kitu, cheo hakiwezi kukusaidia kitu, Mungu ndiye kila kitu katika maisha yetu,
bila fadhili za Mungu huwezi kujikinga na kifo wala huwezi kujikinga na tauni
ya corona, kwa hiyo wakati kila kitu kinasambaratika duniani uko mkono mwingine
mkono wenye nguvu unaoweza kutushika wakati wa mambio mabaya, utakaotuongoza na
kutuweka juu mahali salama ambako hatuwezi kukumwa na dhuruba ya aina yoyote,
ambapo tutasimama na kujisikia kuwa tuko salama huko si kwinhineko ni kwenye
fadhili za Mungu ni kwenye uwepo wake tu, huko ndiko kwenye ngome imara ni kwa
bwana wetu Yesu Kristo yeye pekee ndiye mwenye sifa ya kuokoa hakuna Mungu
mwingine anayeweza kuokoa na kuponya ni Yesu tu yeye ndiye mwenye nguvu na ni
yeye pekee anayeweza kutuweka juu ya mawimbi hata mioyo yetu inapozimia, kwake
yeye ndiko Tumanini letu liliko hata kutokee nini. Usizimie moyo Yesu ni mkuu
kuliko dhuruba tunazozipitia.
Katika
nyimbo za Dini za Kanisa la Anglican kuna
wmbo mzuri unaotutia moyo wakati Mioyo yetu ilipozimia na ukiuimba utahuisha
moyo wako na kukupa ngvu mpya ni wimbo namba 413 tune 246 unaitwa Ee Mungu Baba,
kuna ubeti unaosema Uzimiapo Moyo wangu baba Unipe Roho yako awe name, Roho Mtakatifu
ni faraja kubwa sana tunapozimia Mioyo naye atatuhuhisha tena !
Ee Mungu Baba, Haba Duniani
Imeparuza sana njia yangu,
Unipe Moyo wa kusema hivi
Mapenzi yako yatimizwe
Nikiwa nina taabu na huzuni
Nikae kimya nisinung’unike
Niseme tu alivyosema Yesu
Mapenzi yako yatimizwe
Ninapofarakana na rafiki
Niwapendao niko paka yangu
Ni amri yako name ningejibu
Mapenzi yako yatimizwe
Ujaponiamuru nikiache
kinachonipendeza sicho change
nakupa tu kilicho mali yako
Mapenzi yako yatimizwe
Uzimiapo Moyo wangu baba
Unipe Roho yako awe nami
Mengine yote ninakuachia
Mapenzi yako yatimizwe
Nataka nia yako iwe yangu
Utoe kila kitu ndani yangu
Kinachonizuia nisiseme
Mapenzi yako yatimizwe
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni