Mstari
wa Msingi:- Mwanzo 49:1-2 “Yakobo akawaita wanawe,
akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. Kusanyikeni,
msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.”
Utangulizi:
Wakati huu ulikuwa ni wakati Muhimu sana kwa Yakobo,
kuhitimisha maisha yake na kazi yake hapa Duniani, Yakobo kama mrihi wa Baraka
za Ibrahim na Isaka sasa ana watoto wengi na sasa anataka kuwabariki, kulingana
na kile Mungu alichokikusudia katika maisha yao ya baadaye, lakini kukiwa kwa
kiwango Fulani kimeathiriwa na mwenendo na tabia zao za maisha ya awali, sio tu
Yakobo anataka kuwabariki lakini, Yakobo anataka kutoa neno la kinabii kwa
watoto wake wote, yale atakayoyasema sio tu yana maana kubwa kwa wana wa Israel
na kabila zile kumi na mbili za wana wa Israel bali yana maana pana sana kwa
kila mmoja wetu hebu turudie tena kile ambacho neno la Mungu limekisema:-
Mwanzo
49:1-2
“Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni,
ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa
Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.”
a. Yakobo
anaanza kwa kuwaita wanae ili aweze kuwatabiria na kuwaambia yale yatakayotokea
katika maisha yao siku za baadaye, jambo ambalo pia linaweza kumtokea kila
mmoja wetu, sisi ni wana wa Israel kwa njia ya imani ni watoto wa Ibrahimu na
warithi wa ahadi za Mungu kama ilivyo kwa Isaka na Yakobo, kwa hivyo Yakobo ameita
mtoto mmoja baada ya mwingine ili aweze kuwabariki na kuwatamkia Baraka
sawasawa na matendo yao. Baraka hizo kimsingi zinamuhusu kila mmoja wetu
sawasawa na matendo yake na kwa kadiri ya neema ya Mungu, hivyo kwa kadiri
unavyotenda na kwa kadiri Mungu anavyousoma moyo wako ndio utakavyoona Baraka
zako na namna unavyoyaandaa maisha yako ya baadaye ama namna na jinsi
unavyoweza kuamua kubadilika.
b. Kabla ya
kuanza kuangalia jumbe zile za muhimu sana kuwahusu wana wa Israel ni vema
kwanza tukajua idadi yao na namna wana wa Israel walivyozaliwa.
Yakobo
alikuwa na wana kumi na wawili (12) kwa mujibu wa maandiko na binti mmoja
aitwae Dina, Mwanzo 35:23-26, “Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na
Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni. Wana wa Raheli, ni Yusufu
na Benyamini. Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali. Wana wa
Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa
katika Padan-aramu. watoto wake walitokana na wake zake wawili pamoja na
masuria wake wawili ambao kwa jumla yao ndio walimpatia watoto wale kumi na
mbili 12” Kwa hivyo tumeona maandiko yakituelekeza wana wa Israel 12
pamoja na mama zao:-
a. Kutoka kwa
Lea ni Reuben, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabulon
b. Kutokwa kwa
Raheli ni Yusufu na Benjamin
c. Kutoka kwa
suria kijakazi wa Lea Zilpah ni Gad na Asheri
d. Kutoka kwa
suria kijakazi wa Raheli ni Dani na Naftali
c.
Maana
za majina ya wana wa Israel.
-
Reuben – ni kijana
wa kwanza wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:32 “Lea
akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa
BWANA ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda.” – Maana ya
jina Bwana meona teso langu
-
Simeon – ni kijana
wa pili wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:33 “Akapata
mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi
sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.” – Maana ya
jina Bwana amesikia teso langu
-
Lawi – ni jina la
kijana wa tatu wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:34 “Akapata
mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami,
kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.”
– Maana ya jina Bwana ataungana nami
-
Yuda – ni jina la
kijana wan ne wa Yakobo kwa Leah Mwanzo 29:35 “Akapata
mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita
jina lake Yuda; akaacha kuzaa.” – maana ya jina Mara hii nitamsifu
Bwana
-
Dani – ni jina la
kijana wa tano wa Yakobo kwa Bilhah mjakazi wa Raheli Mwanzo 30:6 “Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia
sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.” –
Maana ya jina lake Bwana amenipa haki yangu
-
Naphtali – ni jina la
kijana wa sita wa Yakobo kwa Bilha mjakazi wa Raheli Mwanzo 30:8 “Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na
ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.” – Bwana
amenipa Ushindi
-
Gadi – ni kijana
wa saba wa Yakobo kwa Zilpa mjakazi wa Leah Mwanzo 30:11 “Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.”
– Bahati njema
-
Asheri – ni kijana
wa nane wa Yakobo kwa Zilpa mjakazi wa Leah Mwanzo 30:13 “Lea akasema, Ni heri mimi, maana wanawake wataniita heri.
Akamwita jina lake Asheri.” Maana ya jina lake – Nimebarikiwa
-
Issakari – ni kijana
wa tisa wa Yakobo kwa Leah, na kijana wa tano kwa Leah Mwanzo 30:18 “Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu
nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari.” Maana
ya jina lake Mungu amenilipa.
-
Zabuloni – ni kijana
wa kumi wa Yakobo na mwana wa sita kwa Leah Mwanzo 30:20 “Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu
atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni.”
Maana ya jina lake Bwana atakaa nami
-
Yusufu
–
ni kijana wa kumi na moja kwa Yakobo mzaliwa wa kwanza kwa Raheli Mwanzo
30:24 “Akamwita jina lake Yusufu, akisema, BWANA
aniongeze mwana mwingine.” Maana ya jina lake Bwana aniongeze.
-
Benjamini
–
Ni kijana wa kumi na moja wa Yakobo mzaliwa wa pili wa Raheli Mwanzo35: 18 “Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa,
akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.” Maana
ya jina lake mwana wa mkono wangu wa kuume.
Yakobo
anawaita wanawe:
Inawezekana ilikuwa ni desturi yake Yakobo kama
Kuhani wa Bwana na Kiongozi mkuu wa familia kuwakusanya wanae, lakini kusanyiko
hili lilikuwa na upekee, lilikuwa na upekee kwa wana wa Israel lakini vilevile
lina upakee kwa kila mmoja wetu leo, Hapa Yakobo hakuwa ametoa wito wa kawaida
tu, hili huenda lilikuwa kusanyiko lake la muhimu na la mwisho, lakini vilevile
lilikuwa ni kusanyiko maalumu la kinabii, Yakobo alikuwa anatangaza Baraka kwa
watoto wake mmoja baada ya mwingine wote walibarikiwa na pia kutabiriwa
sawasawa na jinsi baba yao alivyoona vema na vilevile sawasawa na Matendo yao, baba
yao hakuwa mwenyewe tu Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye, halikuwa kusanyiko
aliloliita yeye tu lilikuwa ni kusanyiko ambalo uwepo wa Mungu vilevile
ulikuwepo ili kuwabariki na kuwatamkia wana wa Israel Baraka zao na kuwakemea
na kuwaonya, Huku kwa kiwango kikubwa matendo yao yakichangia kwa kiwango
kikubwa Baraka zao na utabiri wa nini kinaenda kuwatokea wao katika siku za
mbele ni ukweli ulio wazi kuwa Yakobo anatufundisha kuwa iko siku Bwana
atazihukumu siri za wanadamu kama Yeye alivyohukumu maisha ya wanawe sawa na
matendo yao waliyoyafanya iwe wazi au sirini na kwa kadiri ya mabadiliko na
ukomavu wa mioyo yao, Bwana atazihukumu siri za wanadamu kwa kadiri ya injili
tuliyoipokea ona
Warumi
2:16 “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za
wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.”
Muhubiri
12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi,
pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”
Wito wa Yakobo kwa watoto wake unatukumbusha kuwa
kila mmoja anapaswa kujiangalia namna anavyoenenda kwani hata kama inaonekana
kama Mungu yuko Kimya anahukumu sawa na kutenda kwetu, ni wito wa Mungu kwa
kila mmoja kutenda vema na Mungu amemkusudia kila mmoja atende vema ili aweze
kumkubali na kumbariki na kumtakabali bila upendeleo:-
Mwanzo
4:6-7 “BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una
ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata
kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe,
walakini yapasa uishinde.”
Mungu anatoa wito kwa kila mmoja wetu kushinda uovu
na kutenda vyema, ni ukweli ulio wazi kuwa tukitenda vyema Mungu yuko tayari
kukubariki, lakini pia matendo yako yanaweza kuamua au kugharimu hatima yako,
hiki ndio kinachotokea kwa wana wa Israel mbele ya Yakobo katika siku hii, Ilikuwa
ni siku ya kila mmoja kusikiliza hukumu yake, makemeo yake na ujira wake
kutokana na kile kilichowapata., lakini vilevile kujua hatima yao.
Yatakayowapata
siku za Mwisho:!
Ni ukweli ulio wazi kuwa Israel alikuwa akisema na
watoto wake mmoja baada ya mwingine, alikuwa anawabariki, anawakemea na
kuwaonya lakini alikuwa akiwatabiria yatakayowapata siku zao za mwisho, sio tu
Yakobo alikuwa akitabiri, lakini alikuwa akiyaona yale Mungu atakayowafanyia
kabila moja baada ya jingine katika Israel, lakini sio wao tu Mungu alikuwa
anasema kwa kinywa cha Yakobo yale yatakayotupata wewe na mimi, tabia zetu na
matendo yetu ni ukweli ulio wazi kuwa yanatuunganisha katika kabila hizi, kila
mmoja anaungwa katika kabila mojawapo kutokana na kutenda kwake na hivyo endapo
katika maisha yako, utakuwa kama mmojawapo wa wana hawa wa Yakobo kitabia Basi
Msikilize Israel baba yako anavyokuambia, unabii sio lazima uje kwa mtu kujaa
roho na kuanza kutetemeka au kwa mbwembwe nyingi na makelele ya the major one
kama ilivyo leo au kelele za Prophesy!!!! ni ukweli ulio wazi kuwa Yakobo alikuwa
ameketi kwa utulivu na kusoma tabia za wanawe na alikusanya hata taarifa zao na
maswala mengine aliyaweka moyoni, kule kutenda kwao kwa mujibu wa Yakobo
kulitabiri maswala kadhaa yanayowajia baadaye, Yakobo aliitisha mkutano na
kuwaambia wanawe kusanyikeni niwaambie mambo yatakayowapata siku za mwisho hii
ilikuwa ni muda wa kuwatolea unabii ulio wazi wazi bila mbwembwe, leo na mimi
nitakutolea unabii ulio wazi wazi kwa neno hili bila mbwembwe zozote, Yakobo
aliweza kuwaelezea siri kubwa na za wazi kuhusu siku zao za mwisho na namna
itakavyokuwa katika maisha yao, uwepo wa Mungu ulikuwepo kumfunulia na alijua
wazi kuwa anakwenda kuzungumza nao waziwazi na kuwa mambo hayo yangetokea!
Msikilizeni
Israel Baba Yenu!
Hili ndio eneo muhimu ambalo kila mmoja anapaswa
kusikiliza kwa makini, sio Reuben tu, au Simeoni, au Lawi au Yuda au Isakari,
au Yusufu na kadhalika kila mmoja anapaswa kusikiliza kwa makini sana,
Yakobo anawaita wanawe na ni wazi kuwa
anazungumzia ubinadamu wake ambao kila mtu anao, matendo yetu yote
tunayoyafanya wakati mwingine yanafanyika kwa sababu ya ubinadamu wetu, sisi ni
wana wa Yakobo ni wana wa Adamu sisi ni binadamu hatupaswi kujilaumu kwa sababu
ya ubinadamu wetu, Lakini ubinadamu wetu una nafasi kubwa sana ya kuamua hatima
yaetu ya Kiroho na kama tukikubali tutabadilika kwa msingi huo tusikubali kamwe
kuendeshwa na mwili 1Thessalonike 4:4 “kila
mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;” Yakobo
anapojiita Yakobo alikuwa anakumbuka ubinadamu wake anafahamu kuwa hata watoto
wake wanafahamu kuwa yeye ni binadamu, Lakini Yakobo anaongezea kuwa
wamsikilize tu sio kama Yakobo lakini vilevile kama Baba yao, akiwa kama Yakobo
hata wanawe waliweza kumdanganya, walifahamu historia ya maisha yake hivyo ni
vigumu kumsikiliza sana kama yakobo Yakobo, Yakobo ni mwili, Yakobo ni kipindi
cha mapambano, sasa wamsikilize kama Mtu aliyebadilishwa na Mungu Msikilizeni
Israel, huyu alikuwa ni Yakobo aliyebadilika lakini pia mtu mwenye uzoefu aliyeona
mengi hivvyo wamsikilize kama baba pia kama kiongozi wa familia yao
aliyetembea na Mungu!
1.
Rubeni
(Bwana
ameona teso langu)
Mwanzo 49:3-4 “Reubeni,
u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine
kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu
ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.”
Yakobo
anataka kumbariki Reubeni na anatambua wazi kuwa huyu ndiye kijana wake wa
kwanza mzaliwa wake wa kwanza ni malimbuko yake Duniani, ni mwenye nguvu na ni
mkubwa kuliko wengine lakini Yakobo anaondoa mamlaka kwake, kwa mujibu wa
tamaduni za Israel huyu ni mrithi halali wa Yakobo, na wazaliwa wa kwanza walikuwa na kibali
maalumu kutoka kwa Mungu cha kubeba kusudi lake, Hata kama ni ujio wa Masihi
unapaswa kupitia kwake hata utawala pia Lakini Yakobo anamkataa kwa sababu
kadhaa, Reubeni alikuwa na tatizo, alikuwa hana uadilifu, alikuwa hana adabu,
lakini sio hivyo tu alikuwa ni mtu asiye na nidhamu na asiyeweza kujizuia,
alikuwa ni mtu aliyeshindwa kudhibiti tamaa, na mihemko yake, na hisia zake,
Hivyo hangeweza kuwa kuhani wala hangeweza kuwa mfalme, hawezi kuwa kiongozi wa
kiroho wala wa kijamii wala wa kisiasa kwa sababu alikuwa mwenye tamaa aliweza
kutembea hata na suria wa baba yake hakuweza kujizuia, hakuwa na adabu aliruka
mpaka ona
Mwanzo 35:21-22 “Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili
wa mnara wa Ederi.Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni
akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao
wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.”
Unaona Mungu
katika hekima yake aliamua kuuondoa Ukuhani, Unabii na Ufalme kwa Reuben na
kuwapa wengine, Reuben alilipa gharama kubwa ya uovu wake na haki yake ya
kukosa uadilifu, kwa vyovyote vile Mungu haitaji watu wanaovuka mpaka kama
maji, Dhambi aliyoifanya ilikuwa sio ya kawaida ilikuwa amepitiliza ule mstari
wa kawaida wa utendaji dhambi ni dhambi ambayo ikifanyika hata kwa wapagani
huwa inaweza kuwapa watu taharuki Lakini Reuben alikuwa ni mtu aliyeshindwa
kujizuia lilipokuja swala la tamaa na
uwezo wa kustahimili mihemko yake! Hivyo alimvinjia heshima baba yake!
1Wakoritho 5:12 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa
ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.”
Reuben
alifanya zinaa na mke wa baba yake, hii ilikuwa dhambi iliyopitiliza katika
uadilifu, kwa hiyo ni mwana mkubwa wa Yakobo, Malimbuko ya Israel lakini hana
nidhamu, hana adabu, watu wasio na nidhamu, watu wasioeleweka watu wasiotulia,
watu wasio na misimamo, ni kama maji yanayotokota, ni kama mawimbi ya bahari
hawana utulivu hawa hawawezi kuwa viongozi, hawawezi kuwa watumishi wa Mungu,
ukweli ni kuwa hakuna kuhani, wala nabii, wala mwamuzi aliyetokea kabila la
Reubeni unapoyachunguza maandiko, Yeye
ni mfano wa watu wote wenye tabia mbaya, watu wagomvi, watu wasio na busara,
watu wasio na adabu watu wasiojiheshimu, watu wanaoshindwa kuidhibiti mihemko
yao, watu wanaoshindwa kuheshimu wazazi, Biblia inaagiza wazi kwamba mtu asilale na mke
wa baba yake awe mkubwa au mdogo hiyo ni sawa na kulala na mama yako, aidha
maandiko yameonyesha watu wa karibu ambao kwa uadilifu haikuwa vema
kushirikiana nao tendo la Ndoa ona
Mambo ya walawi 18:5-18 “Kwa ajili ya hayo
mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo;
mimi ndimi BWANA. Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa
jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. Utupu wa baba yako,
wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. Utupu
wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. Utupu wa umbu
lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani
mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.Utupu wa binti ya
mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio
utupu wako mwenyewe. Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba
yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. Usifunue utupu wa umbu lake baba
yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. Usifunue utupu wa umbu la mama yako;
maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. Usifunue utupu wa ndugu ya baba
yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. Usifunue utupu wa mkweo
mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. Usifunue utupu wa
mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.Usifunue utupu wa mwanamke na binti
yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu
wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. Wala usitwae mwanamke pamoja na
nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu
hai.”
Tofauti kubwa
kati ya binadamu na mnyama ni kuwa wanadamu wana utashi na wanaweza kutumia
vema utashi wao na kuamua kwa busara, haikuwa jambo jema mwanamke aliyezaa na
baba yako wewe ukaingia, Reuben anawakilisha watu ambao wangekuwa na uwezo wa
kuwa na nafasi kubwa lakini wanapoteza nafasi zao kwa sababu ya kukosa
uvumilivu na kukosa adabu, huenda wangekuwa watu wakubwa sana lakini kwaajili
ya tabia zao zisizotabirika wamepoteza nafasi zao, sote hatujui Mungu
ametukusudia kuwa watu wa namna gani baadaye kwa msingi huo tangu sasa ni
lazima tuhakikishe tunaishi kwa uadilifu, hususani katika nyakati hizi ambapo
vyombo vya habari, na teknolojia vinauwezo wa kutunza kumbukumbu zetu nzuri na
mbaya pia, kama utakuja kuwa kiongozi mkubwa sana huna budi kuyatunza maisha
yako kuanzia sasa, Mungu atupe neema ya
kutunza tabia zetu. Ni wazi kuwa sifa za mtu anayetakiwa kuja kuwa askofu hazianzi
akiwa askofu bali zinaanza akiwa mtu wa kawaida, na mkristo wa kawaida ndipo
anapokuja kuwa na uwezo wa kufiti katika mazingira yanayokusudiwa baadaye na
Mungu! Usifanye mambo ya kijinga wala usipige picha za kijinga kwa sababu hujui
utakuja kuwa nani baadaye!, Reuben alipoteza sifa za kuwa kiongozi wa
kifamilia, kiroho na kisiasa alijiingiza chini ya laana yeye mwenyewe, kwa
kulala na mke wa baba yake alijiletea laana ona
Kumbukumbu la Torati 27:20 “Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa
amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.” Aidha tabia ya Rubeni inawakilisjha watu
wasioshehimu wakubwa zao kiumri, kazini na popote pale kutokuwaheshimu wazazi
na wakubwa kunatuondolea Baraka Mungu alizozikusudia kwetu ona Waefeso 6:2-3
“Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo
amri ya kwanza yenye ahadi, Upate
heri, ukae siku nyingi katika dunia.” Kuwaheshimu wazazi wetu au
watu waliotuzidi umri ni pamoja na kuwathamini, kutambua mamlaka yao,kuwatendea
kwa heshima, na kuwahifadhi, Reuben alivuka mpaka huo
Reuben
alijiletea shida Roho Mtakatifua alikumbuka tukio lake na Israel aliliweka
moyoni na hivyo alipoteza Baraka iliyokusudiwa kwake, Biblia ya kiingereza
inatumia maneno YOU WILL NO LONGER EXCEL neno Excel katika Kamusi
ya kiingereza ya American Dictionary linasomeka – to do something very well
or be highly skilled and be better than most others or to be extrimly good at
something, Kwa hiyo Yakobo aliposema Reuben usiwe na ukuu, ni kama alikuwa anamaanisha
hakutoakuwa na lolote jema kutoka kwake, Reuben anapoteza haki ya mzaliwa wa
kwanza, anapoteza nafasi ya uongozi, anapoteza heshima, anapoteza mamlaka, kwa
sababu ya kukosa uadilifu, kwa msingi huo kupoteza sifa za uadilifu na
kutokujitia nidhamu kunaweza kutufanya tupoteze nafasi zetu kama viongozi,
mbaya zaidi unapoteza kibali kwa Bwana!, Katika nyakati za Kanisa la kwanza mtu
alipokuwa anataka kujitoa kwaajili ya maongozi ya kanisa ziko sifa ambazo mtu
anapaswa kuwa nazo za uadilifu, ni kweli kuwa sisi ni binadamu lakini maandiko
yanatufundisha kutunza uadilifu ili kupata Baraka za kiungu za kuwa kiongozi wa
wengine kazi ambayo ina heshima kubwa sana kwa Mungu.
1Timotheo 3:2-7 “Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke
mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye
kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa
kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake
vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia
nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka
karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa
kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa
Ibilisi”
Katika
nyakati za leo tunao kina Reuben wengi hauhitaji kutafuta unabii kwanini
hufanikiwi sababu ziko wazi katika maandiko, huitaji kutafuta nani amekuroga
sababu ziko wazi, kama unashindwa kujidhibiti, una hasira, unagombana na kila mtu,
huwezi kuzuia tamaa zako, huna adabu, unatembea na mijimama mikubwa kuliko umri
wako ambao wangestahili kuwa wake za
baba zako, hueshimu huyu ni mke wa nani usitegemee kuwa na ukuu Yakobo anasema,
hivyo ni onyo kwa kanisa vilevile kwamba wengi walio wa kwanza watakuwa wa
mwisho hatupaswi kujivunia lolote, hatupaswi kujiamini kupita kawaida,
hatupaswi, hatupaswi kujikweza, Mungu anaweza kuinua yeyote na kushusha yeyote
Mathayo 19:30 “Lakini
wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
Tabia ya
kupenda ukubwa na kujiamini kupita kawaida na hata kujikweza itawafanya wengi
kushushwa na Mungu, wako watu hawana adabu kwa wale waliowazidi umri na wakati
mwingine wako tayari hata kuwadhalilisha na kuwakosea adabu au kuwafanya
waumbuke hao ni wa kabila la Reuben ni watu ambao hawatatoboa katika ukuu Mungu
atawashusha
Luka 14:11 “Kwa
maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.” 1Petro
5:5-6 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee.
Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu
huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni
chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;”
Kama
tutajirekebisha na kukataa kuwa Reuben leo Mungu atatuinua kwa wakati wake,
wewe kama ni muisraeli leo nasema msikilizieni Israel Baba yenu, Reuben hakuwa
na nafasi tena ya kujirekebisha lakini wewe unaweza kuwa na nafasi ya kutubu na
kuachana kabisa na kabila la Reuben, Bwana akupe neema ya kumsikiliza Israel
baba yetu katika jina la Yesu amen! Reuben alihukumiwa kwa kutokumuheshimu baba
yake lakini kwa habari ya uhusiano na Yusufu Reuben alikuwa na mpango wa
Kumuokoa Yusufu, ila mpango wake wa wokovu haukufanikiwa Israel aliwabariki watoto wake na kuwadhibu
kutokna na namna walivyomtendea yeye au Yusufu au watu wengine, Mungu
atatuhukumu kwa kadiri tulivyomtendea yeye na watu wengine ona
Mwanzo 37:19-22 “Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto
anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi
tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.Reubeni
akasikia akamwokoa katika mikono yao, akasema, Tusimwue. Reubeni akawaambia,
Msimwage damu; mtupeni katika birika hii iliyopo nyikani, wala msimguse; ili
apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake.”
Sio kila mtu
mbaya ana mambo mabaya wakati mwingine yako mema vilevile Yakobo alikuwa
akiwahukumu watoto wake kulingana na uhusiano wakliokuwa nao kwake kama baba na
kwa wenzake ndugu zao kama Yusufu, na kwa watu wengine, Mungu atahukumu
sawasawa na jinsi tunavyojali mahusiano yetu kwake na halikadhalika mahusiano
yetu na watu wengine,
1Yohana 4:20-21 “Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake,
ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda
Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye
Mungu, ampende na ndugu yake.”
2.
Simeon
(Bwana
amesikia teso langu) na Lawi (Bwana ataungana nami).
Mwanzo 49: 5-7 “Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri. Nafsi yangu,
usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika
ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe; Ghadhabu
yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma.
Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.”
Simeoni na
Lawi wote wanapokea unabii unaofanana Israel pamoja na Roho Mtakatifu
wanawatawanya hawa, hawapewi ukubwa hata kidogo, wao wanaitwa vyombo vya
ghadhabu au ukatili, Israel anailaani Hasira kali waliyokuwa nayo, wameshindwa
kujizuia wako tayari hata kuua mtu, walikasirika sana aliponajisiwa dada yao
Dina, hata watu wale walipotaka amani nao wao walikuwa na mpango wa kuwafutilia
mbali watu waliojisalimisha kwao waliwaua kwa makali ya upanga wala hawakuwa na
huruma walikuwa katili, wala hawakutaka ushauri wa baba yao, wao walikuwa na
Hasira kali kiasi ambacho walisahau vilevile kuwa Mungu ni wa rehema Yakobo
1:20 “kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki
ya Mungu.” Ni jambo la kusikitisha sana kuwa wako watu wengi wa
Mungu wanasumbuliwa na hasira na wanadhani wanastahili Baraka za Mungu ilihali
wanayo maeneo ya kutengeneza, kwa sababu ya hasira wengi tumewatamkia maneno
mabaya wengine, tumekimbilia kuwatenga watu na kuwahukumu na kutoa adhabu mbaya
hata bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza na hata bila kujali kuwa wako watu
hawawezi kujieleza, Simeoni na Lawi walifanya hila na kwa hasira waliwaua
washekemu jambo ambalo Israel alilikumbuka na Roho Mtakatifu alilikumbuka ona
ilivyokua
Mwanzo 34:1-31 “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona
binti za nchi. Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa,
akalala naye, akambikiri. Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda
huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri. Shekemu akamwambia
Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu. Basi Yakobo akasikia
ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama
wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja. Akatoka Hamori, babaye
Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja
kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya
upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka.Hamori
akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini,
mpeni amwoe. Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu. Nanyi
mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo,
mkapate mali humo. Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na
nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa. Mjapoongeza sana mahari na
zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke
wangu.Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu
Dina, umbu lao, wakawaambia, Hatuwezi kufanya neno hili, tumpe umbu letu mtu
asiyetahiriwa; ingekuwa aibu kwetu. Lakini kwa sharti hii tu tutapatana nanyi;
mkiwa kama sisi, akitahiriwa kila mwanamume wenu, ndipo tutawapa ninyi binti
yetu, na sisi tutatwaa binti zenu tutakaa pamoja nanyi, nasi tutakuwa watu
wamoja. Lakini kama hamtusikii na kutahiriwa, basi tutamtwaa umbu letu, nasi
tutakwenda zetu. Maneno yao yakawa mema machoni pa Hamori, na machoni pa
Shekemu, mwana wa Hamori. Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana
amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani
mwa babaye. Hamori, na Shekemu mwanawe, wakaja langoni pa mji wao, wakasema na
watu wa mji wao, wakinena, Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika
nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae
binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao. Lakini kwa sharti hiyo moja
tu watapatana nasi wakae wote kwetu, tuwe watu wamoja, kama tukitahiriwa kila
mwanamume, kama hawa walivyotahiriwa. Je! Kondoo zao, na mali zao, na wanyama
wao wote hawatakuwa mali zetu? Basi na tupatane nao tu, nao watakaa kwetu. Wakawasikia
Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa
kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake. Ikawa siku ya tatu,
walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina,
wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote. Wakawaua
Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba
ya Shekemu, wakatoka.Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara
mji kwa sababu wamemharibu umbu lao. Wakachukua kondoo zao, na ng'ombe zao, na
punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni. Wakatwaa
na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani
mwao wakavichukua mateka. Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha,
kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na
mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa,
mimi na nyumba yangu. Nao wakasema, Je! Ni vema amtendee umbu letu kama kahaba?
” unaona jamaa hawa walikuwa na Hasira na wanaitwa
vyombo vya hasira na Israel anasema anawatawanya, hataki kujulikana kupitia
wao, Israel hataitwa kwa jina la watu wenye Hasira kiasi hiki, hawa ni vyombo
vya dola, tatizo kubwa la Simeon na Lawi ni hasira hasira yao iliwafanya
wafanye dhambi, wafanye hata yale ambayo Mungu hakuwa ameyakusudia Waefeso
4:26 Biblia inasema “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na
uchungu wenu bado haujawatoka;” Maandiko yanatutaka tuwe mbali na
hasira, uchungu na ghadhabu na hasira ni mbaya
Wasimeoni hawakupewa ukubwa kwa sababu ya hasira yao Waefeso 4:31 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano
yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;” Israel aliwatawanya
wawe watumishi wa jamii kokote waliko, tena wasiwe na urithi katika Israel,
unabii wa kuwatawanya na kuwagawa haukuwa mwema kwao, kabila la Simeoni ndio
lilikuwa dhaifu kuliko yote katika Israel walikuwa wengi walipotoka misri
lakini Mungu aliwapunguza sana Hesabu 1:23 “wale
waliohesabiwa katika kabila ya Simeoni, walikuwa watu hamsini na kenda elfu na
mia tatu” (59,300), lakini walipofika Kanaani miaka 35 baadaye walikuwa
wachache mno Hesabu 26:14 “Hizi ndizo jamaa za
Wasimeoni, watu ishirini na mbili elfu na mia mbili.” (22,200) kwa
hiyo kabila la Simeoni lilitoweka na kuchanganywa na Yuda. Ona katika Yoshua 19:1
Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya
Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa
zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda”. Nitawagawa
nitawatawanya katika Israel unabii huu ulitimia kwani kabila ya Simeoni
ilitoweka na walawi walipata Baraka ya kuwa watumishi wa Mungu tu, wao
waliponea chupuchupu baada ya kuonyesha utii kwa Mungu wakati kabila nyingine
zilipoasi jangwani Kutoka 32:26-28 “Basi Musa
alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe
dhihaka kati ya adui zao, ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago,
akasema, Mtu awaye yote aliye upande wa BWANA, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote
wakamkusanyikia Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na
ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango
kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila
mtu jirani yake. Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa,
wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.” Walawi waliweza kujiokoa
kwa kumsogelea Mungu, Lakini kabila ya Simeoni ilitawanyika na kupotea, kila
mmoja anaweza kuwa ni mwana wa Israel kila mmoja anaweza kuwa mwamini, tunaweza
kuwa kabisa hatunywi, pombe, hatufanyi zinaa, wala uasherati, wala sio wadhulumaji
na ama watenda maovu mengine lakini Maandiko yanatufundisha kuwa Haisra ni
mbaya mno, ni kwaajili ya Hasira Musa alizuiliwa asiingie katika nchi ya
kanaani, kumbuka Musa ni wa kabila ya walawi, Zaburi 106: 32-33 “Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata
Musa kwa ajili yao, Kwa sababu waliiasi roho yake, Akasema yasiyofaa kwa midomo
yake.” Hasira na ghadhau zinaweza kuwakosesha watu wengi wa Mungu
mbingu, hatuna budi kumuomba Mungu atuwezeshe tusitawanywe na kufutiliwa mbali
na Mungu na kunyimwa urithi kama ilivyokuwa kwa Simeoni na Lawi kwa sababu ya
Hasira Yakobo anailaani hasira ya vijana hawa kwa kiingereza CURSED BE THEIR
ANGER, Ghadhabu yao na ilaaniwe! Kwanini Israel anawaweka Simeoni pamoja na
Lawi, hawa walikuwa ni ndugu na marafiki, ndugu-rafiki, mkubwa alikuwa Simeon
na mdogo wake ni Lawi, walipendana na walikuwa na mtindo wao wa maisha
wanasikilizana mno na wakiamua lao wameamua, Lawi kwa vile alikuwa mdogo alimsikiliza
sana Simeon, kwa hivyo walikuwa watu wenye mambo yao uhusiano wao na baba yao
ni kuwa hawakumsikiliza baba yao walidharau ile hali ya moyo wa baba yao
hawakusikiliza Kumbukumbu la Torati 27:16 “Na
alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.”
Katika uhusiano wao na baba hawakumsikiliza, walijiamulia mambo yao
wenyewe, Katika uhusiano wao kwa wengine na hasa Yusufu Simeon ndiye aliyetoa
wazo la kumuangamiza ndugu yao tena akimuita bwana ndoto ona Mwanzo 37:18-20
“Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia,
wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule
bwana wa ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika
mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje” mtu
mmoja ataniuliza swali tunawezaje kujua kama Simeon ndiye anahusika moja kwa
moja na mpango ule, Reuben hakukubali Yusufu auawe, alitaka kumuokoa baadaye
amrejeshe kwa baba yake, lakini Simon na wengine walikuwa na nia thabiti ya
kutekeleza jambo hilo ona Yusufu aliweza kuwaelewa wote alipowasumbua na
kuwababaisha na kumtia ndani mmoja wao ona Mwanzo 42:15-24 “Mtabainika kwa njia hii; aishivyo Farao, hamtoki hapa,
asipokuja huku huyo ndugu yenu mdogo. Mpelekeni mmoja wenu, aende akamlete
ndugu yenu, na ninyi mtafungwa, hata maneno yenu yahakikishwe, kama mna kweli
ninyi; ikiwa sivyo, aishivyo Farao, ninyi ni wapelelezi. Akawatia wote gerezani
siku tatu. Yusufu akawaambia siku ya tatu, Fanyeni hivi, mkaishi, maana mimi
namcha Mungu. Kama ni wa kweli ninyi ndugu yenu mmoja na afungwe gerezani,
nanyi nendeni mkachukue nafaka kwa njaa ya nyumba zenu, mkamlete ndugu yenu
mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa. Ndivyo
walivyofanya. Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosa ndugu yetu, kwa kuwa tuliona
shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia kwa hiyo shida hii imetupata.
Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, msimkose kijana? Wala
hamkusikia; kwa hiyo damu yake inatakwa tena. Wala hawakujua ya kwamba Yusufu
anawasikia, kwa sababu alikuwapo mkalimani kati yao. Akajitenga nao akalia.
Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga
mbele ya macho yao.”
Yusufu
alifanya upelelezi wa kutosha na wote walibainika namna walivyojihusisha na
maisha yake na Yusufu alipata Muda wa kuelezea upelelezi wake kwa baba yake
kila kilichofanyika kwa hivyo unaweza kuona kitendo cha kumfunga Simeon na
kuruhusu wengine ilikuwa wazi kuwa mwanzilishi wa wazo lile ovu alikuwa ni huyu
Bwana, Mungu yuko tayari kumbariki
yeyote anayefanya vema, watu wa kabila la Lawi baadaye walijifunza kuwa upende
wa Mungu, walibadilika na kuwa watu wenye kushika sharia na uadilifu na hivyo
ingawa walikuwa wametawanywa, wao walifawanywa kama watumishi wa Mungu, Walawi
walijiokoa na laana hii baadaye kwa kusimama upande wa Mungu, ahadi za Mungu na
hata laana za wazazi wetu zinaweza kubadilika kwetu kwa toba na kubadili
mwenendo wetu usiofaa, Bwana ampe neema kila mmoja wetu, kubadilika ili
kujilinda na mawaa na kupata Baraka alizokusudia Mungu katika maisha yetu
katika jina la Yesu ameeen!
3.
Yuda (Mara hii
nitamsifu Bwana)
Mwanzo 49:8-12 “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui
zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika
mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke;
ni nani atakayemwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,Wala mfanya
sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa
watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika
mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.”
Yuda hakuwa
mwema kuliko kaka zake, kila mmoja ana udhaifu wake kama baba yao alivyojieleza
kuwa yeye ni Yakobo, lakini pia ni Israel na ni Baba yao, lakini Yuda alikuwa na moyo wa kukubali kujitoa kwaajili
ya familia yake baba yake na maisha ya Yusufu, Benjamin na baba yake pia,
Mpango wa kwanza wa ukombozi kwa Yuda unaonekana kwanza kwa Yusufu akiwa na
mpango tofauti na nduguze hakutaka auawe alikuwa mwema kwa Yusufu alitafuta
kuokoa maisha yake Mwanzo 37:26 “Yuda akawaambia
ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake?” Yuda
aidha alikuwa tayari kuyatoa maisha yake kwaajili ya Benjamin na kwaajili ya
Maisha ya baba yake ona Mwanzo 44:1-34 “Akamwamuru
yule msimamizi wa nyumba yake akisema, Jaza magunia ya watu hawa chakula kwa
kadiri wawezavyo kuchukua, utie na fedha ya kila mtu kinywani mwa gunia lake.
Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule
mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu.
Asubuhi kulipopambazuka, hao watu wakapewa ruhusa, wao na punda zao. Na
walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa
nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini
mmelipa mabaya kwa mema? Je! Kikombe hiki, sicho anyweacho bwana wangu? Naye
hufanya uaguzi kwa hicho. Mmefanya vibaya kwa kufanya hivi. Akawafuata, akawapata, na kuwaambia maneno
hayo. Wakamwambia, Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Hasha!
Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia
yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa
bwana wako fedha au dhahabu? Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa
wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu. Akasema, Basi na
iwe hivyo kama mlivyosema, Mtu atakayeonekana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu,
na ninyi mtakuwa hamna hatia. Wakafanya haraka, wakashusha kila mtu gunia lake,
na kufungua kila mtu gunia lake. Naye akatafuta, akaanza kwa mkubwa na kuisha
kwa mdogo. Kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini. Wakararua nguo zao,
wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini. Akaja Yuda na
ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia
kifudifudi. Yusufu akawaambia, Ni tendo gani hili mlilolitenda? Hamkujua ya
kwamba mtu kama mimi naweza kufanya uaguzi? Yuda akasema,Tumwambie nini bwana
wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama,
sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi
mwake. Akasema, Hasha! Nisifanye hivi; mtu ambaye kikombe kilionekana mkononi
mwake, ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Nanyi enendeni zenu kwa amani kwa baba
yenu. Ndipo Yuda akamkaribia, akasema, Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na
aseme neno moja masikioni mwa bwana wangu, wala hasira yako isimwakie mtumwa
wako, maana wewe u kama Farao. Wewe, bwana wangu, ulituuliza watumwa wako,
ukisema, Je! Mnaye baba, au ndugu? Tukakuambia wewe, bwana wangu, Tunaye baba,
naye ni mzee, na mwana wa uzee wake ni mdogo, na nduguye amekufa; amebaki yeye
peke yake wa katika tumbo la mamaye, na baba yake anampenda. Ukatuambia watumwa
wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie. Tukakuambia, bwana wangu,
Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa. Ukatuambia
watumwa wako, Asiposhuka ndugu yenu mdogo pamoja nanyi, hamtaniona uso wangu
tena Ikawa tulipokwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamwarifu maneno yako,
bwana wangu. Kisha baba yetu akanena, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo.
Tukasema, Hatuwezi kwenda; ndugu yetu mdogo akiwapo pamoja nasi, tutashuka,
maana hatutaweza kuuona uso wa mtu huyo, ndugu yetu mdogo asipokuwa pamoja
nasi. Mtumwa wako, baba yangu, akatuambia, Mnajua ya kuwa mke wangu alinizalia
wana wawili; mmoja alitoka kwangu, nikasema, Bila shaka ameraruliwa, wala
sikumwona tangu hapo. Na mkiniondolea huyu naye, na madhara yakimpata,
mtashusha mvi zangu na msiba kaburini. Basi, nikienda kwa mtumwa wako, baba
yangu, na huyu kijana hayupo pamoja nasi, iwapo roho yake imeshikamana na roho
ya kijana; itakuwa atakapoona ya kwamba huyu kijana hayuko, atakufa; na watumwa
wako watashusha mvi za mtumwa wako, baba yetu, kwa huzuni kaburini. Kwa maana
mtumwa wako alijifanya mdhamini wa huyu kijana kwa baba yangu, nikisema,
Nisipomrudisha kwako, nitakuwa na hatia kwa baba yangu sikuzote. Basi, sasa
nakusihi, uniache mimi mtumwa wako nikae badala ya huyu kijana kuwa mtumwa wa
bwana wangu; na huyu kijana umwache aende pamoja na nduguze. Kwa maana
nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije
nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.”
Israel pamoja
na Roho wa Mungu walichunguza moyo wa Yuda na kugundua kuwa ndani mwake
kulikuwa na Roho ya wokovu, alikuwa yuko tayari kuyatoa maisha yake kwaajili
yaw engine kwa msingi huo ingawa Yuda anaoenekana kuwa na madhaifu ya kawaida
ya kibinadamu kama kutokutaka kutimiza haki kwa mkwewe tamari na hata kulala
naye kama kahaba
Mwanzo 38:24-26 “Ikawa
baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya
uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
Alipotolewa, alipeleka watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu
mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na
kamba hii, na fimbo hii. Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko
mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.”
Mungu
aliangalia moyo wake na kuona kuwa ni moyo wa tofauti, Baraka zote hizo Mungu
alizitoa kwa neema na kulingana na matendo yao, udhaifu wa maswala Binafsi ya
Yuda haukuwa, sababu ya Mungu kupuuza uwezo wake mkubwa wa kuwapenda ndugu zake
na kuwa tayari kufa kwaajili yao na kwaajili hii unabii kuhusu kuja kwa Masihi
umeunganishwa na moja kwa moja kabila la Yuda hivyo
a.
Yuda Ndugu zake watamsifu – kutokana na wokovu wake
mkubwa kwa jamii yake na kuwafanya ndugu zake wasiingia katika dhambi na
kumwaga Damu ya ndugu yao, kumlinda Benjamin na kumlinda na kujali moyo wa baba
yao na kumlinda Yusufu, wazo lake na mpangio wake ulikubalika katika jamii yake
na alisifiwa kama sababu ya ukombozi wa wanadamu wote.
b.
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya
sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa
watamtii, ni wazi kuwa watawala wengi na manabii wengi na wafalme wengi
walitoka katika kabila hili lakini vilevile Masihi anaunganishwa kuwa ni wa
kabila la Yuda Ufunuo 5:5 “Na mmojawapo wa wale
wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la
Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.”
Baada ya miaka kama 640 hivi alitokea Kiongozi maarufu sana wa kabila la
Yuda aliyeitwa Daudi na baada ya miaka kama 1600 alitokea Yesu Kristo yeye
ambaye mataifa watamtii (Shiloh) Watu wa kabila hili hawaangalii maslahi yao,
ni watu ambao hawana ubinafsi, pamoja na madhaifu yao lakini marazote wako
tayari kufa kwaajili ya wengine wako tayari kujitoa dhabihu, Mungu anaweza
kumtumia mtu kuwa kiongozi, mtu kuwa nabiii, mtu kuwa kuhani kama mtu huyo
anamoyo wa huduma kwa wengine ni watu wenye kujali wengine na kuwa tayari
kuokoa wengina kuwasaidia wengine kujitoa kuwa mbadala wa wengine kuwatetea
wengine ndio ambao wanaweza kutumiwa na Mungu katika Baraka kubwa
anazozikusudia kwa watu wake!
4.
Zabuloni
(Bwana
atakaa nami).
Mwanzo 49:13 “Zabuloni
atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka
wake utakuwa kando ya Sidoni.” Yakobo
anaruka utaratibu (Itifaki) ya mfululizo wa uzaliwa na anakwenda kwa kijana
wake wa kumi kwa kuzaliwa na kijana wake wa tisa lakini akiwa anazingatia
watoto wake kwa Leah, Kabila hili wanatabiriwa kua askari, ni kabila maarufu
sana wakati wa utawala wa Daudi, walitoa askari wengi zaidi kuliko kabila
nyingine, wanasifiwa kuwa ni wanajeshi bora nan i hiodari wa kupanga vita, na
hawana kusitasita 1Nyakati 12:33 “Wa Zabuloni,
watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita
za kila namna, hamsini elfu; askari wastadi wasiokuwa wenye moyo wa kusita-sita.”
Licha ya kuwaona kuwa watakuwa watu wa
namna gani vilevile Israel anaona ni eneo gani la nchi ya kanaani watairithi
siku za usoni kwamba watakaa upande wa bahari mashariki na magharibi kuikabili
bahari, Watu wa kabila hili ni watu wenye moyo wa ujasir, wanaojua kupigana
vita vya kiroho, kupanga mashambulizi na walio na imani wasiositasita katika
mipango yao, watu ambao wako tayari kushiriki tabu pamoja na Daudi kwa faida ya
taifa Waebrania 10:38 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye
akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.” 2Timotheo 2:3 “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi
wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu” Ni
ukweli uolio wazi kuwa Mungu hata sasa anahitaji wapiganaji hodari wa Kiroho,
Biblia inawataka watu stadi wanaojua kupigana vita vya kiroho na kutumia silaha
za Mungu ili kuweza kuzipinga hila za Yule muovu ona Waefeso 6:10-13 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza
wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za
Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu
ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu
hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na
mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Zabuloni walimsaidia sana Daudi wakati wa
vita, walijua kupanga vita, walikuwa mashujaa hawakusitasita, Mungu anatutaka
sisis nasi kupambana katika ulimwengu nwa roho kwaajili ya kazi za mfalme wetu
samba wa kabila la Yuda yaani Yesu Kristo, wale wote wanaopambana kwaajili ya
injili na maombi ni askari wema wa yesu Kristo!
5.
Isakari (Mungu
amenilipa)
Mwanzo 49:14-15 “Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya
kondoo; Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama
bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.”
Isakari
wanatajwa kuwa watu wenye nguvu, na watulivu mfano wa punda, lakini ni watu
wenye kuona wanajua nchi na wanajua nyakati, Kabila la Isakari likikuwa ni moja
ya makabila makubwa sana katika Israel kwa mujibu wa sensa katika kitabu cha
hesabu ndio ilikuwa kabila ya tatu kwa ukubwa
Hesabu 26: 25. “Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao,
sitini na nne elfu na mia tatu.”
Na kutokana
na wingi wao pia walitumiwa mara kadhaa kukabiliana na majeshi ya wageni
yaliokuwa yanataka kuwasulubu Israel kwa hiyo walikubali kuwa walinzi na
wanajeshi wa taifa Lakini kabila hili lilikuwa na wataalamu wenye kujua nyakati
na kujua Israel wanapaswa kufanya nini hivyo lilikuwa na viongozi wengi sana
wakati wa Daudi waliotegemewa
1Nyakati12:31-32 “Na wa nusu kabila ya Manase, kumi na nane elfu,
waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme. Na wa wana wa
Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli
wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini
ya amri yao.”
Watu wa Kabila hili ni watu wenye akili, wenye kujua majira na nyakati,
na kujua Israel wanapaswa kufanya nini walikuwa ni wenye uwezo na viongozi
wakubwa na watu waliwasikiliza, Ni kabila ambalo walijua nyakati na walijua na
mna ya kuzitumia nyakati lakini pia walikuwa ni watu wenye kuwajulisha wengine
nini cha kufanya na nini kimetokea, ukweli huu unazihirika wazi kuwa watu hawa
walikuwa ni watu wa namna Na ni kitu gani Israel wanapaswa
kukifanya, Lilikuwa ni kundi la watu pekee waliokuwa wanajua nini cha kufanya
na wakati wa kufanya, walikuwa na hekima na maono jambo ambalo lilifanya taifa
zima kuwasikiliza, Majira na nyakati za
zamani zlikuwa zinategemea mwandamo wa mwezi, kwa hiyo wana wa isakari walikuwa
na ujuzi huo, walitambua mwenendo wa jua na sayari, walijua ni wakati gani wa
kuabudu na ni wakati gani waweke mfalme walijua kutafasiri nyakati na matukio,
walijua majira ya kisiasa nay a kiroho, walijua ni wakati gani Mungu anataka
nini na anafanya nini, alikini vile vile waliijua sharia ya Mungu sana,
walikuwa na hekima na maarifa na walijua kweli za Mungu ni hatari sana kuishi
maisha yasiyo na muelekeo Mithali 29:18
“Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri
mtu yule aishikaye sheria.” Watu wengi wamefeli masomo kwa sababu
hawana maono, wengi wamepoteza kazi kwa sababu hawana maono, wengi wameshuindwa
kukabiliana na wakati ujao kwa sababu hawajui nini liwapasalo kulifanya mtu
asiyejua nini kinakuja mbeleni huwa hajizuii, kuna faida kubwa sana za kujua
majira na nyakati na nini cha kufanya kwa sababu
a. Kila kitu katika maisha yetu kitaamuliwa na Muda
b. Muda ni moja ya jambo la thamani na la muhimu kwa sababu
ukiupoteza hautakuja urudi tena
c. Kila mtu ana muda wake kwa kila jambo, usijifananishe ne mwingine
d. Hakuna mtu anayejua muda wake aliowekewa
e. Muda ukiutumia vibnaya utajuta
f. Muda ni kama Mwalimu utakufundisha
kama ulikuwa na hekima au ulikuwa mjinga ni lazima ujue muda wako na
uhuheshimu, Isakari waliheshimiwa sana na kabila zote na walimsaidia sana
mfalme kwa sababu walikuwa wanajua nini cha kufanya na wakati wa kufanya
Muhubiri 3:1-11 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila
kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa
kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa
kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa
kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe, na
wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa
kutupa; Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati
wa kunena; Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati
wa amani. Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?
Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Kila
kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya
mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu
anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.”
Moja ya jambo ambalo litakuja kuwafanya watu wengi wajute katika maisha yao
baadaye ni kutokujua majira na nyakati na nini mtu anapaswa au alitakiwa
kukifanya Luka 19:41-44 “Alipofika karibu
aliuona mji, akaulilia, akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii,
yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja,
adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande
zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu
ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.” Watu
wanaojua majira na nyakati nwanaitwa wise man au wenye hekima!
6.
Dani (Bwana amenipa
haki yangu).
Mwanzo 49:16-18 “Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya
Israeli; Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya
farasi, Hata apandaye ataanguka chali. Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.”
Ni
moja ya kabila iliyotoa Mwamuzi muhimu na mkubwa mwenye historoa ya kipekee
aitwaye Samsoni Waamuzi 13:1-24 “Wana wa Israeli
wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya Bwana, Bwana akawatia katika
mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arobaini.Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa
jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa
watoto. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa
u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. Basi sasa,
jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi; kwani
tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya
kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye
ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti. Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia
mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa
malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala
hakuniambia jina lake;lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa
mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho
najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya
kufa kwake. Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule
mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo
kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa. Mungu akasikiza sauti ya Manoa; naye
malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani;
lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye. Basi huyo mwanamke akaenda haraka,
akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama, huyo mtu amenitokea, huyo
aliyenijilia siku ile. Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia
mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke?
Akasema, Naam, ni mimi. Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako
yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni
nini? Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, Katika hayo yote niliyomwambia huyo
mwanamke na ajihadhari. Asile kitu cho chote kitokacho katika mzabibu, wala
asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote
niliyomwamuru na ayatunze. Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana,
Nakuomba, tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako. Lakini
malaika wa Bwana akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate
wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa
kumsongezea Bwana. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa Bwana. Manoa
akamwambia huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili kwamba hapo hayo
maneno yako yatakapotimia nipate kukutukuza? Huyo malaika wa Bwana akamwambia,
Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa kuwa jina hilo ni la ajabu?Basi Manoa
akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea Bwana hapo juu
ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia.Kwa
maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale
madhabahuni, huyo malaika wa Bwana akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu;
nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakainama kifudifudi. Lakini malaika wa Bwana
hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika
wa Bwana. Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu
tumemwona Mungu. Lakini mkewe akamwambia, Kama Bwana angetaka kutuua hangepokea
sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha
mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu. Basi yule
mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua,
Bwana akambarikia.” Unabii wa Israel unatimizwa kupitia maisha ya
Samsoni aliyewaamua watu wake vema Dani atawaamua au kuhukumu watu wake hili
lilifanikiwa kwa kiwango cha juu wakati wa maisha ya Samson, Lakini Israel pia
anaeleza jambo la tofauti kidogo kuhusu Dani, Dani atakuwa nyoka! Hii ni tabia
ya kishetani, ni tabia ya ushirikina, Kabila hili linaonekana kuwa na tabia ya
kumshirikisha Mungu na miungu mingine
Waamuzi 18:30-31 “Kisha wana wa Dani wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga;
na Yonathani mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa ni
makuhani katika kabila ya Wadani hata siku ya kuchukuliwa mateka hiyo nchi.
Basi wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga aliyoifanya Mika, wakati wote ile
nyumba ya Mungu ilipokuwako huko Shilo.”
Tunaona
katika habari ya kuabudu sanamu watu wa Kabila ya dani wakiwa wa kwanza kufanya
hayo, Kabila hili likawa kiini cha ibada za sanamu hata katika wakati wa
utawala wa Yeroboamu 1Wafalme 12:26-30 “Yeroboamu
akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. Kama watu hawa
wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, ndipo
mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao
wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. Kwa hiyo mfalme akafanya
shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu
kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli,
iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili
akamweka katika Dani. Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu
mbele ya kila mmoja, hata huko Dani.”
Tabia hii
iliendelea mpaka wakati nabii Amosi alipotangaza hukumu ya kukomesha ibada ya
sanamu katika Israel na kutangaza kuleta kiu ya neno la Mungu ona
Amosi 8:11-14 “Angalia,
siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya
kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya
Bwana. Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi
hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno
la Bwana, wasilione. Siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kwa kiu.
Na hao waapao kwa dhambi ya Samaria, na kusema, Kama aishivyo Mungu wako, Ee
Dani, na, Kama iishivyo njia ya Beer-sheba, hao nao wataanguka, wasiinuke tena.” Israel
anamuona Dani kuwa licha ya kuwa angekuwa mwamuzi mzuri lakini vilevile
angekuwa nyoka miongoni mwa nduguze hasa kwa sababu ya ibada za sanamu lakini
sio hivyo tu wana theolojia wengi wanaamini ya kuwa huenda mpinga Ksristo
atatokea katika kabila la Dani sawa na unabii wa
Daniel 11:36-37 “Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na
kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa
miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa
yatafanyika. Wala hataijali miungu ya baba zake; wala yeye aliyetamaniwa na
wanawake; wala hatamjali mungu awaye yote; maana atajitukuza mwenyewe juu ya
wote.” Na vilevile unabii wa Yeremia 8:16 “Kutoka Dani kumesikiwa
mkoromo wa farasi zake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi
zake za vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote
wakaao ndani yake.”
Hata hivyo
Yakobo aliamini ya kuwa hatimaye Mungu takuja kumkomboa mwanae pia na jamii ya
kabila la Dani kwa kulia kuwa Wokovu wako nimeungoja ee Bwana, Hapa
aliunganisha taabu za vijana wake na ule mpango wa Mungu wa ukombozi, na bila
shaka anamuona masihi!, Watu wa jamii ya kabila hili ni wenye nguvu kama
samsoni ni watu wazuri, wana moyo wa kusaidia wanampenda Mungu lakini wana
tatizo la ushirikina, Mungu anataka tumtegemee yeye na kumtumikia yeye kwa
nguvu zetu zote
1Wakoritho 10:1-21 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa
baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote
wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula
kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana
waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini
wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Basi
mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya,
kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao
walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama
wacheze. Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka
siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao
walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. Wala msinung'unike, kama wengine wao
walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa
jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya
zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Jaribu
halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni
mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile
jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. Kwa ajili ya hayo,
wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema kama na watu wenye akili;
lifikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si
ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote
twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa
jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? Basi
niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya
kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa
mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani.
Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi
kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.” Bwana ampe
neema kila mmoja wetu kuwa mbali na tabia ya kumshirikisha Mungu na miungu, au
ushirikina au kuabudu sanamu, na kutupa kuwa na uhusiano bora nayeye!
7.
Gadi (Bahati njema)
Mwanzo 49: 19 “Gadi,
jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino.” Israel
anamtaja Gadi kama mwanajeshi ni mpambanaji atashambuliwa lakini vilevile
atashambulia na kupata ushindi, Musa aliongezea unabii huu kuwa kila
atakayemgusa Gadi atararuliwa mpaka utosi wa kichwa ona Kumbukumbu la Torati
33:20 “Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye
Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.” Kabila
hili linaonekana baadaye kujitoa kijeshi wakati wa utawala wa Daudi na
walimsaidia sana Daudi wengi wa wagadi walikuwa ni makomandoo na walikuwa
hodari na wajuzi wa vita sana hawakuogopa chochote na walikuwa wepesi na wenye
uzoefu mkubwa katika medani za kivita sio hivyo tu walikuwa na ujuzi wa kutumia
silaha walizokuwa nazo nyakati hizo 1Nyakati 12:8-16 “Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko
nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki;
ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu
juu ya milima; Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu; Mishmana wa
nne, Yeremia wa tano; Atai wa sita, Elieli wa saba; Yohana wa nane, Elzabadi wa
kenda; Yeremia wa kumi, Makbanai wa kumi na moja. Hao wa wana wa Gadi walikuwa
maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa
mkuu, na elfu. Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza,
ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea
mashariki na magharibi pia.Tena wakafika ngomeni kwa Daudi baadhi ya wana wa
Benyamini na Yuda.” Wagadi walikuwa ni watu wasioshindwa vita
wanaweza kuvamiwa kivita lakini lazima waibuke washindi tu Yeremia 49:1 “Habari za wana wa Amoni. Bwana asema hivi, Je, Israeli
hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake
wanakaa katika miji yake? ” Hii ni Baraka kubwa sana kwamba unakuwa
na watu mashujaa, wanaweza kuvamiwa na maadui lakini hawakati tamaa mwisho
lazima wawe washindi tu. Kumbuka Gadi ni mwana wa Zilpa kijakazi cha Lea,
hatupaswi kuwa watu wa kukata tamaa, tunapaswa kuwa hodari katika bwana na
katika uweza wa nguvu zake, tunapaswa kujua namna ya kutumia silaha za kiroho
na kuhakikisha kuwa tunashinda vita zote hata kama kuna wakati tutazidiwa
Kabila la Gadi walikuwa hodari katika vita, na hawakuwahi kushindwa kivita,
Katika agano jipya Maandiko yanatuasa kuwa hodari katika bwana kuhakikisha kuwa
tunashinda Waefeso 6:10-13 “Hatimaye, mzidi kuwa
hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu
ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili,
juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni
silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha
kuyatimiza yote, kusimama.” Ni muhumu kwa kila mmoja wetu
kuhakikisha ya kuwa anakuwa mpambanaji katika maisha yake, tumia kila nafasi
uliyonayo kuwashinda maadui zako, na kushinda kila aina ya kikwazo unachokutana
nacho, hakikisha ya kuwa unatoboa na kupata mpenyo katika kila eneo la maisha
yako usikubali kuwa “defeated” usikubali kushindwa vita yoyote iliyoko
mbele zako Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini
tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni
na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki
za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima
nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa
dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.” Mashujaa wote wa imani nyakati za Biblia
walishinda kila aina ya kikwazo kilichowakabili mbele yao, sisi nasi Bwana na
atupe neema ya kuwa washindi na watu tusioshindwa na lolote katika jina la Yesu
Kristo amen!
8.
Asheri
(Nimebarikiwa/nina
furaha).
Mwanzo 49:20“Asheri,
chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme” Asheri
alikuwa ni mwana wa pili wa Zilpa kijakazi wa Lea, tunaona tena maneno mazuri
sana kutoka kwa Yakobo kuelekea wana wa Leah huenda kulikuwa na malezi mazuri
mno, Asheri anatabiriwa kukaa sehemu yenye hazina za kifalme ni kama ardhi
yenye madini na starehe zinatabiriwa kwake na hawatakuwa na taabu Musa
anaongezea hilo katika Kumbukumbu la Torati 33:24 -29 “Na Asheri akamnena, Na abarikiwe Asheri kwa watoto; Na
akubaliwe katika nduguze, Na achovye mguu wake katika mafuta. Makomeo yako
yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu
zako. Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu
ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake. Mungu wa milele ndiye
makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali
adui; Akasema, Angamiza. Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke
yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande. Uheri,
Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya
msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako,
Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.” Hawa walikuwa watu imara na
wenye nguvu, wataratibu na wasiopigika, adui akija juu yao lazima atiishwe vita
vyao ni Mungu ndiye anayesaidia, unono umetajwa kuunganishwa na kabila hili,
katika agano jipya mwanamke mmoja anatajwa kutokea Kabila hii alikuwa hodari wa
kufunga na muombaji wa kiwango cha juu sana Luka 2:36-38 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa
kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume
miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne;
haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu
alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu,na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi
katika Yerusalemu akawatolea habari zake.”
Kabila hili
Yakobo anasema litatoa tunu za kifalme kwa mujibu wa maelezo ya marabi, ni kuwa
kabila hili lilikuwa na mabinti wazuri mno na wenye adabu, na makuhani wengi na
wafalme walikwenda kuoa katika kabila hili.
Aidha Kabila
la Asheri walipata ardhi nzuri sana na hivyo ardhi waliyoipata iliweza kuwapa
utajiri wa madini na chakula wao walipata ardhi nzuri katika nchi ya kanaani
karibu na bahari ya mediteraniani Yoshua 19:24-31 “Kisha kura ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana
wa Asheri kwa kuandama jamaa zao. Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, na Hali, na
Beteni, na Akishafu; na Alameleki, na Amadi, na Mishali; nao ukafikilia hata
Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Shihor-libnathi; kisha
ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikilia hata
Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hata Bethemeki na
Neyeli; kisha ukatokea hata Kabuli upande wa kushoto; na Ebroni, na Rehobu, na
Hamoni, na Kana, hata kufikilia Sidoni mkuu;kisha mpaka ulizunguka kuelekea
Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na
matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu; na Uma pia, na Afeka, na
Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa
kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji
vyake.”
Mungu
anapokuwa amekubariki wakati wote unakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji na
kamwe hautakuja ukauke ona, Asheri walikuwa wamebarikiwa sana na walistawi na
walikuwa na furaha, na walifanikiwa sana
Zaburi 1:1-3 “Heri
mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia
ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo
impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti
uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”
Isaya 44:3-4 “Kwa
maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali
pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao
utakaowazaa; nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya
maji.”
Yeremiah 17:7-8 “Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni
tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi
yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa
bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa
matunda.”
9.
Naftali
(Bwana
amenipa Ushindi)
Mwanzo 49:21“Naftali
ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri.” Yakobo
anaitaja kabila hii kama uwakilishi wa watu waungwana sana na wanaozungumza
vizuri, hawala lugha mbaya wana mvuto wazuri kama ayala (Paa) na watu walio
huru, Ardhi ya watu hawa ilikuwa karibu na Pwani ya Galilaya maeneo ambayo
Masihi aliyatembelea sana Musa alionyesha kinabii kuwa Naftali ni watu walioshiba
fadhili na kujaa Baraka ona Kumbukumbu la Torati 33:23 “Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili,
Uliyejawa na baraka ya Bwana; Umiliki magharibi na kusini.”ni ukweli
usiopingika kuwa Yesu alitembelea na kufundisha na kufanya miujiza mingi sana
katika nchi ya Naftali ona Mathayo 4:12-16 “Basi
Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;
akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa
Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi
ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya
mataifa,Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika
nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.” Naftali ni mtoto wa mwisho
wa kijakazi wa raheli. Maandiko yanatutaka tuwe waungwana, tuwe na maneno
mazuri, lugha nzuri, Wafilipi 2:1-4 “Basi
ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi,
ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, ijalizeni
furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja,
mkinia mamoja. Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa
unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila
mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.”
Tofauti na nduguze karibu wote wa upande wa Raheli Naftali walikuwa huru,
lakini hawakuutumia uhuru wao vibaya, walitoa maneno mazuri, walikuwa waungwana
hivi ndio wakristo wanavyopaswa kuwa, wakristo ni watu huru, sio watumwa lakini
nhawapaswi kuutumia uhuru wao kwa kukosa kiasi au nidhamu wakristo wanapaswa
kuwa waungwana katika uzungumzaji, na kujali watu Wakolosai 4:5-6 “Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa
wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi
iwapasavyo kumjibu kila mtu.”. Waebrania
13:1-2 “Upendano wa ndugu na udumu. Msisahau
kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo
kujua.” Tabia ya ukarimu na lugha njema zinaweza kuleta mafanikio
makubwa katika biashara, kazi na kujenga mahusiano, watu wa Mungu waliobarikiwa
na waliowaungwana hawapaswi kuwa na lugha mbovu, lazima tuwajibu watu wote kwa
upole na kuacha majivuno, Mungu atatupa mlango uliofunguka kama Naftali,
tutakuwa huru na tuliojawa na uungwana na kupendeza.
10. Yusufu (Bwana
aniongeze)
Mwanzo 49:22-26 “Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye
kuzaa karibu na chemchemi, Matawi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale
walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Lakini upinde wake ukakaa imara,
Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la
mchungaji, yeye jiwe la Israeli, Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia;
Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya
maziwa, na ya mimba. Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale,
Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu,
Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake.”
a. Mti Mchanga
wenye kuzaa, Yusufu Baraka hizo zinamhusu yeye binafsi na vijana wake ambao
Yakobo alikwisha kuwabariki katika Mwanzo 48
b. Anasifiwa kwa
kuwa na uhusiano mkubwa na Mungu na hivyo alibarikiwa sana alikuwa mtumishi wa
Mungu na alikuwa Baraka kubwa kwa familia yake ndugu zake na dunia ya wakati
ule, alisalitiwa na ndugu zake na kufanyiwa mambo machungu Lakini Mungu alimtia
nguvu na kumpa akili na weledi Mungu alikuwa pamoja naye hata kama hakuwa
anajua hilo, alibarikiwa maradufu na kupokea urithi mara mbili kama mzaliwa wa
kwanza na kupandishwa cheo kuwa mojawapo ya mababa wa Israel na wanawe kuwa
makabila ya Israel kuziba nafasi ya Simeoni na lawi ambao Israel aliwatawanya,
Mibaraka aliyopewa Yusufu ilikuwa ile ambayo baba zake waliipata, Yakobo
anamtaja Mungu wa Yakobo yaani Mungu wake kwa Majina makubwa sana anapotoa
Baraka kwa Yusufu
a. Mwenye enzi
wa Yakobo
b. Mchungaji
c. Jiwe la
Israel
d. Mungu wa baba
yako
e. Mwenye Nguvu
Ujuzi kuhusu
Mungu sasa unajulikana vema kwa Yakobo kutokana na uhusiano wake na Mungu na yale
aliyoyafanya kwa Yusufu tofauti na ujuzi ule wa Mungu wa Ibrahimu, na Isaka
Mwanzo 31:53 “Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa
Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu.” Yusufu alikuwa na
tabia njema tangu mwanzo, alipendwa na baba yake, Mungu alisema naye kuhusu
maisha yake ya baadaye, aliamua kuwa mwaminifu kwa Mungu, alipitia magumu
mengi, lakini Mungu alikuwa pamoja naye alijifunza kujua Mungu ni nani,
alitambua mapenzi ya Mungu hata wakati wa mambo magumu, alijifunza kusamehe na
kumuelewa Mungu vizuri, watu wa kabila hii ni jamii ya watu wanaoyajua makusudi
ya Mungu na kuyafahamu mapenzi yake huku wakiwa na ujuzi kuwa katika mambo yote
Mungu hutenda kazi na wale wampendao
katika kuwapati mema Warumi 8:28-30 “Nasi
twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao
katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale
aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana
wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale
aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia
haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.”
Yusufu ni
mfano mzuri wa mtu aliyekuwa katika imani na uadilifu, aliyajua makusudi ya
Mungu na alihakikisha kuwa anawasamehe nduguze na kuwatunza ona Mwanzo
50:15-21 “Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba
baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu
tuliyomtenda. Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla
ya kufa kwake, akasema, Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako
kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie
kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.Nduguze
wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako. Yusufu akawaambia,
Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali
Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. Basi
sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.”
Yusufu
anapata uristhi maradufu miongoni mwa ndugu zake, watoto wake wawili
wanafanyika kuwa wana wa Israel wakichukua nafasi ya simeoni na lawi ambao Israel
aliwagawa kwa kuwa hawakuwa na rehema Mwanzo 48:3-5 “Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi
ya Kanaani, akanibariki, akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na
kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako
nchi hii baada yako, iwe milki ya milele. Basi sasa wanao wawili uliozaliwa
katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu
na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.” Kwa msingi huo Yusufu anaingia katika
orodha ya mababa Ibrahimu, Isaka, Yakobo na yusufu na watoto wake wanaingia
katika kabila za Israel, Mtu awaye yote aklifanya vema Mungu atambarikia.
11. Benjamin (Mwana wa mkono wangu wa
kuume).
Mwanzo 49:27 “Benyamini
ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua, Asubuhi atakula mawindo, Na jioni
atagawanya mateka.” Hili lilikuwa
ni kabila lenye watu wakali wasiotetereka (aggressive) walikuwa wakatili na wapambanaji
na wakati wote walitafuta kuwa washindi Ehud ni moja ya waamuzi aliyetoka
kabila hili Waamuzi 3:15-23 “Lakini wana wa
Israeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera,
Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni
mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi. Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa
na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya
nguo yake katika paja lake la mkono wa kuume. Kisha akamsongezea Egloni, mfalme
wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyewanda sana.Naye hapo
alipokuwa amekwisha kuisongeza hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua
tunu, wakaenda zao. Lakini yeye mwenyewe akageuka kutoka huko kwenye sanamu
zilizokuwa karibu na Gilgali, akasema, Mimi nina ujumbe wa siri kwako wewe, Ee
mfalme. Naye akasema, Nyamazeni kimya. Watu wote waliokuwa wanasimama karibu
naye wakatoka na kumwacha. Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke
yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa
Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake. Ehudi akaunyosha mkono wake
wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia
tumboni mwake; hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe;
nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga
tumboni; nao ukatokea kwa nyuma. Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia
milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo.” Aidha ni kabila
lililotoa mfalme wa kwanza kabisa kuitawala Israel 1Samuel 9:1 “Basi, kulikuwa na mtu mmoja wa Benyamini, jina lake
akiitwa Kishi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa
Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa, mwenye nguvu.” Mfalme huyu
alikuwa hodari sana katika vita 1Samuel 14:47-52 “Basi Sauli alipokwisha kuutwaa ufalme juu ya Israeli,
alipigana na adui zake zote pande zote, juu ya Moabu, na juu ya wana wa Amoni,
na juu ya Edomu, na juu ya wafalme wa Soba, na juu ya Wafilisti; na po pote
alipogeukia, akawashinda. Naye akatenda kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na
kuwaokoa Waisraeli katika mikono yao waliowateka nyara. Basi, wana wa Sauli
walikuwa ni hawa, Yonathani, na Ishvi, na Malkishua; na majina ya binti zake
wawili yalikuwa haya; jina lake wa kwanza aliitwa Merabu, na jina lake mdogo
aliitwa Mikali; na jina lake mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu, binti Ahimaasi.
Tena, jina la jemadari wa jeshi lake aliitwa Abneri, mwana wa Neri, aliyekuwa
baba mdogo wa Sauli. Na Kishi, babaye Sauli, na Neri, babaye Abneri, walikuwa
wana wa Abieli. Tena, kulikuwa na vita vikali sana juu ya Wafilisti siku zote
za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu ye yote aliyekuwa hodari, au mtu ye yote
aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.” Katika agano jipya
tunaelezwa habari za Sauli au Paulo mtume namna alivyokuwa na hatimaye baadaye
Mungu alimtumia sana na akafanya kazi kuliko mitume wote Matendo 8:1-3 “Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika
Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao
mitume. Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.Sauli
akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na
kuwatupa gerezani.” Israel anamfananisha Benjamin na Mbwa mwitu
kwamba mbwa hawa ni wadogo, lakini wako makini nan i wawindaji wazuri na wakali
hawana mchezo wanauwezo wa kurarua rarua wana umoja na huwinda kwa kufunga mtaa
wanaogopwa na wanyama wengi hata wakubwa, mbwa mwitu hakubali kushindwa,
anaamini katika ujamaa, wanapiga kazi na hawachoki, wakishiba wao hushinda
wanacheza na kufutrahi, na ukitaka vita nao gusa watoto wake, watu wenye Kabila
hii wanafanikiwa katika kila wanachokitamani na kutimiza kila jukumu wanalopewa
na kulifanikisha
Yakobo Anakamilisha kazi yake Duniani
Baada ya
Israel Kumaliza kuwabariki vijana wake kazi yake ikawa imekamilika aliagiza
azikwe Israel katika mji wa Hebron Pale pale walipozikwa wazee wake, kwanini
alikifumbua kinywa chake alitaka kuwabariki, alitaka kuwatabiria, tabia zetu na
mwenendo wetu utaamua kuwa sisi tuwe watu wa aina gani, Kila mmoja alikuwa na
mambo yake mazuri na kila mmoja alikuwa na mapungufu yake, lakini tunahitaji
neema ya Mungu kuiga mazuri kwa maana sisi sasa ndio hao wana wa Israel, Leo
hii hayuko Benjamin, hayuko Asheri wala Gadi watu hao ni mimi na wewe je
unayasikiliza mausia ya Yakobo? Je unasikiliza Israel baba yako, neno la Mungu
ndio mausia yetu leo, endapo tutalisghika na kulitii na kuliishi litaamua
hatima yetu
Mwanzo 49: 28-33. “Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo
ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake
aliwabariki. Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu
wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni,
Mhiti; katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre
katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti,
pawe milki yake ya kuzikia. Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo
wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; shamba na pango
iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi. Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza
wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake”
Bwana na ampe
neema kila mmoja kubwarikiwa na Roho Mtakatifu, tunapolishika neno lake na
kubadili matendo yetu ili tupate thawabu zinazokusudiwa kwetu amen uongezewe
neema
Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!
~0718990796~