Maombolezo 3:31-33 “Kwa kuwa Bwana
hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya
wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala
kuwahuzunisha.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu
kama baba yetu, ana njia zake za anazozitumia katika kutujenga, kutufunza,
kutubadilisha na kutuonya, katika wakati huo Mungu hutumia njia mbalimbali hata
mateso, vita na hata matishio ya hapa na pale, ili Hatimaye aweze kutuleta
katika toba tumgeukie yeye na kushikamana naye na kumfanya yeye kuwa tegemeo
letu
2Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi
yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi
mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.”
Kusudi kubwa la Mungu ni kutuleta
katika toba, toba maana yake ni mabadiliko, Neno toba katika lugha ya kiyunani
(Greek) ni METANOIA Ambalo maana
yake ni badiliko kubwa la moyo, au kugeuka na kuacha njia isiyofaa na kuendea
njia inayofaa, kwa hivyi Mungu hutumia huzuni kama baba wa kiroho kutuleta
katika makusudi yale yaliyo mema ona
Waebrania
12:5-11 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo
nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala
usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye
humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu
awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa
hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi,
wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili
walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa
roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama
walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu
wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni;
lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.”
Mungu katika hekima yake
anapotaka kutonya, kuturekebisha, kutufundisha anaruhusu mateso, lakini sio kwa
kusudi la kututesa bali kwa kusudi la kutuleta katika toba yaani mabadiliko
makubwa ili hatimaye, tuweze kujenga uhusiano imara na yeye na hatimaye tuweze
kuwa na ukomavu wa kiroho na kumuua yeye na njia zake jambo ambalo litaleta
furaha milele katika maisha yetu, sawa na baba anavyomuonya mwanae kwa makusudi
yale yale ya kumzoeza mtoto kuzaa matunda ya haki na amani.
Bwana hatamtupa mtu
hata milele!
Ni ukweli usiopingika kuwa Mungu
hakutufanya sisi kuwa kama mashetani, ambao walipoasi aliwakataa milele, sisi
ametupa nafasi ambayo kwayo tunaweza kurejesha uhusiano wetu na yeye, Wana wa
Israel katika ufalme wa Yuda walikuwa wameacha kumtegemea Mungu na wakawa
wakitegema mafanikio yao, akili zao na mambo mengine Mungu akiwaonya kwa vinywa
vya manabii huwa angeakatilia mbali kutoka katika nchi njema aliyokuwa amewapa,
na anageruhusu waende utumwani
Yeremia 27:6 -8 “Na sasa nimetia nchi hizi
zote katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu; na wanyama
wa mwituni pia nimempa wamtumikie. Na mataifa yote watamtumikia yeye, na
mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe,
ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye. Na itakuwa, taifa
lile na mfalme yule asiyetaka kumtumikia Nebukadreza, huyo mfalme wa Babeli, na
kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile
kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, asema Bwana, hata nitakapokuwa
nimewaangamiza kwa mkono wake.”
Kwa msingi huo Yeremia alitumiwa
na Mungu mara kadhaa kuwaonya wana wa Israel na kuwataka wakubali kumtumiakia
mfalme huyu wa Babeli kama adhabu kwao
ili baadaye akawabadilishe, Hata hivyo wana wa Yuda hawakutubu wala kuamini
kile alichokionya Nebukadreza, hivyo walichukuliwa utumwani na hekalu lao
lilibomeolewa na kuchomwa moto kila kitu cha kifahari kiliharibiwa vibaya watu
walipitia mateso na walilia na kusaga meno huku Yeremia nabii akiona kila
kilichokuwa kinaendelea jambo
lililomfanya ateseke mno kwani aliona mateso ambayo hajawahi kuyaona japo yeye
akuuawa lakini ndugu zake na jamaa zake walipata taabu sana ndipo Yeremuia anaeleza katika maombolezo
yake
Maombolezo 3:1-18 “Mimi ni mtu aliyeona
mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake. Ameniongoza na kuniendesha katika giza Wala
si katika nuru. Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote.
Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha
uchungu na uchovu. Amenikalisha penye
giza, Kama watu waliokufa zamani. Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka;
Ameufanya mnyororo wangu mzito. Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga
maombi yangu. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito
yangu. Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye, Kama simba aliye mafichoni.
Amezigeuza njia zangu, na kunirarua-rarua; Amenifanya ukiwa. Ameupinda upinde
wake, Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale. Amenichoma viuno Kwa mishale ya
podo lake. Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote; Wimbo wao mchana kutwa. Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga.
Amenivunja meno kwa changarawe; Amenifunika majivu. Umeniweka nafsi yangu mbali
na amani; Nikasahau kufanikiwa. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini
langu kwa Bwana.”
Mfalme huyu katili alifanya
unyama wa ajabu sana ona mukhtasari wa unyama wake:-
1. Aliuzingira
Yerusalem kwa muda wa miaka miwili na kuhakikisha kuwa wanateseka kwa njaaa
2. Aliwavamia
na kuwapiga na kuwachukua mateka vijana wenye nguvu
3. Alilibiomoa
hekalu na kulichoma moto kwa kuliteketeza
4. Aliwaongoza
njiani wayahudi huku akiwaachia wengine waliwe na simba
5. Alihakikisha
kuwa wanapelekwa utumwani Babeli moja kwa moja bila kupumzika ili kuwanyima
wayahudi nafasi ya toba, na maombi ili Mungu wao asije akawaokoa
6. Akiwaasi
vijana wenye hekima na wazuri wasizae tena, na kuwageuza matowashi katika
nyumba yake
Katika historia ya Israel
wanamkumbuka Mfalme huyu kama mfalme katili zaidi kupata kutokea katika
ulimwengu, dikteta asiye na huruma ambaye ataendelea kukumbukwa kwa miaka Mingi
kama anavyokumbukwa “Adolf Hitler” aliyeua
wayahudi wapatao milioni sita, watu wale walioona mateso haya walihuzunishwa
sana na hiki kilichotokea, ilikuwa ni taabu mno na wengi wakasema Mungu
ametutupa, ni ukweli uliokuwa wazi kwamba hata adui za Israel waliita Sayuni
mji uliotupwa, Na ndipo Yeremia alipotoa unabii kuwa Mungu ataujenga tena
Sayuni
Yeremia 30:17-19 “Maana nitakurudishia
afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye
kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. Bwana asema hivi,
Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao
yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa,
kama ilivyokuwa desturi yake. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao
wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza,
wala hawatakuwa wanyonge.”
Mungu ametuahidi kuwa hatatutupa kamwe !
Ni ahadi ya Mungu kuwa hatatutupa
milele, Yesu alisema kila ajae kwangu sitamtupa nje kamwe Yohana 6:37-39 “Wote anipao Baba watakuja
kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Kwa kuwa mimi sikushuka
kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa
nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.”
Ni wajibu wetu kufahamu kuwa tunaweza kupita
katika giza, tunaweza kupitia mateso na huzuni nzito, mashaka na woga,
mashutumu na masengenyo, giza na kutokufanikiwa, mashambulizi ya adui pande
zote, kizibiwa niia, kama milango imefunga kila mahali lakini hatuna budi
kukumbuka neno la Mungu na Bwana wetu Yesu ametuahidi kuwa hatatuacha milele,
wala hatatutupa kamwe, wanadamu wanaweza kututupa, wanaweza kutudharau,
wanaweza kutuweka pembeni, wanaweza kutozomea lakini Mungu hawezi kamwe
kuwatupa watu wake, tunapohisi kuwa tunapita katiika huzuni na mateso kumbuka
kuwa hatujaweka tumaini letu kwa mwanadamu wala kwa miungu tutaendelea kuliitia
jina la bwana Mungu wetu mpaka kielelweke
a.
Endelea
kuliitia jina la Bwana na kumpazia sauti
Zaburi 77:7 – 1-2, “Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye
atanisikia. Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa
usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.” 7-9 “Je! Bwana atatupa milele na milele? Hatatenda fadhili
tena kabisa? Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi
vyote? Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?”
b.
Kumbuka
wewe ndio urithi wa Bwana na hakuna mwingine Zaburi
94:14 “Kwa kuwa Bwana hatawatupa watu wake, Wala
hutauacha urithi wake,”
c.
Kumbuka
tunalibeba jina lake kuu na Bwana amekusudia kutufanya kuwa watu wake 1Samuel
12:20-22 “Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli
mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata Bwana, bali
mtumikieni Bwana kwa mioyo yenu yote. Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu
vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana
Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza
Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.”
d.
Kumbuka
kuwa mapito yako ni ya kitambo tu na kuwa Bwana hatamtupa mtu hata milele! Maombolezo 3:31-33 “Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana
ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake
hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.”
Wewe ni Mungu mpasua bahari, haufananishwi
na kitu kingine, haulinganishwi. na kitu kingine unafanya mambo ambayo
mwanadamu hawezi kufanya, unatoa faraja ambayo mwanadamu hawezi kutoa
haulinganishi na kitu kingine.
Na Rev. Innocent Samuel Jumaa Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni