Zaburi 116:1-6 “Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na
dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na
huzuni; Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu.
Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. Bwana
huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.”
Utangulizi:
Ni moja ya zaburi ya kipekee
sana, Mwandishi haonyeshi kama iliwahusu watu wote lakini ilimuhusu yeye
binafsi na hali iliyomzunguka na anaonyesha njinsi anavyompenda Bwana kwa kuwa
anamsikia zaburi hii imegawanyika katika maeneo makuu matatu, anamsifu Bwana na
kuonyesha ji kwanini anamsifu na anampenda, lakini pia anaelezea mambo magumu
yaliyomkuta na jinsi bwana alibyomuokoa na anaelezea namna anatavyo mshukuru,
kwa hiyo ni zaburi ya shukurani binafsi kutokana na kuokolewa na mitego au kama
au hali zinazolazimisha afe!
Zaburi hii haijulikani mwandishi
ni nani na tukui husika ni lipi lakini inaonekana mwandishi alikuwa akimshukuru
Mungu kwa kumuokoa na mauti au hali za kifo zilizokuwa zikimuandama, uchunguzi
wa kimaandiko unaonyesha kuwa huenda zaburi hii ni ya Nabii Yona ingawa hatuna
ushahidi wa kutosha kama Yona alitunza Zaburi, vyovyote vile iwanvyo inaonekana
Yiona akliisema zaburi hii alipookuwa akimuomba Mungu kwenye tumbo la Nyangumi,
na kinabii inamuhusu Masihi ambaye alipokufa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu
tuona
Yona 2:1-10 “Ndipo Yona
akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, Akasema, Nalimlilia
Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu
naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo
wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na
gharika zako zote zimepita juu yangu.
Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena
kukabili hekalu lako takatifu.Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi
vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu;
Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake
yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee
Bwana, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana;
Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo
ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; Lakini mimi nitakutolea
sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa
Bwana.Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.”
Unaona
ni Zaburi ambayo tukio lake linafanana kabisa na tukio la Yona Lakini mambo ambayo
tunaweza kujifunza kutoka katika zaburi hii ya shukurani ni maswala makubwa
matatu
1.
Mwimbaji anaonyesha sababu za kumshukuru
Mungu
2.
Mwimbaji anaonyesha nini cha kufanya
tunapozungukwa na kamba za Mauti
3.
Mwimbaji anaonyesha mwitikio wa Mungu wetu
tunapoliitia jina lake
Sababu za Kumshukuru Mungu.
Ziko sababu nyingi sana za sisi
wanadamu kumshukuru Mungu, na kumpenda hata tunapokuwa katika wakati mgumu,
sisi kama wenye dhambi Mungu anapotuonyesha kuwa hatustahili na kuwa wakati
wowote anaweza kutuangamiza kwa hasira yake kwa kuwa hakuna hata mmoja anayefaa
tunaweza kujikuta tunataabika sana na tunajawa na hofu kubwa na huzuni, Hakuna
mwanadamu hata mmoja anayestahili kuwa hai wakati Mungu anapoikasirikia Dunia,
hakuna anayeweza kudhani ya kuwa yeye anafaa, hakuna kuhani wala nabii, sheihk
wala padre askofu wala mpagani, hakuna hata mmoja tunayeweza kusema hastahili
kutubu Ni kwa rehema zake tu ndio maana hatuangamii, hakuna asiyejaribiwa au
kujaribika hata mmoja ujumbe wa toba unamuhusu kila mmoja kwa sababu neno la
Mungu linasema wote wamepotoka wameoza wote pia hakuna mtenda mema kla hata
mmoja kwa tendo moja tu la kuwa na uhai na kugundua kuwa yuko Mungu huilo pekee
linalazimisha tumpende Mungu na kama tukimuita na akatuitikia hilo nalo
linapaswa kuongeza upendo wetu kwake, Yona alipogundua tu kuwa Yuko hai na
alipokuwa akimuitia Mungu kama nabii na kujua kuwa Mungu anamuitikia akikumbuka
jinsi alivyokataa kutii kwa makusudi akikumbuka jinsi mauti ilivyokuwa
ikimuandama hata kura za kifo zilimuangukia yeye akikubalia kwa hiyari yake afe
ili wengine wawe salama kwenye melikebu, alimezwa na samaki, alilia katika
tumbo la Nyangumi na kuweka nadhiri na Mungu akamisikia tukio hili pekee
lilimfanya awe na wingi wa shukurani!
Yona 1:6-17 “Basi nahodha akamwendea,
akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda
Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee. Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na
mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga
kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe
ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe
umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Akawaambia,
Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na
nchi kavu. Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili
ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso
wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. Basi wakamwambia, Tukutende nini,
ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Naye akawaambia,
Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni
kwa ajili yangu tufani hii imewapata. Lakini wale watu wakavuta makasia kwa
nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia
sana. Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba,
tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu
isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda. Basi
wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. Ndipo wale
watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri. Bwana
akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la
samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku”
Unaona ni kupitia hali hii bahari
ilichafuka na kura zilionyesha kuwa yuko mtu ameacha kumtii Mungu na ni
kwaajili yake mabaya yanatokea hivyo ingawa alikuwa amelala hana wasiwasi Yona
alikuwa anakambiliwa na mauti, kamba za mauti zilikuwa zimemzunguka na kwa
kuliitia jina la bwana akaokolewa na hali ile ni kwa sababu hii anaona ziko
sababu za kumshukuru Mungu, Yuko Munghu anayeisikiliza sauti yetu hata kama
tumemkosea hili ni jambo la kushukuru kwamba tukiliitia jina lake atatusikia na
atatujibu, wakati huu sasa dunia inapitia katika majanga ya aina mbali mbali
mazito na tishio kubwa sana la kiuchumi hakuna mtu anayeweza kujigamba kwamba
yuko salama wote tumeasi, wote tumekosea kuna mahali hatuko sahihi, hatuwezi
kuwasingizia watu fulani tu wala hatuwezi kusema kuwa sisi ni bora kuliko
wengine Mungu yu atuita katika toba, sio toba ya Kenya pekee, wala sio toba ya
Tanzania pekee wala New York Pekee wala Brazil, Ni toba ya ulimwengu mzima nchi
chache zimeweza kugundua siri ya kuliitia jina la bwana walifanya vema nchi
chache na viongozi wachache sehemu fulani fulani za dunia wameweza kufunnga na
kuomba kwaajikli ya janga hili la Corona ambalo ni janga la dunia sasa ni wakati
wa umoja wa mataifa kutambua kuwa yuko Mungu wa kweli, sio kenya pekee wala
tanzania pekee wala Brazil pekee wao wameshafanya sehemu yao kila mtu anapaswa
kufanya toba kwa sehemu yake Lakini wito kwa viongozi wa umoja wa mataifa na
mashirika makubwa ya kimataifa ulimwenguni wanapaswa kutambua kuwa Yuko Mungu
aliyehai, ambaye tukimuita kwa pamoja bila jujali itikadi zetu atatuitikia
katikamelikebu wale watu waliomba na Yona waliomba bila kujali itikadi zao na
melikebu ikatulia Yona naye aliomba kwa namna yake na Mungu akamsikia Yona hapa
anawakilisha Israel na watu katima melikebu wanawakilisha ulimwengu na Nahodha
wa melikebu anawakilisha umoja wa mataifa kupata suluhu hapa ni kuliitia jina
la Mungu aliye hai kwa dunia nzima, tukifanya hivi dunia itatulia na wote
tutampenda Mungu, Lazima sasa dunia ionyeshe upendo kwa Mungu kwa sababu yeye
alitupenda kwanza
1Yohana 4;19 “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.”
Mwandishi anampenda Mungu aamtukuza kwa kuwa ni Mungu anayesikia maombi na
kuyajibu.
Tunapozungukwa na Kamba za mauti
Kifo ni moja ya adui yetu mkubwa
duniani chenyewe huanza kututafuta dakika moja kuanzia unapozaliwa kitakuandama
tu kuhakikisha kuwa kinakuondoa duniani, hivyo hatupaswi kujisahahu hata
kidogo, tunazungukwa na kamba za mauti zinatuvuta tufe Mungu ametufundisha
mambo ya ajabu kupitia gonjwa hili la corona linatunyoosha linatishia kifo cha
kiuchumi, linatishia matajiri linatishia masikini Mungu ameruhusu, ni kamba za
mauti zinatuzunguka kila mahali bila kujali wewe ni nani, narudia tena bila
kujali wewe ni nani? Kama mtoto wa malikia wa uingereza anaugua Corona, kama
waziri Mkuu wa uingereza anaingia ICU kwaajili ya Corona, ni Fundisho kuwa wewe
na mimi kama si Bwana hatuwezi kupenya, bila neema ya Mungu hatuwezi kutoboa ni
kamba za mauti zinazunguka kila mahali, je ni nabii gani sasa anaitisha
maombezi dhidi ya korona mbona imebadili mifumo yatu ya maisha mpaka mifumo ya
kuabudu, Je ni shetani? Je ni Pepo? Vyovyote iwanvyo yesu ndiye mwenye funguo
za mauti na kuzimu bila ruhusa yake corona haiwezi kuitikisa dunia ukiona hili
Mungu maeruhusu, ili tuwe wanyenyekevu, ili tukumbuke kumuheshimu, ili
tukumbuke kuwa yeye yupo ili tukumbuke kuwa dunia sio ya taifa fulani, Hatari
za kifo zilimzunguka mwandishi wa zaburi hii na sio hatari tu mwenyewe anaziita
kamba za mauti, shida za kuzimu na taabu na huzuni vilimuandama hii ndio hakli
ya dunia kwa sasa, Dunia inazungukwa na kamba za mauti kila mahali watu wamejaa
hofu ya kifo, idadi ya wagonjwa inaongezeka na idadi ya vifo inaongezeka, hakuna
usalama watu hawaaminiani wala hawajiamini hata wao wenyewe, wale wanaougua
ndio zaidi na hata wale waliopona wanaweza kukusimulia maumivu makali
waliyokutana nayo, ndoto nza kaburi walizoziona je unapopokea taarifa kuwa una
Corona unakuwa katika hali gani, familia ambazo ndugu zao au jamaa zao
wamebainika kuwa wana Corona na hata wataalamu wa Afya wanaowauguza wagonjwa
hao wako katika hali gani? Unaposafiri nani anakuamini, mbuga za wanyama zina
hali gani, sekta za usafiri zina hali gani, secta ya utalii ina hali gani,
wafanyakazi wa serikali na secta binafsi zina hali gani wakati huu? Hata
makanisa na mkisikiti na vionghozi wa dini tuna hali gani? Kamba za mauti
zinaizunguka dunia, Mwandishi anasema
Zaburi
116:3-4 “Kamba
za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;
Nikaliitia jina la Bwana nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu”
Hii ni
halia inayomzunguka mtu aliye hai lakini anayezingirwa na halia ya mauti
anakiona kifo kikiwa kinamuwania kwa kila namna hatuwezi nkukikwepa kiko hewani
tu, hata kiliowakuta walitoka wakijiamini kama wewe na mimi, Mwandishi anasema
alipoona anazungukwa ma kamba za mauti na shida za kuzimu zilimpata na aliona
taabu na huzuni yeye aliliitia jina la Bwana, dunia inaangalia suluhu kwamba
itapatikana wapi pamoja na tahadhari zote tunazozichukua suluhu ni kuliitia
jina la Bwana
WARUMI 10:13 “KWA KUWA KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA”
hakuna nafasi kwa mwanadamu kujiokoa yeye mwenyewe Mungu alimleta mwokozi
kwaajili ya ulimwengu wakati huu ni lazima tumuite Yesu kwaajili ya usalama
wetu tumeweza kufanya kitaifa lakini kanisa linaweza kuendelea, Biblia inatuagiza
kuomba bila kukoma, kwa nini tumuombe yeye Mungu mwandishi anasema Mungu ni
mwenye rehema ona
Zaburi 116:5-6 “Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye
rehema. Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika akaniokoa”,
unaona Mungu ataziokoa nafsi zetu, Mungu ataiokoa nafsi yako kwa sababu ni wa
neema na haki, kwa sababu ni mwenye trehema kwa sababu huwalinda wasio na hila
na tunapodhikika hutusikia ni maombi tu ndio njia pakee ya kututoa katika janga
hili Yesu Kristo mwenyewe alitufundisha kivitendo umuhimu wa kumuomba Mungu
Luka 6;12
“Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili
kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.”
Mungu
atashughulika na kila aina ya kamba za mauti zinazokuzunguka. Ukiacha corona
ziko kamba nyingine za mauti zinazokuzunguka zote kumbuka kuzisogeza mbele za
Munhu wetu naye atakusaidia hatoakuacha
Mwitikio wa Mungu wetu tunapoliitia jina lake
Mwandishi alipokuwa katika hali
hizo ngumu zlizomzunguka katika maisha yake na taabu zilizomzunguka katika
maisha yake na magumu yaliyokuwa yakimzunguka katika maisha yake Mungu
aklimuitikia kwa msingi huo aliweza kugundua kuwa kwekli Mungu ni mwema mno
Mungu ni mwingi wa rehema , mwenye huruma na neema naye huwahurumia watu wake
wanaoteseka na huwaokoa ndivyo neon lake lisemavyo angalia
Zaburi 86:5 “Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,
Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.”
Hatustahili kuishi, tulistahili kufa kwa sababu wote ni wenye dhambi hakuna
aliye mwema lakini trehema za mungu na neema yake zinamfanya atuitikie na
zinamfanya atuokoe na mauti na kutuweka huru kutoka katika kamaba za Mauti,
jambo pekee litakalotuletea neema ya mungu ni kumlilia yeye na kumwambia
Eeebwana utuhurumie, eee mwana wa Daudi utuhurumie Roho Mtakatifu utuhurumie,
roho zetu na za familia zetu na za watu wa taifa letu na taifa lako Israel na
jamii ya dunia na irehemiwe mbele zako na Mungu atasikia dua zetu, tuache
ushabiki, wakati huu, tusijitukuze sana wakati huu na kujifikiri kuwa sisi ni
bora sana wakati huu hapa ni toba tu bila kujali wewe ni nani na kuziitia
rehema za Mungu
Mungu atafanya nini? Zaburi 116:
6 “Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika,
akaniokoa” Mungu alimuokoa na Mungu
alimlinda mtumishi wake mwandishi wa zaburi hii kwa sababu wakati huu aliacha
hila aliacha nia mbaya aliacha kiburi na alijinyenyekeza, Neno hilo Nalidhilika
maana yake nilijishusha nilijinyenyekesha sikujifanya mtu maalumu, nilijishusha
nilishuka chini, nilijinyenyekeza kwenye nafasi ya mtu anayehitaji msaada,
wakati huu tuache kiburi cha kidhehebu, tuache kiburi cha kidini, tuache
kujifanya sisi ndio manabii na mitume na wachungaji wakubwa na kadhalika
tujinyenyekeshe na Mungu wetu ataturehemu, wakati mambo yanapokuwa mabaya acha
kujitokeza na kujifanya kuwa wewe ndio msemaji wa Mungu, pekee duniani, Ndio
maana wako waliosema corona itafutika na corona ikaendelea huu sio wakati wa
kujifanya wewe ni mtu maalumu ni wakati wa kujidhili na wakati wa magoti, ni
wakati wa kutulia na kumuacha Mungu atusaidie Mungu asipokuwa msaada wakati huu
nafsi zetu zitanyamazishwa ona
Zaburi
94:17 “Kama Bwana asingalikuwa msaada wangu, Nafsi
yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.” Wale wenye hekima ya dunia
hii na wenye kiburi wanaweza kudhani kuwa Mungu sio msaada wao wakati huu,
Lakini huu sio wakati wa kujitukuza na kutafuta kiki, lazima sasa tumuachie
Mungu apangue, asafishe afanye yaliyo mapenzi yake na kwa unyenyekevu Mkubwa
Mungu atatuponya tu, kwa sababu tuko mbali na hila na kiburi na tumeamua
kujinyenyekeza, kumbuka kuwa Bwana
huwapinga wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema, sote tuko katika umbo la
Nyangumi na tunapaswa kuomba rehema za Mungu naye atatusaidia katika njia
anayoijua yeye, sio wakati wa kunyooshea kidole mtu Fulani dhilika yaani
nyenyekea, usijifany mwenye hekima wakati huu zaidi ya toba hekima kubwa wakati
huu ni toba wala tusidhani imetosha nni toba wala tusiombee kingine chochote ni
toba na rehema tu na Mungu atatuitikia alimuitikia yona kwenye tumbo la
Nyangumi atatuitikia na sisi katika nchi ya walio hai haleluya!
1Wakoritho 1:27” bali
Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu
alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;” asomaye
na afahamu.
Na Mchungaji. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni