2Nyakati 32:7-8 “Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike
kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa
maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye; kwake upo mkono wa mwili;
ila kwetu yupo Bwana, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na
watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.”
Utangulizi:
Kwa maana yuko Mkuu pamoja nasi! Ni maneno ya kutia moyo katika
wakati Mgumu, wakati ambapo Mfalme senekarebu wa Ashuru, alipokuja kuizingira
Yerusalem ili auangamize, Mfalme huyu alikuwa anapata ushindi kila alikokwenda,
na kwa sababu alikuwa akiabudu miungu aliamini ushindi wake umetokana na Mungu
aliyemuamini, Yeye alikuwa ameshinda vita zote za kaskazini wakati wa kampeni
yake ikiwemo ufalme wa Israel ya kaskazini maarufu kama samaria, Ushindi wake
dhidi ya mataifa mengine na hata Israel ya kusini ulimpa kiburi na kujiona kuwa
yeye sasa ni super power kingdom na kuwa ana uwezo wa kumshinda yeyoye, kwani
hata hao waliodai kutegemea miungu ya aina mbalimbali pia aliwashughulikia ona
maneno yake
2Nyakati 32:9-19 “Na baada ya hayo
Senakeribu mfalme wa Ashuru, akatuma watumishi wake waende Yerusalemu, (naye
alikuwapo mbele ya Lakishi, na uwezo wake wote pamoja naye,) kwa Hezekia,
mfalme wa Yuda, na kwa Yuda wote waliokuwako Yerusalemu, kusema, Senakeribu,
mfalme wa Ashuru, asema hivi, Mwatumainia nini hata mkae mkihusuriwa katika
Yerusalemu? Siye Hezekia anayewashawishi, mtolewe kufa kwa njaa na kwa kiu,
akisema, Bwana, Mungu wetu, atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru? Si yeye
Hezekia huyo aliyeondoa mahali pake pa juu, na madhabahu zake, akawaamuru Yuda
na Yerusalemu, akisema, Abuduni mbele ya madhabahu moja, na juu yake mtafukiza
uvumba? Je! Ninyi hamjui mimi na baba zangu tuliyowafanyia watu wote wa nchi?
Je! Miungu ya mataifa wa nchi iliweza kuokoa kwa lo lote nchi zao na mkono
wangu? Ni yupi miongoni mwa miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba
zangu, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, hata Mungu wenu aweze kuwaokoa
ninyi na mkono wangu? Basi sasa asiwadanganye Hezekia, wala asiwashawishi kwa
hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lo lote, wala wa ufalme
wo wote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au na mkono wa baba
zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu? Na watumishi wake
wakazidi kusema juu ya Bwana Mungu, na juu ya Hezekia, mtumishi wake. Tena
akaandika waraka, kumtukana Bwana, Mungu wa Israeli, na kumwambia, akisema,
Kama vile miungu ya mataifa wa nchi isivyowaokoa watu wao na mkono wangu, vivyo
hivyo Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake na mkono wangu. Wakawalilia kwa
sauti kuu, kwa lugha ya Kiyahudi, watu wa Yerusalemu waliokuwako ukutani ili
kuwaogofisha, na kuwafadhaisha; hata wapate kuutwaa mji. Wakamnenea Mungu wa
Yerusalemu, kana kwamba kuitaja miungu ya mataifa wa nchi, iliyo kazi ya mikono
ya watu.”
Ushindi wake dhidi ya mataifa mengine na Israel ya Kaskazini
ulimfanya Senekarebu ajivune na kufikiri kuwa hakuna Mungu mwingine anayeweza
kumshughulikia, Hili lilikuwa tishio kubwa sana kwa Hezekia kwani senekarebu
alichiokuwa anakisema ni kweli, na alikuwa ameshinda vita zote na sasa
anaikabili Yuda na anaukabili mji wa Yerusalem, na alikuwa na kombaini kubwa
sana ya majeshi, Yeye ndio alikuwa taifa kubwa Duniani kwa wakti ule na hakuna
taifa lolote lililoweza kusimama mbele yake kwa miaka Mingi, Senekarebu alikuwa
amejiimarisha vya kutosha akiwa na jeshi lenye nguvu kweli kweli na alikuwa
tayari anaumiliki ulimwengu wa wakati ule na tayari hata taifa ndugu la Israel
lilikuwa limesalimu amri, na kama ilivyokuwa desturi ya vita hapa senekarebu
anapeleka vitisho na athari za kisaikolojia kwa utawala wa kiyahudi!
Mfalme Hezekia akiwa na ujuzi mkubwa wa siri ya ushindi, alimuomba Mungu lakini vilevile alitumia Hekima na akili ya kujilinda Yeye Pamoja na nabii Isaya walimuomba Mungu na kumlilia kwa nguvu hata mbinguni ona 2Nyakati 32:20 “Na kwa ajili ya hayo Hezekia mfalme, na Isaya nabii, mwana wa Amozi, wakaomba, wakalia hata mbinguni.” Hezekia aidha alihakikisha kuwa maji hayatiririki kuwafikia maadui, hivyo yeye na watu wake waliwakati amaji kwa kuifunga mifereji ya kupeleka maji ili majeshi ya maadui wapatwe na kiu ona , Lakini pia alijenga ukuta wa Yerusalemu uliokuwa umeanguka, na kufanya maandalizi ya kivita kwa kutengeneza silaha na kuandaa maakida au makamanda aidha yeye mwenyewe alitoa speech ya kuwatia moto na kuwafurahisha watu ambayo ilikuja kuwa tumaini kubwa kwa watu na kuleta utayari wa vita ona
2Nyakati 32:2-6. “Basi Hezekia, alipoona ya kuwa Senakeribu amekuja, na kuazimia
kupigana na Yerusalemu, akafanya shauri na wakuu wake, na mashujaa wake, kuzuia
maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya mji; nao wakamsaidia. Wakakusanyika watu
wengi, wakazizuia chemchemi zote, na kijito kilichopita kati ya nchi, wakisema,
Kwa nini, wakifika wafalme wa Ashuru, waone maji mengi? Akapiga moyo konde,
akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje,
akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele. Akaweka
maakida wa vita juu ya watu, akawakusanya kwake uwandani penye lango la mji,
akawafurahisha mioyo; akisema”
Hezekia alikuwa na ufahamu kuwa Israel haiku yenyewe hivyo pamoja na maandalizi ya vita , na maombi yeye alikumbuka wazi kama nabii Elisha aliyemtia moyo mtumishi wake kuelewa kuwa katika ulimwengu war oho watu wamuaminio Mungu hawako pake yao hatuko peke yetu ona
2Wafalme 6:15-16 “Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.”
Hezekia alikuwa na ufahamu huo aliliamini neno la Mungu, alikuwa
amejifunza kuwa watu wanaomuamini Mungu hawako peke yao, aliamini kuwa kuna
zaidi ya majeshi ya kimwili yanayoonekana, na kuna majemadari zaidi ya
majemadari wa kimwili wanaoonekana Hauijalishi kuwa senekarebu ana nguvu kiasi
gani, ana historia ya ushindi na uonevu kiasi gani yeye hakuwa anatoa
propaganda za kawaida za kijeshi yeye alikuwa anazungumza ukweli ulio wazi
kwamba yupo Mkuu Pamoja nasi !, na kuwa
mfalme Senekarebu na majeshi yake yote hayana kitu kwa huyu Mungu wa wayahudi,
na kwa kuwa mfaklme huyu alitoa maneno ya kejeli na kumtukana Mungu wa Israel Mungyu
alileta ushindi wa ajabu sana safari hii Mungu alituma malaika mmoja tu na
akadhalilisha jeshi zima la waashuru ona
2Nyakati 32:21-22 “Naye Bwana akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa
wote, na majemadari, na maakida, matuoni mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia
nchi yake mwenye haya ya uso. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, wale
waliotoka viunoni mwake mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga. Ndivyo Bwana
alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji wa Yerusalemu, na mkono wa Senakeribu, mfalme
wa Ashuru, na mikononi mwa wote, akawaongoza pande zote.”
Nisikilize sio kila wakati Mungu atawatawanya maadui zako
wasikuzingire, Mungu atawaacha wakufkie wakutishe, lakini ukisimama imara na
ukawa na uelewa kuwa Mungu anafanya kasi namna gani wataaibika na kufedheheka
wanaokutafuta nafi yako kumbuka maandiko yanasema “Waandaa meza mbele yangu machioni pa
watesi wangu” Zaburi 23;5. Tunaye Mungu ambaye wakati wote anawajali
watu wamuaminio na kumtumaini yeye atwaacha adui zetu waingine kwenye 18 zake
kisha atawateketeza, aliwaacha wamisri waingie kwenye bahari ya shamu na kisha
akawafytilia mbali, alimuacha Senekarebu afike na kuizunguka Yerusalem lakini
alimfutilia mbali
Siku zote nasema tukimtumaini Bwana na kumtegemea yeye tutakuwa
salama, jambo kubwa la msingi la kuelewa ni kuwa Yule mkuu aliye pamoja nasi,
ndio Emmanuel Mungu pamoja nasi, kila aina ya adui zako watapotea na Mungu
atawaaibisha senekarebu alirudi kwa aibu kwao na kupinduliwa na watoto wake
mwenyewe kupigo alichokipata kilikuwa kipigo cha kushangaza, hakupigwa na wingi
wa majeshi alishughulikiwa na Askari mmoja tu kutoka Mbinguni, Bwana ni Mungu
nwa Majeshi na atatupigania dhidi ya adui zetu na wale wanaotuandama na
kututisha bila kujali historia zao kuwa wana nguvu kliasi gani, wana fedha
kiasi gani ni maarufu kiasi gani Yuko mkuu pamoja nasi, yuko mkuu pamoja name,
Yuko mkuu pamoja nawe, yuko mkuu ni Mungu pamoja nasi anatosha peke yake kusambaratisha
maadui na ikuwarudisha nyumbani kwao kwa aibu wakafie mbele
Rev. Innocent Samuel
Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye
Hekima !
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni