Zaburi 126:1-6 “Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama
waotao ndoto. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za
furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu. Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa
tukifurahi. Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.
Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake
akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake.”
Utangulizi:
Zaburi ya 126 ni mojawapo ya
zaburi zilizoitwa zaburi za kupandia yaani ziliimbwa wakati watu wanapanda
kwenda nyumbani mwa bwana Hekaluni aidha pia ni zaburi ya kihistoria
inayoelezea maisha ya wana wa Israel
hususani Wayahudi waliorudi kutoka uhamishoni Babeli, Wayahudi hao
walichukuliwa mateka wakati wa Mfalme Nebukadreza kwa kusudi la kuwatumikisha
hivyo waliishi uhamishoni kama watumwa walifanyishwa kazi kwa faida ya taifa la
wakaldayo, Hata hivyo baada ya miaka kadhaa kupita Mungu aliwajia tena watu
wake na kuwaletea ukombozi, yaani walirejea katika nchi yao kwa amri ya mfalme
Koreshi, makundi matatu ya wayahudi walirejea nyumbani kundi la Kwanza wakati
wa Zerubabel na kundi la pili wakati wa Ezra na la tatu wakati wa Nehemia hivyo inaaminika kuwa zaburi hii inaaminika
iliimbwa na wana wa Asafu waliorejea kutoka uhamishoni wakati wa Ezra ona
Ezra 2:1-2, 41. “1.
Basi hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao
waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua
mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; 2.
ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya,
Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya
wanaume wa watu wa Israeli; 41 Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na
wanane.”
Wimbo huu ulijulikana kama wimbo wa kupandia yaani wayahudi
walikuwa wakiuimba kila wakati walipokuwa wakipanda kwenda Yerusalemu kuabudu
Hekaluni, Kumbuka kuwa Nyumba ya Mungu
yaani Hekalu lilijengwa juu yam lima yaani sayuni na hivyo mara kwa mara mtu
alipoenda nyumbani kwa Bwana ilikuwa ni kama anapanda, Zaburi hii ilitungwa na
wana wa Asafu wakati wa Ezara na wimbo
huu ulitumika katika maeneo makuu matatu kushukuru, kuomba na kutia moyo
1. Kama
njia ya kumshukuru Mungu kwa wale waliokuwa wamerejea kutoka utumwani kwamba Mungu alikuwa amewatendea mambo
makubwa sana amewakomboa amewapa uhuru, nyakati za ukoloni wa kizamani mataifa
yenye nguvu walipowateka watu waliwachukua kuwa watumwa katika nchi zao, ni
watu wa ulaya kama Wayunani na warumi ndio walioanzisha iana ya utumwa au
utawala wa kumtawala mtu katika taifa lake lakini wakaldayo na mataifa ya kale
waliua watu na wengine waliwahamisha
hivyo kurudi nyumbani hasa wayahudi
kurudi Israel kwao ni Muujiza mkubwa sana ni kurudi katyika uwepo wa
Mungu ni jambo la kushangaza mataifa hivyo katika zaburi hii wanashukuru kurejea
nyumbani
Zaburi 126:2-3 unaonyesha “Ndipo kinywa
chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema
katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu. Bwana alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa tukifurahi.”
2. Aidha wimbo huu pia ulitumika kuwaombea dua na kuwatia moyo na kuwataka wale ambao bado walikuwa wamesalia huko utumwani kuendelea kumuomba Mungu ili nao waweze kutoka katika utumwa walikumbuka kuwa wako ndugu zao ambao bado hawajarejea hivyo walitoa wito na kumsihi Bwana awarejeza ndugu zao walioko kifungoni utumwani nchi ya mbali ona
Zaburi126:4 “Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.”
3. Na
eneo la tatu lilitumika kuwatia moyo watu wote waliokuwa wanapitia shida za
aina yoyote na changamoto za aina yoyote katika maisha kuwa maisha yao wanayoyapitia
ya aina yoyote ile yanafananishwa na maisha ya mkulima na kuwa mtu awaye yote
anapopitia taabu na machungu ya aina Fulani ni lazima aelewe kuwa wakati huo katika
maandiko unafananishwa na wakati wa kupanda, kupanda kunajumuisha maandalizi ya
shamba, kulima na kukatua ardhi na ujuzi
wa nyakati kwamba mvua zitaanza lini? huu ni wakati wa taabu na shida ambayo
inahitaji uvumilivu na kwa kweli wakati
wa kuandaa shamba mpaka kupanda ndio wakati Mgumu sana kwa mkulima kuliko
wakati wa kuvuna, wakati wa kuandaa shamba na kupanda wakulima wengi
hawaonekani mjini wala nyumbani, wanaamka mapema sana kwenda shambani ili
walime kabla jua halijawa kali, wakulima hupata taabu sana wanapojiandaa
kupanda kwa huku wakijua kuwa uko wakati watafurahia mavuno hivyo kipindi hiki
ni kipindi cha machozi. Wana wa Asafu
wanafananisha kipindi cha kupanda kama kipindi cha machozi na wakati wa kuvuna
kama wakati wa furaha, ona
Zaburi 126:5-6
“Wapandao
kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo
miganda yake.”
Ni muhimu kufahamu hili kuwa maisha ya mwanadamu yana
nyakati tofauti tofauti na kila wakati una umuhimu wake na wakati mwingine
wakati mmoja una maana sana kwaajili ya wakati mwingine na kila wakati ni
muhimu mno kwa msingi huo ni muhimu
kufahamu majira na nyakati ili uweze kujipanda vema kujua kuwa wakatio huu ni
wa kupanda au wa kuvuna ukichanganya nyakati utapata tabu sana ! huwezi kuishi maisha ya mavuno wakati wa
kipindi cha kupanda ukifanya hivyo utapata hasara kubwa sana ona
Muhubiri 3:1-8 “Kwa
kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati
wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa
yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati
wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na
wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati
wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Wakati wa kutafuta, na wakati wa
kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Wakati wa kurarua, na wakati
wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; Wakati wa kupenda, na
wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.”
Maisha yetu
yanapofananishwa na nyakati zozote za taabu katika Biblia wakati huo
unafananishwa na wakati wa kupanda “it’s a labour time” ni wakati wa taabu ni
wakati wa subira ni wakati wa uvumilivu, wakulima huwa wanajitoa muhanga sana
wakati wa kupanda yaani kuandaa mashamba kukatua ardhi huku wakivizia wakati
sahihi wa kufanya hivyo, sasa wanadamu wenye akili timamu wanapaswa kujua ni namna
gani watacheza au wataenenda na mapigo ya huo wakati, huwezi kuishi wakati wa
kupanda kama ndio wakati wa kuvuna ni lazima ujue nyakati kwani wakati mmoja
hutengeneza wakati mwingine, mtu akiishi kwa anasa wakati wa kupanda atakuwa na
msiba wakati wa mavuno, maana wenzake walivumilia wakajitoa kupanda hivyo
wakati wa mavuno watafurahi, wakati wa kupanda ni wakati wa subira na uvumilivu
wala sio wakati wa kupendeza, maandiko yanavyotuasa wakati wote tutapopitia
changamoto zinazotuonyesha kuwa ni kama tuko katika wakati wa kulia, au tuko
katika wakati wa kufanya kazi ni wakati
ambao unahitaji uvumilivu kwani hatimaye Mungu ataleta mvua na mazao yatakua na
tutavuna kwa furaha kubwa on
Yakobo
5:7-8,,10 -11 “7. Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata
kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani,
huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. 8.
Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana
kunakaribia.10-11 “10. Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe
mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.11. Angalieni, twawaita heri wao
waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya
kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”
Kimsingi neno la Mungu linatujuza
kuwa uko wakati Mungu atatutendea mema, jambo kubwa la msingi ni kujua nyakati
ni kuwa na hekima na ujuzi kwamba wakati huu ni wakati wa namna gani na ni jambo gani tunapaswa
kulifanya tusiishi kizemba kumbuka katika Israel kulikuwa na Kabila moja
waliojulikana kama wana wa Isakari hawa waliitwa watu wenye akili sana na kazi
yao kubwa walikuwa ni watu wenye kujua nyakati sio tu kujua nyakati bali pia
kujua jambo gani linapaswa kutendeka kwa wakati huo ona
1Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu
wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao
walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao”.
Kila mmoja wetu anapaswa kujua
nyakati na kuwa na akili kama wana wa isakari kujua nini kinatupasa kutenda kwa
wakati, mwezi januari mpaka machi ni miezi muhimu sana kwa wanafunzi na walimu
kujipanga kufundisha kwa bidii na kujifunza kwa bidii katika wakati huu wa mwanzo kama hatutajua
yatupasayo kufanya tukajifanya tunacheka na kumbe ni wakati wa kulia tunaweza kujikuta tunakosea, mkulima anapaswa
kujua wakati huwezi kupanda wakati wa hari, kama mwanafunzi anataka kustarehe
wakati anajua wazi ni wakati wa kujisomea kwa bidii wakati wake wa mavuno
utakuwa wakati wa majuto matokeo yatakapotoka anaweza kulia badala ya kufurahi
kwa vile hakufahamu ni wakati gani alipaswa kusoma kwa bidii, wote tunajua kuwa
ni mbaya sana mwanafunzi kuja na simu shuleni, wazazi pia wanapaswa kufahamu,
unampa mtoto simu aje nayo shuleni atasomaje? Hii ni sawa na kuutumia wakati
vibaya au kutokujua wakai na jambo la kufanya kwa wakati huo, huwezi
kuchanganya masomo na mapenzi, au uvutaji wa bangi na tabia za ajabu ajabu
wakati ukiwa mwanafunzi au kutumia ulevi au kufanya biashara ni dhahiri kuwa
huo sio wajati wa kufanya hayo kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa kuna wakati wa
kupanda wakati huu huwa kama wakati mchungu lakini kuna wakati wa kuvuna huu ni
wakati ambapo tutayafurahia matunda ya kazi zetu, tunapoanza shughuli za kila aina
mwanzoni mwa mwaka huu basi na tufanye kazi kwa bidii sana kama tupandao,lipa
ada ya shule kama uliila wakati wa disemba hukujua kuwa kuna januari
hukutofautisha wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna? Ahaa ulivuna kabla ya
kupanda sisi tutakudai ada ya shule tu! Wakati
ukiwa shuleni mwanafunzi tujisiomee kwa
bidii, tuhudhurie kazini kwa bidii, tuombe na kufanya ibada na kila lililowajibu wetu kwa bidii tukijua wazi
kuwa wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha na Mungu atatupa wakati wa faraja hatatuacha
tuumie tu atakuwa pamoja nasi na tutafurahia uwepo wake kwa nguvu na ushujaa
mwingi ataleta mvua yaani neema atayakuza mapando yetu na atatupa wakati wa
mavuno, wakati wa matokeo mazuri, wakati wa kuvuna kwa hiyo ni muhimu kwetu
tunapoendelea na wiki hii ya kazi ndani ya mwaka huu 2021 tujitoe kwa ngubvu
zetu zote tukijua ya kuwa wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha ! .
Wimbo wa Marehemu Fanuel sedekia
unatukumbusha umuhimu wa kujua Majira na nyakati na kuzitumia kwa utukufu wa
Mungu:-
Nitaimba haleluya asubuhi,
nitaimba haleluya Mchana, nitaimba haleluya jioni haleluya na hata usiku X2, Muhubiri
anasema kila jambo na wakati wake; wa kupanda na kuvuna wa kulia na kucheka x2 Haleluya nina wimbo; wa kila wakati na kila majira wimbo wa nyakati zote
na marira yote; wimbo huo ni Haleluya Nitaimba
haleluya asubuhi, nitaimba haleluya Mchana, nitaimba haleluya jioni haleluya na
hata usiku X2, – Fanuel Sedekia
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni